Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104776 articles
Browse latest View live

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya May 2, Ikiwemo ya Magufuli Kutafuna Mfupa wa JK

$
0
0

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya May 2

Picha: Watangazaji Gerald Hando na PJ Waanza kazi EFM kwa Mkwara Huu

$
0
0
Ushindani kwenye vituo vya redio nchini umefika katika ubora wake.

Gerald Hando, Adella Tillya na Paul James wakiwa nje ya jengo la K-Net wakiendesha kipindi chao live

Kwa siku nyingi wapenzi wa redio walikuwa wakiwasubiri kwa hamu Gerald Hando na Paul James waliohamia EFM kuona wana kipya gani.

Leo, May 2, wawili hao wameanza kwenda hewani kupitia kipindi cha Joto la Asubuhi. Aliyekuwa mtayarishaji wa kipindi cha Power Breakfast cha Clouds FM walikokuwa wawili hao, Abel Onesmo naye ameungana nao.

Hata hivyo wawili hao wameanza kazi kwa mtindo wa aina yake. Kipindi cha Joto la Asubuhi kimezinduliwa upya kwa matangazo kurushwa live nje ya jengo la K-Net zilipo studio zake maeneo ya Maringo – Kona ya Kawe.

Video: Davido akimpiga shabiki wake nchini Uingereza

$
0
0
Davido ameonekana kwenye kipande cha video kinachomuonyesha akiwa na watu wake wakimpiga mtu mmoja anayedaiwa kuwa ni shabiki nchini Uingereza.

davidoz

Kipande hiko cha video chenye urefu wa dakika moja kimesambaa na kuzua maswali mengi kwa mashabiki wake kama hilo tukio linaloonekana ni kweli au ilikuwa ni drama.

Ngoja tuone nini kitatokea baada ya tukio hilo kama ni kweli Davido amelifanya au ilikuwa ni kutafuta kick ya lebo yake ya DMW aliyoianzisha hivi karibuni.


Raila Rubbishes Uhuru Ivory Burning...

$
0
0
Opposition leader Raila Odinga has rubbished Saturday's burning of ivory stockpiles as a public relations gimmick by the Jubilee Administration designed to please the international community.

Raila said that the poachers and the kingpins behind the poaching syndicate in the country enjoyed their freedom ridiculing the burning spectacle.

“These people are known and they were probably just laughing as the ivory went up in flames. They are known and should be arrested and punished. We should shame them publicly instead of burning stockpiles of ivory,” the former Prime Minister noted while speaking in Meru County.

Odinga was accompanied by 14 MPs from ODM where he officially opened the regional party office.

On Saturday, President Uhuru Kenyatta joined other world leaders and Holywood celebrities in setting fire to 105 tonnes of ivory and 1.35 tonnes of rhino horns at the Nairobi National Park to underline Kenya's resolve to tackle run away poaching in the country.

Amid debate on why Kenya was burning the ivory instead of selling it and using the proceeds to conserve the environment, the Head of State said:  “While I agree that Kenya is a poor country, we have a rich heritage. Those who say this act will not work and that poaching will be on the rise, time has come to fight these vices.”

President Kenyatta was cheered on by world leaders, dignitaries and celebrities at the ceremony conducted at the Nairobi National Park.

Wanawake Muwe Makini… Huyu Amefariki Guest House kwa Kulishwa Sumu, Mwanaume Kakimbia

$
0
0
Tukio limetokea Guest House Kimara Dar es salaam usiku wa May 1 2016 ambapo Mwanaume mmoja aliyeingia kwenye nyumba hiyo ya Wageni akiwa na Mwanamke, alikimbia kwa kusingizia kwenda dukani kununua vocha wakati Mwanamke huyo akikaribia kukata roho na hakurudi tena.

Wakati tunasubiri uchunguzi wa Polisi, mashuhuda kwenye eneo la tukio wamesema inavyoonekana Mwanamke huyo atakua kawekewa sumu kwenye chips alizokua anakula ndani ya chumba cha nyumba hiyo ya Wageni chips ambazo inadaiwa walitokanazo kwenye safari yao na kuja nazo Guest House.
Chanzo:Millard Ayo

Haya Hapa Matokeo ya Simba na Azam Yaliyofanya Mashabiki wa Yanga Waendelee Kuchekelea Kileleni...

$
0
0
Ligi Kuu soka Tanzania bara imeendelea leo Mei 1 2016 kwa mchezo kati ya Simba dhidi ya Azam FC kuchezwa katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam, huu ni mchezo wa 26 kwa vilabu vyote na ulikuwa mchezo muhimu kwa kila klabu hili kujiweka pazuri katika nafasi ya kuwania ubingwa.

Azam FC kabla ya mchezo dhidi ya Simba kumalizika kwa sare ya 0-0 walikuwa na point 58 wakiwa nafasi ya pili ya Ligi, wakati Simba walikuwa nafasi ya tatu wakiwa na point 57 wakiongozwa na Yanga ambao wapo kileleni wakiwa na point 65 na michezo 26. Sare ya mchezo huu ilikuwa ni furaha kwa Yanga ambao wameongeza tofauti ya point kwa Azam FC na Simba.

Kwa idadi ya mechi Simba na Azam FC huu ulikuwa ni mchezo muhimu kwao kuhakikisha wanapata point tatu ili kuweza kupunguza tofauti yao ya point na Yanga wanaoongoza Ligi wakiwa na tofauti ya point sita na Azam FC anayefuatia, umuhimu wa mchezo kwa pande zote mbili ndio ulifanya mchezo kuwa na tension kubwa kitu ambacho kilifanya wachezaji wa pande zote kukosa magoli ya wazi wakati mwingine.

Prof. Lipumba Apongeza Mipango ya Rais Magufuli

$
0
0
Mwanasiasa mkongwe ambaye pia ni mtaalamu wa masuala ya uchumi nchini Profesa Ibrahimu Lipumba amesema anaunga mkono mpango wa serikali wa miaka mitano huku akisema ni vema serikali ihakikishe inawekeza zaidi katika nishati ya umeme ili kufikia lengo la kuwa nchi ya viwanda.

Wakati tayari mpango wa serikali ukiwa umekwishawasilishwa kwa miaka mitano ijayo, ambapo umeanisha namna utakavyofanikisha asilimia 40 ya ajira ifikapo mwaka 2020 zikitokana na viwanda, huku miongoni mwa miradi mikubwa uinayotarajiwa kutekelezwa ya viwanda ni ujenzi wa kiwanda cha chuma.

Aidha Mchumi huyo pia amesema adhima ya serikali ya kujenga nchi ya viwanda itafanikia ikiwa itawekeza katika nishati ya umeme wa uhakika, licha ya miradi mikubwa kama ya Power Afrika na MCC kusitishwa huku akiishauri serikali kufanyia kazi maazimio ya bunge kuhusu sakata la Tegeta esrow.

Mahojiano hayo maalum yamefanyika Dar es Salaam, muda mfupi baada ya Prof Lipumba kupokea ujumbe maalum wa wawafuasi wa chama cha CUF kutoka mjini bagamoyo waliokuwa lengo la msihi kurejea kwenye nafasi yake ya uenyekiti wa chama cha CUF.

Zitto: Millioni 50 za Magufuli Kila Kijiji ni Hadaa Kwa Wananchi.

$
0
0
MBUNGE wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe, amesema Serikali ya Awamu ya Tano imewahadaa wananchi kuhusu kuwapa Sh. milioni 50 kila kijiji/mtaa huku akiamini ahadi hiyo haitekelezeki.

Zitto alisema ahadi hiyo "kimahesabu, haitekelezeki."

"Kwanza kwenye bajeti ya Waziri Mkuu, fungu lililotajwa la Sh. bilioni 59 halipo. Na hata kama lipo Tamisemi wanakodai wao (Ofisi ya Waziri Mkuu), halitoshi kuvikopesha vijiji vyote Tanzania," Zitto alisema na kuongeza:

"Sh. bilioni 59 katika mwaka wa fedha 2016/17 maana yake vijini 1,000 tu vitapatiwa fedha. Kama serikali inatekeleza ahadi hiyo kwa vijini 1,000 kila mwaka, maana yake ni kwamba katika miaka mitano ya Rais Magufuli Ikulu, ahadi hiyo itatekelezwa katika vijiji 5,000 tu.

"Huku ni kuwahadaa wananchi. Tanzania ina zaidi ya vijiji 15,000. Kwa fungu linalotengwa, vijini zaidi ya 10,000 havitapata fedha hii."

MASHARTI MAGUMU

Wakati Zitto akitoa tahadhari hiyo, imebaini kuwepo kwa vigezo vya kupata fungu la Sh. milioni 50 za kila kijiji/mtaa ni vigumu.

Akihitimiha mjadala wa makadirio ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu katika mwaka wa fedha 2016/17 wiki iliyopita Majaliwa, alivitaja vigezo saba vitakavyotumika kugawa fedha za mradi huo, huku vyote vikionekana vitakuwa na ugumu kunufaisha wananchi wengi hasa katika maeneo ya vijijini.

Majaliwa alisema mradi huo unalenga kuwawezesha wananchi kiuchumi kwa njia ya kukopesha vikundi vya wajasiriamali kupitia ushirika wa kuweka na kukopa katika vijiji.

Alivitaja vigezo vya kukopeshwa fedha hizo kuwa ni kikundi cha kifedha kiwe kimesajiliwa na Halmashauri na Tume ya Ushirika, kikundi kiwe na Katiba, uongozi uliochaguliwa kidemokrasia na kupata mafunzo ya mikopo pamoja na kikundi hicho kuwa chini ya Asasi ya Kiraia inayotambulika na yenye uzoefu wa shughuli za mikopo.

Majaliwa alikitaja kigezo cha nne kuwa ni kikundi husika kionyeshe uzoefu wa kukopeshana kwa muda wa mwaka mmoja tangu kuanzishwa na historia ya urejeshaji mikopo ya asilimia 95 na cha tano ni kuwa dhamana ya serikali itakuwa kwenye kiasi cha msingi cha mkopo na si kwenye kiasi riba.

"Kigezo cha sita ni kikundi kuweka amana ya akiba ya fedha kwenye benki katika akaunti maalumu (Fixed Deposit) asilimia 10 ya mkopo," alisema.

Majaliwa alisema kigezo cha saba ni kuzingatiwa kwa Sheria ya Vyama vya Ushirika ya mwaka 2013 kuhusu mkopo kwa SACCOS.

Alisema serikali imeandaa mpango wa kutoa elimu kwa wananchi kuhusu suala hilo hususan masuala ya ujasiriamali na biashara

Chanzo: Siasahuru.com 

Meya wa Kinondoni Agawa Bure Maeneo ya Biashara Leo na Kufuta Umiliki wa Vibanda na Vizimba 100

$
0
0
Meya wa Manispaa ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam Mstahiki Boniface Jacob amezua taharuki kwa wamachinga wa ubungo na kukimbia biashara zao wakiambatana naye mithili ya Maandamano mara baada ya kutangaza kufuta umiliki wa vizimba na mabanda takriban 100 yaliyokuwa yakimilikiwa na watendaji na Madiwani wa Manispaa ya Kinondoni katika soko la Mawasiliano Maarufu kama Simu 2000 akiagiza wapewe bure.

Mstahiki Jacob aliyefuatana na watendaji wa Manispaa hiyo alitembea kwa miguu akiongea na wamachinga mmoja mmoja na makundi kuanzia Ubungo Plaza hadi ubungo maji akiwaelimisha umuhimu wa oparesheni ya kuwaonda barabarani ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya ujenzi wa njia za juu na kuanza kwa usafiri wa mabasi ya kasi Dart ambao hali ilibadilika pale alipotaja Manispaa kuwa na masoko 26 yaliyohodhiwa na viongozi kwa kuingia Mikataba ya kupangisha wakati wamejiagawia bure.

Aidha Mstahiki Meya Boniface Jacob amesema katika kuhakikisha wafanya biashara wadogo wanatengewa maneo yao watafanya uhakiki katika masoko yote kubaini viongozi na watendaji waliojimilikisha na kuwanyang’anya ili masoko yatumiwe na walengwa ikiwa ni hatua ya kuboresha mazingira ya jiji huku mtendaji wa kata ya ubungo Bw. Gilbati Mushi akieleza hatua hiyo kudhirisha utawala bora.

Lulu Michael:Mastaa Bongo Mtaishia Kuchambana Instagram tuu

$
0
0
ZA uso laivu! Staa mwenye mvuto Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amefunguka kuwa mastaa wengi Bongo wataishia kuchambana kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram badala ya kutafuta elimu ili siku moja wapate nyadhifa serikalini.

lulu2342 (1)

Akizungumza na Ijumaa Wikienda, wikiendi iliyopita, Lulu alisema kwamba, amegundua kuwa elimu ndiyo kila kitu hivyo amewasihi mastaa wenzake waache kuchambana na kutuma picha kwenye mitandao ya kijamii badala yake watafute njia ya kujikwamua kielimu.

“Jamani mmemuona mwanamama mwenzetu Dk. Tulia alivyojinyakulia unaibu spika? Hiyo ndiyo raha ya elimu. Mastaa kazi kutukanana kwenye mitandao ya kijamii na kuweka picha, mwisho wenu utakuwa hivyohivyo,” alisema Lulu.


Mch. Peter Msigwa, kwa Mahojiano ya ITV Jana Umechemka

$
0
0
Kama vile amesahu ahadi za Ukawa kutoa elimu bure kuanzia Darasa la kwanza hadi chuo kikuu. Jana Msigwa alipinga vikali swala la elimu bure huku akipata kigugumizi kujibu kwa ufasaha Maswali ya Muandishi wa ITV. Kwa hili kweli kabisa Mimi nimekushusha kabisa kwasababu Muitikio wa elimu bure ni mkubwa sana na kila mtu anafaidi keki ya Taifa kupitia hili la elimu bure na bila shaka ni jambo bora kabisa kumpa mtoto wa kitanzania elimu.

Pili ni kupinga swala ya Kubana matumizi hasa kutotumia hela kwenye sherehe na kuzielekeza kwenye Maendeleo ni jambo jema kabisa kila mtu analisapoti kasoro wewe tu Mtumishi. Magufuli anania ya dhati kuua Siasa za kuropoka ropoka . Zije siasa za watu wabunifu kama Professa J maneno machache vitendo vingi.

By Pascal Ndege

Mtoto Wa Miaka Mitatu Afariki Dunia Papo Hapo Baada Ya Kugongwa Na Gari.

$
0
0
Mtoto wa miaka mitatu aliyefahamika kwa jina la JANET PONSIAN mkazi wa Matemela Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya alifariki dunia papo hapo baada ya kugongwa na Gari yenye namba za usajili T.957 CWJ aina ya Isuzu Journey ikiendeshwa na dereva aliyefahamika kwa jina la ELIABU MYEKO (33) mkazi wa Makambako Mkoa wa Njombe.

Tukio hilo limetokea mnamo tarehe 01.05.2016 majira ya saa 17:45 jioni huko katika Kijiji cha Matemela, Kata ya Ipwani, Tarafa ya Rujewa, Wilaya ya Mbarali, Mkoa wa Mbeya.

Aidha chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi na uzembe wa Dereva wa Gari hilo. Dereva alikimbia mara baada ya tukio na jitihada za kumtafuta kwa kushirikiana na mmiliki wa Gari zinaendelea. Mwili wa marehemu umehifadhiwa Kituo cha Afya Ipwani Wilayani Mbarali kwa uchunguzi wa kitabibu.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi wa Polisi EMANUEL G. LUKULA anatoa wito kwa madereva kuwa makini wanapotumia vyombo vya moto ikiwa ni pamoja na kuzingatia sheria, alama na michoro ya usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika. Aidha anatoa wito kwa yeyote mwenye taarifa zitakazofanikisha kukamatwa kwa dereva huyu azitoe kwa mamlaka husika ili akamatwe.

Katika Misako:
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia mtu mmoja mkazi wa Matemela aliyefahamika kwa jina la HUSSEIN BAKARI (59) baada ya kukutwa na miche 25 ya Bhangi akiwa amepanda kwenye bustani yake ya mbogamboga.

Mtuhumiwa alikamatwa katika msako uliofanyika mnamo tarehe 01.02.2016 majira ya saa 16:00 jioni katika Kijiji cha Mayota, Kata ya Lugelele, Tarafa ya Rujewa, Wilaya ya Mbarali, Mkoa wa Mbeya.

Aidha katika msako mwingine, Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la WILSON PHILIP (19) mwendesha Pikipiki @ bodaboda, mkazi wa Msasani anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya akiwa na Bhangi yenye uzito wa Gram 10.

Mtuhumiwa alikamatwa na askari katika msako uliofanyika mnamo tarehe 01.05.2016 majira ya saa 17:05 jioni huko Mtaa wa msasani, Kata ya Bagamoyo, Tarafa ya Tukuyu Mjini, Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya.

Watuhumiwa watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamiliki.

Imesainiwa na:
(EMANUEL G. LUKULA – ACP)
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Baada ya Kutoka Marekani Mtoto Getrude Clement Akaribishwa Bungeni Leo

$
0
0
Getrude Clement mwenye umri wa miaka 16 ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha tatu anayesoma shule ya Sekondari Mnarani iliyopo jijini Mwanza, leo amepata nafasi ya kufika bungeni Dodoma baada ya kupewa mwaliko wa Serikali

Hivi karibuni Getrude  alihutubia viongozi mbalimbali wa dunia kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa uliohusu mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika New York Marekani ambapo leo Bungeni  amewahimiza Watanzania kutunza mazingira na kufuata maelekezo yanayotolewa na Serikali na wataalamu wa mazingira ili kuyatunza mazingira wanamoishi.

Getrude amesema kuwa amefarijika kwa kuwawakilisha vijana wa Tanzania na dunia kwenye mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi ambapo mataifa 175 yalikutana kusaini makubaliano ya Paris.

Katika kuwahimiza vijana kujenga tabia ya kutunza mazingira, Getrude amewaasa vijana hasa wanafunzi kusimamia suala la utunzaji wa mazingira wakiwa shuleni kwa kwa kujiunga na klabu mbalimbali ambapo yeye amejiunga na klabu ya “Mali Hai” iliyopo shuleni anaposoma.

Kwa upande wa Watanzania kwa ujumla kwenye utunzaji wa mazingira, Getrude amesema kuwa ni vema wajifunze kutoka mataifa mengine yanavyosimamia utunzaji wa mazingira hasa matumizi ya mifuko ya plastiki.

Mwanafunzi huyo amekaribishwa na kutambulishwa kwa wabunge leo mjini Dodoma kwa heshima ya kuliwakilisha vema taifa wakati wa utiaji saini makubaliano ya namna ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki moon alimkaribisha Getrude kwa viongozi hao na kusema “Ni furaha yangu kumualika Getrude Clement ambaye pia ni mwakilishi wa vijana anayeishi Tanzania na anaziwakilisha sauti za vijana”.

Waziri Makamba Awasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.

$
0
0
Serikali inaendelea kusimamia mazingira na kuhakikisha mifuko ya plastiki inayotumika nchini iwe ni ile inayokidhi viwango vianavyokubalika ili kuondokana na changamoto ya kuzagaa kwa mifuko hiyo katika maeneo mbalimbali.

Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano January Makamba alipokuwa akitoa hoja ya wizara yake kuidhinishiwa maombi ya fedha kwa mwaka wa fedha 2016/2017.

Makamba amesema kuwa sababu kubwa ya kusambaa kwa mifuko ya plastiki inatokana na mifuko hiyo kutolewa bure na hivyo kuchafua mandhari na kuziba mifereji sehemu mbalimbali hali inayosababisha athari kubwa katika mazingira.

“Asilimia kubwa kwenye mito, maziwa na fukwe za bahari imejaa mifuko ya plastiki, hali hii ni hari kwa usalama wa mazingira yetu” alisema Makamba.

Akiwasilisha hotuba yake, Waziri Makamba amesisitiza kuwa mifuko ya plastiki isiyotakiwa kutumika nchini ni ile yenye unene chini ya maikroni 50 ambayo hairuhusiwi kuzalishwa wala kuingizwa.

Kwa mujibu wa maelekezo ya bajeti ya mwaka wa fedha 2015/2016, Waziri huyo amesema kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais imekamilisha kanuni mpya ya mifuko ya plastiki zinazorekebisha viwango vya unene unaoruhusiwa kutoka Maikroni 30 kwenda Maikroni 50.

Waziri Makamba amesema kuwa kanuni hizo tayari zimesainiwa kupitia tangazo la Serikali Na.271 la mwaka 2015 na kutolewa katika Gazeti la Serikali Julai 17, 2015 na kupewa Na. 29.

Mose Iyobo: Mimi na Aunt tupo sawa, akanusha Aunt Ezekiel kuchepuka

$
0
0
Baada ya kuzagaa tetesi kwenye mitandao ya kijamii kuwa dansa wa Diamond, Mose Iyobo na mama mtoto wake Aunt Ezekiel, wameachana na kila mtu anaishi kwake, Mose amefunguka na kusema mahusiano yao yapo salama kabisa.

Akizungumza na Bongo5 Jumamosi hii, Mose alisema habari za kwamba ameachana na Aunt Ezekieli kisa Aunt amechepuka sio za kweli.

“Hivi vitu naviona na najua ni vitu vya kuzusha tu, mimi na mama Cookie tupo vizuri na hatuja kwaruzana. Kwa hiyo hivyo vitu sio vya kweli na wala hatujaachana,” alisema Mose.

“Kugombana tunagombana, ni vitu vidogo vigogo vya ndani ya nyumba. Pia nilisikia sisi tumeachana kila mtu anaishi kwake, sio kweli, kipindi hicho mimi nilisafiri sasa walivyokuwa wanamuona yupo peke yake, ndio wakazusha hivyo,” aliongeza.

Mose amesema hizi tetesi hazimuumizi kichwa kwa kuwa tayari anajua sio vitu vya kweli.

Masoud Kipanya Aitaja Sababu iliyomrudisha Clouds FM

$
0
0
Masoud Kipanya amerejea tena Clouds FM baada ya miaka minane kuondoka. Mchoraji huyo maarufu wa katuni ya Kipanya, anasikika kwenye kipindi cha Power Breakfast.

“Sijui kama unajua kuwa mimi Clouds nilifukuzagwa kazi! Msingi wa kutoka Clouds ni kwamba sikutoka kwasababu nilikuwa labda niko hivi hapana, tulikuwa tunafanya kazi zetu kama kawaida baadaye kuna mambo yaliyotokea tukaonekana [Yeye na Fina Mango] ni watovu wa nidhamu tukafukuzwa,” alisema Masoud kwenye kipindi cha Danga Chee cha Channel Ten.
“Kwahiyo I was fired, nilifukuzwa kazi. Sasa miaka minane baadaye watu hao hao wakikuapproach kufanya nao kazi kwa terms ambazo mnakaa chini sasa kama watu wazima, watu ambao wanaona kabisa kwamba miaka minane umekaa bila wao na ya kwako yanakuendea. Kwanza hapo kuna heshima kubwa sana, katika hali ya kawaida nilitakiwa niwe nimeshadondoka, sipo, sifai, siwezekani tena. Lakini kama watu wamekuona kwamba unahitajika kwenye ile sehemu ni kipimo kingine cha kuonesha kwamba ‘okay kumbe kitendo cha kubaki kwenye media kama mchoraji katuni thamani iko pale,” aliongeza.

“Lakini namba mbili ni kwamba ninapofuatwa nirudi Clouds, tumekaa mezani tumezungumzia masuala ya mkwanja wa kutosha, wakati huo huo project zangu zote hakuna hata moja inayovunjika, kuna tatizo gani mimi kutengeneza extra money katika masaa matatu au masaa manne?”

Donald Trump Asema Uchina “inaibaka” Marekani

$
0
0
Mgombea mkuu wa chama cha Republican Donald Trump ameshutumu Uchina na kusema imekuwa “ikiibaka” Marekani kupitia sera zake za kibiashara.

Ameambia watu waliohudhuria mkutano wa kisiasa Indiana kwamba Uchina imekuwa ikitekeleza “wizi mkubwa zaidi kuwani kutekelezwa katika historia ya dunia.”

Bw Trump, mfanyabiashara tajiri kutoka New York, amekuwa akiituhumu Uchina kwa kuchezea sarafu yake ili kuwa na ushindani wa kibiashara duniani inapouza bidhaa nje ya nchi.

Hilo, amesema, limeathiri sana wafanyabiashara na wafanyakazi wa Marekani.

“Hatuwezi kuruhusu Uchina iendelee kuibaka nchi yetu, na hilo ndilo tunafanya (kwa wakati huu),” alisema mkutanoni Jumapili.

"Tutabadilisha mambo, na tuna uwezo, msisahau. Tuna nguvu sana dhidi ya Uchina.”

Katika manifesto yake ya kampeni, Bw Trump ameahidi kufanikisha mkataba bora wa kibiashara baina ya Uchina na Marekani ambao utawezesha “wafanyabiashara na wafanyakazi kutoka Marekani kuweza kushindana”.

Obama: Trump haelewi sera za kigeni

Ametaja malengo manne ambayo yanahusisha kutangaza Uchina kuwa taifa linalochezea sarafu yake na kusitisha utoaji wa nafuu za wafanyabiashara wanaouza bidhaa nje ya nchi ambazo anasema ni haramu.

Aidha, anaitaka Uchina kufikisha kikomo mfumo duni wa masharti ya leba na uhifadhi wa mazingira.


Takwimu za karibuni zaidi kutoka kwa serikali ya Marekani zinaonesha pengo la kibiashara baina ya Uchina na Marekani lilipanda na kufikia $365.7bn (£250.1bn) mwaka jana. Kufikia Februari mwaka huu, pengo hilo lilikuwa limefika $57bn tayari.

Hii ni mara ya kwanza kwa Trump kutumia neno “ubakaji” akizungumzia biashara na Uchina, lakini amejulikana kwa kutumia maneno makali kwenye kampeni yake.

Alikabiliwa na mamia ya waandamanaji jimbo la California Ijumaa kabla yake kutoa hotuba katika mkutano wa chama cha Republican Ijumaa.

Alilazimika kutumia mlango wa nyuma kuingia.

Waziri mkuu wa Uchina Li Keqiang amesema Wachina wanafuatilia kwa karibu uchaguzi nchini Marekani.

Hata hivyo anasema wengi wanamtazama Bw Trump kama mtu wa kuenziwa badala ya adui.

Je Zari na Aliyekuwa Mumewe Ivan Wamerudiana? Hizi Picha zazua Utata Mkubwa Huko Insta

$
0
0
Huku Instagram picha hizo mbili zimekuwa gumzo leo baada ya Mama mtoto wa Diamond kwasasa Zari Hassan na aliyekuwa mumewe Ivan Kuonekana wamepiga picha sehemu moja inayofanana kwenye sehemu ya kuogelea..Picha hizi zimeleta wasiwasi kuwa huenda wawili hao walikuwa pamoja wakiogelea huku wengine wakimtetea Zari na kusema kuwa yeye alikuwa hiyo sehemu siku nyingi lakini Ivan ameenda sehemu hiyo hiyo na kupiga picha na kuzitupia mtandaoni leo kumuumiza Diamod  na kuwapa watu cha kuongea

Bora Ukimwi Kuliko Kutumia Dawa za Kulevya-Ferooz

$
0
0
Msanii wa kizazi kipya Ferooz amefunguka na kusema ni bora mtu apate virus vya Ukimwi kuliko kutumia madawa ya kulevya kwani anadai mtu akitumia dawa za kulevya mwisho wake ni kuaibika na kushindwa kufanya mambo ya msingi katika jamii.


Akizungumza kwenye kipindi cha eNewz Ferooz alidai kuwa yeye anaona ni bora mtu apate Ukimwi kwani itawezekana mtu huyo kuishi kwa matumaini, huku akiendelea kufanya mambo yake ya msingi katika jamii na kudai tofauti na mtumiaji wa dawa za kulevya kwani hataweza kufanya jambo lolote la maendeleo.

“Madawa ya kulevya ni zaidi ya kupata HIV, ni mara kumi upate Ukimwi kuliko ukiwa unatumia madawa ya kulevya, sababu Ukimwi unaweza kuishi kwa matumaini na ukatumia madawa za ARVs ukaishi miaka mingi ukadumu,lakini madawa ya kulevya utaadhirika na hautafanya kitu chochote katika maisha yaani utakuwa ‘nothing’ (bure) katika maisha, kwa hiyo ni tatizo baya zaidi hivyo madawa ya kulevya si ya kuyasogelea kabisa,” alisema Ferooz.

Mbali na hilo Ferooz alieleza kuwa wasanii wengi wanajikuta wanaingi kwenye matumizi ya madawa ya kulevya kutokana na msongo wa mawazo kwa kazi zao kutochezwa kwenye vyombo vya habari na kazi hizo kutopokelewa vyema na mashabiki jambo ambalo linawapelekea kuwaza sana hivyo wengine wanaona njia ya kupunguza mawazo hayo ni kunywa viroba kama si kwenda kutumia dawa za kulevya

Mahakama ya Kisutu Yatoa Hati ya Kukamatwa kwa Meya wa Kinondoni, Boniface Jacob

$
0
0
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar imetoa hati ya kukamatwa kwa Meya wa Kinondoni, Boniface Jacob (Pichani)kutokana na kutofika mahakamani.

Meya huyo anakabiliwa na shitaka la kumshambulia  mwandishi wa Habari wa gazeti la Uhuru, Christopher Lissa na kumsababishia maumivu makali.

Kesi hiyo jana ililetwa mbele ya Hakimu Mkazi Hellen Riwa kwa ajili ya usikilizwaji ambapo upande wa mashitaka ulikuwa na shahidi mmoja.

Wakili wa serikali Onolina Mushi alidai kwamba,kesi hiyo ililetwa kusikilizwa lakini mshitakiwa pamoja na wakili wake hawajafika mahakamani.

Kutokana na hali hiyo,aliiomba mahakama itoe hati ya kukamatwa kwa mshitakiwa huyo pamoja na kupanga tarehe nyingine ya kuendelea kusikiliza shauri hilo.

Hakimu alikubali maombi hayo ikiwemo ya kutolewa hati ya kukamatwa kwa Meya huyo.Kesi hiyo iliahirishwa hadi Mei 23 mwaka huu kwa ajili ya usikilizwaji.

Katika kesi hiyo,Boniface anadaiwa kutenda kosa hilo  Septemba 11, mwaka jana, maeneo ya Kinondoni, Dar es Salaam, kipindi hicho akiwa na cheo cha Udiwani kata ya Ubungo.
Ilidaiwa kwamba,mshitakiwa huyo alimpiga Lissa kwa mateke na ngumi sehemu mbalimbali za mwili wake na kumsababishia majeraha makali.

Shitaka la pili ilidaiwa kwamba ,mshitakiwa huyo katika tarehe hiyo kwa makusudi na kinyume cha sheria aliharibu kamera aina ya Nicon yenye thamani ya sh. milioni nane mali ya Kampuni ya Uhuru Publication Limited.
Viewing all 104776 articles
Browse latest View live




Latest Images