Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104429 articles
Browse latest View live

Chama cha Wasiomwamini Mungu Chapigwa Marufuku

0
0
Wakenya wasiomwabudu Mungu walipata pigo Jumamosi baada ya Mwanasheria Mkuu, Prof Githu Muigai kuharamisha chama chao.

Hatua hiyo ilitokea siku moja tu baada ya viongozi wa kidini kutoa wito kwa Prof Muigai kujiuzulu kwa kusajili muungano huo mwanzoni mwa mwezi Aprili.

Kwenye taarifa iliyotolewa na afisi ya Mwanasheria Mkuu, hatua ya kufutilia mbali muungano huo ilitokana na malalamishi mengi ambayo yalikuwa yanatolewa na mashirika tofauti mbali na viongozi wa kidini.

“Kutokana na kupokewa kwa maoni mbalimbali katika Afisi ya Mwanasheria Mkuu kutoka kwa viongozi mbalimbali wa dini na mashirika mengine kuhusu kusajiliwa kwa Chama cha Wasioamini Mungu cha Kenya, Mwanasheria Mkuu ameagiza Msajili wa Vyama vya Kijamii afutilie mbali mara moja usajili huo,” ikasema taarifa hiyo.

Iliongeza kuwa uamuzi umetolewa kwa msingi wa Ibara 12(1)(b) ya sheria ya vyama vya kijamii hadi wakati Mahakama ya Juu itakapoamua kuhusu uhalali wa chama hicho na ikiwa kinalingana na katiba.

Viongozi wa kidini Ijumaa walimtaka Prof Muigai ajiuzulu, huku wakisema usajili wa chama hicho ulikiuka katiba.
Kulingana na Muungano wa Kitaifa wa Makanisa ya Kipentekosti (KNCPCM), katiba inatambua ukuu wa Mungu kwa hivyo ni kinyume kusajili chama cha wasioamini Mungu.

Naibu mwenyekiti wa muungano huo Askofu Stephen Ndichu alisema Mwanasheria Mkuu hataki kutambua masuala ya dini humu nchini.

Shinikizo
“Tunatamka Mwanasheria mkuu afutilie mbali usajili wa chama hicho la sivyo tutaenda kortini kutaka kifutiliwe mbali kwa kuwa kilisajiliwa kinyume na sheria,” akasema Bw Ndichu.

Viongoi hao wa dini walikuwa wamepanga kuleta pamoja waumini wa dini tofauti wakiwemo Waislamu na Wahindi ili waungane kufanya maandamano makubwa kulalamikia hatua ya kusajiliwa kwa chama hicho.

Chama cha wasiomwamini mungu kilisajiliwa Februari 17, kisha cheti kikatolewa rasmi kwa mwenyekiti wao Bw Harrison Mumia Aprili 7.

Wakati huo, Bw Mumia alisifu hatua hiyo na kusema ilikuwa hatua nzuri ya kuhakikisha serikali inatambua Wakenya wote kwa kiwango sawa licha ya imani yao.

Jack Wolper Awapa Suprise Mashabiki Wake Kwa Picha Hizi za Ujauzito

0
0
 Zikiwa zimepita siku kadhaa toka Jack Wolper atupe somo la mapenzi kipindi hichi cha baridi leo amewapa Suprise Mashabiki Wake Kwa Picha Hizi za Ujauzito , Jack Wolper inasemekana kwa sasa yupo South Africa na Mkongo Man....Hongera Jack 

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumanne ya May 3, Ikiwemo ya Diamond Kulishwa Sumu

Aliyejifungua Watoto 3 Anaomba Asaidiwe kwani naye ni Mgonjwa wa Pumu

0
0
MKAZI wa Kijiji cha Mapinduzi Kata ya Kigwe Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma Julietha Sokoine (24) amejifungua watoto wa watatu na ameiomba serikali, taasisi,mashirika na watu binafsi kumpatia msaada wa kifedha utakaomsaidia kuwatunza watoto hao.

Pia alisema msaada huo pia utamuwezesha kupata tiba ya ugonjwa wa pumu ambao umemsababisha kuvimba mwili wote.

Akizungumza mwishoni mwa wiki, Sokoine ameiomba jamii kumsaidia kutokana na kukabiliwa na tatizo la ugonjwa wa pumu ambao pia umesababisha kuwa na hali ngumu ya kimaisha ambayo inamfanya kushindwa kuwatunza vizuri watoto wake.

Alisema watoto hao, Daniel Sokoine,David Sokoine na Davis Sokoine walizaliwa kwa pamoja Machi 22, mwaka huu katika hospitali ya mkoa wa Dodoma huku kati ya wawili wa wakiwa na uzito kilo mbili na nusu na wa mwisho kilo mbili.

“Hali yangu siyo mzuri kutokana na mimi mwenyewe kukabiliwa na tatizo la ugonjwa wa pumu,ambapo wakati mwingine nalazimika kuwanywesha maziwa ya ngombe watoto hao pindi ninapozidiwa na ugonjwa huo”alisema .

Kwa upande wake baba wa watoto hao Sokoine Chipanta alisema pamoja na juhudi za kilimo hata hivyo mazao  yake yalinyauka na jua.

Alisema kutokana na hali hiyo analazimika kutafuta vibarua ili kuweza kupata fedha kwa ajili ya kununua chakula pamoja na matunzo ya watoto hao.

Alisema kwa wale wote watakaoguswa na kuamua kumpa msaada wawasiliane naye kwa namba ya simu +255 652 744 510.

LEAKED: Ngoma mpya ya Harmonize & Raymond ‘Penzi’, unaweza kuisikiliza hapa

0
0
Wakati ngoma za ‘Bado’ ya Harmonize ft Diamond inaendelea kufanya vizuri na ‘Kwetu’ ya Raymond inaendelea kufanya vizuri, leo Mei 2 2016 Harmonize na Raymond wameingia kwenye headlines baada ya ngoma yao waliofanya pamoja ya ‘Penzi’ kuvuja, millardayo.com imeinasa na kukusogezea track hiyo:

Wasafi Wadaiwa Kumpora Producer Frag Ngoma ya 'Bado' iliyoibwa na Harmonize Feat. Diamond

0
0
Producer Frag kutoka Uptown Music ametumbua jipu baada ya kuibuka na kusema kuwa yeye ndiye aliyetengeneza wimbo wa Bado wa Harmonize na Diamond.

Frag aliiambia Enewz kuwa pamoja na kazi kubwa aliyoifanya kuhakikisha ngoma hiyo inakuwa poa lakini bado WCB wakamzima na hawakumlipa hata senti tano na kuambulia elfu thelathini pekee ya nauli.

“Kawaida nikifanya kazi uptown music lazima saini zangu ziwepo lakini kwa kule wasafi saini zangu hazikuwekwa, na sijajua kwasababu gani hazikuwekwa wangeweka tu ata ile saini ya jina langu ili kunitengezea heshima kwa watu wengine ”, alisema Frag.

Punguzo Kodi ya Mishahara Kwa Wafanya Kazi Laibua Mapya

0
0
Uamuzi wa Rais John Magufuli kupunguza asilimia mbili ya Kodi ya Mshahara (PAYE) umeibua mjadala baada ya kubainika kuwa utampa nafuu ndogo mfanyakazi, huku wachambuzi wakihamia kwenye kodi nyingine ya mapato kwa kuzingatia viwango vya mishahara.

Baadhi ya wadau wanapendekeza kodi hiyo, inayoitwa excess charge, ipunguzwe kumpa unafuu mfanyakazi, huku wengine wakishauri kuweka nguvu kwenye uchumi wa viwanda na kilimo na baadhi wakishauri juhudi zifanyike kudhibiti mfumuko wa bei ili mshahara utosheleze mahitaji ya mfanyakazi.

Baadhi ya wadau wanapendekeza kodi hiyo, inayoitwa excess charge, ipunguzwe kumpa unafuu mfanyakazi, huku wengine wakishauri kuweka nguvu kwenye uchumi wa viwanda na kilimo na baadhi wakishauri juhudi zifanyike kudhibiti mfumuko wa bei, ili mshahara utosheleze mahitaji ya mfanyakazi.

Juzi katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, Rais alitangaza kupunguza kodi ya PAYE kutoka asilimia 11 hadi tisa, lakini kwa mujibu wa wahasibu uamuzi huo ni punguzo la Sh1,100 kwa wafanyakazi wa mshahara wa kima cha chini na Sh3,800 kwa mshahara unaoanzia Sh360,000 na kwenda juu.

Akifafanua kuhusu PAYE, mkurugenzi wa huduma na elimu kwa mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Richard Kayombo alisema kiwango cha mapato kisichozidi Sh170,000 hakina kodi, lakini mapato ya kati ya Sh170,000 hadi 360,000 yalikuwa yanakatwa asilimia 11 na hivyo sasa yatakatwa asilimia tisa.

Alisema mapato yanayoanzia Sh360,000 hadi 540,000 hukatwa PAYE pamoja na asilimia 20 ya excess charges, wakati mshahara unaozidi Sh540,000 hukatwa PAYE pamoja na asilimia 25 ya makato ya excess charges.

Suala hilo pia lilizungumzwa na mchambuzi wa masuala ya kijamii na kisiasa, Godlisen Malisa katika waraka alioutuma kwenye mtandao kuchambua punguzo hilo la Rais Magufuli.

Malisa alionyesha kushangazwa na kitendo cha baadhi ya watu kusifu punguzo hilo, wakiwamo wabunge wa upinzani.

“Kama Rais angepunguza excess charges, angalau zikafika 10% kutoka 30% ziliko sasa, ingekua na maana kubwa sana kuliko kupunguza PAYE,” anasema Malisa katika waraka huo.

“Kwa kifupi ni kuwa punguzo hilo litawanufaisha zaidi wenye mishahara chini ya 720,000/= lakini kwa wanaolipwa zaidi ya hapo hakuna benefit (manufaa) yoyote. Hata hao wanaolipwa chini 720,000/= bado watanufaika kidogo sana.”

Alidai kwamba kama kuna mbunge yeyote anayeshangilia punguzo ni wazi kuwa hajui hesabu, hivyo anatakiwa kukumbushwa ili aelewe kuwa kupunguza PAYE wakati makato yanayozingatia viwango vya mishahara yako palepale, ni kiini macho.

“Yaani Rais JPM alichofanya ni kutulazimisha tukatae ongezeko la mshahara,” anasema.

Alisema ni kweli wapinzani waliomba PAYE ipunguzwe tangu mwaka 2011 kwamba isomeke kwa tarakimu moja na ndivyo alivyoahidi JPM, lakini pia walishauri kuwa gharama za makato hayo ya zaidi yalingane.

“Nimeamua kusema hivi maana naona wabunge wengi wa (vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi) Ukawa wanacheza ngoma ya Magufuli. Wanaanza kujitapa (kwamba) upinzani tulishauri jambo hili tangu mwaka 2011,” anasema.

“Wengine wanapiga picha hadi hotuba ya kambi ya upinzani iliyozungumzia jambo hilo. Waambieni wakae kimya na wasiendelee kuongea vitu wasivyovijua.”

Mtaalamu wa masuala ya kodi, Dk Mariam Nchimbi alisema kiwango cha mshahara kingepandishwa ni wazi kingesaidia wengi kujipanga vyema, ikiwa ni pamoja na kuendelea kulipa kodi zinazostahili.

“Ni wazi kwamba kwa hatua hiyo ya Rais imewasaidia kwa kiasi fulani wale wanaolipwa mishahara ya kiwango cha kati, lakini wale wa kiwango cha juu pia walipaswa kupunguziwa japo kwa asilimia 28 badala ya 35 inayokatwa sasa,” alisema.

Lakini wachambuzi wengine waligeukia suala la kukuza uchumi wakisema ndilo litakalosaidia mfanyakazi kunufaika na mshahara wake.

Profesa Humphrey Moshi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) alisema mshahara wenye nafuu kwa maisha ya wafanyakazi wengi utapatikana kutokana na uwepo wa viwanda vya kutosha pamoja na kilimo kuimarishwa.

“Kuna mambo mengi ya kuangalia ili mfanyakazi awe na mshahara ambao unampa unafuu wa maisha,” alisema Profesa Moshi.

“Pato la Taifa linahusika kwa kiasi kikubwa, hivyo kama litajengewa mazingira ya kukua, itakuwa vyema. Inatakiwa viwanda vichangie pato hilo kwa asilimia 25 na si asilimia nane kama ilivyo sasa.”

Alisema anaamini baadhi ya viwanda hivyo vitakuwa vya kusindika mazao, kutakuwa na kilimo cha biashara ambacho kitaongeza tija.

“Ninaamini kuwa mbali na maeneo hayo, viwanda vingine vingi vinaweza kuendelezwa kama vya usindikaji mazao ya kilimo na uzalishaji ,” alisema.

Alisema kwa upande wa Serikali mshahara wenye nafuu ya maisha kwa watumishi wake unapaswa kujengewa mazingira labda kwa kuweka idara maalumu ambayo inaangalia viwango vya mishahara.

“Kwa ilivyo sasa ni wazi kuna watumishi ambao wananufaika kama alivyowahi kueleza Rais. Yaani watu wanalipwa mishahara kama wapo Ulaya. Sasa mfano unaweza kukuta mtu kaajiriwa hapa UDSM ni msomi kwa viwango, lakini analipwa Sh3 milioni wakati mwenye digrii aliye Benki Kuu analipwa Sh6 milioni,” alisema.

Profesa Moshi alihoji kwa viwango hivyo viwili tofauti, nini kimetumika kuamua mwenye elimu kubwa alipwe kidogo na mwenye elimu ndogo alipwe zaidi.

Alisisitiza kuwa Serikali inapaswa kuzibana bodi za taasisi zake ambazo zimejijengea mazingira ya kulipa mishahara ya mamilioni ya fedha bila kujali hali ya nchi kwa ujumla.

Msomi mwingine, Dk Ulingeta Mbamba kutoka Shule ya Biashara ya UDSM, alisema Serikali inabidi idhibiti mfumuko wa bei.

“Ni wazi kwamba hata kama Serikali itaongeza mshahara, bidhaa zikawa zinapandishwa kiholela, hakuna siku kiwango cha mshahara kinaweza kutosheleza maisha ya watumishi,” alisema.


Siri Kuu Kuhusu Escrow zafichuka

0
0
SIRI kuu ya James Rugemalira, kumwaga mabilioni ya shilingi kwa baadhi ya majaji wa mahakama kuu, viongozi waandamizi serikalini na madhehebu ya kidini, wabunge na viogogo wa Ikulu, zimeanza kufumuka.

Nyaraka mikononi mwa gazeti hili zinaonesha zaidi ya asilimia 90 ya wale waliopewa fedha na Rugemalira, ni wale waliomsaidia “kufanikisha ukwapuaji wa zaidi ya Sh. 324 bilioni kutoka Benki Kuu (BoT) na kujinasua katika mikono ya sheria.”

“Rugemalira alishika kila mmoja. Kuanzia Ikulu ya Jakaya Kikwete, TAKUKURU, mahakama, BoT, hazina, ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali, viongozi wa madhehebu ya kidini na hata baadhi ya mawaziri wa zamani wenye ushawishi serikalini,” ameeleza kiongozi mmoja mwandamizi kutoka Ikulu.

Amesema, “…fedha katika akaunti ya Escrow zilihusisha mtandao mpana ulioratibiwa na Rugemalira na Harbinder Sigh Seth (Singasinga).”

Majaji wa mahakama kuu, Aloycious Mujulizi na Eudeus Ruhangisa, ni miongoni mwa waliokuwa na mawasiliano ya mara kwa mara na Rugemalira; na walikuwa washauri wake wakuu wa kisheria.

Mawasiliano kati ya Jaji Mujulizi na Jaji Ruhangisa yalifanyika kupitia kwa Rugemalira mwenywe na katika eneo jingine kupitia kwa mkewe, Benedicta.

Jaji Mujulizi na Jaji Ruhangisa walitajwa bungeni na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), kuwa miongoni mwa vigogo waliopewa mgawo wa fedha hizo na Rugemalira.

Bunge liliagiza majaji hao wachunguzwe na wachukuliwe hatua za kinidhamu na kisheria.

Hadi sasa, hakuna taarifa zozote kuwa majaji walichunguzwa na kuchukuliwa hatua.

Rugemalira alikuwa akimiliki asilimia 30 ya hisa katika kampuni ya kigeni ya IPTL kupitia kampuni yake ya VIP Engineering and Marketing Limited.

Jaji Mujulizi na Ruhangisa walilipwa na Rugemalira kila mmoja Sh. 404 milioni.

Mabilioni ya shilingi yaliyohifadhiwa katika akaunti ya Escrow yalikwapuliwa na Harbinder Sigh Seth, aliyejiita mmiliki wa IPTL kwa msaada mkubwa wa Rugemalira na kile kilichoitwa, “amri ya mahakama.”

Seth alidai kumiliki IPTL kupitia kampuni yake ya Pan African Power Tanzania Limited (PAP).

MwanaHALISI linaweza kuthibitisha kuwa kati ya tarehe 13 na 26 Novemba 2014, kilikuwa kipindi ambacho Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), ilimhoji Rugemalira juu ya ukwapuaji wa fedha katika akaunti ya Escrow.

Aidha, ni katika kipindi hichohicho, Rugemalira alikuwa na mawasiliano ya mara kwa mara na Jaji Mujulizi na Ruhangisa.

Wengine waliokuwa na mawasiliano na Rugemalira katika kipindi hicho, ni waziri wa nishati na madini, Prof. Sospeter Muhongo; aliyekuwa waziri wa mambo ya nje na uhusiano wa kimataifa, Bernard Membe na aliyekuwa katibu mkuu wa wizara hiyo, Eliakimu Maswi.

Aliyepata kuwa waziri wa utawala bora, Mathias Chakawe; aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU, Edward Hoseah; aliyekuwa mwanasheria mkuu wa serikali (AG), Frederick Werema na aliyekuwa waziri wa viwanda na biashara, Dk. Abdallah Kigoda, walikuwa pia na mawasiliano na Rugelalira.

Wengine ni naibu gavana wa BoT, Dk. Enos Bukuku; aliyekuwa Mnikulu Mkuu wa Ikulu, Shaban Gurumo; aliyekuwa Kamishna mkuu mamlaka ya mapato (TRA), Rished Bade na aliyekuwa mwanasheria mkuu wa serikali wakati wa ujio wa IPTL nchini (1994), Andrew Chenge.

Orodha ya waliokuwa katika mawasiliano na Rugemalira inahusisha pia mawaziri wa zamani, Paul Kimiti na Wilson Masilingi; aliyekuwa mhariri mtendaji wa magazeti ya serikali – Daily News na Habari Leo – Gabriel Nderumaki; aliyewahi kuwa waziri wa nishati na madini, Wiliam Ngeleja na mkurugenzi wa kampuni ya G and S Consultancy Limited, Dk. Gideon Shoo.

Wengine ni aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Kagera, Kanali mstaafu Constantine Massawe; Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba, Methodius Kilain; Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Eusebius Nzigilwa na aliyekuwa waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi, Prof. Anna Tibaijuka.

Prof. Tibaijuka alikiri kupokea kiasi cha Sh. 1.6 bilioni kutoka kwa Rugemalira. Hata hivyo, alisema kuwa fedha ambazo alipokea zilikuwa ni mchango wa shule yake ya Barbro Johanssen ya jijini Dar es Salaam na Kajumulo Girls High School iliyoko Bukoba.

Kwa mujibu wa taarifa, Dk. Hoseah alimruhusu Rugemalira kutafuta msaada popote pale, ikiwa ni pamoja na nje ya nchi na kwamba ofisi yake “ingetoa maofisa kumsaidia.”

“Kama una jambo la msingi kufanya nje ya nchi, una baraka zangu zote. Watakapohitajika maofisa wa TAKUKURU kwa ufafanuzi, wako tayari kukusaidia pale uliko,” anaeleza Dk. Hoseah na Rugemalira andishi lake la 16 Novemba 2014.

Dk. Hoseah anamaliza kwa kumueleza Rugemalira, “…nakutakia kila la kheri.”

Rugemalira alikuwa anaomba TAKUKURU kuingilia kati kile kinachoitwa, “mgogoro wa hisa kati ya IPTL na Benki ya Standard Chartered (SCB) ya Uingereza.”

Hata hivyo, Rugemalira anaonywa na Masilingi, ambaye wakati huo alikuwa balozi wa Tanzania nchini Uholanzi, kuwa mwangalifu na mtulivu wakati suala hilo linaendelea.

Alisema, “mimi nikiwa mwanasheria, ninakushauri wewe na kampuni yako kushirikiana kwa ukamilifu na TAKUKURU. Suala la IPTL ni gumu. Limekuwa na mchanganyiko mkubwa. Akili nyingine haziwezi kulielewa.”

Masilingi anasema, “…nimebaini kwamba TAKUKURU ndio wanaolichukulia suala hilo kwa usiri mkubwa katika hatua za uchunguzi na wenyewe wanaweza kukusaidia kupata hukumu iliyo ya haki.”

Benki ya Standard Chartered ilikuwa inadai na mpaka sasa bado inadai kuwa mitambo ya kuzalisha umeme ya IPTL na fedha zilizopo kwenye akaunti ya Escrow, ni mali yake.

Inadai kuwa kampuni ya MECHMAR ya Malasia ilishindwa kurejesha mkopo iliochukua benki na kwamba hilo ni jambo linalosababisha mitambo ya IPTL iliyopo Tegeta Salasala, jijini Dar es Salaam, kuwa mali yake.

Akihutubia taifa kupitia wazee wa mkoa wa Dar es Salaam, wiki tatu baada ya Bunge kuagiza waliohusika katika wizi wa fedha za Escrow wachukuliwe hatua, aliyekuwa Rais wa Jamhuri, Jakaya Mrisho Kikwete alikiri kuwapo udanganyifu katika kufikia utoaji wa fedha hizo.

Alikiri baadhi ya nyaraka kughushiwa. Akakiri kuwa kampuni ya PAP imekwepa kodi ya serikali na kudai kuwa serikali yake bado inaendelea kuitafuta kampuni ya MECHMAR iliyodaiwa kuuza asimia 70 ya hisa zake ndani ya IPTL.

Rais alikiri kuwa aliyepewa fedha na serikali – PAP – hakuwa na sifa; serikali yake haikufanya uchunguzi yakinifu kuhusu historia, uhalali, sifa na uwezo wa kampuni ya PAP katika uwekezaji wa umeme, ununuzi wa mitambo na mtaji.

Naye mwanasheria wa Rugemalira, Camilo Schutte, katika barua aliyomwandikia Rugemalira, anasema “…baada ya kusoma ushauri wa Masilingi juu ya msaada wa TAKUKURU, itakuwa busara kuomba TAKUKURU kusubiri hukumu kati ya Standard Chartered na IPTL.”

Anasema kampuni ya Rugemalira (VIP) “…inapaswa kuomba TAKUKURU kufanya uchunguzi juu ya sera ya benki ya Standard Chartered kuhusu ununuzi wa madeni ambayo mchakato wake unaweza kuwa na rushwa.”

Camilo Schutte anamueleza Rugemalira katika barua yake hiyo na ambayo imenakiriwa kwa majaji, mawaziri, kiongozi wa TAKUKURU, maofisa wa Ikulu na watu wengine kuwa, “…tatizo la benki ya Standard Chartered, kama zilivyo taasisi nyingine, ni kufanya biashara ili kujipatia faida kubwa.”

Akiandika kwa Dk. Gideon Shoo, mwanasheria wa Rugemalira (Camilo Schutte) anaelekeza kufanyika mambo matatu kwa haraka.

Kwanza kutafuta, kwa “gharama yoyote ile,” watu wote wenye ushawishi mkubwa kwenye jamii ambao wanapigia kelele ukwapuaji wa fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow.

Miongoni mwa waliotajwa, ni Zitto Kabwe, mbunge wa sasa wa Kigoma Mjini; David Kafulila, ambaye alikuwa mbunge wa Kigoma Kusini; Balozi wa Uingereza nchini, Dianna Melrose; Wilson Masilingi na balozi wa Finland nchini.

Pili, Camilo Schutte anasema, ni sharti mtandao wao ujiridhishe ikiwa watu wanaolizungumzia jambo hilo wanalifahamu kwa undani au wanalijua nusunusu au hawalijui kabisa.

Kwa maoni ya mwanasheria wa Rugemalira, wabunge waliokuwa wameshupalia jambo hilo walikuwa hawana taarifa zozote muhimu kuhusu suala hilo.

Tatu, mwanasheria alimtaka Dk. Shoo kuangalia athari za taarifa zilizosambazwa juu ya ukwapuaji wa fedha hizo, kwa kampuni ya IPTL na Rugemalira binafsi.

“Baada ya kukamilisha haya, naomba unijulishe haraka ili tuweze kupanga mikakati ya kukabiliana na kila tatizo nililolitaja hapo juu,” anaeleza Camilo Schutte.

Kupatikana kwa mawasiliano haya kumekuja mwaka mmoja na nusu baada ya mabilioni ya shilingi kukwapuliwa BoT; na Bunge kuelekeza serikali kufanya uchunguzi.

Aidha, kupatikana kwa taarifa kuwa Rugemalira alikuwa na mawasiliano ya karibu na “kindungu” na mkuu wa TAKUKURU, kumekuja wakati ambapo taasisi hiyo imeshindwa kuanika orodha ya watu walionufaika na mgawo wa fedha hizo kutoka benki ya Stanbic.

Bunge liliagiza serikali kufikisha mahakamani watuhumiwa wote wa Escrow, ikiwa ni pamoja na kufilisi mtambo wa IPTL na kuitangaza benki ya Stanbic kuwa taasisi ya kutakatisha fedha.

Bunge liliagiza pia kuchunguza na kuwajibisha majaji waliotajwa kunufaika na mgawo wa fedha kupitia benki ya Mkombozi na kumfukuza nchini, anayejiita mmiliki wa IPTL, Harbinder Sigh Seth.

Akizungumzia kutajwa kwa Dk. Hoseah na baadhi ya majaji katika mawasiliano na Rugemalira, mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu amesema jambo hilo linaongeza shaka juu ya uadilifu wa viongozi wa CCM na serikali yake.

Ameliambia gazeti hili katika mahojiano kwa njia ya simu, “…hili liserikali lote limeoza. Kuanzia Ikulu, mfumo wa mahakama hadi viongozi wa madhehebu ya kidini; kote kumejaa rushwa.”

Lissua ameongeza, “Tulisema ndani ya Bunge, kwamba majaji wamehongwa na hivyo tukataka wachunguzwe, lakini serikali ya CCM imegoma kwa kuwa walioiba waliwajua na walishirikiana nao.”

Mwanasiasa huyo wa upinzani anasema, “utapeli huu ulifanywa na serikali ya Rais Kikwete, BoT, Benki ya Stanbic na PAP.”

Amesema, “…sasa kama kweli wanataka kusafisha nchi, basi waanzie hapo. Siyo kukimbizana na vidagaa. Waanze na maofisa wao wa Ikulu waliokuwa wameigeuza ofisi ya umma kuwa ofisi binafsi.”

Chanzo: Mwanahalisi

Washindi wa Bahati Nasibu DKT Tanzania 'Fiesta Condoms' Warejea Kutoka Dubai

0
0
Katika jitihada za kutangaza matumizi ya njia za uzazi wa mpango na kuzuia mimba zisizotarajiwa na magonjwa yanayo ambukizwa kwa kujamiiana (STDs) nchini, miezi miwili iliyopita katika siku ya wapendanao (valentine day), DKT International Tanzania shirika lisilo la kiserikali ambalo ni moja kati ya watoaji wakubwa wa bidhaa za uzazi wa mpango na afya ya uzazi nchini ilifanya uzinduzi wa aina mbalimbali za kondom zenye ubora zilizopewa jina la “Fiesta kondom” huko Bahari Beach Ledger Plaza hotel, Dar es salaam.

Wakati wa uzinduzi, shindano la bahati nasibu lilifanyika ambapo wanandoa watatu walishinda safari iliyolipiwa kila kitu ya kwenda na kurudi Zanzibar, Afrika ya kusini na Dubai.

Wakielezea msisimko wao wakati wa kurudi kutoka katika safari yao mwishoni mwa wiki katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), washindi wa safari ya kwenda Dubai ambao walitembelea Dubai kwa mara ya kwanza walifurahia wiki nzima ya kukaa na kutalii Dubai na Abu dhabi, waliishukuru DKT International Tanzania kwa kutimiza ahadi yao na kwa kuifanya safari yao kuwa ya kukumbukwa.
Katika mahojiano wakiwa uwanja wa ndege, washindi walisema kuwa safari imewapa fursa ya kutembelea sehemu za kusisimua huko Dubai kama Burj Khalifa, ambalo ni jengo refu kuliko yote Dubai, maduka makubwa ya kufanyia manunuzi pamoja na mashindano ya mbio za magari ya Formula one huko Dubai.

“Nimefurahia sana kupata safari hii ya kusisimua kwenda Dubai na mke wangu. Tuliweza kujionea wenyewe na kushuhudua mengi yanayoongelewa kuhusu jiji la maajabu. Ninapenda kuishukuru DKT International Tanzania kwa fursa hii nzuri na tunaahidi kuendelea kuwa mabalozi wazuri wa Fiesta kondom kila wakati ambapo tutahitajika kufanya hivyo. Alihitimisha bwana Justin Tinieshimo.



Kwa upande wake, Meneja Masoko wa Fiesta Kondom bwana Davis Kambi amesema “Tunafuraha kuhitimisha safari ya washindi wetu wa safari ya Dubai na wanashukuru kuwa na fursa hiyo ya kukumbukwa wakiwa Dubai.” Nyakati kama hizo ndizo ambazo zinahusu bidhaa ya Fiesta Kondom, kuleta wanandoa karibu katika nyakati za upendo; DKT International Tanzania imejidhatiti kulete wanandoa pamoja chini ya kampeni za Intimacy by Fiesta ambazo zitahakikisha wanandoa wengine wanapata safari ya kwenda katika sehemu za mbalimbali mwaka huu.

Bwana Kambi alitumia fursa hiyo kuhakikisha kuwa washindi wa zawadi ya safari ya kwenda Zanzibar tayari walisha kwenda na walisha rejea.

Aliwashukuru wote walioshiriki katika kuhakikisha kuwa shindano la bahati nasibu la uzinduzi wa Fiesta Kondom Valentine limefanikiwa. Fiesta Kondom itafanya tena tamasha la kukutana la wanandoa mwaka ujao ambapo wanandoa wataweza kushinda zawadi nzuri.

Bidhaa ya Fiesta Kondom ya DKT International Tanzania ilizinduliwa zaidi ya miaka 20 iliyopita na inapatikana katika nchi zaidi ya 40 duniani kote na sasa katika mikoa yote mikubwa ya Tanzania. Fiesta ina zaidi ya ladha 55 tofauti za kondom na zaidi ya aina 60 tofauti. Lakini kwa kuanzia DKT International Tanzania imetambulisha aina 5 tofauti; Fiesta Heat, Fiesta Ultra-thin, Fiesta Strawberry, Fiesta Max dotted and Fiesta Neon! DKT International Tanzania inapanga kuzindua aina zingine 3 za kondom zinazokamilishwa kwa utofauti wa aina mbalimbali kabla ya mwisho wa mwaka 2016.



MWISHO
Kuhusu DKT International Tanzania
DKT InternationalTanzania ni moja kati ya watoaji wanaoongoza wa bidhaa za uzazi wa mpango na afya ya uzazi Tanzania. Taasisi hii imekuwa ikifanya kazi zake tangia mwaka 2014. Katika mwaka 2015, DKT International Tanzania ilikuwa ni taasisi ya kwanza kufungua kiliniki maalumu kwaajili ya uzazi wa mpango, kliniki 3 za Trust Health & Wellness zinafanyakazi kwa sasa na ya nne itaanza kufanya kazi mwaka huu. DKT International Tanzania Inajengwa au kukamilishwa na mtandano wa wadau 30 wa Trust franchise katika mikoa 4.
DKT International Tanzania pia inatoa aina mbalimbali za bidhaa za kupanga uzazi zenye ubora wa hali ya juu kwa bei nafuu. Kutoa uchaguzi wa mbinu, kutambulisha teknolojia ya kibunifu na kuziba pengo katika mnyororo wa usambazaji ambao utasaidia kunusuru mahitaji. Ukichukulia idadi ya vijana wa Tanzania na kukua kwa matumizi ya uzazi wa mpango, DKT International Tanzania pia imeanzisha uwepo imara na wenye nguvu wa kidigitali na katika mtandao wa kijamii kuweza kuwafikia vijana. Kila mwezi zaidi ya watu laki moja wanafikiwa katika mtandao, na idadi hii inaendelea kukua kila mwezi.

Katika mwaka 2015, DKT International Tanzania iliuza zaidi ya kondom 670,608, 8,200 vifaa vya kupanga uzazi vya dharura, ana zaidi ya 18,000 za IUDs. Hii ni sawa na ulinzi wa wanandoa 225,600 kwa mwaka.


Kwa taarifa zaidi wasiliana na:-
Meneja Masoko wa Fiesta Kondom
Davis Kambi
Simu: 0652-687 800
Barua Pepe: davis@dkttanzania.org

Tafadhali pia Tembelea:-
Kondom chapa ya Fiesta Condoms
Facebook:  https://www.facebook.com/Fiesta-Condoms-TZ
Instagram:  turnonfiesta

Kondom chapa ya Bull
Tovuti:  www.kileleland.com
Facebook:  https://www.facebook.com/KileleLand
Instagram: kileleland

Chapa ya uzaizi wa mpango ya Trust
Tovuti: www.trustlife.co.tz
Facebook: http://www.facebook.com/Trustlifetz
Twitter: @trustlifetz
Instagram: trustlifetz

Mwimbaji Baraka De Prince Atoa Masharti Kama Unataka Kushirikiana Naye Katika Wimbo Wako

0
0
Mwimbaji Baraka De Prince Amefunguka na kusema kuwa ili ufanye nae Collabo kwenye wimbo wako ni lazima kwanza ausikilize wimbo wako alafu aupende , asipoupenda hata umpe hela yoyote hawezi fanya Colloba na wewe, Ameongeza kwa kusema kuwa hata kama ukipitia kwa management yake kama wimbo ni mbaya hafanyi Collabo....

Mwanamuziki Asifiwa na Wengi Kwa Kufanya Hili Jambo...

0
0
Wanasema ukipenda boga, penda na maua yake.
Kwa Diamond kumpenda Zari the Bosslady kunaamanisha kuyapenda pia maua yake matatu ya mwanzo. Unapompenda mwanamke ambaye tayari ana watoto watatu kabla yako, ni lazima ukutane na changamoto nyingi hasa za kutengeneza ukaribu na watoto hao. Wapo waliofanikiwa na wengi wameshindwa. Kwa Diamond lakini ameonekana kuucheza vyema mchezo huu na watu wamemsifia.

Jana ilikuwa ni birthday ya mtoto wa tatu wa Zari, Lil Q ambaye katika wote anaonesha kumkubali zaidi Diamond kuliko wale wawili wakubwa. Kuonesha kuwa anamkubali pia dogo huyo mkali wa kunyuka pamba, Chibu alimtumia salamu za birthday kwenye Insagram zilizowavutia wengi.

“Happy Birthday to my Little Handsome… Mr Swag on point… i know he’s your Bae.. @lilQ_is_Bae,” aliandika.

Kwa post hizo, Diamond alichukua pointi zake tatu jana.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Video: Mange Kimambi Anasema Uhuru wetu ni Muhimu Sana Kuliko Mabilioni Anayookoa Magufuli

0
0
Wote ambao bado mmelogeka Na majipu ya JPM mpaka hamuoni hatari kubwa itakayotokea huko mbeleni kutokana Na Bunge kuzimwa tutawaweka kwenye sala zetu ili Mpate kuamka usingizini before it's too late and join with us. .

Yoyote anae support JPM kuminya Bunge La Tanzania atakuwa hajaenda shule Na Kama ameenda shule itakuwa hakusoma masomo ya history Au politics Maana Kama umesoma masomo hayo ungekuwa unajua kabisa serikali yoyote ya kidemokrasia inapoanza ku-silence vyama vya upinzani Kwa namna yoyote ile that country is going down the drain. Vyama vya upinzani Ni watanzania pia so Kama JPM anaweza kuwanyanyasa hao trust me eventually yoyote Yule ambae hatokubaliana Na JPM will meet the same fate! Trust me on that one.

PENZI la Mwanamuziki Shaa na Master Jay...Shaa Afunguka Kinachoendelea Kwa Sasa....

0
0
Master J na Shaa wamekuwa kwenye uhusiano kwa miaka mingi sasa na wameendelea kuwa imara.

akini pamoja na kuwa hivyo, bado uhusiano wao wa kikazi una nafasi kubwa zaidi. Hali hiyo ndiyo imemfanya Shaa kujitahidi kutofautisha uhusiano wao na kazi kwakuwa kwake Master J ni bosi wake.

“Bosi wangu meaning ni CEO wa MJ Records, label iliyonisaini na ananisupport sana namshukuru mwenyezi Mungu, ni CEO lakini ni one of my best friends, nimemfamu sasa for ten years,” Shaa alikiambia kipindi cha Chill na Sky.

“He is one of my close advisors, ananishauri sana na nasikiliza sana ushauri wake, akikataa kitu nazingatia, akiniambia fanya hivi nasikiliza. Kwahiyo kama Shaa, Master ni my CEO, my boss and my very close friend, kama Sarah hayo ni ya Sarah.”

Master J na Shaa walikutana kwa mara ya kwanza kwenye mradi wa Cocacola Popstars takriban miaka 10 iliyopita.

Wabunge Watwangana Ngumi BungenI..

0
0
Wanachama wa chama tawala cha Uturuki cha AK na chama kinachoungwa mkono na Wakurdi wamepigana ngumi bunge kuhusiana na mpango kuwaondolea kinga wabunge ya kutoshitakiwa.

Wabunge wakionyeshana umwamba Bungeni nchini Uturuki
Ngumi hizo ziliibuka bungeni wakati kamati ya bunge ilipokutana kujadili mabadiliko hayo yanayoungwa mkono na serikali ili kubadili Katiba kuwaondolea kinga hiyo wabunge.
Baadhi ya wabunge walikunjana mashati kwenye meza, wengine wakirusha chupa za maji na kurushiana ngumi bungeni.

Ole Wao Wanaowapa Ujauzito Wanafunzi-Ummy

0
0
Serikali imewaagiza Maafisa maendeleo ya Jamii na maafisa ustawi wa Jamii wa wilaya,kata na mikoa nchini kuwafatilia wanaume wanaowapa ujauzio wanaume wanaowapa ujauzito watoto wa shule na kuwafikisha Mahakamani.

Akizungumza leo bungeni katika kipindi cha maswali na majibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu, amesema serikali haitamvumilia mwanaume yoyote anaempa mwanafunzi ujauzito.

Mhe. Ummy amesema kuwa serikali ya awamu ya tano itawachukulia hatua wanaume wote na hakutakuwa na huruma juu ya hilo huku akisisitiza wanawake ambao si wanafunzi ni wengi mitaani.
Hapo awali Akijibu Swali la Mbunge wa Ileje, Mhe. Janeth Mbene, Naibu Waziri wa TAMISEMI, Mhe. Seleman Jaffo amesema kuwa tatizo la watoto kupewa ujauzito nchini linatokana na vishawishi wanavyokutana wakiwa njiani wakati wanakwenda mashuleni.

Baada ya Skendo kubwa ya Usaliti, Pepsi Wametoa Kauli juu ya Tiwa Savage Kuwa Balozi wao

0
0
Kampuni ya kinywaji cha Pepsi wamethibitisha kuwa baada ya skendo kubwa ya usaliti iliyomkumba Tiwa Savage, bado msanii huyu ni balozi wa kinywaji hicho.

Nigeria imemuangukia Tiwa Savage kwa tuhuma za usaliti zilizosambazwa mitandaoni na kurasa ya instagram ya mume wake ambaye baadae alisema kurasa hio ilivamiwa.

Siku mbili zilizopita Tiwa Savage alikanusha kumsaliti mume wake na kusema Mume wake TeeBillz alikuwa anahusishwa na uuzaji wa dawa za kulevya na pia anajua amemsaliti na sio mara moja.

Pepsi wameandika hivi"

"@Pepsi_Naija and @TiwaSavage as strong as ever"

Hii inamaanisha kuwa Pepsi na Tiwa Bado wako pamoja hawakutetereshwa na skendo zinazoendelea

Umoja wa Ulaya Wapongeza Hatua Zinazochukuliwa na Rais Magufuli

0
0
Umoja wa Mataifa ya Ulaya umepongeza hatua zinazochukuliwa na rais Dkt. John Magufuli,katika kudhibiti vitendo vya rushwa nchini na kuahidi kutoa misaada zaidi ili kuboresha huduma za kijamii na kiuchumi.

Pongezi hizo zimetolewa Jijini Mwanza na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguezi,pamoja na Mkuu wa idara ya siasa na mawasiliano wa umoja wa ulaya walipomtembelea Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella.

Pamoja na mambo mengine Umoja huo wa Ulaya umetembelea mkoa wa Mwanza kwa ajili ya kuangalia fursa za uwekezaji ambapo umeiomba serikali ya Tanzania kuondoa urasimu katika upatikanaji wa vibali vya uwekezaji.

Licha ya Kupongeza hatua hizo za rais John Magufuli katika kupambana na rushwa Ujumbe huo wa Umoja wa ulaya umetaka serikali iweze kuchukua hatua zaidi dhidi ya wale wote watakaobainika kuhusika na vitendo hivyo vya rushwa.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, amesema kuwa hiyo ni fursa kwa wakazi wa mkoa wa Mwanza katika kuchangamkia fursa za miradi inayofadhiliwa na Umoja huo lakini pia ni njia moja wapo ya kudumisha mahusiano ya Kimataifa.

Ujumbe huo umetembelea baadhi ya miradi wanayoifadhili mkoani humo ikiwemo mradi wa maji safi na usafi wa mazingira Jijini Mwanza pamoja na mradi wa kuongeza thamani ya ngozi katika chuo cha Teknolojia DIT tawi la Mwanza.

SHILOLE Afunuka ""Mimi ndio Mwanamke Mzuri Bongofleva"

0
0
Msanii Shilole ambaye haishi vituko kwa mashabiki wake amejigamba kuwa kwa Bongo hakuna msanii mzuri kama yeye, kwani ana uzuri wa asili bila vipodozi.

Shilole ameyasema hayo leo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha 5SELEKT kinachorushwa na EATV.

"Mimi ni mwanamke mzuri without make up (bila vipodozi), unaweza ukaniamsha usingizini na nikaenda popote bila makeup, katika Bongofleva mimi ni mwanamke mzuri sana hamna anayebisha,” alisema Shilole.

Pamoja na hayo Shilole amezungumzia suala la kuwa na ukaribu na msanii Nedy Music, na kusema kuwa msanii huyo ni rafiki yake tu na si vinginevyo. “Nedy ni mshkaji wangutu, ananifanya nismile,” alisema Shilole.
Pia Shilole amesema Jumatatu ya wiki ijayo anatarajia kuachia wimbo wake mpya unaoitwa 'Say ma Name'.

Mama wa Msanii Tupac Ambaye pia ni Mwanaharakati Afeni Shakur Davis Amefariki Dunia

0
0
Mama mzazi wa legendary rapa Tupac Shakur amefariki dunia akiwa na miaka 69,Kifo cha Afeni Shakur kimethibitishwa May 3 na taarifa zilitolewa na Polisi wa Marin County mjini California.Ujumbe wa polisi unasema Mama yake Tupac amefariki usiku wa May 2.

KRON wameripoti kuwa alipatwa na mshtuko wa moyo nyumbani kwake San Francisco na kupelekwa hospitalini mida ya  9:45 p.m. nakutangazwa amefariki mida ya 10:30 p.m.

Afeni Shakur alikuwa kwenye harakati za mwisho za kuchukua talaka kutoka kwa mume wake wa miaka 12 Gust Davis.

mama 2 pac 1 mama 2 pac 2

Afeni Shakur kwenye ujana wake alikuwa anatumia dawa za kulevya aina ya Crack na alihusishwa na kundi la vijana la Black Panther.

IGP Mangu: Sina Taarifa Juu ya Agizo la Rais Kumpandisha Cheo Askari

0
0
Amesema hajapewa taarifa za Rais Magufuli kuagiza koplo Deogratius Mbango kupandishwa cheo baada ya kumdhibiti mke wa mmoja wa mawaziri wa serikali yake kwa kosa la kukiuka sheria za usalama barabarani.

" Bado hajapandishwa cheo kwa sababu sijapewa taarifa hizo na nitakapopewa taarifa atalazimika kwenda kwenye mafunzo kwanza, sisi jeshi la polisi tuna taratibu zetu" alisema IGP Mangu .

Chanzo: Nipashe
Viewing all 104429 articles
Browse latest View live


Latest Images