Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104432 articles
Browse latest View live

AUDIO: Mwembe Ambao usiku Hubadilika kuwa Mwalimu Nyerere na Mama Nyerere Wavuta Mamia ya Watu Kuushuhudia Tanga

0
0
Mti wa  ajabu aina ya Muembe umewavuta mamia ya wakazi wa Tengamano Jijini Tanga kuushuhudia ambapo inadaiwa kuwa mwembe huo ikifika majira ya jioni hubadilika na kuwa  na taswira ya mwalimu Nyerere kwa upande mmoja na Mama Nyerere kwa upande wa pili

Tukio hilo limesemekana lilianza kujitokeza June 6 2016.  "Ni kama muujiza fulani sio kwamba jambo hili liliwahi kujitokeza,  hapa nilipo ndio naona hali halisi ya huu mwembe, ni kama mtu alijaribu kuuchonga"- Anasimulia shuhuda wa Tukio hilo  Awadhi Ally

Bonyeza play hapa chini kusikiliza

Baby Madaha: Sina Hobi na Serengeti Boys Kama Shilole na Wolper

0
0
MSANII na mcheza filamu za Kibongo, Baby Madaha amesema hapendi kushiriki mapenzi na wanaume wa umri mdogo ‘Serengeti Boys’ kwani watu hao hawawezi kumshauri mambo ya maendeleo.

Baby alitoa kauli hiyo baada ya kutakiwa kutoa maoni yake juu ya kuongezeka kwa idadi ya wanawake wanaojihusisha kimapenzi na Serengeti Boys.

“Serengeti boys siyo hobi yangu kwa kweli maana watanizingua tu, nawapenda watu wazima maana wananipa akili za kimaendeleo, hao watoto hawawezi kunisaidi chochote cha maana nawashangaa hata hao wanaokuwa nao,” alisema Baby Madaha.

Bodi ya Mikopo Yakanusha Taarifa Zilizosambazwa Mitandaoni Kuhusu Maombi Ya Mikopo 2016/2017

0
0
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inapenda kukanusha taarifa zinazosambazwa kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii kuwa imetangaza sifa na vigezo vitakavyotumika katika uchambuzi wa maombi ya mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2016/2017.

Taarifa hizo zinazosambazwa, pamoja na mambo mengine, zinaeleza kuwa sifa zitakazotumika kuwa ni ufaulu wa waombaji katika mitihani yao ya elimu ya sekondari na diploma. Aidha, taarifa hizo zinaeleza kuwa maelezo rasmi yanapatikana katika tovuti ya Bodi ya Mikopo na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU).

Bodi inapenda kuwataarifu wadau wake wote, wakiwemo wale wanaotarajia kuomba mikopo ya elimu ya juu kuwa taarifa hizo sio za kweli na kuwaomba wawe na subira wakati Bodi inakamilisha taratibu za uombaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2016/2017.

Baada ya kukamilika kwa taratibu hizo, mwongozo wa utoaji mikopo utatolewa rasmi na kutangazwa kwa umma kupitia njia mbalimbali vikiwemo vyombo vya habari na tovuti ya Bodi ya Mikopo www.heslb.go.tz

IMETOLEWA NA:
KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI,
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU,
JUMANNE, JUNI 7, 2016

Taarifa hii pia inapatikana katika tovuti ya Bodi (www.heslb.go.tz)

Upepo wa Edward Lowassa Wazidi Kuyumbisha CCM

0
0
Wabunge wa CCM wameunda kamati maalumu ya wabunge 15 kwenda kutathmini uchaguzi mkuu, badala ya kutegemea ripoti zinazotolewa na makatibu wa wilaya na mikoa pekee.

Katibu wa wabunge hao, Jason Rweikiza alisema kamati ya wabunge hao itawahoji wabunge wote wa CCM 267 kwa sababu ndiyo wahusika wakuu, kuangalia changamoto walizokutana nazo.

Miongoni mwa wajumbe hao ni Joseph Mhagama, Dk Faustine Ndugulile, Joseph Kakunda, Profesa Anna Tibaijuka, Mboni Mhita, Peter Serukamba, Innocent Bashugwa, George Mkuchika, Munira Mustapha, Jasmini Tiisekwa na Abdallah Ulega.

 Katika hatua nyingine, CCM Mkoa wa Ruvuma imewatimua wanachama 62 kwa usaliti ikiwamo kumuunga mkono Edward Lowassa katika Uchaguzi Mkuu 2015.


Bunge Lakanusha Uvumi Ulioenea Kuhusu Afya ya Spika wa Bunge Job Ndugai

0
0
Ofisi ya Bunge imesema Spika wa Bunge, Job Ndugai anatarajiwa kurejea nchini muda wowote akitokea India alipokuwa akifanya uchunguzi wa afya yake.

Taarifa hiyo ya Bunge imekuja siku moja baada ya taarifa kusambaa kwenye mitandao ya kijamii ikieleza kuwa kiongozi huyo yuko katika hali mbaya, jambo ambalo limeelezwa siyo kweli. Takribani wiki ya tatu sasa, Ndugai hajaonekana bungeni.

Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano ya Bunge, Owen Mwandumbya alisema jana kuwa kiongozi huyo amekwenda India kwa uchunguzi.

Alisema Spika aliporejea kutoka India Desemba mwaka jana, alitakiwa kurudi tena baada ya muda kwa ajili ya uchunguzi.

“Atarudi muda wowote kuanzia hivi sasa kwani yuko nchini India,” alisema Mwandumbya.

Alifafanua kuwa hali ya spika iko vizuri na hivi sasa anafanya mambo ya kawaida ili aweze kurejea nchini.

Mwaka jana baada ya Ndugai kuwasili kutoa India, alisema afya yake iko imara na anaendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu na madaktari.

Yanga Imemuongezea Mkataba Mbuyu Twite, Lakini Imemtema Staa Wake Mmoja wa Kimataifa

0
0
Good news kwa mashabiki wa klabu ya Dar es Salaam Young Africans, ikiwa imepita siku baada ya Yanga kufanikiwa kuwasajili wachezaji wawili golikipa Beno Kakolanya kutoka Tanzania Prisons na beki wa pembeni Vicent Andrew kutoka Mtibwa Sugar, leo June 7 wametangaza kumuongezea mkataba kiungo wao wa kimataifa wa Rwanda Mbuyu Twite.

Yanga wamemuongezea mkataba wa miaka miwili Mbuyu Twite, lakini wamempa barua ya kuvunja mkataba kiungo wao wa kimataifa wa Niger Issafou Boubacar, hivyo huenda kukawa na mpango wa kumuongeza staa mwingine wa kimataifa atakayerithi nafasi ya Issafou Boubacar.

Hamisa Mobeto Amlipua Lulu Michael Kisa Kigogo Penzi la Kigogo

0
0
Mwanamitindo ambaye pia ni video queen maarufu Bongo, Hamisa Hassan Mobeto, amemlipua laivu staa wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ kisa kikidaiwa ni lile saga la kugombea penzi la kigogo (jina tunalo) ambapo kwa sasa hali ni tete baina ya wawili hao.

Hivi karibuni kuliibuka vita kali ya matusi mitandaoni kati ya kundi la mashabiki wa Hamisa linalojiita Team Hamisa na lile la Team Lulu ambapo kila kundi lilitaka kuibuka mshindi huku mada kuu ikiwa ni penzi la jamaa huyo.
Wakati hali ikiwa hivyo, ilibidi wawili hao nao kuvunja ukimya na kuanza kujibizana maneno ya nguoni ambayo yalizua taharuki upya kwa kila upande.

Baada ya kushuhudia malumbano hayo huku kukiwa na maelezo kuwa wawili hao wanachonganishwa, Wikienda lilimtafuta rafiki wa karibu wa Hamisa ili kuanika kiunaga ubaga hasira alizokuwa nazo Hamisa ndipo aliamua kufunguka kwa kumpa makavu Lulu. Mtu huyo alisema kuwa maneno aliyoyatumia Hamisa yalitokana na hasira na hayaandikiki gazetini huku akifafanua kuwa yeye ana mtoto lakini Lulu hana uchungu kwa kuwa bado hajazaa.

Baada ya kujazwa data hizo, Wikienda lilianza kwa kumtafuta Hamisa ili kupata ufafanuzi juu ya sakata hilo ambapo alisema kuwa utaratibu aliojipangia kwenye maisha yake ya siku hizi ni kutotoa taarifa zake kwa waandishi wa habari hivyo asingependa ‘ku-coment’ lolote juu ya hilo japokuwa kila suala lipo wazi.

“Kusema kweli maisha ya sasa kuna muda unaweza kujikuta ukiingizwa kwenye ugomvi ambao hukutarajia na hivyo kwa kuzingatia hilo nisingependa kuongelea tena habari hii maana utaratibu wangu ni kutotoa taarifa wala mambo yangu kuyaweka wazi kwenye magazeti ila kilichoonekana ndicho hicho kwa sasa sina coment yoyote,” alisema Hamisa.

Kwa upande wake Lulu alijibu mapigo kwa kuandika waraka mrefu bila kumtaja Hamisa lakini wapenda ubuyu wakatafsiri kuwa ujumbe umefika. Kwa muda mrefu sasa kumekuwa na mgogoro kati ya Hamisa na Lulu huku madai ya msingi yakiwa ni kitendo cha Lulu kumchukulia Hamisa baba mtoto wake.

Chanzo:GPL

Mwakyembe Awamaliza CHADEMA Bungeni!

0
0
Anamshangaa Mbunge Sugu wa Mbeya ambaye hata Shule hajamaliza na anahoji umahiri wa PhD holder!

Kwa kweli hawa Wabunge wa chadema sijui hiki Chama kinawatoa wapi ni shiida hasa Sugu, Msigwa halafu eti ndiyo diplomat wa chadema!

Meno ya Diamond Platnumz Yana Thamani ya Shs Milioni 11

0
0

Msanii Diamond amefunguka kupitia kipindi cha XXL kuwa thamani ya meno yake ya bandia ya dhahabu ambayo amekuwa akionekana nayo siku za karibuni ni shs milioni 11.

My perception: Hivi wasanii wa kibongo mtajifunza lini kuwa na financial discipline? Yaani umetafuta hela kwa kujinyima ukianzia maisha magumu halafu leo mambo yamekunyookea unaanza kutumiatumia ovyovyo kama mtu usiyejielewa?

Mr Nice aliwahi kuwa na hela nzuri sana miaka ya mwanzoni ya 2000, lakini kutokana na matumizi mabaya na kushindwa kuwekeza leo hii nasikia hana chochote cha maana.

Diamond ajue tu kuwa historia ina tabia ya kujirudia. Lakini ana nafasi ya kubadilika akiamua kufanya hivyo.

Kwa Mwendo Huu wa Diamond..Mdogo mdogo Utasikia Kaanza Kubwia na Unga Kabisa

0
0
Somo la kujaribujaribu liende kwa Diamond. Mtindo wake wa maisha unabadilika kwa kasi mno. Labda ni kwa sababu Marekani anakwenda mara kwa mara. Kuna kipindi tulimshuhudia akiwa amebandika kipini puani. Mshtuko ukaibuka, kipini tena!

Katika wimbo, Muziki Gani ambao ameshirikishwa na Nay Wamitego, Diamond mwenyewe anawashangaa wanamuziki wa Hip Hop: “Hata mimi mengi nayajua ila wewe mtemi utaanzisha utata, mchezo wenu kutoboa pua bora ninyamaze usinipige mbata.”

Natambua kuwa kile kipini alibandika, hakutoboa pua, ila tofauti ni nini. Anayetoboa lengo lake ni kuvaa kipini kama ilivyo yeye anavyobandika. Diamond anataka kuwa kama yule tajiri, amejipamba, sasa anaamua kuvaa na vipini puani.

Dunia inakwenda kwa kasi mno! Diamond wa leo ametandaza dhahabu mdomoni. Meno yake sasa hivi utadhani ya Lil Wayne, Tatoo ndio usiseme , Shida kubwa ni kwamba hata kuongea siku hizi anapata tabu. Mdomo wa Diamond umekuwa mzito.

Akiwa anazungumza utafikiri ana mapengo ya chini kwa jinsi anavyopata wakati mgumu. Ndipo alipofikia, Umarekani unamtawala. Siku zijazo tunaweza kuona mengi zaidi yanajitokeza kwa bwa’mdogo huyo aliyetokea Tandale na kufanya matukio makubwa ya kimuziki barani Afrika.

Nachukua fursa hii kumkumbusha Diamond kutambua ustaa siyo mpaka aonekane Mmarekani. Mbona alikuwa hana kipini puani na aling’ara Afrika? Mbona hakuwa na dhahabu mdomo na alimpata mwanamke wake cheupe wa Kiganda, Zari The Boss Lady?

Athari kubwa ya kuigaiga ambayo Diamond anaenda nayo, ipo siku ataambiwa kuwa akina Lil Wayne na Chris Brown wanakuwa vichaa walivyo kwa sababu huwa wanaonja unga, naye itabidi aonje. Na akifika huko, moja kwa moja atageuka kuwa teja. Simuombei afike huko, ila kwa mwendo wake wa kuigaiga, sitashangaa siku nikisikia Diamond anavuta madude.

Na Luqman Maloto

Faiza Ally: Natamani Kuhongwa, Kwa Sababu Sijawahi Kuhongwa Hata Siku Moja

0
0
Muigizaji na mrembo mwenye vituko kibao, Faiza Ally, amesema atafurahi sana endapo atampata mtu wa kumuhonga kwa sababu hajawahi kuhongwa hata siku moja.

Akizungumza kupitia kipindi cha Kubamba cha Times Fm, Bi dada huyo mwenye mtoto mmoja amedai ameanzia mbali kutafuta fedha na karibu kila kitu chake anajihudumia mwenyewe.

Natamani nipate mtu wa kunihonga, coz mimi kila kitu najifanyia mwenyewe, hata biashara yangu nmeisimamisha mwenyewe nilishawahi hata kuuza mama ntilie” Alisema.

Katika hatua nyingine muigizaji huyo ambaye anategemea kuiingiza sokoni filamu yake mpya muda si mrefu, ameweka wazi kuwa amenunua gari ya ndoto yake aina ya Landrover.

Lady Jaydee Ajibu Iwapo ni Kweli Wasanii Wanaogopa Kumshirikisha Sababu Nyimbo zao Hazitachezwa Clouds FM (Audio)

0
0
Kumekuwepo na imani kuwa wasanii wengi wanaogopa kumshirikisha Lady Jaydee kwasababu wanaamini Clouds FM haitoishia tu kutoucheza wimbo huo bali hata zingine zijazo.


Clouds FM na Lady Jaydee wana tofauti ambazo hadi sasa hazijamalizika.

Muimbaji huyo wa Ndindindi amefanikiwa kuelezea suala hilo kupitia kituo cha redio cha Nyemo FM cha mjini Dodoma alikoenda kwaajili ya show yake iliyofana ya Naamka Tena Concert.

“Inawezekana pia lakini hawawezi kusema labda moja kwa moja,” Jide alimjibu mtangazaji wa redio hiyo, Winston Makangale.

“Lakini pia sio vizuri umwongelee mtu ambaye hujui mawazo yake yanafikiria nini au pengine unaweza ukaongea hivyo halafu ikawa sio hivyo ukawa umemsingizia,” aliongeza.

“Kwahiyo nafikiri hilo tuwaachie wao kila mmoja atakuwa anajua kwa nafsi yake kama anaweza au hawezi na sababu zipi zinazopelekea aweze na sababu zipi zinazopelekea asiweze. Lakini la msingi kila mmoja afanye muziki wake kwa nafasi yake na watu waweze kuburudika.”

“Mimi sina tatizo na mtu yeyote ambaye atakuwa yupo tayari kufanya kazi na mimi,” Jaydee alijibu baada ya mtangazaji kusema anatamani kusikia collabo yake na Diamond.

“Bado hatujakutana na wala hatujawahi kukaa kuzungumzia kuhusiana na collabo.”

Msikilize Jaydee hapo chini.

Baraka Da Prince Amdhalilisha Linah Ukumbini..Anaswa Akishika Kifua cha Linah

0
0
Baraka na Linah waliokuwa miongoni mwa mastaa waliokuwa kwenye ratiba ya kuburudisha siku hiyo, walifanya tukio hilo walipokuwa nyuma ya jukwaa (back stage) walipokuwa wakisubiri muda wao wa kutumbuiza ufike.

Paparazi wetu aliyekuwa akifanya ziara ya kushtukiza mara kwa mara back stage, kuna wakati alifanikiwa kumkuta Baraka akiwa ameingiza mkono kwenye kifua cha Linah huku mrembo huyo akionekana kumpa ushirikiano.

“Mh! Huu ni udhalilishaji, hata kama wameamua kuwa na uhusiano, kwa nini haya mambo wasifanyie chumbani? Baraka anamdhalilisha tu Linah. Naye sijui kwa nini anakubali kuingizwa mkono vile,” alisikika shuhuda mmoja.

Alipoulizwa na paparazi wetu kuhusiana na tukio hilo na kama ana uhusiano wa kimapenzi na Baraka, Linah alidai haoni tatizo kwani atakuwa amerejea kwenye himaya yake ya zamani.

“Naona ni bora kumrudia wa zamani ambaye nimemzoea,” alijibu Linah na kuomba aachwe.

Kwa upande wake Baraka ambaye inafahamika ni mpenzi halali wa mtoto mzuri Naj, hakutaka kuzungumzia chochote kuhusiana na tukio hilo zaidi ya kuishia kucheka tu.

Linah na Baraka waliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi kabla ya kila mmoja kuchukua hamsini zake hadi waliponaswa wikiendi iliyopita ufukweni hapo.

Aliyemtukana Rais Magufuli , Isaac Emily Ahukumiwa Kifungo cha Miaka 3 Jela au Kulipa Faini Ya Sh. Milioni 7

0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa Wa Arusha,imemhukumu  Isack Habakuki(40) mkazi Wa Olasiti, kifungo cha miaka mitatu jela au kulipa faini ya shilingi milioni 7 kwa kosa la kumtukana Rais Magufuli kupitia mtandao wa facebook.

Mshtakiwa amekiri kutenda kosa hilo na amekubali kulipa faini ambapo mahakama imeamuru alipe fedha hizo kwa awamu mbili. Katika awamu ya kwanza atalipa July 8 2016 sh mil 3.5 na August 8 2016 atalipa kiasi kilichobaki cha sh mil 3.5.

Isack anayeishi Kata ya Olasite, anadaiwa kutoa lugha ya matusi na dhihaka kwa Magufuli kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook na alikamatwa Machi 23, mwaka huu mjini Arusha na kupelekwa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam kisha alirejeshwa tena Arusha Aprili 14, mwaka huu kwa ajili ya kufunguliwa mashtaka.

Mbele ya Hakimu Mkazi, Augustine Rwizile,  Wakili wa Serikali, Gaudensia Massanja, alidai kuwa Isack alikuwa akikabiliwa na kosa moja ambapo kwa kufahamu na kwa makusudi mtuhumiwa huyo alitumia mtandao wa Facebook kwa nia ya kumtukana Magufuli.

Alidai kwamba mtuhumiwa katika ukurasa wake wa Facebook alichangia maneno yanayosema: “Hizi ni siasa za maigizo halafu mnamfananisha huyu bwege na Nyerere wapi buana.”

Picha zinatisha: Msichana wa Kazi za Ndani Achomwa na Moto Uarabuni

0
0
Msichana Mary Kibwana Kamango (pichani) raia wa Kenya ambaye alinyanyaswa na kujeruhiwa na mwajiri wake huko nchini Jordan amerejeshwa nyumbani.

Mary amesimulia kuhusu unyanyasaji wanaofanyiwa wasichana kutoka Afrika wanaofanya kazi za ndani katika nchi zilizopo katika Falme za Kiarabu.

Tukio lake lilihusisha kupigwa na mwajiri wake na kuchomwa kwa moto wa gesi mapema mwezi Aprili mwaka huu. Pamoja na kuomba msaada hakuna aliyemsaidia ikiwemo vyombo vya usalama nchini Jordan.

Baada ya tukio hilo la kusikitisha, raia wa Kenya wanaoishi katika nchini Jordan walichangishana fedha za nauli na kufanikiwa kumsafirisha mwenzao kurudi nyumbani. Kwa sasa Mary amelazwa katika hospitali ya rufaa ya Kenyatta ambako anapatiwa matibabu ya majeraha ya moto wa gesi.

Mary amewaasa wasichana wenzie dhidi ya unyanyasaji wanaofanyiwa wafanyakazi wa kazi za ndani katika nchi za Falme za Kiarabu.

Mambo Matano Yaliyoibuka Wakati wa Mahojiano ya Zitto Kabwe na Polisi

0
0
Leo June 08 2016 Kiongozi wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe amefika Makao makuu kanda maalum ya Dar es salaam, ikiwa ameitikia wito wa polisi. Zitto amefika kituoni hapo na ametakiwa atoe maelezo kuhusiana na maudhui ya hotuba ambayo aliitoa June 5 2016.

Kupitia ukurasa wake wa facebook chama cha ACT Wazalendo kimeainisha masuala matano muhimu yaliyoibuka wakati wa mahojiano ya Kiongozi wa Chama Cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe na Polisi, Leo Jijini Dar es salaam.

1.Maombi ya Chama Cha ACT Wazalendo ya mkutano ilikuwa ‘Kujenga Chama’ Lakini Chama Kilizindua “Operesheni Linda Demokrasia”.

2. Kusema “Rais Ameropoka kuhusu Sakata la Sukari Nchini” 

3. Kumchonganisha Rais na Wananchi kuhusu suala la kuwaita Vijana wa Kitanzania Kuwa ni “Vilaza” 

4. Kumgombanisha Rais na Wananchi kwa Kusema “Yeye anajifanya Rais wa Masikini (Huku akiwakashifu hao Watoto wa Masikini Kwa Kuwaita “Vilaza”) na hivyo kumgombanisha na wasio Masikini” 

5. Kumwita Rais Dikteta na Kwamba anaendesha Nchi Kiimla 

Kupitia ukurasa huo wametoa taarifa kuwa maelezo ya Jeshi la Polisi ni Kuwa yote hayo yanaangukia kwenye Kifungu Cha 89(1)(a) cha Penal Code, Yaani “Kutumia Maneno ya Matusi yenye Kuweza Kuvunja Amani” (Abusive Language).

Jeshi la Polisi limemuomba Zitto afike Tena Kituoni Hapo Juni 15, 2016 Kwaajili ya Mahojiano zaidi. Mwanasheria wa Ndugu Zitto ameliomba Jeshi la Polisi kupeleka Mashtaka Mahakamani Juu ya Suala Husika, Na Kwamba Ndugu Zitto atakwenda Kuthibitisha Ukweli Na Undani wa Masuala hayo Mahakamani.

Naibu Spika Aagiza Wabunge Watakaokuwa Wanasusia Bunge Kutolipwa Posho

0
0
Kutokana na wabunge wengi waCCM kulalamika na kuomba mwongozo wa spika juu ya wabunge wanaotoka nje baaada ya kujisajili, naibu spika amelipitia suala hilo na hatimaye kuja na hitimisho kuwa wabunge hao hawatapokea posho zao kwa kipindi chote ambacho hawakuhudhuria vikao.

Amesema uamuzi huu ameufikia baada ya kupitia maamuzi mbalimbali yaliyotolewa na bunge juu ya wabunge ambao walikuwa wanaondoka bila kuchangia mjadala ambapo tarehe 08/04/2008 wabunge wa chama cha CUF walitoka bungeni na kususia shughuli zilizokuwa zimepangwa na kiti kilitoa uamuzi wa kutowalipa posho kwa siku zote watakazokuwa nje

PICHA:Muonekano Mpya wa Rapa Chidi Benz Baada ya Wiki Zaidi ya 20 Sober House.

0
0
Chid Benz
Hizi ni post mbili kutoka instagram za kituo cha Clouds Media kuhusu muonekano mpya wa mwanii wa hiphop Tanzania Chid Benz.

Picha za post hizi ziliambatana na Ujumbe wenye maneno haya ” Muonekano mpya wa Chidi Benz Chuma…@CloudsTv pekee inakuonyesha safari za mwana harakati @Kalapina kwenye hatua za kusaidia vijana kuachana na janga la dawa za kulevya kwenye show ya #Harakati. #HarakatiNiVitendo “

Chidi Benz ni msanii aliyepata msaada mkubwa kutoka kwa meneja wa Diamond Platnumz mpaka kupelekea rapa huyu kukubali kwenda kupata matibabu baada ya kuwa mtumiaji wa dawa za kulevya wa muda mrefu jambo ambalo lilimrudisha nyuma kimuziki na maendeleo pia.


Ninavyoishi na Aunt Ezekiel ni ndoa tosha – Mose Iyobo

0
0
Dancer maarufu wa Diamond, Mose Iyobo amesema jinsi anavyoishi na Aunt Ezekiel ni ndoa tosha lakini atafunga ndoa ili watu wa verify kama instagram.
Mose Iyobo na Aunt Ezekiel wamefanikiwa kupata mtoto mmoja [Cookie] mwenye umri wa mwaka mmoja.

Akiongea kwenye kipindi cha E News, kinachoruka kupitia EATV, Iyobo alisema, “Lakini ninavyoishinae ni ndoa tosha kwa sababu tunaishi kama baba na mama hivyo nataka kujithibitisha inabidi nifunge ndoa ili watu wani-verify kama instagram.”

Aidha Iyobo ameongeza kuwa hapendi watu wanavyomzungumzia vibaya mzazi mwenzie huyo wakidai kuwa eti ni mzee kwani angelikuwa hivyo yeye asingelisogea kwa kuwa angelikuwa kama anatembea na mama yake.

Spika Job Ndugai Anaendelea vyema Nchini India....

0
0
Naibu Spika wa Bunge Tulia Ackson amesema kwamba watanzania wasikubali uvumi unaoenezwa na baadhi ya mitandao kwamba Spika wa Bunge Job Ndugai hali yake ni mbaya bali waamini kwamba hali ya Spika ni njema na anaendelea vizuri na matibabu.

Naibu Spika ameyasema hayo baada ya kumalizika kusomwa kwa bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2016 & 2017 na kusisitiza kwamba Naibu Spika ni mzima na anawatakia watanzania mfungo mwema wa mwezi wa Ramadhani.
''Kumekuwa na uzushi mkubwa kuhusu afya yake, ni kweli alikwenda India kwa ajili ya kupata matibabu kama alivyoambiwa na daktari wake alipotoka huko mwaka jana'' amesema Naibu Spika Tulia.
Aidha Naibu Spika amesisitiza kwamba Spika wa Bunge bado anaendelea kuwasiliana na viongozi wa serikali pamoja na baadhi ya wananchi wa jimbo lake.
Hata hivyo Naibu Spika amewataka wananchi kuendelea kumuombea ili aweze kurejea salama kuendelea na kazi zake kama kawaida.
Viewing all 104432 articles
Browse latest View live




Latest Images