Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

Panama Papers: Majina ya Watanzania Waliohifadhi Fedha Nje ya Nchi yatajwa

$
0
0
Kwa wale waliokuwa wansubiri kupekuwa kwenye database ya Panama papers kuona kama kuna vijogoo wa Afrika hususani Tanzania wameficha fedha wanaweza kupekuwa sasa. Kila kitu kimewekwa online.

Baadhi ya majina ni;

Hasnain Ahmed Hassanali Tanzania, United Republic of Panama Papers

Mohamedraza Ahmed Hassanali Tanzania, United Republic of Panama Papers

Ahmedirfan Mohamedraza Hassanali Tanzania, United Republic of Panama Papers

MR. KASBIAN NURIEL CHIRICH Tanzania, United Republic of Panama Papers

Mr. Azizi ROSTAM Tanzania, United Republic of Panama Papers

Nawshad Ahmed Hassanali Tanzania, United Republic of Panama Papers

JORGE MARITINO Tanzania, United Republic of Panama Papers

EDUARDO MARTINO Tanzania, United Republic of Panama Papers

JORGE MARTINO Tanzania, United Republic of Panama Papers

EDUARDO MARITINO Tanzania, United Republic of Panama Papers

JACEK MONLNIK ROGOYSKI Tanzania, United Republic of Panama Papers

BOULDER MINING LIMITED Tanzania, United Republic of Panama Papers

MRS. SUKAINA MANJI Tanzania, United Republic of Panama Papers

Talal Mohamed Abood Tanzania, United Republic of Panama Papers

Abbas Mohammed Jessa Tanzania, United Republic of Panama Papers

NARENDRA VAGHJIBHAI PATEL Tanzania, United Republic of Panama Papers

Ms. Zuzana Kovacicova Tanzania, United Republic of Panama Papers

Mr. Eric PASANISI Tanzania, United Republic of Panama Papers

SAJJAD MOHAMEDHUSSEIN VIRANI Tanzania, United Republic of Panama Papers

Mr. Eric PASANISI Tanzania, United Republic of Panama Papers

Mr. Suril Shah Tanzania, United Republic of Panama Papers

Suril V. Shah Tanzania, United Republic of Panama Papers

Mr Kalpesh Menhta Tanzania, United Republic of Panama Papers

Roberta Thomaz de Mattos Brisolla Tanzania, United Republic of Panama Papers

NICHOLAS CHARLES WILSON Tanzania, United Republic of Panama Papers

SEYDOU KANE Tanzania, United Republic of Panama Papers

KONSEL JAMES WAMBURA Tanzania, United Republic of Panama Papers

Abbas Mohamed Jessa Tanzania, United Republic of Panama Papers

SUN MINING LIMITED Tanzania, United Republic of Panama Papers

Abdulaziz Mohamed Abood Tanzania, United Republic of Panama Papers

ABBAS MOHAMMED JESSA Tanzania, United Republic of Panama Papers

Mohamed Panju Jessa Tanzania, United Republic of Panama Papers

Abbas Mohamed Jessa Tanzania, United Republic of Panama Papers

HARIDATT VAGHJIBHAI PATEL Tanzania, United Republic of Panama Papers

Fauzi Mohamed Abood Tanzania, United Republic of Panama Papers

B.A. KOTECHA Tanzania, United Republic of Panama Papers

R.D. KOTECHA Tanzania, United Republic of Panama Papers

MRS. SUKAINA MANJI Tanzania, United Republic of Panama Papers

SUKAINA MANJI AND YUSUF MANJI AS TRUSTEES OF THE MANJI FAMILY TRUST Tanzania, United Republic of Panama Papers

ANIL VAGHJIBHAI PATEL Tanzania, United Republic of Panama Papers

Mrs Kantaben Manibhai Chhotabhai Patel Tanzania, United Republic of Panama Papers

MRS. ROSMINA KANANI Tanzania, United Republic of Panama Papers

MR. DANIEL LITTMAN Tanzania, United Republic of Panama Papers

Mrs. Aarti Puri Tanzania, United Republic of Panama Papers

Mr. Eric PASANISI Tanzania, United Republic of Panama Papers

Mr. Azizi ROSTAM Tanzania, United Republic of Panama Papers

Andre Schmid Tanzania, United Republic of Offshore Leaks

KANIZ MEHBUB MANJI Tanzania, United Republic of Offshore Leaks

Mr. Stuart Hugh MacDonald Tanzania, United Republic of Offshore Leaks

Mr Rameshchandra Chotalal Somani Tanzania, United Republic of Offshore Leaks

Rameshchandra C. Somani Tanzania, United Republic of Offshore Leaks

Mr. Rameshchandra C. Somani Tanzania, United Republic of Offshore Leaks

MEHBUB YUSUFALI MANJI Tanzania, United Republic of Offshore Leaks

Wengine ni;

LIERVAAG, M.Tanzania, United Republic ofPanama Papers

NICITERETSE, ROGERTanzania, United Republic ofPanama Papers

JAMES BABANTanzania, United Republic of, MauritiusPanama Papers

WHEELOCK HOLDINGS LTD. 26-NOV-1996 British Virgin Islands Tanzania, United Republic of Panama Papers

RICHMOND FINANCE CORPORATION 11-MAR-1986 Panama Tanzania, United Republic of Panama Papers

EXPRO ENERGY LTD. 23-JUL-2014 British Virgin Islands Tanzania, United Republic of Panama Papers

Chanzo: Panama Papers

Mrembo Anayedaiwa Kutoka Kimapenzi na Mwanamuziki Diamond Afunguka

$
0
0
Mrembo huyo aliyeuza nyago kwenye Video ya Wimbo wa Kwetu wa msanii wa Diamond, Irene’ Lynn’.

Mrembo ambaye wiki mbili zilizopita aligeuka gumzo baada ya kudaiwa ‘kuchepuka’ na staa wa Afro-Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Irene’ Lynn’ kisha kuleta mtikisiko kwa mpenzi wa msanii huyo, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ amefunguka kuhusu ishu hiyo.


Akizungumza wikiendi iliyopita baada ya kubanwa aseme ukweli kama anatoka kimapenzi na Diamond, mrembo huyo aliyeuza nyago kwenye Video ya Wimbo wa Kwetu wa msanii wa Diamond aitwaye Raymond alisema kuwa hata yeye ishu hiyo inamshangaza.


 Irene alisema siku zote watu hawajiamini wanapomuona msichana mzuri akifanya kazi na mtu fulani na mara nyingine humwekea wivu na kuibua mambo mengine. Irene aliweka wazi kuwa kilichompeleka Wasafi ni kufanya kazi ya Wimbo wa Raymond na hakuna kingine kilichoendelea.

“Mkataba wangu na Diamond uliisha baada tu ya kufanya video ya msanii wake,” alisema Irene. Mrembo huyo alitiririka kuwa ishu hiyo inamtesa na kumsumbua kwa sababu watu wengi wanajua kuwa ni kweli ametembea na Diamond, jambo ambalo si kweli.

 Skendo ya Irene kutembea na Diamond ilileta mtafaruku mkubwa kwenye familia ya mwanamuziki huyo kiasi cha dada wa mwanamuziki huyo, Esma Platnumz, kuingia kwenye mgogoro mzito na Zari ikielezwa kuwa mrembo huyo ni rafiki yake na alijua kilichokuwa kikiendelea.

Mapenzi ya Barakah Da Prince na Naj yazidi Kunoga (Picha)

$
0
0
Unakumbuka kipindi Kanye West na Kim Kardashian wameanzisha uhusiano wao? Watu waliwapa

Leo hii ni wanandoa, wana watoto wawili na penzi lao bado lipo imara. Ndivyo ilivyoonekana kwa Barakah Da Prince na Naj pia. Ni kwasababu katika kipindi kifupi tangu aanze kuvuma, Barakah alihusishwa kuwa na uhusiano na warembo A-List wakiwemo Linah, Meninah, Masogange na hadi Nisha.

Hivyo wengi walivyosikia kuwa muimbaji huyo wa ‘Siwezi’ kahamishia mapenzi kwa Naj, walijua napo anapita tu. Pia ni kutokana na mahusiano mengi ya mastaa hayadumu. Guess Barakah anaweza kutuprove wrong kwasababu kuna kila dalili kuwa penzi lao limezidi kushika mizizi zaidi na hawataki tena kulificha.

Swali ni je wataendelea kuwa pamoja kwa miaka mingi ijayo?

UKAWA Wadai Rais Magufuli Ndo Chanzo cha Sukari Kuadimika Nchini

$
0
0
Kambi  Rasmi ya Upinzani Bungeni, imesema tatizo la sukari nchini limetokana na uamuzi usio sahihi wa Rais Dk. John Magufuli, kwa kupiga marufuku uingizwaji wa bidhaa hiyo kutoka nje ya nchi bila kufanya tathmini.

Akizungumza jana na waandishi wa habari, Waziri Kivuli wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Anthony Komu, alisema agizo hilo lilitolewa kwa kukurupuka na ndilo lililosababisha sukari kuadimika.

Komu ambaye pia ni Mbunge wa Moshi Vijijini, alisema kama malengo ni kulinda viwanda vya ndani, basi lisifanyike kwa sukari pekee kwa sababu viwanda vipo vingi na bado bidhaa zinaingia kutoka nje nchi.

Alisema kuna harufu ya upendeleo kutokana na Rais kuwa swahiba wa Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, ambaye ni mmiliki wa mashamba ya Mtibwa, hivyo amefanya hivyo kwa kupewa ushauri mbaya huku nchi ikiingia kwenye upungufu mkubwa wa sukari.

Alihoji kwa nini apige marufuku kwenye sukari tu wakati kuna viwanda vya nondo, saruji na vinginevyo na vinaleta bidhaa kutoka nje.

Alisema kilichofanywa na Rais ni kukurupuka na ni kuvunja sheria.

Komu alisema kitendo cha Rais kutoa amri ya walioficha sukari wany’ang’anywe, ni kupora haki za watu na kuua mitaji yao kibiashara.

“Hakuna sheria ambayo inaruhusu kwenda kukagua maghala ya wafanyabiashara na kugawa bidhaa bure, hii hali hata wawekezaji wataogopa kuja kuwekeza nchini kwa sababu wataona mazingira ya hapa nchini ni hatarishi," alisema Komu.

Alisema serikali iandae njia mbadala ya kuwafidia watu walionyang’anywa maana wengine wamekopa kwenye taasisi za kifedha.

“Agizo la Rais lina walakini, kwani ni nani katika biashara za watu...tunakokwenda ni kubaya kwani upungufu wa sukari ulijulikana tangu Februari, lakini akapiga marufuku sukari kutoka nje,” alisema Komu.

Alisema katika tafiti mbalimbali ikiwamo ripoti iliyotolewa na Shirika la BBC, mahitaji ya sukari nchini kwa mwaka ni tani 590,000, lakini uwezo uliopo ni tani 300,000, hivyo serikali ilikuwa ni busara iruhusu kuingizwa kwa sukari kwa sababu viwanda vya ndani vimekosa uwezo.

Alisema Rais anatakiwa kukemewa na kuambiwa kwamba anakwenda kinyume na kwamba wao kambi ya upinzani hawatetei wanaoficha sukari, lakini serikali itafute namna ya kukabili hali hiyo.

Naye Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea, alisema taifa lina viwanda vinne vikubwa vya sukari, lakini bado havina uwezo wa kuzalisha sukari ya kutosha.

Alisema serikali imefanya sukari ionekane kama dawa za kulevya kutokana na kuadimika huko.

Alisema sukari hadi iletwe nchini, ni takriban wiki tano na wanaoingia kwenye Mwezi Mtukufu wa Ramadhani watahitaji sukari kushinda vitu vingine.

“Sisi hatutetei walioficha, lakini wamenunua ili kuuza kwa taratibu kulingana na bei ya soko wasibughudhiwe maana kuna hatari ya benki kushindwa kurejeshewa fedha zilizokopwa,” alisema Kubenea.

UDA Yazikwa Rasmi.....Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Yavunja Mkataba

$
0
0
Hatimaye  uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, umevunja mkataba wa uwekezaji wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam(UDA) na Kampuni ya Simon Group Limited inayomilikiwa na mfanyabiashara, Robert Kisena.

Mkataba huo ambao umekuwa ukipigiwa kelele ndani na nje ya Serikali, umetajwa kutokufuata taratibu za kisheria na kukiuka Sheria ya Manunuzi (PPRA).

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, jana, Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita alisema uamuzi huo umefikiwa, baada ya kufanyika kikao halali cha Baraza la Madiwani.

Aidha baraza hilo la madiwani pia limeamua kwamba, asilimia 51 ya hisa zilizokuwa zinamilikiwa na kampuni hiyo zirudishwe chini ya uongozi wa jiji hilo.

Mwita alisema madiwani walipitia upya mkataba wa uwekezaji kati ya kampuni hiyo na Halmashauri ya Jiji, ambapo walibaini udhaifu katika maeneo mbalimbali wakati wa makabidhiano.

Meya huyo anayetokana na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), aliyataja maeneo hayo kuwa ni pamoja na waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kutoshirikishwa wakati wa makabidhiano.

“Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, imevunja mkataba wa makubaliano ya kuuza Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA) kwa mfanyabiashara Robert Kisena, baada ya kubaini kuwapo udhaifu wakati wa kuuza shirika hili,” alisema.

Mwita alisema halmashauri ya jiji kipindi hicho, haikufuata utaratibu wa utangazaji wa zabuni wakati wa kuuza shirika hilo, hali iliyoonyesha wazi  viongozi waliokuwa madarakani wakati huo, walikuwa na maslahi binafsi katika kukabidhi shirika hilo mikononi mwa kampuni hiyo.

Alisema hadi sasa shirika hilo bado limesajiliwa kwa jina la Halmashauri ya Jiji kwa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), hali inayowapa nguvu ya kuvunja mkataba huo kwa sababu mmiliki wake kisheria bado ni jiji.

“Tuliambiwa Simon Group, alikuwa anakwenda benki kuchukua mikopo kwa hati ya Shirika la UDA, tumefuatilia benki mbalimbali tumebaini hakuna hata hati moja ya shirika iliyowasilishwa kwenye benki  kama dhamana ya mikopo,”alisema.

Alisema shirika hilo hadi sasa lina Sh bilioni 5.9 ambazo zililipwa na Simon Group kama malipo halali ya kuuziana shirika, jambo ambalo haliko sawa.

“Hatuwezi kuona mikataba ya kifisadi inaendelea kuimaliza Serikali, lazima tuchukue hatua ambazo ni pamoja na kuangalia taratibu za kisheria ili kuivunja,’ alisema.

Alisema kutokana na hali hiyo, baraza hilo limeunda timu ya watu watatu wakiongozwa na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee ili kuangalia athari ambazo zinaweza kujitokeza wakati wa kuvunjwa kwa mkataba huo.

Akizungumzia hatua hiyo, Ofisa Habari wa Kampuni ya Simon Group, Deus Bugaywa alisema hadi sasa halmashauri ya jiji haijatoa taarifa yoyote ya kuonesha kama mkataba huo umevunjwa, licha ya magari ya UDA kuanza kazi leo.

“Hatujapewa taarifa yoyote ambayo inasema mkataba kati ya UDA na Halmashauri ya Jiji umevunjwa, tunaamini bado ni wana hisa halali tutafanya kazi kwa ubia kama ulivyo mkataba wetu,”alisema Bugaywa.

Alisema kampuni hiyo, ilifuata taratibu zote za kisheria wakati wa kuingia makubaliano, wala hakukuwa na ukiukwaji wa kisheria.

Alisema kama watakabidhiwa barua ya kuvunjika kwa mkataba huo, wataangalia taratibu za kisheria ili waweze kudai haki yao.

Wizkid Ashika Nafasi ya Kwanza Billboard, Shukrani kwa Drake

$
0
0
Jina la Wizkid linazidi kung’ara duniani, shukrani kwa shavu alilopewa na Drake.

Wimbo ‘One Dance’ wa Drake aliomshirikisha msanii huyo wa Nigeria umekamata nafasi ya kwanza kwenye chati za Billboard Hot 100. Wimbo huo upo kwenye album ya Drake, Views ambayo pia nayo imeshika nafasi ya kwanza kwenye Billboard 200 chart.

BILLBOARD HOT 100 TOP 10

1. Drake feat. Kyla & WizKid – “One Dance”
2. Desiigner – “Panda”
3. Lukas Graham – “7 Years”
4. Mike Posner – “I Took a Pill in Ibiza”
5. Fifth Harmony feat. Ty Dolla $ign – “Work from Home”
6. Rihanna feat. Drake – “Work”
7. The Chainsmokers feat. Daya – “Don’t Let Me Down”
8. Zayn – “Pillowtalk”
9. Calvin Harris feat. Rihanna – “This is What You Came For”
10. Justin Bieber – “Love Yourself”

Prof. Lipumba: Uhaba wa Sukari Umesababishwa na Rais Magufuli

$
0
0
Akihojiwa na Mtangazaji Yvonne Kamuntu kwenye Azam News, Mchumi mbobezi hapa nchini Prof. Ibrahim Haruna Lipumba amesema uhaba wa sukari uliopo kwa sasa nchini umesababishwa na Rais John Magufuli mwenyewe kwa kuzuia sukari ya nje kutoingizwa Nchini, ilhali viwanda vyetu havikidhi idadi inayohitajika katika uzalishaji wake.

Pia Prof. Lipumba amesema hakuna sheria inayoruhusu Serikali au Bodi ya Sukari kupanga bei ya sukari nchini hivyo ametaka siasa kuacha kutumika katika mambo serious na wafanyabiasahara wasitishwe.

Habari Njema Sasa Unaweza Pata Habari za SIASA Kwa Haraka Kupitia SIASA HURU Application Kwenye Simu yako

$
0
0
Kama wewe ni mpenzi wa Habari za Siasa basi hii ni habari njema kwako...Download Siasa Huru Application Kutoka Google Play Store Kwenye Simu yako itakurahisishia upataji wa Habari na Breaking News za Siasa kwa urahisi....

Bonyeza HAPA Kuinstall Kwenye Simu yako fasta....

Au Nenda Google Play Store Kwenye Simu yako Alafu Search 'Siasa Huru' Kisha Install



Swala la Sukari lisitu Sahaulishe Lugumi na Ripoti ya CAG..... Tusiwe Wepesi Wakutolewa Kwenye Reli-Henry Kilewo

$
0
0
Hivi ile kamati ya PAC imeishia wapi na ishu ya Lugumi? Mbona hapa pako kimya? Na tukizingatia ni ishu inayogusa jeshi letu la polisi? Hapa jipu halitumbuliki?

Nimejiuliza maswali hayo nikasema nilini Watanzania tutalazimisha Watawala wajue tumechoka na kusikia ishu zikiibuliwa na kuishia njia.... Au huko Bungeni wanaliongelea na sisi huku hatusikii wala kuona kwakuwa Bunge halipo live?

Swala la Sukari lisitu sahaulishe Lugumi na Ripoti ya CAG..... tusiwe wepesi wakutolewa kwenye Reli, Lugumi na Ripoti ya CAG imeishia wapi ama inaendeleaje?

HUU MCHEZO HAUHITAJI HASIRA

By Henry Kilewo

Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari Ajisalimisha Polisi, Ahojiwa Kwa Masaa 6

$
0
0
Polisi wilayani Arumeru jana iliwashikiliwa kwa muda mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari na madiwani 35 wa Chadema kwa tuhuma za kuvamia eneo na kuharibu mali.

Viongozi hao, wiki iliyopita walivunja uzio wa mabati uliojengwa jirani na halmashauri na mfanyabiashara Itandumi Makere, wakimtuhumu kupata eneo hilo la Serikali kinyume cha sheria.

Nassari na madiwani hao, walishikiliwa kwa muda baada ya kujisalimisha katika Kituo cha Polisi Usa River. Viongozi hao, baada ya kufika polisi saa tatu asubuhi walihojiwa kwa zaidi ya saa sita kwa tuhuma hizo.

Nassari alisema kitendo hicho cha kufikishwa polisi na kuhojiwa hakiwatishi kwani wanachokifanya ni kutetea ardhi ya Wameru.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Meru, Wille Njau alisema wamedhalilishwa na hatua hiyo kwani walikuwa wanatekeleza uamuzi ya Baraza la Madiwani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo alikiri kuhojiwa kwa mbunge na madiwani hao na kusema wanafanya uchunguzi na jalada litawasilishwa kwa mwanasheria mkuu wa Serikali.

Chadema: Bunge la Sasa Kibogoyo Limeng'olewa Meno na Serikali

$
0
0
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Dk Vincent Mashinji amesema kitendo cha Serikali ya Awamu ya Tano kuzuia matangazo ya moja kwa moja ya Bunge ni sawa na kuling’oa meno bunge hilo.

Tofauti na mikutano miwili iliyopita ya Novemba 2015 na Januari/ Februari 2016, Serikali hii inayoongozwa na Rais John Magufuli, iliamua kufuta matangazo ya moja kwa moja ya Bunge la Bajeti lililoanza vikao vyake Aprili 19 kwa maelezo kwamba ni gharama kubwa kwa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC). Badala yake TBC huonyesha kipindi cha maswali na majibu pekee na hurekodi matangazo mengine na kurushwa katika kipindi cha ‘Leo katika Bunge’ saa nne usiku.

Suala hilo lilipingwa vikali na wabunge wa upinzani lakini uongozi wa Bunge ulitia chumvi kwenye kidonda baada ya kukataza vyombo vya habari kupiga picha za video, badala yake wanatakiwa kuchukua picha kutoka kwa televisheni ya Bunge.

Akizungumzia hali hiyo jana alipofanya ziara katika ofisi za gazeti hili zilizopo Tabata jijini Dar es Salaam, Dk Mashinji alisema kuwa huu ni mkakati maalum uliosukwa na CCM ili kuvibana vyama vya upinzani.

Jela Miaka Mitatu Kwa Kumchoma na Pasi Mwanaye

$
0
0
Mahakama ya Wilaya ya Ilala imemhukumu kifungo cha miaka mitatu jela mkazi wa Ukonga Mombasa, Christina Yoram (31) baada ya kupatikana na hatia ya kumjeruhi mtoto wake wa kambo wa kiume wa miaka 11 kwa kumchoma na pasi.

Mshtakiwa huyo pia alimpiga sehemu mbalimbali za mwili mtoto huyo na kumsababishia majeraha.

Akisoma hukumu hiyo jana Hakimu Mkazi Mwandamizi, Juma Hassan alisema mahakama hiyo imetoa adhabu hiyo baada ya kuridhishwa na ushahidi dhidi yake uliotolewa na mashahidi watano.

“Vitendo vya unyanyasaji dhidi ya watoto bado ni tatizo katika jamii, hivyo kutokana na mahakama yangu kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka, mshtakiwa utatumikia kifungo cha miaka mitatu jela ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hizi,” alisema Hakimu Hassan.

Kabla ya hukumu hiyo kutolewa, Wakili wa Serikali Chesenci Gavyole aliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali dhidi ya mshtakiwa huyo ili iwe fundisho kwa wanawake wengine wenye tabia mbaya kama yake. Kabla ya hukumu hiyo, mahakama hiyo ilitoa nafasi kwa mshtakiwa huyo kujitetea ili isimpe adhabu kali.

Katika utetezi wake, aliiomba mahakama hiyo impunguzie adhabu kwa madai kuwa ana Ukimwi, watoto watatu na mama yake mzazi wanaomtegemea na kwamba mume wake amepooza mwili kwa kiharusi.

Awali Wakili Gavyole alidai mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo Machi 20, 2013 eneo la Ukonga Mombasa Wilaya ya Ilala.

Aunt Ezekiel ni Mjamzito? , Mpenzi wake Asema hili Kuhusu Kupata Mtoto Mwingine

$
0
0
Wakati mtoto wa Aunt Ezekiel na Mose Iyobo akikaribia kutimiza mwaka mmoja hivi karibuni, Mose amefunguka kuhusu kupata mtoto mwingine wakiume na mrembo huyo kutoka kiwanda cha filamu.

Akizungumza na Bongo5, Mose amesema kwa sasa anafurahia maisha na mrembo huyo wa filamu na soon watapata mtoto mwingine wakiume.

“Sasa mimi na Mama Cookie tunamipango endelevu, kama hivyo ushamuona Cookie bado kuna kaka yake Cookie anakuja na vitu vingine vitaendelea, soon mtasikia tu,” alisema Mose.

Mose alisema anafuraha kuwa kwenye mahusiano na Aunt Ezekiel.

KUTOKA BUNGENI:Mussa Azzan Zungu Achaguliwa Kuwa Tena Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

$
0
0

KUTOKA BUNGENI: Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Azzan Zungu amechaguliwa leo kuwa tena Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akitoa neno la shukrani Zungu amesema nafasi hiyo sio rahisi lakini ataitumikia kwa uadilifu tena bila kupendelea upande wowote.

Tuhuma Nzito Bungeni..Baadhi ya Wabunge Wadaiwa Kuvuta Bangi na Kutumia Madawa ya Kulevya

$
0
0
Tukio la Zamani Bungeni
Mbunge wa Viti Maalum, Mariam Msabaha (Chadema) ametoa tuhuma nzito kuwa ndani ya Bunge kuna wabunge vijana wanaovuta bangi na kutumia dawa za kulevya.

Mbunge huyo amemuomba Rais John Magufuli kuagiza wabunge wa aina hiyo ambao hata hivyo hakuwataja wapelekwe Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ili kufundishwa nidhamu.

Msabaha ametoa kauli hiyo Bungeni mjini Dodoma wakati akichangia hotuba ya bajeti ya wizara ya Ulinzi na JKT iliyowasilishwa na Waziri mwenye dhamana na Wizara hiyo, Dk Hussein Mwinyi.

“Wabunge nao waende JKT kwa sababu hili Bunge wameingia vijana wengine ambao ni mateja wa unga na wengine wanavuta bangi. Wengine wanawavua mama zao nguo,” amesema Msabaha.

“Wengine mama zao wameshakufa wanakuja humu wanawatukana mpaka wazazi wao. Kwa hiyo niombe Rais Magufuli vijana wote wabunge ambao hawana nidhamu waende JKT,” alisisitiza.

Mbunge huyo amesema wabunge wa aina hiyo hawana viwango vya kuzungumza ndani ya chombo hicho cha kutunga sheria hivyo ni vyema waende JKT ili wakirudi wawe wamejua namna ya kuchangia.

Ingawa hakumtaja Mbunge yeyote, lakini mchango  ulioibua mtafaruku bungeni ni wa Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga aliyedai wabunge wa viti maalumu Chadema huitwa Baby ili kupewa nafasi hiyo.

Tafsiri ya kauli hiyo ni kuwa wabunge wa viti maalum Chadema lazima wafanye mapenzi au kuwa na mahusiano na viongozi wa juu wenye mamlaka ndani ya chama hicho ndipo wateuliwe kuwa wabunge.

TCRA Watoa Onyo Kwa Wanaoflash Simu..Ukikamatwa ni Kifungo cha Miaka 10 Au Faini ya Sh Million 30

$
0
0
Serikali imewataka wauzaji wa vifaa vya mawasiliano vya mkononi (mobile devices) kuacha mara moja tabia ya kubadilisha namba tambulishi (‘kuflash’) za vifaa hivyo kwani  watakabiliwa na kifungo kisichopungua miaka 10 au faini isiyopungua Sh. milioni 30 au vyote viwili.

Kauli hiyo imetolewa na Meneja Mawasiliano wa  Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Innocent Mungy wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.

“Namba tambulishi  (IMEI) za vifaa vyote vya mawasiliano ya mkononi ambavyo vimeibiwa,vimeharibika,kupotea au visivyokidhi viwango vya matumizi katika soko la mawasiliano havitaruhusiwa kuunganishwa kwenye mitandao ya watoa huduma ifikapo tarehe 16 June 2016, "alisema Mungy.

Akizungumzia kampeni ya kuelimisha umma kuhusu matumizi ya simu zote zisizokidhi viwango, Mungy alibainisha kuwa idadi ya  simu hizo imeshuka kutokana na elimu ambayo wameitoa katika mikoa mbalimbali hapa nchini.

Alisema  lengo la elimu hiyo kwa umma ni kujenga uwezo kwa wananchi kutambua simu zisizokidhi vigezo kabla ya kufika ukomo wa matumizi ya simu bandia nchini.

Mungy alifafanua kuwa uchambuzi wa IMEI unaonyesha kuwa hadi Februari,2016  idadi ya namba tambulishi ambazo zilikuwa hazina viwango zilikuwa sawa na asilimia tatu ambapo namba tambulishi ambazo zimenakiliwa zilikuwa sawa na asilimia 18 na simu halisi zilikuwa sawa na asilimia 79.

“Kwa mwezi Machi 2016 ulionyesha kuwa Idadi ya namba tambulishi ambazo hazina viwango ni asilimia nne, na idadi ya zile zilizonakiliwa zilikuwa sawa na asilimia 13 ambapo uchambuzi huu umehusisha taarifa za kampuni zote za simu nchini,’’. alifafanua Mungy.

Aliongeza kuwa matokeo hayo mazuri ni matunda ya ushirikiano mzuri uliopo kati ya mamlaka hiyo, Shirika la Viwango Tanzania (TBS),Tume ya Ushindani (FCC),kampuni za simu, pamoja na wadau wengine katika kuelimisha umma juu ya uhakiki wa simu walizonazo ikiwa ni pamoja na mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa kununua simu ikiwemo kuzihakiki ubora wake.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Usimamizi wa Mawasiliano  wa Mamlaka hiyo, Injinia Gabriel Mruma amesema kuwa ni vyema Watanzania wakajenga utamaduni wa kununua simu  zenye ubora kuepuka usumbufu wakati Tanzania inapoelekea ukomo wa matumizi ya simu bandia.

TCRA ina dhamana ya kusimamia shughuli za mawasiliano ya Kielektroniki na Posta hapa nchini.

Kuwepo kwa Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) ya mwaka 2010 na kanuni zake za mwaka 2011 kumewezesha kutekelezwa kwa mfumo wa rajisi ya namba za utambulisho wa vifaa vya mawasiliano vya mkononi.

Mfumo huu wa kielektroniki ulizinduliwa tarehe 17, Desemba 2015 na unahifadhi kumbukumbu za namba tambulishi za vifaa vya mawasiliano vya mkononi kwa lengo la kufuatilia namba tambulishi za vifaa vilivyoibiwa,kuharibika au kupotea,bandia vya mawasiliano katika soko.

TRA: Sukari iliyokamatwa Mbagala na Tabata, Imeingia Nchini Kihalali, Haitagawiwa Bure

$
0
0
TRA wameachia huru Sukari iliyokamatwa Mbagala na Tabata kwa kile walichodai imeingia nchini kihalali

Sukari iliyoachiliwa ni zile tani elfu 6,757 iliyokutwa kwenye maghala Mbagala Dar es Salaam, baada ya kujiridhisha iliingizwa kihalali nchini.

My Take:

Mimi nlijua Sukari hiyo itagawiwa bure, Nashauri Serikali ipunguze Siasa katika Mambo ya Msingi. Mambo kama haya yanapunguza imani kwa Rais, Haiwezekani rais aseme Sukari itakayokamatwa igawiwe bure halafu nyie Mseme eti Sukari iliingizwa kihalali kwa kufuata taratibu zote.

Je, nani kamdanganya Rais?. Hakika Rais Magufuli anahujumiwa

AY na Mwana FA Waingia Kortini Kuishtaki Kampuni iliyotumia Nyimbo zao Bila Ridhaa?

$
0
0
Kuna uwezekano mkubwa, AY na Mwana FA wamefungua kesi ya masuala ya ukiukwaji wa haki miliki za kazi zao.

Mwanasheria maarufu nchini, Alberto Msando amepost picha Instagram akiwa kwenye mahakamu kuu ya Tanzania akiwa na rappers hao. “At the High Court of Tanzania, Dar Es Salaam. #UsijeMjini #DakikaMoja #Tigo #CopyrightsInfringement #stoppingwizi @aytanzania @mwanafa,” ameandika Msando.

Kuna uwezekano kuwa nyimbo zao Usije Mjini na Dakika Moja zikawa zimetumiwa na kampuni bila ridhaa yao. Makosa ya kukiuka haki miliki kwenye kazi za sanaa huadhibiwa zaidi kwa kwa faini.

Kwa hili la Kukataa Mwaliko wa Uingereza, Rais Sikuungi Mkono

$
0
0
Rais John Magufuli amepata heshima ya pekee kualikwa na waziri mkuu wa Uingereza katika mkutano utakaofanyika kuzungumzia mikakati ya mapambano ya rushwa ikiwa ni nchi mbili tu zimepata fursa hiyo kwa bara la Africa ikiwemo pia Nigeria.

Lakini Rais wetu amedai sasahivi amebanwa na majukumu kwahiyo atawakilishwa na Waziri mkuu mh. Kassim Majaliwa

Chanzo: Cloudz Tv

Mambo Ambayo Wanaume Wanakosea Wakati wa Kutongoza Mwanamke

$
0
0
1.PAPARA
Wanaume wengi tumekuwa na haraka sana tunapokuwa tukitaka kuaproach hali inayomfanya mwanamke akuwekee ugumu.mfano umekutana na dada mzuri mmesalimiana hapo hapo unamuomba namba yake.mjomba hata akikupa ujue utasumbuka sana kumpata coz atakufikiria sana juu ya uharaka wako.

2.KUJIFAKE
Wanaume wengi tumekuwa tukijipandisha au kujionyesha tofauti na hali zetu.ukiwa unaaproach jaribu kuwa real.huwezi kumwambia mdada unafanya kazi benki afu uko na techno

3.KUTOSOMA MOOD YA MWANAMKE
unapomuaproach mwanamke lazma usome mood yake coz sometime unaweza kutoswa coz hujamsoma mwanamke unamtongozaje mwanamke asubuhi?

4.KUMPONDA UR EX LOVER
Mwanamke anakuuliza kwanini uko single,unaanza kumponda ex wako kwa maneno ya kashfa hali kama hii inaweza kumtisha kisaikolojia umtongozae.

5.KULALAMIKA
Unamtongoza mwanamke huku unalalamika juu ya mapenzi oooh mara sijawahi kupendwa mjomba hapo unaonyesha udhaifu wako.

UKITULIA NA KUMTONGOZA MWANAMKE BILA KUYATENDA HAYA MBONA UTAMPATA KILA UMTAKAE

Toa Maoni yako
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images