Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

Frederick Sumaye ( Waziri Mkuu Mstaafu ) Ateuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu Ya CHADEMA

$
0
0
Waziri Mkuu Mstaafu,Fredrick Sumaye ameteuliwa kuwa mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Mwenyekiti wa Chadema – Taifa Freeman Mbowe,amekiambia Kikao cha Kamati Kuu jana kuwa, anampendekeza Sumaye kuwa mjumbe wa CC kwa lengo la kuimarisha chama hicho.

Amesema, dhamira ya Chadema ni kujiimarisha kwa ajili ya uchaguzi ujao, kwa kutumia kila mwanachama kufanya kazi ya uenezi.

Kamati Kuu imeridhia uteuzi wa Sumaye kuwa mjumbe wa Kamati Kuu.

Naye Sumaye amemshukuru Mbowe kwa kumteuwa kushika nafasi hiyo na kuahidi kukitumikia chama hicho kwa nguvu zake zote.

Gigy Money: Siwezi Kumtaja Mchumba Wangu, Nitakosa Wengine

$
0
0
Gigy Money amethibitisha kuwa bado anataka wachumba wengine japo ana mpenzi.

Gigy ni mmoja kati ya watu walio tayari kujilipua mitandaoni kwa tukio lolote bila kujali.

Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo, kinachoruka kupitia EA Radio, Gigy amesema, “mimi nataka wachumba wengine nikimtaja yeye sasa wachumba wengine si wataniogopa!”

“Mwanaume wangu ni mbongo na anafikiri sana, ni mtu mkubwa sana. Kuna wavulana wazuri wewe Dullah usinitanie wewe. Mchumba wangu ni handsome lakini ana elimu sana, mpaka muda mwingine hadi kulala mnatumia elimu. Halafu mimi maisha yangu siyo elimu sana ujanja mwingi,” ameongeza.

Yanga Wagawa Basi..Sasa Wao ni Ndege tu

$
0
0
KLABU ya Yanga imepanga kufanya mabadiliko ya kulitumia basi lao ambalo walipewa na wadhamini wao Kampuni ya Bia (TBL) ambapo litakuwa maalum kwa mashabiki wao badala ya kutumiwa na wachezaji wao.

Hayo yamesemwa na Ofisa Habari wa Yanga, Jerry Muro alipokuwa kwenye uzinduzi wa Tawi la Yanga Uswazi Mbeya eneo la Sokomatola juzi Jumatano wakati Yanga ilipokuwa jijini hapa kucheza na Mbeya City katika mechi ya Ligi Kuu Bara.

Muro amesema uamuzi huo wameufikiria kwa kuwa wamekuwa wakitumia zaidi usafiri wa ndege ambao umezaa jina la wao kuitwa wa kimataifa pamoja na kushiriki michuano ya nje.

“Sisi ni watu wa angani tu muda wote, hivyo hata basi letu tumepanga kuwapa mashabiki walitumie kwa ajili ya kusafiri kuifuata timu kuipa sapoti, wale ndugu zetu wao ndiyo wa kutumia basi.
“Kwa mfano sisi tumeingia hapa asubuhi, tumetoka Dar saa 12 asubuhi, saa moja tumetua hapa, ila watani waliondoka Dar, jana asubuhi hadi leo (juzi) hawajafika Songea,” alisema Muro huku akishangiliwa na mashabiki wa Yanga waliokuwa eneo hilo.

“Msimu ujao pia tutashiriki katika michuano ya kimataifa, hivyo muda mwingi tutakuwa na safari za nje kama ilivyo msimu huu, hivyo hili basi letu litakuwa linatumika kuwafuata mashabiki na kuwapeleka mkoa mwingine pindi sisi tutakapokuwa tunasafiri kwa ndege,” aliongeza Muro.
Alisema kuwa ikiwa uamuzi huo utapitishwa, basi wao watakuwa wanasafiri kwa ndege tu hata katika safari za ndani na basi lao litakuwa linatumiwa na wachezaji katika safari za ndani ya Dar tu.

Rais Magufuli Afanya Ziara ya Kushtukiza Uwanja wa Ndege..Akuta Madudu ya Hatari..Aagiza Hatua Kuchukuliwa

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameiagiza Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi kwa kushirikiana na vyombo vya dola kuchukua hatua mara moja dhidi ya dosari za ukaguzi zilizopo katika kitengo cha ukaguzi wa mizigo na abiria katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (Terminol One) Jijini Dares salaam.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo tarehe 13 Mei, 2016 alipofanya ziara ya kushtukiza katika uwanja huo na kubaini kuwa mashine za ukaguzi za sehemu ya kuwasili abiria na mizigo hazifanyi kazi kwa muda mrefu.

Maafisa wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere waliokuwa wakitoa maelezo juu ya hali ya kitengo cha ukaguzi wa mizigo na abiria katika uwanja huo, walikuwa wakitoa taarifa zinazo tofautiana kuhusu utendaji kazi wa mashine za ukaguzi, hali iliyosababisha Dkt. Magufuli kuamua kuiagiza wizara husika kwa kushirikiana na vyombo vya dola kuchukua hatua mara moja. 'Unajua mimi sipendi kudanganywa, ni vizuri uzungumze ukweli tu, kwa nini nimeanzia hapa huwezi ukajiuliza? eeeh sipendi kudanganywa, ukinidanganya nitachukia sasa, wewe umenidanganya kwamba hiyo ndio mbovu na hii ndio nzima, nikawaambia muiwashe hiyo nzima, akaja huyu mwenzako amezungumza ukweli kabisa, akasema hii ni mbovu kwa miezi miwili. Dkt. Magufuli aliwahoji Maafisa wa uwanja wa ndege. 'Kwa hiyo mizigo inayoingia humu huwa hamuikagui kwa namna yoyote ile, kwa hiyo mtu akiamua kuja na madawa yake ya kulevya, nikija na dhahabu zangu, na almasi zangu na meno ya Tembo kwa kutumia ndege ndogondogo napita tu' Rais Magufuli aliendelea kuwabana maafisa hao wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli amefanya ziara hii ya kushtukiza mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere akitokea Jijini Kampala nchini Uganda ambako jana alihudhuria sherehe ya kuapishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni.

Mwanamume 'Adandia' Helikopta Kenya

$
0
0
Mwanamume mmoja katika mji wa Bungoma, Magharibi mwa Kenya ameshangaza wengi baada ya kudandia helikopta ambayo imepaa na kuondoka naye.

Helikopta hiyo ilikuwa imesafirisha mwili wa mfanyabiashara mashuhuri Jacob Juma aliyeuawa kwa kupigwa risasi jijini Nairobi wiki iliyopita, vyombo vya habari nchini Kenya vinasema.
Video zinazosambaa mtandaoni zinaonesha helikopta hiyo ikipaa juu angani kutoka uwanja wa Posta, mwanamume huyo akiwa amejishikilia kwenye vyuma vya helikopta hiyo.

Taarifa zinasema baadaye ndege imetua kwa dharura katika uwanja wa ndege wa Bungoma na mwanamume huyo akapelekwa hospitalini.

Wengi wameeleza kushangazwa kwao na wengine wanalifanyia mzaha.
Baadhi wanasema mwanamume huyo alisahau leo ilikuwa Ijumaa tarehe 13, ambayo kwa baadhi ni siku yenye kutokea mabaya.

Kenya: Watoto Waliwa na Funza Baba Kudai ni Dhambi Kuua Kiumbe chochote

$
0
0

WAUMINI wa Kanisa la Holy Ghost Tebernacle katika Kaunti ya Murang’a Alhamisi walimvamia mshirika mwenzao waliyemshitumu kwa kuwatesa watoto wake na uvamizi wa funza kwa 'kukataa' kuwatafutia huduma za kimatibabu.

Washirika hao kutoka eneo la Kiamaihwa katika Kaunti ndogo ya Kigumo walidai kuwa muumini huyo wa kiume alikuwa akitii itikadi kali ambazo hupinga mauaji ya kiumbe chochote kilicho hai, wakiitaja kama “iliyopitwa na wakati”.

Pasta Joseph Mwaura wa Kanisa hilo aliambia Swahilihub kwa njia ya simu kuwa “watoto wawili wa muumini huyo wake walikuwa wamevamiwa na funza kila sehemu ya mwili na wakitembea ungedhani walikuwa wakicheza mchezo wa kuigiza uliohitaji wahusika kutembea kana kwamba wanacheza densi na kujikunakuna!”
“Baada ya kupata habari hizo, waumini wenzangu wakiwa zaidi ya 100 walimvamia muumini huyo alipowakataza kutekeleza uokoaji huo wa watoto wake na kisha wakamwamurisha awatoe watoto hao nje watolewe funza,” akasema.

Alisema kuwa watoto hao wote wakiwa ni wa kiume wa kati ya miaka 10 na 13 walikuwa wamevamiwa na wadudu hao na ikabainika kuwa hata hawakuwa wakienda shule.

“Waumini hao walikataa katakata kumsikiza baba watoto hao akisema kuwa walikuwa wakimtakia laana kutoka kwa Maulana ikiwa angewakubalia waue funza hao!"
Aliongeza kuwa aliteta vikali kuwa imani yake haingemruhusu kuua kiumbe yeyote aliyeumbwa na Mungu, akiongeza kuwa funza hao walikuwa wametumwa kukaa katika 'hekalu' - yaani miili ya wanawe.

Funza kutumwa
“Alituambia kuwa wadudu hao wametumwa ndani ya miili ya watoto wake na hakuna vile angeweza kupingana na tukio la kiroho. Alishikilia kuwa Mungu angewaamrisha watoke kutoka miili ya wanake atakapoamua kufanya hivyo,” akasema Pasta Mwaura.

Baba huyo alidaiwa kubishana kuwa imani ya waumini hao waliomvamia kwake ilifaa kuwa ya kulisha watu kiroho wala sio kutibu magonjwa au kutekeleza uokoaji wa watu kutoka na ukarimu wao kwa viumbe wa Mungu.

“Alitulaumu kwa kupotosha waumini kuwa madawa ya kizungu ni suluhu kwa magonjwa, akiyataja kama uchawi wa Kizungu!,” akateta Pasta Mwaura.

Aidha, bwana huyo alisisitiza kuwa hakuna mahali ndani ya Biblia ambapo Yesu alionekana akitafuta matibabu hospitalini.

Hata hivyo, ubishi wake haukumfaa kwa lolote kwa kuwa waumini hao walifanikiwa kuwaokoa watoto hao ambapo waliwatoa funza hao na hatimaye wakapakwa dawa ya kutibu vidonda.

“Aidha, waokoaji hao waliwapeleka watoto hao hadi hospitalini kwa matibabu zaidi ambapo walipewa dawa zaidi ya kupulizia nyumba yao
ili kuuwa wadudu wanaosababisha uvamizi wa funza,” akasema pasta Mwaura.

Alisema kuwa kuanzia Jumatatu ijayo watoto hao watasajiliwa shuleni na ambapo wamemuomba chifu wa eneo hilo kumwandama baba huyo ili atimize hilo.

“Wakati umefika kwa waumini wa Kikristo kutupilia mbali itikadi ambazo zimewasababishia ujinga, magonjwa na umasikini,” akasema.



ULIMWENGU WA PILI BADO UNASUMBULIWA NA FUNZA KWELI!!!

ONLY IN KENYA

Busu la Wema Kwenye Filamu Lamgusa Idris..Kaandika hivi Kuhusu Kuigiza Scene Kama Hizo.

$
0
0
Idris Sultan ambaye kwa sasa anatajwa kuwa ndio mshkaji anaye mmiliki Wema Sepetu ameumizwa na jinsi Wema alivyo kiss kwenye filamu ambayo mpaka sasa haijulikani itatoka lini na itaitwaje.

Hii ilikuwa post ya Idris Snapchat.

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeto ya Leo Jumamosi ya May 14, Ikiwemo ya Magufuli Ataja Mali zake

$
0
0

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeto ya Leo Jumamosi ya May 14, Ikiwemo ya Magufuli Ataja Mali zake

Kibao Chamgeukia NAPE Nhauye Bungeni...Awekwa Kikaangoni na Wabunge..Aitwa Waziri Mzigo

$
0
0
Wabunge wamemcharukia Waziri wa Habari, Nape Nnauye kwamba aliwahi kuwaita mawaziri wa Serikali iliyopita mizigo, lakini yeye amezuia matangazo ya moja kwa moja ya Bunge, ili wananchi washindwe kumpima kama ni mzigo au lumbesa.

Hayo yalijitokeza jana wakati wabunge walipochangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Habari kwa mwaka 2016/2017, iliyowasilishwa bungeni na Waziri Nape.

Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara (Chadema) alieleza kushangazwa na hatua ya Serikali ya Awamu ya Tano kuhimiza wananchi kudai risiti wanaponunua bidhaa, lakini haitaki wananchi waone inavyopanga matumizi yake.

Alisema Nape akiwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, aliwaita baadhi ya mawaziri ni mizigo, lakini amepewa wizara hiyo amezuia mijadala ya wazi ambayo ingesaidia wananchi kumpima.

“Nilipoona amepewa wizara ya habari nikajua ataruhusu mijadala ya wazi ili tumuone yeye kuwa hatakuwa mzigo, lakini yeye akawa lumbesa. Hilo amelizuia kwa hiyo tunashindwa kumpima,” alisema.

Alisema waziri huyo hawezi kukwepa lawama ya hicho kinachoendelea cha kuzuia matangazo ya Bunge, kwa vile wanaopiga picha na kuhariri taarifa zinazorushwa ni watumishi wa TBC.

Udhibiti wa Bunge
Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (Act-Wazalendo), alisema kuwa wabunge wote waliopinga Bunge kutoonyeshwa ‘live’ na kusababisha mtafaruku bungeni, wameitwa kuhojiwa na Kamati ya Maadili ya Bunge.

“Wabunge hapa tulisimama tukapinga na wapo waliounga mkono, lakini kiti chako kimetuita wabunge wote tuliopinga kauli ya Serikali kwenye kamati ya maadili. Jana mimi nimepata barua,” alisema Zitto.

“Kwamba mnatubana kusema. Mnazuia Bunge lisionekane. Hata kutoa maoni ndani ya Bunge tunakwenda kuhojiwa? TBC ni chombo cha umma, siyo chombo cha Serikali, inaendeshwa kwa kodi za wananchi,” alisisitiza.

Baada ya mchango huo, Naibu Spika, Dk Tulia Ackson alisema si kweli wabunge hao wanahojiwa kutokana na michango yao, bali wanahojiwa kutokana na mambo waliyoyafanya kwa kutotii maagizo ya kiti wakati wa mjadala wa ‘Bunge Live’.

Kwa upande wake, Mbunge wa Chemba, Juma Nkamia (CCM), aliunga mkono hoja ya Zitto ya kuifanya TBC iendeshwe kama inavyoendeshwa BBC kwa kupewa  leseni maalumu.

Pia, aliitaka Serikali kupeleka muswada bungeni utakaowabana wamiliki wa vyombo vya habari kuwa na mikataba na waandishi wanaowaandikia, pia, akadai baadhi ya vyombo haviwalipi waandishi wake.

Hata hivyo Mbunge wa Viti Maalumu, Agness Marwa (CCM) alitetea uamuzi wa Serikali kuondoa matangazo ya moja kwa moja ya Bunge, akisema wabunge wanaodai hilo ni wale waliokuwa wakiuza sura.

Katika hatua nyingine, Waitara alisema kitendo cha Nape kuwaalika wabunge kwenye muziki, baada ya bajeti yake kupita ilikuwa ni kuwahonga.

Juzi jioni wakati akitoa matangazo kabla ya kuahirisha Bunge, Naibu Spika alisema baada ya kupitisha bajeti ya Wizara ya Habari, wanamuziki Diamond Plutnum na King Kiki watatumbuiza katika viwanja vya Bunge.

“Mnaposema mnabana matumizi hao wanamuziki wameletwa kwa gharama za nani,” alihoji mbunge huyo.

 “Wabunge wote ambao wataenda katika hiyo miziki ili kuunga mkono habari ya Nape mtakuwa mmekula rushwa,” alisisitiza Waitara, kauli ambayo ilimfanya Naibu Spika, Dk Tulia kufafanua, akisema suala hilo lilitangazwa bungeni kama mengine, lisiingizwe kosa la jina la rushwa.

Upinzani na udikteta
Msemaji mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Joseph Mbilinyi, alisema kitendo cha Serikali kuminya uhuru wa habari ni kuelekea kwenye udikteta.

 “Kana kwamba haitoshi, Serikali sasa imezuia Televisheni ya Umma, inayoendeshwa na kodi ya wananchi (TBC1) kurusha matangazo ya moja kwa moja ya mijadala inayofanyika bungeni. Dalili hizi siyo njema kwa ukuaji wa demokrasia na uhuru wa habari hapa nchini na zinatoa taswira ya utawala wa ki-dikteta,” alisisitiza.

“Tunaitaka Serikali kuliomba radhi Bunge hili, kwa kosa la kuminya uhuru wa habari kinyume na Katiba na kuviacha vyombo vya habari hususan vya umma kufanya kazi zao za kuhabarisha umma kwa uhuru,” alisema.

Maamuzi Mapya ya Chelsea Juu ya Nahodha Wake John Terry

$
0
0
Klabu ya soka ya Chelsea leo May 13 2016 imeamua kutangaza maamuzi ambayo yalikuwa hayatarajiwi na wengi, kuhusu nahodha wake na beki wake wa kati John Terry ambaye ameichezea klabu hiyo kwa zaidi ya miaka 15, klabu leo imeamua kumpa nafasi ya kuongeza mkataba wa mwaka mmoja wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo.

John Terry mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu huu, lakini mwezi January aliweka wazi kuwa ataondoka Chelsea kwa maana hatoongeza mkataba tena, lakini taarifa zilizotoka leo May 13 2016, ni kuwa klabu na mchezaji huyo wamekubaliana kuongeza mkataba wa mwaka mmoja.

Terry akiwa ndani ya klabu ya Chelsea toka mwaka 1998, amefanikiwa kucheza jumla ya mechi 703, mwaka 2005 John Terry alijumuisha katika kikosi bora cha dunia kilitangazwa na Shirikisho la soka duniani FIFA (FIFAPro World XI).

Second Skin: Wanasayansi waja na Ngozi ya Bandia, Kuficha Uzee na Makovu!

$
0
0
Je unazeeka na ngozi yako ya uso au mikono inaonesha uzee huo? Wanasayansi waja na ngozi ya bandia inayoweza wekwa juu ya ngozi ya kawaida na kuonekana kama halisi, na huku ikiwa haiathiriwi na kulowa n.k.

Kundi la wanasayansi kutoka chuo cha Harvard na M.O.T huko Marekani ndio walioweza kufanya jambo hili ambalo kwa wengi linaonekana kama vile limetoka kwenye filamu kuwa jambo la halisi, linalowezekana

Hadi sasa watu 170 wamefanyiwa majaribio ya kujibandika ngozi bandia hii iliyopewa jina la ‘second skin’, yaani ngozi ya pili.

Pia katika majaribio hayo imegundulika hakuna waliogundulika kupata madhara yeyote yale ya ngozi, hili likionesha ya kwamba malighafi (material) waliyotumia hayana madhara kwa ngozi za watu hao.

Wanasema kemikali zinazotumika kutengenezea ngozi bandia hiyo ni zile zinazokubaliwa ya kwamba ni salama zilizopitishwa na Bodi ya Chakula na Madawa ya Marekani.

Ngozi hii bandia ni ‘transparent’, na hivyo ni vigumu kugundulika kama mtu ameweka kitu chochote juu ya ngozi yake. Inaweza valiwa siku nzima bila kusababisha muwasho wowote na inaweza kuhimili jasho na mvua. Utaweza nawa n.k bila kuathiri chochote, haitotoka.


Muonekano wa Second Skin – ‘ngozi bandia’, pale inapokuwa inatolewa

Inasemekana matajiri wengi ambao uzeeka uchagua kufanya oparesheni za kuweka nyuso zao vizuri. Kuvuta na kupunguza ngozi ili kuzipa nyuso muonekano wa ujana. Njia hii isiyohusisha oparesheni inaonekana inaweza ikawa ndio njia bora na rahisi zaidi kufanyika.

 Inasemekana matibabu ya magonjwa kama vile Eczema na Psoriasis yatanufaika na teknolojia hii

Matumizi mengine yanayoonekana yatawezekana ni pamoja na kutumia ngozi hii bandia kushikilia dawa iliyopakwa katika sehemu ya ngozi.

Yaani dawa itapakwa kwenye eneo la ngozi na kisha ngozi bandia kuwekwa juu yake.

Inawekwaje?
 Itakuwa kwenye mfumo wa ‘cream’, yaani kama mafuta ya ngozi. Kuna mchanganyiko wa mafuto hayo, utapaka ya kwanza kisha kupaka nyingine juu yake…baada ya kukaa kwenye ngozi tuu itabadilika na kuwa ngozi ya bandia.

Lipumba Amvaa Rais Magufuli.....Asema Vitisho Vitaangamiza Uchumi wa Taifa, Ampigia Hesabu za Kiuchumi Duniani Kuhusu Sukari

$
0
0
Aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba ameeleza kuchoshwa na utendaji wa Rais John Magufuli katika kukabiliana na changamoto za kiuchumi.

Prof. Lipumba alitoa kauli hiyo jana  mbele ya waandishi wa habari  katika Ofisi Kuu ya CUF iliyopo Buguruni, Dar es Salaam.

Katika kukabiliana na changamoto za nchi hususani sekta ya uchumi, Prof. Lipumba amemshauri Rais Magufuli kutafuta ushauri sambamba na taratibu za kujenga uchumi wa soko shirikishi kutoka kwa Benjamin Mkapa, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu.

Alisema, uzoefu wa Rais Mkapa wa kujenga utawala wa serikali unaweza kumsaidia kufanya uamuzi sahihi utakayosaidia wananchi badala ya kukagandamiza.

Mchumi huyo alieleza kuwa, vitisho na ubabe wa Rais Magufuli vinaweza kuwaogopesha watendaji wake wakiwemo mawaziri na hivyo kushindwa kumueleza hali halisi na kwamba, kitendo hicho kinaweza kuathiri maendeleo ya nchi.

“Kuna dalili kwa baadhi ya watendaji wa serikali hasa mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya za kushindwa kutoa fikra zao zenye lengo la kuimarisha uchumi wa nchi au kueleza hali halisi iliyopo kwa kuhofia vitisho vya rais ili wasitumbuliwe,” amesema.

Prof. Lipumba ametoa kauli hiyo wakati nchi ikiwa kwenye sintofahamu ya upatikanaji wa sukari ambapo kwa mujibu wake (Lipumba), uhaba huo umesababishwa na agizo la rais la kuzuia uingizwaji wa bidhaa hiyo kutoka nje ya nchi.

“Agizo alilolitoa Rais Magufuli Februari 28, 2016 wakati akiwashukuru waandishi wa habari, wasanii na makundi yaliyoshiriki kwenye kampeni zake za uchaguzi 2015 ndilo lililosababisha haya,” alisema na kuongeza;

“Kauli ya serikali ya kuzuia utolewaji wa vibali vya uingizwa wa sukari kutoka nje ndiyo iliyosababisha upungufu wa sukari, asiuaminishe umma kuwa sababu ni wafanyabiashara kuficha sukari.

“Kwa mwenendo huu nchi haitaendelea kutokana na kwamba badala ya vyombo vya dola kushughulikia masuala ya msingi ili kuleta tija katika maendeleo ya Taifa, vinahaha kutafuta sukari zilizofichwa.”

Alitoa mfano wa kitendo cha Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) cha kutafuta wafanyabiashara wanaoficha sukari badala ya kushughulika na masuala nyeti ya ubadhilifu wa mali za umaa kama Tegeta Escrow.

“Wafanyabiashara wanaopata kibali na wanaopitisha sukari kwa magendo wanapata faida kubwa kwa sababu bei ya sukari katika soko la dunia mwezi Agosti 2015 ilikuwa Dola za Marekani 250 kwa tani moja,” amesema.

Alifafanua kuwa, kama dola moja ni sawa na Sh. 2000 tani moja ya sukari iliuzwa Sh. 500,000 sawa na Sh. 500 kwa kilo moja na kwamba, ukiongeza na gharama za usafiri kila kilo moja ya sukari itafika kwa Sh. 600.

“Wafanyabiashara wakubwa na wa kati wanaoingiza sukari nchini hupata faida kubwa ukilinganisha na viwanda vya ndani kutokana na kwamba, uzalishaji sukari viwandani unagharimu mtaji mkubwa na kupelekea bei kuwa kubwa na kusababisha kupoteza soko,” alisema.

Alishauri kuwa, kama serikali ina lengo la kulinda viwanda vya ndani ihakikishe inaanda mfumo wa mnada wa ugawaji wa leseni ili kutoa fursa kwa wafanyabiashara na viwanda kupata leseni za kuingiza sukari inayotoka nje ili viwanda vipate masilahi pamoja na wafanyabiashara.

“Ingawa utolewaji wa vibali utaathiri viwanda vya ndani kutokana na kushindwa kushindana na wafanyabiashara, ni vema serikali ikatoa vibali kwa watu wote,” alisema.

Kama serikali inataka kujenga uchumi wa viwanda haina budi kutoa motisha kwa wawekezaji ili wavutiwe kuwekeza katika sekta zote nchini.

“Rais anahitaji aelewe uchumi wa soko shirikishi, awape nafasi wahusika, asifanye maamuzi kwenye mikutano ya siasa au hadhara,” alisema.

Ibrahimovic Kuondoka PSG Mwishoni Mwa Msimu Huu

$
0
0
Mshambuliaji wa klabu ya Paris St-Germain Zlatan Ibrahimovic anaondoka katika klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu.

Mkataba wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 unakamilika msimu huu na amehusishwa na uhamisho wa Manchester United,kilabu ya Los Angels Galaxy na AC Milan.

”Ninafurahia”,alisema.”Niliwasili kama mfalme na sasa naondoka kama kigogo lakini ntarudi”.

PSG imesema kuwa Ibrahimovic anaondoka kama mshambuliaji bora na mchezaji bora zaidi katika historia ya kilabu hiyo.

Ibrahimovic ameifungia mabao mengi zaidi klabu hiyo licha ya kujiunga nayo mwaka 2012 aiwa amefunga mabao 152 katika mechi 178.

PSG imeshinda taji la Ligue 1 kila msimu tangu Ibrahimovic ajiunge na kilabu hiyo

Mbio za Mwenge: Kudorora Kwa Ukimbizwaji Kipi Kifanyike ?

$
0
0
Nimezoea kuona mbio za mwenge ambazo zimesheheni shamra shamra, vifijo, sanaa na ujumbe kufikishwa kwa wananchi katika uzito unaostahili.

Mbio za Mwenge za safari hii zimengia Zanzibar kimya kimya na uwepo kwa mbio hizo umepoteza haiba, na hamu hata huwezi kuufuatilia.

Mara ya kwanza kusikia habari zake kuwa umeingia Visiwani ni kupitia ZBCTV wakati Kiongozi wa mbio hizo Nd. George Watson alipotoa misaada ya "vitanda vya kamba ( Mayowe)" maarufu vya kukoshea maiti, kwa Wizara ya Afya, Pemba, kwa ajili ya wagonjwa!

Mbio hizo za Mwenge sasa ziko Unguja ambazo pia zimekosa mvuto na umaarufu na kugeuka kuwa mbio za wanasiasa na askari wateule wachache wa FFU.

Msafara wa jeneza (msiba)unaonekana kukusanya watu wengi kuliko ushiriki wa watu kwenye mbio za Mwenge ( furaha).Kulikoni? Tujiulize, Bado una tija, kuhitajika na thamani kwa wananchi? Kipi kifanyike kurudisha ari, mshawasha wa kuupokea na kuuengaenga kama zamani. Au hili linatokea visiwani tu kwenye watu waliokwisha kata tamaa?

Lady Jay Dee Sasa Kuitafuta Haki yake Kwa Njia ya Mahakama..Amtaka Gadner Kuomba Msamaha Mbele ya Umma

$
0
0
Lady Jay Dee Sasa Kuitafuta Haki yake Kwa Njia ya Mahakama..Amtaka Gadner Kuomba Msamaha Mbele ya Umma la sivyo hatua za kumpeleka Mahakani zitaendelea, Soma Hii Hapa Chini:


Serikali Yasalimu Amri..Yaipa NIDA Sh Bilion 2.3 Kulipa Watumishi 597 Waliosimamishwa Kazi

$
0
0

Serikali imeipa Shilingi Bilioni 2.3 Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA), kwa ajili ya kuwalipa watumishi 597 waliosimamishwa kazi.

Malipo hayo yanahusisha mishahara yao ya miezi minne, ukiwemo mshahara wa mwezi mmoja wa notisi ya kusimamishwa kazi, pamoja na malimbikizo ya madeni yao katika mifuko ya hifadhi ya jamii.

Ahukumiwa Kifungo cha Miaka 30 Jela Kwa Kumuoa Bunti Yake wa Kumzaa

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma, jana ilimhukumu kifungo cha miaka 30, Godfrey Mjelwa (48), baada ya kupatikana na hatia ya kuishi kinyumba na binti yake wa kumzaa.

Hakimu Mkazi katika mahakama hiyo, Mwajuma Lukindo alisema ushahidi wa pande zote ulithibitisha kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo la kuishi chumba kimoja na binti yake, kama mke na mume.

Kwa mujibu wa ushahidi uliotolewa, Mjelwa aliamua binti yake mwenye umri wa miaka 15 (jina limehifadhiwa) kuwa mke na kuishi naye katika Mtaa wa Kizota Manispaa ya Dodoma.

Hakimu Lukindo alisema kosa alilokutwa nalo mtuhumiwa ni ‘maharimu’ (kufanya mapenzi na ndugu za damu), licha ya kuwa mtoto huyo bado alikuwa mdogo, lakini ni mtoto wake wa kumzaa.

Mwendesha mashtaka Janeth Mgome, aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mtuhumiwa, ili liwe fundisho kwa wengine ambao wana tabia ya aina hiyo.

Utetezi wa mtuhumiwa huyo uliwavunja mbavu watu waliokuwapo mahakamani hapo, kwani alitaka kupunguziwa adhabu kwa kuwa mtoto wake ana miaka 14 na miezi tisa na siku tisa, siyo miaka 15 kama ilivyodaiwa mahakamani hapo

Jamal Lyon Hatoondoka Kwenye Empire Kama ilivyoripotiwa, Hii ni Sababu

$
0
0
Wiki hii mashabiki wa tamthilia ya Empire walisikitishwa na tweet ya Jussie Smollett anayejulikana kama Jamal Lyon kwenye tamthilia hiyo kuwa atajiondoa.

“I’ve thoroughly enjoyed my time w/ @EmpireFOX. I love you all. Truth. Time 2 make a record & some movies. #Empire,” alitweet muigizaji huyo.

Hata hivyo ripoti zimedai kuwa Smollett haondoki kwenye show hiyo kwasababu bado yupo kwenye mkataba. Tweet hiyo ilikuja baada ya episode mpya ya series hiyo kuonesha Smollett akipigwa risasi na kupelewa hospitali.

Tetesi zinadai kuwa muigizaji huyo anaondoka kwasababu ombi lake la kuongezewa malipo limepuuzwa na FOX.

Sipendi Kuzungumzia Mahusiano yangu Kwenye Radio – Nuh Mziwanda

$
0
0
Msanii Nuh Mziwanda ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wa “Jike Shupa” amesema kwa sasa hapendi kuongelea mahusiano yake kwenye radio maAna inafanya watu wanasahu muziki wake na kuanza kufuatilia mahusiano yake.

Alisema hayo alipo kuwa kwenye kipindi cha Ala Za Roho cha Clouds Fm alipoulizwa kuhusu kumfumania Shilole na Madee hotelini walipofikia wakati wa show ya Nuh Mziwanda. Amekataa kuzungumzia suala hilo na wala hakuthibitisha kuwa aliwafumania kweli japo anasema jambo hilo lilimumiza sana.

Marais Duniani Wavutiwa na Vita ya Ufisadi Tanzania

$
0
0
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema viongozi wakuu wa nchi na washiriki wa Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Rushwa, wamevutiwa na jitihada ambazo Tanzania imezichukua kukabiliana na janga hilo.

Alitoa kauli hiyo jana wakati akitoa ufafanuzi kuhusu ushiriki wake kwenye mkutano wa siku moja wa wakuu wa nchi, ulioitishwakujadili suala la kupambana na rushwa duniani uliofanyika Lancaster House, jijini London, Uingereza.

Waziri Mkuu alisema katika kikao cha kwanza, kilichohudhuriwa na wakuu wa nchi na viongozi wa kitaifa wapatao 20, alipata fursa ya kuelezea jinsi Tanzania ilivyoweza kupambana na rushwa kwa kuzingatia vigezo vikuu vinne.

Waziri Mkuu alivitaja vigezo hivyo kuwa ni kufanya marekebisho ya baadhi ya sheria zinazohusu masuala ya rushwa; uanzishwaji wa mahakama maalum ya mafisadi ambayo inatarajiwa kuanza kazi Julai, mwaka huu; mikakati ya udhibiti wa fedha za miradi ya wananchi na utaratibu wa kubaini wala rushwa kwa kushirikisha jamii ikiwemo kutunza siri za watoa taarifa.

“Ziko sheria ambazo zinafanyiwa kazi hivi sasa ambazo ni lazima zipitishwe na Baraza la Mawaziri kabla mahakama hii haijaanzishwa, zikishapitishwa na Baraza ndipo zitaanza kutumika,” alisema.

Akifafanua kuhusu mikakati ya udhibiti wa fedha za miradi ya maendeleo, Waziri Mkuu alisema kwamba katika bajeti ya mwaka huu, Serikali imeongeza kiasi cha fedha zilizotengwa kwa shughuli za maendeleo kutoka asilimia 27 hadi kufikia asilimia 40.

Waziri Mkuu alisema alipata fursa ya kukutana na Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron ambaye mbali na kupongeza juhudi za Serikali ya Rais John Magufuli katika kupambana na rushwa, pia aliahidi kutoa mwaliko ili Tanzania iweze kushiriki kwenye mkutano mwingine wa masuala ya rushwa utakaofanyika Japan, Julai mwaka huu.

Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images