Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104702 articles
Browse latest View live

Baada ya FA Kupata Jiko… AY Naye Mbioni Kufunga Ndoa

$
0
0
KUFUATIA staa wa Muziki wa Bongo Fleva, Hamis Mwinjuma ‘MwanaFA’ kufunga ndoa na mpenzi wake wa siku nyingi, Helga wiki iliyopita, swahiba wake mkubwa, Ambwene Yessaya ‘AY’ amefunguka kuwa naye yuko njiani. Akizungumza na mtandao huu, AY anayebamba na Ngoma ya Zigo alisema kuwa ni jambo jema kwa rafiki na ndugu yake wa karibu (MwanaFA) kufunga ndoa hivyo imempa hamasa.

“Nimefurahi sana kwa swahiba wangu kufunga ndoa. Naamini FA amefungua ukurasa mpya katika maisha yake ya kuwa na mwenzake. Nami nipo njiani kumfuata Mungu akipenda,” alisema AY bila kumuweka wazi mwandani wake anayetarajia kufunga naye ndoa.

Umuhimu wa Kuhonga Katika Mapenzi...

$
0
0

1. KUHONGA HUBORESHA MAPENZI:

Fahamu kuwa unapomhonga mpenzi wako unamfanya ajihisi kama ni wapekee kwako, atajiona kama ni mmoja wapo kati ya watu wenye thamani kwako na huamini kama kweli upo karibu yake na unamjali.

Hali hii humfanya yeye kushindwa kutolipa mazuri kwako.
Wengi kabla ya kuomba papuchi hutanguliza hongo kwanza, si lazima iwe pesa hata hongo ya sifa za uongo na ukweli.

Kwa kuhonga kwako inamlazimu na yeye kulipa fadhila kwa kuonesha upendo wa dhati na utamfanya azidishe mapenzi kwako.

2. KUHONGA KUNAJENGA SANA KUMBUKUMBU KATIKA MAPENZI:

Fahamu kuwa unapomhonga mpenzi wako inakusaidia wewe kujijenga katika mawazo yake na endapo kama itatokea mkaachana nae basi pindi mpenzi wako atakapokuwa anaziona zawadi zako zitamfanya akukumbuke kwa mengi na atahisi kama kuachana na wewe kwake kuna tofauti na atajihisi kupoteza vingi toka kwako na kamwe kumbukumbu yako kwake haitofutika kila anapoona vitu ulivyomhonga.

Jitahidi sana unapohonga usihonge pesa tu, honga vitu vya kudumu maana huwa asset yako ya baadaye, pindi unapotokea mkwaruzano baina yenu.

Pesa huwa ni hongo inayovutia kwa muda mfupi na husaidia kupata kile unachokitaka kwa muda mfupi, ila jua atazitumia zitaisha utakuwa hujajenga misingi imara ya mapenzi.

Simaanishi kuwa usimpe mpenzi wako hela, hapana ila inabidi ufahamu kuwa pesa hutumika katika kukidhi mahitaji na sio katika kuboresha mapenzi.

Aisee jifunzeni kuhonga mpunguze stress za mapenzi.

Mbunge wa Kawe, Halima Mdee Ataja Rapper wa Kibongo Anayemkubali zaidi Bongo

$
0
0
Mbunge wa Kawe, Halima Mdee amesema Rapper wa kibongo anayemkubali zaidi ni Roma Mkatoliki kwasababu anaimba hali halisi, anatumia sanaa kuburudisha na kuelimisha kwa wakati mmoja.

Je, wewe ni rapper gani wa bongo unamkubali?

VIDEO:Young D Akwidwa, Atiwa Mbaroni..Kisa Kizima Hichi Hapa..

$
0
0
Kimemnukia! Mbongo Fleva, David Genzi ‘Young D’ amejikuta mikononi mwa askari wa Kituo cha Polisi Urafiki, Ubungo jijini Dar madai yakiwa kuharibu simu na kushambulia mwili, Amani lina kila kitu.

Ilidaiwa kuwa, katika siku za karibuni, msanii huyo alimshambulia mrembo aliyejulikana kwa jina moja la Nasra lakini pia aliharibu simu yake yenye thamani ya shilingi 600,000.
Juni 6, mwaka huu, yaani Jumatatu iliyopita, Young D akiwa nyumbani kwake, Sinza Mori jijini hapa, aligongewa mlango na kutakiwa kutoka.

“Lakini alipotoka na kugundua ni askari na wanamtaka waende naye kituoni, alileta ujeuri kidogo, ikabidi wamkwide na kumuweka chini ya ulinzi mpaka kituoni.
“Mbaya zaidi, alikuwa hajavaa shati ni suruali tu, ikabidi aende polisi hivyohivyo. Unajua hawa wasanii wetu bwana sijui huwa wanawaza kitu gani katika ustaa wao,” kilisema chanzo kimoja kilichoshuhudia dogo huyo akiwekwa mtu kati na askari hao.


Habari zaidi zinasema kuwa, Nasra na Young D ni wapangaji wa nyumba moja lakini hawana uhusiano mzuri kwani mara kwa mara wamekuwa wakikwaruzana kwa sababu ambazo hazijulikani kirahisi.

“Siku ya tukio, inasadikiwa kuwa walikwaruzana sana, ndipo dogo (Young D) akaamua kumvaa mwanadada huyo na kumpa vitasa (ngumi) kisha kuivunja simu yake,” kiliongeza chanzo.

Katika Wabongo Fleva wanaotamba, Young D naye yumo ambapo amepata jina kupitia vibao vyake viwili, Ujanjaujanja na Kijukuu.

Askari mmoja wa Kituo cha Urafiki ambaye aliomba asiandikwe jina kwa sababu si msemaji, alipoulizwa na Amani kuhusu hatima ya mwimbaji huyo alisema: “Upelelezi unaendelea, ukikamilika atapelekwa mahakamani.”

Diamond Amuandalia Mwanaye Tiffah Birthday ya Kukata na Shoka itakayofanyika Mlimani City

$
0
0
Mwanamuziki Diamond amethibitisha habari kuwa amemuandalia mwanaye Tiffeh Birthday kubwa ya kukata na shoka, itakayofanyika mlimani City. 

Tiffah mwenye umri wa miezi 10, kwa sasa ana followers zaidi ya 623,049 Instagram, na inadaiwa kuwa ndiye superstar mdogo zaidi kwa Africa.

“Happy 10th Months my little Angel… can’t wait for your first year’s Birthday!!!!! Pale mlimani City patakuwa kama Disney Land!!!! @princess_tiffah,” ameandika Diamond kwenye Instagram.

Naye mama yake alimpongeza kwa kuandika: Yesterday you were mummy’s tiny baby and today you are mummy’s big girl. Happy 10 my beautiful princess the apple of my eye, the air I breathe. Plse don’t grow so fast, mummy will miss you being her baby.”

Staa wa Kenya, Huddah ni miongoni mwa mastaa walio na hamu kubwa ya kuwepo kwenye birthday hiyo.

“Our baby @princess_tiffah Turning ONE soon…. The ROYAL DUTCHESS of TZEE . Hii Sio party ya kikosa Jamani . There will be a BIG SURPRISE that day! Asiye na wake aeleke jiwe….Mimi I’ll be there na mawe zangu khaa! Mama Tiffa @zarithebosslady give us LOCATION Basi …. We need to book tickets EARLY,” aliandika.

Picha: Raymond wa ‘WCB’ Aringishia Mabunda ya Hela Instagram

$
0
0
Wakati mtaani raia wakilalamika kuhusu ukata wa hela toka Rais Magufuli aingie madarakani, mkali wa wimbo ‘Kwetu’ kutoka WCB, Raymond ‘Rayvanny’ ameamua kuringisha mabunda ya hela kupitia ukurasa wake wa instagram.

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Natafuta kiki’ amepost picha kupitia instagram yake na kuandika jina la wimbo wake huyo, huku mashabiki wakitoa maoni yao juu ya wingi pesa hizo.

Raymond alisaini ‘WCB’ mapema mwaka huu kabla ya hapo alikuwa anafanya kazi Tip Top Connection huku akiwa karibu zaidi na Madee.

Haya ni maoni ya mashabiki hao.

Tajibetese
Mmmmh @rayvannyy kama unatupenda fans wako hii ndo number yangu 0768046197 hata alfu kumi tuisogeze ramadhan

Blackgal_ake_dede
Hiyo kiki ndio yenyewe sio ya mademu fanya kunigawia basi ndugu @rayvanny

Am_coco_
That’s why I love you 😁,… Harmo abaki tu kwa mchaga, mi mpare nakutaka wewe .

Celinn1988
Watu wanavyojua kupangia watu kweny hela zao, mtadhani zenu mmefanyia kitu cha maana au mnaropoka tuu hapa.

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya June 10

$
0
0



SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya June 10

VIDEO:Jionee Wizi Mpya wa Mpesa na Tigo pesa, Jamaa Kaibiwa Sh 720,000

$
0
0
Utapeli umekua mwingi sana hapa mjini, watu wengi wanatapeliwa kila siku. Kutapeliwa ni kutapeliwa tu haijalishi ujanja utakaotumika ni wa sasa au wa zamani. Ila siku za karibuni kumetokea aina mpya ya utapeli ambao wahathirika wakubwa ni watu wanaotoa huduma za Mpesa na Tigo Pesa.

Kama utakavyoona katika video hii ni ngumu sana kugundua kama umeshatapeliwa mpaka baada ya mdaya mda upite. Kwa mfano huyu jamaa aliyetapeliwa hapa kaibiwa 723,000 na matapeli hao. Hebu tazama video hii na wewe usije ukaibiwa kama huyu.


Shamsa: Napenda Sana ‘Chupi’ za Mtumba....

$
0
0
Licha ya baadhi ya mastaa kudai wanavaa nguo spesheli tu, tena zile zilizofungwa kwenye nailoni, staa wa filamu Bongo Shamsa Ford amefunguka kuwa, yeye huwa anapendelea kuvaa nguo za mitumba zikiwemo nguo za ndani ‘makufuli’.

shamsaAkizungumzia nguo anazopenda kuvaa, mdada huyo ambaye ni mama wa mtoto mmoja aitwaye Terry alisema, kuna mtu huwa anampelekea nguo ‘classic’ za mitumba na anachagua zile zinazomfaa, ananunua na kuzivaa.

“Niseme tu ukweli kwamba, napenda sana nguo za mtumba, hata makufuli. Huwa nanunua, nazifua na kuziweka ‘sopusopu’ kisha navaa, sioni shida katika hilo,” alisema Shamsa.

Serikali iliwahi kupiga marufuku uuzwaji wa nguo za mitumba za ndani kama vile makufuli, brazia na soksi lakini bado nguo hizo zimekuwa ni kimbilio kwa watu wengi wakidai zina ubora na ni za kijanja zaidi.

GPL

TGNP Walaumu Milioni 50 za Magufuli Kuwa Mkopo Kwa Vijiji

$
0
0
Wanaharakati wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) wameikosoa bajeti ya mwaka 2016/17 kutokana na kuzifanya Sh50 milioni zilizoahidiwa na Rais John Magufuli kwa kila kijiji, kuwa za mkopo badala ya kutolewa kama ruzuku.

Katika tamko lao, wanaharakati hao walisema Serikali itafute vyanzo vingine vya mapato ili iweze kutoa ruzuku kwa vikundi vya wanawake kwani walio wengi tayari wana mikopo wliyopewa na taasisi za fedha na hivyo wana mzigo wa madeni.

Akisoma tamko hilo, Janeth Mawinza alisema wanawake wana madeni mengi ambayo wameshindwa kulipa kwa sababu ya kukosa elimu ya kufanya biashara.

 “Tuwape unafuu sasa kwa kuwapa ruzuku, vinginevyo tutawasababishia msongo wa mawazo kwa kudaiwa na taasisi mbalimbali za fedha,” alisema. 

Alisema mpango huo wa mikopo bila kuwapa elimu ya biashara unaweza kusababisha vifo kwa baadhi yao.

“Tumeshuhudia wanawake wananyang’anywa samani zao na kusababisha msongo wa mawazo kwa sababu ya kukosa elimu ya biashara, tutawaua,” alisema.

Master Jay: Tulikuwa Wapenzi Miaka 10 Bila Kujulikana

$
0
0
Akizungumza na MTANZANIA hivi karibuni, Master Jay alisema walikuwa katika mapenzi ya siri kwa muda wote huo hadi walipoamua kuweka wazi hivi karibuni baada ya watu kuhisi uhusiano wao.

“Nilimpenda Shaa kwa sababu ni msichana anayejielewa pamoja na kazi zake anazozifanya ni nzuri, hata hivyo tumeendana katika mapenzi yetu,’’ alielezea.

Mtayarishaji huyo ana watoto watatu kwa mke wake na hawana mtoto na Shaa.


Serikali ya Tanzania ijibu tuhuma nzito za serikali ya Kenya, rais Magufuli asaidiwe kidiplomasia

$
0
0
Serikali ya Tanzania sasa itoke hadharani kujibu Tuhuma za Serikali ya Kenya na viongozi wa Muungano wa JUBILEE kuwa Rais Magufuli anamdhamini kifedha Kiongozi wa Upinzani Raila Amolo Odinga kusababisha Maandamano, ghasia na hatimaye kuipindua serikali ya Rais Uhuru Kenyatta.

Siku Chache Zilizopita Msemaji wa Serikali ya Kenya Erick Kiraithe alisema kuwa tayari kuna taarifa za kijasusi kuwa kuna wanasiasa nchini Kenya wanadhaminiwa na kusaidiwa na Nchi Mbili Jirani maadui wa Kenya kutaka kuvuruga amani na kuiangusha Serikali na kudai kuwa Baraza la Ushauri la Usalama (National Security Advisory Council) lilikutana siku ya Jumatatu kuangalia namna ya kuwashughulikia watu hao

Mbunge wa Jimbo la Starehe Mwenye ushawishi ndani ya Serikali ya JUBILEE akiambatana na wabunge wengine alifanya mkutano na waandishi wa Habari Nairobi Hoteli na Kuwataja marais John Magufuli wa Tanzania na Salva Kiir wa Sudan ya Kusini

Rais Magufuli akiwa mapumzikoni CHATO msimu wa Sikukuu ya Pasaka alikua Mwenyeji wa Raila Odinga anayejiandaa na Uchaguzi nchini Kenya mwaka 2017

Pia Mwezi Desemba nilialikwa na Mwenyekiti wa Vijana wa ODM wakati huo Rashid Mohammed n kwenye mkutano mkuu wa chama cha ODM kumteua Mgombea Urais 2012 nchini Kenya.Mhe.Magufuli pia alikuwepo. Nilimshuhudia Mhe.Magufuli akiwa waziri wakati huo akidai amehudhuria mkutano ule na kutangaza kuwa Raila Odinga ni Rafiki yake na amekuja kumuunga Mkono.Aliendelea kushtua watu Ukumbini akidai kwamba wagombea wengine wanaotarajia kuchuana na Raila Odinga hawawezi kusafiri hata nje ya nchi.Kipindi Hicho Uhuru Kenyatta na Willium Ruto walikuwa wanakabiliwa na mashtaka mahakama ya kimataifa ya ICC.

Mhe.Magufuli akaendelea kusema hata Odinga angegombea jimbo la Chato yeye Magufuli asingethubutu kugombea maana asingeweza kumshinda

Urafiki binafsi wa Raila Odinga na Rais Magufuli sio tatizo jwani hata Mwalimu Nyerere alikua na urafiki na akina Thom Mboya,Jaramogi Oginga Odinga ila tatizo ni pale ambapo Mhe.Magufuli anaposhindwa kuwa senstive kisiasa na Kidiplomasia.Mbaya zaidi tuhuma zinatolewa na serikali ya nchi jirani tena mwanachama ndani ya jumuiya ya Afrika Mashariki kuwa Rais Magufuli anatumia Raslimali za nchi kumfadhili Mpinzani wa nchi jirani kwa lengo la kupindua serikali kwa sababu ya urafiki wao tu

Nikumbushie tu kitendo alichofanya Mhe.Magufuli kipindi kile nilisema na niliandika kuwa kitakuja kuleta matatizo ya kidiplomasia siku za usoni ikiwa ODM wangeshindwa kwani tayari kupitia Udhaifu alioonyesha waziri wa serikali ya Tanzania Mhe.Magufuli wakati Ule walishaaminisha Umma kuwa serikali ya Tanzania inawaunga Mkono.Kosa hili la Kidiplomasia ameendelea kulirudia.

Rais Jakaya Kikwete alikuwa Rafiki wa Kalonzo Musyoka lakini Uhusiano wao haujawahi kuibua mgogoro wa kidiplomasia na au kutoaminiana baina ya serikali hizi mbili

Tuhuma hizi ni nzito na zinazochochea mgawanyiko ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki

Kitendo cha Serikali ya Tanzania kukaa kimya hadi muda huu maana yake kinatoa Silent Consent kuwa nu kweli hasa msemaji wa Serikali anaposema kwa ujasiri kuwa serikali yao ina taarifa rasmi

Mwaka 2013 kulikua na mgogoro wa kidiplomasia uliotishia kuipasua Jumuiya ya Afrika Mashariki .Kenya,Uganda na Rwanda ziliunda Muungano wao wa hiyari (Coalition of The Willing-CoW).Jitihada kubwa za kidiplomasia zilifanyika

Sasa muda huu Rais Magufuli ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Africa Mashariki na Tanzania kama Mwenyekiti hatupaswi kuwa chanzo cha migogoro ndani ya jumuiya kwani sisi ndio tunaopaswa kuonyesha uongozi katika Diplomasia kuhakikisha Malengo ya Mtangamano(Intergration) yanafikiwa.

Jitihada zozote za Serikali ya Tanzania na wapambe wake kutumia propaganda pengine kwa kuibua hoja ya Bomba la mafuta Kutoka Uganda na Kupita Tanzania badala ya Kenya na Suala la Reli ya Rwanda kwamba ndio limesababisha wivu itakua ni uamuzi mbaya kidiplomasia

Serikali ya Tanzania ijibu tuhuma hizi kama si kweli basi Serikali ya Kenya iombe Radhi

Kenya na Tanzania zinahitajiana kipindi hiki kuliko wakati mwingine wowote kiuchumi

Katika tathmini iliyotolewa bungeni jana,biashara ya Kenya na Tanzania imechangia sana katika ukuaji wa uchumi wa nchi hizi

Mawaziri wa Mambo ya Nje ambao ni wanadiplomasia Maahiri Dr.Augustine Mahiga wa Tanzania na Amina Mohammed Jibril wa Kenya wasaidie kunusuru hali hii ambayo inahatarisha Uhusiano wa Kidiplomasia baina ya Nchi hizi Mbili

Na Pia Rais Magufuli asaidiwe ili apate uzoefu wa Kidiplomasia katika maneno na matendo yake.

Kwa mfano kitendo cha kuongea na Rais Kenyatta mwezi March walipokutana Arusha na kuahidi kusaidiana kuondoa vikwazo vya kibiashara baina ya nchi hizi mbili na kisha mwezi mmoja baadae kumwalika Raila Odinga akiwa Mapumzikoni(Inaweza kutafsiriwa alichukua likizo ili akutane na Odinga isionekane amekutana nae ikulu) hakikutoa gesture nzuri kidiplomasia

Wakati Rais Magufuli anahutubia mkutano wa mfuko wa Wafanyabiashara Mwezi Desemba 2015 aliitaja kampuni ya Broakside Dairy Limited kuwa ilikua ikifanya biashara kiadui na kinyume na misingi ya Biashara nchini.Kampuni hiyo ilimilikiwa na familia ya Rais Uhuru Kenyatta.Kidiplomasia Rais hakupaswa kutamka na kuitaja kamapuni ile bali angeweza kukwepa na kutumia namna nyingine au mtu mwingine kama ilikua ni lazima itamkwe.Siitetei kampuni ile isipokua ni udhaifu mkubwa wa kidiplomasia aliouonyesha Rais ingawa anaweza kujitetea kuwa alikua anasimamia Sheria.Diplomasia ni namna ya kumwambia mtu kafie mbali na yeye akakuuliza mbali kiasi gani badala ya kukukasirikia.Rais anapaswa ajifunze hili

Sasa hizi tuhuma za serikali ya Kenya na viongozi waandamizi zijibiwe na kama si kweli serikali ya Kenya Iombe Radhi.

Kama ni kweli inawezenaje Wanachi wa Tanzania wakose Sukari halafu Rais afadhali shughuli kama hizo nchi jirani?Na iweje sasa Serikali yake izuie mikutano ya kisiasa nchini?

Aluta Continua,Victory Ascerta......

Ben Saanane

Vijana, Wadau Kumchangia aliyemtukana Rais Magufuli

$
0
0
Vijana, wadau na wanaharakati wamefungua vikundi vya mtandao wa kijamii kwa ajili ya kuchanga fedha za kumsaidia kijana wa Arusha aliyepatikana na hatia ya kumtukana Rais na kuhukumiwa faini ya Sh7 milioni au kifungo.

Kijana huyo, Isaack Habakuki wa Arusha alipatikana na hatia ya kumtukana Rais kwa kutumia ukurasa wake wa facebook na ametakiwa kulipa fedha hizo kwa awamu mbili na kuzikamilisha ifikapo Julai 7 au kwenda jela miaka mitatu.

Diwani wa Kata ya Levolosi jijini Arusha (Chadema), Ephata Nanyaro ambaye anaratibu michango hiyo kwa mkoa wa Arusha, alisema mpaka sasa wameshakusanya Sh 800,000/- ambazo walizipata kwa njia ya kutuma kwa simu.

Alisema wanatarajia kupata Sh1.7 milioni kutoka mikoa yote.

"Tumesikia familia yake imeweza kutoa 3.5 millioni pekee, sisi tumejitolea kumsaidia ili afikishe 7 millioni kabla ya tarehe 7 mwezi julai,” alisema.

Mimi Sijaumbwa kwa Ajili ya Kuchezea Wanawake – Harmonize

$
0
0
Mkali wa wimbo ‘Bado’ kutoka WCB, Harmonize amesema hana tabia ya kuchezea wanawake hivyo kama wakikubaliana na mpenzi wake wa sasa Jacqueline Wolper watafunga ndoa.
Wolper

Muimbaji huyo ambaye ametoka katika familia ya dini ya kiislamu, ameiambia Bongo5 kuwa dini yake hamruhusu kuwachezea watoto wa kike.

“Kwa sasa kuweka wazi kama tunakaa pamoja au hatukia siyo kitu kizuri cha kuzungumzia kwa sasa,” alisema Harmonize. “Insha’Allah panapo majaliwa tutakaa pamoja kwa sababu mimi sijaumbwa kwa ajili ya kuchezea wanawake,”

Aliongeza, “Nikiwa na mwanamke tunaandaa future, tunakubaliana tukae pamoja, kwa nini tusikae pamoja wakati dini yangu hainkruhusu,”

Harmonize amewataka mashabiki wa muziki wake kutulia kwani kuna mambo mazuri yanakuja.

UKAWA Wamjibu Naibu Spika.....Wamwambia Posho Akawatishie Watoto

$
0
0
Siku mbili baada ya Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson kuagiza wabunge wa upinzani wanaoingia Bungeni na kisha kuondoka wakisusa vikao wasilipwe posho, wabunge hao wamejibu wakiubeza na kuupinga uamuzi huo.

Wakiongea kwa nyakati tofauti, wabunge wa upinzani wamekosoa uamuzi huo wakieleza kuwa Dk. Tulia alihukumu kesi inayomhusu, kitendo walichosema sio haki.

Aidha, wabunge hao walieleza kuwa posho haitakuwa sababu ya kuwarudisha nyuma kwenye uamuzi wao kwakuwa sio hoja wanayoipigania. Walisisitiza kuwa wataendelea kutoshiriki vikao vya Bunge vinavyoongozwa na Dk. Tulia kama walivyoazimia.

“Ukawa haiwezi kutishiwa posho tunapokuwa na hoja na mawazo ya msingi. Hoja yetu hapa si posho, kuna mambo ambayo anayafanya Naibu Spika hayaendi sawa na sio ya kawaida. Hoja ya posho akawatishie watoto, sisi ni watu wazima. Tumekuja hapa tuna utashi mkubwa,” alisema Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara (Chadema).

Naye Mbunge wa Vunjo na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia alisema kuwa uamuzi wa Naibu Spika unawadhalilisha wabunge kwa kuonesha kuwa posho ndio kitu walichokifuata Bungeni hapo.

“Mimi nimekuwa kwenye siasa kwa miaka zaidi ya 25 sasa. Kilichofanywa na Naibu Spika ni kudhalilisha wabunge, ionekane sasa tupo hapa kwa ajili ya kulipwa posho. Tupo hapa kwa ajili ya kutoa huduma kwa Watanzania. Kina Tulia wakiwa shule ya msingi, sisi tunapambana bila kulipwa posho na mtu yoyote,” alisema Mbatia.

Kiongozi wa Kambi rasmi ya upinzani Bungeni, Freeman Mbowe alitoa msimamo wa kambi hiyo kuwa hawatashiriki vikao vyote vya Bunge vinavyoongozwa na Naibu Spika kwakuwa amekuwa wakiwakandamiza na kupendelea upande mmoja. Pia, Mbowe alisema kuwa Dk. Tulia anaongoza Bunge kwa ubabe akilinda maslahi ya Serikali.

Kijana Shoga au Punga Maarufu Dar Apania Kumpokonya Jux kwa Vanessa Mdee

$
0
0
Vanessa Mdee ana ushindani mkali katika himaya yake ya mapenzi na Jux. Ushindani huo si kutoka kwa msichana mwenzake, bali kutoka kwa shoga maarufu Instagram, James Delicious.

Punga huyo amepania kumpokonya Vee Money tonge mdomoni. Pamoja na kuambulia mvua ya matusi kutoka kwa watanzania wanaokerwa na tabia yake hiyo, James haoneshi kujali.

“MI MWENZENUUU.. NATABIA MOJAA.. NIKIMPENDA MTU LAZMAA NIMPATEEE. SO WALA MSIHANGAIKEE. KUNIHUKUMUUU… ET DHAMBI. DHAMBI MMEONA HIII TUU EEH.. VEEPE WALE WANAO DHIN. ???? VEEPE WALE WANAO UWAA??? VEEPE WALE WANAO BAKAA??? VEEPE WALEE WANAO SAGANA?? VEEPE WALEE WANAO SALIT NDOA ZAO??? VEEPE WALE WANAO LOGAA..??? VEEPE WALE WANO JIUZAA..????,” ameandika kwenye picha aliyoiunganisha na ya JUX.

“ZAMBI ZIPO NYINGI SAANA.. SO WALA MSIZANII KAMA HAYO MANNENO YEEENU. YANAWEZA KUNIVUNJA. MOYO. YA SARI YANGU NNAYOIANZA. YA KUMUWEKAA KWENYE HIMAYA YANGU. HUYU NINAE MTAKAA.. NAMPEEENDA MPAKA NAJIIHIS KIZUNGU ZUNGUUUU…😂😂😂😂😂😂.. TUKANA N KUBLOCK…🔐🔐🔐🔏🔏🔏🔏🔏🔏.. NGOJA RAMADHAN IISHE,” ameongeza.

Young Dee Anatafunwa na Kauli ya Meneja Wake wa Zamani Max Rioba..."Utastuka When it’s Very Late"

$
0
0
Asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu. Huu ni msemo ambao naanza nao siku ya leo kutokana mwenendo mbaya wa maisha ya msanii mahiri Hip Hop, David Genzi aka ‘Young Dee’.

Wiki hii kumekuwa na picha pamoja na video ambazo zinasambaa katika mitandao ya kijamii zikimuonyesha Young Dee ‘Rapper Paka’ akivutana na watu wanaodaiwa kuwa ni polisi na baadaye kutiwa mbaroni kwa madai ya kumshambulia jirani yake wa kike maeneo ya Sinza anakoishi na kisha kumvunjia simu yake ya mkononi.

Tukio hili limeibua mjadala mkubwa katika mitandao ya kijamii huku mashabiki wa muziki wake wakishangazwa na style ya maisha ya Young Dee ikiwa miezi michache toka agombane na kuachana na meneja wake, Max Rioba.

Tusiingie ndani sana kuzungumzia ugomvi wake na meneja wake huyo ambaye alishirikiana naye kutengeneza hits kadhaa ambazo bado zinampatia jeuri ya kuishi mjini. Lakini kauli ambayo aliitoa meneja wake wakati wanaachana “Kama usiposhtuka sasa hivi na kugundua kuwa huna hata chumba cha kupanga au hata begi la nguo halafu unajiita msanii wa muziki utastuka when it’s very late. Washkaji zako wote ni wahuni, bangi, cocaine, pombe na mademu wasiojua hata kuandika aeiou. Hayo sio maisha!. Hii ni kauli ambayo inaendelea kumtafuna Young Dee.

Kwa muda mrefu amekuwa akihusishwa na Matumizi ya Madawa ya kulevya japokuwa amekuwa akitumia nguvu kubwa kulikanusha suala hilo mpaka kuamua kuandika wimbo ‘Fununu’ ambao ndani yake aliendelea kuuthibishia umma kwamba hatumii madawa ya kulevya. Lakini matendo na mwonekano wake bado vinawapa watu sababu za kumshuku kwamba anatumia madawa ya kulevya.

Huu ni wakati wa Young Dee kubadilika na kufungua ukurasa mpya wa maisha yake, ajifunze kutokana kaka yake kama TID ambaye mwaka 2008, alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela baada ya kutiwa hatiani kwa kujeruhi. Nadhani hili lingekuwa funzo zuri kwake kwa kuamini hakuna aliyejuu ya sheria.
Young Dee ana nafasi ya kufanya vizuri zaidi kimuziki na kufika mbali zaidi, lakini kama akiweza kutoka katika kifungo cha kauli ya aliyekuwa meneja wake, Max Rioba.

Josephine Mshumbushi: CHADEMA ni Mali ya Mtei, Kimejengwa kwa Misingi ya Unafiki na Nidhamu ya Woga

$
0
0

Ameandika Josephine Mshumbushi mke wa Dr.W.Slaa katika ukurasa wake rasmi wa Facebook

Kwa Vijana wa CHADEMA!

Salaam,

Miaka 15,iliyopita sikuwahi kujua watoto wangu wataishi kuyasoma maandiko yangu nakunihoji au kuniuliza maswali.
Leo hii inatokea.

Ngoja niweke kumbukumbu sahihi!!!!

Kitendo cha kuwaita watu wasaliti ni kwakuwa mtu umeshindwa hoja ya kumshawishi akubaliane na wewe.

(Don't let personal hangups sidetrack the negotiations)

Na hili ndilo limekuwa anguko la CHADEMA toka nilipokijua chama hicho!
Mawazo au maamuzi ya mtu hayahojiwi.

Kwanini unaitwa mtu mzima!!!!!
Ni kwa kigezo kwamba sasa unaweza kufanya maamuzi yako bila shinikizo.

Maamuzi ya mtu lazima yaheshimiwe japo mengine yamekuwa magumu kuyakubali.

"In one of my job interview I was asked,how do you feel when you are asked to fire somebody"

.........very sad,however decisions have to be made for things to move foward."

Ninyi Vijana Hakuna anayeijua CHADEMA, tena Leo ambapo kila mtu ni msemaji.
Anayeijua CHADEMA ni mtu mmoja tu, aliyebeba maono na kukianzisha (Mzee Mtei)

"what the transitions follows non of my business.........."

Mimi na wewe ni .................
Ndiyo maana ndani ya CHADEMA mtu mmoja tu anaweza kuuwa chama.........

Tofauti na CCM.
Mwl hakuianzisha TANU kama taasisi, Bali lilikuwa ni kundi kubwa la watu, na likamchagua kama kiongozi kwa kuwa he has a commanding power element.

Heshima na nidhamu iliendelea kujengwa mpaka Leo kwa viongozi wote.
Huwezi na Hakuna maandiko ya mtu kuitwa msaliti ndani ya CCM. Kwakuwa ni kundi kubwa lililojengwa kwa hulka ya kuheshimu mawazo ya mtu na kuyapa mda yapite.

CHADEMA kimejengwa kwa nidhamu ya woga.Ndiyo Maana wengi waliamini kwa kujiweka karibu na wakubwa ndiyo fursa yao yakuonekana na kufikia malengo.

Mfano kila mtu anafanya jambo awe recognized na Mbowe na enzi hizo na Dr Slaa pia.

Tabia hii imeendelea kuzaa majungu na hofu ya kutojiamini.
Watu wenye mawazo Yao wameshindwa kuyatoa kwa kuhofu kutosikilizwa.
Lakini hata wale wenye mtazamo tofauti wameshindwa kuisimamia wasipoteze nafasi zao.

(Haya yanaishi ndani ya vijana wengi leo)
Ndiyo maana tunaona post nyingi leo ili mradi mtu kaandika kitu. Mbaya zaidi Hakuna mwongozo wa Nini kiandikwe wapi na kwa wakati gani.

Hivyo maamuzi tuliyofanya.

1.We trusted on our strengh.
2.We wanted to end relationship with the problem.

Enyi wafia chama ni vema mkatambua hamjai hata kwenye kiatu changu, nimetengeneza historia yangu, na bado naitengeneza historia yangu.

Yote mnayofanya yanapita ila kitendo cha kumkataa mtu tuliyemuita fisadi kitadumu Milele.

And that is our strength .

Kilio Kwa watumia M-pesa, Tigo Pesa , Airtel Money na Wale wa Kwenye ATM.......Kila ukituma 1000/- utakatwa kodi 280/-

$
0
0
Wachambuzi na wadau mbalimbali wametoa maoni yao kuhusu Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2016/17, huku watumiaji wa huduma za fedha kwa njia ya simu wakikumbwa na maumivu wa kodi.

Hiyo ni siku moja baada ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango kuwasilisha Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 20116/17.

Pamoja na mambo mengine, bajeti hiyo inapendekeza kuongeza ushuru wa vinywaji baridi, maji ya juisi, vinywaji vikali, bia na sigara.

Pia itawagusa watumiaji wa M-pesa, Tigopesa, Airtel Money, Ezypesa   kwa kukatwa Sh 280 kwa kila Sh 1000 watakayotuma.

Jana Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo), alisema hatua hiyo ya Serikali kuendelea kutafuta kodi kwa kuzidi kuwaumiza wananchi inakwenda kinyume na matarajio ya Watanzania wengi.

Alisema katika bajeti hiyo ya Serikali na ukusanyaji wa mapato yake, katika kila Sh  1000 itakayokatwa kwa huduma kwenye ATM kuanzia Julai Mosi mwaka huu, Sh 280 zitachukuliwa na TRA.

Zitto alisema hali hiyo pia itawakumba watumiaji wa miamala ya M-pesa, Tigopesa, Airtel Money, Ezypesa ambalo ndilo kundi kubwa la Watanzania wanaotumia huduma hiyo nchini.

Aawali kodi ya bidhaa ilikuwa asilimia 10 lakini kwa hatua ya kuongezwa kwa kodi ya ongezeko la thamani kodi itapaa na kufikia asilimia 28.

Kwa mantiki hiyo, katika kila Sh 100 kodi ni Sh 28 na  katika Sh 1000 kodi ni Sh 280.

Kutokana na hali hiyo kodi ya VAT hulipwa na mtumiaji wa mwisho ambaye anatuma au kupokea fedha, hali ambayo itawaumiza watumiaji wa mwisho.

“Hivyo hivyo katika miamala ya M-pesa, Tigo pesa na kadhalika, katika kila Sh 1000 itakayokatwa kwa huduma kwenye ATM kuanzia Julai 1, 2016, Sh  280 zitachukuliwa na TRA,” alisema Zitto.

Alisema   ameshangazwa na hatua ya Serikali kuongeza kodi ya VAT kwenye utalii hali ambayo inaweza kusababisha Tanzania kupoteza watalii wengi kwa washindani wake kwa sababu itaongeza gharama kwa watalii.

“Kama tunataka kutumia utalii kama kichocheo cha ajira ni vema kufikiria upya suala hili,” alisema.

Akizungumzia mapendekezo ya Serikali katika Sheria ya Kodi ya VAT ili kutoza kodi bidhaa zinazotoka Zanzibar, alisema hatua hiyo inavunja misingi iliyowekwa na sheria ya zamani ambayo ilifanana na ile za Zanzibar.

“Ikumbukwe kuwa Sheria ya Kodi ya VAT ya 2014 ilivunja misingi iliyowekwa ya sheria ya zamani ambayo ilifanana na ile ya Zanzibar. Mapendekezo ya sasa yana madhara makubwa kwa Zanzibar kwa sababu  hakuna atayewekeza Zanzibar ili kufaidika na soko la Bara.

“Biashara nyingi zinazozalisha Zanzibar zitahamia Tanzania Bara. Mapendekezo haya yanaweza kusababisha  mgogoro kati ya pande mbili za Muungano,” alisema.

Dongo la Mbatia kwa Naibu Spika Dr. Tulia Akson....

$
0
0
"Nina miaka 25 niko kwenye siasa.Wakati tunapambana kwa ajili ya Watanzania miaka hiyo yote hatukuwahi kuwa na posho.Kipindi hicho kina Tulia walikuwa shule ya msingi"

Source: Mh Mbati  James
Viewing all 104702 articles
Browse latest View live


Latest Images