Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live

Aliyemtukana Mtume Kuadhibiwa Kifo Nchini Mauritania

$
0
0
Mahakama ya Rufaa ya Mauritania imepasisha hukumu ya kifo dhidi ya mwandishi aliyemvunjia heshima Mtume Muhammad (saw).

Shirika la Habari la Kimataifa la Qur'ani (IQNA) limeripoti kuwa, Mahakama ya Rufaa ya mji wa Nawadibo huko kaskazini magharibi mwa Mauritania imepasisha hukumu ya kifo dhidi ya mwandishi Muhammad Sheikh Ould Amkhtir wa nchi hiyo kwa sababu ya kuandika makala iliyomvunjia heshima na kumtusi Mtume wa Mwenyezi Mungu, Muhammad (saw) hapo mwaka 2014.

Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mauritania ambaye aliomba kutolewe hukumu ya kifo dhidi ya mwandishi huyo amesema kuwa kunyongwa kwake kutakuwa somo kwa wale wote wanaothubutu kumvunjia heshima Mtume wa Mwenyezi Mungu.

Kuchapishwa kwa makala ya mandishi Muhammad Sheikh Ould Amkhtir hapo mwaka 2014 kulisababisha maandamano makubwa kote Mauritania ambayo hayakutulia ila baada ya kutolewa hukumu ya kifo dhidi ya mwandishi huyo.

Mkuu Wa Mkoa Wa Mwanza John Mongella Atoa Saa 24 Kompyuta Ya Halmashauri Ya Ukerewe Iliyoibwa Ipatikane

$
0
0

Mkuu wa mkoa wa MWANZA John Mongella (pichani) ametoa saa 24 kwa kamanda wa Polisi Wilaya ya Ukerewe Ally Mkaripa, kuhakikisha wanaitafuta hadi kuipata komputa iliyoibwa usiku wa kuamkia April 22, 2016 kwenye chumba kinachotumika na mifumo ya ukusanyaji mapato  na uaandaji wa malipo ya Halmashauri (EPICOR)

Mhe. Mongella ametoa agizo hilo wakati  akizungumza kwenye kikao cha kujitambulisha kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri,ambapo taarifa za awali zilionesha kutokea kwa wizi wa komputa moja iliyofungwa kwenye chumba cha mifumo ya komputa ambayo ndio hutumika kuandaa malipo mbali mbali ya halmashauri.

“OCD kesho nitakwenda kanisani asubuhi, ikifika saa 8.00 mchana nataka taarifa niikute mezani kwangu, vinginevyo hatutaelewana", amesema Mongella na kuongeza sisi tunajua nini chakufanya kama kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa lakini na wewe tumia mbinu zako kuweza kubaini wapi ilipo kompyuta hiyo.

Akizungumza kando ya ukumbi wa mikutano wa halmashauri, kaimu mhazini wa halmashauri hiyo Baraka Munuo, alidai kupokea taarifa za kupotea kwa Komputa hiyo kutoka kwa  afisa TEHAMA wa halmashauri ya Ukerewe akimuelezea upotevu huo.

Katika hatua nyingine mkuu wa mkoa wa MWANZA, amemuagiza mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya  ukerewe,, kupitia mafaili na kubaini watumishi waliofanya kazi katika kituo hicho kwa muda mrefu, jambo ambalo mkuu wa mkoa amedai linachangia watumishi kufanyakazi kwa mazoea.

”Mkurugenzi nakuagiza pitia mafaili ya watumishi ili kubaini wote waliokaa katika kituo hiki kwa muda mrefu. Haiwezekani mtu amekaa hapa miaka ishirini na moja halafu uniambie kwamba atakuwa na maarifa mapya, hapana" alisema Mongella na kuongeza, Sasa nakuagiza pitia mafaili yao na kama kuna mtumishi aliye kaa kwa zaidi ya miaka kumi atafutiwe kituo kingine.

Awali akisoma taarifa ya wilaya hiyo, mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Joseph Mkirikiti,alimwambia mkuu wa mkoa kuwa hali ya ulinzi na usalama ni shwari na wananchi wanaendelea na shughuli zao za maendeleo huku akisema wilaya imefanikiwa kutokomeza ugonjwa wa kipindupindu kilicho kuwa kimepiga kambi katika Wilaya hiyo kwa zaidi ya miezi 6.

Mkuu wa mkoa wa yupo katika ziara yakujitambulisha na hii ikiwa ni wilaya yake ya saba,Mara baada yakutembelea wilaya za Misungwi, Magu, Nyamagana, Ilemela na Kwimba na hii ya Ukerewe inakuwa wilaya ya saba huku akiwa amebakiza wilaya moja ya Sengerema yenye halmashauri za Buchosa na Sengerema yenyewe.

Huyu Sallam Kumbe ndio Kila Kitu Kwa Mwanamuziki Diamond..Mfahamu Hapa

$
0
0
DIAMOND Platinumz ni mwanamuziki mkubwa Afrika, inatajwa kuwa msanii huyo ana timu nzuri nyuma yake ambayo imemwezesha kupata mafanikio mengi makubwa.

Ukiachana na Said Fella na Babu Tale, kuna mtu anaitwa Sallam ambaye inaaminika ni mmoja wa watu muhimu katika menejimenti ya Diamond. Sifa yake kubwa inayotajwa kuwa ni mzuri kutengeneza ‘connection’ nyingi zilizompaisha Diamond kimataifa.

Mashabiki na wadau wengi hawamfahamu kiundani, siku za hivi karibuni staa mwingine wa Bongo Fleva, AY alimtaja Sallam kuwa meneja wake. Sallam amezungumza na gazeti hili na kufunguka mengi:

Championi: Unajulikana kwa jina la Sallam, umetokea wapi na ulianzaje umeneja?

Sallam: Naitwa Sallam Sharaf, nilizaliwa Dar na nikasomea Morogoro. Muziki nilianza muda mrefu tangu nikiwa Shule ya Forest, Morogoro. Tulikuwa na kundi letu la Watukutu, tulikuwa tuna-rap, liliundwa na Puzzo, Swedi na mimi nikijiita OG.

Watukutu ilikuwa ikileta ushindani wa wasanii wa Dar na Moro, wale wa Dar walikuwa ni kina Mr II, Hard Blastaz na Dilpomatz. Profesa Jay yeye alitambulika akitokea Moro akiwa katika Kundi la Simple Guyz. Baadaye likazaliwa kundi lingine la Ze don P la kina Squeezer, kulikuwa na ushindani mkali sana wa makundi kwa wakati huo.

Uliingiaje kwenye umeneja?

Mwanzo nilikuwa napenda kuandaa shoo, niliwahi kuwaleta Prezzo, Hudah Monroe (wa Kenya), Jay Martins (Nigeria), hapohapo kina AY na MwanaFA wakamchukua J wakafanya naye wimbo wa Bila Kukunja Goti halafu nikamuunganisha na Ommy Dimpoz wakafanya ile ngoma ya Tupogo. Hata video ya Bila Kukunja Goti niliisimamia mimi kishkaji tu.

Ulikutana vipi na Diamond?

Kwa kuwa nilikuwa tayari nina ‘connections’ zangu, mwaka 2013 nilipata tenda ya Clouds FM kuwaleta kina Iyanya, Jay Martins na Davido kwenye Fiesta nikiwa wakala, nikapewa hela yangu tukamalizana.

Baadaye Diamond akanipigia simu akasema anataka kufanya kazi na Davido, nikampa masharti yangu akayakubali, nikazungumza na menejimenti ya Davido, tukaelewana, kesho yake ikaenda kufanywa remix ya Number One.

Tukataka kufanya video ya hiyo remix lakini Ogopa Deejayz wakachelewa, Davido akarudi kwao na baadaye ikaenda kufanyika Nigeria. Baada ya hizo harakati, Tale, Fella na Diamond wakasema kama vipi tuungane, tutengeneze timu iendelee kuwa kubwa na tangu hapo ndiyo nikaanza kufanya kazi na Diamond.

Wasanii gani wengine unafanya nao kazi?

AY, MwanaFA ambao wameingia hivi karibuni lakini nilianza kufanya nao kazi tangu awali kabla ya Diamond. Wengine ni Harmonize, Raymond na wasanii wa WCB.

AY si mwepesi wa kukubali kusimamiwa, uliwezaje kukubaliana naye?

Najitahidi kufanya kazi yangu katika ubora siyo ilimradi ikamilike. AY ni mtu ambaye nipo naye sana kila sehemu kuliko hata Diamond, aliliona hilo na kwa kuwa anajua ushindani umekua ndipo akaamua awe na msimamizi wa kazi zake, maana yeye peke yake hawezi kusimamia kila kitu.

Mkataba wako na AY ukoje?

Sina mkataba na msanii yeyote, mikataba yangu ni ya kiimani, tufanye kazi tutalipana hivi na hivi na kama ukiamua kunidhulumu sawa tu. Ila sijawahi kudhulumiwa!

Kazi zako ni zipi kwa msanii na unafaidika vipi?

Meneja ni mfanyakazi wa msanii, unapokuwa msanii tayari wewe ni kampuni inayohitaji watu kama mameneja. Malipo ni katika asilimia ya kazi mnazozifanya, kila sanaa inayofanyika kupitia yeye lazima meneja awe na fungu lake.

Mfano AY au Diamond ni ‘brand’ kubwa, wana nguvu kubwa, unajua kuna asilimia yangu kama kawaida lakini kwa msanii mchanga anayetaka nimsimamie analazimika anilipe yeye.

Hivi kwanini Diamond ana mameneja wengi?

Kwa Diamond hata mameneja watatu hawatoshi. Mfano juzi tulikwenda kwenye ziara Ulaya, hapo lazima uwe na meneja atakayedili na chakula, ratiba, ukumbi na mengine mengi.

Sisi tunakuwa tunapokezana, Tale pia ni meneja wa Tip Top na Madee, wakati huo mimi nakuwa na Diamond. Kuna muda Fella anakuwa na Ya Moto Band, tunakuwa tunabadilishana kama hivyo.

Unatumia njia gani kurahisisha kazi yako?

Ni kujiamini tu, huwa siogopi mtu, nikipewa nafasi naitumia vizuri, nazijua vizuri ‘CV’ za wasanii wangu.

Ikitokea Ali Kiba anahitaji ufanye naye kazi, utakubali?

Sina tatizo kabisa, akitaka tufanye kazi nitamweleza mahitaji yangu akikubali tutafanya kazi. Nilishawahi kukutana na Kiba, Nairobi, alinifuata akaomba tupige picha, sikuwa na kinyongo, tukapiga ikawa safi japokuwa ile picha aliitumia kunitukanisha baadaye.

Kivipi?

Hakuiweka yeye katika mtandao, aliitoa kwa mashabiki wake ambao wakasema nimeenda Nairobi kumfuata Ne-Yo halafu nikafukuzwa, wakasema mimi ndiyo niliomba kupiga picha na Kiba, ikawa gumzo sehemu nyingi.

Ukweli nilikuwa na Ne-Yo na Diamond ambaye alikwenda pale kurekodi, yeye Kiba alikuwa Coke Studio.

Baada ya hapo ulishakutana tena na Kiba?

Ndiyo, akaniomba msamaha akasema yeye aliwatumia waiposti na hayo maneno waliweka wao.

Unamuonaje Kiba kimuziki?

Siwezi kusema anakosea wapi, maana kila msanii ana njia zake. Wimbo wake wa Mwana ni mkali na ulifanya vizuri yawezekana anakosea kwenye ‘market’. Kuna vitu lazima ulazimishe, hata Diamond yupo juu lakini hawezi kutoa kitu halafu akatulia tu akaacha watu wapende wenyewe.

Kila mtu ana staili yake yawezekana yeye hataki kwenda kwenye staili kama hiyo, ndiyo maana kuna muda huwa nasema huwezi kumfananisha Diamond na Ali kwa sababu wanaimba muziki wa tofauti.

Wote ni Bongo Fleva lakini staili zao ni tofauti, kwa mtu anayefuatilia muziki anaweza kugundua hilo.

Ishu ya bifu la Diamond na Kiba ikoje?

Hakuna bifu kabisa, mimi nafahamu hilo. Wameshakutana na kusalimiana na hakuna chochote. Nasema kabisa wanapiga stori na wanaongea ‘fresh’ kabisa.

Mbona kama kuna picha ya kukwepana?

Kinachotokea ni kwamba watu wanawauliza kama wana bifu kwa hiyo wenyewe wanasema hawana bifu basi, lakini kwa kuwa hakuna maelezo mengi watu wanachukulia hivyo.

Ilidaiwa uongozi wa Diamond unafanya fitna ya kuzuia video za Kiba zisipigwe katika vituo vikubwa vya nje kama MTV na Trace, ni kweli?

Siyo kweli. Kiba na ana nguvu kubwa MTV na Trace kuliko Diamond kwa ajili ya Seven (ni mmoja wa wasimamizi wa Ali Kiba).

Seven alikuwa mfanyakazi wa MTV, anawajua watu wote wa MTV, hata yule bosi wa Trace wa sasa alikuwa chini ya Seven, ndiyo maana hata video yake ya Chekecha Cheketua ilichezwa wiki nzima mfululizo ikiwa ni ‘Exclusive’.

Wenzetu katika vituo wanaangalia vigezo vyao. Nikupe siri kuwa wakati naanza kazi na Diamond, alikuwa anabaniwa kweli zisipigwe kabisa hata Channel O.

Nani alikuwa anambania Dimond?

Siwezi kutaja jina lakini nyimbo zilikuwa zinapelekwa DStv hapo lakini anaambiwa hazina viwango, zinarudi. Aliyekuwa anafanya hivi ni Mtanzania na ni mhusika mkubwa wa muziki wa Tanzania.

Nini kilitokea baada ya kugundua hilo?

Nilimfuata nikamchana ‘live’ baadaye tukaamua kazi zetu kuzipitishia Nigeria kisha tukarudi hapa na kila kitu kikawa rahisi. Niwashauri watu kuwa wafanye kazi na watangaze kazi zao dunia ya sasa hakuna kitu kinachoenda chenyewe tu.

Skendo za Diamond huwa zinaathari kwenu?

Hatuathiriki, tunajua watu wanatafuta ‘booster’ kisha wanashindwa kuitumia.

Kwa nini Bongo Fleva imechelewa kutoka kimataifa?

Watu wanapenda vya bure, ‘nisaidie’ zilikuwa nyingi, wenzetu wanatoa fedha ili waingize fedha.

Suala la kwenda nje kutengeneza video limekuwa likizungumzwa sana, unalizungumziaje hilo?

Hapa kwetu vibali ni tatizo, mfano gari za polisi, kupata benki au kituo cha polisi, bado jamii yenyewe haijaona kama muziki ni biashara kubwa. Wenzetu kule mtu anakuachia nyumba ya thamani ya mamilioni, lakini hapa huwezi kuikuta na kama ipo tayari ishatumika mara 30, hakuna kitu kipya. Serikali ilegeze kidogo na kuwe na upatikanaji wa vibali kwa njia rahisi.

Una familia?
Nina mke na mtoto mmoja wa kiume, anaitwa Dayan.

Asante kwa ushirikiano wako.
Asante na wewe, karibu tenasiku nyingine.

Chanzi: Championi

Kosa la Kutukana Kwa Kutumia Mtandao ndio Chanzo cha Siwema wa Nay wa Mitego Kutupwa Jela Miaka Miwili

$
0
0
Mahakama kuu ya mkoani Mwanza imemuhukumu Siwema ambaye ni mzazi mwenzake na Nay Wamitego miaka miwili jela kwa kesi ya kumtukana mtu kwa njia ya mtandao.

Siwema alituhumiwa kumtukana matusi kwa njia ya mtandao mlalamikaji ambaye anafahamika kwa jina la Deo.

Akizunguza na kipindi cha Jahazi, kinachoruka kupitia Clouds FM, Nay Wamitego alisema ‘napambana kile nitakachoweza kuangalia kama kunauwezekano wa kumpa msaada’.

“Kuna vitu nafikiria kuvifanya ili kujaribu kumsaidia, baada ya kupata hizi taarifa kidogo kama siko sawa hivi. Ni mzazi mwenzangu mimi nay eye tulikaa muda mrefu, napambana kile nitakachoweza kuangalia kama kunauwezekano wa kumpa msaada mwingine kwa njia yeyote ili asiwe kwenye mazingira ambayo tayari ameshawekwa. Anayemshtaki najua anaitwa Deo, jina jingine silifaham,” aliongezea.

Nay na Siwema walifanikiwa kukaa kwenye mahusiano kwa kipindi kirefu na kufanikiwa kupata motto mmoja, Curtis kabla hawajachana na kila mtu kushika njia yake.

Imani za Kishirikina Mkoani Geita, Watu Wawili Wauawa Kwa Kukatwa Mapanga

$
0
0
Watu wawili wameuwa kwa kukatwa mapanga sehemu mbalimabli za miili yao mkoani Geita akiwemo muuguzi wa Zahaati ya kagu kwa kile kinachodaiwa kuwa imani za kishirikina.

Tukio la kwanza limetokea juzi majira ya saa moja jioni ambapo Helena Paulo 56 mkazi wa kijiji cha Luhuma alikatwa mapanga wakati akiwa njiani kuelekea nyumbani kwake huku Elizabeti Masango 54 ambaye ni muuguzi wa Zahanati naye alikatwa mapanga akiwa nyumbani kwake.

Wakizungumza na Channel Ten baadhi ya mashuhuda wa matukio hayo wamesema vitendo vya uhalifu wa kukatwa mapanga akinamama vinaongezeka mkoani Geita, jambo linalowafanya kuishi kwa mashaka.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Geita Ali Kidwaka aliyekwenda kutoa pole kijijini Kagu amewataka wananchi kuwafichua watu wanaofanya unyama huo huku mwenyekiti wa kijiji hicho Tanga Daudi amessitiza ulinzi mkubwa wa jadi umeimarishwa kila kona.

Kamanda wa Polisi Mkoani Geita Mponjoli Mwabulambo amesema mtu mmoja anashikiliwa kwa mahojiano kufuatia matukio hayo.

TAZAMA Hapa Video Mpya ya Mwanamuziki Lady Jay Dee-Ndindindi

$
0
0

TAZAMA Hapa Chini Video Mpya ya Mwanamuziki Lady Jay Dee-Ndindindi, Video imefanyika South Africa kwa Director Justin Compus:

Rooney Ndiye Mwanamichezo Tajiri Kwa Uingereza, Wengine ni ..

$
0
0
Gazeti La Sunday Times limemtangaza Wayne Rooney kama mwana michezo tajiri nchini Uingereza.

Rooney ambaye ni mchezaji wa timu ya Manchester United na timu ya taifa ya Uingereza, ndiye mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa kwenye ligi ya uingereza akipokea paundi 300,000 kwa wiki.

Rooney ameingia kwenye list hiyo baada ya kuwa na utajiri wa paundi milioni 82 na kuwazidi wanamichezo wengine wan chi hiyo Andy Murry mwenye utajiri wa paundi milioni 58 na Rory McIlroy mwenye utajiri wa paundi milioni 56.

Rooney amefanikiwa kuongeza paundi million kumi kwa mwaka huu kwenye utajiri wake kutokana na kuwa balozi wa Nike na Samsung.

Hii ni list ya top ten ya wanamichezo matajiri wa Uingereza:

1.Wayne RooneyFootball, Manchester United£82m

2 .Andy Murray Tennis £58m

3.Rory McIlroy Golf £56m

4.Gareth Bale Football, Real Madrid £34m

5.Sergio Aguero Football, Manchester City £33m

6.David Silva Football, Manchester City £31m

7.Cesc Fabregas Football, Chelsea £29m

7.Radamel Falcao Football, Chelsea £29m

9.Samir Nasri Football, Manchester City £22m

10.Eden Hazard Football, Chelsea £18m

11.Amir Khan Boxing £18m

Wasomi Wahoji Ububu wa UKAWA Bungeni....

$
0
0
UAMUZI wa Kambi ya Upinzani bungeni kuingia katika vikao vya Bunge na kugeuka bubu wakati wa mjadala wa Hotuba ya Ofisi ya Waziri Mkuu, umechukuliwa kwa hadhari kuwa unaweza kusababisha kambi hiyo ionekane inalinda posho bungeni.

Hadhari hiyo imetolewa na wasomi na viongozi mbalimbali waliozungumza na gazeti hili jana, walipokuwa wakitoa maoni kuhusu uamuzi wa kambi hiyo kususa hotuba hiyo.

Dk Bana

Mhadhiri wa fani ya siasa na utawala katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Benson Bana, ndiye aliyesema kuwa kama uamuzi huo wa kuwa bubu bungeni hautabadilishwa, kambi hiyo itaonekana inalinda posho na kwamba haipo kwa ajili ya kutetea wananchi.

“Kazi yao ni kuwakilisha wananchi na makundi yote bungeni, sasa kitendo cha kuota ububu na kushindwa kueleza kero za wananchi, ni kutotendea haki wananchi maana ni vema wakae bungeni na kutoa hoja zao la sivyo, itafika wakati watatuomba radhi wananchi,” alisisitiza.

Akizungumzia hoja ya kwanza ya Mwenyekiti wa kambi hiyo, Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe (Chadema), kulalamikia muundo wa Serikali kutowekwa gazetini, Dk Bana alihoji kama Mbowe hajui kuwa muundo wa Serikali hautolewi kwa kila mtu.

Kuhusu suala la fedha zilizokatwa katika Mfuko wa Bunge na kuelekezwa katika utengenezaji wa madawati, Dk Bana aliwashangaa wawakilishi hao wa wananchi wanaopingana na uamuzi wa kumuinua mwananchi wa kawaida.

Alisema wananchi wote walipendezwa na hatua hiyo ya Serikali ya kuchukua fedha zilizotoka bungeni baada ya kubana matumizi na kupeleka katika kununua madawati.

“Hatua hii ni kielelezo kuwa Bunge lilikuwa likipangiwa fedha nyingi kuliko matumizi yake hivyo kusababisha kuwepo matumizi ya hovyo, sasa viongozi wa Bunge kuliona hilo na kurejeshwa kwenye jamii ni jambo jema,” alisema.

Alionya kuwa mikakati ya kambi ya upinzani, ni kutetea wananchi lakini kwenye hilo wananchi wenyewe kila kona wanawashangaa kwani inaonesha kutetea maslahi ya wabunge.

Bashiru Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Bashiru Ally alisema wananchi wanaangalia vitendo vya wabunge wao ndani ya Bunge na watawahukumu kwani michango yao ndani ya Bunge ni muhimu na njia ya kutatua tatizo si kususa, bali kufuata taratibu za kisheria.

Alisema uamuzi wa kutozungumza, unaondoa maana ya vyama vya upinzani ndani ya Bunge kwa kuwa watashindwa kujadili masuala yenye manufaa ya wananchi, kwani mawazo ya kiongozi wa upinzani bungeni ni muhimu na yanawekwa kwenye kumbukumbu.

“Kuwekwa kwenye kumbukumbu mawazo hayo ni kwa ajili ya vizazi vijavyo, sasa kitendo cha Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni kutumia vibaya nafasi anayopewa, ni udhaifu wa kimkakati,” alisisitiza Bashiru.

Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, alisema wanavyofanya wapinzani ni jambo lisilopendeza katika kuleta umoja wa kitaifa, kwani wao ni wawakilishi wa wananchi ndani ya Bunge na kususa siyo jambo la kiungwana.

Kilimanjaro: Watumishi HEWA Wakopa Mamilioni ya Pesa Benki

$
0
0
Msako ulioanzishwa na Rais John Magufuli wa kutokomeza tatizo la wafanyakazi hewa katika utumishi wa umma, umeendelea kuibua mazito, ambapo mkoani Kilimanjaro, Benki ya CRDB imejikuta ikitoa mkopo kwa waliokuwa wafanyakazi hewa.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai, Helga Mchomvu aliyasema hayo akidai kuwa, yamegundulika baada ya Serikali kuunda kamati za uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu wa zaidi ya Sh milioni 500 katika halmashauri hiyo.

Kabla ya kuibuka kwa kisa hicho kinachoonesha namna wafanyakazi hewa alivyokuwa wakiibia nchi, hivi karibuni mkoani Singida, Mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Imani Nyamangaro, alipandishwa kizimbani akidaiwa kujilipa mishahara ya wastaafu 57, yenye thamani ya Sh milioni 29.4.

Mbali na mhasibu huyo, Rais Magufuli alipokuwa mapumziko kijijini kwake Mlimani, katika Wilaya ya Chato mkoani Geita, alieleza kisa kingine kilichoshitua jamii kuwa katika Mamlaka ya Mapato (TRA), kulikuwa na mtumishi mmoja ambaye alikuwa akilipwa mishahara ya watu 17.

Benki ya CRDB Hai
Akizungumza jana, Mchomvu alidai kuwa watumishi watatu wa halmashauri hiyo; wawili wa Idara ya Utumishi na mmoja Mchumi, walikopa katika Benki ya CRDB Sh milioni 35.2, kwa kutumia majina ya wafanyakazi hewa.

Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Mkuu Idara ya Utumishi na Utawala, Gudila Mashele, Ofisa Utumishi Daraja la Kwanza, Faraja Ndatu na Mchumi Daraja la Pili, Isaiah Bayege.

Kutokana na tuhuma hiyo iliyoibuliwa na kamati hizo za uchunguzi, Mchomvu alisema Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Hai, limewafukuza kazi watumishi hao.

Mbali na tuhuma ya kujipatia mkopo kwa kutumia majina ya wafanyakazi hewa, Mchomvu alisema kuna watumishi wengine wamefukuzwa kazi kwa tuhuma za wizi wa fedha za muda wa kazi wa ziada wa madaktari na wauguzi katika Hospitali ya Machame wilayani hapa, huku mwingine akifukuzwa kwa kununua dawa hewa za hospitali hiyo.

Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Mhasibu Daraja la Kwanza, Edwin Kalokola na Mhasibu Msaidizi, Valentina Elisha, wanaodaiwa kuiba Sh milioni 24.4 za muda wa kazi wa ziada wa madaktari na wauguzi katika hospitali hiyo.

Mbali na wahasibu hao, yupo pia dereva Derick Urassa, aliyefukuzwa kwa tuhuma za kushiriki katika ununuzi wa dawa hewa katika hospitali hiyo zenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 32.7.

Walioshushwa cheo 
Alisema wapo pia watumishi walioshushwa vyeo kutokana na tuhuma mbalimbali, ikiwemo kughushi nyaraka na kuidhinisha malipo bila idhini ya mwajiri.

Miongoni mwao ni pamoja na Ofisa Muuguzi Msaidizi Daraja la Kwanza, Agness Chami na Katibu wa Afya Daraja la Kwanza, Gilbert Mashamba.

Wengine ni wahasibu waandamizi wawili, Kasisim Herpa na John Bogohe na Mhasibu Daraja la Kwanza, Christopher Manzi, ambao wanatuhumiwa kuidhinisha malipo mbalimbali ya Sh milioni 488.2, bila kuwa na idhini kinyume na taratibu za kazi.

Walivyobambwa
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Saidi Mderu alisema tuhuma hizo ziligunduliwa na Mkaguzi wa Ndani wa halmashauri hiyo, Michael Mosha na kufanyiwa kazi na tume hizo zilizoongozwa na Katibu Tawala Msaidizi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Kilimanjaro, Grace Makiluli.

Baada ya kubainika kwa tuhuma hizo, Mderu alisema baraza hilo lilimpongeza mkaguzi huyo kwa kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa kwa kuwa angeweza kudanganyika kutumia fedha hizo.

Mkuu wa Wilaya ya Hai, Gelasius Byakanwa, amepongeza baraza hilo kwa hatua hizo na kueleza kuwa kazi kubwa ya madiwani ni kusimamia mali na rasilimali za Serikali, ili wananchi wapate huduma bora za Serikali yao ya Awamu ya Tano ambayo ina dhamira ya kuwahudumia.

Mchezaji wa Azam Farid Mussa Awasili Madrid, Hispania Kwa Majaribio

$
0
0

Winga wa Azam FC, Farid Mussa amewasili nchini Hispania kwa ajili ya kufanya majaribio ya kucheza soka ya kulipwa katika klabu za La Liga.

Akizungumza kutoka Madrid, Hispania, Farid amesema leo ndiyo atajua ratiba nzima ya mazoezi.
Farid atakuwa nchini humo kwa muda wa mwezi mmoja akifanya majaribio klabu za Union Deportiva Las Palmas, maarufu kama Las Palmas yenye maskani yake Las Palmas de Gran Canaria na Athletic ya Bilbao.

Farid amewasili Hispania akitoka kuichezea klabu yake, Azam FC katika mchezo wa marudiano hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji, Esperance walioshinda 3-0 mjini Tunis Jumanne

TIMU ya Mbao FC Kutoka Mwanza yatangazwa Kupanda Ligi Kuu Msimu Ujao

$
0
0
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeitangaza klabu ya Mbao FC ya jijini Mwanza kupanda Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu ujao kutoka katika kundi C ya Ligi Daraja la Kwanza chini (StarTimes League).

TFF imeitangaza Mbao FC kufuatia maamuzi ya Kamati ya Nidhamu ya TFF yaliyotolewa April, 2016 ya kuzishusha daraja timu nne kutoka kundi C baada ya kukutwa na hatia ya upangaji matokeo.
Mbao FC imeshika nafasi ya kwanza kundi C kwa kuwa na pointi 12 baada ya kufutwa kwa matokeo ya timu za Geita Gold, Polisi Tabora, JKT Oljoro na JKT Kanembwa zilizokumbwa na mkasa huo wa upangaji matokeo.

Timu ya Mbao FC inapanda ligi kuu (VPL) msimu ujao, sambamba na timu za African Lyon ya jijini Dar es salaam pamoja na Ruvu Shooting ya mkoa wa Pwani.

Wakati huo huo kikao cha Kamati ya Rufaa ya Nidhamu ya TFF kinatarajiwa kukaa Jumamosi ijayo April, 30 jijini Dar es salaam kujadili rufaa mbalimbali ambazo zimekatwa na kutokana na maamuzi ya kamati ya Nidhamu ya TFF.

Kamati ya Rufaa ya Nidhamu ya TFF itasikiliza rufaa za wafuatao waliokata rufaa
(i) Saleh Mang’ola,
(ii) Yusuph Kitumbo,
(iii) Amos Mwita,
(iv) Fateh Remtullah,
(v) Timu ya JKT Oljoro,
(vi) Timu ya Polisi Tabora.
Aidha Kamati ya Nidhamu ya TFF itakutana Jumapili Mei Mosi kupitia taarifa mbalimbali zilizowasiliswa katika kamati hiyo.

Kalapina Anafahamu Vingi Kuhusu Matibabu ya Chid Benz...Kayaongea haya…

$
0
0
Kama unakumbuka March 22, 2016 meneja wa Diamond Platnumz, Babu Tale alimpeleka rapper Chid Benz Sober House iliyopo Bagamoyo iitwayo Life and Hope Rehabilitation Centre kwaajili ya kupata matibabu ya kuacha kutumia madawa ya kulevya na kurudi kwenye hali yake ya mwanzo.

Sasa hapa Ayo TV  imempata msanii wa Hip Hop, Kalapina ambaye hivi karibuni alikwenda Sober House ilipo Bagamoyo kumjulia hali Chid Benz..

‘Chid benz sasa hivi anaendelea vizuri ni tofauti na vile mwanzo alivyokuwa, inategemea na mtu alivyoathirika atakaa siku ngapi mtu anaweza anakaa miezi sita au miezi saba Chid Benz ana siku 29 inategemea pia na dawa gani anazopewa ili mwili urudi kama zamani’– Kalapina

Itazame hii video hapa Kalapina amezungumza mengi kuhusu matibabu ya Chid Benz


Serikali Yapangua Hoja Moja ya UKAWA

$
0
0

SIKU moja baada ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kususa kuchangia hotuba za bajeti, Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Florence Mwanri, amesema serikali haikukosea kuipa Wizara ya Ujenzi fedha zaidi ya zilizokuwa zimeidhinishwa na Bunge.


Hoja hiyo ni moja kati ya tatu ambazo juzi ziliibuliwa bungeni na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe.


Badala ya kuwasilisha Mpango Mbadala wa Maendeleo wa Taifa na maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani kuhusu mpango wa serikali pamoja na maoni ya kambi hiyo kuhusu hotuba ya Waziri Mkuu, juzi Mbowe alisema wabunge wa upinzani watakuwa wanaingia kwenye Ukumbi wa Bunge lakini hawatachangia hotuba ya bajeti mpaka pale hoja zao zitakapojibiwa.


Mbowe alidai kuwa uamuzi wao huo umetokana na Serikali kufanya kazi bila kuwa na mwongozo wa utendaji kazi kwa wizara mbalimbali, kuvunjwa kwa Katiba na sheria za nchi na kupokwa uhuru na madaraka ya muhimili wa Bunge.


Mwenyekiti huyo wa Chadema na Mbunge wa Hai, alikwenda mbali zaidi akieleza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imekiuka sheria kwa kuipatia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Sh. bilioni 607.4 ikiwa ni fedha za ndani kwa ajili ya bajeti ya maendeleo ya mwaka wa fedha 2015/16 wakati Bunge liliidhinisha Sh. bilioni 191.6.


Wakati Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge, aliyeongoza kikao cha juzi akieleza kuwa madai ya upinzani ni mazito na kushauri waende mahakamani, Serikali imejibu moja ya hoja tatu za Mbowe.


Akiongea na waandishi wa habari  katika  jengo la Wizara ya Fedha na Mipango  jana asubuhi, Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Mwanri, alisema Serikali ya Awamu ya Tano haijafanya makosa kuipa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kiasi hicho cha fedha.


Ofisa huyo wa serikali alisema Sheria ya Bajeti ya Mwaka 2015 inaruhusu Ofisa Masuhuli na Waziri kufanya uhamisho wa fedha za mradi mmoja kwenda kutekeleza mradi mwingine.


"Sheria ya Bajeti ya Mwaka 2015 inaruhusu Ofisa Masuhuli kufanya 'reallocation' (uhamisho) ya matumizi ya fedha lakini isizidi asilimia saba ya 'Vote' (Fungu) husika," alisema na kuongeza:


"Sheria hiyo pia inamruhusu Waziri kufanya 'reallocation' ya matumizi ya bajeti husika lakini haipaswi kuzidi asilimia 10. Pesa ilizopewa Wizara ya Ujenzi zimezingatia sheria na fungu walilopewa limo ndani ya sheria."


Florence alisema wizara hiyo ina madeni makubwa ya wakandarasi, hivyo kutoyalipa ni kuendelea kukuza mzigo kwa serikali kwa kuwa riba inaongezeka.


"Serikali iliamua kutoa kiasi hicho cha fedha (Sh. bilioni 607.4) ili kuyapunguza madeni ya Wizara ya Ujenzi. Tukumbuke kuwa wizara hii, ndiyo yenye madeni makubwa," alifafanua zaidi ofisa huyo wa serikali.


Katika maelezo yake ya msingi aliyoyawasilisha bungeni juzi, Mbowe alisema kuwa kwa kuipa wizara hiyo kiasi hicho cha fedha badala ya Sh. bilioni 191.6 zilizoidhinshwa na Bunge, Serikali ya Awamu ya Tano imevunja kifungu cha 41(1) cha Sheria ya Bajeti ya Mwaka 2015.


Kwa mujibu wa Katiba hiyo, kifungu hicho kinasema: “Serikali itawasilisha bungeni kwa idhini, bajeti ya nyongeza ya fedha zilizotumika ambazo zimezidi kiwango kilichoidhinishwa na Bunge au kwa madhumuni ya kugharamia mahitaji ambayo hayakupangwa”.


Mbowe alisema utaratibu huo pia unatiliwa nguvu na Sheria ya Fedha za Umma wa mwaka 2001 (Public Finacne Act, 2001) ambayo kifungu cha 18 (3) na (4) inaitaka serikali kupeleka bungeni bajeti ya nyongeza (mini-budget) kwa ajili ya kupata idhini ya Bunge ikiwa fedha zilizoidhinishwa awali hazikutosha

Kigogo wa TRA Aliyekuwa akijilipa Mishahara 17 Hewa Afukuzwa Kazi

$
0
0

Mfayakazi wa Mamlaka ya Mapato Nchini aliyetuhumiwa na Rais John Magufuli mwezi uliopita kujilipa mishahara 17 ya watumishi hewa, hayupo kwenye ajira ya TRA kwa siku nyingi zilizopita, imefahamika.

Habari kutoka ndani ya Mamlaka hiyo zimesema kuwa mfanyakazi huyo alikuwa ni wa Idara ya Uhasibu ya TRA lakini alishafukuzwa kazi siku nyingi zilizopita.

Chanzo cha kuaminika kutoka Makao Makuu ya TRA kimeiambia Nipashe kuwa mfanyakazi huyo alifukuzwa kazi baada ya kubainika kujilipa mishahara hiyo katika akaunti yake.

Chanzo chetu cha habari ambacho hakikupenda kutajwa jina  kwa sababu si msemaji wa mamlaka, kilisema mfanyakazi huyo baada ya kuhojiwa alikiri kujilipa mishahara hiyo.

“Huyu mfanyakazi alikuwa Idara ya Uhasibu… ni kweli alijilipa mishahara hiyo na baada ya kuhojiwa alikiri ndipo tukamfukuza kazi na kumpeleka mahakamani,” chanzo hicho kilieleza.

Rais Magufuli alimfichua mfanyakazi huyo hivi karibuni akiwa nyumbani kwake katika Kijiji cha Mlimani, Wilaya ya Chato mkoani Geita, alipokuwa alihutubia kwa mara ya kwanza tangu achaguliwe kuwa Rais Oktoba 25, mwaka jana.

Hizi Hapa Shida Zinazo Wapata Wanawake Wenye Makalio Makubwa Kwenye Mapenzi

$
0
0

Mara nyingi wanaume wengi hupenda ama kuvutiwa na wanawake wenye makalio makubwa. kwa sasa mwanamke mwenye makalio makubwa yaliyojazia sawasawa huonekana anasoko kuliko wale wenye makalio ya wastani, Lakini mara nyingi hawadumu kwenye mahusiano kwani Wanaume wengi ambao hawana mapenzi ya kweli huwa wanataka kuonja tu na mara nyingi wanakuta kile ambacho hakutegemea hivyo kukimbia...na kumwacha mwanamke anaumia....Takwimu zinaonyesha wanawake wanene wanaongoza kuumizwa na wenza wao kulilo vipotaable...

Watu wengi huzimika na wanawake wenye makalio makubwa lakini ukweli ipo tofauti kubwa kati ya wenye makalio madogo na makubwa kwani wanawake hawa wamekuwa na kero kadhaa ambazo ni sugu na zifuatazo ni kero  kuu tatu.


1.Mwanaume huwa hapati mwanya au nafasi nzuri wakati wa tendo hushindwa kupata ladha inayotarajiwa, kwani mara nyingi ukubwa wa makalio huzuia uume kusakua uke kisawasawa hivyo badala ya kupata burudani unakesha ukihangaika kupekenyua  makalio na kujikuta wamefikia mshindo bila kufaidi tendo.

2.Wanawake wenye mzigo mkubwa wa makalio huwa wazito na hivyo hushindwa kubadili manjonjo wakati wa tendo la ndoa. Hii hupelekea wawili hawa kutumia ‘staili’ moja almaarufu kama kifo cha mende wakati zipo staili nyingi na tamu kupita maelezo ambazo wanawake wengi wenye mafurushi ya makalio hawawezi kukaa.

3.Asilimia kubwa ya wanawake wenye makalio makubwa wamekuwa wavivu katika uzungushaji wa kiuno na mautundu mengine ya kitandani ambayo yanahitaji mdada mwepesi ili aweze kumrusharusha mwanaume huku na kule jambo linalomfanya mwanaume kupagawa wakati wa kufanya mapenzi.

Kumridhisha mwanamke mwenye makalio makubwa inahitaji ufundi mithili ya mtu anayewinda digidigi, hivyo sio kila mwanamke mwenye bambataa anauwezo na mbinu za kumridhisha mwanaume hivyo ni vyema ikatambulika wazi asilimia kubwa husifika kwa kushindwa kujifanyia usafi wa miili yao na wakati mwingine kutoa harufu mbaya.

Sad News: Mwanamuziki Nguli wa Congo Papa Wemba Afariki Dunia

$
0
0
Mwanamuziki nguli wa Congo Jules Shungu Wembadio Pene Kikumba maarufu kama Papa Wemba amefariki dunia huko Abidjan, Ivory Coast, usiku wa kuamkia leo.

Habari zilizotufikia hivi punde zinasema marehemu Papa Wemba amefia hospitali alikokimbizwa mara baada ya kuanguka na kupoteza fahamu wakati akiwa katika onesho jukwaani.

Papa Wemba alizaliwa June 14, 1949 huko Lubefu katika wilaya ya Sankuru nchini Congo. Alijipatia umaarufu sana kwa sauti nyororo na midundo ya Soukous ulimwenguni kote, ikiwamo Tanzania ambako amezuru mara kadhaa na kujizolea mashabiki wengi

Maalim Seif Aendelea Kummwagia Lawama Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Kwa Kupindua Matokeo ya Uchaguzi Mkuu Zanzibar

$
0
0
Katibu Mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamad ameendelea kumtupia lawama Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete akidai kuwa alitumia dola ‘kupindua’ demokrasia ili kuinusuru CCM iliyokuwa imebwagwa kwenye Uchaguzi Mkuu uliopita.

Alisema Kikwete ambaye wakati huo alikuwa Amiri Jeshi Mkuu, anastahili lawama kwa madai kuwa alituma vyombo vya dola kugeuza uamuzi wa Wazanzibari waliokuwa wameufanya kupitia masanduku ya kura Oktoba 25 mwaka jana.

Maalim Seif aliyasema hayo jana pale wananchi walipomtaka kutoa neno la kuwasalimu alipopita katika Msikiti wa Ijumaa wa Masjid Swahaba, Mtoni Garagara, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja.

“Kilichofanyika si kitendo cha kiungwana hata kidogo, ni uhuni wa hali ya juu uliopangwa kwa makusudi na watu wasioitakia mema Zanzibar na hivyo wakaamua kutoheshimu haki na uamuzi halali wa wananchi,” alisema.

Maalim Seif alisema nchi ni mali ya wananchi ambao siku zote watabaki kuwa sehemu muhimu ya uamuzi wa nani awaongoze.

Katibu mkuu huyo ambaye alikuwa mgombea wa urais wa Zanzibar katika uchaguzi huo, alisema watawala wanapaswa kutambua wananchi ndiyo huamua watu wanaowataka na siyo mabavu ya kulazimisha kwa kutumia dola au majeshi.

Hata hivyo, Maalim Seif alisema anaelewa hali ilivyo katika jamii na pia katika mioyo za Wazanzibari ambao uamuzi wao ulipinduliwa.

Maalim Seif aliyedai kushinda nafasi hiyo, aliwataka Wazanzibari kuendelea kuwa watulivu wakielewa kuwa wao ndiyo washindi na ushindi hautapotea.

Mwanasiasa huyo alisema juhudi zinaendelea kuhakikisha haki ya uamuzi wao kupitia masanduku ya kura inapatikana.

Wananchi walioibuka kwa wingi katika eneo hilo baada ya kubaini sauti iliyokuwa ikizungumza kwenye kipaza sauti ni ya Maalim Seif, walielezea kufurahishwa na kiongozi huyo.

“Tumejisikia furaha angalau kusikia sauti ya simba wa nyika, Maalim Seif akinguruma,” alisema mkazi wa Mtoni Kidatu, Bura Juma.

Slim Said alisema: “Unajua Maalim ni kipenzi cha watu, sasa ukimsikia tu unaondoka na hisia za matumaini.”

Msafara huo wa Maalim usiokuwa na king’ora kama ilivyozoeleka ulionekana ukiingia taratibu, hali ambayo haikuamsha shangwe mwanzoni kabla ya watu kupashana habari na hatimaye kujaa mahali alipokuwa.

Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana ulitawaliwa na mvutano wa kisiasa visiwani Zanzibar baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha kufuta matokeo akidai kuwa sheria na taratibu zilivunjwa. Kutokana na hatua hiyo, baadaye Jecha alitangaza uchaguzi wa marudio Machi 20 mwaka huu ambao uligomewa na vyama 10 kati ya 14 vilivyoshiriki uchaguzi wa awali.

Katika uchaguzi wa marudio, Dk Ali Mohamed Shein alishinda kwa asilimia 91.4.

Watumishi Hewa: Kompyuta yenye Rekodi Yaibwa, Wakopa Benki Kwa Majina Hewa

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella ametoa saa 24 kwa kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Ukerewe, Ally Mkaripa, kuhakikisha wanaitafuta hadi kuipata komputa iliyoibwa usiku wa kuamkia April 22, 2016 kwenye chumba kinachotumika na mifumo ya ukusanyaji mapato na uandaaji wa malipo ya Halmashauri (EPICOR)

Mhe. Mongella ametoa agizo hilo wakati akizungumza kwenye kikao cha kujitambulisha kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ambapo taarifa za awali zilionesha kutokea kwa wizi wa komputa moja iliyofungwa kwenye chumba cha mifumo ya komputa ambayo ndio hutumika kuandaa malipo mbali mbali ya halmashauri.

“OCD kesho nitakwenda kanisani asubuhi, ikifika saa 8.00 mchana nataka taarifa niikute mezani kwangu, vinginevyo hatutaelewana", amesema Mongella na kuongeza sisi tunajua nini chakufanya kama kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa lakini na wewe tumia mbinu zako kuweza kubaini wapi ilipo kompyuta hiyo.

Akizungumza kando ya Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri, Kaimu Mhazini wa Halmashauri hiyo, Baraka Munuo alidai kupokea taarifa za kupotea kwa Komputa hiyo kutoka kwa afisa TEHAMA wa halmashauri ya Ukerewe.

Katika hatua nyingine mkuu wa mkoa wa Mwanza, amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe kupitia mafaili na kubaini watumishi waliofanya kazi katika kituo hicho kwa muda mrefu, jambo ambalo Mkuu wa Mkoa amedai linachangia watumishi kufanyakazi kwa mazoea.

”Mkurugenzi nakuagiza pitia mafaili ya watumishi ili kubaini wote waliokaa katika kituo hiki kwa muda mrefu. Haiwezekani mtu amekaa hapa miaka ishirini na moja halafu uniambie kwamba atakuwa na maarifa mapya, hapana" alisema Mongella na kuongeza, Sasa nakuagiza pitia mafaili yao na kama kuna mtumishi aliye kaa kwa zaidi ya miaka kumi atafutiwe kituo kingine.

Wakati huo huo, MSAKO ulioanzishwa na Rais John Magufuli wa kutokomeza tatizo la wafanyakazi hewa katika utumishi wa umma, umeendelea kuibua mazito, ambapo mkoani Kilimanjaro, Benki ya CRDB imejikuta ikitoa mkopo kwa waliokuwa wafanyakazi hewa.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai, Helga Mchomvu aliyasema hayo akidai kuwa, yamegundulika baada ya Serikali kuunda kamati za uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu wa zaidi ya Sh milioni 500 katika halmashauri hiyo.

Kabla ya kuibuka kwa kisa hicho kinachoonesha namna wafanyakazi hewa alivyokuwa wakiibia nchi, hivi karibuni mkoani Singida, Mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Imani Nyamangaro, alipandishwa kizimbani akidaiwa kujilipa mishahara ya wastaafu 57, yenye thamani ya Sh milioni 29.4.

Mbali na mhasibu huyo, Rais Magufuli alipokuwa mapumziko kijijini kwake Mlimani, katika Wilaya ya Chato mkoani Geita, alieleza kisa kingine kilichoshitua jamii kuwa katika Mamlaka ya Mapato (TRA), kulikuwa na mtumishi mmoja ambaye alikuwa akilipwa mishahara ya watu 17.

Akizungumza jana, Mchomvu alidai kuwa watumishi watatu wa halmashauri hiyo; wawili wa Idara ya Utumishi na mmoja Mchumi, walikopa katika Benki ya CRDB Sh milioni 35.2, kwa kutumia majina ya wafanyakazi hewa.

Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Mkuu Idara ya Utumishi na Utawala, Gudila Mashele, Ofisa Utumishi Daraja la Kwanza, Faraja Ndatu na Mchumi Daraja la Pili, Isaiah Bayege. Kutokana na tuhuma hiyo iliyoibuliwa na kamati hizo za uchunguzi, Mchomvu alisema Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Hai, limewafukuza kazi watumishi hao.
CHANZO: Habarileo

Kwa Makomredi Hawa Museveni Asingeitosa Tanzania Hata Siku Moja Kwenye Bomba la Mafuta....

$
0
0
Nimekuwa nikilifuatilia kwa umakini mkubwa sana hili suala la wapi Bomba la Mafuta lipite huku Ndugu zetu Wakenya WAKIJITUTUMUA kama kawaida yao kutaka KUMILIKI kila kitu hapa Afrika ya Mashariki kana kwamba Mwenyezi Mungu aliwabariki wao tu wakati si kweli.

Rais wa Kenya Kenyatta pamoja na team wake wamejitahidi na kwa taarifa nilizonazo zinasema kuwa mpaka jana Jumamosi bado Kenya ilikuwa inaendelea na lobbying kwa Rais wa Uganda Mzee Museveni ili apitishe Bomba hilo kwao na Tanzania tuambulie patupu.

Ila Wakenya na hasa Rais wao Uhuru Kenyatta wamesahau historia ya KUTUKUKA ya Rais Yoweri Kaguta Museveni na nchi yetu hii ya Tanzania. Hakuna ubishi kuwa Rais wa Uganda Mzee Museveni bila jitihada za Tanzania leo hii asingekuwa hapo alipo.

Ukianzia zile harakari zake za kuiokomboa nchi ya Uganda akiwa anatokea huku huku Tanzania na wakati huo huo makazi ya familia yake hasa mkewe Janet na Watoto wao wawili wa kwanza wa Kiume Muhoozi Kainerugaba na Natasha Nankuunda ambao waliishi vizuri sana pale Upanga mkabala kabisa na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili huku.

Baada ya Mzee Museveni kumaliza masomo yake UDSM alianza kazi ya kufundisha Chuoni huko Mkoani Kilimanjaro lakini hapo hapo tena akiendeleza harakati zake za kupambana vita ya msituni kuuondoa Uongozi wa Milton Obote akishirikiana na wenzie kama Jemedari Serwanga Lwanga ( R.I.P ), mdogo wake Caleb Akandwabaho ( Salim Salehe ), Kahinda Otafiire, Paul Kagame ( Rais wa Rwanda ), Samson Mande aliyekuwa Ugandan Millitary Attache to Tanzania 1995 - 1998 na wengineo wengi tu ambao kwa msaada wa Tanzania waliweza kufanikisha Wapiganaji wa NRA waliokuwa wakiongozwa na Mzee Museveni kuiteka Uganda na kuwa Watawala mpaka leo japo kuna waliotangulia mbele za haki huku wengine wakitofautiana Kisiasa na Mzee Museveni.

Leo nataka tu niwapashe Wakenya kuwa walikuwa wanapoteza tu muda kufanya USHAWISHI wao kwa Mzee Museveni Rais wa Uganda kwani kwa aina ya Marafiki wa KUFA na KUZIKANA hawa Wafuatao wa Rais Museveni asingeitosa Tanzania yetu hata iweje. Nitawagawa hawa Marafiki wa karibu wa Museveni kwa makundi ili Wakenya mfahamu kuwa mlikuwa ( Wakwere wanasema ) KUZOZA mnapiga tu soga na kupoteza muda wenu.

MARAFIKI WA KARIBU wa Rais Museveni wa KUFA na KUZIKANA ni:
Hayati Baba wa Taifa Nyerere na sasa Familia yake nzima.
Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Mwalimu Nyerere Mzee Joseph Butiku.
Balozi Mstaafu na aliyekuwa Mshauri wa Masuala ya Nje na NYETI Mzee Adam Marwa.
Hayati Brigadier Hashim Mbita.
Mkurugenzi Mtendaji wa MKUKI Publishers Mzee Walter Bgoya.
Aliyekuwa Mbunge wa Karatu Hayati Mzee Patrick Qorro.
Mkuu wa Majeshi Mstaafu Mzee David Bugozi Musuguri.

MARAFIKI WA KUHESHIMIANA wa Rais Museveni ni :
Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mzee Ally Hassan Mwinyi.
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mzee Benjamin William Mkapa.
Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mzee Jakaya Mrisho Kikwete.
Waziri Mkuu Mstaafu Mzee Joseph Sinde Warioba.
Balozi Mstaafu wa Tanzania nchini Uganda Mzee Tambwe.
Naibu Balozi Mstaafu wa Tanzania nchini Uganda Hayati Mzee Mufungo Mujaya.

MARAFIKI wa KUHESHIMIANA KIUTENDAJI wa Rais Museveni ni :
Jeshi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ )

MARAFIKI wa KIUPENDO kwa UKARIMU kwa Rais Museveni ni :
Wananchi wote wa Tanzania hasa hasa Wakazi wa Dar es salaam, Kilimanjaro na Kagera.
NB: Japo nimewataja Watu kadhaa hapo kwa umuhimu wao ila hakuna Watu ambao hadi dakika hii Rais wa Uganda Mzee Yoweri Kaguta Museveni anawasikiliza na kila mara kuomba ushauri kwao kama Mjane wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere na Mwanae Madaraka, Katibu Mkuu Kiongozi Mzee Joseph Butiku na Balozi Mstaafu Mzee Adam Marwa na nakumbuka ili kuonyesha kuwa Museveni ANAWAHESHIMU na KUWAPENDA hawa Watu watatu niliowataja hapa takribani miaka mitano ( 5 ) iliyopita tu katika Sherehe za Uhuru wa Uganda Rais Museveni aliwavisha TUZO ZA JUU na za HESHIMA KWA NCHINI Uganda Rais Mstaafu Mzee Kikwete kwa niaba ya Tanzania, Mama Maria, Mzee Butiku na Mzee Marwa na nakumbuka akiwa anahutubia pale Viwanja vya Kololo jijini Kampala mbele ya Waganda huku Rais wetu Mstaafu wa awamu ya nne ( 4 ) Mzee Kikwete akishuhudia Rais Museveni alisema maneno haya kwa Waganda namnukuu " today I am very happy that We are celebrating our independence together with people whom I call the true Comrades of Uganda. May I take this opportunity to introduce to you my other Mum, brothers and good friends from Tanzania the country that have a great history with Uganda. This is His Excellency President of Tanzania Jakaya Kikwete and next to him is Mama Maria Nyerere the former first lady of Tanzania and Nyerere's widow then these two are not only my friends but they are now my relatives ( akawatania Waganda kwa kuwaambia...) so you Ugandans if you think once you chase me from here I will have no where to go you're just wasting your time because Tanzania is my second home. This is Mr. Joseph Butiku former chief secretary of Tanzania and this one is Mr. Adam Marwa retired ambassador and a former close aide to late President Nyerere. Please together lets give them a hand of applause and wish them well " mwisho wa kumnukuu Rais wa Uganda Mzee Museveni kisha akawapa hizo TUZO tena kwa KUWAVISHA kwa MADAHA yote na Rais Museveni akionekana ni mwenye FURAHA ILIYOTUKUKA.

Hata hivyo najua na nikiri pia kuwa zipo sababu nyingi na tena muhimu pengine hata nje ya hii au hizi ambazo pia zimewezeshesha Uganda kukubali kupitisha Bomba lake nchini Tanzania badala ya Kenya lakini ni ukweli usiopingika kuwa Rais wa Uganda Yoweri Museveni ana UPENDO WA DHATI na ULIOTUKUKA kwa Nchi ya Tanzania na ANATUHESHIMU pengine hata kuliko Waganda anaowaongoza. Sababu hizo KUU za kihistoria na kirafiki ndizo zimekuwa HUKUMU kwa nchi ya Kenya.

Poleni sana Wakenya ila msihofu FURSA bado zipo nyingi tu tutawashirikisheni na zingine pia ila acheni MAJUNGU na WIVU wenu kwetu Watanzania.

Akhsante Rais Yoweri Kaguta Museveni kwa kuwaonyesha Wakenya kuwa Tanzania ndiyo kila kitu kwako na kwa Waganda wote na usichoke kutupa fursa zingine.

Imeandikwa na GENTAMYCINE/Jamii Forums

Unabii wa Prof Kitila Mkumbo Juu ya Uhai wa vyama vya Upinzani Nchini Unaelekea Kutimia

$
0
0
Kwa namna ambavyo hali ya kisiasa ya vyama vya upinzani inavyozidi kupoteza mvuto mbele ya jamii kipindi hiki cha utawala wa awamu ya tano,huenda unabii wa Profesa Kitila ukatimia.

Muda mfupi mara tu baada ya utendaji uliotukuka wa serikali ya CCM chini ya Dr Magufuli,Prof Kitila mkumbo aliandika kupitia account yake ya twitter na hapa namnukuu;

"Tunahitaji upinzani utakaojikita katika sera mbadala.Upinzani unaotegemea makosa ya serikali ya CCM pekee unaweza kupwaya sana kipindi hiki",mwisho wakumnukuu.

Nafikiri kwa hali ilivyo sasa juu ya taswira ya siasa za vyama vya upinzani nchini ilivyo ni dhahiri utabiri huu unajidhihirisha kwani ni kweli wapinzani hasa CDM walizoea sana siasa za matukio ili kuimarisha chama.

Lakini prof Kitila Mkumbo hakuishia hapo kutoa tahadhari kwa vyama vya upinzani,siku nyingine kupitia account yake ya twitter aliandika tena na hapa namnukuu,

"Upinzani uchwara hushamiri sana wakati wa serikali dhaifu.Upinzani makini huibuka wakati wa serikali makini na yenye chembe ya udikteta",mwisho wa kumnukuu.

Nafikiri kama wapinzani hawataacha siasa za kuishi kwa matukio kama walivyozoea CHADEMA,Kipindi hiki cha utawa wa CCM chini ya Magufuli huenda tukashuhudia anguko kubwa la vyama vya upinzani nchini.

Imeandikwa na Gimmy's
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live




Latest Images