Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104776 articles
Browse latest View live

Ripoti ya Mrundikano wa Watoto wa Vigogo BoT (Benki Kuu) yatua Mezani kwa Magufuli

$
0
0
Hatimaye ile ripoti iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu inayotishia hatima ya ajira za watoto kadhaa wa vigogo ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imekamilika na kuwasilishwa mezani kwa Rais John Magufuli, Ikulu.

Inasemekana kwa sasa hali si shwari BoT, baada ya kuwepo tetesi za kupunguza watumishi ambao wengi ni watoto wa vigogo waliongia kwa migongo ya wazazi wao.

==========================

Akizungumza na Nipashe jana, Gavana wa BoT, Prof. Benno Ndulu, alisema maagizo ya Rais Magufuli juu ya kupitia upya ajira za watumishi wote wa taasisi hiyo yameshafanyiwa kazi na ripoti yake imekamilika.

Machi 10 mwaka huu, Rais Magufuli alifanya ziara ya kushtukiza Makao Makuu ya BoT na kutoa maelekezo mbalimbali kwa menejimenti ya taasisi hiyo nyeti kwa mustakabali wa taifa kiuchumi.

Rais Magufuli alimuagiza Gavana wa BoT (Prof. Ndulu) kupitia upya ajira za watumishi wa taasisi hiyo na kupunguza idadi ya watumishi hao hasa ikibainika kuwa kazi zao zinaweza kufanywa na watu wengine.

Katika mazungumzo yake hayo na uongozi wa BoT, ilibainika kuwa benki hiyo ina watumishi takriban 1,391; idadi ambayo ilionekana kuwa ni ya juu kulinganisha na ukubwa wa taasisi hiyo na hivyo kumshangaza Rais Magufuli.

Wakati akizungumza na Nipashe jana, Prof. Ndulu alisema kazi hiyo (ya kupitia ajira za watumishi) ilishafanyika na ripoti yake imeshawasilishwa kwenye vyombo husika.

"Hiyo kazi ilishafanyika kama alivyoagiza Mheshimiwa Rais na tayari vyombo vinavyohusika vimeshapewa taarifa hiyo," alisema Prof. Ndulu na kuongeza:

"Hatutoi taarifa kama hizo magazetini bali kwenye vyombo husika--sisi tukishakamilisha kazi tunapeleka ripoti kwenye mamlaka husika na ndivyo tulivyofanya."

 AJIRA ZA WATOTO WA VIGOGO

Alipotembelea benki hiyo Machi, Rais Magufuli alisema anashangazwa kuwapo kwa wafanyakazi wengi ndani ya BoT ambao baadhi hata kazi wanazofanya hazijulikani wazi.

"Haiwezekani tukawa na kundi kubwa la wafanyakazi, wanalipwa mishahara wakati hata kazi wanazofanya hazijulikani," alinukuliwa Rais Magufuli.

Kabla ya ziara ya Rais Magufuli, majina kadhaa ya watumishi wa BoT yalikuwa yakiibua mijadala mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii kwa madai kuwa ajira zao zimetokana na kubebwa na wazazi ama ndugu zao ambao wana ushawishi mkubwa serikalini kutokana na nafasi mbalimbali walizo nazo au kuwahi kuwa nazo.

Orodha ya watu wanaodaiwa kuwa ni ya watoto wa vigogo, na ambayo Prof. Ndulu alisema siyo mpya kwani ilishaandikwa na kujadiliwa sana hapo kabla ni pamoja na Pamela Lowasa, anayedaiwa kuwa ni mtoto wa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowasa.

Wegine ni Filbert Sumaye anayedaiwa kuwa ni mtoto wa Waziri Mkuu mstaafu katika serikali ya awamu ya tatu, Fredrick Sumaye na Zaria Kawawa, anayedaiwa ni mtoto wa aliyewahi kuwa Waziri Mkuu katika serikali ya awamu ya kwanza, Marehemu Rashid Mfaume Kawawa.

Mwingine ni Harriet Lumbanga anayedaiwa ni mtoto wa aliyewahi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi wakati wa utawala wa serikali ya awamu ya tatu, Marten Lumbanga.

Aidha, orodha hiyo pia ina jina la Salama Ali Hassan Mwinyi anayedaiwa ni mtoto wa aliyekuwa Rais wa awamu ya pili, Alhaji Hassan Mwinyi; Rachel Muganda anayedaiwa ni mtoto wa aliyekuwa Balozi katika serikali ya awamu ya nne, Alexender Muganda. Salma Omar Mahita, katika orodha hiyo anadaiwa kuwa ni mtoto wa aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi wakati wa utawala wa awamu ya tatu, IGP mstaafu Omar Mahita.

Wengine ni Justina Joseph Mungai anayedaiwa kuwa ni mtoto wa aliyewahi kuwa Waziri wa Elimu na Utamaduni katika serikali ya awamu ya tatu, Joseph Mungai. Pia yumo Keneth Nchimbi anayehusishwa na kada wa CCM aliyewahi kuwa kigogo wa Jeshi la Polisi John Nchimbi. Blasia William Mkapa, anadaiwa kuwa ni mtoto wa Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkpa katika orodha hiyo yenye pia jina la Violet Phillemon Luhanjo, ambaye anadaiwa kuwa mtoto wa aliyewahi kuwa Katibu Mkuu kiongozi wakati wa serikali ya awamu ya tatu na nne, Phillemon Luhanjo.
Liku Kamba anadaiwa kuwa mtoto wa aliyekuwa kada wa CCM wa muda mrefu, Kate Kamba.

Wengine wanaotajwa katika orodha hiyo ni Thomas Mongela anayedaiwa kuwa mtoto wa kada mashuhuri ndani ya CCM; aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali zikiwamo za ubunge, Getrude Mongela. Jina la Jabir Abdalah Kigoda linadaiwa kuwa ni mtoto wa aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara katika serikali ya awamu ya nne, marehemu Abdalah Kigoda.

Machi mwaka huu, mara baada ya agizo la Rais Magufuli kuhusiana na ajira za watumishi wa taasisi hiyo, Nipashe ilizungumza na Prof.

Ndulu kwa njia ya simu kutaka kujua kama kweli orodha ya watoto hao ni miongoni mwa watumishi wa BOT na majibu yake kwa mwandishi, ambaye alimsomea majina hayo kuanzia mwanzo hadi mwisho, ni kwamba orodha hiyo 'haina jipya'. Prof.

Ndulu alieleza zaidi kuwa hakuna ubaya wowote kwa mtu mwenye sifa kuajiriwa na BoT, bila kujali jina lake.

"Hayo majina kwani kwako wewe ni mapya? Mbona yameshaandikwa na kujadiliwa sana hayo--mimi nasema hakuna jipya hapo," alisema Profesa Ndulu na kuongeza:

"Hivi ukiwa na jina kubwa halafu ukiwa na akili ama sifa za kufanya kazi fulani, unataka kuniambia usipewe hiyo kazi kwa sababu una jina kubwa?"

 HOFU YATANDA

Licha ya ufafanuzi wa Prof. Ndulu kuhusiana na madai ya kuwapo kwa watumishi walioajiriwa kwa sababu ya ushawishi wa wazazi wao ambao ni vigogo serikali, bado mijadala mbalimbali iliendelea kutawala katika mitandao ya kijamii kuhusiana na orodha hiyo.

Aidha, imedaiwa kuwa hofu imetanda miongoni mwa watumishi hao na wengine wengi kutokana na kile kinachoelezwa kuwa huenda kukawa na punguzo kubwa la watumishi kutoka idadi iliyopo sasa ya wafanyakazi 1,391; jambo ambalo linaweza kutekelezwa wakati wowote kulingana na kile kilichomo ndani ya ripoti na kumfikia Rais Magufuli.

Wengi wa wachangiaji katika mitandao ya kijamii kuhusiana na majina ya watoto wa vigogo ni madai kwamba ajira zao zilitokana na ushawishi wa majina makubwa ya wazazi wao katika medani za uongozi nchini na siyo sifa za kuajiriwa kwenye taasisi hiyo na hivyo, upo uwezekano kuwa wengi miongoni mwao hawatasalimika pindi kazi ya kuwapunguza watumishi (wa BoT).

Source: Nipashe

Mikataba ya Polisi Yaitishwa Wizarani

$
0
0
BAADA ya Rais John Magufuli kuizungumzia mikataba ya ujenzi ya Jeshi la Polisi iliyoingia na wawekezaji, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ameitisha mikataba yote ya jeshi hilo.

Jeshi la Polisi nchini limetakiwa kuwasilisha mikataba ya miradi ya ujenzi wa nyumba za kuishi askari eneo la Kunduchi, Mikocheni pamoja na Kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini Dar es Salaam pamoja na ule wa majengo mbalimbali ya mwekezaji ambaye Jeshi la Polisi limeingia mkataba naye.

Agizo hilo limetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira ikiwa ni miezi miwili tu tangu Rais Magufuli kuzungumzia mikataba hiyo na kuitilia shaka wakati akifungua kikao kazi cha makamanda wa Polisi wa mikoa, mawakili wafawidhi wa serikali wa mikoa na wakuu wa upelelezi wa mikoa na vikosi mjini Dodoma.

Meja Jenerali Rwegasira alisema mradi huo ni mkubwa na wa muda mrefu na hivyo ameliagiza jeshi hilo kuuwasilisha mkataba huo, ambao utekelezaji wake unaendelea ili aufahamu vizuri mkataba huo, unaolihusisha Jeshi la Polisi na Mwekezaji wa Kampuni ya Mara World Tanzania Limited.

Kwa mujibu wa taarifa ya wizara hiyo jana kwa vyombo vya habari, Katibu Mkuu huyo ametoa agizo hilo muda mfupi baada ya kukagua miradi hiyo katika maeneo ya Kunduchi na Mikocheni, ambako zinajengwa nyumba za kuishi askari wa Jeshi la Polisi na kwamba ujenzi wake bado unaendelea.

Mradi mwingine alioutembelea ni ujenzi wa Kituo cha Polisi eneo la Polisi Oysterbay na kuona maendeleo ya ujenzi huo sambamba na kufahamu hatua iliyofikiwa hadi sasa katika maeneo hayo ya Jeshi la Polisi.

Katika mradi huo wa Ujenzi wa Kituo cha Polisi Oysterbay, unaotekelezwa na mwekezaji Kampuni ya Mara World Tanzania Limited, pia kutajengwa ofisi za kukodisha, hospitali, maduka makubwa na hoteli.

Rais Magufuli wakati akihutubia makamanda hao wa Polisi Aprili mwaka huu, alisema miongoni mwa vitu ambavyo vinalisumbua jeshi hilo ni mikataba ya hovyo akisisitiza umuhimu wa fedha za jeshi hilo kutumika vizuri.

Rais Magufuli alisema kuna taarifa zinaonesha Jeshi la Polisi, limekuwa likihusishwa na matumizi mabaya ya fedha, hali inayoongeza ukubwa wa matatizo yanayokwamisha utendaji wake wa kazi.

Alitoa mfano wa taarifa za matumizi mabaya ya fedha, zinazotolewa kwa ajili ya kununua vifaa na sare za askari ama mikataba yenye mashaka inayotiwa saini kati ya Polisi na wawekezaji kuwa ni baadhi ya mambo yanayoongeza hali ngumu ya utendaji kazi kwa jeshi hilo.

“Oysterbay pale ni eneo ambalo ni zuri sana, kila mmoja anajua, mmeingia kwenye mikataba mnayoijua ninyi, mkapewa mtu anawajengea pale, sifahamu kama majengo hayo yanafaa.

“Palikuwa na ubaya gani eneo la Oysterbay likawa na hati, mkaitumia hiyo hati kwenda kukopa benki na kujenga nyumba hata za ghorofa 20 pale, mkaweka kitega uchumi na polisi wenu wakakaa pale?

“Nimesema lazima nizungumze kwa uwazi, nisiposema kwa uwazi nitajisikia vibaya nikimaliza mkutano huu. Nataka muelewe na muelewe ukweli mwelekeo ninaoutaka mimi,” alisema Rais Magufuli.

Zari the bosslady Aamua Kumwaga Mboga..Kuwazima Wanao Sema Anavaa Vigodoro

$
0
0

Zari the bosslady ameamua kumwaga mboga, kutoboa sufuria na kuzima moto kwa vikurumbembe wanaomsema anavaa kigodoro kwa kupost picha inayoonesha "ze utamu" live.....

Video: Mambo Yakufahamu Baada ya Taarifa za Chid Benz kutoroka Sober House Kusambaa

$
0
0
March 22, 2016 meneja wa Diamond Platnumz Babu Tale alimpeleka  msanii wa muziki wa Hip Hop kutoka Ilala, Rashid Makwilo aka Chid Benz  Sober House iliyopo Bagamoyo iitwayo Life and Hope Rehabilitation Centre kwaajili ya kupata matibabu ya kuacha kutumia madawa kulevywa na kurudi kwenye hali yake ya mwanzo.

Headline za kutoroka kwa msanii huyo kwenye nyumba hiyo ya kuhudumia waathirika wa dawa za kulevya zilianza baada ya watu kumuona msanii huyo akiwa mtaani June 5 2016 Mkuu wa Kituu hicho cha Sober House ameelezea ukweli wa msanii Chid Benz kwenye kituo hicho.

Video : Jionee Diamond Platnumz Akicheza Kigodoro Nyumbani Kwake, Noma sana.

$
0
0
Kwa wakazi wa Dar na mikoa ya pwani mtakubaliana na mimi kua mziki aina ya kisingeli kwa sasa unakubalika sana. Kwa mfano ukikatiza  mitaa mingi ya Dar lazma utakuta sehemu au ndani ya bodaboda au bajaji wakipiga singeli.

Japo haupigwi sana katika vituo vingi vya radio ila watu wengi waukubali sana. Siku chache zilizopita msanii Diamond Platnumz aliandaa party nyumbani kwake ya kumkaribisha msanii mwenzake Rich Mavoko katika Label ya WCB. Na katika party hiyo Diamond alionekana akicheza kwa furaha mziki aina ya kisingeli kama ambavyo utaona katika video hii hapa chini....

Video : Ommy Dimpoz Nae Kaamua Kutoboa Pua na Kusema Haya....

$
0
0
Kuna uwezekano mkubwa hii style mpya ya wasanii wa kiume kutoboa pua ikaenea kwa wasanii wengi zaidi. Ilianza kwa msanii Chid Benz ambae mara baada tu ya kuonekana katoboa pua ilikua gumzo sana sio tu magazetini hata mitandaoni huku wasanii wengi wakipingana na maamuzi yake.

Itakumbukwa pia kua Diamond Platnumz alifikia hatua hadi ya kumuimba Chid kua katoboa pua ila cha kushanaza mwaka huu nae Diamond katoboa pua. Ishu ya Diamond kutoboa pua ishasambaa sana ila mpya kwa sasa ni Ommy Dimpoz nae kutoboa pua!!!

Imenaswa video ikimwonyesha Ommy Dimpoz akiwaonyesha mashabiki wake kua nae katoboa pua, hadi akatoa heleni ya sikioni na kuiweka puani. Unaweza ona video hiyo hapa chini.....

Polisi Jijini Mwanza Wapambana na Majambazi kwa Saa 16, Wakamata Silaha Nzito, Watatu Wauawa

$
0
0
Watu watatu wanaosadikiwa kuwa majambazi,wameuawa katika majibizano ya risasi na askari polisi mkoani Mwanza,alfajiri ya kuamkia jana jumapili katika mapango ya mlima wa Utemini yaliyopo kata ya Mkolani jijini Mwanza.

Kamanda wa polisi mkoani Mwanza Ahmed Msangi,amewataja majambazi waliouwa katika majibizano ya risasi usiku kucha kuwa ni Omar Francis Kitaleti mkazi wa Nyegezi Kona,said Khamis Mbuli maarufu kama fundi bomba mkazi wa bugarika na jambazi mwingine ambaye jina lake bado halijafahamika.

Amesema majambazi hayo yalikuwa yamejificha kwenye mapango ya mlima wa Utemini kabla ya askari polisi kufanikiwa kuyaua.

Jambazi mmoja aliyeuawa ambaye hajafahamika jina lake mwenye umri kati ya miaka 20 hadi 25 alikuwa akiwashambulia polisi kwa kutumia bastola ambapo baada ya polisi kumpiga risasi walimpekua na kumkuta akiwa na bastola aina ya Chinese,iliyokuwa na risasi tatu ndani ya magazine,huku majambazi wengine waliokuwepo kwenye mapango hayo wakiendelea kujibishana kwa risasi na askari polisi.

Kamanda Msangi ameongeza kwamba Ijumaa Juni 3,askari polisi kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama,walimkamata Omar Francis Kitaleti kwa jina maarufu kiberiti,mkazi wa Nyegezi Kijiweni ambaye alikuwa akituhumiwa kuhusika katika matukio ya unyang’anyi wa kutumia silaha kwenye maduka ya M-pesa,Tigo Pesa na Airtel money jijini Mwanza ambaye baada ya kuhojiwa alikiri kuhusika katika matukio hayo na aliwataja wenzake anaoshirikiana nao na mahali walipojificha.

Amesema ilipotimu majira ya saa kumi na moja kamili jioni siku ya Jumamosi Juni 4,polisi walifika katika mlima huo na walipoyakaribia mapango hayo ghafla walianza kushambuliwa kwa risasi na majambazi waliokuwa wamejificha ndani ya mapango hayo.

Omary Francis Kitaleti @Kiberiti, mmoja wa majambazi aliyeuawa na wenzake kwa risasi.

Katika mapambano hayo ya risasi na askari polisi,risasi hizo ziliweza kumpata jambazi mwenzao aitwaye Omary Francis Kitaleti aliyekuwa anawaongoza askari polisi na kufariki dunia papo hapo, na risasi nyingine ilimjeruhi askari kwenye unyayo wa mguu wake wa kulia.

Amesema polisi kwa kutumia mbinu za medani za kivita waliweza kuzingira maeneo hayo ya mlima wa utemini hadi alfajiri ya kuamkia Jumapili Juni 5,huku wakijibishana risasi na majambazi hao na baada ya kuona yamezidiwa nguvu huku kukikaribia kupambazuka ndipo yalipoamua kuondoka ndani ya mapango hayo kwa kurusha bomu moja la kutupa kwa mkono huku yakizidisha mapigo ya risasi kwa kutumia silaha walizokuwa nazo.

Ameongeza kuwa polisi wamekamata bunduki moja aina ya SMG iliyokuwa na risasi nane na kisu kimoja.

Kamanda Msangi amesema majambazi watatu walifanikiwa kutoroka kutoka kwenye mapango hayo kuelekea maeneo ya Nyasaka na baada ya jambazi mmoja kubaini kuwa askari polisi walikua wanamfuatilia alitoa bunduki  na kutaka kuwapiga askari polisi lakini polisi waliweza kumuwahi na kumfyatulia risasi sehemu mbalimbali za mwili wake na kufariki dunia papo hapo.

Amesema askari polisi wamefanya upekuzi kwenye mapango ya mlima wa Utemini na kufanikiwa kupata vitu mbalimbali vilivyoachwa na majambazi hao ambavyo ni pamoja na risasi nne,kisu kimoja chenye damu,kofia ya kuficha uso nyeusi moja (mask),jiko la stove,masufuria ya kupikia, unga wa mahindi,sukari,dagaa,chakula kilichopikwa,ngoma mbalimbali,na simu tatu za mkononi.

Askari aliyejeruhiwa amelazwa hospitali ya rufaa ya bugando na hali yake inaendelea vizuri,polisi bado wanaendelea na msako wa kuwatafuta majambazi waliofanikiwa kutoroka.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, akiongozana na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo alitembelea kwenye mapango ya Utemini na kuwaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi katika kuwafichua wahalifu

Msanii Diamond Atoa Msaada Wa Madawati 600 Kwa Mkuu Wa Mkoa Wa Dar Es Salaam Mhe. Makonda

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda akimpongeza Mkurugenzi wa WCB, msanii Naseeb Abdul 'Diamond Platinumz' mara baada ya kumtembelea ofisini kwake na kutoa mchango wake wa madawati yapatayo 600 kwa ajili ya kuchangia maendelea ya mkoa.

Akiongea katika makabidhiano hayo msanii huyo alisema ni jambo jema kwao kuweza kujitolea mchango huo ili kuweza kumuunga mkono Mhe. Makonda katika kukabilana na changamoto za elimu.
  
Mkurugenzi wa WCB, msanii Naseeb Abdul 'Diamond Platinumz' akiongea mara baada ya kukabidhi msaada wa madawati yapatayo 600 kwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda ili kuweza kupunguza tatizo la wanafunzi kukaa chini. Makabidhiano hayo yalifanyika leo Juni 6, 2016 ofisini kwa mkuu wa mkoa jijini Dar es Salaam.
  
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda akitoa shukrani zake za pekee kwa Mkurugenzi wa WCB, msanii Naseeb Abdul 'Diamond Platinumz' kwa kuweza kutoa madawati 600 ikiwa ni mchango wake katika elimu ya kuweza kufanya wanafunzi kukaa sehemu salama. Mhe. Makonda alisema kuwa wakati umefika kwa wasanii wakaweza kujitoa katika jamii ambayo imekuwa ikiwapa wao sapoti na msanii Diamond amekuwa wa kwanza kuonyesha moyo wa pekee kwa kurudisha fadhila.
  
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa WCB mara baada ya kumtembelea ofisini kwake.


Tucheke Kidogo na Video Hii ya Masanja Akisifia Msosi Huu Kutoka Kwa Wajaruo

$
0
0
Wengi wameshamzoea kumuona Masanja Mkandamizaji akichekesha katika vipindi vya TV ila ni wachache sana wanaojua kua Masanja ni mchekeshaji zaidi pale anapokua nje ya kamera. Wiki iliyoisha Masanja au Mchungaji Masanja anavyopenda kujiita akiwa abatoa huduma ya neno la Mungu alitoa kali ya mwaka.

Akiwa katika kijiji cha Shilati yeye na wahubiri wenzake walialikwa katika chakula cha mchana na vituko alivyowafanyia wenyeji wake viliwavunja mbavu sana. Alisifia chakula hicho kwa njia ambayo ni lazima ucheke. Unaweza tazama video ya Masanja akiombea msosi huo hapa chini......

Taarifa ya Ofisi ya Spika kuthibitisha kupokea hoja ya kumeondoa madarakani Naibu Spika

$
0
0
Ofisi ya Spika imepokea taarifa ya kusudio la kuleta Bungeni Hoja ya kumwondoa madarakani Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb) iliyowasilishwa na Mbunge wa Simanjiro Mhe. Mhe. James Kinyasi Millya siku ya Jumatano tarehe 1 Juni, 2016.

Utaratibu huo ni wa Kikatiba na upo chini ya Ibara ya 85(4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 ambapo pia umeainishwa katika Kanuni ya 138 (1), ya kanuni za Kudumu za Bunge kuhusu utaratibu wa Kumwondoa Naibu Spika Madarakani.

Baada ya kupokea kusudio hilo, Kanuni za Bunge zinamtaka Spika kuiwasilisha hoja hiyo katika Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ili ifanyiwe kazi.

Kutokana na msingi huo wa kikanuni, Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (Mb) anakusudia kuliwasilisha swala hilo kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kama Kanuni inavyoelekeza ambapo kamati hiyo itaangalia msingi wa hoja na endapo itaridhika, kanuni inaitaka Kamati kuwasilisha hoja hiyo Bungeni ili ijadiliwe.

Aidha, Kanuni ya 138 (3) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, inamtaka Spika kukalia kiti wakati wa mjadala wa hoja ya kumwondoa Naibu Spika Madarakani.

Hivyo basi, suala lililowasilishwa na Mhe. James Kinyasi Millya kuhusu kusudio la kumwondoa Naibu Spika Madarakani, tayari limepokelewa na lipo katika Ofisi ya Spika kwa ajili ya utekelezaji wa masharti ya Kanuni.

Imetolewa na,
Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano
Ofisi ya Bunge
DODOMA
6 Juni, 2016.

Shishi Baby Amlia Mingo Raymond wa WCB..Wanaswa Kona Wakipeana Denda...

$
0
0
Meneja wa WCB alisema ''Wasanii wa WCB wanapenda wanawake waliowazid umri kwasababu...)

Yule Ngapepe Sukari ya vijana aka Mario ajulikane kama Shishi Baby juzi kwenye party ya kumkaribisha Rich Mavoko kwenye Lebo kubwa ya Muziki Tanzania WCB alionekana kagandana na kijana mdogo Rayvan mzee wa hapa kwetu huku wakipeana milenda milenda ndimi nje bila kujali watu waliopo.

Sasa sijui ilikuwa ni furaha, pombe, mapenzi au ndio mambo ya kiki!!

Kila laheri kijana.

Faiza Ally: Sipo tayari kurudiana na ‘Sugu’ ila akihitaji mtoto mwingine nipo tayari ‘kumpatia’

$
0
0
Muigizaji na mrembo Bongo, Faiza Ally amesema hayupo tayari kurudiana kimapenzi na baba watoto wake ambaye ni Mbunge wa Mbeya mjini Joseph ‘Sugu’ Mbilinyi, ila yupo tayari kuzaa nae mtoto wa pili.

Akiongea kupitia kipindi cha Kubamba cha Times Fm Jana, bidada huyo Mama wa mtoto mmoja aitwae Sasha amedai hamkumbuki Sugu kwa kuwa hakuwa ‘Romantic’ na alizo nazo kwake ni hisia tu za kupata mtoto wa pili na yeye.

“Sitaki kuzaa na kila Mwanaume, nieleweke wazi sitaki kurudiana na Sugu ila akinifata akidai anataka tuzae mtoto wa pili nipo tayari” Alisema.

Katika ‘line’ nyingine Mama Sasha alisema anajutia kitendo chake cha kutokutumia kinga alipojamiiana na Baba mtoto wake huyo kitendo ambacho kilisababisha kupata Ujauzito.

Diamond: Nadhani Wema Sepetu ameanza kunikubali kimya kimya

$
0
0
Akiwa kwenye kipindi cha Friday Night Live cha EATV, Diamond Platnuzm amesema kitendo alichofanya Wema kupost kazi zake anadhani Wema Sepetu ameanza kumkubali kimya kimya na ameona labda hakuna sababu yeye kuendelea kumchukia Diamond Platnumz, ndiyo maana ameonyesha upendo kwa kusupport kazi zake na za wasanii kutoka kwenye Label yake.

“Kuna wakati inafika watu mnakuwa mmekuwa labda, mtu anaona hana sababu ya kuendelea kukuchukia au kuwa na vita na wewe, sababu mwanzo mwanzo mkiwa bado mnaenda mnaona kuna vitu mko navyo ndiyo maana kuna kuwa na chuki kubwa, lakini ikifika wakati kila mtu amesonga mbele na maisha yake, ameridhika na maisha yake anaona kwanini nimuwekee vita mtu fulani.
Hivyo nadhani labda wakati huo ndiyo huu maana mwenyewe nimeona kweli amepost BET, amepost promo ya Rich Mavoko kwangu mimi nafurahi kwa sababu naona haina faida kwa sisi wasanii kuwekeana vita” alisema Diamond Platnumz.

Mbali na hilo Diamond Platnumz alidai toka ameachana na Wema Sepetu hana namba yake ya simu, hajawahi hata siku moja kumpigia simu wala Wema Sepetu hajawahi kumpigia simu Diamond Platnumz.

CCM Yatangaza Kuzunguka Nchi Nzima Kuwakabili CHADEMA Waliojipanga 'Kumharibia' Rais Magufuli kwa Wananchi

$
0
0
Siku chache baada ya Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutangaza kufanya mikutano nchi nzima kwa lengo la kuishtaki kwa wananchi Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli, CCM wamejibu mapigo  kwa kuapa kuwafuata kila kona watakayopita.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka alisema kuwa chama hicho hakiwezi kuvumilia kuona Chadema wanazunguka kuharibu taswira ya Rais Magufuli na Serikali yake ambayo alieleza kuwa imefanya kazi kubwa kuwatumikia wananchi katika kipindi kifupi.

Alisema kuwa wamepata taarifa zisizo na shaka kuwa Kamati Kuu ya Chadema iliyokutana Mei 16 mwaka huu ilibaini kuwa kwa muda mfupi, Magufuli ametekeleza ajenda zote ilizokuwa ikinadi wakati wa Uchaaguzi Mkuu.

Ole Sendeka alisema kuwa utendaji wa Rais Magufuli unatuma ujumbe wa dhahiri kuwa Chadema watashindwa tena katika uchaguzi wa mwaka 2020.

Aliongeza kuwa malalamiko ya udikteta wanayoyasambaza yanaonesha kuwa hawana mjadala wowote wa kumkosoa Rais Magufuli.

“Tunawaonya viongozi wa Chadema. Wanapaswa kutumia majukwaa hayo kunadi sera za Chadema. Nataka kuwahakikishia kuwa, kama Chadema wataenda sehemu fulani Jumatatu, sisi tutakuwa pale Jumanne kusafisha hali ya hewa kwa kuwaeleza ukweli wananchi,” alisema Ole Sendeka.

Chadema wamepanga kufanya mikutano nchi nzima kwa kile walichoeleza kuwa ni kuishtaki Serikali kwa wananchi kuhusu mwenendo wa Serikali ikiwa ni pamoja na kubanwa kwa Demokrasia na Bunge kwa ujumla na utumbuaji majipu usiofuata sheria na taratibu.

Nipo Tayari Kufanya Kazi na lebo ya WCB Inayomilikiwa na Diamond– Abdu Kiba

$
0
0
Abdul Kiba amesema yupo tayari kujiunga na lebo ya WCB inayomilikiwa na Diamond kama hela itawekwa mezani.

Bifu la Alikiba na Diamond linaonekana kuathiri mpaka mfumo wa watu wa pembeni wanaowazunguka wasanii hao japo kila mmoja anakubali kuwa hana tatizo na mwenzake huku ukweli wa kila mmoja ukibaki moyoni mwake.

Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo, kinachoruka kupitia EA Radio, Abdu Kiba alisema kuwa kama watakuwa na pesa za kutosha na makubaliano mazuri anaweza kufanya kazi chini la Label hiyo [WCB].

“Nipo tayari naangalia pesa, kama pesa zitakuwepo na wakihitaji kufanya kazi na mimi naweza nikafanya kazi chini ya lebo hiyo,” aliongeza.

Siku chache zilizopita Abdu Kiba ameachia video ya wimbo wake mpya ‘Bayoyo

Polisi Watumia Mabomu ya Machozi Kuwatawanya Wafuasi wa CHADEMA

$
0
0
Polisi mkoani Kahama wametumia mabomu ya machozi kutawanya makundi ya wananchi wanaokutwa wamekusanyika katika maeneo mbalimbali.

Mabomu hayo yameendelea kurindima katika viwanja vya CDT ili kuwatawanya wananchi hao waliokusanyika kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa hadhara wa Chadema.

Mkutano huo ulipangwa kufanyika leo kuanzia saa 9.00 alasiri kabla ya polisi kuupiga marufuku na jeshi hilo kuzuia mikutano mingine kama hiyo nchini.

Kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyotolewa jioni la leo na Kamishna wa Polisi Operesheni na Mafunzo, Nsato Mssanzya amepiga marufuku maandamano na mikutano ya hadharahadi hali ya usalama itakapotengemaa.

Amesema Jeshi la Polisi halitasita kuchukua hatua kali za kisheria kwa mtu yoyote au chama chochote kitakachokaidi agizo hilo.

Menejimenti za Muziki za Kimataifa Hazifahamu Soko la Kiafrika; Wasanii Wawe Makini

$
0
0
Imeandikwa na Kennedy Daima Mmari na Alpha Wawa

Hakuna shaka kuwa menejimenti nzuri ina mchango mkubwa katika mafanikio ya msanii. Dhana hii inaweza kudhihirika kwani kuna wasanii wengi na wakubwa ambao mafanikio yao makubwa yanatokana na kuwa chini ya utawala ambao unaweza kumudu kuwasaidia kuendesha shughuli zao za kimuziki.

Kiuhalisia, menejimenti nzuri haiishii tu kupanga ni lini nyimbo itoke, ni nyimbo ipi na ya aina gani itoke, msanii apande jukwaa lipi na lipi asipande, mkataba upi asaini na upi asisaini bali pia huenda mbali zaidi na kumsaidia msanii katika kutawala maisha yake ya kila siku, kitu gani afanye na nini aseme, na pengine skendo gani aitengeneze na ipi aiepuke jambo ambalo hutengeneza mustakali mzuri katika kuhakikisha mafanikio hayaepukiki kwa msanii husika.

Kutokana na hali hii, basi ni muhimu menejimenti au lebo za muziki zikafahamu kwa undani mzunguko mzima wa sanaa na maisha ya msanii husika kabla ya kuamua kumsaini na kumsimamia. Katika kuthibitisha dhana ya kuwa menejimenti kubwa za kimataifa hazifahamu vizuri muziki wa kiafrika, mara kadhaa ambapo wasanii wamesainiwa wameishia kupoteza hata kile walichokuwa nacho.

Dbanj aliyekuwa anasimamiwa na Mo’ Hits Records chini ya Don Jazzy hakuja kuwa Dbanj aliyekuja kusaini na Good Music ya Kanye West, kwanini? Kwasababu Good Music haifahamu muziki wa kiafrika ambapo D’banj ana mashabiki wengi zaidi.

Ni dhahiri shahiri kuwa hakuna msanii ambaye asingependa kusaini kwenye lebo za menejimenti za muziki kubwa kama Sony Music Entertainment, Good Music, Roc Nation, Universal Music Group Konvict au lebo nyingine kubwa lakini pia kabla hajakata shauri la kuingia katika mkataba wa aina hiyo, anatakiwa kufikiria ni nini anakihitaji na soko la muziki wake liko wapi.

Msanii aliyeshinda Airtel Trace Muic Star 2015, shindano linalosimamiwa na kudhaminiwa na Airtel Africa na kituo cha runinga cha kimataifa cha Trace Urban kilichopo Nigeria ni kielelezo kingine kuwa lebo hizi hazitambui soko la Afrika. Mwaka mmoja baada ya kushinda shindano hilo alikuwa amefanya nyimbo moja tu chini ya menejimenti ya Universal Music Group, unafikiri ni kwanini?

Kwasababu jamaa wa menejimenti hii hawafahamu muziki wa kiafrika ni mapambano na mashindano ya kutoa nyimbo na video kali ili uweze kuwa hai kwenye kiwanda cha muziki. Mayunga ameondoka Universal Music Group, hii ina maana rahisi kuwa jamaa wamemshindwa, wameshindwana!

Jambo lingine linaloweza kuwa linaathiri ufanisi wa lebo hizi kwa wasanii wadogo hasa wa kiafrika ni kujikita na na kuweka rasilimali nyingi kwa wasanii wakubwa waliopo katika lebo hiyo. Mfano, Alikiba amesainiwa Sony Music Entertainment, je atapewa kipaumbele sawa na Davido ambaye alipewa dola milioni moja kusaini au Adele ambaye atapewa dola milioni 18 kwa mwaka? Ni wazi kuwa watajikita kule pesa ilipo.

Sony au Universal hawafahamu kabisa kuwa Mayunga au Alikiba anauza muziki wake zaidi nyumbani Tanzania au Afrika Mashariki, na si rahisi wao kuona umuhimu wa kuwasimamia katika misingi ambayo itawasaidia kukita mizizi Tanzania na kuongeza wingi wa mashabiki ambao watawafanya waonekane bara zima la Afrika, badala yake wanachukulia kama wanamsimamia Chris Brown au Justin Bieber ambaye anafahamika kila kona.

Rapper wa kike wa Uganda Keko aliichana na lebo ya Sony kabla ya kuondoka kuwa imekuwa kikwazo katika ukuaji wa muziki wake, na ni kwasababu lebo ilikuwa haimsikilizi na haitaki kutoa nyimbo zake ambazo alisharekodi wakati ambao yeye aliamini kuwa mashabiki wake walihitaji kumsikia zaidi.

Katika hali inayoonesha kuwa lebo hizi pengine huwasaini wasanii ili kujiongezea soko au umaarufu katika nchi wanazotokea, Sony ilishawahi kuwasaini Rose Muhando na Nakaaya Sumari miaka iliyopita, ingekuwa ni lebo inayotambua soko la Afrika linahitaji nini, basi bila shaka wasanii hawa wangekuwa mbali zaidi ya walipo hivi sasa.

Ni dhahiri ya kwamba muziki wa Kiafrika hauhitaji menejimentIi ya nje ya Afrika ili kufanikiwa. Miaka ya tisini kipindi muziki wa Kongo ulisikika Afrika nzima hakuna hata lebo moja ya nje ya Kongo ilikuwa ikimsimamia msanii wa Kongo bali ni watu kama wakina Logaloga ambao walifanikisha na wasanii wa Kongo wakaweza kusikika Afrika na duniani wakifanya matamasha makubwa yanayojaza viwanja Ulaya, kwanini? Ni kwa sababu tu ya kujua ni upi msimu wa Zouk, upi msimu wa Rhumba, lini na kwanini msanii aimbe lingala na lini achanganye lingala na kifaransa.

Msanii kama Wizkid anashirikishwa na msanii mkubwa kama Drake sio kwasababu ana menejimenti ya Marekani bali ni menejimentI yake ya Nigeria imehakikisha inambrand vizuri msanii wao.
Lebo kubwa kama Sony, Universal, Good Music au hata Roc Nation ni ngumu kupenya kwenye soko la Afrika labda kama uongozi wa Sony Africa ungekuwa ni wa Waafrika wenyewe, kina Don Jazzy, kina Babu Tale nk kwa sababu muziki wa Afrika una mazingira tofauti na Marekani na Ulaya.

Hapa kwetu kuna ushkaji, nani anamjua nani (wadau) na rafu za hapa na pale, sasa wale wazungu hawatambui hayo wenyewe wanachojua ni professionalism (weledi) wakati soko linahitaji weledi,fitna na figisu figisu. Hawafahamu kuna wakati msanii mkubwa anaweza akapigishwa show bure na yeye kukubali kwasababu ya kujitengenezea kesho yake(udau), hawajui muziki wa kitanzania una msimu wake wa show msanii analenga atoe nyimbo yake ili avizie msimu huo, hawajui kuna ushindani baina ya fulani na fulani hivyo msanii anaweza taka nyimbo yake itoke ili igombanie tuzo na airwaves na msanii fulani.

Kwa ushauri tu, wasanii wawe na menejimenti za ndani kwa ajili ya soko la ndani na menejimenti za kimataifa kama Sony kwa ajili ya soko la nje.

Rais Magufuli Apokea Shilingi Bilioni 12 Ya Tume Ya Uchaguzi Zilizokuwa Zimebaki Baada ya Uchaguzi Mkuu

$
0
0
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imekabidhi shilingi Bilioni 12 kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, zilizobaki baada ya uchaguzi mkuu wa Madiwani, Wabunge na Rais uliofanyika tarehe 25 Oktoba, 2015.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva amekabidhi hundi ya kiasi hicho cha fedha kwa Rais Magufuli leo tarehe 07 Juni, 2016 Ikulu Jijini    Dar es Salaam na kueleza kuwa bakaa ya fedha hizo haikuathiri kwa namna yoyote uchaguzi mkuu wa mwaka jana.

"Mheshimiwa Rais fedha ambazo tunakukabidhi, tulijibanabana sana, japo muda wenyewe ulikuwa mfupi lakini tulijibanabana sana bila kuathiri utendaji wa shughuli za uchaguzi, isije ikawa inatoa sura kwamba iliathiri, haikuathiri, na katika hali hiyo kama ambavyo wengi ni mashahidi, hatujisifii, lakini uchaguzi ulienda vizuri" Amesema Jaji Mstaafu Lubuva.

Akizungumza baada ya kupokea mfano wa hundi hiyo, Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameipongeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuokoa fedha hizo na kuzirejesha serikalini ili zipangiwe majukumu mengine na ametaka taasisi nyingine za serikali ziige mfano huo wa uzalendo na kutanguliza maslahi ya taifa.

"Kitendo hiki ambacho mmekionesha leo, kinaonesha ni kwa namna gani Tume ya Taifa ya Uchaguzi chini ya uongozi wako Mheshimiwa Mwenyekiti ilivyo na watu makini na waadilifu sana, kwa sababu hizi fedha ambazo kwa lugha uliyotumia ni bakaa, kutokana na zile ambazo mlipewa zaidi ya Shilingi Bilioni 270, mkatumia shilingi Bilioni 261.6, mkabakiza shilingi Bilioni 12, mngeweza kuamua kusema hamkubakiza na hakuna mtu yeyote ambaye angewauliza, na saa nyingine pengine hakuna mtu yeyote ambaye angejua, mngeweza pia kusema kiasi mlichotupa hakijatosha, tunaomba mtuongezee ama mngetengeneza maneno mazuri mazuri ya matumizi, bado nina uhakika serikalini wasingejua" Amesema Rais Magufuli.

Pamoja na kukabidhi hundi ya bakaa ya shilingi Bilioni 12, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva amemuomba Rais Magufuli aisaidie tume hiyo kupata jengo lake la ofisi kwa kuwa hivi sasa tume inatumia majengo ya kupanga ambayo yanaigharimu tume hiyo takribani shilingi Bilioni 1 na Milioni 400 kila mwaka kwa kulipia kodi ya pango, usafiri na gharama nyingine za uendeshaji.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli amelikubali ombi hilo na kuamua kuwa fedha ambazo Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeziokoa (Shilingi Bilioni 12) kutoka kwenye Uchaguzi Mkuu wa Mwaka jana zitumike kujenga ofisi ya tume, na amependekeza ofisi hiyo ijengwe mkoani Dodoma.

"Na mimi ningefurahi zaidi kama hilo jengo lingejengwa Dodoma, kwa sababu Dodoma ndio makao makuu ya nchi hii, na hasa kwa sababu Dodoma ni katikati ya Tanzania" Amesisitiza Rais Magufuli.

Rais Magufuli pia amelikubali pendekezo la tume hiyo la kuanzishwa kwa mfuko wa tume ya uchaguzi ambao utakuwa unakusanya fedha kila mwaka kwa ajili ya uchaguzi mkuu unaofuata, badala ya kuendelea na utaratibu wa sasa wa kusubiri mwaka wa uchaguzi ndipo zitengwe fedha zote za kugharamia uchaguzi huo.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es Salaam

07 Juni, 2016

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya June 8, Ikiwemo ya Wema Sepetu na Madam Rita Wazua Gumzo

$
0
0


SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya June 8, Ikiwemo ya Wema Sepetu na Madam Rita Wazua Gumzo

Zitto Kabwe Aitwa Polisi Kwa Mahojiano

$
0
0
Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe jana tarehe 7/6/2016  aliitwa Polisi  na Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalumu ya Dar es salaam  ACP Camilius Wambura.

Kwa mujibu wa Katibu Itikadi, Mawasiliano na Uenezi wa chama hicho  Ado Shaibu, amesema ACP Wambura amemuita Zitto Kabwe kuhojiwa ikiwa ni siku moja imepita tangu azindue operesheni Linda Demokrasia ambayo inatarajiwa kuzunguka nchi nzima kupinga ukandamizwaji wa Demokrasia nchini

Amesema licha ya Zitto kuitwa na Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalumu ya Dar es salaam  Wambura aliomba Zitto  asiende jana kwa kuwa ni karibu na masaa ya kufuturu na  kumtaka  aende leo  saa tatu asubuhi.

Kwa upande mwingine  Shaibu amesema  Chama cha ACT-Wazalendo kitawasiliana na wanasheria wao ili kupata tafsiri ya kimahakama ya uhalali wa jeshi la polisi kuzuia mikutano ya vyama vya siasa ambayo inatambuliwa na kulindwa na katiba.
Viewing all 104776 articles
Browse latest View live




Latest Images