Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104429 articles
Browse latest View live

Wema adai kwa wiki anatumia Tsh milioni 1.2 kwa ajili ya nywele zake

0
0
Msanii wa filamu, Wema Sepetu, ameweka wazi kwamba hutumia shilingi milioni 1.2 kwa ajili ya kutengeneza nywele zake kwa wiki moja.

Pia hutumia Sh 30,000 ya chakula kwa siku na kama atanunua na chakula cha mbwa wake huwa anatumia Sh 50,000 kwa siku.

Wema aliliambia gazeti la Mtanzania kwamba si kila wakati hutumia kiasi hicho cha fedha, bali hutegemeana na aina ya nywele anazotengeneza.

Alifafanua zaidi kwamba gharama hizo pia zinatokana na kutumia ‘weaving original’ lakini wakati mwingine hutumia hadi laki moja na nusu kwa nywele za kawaida kama rasta.

“Huwa nabadilisha nywele kila baada ya wiki ambapo siku nyingine natumia milioni moja, siku nyingine laki saba au tano kwa sababu sipendi kukaa na nywele muda mrefu na nywele zangu ni ‘orijino’,” alisema.

Wema aliongeza kwamba anachopenda zaidi kwake ni kuwa na muonekano mzuri wa urembo kwa kuwa urembo upo kwenye damu yake

Source:Mtanzania

Mange‬ Kimambi Alia na Jeshi la Polisi Kutokana na Kukithiri kwa Matukio Kuchinjwa Kinyama, Ahoji Vipi WAPO Busy Kukamata Boda Boda na Bajaj Kama TRA

0
0

Ameandika haya katika Ukurasa wake wa Instagram..

Mangekimambi
"What's going on jamani????? 🏽🏽🏽🏽🏽🏽 it's like kuchinjana imekuwa fashion Tanzania. Dah!
Hivi polisi wanaona hili Janga? Au Ndo wako busy kutafuta na kuwabeba Kwa madefender wanaoweka status Facebook, kukusanya mapato barabarani kama TRA na kukamata bajaji na bodaboda???? " Mange Kimambi

Je Kuna Ukweli?

Kijana Anusurika Kifo Baada Ya Kupanda na Kujirusha Kutoka Kwenye Mnara Wa Simu Jijini Mwanza

0
0
Kijana Mmoja (pichani aliyeshikiliwa ) ambaye jina lake halikupatikana kwa haraka, mkazi wa Jijini Mwanza amenusurika kifo baada ya kujirusha kutoka katikati moja ya minara wa simu iliopo jijini humo, mchana wa leo.

Tukio hilo limetokea hii leo na kuvuta watu wengi waliofika kumshuhudia kijana huo ambae amepanda katika mnara huo tangu majira ya asubuhi na kukatalia mnarani hadi majira ya saa sita mchana.

Mashuhuda wa tukio hilo ambao pia ni marafiki wa karibu na kijana huyo, wamesema huenda kijana huyo amefikia maamuzi hayo kutokana na ugumu wa maisha ambao amekuwa akiulalamikia huku wengine wakisema ni kutokana na kuathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya ikiwemo gundi ambayo amekuwa akiyatumia.

Akizungumza kwa niaba ya Kamanda wa Jeshi la Uokoaji na Zima Moto mkoani Mwanza, mmoja wa maafisa wa uokoaji Mussa Kaboni, ametoa rai kwa makampuni yenye minara ya simu kuimarisha ulinzi katika minara hiyo ili kuondoa hatari inayoweza kujitokeza kutoka kwa raia wasio wema.

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo walionekana kuchukizwa na kitendo cha kijana huyo na kusikika wakifoka kwa hasira na makelele ya hali ya juu "rukaa, ruka sasa, jirushe kama wewe ni mwanaume" hali ambayo ilikuwa ikimuongezea morari kijana huyo na hivyo kujirusha kweli kutoka katikati ya mnara huo.

Baada ya kijana huyo kujirusha kutoka katikati ya mnara hadi chini, alipoteza fahamu na kukimbizwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza, Sekour Toure kwa ajili ya huduma ya kwanza.


Mambo ya Msingi Kuyafanya Kabla ya Kuoa/Kuolewa

0
0
Ndoa nyingi zinaingia kwenye migogoro kwa sababu ya mambo ya kukurupuka na kufanya haraka bila wahusika kufahamiana vizuri, hebu tuzingatie yafuatayo ili tusiseme 'NINGEJUA NISINGEOA/NISINGEOLEWA'

1. Chanzo cha uhusiano wenu kiwe ni upendo wa dhati
2. Chunguza kwa mwenzio juu ya tabia:nidhamu, adabu, hasira, ulevi na umalaya
3. Mpeane muda wa kutosha kufahamiana
4. Mtembee pamoja maeneo tofautitofauti kama michezoni, bar na out mbalimbali ili muone interest za kila mmoja
5. Muwe wa imani moja. ila kama mmeshibana sana na mwaweza kuvumiliana hata wa imani tofauti ni sawa.
6. Wajue ndugu wa mwenzio ili kupata habari zao zitakazokufahamisha mwenzao pia yukoje
7. Pimeni afya zenu bila aibu. kuna maradhi mengi kama HIV/AIDS na mengine.
8. Kama ni Mkristo au Muislam funga ndoa Kanisani au Msikitini na siyo Bomani.
9.Kwa Wakristo ndoa haina talaka. huu ni mpango wa Mungu. kuachana na kuoa mwingine ni dhambi.

N.B: kama mwenzio ana tabia usiyoipenda, usifunge ndoa naye ukitegemea atabadilika.abadilike wakati mkiwa wachumba na siyo kwenye ndoa, labda kama umeshamkubali kama alivyo

Wolper ni Mke Wangu, Bado Ubani tu – Harmonize

0
0
Baada ya Jacqueline Wolper kuthibitisha penzi lake kwa msanii wa WCB, Harmonize, muimbaji huyo wa ‘Bado’ ameibuka na kudai kuwa muigizaji huyo ni mke wake, na anachosubiri ni kuhalalisha tu.

Uhusiano wa wawili hao hauna hata mwezi tangu uweke bayana.

Akiongea na kipindi cha The Premier cha Kings FM, Harmonize alisema hajali watu wanavyosema kuwa Wolper ana umri mkubwa kumzidi.

Msikilize zaidi hapo chini akiongelea mahaba yake na Wolper.


Ushauri: Nina Naumbile Madogo ya Uume (Kibamia), Naogopa Kutembea na Wasichana

0
0
Amakweli mungu hakunyimi vyoote na haupi vyoote pia. Mimi ni kijana wa miaka 21, mwembamba kiasi nina body naturaly,maji ya kunde, mrefu wastani sio handsam sana but mtanashati najiheshimu, mstaarabu kutokana na sifa nilizo kuwa nazo imepelejea kupendwa sana na wanawake.
Wengine hupigana na kupelekana hadi polisi kwajili yangu pasipo mimi kuwa na mahusiano nao yani ni wivu tu na nimetongozwa na wanawake tangu nikiwa na miaka 15 na wengine ni wakubwa kwangu na wengine wanakuja hadi mbele ya mama na kueleza hisia zao kwangu ila mimi sina mpango nao kabisa yani.

Hii inapelekea hadi mama yangu kupoteza imani na mimi kwa kuhisi huenda mwanae ni shoga ama sifanyi kazi kama dume.Ila mimi sio kama siwatamani au siwataki ila nina tatizo moja linalonifanya mpaka nishindwe kujielewa wakati mwingine najipiga ukutani kwa hasira, but nashindwa nifanye nini.
Ninawaza sijui nimwambie mama yangu au baba yangu ila nawaza nitaanza je kuwaambia tatizo langu ikiwa baba ni mkali sana na mda mwingine hataki hata salamu na katika familia walio nitangulia kuzaliwa ni wanawake wote daaaah.! inaumasana ninapo muona mamayangu akitoa chozi pindi akiwa na waschana Wanaokuja mbele yake kwaajili yangu.

Pia hii imenifanya nishindwe hata kutembea mtaani kwa kuhisiwa mimi ni shoga ila tatizo langu sio kabisa yani daah..! Nawaza nitafanya vipi mapenzi na msichana ikiwa mimi nina UUME MDOGO saana nilipo upima kwa rula ni wa nchi 4 so hivi msichana yeyote anaweza kuhisi uume huu kweli daaah..
Why mimi waungwana naombeni msaada ni nini nifanye nimwambie mama akamueleze baba labda atanisaidia kupata dawa au kama kuna dawa ni wapi napata na ni ipi coz naona ninakoelekea sio kabisa.

Naombeni msaada naombeni

EXCLUSIVE: Aunty Ezekiel Kaelezea Siku Mose Iyobo Alipohisi Mtoto Sio Wake

0
0
Mwigizaji Aunty Ezekiel amekaa kwenye Exclusive ya AyoTV na kuelezea vitu kadhaa kwenye mapenzi yake na Dancer wa Diamond Platnumz  Mose Iyobo ambapo miongoni mwa alivyoongelea ni pamoja na siku ambayo Mose alihisi ujauzito aliokua nao Aunty sio wa mtoto wake.

‘Kwanza Mose Iyobo aliniambia niitoe hii mimba nilipomuuliza kwanini akasema najua wewe Aunty Ezekiel huwezi kuzaa na mimi, akaniambia hajajipanga sababu ana mtoto mwingine, nilimwambia hii mimba ni yangu na kila afanye maisha yake kama ni hivyo….‘ – Aunty Ezekiel

Video : Ommy Dimpoz Ana Utajiri wa Milioni 400? Msikie Mwenyewe Hapa

0
0
Basi Dimpoz atakua na pesa ndefu, Ommy Dimpoz anapiga madili ya hela ndefu. Siku chache zilizopita Ommy Dipoz akiwa na mastar wenzake alipokea simu ya dili la milioni 400 unajua alichokisema???? Utashangaa sana hebu mskie mwenyewe kwenye video hii.....


Video : Sikiliza Kionjo cha Wimbo Mpya wa Nay Wamitego - Kati Patamu...TCRA Watauacha??

0
0
Wengi wanamjua Nay Wa Mitego kwa kutoa nyimbo nyingi sana zikiwa za utata, mara nyingi hua anawachana watu maarufu bila kuwaogopa au ujumbe ndani ya nyimbo kua na utata. Haya basi katika pitapita zetu tumepata kionjo cha wimbo wake mpya ambao bado haijajulikana hasa utatoka lini.

Wimbo huo unaenda kwa jina la pale kati patamu, kwa tafsiri za kwetu mtaani nina uhakika kabisa kua huu wimbo ukiachiwa utakua gumzo sana . Sio tu mtaani hata huko mitandaoni ambapo nadhani TCRA wanaweza kufanya yao. Unaweza skiliza video ya wimbo huo hapa chini......

Video : Idriss Alimfanyia Wema Sepetu Haya, Mara Baada ya Kusikia Wema Sepetu Katukanwa na Harmonize

0
0
Baada ya kusambaa kwa video ya Harmonize akimsema vibaya Wema Sepetu, watu wengi walilaani kitendo hicho huku kuna baadhi yao wakimpongeza Harmonize. Habari kutoka kwa marafiki wa karibu wa Wema Sepetu zinasema kua aliumia sana alipoiona video hiyo kwa mara ya kwanza.

Wengi walitaka kujua Idriss alipokeaje swala hilo, basi hii ni Exclusive kutoka kwa Wema akielezea kitu alichofanyiwa na Idriss na kumtia moyo katika kipindi hicho kigumu. Wema alimshukuru sana Idriss kwa wema wake,

Unaweza tazama video ya alichokisema Wema Hapa....

John Heche: Rais wa China Alipokuja Tanzania Aliondoka na Pembe za Tembo

0
0
Akichangia kwenye bajeti ya mali asili na utalii mbunge John Heche amezungumzia operesheni tokomeza jinsi ilivochezea watu rafu na kuuawa kama wanyama.

Hapo hapo amegusia kuwa Rais wa China alipokuja Tanzania aliondoka na pembe za tembo na hii iliripotiwa na vyombo vikubwa vya habari duniani kama Al Jazeera na BBC lakini serikali haikujibu wala kuchukua hatu.

Lakini serikali hii iliwaua wananchi na kuua mifugo yao ili kutokomeza ujangiri kumbe majangiri ndio wao wenyewe 

 Video Hapa:

Video : Wema Sepetu na Martin Kadinda Wakiimba Wimbo wa Harmonize na Diamond Platnumz

0
0
Hii imekua ni wiki mbaya kidogo kwa msanii Harmonize kutoka WCB, mara baada ya video moja kusambaa sana mitandaoni ikimwonyesha akimtukana mwanadada Wema Sepetu. Ukweli ni kua Wema ameumizwa sana na video ile hadi kuenea kwa habari ambazo hazijathibitishwa kua kamfungulia kesi Harmonize.

Ambacho Harmonize hakujua ni kua Wema ni shabiki wake mkubwa kwani ni zaidi ya mara moja wema ameonekana akiimba wimbo wa msanii huyo. Na kitendo cha Wema kuona video ile kunaweza kufanya akaacha kua shabiki wa Harmonize.

 Unaweza tazama video ya Wema Sepetu na Martin Kadinda wakiimba wimbo wa Harmonize hapa chini

Mbaroni Kwa Kukutwa Wakitoa Mamilioni Kwa ATM Za Watu 19

0
0
Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kukamatwa wakiwa wanatoa fedha benki ya NMB tawi la Mpanda kiasi cha shilingi 3,680,000 wakiwa na kadi za ATM 19 mali za watu tofauti pamoja na namba za siri za kadi hizo. .

Kaimu Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Katavi Damasi Nyanda amesema watuhumiwa hao watatu walikamatwa jana majira ya saa tatu usiku katika Tawi la NMB Mpanda .

Watuhumiwa hao ambao majina yao yamehifadhiwa kwa kuwa upelelezi bado unaendelea, wamekamatwa na askari wa jeshi la polisi waliokuwa wakilinda Benki hiyo.

Nyanda ameeleza kuwa watumiwa walikamatwa baada ya askari polisi kuwatilia mashaka kutokana na kuwaona wakiwa wamekaa muda mrefu kwenye chumba cha mashine ya kutolea fedha .

Amesema baada ya kuwatilia mashaka polisi waliingia ndani ya chumba hicho na kuwakuta watuhumiwa hao wakiwa wanaendelea kutoa fedha katika mashine tatu zilizomo kwenye mashine za kutolea fedha.

Kaimu Kamanda alieleza ndipo askari polisi walipoamua kuwapekua watuhumiwa na waliwakuta wakiwa na kadi za ATM 19 mali za watu tofauti pamoja na namba za siri za kadi h izo na walikuwa tayari wameishatoa kiasi cha fedha taslimu shilingi 3,680,000.

Amezitaja Namba za Kadi za ATM walizokamatwa nazo watuhumiwa kuwa ni AC 61908000058,AC 61902403196,AC61902400417,AC61908000427,AC 61902240100,AC 61908000237, AC 61902400518 AC 61910000645, AC 61910004240,AC 61908000609 AC 61902403168.

Kaimu kamanda Nyanda amezitaja kadi za ATM zingine zilizokamatwa kuwa ni zenye namba AC 61910000537,AC 61902402653, AC 61910000250, Ac 61902400818, AC 61908000449,AC1902403219 AC 61910002329 na AC 70408100131.

Amesema watuhumiwa wanatarajia kufikishwa mahakamani baada ya uchunguzi wa tukio hilo kukamilika na bado watuhumiwa wote watatu wanaendelea kushikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano zaidi .

Kaimu kamanda ametoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kutoa siri kwa watu za namba zao za siri za kadi wanazozitumia kwenye  ATM za  benki .

VIDEO:Mkuu wa Mkoa Afumaniwa Akifanya Mapenzi na Mwanae

0
0
Mkuu wa zamani wa Mkoa wa Kaskazini Pemba na mshauri wa Rais wa Zanzibar kisiwani humo, Dadi Faki Dadi amekamatwa akituhumiwa kufanya mapenzi na mtoto wake wa kambo.

Dadi alikamatwa juzi akidaiwa kukutwa na mtoto huyo wa mkewe wa ndoa mwenye umri wa miaka 21 katika nyumba ya kulala wageni inayoitwa Executive, jirani na makao makuu ya Uhamiaji Zanzibar katika eneo la Kilimani chini na Maisara, mjini Unguja.

Mwanasiasa huyo alijikuta akipigwa pingu na polisi akiwa kifua wazi mbele ya mkewe na wanafamilia na kisha kupelekwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Mwembemadema.

Picha za video zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, zilimwonyesha Dadi akikabiliwa na mashambulizi makali ya maneno kutoka kwa watu waliomkamata, akiwamo mkewe.

“Mwacheni avae nguo kwanza, mpeleke bwana, twende bwana..." ni baadhi ya maneno yanayosikika katika video iliyorekodiwa wakati wa kumtia mbaroni.

Taarifa zilizopatikana miongoni mwa wanafamilia ya kiongozi huyo, zilidai kwamba alikamatwa baada ya kumtilia shaka binti huyo kutokana na mienendo yake ya hivi karibuni na kuamua kumfuatilia.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkadam Khamis Mkadam alithibitisha kumshikilia Dadi kwa muda kabla ya kumwachia kwa dhamana.

“Kijamii alitenda kosa, lakini sisi tunaendelea kufanya uchunguzi, iwapo tutabaini ametenda kosa la kisheria na anaweza kuwa mashtaka tutamkamata ili kumpeleka katika vyombo vya sheria,” alisema Mkadam.

Mmoja wa wanafamilia ambaye aliomba jina lake lisitajwe alisema: “Mwizi siku zake ni arobaini, tulimtega na hatimaye tumemnasa sasa tuone mwisho wake utakuwa nini na kipi kitajiri baadaye.” Tazama Video:

Isabela Afunguka 'Inaniuma Sana Kalama Kuniacha Mimi na Kumuoa Shoga Yangu'

0
0
Luteni Kalama na Mkewe aliyefunga naye ndoa hivi karibuni
SIKU chache baada ya Mbongo Fleva, Kalama Bakari ‘Luteni Kalama’ kuvuta jiko, hatimaye, aliyekuwa mchumba wa muda mrefu wa msanii huyo ameibuka na kusema anaumia kuona aliyeolewa alikuwa ni rafiki yake wa karibu.

Kalama alimuoa binti aitwaye Aisha Yassin wiki iliyopita ambapo saa chache baada ya ndoa hiyo kufungwa na picha kusambaa mitandaoni, wapenda ubuyu waliibuka na kuanza kueleza kuwa Kalama ameona shosti wa Isabela.

“Hili jambo sio siri limetuacha midomo wazi sisi tunaowajua vizuri hawa watu, walikuwa wanajifanya shemeji shemeji huku wanazima taa, isitoshe kwanza nasikia ana mtoto wa mwaka mmoja, yani ni majanga tupu, bora angemuachia Isabela aendelee na mtu wake waliyetoka mbali,” alisema mdaku mmoja.

Akiizungumzia ishu hiyo, Isabela alisema ameumia kuona Kalama amekwenda kwa rafiki yake kwani bora angemchukua mtu mwingine.
Luteni Kalama akiwa na Mkewe wa zamani, Isabela Mpanda

“Nimeumia. Rafiki yangu wa damu ambaye alikuwa anakuja tunakunywa wote na akionyesha kumheshimu Kalama kama shemeji yake eti leo kanigeuka, hii yote sababu yule mwanaume naye anapenda kulelewa halafu yule demu kidogo yupo vizuri kifedha.

“Japo nilikuwa nimeshamuacha Kalama kwa kuwa niliona ananipotezea muda, niliumia sana kwamba kwa nini awe rafiki yangu? Mungu atawaadhibu,” alisema Isabela.

Alipotafutwa Kalama na kusomewa mashtaka ya Isabela, alisema mwandani wake huyo wa zamani kakosa cha kuongea yeye aliachana naye kwa kuwa walishindwana na wala huyo mke wake hakuwa rafiki yake.

“Anatapatapa tu Isabela, ninachofahamu mimi ndio mume halali wa Aisha, kuhusu kuwa rafiki yake wala Bela hamjui huyo mwanamke vizuri, sioni cha ajabu kuoa mtu mwenye mtoto, atuache tufurahie maisha ya ndoa,” alisema Kalama.

Wimbo wa Aje Ilikuwa Suprise kwa Wema Sepetu – Alikiba Afunguka

0
0
Akiongea kwenye kipindi cha Friday Night Live, Alikiba almesema wimbo huo hajamuimbia Jokate na wala hajawahi kumuimbia mtu yeyote, bali aliimba kwa ajili ya mashabiki wake.


” Sijamuimbia mtu yeyote kwa kweli, mi nimeimba kwa ajili ya mashabiki wangu, kwanza sijawahi kumuimbia mtu kabisa, sijawahi, so ni kwa ajili ya mashabiki wangu”,.

Lakini pia Alikiba alisema kuwa kitendo cha kuwataja wasanii wa Filamu Wema Sepetu na Lulu kwenye wimbo huo, ilikuwa ni suprise, hivyo wenyewe hawakujua kuwa wameimbwa, isipokuwa alishawahi kumdokeza Wema Sepetu ambaye ametaja kuwa ni rafiki yake mkubwa.

“Wenyewe walikuwa hawajui kuwa nimewaimba, ila Wema nilimwambia siku moja kuwa bichwa nina suprise yako, ila Lulu sikuwahi kumwambia na hata sijui ameipokeaje, ila naamini kaipokea fresh”, alisema Alikiba.

Kitu ambacho bado kinawapa kigugumizi watu ambao walikuwa wakifuatilia kipindi hicho, pale aliposhindwa kuchagua kati ya Wema Sepetu na Jokate, na kusema anawachagua wote, na kuzidi kuweka hali ya sintofahamu kwa wawili hawa (KIba na Jokate) huenda bado wako pamoja.

Wimbo wa 'Panya' Wakiponza Kitua cha EATV, Chapigwa Faini ya Milioni 3 na TCRA

0
0
Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), imevitoza faini vituo vya East Africa Television na Entertaiment FM (E- FM) baada ya kukiuka kanuni za utangazaji.


Akisoma nakala ya hukumu hiyo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya TCRA, Joseph Mapunda alisema baada ya kupitia maelezo ya utetezi kutoka kwa viongozi wa vituo hivyo, kamati hiyo imeamua kuitoza EATV faini ya Sh3 milioni na Sh4 milioni kwa E-Fm.


“Pamoja na adhabu hiyo tumetoa onyo kali kwa kukiuka kanuni ya maudhui, lakini pia endapo kosa hili litajirudia tunaahidi kutoa adhabu kali zaidi,” alisema.


Katika maelezo ya awali ya hukumu hiyo, Mapunda alisema adhabu ya EATV imetolewa baada ya kituo hicho kupitia kipindi chake cha muziki mnene kurusha video ya wimbo wa Panya wa kundi la muziki la Bracket kutoka nchini Nigeria uliomshirikisha msanii Techno.


“Baadhi ya mavazi yaliyotumika katika wimbo huo hayaendani na maadili ya Kitanzania. Na kwa upande wa E-FM wameadhibiwa baada ya kurusha kipindi cha Ubaoni kilichotoa simulizi ya msichana mchawi aliyekiri kuua,”alisema Mapunda.


Baada ya kupokea nakala ya hukumu hiyo, Mkurugenzi wa EATV, Regina Mengi alisema hawana tatizo na adhabu hiyo na kwamba, atalifikisha suala hilo kwa uongozi wa kampuni yao.


“Bado siwezi kujibu lolote, uamuzi wa kuikubali au kukata rufaa itategemea na uamuzi wa bodi,” alisema.


Mkurugenzi wa E-FM, Scolastica Mazula alisema ameridhishwa na hukumu iliyotolewa, hivyo haoni kama kuna sababu ya kukata rufaa.


Mamlaka hiyo imevitaka vyombo vyote vya utangazaji nchini kuzingatia maadili na taratibu za sheria zinapofanya kazi ili kuepuka kuleta athari katika jamii.

Serikali Yaifungia Kuandikisha Wanafunzi Shule ya Al Muntazir Kwa Kupandisha Ada na Kutoza Faini

0
0
Serikali imeifungia kuandikisha wanafunzi kwa vidato vya kwanza na tano shule ya Al Muntazir iliyopo jijini Dar es salaam kwa kupandisha ada kinyume cha taratibu na Wizara ya elimu.

Pia shule hiyo imetuhumiwa kuwatoza faini wazazi wanaochelewa kulipa ada.

Ikumbukwe kuwa mwanzoni mwa mwaka huu serikali serikali ilipiga marufuku shule binafsi kupandisha ada kiholela na ikiwa shule inataka kufanya hivo ilitakiwa kuomba kibali kwa kamishna wa elimu.

Apigwa Risasi na Kuuwawa na Majambazi Mbezi

0
0
Jana usiku yametokea mauwaji ya mtu mmoja mwanaume kwa kupigwa risasi na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi katika Bar ya Kadabla iliyopo katikati ya Mbezi kwa Msuguli na Kibanda cha Mkaa.Mauwaji hayo yametokea kati ya majira ya saa tano usiku hadi saa saba usiku

Mashuhuda wa tukio katika eneo hilo wanasema marehemu alifika katika Bar hiyo ambayo amezoea kufika mara kwa mara anapokuwa anatoka kwenye mihangaiko yake maeneo ya K'koo,usiku wa jana alifika akiwa peke yake na kuegesha gari kisha kuanza kupoza koo.

Baada ya muda kupita,alimpigia mkewe ambaye wanaishi nae maeneo ya Mbezi Mwisho eneo la Tanesco njia ya kwenda Malamba Mawili,wito huo kwa mkewe ilikuwa kwa ajili ya kukaa wote ili waagize "kitimoto" na kuburudika pamoja.Katika ya burudani ya moja moto na mbili baridi huku kitimoto ikiwa inakaangwa jikoni kwa Mangi,walikuja watu wasiopungua wawili na kuanza kugongagonga gari lake,ilibidi aamke ili kujua kulikoni watu hao kugonga gari lake?

Baada ya maulizo hayo,wale jamaa wakamwambia wao wanataka pesa,wanajuwa ana pesa ndani ya gari,hivyo wanazitaka.Yakatokea mabishano na baadae jamaa wakampiga risasi mbele ya mke wake na kuchukua maisha yake huku wakitokomea na kiasi cha pesa kilichokuwepo.Kulizuka taharuki na watu kuacha vinywaji vyao na chakula juu ya meza na kutawanyika,hata waliokuwa "tungi" waliweza kukimbia bila kuyumba.

Msiba uko nyumbani kwa marehemu maeneo ya Mbezi Mwisho(Tanesco Maghorofani) njia ya kwenda Malamba Mawili.Bwana alitoa na bwana ametwaa,Jina lake lihimidiwe.

Polisi iamke na kutazama matukio haya ya uhalifu maana watu wanauwa wazi wazi na silaha za moto zimeenea hovyo hovyo.

Mama Ngwea Afunguka Kuhusu Ngwea Kutumia Madawa

0
0
Akiongea na Planet Bongo ya East Africa Radio, Mama wa Mangwea Bi. Denisia Constantino amesema mwanaye hakuwa mtumiaji wa madawa hayo, kwani yeye kama mzazi alishawahi kumuuliza na kukataa, na kusema iwapo angekuwa mtumiaji angemgundua.

“Kusema kweli mimi naweza nikasema hicho kitu wanachosema wenzake, naweza nikakataa kwa sababu alivyokuwa akija hapa nilikuwa najaribu kuongea naye, kumuelekeza, na kama hayo ni masuala sijui kuhusu dawa, ye alikuwa nasema mama kwa nini mtu ujiumize? Mimi vitu kama hivyo kwa kweli sipo, na ndio maana napenda ku-crush hasa mtu kama anataka kuniongelesha vitu ambavyo haviendani kabisa na utaratibu katika maisha yakwangu, bora nishike ninalojua mwenyewe nafanya nini katika kazi zangu”, alisema mama yake Mangwea Bi. Denisia Constantine.

Pamoja na hayo mama wa msanii huyo amesema kabla hajafariki Ngwea alikuwa akimlalamikia kubaniwa kazi zake, lakini hakuonesha kukata tamaaa.
Viewing all 104429 articles
Browse latest View live




Latest Images