Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104670 articles
Browse latest View live

Amboni Tanga: Watu 8 Wauawa kwa Kufichua vitendo vya Kihalifu

$
0
0

Watu kadhaa wa kijiji cha Mikocheni karibu na mapango ya Amboni mkoani Tanga wameuawa usiku wa kuamkia leo.

Inasemekana watu waliouawa wanadaiwa kufichua vitendo vya uhalifu kijijini hapo na kwamba miili ya watu hao waliouawa imepelekwa hospitali ya rufaa ya Mkoani humo.

Chanzo : Radio One.

Mya Take : Ulinzi shirikishi unaweka rehani maisha ya raia wema.

Baada ya Kusimamishwa Kuhudhuria Vikao vya Bunge, Zitto Kabwe Acharuka

$
0
0
Rais Magufuli tunakuunga mkono kwa dhati kupambana dhidi ya ufisadi. Tunakupinga kwa nguvu zote kupambana dhidi ya demokrasia.

Kuanzia mwanzo tumekuunga mkono dhidi ya ukwepaji kodi, ubadhirifu, uvivu na uzembe. Tangia mwanzo tulionya kuwa ni lazima udhibitiwe na Bunge ili ufanye kazi kwa mujibu wa Katiba. Hivi sasa wewe Rais ndio unaendesha Bunge kwa remote control. Tutakupinga kuturudisha nyuma. Hutafanikiwa kamwe kubomoa misingi ya taasisi za uwajibikaji tulizoanza kuzijenga.

Narudia nukuu muhimu sana " ukitaka kutawala tawala peke yako. Ukitaka kuongoza ongoza na wenzako". Rais Magufuli Tanzania inataka uongozi madhubuti na sio itawapendeza wa imla. Huko tumeshatoka na Watanzania hawatakubali kurudi huko.

Haya kayaandika kwenye ukurasa wake wa Facebook

Ally Kessy awashukia Zanzibar, Awataka Wabunge wa Zanzibar watoke nje kwa mambo yasio ya Muungano

$
0
0
Awataka wabunge wa Zanzibar kuanzia sasa wachangie Wizara zinazo wahusu, Awataka wawe wanatoka nje pale bunge linapojadili mambo yasiyo ya Muungano, sio wanatujazia foleni ya kuongea hata kwa mambo yasio ya Muungano.

Hivyo kasema Wanapaswa kutoka nje Zinapojadiliwa Wizara Zisizoihusu Zanzibar.

Ally Kessy Mbunge wa Nkasi, amesema Wazanzibar waache kuwanyonya Watanganyika. ameyasema hayo wakati wa kuchangia Wizara ya mambo ya Nje.

Amesema Wabunge kutoka Zanzibar wapo zaidi ya 54, wangekaa kule kwao hata Bunge lao lingeonekana dogo, wasingepata pa kukaa, hivyo wanapokuja wawe wapole.

Amedai wabunge wa Zanzibar wanataka haki sawa katika Uteuzi wa Mabalozi wakati wakati Mabalozi wenyewe ni 21 tu. Kasema kwa kuwa Zanzibar inachangia Asilimia 4, hivyo na mabalozi inabidi wawe asilimia nne. Hata kama wapo Manaibu Balozi wamependelewa tu.

Diva Azungumzia Mabusu yake na GK Yaliyozua Mjadala Mtandaoni

$
0
0
Diva the Bawse anasema hataki kusikia kitu kinachoitwa ‘mila na desturi’ za Mtanzania hasa pale anapofanya kitu kinachompa furaha.

Wiki hii mtangazaji huyo wa Clouds FM amesababisha mjadala mkubwa kwenye Instagram baada ya kupost video inayomuonesha akipigana French kiss na mpenzi wake rapper GK.

“Trying kanye west n kim k yummy tongie crazyyy kiss… guess what. wedding very soon #theregoesmybabyyyyy,” aliandika kwenye video hiyo.

“Nataka niishi the life that I want, mimi I don’t live to please anyone. I just live me as Diva, I just want to be happy,” Diva ameiambia Bongo5.

“The kiss to happiness – tongue kiss is the key to happiness ndio maana mimi sioni ajabu kumkiss mtu.” Mtazame Hapa:

Hakuna Record Label Ninayoweza Kukubali Inisainishe, Watanipa nini Ambacho Sijafanya! – Diamond Platnumz

$
0
0
Diamond Platnumz hana mpango wa kuwa chini na record label yoyote duniani. Infact hitmaker huyo amedai kuwa makampuni kibao yamewahi kummendea yakitaka awe chini yake lakini akayapiga kibuti.

“Mimi nimeshaapprochiwa na makampuni mengi sana kutaka kunisaini, mengi sana, mengi hata wanayoyasikia, mengine wanayasikia,” Diamond ameiambia 255 kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM.

“Lakini nafikiria kwamba unapotaka kunisaini mimi unataka kunifanyia nini? Una kitu gani cha kunioffer cha kuona mimi unisaini? Video? Mimi naweza kufanya video zangu hadi za wasanii wangu. Collabo? Collabo mimi naombwa napigiwa simu, msanii wa Marekani wa Tanzania, yeyote nikitaka kufanya chochote naweza kufanya naye,” ameongeza.

“At the end of the day is all about money, nina capital, nina network, ndio maana nikasema kwa nilipofikia sio nibaki mimi tu, niwe na record label yangu. So sifikirii kusainishwa, nafikiria kusaini watu ili kuweza kusaidiana wenyewe kwa wenyewe.”

“Kwa mfano unataka kunisaini, unataka kunifanyia nini? Nikaperform mbinguni? Tuzo zote ambazo mwaafrika anatakani kuziwin.. sijawahi kupata BET na Grammy tu, nataka nipige na Grammy nioneshe kabisa napiga na Grammy. Ukiniambia nasainiwa it doesn’t make sense. Naamini management yangu ni kubwa kuliko mtu yeyote akinisaini, akisema anifanyie promotion hatoweza kufanya promotion ninayoifanya mimi,” amesisitiza.

Diamond aliyeanzisha record label yake, WCB tayari amewasaini Harmonize na Raymond huku kukiwa na uwezekano kuwa amemshamsaini Rich Mavoko.

Video : Idris Sultan Aanza Kutoza Pesa Kwa Wanaotaka KIKI Kutoka Kwake

$
0
0
Kiki ndio kila kitu hapa mjini, wasanii na watu wengi hapa Bongo wamekua maarufu kutokana na Kiki au Skendo zinazosambazwa kuwahusu wao. Wapo waliofanikiwa hadi maisha yao kua mazuri kutokana na kiki au skendo wanazojizushia ili wajulikane na watu.

Sasa kutokana na watu kuhitaji kiki basi Idriss Sultan ambae kwa sasa anatoka na Wema amenzisha kitu kinaitwa KikiPesa. Yani kama unahitaji kiki kutoka kwake lazma umlipe kwani kupitia yeye unaweza kupata pesa au umaarufu kupitia jina lake. 

Unaweza mskiliza mwenyewe akielezea huduma yake hiyo mpya hapa kwenye video...

Wahadhiri UDOM Wataja Kiini cha Mgomo Kilichosababisha Wanafunzi 7802 Warudishwe Nyumbani

$
0
0
JUMUIYA ya Wanataaluma ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOMASA) imesema kilichotokea si walimu kugoma kufundisha programu ya Stashahada Maalumu ya Elimu, Sayansi, Hisabati na Tehama, bali tatizo ni kutoelewana na Menejimenti ya chuo kutokana na mazingira mabovu ya uendeshaji wa programu hiyo chuoni hapo.

Aidha, imelaani kitendo cha wanafunzi 7,802 wa Programu Maalumu ya Ualimu wa Msingi na Sekondari, waliorudishwa nyumbani bila kupewa muda wa kutosha kujiandaa kwa kuzingatia umri wao na mazingira waliyokuwa wanaishi, hali inayofanya wazagae mitaani huku wakiwa hawana pa kwenda.

Hayo yako kwenye tamko lililotolewa jana na Katibu wa jumuiya hiyo, Lameck Thomas, ambalo lilieleza kuwa lawama zimekuwa zikitupwa kwa walimu kutokana na taarifa hizo kutolewa na upande mmoja, ambao ni Menejimenti ya chuo kwenda serikalini bila kuwepo na taarifa yoyote kutoka kwa walimu kupitia jumuiya yao.

Thomas alisema si kweli kama walimu waligoma kufundisha lakini tatizo kubwa ni kutoelewana kati ya walimu na Menejimenti ya chuo kutokana na mazingira mabovu ya uendeshaji wa programu hiyo chuoni hapo.

"Hatuzungumzii fedha zaidi tunazungumzia suala la kuboresha elimu ili taifa lipate walimu wa baadaye katika kufundisha Sayansi, Hisabati na Tehama, vifaa vya kufundishia navyo ni changamoto kubwa,” alisema.

Katibu huyo alisema kama Jumuiya ya Wanataaluma wanapata hisia kwamba Wizara ya Elimu, imeamua kwa makusudi kushirikiana na uongozi wa chuo kupotosha uhalisia wa jambo hilo kwani hakuna hata wakati moja ambao wamefanya mawasiliano na walimu wenyewe kupata ukweli kutoka upande wao.

“Alichosema waziri bungeni juzi ni taarifa ya upande mmoja ambayo haitatupeleka kwenye utatuzi wa kudumu wa suala hili kutokana na ukweli kwamba walimu nao wana mengi ya kuzungumza,” alisema katibu huyo.

Alisema serikali imejenga desturi ya kuonana na menejimenti za vyuo pindi yanapotokea matatizo bila kupata taarifa kutoka vyanzo vingine hali ambayo imekuwa inasababisha vyanzo sahihi vya matatizo kutojulikana kwa uwazi.

Alisema changamoto za ufundishaji kutokana na uhaba na walimu kulingana na idadi ya wanafunzi waliopo. Akitoa mfano alisema kwa sasa Chuo cha Sayansi Asilia na Hesabu, kina upungufu wa walimu 128 waliokuwa wanahitajika kufundisha programu hiyo kwa ufanisi; na kwa muhula uliopita walimu 72 tu ndio walibeba mzigo wa upungufu huo na muhula huu hali ilikuwa inaelekea kuwa mbaya zaidi.

“Wingi wa wanafunzi na uhaba huu wa walimu ulisababisha upangaji wa ratiba na kufundisha kutokana na ukweli kwamba kozi ziligawanywa katika mikondo mingi ambayo walimu walilazimishwa kuifundisha huku wakiwa na majukumu ya kufundisha kozi za shahada na majukumu mengine,” alifafanua.

Alisema chuo kimekuwa na desturi ya kupokea wanafunzi wengi bila kuzingatia idadi ya walimu waliopo na miundombinu ya kufundishia na kujifunzia na hiyo si mara ya kwanza kwa chuo kufanya hivyo, kwani mwaka 2008 walileta wanafunzi wengi ambao matokeo yake walimu kufundisha masomo mengi kuliko uwezo wao wa kazi.

Alisema taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma ilipotoshwa, kwani haijaeleza ukweli wa madai uliowasilishwa na chuo husika.

Alisema katika Chuo cha Sayansi Asilia na Hesabu taarifa inasema yaliyowasilishwa ni madai ya Sh milioni 367.8 na kupungua mpaka Sh milioni 90 wakati uhalisia ni kwamba madai hayo hata yangebanwa namna gani yasingepungua mpaka chini ya Sh milioni 223.7.

Alisema mfano mwingine ni Chuo cha Elimu Masafa na Sayansi za Kompyuta ambao taarifa inasema waliwasilisha madai yanayozidi Sh milioni 100 wakati taarifa ya chuo inasema ni madai ya Sh milioni 53.7 tu.

Mwenyekiti wa jumuiya hiyo, Edson Baradyana alisikitishwa na yaliyotokea na kuitaka serikali kufanya jitihada za makusudi ili kumaliza mgogoro huo na hilo litawezekana kama walimu, wanafunzi na Menejimenti kukaa pamoja.

Baradyana alisema wanafunzi hawakutendewa haki kwani ilitolewa notisi ya ghafla ya kuondoka chuoni huku wengine wakiwa hawana nauli na hawakujua pa kwenda hali inayofanya waendelee kuzurura mitaani.

Alisema wanaamini kama Menejimenti ya chuo ingeonesha ushirikiano wa karibu kwa walimu wanaofundisha programu hiyo na kushirikiana, hayo yasingetokea au yasingekuwa makubwa kiasi hicho.

“Lazima kuangaliwa na kutatuliwa kwa changamoto nyingine zilizoibuliwa na wanataaluma na wanafunzi katika uendeshaji wa programu hiyo badala ya kujikita kwenye suala la malipo tu, serikali iwe na utaratibu wa kuwasiliana na walimu na wanafunzi mara kunapotokea matatizo vyuoni ili kupata taarifa toshelezi kutoka pande zote,” alisema Mwenyekiti wa Udomasa.

Aidha, wakati wa kurejeshwa nyumbani kwa wanafunzi hao wa Udom kukibebwa kisiasa na vyama vya upinzani, taarifa ya serikali imeeleza kuwa wahadhiri waliogoma, walitaka kulipwa posho ya zaidi ya Sh milioni 900.

Akitoa taarifa ya pili bungeni juzi usiku, Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako  alisema wanafunzi hao si sehemu ya kazi zilizoko katika mikataba ya ajira ya wahadhiri hao, ila ni sehemu ya kazi ya ziada.

Kwa kuwa kazi hiyo ni ya ziada, Profesa Ndalichako alisema walikubaliana walipwe posho ya kazi ya nyongeza ambayo uongozi wa Chuo Kikuu cha Dodoma ulikuwa tayari kutoa zaidi ya Sh milioni 200.

Kwa mujibu wa Profesa Ndalichako, wahadhiri hao walisisitiza kuwa wanataka posho hiyo iwe zaidi ya Sh milioni 900, jambo lililokataliwa na Mkaguzi wa Ndani wa Mahesabu wa Udom aliyesema kuwa kiwango hicho ni kikubwa kuliko uhalisia wa kazi yenyewe.

Kutokana na kutokubaliana kati ya wahadhiri hao na uongozi wa Udom, wahadhiri hao ndio wakaitisha mgomo wa kufundisha wanafunzi hao huku wakiendelea na kazi za kufundisha walio katika programu za shahada ya kwanza na kuendelea.

Profesa Ndalichako alisema kwa uamuzi huo wa wahadhiri, serikali isingeweza kuwachukulia hatua kwa kuwa wamegomea kazi ya ziada na si kazi waliyoajiriwa na kuingia mkataba na chuo.

Kwa hali hiyo, Profesa Ndalichako alisema serikali ililazimika kuingilia kati ambapo Mei 10, mwaka huu Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Stella Manyanya alikwenda chuoni hapo kutafuta suluhu.

Mbali na Naibu Waziri, alisema hata makatibu wakuu wa wizara hiyo nao walikwenda kuzungumza na wahadhiri hao bila mafanikio, huku wanafunzi hao wakikaa chuoni bila kuingia darasani kwa wiki ya tatu.

Profesa Ndalichako alisema mbali na madai ya wahadhiri hao, pia wakati wa kutafuta suluhu ya jambo hilo, walitazama suala la tija kwa wanafunzi hao wa diploma maalumu ambao ni zaidi ya 7,800 na pia kwa wanafunzi wa shahada ya kwanza ambao pia wanapaswa kufundishwa na wahadhiri hao.

Kutokana na kukosa masomo kwa wiki tatu mfululizo na kuwepo kwa uwezekano wa kukosekana tija katika ufundishaji, Profesa Ndalichako alisema ndio uamuzi wa kuwarudisha nyumbani wanafunzi hao ukafanyika ili serikali iangalie upya utaratibu wenye tija zaidi wa kuwaendeleza wanafunzi hao.

Aidha, Profesa Ndalichako alisema wakati wanafunzi hao wakitakiwa kurudi nyumbani, walizingatia hali yao ya kipato, kwa kuwa tayari walikuwa wameshapewa fedha za kujikimu za siku 60 tangu Aprili 21, mwaka huu.

Profesa Ndalichako aliwataka wanafunzi hao kuvuta subira wakati serikali inatafuta namna bora ya kuwapatia elimu hiyo kwa kuzingatia tija kwao.

Video : Kwa Uzuri Huu wa Demu Mpya wa Diamond Platnumz, Zari Atasubiri Sana

$
0
0
Japo kua Diamond amezaa na Zari na kupata mtoto Tiffah, ila kwa sasa kuna tetesi kua Diamond Platnumz anatoka na demu mpya Aitwa Irene. Kwa taarifa zakuaminika kutoka kwa watu wa karibu wa Diamond zinaonyesha ni kweli Diamond anatoka na msichana huyo Toka Mwaka jana.

Sasa huko instagram kumekua na ubishani mkubwa kuhusu nani ni mrembo zaidi kati ya Zari na Irene. Kwa muono wa macho yangu naona Irene aka Bi mdogo ndio mrembo kuliko hata Zari. 

Hebu tazama video yake hapa kisha niambie nani mrembo zaidi kati ya ZAri na Irene....


Rais Magufuli Awatangazia Vita Wafanyabiashara ‘Wajanja’

$
0
0
Rais John Magufuli amesema Serikali yake itaendelea kupambana na wanaoingiza bidhaa zilizochini ya kiwango na wale wanaokwepa kodi.

Amesema kwa kufanya hivyo, wanachangia kuviua viwanda vya ndani ya nchi.

Rais Magufuli ameyasema hayo jana kwenye hafla ya utaoji wa Tuzo ya Rais ya wazalishaji bora wa viwandani kwa mwaka 2015 zilizofanyika jijini Dar es Salaam.

Tuzo hizo zimeandaliwa na Shirika la Wenye Viwanda Nchini (CTI).

Rais amesema pia hatawavumilia watendaji wote watakao wakwamisha wafanyabiashara wenye nia ya kuanzisha viwanda nchini kwa sababu zisizo za msingi na kuwaahidi kuwasaidia waweze kufanikisha ndoto zao.

Pia, amesema ni vizuri wafanyabiashara wote nchini wakatumia fursa zipatikanazo katika awamu hii ya uongozi wake, ili wasije kuzijutia baadaye.

“Nasema kwa dhati kutoka moyoni, you have my support, mkishindwa katika kipindi cha awamu ya tano basi hamtaweza tena,” alisema.

Rais Magufuli alisema nchi inapokuwa na viwanda vingi vitatoa ajira kwa Watanzania, vitaongeza mapato kwa Serikali na kuingiza fedha za kigeni kwa kuuza bidhaa nje ya nchi.

“Nina dhamira ya dhati ndani ya moyo wangu kuwasaidia wenye nia ya kuanzisha ya viwanda, siwachukii matajiri nawapenda matajiri,” alisema.

Rais Magufuli aliwapa moyo wafanyabiashara wenye viwanda kuanzisha vingine ili Serikali iweze kunufaika zaidi.

Alisema Tanzania ina rasilimali nyingi kama maliasili na madini na akawahakikishia wawekezaji kuwa lipo soko kubwa la bidhaa watakazozitengeza lenye watu milioni 160 katika nchi za Afrika Mashariki na Kati.

Magufuli alisema sekta ya viwanda ni muhimili mkubwa wa uchumi katika nchi huku akitolea mfano wa nchi za China, India, Korea Kusini, Malaysia, Thailand na Vietnam  ambazo zimekuwa kwa kasi kwa sababu ya uwepo wa viwanda.

Alisema viwanda vinapoanzishwa nchini badala ya kuuza mali ghafi kwa bei ndogo zitatengenezwa bidhaa ambazo zitauzwa nje ya nchi na kutoa ajira kwa Watanzania.

“Badala ya kuuza ngozi tutengeneze viatu hapa hapa nchini au badala ya kuuza ng’ombe Comoro tumepeke nyama iliyosindikwa,” alisema.

Alisema nchi kama ya Sudan Kusini ina mahitaji makubwa ya unga wa mahindi.

“Lakini wanaofaidika na soko hilo ni Wakenya ambao wanakuja nchini wananunua mahindi, wanasaga na kuyapeleka huko,hivi wafanyabiashara tunashindwa hata kuanzisha viwanda vya kusaga mahindi,” alisema

Alisema Mkoa wa Arusha una ng’ombe wa  maziwa lakini yananunuliwa na Wakenya ambao wanayasindika kwenye viwanda vyao na kuja kuyauza hapa nchini.

Hata hivyo, alisema Serikali inaangalia uwezekano wa kuanzisha benki ya maendeleo ya viwanda kwa lengo la kutoa mikopo yenye masharti nafuu na riba ndogo.

Kuhusu kuondoa kwa changamoto mbalimbali zinazokwamisha maendeleo ya viwanda nchini, Magufuli alisema Serikali imeshatenga Sh1trilioni katika mwaka wa fedha ujao kwa ajili ya ujenzi wa reli ya kati kwa ajili ya kurahisisha usafirishaji wa bidhaa mbalimbali.

Pia, Serikali imeunda kamati maalumu itakayoangalia mazingira ya ufanyaji biashara nchini ikiwamo kodi na tozo mbalimbali.

“Nchi yetu inakuwa na kodi za ajabu ajabu, mfano zao la kahawa kulikua na zaidi ya kodi 30. Haya ndiyo tunayoyaangalia,” alisema.

 Kuhusu upatikanaji wa mitaji na riba kubwa zinazotozwa na benki, alisema katika kukabiliana na matatizo hayo Serikali inajiandaa kuanzisha benki ya viwanda itakayowasaidia wenye wawekezaji.

Kwa upande wake  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage alisema Serikali imejikita katika kuhamasisha ujenzi wa viwanda vingi zaidi nchini.

“Tumeandaa mkakati wa pamba hadi inakuwa nguo, alizeti hadi mafuta na tunaendelea kufufua viwanda vilivyokufa,” alisema.

Akizungumzia changamoto zinazowakabiri wenye viwanda nchini, mwenyekiti wa Shirikisho la Wenye Viwanda (CTI), Samuel Nyantahe alisema uchakavu wa miundombinu ya umeme na miundombinu ya barabara imekuwa ikiongeza gharama za uzalishaji.

Pia, alilalamikia uwapo wa utitiri wa kodi, mamlaka za usimamiaji biashara na uwapo wa bidhaa bandia zinazotishia bidhaa za ndani

Wema Sepetu Amempongeza Kim Kardashian Kwa Kutumia Lipstic yake

$
0
0
Mnyange na mfanyabiashara wa vipodozi jijini Dar es salaam amempongeza her American counterpart kwa kuweza kutumia bidhaa zake za midomo.Hali hiyo ilitokea baada ya Kim kuweka picha yake kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram ambapo Wema alikoment maneno haya huku akitumia hashtags kibao:

"Thank you sweetheart kwa kutumia bidhaa zangu #KissbyWema #TeamWema #MadamRange #TeamSonny #Wanawaketunaweza #huuMchezohauhitajiHasira #HapaKaziTu #MissTz2006 #BetAwards.

Mimi binafsi nampongeza kama ni kweli kavuka mipaka

Hapa Nimekuwekea Video ya Mwanamuziki Diamond Akionyesha Meno yake ya Dhahabu Aliyonunua Kwa Bei Mbaya

$
0
0
Itakumbukwa kua wiki chache zilizopita video ya msanii Diamond ikionyesha akiwa katoboa pua ilisambaa na kusababisha watu wengi kumlalamikia kua kitendo hicho hakileti picha nzuri kwa jamii hasa ukizingatia kua yeye ni msanii mkubwa.

Ila sio wote waliochukizwa na jamba hilo, wapo waliomtetea wakisema yale ni maisha yake na ni ruksa kufanya jambo lolote lile analoamua. Sasa ikiwa ishu ya pua haijasahaulika sasa Diamond ameamua kuweka meno ya dhahabu akiwa nchini Marekani.

Diamond kupitia mtandao mmoja aliupload video kadhaa zikimwonyesha akiwa na meno hayo ya Dhahabu.

 Unaweza kumtazama Diamond akiwa na meno hayo hapa chini....

Taarifa toka Ikulu kuhusu uteuzi Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TANESCO

$
0
0
TAARIFA KWA UMMA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Dkt. Alex L. Kyaruzi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Kufuatia uteuzi huo, Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Profesa Sospeter M. Muhongo (Mb.), amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa TANESCO kuanzia tarehe 31/5/2016 hadi tarehe 30/5/2019;
1.   Dkt. Samwel Nyantahe
2.   Dkt. Lugano Wilson
3.   Bw. David Elias Alal
4.   Mhandisi Stephen Peter Mabada
5.   Mhandisi Leonard R. Masanja

Aidha, Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Profesa Sospeter Muhongo (Mb) amekamilisha uteuzi wa Wajumbe wa Bodi ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), kuanzia tarehe 30/5/2016 hadi 29/5/2019 wajumbe  hao ni :

    Bw. Abdalah H. Musa
    Dkt. Coretha Komba
    Bw. Felix M. Maagi
    Dkt. Lightness Mnzava
    Bw. John B. Seka

Uzinduzi wa Bodi hizo utafanyika Makao Makuu ya Mashiriki hayo Siku ya Alhamisi tarehe 2 Juni, 2016, saa 4:00 asubuhi kwa Bodi ya STAMICO na saa 8:00 mchana kwa Bodi ya TANESCO.

Imetolewa na;
KATIBU MKUU
31 MEI, 2016

Bifu la Lulu Michael na Hamisa Mobeto Mtandaoni Lasababisha Mange Kimambi Kumlipua Majizo Kuwa ni Muuza Madawa ya Kulevya

$
0
0
Lile bifu linolotikisa kwenye mitandao ya kijamii kwa sasa, linalowahusisha mastaa wenye mvuto wa aina yake bongo, namzungumzia Hamisa mobeto (I phone) na lulu michael (Techno) limefikia mahali pabaya.

Ambapo usiku wa jana mwana mama mwenye vituko vya aina yake aishiye Marekani aitwaye Mange Kimambi amemlipua mwanaume anayedaiwa kuwagombanisha Lulu na staa aitwaye Majizo kuwa ni muuza mada ya kulevya maarufu hapa mjini na ana pesa chafu sana inayowazuzua warembo hao mpaka kufikia hatua ya kuchafuana mitandaoni.

Either mwana mama huyo ameahidi kuanika siri za mwanaume huyo ambaye anasadikika kuwa na utajiri wa kutisha ukilinganisha na umri wake mdogo.

Mange Ameandika haya Katika Ukurasa wake wa Instagram:

mangekimambi_
"Kumbe huyo Majizo mwenyewe ndo wale adui zangu 😡😡😡.Majizo mwenyewe anaepiganiwa na Lulu na Hamisa ni muuza Unga wa Long time. 🙆🏽🙆🏽🙆🏽🙆🏽🙆🏽... Unaambiwa kijana ana pesa chafuuuuuuuuuuuuu Hiyo Efm Kafungua tu ili asafishe hiyo pesa ya Unga, yani unaambiwa ana helaaaaaaaa acha!!! Huyu jamaa alikuwaga ni DJ tu wa Magic FM na Channel Ten taratibu akaanza kujiingiza kwenye biashara ya unga ndo mpaka katajirika na yeye kafungua Redio yake!! . Unaambiwa huo mjumba wake huko Kigamboni ni kufuruuuuuuuuuuu Mengi mwenyewe hana nyumba kama ya huyu kijana, unaambiwa ni balaa. Ila Ndo hivyo mateso ya Kina Ray C Kina Chidi Benzi na vijana wa Kitanzania ndo yanayojenga hayo majumba.Tena nimekuwa warned unaambiwa jamaa mtandao wake ni high level hawezi guswa na mtu hapo Tanzania.... Mtandao wake ni wa vigogo Yani.... 🙆🏽🙆🏽🙆🏽🙆🏽 . Jinsi Maisha yalivyo magumu kuna kijana anaweza Kuwa inspired na story ya Majizo, don't be mwisho wa hawa watu huwa sio mzuri. Siku zooote mwisho wao huwa ni mmbaya. Kulikuwa na muuza Unga tajiri Tanzania kama Shkuba? Jiulize yuko wapi sasa Hivi? Ananyea ndoo mabilioni watu wanayala huko nje, tena bora kipindi cha JK alikuwa anaishi jela kama kwake na mkewe alikuwa anapelekewa every weekend Sasa Hivi ni mfungwa kama wafungwa wengine....😭😭... . . Hivi Magu ile vita ya wauza Unga imeishia wapi???? Mbona ilianza na moto sasa hivi kimyaaaaa?? Watuondelee hawa watu jamani, wanatuulia vijana wetu!! And I'm sure hao Lulu na Hamisa wote wanajua kazi ya bwana yao Ila ndo hivyo wanataka Maisha ya juu so hawajali kuwa wenzao wanakufa, familia zinasambaratika ili tu wao wapendeze na waishi Maisha ya juu😏😏😏😏... Yani nawachukia wauza Unga especially waliotajirika maana it shows wameuwa watu wangapi. Although siamini kuna kitu kama hiko Ila Haki ya Nani for the first time nimewish ingekuwa kweli Lulu awe na jini la kuuwa wanaume ili huyu jamaaa tumpotezee. Wanatumalizia nguvu ya taifa hawa watu. . . Huyu jamaa keshaingia kwenye black list yangu ya wauza Unga.Ntakuwa nawapa habari zake." Mange

Video : Kwa Mtoko Mmoja Wema Sepetu Anavaa Vitu Vyenye Gharama ya Zaidi ya Milioni Mbili

$
0
0
Moja ya kitu kinachomtofautisha mtu maarufu na wakawaida mara nyingi ni kujulikana kwake na mavazi anayovaa. Kwa mfano mzuri tu ni hapa Bongo watu wengi maarufu wamekua wakionekana nadhifu sana kwa kuvaa nguo za gharama.

Kwa mwananchi wa kawaida kununua nguo ya Laki moja ni jambo gumu sana ila kwa star kama Wema Sepetu ni jambo la kawaida sana. Akihojiwa katika EFM Radio Wema Sepetu alifunguka kua kwa kila siku anayotoka vitu anavyovaa gharama yake ni kama milioni 2 za kitanzania.

Hebu msikie kwenye video hii hapa chini..

Babu Tale Alimtelekeza Chidi Benz Sobber House - Mkuu wa Kituo

$
0
0
Akizungumza na E news ya East Africa Tv mkuu wa Bagamoyo sobber house amesema chanzo cha Chidi Benz kuondoka kwenye kituo chao ni kutelekezwa na waliompeleka.

Anasema tangia Chidi apelekwe pale hakukuwa na huduma zozote zinazotumwa kama walivyokubaliana na kila walipokuwa wanamtafuta Babu Tale hakuwa tayari kupokea simu wala kutoa ushirikiano.

Anasema pia kukosekana kwa vitu muhimu ndio vilifanya Chidi aondoke na wala hakutoroka.

Japo Sijajua ni vitu gani walikubaliana awe anapeleka.


My take, kama ni kweli hii ishu basi Tale amekosea sana hakufanya uungwana. Ni kama kamtumia Chidi kupata kick

Mauaji ya Kutisha: Watu 8 Wakamatwa Kwa Mwenyekiti wa Kitongoji na Kuchinjwa Kinyama

$
0
0
MAUAJI ya Watanzania kwa njia ya kuchinjwa yanaendelea kushika kasi baada ya usiku wa kuamkia jana wakazi wanane wa kitongoji cha Kibatini, kata ya Mzizima jijini Tanga kukusanywa kwa mwenyekiti wa kitongoji na kisha kuuawa kwa kuchinjwa shingo na watu wasiojulikana.

Watu hao ambao inadaiwa kuwa ni majambazi walivamia usiku wa kuamkia jana kwa kuvunja milango ya nyumba tatu ambazo wakazi hao walikuwa wamelala na kuwachinja kisha kuiba biskuti, mchele na sukari na kutokomea navyo kusikojulikana.

Wauaji hao inadaiwa wana uhusiano na wahalifu ambao wamekuwa wakijificha ndani ya mapango ya Majimoto na kujihusisha na matukio kadhaa ya uvamizi ili kupora vyakula na kusababisha mauaji ya wakazi wa Jiji la Tanga, ikiwamo katika duka kuu la Central Bakery mwishoni mwa Aprili mwaka huu.

Mmoja wa shuhuda wa mauaji hayo, Kea Leonard (70) ambaye pia ni mkazi wa Kibatini, katika mahojiano jana alisema wanaamini kwamba chanzo cha mauaji ya wenzao ni kulipiza kisasi.

“Wiki iliyopita majira ya saa tano asubuhi hapa tulikamata vijana saba kati ya wanane wenye umri wa kama miaka 13 ambao walikuwa wakiranda randa hapa kitongojini ili kutafuta namna ya kuvuka mto kwenda ng’ambo ya pili na ndipo mmoja wao alipotutoroka,” alieleza Leonard na kuongeza:

“Watoto hao tulipowaweka chini ya ulinzi na kuwahoji tukaanza kuwatilia shaka hivyo mwenyekiti aliamua kuripoti Polisi na ndipo hao wakawachukua kwa ajili ya mahojiano na hatukufuatilia tena kujua kwamba waliachiwa au la kwa sababu hao watoto sio wenyeji wala wakazi wa eneo hili.”

Aliongeza kwamba wakati wahalifu hao wanavamia nyumba ya mjumbe wa serikali ya kitongoji kabla ya kumtoa nje walisikia mmoja wa watu hao akimhoji kuhusu mahali walipopelekwa watoto saba.

Diwani wa Kata ya Mzizima, Fredrick Charles alizungumza na waandishi wa habari na kuthibitisha kwamba kati ya watu waliokufa mmoja ni Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Mleni uliopo kwenye kata hiyo.

“Hali ya usalama hapa kwetu Mzizima si shwari kwa sababu wananchi wangu wa Kibatini wamevamiwa na kuchinjwa usiku wa kuamkia jana majira ya saa sita usiku,” alisema Chiluba.

Naye Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mleni kilichopo kitongoji hicho, Shabani Amani alisema wamepatwa na hofu kubwa kuhusu matukio hayo.

“Tunadhani kuna mapungufu katika suala la ulinzi hapa kwa sababu baada ya kutokea matukio kadhaa eneo letu hasa baada ya kudaiwa kwamba mapango waliyojificha wahalifu yako hapa jirani na kwetu kikosikazi cha mchanganyiko wa askari polisi na wa JWTZ wanafanya doria kwa saa 24 lakini tunashangaa kwa nini matukio yanaendelea,” alisema Amani.

Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Leonard Paul alithibitisha mauaji hayo. “Mei 30, mwaka huu majambazi waliokuwa na visu na mapanga walivamia kaya tatu na kuua wananchi majira ya saa saba usiku,” alisema Kamanda Paul.

Aliwataja waliouawa ni Issa Hussein (50) ambaye ni mmiliki wa kaya hiyo pamoja na kuibwa biskuti, mchele na sukari katika duka dogo. Wa kaya nyingine ni Mkola Hussein (40) na Hamis Issa (20), Hamis Issa (20) na aliyemtaja kwa jina la Mikidadi (70).

Kamanda aliwataja marehemu wengine ni Mahamud (35) ambaye ni mkwe wa Mikidadi, Issa Ramadhani (25), Kadir (25) na Salum ambao ni wachunga ng’ombe kijijini humo.

Hata hivyo, mashuhuda wa tukio hilo akiwemo mke wa marehemu Mkola aitwaye Aisha Saidi, alisema walipofika nyumbani hapo waligonga mlango na kumtoa nje Mkola na kuondoka naye.

“Nimeachwa mjane na watoto sita... Baada ya hao watu kuingia walimkamata Mkola na kumdai aeleze kwamba watoto wao saba wamepelekwa wapi na alipojibu sijui wakamtoa nje na kumkusanya pamoja na wanakijiji hao wengine na kuwachinja eti tu kwa sababu hawakutaja mahali walipopelekwa watoto,” alisema Aisha.

Katika hatua nyingine, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imesikitishwa kupokea taarifa za vitendo vya mauaji ya kikatili vinavyoendelea kutokea katika maeneo mbalimbali nchini.

“Wimbi hili la matukio ya vitendo vya mauaji na ukatili uliojitokeza kwa kufuatana mwezi Mei 2016 yanavunja haki ya kuishi ambayo ndio msingi wa haki zote za binadamu kwa ujumla wake.

"Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora inalaani vikali mauaji haya yote na matendo yote ya kikatili dhidi ya mwanadamu yanapotokea popote nchini,” ilieleza taarifa ya Mwenyekiti wa Tume, Bahame Nyanduga.

Tume iliishauri serikali kupitia Jeshi la Polisi ichukue hatua mahsusi kuhakikisha ulinzi wa wananchi dhidi ya mauaji na vitendo hivi, kwani jukumu la kwanza la kuhakikisha usalama wa wananchi ni jukumu la serikali.

Jeshi la Polisi lihakikishe watu wote waliohusika kutekeleza mauaji haya wanakamatwa ili sheria ichukue mkondo wake, ilieleza.

Mbowe: Tupo Tayari Kutimuliwa Wote BungeniSababu ya Naibu Spika Tulia Ackson

$
0
0

Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson sasa amesababisha makubwa zaidi; wabunge kutoka vyama vya upinzani wako radhi kutimuliwa wote iwapo kiongozi huyo ataongoza vikao vyote vilivyosalia na wao kuendelea na msimamo wao wa kumsusia. 


Jana, Dk Ackson aliingia kuongoza kipindi cha maswali na majibu na wabunge wote wa vyama vya upinzani wakatoka ndani ya ukumbi na alipomuachia mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge kuendelea na shughuli zilizosalia, walirejea ukumbini. 


“Kama Naibu Spika atakuwepo kwenye kile kiti, hatatuona bungeni, hata kama ni leo, ni kesho hata Bunge lote. Tuko tayari kuchukua gharama hiyo,” alisema kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani, Freeman Mbowe akiwa nje ya ukumbi wa Bunge baada ya kuongoza wabunge wenzake kutoka ukumbini wakati wa kipindi cha maswali na majibu. 


Kauli hiyo ya Mbowe imekuja siku moja baada ya Dk Ackson kukataa Bunge kujadili sakata la wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) waliotimuliwa kwa maelezo kuwa hawafundishwi kwa muda mrefu kutokana na walimu wao kugoma wakidai malimbikizo yao. 


Kitendo cha Dk Ackson kukataa hoja hiyo ijadiliwe, kilisababisha vurugu bungeni kiasi cha kuita askari kuingia kuwatoa wabunge waliokuwa wakipiga kelele na baadaye kuwaamuru waliokataa kukaa waondoke ukumbini. 


Wakiwa nje, walifikia uamuzi wa kususia vikao vyote vitakavyoongozwa na Naibu Spika na wakaanza kutekeleza uamuzi huo jana asubuhi. 


Kauli ya Mbowe pia imekuja siku moja baada ya Kamati ya Maadili, Kinga na Haki za Bunge kuwasimamisha wabunge saba kutoka vyama vya upinzani kuhudhuria vikao vya kuanzia mkutano huu hadi ujao kwa maelezo kuwa walifanya fujo wakati wakipinga hoja ya Serikali ya kusimamisha matangazo ya moja kwa moja ya baadhi ya shughuli za Bunge. 


Jana, Mbowe alisema wako tayari kutimuliwa wote kama uamuzi huo utawapendeza viongozi wa Bunge kwa kuwa siasa inaweza kufanywa ndani na nje ya Bunge. 


Mbowe alisema kuwa hali ilishafika hatua nzuri ya kujenga demokrasia nchini na kwamba pamoja na matatizo yaliyokuwepo, hali ilikuwa ikienda vizuri. 


“Lakini tangu kuingia kwa Serikali ya Awamu ya Tano mnaweza kuona Bunge limegeuka kituko. Bunge limegeuka mahali pa kukomoana. Bunge limekuwa mahali pa kutishana,” alisema Mbowe. 

“Naibu Spika anaamua kusitisha mjadala wa maana ili apate muda wa kuwadhibiti na kuwafukuza wabunge bungeni na anaona sifa. 


Tunaacha kujadili hoja ya msingi kama mambo ya Udom. Watoto wadogo wanalala nje haoni ni muhimu, anaona muhimu ni kuwafukuza wabunge wa upinzani.” 

Mbowe, ambaye pia ni mbunge wa Hai, alisema hawezi kukaa, kumsikiliza na kumheshimu Dk Ackson, bali wapinzani wataheshimu anayewaheshimu bila kujali anatoka chama gani na hawatamuheshimu asiyewaheshimu bila kujali cheo chake. 


“Sasa leo (jana) tumekataa kushiriki kipindi cha maswali na majibu kwa sababu yeye (Dk Ackson) anasimamia kipindi hicho na akitoka tutarudi bungeni. 


Akija mwenyekiti, akija Spika mwenyewe tutarudi bungeni. Lakini kama Naibu Spika atakuwepo kwenye kile kiti hatatuona bungeni, hata kama ni leo, ni kesho hata Bunge lote. Tuko tayari kuchukua gharama hiyo,” alisema Mbowe.


Wabunge Waliosimamishwa Wazidi Kubanwa...Waongezewa Adhabu Nyingine

$
0
0

Wabunge saba wa upinzani waliosimamishwa bungeni, watakumbana na kibano kingine cha kukatwa mshahara na posho kwa kipindi chote cha kutumikia adhabu.


Wabunge hao ambao Jumatatu walisimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge kwa muda tofauti kwa madai ya kukiuka kanuni ni Zitto Kabwe (Kigoma Mjini), Tundu Lissu (Singida Mashariki), Halima Mdee (Kawe), Ester Bulaya (Bunda Mjini), John Heche (Tarime Vijijini) na Godbless Lema (Arusha Mjini).


Adhabu hiyo ilitolewa  kama azimio la Bunge baada ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kupendekeza wabunge hao waadhibiwe kutokana na kuomba mwongozo wa kiti cha Spika kwa jambo ambalo tayari lilishatolewa uamuzi.


Habari zilizopatikana bungeni zilieleza kuwa wabunge hao watakumbana na Kanuni ya Bunge ya 75, ambayo inahusika na masharti ya mbunge aliyesimamishwa kazi.


Naibu Katibu wa Bunge (Shughuli za Bunge), John Joel alithibitisha kuwa utekelezwaji wa kanuni hiyo utafuatwa kwa wabunge wote ambao wamefukuzwa.


Akizungumzia hatua hiyo, Heche alisema hadi sasa hajapata barua ya kusimamishwa Bunge, hivyo hata kama watakata posho au mshahara haimsumbui kwa kuwa hawezi kusikitikia kitu hicho wakati haki inaminywa.


Zitto alisema hajasikia taarifa hizo za kukatwa mshahara kwa kuwa hajapewa barua inayoeleza mambo hayo wala ya kusimamishwa Bunge.


Mwimbaji Country Boy ajitokeza na Kumtetea Young Dee Kuhusu Madawa ya Kulevya

$
0
0




Rappa Country Boy amesema hajawahi kushuhudia rafiki yake wa zamani Young Dee akitumia Madawa ya kulevya.

Young Dee amekuwa akikanusha mara kadhaa taarifa ya kutumia Madawa ya kulevya lakini bado amekuwa akiandamwa na maswali mengi kuhusu matumizi ya Madawa ya kulevya.

Akiongea na Bongo5 Jumapili hii, County Boy ambaye alikuwa rafiki wa karibu wa Young Dee, amesema hajawahi kushuhudia rafiki yake huyo akitumia Madawa ya kulevya lakini kama anatumia basi atakuwa amuheshimu sana ndio maana hajawahi muonyesha dalili yoyote.

“Young Dee nimekaa naye kwa muda mrefu kiukweli, kusema kweli kabisa sijawahi muona akitumia,” alisema Country Boy. “Maneno yapo na kila kitu kinatokea na kila kitu kinasikika, kama ni kweli anatumia basi nahisi alikuwa ananiheshimu sana, kwa sababu ni mwanangu nimekaa naye pamoja kwa muda mrefu sijawahi kuona kitu chochote kibaya zaidi tu ya ulevi wa kawaida, pombe tu,”

Aliongeza, “Lakini hiki kitu sio vizuri kwa mtu yeyote yule, kwa sababu hakina faida yoyote zaidi ya kukupoteza,”

Country Boy na Young Dee kwa sasa sio washikaji kama zamani, kwa wawili hao walipisha lugha baada ya Young Dee kujiondoa katika Kundi la ‘Mtu Chee’ ambalo lilikuwa linaundwa na Young Dee, Stamina pamoja na country boy


Mwanamke aliyekataa kuolewa achomwa hadi kufa Pakistan

$
0
0

Mwanamke mmoja wa Pakistan aliyechomwa kwa kukataa wito wa ndoa amefariki kutokana na majeraha yake.

Maria Sadaqat ,mwalimu wa shule aliye na umri mdogo alishambulia nyumbani kwake na kundi moja la wanaume siku ya jumapili na kufariki katika hospitali mjini Islamabad siku ya Jumatano.

Familia yake imesema kuwa alikataa kuolewa na mtoto wa mmiliki wa shule ambayo amekuwa akifunza.

Wanakampeni wanasema kuwa visa vya mashambulio dhidi ya wanawake wanaokataa kuolewa ni vingi nchini Pakistan.

Waziri mkuu wa Punjab Shahbaz Sharif alianzisha uchunguzi kuhusu mauaji hayo.

Babake Maria amesema kuwa mmiliki wa shule hiyo ni mojawapo ya watu waliomshambulia mwanaye.

Polisi wameambia BBC kwamba wanaume hao walimpiga kabla ya kumwagia mafuta ya petroli na kumchoma karibu na eneo la kitalii la Muree,karibu na mji mkuu.


Viewing all 104670 articles
Browse latest View live




Latest Images