Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104775 articles
Browse latest View live

Kikwete 'Agoma' Kumkabidhi Rais Magufuli Chama......Mwinyi,Mkapa,Malecela Kukutana kwa Dharura Kumjadili

$
0
0

Hali si shwari ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutokana na mchakato unaoendelea wa kumkabidhi Rais Dk. John Magufuli uenyekiti wa chama hicho, kukumbwa na sintofahamu.


Taarifa kutoka ndani kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (CC), kilichofanyika juzi Ikulu ya Chamwino, mkoani Dodoma, zimethibitisha kutokea mgawanyiko wa vigogo ndani ya chama hicho.


Hali hiyo imekuja baada ya kutokea kwa mvutano juu ya tarehe rasmi ya kufanyika kwa mkutano mkuu maalumu uliopangwa Juni mwaka huu, ambao pamoja na mambo mengine Mwenyekiti wa chama hicho taifa, Rais mstaafu Jakaya Kikwete atakabidhi kijiti kwa Rais Magufuli.


Chanzo cha kuaminika ndani ya kikao hicho kilidokeza  kuwa, kabla kilifanyika kikao kidogo kilichokuwa na wajumbe wanne ambao pamoja na mambo mengine walijadili ajenda muhimu  ikiwamo ya kupanga tarehe kwa ajili ya mkutano huo.


Kwa mujibu wa chanzo hicho, kikao hicho kidogo kilishirikisha viongozi wanne akiwemo Mwenyekiti wa chama hicho Jakaya Kikwete, Rais Dk. John Magufuli, Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.


Habari hizo zinaeleza kuwa, katika kikao hicho kidogo viongozi hao walikubaliana wakatangaze tarehe rasmi, na Rais Magufuli alikubali kukabidhiwa uenyekiti wa chama kama ulivyo utaratibu wa CCM lakini baada ya kikao cha Kamati Kuu kuanza, Kikwete alikataa kuruhusu hoja hiyo ijadiliwe, hatua iliyozua mfarakano.


“Baada ya kumalizika kwa kikao kile viongozi hao wanne waliingia ndani ya kikao cha CC ambacho kilikuwa na ajenda kadhaa ikiwemo ya mkutano mkuu maalumu ambapo mwenyekiti alirusha na kutaka hoja ya tarehe isijadiliwe,” kilisema chanzo hicho.


Kwa mujibu wa chanzo hicho, ilipofika ajenda ya tatu ambayo iliwasilishwa na Katibu Mkuu, Kinana kuhusu kutangazwa kwa tarehe ya mkutano mkuu maalumu, Kikwete aligoma isijadiliwe na badala yake aliahirisha kikao na kutoka nje.


Chanzo hicho kilisema, uamuzi wa Mwenyekiti Kikwete wa kuahirisha kikao ulijikita katika suala la gharama za mkutano ambazo zinakadiriwa kuwa ni zaidi ya Sh bilioni mbili, hivyo aliwataka wajumbe waahirishe kikao ili kutoa fursa ya kutafuta fedha.


Taarifa hizo zilieleza kuwa, kutokana na hali hiyo yaliibuka makundi mawili, moja linalomuunga mkono Kikwete na jingine linalopingana na hoja hiyo, likidai kuwa fedha si tatizo kwa chama hicho kwa kwani kina miradi, ruzuku na marafiki wengi.


“Wanaompinga mwenyekiti walishangazwa na hoja hiyo wakisema kuwa, suala la fedha ni la watendaji wa chama na si la mwenyekiti, kitendo ambacho wamekitafsiri kwamba mwenyekiti hana dhamira ya dhati ya kukabidhi chama kwa sasa,” kilisema chanzo hicho.


Chanzo hicho kiliendelea kutoa taarifa kuwa, baada ya Kikwete kugoma kujadili tarehe alisimama mjumbe Jenista Mhagama, ambaye alipinga uamuzi huo, huku akisema suala hilo ni lazima lijadiliwe kwa kina na tarehe ya mkutano mkuu itangazwe.


“Kauli ya mwenyekiti inaonekana iliwaudhi baadhi ya wajumbe, lakini Jenista alizungumza vizuri sana na kumhoji mwenyekiti inakuaje hataki kusema lini utafanyika mkutano mkuu maalumu ili akabidhi chama.


“Maana suala la makabidhiano ni la utamaduni wa ndani ya CCM, Jenista alisema aliyekaa muda mrefu alikuwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere pekee lakini na yeye alikabidhi kwa mzee Mwinyi (Ali Hassan) na pia ilipofika wakati kama huu mzee Mwinyi naye alikabidhi kwa mzee Mkapa.


“Si hilo tu hata mzee Mkapa naye alikabidhi chama kwake (Jakaya Kikwete), sasa inakuwaje yeye leo hataki kufuata utaratibu huo ambao ni wa kawaida ndani ya chama?,” kilihoji chanzo hicho.


Chanzo kingine cha habari kilisema kuwabaada ya mwenyekiti huyo wa CCM taifa kuahirisha kikao hicho juzi, aliondoka na kurejea jijini Dar es Salaam kwa gari tofauti na ratiba iliyokuwa imepangwa.


“Ratiba ya chama ilikuwa baada ya kikao cha jana (juzi) mwenyekiti angelala Dodoma na badala yake alipoahirisha kikao kwa utata alipanda kwenye gari na kuondoa hali ya kuwa alitakiwa kurejea Dar leo (jana).


“Baada ya kikao hicho alitoka mzee Kinana akiwa amekasirika sana, tena huku akiwa amekunja sura, unajua siku zote mzee Kinana anaamini kwamba kile kilichokuwa kinapiganiwa na chama hivi sasa ndicho kinachotekelezwa na Rais Magufuli tena kwa vitendo tofauti na huko nyuma,”kilisema chanzo chetu.


Baraza la Wazee kukutana

Taarifa nyingine zinaarifu   kwamba, kutokana na hali hiyo Baraza la Wazee la CCM linaloundwa na viongozi wastaafu, linatarajiwa kukutana kati ya leo na kesho kwa lengo la kujadili hali hiyo ili kuondoa mtanziko huo uliojitokeza.


“Ninachotaka kukuambia katika kipindi cha siku mbili baraza la ushauri la wazee litakutana na kujadili hali hii na baada ya hapo watakwenda kwa mwenyekiti kumshauri juu ya uamuzi wake na autafakari kwa kina.


“Tunajua tunakwenda vizuri katika hili na hakuna kitakachoharibika na wazee wetu watamshauri vema mwenyekiti ili kupata mwafaka wa kudumu na mkutano mkuu utafanyika mwezi uliopangwa,” chanzo hicho kilisema.


Baraza la Ushauri la Wazee wa CCM, linaongozwa na Rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi (Mwenyekiti), Pius Msekwa (Katibu) na wajumbe ni Rais mstaafu Benjamin Mkapa pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM mstaafu (Bara), John Malecela.

Wabunge Waja Juu...Wadai wao Sio Wanafunzi Wakusign Kila Waingiapo Bungeni Asubuhi na Wakitoka Jioni

$
0
0

Wabunge wameitaka Ofisi ya Bunge iwaondolee mara moja utaratibu wa kusaini kwa kutumia vidole mara mbili kwa siku kwa kuwa wao si wanafunzi.


Hoja hiyo iliwasilishwa kwa njia ya mwongozo na kuungwa mkono na wabunge wote isipokuwa mawaziri na Mbunge wa Konde, Khatib Said Haji (CUF) mjini Dodoma jana.


Katika Mwongozo wake, mbunge huyo alisema kitendo cha kutakiwa kusaini mara mbili kwa siku ni kero kwa wabunge na uonevu kwa kuwa hata Bunge limekuwa likitumia muda wa mapumziko wa wabunge kwa kazi za Bunge.


“Mheshimiwa Naibu Spika wewe mwenyewe muda mfupi umetangaza matangazo mbalimbali yanayotaka baadhi ya wajumbe wa kamati wakutane baada ya saa saba mchana, tunafanya kazi nje ya mapumziko yetu, haya haina tatizo... “...tatizo langu ni kitendo cha wabunge kutakiwa kusaini mara mbili kwa siku asubuhi na jioni, wakati mwingine tunatoka hapa saa saba, wabunge tunashughulikia mambo mpaka saa 12, mbunge anatumia muda wake wa mapumziko na ule wa kuhudhuria kikao cha jioni,” alisema Haji.


Alisema inasikitisha kuona mbunge anatolewa kwenye kazi za kujenga taifa ili aje tu asaini kwa kidole tena mara ya pili.


Alisema jambo hilo linawatatiza wabunge kwa kuwa wanajiona kama wanachukuliwa kama wanafunzi kwa kufuatiliwa kwani hata kwenye benki wafanyakazi hawasaini na kufuatiliwa kama ilivyo kwa wabunge hao.


Alifafanua kuwa kabla ya kuomba Mwongozo huo, alifanya utafiti kwenye benki mbalimbali ikiwemo Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambao nao wana utaratibu kama huo wa Bunge lakini hakuna mahali wanapotakiwa kusaini kwa vidole mara mbili.


“Kutokana na uzito wa jambo hili naomba kutoa hoja wabunge mniunge mkono mpango huu ukome,” alisema na wabunge takribani wote walisimama ishara ya kumuunga mkono na kumpigia makofi na vigelegele.


Kwa upande wake, Naibu Spika, Dk Tulia Ackson alisema kutokana na namna wabunge hao walivyopokea suala hilo, pamoja na kwamba kikanuni jambo hilo halikutakiwa kuombewa mwongozo bado litaangaliwa.


“Hata hivyo, nifafanue kuwa kusaini mara mbili lengo lake si kuwafanya wabunge wanafunzi, ila lengo ni kutaka kujua nani wapo humu ndani (bungeni),” alisema Dk Ackson.

Mwanamuziki Snura Awaomba Radhi Watanzania Kwa Video ya Chura

$
0
0

Baada ya kufungiwa na Serikali jana, msanii Snura awaomba radhi Watanzania kwa video isiyo na maadili, ajisajili upya BASATA.

Amesema hatotoa tena video yenye maudhui ambayo sio ya kitanzania na tayari ameruhusiwa kufanya show katika majukwaa mbalimbali

Stori Kuhusu Ali Kiba Kutoa Wimbo Mpya Hii Hapa

$
0
0

Alikiba anatarajia kuachia wimbo wake mpya alioupa jina ‘Aje.’

Hajasema wimbo huo utatoka lini lakini dalili zinaonesha kuwa unaweza ukaachiwa mwezi huu.

Huo unakuwa wimbo wake mpya mwenyewe tangu aachie Lupela. Kwa sasa Kiba anafanya vizuri na wimbo aliofanya na Sauti Sol, Unconditionally Bae.

Mwanamke Apatikana Hai Kwenye Vifusi Nairobi Siku Sita Baada ya Ghorofa Kuanguka

$
0
0

Jengo hilo liliporomoka baada ya mvua kubwa kunyesha Ijumaa

Mwanamke amepatikana akiwa hai kwenye vifusi siku sita baada ya jumba kuporomoka katika mtaa wa Huruma, Nairobi.

Juhudi za uokoaji bado zinaendelea ingawa kuna wasiwasi kwamba muda wa kupata manusura wakiwa hai unayoyoma.

Mtoto mchanga atolewa kwenye vifusi Nairobi

Idadi ya waliofariki kufikia sasa imefikia 33.

Watu 80 kufikia sasa bado hawajulikani walipo.

Mmiliki wa Timu ya TP Mazembe Atangaza Kuwania Urais Jamhuri ya Demokrasia Congo

$
0
0

Mwanasiasa mashuhuri nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo Moise Katumbi amethibitisha kuwa atagombea urais kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Novemba. Mfanyabiashara huyo na gavana wa zamani wa jimbo la Katanga alitoa tangazo hilo kupitia kwa mitandao ya kijamii.

Muungano wa vyama kadha vya upinzani uliamua kumuidhinisha Bw Katumbi kuwa mgombea


Bw Katumbi, akitangaza kuwania kwake, amepuuzilia mbali madai kwamba alipokuwa waziri wa hati alitumia mamluki kutoka nje akisema habari hizo ni za uongo.

Moise Katumbi anaweza kuwa rais DR Congo?

Kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo Rais Joseph Kabila anatakiwa kuondoka madarakani mwaka huu lakini wapinzani wake wana hofu kuwa huenda ana mipango ya kusalia madarakani.

CCM Yakanusha Mwenyekiti wake Jakaya Kikwete 'Kugoma' Kukabidhi Uenyekiti kwa Rais Magufuli

$
0
0

Baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vinatoa taarifa potofu kuhusu mchakato wa  Mwenyekiti wa sasa wa CCM Dkt. Jakaya Kikwete kukabidhi kijiti cha uongozi wa CCM kwa Rais John Pombe Magufuli kama ilivyo mila na desturi ya Chama Cha Mapinduzi. Yamekuwepo madai eti Mwenyekiti amekataa au anachelewesha kukabidhi kijiti.


Habari hiyo sio kweli kabisa na ni kinyume chake, kwani Dkt. Kikwete amekuwa akisisitiza kukabidhi madaraka mapema iwezekanavyo. 


Kwa ajili hiyo kwenye kikao cha Mei 3, 2016 alikataa kusiongezwe agenda nyingine ambazo zitalazimisha Mkutano Mkuu Maalum kuchelewa kufanyika kwa sababu ya kukamilisha maandalizi ya agenda hizo. Alisisitiza agenda iwe moja tu.


Dhamira ya kufanyika Mkutano Mkuu maalum mwezi Juni, 2016 iko pale pale.Kilichoelezwa kwenye kikao ni kutaka kukamilisha utaratibu wa kupata fedha za kugharamia mkutano huo. Taratibu zikikamilika tarehe itapangwa. Mipango ya kutafuta pesa inaendelea na ikikamilika tarehe itatangazwa.


Tunawataka wana-CCM wasihamanike wala kubabaishwa na taarifa za upotoshaji zinazofanywa na watu wenye nia mbaya na CCM. Hawa ni wale wale ambao wamekuwa wakiiombea mabaya CCM bila ya mafanikio.


Pia tunapenda kukanusha madai ati kuwa Mwenyekiti Kikwete aliwatahadharisha Wajumbe wa Kamati Kuu kuhusu ukimya wa Ndugu Edward Lowassa. Hakuna wakati wowote kauli kama hiyo aliitoa. Ni uzushi mtupu. Jina la Ndugu Lowassa halikutajwa kabisa.


Aidha, tunapenda kukanusha madai ya kufanyika mkutano baina ya Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Jamhuri ya Muungano, Makamu wa Rais na Katibu Mkuu wa CCM kuhusu uchaguzi wa Katibu wa Kamati ya Wabunge wa CCM. 


Hapajawahi kufanyika mkutano wa aina hiyo siku yoyote na mahali popote. Hivyo madai ya kuwepo kwa tofauti baina ya Viongozi wakuu kuhusu nani achaguliwe kuwa Katibu wa Wabunge wa CCM hayana msingi wowote.


Kamati Kuu iliteua Wabunge wanne kugombea na kuwaachia Wabunge wa CCM kuamua. Kuhusisha Viongozi na hasa kuzua kuwepo kutokuelewana ni jambo la kusikitisha. Ni taarifa ya uongo yenye nia ovu kwa CCM na Viongozi wake.


Tunapenda kuwatahadharisha waandishi wa habari kuandika habari za ukweli. Waache kuzua mambo yenye kupandikiza chuki na mgawanyiko usiostahili kuwepo ndani ya CCM na kuyaeneza kwa watu. Waheshimu maadili ya kazi zao.


Napenda kuwahakikishia na kusisitiza kuwa hakuna mgogoro wa kukabidhi kijiti cha uenyekiti katika CCM na wala hautakuwepo.


Imetolewa na;

 

Ndugu Christopher Ole Sendeka  

MSEMAJI WA CCM                 

MJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,

05/05/2016

Mchezaji wa Azam Farid Mussa Afaulu Majaribio Nchini Hispania....

$
0
0
WINGA wa kimataifa wa Tanzania, Farid Mussa Malik (pichani kulia) wa klabu ya Azam ya Dar es Salaam amefaulu majaribio katika klabu ya Deportivo Tenerife ya Ligi Daraja la Kwanza nchini Hispania.
Mkurugenzi wa Azam FC, Yussuf Bakhresa anayefuatilia majaribio ya mchezaji huyo Hispania, amesema kwamba CD Tenerife sasa inatarajiwa kuingia katika mazungumzo na Azam FC juu ya kumnunua mchezaji huyo.

“Tunatarajia kuanza mazungumzo nao juu ya suala la Farid, ingawa wazo lao la awali ni kumchukua kwa mkopo wa miaka miwili. Sasa tunasubiri ofa yao rasmi, kisha Bodi ya Ukurugenzi itajadili na kutoa maamuzi,”amesema Bakhresa.

Kwa upande wake, Farid amefurahia matokeo hayo na kusema haikuwa kazi nyepesi kwake kuweza kuwaridhisha maofisa wa benchi la ufundi la Tenerife.

“Kwa kweli nimefurahi sana na ninamshukuru Mungu kwa kufuzu majaribio, ila haikuwa kazi nyepesi, mpira wa Ulaya mgumu,”amesema.

Awali, Farid ilikuwa apelekwe moja ya klabu za Ligi Kuu ya Hispania, maarufu kama La Liga, kati ya Las Palmas na Athletic ya Bilbao kwa majaribio, lakini wakala wake akashauri mchezaji huyo aanzie timu ya Daraja la Kwanza Hispania ili kupata nafasi ya kucheza na kuinuka haraka.

Mwita Waitara Azusha Tafrani Bungeni.......Ni Baada ya Kutaka Kumchapa Ngumi Mbunge wa Kasulu Aliyedai Tundu Lissu na Mnyika Ni Vichaa

$
0
0
Mbunge  wa Ukonga, Mwita Waitara (Chadema) ametolewa nje ya Bunge baada ya kutaka kumkwida Mbunge wa Kasulu Vijijini, Agustine Holle (CCM) aliyedai kuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na Mbunge wa Kibamba, John Mnyika wote wa Chadema kuwa wanaugua kichaa.

Waitara alionesha kukerwa na kauli hiyo hasa pale Holle alipokataa kufuta kauli yake, licha ya kutakiwa kufanya hivyo na Naibu Spika, Dk Tulia Akson.

Wakati Holle akichangia, Waitara alinyanyuka kwenye kiti chake na alipofika alipo mbunge huyo alimzungumzisha maneno ambayo hayakusikika na kuonesha kama kutaka kumpiga kabla ya kukaa kwenye kiti kilicho mbele yake ndipo, Holle alisikika akisema “wewe unataka nini” ndipo Naibu Spika alipogundua kuwa Waitara anataka kumpiga Holle na kumuamuru atoke nje lakini hakutii amri hiyo.

Kutokana na kutotii, Naibu Spika aliamuru askari wamtoe ndipo walipoingia zaidi ya askari watano na kutoka naye hadi nje ya geti kubwa la kuingilia bungeni.

Holle wakati anachangia bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka wa fedha 2016/2017, alimtaja Lissu ambaye ni Waziri Kivuli wa Wizara hiyo kuwa ana taarifa kuwa Lissu amewahi kuugua ugonjwa wa kichaa na hadi sasa ana faili kwenye Hospitali ya Vichaa ya Mirembe iliyopo mkoani Dodoma.

Hata hivyo, alipopewa nafasi na Naibu Spika kufuta kauli yake akasema “nafuta kauli yangu lakini kwa taarifa zilizozagaa nimeamini ni kweli na mbona kwao(Chadema) wapo wengi hata Mnyika sasa hivi yupo Muhimbili anatibiwa kichaa”.

Kutokana na kauli hiyo, Lissu alisema licha ya kuifahamu Hospitali ya Mirembe, hajawahi hata kuingia kwenye geti la hospitali hiyo wala kuugua ugonjwa huo na kutaka kiti cha Naibu Spika kimtake Holle athibitishe ; na akishindwa kanuni zielekeze hatua za kuchukua kama zilivyowekwa.

Wabunge wa UKAWA Wamzomea Profesa Tibaijuka huku Wakimwita Mwizi.......Ni Baada Ya Kupingana na Hoja za Tundu Lissu Aliyedai Zanzibar Ni Koloni La Tanganyika

$
0
0
Mbunge wa Muleba Kusini (CCM), Profesa Anna Tibaijuka jana alikuwa mkali bungeni akisema yeye si mwizi na kuwabeza wanaomuita hivyo kuwa wataisoma namba.

Profesa Tibaijuka alifikia hatua hiyo baada ya kuhamaki kutokana na baadhi ya wabunge wa upinzani kupaza sauti na kumuita mwizi wakati akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria.

Profesa Tibaijuka alianza kwa kuwataka wabunge wamuunge mkono Rais John Magufuli kwa kuwa amechaguliwa na wananchi.

“Wenzetu ambao kazi yao ni kuja kutusimamia sisi (upinzani) wana haki ya kusema wanayoyasema, lakini hata sisi tuna haki ya kuyaweka vizuri ili yaeleweke kwa wananchi,” alisema.

Profesa Tibaijuka alisema upinzani ukifilisika utabaki kukemea kwa sababu ni lazima tu useme kitu, Bunge linageuka kijiwe na bungeni si mahali pa kupeleka hoja za vijiweni.

Kauli hiyo iliwakera wabunge wa upinzani ambao walianza kupaza sauti zao dhidi yake, hali iliyoonekana kumchanganya.

Akirejea hotuba ya msemaji wa kambi ya upinzani bungeni, Tundu Lissu kuwa Tanganyika inainyonya Zanzibar na kuifanya koloni lake, Profesa Tibaijuka alihoji: “Tanganyika inainyonya Zanzibar katika lipi? Hili ni jambo la kujiuliza. Nimejiuliza mimi kama mchumi. Kazi yangu ya kwanza nyinyi mnanijua nilikuwa kwenye shirika la makazi duniani, hamjui kwamba nilikuwa kwenye Shirika la Biashara la Dunia?” alihoji.

Kutokana na zomeazomea kuendelea, Spika wa Bunge, Job Ndugai aliingilia kati: “Waheshimiwa wabunge namlinda mzungumzaji, naomba muwe wavumilivu. Mheshimiwa Profesa endelea."

“Kwa wale wanaosema nimeiba mtaisoma namba, mimi si mtu wa kutishwa na vitu vya ovyoovyo.

"Mimi sitishwi na hoja za ovyoovyo, huyo (mtu) akaisome namba. Nasimama hapa kwa sababu nataka nitetee vitu. Mtu anapopotosha anaweza kuleta hatari. Tanganyika kwa mtizamo wa kiuchumi haiwezi kuinyonya Zanzibar.

“Katika Dunia ya ustaarabu unasikia hoja. Lissu hapa angeweza kuzomewa, lakini wastaarabu wakamsikiliza wamekomaa kisiasa,” alisema huku baadhi ya wabunge wakiendelea kumzomea.

Tibaijuka aliwahi kuwa waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakati wa utawala wa Rais Jakaya Kikwete na aliondolewa baada ya kutuhumiwa kupata mgawo wa fedha za Tegeta Escrow

Mfanyabiashara Dangote Atajwa Kutumbuliwa kwa Juliet Kairuki TIC

$
0
0
Wakati aliyekuwa Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), ametajwa kutenguliwa uteuzi wake kwa kukataa kuchukua mshahara wa Serikali kwa miaka mitatu mfululizo, uchunguzi umebaini kuwa jipu la kusamehe kodi Kampuni ya Saruji ya Dangote ndilo lililomwondoa.

Uchunguzi uliofanywa umebaini kuwa mbali na Juliet Kairuki kutochukua mshahara wa Sh 5,000,000 kila mwezi aliopangiwa na Serikali kwa miaka mitatu, kwa maana kuwa ameacha kuchukua wastani wa Sh milioni 180 kwa muda huo, anatuhumiwa kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwa wawakezaji bila kufuata utaratibu au sheria za nchi.

“Hili la mshahara ni cha mtoto. Amewadanganya wawekezaji wengi kuwa anaweza kuwapa msamaha wa kodi ya VAT, na sasa Serikali hii ilipoingia madarakani ikasema hana mamlaka hayo. Mwekezaji wa kwanza aliyedanganywa ni Dangote,” anasema mtoa taarifa wetu.

Uchunguzi uliofanywa umebaini kuwa Novemba, 2015 Kampuni ya Dangote iliingiza nchini makaa ya mawe tani 35,000 kutoka Afrika Kusini na kutaka makaa haya yasamehewe kodi zote.

“Kwa kweli tulishangaa sana. Kwanza, makaa ya mawe si bidhaa za mtaji (capital) bali ni za matumizi tu (consumables). Vifaa vinavyosamehewa kodi ni zile zinazotumika kuzalisha bidhaa nyingine leo, kesho, mwakani au miaka mitano ijayo na kuendelea, ila makaa ya mawe ukiyachoma yanaisha siku hiyo hiyo, hivyo hii si mtaji.

“Ukiacha hilo, hawa watu wa Dangote wameambiwa wanunue makaa ya mawe kutoka Kiwira au Ngaka, lakini hawataki,” kinasema chanzo chetu na kuongeza kuwa kwa mwaka uliopita, waliagiza tani 2,000 tu za makaa ya mawe kutoka Tancoal kinyume cha makubaliano ya kuongeza ajira nchini.

Afisa kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) amefichua katika uchunguzi huu kuwa kinachoendelea kwenye Kampuni ya Dangote ni balaa. “Hii kampuni tulidhani imekuja hapa kukomboa wananchi, lakini uhalisia siyo.

“Kampuni hii inafanya malipo bila kutoa kodi ya zuio, bidhaa inazoingiza nchini pamoja na nyingine kupata misamaha ya kodi bado inaongeza bei zinakuwa ghali mno kwa maana ya kuongeza gharama za uzalishaji na hivyo kupunguza kiasi cha kodi kinachostahili kulipwa… ni shida,” anasema afisa huyo kwa uchungu.

Kutokana na mkanganyiko huo, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata, ameunda timu ya kufanya ukaguzi maalumu kwa Kampuni ya Dangote ambayo imewakuta na hatia.

“Hiyo bilioni 20 ni uchunguzi wa awali, tunaweza kupata kiasi kikubwa zaidi. Tunawashukuru kwa kuandika habari za ukwepaji kodi, na nakuhakikishia sisi tunafuatilia kila mnachochapisha,” anasema mtoa habari wetu.

Afisa mwingine wa TRA anasema mbinu kubwa inayotumiwa na Dangote na kampuni nyingine ambazo tayari TRA imekwishaibaini mbinu wanazotumia kupunguza faida (Tax Base Erosion), kwa kuingia mikataba yenye gharama kubwa na kampuni walizo na uhusiano nazo kibiashara, kuonesha wametumia gharama kubwa wakati uhalisia wanafanya mbinu za kukwepa kodi.

Akizungumzia sakata hili, Mejena Mkuu Mwandamizi wa Kampuni ya Dangote, Vidya Dixit, amekiri kupokea ankara ya malipo kutoka TRA yenye thamani ya bilioni 20 na akasema: “Wakaguzi wa TRA wako hapa, wamefanya uchunguzi wao, wametuletea madai yao, na sisi tunawasiliana na mshauri wetu wa masuala ya kodi, ikithibitika kuwa tunadaiwa kiasi hicho Dangote ni kampuni kubwa, tutalipa.”

Dixit amesema TRA wamekagua mikataba mbalimbali wanayotumia akina Dangote kuagiza bidhaa na huduma, na wakaja na kiasi hicho, hivyo kwake halioni kama ni tatizo, washauri wao wa masuala ya kodi wakikuta ni kweli watalipa tu. Chanzo chetu kimetueleza kuwa mshauri wao ni Kampuni ya PriceWaterhouseCoopers (PWC) ya Afrika Kusini.

Meneja huyo alijibu pia swali kuwa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TRA) inawadai dola 2,867,400 za Marekani (sawa na Sh bilioni 6.3), kwa kusema: “Mimi sisimamii idara ya uhasibu. Madeni hayo yanaweza kuwapo, ila Dangote ni kampuni kubwa, kama kuna madeni ya aina yoyote tutalipa tu baada ya kujiridhisha kuwa ni madeni halali.”

Kuhusu suala la tani 35,000 za makaa ya mawe kutoka Afrika Kusini, alisema wao kama Dangote hawapaswi kulaumiwa kwani walifuata taratibu zote: “TIC walitupa sisi msamaha wa kodi, sasa tumezungumza na Waziri wa Fedha akasema TIC hawana mamlaka ya kutoa msamaha wa kodi bila kutangaza kwenye Gazeti la Serikali (GN) na kweli hakukuwapo GN yoyote.

“Sasa hapa tunapata tabu kidogo, idara moja ya Serikali inasema hivi na idara nyingine inasema vile, tunapata shida kidogo,” anasema Dixit. Katika makaa hayo ya mawe pekee ambayo wanatakiwa kuyanunua kutoka nchini, Dangote wanadaiwa wastani wa Sh bilioni 1.1.

Kuhusu tuhuma zinazoelekezwa kwa kiwanda hicho kuwa kimewageuka wafanyabiashara wadogo na kupendelea wafanyabiashara wakubwa kwa njia ya kuwauzia saruji nyingi na kutowajali wadogo, Dixit anasema wao hawana ubaguzi na ucheleweshaji unaweza kutokea kunapotokea dharura.

Anasema kuna wakati wanaangalia nani ana ghala kubwa la kuhifadhia saruji kiasi gani, ila hiyo haiondoi ukweli kwamba hawabagui yeyote anayetaka kununua na kuuza saruji ya Dangote.

“Ukisema kuna walioshindwa kupata saruji kwa wiki moja au mbili, hilo naweza kukuelewa, lakini miezi miwili, wala asikudanganye mtu. Hilo haliwezekani. Ni kweli kule Lindi tunakotoa chokaa, machimbo yote kwa siku tatu zilizopita yalijaa maji, tukashindwa kupata chokaa, lakini zaidi ya hapo kila mtu anapewa fursa sawa ya kununua saruji bila ubaguzi,” anasema Dixit.

Awali, baadhi ya wafanyabiashara waliilalamikia Kampuni ya Dangote kuwa inauza saruji kwa upendeleo, hali inayowafanya wakose mapato kwani wamekopa mikopo benki na wanaishia kutopata saruji kwa wakati hivyo wanashindwa kulipa hiyo mikopo.

“Kuna mfanyabiashara ameweka kwenye akaunti ya Dangote Sh bilioni 2.5, huyu ndiye anayepewa saruji sisi wengine tunapuuzwa. Watanzania wengi wamekopa benki wastani wa Sh milioni 20, 30 au 50 wanaziweka kwenye kampuni ya Dangote na hawapati hiyo saruji. Hii inatutia hasara mno. Tunataka usawa katika biashara hii,” anasema mmoja wa wafanyabiashara anayedai ameweka Sh milioni 25 kwenye Kampuni ya Dangote, lakini hapatiwi saruji.

Pia, wanalalamikia bei kubwa ya saruji ya Dangote kwani wakati kiwanda kinaanza kujengwa Watanzania walitangaziwa kuwa mfuko mmoja wa saruji ungeuzwa kwa Sh 8,000, lakini sasa bei inafikia Sh 16,000 kwa mikoa kama Mwanza na kwa Dar es Salaam inauzwa kati ya Sh 10,800 na 12,500.

Kamishna Mkuu wa TRA, Kidata, hakuwa tayari kulizungumzia kwa undani suala la Dangote zaidi ya kusema: “Hili suala lipo, tunalifanyia kazi, ni mapema mno kulizungumzia kwa sasa.”

Hata hivyo, afisa mwingine mwandamizi alishangaa kusikia kuwa Dangote bado wanatafuta ushauri wa kisheria kama walipe kodi hiyo au la: “Hawa waliishakwenda hadi kwa Bwana Mkubwa wakakubali kulipa, sasa leo inakuwaje wanatafuta ushauri?” Alihoji afisa huyo.

Alichosema ni kuwa kila mfanyabiashara mkubwa kwa mdogo ajiandae kulipa kodi. “TRA haitaingilia mapato halali ya mfanyabiashara yeyote, ila kwa yeyote anayekwepa kodi hili halitavumiliki. Serikali ya sasa inasema hapa ni kazi tu, hakuna habari ya jina kubwa au dogo. Jipu ni jipu tu, bila kujali ni kubwa au dogo, yote yatakamuliwa tu.”

Mheshimiwa Rais Wanaodhani Wako Juu ya Sheria ni Wengi Sana...Soma Kisa Hichi

$
0
0
MIAKA michache iliyopita, wakati wa Serikali ya Awamu ya Nne ambayo imeshapita, kuna jambo moja lilinishangaza sana.  Jambo hili lilimhusu Waziri wa Serikali hiyo na mlinzi wa benki.
Kilichotokea ni kwamba Mheshimiwa Waziri alikwenda kwenye mashine ya kutolea fedha, maarufu kama ATM, huenda kwa ajili ya kutoa fedha.  Akiwa ndani ya kile chumba akaanza kuzungumza na simu. Akazungumza na simu kwa muda mrefu, hali iliyosababisha wateja waliokuwa wakiisubiri huduma hiyo kuanza kulalamika na kumlazimu mlinzi kumuomba Waziri awapishe wateja wengine waweze kupata huduma.

Hilo halikumfurahisha Waziri yule na badala yake akaanza kumwuliza mlinzi kama anajua yeye ni nani, kwa kuwa yeye kama Waziri ana mambo mengi ya maana na alikuwa akizungumza na simu muhimu.  Kwa huyo Waziri, suala la kuzungumza kwenye chumba cha ATM na kuwanyima fursa wateja wengine kama yeye kuipata huduma waliyokuwa wakiihitaji kwa wakati, halikuwa tatizo kabisa.

Sakata la Mheshimiwa Waziri na mlinzi wa benki liliripotiwa kwenye vyombo vya habari na bahati mbaya mwisho wake ulikuwa wa kusikitisha, kwani mlinzi alifukuzwa kazi kutokana na kutimiza majukumu yake.  Baadhi ya watu walipiga kelele, lakini hakuna kilichotokea.  Sana sana, baba wa watu akabaki bila kazi, huku akiwaza ataitunzaje familia yake iliyokuwa ikimtegemea.
Sasa juzi hapa hali hiyo imejirudia tena.  Safari hii, hata hivyo, imemhusisha Mke wa Mheshimiwa Waziri mwingine, ambaye alibishana na askari wa usalama barabarani aliyekuwa akitimiza majukumu yake ya kazi kwa kumweleza makosa ya barabarani aliyoyatenda.  Badala ya kusikiliza makosa yake na kuadhibiwa kwa kadiri ya matendo yake, mke huyu aliitumia karata yake ya kupitia mgongo wa mumewe na kutoa kauli za kuudhi zisizofaa kwa yule askari.

Kwa mara ya kwanza katika kipindi kirefu sana, mambo yanaelekea kubadilika na wale waliokuwa wakidhani wapo juu ya sheria, wanakumbushwa tena kwamba Tanzania sio ya kwao peke yao.
Taarifa zinasema kwamba Rais John Pombe Magufuli ameamuru askari wa usalama barabarani aliyekuwa akifanya kazi yake na kuishia kutolewa maneno yasiyofaa na Mke wa Waziri, apandishwe cheo.  Vilevile, ameshamuonya Waziri na Mke wake kuhusiana na tukio hilo, kwani hakuna mtu aliye juu ya sheria.

Binafsi, taarifa hiyo imenifurahisha sana.  Tuseme tu ukweli kwamba Tanzania ilikuwa nchi ya ajabu sana.  Ilikuwa na matabaka makubwa sana kiasi cha watu kuzungumzia kutaka hata kukimbilia kuishi nje ya nchi, kutokana na kujiona hawathaminiwi, huku wengine wakitamba mitaani na kufukuzisha watu kazi kana kwamba wao ndio wamiliki halali wa nchi hii.

Tanzania ilifika mahali ambapo huyu askari wa usalama barabarani ambaye Rais ameamua kumpandisha cheo, angekuwa katika hali ngumu sana.  Kwanza angetafutiwa zengwe, kisha angehamishwa kituo cha kazi na kupelekwa kijijini huko kwenye kitengo cha kawaida kabisa.  Wale aliowaudhi, wangehakikisha kwamba jamaa harudi tena mjini, na anasahaulika kabisa.
Lakini yote hii ni kutokana na ulimbukeni wa kada fulani kudhani wako juu ya sheria na hawatakiwi kuguswa, huku sie akina yakhe tukiendelea kulipa faini halali na wakati mwingine kuadhibiwa na askari mwenye hasira za kutendwa na watu wa aina ya Mke wa Waziri.
Lakini pamoja na taarifa njema hizi tulizozisikia mwishoni mwa wiki, bado tuna safari ndefu sana.  Bado wapo watu wanaodhani wako juu ya sheria, hawatakiwi kuguswa na wanaruhusiwa kufanya chochote wanachojisikia kukifanya kwa kuwa wao ni wao na hawawezi kulinganishwa na Watanzania wengine.

Katika hili, naomba nizungumze na Mheshimiwa Rais na kumweleza maajabu ya Tanzania, ambayo bado hayajaandikwa kwenye Kitabu cha Guinness Book of Records.
Mheshimiwa Rais, hivi unafahamu kwamba kwenye nchi hii mtu akiwa na gari lenye nembo za Serikali, kama vile STK, huwa anavunja tu sheria za barabarani na haulizwi chochote?  Ataona watu wote tupo barabarani, tumesimama kwenye foleni, tunasubiri nafasi yetu ifike ili tuendelee na safari, lakini yupo radhi kupita hata njia za pembeni za watembea kwa miguu na hataguswa.  Eti ile nembo tu ya STK inamfanya awe juu ya sheria.

Mheshimiwa Rais, wapo pia hawa wengine ambao wanadhani kwamba kutokana na vyeo walivyonavyo, vyeo ambavyo aidha wewe ama watangulizi wao mmewapa, basi hata wakifika maeneo ya huduma za umma, kama vile hospitali, hawahitaji kufuata utaratibu wa kusimama kwenye foleni kama sisi wengine tufanyavyo.  Watafika, watawaona mmesimama, watapitiliza bila kuwasemesha huku wakiwa wamekunja nyuso zao kwa hasira na ukijaribu kuhoji, watakuuliza “unajua mimi ni nani?”  Hawa pia wanadhani wako juu ya sheria.

Mheshimiwa Rais, wapo pia wale ambao wanajiona wapo ‘grade’ ya juu zaidi.  Hawa hufikia mahala pa kutumia magari ya umma, magari ambayo sisi tunayalipia kodi ili yanunuliwe, yakarabatiwe na yajazwe mafuta, lakini wao kuamua kuyatumia kwa mambo yao binafsi.  Magari haya yatakwenda sokoni kununua mchicha na vitunguu, yatapaki saluni kumsubiri ‘mama’ ajiweke vizuri na yatapaki baa kusubiri bosi apate mapumziko ya kutosha, hata kama ni hadi usiku wa manane.  Yaani sisi tunakatwa kodi ili wao watumbue maisha, kwani wanadhani kwamba wako juu ya sheria.

Mheshimiwa Rais, wapo na wale ambao hata tukiwa kwenye foleni za benki, basi wao wataingia na kupitiliza ili wahudumiwe kwanza, kana kwamba wengine tuliosimama pale ni milingoti ya TANESCO na hatuna mambo mengine ya kufanya. Ukihoji, utasikia: “kwani wewe hujui mimi ni nani?  Nina mambo muhimu ya kitaifa ya kufanya.”  Unabaki unajiuliza, hivi kumbe kuna watu na WATU.  Kwa kila kitu, wao wapo juu ya sheria.

Naomba tu niseme kwamba hali hii ilikera kiasi kwamba tukaizoea na ndio maana hata Mke wa Waziri alipotoa maneno yasiyofaa kwa askari wa usalama barabarani, hakuna aliyejua kwamba askari yule angepandishwa cheo na Waziri kuonywa.  Sana sana, tulikuwa na uhakika kwamba hili litasambazwa sana kwenye mitandao ya jamii, huku wale wanaotukana askari kwamba wanachokitaka ni rushwa tu, wakiendeleza kauli hizo za kuudhi.

Watu walijiona kwamba wao ndio Watanzania halisi na wengine ni wa kusingiziwa.  Watu walijiona kwamba wao ndiyo pekee wenye haki miliki ya nchi.  Watu walijiona kwamba wao wako juu ya sheria. Mheshimiwa Rais, naomba nikuhakikishie kwamba watu hao bado wapo wengi…

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya May 6, Ikiwemo ya Mabaki ya Lowassa Yawatesa CCM

$
0
0

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya May 6, Ikiwemo ya Mabaki ya Lowassa Yawatesa CCM

Nuh Mziwanda Afunguka Kuhusu Kurudiana na Shilole

$
0
0
Msanii Nuh Mziwanda ambaye kwa sasa anafanya poa na wimbo wake mpya ambao amemshirikisha Alikiba amefunguka na kusema kuwa hata kama ikitokea mpenzi wake huyo wa zamani akitaka kurudiana na yeye ni kitu kisichowezekana kwa sasa.

Akizungumza kwenye kipindi cha 5SELEKT kinachorushwa na ting’a namba moja kwa vijana Nuh Mziwanda amesema kuwa kwa sasa yeye amefunga ukurasa wa mapenzi na Shilole hivyo hata ikitokea akataka kurudiana na yeye hawezi kufanya hivyo kwani ameshaanza maisha mapya ambayo anaona ni ya furaha zaidi.

Mbali na hilo Nuh Mziwanda ameeleza kuwa kwa sasa hataki tena maisha ya kiki na skendo alizoita kuwa ni za ajabu ajabu bali anataka kujenga jina lake kutokana na kazi zake kwenye muziki pamoja na kutengeneza muziki kama ‘Producer’

CHADEMA na Katibu Mkuu mfu..Ukimya Wake ni Hatari kwa Mustakabari wa Chama

$
0
0
Kiukweli huyu katibu mkuu hajui hata pa kuanzia Chama kinaonesha dalili za kuifuata TLP na UDP sioni harakati zake ki ukweli CHADEMA ilikosea sana Dr. Mashinji ni unpopular figure hata akitembea kwa miguu Karikoo hakuna wa kumshitukia kuwa ni kiongozi.

Ukimya wake ni hatari kwa mustakabari wa chama kwani watu wasiokuwa na vyeo kama akina Lowassa ndo wamekuwa msaada mkubwa kukisemea chama kwa sasa. Anaonekana kabisa ni uteuzi ambao ulikosewa na ni mtu asiyekua na ushawishi ndani ya chama.

Kutoka kwenye nchi ya viwanda mpaka nchi ya majipu alikuwa ana mengi ya kuongea lakini yupo kimyaa wakisubiri kuzungusha mikono mwaka 2020.

Huku serikali ya Magufuli ikijisafishia njia inaonekana haitapata upinzani mwaka 2020 kutokana na uchakavu wa CHADEMA.

By Allen Snr

PICHA: Jionee kaburi atakalozikwa Papa Wemba

$
0
0
Picha hii inasemekana ndilo kaburi atakapozikwa mwanamziki Maarufu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo maarufu kwa jina la Papa Wemba.

Huu ni zaidi ya ufahari, lakini mimi naona hauna maana..

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Singida Asimamishwa Kazi Baada ya Kutoa Taarifa za Uongo Kuhusu Watumishi HEWA

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Singida, Simion Mumbee amesimamishwa kazi baada ya kudaiwa kutoa taarifa za uongo kuhusu watumishi hewa.

Katika taarifa hiyo, Mumbee anadai watumishi hewa 19 waliogundulika kwenye halmashauri hiyo hawajaisababishia hasara Serikali jambo linalodaiwa kuwa si kweli.

Akizungumza jana kwenye ufunguzi wa kikao cha maendeleo mkoani humo, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mathew Mtigumwe alisema anamsimamisha kazi mkurugenzi huyo ili kupisha uchunguzi.

“Nilipotuma tume kufuatilia suala la watumishi hewa katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida, ilibaini wapo na wameisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh125 milioni,” alisema Mtigumwe.

Alisema taarifa ya Mumbee ililenga kuidanganya Serikali. Mtigumwe alimuagiza Katibu Tawala wa Mkoa, Dk Angela Lutambi kumuandikia barua ya kumsimamisha kazi mara moja.

Mtigumwe alisema hana nafasi ya kufanya kazi na watumishi wa aina ya Mumbee.

Wakati huo huo; Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu amemsimamisha kazi Ofisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea, Philbert Mtweve kwa tuhuma za kuwalipa mishahara watumishi hewa wanane na kuisababishia Serikali hasara ya Sh27 milioni.

Mwanaharakati Joyce Kiria Alia Ukata wa Fedha..Adai Kikwete Amestaafu Urais na Pesa

$
0
0
Mtangazaji wa Kipindi cha Wanawake Live, Joyce Kiria. Ameandika kwenye page yake ya Facebook
''Dady i miss u 😭. pesa imestaafu na wewe, maisha magumu kweli, siku hizi pesa naiona kwenye taarifa ya habari, habari za biashara''

Mange Kimambi Hongera Sana Ujasiri wa Kuvalia Njuga Mambo Yenye Maslahi Kwa Taifa...

$
0
0
Napenda kuchukua nafasi hii kumpongeza mwanadada jasiri asiyeogopa matokeo ya harakati anazofanya, ambazo nyingi zina maslahi kwa nchi yetu kwa ujumla wake.

Nafahamu kwamba kuna watu wengi tu wanamchukia huyu dada kwa tabia yake ya kuweka kila kitu wazi bila kujali madhara yake katika jamii au kwake yeye na hata familia yake.

Rejea madawa ya kulevya, na hata sasa alivyoamua kuacha kila kitu kikiwemo kile akipendacho UMBEA na kuweka maslahi ya Taifa mbele na zaidi akiungana na upinzani katika kuhakikisha kwamba Bunge linaonyeshwa live.

Hili la Bunge kutokuwa live lilionekana kwa watu wengi kama jambo zuri lakini hawa watu hawakujua ni kwanini serikali ilianza harakati hizi za kuminya haki ya kupata habari ambayo ni haki ya kikatiba kwa watanzania wote.

Hatahivyo, kati ya watu wachache waliojitolea kuungana na wabunge wa upinzani na wadau wengine ni huyu Mange Kimambi.

Mange, nakupongeza sana kwa ujasiri wako wa kukosoa yale yanayoonekana kuwa na matokeo chanya kwa jamii yetu in a long-run.

Hongera sana Mange na hongereni sana Wabunge wa Upinzani.

Japo mimi ni mwana-CCM, lakini nilikuwa ni moja kati ya watu waliokerwa sana na hatua ya Serikali kuingilia Bunge na hivyo kulikuwa na hatari ya Bunge kama Muhimili muhimu wa kuisaidia serikali katika kuendesha nchi kukosa nguvu na kuwa sehemu ya serikali.

Jambo hilo likitokea, basi tulipokuwa tunaelekea ni kubaya kuliko tulipotokea.

NARUDIA TENA, HONGERA SANA DADA MANGE KIMAMBI NA MUNGU AZIDI KUKUPIGANIA WEWE NA FAMILIA YAKO.

By JATELO1

Simba Kushushwa Daraja kwa Kupuuza Agizo la FIFA

$
0
0
Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), limeipiga faini ya Franc 2,000 za Uswisi (Sh 4,582,000 za Tanzania), Klabu ya Simba baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kupuuza maagizo ya Idara ya Utatuzi wa Migogoro (Desputes Resolution Chamber) ya FIFA.


Kamati ya idara hiyo iliyokutana na Aprili 20, 2016 huko Zurich, Uswis ilitumia Franc 500 (sawa na Sh 1,145,500) hivyo Simba pia imeagizwa kuzilipa ikiwa ni gharama za kikao cha kufuatilia utekelezaji sakata la mchezaji huyo, raia wa Kenya.
Simba imeelezwa kupuuza kumlipa mchezaji Donald Musoti Omanua kwa wakati tangu mkataba wake uvunjwe.

Musoto aliyesajiliwa na Simba msimu wa 2014/15 na kuachwa alilalamika FIFA ambayo iliona ana hoja na hivyo Simba kutakiwa kumlipa dola 29,250 (sawa na Sh 62.8 milioni) na kiasi kingine anachodai ni Dola 600 (Sh 1,290,000) zilizobaki katika usajili ambapo jumla yake ni Sh 64.2 milioni.
Pia Mosoti anamlipa Mwanasheria wake dola 2,000 (Sh 4.3 milioni) kwa ajili ya kusimamia kesi hiyo.

Felix Majani, Mwanasheria wa Musoti, ambaye pia ni mmoja wa wanasheria wa FIFA, alifungua kesi katika shirikisho hilo kuwashitaki Simba kwa kukiuka makubaliano ya mkataba na mteja wake.
Kwa kosa hilo Simba inatakiwa kulipa faini ya kiasi hicho cha fedha ndani ya siku 30 kuanzia tarehe ya kupokea barua hiyo ya FIFA iliyoandikwa Mei 3, mwaka huu na kufika Tanzania leo Mei 6, 2016. TFF imekuwa nakala na maagizo kuisimamia Simba inalipa kiasi hicho cha fedha.

Simba imeagizwa kulipa stahiki zote za Mosoti ndani ya siku 30 kuanzia tarehe ya kupokea barua hiyo ya FIFA iliyoandikwa Mei 3, mwaka huu na kufika Tanzania leo Mei 6, 2016.
Katika barua hiyo ambayo TFF ina nakala yake, Simba imepewa amri ya kuhakikisha inalipa na isipotekeleza agizo hilo mara moja itakatwa pointi tatu katika mechi zake Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara –VPL.

FIFA imekwenda mbali zaidi ikisema ikiwa klabu hiyo kama haitalipa katika muda uliopangwa yaani siku 30 kutoka sasa, FIFA itaishusha Simba daraja kutoka Ligi Kuu Tanzania Bara hadi Ligi Daraja la Kwanza au zaidi.
Kwa upande wake, TFF imagizwa kuhakikisha uamuzi huo unasimamiwa vema utekelezwaji wa maagizo hayo vinginevyo itachukuliwa hatua stahiki ikiwamo kuiondoa Tanzania katika mashindano ya kimataifa.
Viewing all 104775 articles
Browse latest View live




Latest Images