Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104415 articles
Browse latest View live

Breaking News:David Kafulila ameshindwa katika kesi aliyoifungua kupinga ushindi wa Hasna Mwilima wa CCM.

0
0

TABORA: Aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila ameshindwa katika kesi aliyoifungua kupinga ushindi wa Hasna Mwilima wa CCM.

Kesi ilifunguliwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Tabora na ilikuwa chini ya Jaji Ferdinand Wambari.

Katika kesi hii upande wa mlalamikaji (Kafulila) uliongozwa na mawakili Prof. Abdallah Safari, Tundu Lissu na Daniel Lumenyera, Ili hali upande wa mlalamikiwa (Husna) uliongozwa na wakili Kennedy Fungamtama pamoja na Mawakili wa Serikali upande wa mwanasheria mkuu wa Serikali.

Kutoielewa sheria ya makosa ya mtandao kutawaponza wengi

0
0

Tecno, Huawei na simu zingine za sqmartphone zenye bei chee zimewafanya watu wengi kuweza kufaidi ukuaji wa teknolojia. Lakini pia uwepo wa simu hizo, usingeweza kukamilika pasipo makampuni za mitandao ya simu hapa nchini kuboresha miundombinu ya internet.

Kwa sasa kila mwananchi, hata wale wa vijijini wana access na internet. Hadi sasa kwa mujibu wa mamlaka ya mawasiliano nchini, TCRA zaidi ya watanzania milioni 17 wanatumia internet. Ndio maana kuna ongezeko kubwa la matumizi ya mitandao ya kijamii hususan Facebook, Instagram na WhatsApp. Ni WhatsApp kutokana na umuhimu wake imetokea kuwa mtandao unaotumiwa na wabongo wengi.

Huko kuna makundi ambayo watu huchat, hutumiana video na picha kutaarifiana na mara nyingi kujifurahisha. Lakini pia ongezeko la matumizi ya simu, internet na mitandao ya kijamii imefanya kuwepo na matumizi mabaya na hivyo kupelekea kuanzishwa kwa sheria ya makosa ya mtandao.

Lakini bahati mbaya ni kuwa pamoja na Watanzania wengi kujua kuwa sheria hii inafanya kazi, hawajui ni makosa gani hasa yanayoangaliwa na yana adhabu gani. Ndio maana tukio lililotokea wiki hii huko Dakawa wilayani Mvomero, Morogoro la msichana aliyedhalilishwa kimapenzi na wanaume wawili na kumrekodi kisha kusambaza picha na video zake limewaponza wengi.

Ni kwasababu pamoja na kwamba watu hawa wanaodaiwa kuwa ex na mwingine mpenzi wa sasa wa binti huyo walitenda kosa la ubakaji, walikuwa hawajui kuwa kwa kumrekodi na kusambaza video na picha zake walikuwa wanazishika sharubu za sheria hii.

Kwa akili yake, Zuberi Thabiti, mpenzi wa msichana huyo aliamini kuwa kwa kumrekodi binti huyo akifanyiwa ukatili huo atakuwa amelipiza kisasi kwa usaliti anaodaiwa kufanyiwa baada ya mpenzi wake kutembea na dereva wake na maisha yataendelea kama kawaida.

Lakini kuna kundi jingine la watu ambalo limeponzwa na kutokujua kuwa kusambaza picha au video za aina hiyo ni kosa kisheria. Tayari polisi wanawashikilia watu 9 wengine (tofauti na wawili waliohusika kwenye tukio) kwa kusambaza picha hizo. Hawa wamevunja sheria ya makosa ya mtandao kifungu namba nne, kifungu kidogo (1) (a): Kifungu hicho kinasema:

14.-(1) Mtu hatachapisha au kusababisha
kuchapishwa kupitia katika mfumo wa kompyuta-
(a) ponografia; au
(b) ponografia yoyote iliyo ya kiasherati au chafu.

Sheria ya makosa ya mtandao imeweka adhabu kali zaidi katika mambo ya ponografia:

(2) Mtu atakayekiuka kifungu kidogo cha (1)
atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani, atawajibika, iwapo ni uchapishaji kuhusiana na-
(a) ponografia, kulipa faini isiyopungua shilingi
milioni ishirini au kutumikia kifungo kwa
kipindi kisichopungua miaka saba au vyote kwa
pamoja; au
(b) ponografia iliyo ya kiasherati au chafu, kulipa
faini isiyopungua shilingi milioni thelathini au
kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua
miaka kumi au vyote kwa pamoja.

Kwahiyo pasipokujua, watu wengi watajikuta wanafungwa ama kulipa faini kwa kusambaza video za matusi kwenye makundi yao WhatsApp wakitarajia kupongezwa kwa kuchangamsha ‘genge.’

Na Ponografia ni sehemu moja tu ya makosa ya mtandao. Makosa mengine ambayo Watanzania wanapaswa kujiepusha nayo ni pamoja na:

5. Kubaki katika mfumo wa kompyuta kinyume cha sheria.
6. Kuingilia mawasiliano kinyume cha sheria.
7. Kuingilia data kinyume cha sheria.
8. Ujasusi data.
9. Kuingilia mfumo kinyume cha sheria.
10. Kifaa kisicho halali.
11. Kughushi kunakohusiana na masuala ya kompyuta.
12. Udanganyifu unaohusiana na kompyuta.
13. Ponografia za watoto.
14. Ponografia.
15. Makosa yanayohusiana na utambuzi.
16. Kutoa taarifa za uongo.
17. Ubaguzi.
18. Matusi ya kibaguzi.
19. Mauaji ya kimbari na makosa dhidi ya binadamu.
20. Ujumbe unaotumwa bila ridhaa.
21. Ufichuaji wa taarifa za upelelezi
22. Kuzuia upelelezi.
23. Unyanyasaji kwa kupitia mtandao.
24. Ukiukaji wa haki bunifu.
25. Wakosaji wakuu.
26. Jaribio la kufanya uhalifu.
27. Kula njama ya kutenda kosa.
28. Ulinzi wa miundombinu muhimu ya TEHAMA.
29. Makosa yanayohusu miundombinu muhimu ya TEHAMA

Sababu 5 kwanini wanawake wenye akili nyingi hupata tabu ya kupata mapenzi ya kweli

0
0

Akili nyingi ni zawadi na laana. Wanapojiangalia kwenye kioo, wanawake wenye akili nyingi huona picha ya mtu mwenye nguvu mwenye malengo, anayejua anachotaka. Kuwa na akili nyingi ni kitu muhimu kuwa nacho, lakini wakati mwingine kinaweza kuwatisha wengine.

Pengine ndio maana watu wenye akili nyingi hupata shida ya kupata pendo. Kama unajiuliza kwanini bado upo single, hizi ni sababu tano kwanini unaweza ukawa unapata shida kupendwa.

1. Unakuwa mchambuzi mno

Wasichana wenye akili mara nyingi huchambua sana vitu. Huwa na shaka na kesho yao, njia nzuri za kuimarisha mahaba, na wanataka sana kumpata mtu sahihi. Hiki hata hivyo sio kitu kibaya.

2. Unajua ni bora kuwa peke yako kuliko kuwa na mwenza asiye sahihi

Na hakuna tatizo katika hilo pia. Watu wenye akili wako makini katika kumpata mwenza sahihi ambapo wanaweza kuamua kubaki wenyewe kama asipopatikana.

3. Unajua kuwa mahusiano mara nyingi hufa

Hawa hujua ukweli unaouma kuwa mahusiano mengi hayafiki popote. Matokeo yake, wakati mwingine hufanya mambo pole pole na kuwa na shida katika kuingia miguu miwili. Lakini mwenza sahihi ataelewa hilo.

4. Unaweza kuwa unaogopesha

Sio kwamba watu wenye akili huwatisha mambumbu lakini hata wenye akili pia. Wanaweza wasiwe comfortable na ukweli kuwa unafanya vizuri katika eneo la maisha ambayo hawapo.

5. Unajua kujilinda mwenyewe

Watu wenye akili katika dunia hii wanaelewa sana hatari katika hali yoyote na hiyo inahusisha pia dating. Huwa makini, waangalifu na huweka vikwazo kujilinda wenyewe.


Chanzo: Life Box Today

Mkenya Auawa na Polisi Kwa Kipigo .....Walikuwa Katika Maandamano Kutaka Tume ya Uchaguzi Iundwe Upya

0
0

Kijana mfuasi wa muungano wa upinzani nchini Kenya(CORD), Ben Ngari aliyeshambuliwa kinyama na polisi jana amefariki dunia kwa sababu ya majeraha yaliyompata

 

Wafuasi wa CORD jana waliandamana kushinikiza kuundwa upya kwa Tume ya Uchaguzi (IEBC)

David Kafulila Afunguka Haya Baada ya Kushindwa Kesi yake leo

0
0
David (NCCR Mageuzi) Kafulila kayaongea haya Baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Tabora kutoa maamuzi ya Kesi ya kupinga Matokeo ya uchaguzi aliyokuwa Ameifunguwa na hivyo kumpa ushindi Hasna Mwilima( CCM).

Mkubwa Fella Afunguka Namna milioni 50 za Kayumba zilivyotumbuliwa

0
0
Fella amedai pesa za milioni 50 za Kayumba alizoshinda kwenye BSS amenunulia gari na zilizobaki akaanza ujenzi ambao ataumalizia akipata pesa za show.

FAIZA ALLY:Toka Niachane na Sugu Sitamani Kuwa na Mahusiano na Mtanzania

0
0
Msanii wa filamu na Mama wa mtoto mmoja aitwae Sasha, Faiza Ally amedai hajawahi kufanya kutoka kimahaba na mtanzania yeyote toka aachane na aliyekuwa mume wake Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ kwa madai kuwa anaogopa kudhalilishwa.

Muigizaji huyo amesema hali hiyo imekuja kutokana na matukio ya udhalilishaji wa wanawake ambayo yanaripotiwa kutokea katika sehemu mbalimbali hapa nchini.

Faiza ameandika:

Wanaume acheni kudhalilisha wanawake, video imenisikitisha na mwanamke yoyote atakaye ipost ni mjinga, maana ana chofanya naye ni udhalilishaji. Kusema kweli toka niachane na Baba Sasha sija date na mtanzania Kwa sababu naogopa unaweza ukahisi unatongozwa kwa heri Kumbe mtu kakupania kukudhalilisha! Nimesikitishwa lkn kwa hatua zilizo chukukuliwa na serekali na juhudi za muandishi nimeshukuru sana sana!

Na Niko tayari hata kuandamana kupinga wanaume wazalilishaji# na nukuu maneno kutoka bungeni #wanawake ni mama zenu#dada zenu#mabinti zenu#shangazi zenu #ACHENI KUTUDHALILISHA


Idris Sultan Amwandikia Wema Sepetu Ujumbe Mzito

0
0

Uhusiano wao umepitia misukosuko mingi ikiwemo kuachana mara kadhaa lakini Idris Sultan na Wema Sepetu hawajalikatia tamaa pendo lao.

Ni muda mrefu tangu Idris aandike kitu kwenye mitandao ya kijamii kuhusu penzi lake na Wema baada ya kudai wameamua kuuweka uhusiano wao private kwa sasa. Lakini sasa mshindi huyo wa Big Brother Africa ameshare ujumbe mahsusi kwa mpenzi wake huyo.

“I am proud to say the mistakes we have made have not only made us stronger but better, faster, wiser, love too strong, stronger than any of us,” Idris ameandika kwenye picha ya Wema aliyoiweka Instagram.

“We ni kasumbufuuu, unasusasusa, wivu ndo usiseme, kugombana hadi kulia but in the end of the day i will open my arms na utajileta mwenyewe utaniangalia usoni and tell me “I hate you” and lay on my chest. I will smile and say “I love you too”. We have gone through heaven and hell and now you’re my bestfriend, family, wifey, lover you’re my cherry . #WolfQueen.”

Hivi karibuni wawili hao waliingia kwenye matatizo makubwa baada ya video inayomuonesha Wema akimbusu mwanaume mwingine kusambaa mtandaoni. Idris alikiri kuumizwa na jambo hilo.

Hii ‘Aje’ ya Alikiba ni Kiboko- Mwana FA

0
0
Msanii wa muziki wa bongo fleva Mwanafalsafa A.K.A Mwana FA amefunguka na kuonyesha hisia zake kuikubali kazi mpya ya msanii Alikiba ambayo inafahamika kwa jina la ‘Aje’

Mwana FA kupitia account yake ya twitter aliandika ujumbe wenye kuonyesha kuwa kazi hiyo ya msanii huyo ni kiboko na kusema amesikiliza mara nyingi sana lakini hajaweza kugundua kosa lolote lile kutokana na ngoma hiyo kuwa ni kali.

“hii aje ya kiba nyo*** bana, its perfect Wakazi. Ukiisikiliza mara nyingi kama mimi unakuwa na uwezo wa kuona makosa,Siyaoni hata kwa kuyasaka” Mwana FA

Mbali na Mwana FA msanii mwingine Wakazi pamoja na Shaa wameungana na Mwana FA na kusema kuwa wimbo huo ni kiboko na jinsi ulivyopangiliwa

Download Application ya SIASA HURU Blog Kwenye Simu yako Kupata Habari za Siasa Kwa Urahisi

0
0
Kama wewe ni mpenzi wa Habari za Siasa basi hii ni habari njema kwako...Download Siasa Huru Application Kutoka Google Play Store Kwenye Simu yako itakurahisishia upataji wa Habari na Breaking News za Siasa kwa urahisi....

Bonyeza HAPA Kuinstall Kwenye Simu yako fasta....

Au Nenda Google Play Store Kwenye Simu yako Alafu Search 'Siasa Huru' Kisha Install


Bwana Mdogo Mayunga(Mtanzania) Azidi Kung'aa Mziki wa Kimataifa Akishirikiana na Akon

0
0
Huyu dogo alishinda tuzo ya "Airtel Talent"(?) pale Nairobi Kenya na baadae akapata offer ya ku-record wimbo na Akon,kabla ya hapo alikuwa ameimba na Mr Blue

Kwa sasa "single" yake aliyomshirikisha Akon imetoka,ni wimbo mzuri,hakika umemvusha dogo toka hatua moja kwenda nyingine.Wimbo mzuri na unasikiliza,"Dont Go Away" ndio habari ya town kwa sasa Usikilize Hapa chini:

Mganga Mbaroni Akidaiwa Kugoma Kumhudumia Mjamzito

0
0
Polisi mkoani Mara inamshikilia mganga wa zahanati katika Kijiji cha Rwamchanga wilayani hapa kwa madai ya kushindwa kumhudumia mjamzito aliyejifungua mapacha na kusababisha kifo mtoto mmoja.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Ramadhan Ng’anzi amesema tukio hilo lilitokea Mei 15.

“Tunamshikilia kwa makosa matatu, likiwamo la uzembe, kufanya makusudi na kushindwa kuwajibika sawa na kiapo cha kazi yake, tunaendelea na mahojiano yatakapokamilika atafikishwa mahakamani,” amesema Ng’anzi.

Akisimulia chanzo cha mwanae kupoteza maisha, Shida Mugesi akiwa katika Hospitali ya Nyerere alisema alifika hospitalini saa 12 asubuhi na kumuomba mganga amuhudumie, lakini alikataa.

“Nilikaa kwa muda wa saa mbili bila kupatiwa huduma, ghafla nilihisi uchungu wa kusukuma mtoto tukamuita mganga wa zamu ili anisaidie aligoma na kudai nimsubiri anakwenda kuoga na wakati huo alikuwa anazungumza kwa simu bila kuonyesha ushirikiano. Baada ya kugoma kunisaidia nilianza kujifungua mwenyewe,” alisema.

Muuguzi ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema walipopima uzito wa watoto kwa mjamzito huyo walibaini kuwa aliyefariki alikuwa na kilo 2.5 na mwingine 2.3.

Muuguzi wa zahanati hiyo, Frida Kasonga alisema aliposikia taarifa ya kuwapo kwa mgonjwa huyo alilazimika kurudi kituoni kumsaidia lakini alikuta mtoto mmoja ameshafariki dunia.

“Haikuwa zamu yangu ila nililazimika kurudi baada ya kusikia mganga aliyekuwa zamu kagoma kuwasaidia,” alisema Frida.

Ofisa mtendaji kata, Fdhila Nyamburapi na Mwenyekiti wa kitogoji cha Kazi, Samwel Nyakande walilaani kitendo hicho na kutaka sheria ichukue mkondo wake.

Ushauri kwa Mr Hashim Lundenga, Jitoe Miss Tanzania. Huaminiki tena

0
0
Nimeona kwenye habari hashim lundenga anaomba serikali imsaidie kutafuta wafadhili wa Miss Tanzania..

Kama yupo humu au jamaa yeyote aliyopo humu amfikishie huu ushauri.

Ni vizuri akakaa pembeni ya Miss Tanzania maana hakuna kampuni yeyote yenye akili itakayotoa pesa zake kwa Miss Tanzania ya lundenga...

Seke seke la Siti mtemvu ni kubwa sana limemvunjia sana trust... na kurudisha trust sio kazi ndogo.

Hata kama Lundenga anategemea shughuli za Miss Tanzania kupata hela yake ya kuishi... ni vizuri akatumia.mbinu za yeye kukaa pembeni na kuweka sura nyingine kama mwandaaji kwa ajili ya kupata trust ya mashabiki na wadhamini...

Ila yeye kama yeye mzee lundenga na skendo ya Siti Mtemvu hawezi fanikiwa tena kama enzi zile za zamani

Nakua Kama Chizi Kwa Wivu wa Mke Wangu...

0
0
Nina mke mmoja ambae tunapendana sana tatizo ana WIVU kupindukia.


  1. Ninapoingia tu home ananidaka na kuninusa nguo,akisikia pafyum kwa mbali MATATIZO,mim situmii pafyum ila usafiri wa kwetu ni shida,mnabana hadi kupumua shida Matokeo yake sipendi watu waniguse kitu ambacho ni kigumu kwenye usafiri wa jumuiya!



  1. Kila ninapoenda anataka nitume picha kwa whatsap hata kama kwenye daladala nimesimama anataka nipenye dirishan nipige hilo eneo au nijipige kitu ambacho watu hawakubali maana wanaona unawapiga wao!Hata wakati mwingine ananiambia chukua jiwe weka sehem flani then piga picha.

Hii inanifanya nionekane chizi mbele za macho ya watu ambao hawajui kinachoendelea..Nikikataa kufanya anachotaka ananuna siku nzima na Papucha nanyimwa

,JE NIFANYEJE MAANA NAMPENDA SANA

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano ya May 18, Ikiwemo ya Sheria Hatari Kwa Magufuli

0
0

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano ya May 18, Ikiwemo ya Sheria Hatari Kwa Magufuli

Tumbua Tumbua Yamgeuka Magufuli

0
0
DHANA ya utumbuaji majipu sasa imemgeukia Rais John Magufuli kutokana na kuongoza wizara iliyotawala na ubadhirifu wa fedha za umma, anaandika Regina Mkonde .

Katika Serikali ya Awamu ya Nne chini ya Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete, Dk. Magufili alikuwa Waziri wa Ujenzi – wizara ambayo inatajwa kujaa ubadhirifu wa pesa za umma na kwamba, rais huyo ameshindwa kuchukua hatua.

Kutokana na hali hiyo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imemtaka Rais Magufuli kutumbua majipu yake wake wakati akiwa kwenye wizara hiyo.

James Mbatia, Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano amesema, katika wizara hiyo kuna ubadhilifu wa fedha za umma.

Pia kumekuwepo na utendaji mbovu wa watumishi na kwamba, serikali haina mpango wa kuwachukulia hatua za kisheria wahusika kutokana na kutoonesha jitihada.

“Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inajiuliza kama  serikali ya awamu ya tano inafanya kazi yake kwa haki, uadilifu, uwazi na usawa kwa wote na hasa kwa kile kinachojulikana kama utumbuaji majipu, swali hapa ni nani amfunge paka kengele? au mkuki mtamu kwa nguruwe mchungu kwa binadamu?” amehoji Mbatia.
Wakati akitoa hotuba ya maoni ya kambi ya upinzani leo Bungeni mjini Dodoma kuhusu mapato na matumizi ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017 Mbatia amefafanua baadhi ya dosari zilizofanywa na wizara hiyo.

Moja kati ya dosari hizo ni kitendo cha Wakala wa Barabara nchini TANROADS cha kuitia hasara zaidi ya Sh. 5 bilioni serikali.

“TANROADS imebainika kuwa na utendaji mbovu kama ambavyo mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) alivyobaini juu ya usimamizi mbovu katika mikataba ya ujenzi wa barabaa na madaraja ambapo ilikuwa chini ya iliyokuwa wizara ya ujenzi katika serikali ya awamu ya nne,” amesema.

Mbatia ameongeza kuwa “TANROADS wakati wa kipindi hicho, iliitia hasara serikali ya jumla ya Shilingi 5,616,652,051 kutoka kwenye riba (interest) inayoongezeka kila siku kutokana na TANROADS kuchelewa kuwalipa wakandarasi 11.”

Amesema kuwa, hasara hiyo iligundulika kati ya kipindi cha mwaka 2012 na mwaka 2015 kwa mujibu wa Ripoti ya CAG ya Hesabu za Serikali Kuu wakati wa ukaguzi wa taarifa za fedha kwa mwaka ulioishia tarehe 30 Juni 2015 iliyotolewa mwezi Machi 2016 (Ukurasa wa 134 na 135).
Dosari nyingine ni ile ya serikali kuruhusu matumizi ya matairi yanayofahamika kwa jina la Super single tires ambayo yanaharibu barabara.

“Utafiti unaonesha matairi haya (super single tyres) yanaharibu barabara. Matairi haya yameanza kutumika takribani miaka mitano iliyopita na mzigo uliokuwa unabebwa na matairi 24 sasa unabebwa na matairi 12,” amesema.

Mbatia amesema, uruhusiwaji wa matumizi ya matairi hayo haukuwa wa busara kutokana na kwamba matokeo yake ni uharibifu mkubwa wa barabara.

“Uamuzi wa kuruhusu matairi haya haukuwa na busara maana barabara zetu hazijabuniwa kuhimili shinikizo la uzito (excessive pressure) linalotokana na matairi hayo,” amesema.
Ameitaka serikali kuzuia mara moja matumizi ya matairi hayo ili kuzinusuru barabara lakini pia kuokoa fedha za walipa kodi zinazotumika kurekebisha mara kwa mara barabara hizo na kunyima fursa maeneo mengine kupata barabara za kiwango cha lami.

Akizungumzia uuzwaji wa nyumba za serikali Mbatia amesema, serikali iliuza nyumba zake kwa bei ya hasara hivyo kuigharimu nchi.
“Katika muktadha huo kambi Rasmi ya Upinzani  inalikumbusha Bunge kwamba, kati ya mwaka 2002 mpaka 2004  Serikali iliuza nyumba  zipatazo 7,921 na mpaka mwaka 2008 Serikali ilikuwa imejenga nyumba 650 tu,” amesema.

Amesema kuwa, katika biashara ya kuuza nyumba zilizokuwa mali ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), serikali ilipata Sh. 252,603,000/-
ambazo haziendani na thamani halisi ya nyumba hizo.

“Hivi sasa serikali inahitaji kusaka nyumba  zaidi ya mara dufu ya kiasi hicho kujenga nyumba za fidia.
Kwa mujibu wa taarifa ya utekelezaji wa maazimio ya Bunge juu ya uuzaji wa nyumba za serikali kinyume cha taratibu, serikali itatumia Sh. 677,606,000/- kujenga nyumba mpya ili zirejeshwe kwa Tamisemi, Rejea taarifa ya Serikali Bungeni tarehe 25 April 2008,” amesema.
Mbatia amesema, waliouziwa nyumba hizo, kuna taarifa kuwa kati yao wapo walioziuza na kujipatia faida kubwa kinyume na mikataba ya mauzo hayo,na kwamba KRUB inapendekeza wanyang’anywe nyumba hizo kwa kukiuka mikataba na malengo ya mauzo.

“Kumbukumbu za taarifa rasmi za Bunge zinaonesha kwamba, serikali ilitoa taarifa ndani ya Bunge hili kuwa, kuna kamati iliundwa kuchunguza mchakato wa mauzo ya nyumba ya serikali.
“Kamati hiyo ilitegemewa kumaliza kazi mwezi Februari, 2007, lakini hadi Bunge la Tisa na Bunge la Kumi linamaliza uhai wake hakuna taarifa iliyotolewa na serikali. Kambi Rasmi ya Upinzani Buneni inaitaka serikali ya awamu ya tano irejeshe nyumba hizo,” amesema.

Mbatia amesema, kuna maadhimio kadhaa yaliyoadhimiwa na bunge ikiwemo kuitaka serikali kurejesha nyumba zilizouzwa kinyume cha taratibu na kwa watu ambao hawakuwa watumishi wa umma.
“Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imeiitaka Serikali kutekeleza azimio hilo la Bunge, na kwa njia hiyo ile kauli mbiu ya hapa kazi tu, iweze kutafsiriwa kwa vitendo,” amesema na kongeza;
“Tunajua uuzwaji huo ulisimamiwa na Wizara aliyokuwa akiiongoza yeye na kuna uwezekano mkubwa kwamba alisimamia maamuzi ambayo hakuwa na uwezo wa kuyakiuka.”

Amesema, sasa ni muda sahihi Rais Magufuli kurekebisha kasoro alizozisimamia na katika mchakato huo ili kurejesha imani katika jamii.

“Tukumbuke kuwa Rais Kikwete alielekeza nyumba hizo zirudishwe serikalini lakini alikosa uthubutu wa kusimamia kauli yake,” amesema.

Mtoto wa Chacha Wangwe Abadili Msimamo Mahakamani Kwenye Kesi ya Kuchapisha Taarifa za Uongo Mtandaoni

0
0
Mtoto wa Chacha Wangwe Akiwa Mikononi Mwa Polis
Mtoto wa aliyekuwa mwanasiasa machachari na Mbunge wa Tarime, Chacha Wangwe, amebadili msimamo mahakamani katika kesi ya kuchapisha taarifa za uongo kupitia mtandao wa kijamii, kuwa Zanzibar inakandamizwa na Tanzania Bara na kwamba ni koloni lake.

Mtoto huyo, Bob Chacha Wangwe (24), ambaye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alibadili msimamo jana aliposomewa shtaka hilo kwa mara ya pili, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Wangwe alipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza Mei 11, na alisomewa shtaka linalomkabili na alikiri kutenda kosa hilo.

Mshtakiwa anapokiri kosa, kwa kawaida Mahakama inaweza kumtia hatiani na kumpa adhabu kwa mujibu wa sheria, kulingana na kosa siku hiyo hiyo au siku nyingine yoyote.

Baada ya kusomewa shtaka na kukiri, Hakimu Mkazi Mkuu, Waria lwande Lema, aliamuru mshtakiwa huyo apelekwe rumande hadi jana, Mei 17, kwa kuwa hakimu aliyepangwa kusikiliza kesi hiyo hakuwapo.

Hata hivyo, jana mshtakiwa huyo alipopandishwa kizimbani na kusomewa shtaka hilo, ili kusomewa maelezo ya awali kabla ya Mahakama kumtia hatiani na kumhukumu, tofauti na siku ya kwanza, alikana kutenda kosa hilo.

Kutoka na mshtakiwa huyo kukana kosa, Wakili wa Serikali, Salim Msemo, aliieleza Mahakama kuwa upelelezi bado haujakamilika, hivyo aliiomba ipange tarehe nyingine ya kutajwa kwa kesi hiyo.

Wakili wa mshtakiwa huyo Peter Kibatala aliiomba Mahakama impe dhamana kwa kuwa shtaka linalomkabili linadhaminika, maombi ambayo yalikubaliwa na aliachiwa kwa dhamana na kesi iliahirishwa hadi Juni 15.

Wangwe ambaye baba yake kwa sasa ni marehemu, anadaiwa Machi 15, jijini Dar es Salaam, alisambaza taarifa za uongo kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook.

Trump: Sitaelewana kabisa na Waziri mkuu wa Uingereza nikiingia madarakani

0
0
Donald Trump
Mgombea anaewania urais nchini Marekani Donald Trump ameonya kuwa hatakuwa na uhusiano mzuri na waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron — Ikiwa atakuwa rais wa Marekani.

Mwezi Disemmba, Bwana Cameron alimtaja Trump kama mtu mwenye “ubaguzi, mjinga, na mwenye makosa” kufuatia kauli yake kwamba ataweka marufuku ya muda ya kuingia Marekani dhidi ya waislam.

Bwana Cameron amekataa kufuta kauli zake dhidi ya Bilionea Trump , ambae anatarajiwa kuwa mgombea wa urais wa Marekani kupitia chama cha Republican katika uchaguzi wa mwezi Novemba.

Akizungumza katika kituo cha televisheni cha Uingereza ITV kwa mara ya kwanza mbele ya umma tangu akosolewe Bwana Trump, alisema yeye si mjinga ama mbaguzi stupid bali ni”muunganishi”.

Kuhusu kauli za Bwana Cameron, Bwana Trump alisema : “yaelekea hatutakuwa na uhusiano mzuri sana, nani anajua.
“natumai kuwa na uhusiano mwema na yeye, lakini inaonekana ni kama hataki kutatua tatizo.”

Donald Trump pia alimkemea Meya wa London , Sadiq Khan, kwa kumuita “mjinga”.
Alielezea kauli yake kama kosa na isiyokua na ya heshma, huku akimtaka Bwana Khan afanyiwe vipimo vya uwezo wa akili yake (IQ).

Charles Kitwanga : Serikali Haifichi Mkataba wa Lugumi

0
0
Charles Kitwanga
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga amesema serikali haifichi mkataba wowote ukiwamo wa Lugumi Enterprises, isipokuwa wabunge wanapaswa kufuata taratibu ili kuona mikataba hiyo kama kanuni zinavyowaelekeza.

Kitwanga alisema hayo juzi usiku bungeni wakati akifanya majumuisho ya mjadala wa hotuba yake ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2016/17. Kuliibuka mjadala mzito kuhusu masuala ya mikataba ukiwamo wa Lugumi na Jeshi la Polisi, kiasi cha kuwa moja ya sababu za wabunge wa upinzani kukataa kusoma maoni yao kuhusu hotuba hiyo ya Waziri Kitwanga.

Kitwanga alipojibu hoja za wabunge, alisema hakuna anayeficha mikataba yoyote katika wizara hiyo kwani hata hiyo mikataba inayozungumzwa aliiwasilisha katika Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama alipotakiwa kufanya hivyo.

“Hata huu mkataba wa Lugumi unaweza kuonwa na mbunge yeyote ila kuna taratibu zake. Pia wabunge msisahau haya ni masuala ya usalama, yanaiweka nchi katika hali ya utata,” alisema Kitwanga. Aliendelea, “Mkataba upo na uko wazi, lakini hizi kelele za magazeti zinaiweka nchi katika hatari.

Hakuna anayeficha kitu, lakini tufuate taratibu zilizowekwa. Tunapiga kelele sana. Tunalo (wabunge) jukumu la kulinda usalama. Tufuate taratibu zilizo sahihi kuomba taarifa tunazohitaji.” Kitwanga alisema amesikitishwa na maneno yaliyowekwa katika maoni ya Kambi ya Upinzani ambayo yalitakiwa kufanyiwa marekebisho kabla ya kusomwa bungeni juzi asubuhi.

“Baada ya kusoma bajeti mbadala nimesikitika sana. Bila CCM nchi hii haina serikali mbadala. Yaani hotuba nzima imejaa rejea ya magazeti. Kambi ya Upinzani iliyopo ni kambi ya upingaji,” alisema Waziri Kitwanga.

Alisema badala ya wapinzani kujikita katika rejea ya magazeti na maneno ya kusikia, alitarajia waseme kile wanachowaza wao. “Niko serikalini kwa miaka 35 sasa. Natambulika kama Mr STK, Mzee wa STK – Sheria, Taratibu na Kanuni.

Nimewasilisha fomu yangu Sekretarieti ya Maadili kwa mara ya kwanza mwaka 1998. “Hivyo vinatosha kuwapa taarifa mimi ni mtu wa aina gani, sipendi kusema, napenda kutenda,” alisema Kitwanga ambaye ni Mbunge wa Misungwi mkoani Mwanza.

Akijibu hoja nyingine, alisema uhakiki wa madeni ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) unaendelea. Alisema zipo taasisi tatu za umma; Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) na Mamlaka ya Ununuzi wa Umma (PPRA) zinafanyia kazi masuala mbalimbali ndani ya Nida.

Alisema Sh bilioni 50 zipo Hazina na ziko tayari kulipa wafanyakazi ambao waliamuriwa kuachishwa kazi. Hata hivyo alisema, hilo litafanyika kwa uhakiki ili kutolipa wafanyakazi hewa.

Alikiri kuwa askari hawana makazi mazuri na bado maslahi yao ni ya kiwango cha chini. Alisema serikali inayafanyia kazi ikiwamo ujenzi wa nyumba za kuishi pamoja na kuongeza mishahara yao.

Akijibu hoja za wabunge kuhusu kuongezwa fedha kwa Nida ili ikamilishe kazi zake mwishoni mwa mwaka huu, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango, alisema fedha zilizotengwa kwa mamlaka hiyo katika bajeti zinatolewa ili kazi zifanyike.

MAISHA: Uzuri wa Mke ni Tabia. Je, Uzuri wa Mume ni Nini?

0
0
Huwa nasikia mara nyingi watu wakisema na hata kuimba ni nini. Msisitizo umekuwa kuweka vigezo vya kijumla kwa mwanamke, sijaona kukiwa na msisitizo wa vigezo vya jumla kwa wanaume.

Ninajua kila mwanamke anakuwa na vigezo vyake binafsi vya kuchagua mume anayefaa.

Naomba waungwana kujuzwa endapo kuna vigezo vinavyoweza kuangaliwa na wanawake kupima uzuri wa mume.

Nawasilisha.
Viewing all 104415 articles
Browse latest View live




Latest Images