Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104747 articles
Browse latest View live

Msigwa: Serikali na Wabunge 250 Kuogopa Hotuba ya Kurasa 30 Hawawezi Kuongoza nchi

$
0
0
Msigwa anasema,

''Serikali imepewa mamlaka ya kuongoza nchi na inajinadi bungeni kuwa wanaongoza vizuri na wapinzani nao wanakuja kuwarekebisha kuwa hoja zao haziwezekani , sasa serikali inayosema 'hapa kazi' inayoungwa mkono na wabunge 250 wa chama cha mapinduzi inashindwa kujibu hotuba ya kurasa 34, inataka kuwaambia nini watanzania?

Je, mpo matured kuiongoza serikali? Njooni na hoja muonyeshe udhaifu wa upinzani uko wapi, muwashawishi watanzania kuwa kweli mnaweza kuongoza lakini hamuwezi kukabiliana na hoja mnaweka mpira kwapani mnataka msaidiwe na refa ,are you fit to lead this country?

Nani asiyejua mizengwe ya nyumba zilizouzwa nchi hii? nani asiyejua nchii hii ina mikataba mibovu?''

''Huyu Rais mwema ambaye anatakiwa kushangiliwa kama King Kanuti, hatakiwi kuguswa katika bunge hili?''

Msigwa anaendelea kuongea wabunge wengine wanazomea wengine wanashangilia chaos tupu.

Sikiliza hapa:



Deal ya Ali Kiba na Sony, Makosa Yanayojirudia

$
0
0
Huko kwenye mitandao ya kijamii kumechafuka habari ya Ali kusign deal na Sony wengi wakiamini huo ndio utakuwa mwanya wa msanii huyo kutoboa kimataifa.. Jambo ambalo mashabiki wake wanashindwa kuelewa ni kuwa huo unaweza kuwa anguko la King Kiba badala ya kuwa neema..

Kwanza kabisa kitu ambacho hawakielewi ni kuwa Ali hajasaini na Sony Music Ent. BMG (ishu yake sio 'global deal') bali amesaini na Sony Music Africa ambayo ni subsidiary ya Sony Music Entertainment!! Kwa ninavyoelewa Sony Music Africa wana sambaza mziki na kumanage wanamuziki ndani ya Africa pekee.. Sasa eidha Ali hajui alichosaini au chumvi inaongezwa kunogesha habari..

Kingine watu wanaona hii ni kama Bahati Ali amepata wanachoshindwa kuelewa ni kwamba wasanii wakubwa Africa huwa wanakataa kusign na hizi kampuni zenye asili ya marekani na ulaya kutokana na kampuni hizi kushindwa kutimiza malengo na kutoelewa mazingira ya soko la mziki Africa! Kwa mfano wasanii wote ambao wamewahi kusign na Sony karibia wote walikuja kufa kimuziki kutokana na Sony kushindwa kuwa market kutokana na kutoelewa mziki wa Africa; mfano wasanii kama Nakaaya Sumari, Nneke Egbuna (Nigeria), Luncvile (SA), Nathan Ro (SA) wote hawa wamepotea kwenye mziki..

Mfano mwingine ni msanii D'banj ambaye aliondoka Mavins na kujiunga na label ya GodLife chini ya kanye west, mpaka sasa D'banj anasafiria jina lake tu lakini kimuziki ameshuka vibaya sana!! Kampuni za kimarekani hazina record ya kuwatoa wasanii wa kiafrika na hii inatokana na kutoelewa industry yetu na ndio maana Psquare walikataa mabilioni waliyotaka kupewa ili wasign Convict records..

Kingine kinachosemwa na watu ni kwamba hizi kampuni zina mambo mengine makubwa zaidi kwahiyo inakuwa nguvu kwao kuwa serious sana na mwanamuziki mmoja mmoja; kwa mfano kampuni mama ya Sony Music Africa (Sony Entertainment BMG) ina zaidi ya label 25 ndogo ndogo kama hii aliyosign kiba na ina wasanii karibia katika kila nnchi ya ulaya, Asia na Amerika ya kusini. Wana zaidi ya wasanii elfu moja wanaowasimamia so inakuwa ngumu kwao kutoa macho kwa msanii mmoja mmoja na ndio maana wasanii wengi wakubwa wa Africa wanakataa kusign chini yao wanaona ni afadhali watengeneze timu zao wenyewe za management ambazo macho yao na attention yote itakuwa kwao wao kama wasanii..

Anyways, let me just assume management ya Ali inafahamu vitu ambavyo mimi sivifahamu na wamefanya research ya kutosha kabla ya kusign na hatimaye watatuprove wrong wote ambao tuko sceptical about this deal.!!
Kama kijana mwenzangu namtakia kilala kheri na mafanikio katika safari yake mpya...

By The bold

Nay wa Mitego: Gigy Money Anatafuta Kiki Kwangu

$
0
0
MKALI wa Ngoma ya Saka Hela, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ ameamua kumfungukia muuza nyago kwenye video za Kibongo, Gift Stanford ‘Gigy Money’ kuwa anatafuta kiki kutumia jina lake katika mahojiano anayofanya na vyombo mbalimbali vya habari.

Akichonga na Showbiz Xtra, Nay alisema kuwa amekuwa akisikia juu ya Gigy akimsema si chochote kwake na kwamba ni mbahili alishawahi kumlipa elfu ishirini baada ya kumaliza kutengeneza video zake.


 “Yaani huyo Gigy anatafuta kiki, namshangaa sana kila sehemu kunisema hovyo, kwanza hatuendani kwa chochote,” alisema Nay.

Hivi karibuni katika mahojiano na Global TV Online, Gigy alisikika akimponda Nay kuwa ni mtu bahili na haitakuja kutokea yupo naye iwe kikazi ama vyovyote kwa kuwa hana hadhi ya kuwa naye.

Ukiona Haya Kwa Mkeo Kuwa Dikteta Haraka la Sivyo....

$
0
0
Kama mkeo anasali kwa walokole au amehamia kusali kwa walokole ndugu yangu hakikisha unamdhibiti sana na mapema kabla hajaharibiwa asali akiwa anajitambua

Wachungaji wa Kilokole(wanajiita manabii) kwa sababu sadaka inayotolewa kanisani huwa ni ya kwao(tofauti na Roma na Sabato ambako sadaka inapelekewa uongozi wa juu)

Basi kipato cha wachungaji hawa hutegemea waumini zaidi katika utoaji wa sadaka zao.

Asilimia kubwa wamekuwa wakiwatumia wanawake kwa sababu ni wepesi kuhadaika!

Mke wako anajazwa upepo wa kiimani na kufikia kuwa na mapenzi na imani yaliyopitiliza mipaka!

Ukianza kuona mkeo anabadilika taratibu ndani maombi ya kukemea yanazidi,muda wa kanisani unazidi na matoleo yanazidi kule kanisani ndugu tangu kuwa dikteta ghafla na hata ikiwezekana mzuie kama hawez kusali kawaida tu kwa kumtegemea mungu aache tu

Ukipuuzia jiandae kwa mkeo kutumia kipato chake chote kanisani/ mkeo kutumia robo tatu ya muda wake wote kanisani( kukesha na kila weekend kushinda wakimsaidia nabii wao kazi) hapa mpaka kazi zake kama mke anasahau

Ukicheza anafikia hatua ya kuliwa kabisa!

Mara nyingi wengi wetu tumeshakutana na kesi za hivi! Mke anapeleka kila kitu kanisani vikiisha ndo anashtuka alikuwa anaibiwa!

Sijaongea hivi kuharibia wachungaji wa kilokole hapana ila na wao nawashauri waache kutumia imani kutapeli na kuvunja ndoa za watu

Tumieni imani kuokoa na kusaidia watu ili waje kuupata wokovu na sio kutumia imani kujitajirisha


Kwa nitakayemkwaza anisamehe lakini huu ndio ukweli

Nawasilisha!!

Lema Akichangia Hotuba ya Wizara ya Nishati na Madini, Manji Anaila TANESCO

$
0
0
Akichangia bajeti ya Wizara ya Nishati Na Madini leo Bungeni Mh.Lema ameishangaa kampuni ya TANESCO kumpa tenda Manji kuagiza Transformer toka India wakati Malawi Na Msumbiji wananunua Transform toka Tanzania.

"Mheshimiwa Mwenyekiti inashangaza kuona Malawi Na Msumbiji wakinunua Transformer toka Tanzania, lakini TANESCO wamekuwa wakimtumia Manji Na kumpa Tenda ya kuagiza Transformer toka India kwa bei ya Mara mbili hadi Tatu zaidi ya bei iliyopo nchini."
nememunukuu Leama

NB: Hii nchi ngoja Magufuli aindeshe kichizi chizi kwanza hadi tukae sawa, maana kwa tulikofikia inahitaji akili ya kiuendawazimu kuirudisha.

Asante Lema kwa kumsaidia Rais kutumbua majipu.!

Diamond ni Noma! Achaguliwa Tena Tuzo za BET Marekani

$
0
0
Best International Act Africa

AKA (SOUTH AFRICA)
BLACK COFFEE (SOUTH AFRICA)
CASSPER NYOVEST (SOUTH AFRICA)
DIAMOND PLATNUMZ (TANZANIA)
MZVEE (Ghana)
SERGE BEYNAUD (COTE D’IVOIRE)
WIZKID (NIGERIA)
YEMI ALADE (NIGERIA)

Pongezi nyingi kwa Diamond Platinumz kuzidi kuupeleka muziki wetu mbali. Kikubwa tuendelee kumpa sapoti balozi wetu huyu wa muziki wetu.

Kuwa nominated pekee ni ushindi tosha.

Sakata la Escrow na IPTL Laibuka Upya Bungeni

$
0
0
Kambi ya upinzani imeliibua upya  bungeni sakata la Escrow, Richmond na umiliki wa kampuni ya IPTL, huku ikihoji sababu za Rais John Magufuli kutoheshimu maazimio ya Bunge ya kumwajibisha Sospeter Muhongo, badala yake kumteua tena kuwa Waziri wa Nishati na Madini.

Hoja hizo ziliibuliwa na Waziri Kivuli wa Nishati na Madini, John Mnyika wakati akiwasilisha maoni ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2015/16 na makadirio ya matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka 2016/17.

Muhongo alikuwa akiiongoza wizara hiyo wakati kashfa ya uchotwaji wa zaidi ya Sh300 bilioni kutoka kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow iliyofunguliwa kuhifadhi fedha za malipo umeme kusubiri kumalizika kwa mzozo wa kimkataba baina ya kampuni ya IPTL, inayozalisha umeme  na Shirika la Umeme (Tanesco).

Bunge lilimuona Profesa Muhongo kuwa alishindwa kuwajibika na kusababisha Serikali kupoteza mapato.

Profesa Muhongo alilazimika kujiuzulu wadhifa huo saa chache kabla ya Rais wa Serikali ya Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete kutangaza baraza jipya.

Hata hivyo, Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma lilimsafisha na kashfa hiyo iliyohusisha malipo yaliyofanywa kwa mawaziri, majaji, wabunge na watumishi waandamizi wa umma.

Jana, Mnyika, ambaye ni mbunge wa Kibamba (Chadema), alirejea maazimio ya Bunge la Kumi akisema lilishafanya maamuzi kuhusiana na mikataba ambayo Serikali inaingia na kampuni mbalimbali, hasa kwenye sekta ya nishati na madini.

“Katika maazimio ya Bunge kuhusiana na fedha, ufisadi uliofanyika katika akaunti ya Tegeta Escrow na umiliki wa IPTL yanayohusu sekta ya nishati na madini, bado hayajatekelezwa kwa ukamilifu wake,” alisema Mnyika.

 Akinukuu Azimio Namba 2, Mnyika alisema liliagiza kwamba Serikali iangalie uwezekano wa kununua mitambo ya kufua umeme ya IPTL na kuimilikisha kwa Tanesco kwa lengo la kuokoa fedha inazolipa kwa kampuni hiyo binafsi.

Alisema kambi hiyo inasikitika kuona kwamba mbali ya Serikali kushindwa kununua, bado inaendelea kulipia gharama za uwekezaji na hivyo kuendelea kukiukwa kwa azimio hilo.

Akizungumzia azimio la saba linalohusu kuwajibishwa kwa mawaziri na watendaji wakuu wa wizara na bodi ya Tanesco, Mnyika alisema Profesa Muhongo naye aliwajibishwa kwa uteuzi wake kutenguliwa, lakini Rais Magufuli amemteua tena kuongoza wizara hiyo.

“Rais bila ya kujali nini Bunge lilishaazimia katika kikao ambacho na yeye alikuwa sehemu ya azimio hilo, akamteua Muhongo kuendelea kuiongoza wizara hii. Kambi ya upinzani inaliona jambo hili kama ni dharau sana kwa Bunge na ni fedheha binafsi kwake,” alisema.

Alisema kambi ya upinzani imelazimika kunukuu maazimio hayo kutokana na ukweli kwamba Serikali imeshindwa kabisa kutekeleza maazimio ya Bunge na badala yake mikataba hiyo inaendelea kutekelezwa kama ilivyoingiwa.

“Mfano mzuri ni Tanesco kuendelea kuilipa IPTL fedha za capacity charge mpaka sasa. Jambo hili linazidi kuliondolea shirika hilo la umeme uwezo wa kuwahudumia wateja wake kwa kuwa haliwezi kuwekeza zaidi katika miundombinu ya kusambaza umeme kutokana na kutokuwa na fedha za kutosha,” alisema.

Serengeti Boys yatoka sare na Korea Kusini watinga nusu fainali mashindano ya (AIF Youth Cup 2016 U-16)

$
0
0
Timu ya soka ya taifa ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ Mei 19, 2016 wametinga hatua ya nusu fainali baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 na Korea Kusini katika mfululizo wa michuano maalumu ya kimataifa iliyoandaliwa na Shirikisho la Soka nchini India (AIF Youth Cup 2016 U-16).

Katika mchezo huo uliofanyika uwanja wa Tilak, Maidan mjini Goa, India, mabao ya Serengeti yalifungwa na Assad Juma katika dakika ya 12 na Maulid Lembe katika dakika ya 87 ambaye alisawazisha baada ya Korea kutangulia kwa mabao 2-1. Matokeo hayo yanaifanya Serengeti Boys ifikishe pointi tano na kwamba inasubiri matokeo ya mwisho kati ya Korea Kusini na Marekani yatakayotoa mwanga wa timu itakayocheza fainali.

Serengeti Boys watashuka dimbani tena dhidi ya Malaysia Mei 21, 2016,Fainali ya michuano hiyo itachezwa Mei 25, 2016 na kabla ya mchezo wa fainali, utachezwa mchezo wa mshindi wa tatu katika uwanja huo huo Tilak Maidan, Vasco, Goa nchini India. India imeandaa mashindano ya vijana wenye umri chini ya miaka 17, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kikosi chao kwa ajili ya fainali za kombe la dunia kwa Vijana zitakazofanyika nchini humo mwaka 2017.

Lady Jaydee Kumuanika Mpenzi wake Ambae ni Mrithi wa Gardner Leo!

$
0
0
Exclusive! Lejendari wa Bongo Fleva kwa zaidi ya miaka kumi na tano, Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee au Jide’, anatarajia kumuanika mrithi wa aliyekuwa mumewe, Mtangazaji wa Kituo cha Radio CloudsFM, Gardner G. Habash ndani ya saa 24, Ijumaa lina data kamili.

HABARI ZA KUAMINIKA
Kwa mujibu wa habari za kuaminika zilizothibitishwa na uongozi wa staa huyo, Jide atamtambulisha mchumba wake huyo kwa mara ya kwanza ndani ya Ukumbi wa Mlimani City leo, Dar ambapo pia atafanya shoo ya saa tatu mfululizo, inayokwenda kwa jina la Naamka Tena.
“Itakuwa ‘sapraizi’ kwa mashabiki wote wa Jide ambapo sapraizi hii itaendana na shoo ya kihistoria ya Naamka Tena atakayoipiga kwa saa tatu akiwa na bendi yake (Lady Jaydee and The Band),” alisema mmoja wa viongozi wanaomsimamia ambaye hakutaka kutajwa gazetini.


JIDE ALIPOTOKEA
Jide alifunga ndoa na Gardner Mei 14, 2005 ambapo waliishi na kufanikiwa kuwa na mali mbalimbali ikiwemo ujenzi wa nyumba, Ukumbi wa Nyumbani Lounge na Bendi ya Machozi

FIGISUGISU NA GARDNER
Mvutano wa wawili hao ulidaiwa kuanzia kwa Jide aliyeamua kuomba talaka kwa kile kilichosemekana kuwa Gardner alipata kazi ya kutangaza redio moja nchini Kenya hivyo kama angeenda huko wakati ni meneja wake, angeshindwa kuwa naye huku pia figisufigisu nyingine nyingi zikijitokeza kama kubadilisha jina la Ukumbi wa Nyumbani Lounge na kuwa M.O.G na mambo mengine ikiwepo kusalitiana na kupigana.

WAFIKISHANA MAHAKAMANI
Baada ya mvutano wa muda mrefu, wawili hao walifikia hatua ya kufikishana katika Mahakama ya Mwanzo ya Manzese jijini Dar, miezi michache iliyopita na mahakama kuamua kuvunja rasmi ndoa yao ya Kikristo na kila mmoja kupewa hati yake ya talaka.

Chanzo: Global Publishers

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Ijumaa ya May 20, Ikiwemo ya Sinema Mpya Sakata la Lugumi

$
0
0


SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Ijumaa ya May 20, Ikiwemo ya Sinema Mpya Sakata la Lugumi

Sakata la Mauaji Msikitini Mwanza: Kundi la Kigaidi la ISIS lahusishwa

$
0
0
YADAIWA ni kisasi baada ya Polisi kuwakamata wanaharakati wa IS saa 24 kabla.

"baada ya swala kumalizika, watu hao waliingia na kuwaamuru kulala chini huku wakitoa bendera nyeusi na maandishi ya meupe ya Kiarabu kisha kumtaka Imamu wa msikiti kujitokeza mbele, bendera hiyo ni kama ile inayotumiwa na kundi la kigaidi la IS"

"Imamu alipojitokeza huku tukiwa tumelala chini, watu hao walisikika wakisema 'Kwa nini mnaswali wakati wenzetu wamekamatwa na polisi, wengine wanapigana 'jihad'...hali hiyo ilitushtua zaidi baada ya Imamu kuanza kuchinjwa kwa panga,"

"Ghafla wakatuamuru kulala kifudifudi na kudai wao ni IS wamekuja kufanya kazi yao, kisha wakaanza kutushambulia na kujeruhi. Mwenzangu niliyekuwa naye pembeni alikatwa panga na kuangukia juu yangu, hali hiyo ilinifanya nionekane kama nimekufa,"

Habari za uhakika ambazo Nipashe imezipata zinasema. Imam huyo na wafuasi wake, waliuwawa na kundi la watu wanane waliokuwa na bunduki moja, mapanga, mashoka na majambia, kwa kuchinjwa ndani ya msikiti na watu wanaosemekana ni washirika wa Kundi la kigaidi la Dola ya Kiislamu (IS), ambalo linaendesha harakati zake katika nchi mbalimbali za Mashariki ya Kati.

Waliouawa katika tukio hilo ni Imamu Feruz Elias (27), mkazi wa Ibanda Relini, Mbwana Rajab (40), mkazi wa Ibanda na Khamis Mponda (28) mkazi wa Mkolani.

Habari kutoka ndani ya duru za uchunguzi mkoani Mwanza, zilizopatikana jana, zilisema polisi ilikuwa ikifuatilia mienendo ya kikundi kinachoonekana kuwa cha kigaidi na kufanikiwa kukamata wafuasi kadhaa kabla ya kutokea mauaji hayo juzi.

"Uwezekano wa kuwapo kwa uhusiano baina ya wauaji hao na kikundi cha kigaidi kinachosakwa na polisi, unatokana na ukweli kuwa kabla ya kufanya mauaji hayo, watu hao walihoji kuwapo kwa ibada hiyo wakati "(Waislamu) wenzetu wamekamatwa na polisi."

Imam wa msikiti na wafuasi hao katika barabara ya kwenda Shinyanga, waliuwawa wakati wa ibada ya saa 2:00 usiku na watu hao waliokuwa na bendera nyeusi yenye maandishi meupe ya Kiarabu kama bendera ya IS na pia wakiwa wameficha nyuso zao.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi, alisema kuwa bado wanaendelea na uchunguzi ili kufahamu kama tukio hilo linahusiana na ugaidi au la.

Habari za kiuchunguzi zinadai polisi ilishtushwa na kuwapo kwa mauaji ya watu yanayodaiwa kuwa ya ujambazi, lakini bila kuwapo kwa ulazima wa majambazi kuwaua watu hao walioporwa mali zao pia.

Chanzo kimoja cha habari kutoka duru za uchunguzi kilisema kwa kawaida, jambazi huwa haui mtu kama hapakuwa na ubishi katika kusalimisha mali au fedha zinazoporwa. Pamekuwa na matukio ya mauaji ya wafanyabiashara ya mara kwa mara, katika maduka ya simu na kutuma na kupokea fedha, ambayo yamegharimu maisha ya takriban watu wanne tangu kuanza kwa mwaka huu mkoani Mwanza.

Katika kufuatilia mauaji hayo, ndipo vyombo vya usalama vilipogundua kuwapo kwa kikundi cha kigaidi mkoani humo.

MASHUHUDA WASIMULIA

Mashuhuda walionusurika katika tukio hilo, wakizungumza na Nipashe jana eneo la msikiti huo, walisema majira ya saa 3.00 juzi usiku baada ya kumaliza swala, waliingia watu wapatao 10 wakiwa wameshika mashoka, mapanga na majambia na kuwaamuru waumini wote kulala kifudifudi.

WALIONUSURIKA

Kijana aliyenusurika katika tukio hilo, Abubakari Makabwa (19), alisema baada ya swala kumalizika, watu hao waliingia na kuwaamuru kulala chini huku wakitoa bendera nyeusi na maandishi ya meupe ya Kiarabu kisha kumtaka Imamu wa msikiti kujitokeza mbele.

Bendera hiyo inafanana na ile inayotumiwa na Kundi la IS.

"Imamu alipojitokeza huku tukiwa tumelala chini, watu hao walisikika wakisema 'Kwa nini mnaswali wakati wenzetu wamekamatwa na polisi, wengine wanapigana 'jihad'...hali hiyo ilitushtua zaidi baada ya Imamu kuanza kuchinjwa kwa panga," alisema Makabwa.

Alisema baada ya Imamu kukatwa kwa panga shingoni, wauaji hao walianza kuwachinja wengine waliolala kabla ya amri ya kutoka kwa mmoja wa wauaji hao, kuwaamuru watoto kuondoka ndani ya msikiti huku wakiendelea kuwachinja wengine.

Makabwa alisema baada ya kutoka akiwa anakimbia na wenzake wanne kupitia mlango wa nyuma, walikutana na mtu mwingine akiwa ameshika bunduki akilinda usalama nje, hali iliyowatia shaka zaidi.

"Tulisikia sauti ya yule mwanamke aliyekuwamo ndani akisema wapige risasi hao. Tulilala vichakani na wala hatukuonekana kutokana na wauaji hao walipofika msikitini walizima taa zote, lakini mshika bunduki hakuweza kurusha risasi yoyote," alisema.

Aidha, alisema baada ya kufanikiwa kukimbia, watu hao walirusha bomu la mafuta ambalo lililipuka huku lingine likishindwa kulipuka ndani ya msikiti huo.

Naye manusura mwingine, Abeid Gati, alisema awali baada ya watu hao kuingia ndani ya msikiti huo, alidhani ni askari polisi hivyo kumfanya akae chini.

"Ghafla wakatuamuru kulala kifudifudi na kudai wao ni IS wamekuja kufanya kazi yao, kisha wakaanza kutushambulia na kujeruhi. Mwenzangu niliyekuwa naye pembeni alikatwa panga na kuangukia juu yangu, hali hiyo ilinifanya nionekane kama nimekufa," alisema Gati.

Alisema baada ya tukio, alikaa kwa muda mrefu kama mfu hadi waliporusha chupa ya mlipuko na kuunguza ndoo kubwa ya plastiki na nyingine ilishindwa kulipuka, ndipo alikimbia nje kutoa taarifa kwa mwenyekiti wa serikali ya mtaa.

MWENYEKITI WA MTAA

Mwenyekiti wa mtaa wa Utemini, Jukaeli Kiula, alisema alipata taarifa za tukio hilo saa 3:20 usiku kutoka kwa mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Said, aliyekuwa mmoja wa waumini wa msikiti huo.

"Baada ya taarifa hizo, tulikusanyana kama 'wananzengo' (wanajamii) na kwenda msikiti hapo, tuliwakuta watu watatu wakiwa wamepigwa mapanga na kujeruhiwa vibaya sana, nilipiga simu polisi nao walifika eneo la tukio muda mfupi baadaye," alisema Kiula.

Kiula alisema msikiti huo una waumini zaidi ya 20 wanaoswali hapo, hivyo baada ya kuvamiwa na watu hao walishindwa kujitetea kwa lolote kutokana na mazingira yaliyopo kwenye msikiti huo.

Katika hatua nyingine aliwaomba, wananchi wa mtaa huo kutoa ushirikiano ili watu hao waweze kupatikana kwani ni sehemu ya watu waliopokelewa na kuhifadhiwa na jamii ya eneo ulipotokea uhalifu huo.

MCHUNGA NG'OMBE

Eneo lililotokea mauaji hayo kuna misikiti miwili huku mmoja ukimilikiwa na dhehebu lililopo chini ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) na mwingine uko chini ya Aswar al Sunn.

Mchunga ng'ombe anayechunga maeneo karibu na msikiti wa Sunn, Mussa Masanja, alisema kuna eneo ambalo linamilikiwa na msikiti huo, huwa anawashuhudia vijana wakifundishwa mchezo wa ngumi na karate karibu na mlima.

"Nilikatazwa na mtu mmoja wa msikiti wa Sunn kuchungia ng'ombe kwa madai nitaharibu miti, lakini baada ya kuchungulia kwa mbali niliwaona watu wazima wawili wakiwafundisha ngumi na karate vijana hali iliyonitisha," alisema Masanja.

KAMANDA WA POLISI

Akizungumzia tukio hilo, Msangi alisema juzi saa 2.30 usiku, katika msikiti huo, watu wasiozidi 15 wakiwa wamevalia 'kininja' huku wakiwa na silaha mbalimbali kama mashoka, mapanga na bendera nyeusi yenye maandishi meupe, waliingia ndani ya msikiti huo na kuzima taa.

"Watu hao walisikika wakiwaambia waumini hao, kwanini wanaswali wakati wenzao wamekamatwa na kushikiliwa na polisi, hali iliyowafanya waanze kuwashambulia papo hapo,"alisema Kamanda Msangi.

Msangi alisema watu hao waliwashambulia kwa silaha hizo watu wanne msikiti hapo na kuwajeruhi vibaya kichwani na shingoni, lakini kati yao watatu walifariki dunia na mwingine mtoto wa miaka 13, kujeruhiwa.

Hata hivyo, alisema baada ya tukio hilo, polisi mkoani hapa inawashikilia watu watatu huku msako mkali wa kuwasaka wengine ukiendelea maeneo mbalimbali ya mkoa huo.

Source: Nipashe

Serikali Yajibu Hoja za Kivuko cha MV Dar es Salaam na Uuzwaji wa Nyumba Zake

$
0
0
Serikali imejibu hoja za upinzani kuhusu uuzwaji wa nyumba za Serikali na kutetea ununuzi wa kivuko cha MV Dar es Salaam ambacho kilitakiwa kufanya safari zake kati ya Dar na Bagamoyo.

Hoja hizo ziliibuliwa katika hotuba ya Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani kwa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, James Mbatia akitaka kutekelezwa kwa azimio la Bunge la urejeshwaji wa nyumba hizo serikalini lililotolewa Aprili 2008.

Pia, ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ilibainisha upungufu katika kivuko cha MV Dar es Salaam ambao ni kutolipiwa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), kutokuwa na kasi kadri ya mkataba na kutokuwapo hati ya makabidhiano.

Hoja hizo za upinzani zilijibiwa juzi jioni na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa ambaye alisema hakuna taratibu zozote zilizokiukwa wakati wa ununuzi wa kivuko hicho ambacho kwa zaidi ya mwaka hakijaanza kazi.

Alisema wizara ilipata taarifa ya CAG ambayo ilibainisha upungufu kadhaa ikiwa ni pamoja na kivuko hicho kununuliwa kwa Dola za Marekani 4.9 milioni (Sh7.9 bilioni) bila kulipiwa VAT, lakini akasisitiza kwamba hakukuwa na ukiukwaji wowote wa taratibu za ununuzi.

“Ni kweli kivuko kina mapungufu ikiwamo kasi ndogo, lakini hakuna ukiukwaji wowote wa taratibu wakati wa ununuzi. Temesa ilitangaza zabuni na baada ya maombi kupitiwa, kampuni ya MS Jones Gram Hansen ilishinda zabuni hiyo kwa kuwa na bei nafuu,” alisema Profesa Mbarawa.

Alisema baada ya kivuko kuletwa nchini Desemba 2014, kilifanyiwa majaribio na kubainika kwamba hakikuwa na kasi ya kuridhisha. Alisema makubaliano yalikuwa ni kujenga kivuko chenye kasi ya nots20, lakini hicho kilikuwa na kasi ya nots 15.7.

Kutokana na hali hiyo, alisema Serikali ilimtaka mkandarasi kurekebisha kasoro hiyo kwa gharama zake na kuwa ameshawasilisha andiko juu ya namna atakavyoifanya kazi hiyo.

“Mpaka sasa mzabuni huyo hajalipwa asilimia 10 ya malipo yaliyokubaliwa mpaka pale atakapokamilisha kazi hiyo. Kwa hiyo, taratibu zote zilifanyika kwa mujibu wa sheria,” alisema.

Kuhusu nyumba, Profesa Mbarawa alisema Serikali iliidhinisha mpango huo Aprili 24, 2008 baada ya kupata ridhaa ya Bunge ilipopeleka suala hilo kujadiliwa.

“Suala la uuzwaji wa nyumba za Serikali, pia taratibu zilifuatwa. Serikali ilileta mpango huo bungeni na kupata ridhaa ya wabunge wote. Kwa hiyo, niwaambie tu wabunge kwamba suala hili lilipata baraka zao,” alisema waziri huyo.

Uuzwaji wa nyumba za Serikali na ununuzi wa kivuko cha Mv Dar es Salaam vilifanyika wakati Rais John Magufuli akiwa waziri wa ujenzi kwa nyakati tofauti.

Kambi ya upinzani imekuwa ikisisitiza kwamba kuna ukiukwaji wa sheria uliofanyika wakati wa uuzaji wa nyumba na ununuzi wa kivuko hicho. Hata hivyo, Serikali imeshikilia msimamo wake kwamba sheria zilifuatwa.

Huyu Alikiba Mumuache Kwa Kweli- Wema Sepetu

$
0
0
Msanii wa filamu nchini Wema Sepetu amefunguka na kusema kuwa msanii Alikiba ni mtu wa kumuacha kutokana na uwezo wake wa kuimba na namna ambavyo anaweza kuipangilia sauti yake kwenye muziki.

Wema Sepetu amezidi kuonyesha mapenzi aliyonayo kwenye kazi za msanii Alikiba na kusema huwa zinamkosha sana na kudai hajawahi kumuangusha siku zote

"Ila huyu bichwa wangu mimi ananikoshaga sana. Na mumuachage tu kwakweli. Bichwa una sifa lakini maana si kwa Vocal hizi. Halafu mimi siwezi kukubania namba bana. Naupenda sana huu wimbo jamani. Wajua kutukunaga mashabiki wako. Good work Bichwa wangu Officialalikiba did it again ladiez & Gentlemen" aliandika Wema Sepetu

Mbali na hilo Wema Sepetu amempa pongezi msanii Alikiba kwa kuweza kusaini mkataba chini ya kampuni ya muziki ya 'Sony Music' na kusema kuwa alistahili hilo na zaidi ya hilo kwani anakipaji kikubwa.
" God Grants accordingly... Congrats Bichwa wangu for that Big Contract... You deserve it & more... Time Heals all wounds... The Sky remains to be the only Limit for u baba..."

Kigogo wa CCM Ataka Maalim Seif Sharif Hamad Akamatwe

$
0
0
Kigogo wa CCM aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana CCM (UVCCM) na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Sukwa Said Sukwa amevishauri vyombo vya dola visiwani Zanzibar kumchukuliwa hatua haraka Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad kwa kauli yake aliyoihusisha na kosa la uhaini.

Sukwa aliitaja kauli ya Maalim Seif aliyoitoa alipokuwa akihutubia katika mkutano wa hadhara kisiwani Pemba kuwa Dk. Ali Mohamed Shein hatamaliza kipindi chake cha urais mwaka 2020 na kwamba ni dikteta.

Sukwa amesema kuwa kauli hiyo ya Maalim Seif haipaswi kupuuzwa hata kidogo kwakuwa kauli kama hizo ni zaidi ya sumu.

“Sivilazimishi vyombo vya dola kufanya ninavyotaka, lakini tunashauri tu visipuuze ushauri wetu kwa sababu ulimi wa mtu unaweza kuwa sumu hatari kuliko matendo yake,” Sukwa aliliambia gazeti la Raia Tanzania.

Maalim Seif amekuwa akifanya mikutano kuwataka wananchi kumuunga mkono kuikataa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayoongozwa na Rais Shein, akieleza kuwa uchaguzi wa marudio haukuwa wa haki.

Sakata la Wema Sepetu na Petit Man Kutoelewana..Msanii Mirror Amkana Petit Man Laivu

$
0
0
Baada ya kuenea kwa tetesi kuwa kuna kutoelewana kati ya Petiti Man na Wema Sepetu,bado kumezidi kuwepo na kizungumkuti juu ya yupi msimamizi wa msanii Mirror ambae yupo chini ya Endles Fame.

Wakizungumza na Enewz kwa nyakati tofauti Petiti alisema kuwa yeye bado ni Manager wa msanii huyo lakini Mirror akikana kuendelea kusimamiwa na Manager huyo huku tukiona katika akaunti yake ya instagram amebadili jina la Mirror na kuweka wasanii wengine.

Kwa upande wa Mirror ameiambia Enewz kuwa Petiti anakusanya pesa kwa wadau kwaajili ya kazi zake lakini hafanyi kazi badala yake anatumia kwa matumizi yake binafsi huku akiongeza kuwa kisa kikubwa cha kutosimamiwa na yeye ni baada ya kumuona akijishughulisha na wasanii wengine.

Gardner Amjibu Lady Jay Dee, Agoma kuomba Radhi Hadharani...Soma Barua ya Mawakili Wake Hapa

$
0
0
Hatimaye mtangazaji wa Clouds Fm, Gardner G. Habash amemjibu aliyekuwa mkewe, Lady Jay Dee, aliyemtaka aombe radhi ndani ya siku saba kwa kauli aliyoitoa iliyodaiwa kuwa imelenga kumdhalilisha. Katika majibu yake amekana madai hayo.

Siku chache zilizopita, Gardner alionekana katika kipande cha Video akisherehesha tukio la kumsaka mrimbwende wa chuo cha Tanzania Institute of Accountancy (TIA) jijini Dar es Salaam, ambapo alisema kuwa “yule binti sina tatizo naye, nimeshamkojoza kwa miaka kama 15 hivi…”, kisha wimbo wa ‘Ndindindi’ wa Jay Dee ukachezwa na DJ.

Kama ilivyokuwa kwa Lady Jay Dee aliyetoa siku saba za kuombwa radhi kupitia kwa mwanasheria wake Amani Tenga, Gardner amejibu kupitia mwanasheria wake Stephen Axwesso.

Katika barua yake kwa mwanasheria wa Lady Jay Dee, mwanasheria huyo wa Gardner amekiri kuwa ni kweli mteja wake alizungumza maneno hayo alipokuwa katika shughuli iliyotajwa, lakini alidai kuwa hakuna sehemu aliyomtaja mkewe huyo wa zamani.

Alisema kuwa madai ya upande wa Lady Jay Dee hayana mashiko na alimshauri mwanasheria huyo kupitia upya sheria inayozungumzia wanandoa waliotalakiana ili aweze kumshauri vizuri mteja wake kuhusu suala hilo.

Nakala ya barua hiyo pia imetumwa Clouds Media Group na kwa Rais wa Wanafunzi wa Chuo cha TIA.



Samatta Acheza Dakika 90, Aisaidia Genk Kupata Ushindi Mnono

$
0
0
Mbwana Samatta amecheza dakika zote 90 za mchezo kati yake ya Genk dhidi ya Anderlecht na kuisaidia Genk kuibuka na ushindi wa magoli 5-2 katika kampeni za kuhakikisha timu yao inapata nafasi ya kushiriki michuano ya Europa League.

Anderlecht walianza kufunga goli la kuongoza dakika ya 25 kupitia kwa kiungo wao Filip Djuricic lakini goli hilo lilisawazishwa na Leon Bailey dakika ya 45 na kuufanya mchezo huo kwenda mapumziko timu zote zikiwa sare kwa kufungana goli 1-1.

Kipindi cha pili Suarez aliiweka tena mbele Anderlecht kwa kuifungia bao la pili dakika ya 60 lakini dakika tano baadaye Buffel aliisawazishia Genk. Dakika ya 76, Pozuelo aliiweka mbele Genk kwa kutupia bao la tatu kisha Ndidi akaongeza bao la nne kabla ya Nikos Karelis hajamaliza shughuli kwa kufunga goli dakika ya 90 ya mchezo.

Samatta kucheza dakika zote 90 ni faraja kubwa kwasababu mchezo uliopita alitolewa kipindi cha kwanza wakati Genk ilipocheza na KV Oostende.

Samatta amesema sababu kubwa iliyopelekea kushindwa kuendelea na mchezo ule ilikuwa ni majereha aliyoyapata wakati wa kipindi cha kwanza cha mechi hiyo.

“Mechi iliyopit nilipata majeruhi kwenye kipindi cha kwanza cha mechi hiyo, niliumia eneo la nyonga kwa hiyo baada ya kurudi vyumbani na kuwaeleza madaktari, waliniambia nipumzike kwasababu ningeweza kuendelea lakini wasiwasi ukawa ni kwamba huenda majeraha yangeongezeka halafu ingechukua muda zaidi kupona”.

“Kwahiyo madaktari waliamua nipumzike baada ya kupata maumivu, madaktari walijitahidi nipone haraka kwa ajili ya mchezo wa leo na jana nilifanya mazoezi pamoja na timu, kucheza au kutocheza kwenye mchezo wa leo ilikuwa ni mipango ya mwalimu.”

Endapo Genk watashinda mchezo wao wa mwisho siku ya Jumapili, watafuzu moja kwa moja kucheza Europa League lakini kama watamaliza wakiwa nafasi ya nne basi watalazimika kucheza play off nyingine dhidi ya mshindi wa play off II kuwania nafasi ya kushiriki michuano ya Europa.

Rais Magufuli Atengua Uteuzi wa Waziri Wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga Baada Ya Kuingia Bungeni Akiwa Amelewa

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa Charles Kitwanga kuanzia leo tarehe 20 Mei, 2016.

Rais Magufuli ametengua uteuzi huo kufuatia kitendo cha Mheshimiwa Charles Kitwanga kuingia bungeni na kujibu swali linaloihusu wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi akiwa amelewa.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam

20 Mei, 2016

Waziri Mkuu Afafanua Kuhusu Kutenguliwa Kwa Uteuzi Wa Waziri Kitwanga

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema uamuzi wa Rais Dk. John Pombe Magufuli kutengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Bw. Charles Kitwanga umefuata kanuni za utumishi wa umma ambao unakataza mtumishi kulewa akiwa kazini.

“Zipo sheria za utumishi ambazo mtumishi hatakiwi kunywa pombe na wala hapaswi kulewa akiwa kazini… mtumishi anapaswa kuwa na akili timamu inayokuwezesha kufanya kazi za Serikali,” alisema.

Ametoa ufafanuzi leo usiku (Ijumaa, Mei 20, 2016) wakati akijibu swali la mwandishi wa TBC1 aliyetaka kujua kama taarifa zilizoenea kuhusu kutenguliwa kwa Waziri huyo ni za kweli.

“Ni kweli Mheshimiwa Rais, Dk. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mheshimiwa Charles Kitwanga kuanzia leo tarehe 20 Mei, 2016 baada ya kuonekana amelewa wakati wa kazi. Na hili lilibainika pale alipokuwa akijibu maswali ya wizara yake leo asubuhi,” alisema Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu amesema kuna swali aliloulizwa ambalo hakulijibu vizuri na kwamba swali hilo litapaswa kurudiwa kuulizwa baada ya wabunge kuomba muongozo wa swali hilo.

IMETOLEWA NA: OFISI YA WAZIRI MKUU,
S L. P. 980,
DODOMA.
IJUMAA, MEI 20, 2016

Maoni ya Zitto Kabwe baada ya Rais Magufuli Kumfuta kazi Waziri Charles Kitwanga

$
0
0
Habari kubwa iliyoteka vyombo mbalimbali vya habari jana usiku ni habari ya Rais Magufuli Kumfuta kazi Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Charles Kitwanga

Mbunge wa Kigoma Mjini na kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe ametumia ukurasa wake wa facebook kuandika mtazamo wake baada ya Rais Magufuli kufanya maamuzi hayo .

“Uamuzi wa Rais kumfukuza kazi Waziri wa Mambo ya Ndani unatuma ujumbe mmoja – hataki mchezo. Rais amethibitisha kuwa anao uwezo wa kutumbua hata aliowateua. Ni maamuzi muhimu sana kwa Kiongozi wa aina yake. Wale vijana waliokuwa wanatumwa kumtetea wasimame kumtetea. Rais kaonyesha Uongozi ‘ no nonsense “
Viewing all 104747 articles
Browse latest View live




Latest Images