Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104415 articles
Browse latest View live

MAKALA : SITTA, ULIOMBA, UKAAMINIWA, SASA TULIPE!

0
0
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na Mwenyekiti Mteule wa Bunge hilo Bw. Samwel Sitta akibadilishana Mawazo na Mjumbe wa Bunge hilo Mohamed Seif Khatib ndani ya Bunge Maalum la Katiba.
NIANZE kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia afya, mimi pamoja na wewe unayesoma hivi sasa makala haya. Bila yeye kutulinda, huenda hivi sasa tusingekuwa hapa tulipo, tungekuwa sehemu nyingine kabisa ambayo isingetupa fursa ya kuwasiliana kama hivi.
Wiki iliyopita Bunge Maalum la Katiba lilimchagua kwa kura nyingi, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel John Sitta kuwa Mwenyekiti wake wa kudumu na Samia Suluhu Hassan kuwa makamu wake baada ya kazi kubwa kufanywa na Mwenyekiti wa Muda, Pandu Ameir Kificho, ambaye kwa siku 21, aliweza kukiongoza chombo hicho kutengeneza kanuni ambazo sasa zitatumika kuijadili Rasimu ya Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kama ilivyowasilishwa na Tume Maalum ya Mabadiliko ya Katiba chini ya Jaji Joseph Sinde Warioba.
Sitta, ambaye aliwahi kuliongoza Bunge la Tisa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa spika, alijipatia sifa kubwa kwa kuruhusu mijadala bila upendeleo, akiweka mbele kile ambacho mwenyewe amekuwa akidai kuwa ni masilahi ya taifa.
Watu wengi, wakiwemo wanasiasa wa upinzani, walikuwa wakimuona Sitta kama mtu aliyestahili kuchukua nafasi hiyo kutoka CCM, kuliko watu wengine waliokuwa wakitajwa, kitu kinachoonyesha kuwa waliridhishwa kwa kiasi kikubwa na utendaji wake wakati akiwa amekalia kiti ambacho sasa kipo kwa Anne Makinda.
Ingawa mara nyingi historia imekuwa ikitufundisha kujikumbusha, wakati mwingine yapo mambo ambayo hatuhitaji historia ili kujiridhisha kuwa yanaweza kutokea.
Miongoni mwa mambo hayo, ni hili ambalo sasa lipo mbele ya Mheshimiwa Sitta. Analo deni analodaiwa na Watanzania wapatao milioni 45, wanaomtaka asimamie kwa umakini, uzalendo na masilahi ya taifa, wakati akiliongoza Bunge hili maalum kutupatia katiba mpya itakayokidhi matakwa ya wananchi wote.
Inafahamika Sitta ni kada mwaminifu na huenda mtiifu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wote tunajua msimamo wa chama hiki katika baadhi ya mambo makubwa yanayotarajiwa kuchukua muda mwingi wa majadiliano ambayo yanagusa uhai wetu kama taifa.
CCM inataka Muungano wa serikali mbili kama ilivyo hivi sasa na pia inataka upigaji kura wakati wa kupisha vifungu vya katiba hiyo kufanywa kwa uwazi. Kwa nini chama chake kinataka iwe hivyo? Inafahamika. Muundo wowote wa serikali tofauti na nia ya CCM, maana yake ni anguko lao. Wasingependa litokee.
Na ili hilo lisitokee, ni lazima zipigwe kura za wazi ili wawaone watakaoenda kinyume na msimamo wa chama. Ni dhahiri, hakuna aliye tayari kwenda kinyume hadharani, huku akionekana na vigogo wa chama hicho.
Hatuna matatizo na msimamo wa CCM kwa sababu kila chama kilichomo kwenye bunge hili kina msimamo wake. Watu wote hawawezi kuwa na mawazo yanayofanana, hasa katika baadhi ya mambo yanayogusa masilahi ya taifa.
Ni kwa sababu hii, tunahitaji Mwenyekiti Sitta kutulipa kwa kututendea haki katika mchakato huu muhimu. Hatutegemei kama anaweza kukiangusha chama chake, lakini tunaamini atatuangalia zaidi sisi kama Watanzania na kujua tunachohitaji.
Hatutaki aweke mbele masilahi ya chama chochote, isipokuwa taifa kwanza. Vyama vinaweza kupotea siku yoyote na kusiwe na shida, nchi ikaendelea, lakini taifa likipotea vyama navyo vitapotea. Hoja ziamuliwe kwa busara inayotetea masilahi ya wengi.
Wapo watu wanaomnadi Sitta kama mtu anayefaa kuwa rais ajaye wa Tanzania. Sehemu pekee ya kuthibitisha uwezo huo, ni kutuongoza kupata katiba bora ambayo watu watapata haki zao za msingi na lazima bila kujali chama gani cha siasa kipo madarakani.
Katiba hii inahusu uhai wa Watanzania. Tunategemea itatufaa kwa miaka mingi ijayo, tukiishi bila uhasama wala manung’uniko. Na ili hili lifanikiwe, ni lazima tuwafanye wananchi, ambao hawapo bungeni, kuwa ndiyo walengwa wakuu, badala ya vigogo wanaotetea masilahi yao ya sasa.
Siku zote, mwenye dhamira njema hulindwa na Mungu na hili ndilo tunalolitegemea kutoka kwa Mhe. Sitta ambaye ameapa kwa Mungu kutopendelea. 
siwezi kuolewa na Mbongo.”

WEMA SEPETU AWEKA RECORD YA KIPEKEE MTANDAO WA INSTAGRAM TANZANIA

0
0
Picha ya Diamond Platnumz inayomuonesha akiwa amelala na huku shavuni kukiwa na lipstick za mwanamke iliyowekwa kwenye ukurasa wa Instagram wa Wema Sepetu, imevunja rekodi ya mtandao huo kwa Tanzania kwakuwa na comments nyingi zaidi.
Hadi sasa picha hiyo ina comments 1,786 na hivyo kuizidi picha nyingine aliyoiweka mwezi uliopita ambayo ndio ilikuwa picha ya kwanza inayomuonesha Wema akiwa na Diamond tangu warudiane. Picha hiyo ilipata comments 1,601.

Wakati huo huo Diamond ndiye staa wa Afrika Mashariki mwenye followers wengi zaidi kwenye Instagram (ukimtoa Lupita Nyong’o mwenye followers 930,744, au wengine wanaoishi diaspora). Hadi sasa staa huyo ana followers 95,900+ akifuatiwa na mpenzi wake Wema mwenye followers 82,870+.
Bongo5

MWANAMUZI NAZIZI AKANUSHA KUWA NA UHUSIANO WA KIMAPENZI NA PRODUCER WA TANZANIA

0
0
Week iliyopita kulikuwa na Habari kuwa Mwanamuziki Nazizi kutoka Kenya Ambae Pia ni Couzin ya Mwanamuziki wa Bongo Flava Jaffaray kuwa anatoka kimapenzi na Producer wa Muziki Mmbongo ambaye anafanya kazi Huko Nairobi Kwa Jina la Sappy ....Baada ya Habari hizi Nazizi Amejitokeza na kusema kuwa toka aachana na Mume wake hajawahi kuwa mapenzini na mtu yoyote ..japo ana marafiki wengi wavulana na amepiga nao picha nyingi ikiwemo hizo alizopiga na Sappy...Na amesema msishangae zikatoka picha nyingine zaidi akiwa na marafiki zake wa kiume...

-John K

DHARAU ZINGINE HUWA HAZINA FAIDA..ONA HUYU DADA ALIVYOADHIRIKA

0
0
Leo Asubuhi Nikiwa Ubungo bus terminal....
Leo asubuhi nikiwa stand ya mabasi ya ubungo,mdada mmoja wakati anapanda kwenye kagari kake akadondosha simu.Mimi nikamuita ili nimweleze kilichotokea,akanisonya tena msonyo wa dharau sana na nikajuta kumgusa bega kwasababu ya kibao alichonipiga.

Alipoondoa gari nikaiokota hiyo simu na kuondoka zangu,wala sikuizima.


Nafika town simu hiyo ikaita nikapokea kwa shauku ya kujua nani,haya ndo ya kawa maongezi yetu na mpigaji.

Mimi; Hallo habari yako
Yeye; Nzuri
Mimi; nani wewe 
Yeye; Mimi ndo mwenye hiyo simu ....
Mimi; Na mimi ndo nilokuita na ukanizaba kibao Pale stand ya ubungo leo na ukanisonya
Yeye; Basi kaka nisamehe naomba unambie ulipo nije tuelewane 
Mimi; Nitakwambia baadaye (nikakata simu na kuzima)

Swali nimwambie napatikana wapi au nimpotezee ili liwe fundisho kwake?

BUNGE LA KATIBA LACHAFUKA DODOMA

0
0
 Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba jana jioni alisimama kwa dakika tatu mbele ya kipaza sauti lakini akashindwa kuwasilisha Rasimu ya Katiba kutokana na vurugu zilizojitokeza bungeni.

Vurugu hizo zilitokea muda mfupi baada ya Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta kumwalika kuwasilisha Rasimu ya Katiba kwa muda wa dakika 120.

Jaji Warioba alisimama kwenye mimbari ya Bunge saa 11:02 jioni tayari kuhutubia lakini kabla ya kufanya hivyo, wajumbe kadhaa walisimama na kuomba mwongozo wa mwenyekiti.

Waliosimama ni Profesa Ibrahimu Lipumba, James Mbatia, Freeman Mbowe na Tundu Lissu.

Hata hivyo, Sitta aliwanyima fursa akisema: “Hakuna mwongozo hapa, naomba Mwenyekiti uendelee, waheshimiwa wabunge hakuna mwongozo naomba Mwenyekiti uendelee kwa ajili ya hansard.”

Kauli hiyo ilionekana kuchafua hali ya hewa kwani Jaji Warioba alipowasha kipaza sauti tayari kuanza kuhutubia, baadhi ya wajumbe walianza kupiga kelele, wengine makofi na kugonga meza hivyo kumfanya ashindwe kufanya kazi hiyo ya uwasilishaji.

Waliokuwa mstari wa mbele kupinga Jaji Warioba kuwasilisha Rasimu ya Katiba kwa sehemu kubwa walikuwa ni wajumbe wanaounda kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Jaji Warioba akiwa anatafakari mbele ya mimbari, Sitta aliwasha kipaza sauti na kumtaka aendelee kuwasilisha Rasimu ya Katiba ... “Endelea Mwenyekiti, endelea kwa ajili ya kumbukumbu rasmi (hansard).”

Lissu akisikika akijibu kauli hiyo akisema: “Fuata kanuni mwenyekiti... fuata kanuni mwenyekiti,… huku akipiga kelele na kugonga meza na wakati huo Profesa Lipumba akiwa amewasha kipaza sauti chake kutaka kuzungumza huku naye akiendelea kupiga meza kwa nguvu.

Wengine waliosimama ni Mchungaji Christopher Mtikila, Ezekiel Oluoch, Philimon Ndesamburo, Moses Machali na Mchungaji Peter Msigwa.

Dakika tatu zilikatika huku kukiwa hakuna dalili za hali kutulia na kuona hivyo, Jaji Warioba aliamua kuondoka kwenye mimbari na kuketi kimya akiwa na Makamu Mwenyekiti wake Jaji Augustino Ramadhani.

Baada ya hapo, Sitta alisimama na kuwasha kipaza sauti na kusema: “Waheshimiwa wajumbe, katika mazingira haya tuliyonayo, naomba kutangaza kuwa nasitisha shughuli za Bunge hadi hapo tutakapotangaziwa tena.”

Licha ya kauli hiyo, baadhi ya wajumbe waliendelea kupaza sauti zao wakisema kwamba walikuwa wanaburuzwa.

Wakati hayo yakitokea, kikosi cha askari wa Bunge kiliingia ndani ya ukumbi na kusimama katika lango kuu hali iliyoonekana kuwa ni kuchukua hadhari endapo hali ya usalama ingechafuka.

Baada ya tamko la kuahirisha mkutano, askari hao waliingia moja kwa moja hadi alipokuwa ameketi Jaji Warioba na kumsindikiza hadi nje na jitihada za waandishi wa habari kumfuata ili kupata maoni yake hazikufanikiwa.

Kilichofuata baada ya hali hiyo ni kurushiana maneno kwa baadhi ya wajumbe akiwamo Dk Ave Maria Semakafu ambaye nusura azipige kavukavu na mjumbe mwingine ambaye jina halikuweza kupatikana mara moja.

Hata hivyo, baadhi ya wajumbe akiwamo Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais (Utumishi), Celina Kombani waliamulia ugomvi huo kabla ya kuwa mkubwa.

Wajumbe walionekana kukaa katika vikundi ndani ya Bunge huku wakijadiliana juu ya kilichotokea wakati Sitta, Katibu wa Bunge, Yahaya Khamis Hamad na msaidizi wake, Dk Thomas Kashililah wakiwa katika kikao cha faragha.

Baada ya kujadiliana kwa nusu saa, Hamad akiwa ameongozana na Dk Kashililah, alirejea katika ukumbi wa Bunge na kuwataka wajumbe kutawanyika hadi hapo watakapojulishwa.

Hali hiyo iliibua kelele kutoka kwa wajumbe wakitaka kujua iwapo waondoke katika maeneo ya Bunge au la. Hamad alisisitiza kwamba warejee nyumbani hadi hapo watakapojulishwa.

DIAMOND PLATNUMZ BANA..ETI MAHABA NIUE..KIPARA NINYONGE

0
0
 Diamond Platnumz bana eti ‪#‎mahaba_niue‬ ‪#‎kipara_ninyonge‬!!!
Kapendeza  ama?

HAJI RAMADHANI WA BSS "KI UKWELI KIMUZIKI NIPO JUU KULIKO NEY WA MITEGO HATA AKINIPONDA"

0
0
Haji Ramadhani ni msanii aliyetajwa kwenye line za wimbo wa Salaam zao wa Ney wa Mitego kwenye wimbo ambao baadhi ya mashairi ya wimbo huo yanawataja yeye Haji Ramadhan na Water Chilambo kuwa hawana pesa na wako tu mtaani bila ramani yoyote.
Sasa kupitia Exclusive Interview na millardayo.com Haji Ramadhan ametoa jibu la kamili kwa kusema>>’Ney kama Ney ameamua kuongea kwa sababu ameamua kufanya style fulani ya kutokea,labda alimlenga mtu aliye nae karibu lakini kwangu mimi hajui na wala hatuko karibu’
‘Mimi sijafulia mimi nina maisha yangu mazuri naishi vizuri nimekutana na Ney kwenye Fiesta Leaders ye akaanza kulalamika eti mshkaji unanikanda sana,Ney hajui muziki ni basi kipaji tu amejaaliwa kupendwa na watu wala hawezi kunigusa hata chembe’
‘Mimi kwangu Ney ni dogo mwili tu ule nikamwambia dogo wewe unanichafua binafsi haikuniathiri kwa sababu mimi ni mwanamuziki mkubwa kuliko Ney kiukweli,kimuziki nipo juu ya Ney labda kijina yeye ana jina kubwa kuliko mimi,maneno ya Ney hayanishushi na mimi sijafulia’.

HONGERA PETRIDA FASHION (MKE YA MUZUNGU) KWA KUFUNGA NDOA

0
0




Hongera petrida fashion(Mr and Mrs Karch) kwa kufunga ndoa.

Ameolewa na Mjerumani  iliyofanyika huko huko Ujerumani Sasa Ameanza Maisha Mapya baada ya Kumpata Mwenye Mahaba Niue kutoka Ujerumani...Hongera Sana Petrida..
See More Photos @ http://petridafashions.blogspot.com/

WARIOBA AKATA NGEBE ZA CCM

0
0
MWENYEKITI wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, amezima rasmi sakata la makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kulazimisha Bunge Maalumu la Katiba kukataa pendekezo la Tume ya Mabadiliko ya Katiba kuhusu muundo wa Muungano wa serikali tatu.

Akiwasilisha Rasimu ya Pili ya Katiba bungeni jana, Jaji Warioba alisema uchambuzi uliofanywa na tume yake umezingatia maoni ya wananchi, historia  na hali halisi, na kwamba ili muungano udumu serikali tatu hazikwepeki.

Alisema tume ilitafakari maoni mbalimbali yaliyotolewa na wananachi na makundi, na ilirejea ripoti kadhaa za miaka zaidi ya 20 mfululizo, ikazingatia malalamiko ya Zanzibar na Tanganyika, mgongano wa kikatiba kati ya Katiba ya Zanzibar na ya Muungano, na mengine mengi.

MASKINI SHEIKH PONDA ..AENDELEA KUSOTA

0
0
JITIHADA za Sheikh Ponda Issa Ponda, kutaka Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ifanyie marejeo uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro Oktoba mosi mwaka jana, zimegonga mwamba baada ya mahakama hiyo kulitupa ombi hilo.

Uamuzi huo ulitolewa jana na Jaji Agustino Mwarija, ambaye alisema mahakama imesikiliza hoja za pande zote mbili na imefikia uamuzi wa kukubaliana na pingamizi la awali lililowasilishwa mahakamani na mjibu maombi ambaye ni Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Dk. Eliezer Feleshi, aliyetaka ombi hilo litupwe.

Februari mwaka huu, Feleshi aliiomba mahakama hiyo ilitupe ombi la Ponda, kwa sababu linakiuka matakwa ya Kifungu cha 372(2) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002, ambacho kinakataza amri za muda, awali  zinazotokana na mahakama za chini zisikatiwe rufaa katika Mahakama za juu kama Ponda alivyofanya.

ETOO TENA..AWAPA ZAWADI CHELSEA...GALATASARAY HOI

0
0
Jana Usiku palikuwa na kipute Kikali kati ya Chelsea na Galatasaray Ambao Chelsea walikuwa Uwanja wa Nyumbani ...Kama kawa mtu alichukua mbili Mbili huku Etoo Akiwa mmoja wa wafungaji wa Chelsea katika Dakika ya 4, Mfungaji mwengine alikuwa Cahil dakika 42

ZITTO AUNGA MKONO SEREKALI TATU BAADA YA HUTUBA YA JAJI WARIOBA JANA

0
0
Zitto ameonekana Kufurahishwa na ufafanuzi wa Jaji Warioba na hata Kupelekea kuwashawishi Wajumbe wenzake kwamba, hawana budi kujadili namna ya Kuuboresha zaidi muundo huo wa Serikali tatu badala ya kujadili Serikali mbili ambazo yeye mwenyewe amekiri kwamba hazitakuwa Suluhisho la Kero za muungano kupitia ukurasa wake wa facebook.

Hii imemtokea baada ya jana Kuusikiliza kwa makini ufafanuzi wa Jaji Warioba kuhusu muundo huo wa Serikali tatu, pia Kwa mujibu wa Maelezo ya Julius S. Mtatiro Naibu Katibu Mkuu wa CUF Tanzania Bara ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge maalum la Katiba amesema Idadi kubwa ya Wajumbe wa CCM, jana baada ya kutoka ndani Ukumbi wa Bunge, walionekana kuridhishwa na ufafanuzi wa hotuba ya Warioba huku wengine wakitamka wazi kuwa Serikali tatu ndio mpango mzima. 

Nawasilisha!

Chanzo: Zitto Kabwe's facebook page..

WASTARA ACHUMBIWA THEN ABWAGWA

0
0
Stori: Imelda Mtema
STAA wa sinema za Kibongo, Wastara Juma ametoboa kuwa, kuna wanaume kibao walimchumbia kwa nyakati tofauti, lakini wakabadilisha uamuzi huo na hivyo kumfanya aendelee kubaki mpweke.

Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, wikiendi iliyopita jijini Dar es Salaam, Wastara alisema, wanaume hao wanafikia uamuzi huo kutokana na magazeti na mitandao mbalimbali kuripoti mara kwa mara kuhusu uhusiano wake na Mtangazaji wa Channel Ten, Bond Binslum, habari ambazo anazikanusha.

IKOJE?
Wastara alisema, tangu kifo cha mume wake, Juma Kilowoko ‘Sajuki’, magazeti yamekuwa yakimwandama kwa habari za skendo badala ya kuangalia mambo ya msingi na hivyo kumkosesha mume mwema.
“Maisha yangu ni kama yanaendeshwa na magazeti, kila siku utakuta habari zangu kwenye magazeti tena siyo nzuri, sasa zinanisababishia matatizo.

Angalia sasa, kuna watu walijitokeza na kuonyesha nia ya kunioa, lakini wakija kuona habari kwenye magazeti wanabadilisha mawazo.
“Kwa kweli nawashukuru sana nyie (Global) huwa hamuandiki habari bila kuniuliza kwenye simu, lakini wapo wengine sijui wanatoa wapi maneno, wanayaweka kwenye gazeti hivyo hivyo. Yaani tangu nimepata misukosuko, sijatulia kabisa, kila siku ni mikasa baada ya visa,” alisema. 

KUHUSU BOND
“Watu wanaandika mimi nina uhusiano na Bond, tangu lini? Hata wakiniuliza nikikataa, bado wanaendelea kuandika kuwa Bond ni mpenzi wangu, si jambo la kweli. Sikia... kuna mwanaume mstaarabu sana, tena Muislam safi, alijitokeza nyumbani kistaarabu, akaniposa.
“Mambo yakaenda vizuri, lakini baadaye kidogo akaja kusoma kwenye magazeti eti mimi na Bond tunapika na kupakua, akabadilisha mawazo. Ilikuwa kazi ngumu kumuelewesha kuwa siyo kweli, hakuniamini kabisa.”

MAHARI YARUDISHWA
“Mwingine tulifikia mahali pazuri kabisa, hadi mahari alishatoa, baadaye akaona kwenye mitandao kuwa nimeonekana kwenye magazeti nikiwa na Bond, akahairisha kila kitu na akataka arudishiwe mahari yake - akapewa.

Hebu angalia ni mambo gani hayo?
“Huko ni kuharibiana. Naishi maisha ya huzuni kila siku, kwanini wasiandike mambo ya msingi ya kunisaidia badala ya kuzusha mambo kama wanavyofanya sasa?”

NDOA IPO LAKINI...
“Mimi ni mwanamke, nimekamilika. Siwezi kuishi peke yangu siku zote, kwa hiyo kuwa na mwanaume siyo kosa, ila sasa muda haujafika. Nikiwa na mtu wangu, kwa nini nisiwe mkweli? Habari za mimi kuwa na Bond zinazushwa tu, watu waachane na hayo mambo wafanye mengine ya muhimu.

“Kwa sasa niachwe nipumzike, najua ipo siku atatokea mwanaume wa ukweli, tutakamilisha taratibu zote, atanioa. Ikifika hatua hiyo, sitakuwa na sababu ya kuficha. Watu wanipe muda kwanza.”

MSIKIE HUYU
Risasi Mchanganyiko liliwasiliana na mmoja wa mashosti wa karibu na Wastara na kuzungumza naye kuhusiana na malalamiko ya Wastara ambapo alisema inawezekana shoga yake akawa na hoja lakini bado ishu hiyo ipo mikononi mwake.

Kwa sharti la kutotajwa gazetini, shosti huyo alisema: “Lakini rafiki yangu naye kayataka mwenyewe. Kama hatoki na huyo Bond, sasa mapicha aliyokuwa akiyaweka kwenye mitandao ya kijamii akiwa naye karibu ya nini? Maana chanzo cha yote ni hizo picha.

“Namshauri tu atulie, afanye mambo yake kimyakimya, kuweka picha kwenye mitandao ni hatari... yeye mwenyewe anaamua kuyaendesha maisha yake kupitia vyombo vya habari.
GPL

LINAH AMWANIKA MWANAUME WAKE

0
0
Stori: Paparazi Wetu
BAADA ya minong’ono ya muda mrefu, hatimaye staa wa Bongo Fleva, Estelina Sanga ‘Linah’ ameweka wazi kuwa anatoka kimapenzi na Nagari Kombo.

Akiteta na kona hii, wikiendi iliyopita jijini Dar es Salaam, Linah alisema: “Ni kweli kwa sasa natoka na Kombo, ndiye mwanaume wangu, sina haja ya kuficha. Mimi na Amini imebaki stori tu, hata yeye ana mtu wake.”

Kombo alijipatia umaarufu siku za nyuma baada ya kuingia uwanjani na kumkumbatia mchezaji Ricardo Kaka wa Timu ya Taifa ya Brazil iliyokuwa ikichuana na Taifa Stars katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
GPL

KWANINI BEYONCE HATAKI KUHUDHURIA ARUSI YA KANYE WEST NA KIM KARDASHIAN?

0
0
Kim Kardashian na Kanye West wametangaza siku ya harusi yao, lakini kuna mtu mmpja muhimu anayedaiwa kuwa hatohudhuria – Beyonce.

Wakati ambapo inadaiwa kuwa Jay Z hakuwa tayari kuwa best man wa Kanye, sasa, Beyonce anadaiwa kumwambia Jay-Z na Kanye kuwa hataki kurekodiwa kwenye video wakati wa harusi hiyo. Beyonce anaiwa kusema haiwezekani yeye kuwa sehemu ya video hiyo itakayotumika kwenye reality show ya familia ya Kim.

Mtandao wa RadarOnline umedai kuwa Beyonce amekuwa akiwaambia marafiki zake kuwa hataki kwenda kwenye harusi hiyo kwakuwa idea ya harusi hiyo ni ya kipuuzi kwakuwa harusi yake na Jay Z ilikuwa ya siri.

“Beyoncé’s motto has always been, less is more. But clearly when it comes to Kim, more means more. She knows she’ll have to go to the wedding, but really does not to want to,” kilisema chanzo.

Harusi hiyo itafanyika jijini Paris, May 24 na ofcourse Beyonce atalazimika kuwepo kwasababu tu mume wake Jay Z na Kanye ni marafiki wa damu.
Bongo5

UJUMBE KUTOKA KWA DIAMOND PLATNUMZ KUJA KWAKO

0
0
Morning Africa,...SIKU YA LEO UPATAPO NAFASI,HEBU JARIBU KUFANYA MOJA YA HAYA NA UTAKUWA UMEBADILISHA MAISHA YA MTU FLANI. 
-Una mlinzi?instead ya kumfokea,Hebu leo kumbuka kumsalimu na kumtakia siku njema huytu mtu anayekesha getini kulinda nyumba yako,bila shaka wengi hawafanyi hili

1: shiriki bure sehemu ya chakula chako na yeyote mwenye njaa na kuhitaji

2: Shiriki nyimbo nzuri kwa mtu mwenye huzuni ama anye feel down
3: Mfundishe mtu ,jambo analotamani kulifaham na halifaham na ni wewe pekee unafahamu
4: Una nguo ama chochote usichokihitaji tena?hapana usikitupe,mpatie yule mwenye kuhitaji
5: Una rafiki ama jamaa mpweke na pengine hana mtu wa karibu wa kushare nae yanayomsibu,make a call am text kwake,mfanye ajiskie hayupo peke yake,kwani kuna siku nawe utakuwa mpweke na utatamani mtu wa kuzungumza nae.
6: Panga ku donate damu,damu yako kidogo inaweza ikaokoa maisha ya mtu sehemu flani..

7: Saidia mzee,ama mtoto kuvuka barabara.
8: Ambia rafiki,family member ama mtumishi ni kiasi gani una mwappreciate
9: Saidia mji wako kuwa msafi,si kazi kubwa kuokota kipande cha uchafu na kuweka sehemu husika
10: Mpigie mzazi wako na kumwambia ni kiasi gani unampenda
11: Motivate mtu flani atimize ndoto zake
12: Jipe amani ya moyo kwa kusamehe
13:  la mwisho,jifanyie wewe mwenyewe,Acha kufanya kitu kibaya ulichokuwa unaufanyia mwili wako,pengine uvutaji wa sigara,ulevi wa kupita kiasi etc
....HAIJALISHI NI KIDOGO KIASI GANI UTAKACHOKIFANYA,KUWEKA TABASAMU KWA MTU,NDICHO KINACHO MATTER ...Siku njema

VICTORIA KIMANI "PICHA NILIYOPIGA NA DIAMOND HAIMANISHI KUNA MAMBO MENGINE YANAENDELEA"

0
0
Mwimbaji wa Kenya Victoria Kimani ambaye amekuwa Tanzania kwa siku kadhaa sasa akiutangaza muziki wake pamoja na kufanya collabo na wasanii wa Bongo, amezungumza maneno ya kuondoa ukungu wowote uliokuwepo hasa kuhusu yeye na Diamond Platnumz.

Mwezi uliopita aliyekuwa mwakilishi wa Kenya kwenye BBA, Huddah Monroe na Colonel Mustafa walitangaza uhusiano wao wa kimapenzi kwenye kipindi cha ‘Kiti Moto’cha KTN.
Victoria amepost picha aliyopiga na mastaa wawili Ommy Dimpoz na Diamond Platnumz iliyosindikizwa na ujumbe huu:

“ Mafans wangu wote, nawapenda sana sana. Nafanya kazi ya muziki kwa bidii na kwa sababu yenu. Nimepiga picha na wanamuziki wengi na wakubwa sana kote duniani. Na hiyo HAIMAANISHI KUNA MAMBO MENGINE YANAENDELEA NJE ya KAZI YA MUZIKI. Kwa hayo machache, ninafuraha sana kufanya kazi na wanamuziki wakubwa zaidi wa Bongo @ommydimpoz na @diamondplatnumz kwenye single moja. Mimi ndiye msanii wa kwanza wakike kufanya single moja na hawa wawili. Tunafocus na mambo makubwa zaidi ili East Africa iende mbele kimuziki. NAWAPENDA WOTE. Mimi wenu VICTORIA KIMANI. “

Wiki iliyopita U heard ya Soudy Brown iliibua taarifa ya ugomvi uliotokea studio baina ya Abdul Naseeb aka Diamond na mpenzi wake Wema, baada ya Wema kufika studio walipokuwa Ommy na Diamond wakirecord na Victoria.

5 COMMON REASONS WHY PEOPLE BREAK UP

0
0
When two people are falling in love, the love factor tends to be stronger such that they overlook any differences that may see them break up. However, when such differences erupt and as love factor meets reality as time goes by, break ups come knocking.

Here are some of the root causes of relationship and marriage break ups:

1. Mental and/or physical abuse among the couple

Of late, the idea of a woman being equal to a man in a relationship has seen many couples get traumatized and in the end seek ways out which in simple terms are break ups. Being a major causal factor, mental and/or physical abuse in a relationship is brought about by sadistic attitude by either one or both partners which leads to spousal manipulation, control and intimidation. Most partners fail to take the heat and opt for break up.

2. Infidelity and Cheating

Infidelity is the number one cause of divorces among married couples while cheating is killing almost every relationship once it advances to the revealing or noticeable stages.

3. Selfishness

Once the honeymooner stage is over, most partners develop a feeling of selfishness which in turn starts ruining the essence of love factor in a relationship hence breaking up becomes the only option.

4. Incessant quarrels and arguments

If partners in a relationship fail to understand the importance of agreeing for a compromise, fights, quarrels and arguments become rampant. As such, the relationship goes out of control hence breaking up resorts to be the only option.

5. Jealousy

Break ups are sometimes triggered by jealousy within a relationship as it causes great devastation. If you start thinking that your partner is filtering most of his attention towards someone else, you may begin seeing him as less attracted to you hence devastation crops in which in turn leads to break ups.

In order to keep your relationship steady, remember to avoid all of these things and you will live up to your dreams.

NIMEIPENDA HII .."CHELSEA BADO WANAMSAMINI DROGBA WAMPA ZAWADI JANA USIKU"

0
0
Didier Drogba to get Silver shoe from Chelsea for his services to the club....Nimeipenda sana hii Jamaa Jana usiku wakati wa Mechi ya Chelsea na Galatasaray , Uongozi wa Chelsea walimwandalia Mchezaji Drogba zawadi ya Kiatu cha Silver kwa kuonesha kuukubali mchango wake wakati anachezea hiyo Team kabla ya kuondoka....Kibongo Bongo hii ipo Kweli ?


KILA WAKATI ANATAKA NIMGEGEDE..HATAKI HATA NIENDE KAZINI...USHAURI

0
0

Jamani yamenikuta , nililia Mapenzi wakati sina hadi nilikuwa najiona sina bahati ya kupendwa sasa jamani nimepata msichana wa Kitanga ananipenda kufa, Sijui ni kawaida ama la huyu nilie mpata sasa anapenda sana mchezo yaani kila saa anataka tufanye hata ananikataza kwenda kazani mimi ninafanya biashara sasa huwa naenda kusimamia biashara zangu , Binti huyu nimeanza kaa nae nina week ya Pili sasa toka ahamie kwangu huwezi amani sijatoka ndani ananizuia kwa mitego ya khanga moko....Mwee mpaka naona biashara zangu zinadoda....Kweli ndio Mapenzi haya au ?
Viewing all 104415 articles
Browse latest View live




Latest Images