Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104663 articles
Browse latest View live

Video ya Sekunde 80 ikionyesha Tukio la Papa Wemba Kuanguka Jukwaani Akitumbuiza na Kufariki

$
0
0
Lilikua ni tamasha ambalo linaonekana live kwenye TV ambapo mkongwe huyu wa muziki kutoka Congo DRC alikua akitumbuiza na band yake huko Abidjan Ivory Coast lakini ghafla akaanguka na kufariki muda mfupi baadae.

Tazama Video:


Matokeo ya Yanga na Coastal Union Haya Hapa...Mechi Yashindwa Kumalizika Baada ya Mashabiki Kuleta Fujo

$
0
0
April 24 2016 ndio siku iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka Tanzania, kwani ndio ile siku ambayo ilikuwa inasubiriwa na mashabiki kushuhudia nusu fainali ya Kombe la FA (Azam Sports Federation Cup), kwa upande wa Yanga walikuwa wageni wa Coastal Union katika uwanja wa Mkwakwani Tanga.

Kutoka katika uwanja wa Mkwakwani Tanga mechi imeshindwa kumalizika baada ya mashabiki wa Coastal Union kutoridhishwa na uchezeshaji wa refa hivyo mchezo umeshindwa kuendelea kutokana na kuwa na giza na vurugu za mashabiki, dakika 90 za mchezo huo ulimalizika kwa sare ya goli 1-1, hivyo muamuzi akaongeza dakika 30

Lulu Michael Avalishwa Pete ya Uchumba..ila Mwenyewe Kaandika Haya yaliyowaacha Mashabiki Njia Panda

$
0
0

Lulu leo amewaacha mashabiki wake njia panda baada ya kuweka picha kwenye ukurasa wake wa Instagram ikionyesha akiwa na pete ya uchumba...

Kwenye hiyo picha ameandika maneno haya:
Asante MUNGU Wangu Kwa Neema Zako ambazo hazijawahi kuniacha Maana Hata hiki kitendo cha kishujaa kujinunulia Pete Nzuri Kama hii Ni Kwa Neema tu Haya Acheni Umbea,hyo michezo yenu ya kuitana cjui kutagiana mtavunja Vidole....Kwa akili Yako nikinunuliwa/kuvalishwa ntakutangazia ?Jumapili Njema" Ameandika Lulu

Matangazo ya LIVE Bungeni Shinikizo Lazidi Kuongezeka

$
0
0
Vyama vya siasa na wadau mbali mbali wameendelea kupinga hatua ya bunge la jamhuri ya Muungano kuzuia vyombo vya habari kurusha mijadala ya bunge kwa njia ya television na radio mpaka pale habari hizo zitakaporekodiwa na kitengo cha habari cha bunge na kusambazwa ktika vyombo vya habari ili zirushwe.

M/kiti wa chama cha kijamii cha CCK Renatus Muhabi akizungumza na waandishi jijini dsm amesema hatua ya bunge kuzuia waandishi wa habari kupata habari au kurusha moja kwa moja inarudisha nyuma maendeleo,kuwanyima wananchi kupata habari kwa waliowachagua lakini pia ni ukiukwaji mkubwa wa demokrasi ya habari nchini.

Katika hatua nyingine chama hicho leo kimewapokewa Viongozi waandamizi kutoka chama cha UDP ambao wameamua kujiunga na CCK kwa ajili ya kuendesha harakati za kisiasa nchini.

Wakizungumza mara baada ya kukabidhiwa kadi na M/kiti wa Cck wamesema wamehama UDP kwa madai kuwa chama hicho kimeshindwa kuleta mabadiliko ya kweli .

Madereva Wakaidi Agizo la Serikali la Kutopitisha Magari yenye Uzito Mkubwa Kigamboni

$
0
0
Siku cheche baada ya Serikali kuzindua daraja jipya la Kigamboni jiji  Dar es Salaam na kukataza Magari yenye uzito zaidi ya tani kumi kutopita katika daraja hilo baadhi ya madereva wasiofuata sheria wamekuwa wakikiuka agizo hilo nakuonekana kupita katika daraja hilo.

Akitekeleza majukumu yake Inspekta Hassan Amadi ambaye ni mkuu wa usalama barabani wilaya kipolisi Kigamboni amesema kwamba ifike kipindi madereva waache kuvunja sheria na kufuata maelekezo nakuwataka madereva wengine wanaovunja sheria sehemu mbali mbali  hususani wanao tumia daraja hilo kufuata sheria zilizowekwa na kuepuka  makosa kama hayo.

Naye dereva aliyevunja sharia akijaribu kujitetea amesema kwamba hkufahamu utaratibu mzima wa upitaji katika barabara hiyo hivyo anakiri kosa alilofanya nakuwasihi madereva wenzake wafuate  sheria Barabarani.

Tatizo la Kunuka Kikwapa..Tiba yake Hii Hapa..

$
0
0
Kikwapa  ni  tatizo la kutoa harufu mbaya  sehemu ya kwapani katika mwili wa binadamu. Tatizo la kikwapa husababishwa na bakteria wanaovutiwa na jasho au unyevunyevu  chini ya kwapa.
Tatizo la Kikwapa ni kero kwa sababu husababisha mtu kutoa harufu inayokuwa kero kwako na kwa mtu mwingine aliyeko jirani yako.

Ili kwapa lako liwe na harufu nzuri, kavu na safi fanya yafuatayo


  • Paka kipande cha limao kwenye kwapa na kuacha lipate hewa  safi ili kuua vijidudu na kutoa tezi za jasho kuondoa harufu mbaya
  • Vaa nguo safi zenye nyuzinyuzi za asili kama pamba, hariri na sufu zitasaidia kufyonza unyevu na kuliacha kwapa lako kavu, safi na bila harufu mbaya
  • Oga kila siku na safisha nguo kwa maji safi itasaidia kuua bakteria na ambao husababisha harufu mbaya
  • Kunywa maji mengi kila siku yatakusaidia kutoa sumu mwilini na hivyo kupunguza harufu mbaya ya kwapa.
  • Osha kwapa mara kwa mara kwa kutumia sabuni zenye dawa (medicated soaps)
  • Punguza kula chakula chenye viungo vingi hasa vitunguu
  • Kumbuka kutumia pafyume na Spray zitasaidia kuondoa harufu mbaya kwa muda na sio kutibu tatizo moja kwa moja.
  • Baada ya kuoga jifute kwa taulo au kitambaa safi na usiache unyevu unyevu ambao uwavutia bakteria kukua katika eneo ili.
  • Jitahidi kunyoa nywele za sehemu hii mara kwa mara.
  • Epuka kukaa sehemu zenye joto kupita kiasi kwa muda mrefu.

Tamko La Jukwaa La Wahariri Juu Ya Matangazo Ya Bunge

$
0
0
Bodi ya Jukwa la Wahariri Tanzania (TEF) iliyokaa Ijumaa Aprili 22, 2016 jijini Dar es Salaam pamoja na mambo mengine ilijadili hali ya mwenendo wa tasnia ya habari nchini hasa juu ya haki ya wananchi kupata habari.

Katika kujadili hali hiyo, TEF imeguswa kwa namba ya kipekee kabisa na mwenendo mzima wa urushaji wa bahari za Bunge kwa njia ya redio na luninga, hususan katika mkutano wa tatu wa Bunge la 11 unaoendelea mjini Dodoma kwa sasa.

Itakumbukwa kwamba Muhimili wa Bunge kupitia Kitengo chake cha Habari, Elimu na Mawasiliano, Aprili 15 2016 ulitoa taarifa kwa umma ikieleza utaratibu mpya ambao sasa umeanza kutumika katika kurusha matangazo ya redio na luninga kutoka Bungeni.

Katika taarifa hiyo, Ofisi ya Bunge ilisema kuwa imeamua kuboresha mfumo wa urushaji wa Matangazo ya Bunge kwa Bunge lenyewe kurusha Matangazo ya Vikao vyake pamoja na Vipindi mbalimbali vyenye Maudhui kuhusu Shughuli za Bunge ambazo hazijapata fursa ya kufahamika vyema kwa umma kuanzia katika Mkutano wa Bunge la Bajeti unaoendelea sasa.

Ofisi hiyo ilisema kuwa mfumo huo mpya ni Utamaduni wa kawaida kwa kila Bunge hususani Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola kuwa na Studio zake kwa lengo la kurusha Matangazo ili yawafikie wadau kwa lengo la kurusha kupitia vituo vyao. Kwa maana hiyo, Bunge lilisisitiza kuwa chini ya utaratibu huo mpya, jukumu la kurusha Matangzo ya Vikao vya Bunge litafanywa na Bunge lenyewe kupitia FEED MAALUM ili kurahisisha kila Kituo cha Radio na Televisheni kupata Matangazo hayo kwa sehemu walipo bila kufunga Mitambo yao Bungeni Dodoma.

Katika kutekeleza uamuzi huo na mfumo huo mpya, kila kituo cha Televisheni na Redio sasa watatumia Masafa ya Matangazo ya Bunge (Frequencies) bure kupitia FEED MAALUM itakayorushwa na Satellite ya INTELSAT 17 ambayo iko nyuzi 66 Mashariki kwa masafa maalum ambayo pia yaliwekwa wazi.

Kwa mantiki hiyo, Bunge sasa limezuia vituo vyote vya televisheni nchini kupeleka kamera zake ndani ya Bunge kwa kuwa habari hizo zitapatikana kwenye feed maalum ambayo ni ya Bunge ambayo inasimamiwa na waandishi wa Bunge ambao pia ndio wanaamua nini kionyeshwe kwa utashi wao.

Baada ya kutafakari hatua hizi mpya za Bunge na baada ya kufuatilia kile kinachorushwa, mambo kadhaa yamethibitika:-

Mosi, habari kutoka ndani ya Bunge sasa zinachujwa mno kupitia mfumo huu mpya wa feed maalum;

Pili, ubora za picha zinazorushwa kupitia feed hii nao ni wa kiwango cha chini pia;

Tatu, kwa mantiki ya kawaida kabisa, hatua hizi zote zimepunguza na kukwaza haki ya wanahabari kufanya kazi yao kwa uhuru, lakini pia inawanyima wananchi haki ya kupata kwa uhakika na bila kuchujwa kile kinachofanywa na wawakilishi wao.

Kwa kuzingatia haya yote, TEF inasema bayana kwamba:

 Hatua hizi mpya za kuzuia kamera za televisheni kuingia Bungeni ni hatua za dhahiri kabisa za kukwaza uhuru wa habari nchini na kukuza censorship nchini. Hali hii haisaidii siyo Bunge tu, bali hata wabunge, wananchi na taifa kwa ujumla katika kupiga hatua za kweli katika kujenga demokrasia na kulinda haki za kupata habari na uhuru wa kujieleza nchini;

    TEF imeanza kuingiwa na hofu kwamba sababu za awali zilizokuwa zimetolewa za kuzuia utangazaji wa moja kwa moja wa Bunge kupitia TBC kwa sababu ya gharama, huenda hazikuwa za dhati. Hali hii imejionyesha hasa baada ya vituo binafsi vya televisheni kujitokeza na kuendelea kuonyesha vikao vya bunge moja moja, lakini navyo sasa vimenyimwa fursa hiyo kwa utaratibu huu mpya wa feed maalum.

    Ni dhahiri sasa, ushiriki wa wananchi katika kufuatilia mwenendo wa Bunge na wabunge wao umekwazwa sana kwa hatua hizi mpya na kwa maana hiyo, kupunguza ushiriki wa wananchi katika mfumo wa utawala wa nchi yao.

Kwa kuzingatia haya yote, TEF inatoa rai kwa uongozi wa Bunge kufikiria upya hatua hizi za kuzidi kufunika shughuli za Bunge kwenye blangeti zito la usiri na censorship, hivyo uruhusu kituo chochote cha televisheni chenye nia, uwezo na utayari wa kurusha matangazo ya Bunge moja moja bila kulazimika kujiunga na feed maalum iliyoanzishwa.

Tunaamini kwamba kama hali hii ya kutumia feed maalum itaachwa iendelee hakika Tanzania kama taifa tunapiga hatua nyuma kwa yale mazuri machache tuliyokuwa tumeyafikia, mojawapo, uhuru wa Bunge kuendesha mambo yake kwa uhuru na uwazi mkubwa hivyo kuwa mfano mojawapo wa taasisi za umma zinazojiendesha kwa uwazi.

Imetolewa leo, Jumapili Aprili 24 2016 jijijni Dar es Salaam na Jukwaa la Wahariri Tanzania.

Theophil Makunga                 Neville Meena

Mwenyekiti                             Katibu

IGP Mangu: Lugumi ilitekeleza Mkataba wake na Jeshi la Polisi

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi – Inspekta Jenerali (IGP), Ernest Mangu amekanusha madai ya wabunge na
hata taarifa zinazosambaa mitandaoni na kwenye vyombo vya habari kuhusu kampuni ya Lugumi kushindwa kufunga mashine kwenye vituo vya Polisi 108 kama mkataba wake ulivyomtaka.

Akizungumza mwishoni mwa wiki, IGP Mangu alisema anashangazwa na habari hizo na kueleza kuwa kampuni ya Lugumi ilitekeleza mradi wa kufunga mashine hizo kama ilivyokubaliana na serikali.

“Siyo kweli, watu wana ugomvi wao, lakini nakueleza wazi kwamba, tembelea vituo vyote tulivyokubaliana, utakuta mashine zipo. Inawezekana zingine hazifanyi kazi kwa sababu ya kukosekana kwa intaneti,” aliongeza mkuu huyo wa polisi.

Alipoulizwa mwenye jukumu la kufunga mtandao wa intaneti ni nani, IGP alijibu, “...ni TTCL (Kamuni ya Simu) ingawa sehemu nyingi ofisi zetu zimekatiwa huduma hiyo kwa kuwa jeshi halijalipa.”

Paul Okoye wa kundi la P-Square Anaswa South Africa Akiwa Amevaa Kofia ya WCB Wasafi ya Diamond..

$
0
0
Ukimuona Paul Okoye wa kundi la P-Square akiwa amevaa kofia ya WCB na yupo Johannesburg, Afrika Kusini ambako Diamond yupo huko tangu mwanzoni mwa wiki hii kuzindua video ya Colors of Africa, ujue mambo yameiva.

Paul amepost picha Instagram akiwa amevaa kofia nyeupe ya WCB, label ya Diamond na kuashiria kuwa huenda wiki hii wakali hao wakashoot video ya collabo yao. Diamond aliingia studio na P-Square mwaka jana.

Kituo cha runinga cha MTV Base kiliripoti wiki hii kuwa Diamond atashoot video ya wimbo huo hivi karibuni.

Habari Mbaya Kutoka Ubelgiji...Mchezaji Samatta Aumia Pua Mchezoni..Anasubiri Vipimo Kujua Kama Pua Imevunjika

$
0
0
Jumapili April 24 usiku timu ya Genk ilishuka dimbani kuchuana na Gent lakini taarifa mbaya kuhusu star wa Bongo kwenye ligi ya Ubelgiji Mbwana Samatta ni kwamba, amepata majeraha katika mchezo huo ambao alianza kwenye kikosi cha kwanza lakini hakuweza kumaliza dakika zote 90.

Kipindi cha pili Samatta alishindwa kurudi uwanjani kuendelea na mchezo kutokana na maumivu aliyoyapata kipindi cha kwanza baada ya kugongwa pua. Ilibidi nafasi yake ichukuliwe na Nikolaos Karelis aliyeingia dakika ya 46 kipindi cha pili.

Timu ya Genk imepoteza mchezo wake wa Jupiter League baada ya kukubali kipigo cha 2-1 vs Gent.

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya April 25, Ikiwemo Takururu Kuchunguza Mabilioni ya Kikwete

$
0
0

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya April 25, Ikiwemo Takururu Kuchunguza Mabilioni ya Kikwete

Mwafrika wa Kwanza Kushinda Tuzo ya Mwanasoka Bora wa Kulipwa Ulaya Ametangazwa, Amewahi Kuifunga Tanzania

$
0
0
Usiku wa April 24 imetangazwa good news  kwa soka la Afrika, huu sio ushindi wa taifa la mchezaji husika ila  ni fahari ya Afrika nzima, winga mshambuliaji wa kimataifa wa Algeria anayeichezea klabu ya Leicester City ya Uingereza Riyad Mahrez ametangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya PFA 2015/2016 (Professional Footballers Association).

Riyad Mahrez ametangazwa kushinda tuzo hiyo mbele ya wachezaji kama Mesut Ozil wa Arsenal, Jamie Vardy wa Leicester City, Harry Kane wa Spurs, N’golo Kante wa Leicester City, Dimitri Payet wa West Ham United, PFA ni tuzo za wachezaji bora wa kulipwa.

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Riyad Mahrez ndio alikuwa mchezaji wa Algeria aliyefunga goli la nne dakika ya 43 katika ushindi wa goli 7-0 dhidi ya Taifa Stars November 17 2015 na kuIondoa Tanzania katika mbio za kuwania kufuzu michuano ya Kombe la Dunia 2018.

Sababu za Bandari ya Tanga Kuteuliwa Kutumiwa na Bomba la Mafuta Kutoka Uganda

$
0
0
Serikali ya Uganda imetangaza rasmi uamuzi wa kutumia bandari ya Tanga baada ya kuwepo na ushindani na bandari za Lamu na Mombasa za nchini Kenya. Bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima katika Ziwa Albert nchini Uganda litapita katika ardhi ya Tanzania kwenda Bandari ya Tanga ambako ndiko meli kubwa za mafuta, zitakapotia nanga kubeba mafuta hayo kwenda sehemu mbalimbali duniani.

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo April 24 2016 amewasili Tanzania akitokea Uganda alipokwenda kwenye mkutano wa majadiliano ya bomba hilo la mafuta lipite wapi kati ya Tanzania au Kenya. Akizungumza baada ya kuwasili Prof. Muhongo ameeleza sababu zilizofanya Bandari ya Tanga kuchaguliwa ambapo ushindani ulikuwa ni wa ubora wa bandari na ubora wa njia ambako bomba litapita……….

’Tanga ni bora kwa sababu ina kina kirefu kulinganisha na bandari za mombasa na Lamu, Bandari ya Tanga ina kina cha zaidi ya mita 23 ambayo kimataifa inatakiwa ili meli kubwa inayokuja kuchukua shehena ya mafuta iweze kutia nanga na kupakia mafuta nakuondoka, tumewapiku wenzetu kwa kina, na pili bandari yetu inaweza kufanya kazi kwa siku zote za mwaka yaani siku 365′:-Profesa Sospeter Muhongo

Bomba hilo litaingilia Mkoa wa Kagera kutoka nchini Uganda na kupita katika mikoa ya Geita, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma hadi Bandari ya Tanga. Bomba hilo linatarajiwa kukamilika mwaka 2020 katikati.

Nape Ataja Majipu Manne Katika Sanaa Nchini,aahidi Kuyatumbua

$
0
0
Waziri wa Habari,Utamaduni,sanaa na michezo nchini,Nape Nnauye ametaja mambo manne ambayo ni vikwazo ndani ya sekta ya sanaa ya filamu nchini na kuyaita kwamba ni majipu huku akisisistiza kwamba serikali itakwenda kutunga sera ya sekta hiyo katika mwaka wa fedha 2016/17.

Nape,aliyataja mambo hayo na kuyafananisha na majipu kuwa ni uporaji wa kazi za wasanii nchini,ujenzi duni wa miundombinu ya kazi za wasanii nchini,usimamizi mbovu wa bodi ya filamu nchini sanjari na tatizo la mfumo mbovu wa usambazaji wa kazi za wasanii nchini.

Akizindua tamasha la filamu la Tanzanite International Film
Festival(TIFF) jijini Arusha juzi ambao ulihudhuriwa na wasanii maarufu wa filamu nchini waziri huyo alisema kwamba jipu la kwanza ambalo atakwenda kulitumbua ni uporaji wa kazi za wasanii nchini.

“Jipu la kwanza tutalitumbua kwenye bajeti yetu ya mwaka 2016/17 ni uporaji wa kazi za wasanii nchini wengi wananyonywa jasho lao”alisema Nape

Hatahivyo,alisema kwamba jipu la pili ni ujenzi duni wa miundombinu ya kazi za wasanii za filamu nchini na kudai kwamba chini ya uongozi wake atahakikisha anaimarisha miundombinu bora kwa lengo la kuwasaidia wasanii hao pamoja na kulinda haki zao.

Alisema ya kwamba mfumo wa kazi za usambazaji wa kazi za wasanii nchini pamoja na hakimiliki ni wa kinyonyaji huku akitolea mfano wa kazi za msanii maarufu wa sanaa hiyo nchini marehemu Stephen Kanumba na kusema kwamba familia yake hainufaiki na matunda ya kazi zake hadi sasa kutokana na mfumo mbovu wa usimamizi wa kazi za wasanii nchini.

Alitaja takwimu kwamba mwaka 2011/12 jumla ya filamu 218
zilitengenezwa nchini na mwaka 2014/15 kazi hizo ziliongezeka hadi kufikia 14,00 huku akidai hilo linadhihirisha kwamba sekta hiyo inakua kwa kasi nchini na kuongeza ajira

Hatahivyo,Rais wa shirikisho la wasanii wa filamu nchini(TAFF),Simon Mwakifamba aliwataka wasanii wa filamu nchini kujiandaa kisaikolojia kukabiliana na soko la ushindani wa filamu duniani kwa kuwa wabunifu.

“Serikali tunaiomba iandae sera itakayoandaa mazingira mazuri kwa wasanii nchini kuhusu usalama wa kazi zao”alisema Mwakifamba

Naye, muaandaji wa tamasha hilo,Said Sassi alisema kwamba tatizo la uharamia wa kazi za wasanii nchini limetanda na kuwaomba wafanyabiashara na makampuni kujitokeza kudhamini vipindi mbalimbali vya luninga kwa lengo la kuinua sekta hiyo.

Mkurugenzi wa kampuni ya uchimbaji wa madini ya vito ya Tanzanite One Mining Ltd ambao ni miongoni mwa wafadhili wa tamasha hilo,Feisal Shabhai alisema lengo la kampuni yao kujitosa kufadhili tamasha hilo ni kutoa mchango wao katika kusaidia jamii kupitia faida wanayoipata ili kuinua sekta ya ajira nchini.

TAKURURU Washtuka Sasa Yaanza Kuchunguza Mabilioni ya Kikwete

$
0
0
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), imeanza kuchunguza fedha za uwezeshaji maarufu kama ‘Mabilioni ya JK’ ambazo hazikurejeshwa na wakopaji nchi nzima.

Msemaji wa Takukuru, Tunu Mleli alisema jana kuwa taasisi hiyo imechukua jukumu hilo kwa sababu moja ya majukumu yake ni kuchunguza masuala ya rushwa na kutoa rai kwa mtu mwenye ushahidi au taarifa kuhusu suala hilo kuzitoa kwa taasisi hiyo.

“Takukuru ipo wazi kuzipokea taarifa hizo ili zitusaidie kwenye uchunguzi,” alisema Tunu.

Kati ya Sh50 bilioni zilizotolewa na Serikali ya Awamu ya Nne chini ya Rais mstaafu, Jakaya Kikwete, ni Sh43 bilioni tu zilizorejeshwa, huku Sh7 bilioni zikidaiwa kutafunwa.

Fedha hizo zilitolewa na Kikwete kwa ajili ya kuwawezesha kimitaji, wajasiriamali nchi nzima, mikopo ambayo ilipitia benki za CRDB, NMB, Community Bank na Benki ya Posta Tanzania.

Fedha hizo kutoka Mfuko wa Rais, zilikuwa zikikopeshwa kwa riba ya asilimia 10, ambapo asilimia mbili ilikuwa inaingia serikalini na nane ilikuwa inabaki kwenye benki hizo.

Hata hivyo, baadhi ya vyama vya Akiba vya Kuweka na Kukopa (Saccos), vilivyopewa fedha hizo, vilitoa mikopo hiyo kiholela, huku baadhi ya viongozi wakidaiwa kutengeneza majina feki na kukopeshana fedha hizo.

Imedaiwa kuwa Saccos nyingi ambazo zilifuja fedha hizo katika mikoa mbalimbali, viongozi wake wengi walikuwa pia ni viongozi wa kisiasa na wengine wakiwa na nyadhifa serikalini.

Kwa mujibu wa uchunguzi huo, baadhi ya waliokopeshwa fedha hizo na Saccos mbalimbali, hawakuwa wanachama, bali walichomekwa baada ya kuonekana kuna fursa ya ‘kupiga dili’.

Chanzo kutoka Takukuru, kimedokeza  kuwa makamanda wa taasisi hiyo katika mikoa mbalimbali, wamepewa maelekezo ya kuchunguza mahali yalipo mabilioni hayo na nani waliyafuja.

 “Ni kweli tumepewa maelekezo ya kuchunguza fedha hizo. Unajua hizi ni fedha za umma haziwezi kutafunwa tu hivihivi na Serikali ikakaa kimya,” alidokeza mmoja wa maofisa wa Takukuru. 

Machi mwaka jana, aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji), Christopher Chiza aliagiza kufanyika kwa ukaguzi wa kina wa fedha hizo.

Alitoa agizo hilo wakati wa ziara yake katika Baraza la Taifa la Uwezeshaji Kiuchumi (Neec), ambako aliagiza watakaobanika kuhusika na ubadhirifu wa fedha hizo wachukuliwe hatua za kisheria.

“Lazima tuangalie mabilioni ya JK yalipotelea wapi, yalivyofujwa na wahusika wapo wapi ili sheria ichukue mkondo wake. Nimeambiwa kuna zilizobaki tujue ziko wapi,” alikaririwa Chiza akisema. 

Lakini Desemba 24, 2013, mtangulizi wa Chiza, Mary Nagu alikaririwa akisema Sh43 bilioni kati ya Sh50 bilioni za mabilioni ya JK zilizokopeshwa kwa wajasiriamali 74,701 zilikuwa zimerejeshwa.

Nagu alitoa takwimu hizo alipokuwa akizungumzia mafanikio ya Serikali ya Rais Kikwete katika, utaratibu uliofanywa pia na wizara nyingine.

Suala la mabilioni hayo ya JK limekuwa likiibuka mara kwa mara bungeni na katika mitandao mbalimbali ya kijamii huku wananchi wakitaka zirejeshwe.

Kauli ya Kwanza ya Mkurugenzi wa TFF Baada ya Mchezo wa Yanga na Coastal Union Kuvunjika Jana...

$
0
0
Baada ya mchezo huo kuvunjika uliyokuwa unarushwa Live kupitia Azam Tv, ripota wa Azam Tv alifanya mahojiano mafupi ya Live kutoka katika uwanja wa Mkwakwani Tanga na kaimu mkurugenzi wa mashindano wa TFF Jemedali Said ilikujua mambo yatakuwaje mchezo utarudiwa au inakuwaje?

“Kiukweli mchezo umevunjika lakini haya mashindano yanaendeshwa kwa kanuni na taratibu ila sisi tunasubiri ripoti ya muamuzi na kamisaa wa mchezo ili tuweze kufanya maamuzi” Alisema Jemedali Said

Nafasi za Ajira leo Tembelea www.ajirayako.com 

Vyeti Feki Vitampa Magufuli Maadui Wengi kuliko Hata "Ufisadi"

$
0
0
Kama kweli Rais Magufuli atahamia katika ukaguzi wa vyeti feki akimaliza ishu ya watumishi hewa ni wazi atapata maadui wengi na idadi yao itakuwa kubwa kuliko anaowapata katika vita yake dhidi ya ubadhirifu.

Watumishi wenye vyeti feki katika utumishi wa umma na makampuni binafsi ni wengi mno. Wengi wao wanafahamika na ndugu zao, marafiki zo na hata majirani zao kwa aidha kufahamu historia zao au kwa kutumia majina tofauti na yale waliyozaliwa nayo au kubatizwa nayo.

Wengi wa watumishi hawa wamepanda ngazi mbalimbali katika utumishi wa umma na hata wengine kufikia ngazi za juu. Wakati mchakato wa vitambulisho vya taifa ulipoanza suala hili linasemekana lilijitokeza kwa kiasi kikubwa katika idara nyeti za serikali lakini kutokana na ukubwa wake ikaamuliwa lifumbiwe macho.

Vyeti feki vinagusa karibu kada zote na katika ngazi mbalimbali mpaka hata zile ngazi zinazoonekana za watu wasioguswa.

Kama Rais JPM akiingia nakugusa huku ni wazi atakuta amegusaa idadi kubwa ya watanzania ikiwemo ile inayomuunga mkono. Tegemezi wa vyeti feki na vyeti feki wenyewe wataendelea kumuunga mkono zamu yao ya kutumbuliwa ikifika? Ndio maana nachele kusema kuwa zoezi la utambuzi wa vyeti feki litamuacha Rais Magufuli na maadui wengi kuliko atakaowapata katika zoezi la ubadhirifu hivyo serikali yake inaweza kupoteza umaarufu ilioanza kuupata. Homa imepanda kiasi kwamba wenye vyeti feki wanaongoza mashambulizi makali ya ukosoaji katika mitandao ya kijamii na popote wapatapo fursa dhidi ya utendaji wa JPM ili kumpunguza nguvu.

CAG Kuanika Mafisadi Bungeni Leo Wakati Akiwasilisha Ripoti Yake

$
0
0
Mdhibiti  na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) leo anawasilisha bungeni ripoti ya mwisho ya ukaguzi wa hesabu za serikali ya mwaka 2014/15.

Ingawa haijajulikana rasmi nini kilichomo ndani yake, baadhi ya watu waliohojiwa wanatarajia CAG kubaini mchwa wanaotafuna fedha za umma na namna ya kukabiliana nao.

Aidha wengine wanatarajia taarifa ya hali bora zaidi ya usimamizi wa fedha za umma kuliko kipindi cha nyuma.

Ripoti hiyo awali ilikuwa imepangwa kuwasilishwa bungeni mwishoni mwa wiki (Aprili 22) kabla ya kuahirishwa hadi leo.

“Ni kweli CAG atawasilisha ripoti kesho (leo) bungeni, ”Naibu Katibu wa Bunge na Utawala, Joel Joel alithibitisha juu ya kuwasilishwa kwa ripoti hiyo leo. 

Miongoni mwa wabunge waliozungumza na mwandishi wa habari hizi, wamesema wanatarajia CAG kuonesha mambo mazuri kwa maana ya taasisi zilizofanya vizuri katika usimamizi wa fedha za umma lakini pia mambo mabaya.

“Lazima ripoti itaibua madudu maana walizoea (watendaji serikali) kana kwamba hapakuwapo na serikali,” alisema Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ally Keissy na kusisitiza kuwa pamoja na wabunge wenzake, watamsaidia Rais John Magufuli kupambana na ubadhirifu serikalini.

Keisy alisema akiwa mbunge, anaamini pamoja na wenzake, wanachosubiri ni kuona ripoti hiyo na kuhakikisha wanaohusika na kuchezea fedha za serikali, kabla ya kufikishwa mahakamani, wanarudisha fedha hizo.

“Atakachosema CAG sisi tutakuwa tayari kusimama kusaidia Rais aendelee kupambana na ubadhirifu,” alisema.

Kwa upande wake, Mbunge wa Mbinga Vijijini, Martin Msuha, alisema ripoti hiyo ni muhimu katika usimamizi wa serikali na inategemewa kuwa na mambo mazuri na mabaya kwa maana ya majipu ambayo yatapaswa kutumbuliwa.

Mbunge wa Bukoba Vijijini, Jasson Rweikiza alisema matarajio waliyo nayo ni kwamba ubadhirifu na wizi utakaoibuliwa na ripoti hiyo utashughulikiwa mara moja.

 “Kama kuna ubadhirifu, mishahara hewa na wizi vyote vishughulikiwe...kama kuna ubadhirifu na wizi wowote, mwizi mahali pake ni jela,” alisema Rweikiza akishutumu uwapo wafanyakazi hewa katika halmashauri yake.

Gigy Money Aopoa Kigogo wa Madini..Mwenyewe Adai Wameshibana

$
0
0
Kazi ipo! Video Queen asiyeishiwa vituko Bongo, Gift Stanford ‘Gigy Money’ anadaiwa kuopoa kigogo ambaye ni mfanyabiashara wa madini, mkazi wa jijini Arusha ambaye ndiye mwandani wake anayempa jeuri kwa sasa.

‘Ubuyu’ kutoka kwa chanzo chetu ambacho ni mtu wa karibu wa mwanadada huyo unatonya kuwa, licha ya ‘umapepe’ wa Gigy ambaye kwa sasa safari za Dar na Arusha hazikauki, ukweli ni kwamba jamaa huyo hapindui kwake.

Ili kupata mzani wa ubuyu huo, Over Ze Weekend lilimsaka Gigy, alipopatikana kwa njia ya kilongalonga alikiri kuwa na kigogo huyo na kudai kwamba wameshibana sana.

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Elimu (Duce) Auawa Kwa Kuchomwa Kisu na Mpenzi Wake

$
0
0

Mwanafunzi wa mwaka wa pili katika Chuo Kikuu cha Elimu (Duce), jijini Dar es Salaam, Bertha Mwarabu (23), ameuawa na mwanafunzi mwenzake kwa kuchomwa kisu kwenye titi na tumboni kwa kinachodaiwa ni kutokana na wivu wa mapenzi.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Mark Kalunguyeye, tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana katika hosteli za chuo hicho zilizopo Mabibo, jijini Dar es Salaam.

Kamanda Kalunguyeye amemtaja mtuhumiwa wa mauaji hayo kuwa ni Masamba Musiba (27) ambaye pia ni mwanafunzi wa mwaka wa pili katika chuo hicho, ambacho ni sehemu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Amesema mauaji hayo yalitokea juzi saa 3:45 usiku baada ya Musiba kuingia chumbani kwa marehemu ambaye inadaiwa alikuwa mpenzi wake na kuanza kumshambulia kwa kisu.

Ameongeza kuwa baada ya marehemu kuanza kushambuliwa, alipiga kelele kuomba msaada na ndipo wanafunzi wenzake walipokwenda na kumkamata mtuhumiwa wakati akijaribu kukimbia.

Amesema kelele za marehemu, ndizo zilizowashtua wanafunzi wenzake.

Kamanda Kalunguyeye alifafanua kuwa marehemu alikimbizwa hospitali kupatiwa matibabu lakini alifia njiani.

Mtuhumiwa anashikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala.

Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mukandala, amesema tukio la mauaji hayo ni la kwanza kutokea chuoni hapo.

Profesa Mukandala alisema tangu aanze kufanya kazi chuoni hapo kwa miaka mingi, hajawahi kushuhudia tukio la namna hiyo na kuongeza kuwa amesikitika kwa kuondokewa na mwananfunzi huyo.
Viewing all 104663 articles
Browse latest View live




Latest Images