Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104416 articles
Browse latest View live

Vijana Wanaovaa Suruali Chini ya Kiuno Kuchapwa Viboko 70

0
0

Wakazi wa Kata ya Karansi, Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro wametoa uamuzi kuwa wanawake watakaovaa sketi fupi na vijana watakaovalia suruali chini ya kiuno, wataadhibiwa kwa kuchapwa viboko 60 hadi 70.

 

Uamuzi huo umefikiwa na wakazi zaidi ya 200 wakisema uvaaji huo ni kinyume na mila na desturi za Kiafrika.
 

Vazi lingine lisilotakiwa kwa wanawake ni kuvaa suruali pamoja na vijana kunyoa ndevu mitindo isiyofaa.
 

Mkutano huo ulioandaliwa na wazee wa kimila jamii ya Meru (Wachili) na Wamasai (Malaigwani), uliwavutia wananchi wengi ambao walihudhuria.
 

Sambamba na uamuzi huo utakaokuwa unafanyika hadharani, pia adhabu hiyo itawahusu wezi wa mali na wanaopenda kucheza pool table wakati wa kazi.
 

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Wilbrod Mutafungwa alipinga uamuzi huo akisema kwa maazimio hayo ya kuwaadhibu watuhumiwa kwa kuwachapa viboko ni kujichukulia sheria mkononi na ni kinyume na sheria.

Kwanini Nyimbo za Alikiba Huvuja Kabla ya Muda?

0
0
Imekuwa kawaida sana Ali kiba Kabla ya kutoa nyimbo zake huvuja mapema,Amepanga kuitoa Nyimbo yake mpya ya Aje kesho pamoja na video yake ikiianzia Mtv lakini bahati mbaya nyimbo tayari watu tunayo mda mrefu hata kabla ya kesho haijafika

Sasa najiuliza Lupela ilienda hivi na hii nayo ipo hivi hivi sijaelewa Alikiba ana matatizo Gani,katika Kutoa nyimbo zake kwanini zinatoka mapema kabla ya yeye ku relese na bahati mbaya huwa haizuii anaitoa kama ilivyo tatizo ni nini

Kwangu mimi bila unafiki Lupela ndo the Best kuliko hii nyimboo sijaona cha maana alicho kiimba yule alie shirikishwa zaidi ya kusema naweza kuimba kiswahili nakusema hicho kiswahili jamani Mziki ni kazi ngumu

Serikali Yanasa Kilo 34,000,000 za Sukari Mafichoni

0
0
Shehena ya sukari ya kilo milioni 34 zilizokuwa zimefichwa kwenye maghala ya wafanyabiashara watatu Kilimanjaro imekamatwa na vyombo vya usalama, na serikali mkoani humo imetangaza kuiuza kwa wananchi kuanzia jana kwa bei elekezi ya Sh. 1,800.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Mecki Sadiki alithibitisha jana kukamatwa kwa shehena hiyo, baada ya makachero wanaoongoza timu maalumu ya ukaguzi wa maghala ya wafanyabiashara na mawakala wa sukari kubaini kufichwa kwa bidhaa hiyo.

“Tumefanya ukaguzi katika maghala 45 na katika harakati hizo tumenasa kilo milioni 34 za sukari iliyokuwa imefichwa," alisema.

"Katika zoezi hilo kuna mfanyabiashara mmoja mkubwa, yeye alikutwa na tani 31.33 lakini alikuwa akiiuza, isipokuwa bado tumewapa kazi Mamlaka ya Mapato (TRA) ichunguze kama imehodhiwa isivyo halali,” alisema Sadiki.

Kiasi cha sukari iliyobakia, alisema Mkuu wa M koa huyo, kilikamatwa kwa wafanyabiashara wengine wawili, ambao walikuwa na tani nne kasoro, Moshi mjini na Marangu.

Kwa mujibu wa Mkuu huyo wa mkoa, shehena hiyo ya sukari hadi jana mchana ilikuwa ikishikiliwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya kukamilisha taratibu za kiuchunguzi na kwamba ametoa amri igawiwe kwa wananchi kwa bei elekezi iliyotangazwa na serikali.

Kuhusu upungufu wa sukari Kilimanjaro, Sadiki alisema "Sisi kama mkoa tumefanya mawasiliano na mawakala walioko Dar es salaam, ambao sukari yao ilikuwa inashikiliwa na vyombo vya usalama na wametuahidi kuukabili uhaba wa sukari uliopo hapa kwetu.

“Jana (juzi) niliwasiliana na Mmiliki wa Kampuni ya Zakaria Enterprises na amekubali kuwapa bidhaa hiyo mawakala ambao ni wadau wa Kiwanda cha Sukari cha TPC," alisema Sadiki.

"Kwa hiyo tunakwenda vizuri na tumejipanga kuhakikisha kwamba uhaba huo tunaupatia ufumbuzi wa kudumu.Ila ninawaomba wananchi wangu wawe wavumilivu kwa sasa.

"Mawakala wakubwa wa sukari wa Kilimanjaro na mikoa ya Kanda ya Kaskazini ni mfanyabiashara Vicent Laswai ambaye atapatiwa tani 600 za sukari kutoka Kampuni ya Zakaria, alisema Mkuu wa Mkoa huyo.

Aidha, Laswai atapokea tani 640 toka katika Kampuni ya Mohamed Enterprises, alisema.

Kampuni ya Zakaria pia imekubali kutoa tani 640 kwa Kampuni ya Marenga Investment, alisema Sadiki na kubainisha kuwa Mohamed Enterprises imemuahidi kuziba pengo la upungufu utakaojitokeza.

Tangu Rais Magufuli apige marufuku uingizaji sukari kutoka nje ya nchi Februari 17 mwaka huu, baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu wamekuwa wakificha bidha hiyo kama njia ya kuihadaa serikali kwamba kuna uhaba mkubwa.

Wakati akipiga marufuku, Magufuli alisema kama kutakuwa na uhitaji wa sukari kuingia nchini, vibali atavitoa yeye si mtu mwingine yeyote ili kuviwezesha viwanda vya ndani viendelee kuzalisha bidhaa hiyo, kuendelea kutoa ajira na kuinua kipato cha wakulima wa miwa.

Alisema inasikitisha kuona sukari ikiingizwa nchini kutoka nje wakati nchi ina viwanda vingi vya bidhaa hiyo na kusababisha Watanzania wengi kupoteza ajira kutokana na sukari wanayozalisha kukosa soko.

"Nakuagiza Waziri Mkuu, kuanzia leo, marufuku mtendaji yeyote wa Serikali kutoa kibali cha kuagiza na kuingiza sukari kutoka nje ya nchi...vibali vyote nitatoa mimi," alisema Rais Magufuli.

"Katika kampeni zangu mwaka 2015, nilisema Serikali yangu itakuwa ya viwanda hivyo lazima tuvithamini viwanda vya ndani na kulinda bidhaa zinazozalishwa."

Machangudoa Waja Juu Wataka Biashara yao Ita

0
0

Baadhi ya wanawake wanaojiuza katika mitaa ya Majengo B na Fisi, mjini Mpanda mkoani Katavi wameitaka Serikali kuandaa utaratibu wa kuwatambua ili nao waweze kulipa kodi na kuliingizia taifa pato kutokana na shughuli wanayofanya ya kuuza miili yao.


Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana usiku, baadhi yawanawake hao walisema wanafanya kazi kama zilivyo kazi nyingine kwani zinawaingizia kipato kizuri kinachowasaidia kutimiza mahitaji yao ya msingi hivyo kazi hiyo inapaswa kuheshimiwa na kutambuliwa na serikali.


Mmoja wa wanawake hao aliyejitambulisha kwa jina moja la Joyce, alisema ni wazi Serikali ikiandaa utaratibu mzuri wa kuwatambua itawafanya waweze kulipa kodi ambayo italiongezea pato taifa tofauti na ilivyo sasa ambapo wamekuwa hawalipi kodi kwa kuwa hawatambuliwi.


" Sisi kazi yetu ina kipato kizuri kutokana na makubaliano yanayofanyika kati na wateja wetu lakini Serikali haitaki kututambua hivyo sio rahisi hata kututaka tulipe kodi, nchi nyingine watu kama sisi tumetambuliwa na tunalipa kodi serikalini" alisema Rosemary Kazeze.


Aliongeza kwamba kipindi hiki ambacho Serikali inatafakari au haioni umuhimu wa wao kutolipa kodi, anawashauri kina dada poa wenzake kuacha tabia ya kukwepa kwenda Nyumba za kulala wageni zinazotambuliwa na Serikali kwani kufanya  hivyo kunaikosesha serikali mapato


Alisema kuwa siku za nyuma walikuwa wanafanya biashara hiyo katika madanguro kitendo ambacho polisi walikuwa wakiwasumbua kwa kuwakamata kutokana na misako ya mara kwa mara, lakini hivi sasa hawasumbuliwi kwani wamepanga vyumba katika gesti halali na wanalipia vyumba hivyo na mmiliki analipa kodi kwa msingi huo nao wanachangia pato la taifa.


“ Kaka yangu mwandishi tunashukuru sana hata wewe kutufikia, wanatudharau na kutunyanyasa sisi lakini wateja wetu wakubwa ni hao hao viongozi wa serikali na tasisi nyingine lakini wajue kufanya biashara ya ukahaba sio sababu ya kuto muunga mkono Rais wetu katika suala la mapato ya serikali”…alisema Mayasa Hussein

Waziri Mkuu Mh Majaliwa Amesema Serikali Kusaka Waliokula Fedha za Watumishi Hewa

0
0

Waziri mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imeamua kupambana na wala rushwa ili kiasi kidogo cha rasilmali kilicholengwa kiweze kuwafikia wananchi.

Ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Watanzania waishio Uingereza kwenye mkutano uliofanyika kwenye Ubalozi wa Tanzania jijini London, Uingereza.

“Jambo tuliloamua kuanza nalo ni kupambana na rushwa. Tumeamua kufanya hivyo ili kurudisha umoja na maelewano miongoni mwa Watanzania, tunataka tuibadili Tanzania ili iwe ni ya Watanzania wote… tumechoka kuambiwa sehemu fulani mradi umekamilika halafu ukienda kuangalia hukuti kitu na fedha ile haipo,” alisema huku akishangiliwa.

Akizungumzia zoezi la kusaka watumishi hewa, Waziri Mkuu alisema Serikali itawashughulikia wale wote waliohusika na zoezi hilo. “Wafanyakazi hewa wamefikia zaidi ya 10,000 na tumeokoa zaidi ya sh. bilioni 4.5 zilizokuwa zikipotea kila mwezi. Tukikamilisha zoezi la kusaka watumishi hewa, sasa tutataka kujua ni akina nani walikuwa wakipokea fedha hizo. 
Waliohusika tutashughulika nao,”  alisisitiza.

Alisema hivi sasa Serikali inalenga kuwa na watumishi ambao wanafanya kazi kwa uaminifu, uadilifu na uwajibikaji mahali pa kazi. “Hiki ndicho kipaumbele cha Serikali ya awamu ya tano na tena zoezi hili litakuwa endelevu”, alisema Waziri Mkuu.

Akizungumzia kuhusu ukuaji wa uchumi, Waziri Mkuu ambaye alikuwa London kuhudhuria mkutano uliojadili mapambano dhidi ya rushwa kwa niaba ya Rais Dk. John Pombe Magufuli, alisema lengo la Serikali hivi sasa ni kuona kuna ukuaji wa uchumi unaoenda sambamba na huduma zinazotolewa kwa wananchi.

Alisema viwanda vingi viliuzwa na watu waliovinunua wakageuza kuwa ni maghala ya kufugia wanyama. Sisi tunataka vifufuliwe ili teknolojia mpya na za kisasa zije Tanzania. Nafasi ya kuwekeza iko kwa Watanzania wote walioko nyumbani na ninyi mlioko nje,” alisema.

Alisema ardhi ipo ya kutosha na akawataka wawaalike marafiki zao waje kuwekeza nchini, ili mradi wawe ni watu makini, wenye nia ya dhati ya kuwekeza nchini na wenye mitaji na siyo madalali (middlemen). “Tunataka usindikaji wa mazao na bidhaa ufanyike nchini mwetu badala ya kupeleka mazao ghafi nje ya nchi, kwa njia hiyo tutakuwa pia tumezalisha ajira kwa watu wetu,” alisema.

“Kuna Watanzania wanaishi Botswana, Ujerumani na Poland wameshaleta wawekezaji nchini. Kwa mfano wa Poland wameleta mradi wa umeme katika vijiji vitani wilayani Ileje. Kwa hiyo ninyi endeleeni kuishi Uingereza lakini mhakikishe kuwa ukaaji wenu hapa, unaleta tija kule nyumbani. Kumbukeni Tanzania na muwe tayari kuihudumia Tanzania,” alisema.

“Serikali inaamini itanufaika na uwepo wenu hapa Uingereza. Muweke kipaumbele cha kuwekeza nyumbani na mkishindwa mtutafutie marafiki zenu. Mwenye uwezo andaa andiko la mradi halafu uwasiliane na Balozi ili akusaidie kutafuta wahusika kule nyumbani,” aliwaasa.

Akijibu swali kuwa ana maoni gani juu ya Bunge kutorushwa ‘LIVE’, Waziri Mkuu alisema hatua hiyo ilichukuliwa ili kuwawezesha watu kufanya kazi kama ambavyo kaulimbiu ya Mhe. Rais Magufuli ya Hapa Kazi Tu inavyosema.

“Bunge la Tanzania lilikuwa ni bunge pekee katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na duniani ambalo lilikuwa likirushwa LIVE kuanzia asubuhi hadi usiku. Ina maana katika kipindi cha Bunge la bajeti, ambalo linaendeshwa kila siku kwa miezi mitatu, Watanzania nao wangekuwa LIVE kwa miezi mitatu,” alisema.

“Tulilazimika kujifunza kutoka kwenye mabunge mengine. Hivi hapa Uingereza mnaangalia Bunge live kila siku?” alihoji Waziri Mkuu na kujibiwa kuwa linarushwa LIVE kwa pipindi kisichozidi dakika 15 wakati wa maswali kwa Waziri Mkuu tu.

Akitoa ufafanuzi, aliwaeleza kwamba Bunge la Tanzania linarusha ‘LIVE’ kila siku asubuhi wakati wa maswali ya kawaida na Alhamisi asubuhi wakati wa maswali kwa Waziri Mkuu lakini mijadala yote hurekodiwa na kuhaririwa na kisha kurushwa kuanzia saa 8-9 mchana na saa 3-4 usiku kwa siku husika.

Kwa Watanzania wanaopenda kufanya kazi na wanapenda kufuatilia mambo ya Bungeni, walikuwa hawaoni LIVE coverage kwa sababu walikuwa kazini lakini sasa hivi wanaweza kufuatilia masuala ya bunge kwani muda wa jioni uliopangwa mtu anakuwa ametoka kazini na anaweza kuangalia televisheni akiwa nyumbani baada ya kutoka kazini.

Jaji Mkuu: Sheria Ya Makosa ya Mtandaoni Haina Lengo la Kuwakandamiza Watanzania

0
0

JAJI MKUU wa Tanzania, Mohammed Chande Othman amesema sheria ya mitandao ilipitishwa kwa lengo jema la kulinda watumiaji, wanajamii na usalama wa Taifa la Tanzania.

 

Ametoa kauli hiyo jana (Jumamosi, Mei 14, 2016) wakati akijibu baadhi ya maswali kutoka kwa Watanzania waishio Uingereza kwenye mkutano uliofanyika kwenye Ubalozi wa Tanzania jijini London, Uingereza.

 

Alisema watu watatu kati ya wanne nchini Tanzania wakiwemo watoto, wanamiliki simu za mkononi ambayo ni sawa na watu milioni 35 kati ya milioni 45.

 

Alisema sheria hiyo ilitungwa kwa misingi mitatu moja ikiwa ni kumpa mtumiaji uhuru wa kutoa maoni au taarifa, uhuru ambao alisema unalindwa kikatiba lakini akaonya kuwa kila uhuru unaotolewa pia una mipaka yake kama ilivyoainishwa kwenye ibara ya 30(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 

Alisema sheria hiyo pia inatoa uhuru wa mtu kuwa na faragha (privacy) na msingi wa tatu ni sheria hiyo kuzingatia matumizi ya mitandao ili kulinda usalama wa nchi.

 

“Sheria hii inakupa uhuru wa kutumia mtandao kumlinda mwanajamii wenzako. Hapa Uingereza nimeongea na mwendesha mashtaka mkuu ambaye aliniambia kuwa asilimia 60 ya makosa yanayofanyika chini ya sheria ya makosa ya kujamiiana (S3x.ual Offencea Act) yanatokana na mitandao,” alisema Jaji Mkuu wakati akijibu swali kuhusu sheria ya makosa ya mitandao.

 

Naye Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Dk. Augustine Mahiga alisema kuitishwa kwa mkutano wa kupambana na rushwa nchini Uingereza ni mojawapo ya jitihada za Waziri Mkuu wa nchi hiyo kuanzisha vuguvugu la uanaharakati wa mapambano dhidi ya rushwa.

 

“Kukosekana kwa utawala bora, changamoto za ugaidi, biashara za dawa za kulevya, biashara ya kusafirisha binadamu na uwepo wa rushwa na ufisadi ni baadhi ya mambo yaliyofanya dunia ibadilike. Haya mambo zamani yalikuwa hayana mahali pa kuzungumzwa, kwa hiyo vikao kama hivi vitasaidia kukabili tatizo hili,” alisema.

 

“Rushwa ni kama pweza mwenye vichwa vingi na mikia mingi. Waziri Mkuu David Cameron ameamua kuanzisha movement hii ili kutafuta njia za kukabili janga hili kubwa,” alisema.

 

"Sote tunatambua kuwa mataifa mengi yangependa kuwemo katika hii movement lakini ni faraja kuona kwamba Tanzania imo miongoni mwa waanzilishi na hii ni kwa sababu ya uongozi na ujasiri wa Rais Dk. John Pombe Magufuli ambaye kwa kweli ni game changer  (akimaanisha kuwa amebadili mwelekeo wa Taifa hili) kwani ana utashi wa kisiasa na ana ujasiri wa kukemea maovu,” alisema huku akishagiliwa

 

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Bw. Valentino Mlowola alisema vita ya rushwa nchini Tanzania ni endelevu na inafanyika kuitikia wito alioutoa Rais Magufuli wakati akizindua Bunge la Tanzania Novemba 20, 2015.

 

Alisema wanatumia mbinu mbalimbali kupambana na rushwa lakini kubwa wanayoenda nayo hivi sasa ni kutoa elimu kwa watoto na vijana ili kuwabadilisha tabia na utamaduni uliojikita kwenye jamii.


IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU

JUMAPILI, MEI 15, 2016.

12 Wakamatwa Wakituhumiwa Kuhusika na Mauaji ya Watu Saba Jijini Mwanza

0
0
Siku chache baada ya watu saba wa familia moja kuuawa kwa mapanga wilayani Sengerema mkoani Mwanza, polisi wamefanikiwa kuwatia mbaroni watu 12 kwa tuhuma za mauaji hayo huku mmojawapo akikamatwa kwa mganga wa kienyeji alikokuwa akijitibu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema hadi jana upelelezi wa tukio hilo lililozua hofu kwa wakazi wa Kijiji cha Sima unaendelea na tayari watuhumiwa 12 wamekamatwa.

“Hakuna jiwe litakalobaki bila kugeuzwa katika upelelezi wa jambo hili, tutawasaka na kuwakamata wote waliohusika kwa njia moja au nyingine na mauaji haya ya kinyama,” alisema Msangi.

Habari zilizopatikana kutoka kwa mtu wa karibu na familia ya marehemu Zakaria Mbata iliyopoteza mama na watoto watatu katika tukio hilo, zinaeleza kuwa wauaji walilenga kupora fedha zilizohifadhiwa kwenye mtandao wa simu.

Pia, chanzo kimoja cha habari kilisema kuwa polisi walimkamata mmoja wa watuhumiwa hao akiwa kwa mganga wa kienyeji alikokuwa akijitibu jeraha alilopata siku ya tukio.

“Katika purukushani za mauaji hayo, huyo mhalifu alijeruhiwa usoni, inaonekana alipigwa na kitu kizito, akakutwa kwa mganga wa kienyeji na amekamatwa kwa mahojiano,” kilisema chanzo hicho

Tukio Lenyewe
Usiku wa kuamkia Mei 11, watu wasiojulikana walivamia familia ya Zakaria Mbata na kuua watu saba kwa kuwakata mapanga sehemu mbalimbali za mwili.

Waliouawa katika tukio hilo ni mama wa familia hiyo, Augenia Philipo (62), mdogo wake Maria Philipo (56) na watoto wake; Yohana Mabula (20), Regina Aloyce (12) na Mkiwa Philipo (13).

Wageni wawili wa familia hiyo, waliojulikana kwa jina mojamoja ya Donald na Samson nao pia waliuawa katika tukio hilo.

UVCCM Wafikishana Polisi

0
0
Sakata la uuzwaji kinyemela wa zaidi ya hekari 200 za shamba la Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Mkoa wa Iringa limechukua sura mpya baada ya aliyekuwa katibu wa mkoa huo, Ally Nyawenga kukamatwa na polisi.

Shamba hilo lililopo eneo la Igumbiro, nje kidogo ya mji wa Iringa, linadaiwa kuuzwa mwaka jana kwa zaidi ya Sh800 milioni baada ya baadhi ya viongozi kubadili matumizi yake na kuwa viwanja.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, John Kauga alisema jana kuwa kiongozi huyo alikamatwa Morogoro siku chache zilizopita.

“Tulituma askari wetu na leo hii wanamleta. Taarifa za kumkamata ni hizo za uuzwaji wa shamba hilo kwa hivyo tutafanya naye mahojiano zaidi, lakini kwa sasa sina taarifa zaidi ya hapo labda tuwasiliane kesho (leo),” alisema.

Nyawenga alisimamishwa kazi mwishoni mwa mwaka  jana, akituhumiwa kusimamia uuzwaji wa shamba hilo kinyume cha utaratibu wa jumuiya hiyo.

Mali zote za jumuiya hiyo zipo chini ya Baraza la Wadhamini, linaloongozwa na Mwenyekiti, Dk Emmanuel Nchimbi.

UVCCM ilianza kumiliki shamba hilo miaka ya 1970 likitumika kwa ajili ya kilimo kwa kukodisha vijana kwa bei nafuu ili kuwasaidia kujiendeleza kiuchumi.

Ally Simba aliyedaiwa kuwa msimamizi wa shamba hilo alikana nafasi hiyo huku akisema hakuhusishwa katika mipango hiyo.

“Sikuwa msimamizi, bali mjumbe tu wa kamati ya utekelezaji, msimamizi alikuwa Katibu wa UVCCM,” alisema Simba ambaye kwa sasa ni Katibu wa UVCCM Wilaya ya Mbinga.

Alisema kabla ya kuondoka Iringa mwaka 2014, hakuwahi kusikia vikao wala mipango ya uuzaji wa shamba hilo na kwamba hahusiki.

Akizungumzia kukamatwa kwa Nyawenga, Katibu wa UVCCM Mkoa wa Iringa, Abdulkarim Halamga alisema: “Kwa sababu ni mali ya vijana na katibu aliyekuwapo anahusika, hivyo kwa kushirikiana na polisi, tumemkamata baada ya waliouziwa viwanja kuanza kutudai huku vijana wakipinga kuuzwa kwa eneo lao. Kwa sababu hakuwa peke yake, taratibu nyingine zitafuatwa akishafikishwa Iringa.”

Mjumbe wa kamati ya utekelezaji ya UVCCM mkoani hapo, Thom Muyinga alisema kuuzwa kwa shamba hilo kumesababisha mpasuko ndani ya umoja huo. “Vijana wanataka mali yao, haiwezekani mali hiyo iuzwe kinyemela na kunufaisha kundi la watu wachache,” alisema.

Mmoja wa vijana hao, Katula Kalinga alisema japo tayari tume ya UVCCM ya kuchunguza mgogoro huo ilishakwenda Iringa, hakuna kinachoendelea.

Alimuomba Rais John Magufuli kufuta hati za viwanja hivyo ili shamba hilo, lirejeshwe kwa UVCCM.

Pia, walimuomba Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete kutumbua majipu yanayokitafuna chama kwenye mkoa huo, ili vijana waendelee kunufaika na mali yao.

Walitaka kamati ya utekelezaji jumuiya hiyo Mkoa wa Iringa isimamishwe wakati uchunguzi ukiendelea.

John Terry Aongezewa Mkataba wa Mpya Chelsea

0
0
Klabu ya Chelsea imethibitisha kumuongezea nahodha wao John Terry mkataba mpya wa mwaka mmoja sasa ni juu yake kubaki au kuondoka Stamford Bridge msimu ujao.

Msemaji wa klabu amesema; “Marina Granovskaia na Bruce Buck wamekutana na John na wakala wake na kumpa ya Mkataba wa mwaka mmoja abaki,”.
“Na wakati msimu unaelekea ukingoni, haya ni maamuzi mazito kwa John na familia yake na kitu ambacho wanakifikiria kwa sasa,”.

Mashabiki wa Chelsea walikuwa wakimpigia debe Nahodha huyo usiku wa Jumatano Uwanja wa Anfield wakitaka Terry aongezewe Mkataba mpya huku wakiwa wamebeba mabango yanayoonyesha mataji mengi ambayo klabu ilishinda chini ya uongozi wake.

Pamoja na kwamba umri umeenda na kiwango kimeshuka, lakini Terry bado ni kipenzi cha mashabiki wa Stamford Bridge haswa wanapokumbuka mchango wake enzi zake.

Makonda: Wanawake Ndiyo Chanzo Cha Ufisadi Nchini

0
0
Na Dotto Mwaibale

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema wanawake wamekuwa ni chanzo cha ufisadi nchini kutokana na kupokea zawadi zitokanazo na fedha za kifisadi.

Makonda aliyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Mnyamani Vingunguti Dar es Salaam jana katika mkutano wa kujadili namna ya kupata mikopo mbalimbali kutoka Benki ya Wananchi Dar es Salaam (DCB).

” Ninyi wakina mama mmekuwa chanzo cha ufisadi kwa vile mmekuwa mkipokea fedha na zawadi mbalimbali kutoka kwa watoto wenu lakini mmekuwa hamuwahoji wanako zitoa fedha hizo kwani zingine zinakuwa za kifisadi” aliseama Makonda.

Makonda aliwaambia wanawake hao kuwa hata katika suala zima la usafi linaanzia na malezi ya usafi ya wakina mama kwa watoto wao tangu wakiwa wadogo jambo ambalo lingesaidia kipindi hiki ambapo kunachangamoto kubwa ya kusafisha miji yetu.

Katika hatua nyingine Makonda alitoa pongezi kwa Kaimu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omari Kumbilamoto kwa kuwa jirani na wananchi wa kata yake kwa kufanya maendeleo bila ya kujali itikadi za vyama hasa katika kujipatia mikopo kutoka katika Benki ya Wananchi Dar es Salaam (DCB).

“Nimefurahishwa na diwani wenu Kumbilamoto kwa kushirikiana nanyi ili  kujiletea maendeleo ni jambo zuri na wakati huu ni wa kukutana kubuni na kuangalia jambo gani litawakwamua kiuchumi badala ya kuwaza maandamano yasiyo na tija” alisema Makonda.

Shambulio la Kujitoa Mhanga Laua Watu 14 Iraq

0
0
Takribani watu 14 wamepoteza maisha huku zaidi ya 20 wakijeuhiwa vibaya katika shambulio la kujitoa mhanga lililotokea kwenye kiwanda cha gesi kaskazini mwa mji Mkuu wa Iraq, Baghdad.
gari

Msemaji wa Jeshi la Iraq amesema gari lililokuwa limetegwa milipuko lililipuka karibu na lango la kuingia kwenye kiwanda hicho leo asubuhi na baadaye washambuliaji sita wa kujitoa mhanga wakaingia ndani ya kiwanda hicho ambapo walikabiliana na maofisa wa usalama.
Kundi la IS limekiri kuhusika na shambulio hilo.

Mtoto wa Michael Jackson Aanza Kufuata Nyayo za Baba yake

0
0
Mtoto wa nyoka ni nyoka tu.
Hatimaye mtoto wa Michael Jackson, Pris Jackson (18) ameanza kufuata nyayo za baba yake kwa kuanza kutoboa ulimi. Paris amepost picha inayomuonyesha akiwa ametoboa ulimi na kuweka kipini na kuandika: “almost like ring-toss. but with noodles and needles.”

Miaka kadhaa nyuma kabla ya kufariki, Michael Jackson aliwahi kujibadili muonekano wake wa ngozi na kuzua maswali mengi kwa mashabiki duniani.

Kiwanda Cha Bia Serengeti Breweries Limited (SBL) Chapigwa Faini

0
0

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira na Muungano), Luhaga Mpina amekiamuru Kiwanda cha Serengeti Breweries Limited (SBL), kulipa faini ya Sh16 milioni kwa kosa la kutiririsha maji yasiyo salama kwenye makazi ya watu.

Uamuzi huo ulichukuliwa mwishoni mwa wiki iliyopita mbele ya baadhi ya viongozi wa SBL kilichopo Chang’ombe Manispaa ya Temeke na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (Nemc), baada ya kujiridhisha kuwa kilikiuka taratibu za utunzaji mazingira na kutotekeleza amri halali kwa zaidi ya miaka miwili.

Mpina aliigiza kiwanda hicho, kulipa faini ndani ya siku saba na kwamba asieleweke vibaya kuhusu uamuzi huo, bali anasimamia sheria.

“Nasimamia sheria wala sina nia mbaya na kiwanda chenu, naomba nieleweke hivyo na faini hii mlipe kwa wakati,” alisema Mpina.

Mkurugenzi Mkuu wa Nemc, Bonaventure Baya alisema baraza hilo limejijengea utaratibu wa mara kwa mara kufuatilia kanuni za afya za kiwanda hicho hasa majitaka yanayotiririka kuelekea kwenye makazi ya watu.

Meneja Mhandisi Biashara wa SBL, Peter Mkongwa alikanusha tuhuma hizo na kwamba, maji hutibiwa kwa dawa kabla ya kutiririshwa katika makazi ya watu. Alisema: “Tunasubiri mashine maalumu ya kuvuta maji hayo ili yaingie katika bomba.”

Mange Kimambi Afunguka Kuhusu Video ya Msichana Aliyepigwa Video Akiwa Uchi na Kubakwa Morogoro

0
0
Blogger maarufu Mange Kimambi ameguswa na tukio la msichana kurekodiwa video akiwa uchi na kulazimishwa kufanya mapenzi na kisha video kusambazwa mitandaoni , ameandika haya katika ukurasa wake wa Instagram

mangekimambi_ Jamani watz tuachage kutengeneza story za uwongo. Ile story ya facebook yani walaaa. So issue iko hivi, Huyu dada alikuwa anatoka na bosi wa matrekta huko vijijini- Morogoro. Dizain jamaa kaoa ana familia yake so demu na yeye akawa anachepuka na mtu mwingine wa saizi yake. Ndo huyo jamaa kuambiwa kuwa demu anam cheat ndo akamuita hapo lodge, inaitwa Tiff Lodge iko Dakawa-Morogoro(jina la lodge limeandikwa kwenye mashuka, nimeona kwenye video)Demu akaenda akijua anaenda kuonana na jamaa yake hakuna issue, Kumbe jamaa keshampanga huyo njemba aje kumbaka alafu yeye akae arekodi then asambaze kwenye social media.Imagine Huyu jamaa alivyomind demu kuchepuka mpaka kumdhalilisha dada wa watu hivi utasema alikuwa na plan za kumuoa au hata kumchumbia kumbe ni mume wa mtu.
.
Huyu binti kwanza anamuogopa huyo jamaa kufa. Baada ya kufanyiwa huu unyama alipofika nyumbani alimweleza mamake Ila binti aligoma kabisaaa kwenda polisi, mama yake ndo akaenda polisi, polisi nao wakagoma kufungua kesi mpaka binti aende mwenyewe. Yani unaambiwa hiyo kumfanya binti akafungue kesi tu ilikuwa mshike mshike, nasikia ni baada ya hii video kusambaa ndo akakubali kufungua kesi. Jamani Huyu binti Inabidi mtu amshikee ampe moyo mpaka siku atakayoingia mahakamani kutoa ushahidi la sivyo hachelewi kuogopa... Lakini uzuri wa hii kesi serikali wala haimuhitaji sana mlalamikaji yani video inajielezea yenyewe.
.
Sasa jamani naomba tushirikiane hapa. Hawa jamaa wako ndani kesho ndo wanafikishwa mahakamani . Mkuu wa wilaya ya Mvomero- Morogoro ambako ndo issue ilipotokea ni Betty Mkwasa na yeye keshapewa habari hii, Ila Sasa it seems polisi hawana hizi video. .Nimepewa number ya Betty Mkwasa Ila nashindwa kumuadd whatsapp Naomba mtu amwambia ani add nimpe hizo video +1 424 333 2650, Au Nyie wadau ambao mnazo hizo video na mnaijua number ya Betty Mkwasa pls mtumieni ili azifikishe polisi leo hiii Kabla ya Kesho mahakamani. Jamani hawa mbwa wasipate dhamana Kesho... Also nyinyi ambao mnazo hizi video Tafadhali msimtumie mtu yoyote yule Maana tunazidi kumdhalilisha huyo dada kwa kuzisambaza.Kama unataka kumsaidia huyo dada zikifishe video polisi ya Mvomero - Morogoro leo hiii....

Diamond Platnumz Alibomoa ile Nyumba yao Tandale na Kujenga Hii Mpya..Itazame Hapa


Meseji Zingine za Mwanamuziki Harmonize na Jackline Wolper Zavuja Mtandaoni

0
0
Hii ni post nyingine inayosambaa mitandaoni ikionyesha maongezi ambayo sio ya moja kwa moja kati ya Jackline Wolper na Harmonize.

Ni Couple mpya inayozungumziwa zaidi Bongo kwa sasa.

Aibu, Fedheha ya Mabasi ya Mwendo Kasi, Jiji, Manispaa Dar

0
0
IKIWA ni siku tano kupita baada ya mabasi ya mwendo kasi kuanza kusafirisha abiria katika Jiji la Dar es Salaam, hali ya vituo vyake inatisha, anaandika Happiness Lidwino.

Baadhi ya vituo hivyo vinatoa harufu kali, vimeenea mikojo, kinyesi na takataka ngumu ambapo Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na manispaa husika vimedai kutohusika na usafi wake.
Miongoni mwa vituo alivyotembelea mwandishi wa habari hii ni pamoja na Moroco (Kinondoni), Kinondoni B, Manyanya na Kimara Baruti ambapo vituo hivyo vimekuwa na hali inayotia shaka usalama wa abiria wanaotumia vituo hivyo kusubiri usafiri.

Gatson Makwembe, Msemaji wa Jiji alipoulizwa kuhusu ufuatiliaji wa usafi kwenye vituo hivyo baada ya hali kuwa mbaya, amedai jiji halihusiki.
“Mimi siwezi kuzungumzia suala hilo kwani sisi halituhusu labda uwatafute Dart au Msemaji wa Manispaa ya Kinondoni,” amesema Makwembe.

Sebastian Mhowera, Ofisa Uhusiano wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni alipoulizwa, alidai kazi ya Manispaa ya Kinondoni ni kusimamia usafi wa barabarani pekee.

“Sisi kazi yetu ni kusimamia usafi barabarani ndani ya manspaa hii na sio uchafu uliopo ndani ya vituo vya mabasi ya UDA. Siwezi kuzungumzia uchafu uliopo kwenye nyumba ya jirani,” amesema.
Alipotafutwa William Gatambi, Msemaji wa Kampuni ya Dart inayosimamia UDA hakupatikana kujibu aliye na dhamana ya kufanya usafi kwenye vituo hivyo.

Hali ya wasiwasi inaendelea kutawala kwa wananchi kutokana na vituo hivyo kuwa na hali mbaya, kukosa ulinzi na hata kugeuka kuwa maeneo ya vibaka, mateja na watoto wa mitaani kupata hifadhi ya usingizi.

Kituo cha Kimara Baruti kimekuwa na mlundikano mkubwa wa watu, harufu mbaya inayotokana na kinyesi, mkojo huku mwingine ukiwa umefungwa kwenye chupa za maji na kutupwa hovyo. Uchafu wa kituo hicho unafanana na vituo vingine.

John Mgonja, mmoja wa abiria aliyekuwa akisubiri usafiri katika Kituo cha Moroco ameeleza kushangazwa na huduma mbovu za vituo hivyo.
“Kwanini vituo havina ulinzi, hakuna maji, sakafu chafu, taka ngumu kila mahali na harufu mbaya mpaka imekuwa kero.

“Sijui sisi tuna tatizo gani, hivi haya mambo yote hayakuwa kwenye mpango wao. Wao wanachojua ni kukusanya fedha kwa ajili ya nauli tu?” amehoji Mgonja.

Amesema, watu wanalazimika kufanya hivyo kwa kuwa, kama amebanwa na haja na vyoo vipo kwake anaona ni bora kikudhi haja yake kwanza mengine mbele kwa mbele.
“Sasa kama umefika hapa na umebanwa kwanini usijisaidie, lakini hata kama utaacha vyoo vichafu nani atakukamata? Hakuna mlinzi na hakuna usalama wowote,” amesema.

KENYA: Atiwa Mbaroni Kwa Kudandia Helikopta..Mwenyewe Adai Alinaswa Mguu

0
0
Polisi wa Kenya wanamshikilia mtu mmoja mjini Bungoma baada ya kuning’inia kwenye helikopta iliyoubeba mwili wa aliyekuwa mfanyabiashara Jacob Juma.

Mtu huyo, Saleh Wanjala ambaye hakutoa sababu za kufanya hivyo, alishikiliwa na polisi huku akipata matibabu kwenye Hospitali ya Rufaa Bungoma.

Wanjala alionekana akining’inia kwenye helikopta iliyobeba mwili wa mfanyabiashara huyo wakati ikipaa kutoka kwenye Uwanja wa Posta mjini Bungoma baada ya wananchi kutoa heshima za mwisho.

Wanjala aliamua kuidandia helikopta hiyo wakati ikiondoka kupeleka mwili wa Juma nyumbani kwake katika Kijiji cha Mungore.

Akisimulia mkasa huo, Wanjala alisema alikuwa karibu na helikopta hiyo wakati ikianza kupaa na kwamba aliumia baada ya mguu wake kukwama.

“Nilikuwa nimeketi chini ya helikopta na wakati ilipokuwa inaanza kupaa, mguu wangu ulikwama hapo ikabidi nijishikilie vizuri ili nisianguke,” alisema Wanjala.

Rubani wa helikopta hiyo alilazimika kumpeleka hadi uwanja wa ndege wa Bungoma mita 700 kutoka kwenye uwanja huo lakini Wanjala aliamua kuruka na kuumia vibaya miguu na mikono. Muuguzi wa Hospitali ya Bungoma, Leah Atsewa alisema bado wanamfanyia uchunguzi.

Giggy Money: Gardner Kwangu Hachomoki

0
0
MUUZA nyago kwenye video za Kibongo, Gift Stanford ‘Giggy Money’ amefunguka kuwa mtangazaji maarufu Bongo anayeuza maneno katika Kituo cha Redio cha Clouds FM, Gardner G. Habash hachomoki kwake na hadi sasa wako kwenye uhusiano wa mapenzi kwa muda wa miezi sita, Risasi Jumamosi  linakumwagia ubuyu wote.

Akichonga na gazeti hili baada ya picha zinazomuonesha akiwa kwenye mapozi ya kimahaba na Gardner kusambaa kwenye mitandao ya kijamii, Giggy alisema mtangazaji huyo amekuwa mtu wa muhimu kwake kwa sasa.

“Kwani kuna tatizo nikiwa na Gardner? Yule ni mtu muelewa na sahihi kwangu, ninafikiri kupitia yeye nitajifunza mambo mengi na kuzidi kufanikiwa kwa sababu yeye ni moja kati ya watu ambao wako kwenye tasnia ya burudani kwa muda mrefu,” alisema Giggy Money.

Gazeti hili lilimtafuta pia Gardner ili aweze kufungukia ubuyu huo, alipopatikana alisema;
“Nipo karibu na Giggy lakini hatuna uhusiano wa kimapenzi, kwa hiyo kama anasema hivyo si kweli lakini yeye ni shabiki wangu na mimi ni mshabiki wake, ninapenda pia kazi anazozifanya,” alisema Gardner.

Lady Jaydee Kutoa Kauli yake Leo Baada ya Kudai Kudhalilishwa na Gardner

0
0
Siku 14 tangu Mtangazaji wa Clouds Fm Gardner Habash kudaiwa kutoa lugha ya udhalilishaji dhidi ya aliyekuwa mke wake Judith Wambura, mwanamuziki huyo maarufu kwa jina la Lady Jaydee, amesema leo anatarajia kutoa tamko rasmi kuhusu suala hilo.
Buff Bantam Hen {Gallus gallus domesticus} with nine of her ten chicks, 2-days-old. The tenth chick is under her

“Nipo katika maandalizi ya tamasha langu ndiyo maana ilikuwa vigumu kwangu kulizungumzia hili, Jumatatu (leo) nitatoa tamko,” alisema Jaydee.

Mei 13 kupitia mwanasheria wake Amani Tenga kutoka kampuni ya Law Associates Advocate, alimwandikia barua ya kumtaka mtangazaji wa Clouds Fm, Gardner Habash kuomba radhi mbele ya umma ndani ya siku 7 kwa kauli ya udhalilishaji aliyoitoa dhidi yake.

Gardner anadaiwa kutamka maneno ya udhalilishaji dhidi ya Jaydee Mei 6 mwaka huu na kurekodiwa kisha video kusambazwa katika mitandao ya kijamii, katika ukumbi wa CDS PARK (zamani TCC) alipokuwa akisherehesha tamasha la Miss TIA 2016,

Taarifa iliyosomeka katika barua hiyo ya mwanasheria ilimtaka Gardner aombe radhi na iwapo akikaidi, akishindwa au kuzembea ndani ya siku saba, atachukuliwa hatua stahiki ikiwa ni pamoja na kufunguliwa kesi ya udhalilishaji na kashfa.

Mwananchi lilimtafuta Gardner na kumuuliza iwapo amepokea barua hiyo na matarajio yake ya kujibu tuhuma zinazomkabili, lakini mtangazaji huyo alikaa kimya kwa muda wa sekunde 10 na baadaye alisema; “sina maoni yoyote kuhusu jambo hili.”

Barua iliyoandikwa na mwanasheria huyo ilisomeka kuwa kauli ya Gardner, maneno yake hayo yalikuwa yanamhusu Jaydee moja kwa moja hivyo kusababisha udhalilishaji mbele ya umma.
Viewing all 104416 articles
Browse latest View live




Latest Images