Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104712 articles
Browse latest View live

Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL) Imekanusha taarifa za Kuficha Sukari

$
0
0
industrial sugar
Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL) imekanusha taarifa ambayo ilitolewa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa kampuni hiyo imeficha sukari tani 2,990 katika Bandari Kavu (ICD) ya PMM iliyopo Vingunguti, Dar es Salaam.
Taarifa hiyo imekuja baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutembelea ICD na kukuta tani 2,990 ambazo aliambiwa kuwa ni mali ya Mohammed Enterprises jambo ambalo halikuwa na usahihi bali ni mali ya Tanzania Commodities Trading inayomilikiwa na Murtaza Dewji.
Kwaa mujibu wa Murtaza Dewji ambaye ndiyo mmiliki wa sukari hiyo amesema kuwa sukari hiyo iliingia nchini kwa kufata utaratibu wote kama jinsi inavyotakiwa na anashangazwa kwanini hakufatwa ili kutoa maelezo kuhusu sukari hiyo.
“Tulifuata taratibu zote zikiwepo mamlaka husika za nchi kma bodi ya sukari, Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na vyombo vyote vya ulinzi na usalama,” amesema Murtaza.
Akifafanua zaidi amesema kuwa sukari hiyo ilikuwa njiani kuelekea nchini Uganda na vielelezo vyote vipo lakini kutokana na uhaba wa sukari nchini, serikali iliagiza mzigo huo kubaki nchini na kuingiza sokoni ili kumaliza tatizo hilo ambapo ulitakiwa kuanza kuingia sokoni kati ya Mei, 12 na Mei, 13.
Aidha ameelezea kuwa ni jambo la kawaida kuagiza sukari kutoka Dubai kwani hutumia siku 7 pekee kufika nchini tofauti na sukari kutoka Brazil ambayo hutumia siku 50 hadi 60 ikiwa njiani hadi kufika nchini.
“Wafanyabiashara wote wanaojua biashara walioko karibu na Dubai hufanya hivyo na sisi sio wa kwanza kuagiza sukari kutoka kwa wauzaji wa Dubai,” amesema Murtaza.
Pia Murtaza amewatoa hofu Watanzania kuhusu uhaba wa sukari kwa kusema kuwa tayari sukari imeagizwa na ndani ya wiki mbili kutakuwa na sukari ya uhakika nchini hivyo kuwataka kuondoa hofu iliyokuwapo hapo awali.
Kibali halali cha TFDA hiki hapa chini

Kuongea Kiingereza ni Kipaji – Shilole Afunguka

$
0
0
Msanii wa muziki, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amefunguka kwa kudai kuongea Kiingereza siyo kitu cha mchezo kama watu wanavyofikiria.

Akizungumza katika kipindi cha Enewz cha East Africa Television Jumatano hii, Shilole alisema yeye amepigana mpaka ameweza kuongea Kiingereza.

“Kiingereza ni kipaji jamani, mimi naongea Kiingereza wakati ambao najisikia. Lakini asikwambie mtu, kuongea Kiingereza ni kipaji,” alisema Shilole.

Muimbaji huyo ameachia kazi mpya iitwayo ‘Say My Name.’

Tisa Mbaroni kwa Kuuza Sukari Kinyume cha Bei Elekezi

$
0
0
Polisi mkoani Arusha inawashikilia watu tisa kwa kosa la kuuza sukari tofauti na bei elekezi ya Sh1,800.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amesema leo kuwa watu hao wamekamatwa kwa nyakati tofauti na watashtakiwa kwa makosa ya uhujumu uchumi.

Mkumbo alisema mmoja wa watu hao amekutwa akiuza kwa Sh5,000 kwa kilo moja.

Alisema wengine walikamatwa wakiuza sukari Sh6,200; Sh3,000; Sh2,500  na Sh4,500 kwa kilo.

Kamanda Mkumbo amesema kamatakamata ya watu wa aina hiyo ni endelevu na aliwashauri wafanyabiashara wote mkoani Arusha kuuza sukari kwa bei elekezi iliyopangwa na Serikali.

Kwa Hili Mafikizolo Watasimulia Kwao-Diamond Platnumz Afunguka

$
0
0
Diamond Platnumz amedai kitendo cha serikali kuwapa nafasi kuja bungeni leo kumeonyesha jinsi gani serikali inajali vipaji vya Tanzania hivyo hiyo ni picha nzuri ambayo wasanii hao wa kundi la Mafikizolo wataondoka nayo pindi watakapo rejea nyumbani kwao.
"Unajua leo tuna show hapa Dodoma mimi na Mafikizolo hivyo serikali kupitia kwa Waziri Nape Nnauye walitualika bungeni japo ni kwa muda mchache lakini kitendo hiki kinaonyesha jinsi gani serikali yetu inajali wasanii, unajua hawa wenzetu wanapokuwa kwao na sisi tunapokwenda huwa tunapata mapokezi mazuri sana hivyo na mimi nashukuru kwa hili kwani itafanya hata wenzetu wajue serikali yetu inajali wasanii wake". alisema Diamond Platnumz.

"Kesho na kesho kutwa wenzetu wakirudi kwao watasema wale wenzetu wale serikali yao inawajali na kuwa support wasanii wake kwani tulikwenda tukapata nafasi kwenda mpaka bungeni na watasimulia mambo mbalimbali ambayo wao wamejionea hivyo ni kitu kizuri" aliongezea Diamond Platnumz

Mbali na hilo Diamond Platnumz alielezea wimbo wao huo wa pamoja ambao unaitwa 'Colours of Africa' ni wimbo ambao unazungumzia tamaduni za Kiafrika, ushikamano na umoja wa bara la Afrika.

Suala la Yanga na Ndanda Kuchezea Uwanja wa Taifa, Simba yasema ni Rushwa

$
0
0

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano Jerry Muro amesema, Ndanda FC itakapoutumia Uwanja wa Taifa itamaanisha kwamba Ndanda FC watakuwa nyumbani na hata mapato katika mgao asilimia kubwa ataipata Ndanda hivyo haoni sababu ya wengine kuanza kuongea kwa kuona ni makosa katika mchezo huo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Klabu ya Simba Zacharia Hans Pope amesema, mchezo huo ni sio halali kwani inaonekana ni rushwa ya waziwazi kwa timu hizo, kwani haiwezekani umfadhili mpinzani wako ambaye unashindana na ukategemea matokeo ya halali.
Yanga ambayo ndio bingwa wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara msimu wa 2015/16 wakiwa wamesalia mechi mbili mkononi itakutana na Ndanda F Jumamosi Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo mara baada ya kukamilika kwa mchezo huo, Yanga watakabidhiwa Kombe la Ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Download Application ya SIASA HURU Blog Kwenye Simu yako Kupata Habari za Siasa Kwa Urahisi

$
0
0
Kama wewe ni mpenzi wa Habari za Siasa basi hii ni habari njema kwako...Download Siasa Huru Application Kutoka Google Play Store Kwenye Simu yako itakurahisishia upataji wa Habari na Breaking News za Siasa kwa urahisi....

Bonyeza HAPA Kuinstall Kwenye Simu yako fasta....

Au Nenda Google Play Store Kwenye Simu yako Alafu Search 'Siasa Huru' Kisha Install


SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya May 13, Ikiwemo ya Zitto Kusema Serikali Imekata Tamaa

$
0
0

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya May 13, Ikiwemo ya Zitto Kusema Serikali Imekata Tamaa

Diamond Hakamatiki..Hivi Ndivyo Alivyowasha Moto Jana Dodoma Akiwa na Mafikizolo

$
0
0
Mwanamuziki wa kizazi kipya Nasibu Abdul “Diamond Platinum’s” akiwaimbia kwa hisia wakati wa mashabiki wake waliofika kwenye Tamasha la Vodacom Kichuo zaidi lillilofanyika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) jana
Mwanamuziki wa kizazi kipya Nasibu Abdul “Diamond Platinum’s” pamoja na kundila muziki la Mafikizolo wakiimba wimbo wao wa Color of Afrika wakati wa Tamasha la Vodacom Kichuo zaidi lillilofanyika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)
Nyomi ya  mashabiki wa muziki waliofika kwenye Tamasha la Vodacom Kichuo zaidi lillilofanyika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)
Msanii wa muziki wa kundi la Mafikizolo kutoka Afrika ya kusini,Theo  Kgosinkwe  akionyesha umahiri wake wa kucheza muziki  katika Tamala la Vodacom kichuo zaidi lililofanyika  chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) jana

Mbunge Apewa Siku 3 Atoe Ushahidi wa Magari 777 ya Washawasha

$
0
0
SPIKA wa Bunge, Job Ndugai amempa siku tatu Mbunge wa Viti Maalumu, Susan Lyimo (Chadema) awasilishe mbele ya Kamati ya Maadili ya Bunge, maelezo ya utetezi dhidi ya madai aliyotoa bungeni kuhusu Serikali kununua magari ya washawasha 777.

Ndugai alitoa amri hiyo kutokana na mwongozo ulioombwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yussuf Masauni juzi akitaka Lyimo athibitishe au afute kauli yake juu ya madai hayo wakati serikali imenunua magari 32.

“Hata kwa akili ya kawaida haiwezekani Serikali ikaagiza magari yote hayo 777 ya washawasha. Ninachokumbuka mimi Waziri huyu aliwahi kusema hapa bungeni kuwa magari hayo 777 ni idadi ya magari yote ya aina mbalimbali yaliyonunuliwa kwa ajili ya matumizi ya polisi,” alisisitiza Ndugai.

“Sasa nakutaka uniandikie rasmi majibu vizuri kuhusu kauli yako hii, nakupa siku tatu uwe umeniletea na baadaye nitaipeleka taarifa yako kwa Kamati ya Maadili ya Bunge, ili kujadili suala hili kwa mapana,”alisisitiza Ndugai.

Awali mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu, Ndugai alimpatia mbunge huyo nafasi ya ama kufuta kauli yake hiyo au aithibitishe kabla ya hatua za kikanuni za Bunge hazijachukuliwa dhidi yake.

Lyimo alikataa kufuta kauli hiyo na kudai kuwa anao uthibitisho juu ya idadi hiyo ya magari aliyoitamka na kusisitiza kuwa amenukuu taarifa za idadi hiyo kupitia taarifa iliyotolewa na mtandao wa Jamii forum pamoja na taarifa za Hansad za Bunge.

“Mheshimiwa Spika mimi ni mtu mzima siwezi kwenda kwa hisia za watu, ni kweli jana niliombewa mwongozo bahati mbaya sikuwepo ndani ya Bunge. Nathibitisha kauli yangu na wala siifuti kwa kuwa nina uhakika na idadi ya magari niliyoisema,” alisisitiza mbunge huyo.

Alisema kwa mujibu wa Kanuni ya 63 (2) ya Bunge, mbunge hatasema uongo endapo chochote atakachokisema ndani ya Bunge atakuwa amekirejea kwenye chombo cha habari au taarifa za Bunge.

Magufuli Anasema Tumbueni Majipu laivu, Samia Anasema Tumbueni kwa Kufuata Utaratibu...Viongozi Wamfuate Nani?

$
0
0
Katika utumbuaji majibu kwa watumishi wa umma Rais Magufuli alitamka kwa msisitizo kuwa hakuna kuwapa nafasi watu wanaotuhumiwa kuharibu kazi zao Bali ni kuchukua hata mengine baadae yatajulijana. Kuna waliopiga kelele kuwa kanuni za utumishi hapo zinakiukwa. Nae akajibu potelea mbali alipokuwa anazungumza na viongozi wa ccn Ikulu.

Jana Makamu wa Rais Samoa akiwa Geita kaagiza viongozi wa serikali na kisiasa (kisiasa nadhani ni mawaziri,RC na DC) kuacha kuchukua hatua kwa watumishi bila kufuata kanuni za kazi na kusikiliza upande wa pili.

Jee huku nikufuta kauli ya Rais baada ya kuona imekwenda kinyume au ni kila mtu na agizo lake? Viongozi walioagizwa wafuate kauli ioi hapo?

By Chakaza

Kumbe Madee Alimkwichikwichi na Shilole na Nuhu Kuwafumania !

$
0
0
Aisee hii hata mimi nilipitwa nayo ama kweli mimi mapenzi basi nimeyavulia Shati akuu mapenzi sio ubondia bora nijitoe

Leo akihojiwa na Diva clouds Fm Mziwanda amekiri kuwa Madee alitembea na Shilole kipindi wapo wote na Aliwafumania na kumkuta mmoja wao akiwa hana nguo,Diva anakiri kusikia hizo habari ila alitaka Nuh athibitishe Nuh anasema inauma sana ila ana muheshimu sana Madee ana Muheshimu pia Shilole japo Inauma sasa wali kwichi kwichi na kuwafumania

Oyo nitakupigia nitakupia baadae noma noma noma sanaaaaa

Hapa Miguu pande hapa Say my name Shishi hapa Jike shupa oyooooo

Download HAPA Wimbo Mpya wa Ali Kiba Unaoitwa 'Aje'

$
0
0
'Alikiba's new song featuring 'MI' titled 'Aje' has been making rounds on social media for weeks now but finally has been released officially today. The audio has however left his fans speechless as this time around 'King Kiba' spiced the song by mentioning  famous celebrities like 'Wema Sepetu' and 'Lulu'. From the lyrics to the beat, there is doubt that the Tanzanian star took his time to come up with this one.

'M.I' who is a popular Nigerian rapper has given the song a major boost by opting to sing his verse in Swahili. The Swahili vibe could be a new trend for the Nigerian artistes as we have seen 'Yemi Alade' and 'Cynthia Morgan' do the same.

CLICK HERE to DOWNLOAD

Chadema Waungana na CUF Kutomtambua Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein.

$
0
0
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetangaza rasmi kutoitambua Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), inayoongozwa na Dk Ali Mohamed Shein.

Mbali na kutoitambua Serikali hiyo, chama hicho kimesema leo kitatoa mkakati mzito wa namna ya kushughulikia suala la matangazo ya Bunge la Kumi na Moja kutoonyeshwa moja kwa moja (live) na televisheni.

Msimamo huo ulitangazwa kwa waandishi wa habari jana mjini Dodoma katika kikao cha pamoja kati ya Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vicent Mashinji, manaibu wake wawili, John Mnyika (Bara) na Salum Mwalimu (Zanzibar).

Pia walitoa taarifa juu ya mambo yanayojadiliwa katika kikao cha siku mbili cha Kamati Kuu (CC) kinachofanyika chini ya Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe.

Akizungumzia hali ya kisiasa Zanzibar, Mwalimu alisema chama hicho hakitampa ushirikiano Dk Shein.

“Kikao maalumu cha Kamati Kuu ya Chadema kilichoketi Jumatatu, tumefikia msimamo wa kutoitambua Serikali ya SMZ. Msimamo wa Maalim Seif Shariff Hamad ndiyo msimamo wetu,” alisema.

Maalim Seif aliwania urais Zanzibar kupitia CUF katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana kabla ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), kufuta matokeo yake na kutangaza uchaguzi wa marudio ambao mgombea huyo na chama chake walisusia.

“Hatutatoa ushirikiano kwa SMZ na katika kikao cha leo (jana) cha CC tutawasilisha azimio hilo.Hali ya kisiasa Zanzibar ni mbaya mbaya sana. Wazanzibari wanaelekea kununa,” alisema Mwalimu.

Mwalimu alisema hawatafanya maandamano Zanzibar lakini hali itakuwa mbaya zaidi kwani Wazanzibari wengi wanaelekea kununa na kwamba hilo litasababisha hali mbaya zaidi.

“Hali ya Zanzibar si nzuri kama CCM wanavyoeleza.  Watu hawazikani, hawatembeleani tumerudi kulekule kama mwaka 1995 kabla ya kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa,” alisema.

Mashinji alisema kikao hicho cha kamati kuu kitapokea taarifa kutoka kwa wabunge wa Chadema, kuhusu Bunge kutoonyeshwa ‘live’ na athari zake kwa wananchi.

“Uhuru wa wananchi kupata habari litajadiliwa kwa kina. Sasa hivi Bunge letu liko gizani tunapata habari za kupapasa tu. Tutatoka na mkakati kabambe wa kushughulikia suala hili,” alisema.

Akizungumza hatua hiyo iliyochukuliwa na Bunge, Mnyika alisema kinachoonekana sasa ni kama chombo hicho kimetekwa na Serikali na hilo litatolewa tamko zito rasmi leo na Mbowe mwenyewe.

“Kuna mambo makubwa tuki- yawekea mkakati huwa Serikali inasalimu amri. Tunataka kutoka kwenye huu mkwamo ili Bunge lionyeshwe live,”alisema.

Januari 27, Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye alitangaza Serikali kusitisha matangazo hayo ya moja kwa moja kama njia ya kubana matumizi.

Waziri huyo aliliambia Bunge matangazo hayo yatarushwa vipande muhimu vya mijadala usiku katika kipindi maalumu cha Leo katika Bunge ambacho kitarushwa saa nne za usiku uamuzi ambao ulipingwa vikali ndani na nje ya Bunge.

Leo, Nape atawasilisha bajeti ya wizara yake bungeni ambako mjadala mzito unaotarajiwa kulitikisa Bunge ni suala hilo la kutoonyeshwa moja kwa moja kwenye televisheni.

Wadau wa habari wamepiga kambi mjini hapa kujaribu kuishawishi Serikali na Bunge kubadili msimamo huo

Shombo ya Samaki Marufuku Mabasi ya Kasi Dar es Salaam

$
0
0
ABIRIA wenye mizigo mikubwa na samaki wasiohifadhiwa vizuri, hawataruhusiwa kupanda mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam.

Hatua hiyo imelenga kuwapunguzia bugudha na shombo watumiaji wengine wa vyombo hivyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni inayoendesha mabasi hayo UDA-RT, David Mgwasa, aliyasema hayo alipozungumza na gazeti hili jana, alipoulizwa kuhusu abiria wanaosafiri na samaki kutoka Kituo cha Kivukoni kwenye Soko la Kimataifa la Samaki na kwingineko.

Alisema ili kuepuka abiria wengine kubugudhiwa na kupata shombo ya samaki, abiria wenye mizigo mikubwa hawataruhusiwa na wenye samaki lakini watakaohifadhi samaki vizuri kwenye ndoo safi, watatumia huduma hiyo.

UDA-RT ilianza kutoa huduma ya usafiri kwa mabasi hayo kuanzia Jumanne wiki hii na inaendelea kusafirisha abiria bure hadi Jumapili, lengo likiwa ni kutoa muda wa elimu ya namna ya kutumia mabasi hayo.

Aidha, Mgwasa alisema leo mabasi hayo yataanza saa 12 asubuhi mpaka saa tano usiku.

Alisema kuwa wamekuwa wakiongeza muda zaidi nyakati za usiku, kutokana na changamoto za nyakati hizo, kabla ya kuanza rasmi huduma hiyo Jumatatu.

Kwa mujibu wa Mgwasa, kwa sasa kuna mabasi 80 barabarani katika njia zote. Kesho kutwa, Jumapili, UDA-RT itahakikisha mabasi yote 140 yanakuwa barabarani, kufanya majaribio ya kubadilisha abiria.

“Tunazidi kuongeza muda wa kulaza mabasi, na pia Jumapili tutatoa mabasi yote, kwani mbali na kuangalia suala zima la abiria na uendeshaji pia tunaangalia namna nzuri ya madereva kubadilishana, maana haiwezekani dereva akaamka saa 10 aendeshe hadi usiku,” alisema.

Uwezo wa magari Mgwasa alisema mabasi makubwa yana uwezo wa kubeba abiria 150 kwa safari moja na madogo yanabeba abiria 90.

Wingi wa watu unaoonekana kwenye mabasi hayo kwa sasa, unatokana na kuruhusu mabasi machahe kuwa barabarani. Kadi (tiketi) Mgwasa alisema kadi maalumu ambazo zitauzwa kwa Sh 5,00 kwa bei ya promosheni, itakuwa ikitumika kwa mtu mmoja wakati wa safari.

“ Mtu kama ana kadi moja na anasafiri na familia yake, kadi hiyo itatumika kwa mtu mmoja na wengine watalazimika kukata tiketi, kwani kadi itamruhusu mtu mmoja wakati wa kuingia na kutoka,” alisema.

Exclusive… DJ Maarufu Dar Adai: Nimezaa na Mama Diamond Platnumz

$
0
0
Kumekuwepo na usiri juu ya baba wa mdogo wa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Esma Platnumz lakini huenda utata ukafika mwisho baada ya aliyekuwa DJ maarufu jijini Dar kuibuka na kudai kuwa ndiye aliyemzaa mtoto huyo na mama Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ akimpinga na kuamua kumuweka wazi baba halali wa Esma.

ILIKUWAJE?
Mapema wiki hii, mtu mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Jerry Kato mkazi wa Boko jijini Dar, alipiga simu kwenye chumba cha habari cha gazeti hili na kueleza kuwa, ana jambo linaloutesa moyo wake na kwamba amekuwa akitafuta kuwasiliana na Magazeti ya Global kwa muda mrefu hivyo angependa kukutana na mwandishi wetu ili atoe lililoukamata moyo wake.

WAKATUNA BOKO
Baada ya kufanyika mawasiliano, mwandishi wetu na Jerry walikutana na jamaa huyo huko Boko, nje kidogo ya Jiji la Dar ambapo alifunguka kuwa, yeye ndiye baba mzazi wa Esma Platnumz ila anashangaa mama wa mtoto huyo amekuwa akikwepa kumtambulisha.


MSIKIE MWENYEWE!
“Mimi naitwa Jerry Kato, nakumbuka mwaka 1982, nilikutana na huyu Sanura (Mama Diamond) pale Mbowe Hotel (sasa Bilicanas iliyopo Posta jijini Dar). Alikuja na jamaa mmoja anaitwa Spencer wakati mimi nafanya kazi ya U-DJ pale, tukatokea kupendana na kuanzisha uhusiano.
“Baada ya muda mrefu, Sanura alinasa ujauzito wakati huo mimi nakaa palepale Mbowe Hoteli, yeye anakaa Saigon (Kariakoo, Dar). Basi akawa anakuja pale hotelini na kunisumbua, si unajua tena mambo ya mimba.

 ….“Akaniambia alikuwa ananitafuta lakini aliambiwa nimekufa. Basi tukapanga tuonane, akaniambia niende mpaka Sinza (Mori) pale Big Bon, nikifika pale nimpigie simu atanifuata.
…..“Mara akaanza mazungumzo na kuniambia, ‘Jerry unakumbuka?’ nikamwambia nakumbuka, basi akaniambia, ‘sasa leo nataka nikuoneshe mtoto wako’. Akaita Esmaaa…, yule binti akaitika, akaja, akaita tena Nasibuuu, ndiyo akatokea Diamond…”.
“Hapo ndiyo akafanya utambulisho kwa Esma na kumwambia mimi ndiye baba yake hivyo asimsumbue tena. Na kweli nilipomtazama (Esma) anafanana na mama yangu mzazi hata rangi. Ikawa ni furaha tukakumbatiana na maisha yakaendelea.

Chanzo :Global Publishers

Nikitaka Kuolewa Nitaolewa tu Muda Wowote -Wastara Afunguka

$
0
0
Msanii wa bongo Movie Wastara Juma afunguka juu ya stori zinazozagaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii na magazeti ya udaku kuwa hataki tena Ndoa.

Akizungumza na Enewz Wastara alikanusha tuhuma hizo na kusema kuwa ndoa yake na mheshimiwa ilikua imejaa timbwili timbwili na makubwa mpaka ikapelekea akadai talaka na baada ya mheshimiwa kusanda pia wametokea wengi kutaka kumuoa bila kujali hali yake.

“Kusema sitaki ndoa ni kitu ambacho hakiwezekani isipokuwa tu kwamba kila hatua moja ninavyopiga najifunza kutokana na makosa mimi nikisema sitaki tena mapenzi nitakuwa namkufuru mungu nikitaka kuolewa nitaolewa tu muda wowote”,alisema Wastara

Diamond na Zari Wanachepuka? Ukweli Huu Hapa

$
0
0
Star wa Bongo fleva Diamond Platnum akanusha juu ya stori zilizozagaa mitandaoni kuwa mpenzi wake Zarina ama mama Tiffa anachepuka na Ivan huku yeye akichepuka na video Quuen wa Ketu ya

Akizungumza na Enewz Diamond alisema kuwa hizo ni stori tu ambazo mapaparazi waliamua kuzitengeneza lakini Zari hakuwahi kuwa na uhusiano wowote na Ivan tangu awe na yeye.

mahusiano yetu ni ya kimaarufu ambayo yamempelekea hadi X wake nae pia kuwa maarufu so unapokuwa maarufu vitu vinakuwa vingi na kwa Irene wanahisi hivyo kwakua ni mzuri na kwakuwa naonekana maarufu na ninauwezo na vile pia Ray ni msanii wetu so wanahisi naweza kufanya hivyo pia.

Stori zilizozagaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii ni kuwa Zari amerudiana na mpenzi wake wa zamani na inasemekana kwa sasa Zari na Ivan wanachepuka huko South Africa wakati Mondi naye akijiachia na Irene ambae ni video Queen wa Raymond katika nyimbo ya Kwetu.

Picha za Waziri wa Sudan Zazua Gumzo Mtandaoni.

$
0
0
Waziri wa Maji na Umwagiliaji wa Sudan Kusini Mh. Mabior Garang De Mabior ambaye ni mtoto wa Rais wa kwanza wa Sudan Kusini na kiongozi wa zamani wa kikundi cha waasi cha SPLA/M cha Sudan Dr. John Garang amekuwa gumzo mitandaoni baada ya picha zake zenye utata kusambaa katika mitandao ya kijamii.

Mabior Garang ambaye ni mtoto mkubwa wa Marehemu John Garang ambaye aliongoza kikundi cha waasi kwa muda mrefu kabla ya kufariki katika ajali ya Helkopta mwaka 2005 akiwa Rais wa Sudan Kusini, alifukuzwa katika kikao cha Baraza la mawaziri na Rais wa nchi hiyo Salva Kiir kwa kile kilichosemwa kuvaa mavazi yasiyostahili.

Mwaka 2014, Mabior aliwahi kukamatwa na maafisa usalama wa Ethiopia kwa kile kilichohisiwa kuwa jaribio la kutaka kumuua Rais wa sasa wa Sudan Kusini Salva Kiir baada ya kukamatwa akiwa hotelini na bastola ikiwa na risasi sita. Baada ya kukamatwa na kuhojiwa alisema alitaka kukutana na Rais Kiir kwani ameharibu kazi kubwa na nzuri iliyofanywa na Baba yake John Garang.

Mabior Garang anahudumu katika Serikali ya Umoja kupitia Dr Riek Machar ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Sudan Kusini

Mwanamuziki Linah Asimulia Jinsi Alivyotumia Simu Kusaka Mpenzi

$
0
0
Msanii wa Bongo fleva Linah a.k.a ndege mnana amefunguka moja kati ya vitu ambavyo hawezi visahau katika maisha yake yote.

Akizungumza na Enewz Linna alisema kwamba moja ya kitu hicho ni tukio ambalo walilifanya yeye na mwenzie kipindi wanasoma kwani walikuwa wana tabia ya kujaribu kupiga namba tofauti tofauti ili kutafuta mpenzi.

“Nilifanikiwa kumpata mwanaume ambae nikawa ninawasiliana nae lakini siku tunaenda kuonana nae tulikutana na kitu hicho ambacho siwezi kusahau maana tulikutana na mtu ambae hatukutegemea kutokana na sauti yake ambavyo tulikuwa tukiisikia katika simu tukaamua kutojitokeza “,alisema Linna.


Tigo Yapinga Kuwalipa AY, MwanaFA Shilingi Bilioni Mbili

$
0
0

Kampuni ya simu ya MIC Tanzania (Tigo) imekata rufaa kupinga hukumu iliyoamuru iwalipe Sh2 bilioni wanamuziki wawili, Ambwene Yesaya na Hamisi Mwinjuma kutokana na kutumia bila ya ridhaa yao, nyimbo za wasanii hao nyota nchini.

Yesaya, ambaye ni maarufu kwa jina la kisanii la AY na Mwinjuma anayejulikana kwa jina la MwanaFA, walifungua kesi hiyo ya madai kwenye Mahakama ya Wilaya ya Ilala kupinga kitendo cha kampuni hiyo ya huduma za simu kutumia nyimbo zao kwenye miito ya simu bila ya ridhaa yao.

Nyimbo mbili zilizotumika kwenye miito hiyo ya simu ni “Dakika Moja” na “Usije Mjini” ambazo nyota hao wameshirikiana.

Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Juma Hassan alitoa hukumu ya kesi hiyo Aprili 11, akiwapa ushindi wasanii hao maarufu katika muziki wa vijana uliopachikwa jina la Bongo Fleva.

Katika hukumu hiyo, Mahakama iliiamuru Tigo kulipa Sh5 milioni kama faini ya uharibifu na kulipa Sh2.16 bilioni kama faini ya jumla.

Iwapo wasanii hao watashinda rufani hiyo, watakuwa wameandika historia katika matumizi ya Sheria ya Haki Miliki na watakuwa wasanii wa kwanza wa muziki wa kizazi kipya kufungua kesi na kushinda.

Katika rufaa hiyo, Tigo kupitia kampuni ya Law Associates imeainisha sababu saba za rufani, ikidai hakimu wa Mahakama ya Ilala alikosea kisheria kuwapa ushindi wasanii hao kwa kuwa hawakuthibitisha madai yao wala hasara waliyopata.

Kampuni hiyo pia inadai kuwa mbali na kutoeleza hasara waliyoipata kutokana na kazi zao kutumika kwenye miito ya simu, walitakiwa kueleza faida ambayo wangepata kama kazi zao zisingetumika kwenye miito hiyo.

Sababu nyingine ya Tigo kukata rufaa hiyo ni wasanii hao hawakuwa wamesajili kazi zao Chama cha Hakimiliki Tanzania (Cosota).

Tigo inadai kuwa wakati wa usikilizwaji wa kesi ya msingi, wadai walisema wamesajili kazi hizo, lakini waliwasilisha barua ya Baraza la Sanaa (Basata) ya kutambua kupokea kazi zao na si cheti cha usajili cha Cosota.

Kwa mujibu wa Tigo, wanamuziki hao walipaswa kuwasilisha mahakamani cheti cha usajili wa Cosota ambako kuna utaratibu wa kujisajili ikiwa ni pamoja na kujaza fomu maalumu baada ya kulipia malipo ya usajili ya kila mwaka.

Kampuni hiyo inasisitiza kuwa wasanii hao hawakuwa na haki ya kudai fidia hiyo wakati hawajasajili kazi hizo Cosota na hivyo kuiomba Mahakama Kuu itengue hukumu iliyowapa ushindi.

Akizungumzia hukumu iliyowapa ushindi, MwanaFA alisema huu ni wakati wa mabadiliko.

“Wale waliokuwa wanachukulia Sheria ya Hakimiliki kama mzaha, watambue kwamba zama zimebadilika,” alisema nyota huyo wa muziki wa rap ambaye aliingia kwenye muziki akijitambulisha kama Mwanafalsafa kabla ya kufupisha jina lake na kuwa MwanaFA.

“Hakuna anayetilia maanani kutumia kazi za wasanii bila ridhaa yao huku akinufaika na wasanii kubaki wanalialia. Huu ni wakati wa kutambua kuwa inawezekana kupata haki yako iwapo utasimama kidete kuitetea kwa sababu sheria zipo.”

Akisisitiza, AY ambaye pia ni nyota katika muziki wa rap aliyeimba R&B akishirikiana na Diamond katika siku za karibuni, alisema huo ni mwanzo wa wasanii kufunguka masikio na kutambua haki zao.

Alisema wasanii wamekuwa wakilalamika juu ya haki za kazi zao, lakini hawachukui hatua.

“Wakati ni sasa, muziki ni kazi kama kazi nyingine na ni ajira pia, hivyo unastahili kuheshimiwa,” alisema AY
Viewing all 104712 articles
Browse latest View live




Latest Images