Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104429 articles
Browse latest View live

Imebainika Bifu ya Vanessa Mdee na Shilole ilikuwa Kiki tu....Soma Hapa

0
0
Siku hizi kutafuta Kiki hata kwa kutukanana na mabeef imekuwa kitu cha kawaida kwa wasanii wetu hapa Tanzania...
Unaambiwa Ile bifu ya Wanamuziki warembo wawili Vanessa Mdee na Shilole imekuja kubainika kuwa ilipangwa ili kuvutia watu katika Show yao ya pamoja inayotarajiwa kufanyaka Club ya Bilcanas jijini Dar Jumapili hii...

Kwenye show hiyo Vanessa Mdee na Shishi Watapanda jukwaani kuonyeshana nani mkali kati yao..

Usikose mtu wangu...Chaaaaa Unakosaje sasa kushuhudia magumi na makofi ya Shilole akimchapa Vanessa Mdeee

Baada ya Kutokuwa na Maelewano na Wema Sepetu, Petit Man Arudisha Majeshi Kwa Esma Platnumz na Mtoto wake

0
0
DADA wa staa wa Muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Esma Abdul na mumewe, Petit Man wameonesha wako katika mahaba mapya baada ya kipindi cha nyumba kutengana kwa muda.

Esma na mumewe huyo walionekana wako ‘beneti’ kwenye sherehe ya kuzaliwa mtoto wa staa wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel iliyofanyika hivi karibuni Hoteli ya Serena jijini Dar ambapo muda wote walikuwa katika nyuso za furaha na mtoto wao, Taraj.

 “Naona sasa hivi Esma na Petit Man mapenzi yamerudi upya Mungu awaongoze,” alisikika mdada aliyekuwepo kwenye sherehe hiyo.

Kwa upande wa Petit Man alisema Esma ni mkewe na pia ni mzazi mwenzake  hivyo hawezi kumuacha kirahisi.

Mrema Alaani Hatua ya Katibu Mkuu CUF Maalim Seif Kutangaza Kumwondoa Rais wa Zanzibar, Dr Shein Madarakani kabla ya 2020

0
0
Mwenyekiti wa Taifa wa chama cha Tanzania Labour Party  ( TLP), Augustino Mrema amelaani hatua ya Katibu Mkuu wa  CUF Maalim Seif kutangaza kumwondoa Rais wa  Zanzibar, Dr Shein  madarakani kabla ya 2020 huku akiwataka wazanzibar kutoyumbishwa na kauli za mwanasiasa huyo.

Mrema amezungumza hayo leo jijini Dar es salaam mbele ya waandishi wa habari na kusema kwamba amani ya Zanzibar ni muhimu kuliko maslahi binafsi hivyo ni vyema kuzitafakari kauli ambazo zinaweza kuleta machafuko.

Amesema hakuna mtu aliye  juu  ya sheria hivyo kuwepo kwa watu wanaochochea  vurugu  ni kama waahini pia ni  vyema  hatua zichukuliwe dhidi yao katika kuhakikisha  wananchi wanakuwa salama

Aidha Mrema amesema kwamba amani ya Zanzibar ikiharibika hata bara haiwezi kuwa salama hivyo ni vyema kauli za kuvuruga amani zizingatiwe ili kulinda maslahi ya wananchi wa pande zote mbili.

Amesema Zanzibar ina historia ya kuuawa watu mwaka 2001 kutokana na vurugu za kisiasa hivyo lazma  kwa  sasa suala la ki uchochezi liangaliwe kwa macho mawili dhidi ya watu wanaotaka kuvuruga amani katika mazingira hayo.

Mrema amesisitiza hakuna chama cha siasa ambacho  kinajengwa kwa kususia uchaguzi bali kwa kufanya hivyo ni  kuwanyima wapiga kura haki pia ni hatari na  kunaweza kusababisha chama kusambaratika kama kulivyotokea kwa baadhi ya vyama mfano, UPC cha Uganda na vinginevyo.

Pamoja na hayo mrema amefafanua kwamba mahakama ya ICC haingalii tu viongozi wa serikali bali hata viongozi wa kisiasa ambao wamesababisha mauaji kutokana na kauli wanazozitoa.

Pia mwenyekiti huyo wa TLP amewataka wahisani kutoingilia mambo ya ndani ya nchi kwani kusitisha misaada kwa hoja ya kufutwa uchaguzi wa Zanzibar na sheria ya mitandao ni kuingilia uhuru wa watanzania.

Bob Junior Afunguka Kuwatoa Kina Diamond Kishkaji tu....

0
0
Msanii Bob Junior amefunguka juu ya kitendo chake cha kuwatoa kimuziki wasanii Diamond Platnumz na Nyauloso, ambao kwa sasa wanafanya vizuri kwenye muziki.

Akiongea kwenye PlanetBongo ya East Africa Radio, Bob Junior amesema aliamua kuwasaidia kwa kuwa aliona ni wasanii wenye vipaji, na yeye alikuwa na vifaa na studio, na ujuzi wa kutengeneza beats.

“Kina Diamond niliwatoa kishkaji tu, unajua niliona wana kipaji,halafu unakuta mtu ana vifaa na studio, hivyo nikaamua kuwafanyia kazi kishkaji kabisa”, alisema Bob Junior.

Pia Bob Junior amezungumzia ukimya wake wa muda mrefu bila kutoa kazi yoyote mpaka sasa alipokuja kuachia wimbo wake na Jose Chameleon wa Uganda, na kusema kuwa alikuwa anajipanga vizuri na kwa sasa watu watarajie kazi za mfululizo kutoka kwake.

“Sasa hivi nimerudi kama unavyoona nina ngoma hiyo na Jose Chameleon, hata hiyo nimeichelewesha kumpisha Barnaba Clasic baada ya kuona naye anaachia ngoma na Chameleon, ila kwa sasa watu wajiandae kila baada ya miezi mitatu nitakuwa naachia ngoma mpya”, alisema Bob Junior.

Ali Kiba Kuwatambulisha Wasanii Ambao Wako Chini ya ‘Label’ Yake

0
0
Hivi unajua kama Ali Kiba aliwahi kuwasimamia wasanii kadhaa chini ya ‘label’ yake kama tunavyoona kwa baadhi ya wasanii wa hapa nchini kwa sasa,iliishia wapi ana mpango wa kurudi tena kusimamia wasanii.

’Hivi vitu nilikuwa navyo muda mrefu ila havikuwa ‘promoted’unajua vitu vyangu vingi huwa vinakuwa kimyakimya nilikuwa na wasanii wengi lakini nilivyopumzika kufanya muziki kipindi kile ilibidi niwapumzishe kwasababu ya vitu ambavyo vilitokea nilichukua likizo, na sasa ili niweze kukaa sawa ndio lazima waweze nao kufanikiwa katika vitu vyao vya muziki, siwezi mimi nikawa nimepumzika halafu mashabiki wakawa wamenimis halafu nikamtoa msanii na watu wanielewa, hapana kiukweli lazima niwe vizuri na nikawaonyesha msanii wangu si unaona hadi sasa hivi nimerudi lakini mdogo wangu Abdul Kiba bado sijamleta lakini wapo wasanii wengi kama Dalila, na wengine ambao hawajasikika lakini kazi zao zipo studio, lakini kwasasa nipo vizuri ataanza Abdul na wengine watafuata’’ Alisema Ali Kiba.

Soma Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Ijumaa ya May 27, Ikiwemo ya JPM Kusema Hakuna Aliyempa Urais

0
0


Soma Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Ijumaa ya May 27, Ikiwemo ya JPM Kusema Hakuna Aliyempa Urais

Exclusive Video : Wema Sepetu Ajitabiria Kifo, Mskie Mwenyewe Hapa..

0
0
Watu wengi hupenda mafanikio au wengi hupenda kua maarufu, mfano mzuri ni mwanadada Wema Sepetu. Ni mmoja wa waigizaji wa kike wachache wenye mashabiki wengi zaidi. Na katika hilo amefungua miradi mingi ikitumia jina lake mfano ni ile TV Show yake ya Wema In My Shoes, Lipstick za Kiss By Wema Sepetu na mwisho kabisa ni Wema Sepetu Application ambayo ameianzisha hata wiki haijaisha.

Pamoja na watu wengi kuona mambo yanamnyookea star huyo, Wema Sepetu amekua na mawazo yakimsumbua sana kichwani. Kwani siku za karibuni amekua akiota kua siku yake ya kufa imekaribia. Mara nyingi ameota kua kafa na kazikwa.

Tumebahatika kupata video Exclusive ya Wema Sepetu akielezea ndoto hizo. Unaweza mskiliza hapa chini......

Dada wa Bilionea Erasto Msuya Auawa Kinyama Kwa Kuchinjwa Nyumbani Kwake Dar es Salaam

0
0
Mtumishi wa Wizara ya Fedha, Aneth Msuya (30) ambaye ni mdogo wa Bilionea Erasto Msuya aliyeuawa kwa kupigwa risasi 22 KIA, ameuawa kwa kuchinjwa nyumbani kwake eneo la Kigamboni jijini Dar Es Salaam.

Mmoja wa ndugu wa familia hiyo, Shujaa Khamis, jana alithibitisha kuuawa kwa Aneth, lakini alikataa kuingia kwa undani.

“Ni kweli wamemchinja usiku wa kuamkia leo (jana) na hapa nipo kwenye msiba hapa nyumbani (Mererani) kwa baba. Tumeambiwa wamechukua Tv tu,” alisema.

Hata hivyo, Khamis alikataa kueleza lolote kama wana mashaka na mauaji hayo zaidi ya kuliomba Jeshi la Polisi nchini, kuchunguza kiini cha mauaji hayo na kuwasaka waliohusika.

Habari nyingine kutoka Wizara ya Fedha, ziliwakariri baadhi ya watumishi wakisema wamepata taarifa za msiba huo, lakini hawajapewa taarifa rasmi.

“Tuna taarifa tunazisikia sikia kuwa ameauawa, lakini jana (juzi) tulikuwa naye kazini ila leo (jana) ndiyo tunasikia amechinjwa na watu wasiojulikana. Imetusikitisha sana,” alisema mmoja wa watumishi hao ambaye hakutaja jina kwa kuwa si msemaji.

Kamanda wa mkoa wa Kipolisi wa Temeke, Andrew Satta alipofutwa jana kuthibitisha taarifa za mauaji hayo alisema yuko kwenye kikao.

Video : Lulu Afunguka Kama Alimwibia Hamisa Mobeto Mchumba Wake

0
0
Lulu na Majay ni couple ya watu wawili maarufu hapa Bongo, ilianza kama tetesi mwanzoni ila Lulu akaja kufunguka mwenyewe kua wao ni wapenzi. Ila ikumbukwe kua Majay kabla ya kua na Lulu alikua na uhusiano wa Kimapenzi na Hamisa Mobeto. Hadi kupelekea kupata mtoto wa kike.

Habari zilizozagaa mtaani ni kua Lulu alimwiba Majay kwa Hamisa Mobetto. Ila kwa kipindi kilefu Lulu alikua hajasema lolote kuhusiana na hilo. Hatimae lulu kafunguka ukweli kuhusiana na yeye kumwibia bwana Hamisa, mskilize hapa chini .....

Mr II Sugu Kuhojiwa na CloudsTV Kwa Mara ya Kwanza Toka Amalize Tofauti

0
0
Joseph Mbilinyi ameanza ku-trend kwenye mitandao ya kijamii kupitia tangazo linaloonyesha atahojiwa na CloudsTV Ijumaa May 27 2016, ameanza kutrend hata kabla Interview yenye haijaonyeshwa na hii ni kutokana na sababu kadhaa ikiwemo ya kuwa hii ni Interview yake ya CloudsTV ya kwanza toka amalize tofauti zake na CMG.

Mbunge huyu wa Mbeya mjini ambaye ni mmiliki wa single mpya ya Freedom aliipost hii picha kwenye page yake ya Instagram na kuonyesha wazi ameshaachana na tofauti zilizokuwepo na kwa roho safi maisha yanaendelea bila beef : ‘Rapper/MP/ CEO / AUTHOR / BUSINESSMAN /INVESTOR ni kesho asubuhi Freedom to all media, freedom from beefs’

Shilingi Bilioni 3 na Mali za Bilioni 10 zataifishwa na TRA Kutoka kwa Wakwepa Kodi Bandari Kavu ya Azam

0
0
Mamlaka ya kukusanya kodi TRA kupitia madalali wa Yono Auction Mart wamekusanya mali za bilioni 3 pamoja na kutaifisha mali za bilioni 10 kutoka kwa wafanyabiashara waliopitisha makontena 329 kupitia bandari kavu ya Azam bila kulipa kodi na bado wanaendelea na msako bara na visiwani.

Madalali hao wamesema watu walipe kodi na watoe risiti za elekroniki la sivyo mali zitakamatwa.


Rais Magufuli Atoa Mchango wa Milioni 10 Kusaidia Matibabu ya Mwafunzi Aliyepata Upofu

0
0
Rais John Magufuli ametoa mchango wa Sh. milioni 10 kwa ajili kusaidia matibabu ya mwanafunzi Bernadetha Msigwa aliyepata upofu hivi karibuni.

Msichana huyo anayesoma mwaka wa tatu katika Chuo Kikuu cha Mzumbe, ni miongoni wa wasichana ambao tatizo lake limeibuliwa kupitia kampeni ya Kipepeo, iliyoanzishwa na kampuni ya Clouds Media, Mei Mosi mwaka huu.

Kupitia matangazo yanayorushwa na kampuni hiyo, Rais Magufuli baada ya kusikia tatizo la Msigwa, ambaye pia picha yake imekuwa ikisambaa kwenye mitandao ya kijamii, akiwaomba Watanzania wamsaidie mchango wa fedha ili aweze kutibiwa. aliguswa na kuamua kutoa mchango huo.

Meneja wa kipindi cha 360 kinachorushwa kila siku za wiki asubuhi na televisheni ya Clouds, Hudson Kamoga alisema baada ya Rais kuona tangazo hilo, lililorushwa muda mfupi kabla ya kuanza uchambuzi wa magazeti, alimpigia simu.

“… Alisema ameguswa na stori ya Bernadetha, hivyo yeye na familia yake watachangia Sh10 milioni ili kumsadia,” alisema Kamoga.

Kamoga ambaye aliwahi kupigiwa simu na Rais Magufuli akiwa katika ya kipindi hicho na kuwasifu yeye na wenzake wanaokiendesha, alisema baada ya muda mfupi, Rais alimwagiza msaidizi wake apaleke mchango huo.

“Zilipita kama dakika 30 hivi au 45, akawa amemtuma mtu alete zile hela,” alisema Kamoga.

Mbali na Rais Magufuli, Kamoga alisema viongozi wengine walioguswa na tatizo la Msigwa ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi ambaye alikuwa mgeni kwenye kipindi cha 360 jana asubuhi, alichangia Sh2 milioni.

Pia, Manaibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu), Anthony Mavunde Dk Abdallah Posi kila mmoja alichangia Sh1 milioni na Mkurugenzi wa Kampuni ya TSN, Farough Baghozah alichangia Sh3 milioni.

Kamoga alisema mwitikio wa Watanzania umekuwa mkubwa na hadi jana, michango iliyokuwa imetolewa ilikuwa zaidi ya Sh30 milioni anazohitaji Msigwa kwa ajili ya matibabu.

Kamoga alieleza kuwa msichana huyo alianza kupata maumivu makali ya kichwa mwaka huu na baada ya muda, alipoteza uwezo wa kuona.

“Hakuzaliwa kipofu. Amepata tatizo mwaka huu, wakiwa chuo mwaka wa tatu,” alisema Kamoga.

Alisema aliomba msaada kwao hivyo kupitia kampeni ya kipepeo, tatizo lake limefahamika na wengi na Watanzania wamemchangia ili aweze kutibiwa na kuona tena.

Video : Wema na Petitman Watakua na Bifu Kubwa Sana, Msikie Wema Sepetu Hapa

0
0
Ni kwa zaidi ya miaka minne Wema Sepetu na Petit Man walikua marafiki. Kwani walionekana pamoja katika kila jambo hata pale Wema alipoamua kugombea ubunge viti maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi Petit alijitokeza na kua nae Bega kwa Bega.

Siku za karibuni kulikuepo na tetesi kua kuna ugomvi mkubwa kati ya Wema Sepetu na Petit huku chanzo kikiwa hakijulikani. Ikafikia hadi Mirror, msanii aliekua chini ya Petit Man kutangaza kua kwa sasa Petit si meneja wake tena na kwa sasa Mirror yupo Benet sana na Wema.

Baada ya mashabiki kumuuliza Wema kuhusu ishu ya Petit Wema alikua mkali na kuongea maneno mengi ambayo ukiyasikiliza utagundua kua wawili hawa sasa hawapikiki chungu kimoja. Mtizame Wema akifunguka hapa chini....

Makahaba Dar es Salaam Wamzidi Nguvu Paul Makonda

0
0
Ving’ang’anizi! Agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda la kuwataka akina dada wanaouza miili ‘makahaba’ kuondoka kwenye ‘masoko’ yao mitaani limeshindikana baada ya hivi karibuni kuonekana kwenye vijiwe vyao, Ijumaa linakupa zaidi.

Usiku wa Jumatatu na Jumanne iliyopita, makamanda wa kikosi maalum cha Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ cha Global Publishers kiliingia mitaani usiku wa saa nne kwa lengo la kuona kama madadapoa hao wamerudi baada ya kuadimika hapo kati kufuatia agizo la Makonda.


OFM ilifanikiwa kuzunguka kwenye vijiwe vya Sinza- Afrika Sana, Sinza Mori (barabara ya kuelekea Meeda Bar), maeneo ya Corner Bar, Kinondoni, Buguruni na Manzese Tip Top jijini Dar na kufanikiwa kuzungumza na baadhi yao licha ya kuwa wakali.

“Tumeamua kurudi kwa sababu ya njaa. Serikali iliposema tutoke mitaani ilitakiwa kutupeleka sehemu kufanya kazi au kutupa mitaji ya kufanyia biashara.

“Kitendo cha kuambiwa ondokeni tu halafu hatujui twende wapi wakati kula yetu, vaa yetu na watoto kusoma vyote vinategemea biashara hii, si sawasawa,” alisema Paulina Maute anayepiga kambi yake, Sinza Mori.

Mwanahawa Magembe, yeye anafanya biashara hiyo ya ukahaba maeneo ya Kinondoni ambapo kwa upande wake alisema kuwa, aliposikia agizo la Makonda kuwataka waondoke kwenye vijiwe vyao alikaa wiki moja nyumbani  lakini sasa:

“Lakini sasa njaa kaka yangu, hakuna lingine njaa tu. Unaamka mpaka unalala bila kuingiza kitu kinywani. Nikaona cha kufia, ndiyo na mimi nikaamua kurudi.

“Lakini nimefika hapa na kukuta wenzangu wengine nao wamerudi.”

Hata hivyo, mazungumzo kati ya OFM na Mwanahawa yalikatishwa na wenzake waliokuja juu kwa OFM wakitaka hata kurusha mawe baada ya kubaini kuwa, kuna kamera kwenye mikono ya makanda hao.

“Mnajifanya watu wazuri kwetu kumbe hamna lolote. Kwendeni huko, tutawaumiza sisi,” walisikika wakisema wakati OFM wakiondoka eneo la tukio.

Habiba Iddi yeye anajiuza kando ya Barabara ya Shekilango eneo la Mapambano ambapo kwa upande wake alisema:

“Biashara ya ukahaba ni ya dunia nzima. Sasa nashangaa serikali yetu inavyotumia nguvu kubwa kutufukuza. Na wanaposema hii ni biashara haramu, uharamu wake uko wapi?

“Mi najua madawa ya kulevya ni haramu kwa sababu yanaua watu, vijana wanaharibika, wanakuwa mateja. Sasa sisi kwanza tunatumia kinga kujilinda na maradhi lakini pia tunapata kipato. Uharamu wake ni wapi sasa?” alihoji Habiba huku akiiomba OFM shilingi elfu tano ili achukue Bajaj kumpeleka kwao, Tandale, Dar akitoa sababu ya wateja kukosekana.

Juzi, OFM walimpigia simu Makonda kwa lengo la kutaka kujua msimamo wake baada ya agizo lake kuwekwa kapuni na madadapoa hao lakini simu yake iliita bila kupokelewa.


OFM wakamtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, ACP Christopher Fuime ili kusikia kauli yake kufuatia kiburi hicho cha machangudoa ambapo alisema:

“Tunaendelea kupambana kuhakikisha biashara hiyo tunaikomesha ingawa ni ngumu kufahamu kuwa wanapungua au wanaongezeka kutokana na kutokuwa na takwimu sahihi za wanawake wanaojiuza Dar.”

Chid Benz Akanusha Kutoroka Rehab ila Ameruhusiwa

0
0
Msanii Chid Benz amekanusha taarifa zilizopo kwenye baadhi ya vyombo vya habari na mitandao kuwa ametoroka rehab Bagamoyo, alikokuwa akipata tiba ya kuacha madawa ya kulevya.

Akiongea na East Africa Radio Chid Benz amesema si kweli kwamba ametoroka, isipokuwa ameruhusiwa kutoka rehab.

"Wameongea uongo hao wajinga, nimeachana nao kwa sababu hatuwezi kubishana nao, mi nimetoka niko sawa, nipo fresh na siwezi kubishana na magazeti, na sasa hivi nipo studio nataka niingie kurekodi, kwa hiyo sio kweli kama nimetoroka rehab, nimetoka kwa sababu nimeruhusiwa", alisema Chid Benz.

Hata hivyo East Africa Radio iliamua kumtafuta mtu wa karibu wa Chid Benz (Madee) ambaye naye yupo chini ya Babu Tale, na kuthibitisha taarifa hizo kuwa hajatoroka kweli.

Chid Benz alipelekwa rehab Bagamoyo mwezi wa 3 mwaka huu, baada ya meneja wa TipTop kujitolea kumsaidia kuacha matumizi ya madawa ya kulevya, ambayo yalikuwa yameshamuathiri.

Mwigizaji Aliyempa Denda la Nguvu Wema Sepetu Wakati Wakitengeneza Movie Afunguka Kwa Mara ya Kwanza

0
0
MWIGIZAJI wa Filamu Swahilihood anakuja juu katika uigizaji Koko Byanko ametamba kufanikiwa kuigiza na msanii nyota katika tasnia ya filamu Bongo Wema Sepetu ‘Madame Wema’ Koko amemshirikisha Wema katika sinema yake aliyoitengeneza hivi karibuni.

“Nilipo posti picha nikiwa na Wema wengi walinituhumu kama natoka naye lakini ukweli sitoki naye bali zilikuwa ni picha tu za location nilizopiga naye katika filamu yangu huyu ni msanii mwenzangu tu,”

FC ilizipata picha hizo pamoja na msanii huyo kueleezea kuwa ni za filamu lakini zipo kiutata msanii huyo amedai kuwa kumpata Wema kushiriki filamu yake haikuwa rahisi kwani ilihitajika ushawishi mkubwa na gharama zake ni kubwa sana.

“Wema alipoiona script yangu ilivyo kali alikubali kuigiza katika filamu na ameigiza katika kiwango kikubwa sana nawaambia wapenzi wa sinema waisubiri kazi bora yenye mastaa kibao,”anasema Koko.

Video : Ukitaka Kumuoa Lulu Michael Lazma Uwe na Vitu Hivi, Mskie Mwenyewe Hapa

0
0
Ikitangazwa shindano la Lulu Husband Search naamini vijana wengi wa kiume watajitokeza kuwania nafasi hiyo moja. Lulu ni mmoja kati ya wadada warembo zaidi hapa Bongo na wanaojua vizuri kuvaa viwalo na wakapendeza.

Ni wengi wanatamani kua wapenzi wa Lulu ila kama utabahatika kua mpenzi wa Lulu basi lazma uwe na sifa hizi alizofunguka Lulu mwenyewe kwenye video hii hapa chini .......

Ni Marufuku Kuvaa Nguo Fupi Wilayani Siha Kilimanjaro, Sheria za Viboko na Faini zimetajwa

0
0
Moja ya matukio ambayo yanamake headlines katika Wilayani Siha Kilimanjaro ni pamoja na adhabu zinazotolewa kwa wale wanaovunja sheria, kingine ni kwamba kijiji cha Sanya Hoye kimepitisha adhabu ya faini ya Shilingi 50,000 pamoja na viboko 15 kwa atakayekutwa baa na mtoto mdogo au kuvaa nguo fupi.

Mwenyekiti wa kijiji cha Sanya  Hoye, Moses Mnuo ametoa ufafanuzi wa maazimio waliyokubaliana katika kikao cha kijiji cha Sanya Hoye………

‘Tumepitisha sheria kwa mtu yeyote anayevaa nguo fupi kwa watoto wa kike ni marufuku tangu siku ile ya kikao kile, wanawake hao wanapotembea hapa usiku wana ajenda walizonazo wanafanya machafu yao kwa hiyo tutawapiga faini na hizo hela watapewa risiti’ Sikiliza Hapa

Chumba Cha Dereva Tax Chazua Kizaa Zaa Mtaa Wa Mbezi Mtoni Gold Star, Jijini Dar Baada ya Kukutwa Kimejaa Makopo ya MIKOJO na KINYESI

0
0
UKIHADITHIWA na kuonyeshwa chumba cha Dereva Tax anayeonekana kitaani na katika kazi zake akiwa amepiga pamba wala hutaamini masikio yako wala macho yako pindi utakapopata bahati ya kufika na kushuhudia chumba hicho kilichopo maeneo ya Gold Star Mtaa wa Mbezi Mtoni Bondeni jijini Dar es Salaam.

Mwandishi wa habari hii alipata fursa ya kufika na kushuhudia yale yaliyokuwa yakisemwa na baadhi ya wakazi wa mtaa huo jana majira ya saa tano usiku baada ya kutokea mtafaruku na sintofahamu katika nyumba hiyo ya Mama Mwakajinga, anayoishi Dereva huyo aliyejulikana kwa jina la Steven al-maarufu kama ‘NYATI’.

Akizungumza na mwandishi kuhusu tukio hilo, Mama mwenye nyumba, alisema kuwa siku ya Mei 23, akiwa ameketi uwaji karibu kabisa na Chumba cha Jamaa huyo huku akichambua mboga, alihisi harufu kali na mbaya iliyokuwa ikivuma kutoka chumbani kwa Dereva huyo aliyepanga katika nyumba yake tangu mwaka 2008 na kuona wadudu aina ya funza wakitoka chumba hicho kupitia chini ya mlango.

Kesho yake Mei 24 baada ya kuona wadudu hao huku harufu ikizidi kuwa kali, alimuita jirani yake na kumshirikisha jambo hilo huku wote wakishikwa na butwaa na kuwa na mashaka na chumba hicho.

Mei 25 Mama mwenye nyumba aliamua kwenda kwa Mjumbe wa eneo hilo Badili Makoye, kutoa taarifa juu ya wasiwasi uliotanda katika nyumba hiyo na kuongozana na Viongozi wengine, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo, Frank Kyaruzi, Wajumbe wengine  Abdalla Mlaliya na Matrida Paston, waliofika na kujionea hali halisi ya chumba hicho.

Baada ya viongozi hao kufika eneo la tukio walimuamuru Mama mwenye nyumba kwenda kutoa taarifa kituo cha Polisi.  Mama huyo alitekeleza agizo na kwenda kuripoti Kituo cha Mbezi Garden na kuongozana na Mkuu wa Kituo hicho na baadhi ya askari hadi nyumbani na kukuta hali hiyo ya sintofahamu.

Walipofika eneo la tukio na kushuhudia hali hiyo, Mkuu wa Kituo aliamuru mlango huo uvunjwe huku wananchi na Viongozi wa Mtaa huo wakishuhudia na kuingia ndani ambako walikuta Chumba kizima kikiwa kimejaa Chupa za Plastiki zilizojaa mikojo, Mifuko ya Rambo ikiwa na Vinyesi, Feni moja iliyochomekwa kwenye Soketi ya Umeme ukutani, Pakiti nyingi tupu za Sigara aina ya Embassy na Kondomu zilizotumika na zisizotumika.

Baada ya zoezi hilo, Mwenyenyumba alimpigia simu mpangaji wake na kumtaka kurejea nyumbani, lakini Dereva huyo alijibu kuwa kwa muda huo alikuwa mbali maeneo ya Kunduchi na kuahidi kuwagongea usiku pindi atakaporejea.

Hadi Mwandishi anaondoka eneo la tukio majira ya saa tano usiku bado wakazi wa maeneo hayo walikuwa wamejazana nje ya Chumba hicho wakiendelea kumsubiri arudi ili kupata ukweli kuhusu mambo waliyoyaona katika chumba chake.

Aidha Mama mwenye nyumba alisema kuwa mpangaji wake huyo, tangu alipohamia katika nyumba hiyo mwaka 2008, hakuwahi kumuona akiingia na mwanamke katika chumba hicho, wala kumuona mgeni wa aina yeyote kwa Dereva huyo,jambo lililomshangaza kukuta Kondom zilizotumika katika chumba hicho. Ama kweli ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Filaun.

Leo hii Mei 27, Mama mwenye nyumba ameripoti kuwa mpangaji wake huyo,hajatokea nyumbani hapo tangu kutokea kwa tukio hilo ambapo leo, amechukua uamuzi wakuwalipa vijana wa mtaa huo ili wasafishe chumba hicho.

"Tayari tumewalipa pesa vijana kiasi cha sh.200,000/= ili wafanya usafi na wameshamaliza na kwenda kufukia bonde la mto Mbezi." Amesema mama huyo

Huyu Ndiye Dereva wa Tax Nyati anayedaiwa kumiliki chumba hicho

Juma Nkamia Adai Wapinzani Wanasura Mbaya Kiasi Kwamba Wanataka Kutapika na Wengine Meno Yao Yameoza!

0
0
Kanuni inayozuia lugha ya kuudhi bungeni ni kiinimacho kwani mbunge wa upinzani akitoa lugha inayokera, mbunge wa CCM ataomba mwongozo kwa Spika na mara akijibiwa atasimama mbunge wa CCM na kutumia lugha hiyo hiyo iliyoombewa mwongozo.

Jana Mbunge wa Chemba, Juma Nkamia (CCM) aliporomosha lugha za kuudhi baada ya kuwaambia wabunge wa upinzani waliokuwa wakishangilia kuwa wanasura mbaya hadi wanatamani kutapika.

Akichangia hotuba ya makadirio na matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi kwa mwaka 2016/17, Nkamia alionyesha kukerwa na hotuba ya upinzani kuhusu wizara hiyo kwenye sehemu iliyozungumzia uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka jana.

Nkamia alisema uchaguzi umepita na mshindi alipatikana ambaye ni CCM na aliufananisha uchaguzi na mpira kwamba unapoisha uwanjani mtu hawezi kulalamika nje.

“Uchaguzi umeisha, leo mtu anasimama hapa anasema ‘ooh tuliibiwa kura’ mlikuwa wapi wakati mnaibiwa kura?”alihoji na kuwataka wapinzani watafute sababu kwa nini walishindwa na si vinginevyo.

"Wanajua mchezaji mmoja akiumia katika timu unachukua mwingine kwenye timu ile ile lakini inakuwaje unachukua mchezaji kutoka upinzani? Kwa hiyo niwaombe tu muwe mnatafakari kwanza,” alisema.

Hali hiyo iliibua kelele na minong’ono kutoka kwa wapinzani, jambo ambalo lilimlazimu Naibu Spika, Dk Tulia Ackson kuwataka wabunge huku akiwataja majina watulie ili mbunge huyo amalizie mchango wake.

Nkamia aliendelea, “We nyosha midomo, fanya nini lakini that is the truth (huo ndiyo ukweli). Utaongea sana na utapiga kelele sana lakini ukweli ndio huo na umekuingia vizuri.

"Mimi kelele wala hazinisumbui. Mimi nataka niwashauri kama wakati ujao mnataka kuwa chama kizuri anzeni kutafuta wachezaji wenu,” alisema.

“Nyie pigeni kelele lakini ukweli ndio huo, wenye akili wanajua na wapiga kelele wanajua na najua limewaingia vizuri sana.”

Kijembe hiki kiliwalenga Ukawa ambao katika uchaguzi mkuu uliopita walimteua aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowasa. Ukawa walimteua Lowasa baada ya kuitema na kuihama CCM ambapo alipambana na John Magufuli (CCM) aliyeshinda.

Nkamia akionekana kumlenga mbunge fulani ambaye hakumtaja jina alisema, “We piga kelele, kwanza meno yako yameoza.”

Kwa kuzingatia kanuni, lugha hiyo ni ya kuudhi lakini Dk Tulia asisitiza Nkamia amalizie kuchangia ambapo alitoa mfano wa mwandishi wa vitabu Bernard Taper aliyewahi kusema kwamba kuna watu wakiamka asubuhi wakijiangalia kwenye kioo wanatamani kutapika.

“Sasa nyie mnaoshangilia humu mna sura mbaya na mnatamani kutapika,” alisema Nkamia
Viewing all 104429 articles
Browse latest View live




Latest Images