Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live

Video ya dakika 7 ikimuonyesha Waziri Kitwanga akijibu swali huku amelewa Bungeni

0
0

Rais  wa Jamhuri  ya  Muungano  wa  Tanzania Dr. John P. Magufuli jana  alitengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa Charles Kitwanga  kufuatia kitendo cha waziri huyo kuingia bungeni na kujibu swali linaloihusu wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi akiwa amelewa.

Hapa chini kuna Video ya dakika 7 ikimuonyesha Waziri huyo  akijibu swali huku amelewa

TANZIA: Aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar, Willson Kabwe afariki dunia

0
0
Ndugu Wilson Kabwe, aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar na baadae kusimamishwa kazi mwanzoni mwa mwezi Mei, amefariki dunia.

Aidha, inasemekana tangu siku ile wamtumbue jipu ktk Daraja la Kigamboni (Nyerere Bridge) alikuwa shocked sana, ila tangu awali inadaiwa alikuwa kalazwa India akipatiwa matibabu.

Arusha: Mwanafunzi Mbaroni kwa Kuwatukana Rais wa Zanzibar, Mkuu wa Majeshi

0
0
Mwanafunzi Mbaroni Kwa Kumtukana Rais Wa Zanzibar Dkt.shein Pamoja Na Mkuu Wa Majeshi Mwamunyage.

Jeshi la polisi mkoani Arusha linamshikilia mwanafunzi wa Mwaka wa tatu wa chuo cha maendeleo ya jamii Tengeru aliyejulikana kwa jina la Harold Mmbando (23) mkazi wa Arusha kwa kosa la kutoa taarifa za uchochezi dhidi ya Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein na Mkuu wa majeshi Davis Mwamunyange pamoja na kusambaza ujumbe wa maneno makali juu ya viongozi hao.

Akiongelea tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo alisema kuwa tukio hilo lilitokea May 17 mwaka huu majira ya saa 09:00 asubuhi.

Alisema kuwa mwanafunzi huyo alitoa taarifa za uchochezi kuhusu mkuu wa majeshi ambapo alimtaka mkuu huyo wa majeshi kupindua nchi na kusema kuwa haiwezekani viongozi wote wawe nje ya nchi huku hakuna kiongozi aliyepewa mamlaka ya kukikaimu kiti.

“Mtuhumiwa huyo aliandika maneno haya 'Mwamunyange pindua nchi haiwezekani wote wawe nje halafu hakuna aliyepewa mamlaka ya kukalia kile kiti' hayo ndio maneno aliyoyasema mtumiwa huyo “ alisema Mkumbo.

Aidha aliongeza kuwa mbali na maneno hayo pia mtumiwa huyo alisambaza ujumbe mwingine wenye maneno yafuatayo, ”Dr. Shein akiuawa kama Karume sitashangaa wala kustuka naomba mungu mauaji ya kisiasa yaliyotokea Zanzibar yawe kwa viongozi wa kisasa hasa watawala na sio wananchi wa kawaida hayo ndio maneno aliyoyaandika mtuhumiwa huyo kupitia mitandao ya kijamii kama Facebook."

Mkumbo alisema kuwa mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani pindi tu upelelezi utakapo kamilika,huku akitoa rai kwa watu wote wanaotumia mitandao ya kijamii kutumia mitandao hiyo ya kijamii pasipo kukiuka sheria na taratiu za kisheria.

Alitumia muda huo pia kutoa onyo kali kwa yoyote atakaye bainika anatumia mitandao vibaya na kusema kuwa atachukuliwa hatua kali za kisheria dhidi yake.

Wakati hayo yakiendelea mshtakiwa wa kesi ya kumtukana Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli Isaac Emily (40), mkazi wa Olasiti jiji hapa inatarajiwa kuanza kusikilizwa mfululizo kuanzia Juni 5 mwaka huu katika mahakama ya hakiku mkazi Arusha.

Swali langu;
Je, hayo ya Mwanafunzi huyu ni sahihi au ndio matumizi sahihi kuhamasisha machafuko kwa kivuli cha uhuru wa kutoa habari?

Magomeni: Basi Lingine la Mwendo Kasi Dar Lagongwa

0
0
Basi la mwendo kasi limepata ajali katika junction ya Sheikh Yahya, Magomeni baada ya gari binafsi kupiga "u-turn" sehemu isiyoruhusiwa.

Mwimbaji Neyo Kutoka Marekani Apokelewa Kama Mfalme Jijini Mwanza

0
0
Msanii wa Kimataifa kutoka nchini Marekani Neyo amewasili jijini Mwanza jioni hii akitokea Dar es Salaam na kupokelewa na umati mkubwa wa wakazi wa jiji hilo kama Mfalme katika Uwanja wa Ndege wa jijini Mwanza.
Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania ndio wadhamini wakuu wa Jembeka Festival 2016 kwa kushirikiana na Shirika la Ndege la Fastjet, SYSCORP Cooperation, CF Hospitals, KK Security, Samsung, EF Outdoor, Lacairo Hotel, Ndege Insurance, Jembe Media Group pamoja na Coca Cola.
Msanii huyo anatarajiwa kutumbuiza katika tamasha hilo kwa kupiga 'Live Music' katika uwanja wa CCM Kirumba ambapo msanii wa kimataifa kutoka nchini, Diamond Platnumz, FID Q, Stamina, Mr. Blue, Ney wa Mitego, Maua Sama, Rubby, Baraka Da Prince, Juma Nature, MO Music na wengine wengi watapanda jukwaa moja na msanii Neyo.
Neyo check out from the hotel Hyatt Regency
Msanii wa Kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo akiondoka katika hoteli ya Hyatt Regency-The Kiliamanjaro kueelekea katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kwa safari ya jiji Mwanza kutumbuiza kwenye Jembeka Festival 2016 ambapo wadhamini wakuu ni Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Ndege la Fastjet, SYSCORP Cooperation, CF Hospitals, KK Security, Samsung, EF Outdoor, Lacairo Hotel, Ndege Insurance, Jembe FM. Kulia ni Meneja wa Hoteli hiyo, Timothy Mlay.
IMG_5465
Attu Mynah and Neyo
Meneja Masoko wa CFAO Motors Group, Attu Mynah ambao wamedhamini usafiri uliotumika kumwendesha msanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo gari aina Mercedes Benz GLE 350 D ya mwaka 2016 katika picha ya kumbukumbu na Msanii huyo kabla ya kuelekea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.
Neyo ta Hyatt Regency-The Kilimanjaro
Msanii wa kimataifa Neyo aki-show love na walinzi maalum kabla ya kuelekea katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere tayari kwa safari ya Mwanza.
Neyo official car Mercedes Benz GLE 350 D of 2016
Msanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo akielekea kwenye gari maalum aina ya Mercedes Benz GLE 350 D ya 2016 lilitolewa na kampuni ya CFAO Motors Group.
Neyo Sorrounded by Tanzanian Bodyguard
Msanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Mwalimu JK Nyerere akiwa amezungukwa na walinzi maalum alipokuwa akielekea jijini Mwanza.
Neyo at Julius Nyerere International Airport
Msanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere akiwa na mlinzi wake wakielekea jijini Mwanza leo jioni.
Costantine Magavilla and Neyo
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Jembeka Festival 2016, Costantine Magavilla (t-shirt ya blue) na Msanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo wakijianda kupanda ndege ya Shirika la Fastjet katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kuelekea jijini Mwanza. Shirika la Ndege la Fastjet ni miongoni mwa wadhamini wa tamasha hilo.
Neyo Crew to Mwanza
Mkurugenzi Mtendaji wa Jembe Media Group, Dr. Sebastian Ndege akiwa na 'crew' iliyoambatana na msanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo wakipanda ndani ya ndege ya Shirika la Fastjet ambao ni miongoni mwa wadhamini wa Jembeka Festival 2016 kutokea jijini Dar es Salaam kuelekea jijini Mwanza.
Jembeka Festival 2016 boarding Fastjest Airline
Neyo arrived in Mwanza
Mkurugenzi Mtendaji wa Jembe Media Group, Dr. Sebastian Ndege na Mwanamuziki wa Kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo wakishuka kwenye ndege ya Shirika la Fastjet ambao ni miongoni mwa wadhamini wa Jembeka Festival 2016 mara baada ya kutua jijini Mwanza. Kampuni ya simu mkononi Vodacom Tanzania ndio wadhamini wakuu wa Jembeka Festival 2016 kwa kushirikiana na Shirika la Ndege la Fastjet, SYSCORP Cooperation, CF Hospitals, KK Security, Samsung, EF Outdoor, Lacairo Hotel, Ndege Insurance, Jembe Media Group pamoja na Coca Cola.
IMG_5597
Baadhi ya wapiga vyombo waliombatana na msanii wa Marekani, Neyo wakishuka kwenye ndege ya shirika la Fastjet katika uwanja wa ndege wa jijini Mwanza jioni. Kampuni ya simu mkononi Vodacom Tanzania ndio wadhamini wakuu wa Jembeka Festival 2016 kwa kushirikiana na Shirika la Ndege la Fastjet, SYSCORP Cooperation, CF Hospitals, KK Security, Samsung, EF Outdoor, Lacairo Hotel, Ndege Insurance, Jembe Media Group pamoja na Coca Cola.
Costantine Magavilla
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Jembeka Festival 2016, Costantine Magavilla (wa pili kushoto) na Mwanakamati ya Jembeka Festival 2016, Sharon wakiwasili na katika uwanja wa ndege wa Mwanza jioni hii.
Sebastian Ndege
Kutoka kushoto ni Mwenyekiti kamati ya maandalizi ya Jembeka Festival 2016, Costantine Magavilla, Afisa Habari wa Jembe Media Group, Gsengo pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Jembe Media Group, Dr. Sebastian Ndege katika picha ya pamoja.
Neyo on Maasai Shuka
Balozi wa Umoja wa Mataifa mtoto mwanabadiliko wa mazingira, Getrude Clement akimvisha shuka la kimasai Msanii wa Kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo baada ya kuwasili jijini Mwanza leo jioni.
Getrude Clement na Neyo
Msanii wa Kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo aki-'show love' na Balozi wa Mabadiliko ya Tabianchi kutoka Umoja wa Mataifa, Getrude Clement aliyefika uwanjani hapo kumlaki na kumvisha shuka la Kimasai. Kampuni ya simu mkononi Vodacom Tanzania ndio wadhamini wakuu wa Jembeka Festival 2016 kwa kushirikiana na Shirika la Ndege la Fastjet, SYSCORP Cooperation, CF Hospitals, KK Security, Samsung, EF Outdoor, Lacairo Hotel, Ndege Insurance, Jembe FM.
Bujora Cultural Troup Mwanza entertain Neyo
Msanii wa kikundi cha ngoma cha Bujora Cultural Troupe cha jijini Mwanza akimshikisha nyoka aina chatu msanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo alipowasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza jioni hii.
Neyo playing with a snake in Mwanza
Jembe FM Journalist Interviewing Neyo
Waandishi wa habari wa jijini Mwanza wakiwemo wa JEMBE FM wakifanya mahojiano na msanii Neyo alipowasili jijini Mwanza.
IMG_5666
Wakazi wa jijini Mwanza wakisalimana na msanii Neyo kwa shangwe na furaha waliofika kumlaki katika uwanja wandege wa jijini Mwanza.
IMG_5667
IMG_5662
IMG_5305
Msafara wa msanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo ukielekea hotelini baada ya kuwasili jijini Mwanza.
Neyo at Malaika Resort
Msanii Neyo alipowasili kwenye hoteli ya Malaika Resorts ya jijini Mwanza akiwapungia wafanyakazi pamoja na wateja katika hoteli hiyo.
Justine Ndege and Neyo
Mwanasheria wa Jembe Media Group, Justine Ndege katika picha ya pamoja na Msanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo katika hoteli ya Malaika Resort.
Sebastian Ndege na Neyo
Mkurugenzi Mtendaji wa Jembe Media Group, Dr. Sebastian Ndege akibadilishana mawazo na msanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo anayetarajiwa kutumbuiza kesho katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Najiogopa Nikivaa Hereni na Kuchora Tatoo – Ben Pol Afunguka

0
0
Ben Pol ni mmoja kati ya wasanii wachache kwenye muziki wa Bongo Fleva wasiokuwa na makuu.

‘Moyo Mashine’ ni moja kati ya nyimbo zinazofanya vizuri kwenye TV na redio na kufanikiwa kuweka rekodi ya kuwa na views nyingi kwa muda mfupi kuzidi nyimbo nyingine ambazo Ben Pol amewahi kuziachia.

Akiongea kwenye kipindi cha Clouds 360, kinachoruka kupitia Clouds TV, Ben Pol amesema, “najiogopa, nawaza hivi itakuwaje nikivaa hereni au kuchora matatoo.”

“Wazazi hawatasumbua, kwa umri wangu huu naweza kufanya kitu chochote. Lakini mimi mwenyewe naona hivi itakuwaje, labda naenda kama benki hivi. Nataka kufocus kwenye muziki mzuri na ubunifu kwenye muziki lakini zile mbwembwe hapana,” aliongeza.

Jerry Muro Amuomba Radhi Haji Manara

0
0
MKUU wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro amewaomba msamaha wapinzani wao, Simba na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa timu hiyo, Hajji Manara.
Kauli hiyo, aliitoa jana ambapo alisema amefuta majina yote aliyokuwa akiwaita Simba kama vile; Wazee wa Mchangani, Wazee wa Youtong, Wahapahapa, Chura na Wamatopeni baada ya Ligi Kuu Bara kumalizika na wao kutwaa taji hilo la ubingwa.

Muro alisema alifikia hatua hiyo kwa ajili ya kulinda ajira yake inayomruhusu kuongea chochote ilimradi asitukane.

Aliongeza kuwa, hayo maneno hayo yalikuwa ni chagizo na hayakulenga kumtukana wala kumkwaza mtu yeyote zaidi ni kuleta changamoto na ushindani.

“Naomba nichukue nafasi hii kuwaomba msamaha mashabiki wote wa Simba, pia rafiki yangu Manara kwa maneno na majina ya utani niliyokuwa nawaita wakati ligi kuu ikiwa inaendelea.
“Naomba nitangaze rasmi majina hayo sitawaita tena baada ya ligi kuu kumalizika.

“Pia ningependa kuwaaga akina Manara, Bwire (Masau) na Kifaru (Thobias) kuwa mimi hivi sasa ni wakimataifa, siyo levo yao tena ninakwenda kupambana na akina TP Mazembe timu nyingine tunazoshiriki nao Kombe la Shirikisho,” alisema Muro.

Amanda Abanwa Kuhusu Ukimwi, Afunguka

0
0
MWIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Amanda Poshi amefungukia taarifa zinazomhusisha yeye kuugua maradhi ya Ukimwi.

Amanda amefunguka hayo baada ya kuvuja kwa picha zake zinazomuonesha akiwa amepungua mwili na kusababisha gumzo litawale kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii watu wakihusisha kukonda kwake na ugonjwa huo ndipo mwanahabari wetu alipombana, akafunguka:

“Nina desturi ya kupima kila wakati, hawanipi presha. Nimeshapima mwaka 2013 kibao na mara ya mwisho ni mwaka jana lakini hayo madai yamekuwa yakiibuka mara kwa mara wananiboa kweli mbaya zaidi hao wanaolazimisha nipime wao wenyewe hawapimi.
amanda

“Nilipokuwa mnene presha ilikuwa inashuka kila mara, namshukuru Mungu kwa sasa nimeanza gym niko imara, nimepungua mwili vizuri.”

baada ya kusema hayo Amanda alimtumia mwanahabari wetu vyeti vyake mbalimbali vyenye majibu ya Ukimwi vikionesha yupo safi.

Hakuna Mtumishi wa Umma Atakaesafiri Bure na Mabasi ya Mwendo Kasi

0
0
Wakala wa mabasi yaendayo kwa haraka nchini Tanzania -UDART imesema kuwa suala la watumishi wa umma wakiwemo walimu na polisi kupanda bure katika mabasi hayo bado halijafanyiwa utaratibu hivyo wataendelea kulipa kama watu wengine.


Akizungumza Jijini Dar es Salaam, jana Meneja Uhusiano wakala wa mabasi yaendayo haraka UDART, William Gatambi, amesema endapo watafanya hivyo italeta mchanganyiko kwa sababu mfumo uliopo hauruhusu mtu kupita bila kulipia.

Bw. Gatambi amesema kwa sasa wanatumia mfumo wa karatasi wakati wakiwa kwenye mchakato wa kuandaa mfumo wa tiketi za kieletroniki ambao wanaweza kufanya utaratibu ambao unaweza ukatoa nafasi kwa watumishi hao kupanda bure.

Aidha, Afisa Uhusiano huyo amesema katika kukabiliana na changamoto za foleni katika vituo hivyo wameamua kuzikata tikeki kabisa ili kusiwe na usumbufu kwa wasafiri wanaowahi kufika vituoni kwa sababu mara nyingine mtandao wa kutoa risiti unafanya taratibu katika utoaji risiti.

Aidha, amesema kuwa abairia hawana haja ya kukimbiala mabasi hayo hata kama limejaa kwa kuwa kupishana kwake yanachukua muda mfupi kituo kwa kituo hivyo ni vyema mtu kusubiri baada ya kuona gari limejaa.

Ne-Yo Ametua Bongo Tayari Kwa Kutoa Burudani Tamasha La Jembeka

0
0
Mwanamuziki mahiri kutoka nchini Marekani, Shaffer Chimere Smith maarufu kwa jina la NE-YO amewasili   katika uwanja wa ndege wa kimtaifa wa Julius Nyerere (JNIA) tayari kwa kutoa burudani ya aina yake katika tamasha kubwa la “Jembeka Festival” litakalofanyika leo tarehe 21 May jijini Mwanza.

Mara baada ya kuwasili msanii huyo alisema alipelekwa katika hotel ya Hyatt Regency ambako yeye na timu yake nzima wamefikia na baadaye alijumuika na waalikwa wachache katika “Meet & Greet Party”

Akizungumza mara baada ya NE-YO kuwasili hotelini hapo Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao alisema “tumefurahi sana kuwa na NE-YO hapa Tanzania na tunataka kuhakikisha kwamba tunawapatia wateja wetu burudani ya Tamasha la Jembeka Festival 2016 limeandaliwa na kampuni ya Jembe chini ya udhamini mkuu wa kampuni ya mawasiliano nchini Vodacom Tanzania litafanyika katika uwanja wa CCM Kirumba.

 Vodacom Tanzania imedhamini ujio wa mwanamuziki huyu ili kuwapatia burudani ya kimataifa wateja wake na watanzania wote kwa ujumla. NE-YO ambaye ataimba steji moja na wanamuziki wa Tanzania wakiwemo Fid Q, Juma Nature, Mr Blue na wengine wengi, sambamba nao pia atakuwepo mwanamuziki nyota wa Afrika Mashariki, Diamond Platnumz.

Kumbuka wawili hawa wako katika matayarisho ya ngoma yao ambapo Diamond amemshirikisha NE-YO na kwa mujibu wa Diamond Platnumz watatambulisha wimbo huo leo  katika tamasha la “Jembeka Festival”


Mkurugenzi wa Vodacom pia aliwahimiza wapenda burudani wote kununua tiketi zao mapema kujiandaa na tamasha kubwa la aina yake . Wateja wa Vodacom wanaweza kununua tiketi kuhudhuria tamasha hili kubwa kupitia M-Pesa kwa kufuata hatua zifuatazo.

1. Piga *150*00# chagua 4 LIPA KWA M-PESA

2. Chagua 3 CHAGUA KWENYE ORODHA

3. Chagua 2 MANUNUZI

4. Chagua 3 JEMBEKA FESTIVAL

5. Weka namba ya kumbukumbu – 200200

6. Weka kiasi

7. Weka PIN yako ya M-PESA

8. Bonyesha 1 kuthibitisha.

Tukutane Jembeka Festival

Unaweza kufahamu zaidi kuhusu mtandao wa 4G na maeneo unapopatikana kwa kubofya HAPA
http://vda.cm/HapaKasiTu

Fastjet yaamuriwa Kumlipa Abiria Fidia ya Sh30 Million

0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeiamuru Kampuni ya Ndege ya Fastjet kumlipa abiria wake, John Mhozya fidia ya Sh30 milioni baada ya kushindwa kumtaarifu kuhusu kuahirishwa kwa safari yake.

Mbali na fidia hiyo ya hasara ya jumla aliyoipata abiria huyo kutokana na safari hiyo kufutwa, pia Mahakama hiyo imeiamuru kampuni hiyo kumrejeshea abiria huyo nauli yake ya Sh43,000 alizokuwa ameshalipa na Sh339,000 alizozitumia kwa nauli baada ya kutafuta usafiri mbadala kutoka shirika jingine la ndege.

Uamuzi huo ulitolewa juzi na Hakimu Mkazi Mkuu Kisutu, Respicius Mwijage baada ya kuridhishwa na madai ya abiria huyo katika kesi aliyoifungua mahakamani hapo ya kampuni hiyo kuvunja mkataba.

Katika kesi hiyo ya madai namba 4 ya mwaka 2013, Mhozya ambaye pia ni wakili wa kujitegemea wa Mahakama Kuu, alikuwa akiiomba Mahakama iiamuru Fastjet imlipe Sh50,000,000, ikiwa ni hasara ya jumla aliyoipata pia imrejeshee fedha zake za nauli alizokuwa ameshalipa kwa mdaiwa pamoja na nauli aliyotumia kwa usafiri mbadala.

Katika hukumu hiyo, Hakimu Mwijage alisema baada ya kupitia ushahidi wa pande zote, hakuna shaka kwamba mdai na mdaiwa waliingia mkataba baada mdai kununua tiketi ambayo iliwasilishwa mahakamani kama kielelezo.

Alisema kwa mujibu wa mkataba huo, mdai alipaswa kusafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza na kurudi na kwamba kwa mujibu wa tiketi hiyo, mdaiwa alikuwa na wajibu wa kuwasiliana na mdai saa tatu kabla kuhusu kufutwa kwa safari.

Katika utetezi wake, mdaiwa kupitia kwa Ofisa Uhusiano na Ofisa Mtendaji, Lucy Mbogoro alidai kuwa baada ya kufuta safari walimtafuta mdai lakini simu yake ilikuwa haipatikani.

Hata hivyo, Hakimu Mwijage katika hukumu yake alisema hakuna ushahidi wowote uliowasilishwa mahakamani kuonyesha kuwa baada ya kufuta safari walimtaarifu mdai kwa wakati kama inavyotakiwa kwenye tiketi.

“Mdaiwa hakujaribu hata kumleta shahidi kutoka kampuni ya huduma za simu za mikononi kuthibitisha madai yake kwamba siku hiyo mdai alipigiwa simu lakini hakupatikana,” alisema Hakimu Mwijage.

Licha ya mdai kueleza kuwa kufutwa kwa safari hiyo kulisababisha usumbufu katika kuhudhuria kesi za wateja wake na vikao muhimu, Mahakama ilisema fidia ya Sh50 milioni aliyoomba ni kubwa.


Sifanyi Muziki Kwa Ajili ya Tuzo-Nay wa Mitego

0
0
Msanii wa muziki wa bongo fleva Nay wa Mitego ambaye alisumbua sana na wimbo wake 'Shika adabu yako' ambao ulifungiwa na Baraza la Sanaa (BASATA)

na sasa ameachia wimbo wake mpya 'Saka hela' amefunguka na kusema kuwa yeye hafanyi muziki ili kupata au kushinda tuzo..

Nay wa Mitego aliyasema haya alipokuwa akihojiwa kwenye kipindi cha eNEWS na kuwataka mashabiki wa muziki wake watambue kuwa yeye hafanyi muziki ili kupata tuzo au kushinda tuzo bali yeye anafanya muziki kutoa burudani, kurekebisha sehemu anapoona si sawa pamoja na kumuingizia kipato ndiyo maana siku zote huwa anajiita mwanamuziki mfanyabiashara.
"Mimi siku zote sifanyi muziki ili nipate tuzo au nishinde tuzo hata mashabiki zangu naomba mtambue kuwa mimi sifanyi muziki kwa ajili ya tuzo" alisema Nay wa Mitego.

Katika hatua nyingine Nay wa Mitego anadai kuwa anapotoa ngoma zake za kuchana watu au kurekebisha baadhi ya mambo kwa watu au jamii huwa zinapokelewa vizuri zaidi na kuleta changamoto kwenye muziki ikiwa pamoja na kuchangamsha muziki wa bongo.

Mauaji ya Askari Kinyogoli kwa Risasi… 15 Mbaroni Akiuwemo Mkewe

0
0
Watu 15 akiwamo mke wa marehemu, Sajenti Ally Salum Kinyogoli wanashikiliwa na polisi wakihusishwa na tukio la kuuawa kwa askari huyo wa kikosi cha usalama barabarani usiku wa kuamkia jana.

Kinyogoli aliyezikwa jana saa 10 jioni kwenye Makaburi ya Mzambarauni, Kitunda, Dar es Salaam alijipatia umaarufu mkubwa kutokana na kutoa taarifa kuhusu hali ya usalama barabarani katika vyombo vya habari.

Kinyogoli aliuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana akiwa nyumbani kwake, Chatembo Kata ya Mwandege, Mkuranga mkoani Pwani mbele ya mtoto wake, mwenye umri wa miaka kumi na moja.

Akizungumzia kukamatwa kwa mjane huyo, Kamanda wa Kipolisi Temeke, Gilles Muloto alisema:
“Sidhani kama mnaweza kuzungumza naye kwa sababu hao waliomshikilia ni polisi na wanakwenda naye kituoni. Hata hivyo, mimi siyo msemaji wa hili anayeweza kulizungumzia ni Kamanda wa Mkoa wa Pwani.”

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Bonaventura Mushongi ambaye hakuwapo msibani alipopigiwa simu ilipokewa na mpambe wake ambaye alisema: “Mkuu leo amebanwa na vikao vingi kuna Mwenge mkoani kwake na hili tukio la kusikitisha.”

Mgogoro wa kifamilia
Mama mlezi wa marehemu, Coletha Ndima alisema mara ya mwisho kuonana na Kinyogoli ni juzi wakati marehemu alipopeleka baadhi ya samani zake kwa kile alichodai mke wake mkubwa alikuwa akiziuza.

“Hatujui kama kuna mgogoro lakini Kinyogoli aliwahi kutuambia kuwa anataka kuoa mke wa pili, sijui alishaoa, kwa sababu alisema atakuja kumtambulisha mchumba lakini hakufanya hivyo,” alisema.

Ndima alisema marehemu aliwahi kumwambia kuwa ana mgogoro na mkewe mkubwa lakini hajui ni wa nini.

Mmoja wa polisi ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe alisema polisi wanamshikilia mama huyo kwa kuwa yeye ndiye aliyemuita Kinyogoli aende nyumbani kwake na mauti kumfika.

“Marehemu alitengana na mke wake mkubwa, lakini siku moja kabla ya kifo, mama huyo alimuita akimwambia watoto wamemkumbuka, usiku huohuo, ndipo walipomuua,” alisema.
Mtoto asimulia mauaji yalivyotokea

Mtoto huyo ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tatu Shule ya Msingi Ebenezer iliyopo Mwandege alieleza kuwa watu wawili walifika nyumbani hapo na kumtaka amuite baba yake.

“Nilipoingia ndani kumuita baba, nilimkuta anatandika kitanda, baba akaniambia waambie nakuja, wakati natoka, baba naye alikuwa nyuma yangu, lakini niliwakuta wale watu safari hii wamevaa ninja (mask) lakini kabla ya hapo walikuwa hawajavaa,” alisema.

Alisema watu wale walianza kumkaripia baba yake wakimtaka awape funguo ya gari lakini alikuwa akibishana nao na kisha kuanza kupambana nao lakini walimpiga bastola ya kichwani na mbavuni.

“Wakati baba anapambana nao alikuwa anawauliza nimefanya nini, lakini hawakumjibu, alianza kupiga kelele, wanangu nakufa, wanangu nakufa,” alisimulia kuongeza:

“Ujue baba alishawaweza wale, lakini walivyoona anawashinda nguvu waliamua kumpiga bastola.”
Baba wa marehemu, Salum Kinyogoli aliwataka polisi kufuatilia suala hilo ili wahalifu hao wapatikane.

Dada wa marehemu, Zainab Kinyogoli aliyeonekana kuchanganyikiwa kutokana na msiba huo alikuwa akilia mfululizo huku akisema: “Ally aje nimbebe, nimemuachia ziwa, nimembeba.”
Maelezo ya polisi

Awali, Kamanda Mushongi aliwaambia waandishi wa habari mjini Kibaha kwamba wauaji hao walifika nyumbani kwa askari huyo wakitumia pikipiki aina ya Boxer na waliingia ndani kwa kuruka uzio.

Hata hivyo, wauaji hao walipofika kwenye gari hilo hawakufanya lolote bali walitelekeza ufunguo huo na kutokomea.

“Naweza kusema ni tukio la kushtukiza kwa kweli kwa sababu ilikua ni muda mfupi tu toka askari aliporudi nyumbani kwake akitokea kazini na hawa wauaji hawakuchukua kitu maana hata ufunguo wa gari waliouchukua pale nyumbani walitoka nao nje na kuuacha,” alisema Mushongi.

Video: Nisher alalamika kupoteza shilingi milioni 3.9 kugharamikia video ya Arosto ya G-Nako aliyoikataa na kuifanya tena na Hanscana

0
0
Nisher analalamika kupoteza takriban shilingi milioni 3.9 kugharamia video ya wimbo wa G-Nako aliowashirikisha Nick wa Pili na Chin Bees ‘Arosto’ ambayo Warawara anadaiwa kuipotezea baada ya kutoipenda.
Nisher amefafanunua kwa kina kwa kupost video Instagram baada ya kubaini kuwa G-Nako aliirudia video hiyo na Hanscana na kuiachia jana.

Nisher anahisi kilichofanyika ni kama usaliti kwake baada ya kuweka nguvu nyingi kwenye video hiyo aliyoitarajia imrudishe kwa kishindo. Anasema baada ya G-Nako kudai ‘hajatisha’ kwenye video hiyo na kwamba ‘ni ya kawaida sana’, Nisher alimuomba kama vipi atoe fedha ili warekebishe makosa hayo.

Anadai Warawara alisema hakuwa na hela ya kufanya hivyo muda huo. Kutokana na uamuzi wa G kuachia video aliyofanya na Hanscana, Nisher ameamua kuitoa yake pia ili kuwapa uhuru mashabiki wahukumu kama kweli video hiyo ni mbovu.

Tazama video zote mbili hapo chini, aliyoongoza Nisher na ile ya Hanscana.

Chanzo:Bongo5

Hili ndiyo jibu la Nay wa Mitego kwa wabaya wake

0
0
Nay Wamitego amewajibu watu wanaomchukulia poa.

Akiongea kwenye kipindi cha E News, kinachoruka kupitia EATV, Nay wa Mitego amewapiga dongo wanaomchukia kwa kuwaambia hafanyi muziki kwa ajili ya tuzo.

“Mimi siku zote sifanyi muziki ili nipate tuzo au nishinde tuzo hata mashabiki zangu naomba mtambue kuwa mimi sifanyi muziki kwa ajili ya tuzo,” alisema.

Saka Hela ni moja kati ya nyimbo za rapper huyo zinazofanya vizuri kwenye TV na Radio kwa sasa japo iliachiwa kwa kushtukiza

Spika Ndugai Msaidie Rais Magufuli kwa kuzuia walevi wasiingie Bungeni

0
0
Kwanza kabisa napenda kumpongeza Rais Magufuli kwa hatua alizochukua dhidi ya aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani ya Bwana Kitwanga kwa kwa kosa la ulevi wakati wa kazi, hii imeonyesha dhahiri kuwa Rais Magufuli ni Rais wa anatembea na maneno yake ya kuwa anataka kazi tu na wala si masihala na hana simile na yeyote yule anayeleta mzaha katika kazi bila ya kujali nafasi yake ya kisiasa au ya kijamii

Ni Rais asiyetaka mchezo mchezo katika mambo yanayohusu maslahi ya taifa, Magufuli ameonyesha anaweza kufanya zaidi ya watangulizi wake katika kusimamia nidhamu na maadili serikali, ameonyesha asiyetaka uswahiba katika mambo ya uongozi wa nchi.

Watanzania kwa ujumla wetu tumsaidie Rais katika kuwatumbua walevi wengine katika maeneo yetu ya kazi pamoja na sehemu zenye huduma za kijamii kama ukienda ofisi unampokuta mlevi haraka sana yafaa kuripoti ili hatua stahiki zichukuliwe dhidi yake.

Waheshimiwa kama kitwangwa wapo wengi sehemu za kazi, na hata bungeni tuwatumbue tu bila ya kuwaonea haya kama alivyofanya Rais Magufuli ili kuwatoa wazembe na wasiowajibika ili nchi yetu isonge mbele.

Natoa rai kwa ofisi ya bunge kuweka vitaa vya utambuzi kwa wanaokunywa pombe na kuingia ndani ya bunge, bunge linapaswa kuhakikisha mheshimiwa yeyote alikunywa pombe asiingie ndani ya bunge na hapo ndipo tutakaa sawa na kudhibiti walevi maeneo ya kazi.

Haiwezikani na si halali hata kidogo waheshimiwa wetu kutufanyia dhihaka ya ulevi ndani ya bunge letu kwa kuingia wakiwa tirarila nia aibu kwa taifa,

Pia nanyi waheshimiwa hebu jiheshimuni na mjipime kwa matendo yenu, haiwezekani tunawalipe, mamilion kwa kodi zetu na magari ya bei mbaya halafu mnatufanyia uhuni haiwekani hata kidogo.

Namuomba Spika Ndugai alisimamie hili la kuhakikisha walevi hawaingii bungeni kwa kufunga vifaa vya utambuzi kwa walevi

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya May 22, Ikiwemo Kitwangwa Azidi Kupigwa za uso

0
0


SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya May 22, Ikiwemo Kitwangwa Azidi Kupigwa za uso

Zari Hassan Anaposema Tatizo ni Diamond, Hii ndio Maana yake

0
0
Watu wengi wanashindwa kumuelewa Zari anaposema tatizo ni Chibu yani Diamond.

Ali Kiba akitoa wimbo mashabiki wake wanakimbilia kwenye page za Diamond au watu wa karibu yake kulazimisha wausapoti uwezi kuwaona kwa wasio mhusu.

Diamond akipata dili ya tangazo wanaibuka watetezi feki wa haki za wanawake na kulia kwa uchungu kwa nini apewe tangazo ilihali anadhalilisha wanawake! Ukiuliza kamdhalilisha nani? Watakwambia Wema. Kivipi? Hakuna majibu ya msingi.


Tuzo zikitangazwa duniani kote lisipokuwepo jina la Diamond zinapita kimya kimya.. Likiwepo jina lake inaanzishwa kampeni kumpigia kura mnaijeria yoyote ili kumpa upinzani Chibu.

Diamond akisaidia wasanii wachanga kwao sio habari nzuri. Diamond akijenga msikiti kwao sio habari nzuri. Diamond akisaidia mashuleni kwao sio habari nzuri.. Diamond akifanya wimbo na mnaijeria na akitolea video south Africa.. Utasikia sioni kwa nini wasanii wanakimbilia kufanya video nje, mara muziki wetu unakuwa wa kinaijeria.. Kesho nao unasikia wamepanda ndege kufanyia video South Africa au wanafurahi wamepata collabo na mnaijeria.. Kwa Diamond muziki unakufa, wao wakivuka boda muziki unakuwa.

Lazima tukubali Diamond kwa sasa ndio daraja letu la kuivusha bongo fleva.. Wapo wasanii wamefanya makubwa kuufikisha huu muziki hapa kina Prof J, AY, Sugu nk lakini kiukweli Diamond amekuja kufanya mapinduzi makubwa mno. Kuna watu walifanya harakati nyingi kuubadili muziki umlipe zaidi msanii wengine waliishia kutukana matusi na ubabe ila Diamond katumia njia za kisayansi kuibadili game yetu na kiukweli game kaibadili mno ata km atupendi kukubali hili. Vitu wanavyofanya na njia wanazopita sasa yeye ametoka huko miaka 4 iliyopita.

Wakati Kiba anafurahi kusainiwa label ya kimataifa. Diamond anapambana kuipeleka label yake kuwa ya kimataifa, baada ya miaka mitatu wengi ndio mtaelewa tofauti ya Chibu na wengine.

Mtamchukia Tiffa, Zari, Babu Tale, Sallam, Fella, Kifesi lakini awa ni kafara tu ishu hapa ni Diamond. Awa wangekuwa mtaani huko awausiki na mafanikio ya Diamond wasingekuwa tatizo.

Ata ugomvi wa kifamilia kati ya Esma, mama Diamond na Zari ishu sio Zari anajisikia ishu ni Diamond kashindwa kubalansi upendo, upendo umeelemea kwa Zari na Tiffa.. Mama na dada wanaona ule umiliki wa imaya unapungua siunajua tena mambo yetu waswahili kukaba ata kama mtu kashaanza maisha ya familia . Kwa hiyo jamani kelele zooote tatizo ni Chibu.

Kajala Amuangukia Rais Magufuli Kuhusu Mume Wake Aliyoko Gerezani Akitumikia Kifungo...

0
0
Mtoto mzuri anayebamba kwenye Bongo Movies, Kajala Masanja ‘Kay’ amemuangukia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli ‘JPM’ kuwa kama ikitokea akatoa msamaha wa wafungwa, amkumbuke mumewe, Faraji Agustino ambaye yupo gerezani Segerea jijini Dar akitumikia kifungo cha miaka saba.


Akizungumza na Amani hivi karibuni, Kajala alisema kuwa amekuwa akimuwaza mumewe huyo na suluhisho kuu kwa sasa litakalomfanya Faraji atoke gerezani ni msamaha wa rais pekee.

“Najua Mungu yupo na atatenda miujiza, namuomba sana Rais Magufuli siku akitoa msamaha kwa wafungwa amkumbuke na mume wangu Faraji,” alisema Kay.

Hata hivyo, mmoja wa wanasheria maarufu Dar aliliambia gazeti hili kuwa kosa alilopatikana nalo mume wa Kay huwa halina msamaha wa rais.

Machi 2013, Faraji alihukumiwa kifungo cha miaka saba jela au faini ya za zaidi ya Sh. milioni 200 baada ya kupatikana na hatia ya kutakatisha fedha haramu kwenye Benki ya NBC, Tawi la Dar ambapo jamaa huyo alishindwa kulipa kiasi hicho cha fedha na kujikuta ‘akiozea’ Segerea huku Wema Sepetu ‘Madam’ akimlipia Kajala faini ya Sh. Milioni 13, iliyomnusuru kwenda jela miaka mitano.

Kilichomuua Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Wilson Kabwe Chatajwa

0
0
Wakati mwili wa aliyekuwa Mkuruenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Wilson Kabwe ukitarajiwa kuzikwa Jumatano ijayo kijijini wake Mamba, Mpinji wilayani Same, chanzo cha kifo chake kimetajwa kuwa ni saratani ya tezi dume na kuharibika kwa ini.

Kabwe (pichani) alifariki dunia juzi alipokuwa akitibiwa katika Hospitali ya Mama Ngoma, Mwenge Dar es Salaam baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Mauti hayo yamemkuta ikiwa ni siku 38 baada ya kusimamishwa kazi hadharani na Rais John Magufuli kwa tuhuma za kuingia mikataba iliyosababisha hasara ya zaidi ya Sh3 bilioni.
Mtoto wa marehemu, Geofrey Kabwe, alisema baba yake alianza kuugua maradhi ya tumbo Julai mwaka jana.

Alisema Ilipofika Desemba, alizidiwa na familia iliamua kumpeleka India kwa matibabu zaidi.
“Alipofika India waligundua kuwa alipata hitilafu ndogo kwenye ini, hivyo akafanyiwa upasuaji, madaktari India walisema chanzo cha tatizo hilo ni dawa alizokuwa akitumia,” alisema Geofrey.
Alisema mwishoni mwa Januari, mkurugenzi huyo alirejea nchini akiwa na afya njema na alianza kwenda kazini Februari huku akihudhuria kliniki katika Hospitali ya Apollo nchini India.
Lakini kadri siku zilivyozidi kwenda, hali yake kiafya ilianza kuzorota na ilifikia hatua familia ilitakiwa kukutana ili kushauriana kuhusu hali hiyo.

“Wiki mbili zilizopita nilipigiwa simu nikiwa Arusha nikaelezwa kwamba hali yake kiafya siyo nzuri, tulimwona daktari wake na akabainika kuwa na Pneumonia (homa ya mapafu), akapewa dawa na sindano,” alisema Geofrey na kuongeza:

“Baadaye tulimpeleka TMJ kwa ajili ya kipimo cha CTScan, jana mchana majibu yalitoka yakionyesha kuwa ini lilikuwa limeharibika na tayari mwili ulikuwa umeanza kuvimba. Ilipofika saa mbili usiku hali ilibadilika akawa anakoroma na saa tatu usiku akafariki dunia,” alisema Geofrey.
Taarifa zilizopatika jana zimeeleza kuwa Kabwe amekuwa nje ya ofisi yake tangu alipoanza matibabu na siku ya kwanza kurejea kazini ilikuwa Aprili 19 ambako alikutana na rungu la Rais John Magufuli.

Msemaji wa familia, Dk Ez Machuve alisema mipango ya mazishi inaendelea: “Atasafirishwa kwenda kuzikwa nyumbani kwake Jumanne jioni baada ya kuagwa hapa nyumbani kwake. Mazishi tunatarajia kufanya kijijini Mamba Mpinji Jumatano.”
Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita alisema katika kipindi chake cha kufanya kazi, hakubahatika kushiriki kazi yoyote na Kabwe kutokana na hali yake kiafya.

“Sikubahatika kufanya naye kazi, baada ya Rais kufanya uamuzi mgumu, aliondoka hivyo sikuwahi kushiriki naye,” alisema Mwita.

Kilichomwondoa kazini
Makosa yaliyosababisha Kabwe kusimamishwa kazi ni madai ya kusaini mkataba kwa kutumia sheria ndogo ya mwaka 2004 kutoza magari yanayotoka kwenye Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo (UBT) Sh4,000 huku akidaiwa kusaini mkataba mwingine wa Sh8,000 chini ya sheria ndogo ya mwaka 2009.

Pia, madai ya kukithiri kwa vitendo vya rushwa UBT hasa kwenye utaratibu wa kutoa magari na kukodisha vyumba vya kupangisha kinyume na taratibu na kuongeza muda wa mzabuni iliyeingia mkataba na jiji wa maegesho ya magari kinyume na taratibu.
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live




Latest Images