Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104762 articles
Browse latest View live

CUF Waitupia Lawama Serikali kwa Kushindwa Kuwajibika na Kuruhusu Uingizwaji wa Simu FEKI

$
0
0

Jumuiya ya Vijana CUF (JUVICUF) imeitaka Serikali kubeba mzigo wa kushindwa kuwajibika ipasavyo kwa kuruhusu uingizwaji wa simu feki nchini.

Kauli ya jumuiya hiyo imekuja wakati imebaki mwezi mmoja kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kuzima simu feki zote.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mtendaji wa JUVICUF, Mahamoud Mahinda Ally alisema Serikali ilishindwa kutimiza wajibu wake wa kuhakikisha simu hizo haziingizwi nchini, hivyo inapaswa kuwajibika.

Ally alisema Serikali ilipaswa kuziba mianya hiyo tangu mwanzo na kwamba inachofanya sasa ni kukosa huruma kwa watu wake.

Alisema kitendo cha wananchi kuachwa wakinunua simu feki siku za nyuma bila ya kudhibiti uingizwaji wake nchini ni kutozingatia matakwa ya haki za binadamu.

“Kuruhusu simu feki ziingie nchini, kisha kuzizima ni mapambano ambayo Serikali inapambana dhidi ya wananchi wake,” alisema Ally.

Akizungumzia kuhusu hilo, Meneja Mawasiliano wa TCRA, Innocent Mungy alisema mamlaka hiyo ilianza kutoa elimu kuhusu ya matumizi ya simu feki tangu mwaka 2010.

Alisema bado TCRA inaendelea na kampeni hiyo kwa wananchi juu ya madhara ya matumizi ya simu feki. Pia, alisema TCRA iliamua kufanya hivyo kutokana na majangili wanaotumia njia za panya kupitisha simu hizo na bila kulipa kodi.

Alisema wafanyabishara hao wasio waaminifu ndiyo wamechangia kuwapo kwa uingizaji wa simu feki nchini, licha ya Serikali kupiga marufuku.

Mungy alisema kutokana na wimbi la uingizwaji wa simu feki kuwa kubwa, waliamua kutumia teknolojia ya kuzima simu feki, ambayo itatumika kuanzia mwezi ujao ili kuwaepusha wananchi na bidhaa hizo kama zinazofanya nchi mbalimbali duniani.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Tanzania (TCRA-CCC), Mary Msuya alisema simu feki kuingizwa nchini ni tatizo la wafanyabiashara wasio waaminifu.

Alisema kuna baadhi ya wafanyabiashara wanaotumia njia za panya kuingiza bidhaa feki nchini. “Siyo simu tu hata bidhaa nyingine.”

Alisema ofisi yake ambayo ni washauri wa watumiaji wa huduma za mawasiliano nchini, imekuwa ikitoa elimu kwa wananchi kuhusu simu feki.

Alisema wananchi wamekuwa wishauriwa kuhakikisha kuwa wananunua simu katika maduka ya simu na wahakikishe wanapewa risiti ya dhamana ya muda wa matumizi ya bidhaa usiopungua miezi 12.

“Mteja asiponunua bidhaa feki hata mfanyabaishara atakosa soko,” alisema.Aliwataka wananchi kuzingatia mafunzo wanayopewa.

China Yakana Kuuza Nyama ya Binaadamu Afrika

$
0
0
Wizara ya maswala ya kigeni nchini China imekana ripoti kwamba kampuni za chakula nchini humo zinaweka nyama ya binaadamu na kuuza barani Afrika kama nyama ya ng’ombe.

Chombo cha habari nchini humo Xhinua kimesema kuwa jarida moja nchini Zambia lilimnukuu kimakosa mwanamke mmoja ambaye hakutajwa anayeishi China.

Alisema kuwa kampuni za China zilikuwa zikichukua miili ya wafu kuitia katika viungo na kuiweka katika mikebe.
Msemaji wa China Hong Lei amesema kuwa ripoti hizo hazina uwajibikaji.

Balozi wa China nchini Zambia,Yang Youming ,amesema kuwa ripoti hizo zililenga kuharibu uhusiano mzuri kati ya mataifa hayo mawili.

“Leo jarida moja linasambaza uvumi , likidai China inatumia nyama ya binaadamu ambayo uihifadhi katika mikebe na kuiuza Afrika.

”Hii ni dhulma ya makusudi ambayo haiwezi kukubalika kabisa kwetu sisi”

Nuh Mziwanda: Miaka Mitatu ya Kuwa na Shilole Imenipoteza Mambo Mengi

$
0
0
Nuh Mziwanda amedai katika miaka mitatu aliyokuwa na uhusiano na Shilole amepoteza mambo mengi.

Akiongea na Bongo5 Nuh amesema hakuna zaidi anachokumbuka kwenye uhusiano huo zaidi ya majuto.

“Kuna vitu muhimu sana ambavyo nimegundua ningeweza kuvifanya na ningekuwa nipo mbali sana,” amesema Nuh. Muimbaji huyo amesema uhusiano huo ulimfanya auchukulie poa muziki na hivyo kushindwa kutengeneza hit song.

Anasema Shilole alihakikisha katika muda wote waliokuwa nao Nuh asihit kwa uoga kuwa akiwa staa atamuacha.

“Yule [Shilole] alikuwa na trick nyingi za kunifanya mimi nijionee staa tayari, nijione mimi napendwa na watu au mimi muziki wangu unavuma kumbe bado halafu yeye huku muziki wake unaenda,” amesisitiza.

Bunge Latolea Ufafanuzi Madai ya Kitwanga Kujibu Swali Bungeni Huku Akiwa Amelewa

$
0
0

Bunge Latolea Ufafanuzi Madai ya Kitwanga Kujibu Swali Bungeni Huku Akiwa Amelewa


SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya May 25, Ikiwemo la Uchunguzi wa Lugumi Kuiva

$
0
0


SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya May 25, Ikiwemo la Uchunguzi wa Lugumi Kuiva

Mateso ya Mrembo Jacklyn Wolper Mpaka Kujikuta Anatoka na Harmonize

$
0
0
Nimekua mda mrefu nikiwachukia wanawake wa bongo movi au mastaa weng wa kike hapa nchini kutokana na tabia zao zenye ishara ya ukahaba.

Jack Wolper nae ametokea kunifanya ni mwone ovyo baada ya kuanza kutoka na mtoto mdogo Harmonize wakati ametoka kuchumbiwa hivi karibuni, mbaya zaid kujiachia na mambo ya chumbani adhara na yule mtoto wa kimakonde ambaye ni mdogo wake na wala hawaendani.

Lakini jana nilipokua nachek take one ya Zamaradi ndipo nilipo muelewa jack na kuona amepitia mateso makali sana kisaikolojia kupitia yule mchumba wake ambaye anaitwa mkongo, alikua too deeper kihisia kuonesha ni kiasi gani alimpenda yule jamaa na mbaya zaid akimvumilia na kugombana na watu wake wa karibu kwa ajili yake,
Mwsho wa siku jamaa kumbe ni mme wa mtu na mtoto, tena bado yupo karibu na familia yake lakini nia yake amharibie maisha mtoto wa watu dada ang mchaga mwenzangu.

Vitendo vya aibu kumpiga picha za uchi pengine hata kumrekodi na mengine mengi inaonekana amefanyiwa huyu dada na jamaa mkongo.

Jacky naye baada ya kuchanganywa mkongoa akaona ajitulize kwa dogo Harmonize ili afute kumbukumbu ya x wake wakati kimsingi anajiongezea matatizo kwa sababu huyu dogo na kundi lake ni ma womanizer atamtumia nakumdampu huku akiwa kajishushia heshima na kujizidishia mkosi ktk maisha yake.
Sasa angetulia akapiga kazi kwani kwa mwanamke wa kichaga mapezi si kitu kwake zaid ya pesa hasa akisha tendwa. Naomba mtu wake wa karibu amfikishie.

My take:
Wadada wa mjini msikurupukie wageni.

By Baba jay'rose

14 Wakamatwa Mauaji ya watu Watatu Msikitini Jijini Mwanza

$
0
0
Jeshi la Polisi Nchini linawashikilia watuhumiwa 14 kufuatia tukio la mauaji ya watu watatu lililotokea katika msikiti wa Rahman eneo la Ibanda relini mkaoni Mwanza, Mei 18 mwaka huu.

Akiongea na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Kamishna Msaidizi Advera Bulimba alisema kuwa msako wa kuwakamata watuhumiwa wengine unaendelea katika maeneo mbalimbali nchini.

Hivyo amewaomba wananchi kutoa ushirikiano mkubwa kwa jeshi hilo ili kufanikisha kuwakamata wale wote wanaotuhumiwa kuhusika na tukio hilo.

“Nitoe wito kwa wananchi kushirikiana kikamilifu na vyombo vya usalama katika kufichua wahalifu kwa kuwa ni watu tunaoishi nao, hivyo hakuna budi kutoa taarifa zao ili usalama na mali zetu uendelee kuimarika”, aliongeza Kamishna Msaidizi Bulimba.

Hata hivyo, alieleza kuwa hali ya usalama nchini iko shwari na kuwatoa hofu wananchi kwamba jeshi hilo limejipanga kikamilifu katika kuhakikisha hali ya usalama inaendelea kuwepo.

“Niwaombe wananchi kuondoa hofu juu ya hali ya usalama na wasiwasi na watoe ushirikiano kwa vyombo vya dola ili kuhakikisha kwamba wote wanaojihusisha na uhalifu wanakamatwa haraka”, alisema Kamishna Msaidizi  Bulimba.

Aliongeza kuwa uchunguzi zaidi wa matukio ya uhalifu nchini unaendelea ikiwemo matukio ya mkoani Tanga, Dar es Salaam na mikoa mingine ili kubaini na kuwakamata wahusika na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Hivi karibuni kumeripotia matukio mbalimbali ya uvunjifu wa amani katika mikoa mbalimbali  ikiwemo mauaji ya watu watatu waliouawa wakiwa msikitini jijini Mwanza.

Baada ya Jackline Wolper kuwa na Harmonize, Kataja jina Analomuita Diamond kwa Sasa

$
0
0
Kwa sasa headlines nyingi katika upande wa mastaa Tanzania ni stori kuhusu penzi la muigizaji Jackline Wolper na msanii wa Bongo fleva kutoka Wasafi Classic Baby (WCB) Harmonize ndio Topic kubwa town.

Katika mahojiano na Take One ya Clouds TV  na Zamaradi Mketema, Jackline Wolper ameeleza mambo kadhaa kuhusiana na penzi lake la Harmonize, Diamond ambaye aliwahi kuwa mpenzi wake anachukuliaje mahusiano yao?

“Diamond rafiki yangu sana ni mtu ambae nategemea hata kuja kufanya nae filamu, Diamondi ni rafiki yangu sana licha ya watu wanaweza wasielewe, lakini sasa hivi Diamond ni baba mkwe wangu,

“kuhusu Harmonize nampenda kwa sababu ana hofu ya mungu, ana heshima sana mwisho hawezi kufanya maamuzi bila kuomba ushauri, katika kunipenda mimi alipiatia pia kuomba ushauri kwa Diamond ambaye ni boss wake kaka yake na kupewa ruhusa kwa hiyo Baraka zimetoka kwa Diamond mwenyewe”

Hiki Ndicho Alichokisema Wema Sepetu Kama Anamchukia Diamond

$
0
0
Sasa tangu mastaa wawili wakubwa hapa bongo, Wema na Diamond Platnumz watemane. Na kila mmoja kwa sasa kaendelea na maisha yake, kwa Diamond Platnumz akiwa na mtoto mmoja huku kwa upande wa Wema akiwa na Boyfriend wake mpya Idris.

Watu wengi wamekua na wamekua wakijiuliza je wanachukiana??? Sasa Wema Sepetu ameamua kuvunja ukimwa na kujibu kama anamchukia Diamond Platnumz au la! Mskie hapa Wema Sepetu akijibu swali hilo

Tazama Video:

Ulikuwa unafuatilia majaribio ya mtanzania Farid Hispania? C.E.O wa Azam FC ana taarifa hii

$
0
0
Baada ya kurejea kwa Farid Musa kutokea Hispania alipokuwa anafanya majaribio katika klabu ya Deportive Tenerife ya Ligi daraja la kwanza Hispania (Segunda), kila mtanzania anatamani kujua nini kinaendelea kwa staa huyo wa Azam FC na Taifa Stars.

Mwanzoni taarifa zilisikika kuwa kafaulu majaribio lakini mazungumzo kati ya Azam FC na Tenerife hayajafikiwa C.E.O wa Azam FC Saad Kawemba katoa taarifa rasmi

“Ni kweli Farid amefuzu na kuna makubaliano tunafikia kwa ajili ya maslahi ya mchezaji, kwanza wanapaswa wampe muda sio akishindwa kufanya vizuri mechi moja wamuache hapana wanapaswa wampe muda”

Kua wa kwanza kusikiliza kionjo cha wimbo wa Ommy Dimpoz aliomshirikisha Ali Kiba

$
0
0
Wengi watakumbuka kua Ommy Dimpoz na Diamond walikua washkaji ile mbaya ila wakaja kutofautiana na kwa inavyosemekana kwa sasa hawaongeleshani wala hawawasiliani kabisa. Kwa muda kidogo Ommy Dimpoz alikua kimya ila wiki chache zilizopita aliamua kumtambulisha msanii wake mpya kutoka katika lebo yake ya PKP.

Pamoja na kumtambulisha Nedy siku si nyingi tutegemee bonge moja la kolabo kati ya Ommy Dimpoz na Ali Kiba. Ndio! Ni huyu huyu Kiba mshindani mkubwa wa Diamond Platnumz. Tumepata Exclusive video ya Ommy Dimpoz na Ali kiba wakiwa studio wakirecord wimbo wao huo. Skiliza kionjo  kidogo cha wimbo huo hapa  chini kwenye video.

Video : Hili Ndilo Jumba la Idris Sultan Analokaa Licheki ndani na nje

$
0
0
Wiki chache zilizopita kupitia kituo kimoja cha Tv huko nchini Kenya Idris Sultan alikiri kua kuna kipindi alifulia kabisa akawa anakosa hata hela ya matumizi. Watu wengi baada ya kuona vile walijiuliza maswali mengi je zile milioni 500 zake alipeleka wapi???

Nusu ya jibu ya swali hilo limepatikana, ukweli ni kwamba Idris anamiliki nyumba ya ghorofa ya kifahari kabisa na kwa jinsi inavyoonekana bei yake haipungui chini ya milioni 200. Hii inatokana na inavyoonekana na eneo linalozunguka nyumba hiyo kama inavyoonekana katika video hii hapa chini.

Tazama Video Hapa Chini:

Milioni 392 Zajenga Barabara HEWA Dar es Salaam

$
0
0
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Boniface Jacob amebaini matumizi ya Sh392 milioni zilizoandikwa kwenye taarifa ya manispaa hiyo kuwa zimetumika kwa ajili ya ukarabati wa barabara ya Sinza - Igesa ambao haukufanyika.

Katika taarifa ya manispaa hiyo, fedha hizo zilidaiwa kutumika kwa ajili ya matengenezo ya mara kwa mara ya barabara hiyo.

Akizungumza kwenye ziara ya Kamati ya Uchumi na Fedha ya Manispaa hiyo, Jacob alisema ni ajabu kuona hakuna matengenezo yoyote yaliyofanyika kama taarifa hiyo inavyoelezwa huku fedha zikionekana kulipwa.

Alisema hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayebainika kuhusika kwenye matumizi hayo huku akiiomba Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) kuchunguza matumizi ya fedha hizo.

“Fedha hizi zinaonekana zimelipwa kwa mkandarasi Skol Building Contract Ltd wakati barabara ina mahandaki na mashimo makubwa, ikionyesha kwamba haijakarabatiwa,” alisema.

Alisema kama wasingeamua kukagua thamani ya fedha za halmashauri hiyo zinavyotumika kwenye miradi hiyo katika kipindi cha Jaruari hadi Machi mwaka huu wasingegundua udanganyifu huo.

Meya huyo aliyeonyesha kukasirishwa na hali hiyo, aliwataka wataalamu wa halmashauri hiyo waliohusika kuandika ripoti hiyo kutoa maelezo ya kina kuhusu udanganyifu huo.

“Hivi kama tungenyamaza tusiamue kukagua miradi hii nani angesimama kueleza hayo? Mnaleta hadithi wakati tayari mmeshalidanganya Baraza la Madiwani kwamba fedha hizi zimetumika kukarabati barabara hii?” alisema.

Akitetea matumizi ya fedha hizo, mchumi wa manispaa hiyo, Huruma Eugen alisema zilizoandikwa kwenye taarifa hiyo zimetumika kwa ajili ya kulipa madeni ya nyuma.

Huku kukiwa na mabishano baina yake na Meya, Eugen alisema awali, ujenzi wa barabara hiyo ulifanyika kwa kukopa kutoka fedha za Mfuko wa Barabara, jambo lililowafanya watumie fedha za mapato ya ndani ya halmshauri kulipa deni hilo.

“Hela ilitoka kwenye mfuko wa barabara na imerudishwa kwenye akaunti, japo huku imeandikwa imelipwa kwa mkandarasi aliyejenga barabara hii,” alisema Eugen.

Hata hivyo, Meya huyo alisema kama fedha hizo zimetumika kwa ajili ya kulipa madeni zingeonyesha wazi kwenye taarifa hiyo badala ya kuandikwa kwamba zimeelekezwa kwenye ukarabati wa barabara, wakati jambo hilo halijafanyika.

Diwani wa Sinza, Godfrey Chindaweli alieleza kushangazwa na taarifa inayoonyesha ukarabati wa barabara hiyo wakati ni miongoni mwa barabara zenye mashimo kwenye kata yake.

Alisema mara kadhaa amepokea malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu ubovu wa barabara hiyo na kuahidi kuikarabati akidhani ipo kwenye mpango.

“Nimeshangaa kuona miongoni mwa miradi iliyotumia fedha za robo ya tatu ya mwaka huu wa fedha, barabara ya Sinza ambayo haijaguswa ipo kwenye orodha, jambo hili linahitaji majibu ya haraka,” alisisitiza.

Diwani wa Makongo, Ndeshukuru Tungaraza aliwataka wataalamu wa halmashauri hiyo kueleza ilikuwaje fedha ziandikwe kwamba zimetumika kwa ajili ya ukarabati wa barabara wakati hazikutumika kwa kazi hiyo.

Tungaraza alisema hakuna sheria ya matumizi ya fedha inayoelekezwa kufanya kama ambavyo manispaa hiyo imefanya, jambo ambalo madiwani hawatakubaliana nalo.

Katika eneo la Mwananyamala kwenye Barabara ya Akachube inayoelekea kwenye kituo cha daladala cha Makumbusho, Meya huyo aliwaagiza wahandisi aliowakuta wakiendelea na ujenzi kukamilisha haraka ili kuondoa usumbufu kwa watumiaji wa barabara hiyo.

Alisema malalamiko mengi ya wananchi kuhusu ubovu wa barabara yanatokana na uzembe wa kutosimamia kwa ukamilifu miradi iliyopo.

Hata hivyo, mkandarasi wa kampuni ya Delmonto, Rajab Athman alisema wanashindwa kukamilisha kwa wakati barabara hiyo kutokana na kupasuka kwa mabomba ya maji.

“Maji yanamwagika mengi, hivyo tunawasubiri Dawasco wakishakamilisha kutengeneza mabomba yaliyopasuka tutaendelea kujenga,” alisema.

Katika ujenzi wa Jengo la Bima ya Afya, katika Hospitali ya Mwananyamala linaloendelea kujengwa, Meya Jacob alionyesha wasiwasi wa jengo hilo kukamilika mapema kabla mpango wa matumizi ya bima kwa wananchi wote kuanza.

“Mpango huu unatarajia kuanza Julai lakini mpaka sasa hali inaonyesha halitakamilika kwa wakati, jambo hili linanipa wasiwasi,” alisema.

Vodacom Tanzania kugawa bonasi ya Tsh bilioni 25 kwa wateja wake kupitia huduma ya M-Pesa

$
0
0
Wateja wapatao milioni 11 wa Vodacom Tanzania wanaotumia huduma ya M-Pesa kuanzia leo wataanza kupatiwa mgao wa bonasi kutoka kwenye fungu la shilingi bilioni 25 zilizohifadhiwa kwenye akaunti maalumu ya M-Pesa kwenye mabenki mbalimbali nchini.

Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao alisema, “Mgao wa fedha hizi kwa wateja wetu ni mwendelezo wa kugawa fedha za bonasi ya M-pesa ambao ni utaratibu wetu. Hapo awali tuligawa takriban bilioni 20; awamu hii inayoanza leo tutagawa bilioni 25 na kuanzia sasa tutakuwa tunatoa gawio kila baada ya kipindi cha miezi mitatu” alisema Ferrao.

Ferrao alisema “kiasi cha fedha atakachopata mteja kwenye mgao wa fedha hizi utategemea matumizi yake ya huduma hii katika kufanya miamala mbalimbali ya malipo ikiwemo kutuma fedha. Natoa wito kwa wateja wetu ambao wameacha kutumia kadi zetu za simu wakati waliwahi kutumia huduma hii wajiunganishe tena kwenye mtandao wetu ili fedha za mgao wao zisipotee bure. Pia wateja wetu wanaotumia huduma hii kuanzia leo wanaweza kuangalia fedha watakazojipatia kwa kutuma ujumbe wa maneno kwa kuandika neno KIASI na kuutuma kwenda namba 15300”

Aliongeza kusema kuwa wateja wa huduma ya M-Pesa wakiwemo mawakala wakubwa na wadogo wanao uhuru wa kutumia fedha zao za mgao watakazopata ambapo wanaweza kuzitumia kununulia huduma mbalimbali za Vodacom kama muda wa maongezi,kujiunga na vipurushi mbalimbali ikiwemo  kifurushi cha DABO BANDO kinachomuwezesha mteja kununua muda wa maongezi na vifurushi vya internet moja kwa moja kwa kutumia M-Pesa, wanaweza kuzituma fedha hizo kwa ndugu na marafiki, kulipia ankra zao mbalimbali au kujiwekea akiba kwenye akaunti za M-Pawa kwenye simu zao. Vodacom pia imetangaza kuwa itaendelea kuboresha huduma za M-Pesa ili utumiaji wake ulete unafuu kwa wateja pia kuwanufaisha mawakala wake.

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa M-Commerce wa Vodacom Tanzania, Sitoyo Lopokoiyit, amesema kuanzia mwezi uliopita imepunguza viwango vya makato kwa watumiaji wa huduma  ya M-Pesa kwa miamala ya hadi shillingi 40,000 kwa asilimia 40% hali inayoleta unafuu kwa wateja na mawakala kuendelea kujipatia faida ya kutoa huduma “M-Pesa imeleta mapinduzi makubwa ya  huduma za kifedha nchini ikiwa na mtandao wa mawakala zaidi ya 85,000.

Paul Makonda: Niliweka Ubinadamu Mbele Nikahudhuria Msiba wa Kabwe

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema licha ya kupewa vitisho kumzuia asihudhurie msiba wa aliyekuwa mkurugenzi wa jiji, Wilson Kabwe, amezingatia ubinadamu na kuweka msimamo kuwa ataendelea kutimiza wajibu wake.

Makonda alisema hayo jana wakati wa kuaga mwili wa Kabwe kwenye ukumbi wa Karimjee, kabla ya kusafirishwa kwenda kijijini kwake Mamba Mpinji wilayani Same, Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi yanayofanyika leo.

Awali, mmoja kati ya wanafamilia alinukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari akisema kuwa familia haihitaji ushiriki wowote wa Serikali kwenye maandalizi ya mazishi hayo.

Alitoa kauli hiyo kutokana na Kabwe kusimamishwa kazi kwa amri ya Rais John Magufuli baada ya kusomewa makosa yake na Makonda mbele ya umati wa watu wakati wa uzinduzi wa Daraja la Kigamboni.

Hata hivyo, ndugu wengine walikanusha kauli hiyo na kueleza kuwa Serikali imekuwa ikishirikiana na familia katika kumuuguza Kabwe na kwamba kifo chake hakikutokana na kusimamishwa kazi kwa kuwa wakati uamuzi huo unatangazwa alishaanza kuugua.

Akizungumza kwenye shughuli hiyo, Makonda aliipongeza familia ya marehemu, akisema imevuka mtihani ambao Watanzania wengi wangeshindwa kutokana na kulivisha tukio hilo sura ya tofauti wakati wa msiba.

“Baadhi ya watu waliniambia nisihudhurie msiba na hata baadhi ya vyombo vya habari vikatengeneza mazingira vinayoyaona kwamba yanafaa,” alisema Makonda.

“Ila nitaendelea kutimiza wajibu wangu na wanafamilia mmeliona hilo na niwape pongezi.”

Makonda aliwasihi Watanzania kuwa watulivu na kushauri watumishi wa umma kuwa waadilifu katika kazi zao.

“Maadam Kabwe amelala, tusitumie fursa hii kumrundikia mizigo eti tukifikiri kwamba tutakuwa salama mbele za Mungu. Tuhakikishe kila mmoja anafanya kwa nafasi yake na kwa wajibu wake ili tusiwatwishe mizigo watu waliotangulia mbele za haki.”

Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa taasisi za kidini, wafanyakazi wa umma na viongozi mbalimbali wa Serikali, akiwamo Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi.

Akitoa salamu za Rais, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachawene alisema kifo cha Kabwe kimewasikitisha na kwamba ameacha pengo, si kwa familia pekee bali hata serikalini.

Simbachawene alisema Kabwe amekuwa mtumishi wa umma kwa miaka 37 na kwamba yapo mengi aliyoyafanya, mazuri na mabaya lakini kwa sasa yakumbukwe yale mema na kuyaendeleza.

“Rais (Magufuli) na Serikali tunatambua mchango mkubwa alioutoa marehemu (Kabwe) katika utumishi wake kwa miaka 37, tunaahidi kuyaendeleza yale yote aliyoyaacha,” alisema Simbachawene ambaye pia ni mbunge wa Kibakwe (CCM) mkoani Dodoma

Petit Money Aelezea Uhusiano Wake Ulivyo Sasa na Shemeji yake Diamond na Bosi wake Wema Sepetu (Video)

$
0
0
Ahmed Hashim Ngahemela kama anavyojulikana zaidi kwa jina la Petit Money anafahamika zaidi kwa kuwa mmoja wa waliokuwa wafanyakazi wa Wema Sepetu na pia aliyekuwa mume wa dada yake na Diamond, Esma.


Tumezungumza naye kutaka kufahamu uhusiano wake na shemeji yake Diamond ukoje licha ya kuwa upande wa Wema ambaye haziivi tena na Diamond.

“Mitihani inakuwa mingi, ni lazima itokee lakini watoto wa kiume mitihani tumeumbiwa sisi. Mitihani mingi sana imetokea, wakati mgumu sana umetokea baina ya timu zile mbili kuwa tofauti na mimi ndio nimebase sehemu zote, huku na huku lakini nashukuru niliplay part yangu vizuri,” amesema Petit.

“Mimi sina tatizo na Diamond, ni shemeji yangu na ni family sababu mimi nilishazaa na dada yake hata kama ikawaje siwezi nikawa na tatizo naye, tukikutana njiani tunasalimiana, mimi ninadili ntampigia, hatuna tatizo.”

Kwa sasa Petit ni meneja wa Billnass na Nuh Mziwanda, kitu ambacho anasema kimesababisha maelewano hafifu na bosi wake wa zamani, Wema Sepetu.

“Mimi sidhani kama nina tatizo na Wema. Ndiye aliyenifanya mimi nijulikane na Wema ndiye mtu ambaye mimi nimetoka naye mbali sana miaka tisa. Kwahiyo hata kama nikiwa nimegombana naye siwezi nikasema siongei naye, kwahiyo mimi nahesabia sina tatizo naye kama watu wanavyodhani,” ameongeza.

Tazama zaidi interview hapo juu.

Iko Siku na Mimi Ntaitwa Mama – Wema Sepetu Afunguka

$
0
0
Wema Sepetu ana kila kitu anachokitaka duniani, fedha, magari na vingine lakini amekosa kitu kimoja tu muhimu – mtoto.

Na Miss Tanzania huyo wa zamani anataka watu wajue kuwa suala la mtoto si kitu anachokichukulia poa hata kidogo. Muigizaji huyo alielezea hisia zake hizo kwa kupost picha akiwa na mama yake na kuandika: Iko siku na mimi ntaitwa Mama.’ Aliongeza emoji za mtu mwenye huzuni.

Miezi kadhaa iliyopita Wema na Idris walitangaza kutarajia kupata watoto mapacha lakini baadaye walitangaza kuwapoteza. Kwa muda mrefu Wema amekuwa muwazi kuhusu tatizo lake la kutoshika mimba katika muda anaotaka kufanya hivyo.

Mashabiki wake wameendelea kumpa moyo na kumtaka asikate tamaa.

“Usikate tamaa @wemasepetu unakumbuka sara wa ibrahim alizaa akiwa mzee sana cha msingi endelea kumwomba mungu na jiweke karbu nae hakuna kinachoshindikana kwake,” ameandika shabiki mmoja.

Chanzo: Bongo5

Martin Kadinda: Petit Bado ni Mfanyakazi wa Endless Fame

$
0
0
Meneja wa Wema Sepetu, Martin Kadinda amesema kuwa petit Man bado yupo Endless Fame Films.

Hivi karibuni kumeonekana kutokea ugomvi kati ya Petit na Mirror. Taarifa zimedai kuwa ugomvi huo umefanya mpaka agombane na bosi wa Endless Fame, Wema Sepetu japo siku chache alipofanya mahojiano na Bongo5, Petit alisema, “Mimi sidhani kama nina tatizo na Wema. Ndiye aliyenifanya mimi nijulikane na Wema ndiye mtu ambaye mimi nimetoka naye mbali sana miaka tisa. Kwahiyo hata kama nikiwa nimegombana naye siwezi nikasema siongei naye, kwahiyo mimi nahesabia sina tatizo naye kama watu wanavyodhani.”

Akiongea kwenye kipindi cha E News, kinachoruka kupitia EATV, Kadinda alisema kuwa ugomvi wa Petit na Mirror siyo mara ya kwanza kutokea.

“Petit bado yupo Endless Fame kwakuwa bado hajaiandikia barua kampuni kuwa anatoka na yote yaliyotokea kati ya Petit na Mirror au Wema ni tofauti zao tu kawaida ambazo si mara ya kwanza kutokea,” aliongeza.

Aidha Petit Man ameacha kumsimamia Mirror na sasa anafanya kazi na Nuh Mziwanda pamoja na Bill Nas.

Serikali Yaivunja Bodi ya TCU, Yawasimamisha Kazi vigogo

$
0
0
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako amevunja Bodi ya Tume ya Vyuo Vikuu nchini Tanzania(TCU ) kufuatia Tume hiyo kupitisha majina ya wanafunzi 486 wasio na sifa kusomea Shahada ya Elimu.

Pia,Waziri Ndalichako amewasimamisha kazi Maafisa kadhaa waandamizi wa TCU kwa kushindwa kusimamia na kutekeleza vyema wajibu wa TCU. Waziri Ndalichako amewateua Makaimu wa nafasi za waliosimamishwa.

Rais Magufuli amteua Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria(OUT)

$
0
0
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI​

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT).

Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Dkt. Asha-Rose Mtengeti Migiro ambaye ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza.

Taarifa iliyotolewa leo tarehe 25 Mei, 2016 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Mheshimiwa Pinda unaanza mara moja.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano,IKULU Dar es salaam
25 Mei, 2016

Viewing all 104762 articles
Browse latest View live




Latest Images