Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104667 articles
Browse latest View live

Tanzia: Mchekeshaji Maarufu Bongo Afariki Dunia..

$
0
0

Mchekeshaji aliyekuwa anakuja juu kwa kasi Mohammed Abdallah "KINYAMBE" amefariki dunia leo usiku huko nyumbani kwako Mbeya. Mmoja wa wanandugu wa Kinyambe ameithibitishia Saluti5 kuwa msanii huyo wa filamu  ambaye pia alikuwa akijulikana kwa jina la James, amefariki baada ya kuugua kwa siku kadhaa.
R.I.P KINYAMBE

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya May 12, Ikiwemo Sukari ya Bil 5 Yakamatwa Dar es salaam

$
0
0
SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya May 12, Ikiwemo Sukari ya Bil 5 Yakamatwa Dar es salaam

Mbunge wa Ulanga, Godluck Mlinga (CCM) Atoa Tuhuma nzito kwa TRA, TCRA, EWURA

$
0
0
Mbunge wa Ulanga, Godluck Mlinga (CCM) ameyatuhumu mashirika ya umma ambayo hayajajiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kuwa watendaji wake wakuu wamepewa malipo ya asilimia 10 ili mashirika hayo yajiunge na kampuni binafsi za bima.

Ameyataja baadhi ya mashirika hayo ya umma yaliyokaidi kujiunga na NHIF licha ya kulazimishwa kisheria kuwa ni Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

“Yapo mashirika ya umma yanakataa kujiunga na NHIF wakati sisi wabunge tumejiunga, wao ni nani? Wakubwa wao wanapata asilimia 10 na wanajiunga na kampuni za bima ya afya binafsi…

“Mimi niliwahi kuwa Compliance Officer wa NHIF nikaenda TRA, nikawaeleza umuhimu wa kujiunga NHIF unachangia pesa kidogo unapata huduma nyingi lakini bosi wao akanijibu pesa si tatizo na afadhali ametumbuliwa huyo bosi wao, yule angekuwa ofisini kwangu asingetoka,” alisema Mlinga na kuongeza:

“Kila sehemu wananitaja Mlinga Mlinga, napata vitisho vingi lakini serikali inanilinda na kama jeshi (JWTZ) limeweza kusambaratisha M23 itashindwa kunilinda mimi…wengine wananiita teja hivi teja anavaa suti iliyonyooka kama mimi, siwezi kukasirika kwa sababu si kweli lakini wangeniita mbilikimo ningekasirika kwa sababu kweli.”

Mbunge huyo alitaka serikali ikomeshe tabia ya wanaume kubaka wazee na kufafanua “najiuliza wanawake wa mikoa yenye ubakaji wa wazee ni wagumu kuelewa hadi wazee wabakwe?”

Naye Mbunge wa Gairo, Ahmed Shabiby (CCM) amesema sasa ataanza kuacha kuwashawishi wananchi wake kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kutokana na mfuko huo kutopeleka dawa na chanjo za watoto kwenye vituo vya afya, badala yake inapeleka kondomu na vifaa visivyo muhimu kwa wananchi.

Makontena 115 Ya Sukari Yanaswa Jijini Dar es Salaam....RC Makonda Aviagiza Vyombo vya Dola Vifanye Uchunguzi wa Kina

$
0
0
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameagiza kuchunguzwa kwa sukari kontena 115 ambayo ni zaidi ya tani 3,000 iliyokutwa katika bandari kavu ya PMM iliyopo eneo la Vingunguti.

Makonda alitoa agizo hilo jana wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika bandari hiyo na kubaini uwepo wa sukari hiyo ambayo ni mali ya Mohamed Enterprises, ambayo kwa taarifa zake aliambiwa zilikuwa kontena 165.

Alisema anazitaka mamlaka zinazohusika kama Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), pamoja na Shirika la Viwango (TBS) kuichunguza sukari hiyo kutokana na sababu mbalimbali zilizojitokeza katika uwepo wa sukari hiyo kama sukari kuagizwa kutoka Dubai lakini imetoka Brazil na imepakiwa Dubai, na upangwaji wa kontena hizo katika bandari hiyo.

“Nashindwa kuelewa kwa nini sukari iagizwe kutoka Dubai lakini itoke Brazil na kufungashwa Dubai inaonesha inaweza kuwa imeshawahi kuisha muda wake hivyo nataka ichunguzwe na tunataka tujue kama Mohamed Enterprises anaficha sukari ili ipelekwe kwa wananchi kwa matumizi,” alisema Makonda.

Mbali na kutoa maagizo hayo, Makonda pia amezuia kutumika kwa sukari mifuko 22,000 iliyokutwa katika ghala la Mohamed Enterprises Tanzania Limited (MeTL) lililopo Barabara ya Nyerere na kutaka wapeleke vielelezo kuhusu sukari hiyo kwa mamlaka zinazohusika kama ya matumizi yoyote.

Alisema sukari hiyo inayodaiwa kuwa ni ya viwandani ni lazima iangaliwe kama kweli ipo kwa ajili ya mahitaji ya viwandani au ilikuwa itumike tofauti na ilivyokusudiwa.

Kwa upande wake, Meneja Operesheni wa bandari kutoka MeTL, Firoz Ebrahim alisema sukari hiyo imefuata taratibu zote na imefika katika bandari hiyo wiki moja iliyopita.

Katika hatua nyingine, Kampuni ya Al Naeem iliyopewa agizo la saa 36 kuanzia juzi iwe imeshaanza kusambaza sukari kwa bei elekezi iliyokuwa katika bandari ya Dar es Salaam, imeanza kutekeleza agizo hilo jana jioni.

Super Bets Dar Kikaangoni Kwa Kushindwa Kumlipa Mteja Aliyeshinda Milioni 160

$
0
0
Mkeka umegeuka shubiri kwa kampuni ya michezo ya bahati nasibu na kubashiri matokeo ya michezo, Super Bets ya jijini Dar es Salaam baada ya kushindwa kuwalipa wateja wake waliodai kushinda kiasi kikubwa cha fedha.

Mmoja kati ya wateja hao anadaiwa kushinda shilingi milioni 164 Jumatatu hii. Msimamizi wa Super Bets aliyejitambulisha kwa jina la Amani, aliongea na kipindi cha Sports Extra cha Clouds FM kuwa watu hao walishinda kimakosa. Amedai kuwa moja ya vyanzo vinavyowapatia matokeo ambayo kwenye mkeka zinaitwa odds ilikuja ndivyo sivyo.

“Baada ya hapo timu yetu ya masoko ilipogundua kuna tatizo hilo limetokea ina maana wakaja wakalifanyia kazi wakatujulisha tukagundua kuwa kuna tatizo fulani lilitokea tukalifanyia marekebisho. Baadhi ya wateja walikuja hapa wakasema wameshinda kutokana na zile odds za 98, tukawaambia wasubiri kwamba tunalishughulikia kwamba kuna matatizo ya kimtandao yalitokea. Tutawalipa kutokana na correct odds ambazo zilitolewa katika mtandao baada ya kurekebishwa hilo tatizo,” alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa bodi ya michezo ya kubahatisha nchini, Abbas Tarimba amedai kuwa wateja hao wamewasilisha malalamiko yao na wanayafanyia kazi.

Amedai kuwa maafisa wa bodi hiyo walienda kwenye ofisi za Super Bets kufanya uchunguzi kwenye server zao ili kubaini ukweli na wamewaomba walalamika siku mbili kukamilisha uchunguzi huo.

Miaka ya hivi karibuni betting kwenye michezo imekuwa biashara kubwa huku kukiwepo na makampuni mengi yanayochezesha na kuwavutia watu wengi hasa vijana.

Mume wa Aunt Ezekiel Kumnyang’anya Iyobo Mtoto Akitoka Jela...

$
0
0
 Imevuja! Mume wa mwigizaji mahiri wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel, Sunday Demonte, huenda akaachiwa huru baada ya kusota gerezani, Abu Dhabi, Falme za Kiarabu alikofungwa tangu mwaka 2014.

Demonte aliyefunga ndoa ya Kiislamu na Aunt Ezekiel, Novemba 2012, alitiwa nguvuni na polisi wa Dubai akikabiliwa na makosa kadhaa, likiwemo la kuishi nchini humo bila kuwa na kibali na kuhukumiwa kifungo jela.

Kwa mujibu wa chanzo chetu ambacho ni rafiki wa karibu wa mwanaume huyo, Demonte anatarajiwa kuachiwa huru katika msamaha maalum unaotolewa kabla ya kuanza kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan kila mwaka, baada ya kuonesha tabia njema katika kipindi chote akiwa gerezani.


“Amebadilika sana akiwa gerezani, muda wote yeye ni mtu wa kuswali, kutokana na tabia nzuri anayoionesha, serikali ya kule imeona bora na yeye aingizwe katika kundi la watu watakaoachiwa kwa msamaha maalum mwanzoni mwa Juni kabla ya mfungo kuanza,” kilisema chanzo hicho.
Chanzo chetu kilizidi kutiririka kwamba, shauku kubwa ya Demonte atakapotoka jela ni kuonana na mkewe huku akisisitiza kwamba hajawahi kumpa talaka hivyo ni mkewe halali.

“Anafurahia sana kutoka gerezani kama Mungu akimjalia lakini shauku kubwa ni kuonana na mkewe tena ili waendelee na maisha kwani anadai kuwa hajampa talaka na anampenda sana,” kilisema chanzo.

Baada ya kupata ubuyu huo, Amani lilianza kumtafuta Aunt Ezekiel ambaye licha ya mumewe kuwa jela, kwa sasa anaminya kimalavidavi na dansa wa Nasibu Abdul ‘Diamond’,  Mose Iyobo kiasi cha wawili hao kufikia hatua ya kupata mtoto.

Jitihada za kumpata Aunt kupitia simu yake ya mkononi, hazikuzaa matunda, hali iliyomlazimu mwandishi wetu kumfungia safari mpaka nyumbani kwake.
Sikia mazungumzo yao yalivyokuwa:

Amani: Hivi una taarifa za kwamba Sunday anakaribia kutoka?
Aunt: Ndiyo najua kwa sababu toka mwaka jana kulikuwa na taarifa hizo.
Amani: Kwa hiyo unazungumziaje kutoka kwake?
Aunt: Daah sasa hapo mimi  nitazungumzaje? Tunamuomba Mungu amjalie atoke kweli.
Amani: Kwa hiyo akitoka itakuwaje na wakati wewe sasa hivi mahabati yamekolea kwa Iyobo na mwenyewe anasema akitoka ataendelea na wewe haijalishi kama uko na mtu?
Aunt: Yaani hiyo naomba tusubiri akitoka ndiyo tutajua, siwezi kuongea chochote kabla mtu hajatoka.

Huko nyuma, Sunday aliwahi kuzungumza baada ya kupata taarifa kuwa Aunt amezaa mtoto na Iyobo na kusema kuwa hawezi kumuacha mkewe huyo kwa sababu mtoto amemzaa akiwa ni mkewe hivyo ataendelea kuwa naye na mtoto ni wake pia.

Chanzo:Global Publishers

Ubonge wa Mwili Wamtesa Joyce Kiria, Ahofia Kuipoteza Ndoa yake...

$
0
0
MTANGAZAJI wa Kipindi cha Wanawake Live kinachorushwa kupitia EATV, Joyce Kiria ameweka wazi kuwa hivi sasa yuko kwenye mikakati ya kupunguza mwili wake ili asije kupoteza ndoa.
 Akizungumza na Amani Joyce alisema, amekuwa akiuweka mwili wake sawa ili usinenepe sana kwa kuwa hataki tena kuonekana mzee akawapa nafasi wasichana ‘potabo’ wakaingilia ndoa yake na kuipoteza.
“Akuu!! Kisa cha kujizeesha na mwili hata ukitembea na mumeo uonekane kama shangazi yake mimi sitaki kabisa, sasa hivi ni diet kwa kwenda mbele kila kukicha nisije kuwapa madungaembe nafasi ya kuingilia ndoa yangu,” alisema Joyce.

Haijawai Tokea, Mwana FA na AY Kulipwa Billion 2 Tshs na Tigo Baada ya Nyimbo zao Kutumika Bila Ruhusa yao

$
0
0
 A court has awarded two Tanzanian musicians Sh2.18 billion in special damages in a landmark ruling that could set a precedent in the application of the copyright law in the country.

The huge award was won by Bongo flava artistes Ambwene Yessaya “AY” and Hamisi Mwinjuma “MwanaFA” who had sued mobile phone company MIC Tanzania (Tigo), for unauthorised use of their music as caller tunes. A caller tune is a tone that is in the form of music that is heard by a person making a call as they wait for the person being called to answer the phone.

Ilala Senior Resident Magistrate Juma Hassan granted the award on April 11 after a four-year court battle between the parties. The award also includes a separate Sh25 million in general damages.

News of the fine against Tigo only came to light this week on Tuesday when the firm went to the High Court to block the execution of the award pending its appeal. History in the copyright field would be made should the High Court uphold the judgement by the Ilala District Court.

MwanaFA said it was time those who had in the past taken the basic copyright laws for granted realised that things have changed.

“This is a key moment in copyright in Tanzania. This is something that has been happening for quite a long time now mainly because of lack of knowledge and maybe because of the costs associated with such cases,” he said.

He added: “Nobody is supposed to use your work without your permission or agreement and if at all he has benefited then he is supposed to share with you according to the price tag you have set for your work.”

The mobile network operator has, however, filed for a stay of execution and has appealed against the judgment and decree for payment at the High Court. The appeal was initially set to be heard on Tuesday but was adjourned to tomorrow. The artistes claim that Tigo sold without permission in the form of caller tunes content that belonged to them without any agreement between the two parties. The two songs at the centre of the controversy are Dakika Moja and Usije Mjini, which were both done in collaboration by AY and MwanaFA.

Although there are no figures that were mentioned by both sides on the precise income derived from the sale of the two songs, the two artistes believe the company generated revenue.

According to the judgment, the artistes did not have any agreement with anyone to distribute the songs, they did not have an agreement with the defendant (Tigo) and neither did they contract a third party to handle this kind of distribution on their behalf.

The court in its decree states that the defendant infringed the rights of the plaintiffs over their registered joint authorship of musical work and in the process infringed the copyright and/or neighbourhood rights to which civil remedies are applicable.

The court, therefore, ordered the company to pay Sh 5 million as general damages and Sh2.16 billion as special damages in addition to the costs of the suit.

The artistes had in their application asked for damages totalling Sh4.3 billion, claiming that the defendant had generated a significant sum of income through the sale of their two songs to its subscribers across the country.

In recent years, mobile phone operators have been at the centre of a controversy over how much they pay artistes for using their content, with some singers claiming they were not benefiting from their work.

Customised mobile phone caller tunes in Tanzania are largely songs by Bongo Flava artistes.

According to the Journal of Intellectual Property Law and Practice, copyright subsisting in caller tunes and ringtones is similar to copyright protection in any other musical recording, comprising an underlying musical work and a sound recording which are protected under the Copyright Act.

This type of copyright protection in Tanzania is similar to those in South Africa, the United Kingdom, the United States and Jordan.

Chanzo: Citizen


Chadema Wabeza Utumbuaji Majipu wa Magufuli, Wadai Bora Kikwete

$
0
0
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Dk Vincent Mashinji ameponda mtindo wa utawala wa Rais John Magufuli wa utumbuaji wa majipu akisema umekosa dira na kinachoendelea ni utashi wa kisiasa na kukurupuka.

Kazi kubwa aliyoifanya Rais Magufuli tangu aingie madarakani, katika kipindi cha miezi sita sasa ni kubana matumizi ya fedha za umma kwa kufuta safari za nje za watumishi, kuzuia mikutano kufanyika mahotelini, kuhimiza mamlaka husika kukusanya kodi, kupambana na watumishi hewa, kuwasimamisha au kutengua uteuzi wa watendaji aliodai kuwa ni wazembe na walioshindwa kwenda na kasi yake pamoja na kuwashughulikia wala rushwa na wahujumu uchumi.

Katika namna inayoonekana ni kufuata upepo wa kisiasa, Rais Magufuli huwatumbua baadhi ya watendaji kwenye mikutano ya hadhara.

“Kuna vitu vingi vinafanyika lakini hatujui kipi ni kipi na wapi tunaelekea. Kuna mambo mengi yanafanyika, lakini hakuna hata mtu mmoja katika nchi hii anayejua Taifa hili lina mpango gani na linaelekea wapi,” Mashiji anakaririwa na gazeti la Mwananchi.

Huku akifananisha utawala wa Rais Magufuli na wa mtangulizi wake Jakaya Kikwete, Dk Mashinji alisema walau ahadi ya “Maisha bora kwa kila Mtanzania” ilikuwa inaeleweka hata kama haikutekelezeka.

“Rais Kikwete alitwambia Maisha bora kwa kila Mtanzania na tulijua maisha hayo yanapatikana kwa kupambana wenyewe na tulipambana. Lakini sasa hatujui tunaelekea wapi. Hapa kazi tu! Umemfukuza huyu kazi halafu nini kitaendelea? Keshaondoka kakuacha, unaajiri mwingine? Tunahitaji mtu wa kujibu hayo maswali. Nchi yote sasa inavurugwa. Halmashauri zinavurugwa,” alisema.

Katibu mkuu huyo alisema kwa sasa kila kitu kinavurugwa jambo ambalo ni hatari kwa mustakabali wa nchi na kwamba inaonekana wazi nchi inaelekea sehemu ambayo mbele kuna giza.

Akitoa mfano wa mfumo ulivyobadilika alisema hivi sasa wakurugenzi wa halmashauri wametangaziwa kusitisha mawakala wote wanaokusanya ushuru badala yake wakusanye wenyewe.

 “Hivi tujiulize halmashauri ina wafanyakazi wangapi ambao wana uwezo wa kukusanya mapato yake? Huku ni kudanganyana,” alisisitiza Dk Mashinji.

Hata hivyo, Dk Mashinji alisema hawapingi anachokifanya bali tofauti yao na Rais Magufuli ni namna ya kukabiliana na jambo.

“Sisi tunaamini katika mfumo na siyo mtu. Huwezi leo kuniambia meya anaiba Sh5 bilioni halafu chama kisijue. Kwa nini chama kisimwondolee udhamini kabla?” alihoji.

 “Anachofanya sasa ni kudhibiti na siyo kurekebisha mfumo. Rais Magufuli hana dhamana na Mungu, asipokuwepo sioni wa kuendeleza falsafa zake. Kwa nini kusiwe na mfumo madhubuti ambao upo kisheria na kila mmoja aujue na kuufuata?” alieleza.

Tudd Thomas vs Nahreel Nani Mkali zaidi?

$
0
0
Hawa ni producers wa mziki waliofanikiwa kutengeneza hit single kitaifa na kimataifa
TUDD THOMAS
1.Number one remix-diamond ft Davido
2.Ndagushima-Ommy dimpoz
3.Make me sing-Diamond ft AKA
4.Na yule-Ruby
5.prokoto-victoria kimini
6.mdogo mdogo-Diamond
7.Bum bum-Diamond
8.utanipenda-Diamond


NAHREEL
1.Gere-Weusi
2.Niroge-Vannesa
3.Nusu nusu-Joh makini
4.Don't bother-Joh makini
5.Hamjui-Vannesa
6.Original-Gnako
7.Game-Navy kenzo
8.Kamatia-Navy kenzo


Nana-Diamond platnumz
waliitengeneza wote

Nani producer mkali kati yao??

Mpinzani wa Museveni , Dr Kiiza Besigye Akamatwa Baada ya Kujiapisha Kuwa Rais

$
0
0

Mpinzani mkuu wa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, Dk. Kizza Besigye ambaye amekuwa akipinga ushindi wa Rais huyo, amekamatwa na polisi wa nchi hiyo baada ya jana kujiapisha kuwa Rais ikiwa ni siku moja tu (leo) kabla ya Museven kuapishwa.


Haijulikani ni vipi Dr Kiiza Besigye alikwepa vizuizi  vya polisi na kuibukia mjini Kampala ambapo alikutana na wandani wa chama chake na ''kula kiapo cha urais wa taifa hilo''.


Katika video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii Dr Besigye anaonekana ''akila kiapo'' mbele ya mtu aliyevalia mavazi sawa na ya ''jaji wa mahakama ya juu''.


Video hiyo ilisambazwa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii na kusababisha mamlaka inayosimamia mawasiliano nchini Uganda kuamrisha kampuni zinazotoa huduma za simu nchini humo kufunga huduma za mitandao ya kijamii


Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilimtangaza Yoweri Museveni kuwa mshindi katika uchaguzi mkuu uliopita akiwaacha kwa mbali wapinzani wake wakuu, Kizza Besigye na Amama Mbabazi.


Kadhalika, Mahakama Kuu nchini humo ilihalalisha ushindi wa Museveni baada ya kutupilia mbali shauri la pingamizi la ushindi huo lililowasilishwa na Amama Mbabazi.

TAZAMA Hapa Video na Picha Jinsi Diamond na Mafikizolo Walivyotinga Bungeni Leo Asubuhi

$
0
0
May 12 2016 kundi maarufu la muziki kutoka Afrika Kusini Mafikizolo pamoja na staa wa bongofleva Diamond Platnumz walipata mwaliko wa kuingia Bungeni Dodoma ambapo wakali hawa wapo Dodoma kwa ajili ya kuidondosha burudani Chuo kikuu Dodoma.

Tazama Video Hapa:


Viongozi Wakuu Wote wa Taifa Wako nje ya Nchi ..Nani Anaongoza Nchi Kwa Sasa?

$
0
0
Viongozi wakuu wote wa Taifa wako nje ya nchi katika ziara za kiserikali kwenye mataifa tofauti.

Rais John Magufuli aliwasili Uganda jana asubuhi kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais mteule wa nchi hiyo, Yoweri Museveni zinazofanyika leo na Makamu wake, Samia Suluhu Hassan alikuwa Kigali, Rwanda kuhudhuria mkutano wa dunia wa uchumi.

Taarifa zilizopatikana na kuthibitishwa na Mwandishi wa Makamu wa Rais, Penzi Nyamngumi zimesema, Makamu wa Rais aliondoka nchini Jumanne akitokea Dodoma na angerejea kesho baada ya mkutano huo.

Kiongozi anayefuatia kwa wadhifa, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisafiri juzi kwenda London, Uingereza kumwakilisha Rais Magufuli katika mkutano wa wakuu wa nchi kujadili mapambano dhidi ya rushwa.

Majaliwa katika ziara hiyo ameongozana na Jaji Mkuu, Mohamed Chande Othman.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju alipotakiwa kutoa ufafanuzi juu ya anayepaswa kukaimu urais, alisema Makamu wa Rais amekwisha rejea nchini na yuko Mwanza.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 37 (3), inaeleza kuwa endapo Rais atakuwa hayupo katika Jamhuri ya Muungano, kazi na shughuli za Rais zitatekelezwa na Makamu wa Rais, kama naye hayupo, yatatekelezwa na Waziri Mkuu.

Hata hivyo, Ibara ya 37 (6) (b) inasema Rais hatahesabiwa kwamba hayupo iwapo atakuwa nje ya Jamhuri ya Muungano kwa kipindi cha saa 24.

Baby Madaha asema ameamua kutulia ili kuitunza ndoa yake

$
0
0
Msanii wa filamu, Baby Joseph Madaha, ameibuka na kudai kwa sasa ameamua kutulia katika ndoa yake na Mwarabu wa Dubai ambaye hakutaka kumtaja jina.
Baby Madaha

Muimbaji huyo ambaye yupo mbioni kuachia video ya wimbo wake mpya wa ‘Corazon’, ameliambia gazeti la Mtanzania kuwa kwa sasa maisha yake ni Tanzania na Dubai.

“Kwa sasa ninaishi nchi mbili, nipo Tanzania na pia nina makazi yangu mapya huko Dubai, nimeolewa na Mwarabu na nimetulia kwenye ndoa yangu najiachia kwangu, ahaaaa!” alijibu kisha akamalizia kwa kicheko.

Madaha amewataka mashabiki wa muziki wake kukaa mkao wa kula kwa ajili ya ujio ya video yake mpya ambayo ameshoot Dubai.

PICHA:Waziri Mkuu Akiwasili Ukumbi wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi London Kumwakilisha Magufuli

$
0
0

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiingia ukumbi wa Lancaster House, London kuhudhuria mkutano wa Wakuu wa Nchi kuhusu mapambano dhidi ya Ufisadi

Waziri Mkuu ameshiriki katika Mazungumzo Rasmi ya Wakuu wa Nchi, akimwakilisha Rais Magufuli

Siri za Matajiri Tanzania Kusajili Kampuni Nje ya Nchi

$
0
0
Wakati Mamlaka ya Mapato (TRA) ikijiapiza kuzifanyia uchunguzi wa kina kampuni za Kitanzania zilizoanzishwa nje ya nchi, wataalamu wameeleza jinsi wafanyabiashara wanavyotumia njia hiyo kukwepa au kuepuka kodi.

Jana, mkurugenzi wa elimu ya mlipakodi wa TRA, Richard Kayombo alisema ripoti ya Panama Papers ni chachu ya mamlaka hiyo kufanya uchunguzi wa kina na wa kimataifa ili kujua iwapo kuna chembechembe za ukwepaji kodi kwa kampuni hizo za Watanzania.

“Kwa kutumia mbinu tulizonazo, tutafuatilia iwapo kampuni hizo zimekwepa kodi wanayopaswa kulipa hapa nchini,” alisema.

 Kayombo alisema watatumia mbinu zote, kama Polisi wa Kimataifa(Interpol) na benki zinazohusika pamoja na kuchunguza miamala iliyofanywa na kampuni hizo kujua iwapo wamekwepa kodi.

“Hatuwezi kuzungumza kwa kina kwa sababu tutaharibu uchunguzi wetu, lakini kwa kifupi tutawa-trace (wafuatilia) wote,” alisema.

 Juzi, timu ya Umoja wa Waandishi wa Habari za Uchunguzi (ICIJ), yenye makao makuu Washington, ilitoa orodha ya zaidi ya watu 200,000 wakiwamo Watanzania wenye kampuni nje ya nchi.

Jumla ya Watanzania 45 na kampuni zaidi ya nane zenye uhusiano na Watanzania zimeorodheshwa kwenye ripoti hiyo iliyobatizwa jina la Panama Papers.

Miongoni mwa Watanzania waliotajwa kwenye ripoti hiyo ni mfanyabiashara maarufu na mwanasiasa aliyestaafu, Rostam Aziz, ambaye ameeleza kuwa hakuna ubaya kuwa na kampuni iliyosajiliwa kwenye visiwa hivyo.

Mwingine ni Yusuf Manji, mkurugenzi mstaafu wa kampuni ya Quality Group Ltd, ambaye pia ameeleza kuwa hakuna tatizo kumiliki kampuni zilizosajiliwa nje.

Pia yumo mbunge wa Morogoro Mjini na mfanyabiashara anayemiliki vyombo vya habari na usafirishaji, Abdulaziz Mohamed Abood, ambaye aliiambia Mwananchi juzi kuwa hana taarifa za ripoti hiyo ya Panama. Ripoti ya Panama inaeleza kuwa kampuni ya sheria ya Mosack Monseca ilihusika katika kusajili kampuni hizo na mwanzilishi wake akiwa ni Ramon Fonseca.

ICIJ imesema nyaraka zilizovuja na kutumiwa kwenye uchunguzi huo haziwezi kuwekwa bayana kwa kuwa zinahusisha baadhi ya watu ambao wanaweza kuwa hawakufanya makosa.

Jinsi wanavyokwepa kodi

Akizungumza na Mwananchi jana, Selius Mkwizu wa kampuni inayojihusisha na uchunguzi wa kodi nchini, alisema kampuni zinazofunguliwa nje ya nchi zinafuata unafuu wa kodi katika visiwa hivyo.

Kwa kawaida, visiwa hivyo huzitoza kampuni za nje ya nchi kodi isiyozidi asilimia 5 au chini ya hapo kwa ajili ya kuvutia soko la wawekezaji.

Hivyo, alisema wafanyabiashara wakubwa au wanasiasa hukimbilia na kufungua akaunti na kusajili kampuni kwenye nchi hizo na wakati huo huo hufanya ujanja ili wasikatwe kodi ya kampuni kwenye nchi yao.

Kwa hapa nchini ili kampuni iliyofunguliwa nje ya nchi ifanye kazi kihalali, inatakiwa ilipe asilimia 30 ya kodi ya kampuni au (corporate tax) kutokana na faida  ambayo  imepata. “Hata hivyo, wafanyabiashara na wanasiasa huhifadhi fedha zao kwenye akaunti za kampuni hizo (nje ya nchi) halafu baadaye huandika ripoti ya uongo inayoonyesha wamepata hasara na hivyo hawakatwi kodi,” alisema.

Kwa kawaida ili kampuni ikatwe kodi, ni lazima iwe imepata faida au wanahisa wamepata gawio  kutokana na faida iliyopatikana.

Mkwizu alieleza zaidi kuwa mara nyingi kampuni hizo ni hewa na jina lake hutumika kwenye akaunti kwa ajili ya kuweka fedha tu. Lakini kiuhalisia hazipo wala hazifanyi shughuli yoyote huko.

Namna wanavyocheza na nyaraka

Mwandishi wa ICIJ iliyotoa ripoti ya Panama, Will Fitzgibbon aliiambia Mwananchi kuwa wamiliki wa kampuni hizo huweza kukwepa kulipa kodi kwa kufanya mambo tofauti.

Alisema kwanza wanaweza kutunga uongo kwenye taarifa za fedha za mwaka na kuonyesha kampuni yao iliyo nje ya nchi imefanya matangazo, imefanya ukarabati, imelipa ada ya usimamizi au imefanya huduma za masoko kwa hiyo imepata hasara.

“Kwa maana hiyo basi, kama taarifa ya fedha ya kampuni hiyo itaonyesha kuwa imepata hasara, basi haitakuwa na vigezo vya kukatwa kodi kwa kuwa  kodi ya kampuni inatokana na faida,” alisema.

Alisema ICIJ wamegundua kuwa licha ya kampuni hizo kudai kuwa zimepata hasara, wanahisa au bodi ya wadhamini wanaonekana kupata gawio, kujenga nyumba za kifahari au kumiliki mali zenye thamani kubwa kwenye nchi hizo.

Alisema kingine kilichobainika ni wamiliki wa kampuni hizo kuwa na kampuni nyingine ambazo wamiliki wake ni ndugu zao kama vile mpwa, dada au kaka . Hivyo, kampuni hizo hupata zabuni kutoka kampuni mama.

“Ujanja mwingine ni kampuni kuwa na bodi ya wadhamini ambao ni ndugu wa karibu, wanafamilia na kampuni yenye jina moja kufanya kazi nchi zaidi ya moja,” alisema.

Hata hivyo, Fitzgibbon alisema bado nyaraka za Panama zitaendelea kutoa taarifa za namna kampuni hizo zinavyokwepa kodi.

Kanuni za  ‘offshore’

Ili kupambana na uhamishaji wa fedha unaohusisha ukwepaji wa kodi, Februari 7,  2014 Tanzania ilitambulisha kanuni mpya ya Kodi ya Mapato inayohusu gharama za kuhamisha fedha (Transfer Pricing Regulations). Kanuni hizi zinawagusa walipa kodi wote walio ndani na nje ya nchi, lakini  iwapo tu kampuni itaonekana haijapata hasara.

Kama kampuni imepata hasara, haitakatwa kodi.

Kanuni za gharama za kuhamisha fedha zinaangalia miamala iliyofanywa na watu au kampuni zinazofanya kazi nje.

Kadhalika zinaangalia namna kampuni hizo zinavyohamisha kiasi cha faida au gawiwo la faida kutoka nchi moja kwenda nyingine.

Hata hivyo, Mkwizu alisema kanuni  hii ni dhaifu kwa kuwa ni vigumu kwa nchi kufuatilia na kujua iwapo kampuni iliyofunguliwa kwenye visiwa hivyo imefanya kazi zilizoainishwa kwenye  taarifa ya fedha na kama kweli ipo.

BOT wazungumza

Wakati TRA ikijipanga kuchunguza suala hilo, Benki Kuu imesema kutolipa kodi kwa sababu yoyote ile ni uhalifu na lazima ushughulikiwe.

Meneja uhusiano wa Benki Kuu, Zalia Mbeo alisema usajili wa kampuni nje ya nchi unatakiwa kufuata taratibu za nchi husika na za kimataifa. Hata hivyo, alisema lazima utaratibu huo uwe na manufaa kwa muhusika na nchi anayotoka.

“Ndiyo maana tuna Watanzania wanaofanya kazi nje ya nchi na ambao wanarejesha nyumbani fedha nyingi za kigeni kutokana na mapato yao halali,” alisema.

“Tunaamini kwamba ukiukwaji wa taratibu za usajili kwa lengo lolote, likiwamo la kutolipa kodi ni uhalifu kama uhalifu mwingine na unapaswa kushughulikiwa na mamlaka husika,” alisema.

Kibarua cha Rais wa Brazil Chaota Nyasi, Apigiwa Kura ya Kutokuwa na Imani Naye

$
0
0
Kitumbua cha Rais wa Brazil, Bi. Dilma Rousseff kimeingia mchanga.

Baraza la senate limempigia kura ya kutokuwa na imani naye. Hiyo inamaanisha kuwa atakaa benchi na kupelekwa kortini. Bi Rousseff anatuhumiwa kulaghai hesabu za kifedha ili kuficha deni la umma linalokua kabla ya uchaguzi wa mwaka 2014, kitu anachokanusha.

Maseneta walipiga kura 55 za kumuondoa katika mkutano uliodumu kwa zaidi ya saa 20. Ni 22 tu ndiyo waliokuwa upande wake. Makamu wa Rais, Michel Temer atakaimu nafasi yake wakati kesi ya Bi Rousseff ikianza kusikilizwa.

Kesi hiyo inaweza kuchukua siku 180 hiyo inaamanisha kuwa atakuwa amesimamishwa katika kipindi ambacho michuano ya Olimpiki jijini Rio de Janeiro itaanza, August 5.

Mbunge Sugu Achague Kuongea Kiswahili au Kiingereza Bungeni Anatuchanganya

$
0
0
Huyu mbunge Sugu akichangia hoja huwa anachanganya kiswahili na kiingereza ili aonekane msomi.Wakati hamna kitu.Ukimsikiliza tu anavyoongea unajua ana elimu ya kuunga unga akitafuta aonekane naye yumo yumo.

Ushauri wangu achague ama aongee kiswahili au kiingereza.Lakini hicho cha kuunga unga na kuokoteza okoteza maneno ya kiingereza anatuchanganya na kutukera.

Picha za Lulu Michael na Muna love Zawa Gumzo Mtandaoni

$
0
0
 Mrembo Lulu Michael na rafiki wa Wema Sepetu Munalove wameachia picha walizopiga pamoja kwenye mtandao wa instagram ambapo zimevuta fans wengi wakiwasifia na wengine kuwasema



Cyrill Kamikaze Akanusha Kuwa na Uhusiano na Mrembo Kidoa

$
0
0
Rapper Cyrill Kamikaze amekanusha kuwa na uhusiano na video Queen wake wa katika video ya ‘Shori’ Kidoa.

Akiongea na E-Newz, Cyrill amesema kuwa yeye na video queen huyo ni washkaji tu. Kuna tetesi kuwa Cyrill alimtosa mwanamke wake wa zamani ili awe na mwananadada huyo.

Kuna picha ambayo Kidoa alipost na kuandika: He is ma real Ma, huku zikiwa zimebebwa na picha za Cyrill. Hata hivyo rapper huyo amekanusha kwa kudai, “Watu tu wameamua kuichukulia hivyo lakini hakuwa huko.”
Viewing all 104667 articles
Browse latest View live




Latest Images