Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104689 articles
Browse latest View live

Masoud Kipanya: Maisha plus ilipoteza mvuto baada ya kuingiza kina mama na mambo ya kilimo

$
0
0
Mchoraji maarufu wa vibonzo na mtangazaji wa Clouds FM, Masoud Kipanya amekiri kuwa misimu miwili iliyopita ya shindano la Maisha Plus ilipoteza mvuto kutokana na kuwachanganya vijana na akina mama na pia kuingiza masuala ya kilimo.

Na sasa Masoud amedai kuwa msimu mpya ambao tayari umeanza usaili utarudisha ile Maisha Plus ya awali yenye burudani zaidi.

“Msimu wa tano unarudi kwa vijana peke yao, hakuna tena kina mama, wakulima wala nani hawahusiki. Sasa hivi ni vijana peke yao. Kwahiyo ule mchakamchaka, ile burudani ya nguvu ambayo vijana walikuwa wanaipata kupitia Maisha Plus ya kwanza nay a pili sasa watakuja kuipata tena katika msimu huu wa tano,” Masoud alikiambia kipindi cha Super Mega cha Kings FM ya Njombe kinachoendeshwa na Divine Kweka.

Mwaka huu shindano litahusisha pia vijana kutoka Afrika Mashariki ambapo kutoka Tanzania watakuwa 14 na nchi zingine 16. Mshindi atajinyakulia kitita cha shilingi milioni 30.

ZITTO KABWE:Serikali ya Magufuli Haipo Tayari Kukosolewa na Wapinzani Inatengeneza Mazingira ya Kuwanyamazisha

$
0
0
ZITTO Kabwe, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo ameonya utawala wa Rais John Magufuli kuacha tabia ya kutaka kuziba midomo wapinzani.

Amesema, Serikali ya Rais Magufuli haipo tayari kukosolewa na wapinzani na kwamba, inatengeneza mazingira ya kuwanyamazisha sambamba na kuminya demokrasia.

Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Mjini amesema hayo leo baada ya kutoka kuhojiwa na Kamanda wa Upelelezi Mkoa wa Kipolisi wa Temeke na Naibu Kamanda wa Upelelezi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa saa tatu.

“Mambo kama haya yalikuwa yanaanza kusahaulika katika mfumo wetu wa kisiasa nchi, lakini nyie ni mashahidi mnaona jinsi demokrasia inavyominywa na kuingia kwenye mashaka makubwa. Ni muhimu wananchi wakasimama kidete ili kuitetea demokrasia,” amesema Zitto na kuongeza;

“Wanatia woga wa watu kuzungumza mawazo yao ya kisiasa jambo ambalo si haki kwa kuwa ni sehemu ya wajibu wetu wa kisiasa. Hofu inayojengwa na serikali juu ya wanasiasa wa vyama vya upinzani haina maana.

“Kama leo polisi wametumia zaidi ya masaa matatu, hayo masaa waliyoyapoteza wangefanya kazi ya kupambana na majambazi, wahalifu na madawa ya kulevya badala ya kupoteza nusu siku kwa kutuhoji maswali,” amesema Zitto.

Anasema kuwa, ratiba ya kuzunguka mikoani itasitishwa kutokana na tamko lililotolewa jana na jeshi hilo.

Jeshi hilo limelizuia mikutano ya kisiasa hadi litakapotoa taarifa na kwamba, wanasheria wa ACT-Wazalendo  wataenda mahakamani ili kupata tafsiri sahihi.

“Lakini kama mnavyofahamu, jana limetolewa tamko la kuzuia mikutano yote hadi tamko lingine litakapotoka, hivyo basi tulikuwa tunashauriana na wanasheria ili wapate tafsiri ya kisheria kutoka mahakama kutokana na kwamba siyo sahihi polisi kuzuia mikutano.

“Lazima tuende mahakamani sababu bila ya kupata tafsiri ya mahakama, hatuwezi kufanya mikutano na hatutaki nchi iingie kwenye fujo,” amesema.

Steven Mwakibolwa, Mwanasheria wa ACT amesema kuwa, Zitto alihojiwa juu ya hotuba aliyoitoa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Jumapili wiki iliyopita na kwamba, yuko nje kwa dhamana isiyo na malipo.

“Tusubiri Jumatano wiki ijayo ili tujue kama atapelekwa mahakamani au upelelezi utajiridhisha kuwa hana makosa.

“Aliulizwa maswali mengi ambayo yalihusiana na hotu yake aliyotoa, amelezea kwa kina alichokisema maswali yote alijibu.”

Mwakibolwa amesema kuwa, kwa sasa si vema kueleza maswali aliyoulizwa kwa kuwa si muda na wakati sahihi wa kuliongelea suala hilo sababu liko chini ya upelelezi.

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya June 9, Ikiwemo ya Bajeti ya Magufuli Pasua Kichwa

$
0
0


SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya June 9, Ikiwemo ya Bajeti ya Magufuli Pasua Kichwa

Kodi ya Kusajili Gari Kwa Kuandika Jina Lako Yaongezeka Kutoka Milioni 5 Hadi 10

$
0
0
Bajeti ya Serikali iliyotangazwa huenda ikapunguza idadi ya watu wanaopenda kuonekana tofauti, kwenye usajili wa magari kwa kuandika majina yao badala ya namba.

Wamiliki wa magari wanaotaka kusajili namba binafsi kama kuweka majina yao, sasa watalipa Sh10 milioni badala Sh5 milioni za awali, kwa kipindi cha miaka mitatu.

Akitoa mapendekezo ya mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka 2016/17 jana, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango aliomba Bunge liridhie kufanya marekebisho ya Sheria ya Magari (Kodi na uhamisho wa umiliki) ili kupandisha usajili wa namba hizo.

Namba hizo binafsi zilizoanzishwa miaka minne iliyopita, zinaruhusu mtumiaji kuandika jina au neno lolote kwenye gari lake tofauti na namba za kawaida zinazotumika nchini.

Video : Wacheki Lulu Michael na Majay Walipohudhuria Harusi Pamoja Kama Mr and Mrs

$
0
0
Kwa sasa sio siri tena kua Lulu msanii kutoka Bongomovies anatoka kimapenzi na Majay msimamizi wa EFM Radio ya Dar. Kwa mara ya kwanza wawili hao waliweka uhusiano wa wazi wakiwa nchini Nigeria ambako Lulu siku hiyo alishinda tuzo moja.

Baada ya kurudi Bongo penzi lao lilikua la kificho ila siku za karibuni wameonekana kwenye viwanja vya starehe wakiwa pamoja. Na hapa juzi tu Lulu na penzi wake huyo walihudhuria harusi wakiwa kama couple na Lulu hakuficha jambo hilo kwani aliupload video ikiwaonyesha wakiwa pamoja huku wakionekana wanapendana sana. Unaweza tazama video ya wawili hao hapa chini......

Kuna Msanii Mkubwa Hakupenda Mimi Kujiunga na WCB – Rich Mavoko

$
0
0
Msanii mpya kutoka lebo ya WCB, Rich Mavoko amesema kuna msanii mkubwa bongo alimkataza kujiunga na WCB.

Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo, kinachoruka kupitia EA Radio, Rich Mavoko amesema kuna msanii mkubwa alimtumia ujumbe wa simu na kumuuliza kwanini amekubali kwenda kusimamiwa na Diamond.

Sijawahi kusema hili ila ukweli ni kwamba wakati nataka kwenda WCB kuna msanii mkubwa alinitumia ujumbe na kuniambia Rich Mavoko unakwendaje kusimamiwa kazi zako na Diamond Platnumz, kiukweli aliniumiza sana ila nilimjibu kwa roho moja kuwa brother wewe hujui mimi nimetoka wapi na nakwenda wapi hivyo huwezi kujua hata hili litakujaje kwangu,” aliongeza.

Rich Mavoko amekuwa juu tangu alipojiunga na lebo hiyo ya WCB na kuachia wimbo wake ‘Ibaki Story’ unaozidi kufanya vizuri kwenye TV na Radio.

Jionee Video ya Sanamu ya Freemason iliyopo Nyumbani Kwa Nay wa Mitego

$
0
0
Wa mitego amekua akihusishwa sana na Freemason, hii ishu haijaanza leo imeanza toka kitambo. Hii ni kuanzia alama ambazo mara nyingi amekua akizionyesha katika video zake na hata namba za gari zake 3 ambazo zimekua zikihusishwa na mambo ya Freemason.

Sasa Nay Wa Mitego kaamua kutuonyesha na sanamu iliyo sebuleni kwake ambayo bila ubishi ni sanamu ambayo hutumika kuwatambulisha Freemason. Katika video hiyo ameonekana Nay akiwa na mtoto wao huku sanamu hiyo ikiwa kama moja ya pambo sebuleni hapo. Jioneee video hiyo hapa chini...

Naibu Spika awavuruga wabunge wa Ukawa, Aagiza wasilipwe Posho wakisusa

$
0
0
Hatimaye Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson ametoa maamuzi kuhusu hoja ya wabunge kulipwa posho au kutolipwa wanapoingia Bungeni na baadae kutoka nje kwa shughuli zisizo za Kibunge.

Akisoma muongozo wake muda mfupi kabla ya kuahirisha kikao cha Bunge jioni hii baada ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Phillip Mpango kusoma Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2016/17, Dk. Tulia alisema kuwa wabunge wanaofanya vitendo hivyo hawatalipwa posho.

Alitoa uamuzi huo baada ya kurejea kanuni za Bunge akitumia kanuni ya tano fasili ya kwanza ya toleo la mwaka 2006 na maamuzi yaliyowahi kufanywa na Spika waliotangulia katika hali kama hiyo.

“Hivyo basi, kwakuwa jambo hili halikubaliki, na kwakuwa miongozo kadhaa imeshatolewa kuwasihi waheshimiwa Wabunge wasitoke nje ya ukumbi wa Bunge kwa shughuli zisizo rasmi.

"Naagiza kwamba wabunge wote wanaojisajili kisha kutoka ukumbini kwa kususia vikao vya Bunge, hawatastahili kulipwa Posho kwa siku zote ambao wamekuwa wakijisajili kuingia ukumbini na kisha kutoka ukumbini,” alisema Naibu Spika.

Wabunge wa Upinzani wamekuwa wakitoka nje ya Bunge muda mfupi baada ya kuingia Bungeni katika vikao vyote vinavyoongozwa na Naibu Spika kwa madai kuwa hawana imani naye kwakuwa amekuwa akiongoza Bunge kwa ubabe na kuwapendelea wabunge wa CCM

Mchanganuo Mzima wa Bajeti ya Serikali 2016/ 2017 Iliyosomwa Jana Bungeni, BOFYA HAPA Kujua nini Kimepanda na Nini Hakijapanda

$
0
0
SERIKALI imewasilisha Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2016/2017 ya Sh trilioni 29.53, ambayo nguvu kubwa imewekwa katika kukusanya mapato kwa kulinda viwanda vya ndani na kubana matumizi ya serikali ili kuelekeza sehemu kubwa ya matumizi katika maeneo ya vipaumbele.

Katika bajeti hiyo, bidhaa za lazima zinazogusa maisha ya wananchi ikiwemo mafuta ya petroli na dizeli pamoja na ushuru wa barabara na maji ya kunywa, havijaguswa huku bidhaa za starehe kama bia, sigara, soda, juisi na nyingine kama nguo za mitumba, huduma za kupanga nyumba na uhamishaji fedha kwa simu, vikipandishwa kodi, huku kiinua mgongo cha wabunge, kufutiwa msamaha wa kodi.

Aidha, makusanyo ya mapato yasiyo ya kodi, ikiwemo mapato ya taasisi za udhibiti kama Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Mafuta (EWURA), Shirika la Viwango (TBS), Jeshi la Polisi (Trafiki) na mamlaka nyingine za udhibiti, sasa yatapelekwa moja kwa moja katika Mfuko Mkuu wa Serikali ambapo mahitaji yao ya fedha yatatolewa na Wizara ya Fedha na Mipango, badala ya kujigawia kutokana na bakaa ya mapato waliyokusanya.

Aidha, maduka ya kutoa huduma katika majeshi, yamefutiwa kodi rasmi na badala yake, Serikali inajipanga kuongeza posho kwa askari, ili iwasaidie kukidhi mahitaji yao, huku taasisi za umma na ofisi zote za Serikali, zikipigwa marufuku kufanya biashara na mzabuni asiyetumia mashine za kodi za kielektroniki (EFD’s).

Kodi juu
Katika bidhaa zilizoongezewa ushuru na kodi ni pamoja na vinywaji baridi, kutoka Sh 55 kwa lita mpaka Sh 58, huku ushuru wa forodha katika maji ya matunda (juisi) yanayotumia matunda yanayozalishwa hapa nchini, ukipanda kidogo kutoka Sh 10 mpaka 11 kwa lita. Juisi zinazotokana na matunda ambayo hayazalishwi hapa nchini, ushuru wake pia umepanda kutoka Sh 200 kwa lita hadi Sh 210 kwa lita.

Bia, vilevi, mvinyo
Kwa upande wa bia, serikali imependekeza bia inayotokana na nafaka ya hapa nchini, ambayo haijaoteshwa kama kibuku, ushuru upande kutoka Sh 409 kwa lita mpaka 430.

Bia zingine, ushuru wake pia umepanda ambao sasa utatoka Sh 694 mpaka 729 kwa lita, huku bia zisizo na kilevi, ikiwa ni pamoja na vinywaji vya kuongeza nguvu, ushuru ukipanda kutoka Sh 508 kwa lita mpaka Sh 534.

Kwa upande wa mvinyo uliotengenezwa kwa zabibu zilizolimwa nchini kwa kiwango cha asilimia 75, ushuru wake umepanda kutoka Sh 192 kwa lita mpaka Sh 202.

Ushuru wa mvinyo unaotengenezwa na zabibu zilizolimwa nje ya nchi kwa kiwango kinachozidi asilimia 25 kutoka Sh 2,130 kwa lita mpaka Sh 2,237. Vinywaji vikali, havikuachwa nyuma maana ushuru umepanda kutoka Sh 3,157 mpaka Sh 3,315.

Sigara
Sigara zisizo na kichungi zinazotengenezwa kwa tumbaku ya hapa nchini kwa kiwango angalau asilimia 75 kutoka Sh 11,289 hadi Sh 11, 854 kwa kila sigara 1,000.

Kwa upande wa sigara zenye kichungi zinazotengenezwa kwa tumbaku ya nchini kwa angalau asilimia 75, ushuru juu kutoka Sh 26,689 hadi Sh 28, 024 kwa kila sigara 1,000.

Sigara zenye sifa tofauti na hizo, ambazo hazina vigezo hivyo vya tumbaku ya ndani, ushuru wake umepanda kutoka Sh 48,285 hadi Sh 50,700 kwa kila sigara 1,000.

Katika tumbaku ambayo iko tayari kutengenezwa kuwa sigara, ushuru wake umeongezeka kutoka Sh 24,388 hadi Sh 25,608 kwa kilo huku ushuru wa sigara aina ya Sigar ukibaki kuwa asilimia 30.

Vilainishi, gesi asilia, simu juu
Katika mafuta ya kulainisha mitambo, ushuru umepanda kutoka Sh 665.50 kwa lita hadi Sh 699 kwa lita, huku ushuru wa grisi za kulainisha mitambo, ukipanda kutoka senti 75 kwa kilo, hadi senti 79 kwa kilo.

Gesi asilia pia ushuru umepanda kutoka senti 43 kwa futi za ujazo mpaka senti 45 kwa futi za ujazo.

Kuhusu viwango vya ushuru wa kuhamisha fedha kwa kutumia simu, serikali imependekeza kutoza ushuru wa asilimia 10, kwenye ada zinazotozwa na watoa huduma wa simu, katika kutuma na kupokea fedha, badala ya ushuru huo kutozwa tu katika kutoa fedha.

Kwa mujibu wa Dk Mpango, kwa utaratibu wa sasa, baadhi ya kampuni zinazotoa huduma zimetumia mwanya wa kuhamisha sehemu kubwa ya ada hizo kwenye kupokea fedha na hivyo kuwa nje ya wigo wa kodi.

Ulaji wa wabunge, hisa
Kwa upande wa kiinua mgongo cha wabunge wakati wa kustaafu, sasa kitatozwa kodi kila mwisho wa muhula wa miaka mitano ili kujenga misingi ya usawa na haki katika utozaji wa kodi kwa kila mtu anayestahili kulipa.

Aidha, mapato yote yatokanayo na hisa katika kampuni mbalimbali sasa yatatozwa kodi, baada ya kufutwa kwa msamaha kwa waliokuwa wakimiliki hisa chini ya asilimia 25.

Kodi ya mishahara
Katika kodi inayokatwa katika mishahara (P.A.Y.E), imepunguzwa kutoka asilimia 11 mpaka tisa kwa wafanyakazi wanaopata mshahara wa kuanzia Sh 170,000 lakini hauzidi 360,000. Kwa wanaopata zaidi ya 360,000 lakini haizidi 540,000, watakatwa Sh 17,100 pamoja na asilimia 20 ya kiasi kinachozidi Sh 360,000.

Kabla ya hapo walikuwa wakikatwa Sh 20,900 na asilimia 20 ya kiasi kinachozidi Sh 360,000.

Wanaopata zaidi ya Sh 540,000 lakini haizidi Sh 720,000, watakatwa Sh 53,100 pamoja na asilimia 25 ya kiasi kinachozidi 540,000.

Kabla ya hapo, walikuwa wakikatwa Sh 56,900 na hiyo asilimia 25 ya kiasi kilichozidi 540,000. Kwa wanaopata zaidi ya Sh 720,000 wao watakatwa Sh 98,100 pamoja na asilimia 30 ya kiasi kinachozidi Sh 720,000.

Kabla ya hapo, walikuwa wakikatwa Sh 101,900 pamoja na asilimia 30 ya kiasi kilichozidi Sh 720,000.

Kodi za nyumba
Serikali pia imependekeza malipo ya kupanga nyumba, nayo yatozwe kodi ambayo haikuweka kiwango, ila imependekeza Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato, apewe mamlaka ya kukadiria kiwango cha chini na cha juu cha mapato yapatikanayo na pango ili yatozwe kodi.

Kodi za nyumba, usajili magari, pikipiki
Mbali na mapato ya kodi za nyumba, Serikali imependekeza kupandisha ushuru wa kusajili magari na pikipiki kutoka Sh 150,000 hadi Sh 250,000 kwa kila gari na kutoka Sh 45,000 hadi Sh 95,000 kwa kila pikipiki.

Kwa watumiaji wa namba binafsi za magari, ada sasa itapanda kutoka Sh milioni 5 kila baada ya miaka mitatu mpaka Sh milioni 10.

Kodi ya majengo
Aidha, kodi za majengo sasa hazitakusanywa na halmashauri, badala yake TRA ndiyo inayopewa mamlaka hayo ya kukadiria, kukusanya, kuhifadhi na kuiwakilisha katika halmashauri husika.

Mbali na TRA kupewa mamlaka ya kukusanya kodi ya majengo, serikali pia imependekeza kupunguza misamaha ya kodi za majengo ili majengo mengi zaidi yaingizwe katika orodha ya kulipa kodi.

Ulindaji wa Viwanda
Saruji aina ya (HS Code 2523.29.00) zinazotoka nje ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ushuru wake wa forodha umepandishwa kutoka asilimia 25 mpaka asilimia 35 ili kulinda saruji inayozalishwa nchini dhidi ya ushindani wa bei ya saruji kutoka nje ya nchi.

Kwa bidhaa za chuma ikiwemo mabati kutoka nje ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, nazo ushuru umetoka asilimia 0 mpaka 10, ili kulinda uzalishaji wa bidhaa hizo hapa nchini, huku bidhaa za nondo kutoka nje nazo zikipandishwa kodi kutoka asilimia 10 mpaka 25, kwa nia ya kulinda viwanda vya ndani.

Nyavu za kuvua samaki kutoka nje ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, ushuru wake umepanda kutoka asilimia 10 hadi asilimia 25 huku vichujia vya vilainishi na petroli kutoka nje ya nchi vikiongezwa ushuru kufikia asilimia 25 kutoka asilimia 10, ili kulinda bidhaa za ndani.

Sukari, ngano, mitumba, mafuta ya kula
Katika sukari, serikali imekusudia kupunguza msamaha wa kodi na hivyo waagizaji wa bidhaa za sukari kutoka nje watalazimika kuanza kulipa ushuru wa asilimia 15 kutoka asilimia 10, huku ikitarajiwa kuongezeka zaidi na kuwa asilimia 20 mwaka 2017/18 na asilimia 25 mwaka 2018.19, ili kulinda viwanda vya ndani.

Kwa upande wa ngano kutoka nje, ushuru umepunguzwa kutoka asilimia 35 mpaka 10, kwa kuwa nchi za Afrika Mashariki hazina uwezo wa kuzalisha kulingana na mahitaji.

Kwa upande wa nguo na viatu vya mitumba Serikali imepandisha ushuru kutoka dola za Marekani 0.2 mpaka dola za Marekani 0.4 kwa kilo, kwa nia ya kudhibiti nguo hizo lakini pia imetangaza kujiandaa kuzuia uingizaji wake.

Kwa upande wa mafuta ya kula kutoka nje nayo ushuru umepanda kutoka asilimia 0 mpaka 10 kwa mafuta ghafi ya kula, ili kuimarisha kilimo cha mbegu za mafuta na viwanda vya ndani.

Tozo za pamba, kahawa, korosho
Miongoni mwa tozo zilizofutwa kuondoa kero kwa wananchi ni mchango kwa kila kiwanda cha kuchambua pamba wa Sh 450,000 na ada ya vikao vya halmashauri wakati wa kujadili wafanyabiashara wa pamba ya Sh 250,000.

Kwa upande wa kahawa, Serikali imefuta ada ya leseni ya kusindika kahawa ya dola za Marekani 250, huku ushuru wa kusafirisha korosho wa Sh 50 kwa kilo, ukifutwa.

Tozo zingine zilizofutwa katika korosho ni ushuru wa chama kikuu cha ushirika Sh 20 kwa kilo, gharama za mtunza ghala Sh 10 kwa kilo, kikosi kazi cha kufuatilia masuala mbalimbali Sh 10 na makato ya unyaufu.

Pia Serikali imepanga kuendelea kufuta tozo nyingine zinazokatwa na halmashauri, wakala na mashirika katika mazao ya wakulima, baada ya kufanya tathmini za kina.

Maduka kambi za jeshi
Serikali imependekeza kufuta msamaha wa kodi uliokuwa ukitolewa katika maduka na migahawa maalumu kwa ajili ya askari wa majeshi, kutokana na msamaha huo kutumiwa vibaya na kupoteza mapato ya serikali na badala yake, askari watapata posho mpya juu ya posho ambazo wamekuwa wakipewa.

Wasiotumia EFDs Marufuku Kufanya Biashara na Serikali

$
0
0
KUANZIA Julai mosi mwaka huu, serikali imepiga marufuku kwa Wizara, Taasisi, Wakala za Serikali, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kufanya biashara na wazabuni na wafanyabiashara wengine ambao hawatumii mashine za kielektroniki - EFDs.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alisema hayo jana bungeni wakati akiwasilisha Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2017 bungeni mjini Dodoma jana.

Aidha, Dk Mpango aliwapongeza wafanyabiashara walioitikia matakwa ya Sheria ya Usimamizi wa Kodi ambayo inamtaka kila mfanyabiashara isipokuwa wale ambao wametangazwa rasmi na Kamishna wa Mamlaka ya Mapato kutotumia mashine za EFD kutoa risiti kila anapouza bidhaa au huduma.

Alisema ili kuwa na usimamizi mzuri wa fedha za serikali na kuhakikisha kwamba zinatumika kama ilivyokusudiwa, kwa mamlaka aliyopewa chini ya Sheria ya Fedha za Umma na kanuni zake, alitangaza kuwa malipo yote lazima yaambatanishwe na ankara za madai au stakabadhi (tax invoice) zilizotolewa na mashine za EFD.

“Kwa sababu hiyo kuanzia tarehe 1 Julai 2016, ni marufuku kwa Wizara, Taasisi, Wakala za Serikali, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kufanya biashara na wazabuni na wafanyabiashara wengine ambao hawatumii mashine za kielektroniki - EFDs.

The Ugly Truth: Wanaume Wote ni Malaya na Wasaliti - Dr. Mwaka

$
0
0
Mwanamke anaweza kuishi katika ndoa au mahusiano bila kucheat kwa asilimia 99 na wanaume wanaweza kuishi bila kucheat kwa asilimia 1 kwa sababu ni nature ya mwanaume kuwa hivyo.Kwahiyo ukiona mumeo au mpenzi wako hujamkamata inabidi umuheshimu saaana kwasababu anafanya kwa umakini na usiri wa hali ya juu ili asiumize hisia zako.wanaume wasiochet ni wale wagonjwa na makasisi wacha Mungu tu. Wengine wooote tupa kule.

Huu ndio ukweli mchungu kuhusu wanaume, Na ukweli unabaki palepale kuwa asilimia 99 ya wanaume wanatoka nje ya ndoa au mahusiano yao tena bila kuwa sababu ya msingi they just do haimaanishi kwa kufanya hivyo hawawapendi wake zao bali ni maumbile yao ndio yanawatuma hivyo. Kwahiyo kama umeolewa au una mpenzi ukimakamata na mwanamke mwingine usimhukumu kwa KUCHEAT bali mhukumu kwa KUCHEAT KIPUMBAVU mpaka akakamatwa wakati wenzake wanacheat na hawakamtwi.

najua kuna mikunguru minafiki itakuja hapa na kubisha ila ukweli ndio huo - By Dr JJ MWAKA

Hivi Wachumi Wetu Soda na Sigara Kuwa Chanzo cha Mapato ni Aibu Toka Tupate Uhuru 1961?

$
0
0
Ni aibu kwa wachumi wetu kuendelea kutegemea soda na sigara kama chanzo cha mapato toka nchi ipate Uhuru 1961.

Nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Kenya ilikwisha acha kutegemea chanzo hicho kwani kimeonekana ni kuwatesa wananchi wake.

Nilitegemea wachumi wetu wangefuta misamaha ya kodi inayotolewa kwa wawekezaji na wafanyabiashara wakubwa

Mitumba Inapozuiwa Bila Kuwa na Misingi ya Kujenga Viwanda

$
0
0
Hivi Unapozuia Mitumba Isiingie Nchini Wakati Huna Kiwanda Hata Kimoja Cha Kutengeneza Nguo Uko Sahihi Kweli? Wananchi Wa Vijijini Wamezoea Kuvaa Nguo Za Bei Nafuu Sh 1000 Wateweza Kweli Kushona Nguo Za Batiki? Nadhani Magufuli Angeanzisha Kwanza Viwanda Vya Nguo Ndipo Azuie Mitumba..

Download Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu yako Kutoka Play Store Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi

$
0
0

Download  Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu yako Kutoka Play Store Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi

Bonyeza Hapa CLICK HERE 

Au Bonyeza hii picha hapa chini

Mama Wema Sepetu Asema Kuna Wakati Anapigana na watu Kumtetea Wema

$
0
0
Mama yake Wema Sepetu, Mariam Sepetu amefunguka na kueleza jinsi anavyoumizwa na stori za uongo kuhusu mwanae ambazo zimekuwa zikiandikwa katika magazeti ya udaku.
wema

Akizungumza katika kipindi cha Clouds E cha Clouds TV Alhamisi hii, Bi Mariam amesema amekuwa akigombana mara kadhaa na baadhi na viongozi wa magazeti ya udaku kuhusu stori za uongo.

“Naumia sana kama mzazi, Wema alishaambiwa kwamba ana maradhi ya ngono, kama mzazi najisikia vibaya sana,” alisema Mama Wema. “Mimi nikishasikia hivyo nawafuata watu wa magazeti, nagombana nao sana. Kuna wakati nampigia Wema namuuliza jana ulitoka, anasema hajatoka, ukiwa kama mzazi inauma sana, wao wanauza magazeti kutokana na stori za uongo za mwanangu,”

Aliongeza, “Nimeshapigana na watu kuhusu Wema, wanakuja nyumbani wanaanza kuongea maneno maneno ambayo hayaeleweki,”

Naangalia Pesa Kabla Sijamkubali Mwanaume – Gigy Money

$
0
0
Msanii wa Bongo Fleva na video queen, Gigy Money amesema kuwa anaangalia pesa kabla hajamkubali mwanaume.

Akiongea na Times FM, Gigy Money alisema, “naangalia pesa kabla sijamkubali mwanaume, unajua kuwa na mtu maskini inaleta stress tu, napenda pia wanaume wazuri,” alisema.

Gigy ametokea kupata umaarufu kutokana na maisha yake controversial

Gardner: Jide Kitu Gani Bana!, Huyu Ndiye Mwendokasi Wangu Kwa Sasa

$
0
0

Miezi michache baada ya wanandoa Judith Wambura Mbibo ‘Jide’ na Gardner Gabriel Fikirini Habash kutalikiana kwenye Mahakama ya Mwanzo Manzese Sinza jijini Dar, mwanaume huyo amemuanika ‘mtu wake’ wa sasa a.ka. ‘mwendokasi’ akisema ndiye mrithi wa mikoba ya mwimbaji huyo nyota wa Muziki wa Kizazi Kipya.

Katika Viwanja vya Escape One, Kawe, jijini Dar es Salaam Jumamosi iliyopita, ambako mwimbaji mahiri wa Muziki wa Dansi Bongo, Christian Bella alikuwa akifanya shoo ya kutimiza miaka 10 katika ‘game’, Gardner alionekana na mrembo huyo akizunguka naye kimahaba kutoka eneo moja kwenda lingine huku wadau wake wakihoji ni nani!

Garder alipohojiwa na mwandishi wa habari hizi alikiri kuwa ni kweli kwa sasa anamiliki kifaa kipya kinachokwenda kwa jina la Vestina.

“Yes! Ndiye huyo kaka. Huyo ndiye mtu wangu kwa sasa na kama nilivyowahi kukudokeza, nimekuwa naye kwa muda mrefu kidogo, lakini sikuweza kumwanika mapema kwa sababu zinazoeleweka au ninazozijua mwenyewe,” alisema Gardner.

Mwandishi: “Vipi kuhusu Jide sasa, ndiyo n’tolee moja kwa moja kwa sababu ya talaka?”

Gardner: “Jide kitu gani bwana? Huyo ndo’ mwendokasi wangu kwa sasa.”

Gardner alimtaja binti huyo aliyekataa kusema umri wake kuwa anaitwa Vestina Jax, mkazi wa jijini Dar es Salaam.

Mwandishi wa habari hizi alilitaka kufahamu kama kuna mipango yoyote ya kufunga ndoa katika siku za karibuni baina yake na mrembo huyo, lakini Gardner alikataa kusema lolote juu ya hilo.

“Duu! Acha basi kaka! Kwa hilo sina comment,” alisema mtangazaji huyo ingawa habari za ndani zaidi zinasema kuwa, mrembo huyo ndiye mkewe mratajiwa.

Wabunge wa UKAWA, Bakini Bungeni Mlisaidie Taifa

$
0
0
Nawaomba kwa ujumla wenu. Najua hamuivi na Naibu Spika kwa mnavyomlalamikia. Najua kuwa mmeshatangaza kutoka kila Naibu Spika anapoliongoza Bunge na mmekuwa mkitoka kweli. Najua mna malalamiko yenye mashiko. Najua mnalilia ulinzi na ustawi wa demokrasia ndani na nje ya Bunge.

Kesho,mjadala wa Bajeti utaanza. Naamini,wakosoaji ndiyo wafuatiliaji na wasomaji. Wasomaji wa nyaraka kwa haraka na baraka Bungeni ni Wabunge wa Upinzani. Ni Wabunge wa UKAWA. Wabunge wa CCM hupumbazwa na uchama na wingi wao.

Msipokuwepo kesho na kuendelea,Wabunge wa CCM hawataijadili Bajeti. Wataisifu;kuisifu Serikali; kumsifu Rais na Naibu Spika na kuiunga mkono bajeti kwa asilimia mia. Bajeti itakosa kuchambuliwa na kukosolewa. Bajeti ni moyo wa nchi. Isipowekwa sawa,wote tutaumia. 

Tafadhalini,Wabunge wa UKAWA bakini Bungeni muifinyange bajeti ya nchi. Fanyeni hivyo kwa kulisaidia Taifa. Msijali yatakayosemwa kuhusu kubaki kwenu Bungeni!

Mzee Tupatupa-Kilaza wa Lumumba,Dar es Sal

Mahakama ya Rufani Yatengua Hukumu ya Mahakama Kuuu Dhidi ya Bosi wa Zamani wa TRA na Wenzake, Yaamuru Jalada Lirudi Mahakama Kuu Kwa Ajili ya Kusikilizwa

$
0
0
Mahakama ya Rufani Tanzania, imeamuru jalada la kesi inayomkabili Kamishna Mkuu wa zamani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya na wenzake kurudishwa Mahakama Kuu kwa ajili ya kusikilizwa rufani ya Jamhuri.

Pia, imeagiza jalada hilo lipangiwe kusikilizwa kwa jaji mwingine dhidi ya rufaa ya kupinga kuondolewa shtaka la utakatishaji fedha katika kesi ya kujipatia Dola za Marekani milioni 6.

Hukumu hiyo ilisomwa jana na Msajili wa Mahakakama ya Rufani, Zahra Maruma baada ya kusikilizwa na jopo la majaji watatu, likiongozwa na Mwenyekiti Salum Masati akisaidiana na Kipenka Musa na Augustine Mwarija.

Msajili Maruma alisema mahakama hiyo imeona kwamba Jaji Mfawidhi Moses Mzuna alikosea kukubali pingamizi la utetezi na kutupilia mbali kusikiliza rufani ya kupinga uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wa kuliondoa shtaka la kutakatisha fedha dhidi ya Kitilya na wenzake.

“Mahakama hii imebatilisha uamuzi uliotolewa na Jaji Mzuna na kwamba imeamuru jalada lirudishwe Mahakama Kuu kwa ajili ya kupangiwa jaji mwingine wa kusikiliza rufani ya upande wa Jamhuri kuhusu kuondolewa kwa shtaka hilo” alisema Msajili na kuongeza.

“Kwa kuondolewa shtaka hilo Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) hakuwa na namna ya kurudi Mahakama ya Kisutu kuomba kufanya mabadiliko ya hati ya mashtaka kwa sababu kila shtaka linajitegemea na kwamba shtaka la kutakatisha fedha lilishaondolewa na kumalizika katika hati hiyo ya mashtaka dhidi ya washtakiwa” alisema Msajili Maruma wakati akisoma hukumu hiyo.

Akifafanua zaidi alisema Mahakama ya Rufani imebatilisha uamuzi uliotolewa na Mahakama Kuu na kuamuru kusikilizwa rufani ya DPP kama ilivokuwa imekatwa.

Mapema Mei 31, mwaka huu upande wa Jamhuri ukiongozwa na DPP, Biswalo Mganga, Naibu DPP, Osward Tibabyekomya, Mawakili wa Serikali Waandamizi, Shadrack Kimaro na Awamu Mbagwa uliomba mahakama hiyo kuangalia uhalali wa kuondolewa shtaka la kutakatisha fedha pamoja na uamuzi wa Jaji Mzuna kutupilia mbali rufani yao.

“Watukufu Majaji ni rai yetu upande wa Jamhuri, tunaomba  mahakama hii iangalie upya na kuiamuru Mahakama Kuu kusikiliza rufaa ya kuliondoa shtaka la kutakatisha fedha …”alidai DPP Mganga.

Akiwasilisha hoja za rufaa hiyo mahakamani hapo, Tibabyekomya alidai kuwa malalamiko yao ni kwamba Jaji Mfawidhi, Mosses Mzuna alikosea kukataa kusikiliza rufaa ya kuondolewa kwa shtaka hilo na mahakama ya chini.

Alidai kuwa kinachashtakiwa katika shtaka ni kosa ambalo limekamilika na kwamba linasisimama kwa kujitegemea.

“Watukufu majaji kitendo cha kufuta kabisa shtaka la nane la kutakatisha fedha dhidi ya washtakiwa kulihitimisha shtaka hilo kama lilivyokua limeshtakiwa  kwa kuwa lilikuwa linajitegema”alidai na kuongeza kuwa.

“Jaji Mzuna alikataa kwamba mahakama yake haina uwezo wa kuruhusu kufanya mabadiliko ya hati ya mashtaka na kwamba uamuzi huo ulionyesha haiwezekani kufanyika mabadiliko amri ambayo inahitimisha shtaka la nane” alidai msaidizi huyo wa DPP.

Mawakili wa utetezi wakijibu hoja za Jamhuri kwa nyakati tofauti; Wakili Majura Magafu alidai kuwa rufaa hiyo haina mashiko ya kisheria na kwamba ilifunguliwa mapema kinyume cha sheria mahakama hiyo itupilie mbali.

“Hakimu Mchauru hakukosea kama inavyodaiwa na Jamhuri kwa sababu alitoa nafasi kwamba wakati utakapofika kisheria wataruhusiwa kufanya mabadiliko… “alidai Magafu.

Dk. Ringo Tenga alidai kuwa baada ya kuondolewa shtaka hilo, upande wa Jamhuri haukuwasilisha maombi ya kufanya mabadiliko ya hati ya mashtaka.

Alex Mgongolwa alidai kuwa hoja zao za utetezi kwamba rufaa hiyo haina sababu za kutosholeza kisheria imefunguliwa kinyume cha sheria mahakama ifutilie mbali.

Mbali na Kitilya, washtakiwa wengine ni, aliyekuwa Miss Tanzania mwaka 1996, Shose Sinare na mwanasheria wa benki ya Stanbic Tanzania, Sioi Solomon

Mwanza, Kagera, Kigoma Zaongoza kwa Umasikini wa Kipato

$
0
0
PAMOJA na maendeleo yaliyotokana na kukua kwa pato la wastani la Mtanzania na kupungua kwa umasikini wa mahitaji ya msingi, serikali imeainisha mikoa mitano iliyokithiri kwa umasikini wa kipato.

Akiwasilisha bungeni Taarifa ya Hali ya Uchumi ya 2015 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa 2016/17, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alisema mkoa unaoongoza ni Kigoma ambao wakazi wake asilimia 48.9, wanakabiliwa na umasikini uliokithiri wa kipato.

Mikoa mingine yenye umasikini wa kipato kiwango chake katika mabano ni Geita (asilimia 43), Kagera (asilimia 39), Singida (asilimia 38.2) na Mwanza (asilimia 35.3).

Katika wilaya zilizokithiri kwa umasikini wa kipato, ni Kakonko mkoani Kigoma na Biharamulo mkoani Kagera, ambapo Dk Mpango alisema katika wilaya hizo, takribani asilimia 60 ya watu wake, wako chini ya mstari wa umasikini wa mahitaji ya msingi.

Tathmini ya hali ya umasikini kimaendeleo iliyoainisha umasikini huo, imetumia takwimu za Sensa ya Watu ya mwaka 2012 na Utafiti wa Hali ya Kipato na Matumizi katika Kaya wa 2012, ulionesha pia ahueni ya umasikini katika mikoa mitano.

Dk Mpango alitaja mikoa hiyo yenye ahueni na idadi ya watu wanaokabiliwa na umasikini wa kipato katika mabano kuwa ni Dar es Salaam (asilimia 5.2), Kilimanjaro (asilimia 14.3), Arusha (asilimia 14.7), Pwani (asilimia 14.7) na Manyara (asilimia 18.3).

Pamoja na tathmini ya kimkoa na kiwilaya lakini katika nchi nzima, alisema kati ya mwaka 2010 na 2015, Pato la Mtanzania liliongezeka kutoka Sh 770,464.3 kwa mwaka mpaka Sh milioni 1.9 mwaka 2015 sawa na mara 2.5.

Aidha kupungua kwa umasikini nako kulikuwa kasi katika kiwango cha asilimia 6.2 ndani ya miaka mitano tu kati ya mwaka 2007 na 2012, ikilinganishwa na kupungua kwa umasikini kwa asilimia 4.6 tu katika miaka 15 kulikotokea mwaka 1992 mpaka 2007.

Kuhusu ajira, Dk Mpango alisema Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi wa mwaka 2014 ulionesha kuwa nguvukazi ya Taifa ilikuwa watu 25,750,116 sawa na asilimia 57 ya watu wote wa Tanzania Bara.

Kati ya nguvu kazi hiyo, wanawake wametajwa kuwa 13,390,678 sawa na asilimia 52 na wanaume ni 12, 359, 438 sawa na asilimia 48.

Pamoja na nguvukazi kuwa watu milioni 25.8, utafiti huo kwa mujibu wa Dk Mpango, ulionesha kuwa watu wenye uwezo wa kufanya kazi walikuwa watu milioni 22.3 tu na sababu za watu kushindwa kufanya kazi zilikuwa ni ulemavu na ugonjwa wa muda mrefu.

Aidha, kati ya nguvu kazi ya taifa; watu milioni 25.8, utafiti huo umeonesha kuwa asilimia 77.8 ndio walikuwa katika ajira, wengi wakiwa wa vijijini sawa na asilimia 82.2 ikilinganishwa na mijini ambapo Dar es Salaam waliokuwa wakifanya kazi ni asilimia 59.8 tu.

Mafanikio ya kupungua kwa umasikini, yameonekana pia katika kuongezeka kwa umri wa kuishi wa Mtanzania kutoka miaka 51 ilivyokuwa mwaka 2001 mpaka miaka 61 kwa takwimu za mwaka 2012.

Vifo vya watoto wachanga chini ya mwaka mmoja, pia vimepungua kufikia 43 kwa kila watoto hai 1,000 mwaka 2015 kutoka vifo vya watoto 51 kwa kila watoto hai 1,000 mwaka 2010.

Kuhusu watoto wa chini ya miaka mitano, pia vifo vyao vimepungua kutoka vifo vya watoto 81 kwa kila watoto hai 1,000 mwaka 2010 mpaka vifo vya watoto 67 kwa kila watoto hai 1,000 mwaka 2015.

Mafanikio hayo ya kupungua kwa vifo na kuongezeka kwa umri wa kuishi wa Mtanzania, katika upande mwingine yameleta changamoto kutokana na kuongezeka kwa wasichana waliopata ujauzito utotoni.

Kwa mujibu wa Dk Mpango, idadi ya wasichana wanaopata mimba katika umri wa miaka 15 hadi 19 imeongezeka na kufikia asilimia 27 mwaka 2015, kutoka asilimia 23 mwaka 2010.

Dk Mpango alisema hali hiyo si dalili nzuri kwani kunaashiria kuongezeka kwa utegemezi na kudumaza jitihada za kuondoa umasikini katika jamii na kuwataka wabunge kushirikiana na Serikali kuhimiza watoto wa kike, kuongeza bidii katika masomo ili kwa pamoja kupatikane manufaa kutokana na mapambano ya umasikini
Viewing all 104689 articles
Browse latest View live


Latest Images