Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104416 articles
Browse latest View live

DONALD Trump Atashinda Uchaguzi USA..Akosekana wa Kumzuia

0
0
1.Wapinzani wa Donald Trump wamejitoa wote baada ya matumaini yao kumzuia kushindikana.
2.Hakuna namna tena ya kumzuia billionea Donald Trump kuwa mgombea urais wa Republican.
3.Chama cha Republican kinashuhudia mgawanyiko na mpasuko mkuwa kabisa kuwahi kutokea kuliko wakati mwingine wowote.
3.Wanachama wa Republican wameonekana kuchoma moto kadi zao za uachama kama hasra zao kwa mgombea ambaye hawamtaki.
4.Wapo wanaosema hawatashiriki kabisa kupiga kura uchaguzi mkuu kwa kuwa Donald Trump hawamtaki na hawawezi kumpigia kura Hillary Clinton.Wapo ambao wanajiondoa katika chama.
5.Wapo wanaosema watalazimika kumchagua Hillary Clinton maana hawako tayari kuona Donald Trump anakuwa Rais wa Marekani.
6.Wapo wanaoona ni bora tu wakubaliane na hali na kumuunga mkono mtu ambaye hawamtaki kwa manufaa ya chama.
7.Aliyekuwa Rais wa 41 wa Marekani George H.W Bush mwenye umri wa miaka 91 amesema atajiweka kando katika uchaguzi huu na hana mpango wa kumuunga mkono Donald Trump.
hii ni mara ya kwanza kwa George H.W Bush kutomuunga mkono mgombea wa chama chake cha Republican katika chaguzi zote.
8.Aliyekuwa rais wa 43 wa Marekani George W Bush(Junior ) naye amesema atajiweka kando katika uchaguzi huu na hatamuunga mkono Donald Trump.
NB:Marais wastaafu wa Republican walio hai ni hawa Bush wawili kwa maana ya baba na mwana.
9.Aliyekuwa mgombea Urais wa Republican 2012 Mitty Romney amesema hatamuunga mkono Donald Trump na ameenda mbali zaidi kwa kusema kuwa hata kwenye mkutano mkuu wa kumtanganza mgombea pale Cleveland hatashiriki.
10.Aliyekuwa mgombea Urais wa Republican 2008 John McCain naye yupo mbioni kutoa taarifa rasmi.Taarifa za awali zinadokeza kuwa naye atachukua msimamo wa kutomuunga mkono Donald Trump na atajiweka kando katika uchaguzi huu.
11.Matajiri wapenzi wa chama nao wamegawanyika kama ilivyo hapo juu kwa makundi mengine wapo ambao wameonekana tayari kumuunga mkono Hillary Clinton kwa kuandika hadharani kauli mbiu ya Hillary Clinton I AM WITH HER (wakimaanisha wanamuunga mkono Hillary Clinton na si mgombea wa chama chao).
Joseph Mshinga.

Kwa Hali Hii ni ‘Ni Ndoto Tanzania Kuwa na Uchumi wa Viwanda

0
0
Wabunge wamesema ni vigumu Tanzania kufikia lengo la kuwa na uchumi wa viwanda iwapo Serikali itaendelea kusuasua kutekeleza miradi yenye mchango mkubwa katika sekta hiyo.

Akisoma maoni ya Kamati ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kwa mwaka 2016/17, Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo, Vicky Kamata alisema hawaridhishwi na namna Serikali inavyotoa fedha za bajeti kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali.

“Kwa kuzingatia takwimu hizi ni dhahiri miradi mingi ya maendeleo iliyopangwa kutekelezwa katika mwaka huu wa fedha haitatekelezwa,” alisema Kamata.

Alisema kamati hiyo inaunga mkono dhamira ya Serikali ya kuifanya nchi kuwa ya uchumi wa viwanda ifikapo mwaka 2025 lakini hairidhishwi na kasi ya utekelezaji wa azma hiyo.

“Hali hii ikiendelea itakuwa vigumu Tanzania kuwa nchi ya viwanda iwapo Serikali itaendelea kuchelewesha utekelezaji wa miradi yenye mchango mkubwa katika sekta hii,” alisema.

Kwa maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuhusu bajeti ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mbunge wa Moshi Vijijini, Anthony Komu alisema: “Kamwe tusijiaminishe kuwa tunaweza kufikia Taifa la viwanda kwa Sh42.159 bilioni kwenye bajeti ya mwaka kama fedha za maendeleo kwa ajili ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji,” alisema.

Akiwasilisha hotuba ya bajeti bungeni jana Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage alisema kati ya viwanda 106 vilivyofanyiwa tathmini, viwanda 45 vinafanya kazi, 24 vinasuasua na 37 vimefungwa.

“Mpango wetu ni kuhakikisha kuwa viwanda 35 vilivyobaki vinafanyiwa tathmini haraka na kabla ya nusu ya kwanza ya mwaka wa fedha unaoanza Julai Mosi mwaka huu, hatima ya viwanda visivyofanya kazi itajulikana,” alisema.

Alisema hatima ya wenye viwanda visivyofanya kazi ni kwa wamiliki kutekeleza mkataba ya mauzo au kupewa wawekezaji wapya ili waviendeleze,” alisema.

Wizara hiyo imeomba kutengewa Sh 81.87 bilioni katika mwaka wa fedha 2016/17 kati ya hiyo, Sh41.87 bilioni sawa na asilimia 51 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Sh40 bilioni ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.

Riyama Afunguka Kutomsamehe Mtu Huyu kwa Kumdhulumu Pesa

0
0
MWIGIZAJI mahiri katika tasnia ya filamu Bongo Riyama Ali amelalamikia madalali wa kazi za wasanii kwa kuwa chanzo cha dhuluma kwa wasanii wanaotengeneza filamu, huku wao wakijinufaisha na jasho lao akiongaea na FC Riyama amedai kuwa ametapeliwa kazi yake ya Kajala.


hajui jinsi gani umepata fedha hadi kuunga unga na kutoa filamu bila ya huruma mtu anakudhulumu mimi kazi yangu Kajala hadi leo nimetapeliwa na mtu aliyeuza kwa Steps amenilipa pesa kidogo na filamu imetoka ina muda sasa,”

Msanii huyu amelalamikia mfanyabiashara maarufu kwa filamu za zaga zaga jina tunalihifadhi kuwa alichukua kazi yake kwa makubaliano kuwa anajuana na msambazaji haiwezi kukaa foleni hivyo angepata malipo yake kwa wakati lakini ameambulia kupewa fedha kidogo huku mtu huyo hapokei simu na kumtishia kuwa yeye anajulikana.

Aidha Riyama amedai kuwa Serikali na vyama vya wasanii viangalie jinsi ya kulinda maslahi ya wasanii wanaibiwa sana,kwani kumekuwa na tabia ya udalali wa filamu kwenda kwa wasambazaji ambao kazi ucheleweshaji ambao unajenga mazingira ya Rushwa.

“Nimekuwa na busara sana kwani nashangaa yeye kulipwa fedha huku filamu ikiwa kila kitu kimeandikwa mimi Riyama Ally ilikuwaje alipwe yeye bila mimi kuwepo?,”anasema Riyama Ally.

Mamlaka ya Mapato (TRA) Yataifisha na Kugawa Bure Sukari Mifuko 5,319 toka Brazil Yenye thamani ya Sh 373.5 milioni

0
0
Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA imegawa Sukari yote ya Magendo Mifuko 5319 yenye thamani ya Zaidi ya Shilingi Million 373.5  kwa Taasisi mbali mbali Mkoani Lindi baada ya kuthibitishwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA kuwa ni Salama kwa matumizi.

Sukari hiyo ilikamatwa mwezi Februari mwaka huu katika bandari ya Lindi ndani ya meli ya MV Hassanat ikiingizwa kinyume cha Sheria ikitokea nchini Brazil kupitia Zanzibar.

Sukari hiyo ilipaswa kulipiwa Kodi zaidi ya shilingi Million 246.

Mama Salama Amtetea Rais Mstaafu Jakaya Kikwete

0
0
SALMA Kikwete, Mke wa Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete ameonesha kukerwa na wale wanaoshambulia utawala wa mumewe (Rais Kikwete) na kwamba, hakuna sababu ya kufanya hivyo.

Mama Salma alisema hayo jana kwenye mkutano wa Umoja wa Wanawake (UWT) unaofanyika mjini Dodoma katika ukumbi wa mikutano wa CCM Makao Makuu.

Alitoa kauli hiyo ikiwa ni siku moja baada ya kujitokeza hadharani kumkingia kifua mtoto wake Ridhiwani Kikwete kuhusu kuhusika kwake na mkataba wenye utata wa Kampuni ya Lugumi.

“Kila mwaka naendelea kuisemea serikali iliyopo madarakani mambo mazuri, acheni hali ya kukaa na kuanza kusema kwamba serikali ile ilikuwa vile na serikali hii iko hivi.

“Wala msisema yule alikuwa vile na huyu yuko hivi, kwa kumalizia hayo napenda kusema mume wangu ambaye ni mwenyekiti wa CCM Taifa anawasalimia sana,” alisema Mama Salma.

Akizungumzia utumbuaji wa majipu alisema, serikali kwa sasa imeanza kutumbua majipu makubwa kuanzia juu lakini zipo taarifa kuwa, yapo majipu mengine ngazi za chini pia ndani ya CCM.

Alisema, “kila anayejitambua kuwa ni jipu kabla hajafikiwa ni bora akajitumbua mwenyewe au ajipake spriti ili jipu hilo lipoke mapema kabla halijatumbuliwa.”

Hata hivyo alionesha wasiwasi kuwa, kuna uwezekano miradi mingi ya UWT ikachukuliwa kutokana na umoja huo kuwa na mali ambazo zinaonekana kumilikiwa bila kufuata taratibu.

Alisema, kwa upande wa ardhi kuna viwanja vingi ambavyo havina hati na vimekaa muda mrefu bila kuendelezwa jambo ambalo kwa sasa mameya wanaweza kuvibadilishia matumizi.

Jukwaa Huru la Wazalendo Tanzania limeguswa na hujuma kwa Rais Magufuli

0
0
Mei 8 2016 Jukwaa huru la Wazalendo Tanzania limekutana na Waandishi wa Habari Dodoma ili kutoa tamko lao kuhusu hujuma dhidi ya Rais John Pombe Magufuli.

Katibu wa jukwaa hilo Mtela Mwampamba amesema
’Kwa miaka mingi Watanzania tumekuwa tukipiga kelele tukilia juu ya kero mbalimbali za Serikali kushindwa kupambana na watumishi wasio wema na wabadhirifu, mafisadi, wala rushwa na wahujumu uchumi‘

‘Vita hii tumekuwa tukipigana sisi wanyonge na baadaye ikaungwa mkono na makundi mbalimbali wakiwemo wanasiasa, Sasa tumempata Rais Magufuli anayefanya kazi bila kuchoka kuifikisha Tanzania tunakokutaka, wanasiasa hao wamegeuka na wanaanza kumhujumu‘

‘Tumeshangazwa zaidi tunaposoma na kusikia katika vyombo vya habari baadhi ya wanasiasa wakianza kumkejeli Rais Magufuli eti anaendesha nchi kinyume cha sheria na kuipeleka katika utawala wa kiimla‘

‘Ni kwasababu hii, sisi wazalendo tunasema hoja za wanasiasa na wasomi kusema Rais analeta utawala wa kidikteta kwa kutumbua majipu tunaona ni hali zilizojaa hisia binafsi na zaidi ujasiri wa hujuma‘

Mwampamba hajaacha lipite hili la Sukari, nalo anasema…>>’Baadhi ya wafanyabiashara kuficha badhaa muhimu ya sukari, tunatumia fursa hii kuwakumbusha kuwa waachane na hujuma hiyo mara moja.‘

‘Wanaoendesha uhujumu huo wa uchumi ni sawa na hawa wanasiasa wanaoendekeza hujuma dhidi ya Rais Magufuli ili asiendeleze mageuzi ambayo Watanzania wenyewe waliyataka na wameyasubiri kwa muda mrefu‘

Mwanamuziki Diamond Atoa Ujumbe Huu kwa Zari Hassan Katika Siku ya Mama Duniani...

0
0

Ujumbe wa Diamond kwa zari (mothers day)

From @diamondplatnumz - A very Special Mother's day to this Beautiful and Humble soul of Mine @zarithebosslady ... i wish you can understand how much i love you, Mpaka natiwa Dripu😥....wenyewe wanasema kuzaa sio tija, ila kumpata Mwanamke akajua kumlea mtoto wako Vyema ndio kazi inakuwaga hapo... Shukran sana kwa zawadi hii kubwa ya Mtoto mzuri na kuendelea kumlea vizuri..... sjui na lile jipu pia Ntumbue😃.... aaagh! Anyway'z😝🙋 tutakutana Mbeleni

Msichana wa Miaka Kumi na 14 Aua Watu Wanne Kwa Sumu Siku ya Harusi yake

0
0

Msichana mdogo alieolewaBi harusi wa miaka 14 nchini Nigeria ameshtakiwa kwa kuwaua watu wanne akiwemo mumewe wa miaka 35 baada ya kuweka sumu ya panya katika chakula alichoandaa kwa sherehe za haruysi yake.

Kesi hiyo imewashangaza wahaharakati wa haki za kibinaadamu ambao wamesema kuwa msichana aliyeozwa kwa mume aliye mara mbili umri wake anafaa kuchukuliwa kama mwathiriwa na wala sio muhalifu.

Wasila tasiu kutoka familia masikini katika eneo la waislamu la kazkazini huenda akakabiliwa na kifo iwapo atahukumiwa.

Shahidi wa kwanza wa kiongozi wa mashtaka Lamido Abba Sorron-Dinka alikuwa msichana wa miaka 7 anayejulikana kama hamziyya,ambaye alikuwa akiishi katika nyumba moja na Tasi'u pamoja na mumewe Umar sani,wakati bi haru huyo alipoweka sumu ya panya katika chakula hicho.

Hamziyya alijulikana tu kama dadaake mke wa kwanza wa bwana Sani,mwanamke aliyeolewa na marehemu awali katika eneo ambapo ndoa za wake wengi zimekithiri.

Msichana huyo wa miaka 7 alisema kwamba Tasi'u alimpa fedha ili kununua sumu ya panya kutoka duka moja jirani mnamo tarehe 5 mwezi Aprili,siku ambayo bwana Sani alifariki.

Alisema kuwa panya wanamsumbua katika chumba chake'',Hamziyya aliiambia mahakama.Upande wa mashtaka baadaye ulisema kuwa badala yake Tas'u aliweka sumu hiyo ya panya katika chakula ambacho alikuwa amekiandaa kwa sherehe za baada ya harusi kwa kuwa alijuta uamuzi wake wa kumuoa bwana Sani.Msichana huyo alikataa kuzungumza mahakamani.

Jaji Mohammed Yahaya,katika mahakama ya Gezawa alitoa hukumu kwamba Tasi'u ambaye alikataa kuongea katika mahakama hana hatia katika kusikizwa kwa kesi mnamo mwezi Octoba ambapo alisomewa mashtaka.

Jaji huyo alikataa ombi la upande wa mshtakiwa la kesi hiyo kupelekwa katika mahakama ya watoto.

Ushahidi wa Hamziyya uliungwa mkono na Abuwa Yussuf muuzaji duka katika mji wa Unguwar Yansoro ambaye alithibitisha kuuza sumu hiyo kwa mtoto huyo.

Jirani ya Bwana Sani mwenye umri wa miaka 30 ambaye ni mkulima, Abdulrahim Ibrahim alitoa ushahidi ambapo alisema kwamba alipewa chakula hicho kilichopikwa na Tasiu.''Nilipoletewa chakula hicho niliona vipande vipande vyeusi''aliiambia mahakama.

Alikula vipande vinne vya madonge vilivyotengezwa na maharagwe lakini hakupendelea ladha yake'',alisema na kuongezea kuwa ni Umar pekee aliyeendelea kula.

Baadaye alisema kuwa alimuona bwana Sani katika bustani ,akiwa mgonjwa na kumpeleka nyumbani.

Lakini alipokuwa akijaribu kumuuguza bwana sani ,aligundua kwamba watu wengine watatu ambao walikuwa wamekula chakula hicho wamefariki kwa ghafla.

Viongozi wa mashtaka walidai kwamba chakula cha Tasiu kilichowekwa sumu kiliwaua watu wanne na hivyobasi kuwajumuisha wanne hao katika kesi moja ya mauaji.

Nigeria haijawahi kumyonga mtoto aliyefanya uhalifu tangu mwaka 1997,ambapo taifa hilo liliongozwa na dikteta Sani Abacha,kulingana na shirika la kibinaadamu la

Rais Magufuli Atetea Uamuzi wake wa Kutimua Wafanyakazi

0
0
Rais John Magufuli ametetea uamuzi wake wa kuwatimua baadhi ya watumishi wa umma wanaokiuka maadili akisema anataka kuirejesha nchi kwenye mstari.

Rais amesema hayo leo alipozungumza na waumini katika misa ya Jumapili katika Kanisa Katoliki parokia ya Tokeo la Bwana Burka jijini Arusha.

Amesema watu katili ni wale ambao walikuwa wanawaibia Watanzania na kuwanyonya wanyonge.

Amesema analazimika kuchukua hatua ya kuwafukuza kazi si kwamba ni katili, bali lengo ni kuwatumikia Watanzania na kuirejesha nchi kwenye mstari.

Rais huyo aliyejibatiza “mtumbua majipu”,  amesema Tanzania ni taifa tajiri, hakuna sababu ya wananchi kulalamika kila kona, kwani kuna ardhi ya kutosha, madini ya kila aina, wanyama wa aina mbalimbali ambao baadhi wameanza hadi kupelekwa nje.

"Ninapochukua hatua nataka kuweka Tanzania iliyonyooka, mimi tayari nimesema nimejitoa sadaka kwa watanzania hasa wanyonge," alisema.

Mauaji Gesti ..Meya Ataka Gesti zifungwe Kamera za Siri...

0
0
Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita ameshauri kufungwa kwa kamera maalumu  za CCTV kwenye  nyumba zote za kulala wageni na hoteli ili kuimarisha ulinzi.

Ushauri huo wa Mwita unakuja baada ya  siku sita  kupita , kutokea kwa tukio la mwanamke mmoja kufariki dunia akiwa gesti.

Mwita ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Vijibweni (Chadema), alisema mamlaka husika wakiwamo wamiliki wa hoteli na nyumba hizo waliangalie suala hilo kwa jicho la tatu kwani litasaidia kwa kiasi kikubwa kuzuia matukio kama hayo.

“Kamera hizi zisifungwe chumbani bali zifungwe maeneo ya nje  na mapokezi kwenye jingo husika.Hii ni njia sahihi ya kupambana na matukio kama haya maana hili lipo hivi linaweza kutoke lingine zaidi ya hili,” alisema Mwita ambaye alishika madaraka hayo Machi 22mwaka huu.

Mbali na hilo, Mwita alisahauri pia kuboreshwa kwa mfumo usalama katika maeneo mbalimbali ili kuzuia vitendo kama hivyo vya kinyama vinavyokatisha uhai wa binadamu.

Hata hivyo , Mwita  aliwaomba viongozi wa dini wa mkoa wa Dar es Salaam, kuendelea kutoa elimu kwa umma ili wakazi wa jiji hilo kumrudia Mungu na kuachana na vitendo vya kinyama.

Pia meya huyo amekanusha taarifa zilizosambazwa kwenye  mitandao ya kijamii zikimnukuu yeye kuwa ameshauri wamiliki wa gesti  kuwapiga picha wageni wanaokwenda kulala kwenye nyumba hizo.

Hivi karibuni mwanamke huyo jina limehifadhiwa alikutwa amefariki dunia kwenye gesti  Bray iliyopoa maeneo Kimara , manispaa ya Kinondoni huku chanzo cha kifo bado hakijawekwa wazi hadi uchunguzi utakapokamilika na maiti huyo amehifadhiwa Hospitali ya Mwananyamala.

Wahitimu Chuo cha Utumishi wa Umma Waonywa

0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Tawala Bora, Angela Kairuki amewataka wahitimu wa Chuo cha Utumishi Umma nchini (TPSC)  kutojihusisha na masuala ya ufisadi, rushwa na matumizi mabaya ya madaraka kazini badala yake wawe  wachapakazi watakapowatumikia Watanzania.

Kairuki alitoa kauli hiyo kupitia hotuba yake iliyosomwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla alipomwakilisha waziri huyo kwenye mahafali ya 24 ya chuo hicho  yaliyofanyika tawi la Mbeya.

 Alisema   wakati Serikali ya awamu ya tano ikiendelea kupambana na watumishi hewa, mafisadi na wazembe kazini, wahitimu katika chuo hicho wahakikishe wanakwenda kufanya kazi kwa  weledi kwa  kuzingatia kanuni, sheria na taratibu za utumishi popote watakapoajiriwa.

  “Huu ni wakati wenu kuonyesha utofauti kati ya aliyehitimu chuo na kuwatumikia wananchi kwa uadilifu, yule ambaye hajapitia chuo chochote, lakini yupo ofisini utendaji kazi wake unadhihirisha kuwa hakustahili kuwapo mahali hapo,” alisema.

Floyd Mayweather Kurudi Tena Ulingoni, Kuzichapa na Staa wa UFC, Conor McGregor

0
0
FLOYD MAYWEATHER na staa wa UFC, Conor McGregor wapo mbioni kuingia ulingoni kuzichapa kwenye pambano kubwa na aghali zaidi la masumbwi katika historia.

Gazeti la The Sun limedai kuwa Mayweather, anatarajia kuzichapa na staa huyo jijini Las Vegas mwaka huu.

Mayweather alitangaza kustaafu ndondi akiwa ameshinda mapambano yote 49 aliyowahi kupigana. Kwenye pambano hilo Mayweather atachukua paundi milioni 100 huku McGregor atachukua paundi milioni 7.

Tangazo rasmi litatolewa wiki chache zijazo.

Chanzo kililiambia gazeti la The Sun kuwa Floyd alichukia baada ya Conor kudai anaweza kumtwanga KO ndani ya sekunde 30 tu na sasa anataka kumuonesha kazi.

Mke Wangu Ataniua Jamani, Anataka Tufanye Mapenzi Kila Siku

0
0
Mke wangu siku hizi mapenzi sijui niseme yameongezeka au sijui niseme ana nikomoa nasema hivi kwa sababu ndani ya wiki kama mbili zilizopita amekuwa akinilazimisha nifanye mapenzi kila siku hapa nilipo kichwa kinaniuma kutokana na mabao nitoayo kila siku.

Leo nimeona nivunje ukimya baada ya kuniamsha usiku wa manane nifanye nae mapenzi nikamueleza mke wangu utaniua naomba tupumzike hata siku tatu mbele target yangu ni kuwa baada ya siku tatu anatarajia kuingia kwenye siku zake so ntapata mapumzo ya kutosha.

Cha ajabu mke wangu kaanza kulia na kulalamika kuwa haamini kauli yangu ya kukataa kufanya nae mapenzi, ilinibidi nimmbeleze kisha nikampoza na kamoja hapa nilipo nipo njiani natoka kazini ameshanitumia massege ananiambia eti niwahi anahamu ya dudu langu nimekaa kimya sikumjibu kanipigia simu anasisitiza alichokiandika kwenye massage yake tena kwa sauti ya majonzi.

Nampenda mke wangu ila ananichanganya kwa vile tabia hii hakuwa nayo mi ndio nilikuwa initiator wa mchezo wetu.

Hebu wadau naombeni mnisaidie itakuwa kapatwa na nini hadi amekuwa hivi? Tabia hii kaanza tangu niliporudi kutoka safarini ambapo nilikaa kule kwa miezi miwili na wiki moja bila kushiriki.

Jahazi la Simba Lazama Mbele ya Timu ya Mwadui Nakuipa Yanga Ubingwa wa Ligi ya Vodacom

0
0
Leo jioni timu ya Simba imekubali kichapo kitakatifu toka kwa timu ya Mwadui ya Shinyanga inayofundishwa na Kocha wa Zamani wa Simba Julio..Kichapo hicho cha goli moja bila goli lililofungwa na Mchezaji Jamal Mnyate Dakika ya 73 linaifanya Yanga Kutangazwa Mabigwa wa ligi ya Vodacom kwa vile hakuna timu inayoweza kufikisha point alizonazo Yanga....

Poyeni Simba....

Utumbuaji Majipu Siyo Ukatili- Rais Dkt. Magufuli Afunguka Kanisani

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amesema hatua anazochukua kwa ajili ya kuwasimamisha watumishi wa umma kazi zisitafsiriwe kama ni ukatili kwakuwa watumishi hao wamekuwa wakifanya mambo kinyume na maadili ya utumishi wa umma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 08 Mei, 2016 ameungana na waumini wa Parokia ya Toleo la Bwana iliyopo katika Jimbo Katoliki la Arusha kusali ibada ya Jumapili, ambapo katika salamu zake amewaomba watanzania kuendelea kuiombea nchi yao ili kazi anayoifanya ya kukabiliana na matatizo yanayowakabili watanzania wanyonge ifanyike kwa mafanikio.
Dkt. Magufuli amesema hayo alipokaribishwa na Mwenyekiti wa Parokia hiyo Bw. Philemon Mushi kuwasalimu waumini wa kanisa hilo, mara baada ya kumalizika kwa ibada ya Jumapili ya kupaa kwa Bwana.

"Niko pamoja na nyinyi ndugu zangu watanzania na wana Arusha wote, napenda kuwaahidi tena sitawaangusha, nitasimama mbele kuwatetea masikini, siku zote nitakuwa upande wenu, siku zote nitatembea na nyinyi, nasema kwa dhati kabisa na nataka muamini hilo kwamba sitawaangusha" amesema Rais Magufuli huku akishangiliwa na waumini walioshiriki ibada hiyo.
Rais Magufuli amewahakikishia watanzania wote kuwa atahakikisha ahadi zote alizoziahidi anazitekeleza na amewaomba watanzania wote kuungana na kushikamana ili kufanikisha juhudi za kuijenga Tanzania bora.

"Ninajua kuongoza ni kazi kubwa, ninajua kuongoza Taifa lililo masikini kama Tanzania inahitaji mkono wa Mungu, kwa hiyo niwaombe sana ndugu zangu Wakristo na watanzania kwa ujumla, muendelee kuliombea Taifa hili, kuniombea mimi, na pia kujiombea sisi wote ili amani tuliyonayo katika nchi yetu iendelee kudumu katika maisha yote.

"lakini siku zote katika matendo yetu kila tunapofanya tumtangulize Mungu kwa sababu Mungu ndio kila kitu, lakini tutambue kwamba siku moja tutakufa, kwa hiyo ni vyema katika matendo yetu tutakapokuwa hapa duniani tujitahidi sana kufanya matendo mazuri kwa ajili ya watu na hasa watu wanyonge, ambao kwa kweli watanzania waliowanyonge wanapata shida sana" Amebainisha Rais Magufuli.

Pia Dkt. Magufuli amewasihi watanzania wote kuachana na ushabiki wa vyama vya siasa na badala yake waungane katika ujenzi wa Taifa na kukabiliana na kero zinazowaumiza

ADC Yawafuta Uanachama Wanachama wake Wanne Akiwemo Mwenyekiti wa Chama hicho Said Miraaj kwa Kususia Uchaguzi mkuu wa Marudio wa Zanzibar

0
0
Chama cha Alliance for Democratic Change ADC kimewafuta uanachama wanachama wake wanne akiwemo Mwenyekiti wa chama hicho Bwana Said Miraaj,Katibu Mkuu Bi.Lydia Bendera,Mkurugenzi wa mipango na uchaguzi Bwana Jumanne Magafu pamoja na Katibu wa Kamati ya ulinzi Bwana Juma Wandwi kwa makosa ya kukiuka katiba ya chama hicho kwa kususia kushiriki uchaguzi mkuu wa marudio wa Zanzibar.

Maamuzi hayo yamefikiwa katika mkutano mkuu wa chama hicho ambapo akizungumza baada ya ufunguzi aliyekuwa mlezi wa chama cha ADC ambaye pia ni Waziri wa Kilimo Zanzibar,Mhe.Hamad Rashid amesema katiba ya chama inasisitiza ushiriki katika kugombea nafasi mbalimbali za uongozi,hivyo kutoshiriki ni kukivunja nguvu chama katika mikakati yake ya kuchukua dola.

Akizungumza na wajumbe wa mkutano mkuu wa -ADC- Msajili Msaidizi wa vyama vya siasa Bwana Sisty Nyahoza amesema kitendo cha chama cha siasa kutoshiriki uchaguzi kinakwenda kinyume na sheria ya vyama vya siasa na malengo ya kuanzishwa chama Chochote cha siasa na kusisitiza ipo haja ya kuangalia mfumo wa usajili wa vyama utakaowezesha kutoa adhabu kwa vikavyoonekana kukataa kushiriki katika chaguzi.

Aidha katika mkutano mkuu huo, wajumbe wamemchagua aliyekuwa mlezi wa ADC ambaye kwa sasa ni Waziri wa Kilimo Zanzibar Mhe.Hamad Rashid kuwa mwenyekiti wa chama hicho taifa na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Bwana Doyo Hassan Doyo amechaguliwa kushika wadhifa wa katibu mkuu wa chama.

Gadna : Sina Ugomvi na Jide, Nimemkojoza Miaka 15

0
0
Gadna ameonekana kwenye video akiwa jukwaani akitamka hayo maneno baada ya kuulizwa kama ana ugomvi na aliyekuwa mke wake Lady Jaydee.

"Sina ugomvi na yule mtoto wa kike, nimemkojoza kwa miaka 15 "

Kisha Dj akapiga Ze ndi ndi ndi na Gadna kuanza kucheza kwa mbwembwe zote.


Ninayo video ila sijui jinsi ya kuiweka.

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu Ya May 9, Ikiwemo ya Sukari iliyofichwa yagawiwa Bure

0
0

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu Ya May 9, Ikiwemo ya Sukari iliyofichwa yagawiwa Bure

Naibu Waziri Anthony Mavunde Apewa Maji Machafu na Wapiga Kura Wake Ili na Yeye Ayanywe

0
0
Wakazi wa Kijiji cha Nala na vitongoji vyake juzi walimpelekea maji machafu Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Anthony Mavunde wakimtaka ayanywe kwa kuwa ndiyo wanayotumia.

Mavunde alikutana na mkasa huo muda mfupi alipoingia kwenye kijiji hicho umbali wa kilomita tisa nyakati za jioni, ambako wakazi wa eneo hilo walikuwa wakimsubiri tangu asubuhi.

Mama mmoja aliyekuwa eneo hilo, alifika na chupa ya maji akimtaka Naibu Waziri ayaonje mbele yao, kwani nao ni binadamu kama yeye na wanayatumia, lakini Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Dodoma Mjini, Paul Luhamo alimzuia kuyanywa.

Pamoja na taarifa ya kijiji iliyotolewa na Ofisa Mtendaji wa Kata, Mathias Ndologa, wakazi hao walilipuka na kupiga kelele wakiipinga taarifa hiyo kwamba iligusa kwa juu matatizo yao, lakini ikaacha jambo kubwa la maji.

Kwenye risala yake, Ndologa alikuwa ameelezea suala la maji, umeme, miundombinu na upungufu wa madawati, lakini kelele zilizidi kutoka kwa wananchi wakisema jambo la msingi kwao ni moja tu, yaani maji.

Muda mfupi kelele zilianza watu wakitaka kuuliza mambo waliyoyaita ni ya msingi, ndipo Mavunde akaamuru wapewe nafasi ya kuuliza kwanza kabla hajasimama kuwasalimia.

Mmoja wa wauliza maswali alikuwa Daudi Lusinde, ambaye alieleza namna wakazi wa kijiji hicho wanavyopata adha kubwa katika kutafuta maji ambayo aliyaita ni kama dhahabu kwao.

Lusinde alisema wamepata tabu hiyo kwa muda mrefu na bado hawajaona mwanga wa matumaini zaidi ya kuendelea kuumia huku ndoo ya maji ikifikia bei ya Sh500.

“Bei ya sukari inapanda kila kukicha, lakini siyo shida hapa tatizo ni maji, mheshimiwa sisi tunanunua maji kwa gharama kubwa na ukishindwa kiasi hicho unalazimika kuchangia maji na mifugo sijui kama tutapona,” alisema Lusinde na kusababisha mkutano kulipuka kwa shangwe.

Uongozi wa kijiji na chama wilaya ulizuia kelele za vijana waliomtaka mbunge huyo aende hadi maeneo wanayochota maji akajionee, ikiwamo uchafu wa maji pamoja na umbali wake.

Akijibu hoja hizo, Mavunde alieleza kusononeshwa na kuahidi kuanzia leo ataanza kutekeleza ahadi yake hiyo kabla ya kufanya jambo lolote.

“Kwa kweli maji ni moja ya ahadi nilizoahidi kwenu, kesho ni Jumapili siyo siku ya kazi, lakini kuanzia keshokutwa (Jumatatu) nitaleta hapa wataalamu kuanza kuchimba kisima kwa gharama zangu,” alisema Mavunde.

Huku akiwa amesimama na maji aliyopewa, alisema yuko tayari kuacha shughuli za Bunge akashirikiane nao kuhangaikia maji, hadi pale watakapoyapata na kuanza kujenga matangi.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mkutano huo, Naibu Waziri alisema katika kipindi cha kampeni alifika eneo hilo na kuahidi kuwapatia maji, lakini muda ulikuwa bado. Hata hivyo, Serikali ya awamu ya tano ina miezi sita madarakani.

“Hiyo ilikuwa ni sehemu ya ahadi yangu kwenye kampeni, kwa hiyo matatizo ya maji hapa nayajua na kweli ni makubwa, ndiyo maana nimeamua kuvuruga kila ratiba ili niokoe watu hawa kweli wako kwenye mateso,” alisema.

Mhandisi wa Maji Manispaa ya Dodoma, Simon Sasala alisema kijiji hicho kina wakazi 7,600 ambao wanahitaji lita 230,000 za maji kwa siku, lakini kuna kisima kinachotoa lita 89,000 na wakati mwingine hakifanyi kazi.

Sasala alisema maji hayo hayatoshelezi kwani yapo kwa asilimia 39, hali ambayo inawapa shida hasa kina mama kutokana na wengi wao kulazimika kufuata maji ya kutumia umbali mrefu.

UKAWA Waigomea Serikali Kuhamishwa Machinga Katikati ya Jiji la Dar es Salaam

0
0
Sakata la kuhamishwa kwa wafanyabiashara wadogo katikati ya Jiji la Dar es Salaam limeingia mdudu baada ya madiwani wa Ukawa kugomea uamuzi uliotolewa na uongozi wa jiji hilo.

Uamuzi huo uliotolewa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Isaya Mngurumi, unadaiwa kutowashirikisha wadau hao na wafanyabiashara wenyewe.

Mwenyekiti wa madiwani wa Ukawa, Manase Mjema amesema Mngurumi ametoa umuzi huo bila pia kumshirikisha hata Meya wa Ilala, Charles Kuyeko.

Wamesema masoko ya Kivule, Tabata Muslim, Ukonga na Kigogo Fresh ambayo mkurugenzi huyo amesema yametengwa kwa ajili ya wafanyabiashara hao, hayajaboreshewa miundombinu yake ikiwamo ujenzi wa vyoo na mabomba ya maji.

Wamemtaka kusitisha mchakato huo mpaka watakapo jadiliana tena.
Viewing all 104416 articles
Browse latest View live




Latest Images