Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104747 articles
Browse latest View live

Huwa Napata Shida sana Nikikutana na Wanawake Wenye Hii Tabia

$
0
0
Huwa napata shida sana nikikutana na Wanawake wenye hii tabia...Unampenda Mwanamke kabisa from ur heart,unajipanga unampiga saundi..anakujibu,''How old are you kaka'' unamwambia am 29 years..utamsikia,''Oh my Ghosh,ur still a kid,mi nadate guys who are 45 years above...Wanajua kupenda,they are so caring,yaani nyie vijana mnasumbua sana''.Sio tunasumbua,anajua kabisa miaka 29 bado ndo unasaka hela,ndo umeanza maisha huna cha kumhonga,ukijitahidi sanaaa utampeleka shopping Karume na hiyo hela itakuuma kishenzi!

Anakuita Kid bila aibu wakati yeye ana miaka 23 tu halafu eti ana mahaba na jitu la miaka 47..Uongo mtupu!Ina maana mtu hawezi kupenda na kucare hadi afike miaka 45??Nyie semeni tu mnawalia timing coz mnajua mtu mwenye miaka 45 anakuwa ameshajipanga,amefanya kazi ana hela,unajifanya unampenda kumbe Parasite tu unataka kumnyonyoa mafao yake ya uzeeni,hamna hata aibu..Mnapenda sana vitu ready made,tengenezeni vya kwenu,ukiona mtu ana miaka 45 jua kuna Mwanamke mwenzio amefanya kazi kumfikisha hapo alipo,we unakuja unadandia tu,,,Kama kweli una mahaba tafuta mwanaume wako,panda nae daladala za Buguruni mrukie wote dirishani,msotee maisha kwa kutembelea TZ 11 hadi siku apate gari mfaidi wote halafu akifika miaka 45 uone kimwanamke cha IFM kinamsogelea eti hes caring uone inavyouma,utatamani umpige patasi ya kisogo...Gold diggers,waone kwanza,msione gesi mtwara mshaanza kuandamana!45years guy waiting for u student of 23 years,ina maana miaka yote hiyo alikuwa Stevie Wonder au??

By  Seth De Jesus Giovanni

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano ya May 11, Ikiwemo Rostam na Manji Wajieleza Sakata la Panama

$
0
0

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano ya May 11

Mwanajeshi Mwanafunzi wa JWTZ Ajiua Kwa Kujipiga na Risasi Kichwani

$
0
0
Mwanafunzi wa Chuo cha Anga (Skua) cha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kilichopo Kange jijini Tanga, Philip Fred (28) amejiua kwa kujipiga risasi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Leonard Paul aliwaambia waandishi wa habari ofisini kwake jana kwamba tukio hilo ni la jana saa 1.15 usiku katika chuo hicho kilichopo kata ya Maweni nje kidogo ya jiji.

Alisema askari mwenye cheo cha Koplo mwenye namba MT 81627 alijiua wakati akiwa katika eneo la lindo chuoni hapo.

“Kimsingi chanzo cha kifo cha askari jeshi huyo bado hakijajulikana na imefahamika kwamba alikuwa ni mwanafunzi wa ‘Level one’ chuoni hapo na mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa Bombo”, alisema Kamanda.

Katika tukio jingine Kamanda alisema askari wanamshikilia mkazi wa mtaa wa Mgwisha, kata ya Pongwe jijini Tanga, Masudi Hamis (22) kwa tuhuma za kukutwa na sare moja ya askari wa JWTZ.

Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron Anaswa Akisema Nigeria ni Vinara wa Rushwa Duniani

$
0
0
Mzozo wa kidiplomasia unatokota baada ya Waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron, kunaswa kwenye Kamera akimwambia Malkia Elizabeth wa Pili kuwa viongozi wa mataifa mawili yenye ufisadi mkubwa kote duniani Nigeria na Afghanistan watakuwa miongoni mwa wageni waalikwa katika kongamano la kupambana dhidi ya zimwi la ufisadi litakalofunguliwa siku ya Alhamisi mjini London.

Matamshi hayo ya Cameron yalitolewa katika kasri la Buckingham bw Cameron alipokuwa amekwenda kumtembelea malkia Elizabeth katika sherehe ya kuadhimisha miaka 90 ya kuzaliwa kwake.

Aidha Cameron alieelezea malkia Elizabeth jinsi mataifa hayo yalivyosakamwa na viongozi mafisadi.

Kiongozi wa kanisa la kianglikana Askofu mkuu wa Canterbury Justin Welby aliyekuwa na viongozi hao wawili anasikika akimkumbusha Waziri mkuu bw Cameron kuwa rais mpya wa Nigeria Muhammadu Buhari si mfisadi.

Afghanistan iliorodheshwa katika nafasi ya 167, nafasi moja pekee mbele ya Somalia na North Korea, katika orodha ya 2015 ya shirika la kupambana na ufisadi duniani Transparency International .
Nigeria iliorodheshwa katika nafasi ya 136

AUDIO: Rais Magufuli ‘Huyu Shetani Aliyetulaani Watanzania Kwanini Asife?’

$
0
0
Ni hotuba ya Rais Magufuli akiwa Arusha kwenye kuweka baraka zake kwenye majengo mapya ya PPF ambapo kwenye hotuba yake iliyochekesha watu wengi aliongelea pia ishu ya madini ya Tanzanite yanayopatikana Tanzania pekee lakini nchi zinazotambulika kuyauza duniani ni India na Kenya.

President Magufuli alisema :
 ‘Siku nyingine hakuna ubaya hata NSSF mkawa ndio wawekezaji wakubwa wa Tanzanite mkawa mnanunua Tanzanite kutoka kwa vijana hawa badala ya kuwa inavushwa mpaka Kenya na kwenda Kenya, badala ya Tanzania kuwa ya kwanza kuuza Tanzanite duniani inajitokeza India alafu inafata Kenya‘

‘Unajua saa nyingine watu wanatuona Watanzania sijui tukoje, huyu shetani aliyetulaani sisi Watanzania kwanini asife? hata hatuhurumii kidogo? basi kama ni kuswali na kusali tusali sana ili tubadilike, tuthamini mali yetu kwa ajili ya vizazi vyetu‘

Kumsikiliza zaidi unaweza kubonyeza play hapa chini…

Mtu na Mkewe Wafariki Dunia Baada ya Kula Chakula Chenye Sumu

$
0
0
Watu watatu wamefariki dunia mkoani Kigoma katika matukio mawili tofauti likiwamo la mke na mme kula chakula kinachohofiwa kuwa na sumu na mtoto kufariki kwa ajali ya moto.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma SACP, Ferdinand Mtui amesema matukio hayo yalitokea Mei 8, mwaka huu.

Amesema tukio la kwanza limetokea katika Kata ya Basanza ambapo Edson Kahenela (68) na mkwe Melisiana Petro (56) walikula chakula cha jioni wakaenda kulala na hawakuamka tena.

Mtui amesema baada ya kuona hawaamki, mdogo wa marehemu aitwaye James Kahenela alipata mashaka na kugonga mlango lakini haukufunguliwa na hivyo kutoa taarifa kwa majirani ambao walivunja mlango na kukuta mke na mme wamekufa.

Katika tukio la pili lililotokea maeneo ya mto Nsima Lugufu wilayani humo ilitokea ajali ya moto katika Nyumba ya Mayala Zalia na kusababisha kifo cha mtoto wake aitwaye Ligwa Mayala

Baada ya Miaka 46 ya Ndoa, Mwanamke Mwenye Miaka 70 Amejifungua Mtoto wa Kwanza Huko India.

$
0
0
Baada ya miaka 46 ya ndoa, mwanamke mwenye miaka 70 amejifungua mtoto wa kwanza huko India.
.
Daljinder Kaur amejifungua mtoto wa kiume baada ya kupata matibabu ya IVF kwenye kliniki za uzazi huko India.

Kwenye picha akiwa na mume wake wa miaka 79, Kaur alisema yeye na mume wake walikuwa karibu kukata tamaa ya kupata mtoto kutokana na umri wao na kuona Kama Mungu amewalaani wasipate mtoto.

Alisema hatimae Mungu amejibu maombi yao na wamepata mtoto na sasa wanajiona wamekamilika.

Aliendelea kusema kuwa yeye na mume wake watamlea mtoto wao wenyewe kwasababu huyo mtoto amewapa nguvu mpya katika maisha. Pia anawasihii wote wenye changamoto za uzazi wamuombe Mungu bila kuchoka.... Aliongezea kusema....".....I can't wait to b a grandma!!

Athumani Machupa Aishauri Timu ya Simba Kukubali Kununuliwa na Mfanyabiashara Mohamed Dewji

$
0
0
Mchezaji wa zamani aliyewahi kutamba na klabu ya Simba na timu ya taifa ya Tanzania Athumani Machupa amevunja ukimya na kuamua kufunguka juu ya mwenendo mbovu wa klabu yake ya zamani.

Machupa amekuja juu pia kuhusu fukuzafukuza wachezaji inayoendela kwenye klabu hiyo ya Msimbazi kwasababu yeye pia ni miongoni mwa wachezaji waliowahi kusimamishwa na kufukuzwa kwenye klabu hiyo.

Nyota huyo aliyekuwa mwiba kwa magolikipa kutokana na uwezo wake mkubwa wa kupasia nyavu, ameishauri pia klabu hiyo kumkabidhi timu MO  kama wanataka mafanikio ya mpira na biashara.

“Simba ndiyo klabu niliyoichezea toka nikiwa mtoto mpaka nakuwa Machupa, mimi ni mchezaji wa zamani wa kimataifa wa klabu ya Simba nadhani watanzania wengi wananifahamu. Kwasasa naishi Sweden ambako pia nafanya shughuli zangu huku nikiendelea kucheza mpira”.

“Klabu ya Simba imefanya vibaya msimu huu kutokana na kuongozwa kimazoea, klabu ya Simba ni kubwa na yenye hadhi barani Afrika lakini kwa sasa haijafanya vizuri katika medani zote kwa muda mrefu nyumbani na kimataifa”.

“Sidhani kama tumekaa chini na kujiuliza lakini upande wa uongozi nafikiri kila tunapofanya vibaya wanadhani tatizo linakuwa kwa wachezaji, lakini je, tatizo ni wachezaji? Na kama tatizo ni wachezaji kwanini wawe na wachezaji wenye matatizo?”

“Swali la pili, je uongozi upo sahihi? Kama uongozi haupo sahihi wachezaji hawawezi kuwa katika hali nzuri na kucheza kwa kiwango kizuri, kwasababu sasahivi mchezo wa mpira ni biashara. Ili ufanikiwe katika soka la kisasa ni lazima uwekeze pesa nyingi, ndiyo maana matajiri wengi duniani wanataka kununua timu kwasababu wanajua mpira ni biashara”.

“Klabu ya Simba inamatatizo ya kufukuzafukuza wachezaji, mimi pia nimewahi kufukuzwa Simba, wapo wachezaji wengine wengi ambao tayari wamewahi kufukuzwa  na kusimamishwa Simba. Mimi niliamua kuachana na Simba baada ya mkataba wangu kumalizika mwaka 2007”.

“Simba ya sasahivi haitakiwi kuongozwa hivi inavyoongozwa, Simba ya sasahivi haitakiwi kuwa na presha ya kufungwa inapokutana na timu kama Ndanda”.

“Simba inahitaji kupata mafanikio lakini sidhani kama viongozi waliopo madarakani wanajua wapenzi, wanachama na mashabiki wanataka nini”.

“Ukiangalia katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, wachezaji wengi wametoka Simba kwenda Yanga na siyo Yanga kwenda Simba, sidhani kama kuna wachezaji 5 au 6 waliotoka Yanga kwenda Simba”.

“Kessy kabla ya kuhamia Yanga alisimamishwa na uongozi wa Simba, unasimamishaje mchezaji kutokana na makosa ya uwanjani ? Inawezekana mchezaji hayupo sawa kisaikolojia kwasababu kuna baadhi ya mambo hajatimiziwa. Mchezaji mkataba wake unamalizika, kwanini msikae meza moja mkazungumza hata kama hamtofikia makubaliano basi mmnaachana vizuri. Lakini labda hatujui pengine alifanya makosa makubwa”.

“Tunaelekea kujiandaa na msimu mpya, viongozi waliopo madarakani wanamawazogani ? wana nini cha kuwaambia wanachama ?  Timu yetu imefanya vibaya kwa sababu gani?”

“Mambo ya kusimamisha na kufukuza wachezaji hadi lini ? Kama mchezaji ni mtovu wa nidhamu mtoeni hata kwa mkopo akacheze kwenye timu nyingine. Tubadilike, tujifunze kwa wenzetu maana tunafatilia vilabu vya nje basi tujifunze kutoka kwao pia”.

“Kama inawezekana, wampe timu MO  kwasababu hawampi timu bure, haichukui Simba na kuipeleka kwao Singida. MO ni mfanyabishara mkubwa barani Afrika na hakuna mtu ambaye ukimwelezea habari ya MO na Simba atakua haelewi kitu”.

“MO ni mwana Simba na anataka kuwekeza kwenye klabu yake anayoipenda tangu akiwa mtoto na anatoa pesa zake, mpeni timu aipeleke panapostahili kwasababu anajua mpira, anajua bishara na anajua Simba inatakiwa ifike wapi.Viongozi kaeni chini mzungumze na wanachama muwaeleze faida na hasara za kumpa timu MO”

Rais Magufuli Awasili Nchini Uganda Leo Kuhudhuria Sherehe Za Kuapishwa Rais Museveni

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika Uwanja wa ndege wa Entebbe, nchini Uganda kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Yoweri Museveni, kesho.

Msajili wa Hazina Agoma Shirika la UDA Kuchukuliwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam

$
0
0
MSAJILI wa Hazina ametupilia mbali maombi ya Halmshauri ya Jiji la Dar es Salaam ya kutaka kurudishiwa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (Uda) kwa kusisitiza kuwa Kampuni ya Simon Group ina hisa halali katika shirika hilo.

Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaac Mwita, alikaririwa na vyombo vya habari jana akimtaka Msajili kukadhibidhi shirika hilo kwa uongozi wa Jiji kwa madai kuwa Simon Group walinununua shirika hilo kinyume cha taratibu.
 
Msajili alisema pia serikali haina mpango wa kuuza hisa zake za asilimia 49 inazomiliki katika shirika hilo.
 
Madiwani wa Jiji la Dar es Salaam waliomba wapewe hisa hizo za serikali ikiwa hawatarudishiwa hisa za Simon Group.
 
Mkuu wa Kitengo cha Habari wa ofisi ya Msajili wa Hazina, Gerard Chami,  jana alisema kuwa ofisi yake haiwezi kubadilisha mkataba wa umiliki wa Uda.
 
“Msajili anakamata hisa za serikali ambazo ni mali ya Watanzania, hazihusiani kwa namna yoyote na hisa asilimia 51 za Jiji ambazo walishaziuza kwa kampuni ya Simon Group. Tunashangaa wanapotaka tuingilie mambo yao ambayo kimsingi hatuhusiki,” alisema Chami.
 
Chami alieleza kuwa kulikuwa na kesi iliyokuwa mahakamani baina ya Jiji na kampuni ya Simon Group Ltd. Iliamuliwa Simon Group ilipe Sh. bilioni 5.5 ili kununua hisa za Jiji na alifanya hivyo na kwa mazingira hayo, Msajili hadi sasa anamtambua kama mwanahisa mwenza wa Uda.
 
Alifafanua kuwa hakuna namna ambayo Msajili atajihusisha na hisa hizo kwa kuwa siyo wajibu wake bali anachotakiwa ni kumtambua mwanahisa mwenzake ambaye kwa sasa ni kampuni ya Simon Group.
 
“Suala hili linachukuliwa kisiasa zaidi, lakini ukweli unajulikana kwani ni sawa mtu alikuwa na mali yake akaamua kugawa sehemu na kumpa mwingine aliyehitaji kwa wakati huo, lakini kwa sababu zake kile alichogawiwa akaamua kuuza kwa mtu mwingine, ni vigumu kurudi kwa sasa kumweleza aliyegawa awali kugawa tena hisa zake," alifafanua.
 
“Yeyote aliyeuziwa hisa hizo sisi tunamtambua ndiye mwanahisa mwenza, tunachojua kwa sasa kampuni ya Simon Group ndiye mwanahisa mwenza kwa kuwa alishamaliza kulipa kwa kutekeleza amri ya mahakama,” alisema.
 
Alibainisha kuwa hisa asilimia 49 za serikali ina hiari nazo kama ni kuuza kwa faida au kwa ajili ya kupeleka fedha katika eneo jingine lenye maslahi ya jamii na siyo kwa Jiji linavyotaka kumpa mwanahisa mwenza katika shirika hilo.
 
Meya Mwita alisema juzi kuwa Baraza la Madiwani la Jiji la Dar es Salaam liliazimia katika kikao chake kuwa fedha zaidi ya Sh. bilioni 5.5 zilizolipwa kwa Jiji na kampuni ya Simon Group kwa ajili ya kununuliwa hisa zisirudishwe hadi tathmini ya kina itakapofanyika na kujiridhisha kuwa hadaiwi chochote kwa kutumia mali mbalimbali za Uda kwa maslahi yake.
 
Pia waliunda kamati ndogo ya wajumbe watatu ambao ni Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, Mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolea na Mwanasheria wa Jiji, Jumanne Mtinangi kwa ajili ya kufuatilia suala hilo.
 
Naye Ofisa Habari wa Simon Group, Deus Buganywa, alisema jana hawajapokea barua yoyote kuhusiana na kutakiwa kurejesha hisa hizo baada ya kuulizwa juu ya sakata hilo la Uda.

Thomas Ulimwengu Afunguka Pengo la Samatta bado lipo TP Mazembe

$
0
0
Mshambuliaji wa kimataifa Thomas Emmanuel Ulimwengu amesema kwamba kwa sasa pengo la Mtanzania mwenzake, Mbwana Ally Samatta linaonekana TP Mazembe.

Ulimwengu akiongea na Clouds FM alisema TP Mazembe kwa sasa inamkosa mshambuliaji mwepesi, mwenye uwezo wa kufunga kama Samatta.

Samatta ameondoka timu hiyo ya DRC Januari mwaka huu baada ya kushinda nayo taji la Ligi ya Mabingwa Afrika na kujiunga na KRC Genk ya Ubelgiji anakoendelea vizuri hivi sasa.

Tangu kuondoka kwa Samatta, Mazembe imeonekana kupoteza makali yake kiasi cha kuvuliwa mapema ubingwa wa Afrika.

Mazembe ilitolewa na Wydad Casablanca ya Morocco katika hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa na kuangukia kwenye kombe la Shirikisho.

Katika mechi iliyopita Mazembe ilipata ushindi mwembamba wa bao 1-0 katika mchezo wa kwanza wa mchujo kuwania kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika dhidi ya Stade Gabesien Uwanja wa Mazembe mjini Lubumbashi.

Ulimwengu aliyecheza kwa dakika 45 juzi kabla ya kutoka uwanjani akiwa anachechemea, alisema timu kwa sasa haina mtaalamu wa kufunga mabao kama alivyokuwa Samatta.

“Pengo la Samatta linaanza kuonekana sasa, pale mbele hakuna na anayeweza kufunga kama Samatta, tunapoteza nafasi nyingi sana, hilo ndilo tatizo,”amesema Ulimwengu.

Sasa Mazembe itakuwa na kazi ngumu katika mchezo wa marudiano wiki ijayo, ikitakiwa kwenda kuulinda ushindi huo mwembamba nchini Tunisia

Binti wa Miaka 19 Anayedai Kuwa na Ujauzito wa Papa Wemba Ajitokeza Hadharani

$
0
0
Binti wa miaka 19 anadaiwa kuspend one night on the same bed na Hayati Papa Wemba amekua gumzo kwenye mitandao ya kijamii ndani na nje ya Congo(D.R.C) akidai kuwa na ujauzito wa Mfalme huyo wa Rhumba aliefariki April 24 mwaka huu baada ya kuanguka jukwaani jijini Abidjan nchini Ivory Coast.

Picha zinazodaiwa kuwa copied kutoka kwenye akaunti za social media za binti huyo,zinamuonesha akiwa kwenye pozi tofauti za kimahaba na Papa Wemba,picha ambazo zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii huku baadhi ya picha hizo zikionesha tumbo lake na nyingine zikimuonesha akikiss na Hayati Papa Wemba.

Mpaka sasa hakuna taarifa yeyote rasmi kutoka kwenye familia ya Papa Wemba juu ya madai ya binti huyo ambae baadhi ya mashabiki wa Mfalme huyo wa Rhumba wameahidi kumsaidia kwa lolote hadi atakapojifungua.

Mwanamke Aunda Boti Lenye Umbo la Uke Wake

$
0
0
Mahakama moja ya Japan imemwachia huru mwanamke mmoja aliyetengeza boti iliyofanana na uke wake.

Jaji aliamuru kwamba boti ya Megumi Igarashi iliofanana na uke wake na yenye rangi nyingi haikuashiria umbo la uke.

Hatahivyo ,alipigwa faini ya dola 3,700 baada ya jaji kuamuru hakuvunja sheria kwa kusambaza data ya uke wake ambayo inaweza kutumika kutengeza umbo la uke wake.

Sheria kali za Japan zinapinga kuonyeshwa hadharini kwa sehemu za siri.

Igarashi mwenye umri wa miaka 42, kwa jina Rokudenashiko au ”good for nothing girl” alikamatwa mwaka 2014 baada ya boti yake kuonyeshwa katika duka moja la vifaa vya ngono mjini Tokyo.

Alishtakiwa chini ya sheria ya mambo machafu kwa kuonyesha boti hiyo na kusambaza data yake kwa wale waliochangisha fedha ili itengezwe.

Siku ya Jumatatu jaji mmoja aliamua kwamba rangi zake zinazong’aa na mapambo yake hayaonyeshi ukweli wa umbo la uke.

“Lakini data yake licha ya kutokuwa na umbo la uke itatumika kutengeza uke wa Bi Igarashi kwa kutumia 3D na hivyobasi ni uchafu,” alisema jaji.

Bi Igarashi alipigwa faini nusu ya Yen 800,000 zilizohitajika na afisi ya mashtaka.

Source:BBC

Justin Kasusura Ashinda Rufaa na Kuachiwa Huru, Alishutumiwa Wizi wa Dola Mil 22

$
0
0
Kwa mujibu wa gazeti la the citizen la leo limeandika kuwa Kasusura kashinda rufaa yake na sasa yupo huru.

Alihukumiwa miaka 30 jela mwaka 2007 kwa kosa la kuiba dola milioni 22. Fedha hizo zilikua zimepokelewa uwanja wa ndege.

-----

 The Court of Appeal has set free Justin Kasusura, the man at the centre of the dramatic theft of $2 million (about Sh4.4 billion at the current exchange rate) that belonged to Citibank, the outcome judges linked to shoddy investigation and poor prosecution.

The court said on Monday prosecution had failed to prove beyond reasonable doubt the case against Kasusura who grabbed headlines in the early 2000 following the robbery of money that was being transported from the Julius Nyerere International Airport to a Citibank branch.

The $2 million in cash was brought in from the United States by Swissair before it was stolen on the way to the branch. “With due respect, we wish to state from the outset that we have noted with great concern that this case has been badly investigated and consequently poorly prosecuted,” said judges Sauda Mjasiri, Mbarouk Mbarouk and Semistocles Kaijage.

Mr Kasusura alias John Laizer was in 2007 sentenced to 30 years in jail after the Kisutu Resident Magistrate’s Court found him guilty of armed robbery and theft.

He was charged along six other persons who were later freed after the court found them to have no case to answer.

Diamond Atoa Sababu ya Kutosema Chochote wakati Anashoot Video na P-Square ‘Video Ninayo Tayari’ (Video)

$
0
0
Diamond Platnumz aliamua kutosema chochote wakati alipokuwa Afrika Kusini kufanya video ya wimbo aliowashirikisha P-Square. Ni Paul na Peter Okoye tu ndio waliopost picha za behind the scenes za uchukuaji wa video hiyo.

“Sometimes naonaga ukianza kuelezea kitu kitakuja, kitakuja, kinakuwa kinaboa,” Diamond ameiambia Bongo5.

“Sema tumeshamaliza tumeshashoot video, nasubiria tu mimi mwenyewe, nimekaa nayo tu ndani naangalia nitoe saa ngapi, imeshaisha kila kitu. Na muziki sometimes unafaa kuchungulia kuangalia unaiweka wapi, na kwasababu sio kutoa tu nyimbo unataka uonekana umefanya wimbo, lakini pia unatoa nyimbo kwa target za kibiashara,” ameongeza.

Mwambaji Shilole Ataja Mpenzi Wake wa Sasa...

$
0
0
Uking’atwa na nyoka ukiguswa na jani lazima utaruka.
Baada ya kuvunjika kwa mahusiano na Nuh Mziwanda, taarifa za chini zimezidi kuenea kuwa Shilole ana mahusiano ya kimapenzi na msanii chipukizi wa Bongo Fleva, Nerd aliye chini ya label ya Ommy Dimpoz, PKP.

Akiongea kwenye kipindi cha Busati, kinachoruka kupitia Magic FM, Shilole amesema hana mpenzi kwa sasa.

“Mimi mpenzi wangu ni hela, Nerd ni rafiki yangu. Ukiwa kwenye mapenzi unakuwa kama kipofu unakuwa hauoni. Ukimkabidhi mtu moyo wako anakuwa anaufinyanga, kwa sasa moyo wangu umestawi tofauti na zamani,” aliongeza.

Hata hivyo Shilole amesema hana namba ya Nuh Mziwanda na hajawahi kuwasiliana naye tangu walipoachana. Kwa sasa muimbaji huyo ana wimbo mpya uitwao Say My Name.

Tahadhari Kuhusu Makachero FEKI Wa TAKUKURU Wanaojifanya Kufuatilia Sakata la Sukari

$
0
0
Tangu kuanza kwa zoezi la kufuatilia wafanyabiashara wanaoficha sukari kwa agizo la Rais wa Jamhuri ya Tanzania Mh. Dr John Pombe Magufuli, kumekuwa na wimbi la watu wanaojiita “makachero wa TAKUKURU  kutoka Makao Makuu” nao wakifuatilia sakata la sukari mkoani Kilimanjaro.

Matapeli  hao ambao kwa sasa wapo  wilayani  SIHA, wamekuwa wakiwasumbua   wafanya biashara kwa kudai kuwa  wametumwa kuwashughulikia huku wakiomba kupewa  fedha ili wawasafishe.

Kiasi cha fedha ambacho kimekuwa kikiombwa ni kati ya Shilingi 150,000/= hadi 500,000/= kama “gharama ya kuwasafisha kwa Mheshimiwa Rais”

Naomba  wafanya baiashara  Mkoani Kilimanjaro waelewe kwamba, TAKUKURU inao mfumo wa utendaji kazi ambao unajali misingi ya utawala bora na kamwe haihusiki na utapeli wa aina hii.

TAKUKURU katika utendaji wake wa kazi, haiwatozi wafanya biashara fedha kama adhabu kwa kuhifadhi sukari kinyume na taratibu. TAKUKURU  inafuatilia, kuhoji na kumtaka mfanyabiashara kuonesha namna  anavyomiliki sukari hiyo kwa kutoa vielelezo husika. Mwisho wa zoezi hili, atakayetoa tamko ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.

Ifahamike kuwa hakuna afisa wa TAKUKURU mpaka sasa aliyetumwa kutoka Makao Makuu kuja mkoani Kilimanjaro kufuatilia zoezi la sukari. Zoezi hili mkoani hapa linaendeshwa na vyombo vya ulinzi na usalama kama timu moja na wala halifanywi na TAKUKURU pekee .

Ifahamike pia kuwa hakuna zoezi linaloihusisha TAKUKURU litakaloendeshwa mkoani bila ofisi ya mkoa kuwa na taarifa.

Kwa misingi hiyo yeyote anayeendesha zoezi hilo nje ya utaratibu nilioufafanua ni tapeli, taarifa zake zitolewe mapema ili akamatwe na kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

Maofisa wote kutoka ofisi ya TAKUKURU mkoa wanavyo vitambulisho na kama watatiliwa shaka basi ofisi yangu ijulishwe kupitia simu namba   0784 998 804 au 0786 089 805 muda wowote.                                                              
                             
IMETOLEWA NA                                                                  
ALEX J KUHANDA
MKUU WA TAKUKURU  MKOA WA KILIMANJARO
11/5/2106.

Picha ya Gigy Money na Mtangazaji Gadner G Habash Yazua Utata....

$
0
0


Mrembo Gigy Money Anaesifika kwa Bongo la Tako Bongo ameweka picha kwenye page yake ya Instagram na kuandika haya maneno:

Precioussada
 Dada jide ulifanya la maana kuondoka maana huyu sio mwanaume ni maradhi
Read more at http://websta.me//n/gigy_money#3WPzayBT2EO0rCtB.99

 Mudy_makinga 
Umekojoleshwa six months mama tukomeshe @gigy_money tem hii nww endelea kukojoleshwa naww miaka 20 ila ss mwambie akujoleshe mmelala sio mmesimama hutozaa nae nww! Take care


Gigy_money:
 Baby chukua #supu
Sinaaa tatzooo na huyu mzeeee mwenzangu amesh......... takriban miez6 @captaintanzania


Hizi Hapa ni Baadhi ya Comments:

Raymondo_soundo
Brother nahisi kama haupo sawa @captaintanzania maisha gani hata???? Basi atakama unafanya kuwe na mipaka unajizalilisha sana. Nimekumind sanaaaaaaaa

 Gstar_s 
Utakojozwa kama Jide ohoo captaaiiiiin!!@gigy_money
 mbea_wa_insta Sasa mkojoze na huyo hadi mavi yawatoke nyote wawili @captaintanzania maana mmekutana wote wacheza ngono mamae .


saraphinam4
 MLIMA KITONGA.......lol mwanaume mpenda mtelemko

nancygodwintillya 
kweli umechanganyikiwa mzee, ulivyokuwa unajiheshimu ukiwa na jide leo umefika huko

Na wewe Embu Tupia Comment yako hapo chini

Jinsi ya Kuchepuka Bila Kukamatwa!

$
0
0
Baada ya taarifa kuenea mitandaoni kuwa mkuu wa kanisa letu anatuhumiwa kubeba mrembo wa watu, nimeona kuna emergency ya kuandika juu ya hii mada. Lengo langu sio ku promote uchepukaji, but no, my position is, mtu anapochepuka humkosea Mwenyezi Mungu, lakini pia humkosea mwenzi wake. Unapomkosea Mwenyezi Mungu ni rahisi kusamehewa ukiomba msamaha, na Mungu anaweza akakupa ka adhabu mambo yakaisha.

Kimbembe mpenzi wako akikudaka, sio rahisi sana kurejesha mahusiano mema na mpenzi wako, that is why am here to 'prevent a major catastrophes' btn you and your partner from happening:

Rule No 1 ya kuchepuka bila kudakwa
Usinogewe na penzi la mchepuko! Mwizi huwa hadakwi siku ya kwanza. Wengi wanaochepuka huwa wananogewa na kujisahau mpaka wanaanza kupiga piga simu na kutuma text hovyo. Mara hujiachia na kujisahau kuwa wanachofanya kinatakiwa kiwe siri. Ukiona umeshaanza kunogewa na penzi la mchepuko, au yeye keshaanza konogewa na wewe, piga chini, ni bora utafute mchepuko mwingine na uanze nao mwanzo...

Rule No 2 ya kuchepuka bila kudakwa
Msifanyie mambo yenu 'machoni pa watu'
Kama mnavyojua kuwa penzi ni kikohozi, basi usikohoe mahali ambapo watu wanajua sauti yako. Kama unachepuka ni bora ukachepukie mbali kabisa na maeneo ambayo umezoeleka. Hii itapunguza kuenea kwa info juu ya uchepukaji wenu.

Rule No 3 ya kuchepuka bila kudakwa
Kumbuka, hakuna siri ya watu watatu. Usimhadithie mtu YEYOTE juu ya uhusiano wako na mchepuko. Mkiweza kuifanya hii ikawa siri yenu wawili, itawasaidia kuliongezea uhai penzi lenu la siri. Pale unapo mwambia rafiki yako, naye atamwambia mwingine na mwingine na mwishowe siri itavuja sehemu isiyotakiwa kufika, so from there mtawekewa mitego na kuanza kufuatiliwa kwa siri.

Rule No 4, ya kuchepuka bila kudakwa
Simu ni adui wa penzi mchepuko
Watu wengi wanaochepuka hudakwa sana kwa njia ya simu. Kuwa muwazi kwa mchepuko wako kuwa upo kwenye serious relationship/ ndoa na so ajicontrol hasa kupiga piga simu na kutuma vi text. Kama vip ni bora utafute kisimu special kwa ajili ya mchepuko wako. Kisajili kwa jina la mtu asiye na uhusiano wowote kabisa na wewe. Then uwe unakitumia kuwasiliana na mchepuko wako. Ili mambo yakibuma, inakuwa ni rahisi kwako kukikana hicho kisimu. Unaweza ukasingizia kuwa labda kuna mtu alikisahau kwenye gari wakati umewapa mafundi lifti kwenda site n.k

Rule No 5 ya kuchepuka bila kudakwa
Dont leave any phyisical evidence.
Jaribu kupoteza ushahidi wowote wa yale yatakayotokea kwenye crime scene! Juzi hapa kuna mdau alileta kisa chake kuwa alichepuka na shem wake alafu shem akasahau bikini master bed room, so wife alivyokuja akaikuta na ikawa msala.
So kama ukiwa na mchepuko, hakikisha hakuna ushahidi utakao watia hatiani pasi na kuacha shaka. Huu ni uzembe mkubwa sana ambao unawafanya watu wadakwe kirahisi.

Hitimisho:
Nadhani ukifuata kanuni hizo hapo juu itakuwa ni msingi mzuri wa kutunza penzi/ ndoa yako kwa mda mrefu zaidi. Mwisho naomba nikuache na agalizo kutoka Mithali 14:12 Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, Lakini mwisho wake ni njia za mauti.

Donald Trump Alegeza Msimamo Wake Kuhusu Waislamu Kuingia Marekani Endapo Atakuwa Rais

$
0
0

Mgombea Urais wa Republican anaonekana kulegeza msimamo kuhusiana na pendekezo lake tata la kuwazuia Waislamu kuingia Marekani.

Katika mahojiano na kituo cha television cha Fox News, Donald Trump akijibu kauli ya meya mpya wa mji wa London Sadiq Khan, ambaye awali alionyesha wasiwasi na kusema hataweza kuingia nchini Marekani chini ya utawala wa Donald Trump, Trump ameiambia Fox News kwamba meya huyo anaweza kuja kwani hayo yalikuwa ni maoni tu.

Hata hivyo, Bwana Khan amekataa ukarimu huo wa Trump ambao unamlenga yeye pekee na sio kwa ajili ya jamii yote ya waislamu.

Pendekezo la kuwazuia waislamu kuingia nchini Marekani lilipata upinzani mkubwa ndani na nje ya Marekani.

Wakati huo huo, Waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron, ameomba msamaha kwa kiongozi wa dini ya kiislamu baada ya kumtaja kuwa ni mfuasi wa kundi la Islamic State.

Cameron alitoa kauli hiyo bungeni wiki tatu zilizopita katika kampeni za kutafuta meya mpya wa London. Bwana Cameron amesema mgombea wa upinzani Sadiq Khan - ni muislamu aliyeshinda kiti hicho cha umeya, ameonekana mara kadhaa na iman Sulaiman Ghani, imamu mstaafu.

Kwa upande wake, Iman Ghani ametishia kuchukua hatua za kisheria kutokana na madai hayo kwamba yeye ni mfuasi wa Islamic State.
Viewing all 104747 articles
Browse latest View live




Latest Images