Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live

Wasanii Wanaona ni Ufahari Kutoka Kimapenzi na Mastaa wa Kike Wenye Umri Mkubwa – Nay

$
0
0
Rapper Nay wa Mitego amesema wasanii wachanga wanajisikia ufahari kutoka kimapenzi na mastaa wa kike wenye umri mkubwa.
nay new2

Akizungumza katika kipindi cha Enewz cha East Africa Television Alhamisi hii, Nay wa Mitego amesema kuwa wasanii wachanga hawawezi kujizuia kutoka kimapenzi na mastaa wa kike waliyowazidi umri kwa kuwa walikuwa wanawatamani kwa muda mrefu.

“Mimi siwezi kuwalaumu hao vijana kuwa na uhusiano nao, unaju inaweza kuwa mtaani siku moja ulikuwa unawishi siku moja kuwa na mtu fulani, halafu ikitokea nafasi kama ile pale aah! Mtu hata upewe ushauri wa dizaini gani mtu ambaye ulikuwa ukimuona kwenye runinga anaingia katika kumi na nane zako mimi siwalaumu japokuwa wanatakiwa kuwa makini”, alisema Nay

Pia Nay alisema wasanii wengi wa kike, wamekuwa wakiutumia udhaifu huo ili kutembea na wasanii wachanga.

Jeshi La Polisi Lamshikilia Mwanamke Mmoja Kwa Tuhuma Za Kutupa Mtoto Chooni

$
0
0
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, linamshikilia, Mwananke mmoja alietambulika kwa jina la Rosemary Khiwili (23) mkazi wa Kimara  kwa kosa la kutupa mtoto katika shimo la choo.

Rosemary ambaye ni mfanyakazi wa Hoteli ya Landmark jijini Dar es Salaam anadaiwa kumtupa mtoto mchanga katika choo cha shimo cha nyumba anayoishi na mtoto huyo amegundulika na mama mwenye nyumba, Upendo Mboma baada ya kuingia kwa ajili ya kumwaga maji machafu na ndipo aliposikia mtoto analia kutokea kwenye choo.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi (CP), Simon Sirro amesema kuwa tukio hilo lilitokea Juni 8 mwaka huu huko maeneo ya Kimara Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Kamishina, Sirro amesema mtoto huyo aliokolewa na akiwa hai na kikosi cha Zimamoto na uokoaji  cha jiji kwa kushirikiana na askari polisi , na mtoto huyo amehifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala kwa uangalizi maalum huku upelelezi ukiendelea na ukikamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi.

Wakati huo huo jeshi la polisi limeokota silaha mbili zilizotengenezwa kienyeji  pamoja risasi sita  zikiwa kwenye begi katika shamba la matuta ya viazi baada kutelekezwa na watu wasiojulikana na jitihada zinaendelea kuwabaini watu hao.

Kamanda, Sirro amesema katika operesheni ambayo wanaifanya kwa wiki hii wameweza kuwakamata watu 711  kwa makosa ya unyang’anyi wa kutumia nguvu, kukutwa bhangi na Gongo , mitambo ya kutengeneza gongo, kucheza kamari pamoja na biashara ya kuuza mwili.

Amesema  Kawe pamoja na Mabibo zinaongoza kwa utengenezaji na uuzaji wa pombe haramu ya Gongo.

Sugu Kikaangoni Kwa Kuwaonyeshea Kidole cha Kati Wabunge wa CCM

$
0
0
Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson ameitaka Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuchunguza tuhuma dhidi ya Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu Sugu anayedaiwa kuwaonyeshea kidole cha kati wabunge wa CCM.

Sugu anadaiwa kufanya kitendo hicho June 6, mwaka huu alipokuwa akitoka katika ukumbi wa Bunge baada ya kuwasilisha maoni ya kambi ya upinzani kuhusu azimio la bunge kuridhia mkataba wa kimataifa wa udhibiti wa matumizi ya dawa na mbinu za kuongeza nguvu michezoni.

Naibu Spika ameitaka kamati hiyo kumchukulia hatua kali kama watamkuta na hatia ya kufanya kitendo hicho

Rais Magufuli Katika Ubora Wake, Ahadi Zimeanza Kutekelezwa

$
0
0
Watu wanasafiri nje ya nchi kila siku wakati watu wanakufa na kipindupindu?.Hakiamungu nikiwa rais mm.......

Ndani ya miezi 6 kipindupindu chaliiiii

Msongamano wa magari dar unalikosesha taifa mapato mengi sana....

Kabla ya miezi sita-magari ya mwendokasi tayari,ni uroda mtupu.

Nitahakikisha inajengwa mahakama maalum kwa mafisadi tu

Ndani ya miezi 3,12b ikatolewa kwa uendeshaji wa mahakama na 2.5b ndani ya miezi sita ujenzi wa mahakama.

Elimu bure drs la 1-12.
Ndani ya miezi miwili tu,sasa watoto wanasongamana madarasani.

Haiwezekani ww mkuu wa mkoa upo alafu watoto wanakaa chini darasani.
Speed ni ya mwendokasi na ni siku takrbani 20 tu zimesalia na kilio hicho kitabaki historia tu.

50M kila kijij kitapata...
Sasa tupo mkao wa kula tutaipokea.

Na mengine mengi ya kubana matumizi ya pesa kama:-
Safari za nje,warsha,makongamano pamoja na semina
Pia kuboresha mishahara ya watumishi na kuwapunguzia makato ya kodi.

Sii hayo tu lkn pia ametumbua majipu kwa kuonesha dhamira ya dhati ya kuichukia rushwa na ufisadi.Na kwahili hata maswahiba wake limewakuta,sina sbabu ya kutonesha makovu.Poleni yaliowakuta kwa namna moja au nyingine.

Huyu kama c mtume bac ni nabii,ni kiongozo wa kipekee kabisa ambaye kama cjakosea,haijawahi kutokea.Amejaribu kumkuna kila mtanzania mnyonge dhidi ya vilio vyetu japo wale majangir na maharamia wa rasilimali zetu wameumia.
Potelea mbali mzee yupo imara sana katika harakati za kulitetea taji la mbingu,hatetereki,hayumbishwi wala hakatishwi tamaa.

Wamemjaribu wengi na kwa mengi sana wakidhani misimamo italegea kumbe ndo kwanza ""akipigwa teke chura,anaongezewa mwendo""

-Mara oooh...jamaa ni dictator...
-Mara oooh...jamaa anabana demokrasia...
-Mara oooh...aliuza nyumba za serikali
-Mara oooh hashauriki...
-Mara oooh...ni nguvu ya soda...
-Mara oooh kajichukulia mamlaka kutumia pesa ya bunge kwa shughuli za maendeleo bila idhin ya bunge...
Ni mengi sana yamesemwa na mengine mtanikumbusha...lakin...
wanaishia kuisoma namba...
Na yote haya hayafanyi kwa kupiga ramli..lah hasha...kumbukeni sisi wenyewe wananchi wanyonge tulishtaki wakati anatuomba kura.

Na hata kwa watani zetu hizi ndo zilikuwa kiki zao za kila cku japo kwa sasa baada ya mzee kujitutumua sasa wao tena wanaanza vijembe.
Lakini binafsi huwa siwashangai maana waliotuhujumu cc na nchi nzima kwa wakati huo,sasa wako upande wao(majina mtajaza)sio kila kitu nimalize.Kumbe nimekubali sasa kwamba ukawa ndio ccm A bila shaka na ccm ndio ccm B bila shaka.Na kwa muktadha huo ni ccmB ya waadilifu inapambana dhidi ya ccmA ya wabadhirifu...
Wataisoma namba!!!
Kwa ujumla sasa hivi watani zetu wapo hoi,kila kunapokucha ni nafuu ya jana.Nahodha wa chombo yuko imara,mawimbi yanakipiga chombo lkn ndo hivo kinazidi kusonga kwa mwendo wa hatareee
Na kwa taarifa,abiria hao wanaotia dhoruba bahari nahodha atawamwaga rasmi kabla chombo hakijafika ufukwe 2020.

CCM hoyeeeeeeeeeeeeeeeee
Magufuli hoyeeeeeeeeeeeeee
Naomba kuwasilisha.

MASKINI: Basi la Mwendokasi Laua Mlemavu Kariakoo

$
0
0
Mlemavu wa viungo amegongwa na basi la mwendokasi na kufa papo hapo usiku huu, eneo la Kariakoo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Lucas Mkondya amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa 2.00 usiku makutano ya barabara za Msimbazi na Uhuru na kwamba, mwili wa mlemavu huyo wa kiume umeokotwa vipandevipande.

Nkondya amesema chanzo cha ajali ni mwendokasi wa dereva, kwani tukio hilo limetokea karibu na makutano ya barabara za Msimbazi na Uhuru ambako kuna mataa, hivyo alitegemea basi lingekuwa kwenye mwendo wa kawaida.

Dk Tulia Akomalia Kuitwa Muheshimiwa Bungeni....Silinde Agoma...

$
0
0
Msemaji wa Kambi ya Upinzani wa Wizara ya Fedha na Mipango, David Silinde, amejikuta kwenye mvutano na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson, baada ya kuanza kusoma bajeti mbadala bila kumuita mheshimiwa naibu spika.

Silinde alianza kuwasilisha bila ya kumtaja Naibu Spika, Dk Tulia Ackson, hivyo kusababisha wabunge wa CCM kuguna.

Kutokana na miguno hiyo, Dk Tulia alimtaka akipe kiti heshima yake, lakini Silinde akamkatalia akisema si lazima kumwita Tulia mheshimiwa kabla ya kukubali kwa shingo upande.

“Kama unataka uheshimiwa sawa,” alisema Silinde na kuongeza: “Basi Mheshimwa Naibu Spika,” alisema na kusababisha ukumbi kupiga makofi.

Hawara wa Mfanyakazi wa ndani Atiwa Mbaroni Akihusishwa na Mauaji ya Aneth Msuya ( Dada wa Bilionea Msuya )

$
0
0
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limewakamata watu wengine wawili, akiwamo mpenzi wa mfanyakazi wa ndani wa Aneth Msuya, aliyeuawa kwa kuchinjwa nyumbani kwake.

Aneth, ambaye ni dada wa Bilionea Erasto Msuya, aliuawa kwa kuchinjwa na watu wasiojulikana Mei 26 nyumbani kwake Kibada, Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Wauaji hao hawakuchukua chochote kwenye nyumba hiyo. Bilionea Msuya aliuawa Agosti mwaka jana kwa kupigwa risasi na tayari watu 12 wamekatwa, wakituhumiwa kuhusika na mauaji hayo.

Kamanda wa Kanda hiyo, Simon Sirro alisema hadi sasa wamekamata watuhumiwa wanne wakihusishwa na mauaji ya dada wa bilionea huyo.

Kati ya watuhumiwa waliokamatwa, yumo mume wa Aneth, msaidizi wa ndani wa Aneth na mtuhumiwa mwingine ambaye Kamanda Sirro hakumtaja jina.

“Mwanzo tulimkamata mume wa marehemu na msaidizi wa ndani wa marehemu, lakini sasa wameongezeka wengine wawili, akiwamo hawara wa msaidizi wa ndani. Tunaendelea kuwahoji na upelelezi ukikamilika tutawafikisha mahakamani,” alisema Sirro.

Kwa mujibu wa mama mdogo wa marehemu, Lilian Benjamin, msaidizi wa ndani wa dada wa bilionea huyo aliondoka saa sita mchana na kuacha funguo nyumba ya jirani.

Lilian alisema msaidizi huyo alimpigia simu ghafla bosi wake mchana na kumwambia anaondoka na hataendelea na kazi.

Mauaji ya Aneth ni mwendelezo wa mauaji yanayoikumba familia hiyo ya Msuya baada ya kaka yake, Erasto ambaye alikuwa ni mfanyabiashara tajiri wa madini, kuuawa Agosti 7, 2013 kwa kupigwa risasi zaidi ya 12 kwa kutumia bunduki ya SMG katika eneo la Mijohoroni wilayani Hai, Mkoa wa Kilimanjaro.

Februari 10, mawakili wanaosimamia kesi ya Erasto, Hudson Ndusyepo, Majura Magafu, Emanuel Safari na John Lundu, waliiambia mahakama kuwa Serikali inakusudia kuita mashahidi 50 kuthibitisha shtaka hilo na kuwasilisha vielelezo 40, ikiwamo bunduki hiyo.

Mawakili hao walidai mipango ya kumuua bilionea Msuya ilianza Julai 26,2013 jijini Arusha, ikiwahusisha washtakiwa na waliotekeleza mauaji hayo wangelipwa Sh5 milioni kila mmoja.

Wakitoa maelezo ya tukio hilo, mawakili hao waliiambia mahakama kuwa washiriki ambao wasingeenda moja kwa moja kwenye mauaji, wao wangelipwa Sh3 milioni kila mmoja.

Mshtakiwa wa kwanza, Shariff Mohamed anadaiwa kuwa ndiye alikuwa mpangaji mkuu na alitoa fedha za maandalizi yote ya mauaji.

Washtakiwa wengine ni Shaibu Jumanne, ambaye anafahamika kwa jina la utani la Mredii, Mussa Mangu, Jalila Zuberi (Said), Karim Kihundwa, Sadick Jabir (Msudani) na Ally Mussa (Mjeshi).

Zitto Kabwe Awachokonoa Wabunge Wenzake..Ataka Posho zao Zikatwe Kodi

$
0
0
Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amewachokoza tena wabunge baada ya kuitaka Serikali kuanza kukata kodi katika posho za wawakilishi hao ili kuongeza wigo wa mapato.

Zitto amesema hatua ya Serikali kuondoa msamaha wa kodi katika malipo ya kiinua mgongo cha wabunge katika bajeti ya Serikali ya 2016/17 ni jambo jema lakini isiishie hapo kwa kuwa viongozi hao bado wana mapato mengi yasiyokatwa kodi yakiwemo ya posho.

Kauli ya mbunge huyo wa Kigoma Mjini ni mwendelezo wa msimamo wake wa kupinga wabunge kulipwa posho ya vikao bungeni na katika Bunge la 10 alipokuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema) aliongoza kampeni ya kupinga ongezeko la posho hiyo bila mafanikio.

Aidha, pendekezo lake kutaka posho za wabunge zikatwe kodi limekuja siku mbili tangu Naibu Spika, Dk Tulia Ackson atangaze kukata posho za wabunge watakaokuwa wakisaini kuingia bungeni na baadaye kuondoka na waathirika wa kwanza wa hatua hiyo watakuwa wapinzani wanaosusia vikao vyake.

Akitoa maoni katika mchaparo wa uchambuzi wa Bajeti ya Serikali ya mwaka 2016/17 ulioandaliwa na Kampuni ya Ukaguzi wa Hesabu ya KPMG juzi usiku, Zitto alisema kiinua mgongo hicho kilichoanza kutolewa mwaka 2010 kimekuwa kikitolewa bila kufuata sheria.

Alisema mwaka 2010 pensheni hiyo iliongezwa mara mbili kinyume na sheria na mwaka jana fedha hizo ziliongezwa tena takriban mara nne zaidi bila kukatwa kodi.

Zitto alisema wanashangaa kwa nini kodi ya kiinua mgongo imeanzishwa mwaka huu wakati wabunge watalipwa mwaka 2020.

Nilichokuwa na natarajia ni kuanzisha kodi kwenye posho. Sisi (wabunge) tuna posho za aina nyingi na kubwa zaidi ni ile posho ya kikao ya Sh220,000 kwa siku,” alisema.

Hii posho haikatwi kodi na wala siyo fedha za kujikimu (per diem) ambayo unapewa kwa ajili ya chakula na malazi.”

Alisema kwa mwaka mbunge anapata takriban Sh40 milioni za posho (Sh200 milioni kwa miaka mitano) wakati kiinua mgongo ni takriban Sh172 milioni baada ya miaka mitano hivyo posho zingeweza kuingiza mapato mengi zaidi.

Katika uchambuzi wa bajeti hiyo, Mkurugenzi wa kodi na huduma wa kampuni wa KPMG, David Gachewa alisema uanzishwaji wa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) katika sekta ya benki utawaumiza wananchi lakini hakukuwa na namna nyingine zaidi ya Serikali kuianzisha ili kuongeza wigo wa mapato.

Hata hivyo, alisema anaona utata katika utekelezaji wa ukusanyaji mapato hayo iwapo Serikali itatoa mashine za kielektroniki za kutolea risiti (EFD) kwa benki hizo au Kamishna Mkuu wa TRA atawaandikia barua kutozitumia mashine hizo kama Serikali ilivyompa madaraka hayo katika bajeti.

Hii siyo mara ya kwanza kuwapo ugumu katika utekelezaji wa baadhi ya hatua za ukusanyaji mapato. Naamini Chama cha Benki Tanzania (TBA) kitakaa na Serikali kuona ni namna gani watalitatua tatizo hilo,” alisema Gachewa.

Kuhusu hatua ya Serikali kuzitaka taasisi zote za umma kutumia huduma za bima za Shirika la Bima la Taifa (NIC), Gachewa alisema si kitu kizuri kwa sababu kitafanya Serikali ianze kushindana na sekta binafsi.

Kuna dalili za wazi kuwa Serikali inafanya biashara jambo ambalo halikutarajiwa. Serikali ilitakiwa iache sekta ya bima mikononi mwa sekta binafsi na yenyewe iweke mazingira wezeshi,” alisema.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM),  Profesa Kitila Mkumbo alisema hatua nyingi zilizochukuliwa katika uandaaji wa bajeti hizo zimekosa ushahidi kama zitatekelezeka ipasavyo.

Mtaalamu huyo wa masuala ya elimu na saikolojia alisema uamuzi wa kupunguza safari za nje una matatizo sababu unaifanya Tanzania kutokuwa na muunganiko na ulimwengu na kitendo cha bajeti hii kubana zaidi matumizi kitaifanya nchi ishushe hadhi yake kimataifa.

 “Jambo la msingi katika udhibiti wa safari za nje lingekuwa kupunguza posho za maofisa wanaosafiri nje ya nchi na siyo kupiga marufuku mpaka kwa kibali maalum,” alisema.

Kuhusu bajeti ya elimu, Profesa Kitila alisema iwapo fedha zote Sh4.4 trilioni zilizopangwa zitatolewa ni jambo jema katika sekta hiyo muhimu katika maendeleo.

Hata hivyo, alionya kuwa historia inaonyesha bado hazitaleta matokeo mazuri kwa kuwa sehemu kubwa huelekezwa katika kulipa mishahara na kuimarisha miundombinu badala ya kugharamia programu za kuongeza ubora wa taaluma.

Wadau wengi waliipongeza Serikali kutenga asilimia 40 ya bajeti katika miradi ya maendeleo ila walionyesha hofu kuwa sehemu kubwa ya kodi inategemea sekta binafsi jambo linaloweka ugumu katika mazingira ya ufanyaji biashara.

Profesa wa Uchumi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Honest Ngowi alisema takriban asilimia 51 ya mapato ya bajeti hiyo iliyowasilishwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Phillip Mpango inagusa sekta binafsi na kuhoji kama kutakuwa na ukuaji mzuri wa sekta hiyo.

 “Uamuzi wa kuanzisha VAT katika utalii haukuwa mzuri badala yake Serikali ilitakiwa ivutie watalii wengi ili ipate kodi katika maeneo mengine ya tozo kutokana na idadi kubwa,” alisema na kuongeza: “Kodi inatakiwa kuwa chombo cha mapato na msingi mkubwa wa maendeleo.”

Wabunge wa Kambi ya Upinzani Wajitoa Kamati ya Bunge ya Ukimwi Baada ya IKULU Kuwanyiima Kibali cha Kwenda Marekani

$
0
0
Ofisi ya Rais Ikulu imewanyima vibali vya kusafiri kwenda Marekani wabunge wawili wa Kambi ya Upinzani, bungeni na kumruhusu mbunge wa Geita Mjini (CCM), John Kanyasu. 

Wabunge hao wa kambi ya upinzani waliochaguliwa kwenda Marekani ni Savelina Mwijage (CUF) na  Mwita Mwaikabwe (Chadema)

Wabunge hao watatu ni wajumbe wa Kamati ya Masuala ya Ukimwi, lakini baada ya kunyimwa vibali hivyo wamejitoa kwenye kamati hiyo wakipinga kitendo hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari bungeni mjini Dodoma, mbunge wa Ukonga (Chadema), Mwita Mwikwabe alisema walipata barua ya kuteuliwa kushiriki safari hiyo kutoka Ofisi ya Bunge Mei 24.

Tunapenda kukufahamisha kuwa Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amekuteua kushiriki mkutano wa ngazi ya juu ya maamuzi kuhusu Ukimwi duniani utakaofanyika 08-10 New York, Marekani,” alinukuu barua hiyo iliyosainiwa na Patson Sobha kwa niaba ya Katibu wa Bunge.

Katika barua hiyo wametajwa wabunge wengine kwenye safari hiyo kuwa ni mbunge wa viti maalum (CUF), Savelina Mwijage.

Nikiwa Tarime nilipata simu kutoka kwa Patson kwamba, Naibu Spika alipokea simu kutoka Ikulu kuwa imezuia vibali vyetu vya kwenda Marekani na badala yake Kanyasu ameteuliwa,” alisema Mwikabe.

Tunashangaa, kuteuliwa tuliambiwa kwa barua, lakini kukataliwa tuliambiwa kwa simu,” alisema Mwita.

Alisema kutokana na kutopewa kibali, wajumbe wote wa kambi hiyo wamejitoa kwenye Kamati ya Bunge ya Ukimwi.

Hayo yote yanafanyika kwa sababu Naibu Spika hatupendi kabisa wabunge wa upinzani ndiyo maana wametufanyia haya,” alisema.

Kwa upande wake, mbunge wa Vunjo (NCCR-Mageuzi), James Mbatia alisema Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliwaambia katika mkutano wa wabunge wote kuwa hawahusiki katika uombaji wa vibali kutoka Ikulu.

Mimi mwenyewe nimeshawahi kusafiri zaidi ya mara tatu mbona sijawahi kuomba kibali kutoka Ikulu?” alihoji Mbatia.

Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah alihoji kama wabunge hao ndiyo wenye haki ya kusafiri. Pia alihoji haraka waliyonayo wabunge hao wakati walishapeleka malalamiko yao kwa maandishi dhidi ya Naibu Spika, Dk Tulia Ackson.

Kwani wanaharaka gani wao? Si walishapeleka malalamiko hayo na yapo kwenye kamati. Wasubiri uamuzi ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge),” alisema.

Huu ni Ushauri Ambao Shaa Alipewa na Lady Jaydee na Hatousahau Maishani Mwake

$
0
0
Shaa alipewa ushauri muhimu na Lady Jaydee ambao hadi leo hatousahau na umemsaidia kwenye maisha yake ya muziki.

"Namquote dada Jide kitambo like 5 or 6 years back aliniambia kwamba ‘ukifanya kazi hii kwaajili ya kupata awards mdogo wangu utagive up’ utakata tamaa. Aliniambia wewe fanya kazi hii focus kwenye malengo yako, tengeneza pesa ujifikishe pale unapotaka,” alisema Shaa kwenye video ambayo Jide aliipost Instagram.

Jide aliandika kwenye video hiyo: Unapompatia mdogo wako ushauri halafu anaamua huufanyia kazi ni jambo la faraja sana. Keep it up my Shaa. Never ever Give up, no matter what.”

Mwanamuziki Young Killer Nae Kusaini WCB? Hili Ndio Jibu Lake

$
0
0
Hivi karibuni kulizuka tetesi kuwa huenda Young Killer akawa msanii mwingine atakayeungana na timu ya WCB.

Picha aliyoonekana akiwa na Diamond kwenye studio za Wasafi ndiyo iliyosababisha tetesi hizo. Tumemuuliza rapper huyo iwapo tetesi hizi ni za kweli.

“Ile ni picha ambayo kweli ilipigwa tulikuwa pale ofisini kwake na ni picha ambayo ilipigwa kwa maana lakini sio ya kuzungumzia sana kutokana na kwamba mipango inakuja na tunamshukuru mwenyezi Mungu akitia baraka na ikawa sawa nadhani tutazungumza sasa hadharani, lakini ni picha ambayo ilipigwa kwa maana nadhani mwenyezi Mungu akitia nguvu watanzania wataona kitu ambacho kipo,” amesema Young Killer.

VIDEO:Upinzani Wakanusha Kuchukua Posho, Wataka zifutwe Kabisa Kama Serikali Inabana Matumizi Kweli

$
0
0
Wabunge wa Upinzani wamesema wao walikuwa hawasaini posho kama naibu spika anavyodai na wanataka posho hizo kufutwa kabisa kama serikali ya JPM inataka kubana matumizi kweli

Mheshimiwa Spika, kabla sijatoa maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani kuhusu bajeti ya Serikali ya 2016/17, napenda kuweka rekodi sawa kuhusu upotoshaji unaofanywa na Wabunge wa CCM kwamba Wabunge wa Upinzani wanaisaini mahudhurio bungeni na kuchukua posho bila kufanya kazi.

Napenda mkumbuke kwamba, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imekuwa ikisisitiza kufutwa kwa posho za vikao kwa maana ya “Sitting allowance”, lakini serikali imekuwa ikipata kigugumizi, hivyo basi Kambi Rasmi inasema kama kweli Serikali ya Rais John Pombe Magufuli inania thabiti ya kubana matumizi ya Serikali basi inoneshe uthabiti huo kwa kuifuta posho ya vikao na fedha hizo zipelekwe kwenye miradi ya maendeleo hususani kuwapatia Watanzania maji safi na salama.

Hata hivyo, tunashauri, wale wanaokaa bungeni bila kuchangia hata kwa maandishi na kuchukua posho, wafuatiliwe na wakatwe mishahara yao, kwa kuwa hawajafanya kazi na hansard itumike kuwabaini.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Hawa Ghasia Akataa Wabunge Kukatwa Kodi Katika Kiinua Mgongo

$
0
0
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti Hawa Ghasia amedai kuwa kuwakata kodi kwenye viinua mgongo ni kuwakata kodi mara mbili kwa kuwa wanakatwa kodi tayari kwenye mishahara yao na ametaka serikali kufikiria tena suala hilo..

Unakaribishwa kuitazama Video ya Jike Shupa ya Nuh Mziwanda ft Alikiba

$
0
0
Zimepita wiki kadhaa toka msanii wa Bongofleva Nuh Mziwanda alivyoachia audio ya hit single ya ‘Jike Shupa’ aliyomshirikisha Alikiba, leo June 11 2016 imeachiwa rasmi video ya hit single ya ‘Jike Shupa’, enjoy kwa kutazama dakika tatu na sekunde 50 za video yenyewe mtu wangu.

Young D: Sijakamatwa na Polisi ila Nilikuwa Nashoot Video ya Wimbo Wangu Mpya

$
0
0
Msanii mdogo mwenye mafanikio makubwa aliyoyapata ndani ya muda mchache amekanusha habari zinazosambazwa na watu wasiompenda kwamba amekamatwa na poliisi. Akitolea maelezo suala hilo kutoka kwenye nyumba yake anayomiliki maeneo ya Sinza alidai kwamba hajakamatwa na mtu yeyote yule ila alikuwa akishoot video ya wimbo wake mpya unaoitwa "Jirani nitakuvunjia simu yako" ambapo director alishauri simu ivunjwe ili kuleta uhalisia ."Unajua director alikuwa too authentic,hata sisi ilibidi tuvunje simu ya jirani"

Pia Young D ametolea ufafanuzi suala la madawa kulevya na kusema yeye angekuwa anatumia madawa ya kulevya asingekuwa anafukuzana kwenye chati na Diamond na Wizkid hapa Afrika pia kuweza kumiliki mtoto mkali Afrika Mashariki .

Mwanza: Kijana Awafungia ndugu zake Ndani na Kuchoma Moto Nyumba

$
0
0

Nyumba moja iliyopo mtaa wa Kiseke wilayani Ilemela mkoani Mwanza imeteketea kwa moto leo asubuhi na kuunguza vitu vingi huku wakazi wa nyumba hiyo wakinusurika. 

Taarifa zinaarifu kuwa,  nyumba hiyo imewaka moto baada ya mmoja wa watoto wa familia hiyo kuamka asubuhi na kumwaga mafuta ya taa katika moja ya chumba cha nyumba hiyo na kisha kuwasha moto.

Imeelezwa kuwa,  kijana huyo ambaye anadaiwa kuwa na matatizo ya akili amekuwa akiwatishia kwa muda mrefu kuwachoma moto lakini wamekuwa wakimpuuza kutokana na matatizo yake ya akili.

Baada ya kumwaga mafuta  na kuwasha moto,  kijana huyo alitoweka na kuwafungia ndugu wengine ndani ambapo majirani walifanikiwa kuwahi kuwaokoa.

CHADEMA Waishitaki Serikali Mahakamani

$
0
0
MWENYEKITI wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, jana alifungua kesi ya madai katika Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, kupinga amri ya polisi kuzuia mikutano ya vyama vya siasa nchini.

Kesi hiyo namba 79 ya mwaka 2016, ilifunguliwa jana na kusimamiwa na mawakili watatu Gasper Mwanalyela, John Mallya na Paul Kipeja.
  
Licha ya kuwepo na ulinzi mkali wa jeshi la polisi uliowekwa katika barabara zote za kuelekea Mahakama Kuu, viongozi na wafuasi wa Chedema walifanikiwa kuvuka vizuizi hivyo.
  
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutoka mahakamani jana jioni, Mbowe alisema sababu za kufunguliwa kwa kesi hiyo ni baada ya kuona demokrasia ya vyama vingi "inabakwa nchini."
  
Mbowe alisema watu wanne waliotajwa katika kesi hiyo ya madai ni Kamanda wa Polisi wilayani Geita, Kamanda wa Polisi wilayani Kahama, Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa polisi (Makao Makuu) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
  
Alisema wadaiwa hao wamefunguliwa kesi kutokana na kukiuka Sheria ya Vyama vya Siasa nchini, kwa kuchukua maamuzi ambayo hayaendani na demokrasia.
  
“Tunaiomba mahakama itangaze amri ya jeshi la polisi ya kuzuia mikutano ya vyama vya siasa ni batili, utekelezaji unaofanywa ni batili, polisi wapewe tangazo la kutowanyanyasa wapinzani na pia itoe amri ya vyama vya siasa kufanya mikutano yake na polisi wawe walinzi wa mikutano hiyo,” alisema Mbowe.
  
Alisema pamoja na polisi kuwabana hawataondoka jijini Mwanza, na wataongezeka zaidi mpaka kieleweke.
  
Alisema upo mkakati wa makusudi kuhakikisha Chadema inafutika katika mikoa ya Kanda ya Ziwa kutokana na baadhi ya viongozi wake kutekwa na kunyanyaswa na polisi.
  
Mkutano huo na waandishi wa habari ulihudhuriwa pia na Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Saidi Issa Mohamed, Dk. Vincent Mashinji (Katibu Mkuu), Salum Mwalimu (Naibu Katibu Zanzibar), Halima Mdee (Mwenyekiti Bawacha) na Pastrobass Katambi (Mwenyekiti Bavicha) na baadhi ya wabunge wa chama hicho.
  
Kesi hiyo ya madai inatarajiwa kupangiwa Jaji Jumatatu ijayo.
  
Polisi ilisambaratisha mkutano wa Chadema uliokuwa ufanyike Kahama katikati ya wiki, ambapo mabomu ya machozi na magari ya 'washawasha' vilitumika kuondoa wafuasi wa chama hicho waliokuwa wasikilize hotuba za viongozi wa kitaifa.
  
Chadema imepanga kufanya mikutano nchi nzima kulaani inachodai uonevu unaofanywa dhidi ya wabunge wake Bungeni.

Mwigulu Nchemba ateuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Tizeba apelekwa Kilimo na Mifugo

$
0
0
Rais John Pombe Magufuli leo tarehe 11 June 2016, amemteua Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi. Mhe. Nchemba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Waziri wa wizara hiyo, Mhe. Charles Muhangwa Kitwanga ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

Wakati huo huo rais amemteua mbunge wa Buchosha Dkt. Charles John Tizeba kuwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na uvuvi, nafasi iliyokua ikishikiliwa na Mhe. Nchemba.

Wateuliwa wataapishwa siku ya Juma tatu majira ya saa 3:00 asubuhi Ikulu.

WCB yatoa mwongozo wa adhabu wanazotoa kama msanii wao akifanya makosa

$
0
0
Akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni, mmoja kati ya viongozi wa juu wa label hiyo, Babu Tale amesema wao kama uongozi watasimama kidete kuhakikisha wasanii wa WCB wanakuwa mfano wa kuigwa kwa jamii.

“Nikijibu hapo kwenye eneo la nidhamu ni kwamba, sisi ni vijana ambao tunaishi na vinaja ambao wametoka kwenye familia zao ambazo zinamalezi tofauti tofauti, lakini wakija hapa ni lazima wafuate sheria zetu. Sitaki kumsifia Dioamond ni mtu ambaye hana nidhamu ya kuigiza, kwa hiyo hawa wengine lazima wafuate tabia za kaka yao,” alisema Babu Tale.

Aliongeza, “Kwetu msanii akitukana kwenye social network , akitukana kwenye stage huyo lazima sisi tumuadhibu. Kuna adhabu ambayo inasukumwa na social network hiyo hatuizingatii kwa sababu kila mmoja ana mapenzi yake na wengine wanachuki zao. Adhabu ambayo tatizo linaonekana wazi kwamba hili ni tatizo, tunayaita matendo kusudi, kiofisi huwenda mtu akasimamishwa bila jamii kujua, kukata pesa kwenye kazi zake bila jamii kujua, hayo mambo tunafanyia hata sisi viongozi pale tunapokosea,”

Nuh Mziwanda athibitisha Jike Shupa alimuimbia Shilole kwa kumtumia video queen anayefanana naye kama pacha

$
0
0
Nuh Mziwanda ameelezea jinsi uhusiano wake na Shilole ulivyokuwa kwa dakika 3:50!

Kwa video ya wimbo wake Jike Shupa aliomshirikisha Alikiba, Nuh ameuelezea uhusiano huo ulitawaliwa na mateso, wivu uliokithiri, kichapo na tabu za kila aina.

Kuthibitisha kuwa wimbo huo unamlenga ex wake, amemtumia msichana anayefanana copyright na Shilole. Kwenye video hiyo pia Nuh hakuacha kuonesha tattoo ambazo Shilole alizichora enzi wakiwa wakiwa wapenzi.

Nuh amemuonesha msichana huyo kama mjeuri na ambaye wakati mwingine anarudi nyumbani akiwa chakari. Ni video nzuri, icheck hapo chini.
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live




Latest Images