Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104774 articles
Browse latest View live

Serikali Yapiga Marufuku Pombe Ya Viroba ya Kwenye Mifuko Ya Plastiki

$
0
0
Mifuko ya plastiki inayofungasha pombe maarufu kama ‘viroba’ imepigwa marufuku na Serikali kuanzia mwakani.

Sambamba na hilo Serikali pia, imepiga marufuku moja kwa moja utengenezaji, usambazaji, uingizaji nchini wa mifuko ya plastiki kuanzia mwaka huo.

Waziri wa Nchi , Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba aliwaambia wanahabari jana sehemu kubwa ya mifuko hiyo inayotolewa bure imekuwa ikichangia uchafuzi wa mazingira kwa kiasi kikubwa.

Wakati Makamba akiyasema hayo, Februari mwaka huu Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Luhaga Mpina aliondoa zuio la matumizi ya mifuko ya plastiki akisema kuwa itaziweka rehani ajira za Watanzania wanaofanya kazi kwenye viwanda vinavyotengeneza mifuko hiyo.

Pia, Mpina alisema itapunguza kasi ya uwekezaji wa viwanda vilivyowekeza katika bidhaa hiyo.

Akizungumza katika siku ya Mazingira Afrika, Mkurugenzi wa Mazingira, Dk Julius Ningu alisema maamuzi hayo yamelenga kulinda viwanda vilivyoajiri mamia ya Watanzania, tofauti na nchi nyingine zinazotegemea wazalishaji wa nje ya nchi.

Makamba akizungumzia uamuzi mpya wa kuzuia mifuko ya plastiki, alisema matumizi ya mifuko inayofungashia vileo na inayotumika katika matumizi mengine husambaa na kuchafua mazingira. Alisema mifuko ya plastiki inatajwa kuziba mifereji na kusababisha mafuriko na athari nyingine za mazingira.

“Leo (Jana), tumeamua kutangaza ili kuwaanda wahusika wasiendelee kuwekeza katika mifuko hii badala yake wasubiri utaratibu mwingine utakaowekwa na Serikali,” alisema Makamba na kuongeza kuwa:

 “Asilimia kubwa ya uchafu kwenye nyanzo vya maji, mito, maziwa na fukwe za bahari ni mifuko ya plastiki.”

Makamba ambaye pia ni Mbunge wa Bumbuli, alisema Serikali inakamilisha majadiliano ya ndani na baadaye itawahusisha wadau kuhusu dhamira ya kupiga marufuku ya moja kwa moja mifuko hiyo.

Alifafanua kwamba Serikali itatoa muda kwa walioajiriwa, kujiajiri na kuwekeza kwenye biashara ya mifuko hiyo ili kujiandaa kuacha shughuli hizo na badala yake itawezesha mazingira ya utengenezaji na upatikanaji wa vifungashio mbadala.

“Kwa wanaotengeza mifuko hii na kuiuza katika soko la nje hatuna tatizo nao waendelee. Ila kwa soko la ndani hawataruhusiwa kufanya hivyo.Zuio hili litakuwa la kisheria siyo kwa maneno,” alisisitiza Makamba.

Aliongeza kuwa katika kuonyesha Serikali imedhamiria kupambana na hali hiyo wizara yake imeamua kutuma timu ya watu watano kwenda Rwanda kujifunza namna bora ya kudhibiti matumizi na kuzuia mifuko hiyo tangu mwaka 2008.

Waziri huyo alitoa wito kwa watengenezaji, wasambazaji na waagizaji wa mifuko hiyo kujiandaa na zuio hilo na katika siku zijazo Serikali itatoa utaratibu na maelekezo ya tarehe ya kuanza zuio huku taratibu nyingine za kina zikifuata ili kuondoa mkanganyiko.

 Katika hatua nyingine, Makamba alisema maadhimisho ya kitaifa ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo hufanyika Juni 5 kila mwaka hayatafanyika kitaifa badala yake wizara imewaelekeza wakuu wa mikoa kufanya maadhimisho katika maeneo yao.

 “Tumewapa miongozo kuhusu utekezezaji wa shughuli hizo za maadhimisho zinazolenga kutoa hamasa ya hifadhi ya mazingira hususan nyanzo ya maji amabayo ni muhimu kwa viumbe hai,” alisema Makamba.

Kwa mujibu wa Makamba, kauli mbiu ya mwaka huu kitaifa juu ya maadhimisho hayo ni ‘ tuhifadhi vyanzo vya maji kwa uhai wa taifa letu’aliwashauri na kuwataka Watanzania kutumia siku hiyo kupanda miti, kudhibiti uchomaji wa misitu

Ofisa Mwandamizi Mazingira wa Nemc, Arnold Kisagala alisema nusu ya mifuko ya plastiki nchini inazalishwa na kuingizwa kutoka nchi jirani ya Kenya.

Alisema agizo la Waziri Makamba litawezekana, lakini linahitaji ushirikiano kutoka kwenye sekta zingine kwa kuwa viwanda vingi vya mifuko ya plastiki vipo Kenya.

"NEMC tayari tulishaanza mazungumzo na wazalishaji kuhusu mifuko ya plastiki,” alisema.

Hii Ndio Ngoma Harmonize Kaamua Amwimbie Mpenzi wake Wolper

$
0
0
Penzi la Harmonize na Wolper lnazidi pamba moto hadi imefikia mpaka Harmonize kumtambulisha Wolper kwa mama yake mzazi. Harmonize alimtambulisha Wolper kwa mama yake mzazi akiwa katika show yake huko Mtwara.

 Inasemekana kua Harmonize kadata na penzi la Wolper hadi kaamua kumtungia wimbo akielezea jinsi gani anampenda Wolper. Unaweza uskiliza hapa chini na itakua poa sana ukituachia maoni yako kuhusiana na wimbo huu

Mbwana Samatta Aipeleka Timu Yake ya Genk Europa League

$
0
0
Mbwana Samatta ameandika historia mpya kwenye maisha yake baada ya kuisaidia timu yake ya Genk kushinda mchezo wa fainali ya play off na hatimaye kufu kucheza michuano ya Ulaya (Europa League).

Samatta ambaye alianza kwenye kikosi cha kwanza cha Genk ameisaidia klabu yake kupata ushindi wa magoli 5-1 kwenye uwanja wao wa  nyumbani (Cristal Arena) dhidi ya Sporting Charleroi.

Katika ushindi huo wa magoli 5-1, Samatta amefunga goli moja ambalo lilikuwa ni goli la pili kwenye mchezo huo. Nikolaos Karelis ambaye amfunga hat-trick kwenye mchezo huo alianza kuifungia Genk goli la kwanza kwa mkwaju wa penati dakika ya 17 kisha Samatta akazamisha bao la pili dakika ya 27 kabla ya Sandy Walsh kupiga bao la tatu dakika ya 45 na kuipeleka Genk mapumziko ikiwa mbele kwa magoli 3-1.

Kipindi cha pili Karelis aliongeza bao la nne dakika ya 56 kisha kukamilisha hat-trick yake dakika ya 71 kwa kufunga bao la tano.

Mchezo huo ulikuwa ni wa marudiano, mchezo wa awali Genk walipoteza kwa bao 2-0 kwa maana hiyo hiyo Genk wamefuzu kucheza michuano ya Europa ligi kwa matokeo ya jumla 5-3.

Genk itaanzia kwenye hatua ya awali ya mtoano kabla ya ile ya makundi, kama watafuzu basi watapangwa kwenye hatua ya makundi.

Ni Sahihi, Polisi Mshika Tochi Kuvaa Kiraia na Kujificha Kichakani?

$
0
0
Kwa mara ya kwanza nimekutana na Askari wengi sana ukitoka Arusha mpaka Bagamoyo kuna Askari kibao wanawakamata watu kwa kupima speed, uku wakiwa wamevaa kiraia, na wanapokuwa wanakupiga Toch wanakuwa wamejificha kichakani.

Pili baada ya kukupiga Toch, anakuacha unampta ndo anampigia trafiki aliyevaa sare ya kazi, na kumwambia umepita kwa speed kiasi gani na kumwambia akukamate..
 Je watu hawa wapo sahihi kisheria?

Breaking News:Hoja ya Dharura Wanachuo 7000 UDOM: Naibu Spika Aahirisha Bunge Baada ya Wabunge Kwa Pamoja Kutoka nje

$
0
0
Bunge limechafuka muda huu baada ya Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nasari kuomba mwongozo wa kujadili hoja ya wanafunzi zaidi ya 700 waliofukuzwa chuoni ijadiliwe kama hoja ya dharura.

Naibu spika akaendeleza ubabe hivyo wabunge wa vyama vyote walisimama na kutoka nje.

Chanzo: Radio One

Baada ya Kutoboa Pua Sasa Diamond Aweka Meno ya Dhahabu...Mashabiki wake Waduwaa

$
0
0
Diamond Platnumz's Baby Mama, Zari shared a pic of her hubby, Diamond Platnumz to ask for the fans to vote for Diamond on BET 2016 Awards, On his Pic Diamond platnumz seems to make changes on his teeth, not yet known even he has attached 'golden teeth' or not and has made fake nose piercing again as few weeks did.

Diamond platnumz is in Dallas for his USA tour, when In Dallas he met with Kenyan Comedian Eric Omondi, See a short Video Diamond shared on his account with his Manager, Babu Tale and Eric Omondi.

Meneja wa Alikiba, Seven Mosha, Afanunua Nini Kitakachokuwepo Kwenye Alikiba TV

$
0
0
Series ya taarifa kubwa za michongo ya kimataifa aliyopata Alikiba mwezi huu imeendelea.

Wikiendi iliyomalizika, kampuni ya usimamizi inayofanya kazi naye, Rockstar4000 imetangaza kuingia naye ubia kwa kuanzisha kile kilichopewa jina ‘Alikiba TV.’

Kwa wengi taarifa hiyo iliyoandikwa kwa Kiingereza haijaeleweka vizuri na hivyo nimelazimika kumtafuta meneja wake, Seven Mosha kumuomba atupe ufafanuzi zaidi.

“Aikiba amezindua Alikiba TV ambayo ni content kuhusiana na kazi yake – matukio yote around him kikazi itakayokuwa inapatikana kwenye YouTube channel yake na pia itaanza kuoneshwa kwenye vituo mbalimbali tukianza na SoundCity,” Seven ameiambia Bongo5.

“Alikiba TV itakuwa chini ya mwavuli wa Rockstar Television,” ameongeza.

Kwa mujibu wa tangazo hilo zaidi ya Soundcity ya Nigeria, vituo vingine vya runinga duniani vitakavyoshirikiana naye kwenye mradi huo vitatangazwa. Kwa sasa mashabiki wameombwa kusubcribe kwenye channel yake ya Youtube ili kutopitwa na chochote.

Wiki mbili zilizopita Alikiba alisainishwa recording deal na label maarufu duniani, Sony Music. Kiba anayefanya vizuri na wimbo wake Aje, amekuwa msanii wa pili baada ya Davido kusainishwa kile wanachokiita ‘global deal’ na label hiyo iliyo nyumbani kwa wasanii wakubwa duniani.

Mchungaji Kenya Ahukumiwa Kwenda Jela Kwa Kosa la Kumbaka Mtoto Akidai Anamtoa Mapepo Ukeni

$
0
0

KENYA: Mchungaji ahukumiwa kifungo cha miaka 20 jela kwa kosa la kumbaka mtoto wa miaka 13 akidai alikuwa anamtoa mapepo kwenye uke.

Mchungaji huyo alifika nyumbani kwa wazazi wa binti huyo na kumkuta mama mzazi hayupo ndipo alipomfanyia kitendo hicho



Rais Magufuli Aampa Shavu la Nguvu Spika Mstaafu Anne Makinda

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Mhe. Jaji Shabani Ally Lila kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.

Kabla ya uteuzi huo Mhe. Jaji Shabani Lila alikuwa Jaji Kiongozi. Uteuzi huu umeanza leo tarehe 30 Mei, 2016.

Wakati huo huo, Rais Dkt. Magufuli amemteua Mhe. Anne Semamba Makinda kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF). Uteuzi wa Mhe. Anne Semamba Makinda ambaye ni Spika Mstaafu wa Bunge Ia Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umeanza tarehe 25 Mei, 2016.

Mhe. Anne Semamba Makinda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Ali Mchumo. Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amemteua Prof. Apollinaria Elikana Pereka kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam (Dar es salaam Institute of Technology -DIT).

Prof. Apollinaria Elikana Pereka ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) Morogoro. Prof. Pereka anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Prof. Fredrick Mwanuzi ambaye amemaliza muda wake. Uteuzi huu umeanza leo tarehe 30 Mei, 2016.


Wanawake Kenya Waandamana Kudai Waume zao Wanashindwa Kuwapa Mimba

$
0
0

Wanawake katika jimbo la Ndeiya nchini Kenya walifahamisha kuwa waume zao wanashindwa kuwapa ujauzito kutokana na mwenendo wa unywaji wa pombe haramu ambazo zinaathiri nguvu za kiume.

Katika maandamano ya amani yaliofanyika katika kituo cha biashara cha Thigio, wanawake walioandamana Akhamisi walifahamisha kukerwa na wanaume wanaojihusisha na ulevi kupita kiasi.
Nancy Wangare alifahamisha kuwa katika kijiji 
hicho wanawake wachache walioolewa wamevumilia kwa kiasi kikubwa kutokana na upungufu wa nguvu za kiume kwa waume zao kutokana na pombe wanazokunywa.
Mmoja miongoni mwa wanawake walikuwa wakiandamana alifahamisha kuwa iwapo tabia hiyo ya ulevi haitorekebishwa basi itawalazimu kutoka nje ya ndoa zao na bila wao kujua lolote na kuwahudumia watoto wasiokuwa wao


Picha: Hasheem Thabeet atua Dar kimya kimya

$
0
0


Tangu nimeanza kumsikia, Hasheem Thabeet hajawahi kuwa mtu wa matangazo mengi pale anaporudi nyumbani. Mchezaji huyo wa kikapu aliyefanikiwa kuchezea timu nne zilizopo kwenye ligi ya NBA nchini Marekani, yupo jijini Dar es Salaam kwa

Mchezaji huyo aliyeenda hewani, Jumamosi alionekana kwenye viwanja vya Leaders alikoenda kwenye tamasha la Nyama Choma.

Akiwa NBA Hasheem alichezea timu nne tofauti zikiwemo Memphis Grizzlies (2009 – 2011), Houston Rockets (2011–2012), Portland Trail Blazers (2012) na Oklahoma City Thunder (2012–2014).

Pia amechezea timu zingine za ligi ya chini, D-League Dakota Wizards, Rio Grande Valley Vipers na Grand Rapids Drive.

Katika misimu yote tisa aliyowahi kucheza, Hasheem alikuwa na wastani wa pointi 2.2, 2.7 rebounds, na 0.8 blocks kwa kila mchezo. Tafsiri yake ni kuwa mchezaji huyo hakuwa na mafanikio sana kwenye ligi hiyo.


Familia ya Hamisi Tambwe Yamtaka Kuachana na Mambo ya Timu ya Simba

$
0
0




Siku chache baada ya mshambuliaji wa Yanga, Mrundi, Amissi Tambwe kudai kuwa kama uongozi wa Simba utamuomba radhi kwa mabaya yote uliyomfanyika wakati akiitumikia klabu hiyo anaweza akarejea klabuni hapo, familia yake imemuonya kuachana kabisa na suala la kuizungumzia Simba.

Tambwe, ambaye ndiye Mfungaji Bora wa Ligi Kuu Bara akiwa na mabao 21, ametakiwa na familia yake kufuta ndoto za kurudi Simba.

Tambwe alisema kuwa baada ya wazazi wake kusikia hivyo, wamemuonya na kusema kuwa Yanga ndiyo sehemu sahihi kwake kwani anaishi kwa amani bili ya masimango yoyote tofauti na alivyokuwa Simba.


“Wameniambia kuwa hawataki kusikia kitu chochote kinachohusiana na Simba ila wanataka kusikia mambo ya Yanga.


“Waliniambia kuwa walikasirika sana kusikia habari hizo, nikawaambia kuwa sikuwa namaanisha kuwa nataka kurudi Simba kwa sasa.


“Nilichokuwa namaanisha ni kwamba kama itafikia siku Yanga wakaamua kuniacha halafu Simba wananihitaji kwa wakati huo, basi watatakiwa kuniomba msamaha kwanza kwa yale yote mabaya waliyonifanyia nilipokuwa klabuni hapo ndipo niweze kujiunga nao,” alisema.


Tambwe hivi sasa yupo kwao Burundi ambako ameenda kwa ajili ya kuitumikia timu yake ya taifa.


Vanessa Mdee na Shilole Wamaliza Beef yao Jukwaani...Picha Ilivyokuwa Nimekuwekea Hapa

$
0
0

Vanessa na Shilole wakijaribu kuelezea juu ya bifu lao.



 Mtangazaji wa kituo cha Clouds FM, Hamisi Mandi ‘B12’, akiwakaribisha Shilole na Vanessa Mdee tayari kwa kufanya shoo hiyo.



 Shilole akifanya makamuzi.



 Vanessa akikamua jukwaani.


 Baadhi ya mashabiki wakifuatilia shoo hiyo.


WAREMBO wanaofanya vyema kwenye tasnia ya muziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Vanessa Mdee, usiku wa kuamkia leo wameweza kuvunja bifu lao ambalo limekuwa likivuma kwenye mitandao ya kijamii baada ya kukamua kwenye steji moja ndani ya ukumbi wa Bilicanas.


     Shilole (kulia)  akipashana jukwaani na Vanessa kabla ya shoo hiyo kuanza.

‎Mange‬ Kimambi Afunguka BAADA Ya ‪‎KUSAMBAA‬ kwa Video ya ‪MAKAHABA‬ waimtukana Rasi ‪‎Magufuli‬ na Paul ‪‎Makonda‬

$
0
0
Blogger Maarufu Amefunguka haya Hapa Chini:

"mangekimambi_ Wengine tunamtukana Magufuli Kwa kutupokonya #bungelive Wengine wanaomtusi Kwa kuwanyima kujiuza..... Nimechoka kabisaaaaaa
.
.
Huyo dada ndo kiongozi wa machangu Dar.... Eeh na wenyewe wana viongozi wao ...
.
.
Ila Magu hajajua jinsi ya Kuwa successful dictactor . Yani hajajifunza how to manage udictactor na wananchi wakatulia ajifunze China. China wananyimwa Kila kitu, no internet sijui social media Yani China hakuna cha Instagram, Facebook wala ushenzi huo, Au hata blog hizi za blogpost hazipatikani, hakuna kuikosoa serikali na wananchi hawafurukuti hakuna anaelilia Facebook wala bungelive, Yani wachina hawana time Unadhani ni kwamba wanaogopa jeshi Lao?? hamna ni kwamba wameridhikaaaa, Yani wananchi wa China wanapewa Maisha mazuri, umaskini unapungua Kila siku, economy inakua Kila siku, GDP inapanda Kila siku, social care nzuri, kibiashara nchi Sasa iko juu ya dunia nzima , Elimu ya China iko juuu Kila siku inazidi Kuwa nzuri, ukiacha Hiyo wananchi wa China wanaachwa watiane wanavyotaka, wajiuze wanavyotaka, China umalaya nje nje, Kila kona unaulizwa ' you want massage?' nakumbuka Hong Kong unakuta mtaa mzima ni madanguro tu wachina wanajiuza tani Yao, Yani ni K yako inaweza kuhimili mechi ngapi hakuna wa kukubugudhi.Sasa watu Kama hao Unadhani watajali eti Raisi awe dictactor?? Hakuna atakaejali maana vitu vya maana wanapata vyooooote. .

Yani ukitaka Kuwa dictactor make sure nchi haina umaskini, Kila mtu ana Maisha mazuri, mhospital mazuri, dawa za kumwaga na watu watu wanafanya NGONO Kwa kujinafasi. Hivyo vitu viwili usipowapa wananchi Alafu unaleta udictactor lazma utanyonywa kamasi za pua na wananchi . binadamu wanataka 2 things only, pesa na ngono finish. Sasa Magufuli yeye Pesa za kuwapa watanzania hana umaskini ndo umezidi Sasa Hivi watu chai wanakunywa bila sukari , watu shida zimewajaaa Hadi makalioni, mpaka Elimu majanga Yani watu hawana future, wanafunzi wanatolewa vyuoni wanaambiwa warudi majumbani, uwiiiiii Alafu na ngono anakataza, ,,, yani Inshort watu hawana hela Alafu na ngono pia wanabanwa then hapo hapo Raisi anataka kuleta udictactor no Bunge live, no kumsema kwenye social media , weeeeee hapo udictactor lazma ufeliiiiiiiiiii" Mange

Kesi ya Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Zanzibar Kufumaniwa Akifanya Mapenzi na Mtoto Wake Yatupiliwa Nje

$
0
0
Kesi ya Faki Dadi Faki yatupiliwa nje maana binti ni mtu mzima ana miaka 21 though yuko form 6. Na sio mtoto wa kumzaaaa so hakuna incest.Na wala binti hakumshtua mamake ilikuwa Ndo mchezo wao mama mtu aliwafatilia mwenyewe.. Hata ile video ukiangalia utamuona binti anavaa chupi huku anapiga kelele analia... Mtu alie panga na manake Kweli anavua Hadi chupi??? Mimi kilichonistua kuhusu story ya Kuwa binti alisema Kwa mamake ni jinsi alivyo Kuwa analia Kwa mshtuko huku akivaa chupi..So conclusion hapa ni kwamba wooooooote wawili they are to blame because binti ni mzeee mzima.. Wengine 21 Tayari tuna mimba za kina Bhoke, 21 ni mtu na akili zake timamu za kujua asitembeeeee na babake.... Angekuwa 16 tungemtetea Ila Kwa 21 Hapana aiseee....


Alikiba Akanusha Kumuimbia Jokate Wimbo ‘Aje’

$
0
0
Alikiba amesema Aje si wimbo aliomuimbia Jokate wala msichana yeyote bali aliimba kwaajili ya mashabiki wake.

“Sijamuimbia mtu yeyote kwa kweli, mi nimeimba kwa ajili ya mashabiki wangu, kwanza sijawahi kumuimbia mtu kabisa, sijawahi, so ni kwa ajili ya mashabiki wangu,” Kiba alikiambia kipindi cha Friday Night Live cha EATV.

Hata hivyo Kiba alikiri kuwa kumtaja Wema kwenye wimbo huo kimekuwa ni kitu cha surprise kwa mrembo huyo.

Aje ni miongoni mwa nyimbo zinazofanya vizuri kwa sasa si tu Tanzania, bali sehemu nyingi za Afrika.

Zitto Kabwe, Lissu, Lema na Halima Mdee Kusimamishwa Ubunge Kisa Hichi Hapa

$
0
0

Zito ameandika haya katika ukurasa wake wa Facebook :

"Wabunge wafuatao tunajadiliwa kusimamishwa kazi za Bunge kwa vipindi tofauti tofauti. Wabunge hao ni Tundu Lissu,Godbless Lema, Halima Mdee, John Heche, Esther Bulaya na Mimi. Kosa letu ni kutaka Bunge lionyeshwe moja kwa moja na televisheni ya Taifa" Zitto Kabwe

UKAWA yatangaza Kutokuwa na Imani na Naibu Spika

$
0
0
UKAWA yatangaza kutokuwa na Imani na spika, Inaandaa mchakato wa kupiga kura ya kumuondoa madarakani.

Yatangaza kususia vikao vyote atakavyo visimamia

Habari kamili Kufuata hivi punde

Ndani ya siku 20 tu, Mabasi 34 ya DART, yashapata ajali

$
0
0
Zaidi ya mabasi 34 katika mradi wa mabasi yanayoenda haraka yamepata ajali kwa kipindi cha siku 20 toka kuanza rasmi mradi huo kutokana na baadhi ya wananchi na madereva wa magari ya kawaida kutumia barabara maalum za mradi wa DART.

Breaking news; Tundu Lissu na Esther Bulaya Wafungiwa Kuhudhuria vikao vyote vilivyobaki vya Bunge

$
0
0
Tundu Lissu na Esther Bulaya wafungiwa kuhudhuria vikao vyote vilivyobaki vya bunge la bajeti na bunge lijalo la mwezinwa tisa. Vilevile Zitto Kabwe, Pauline Gekul, Godbless Lema na Halima Mdee wafungiwa kushiriki vikao vilivyobaki vya bajeti na John Heche afungiwa kuhudhuria vikao kumi mfululizo vya bajeti kuanzia leo.
Huu ni uamuzi wa kamati Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge chini Mh George Mkuchika (Mb)
Viewing all 104774 articles
Browse latest View live




Latest Images