Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104701 articles
Browse latest View live

Wanafunzi Wafundishana Wenyewe Shule ya Kwedichocho Handeni Baada ya Walimu Kuacha Kazi.

$
0
0

Wakazi wa kijiji cha Manga kilichopo kata ya Mkata wilayani Handeni wameiomba serikali kuingilia kati kufuatia walimu wawili wa shule ya msingi Kwedichocho kuacha kazi tangu mwishoni mwa jana na kuwaacha wanafunzi wakifundishwa na wanafunzi wenzao wawili wa darasa la saba kufuatia vitongoji vyao pamoja na shule kuuzwa kwa mwekezaji ikidaiwa kuwa ipo maeneo katika kijiji kingine kinachojulikana kwa jina la Mazingara.

Wakizungumza katika kijiji cha Kwedichocho baadhi ya viongozi wa serikali ya kijiji na wakazi wake wamesema hatua hiyo imekuja baada ya baadhi ya viongozi wa kijiji cha Mazingara kumuuzia mwekezaji hekari zaidi ya 400 zenye makazi ya watu zaidi ya 1000 pamoja na shule hatua ambayo wanafunzi wameanza kutishiwa kuondoka kwa sababu mwekezaji anataka kulifanyia kazi eneo la ardhi ikiwa ni pamoja na majengo ya shule pamoja na nyumba ya mwalimu.

Kwa upande wake mwenyekiti mstaafu wa kijiji hicho Saleh Sadick amesema wakazi wa vitongoji vya Kwedichocho na Mkulumilo vyote vilivyopo katika kata ya Mkata hawatakubali kuondoka katika eneo hilo linalodaiwa kuwa ni eneo la kijiji cha Mazingara hatua ambayo inaweza kusababisha uvunjifu wa amani baina ya pande hizo mbili.

ITV ilifika hadi katika shule ya msingi Kwedichocho ambapo wananfunzi walikutwa darasani wakifundishwa na wenza wa darasa la saba huku wakiimba wimbo unaosema bado mapambano yanaendelea.



CHAMA Cha Kijamii CCK Chamkingia Kifua Naibu Spika Dk Tulia Ackson

$
0
0
CHAMA Cha Kijamii (CCK) kimelaani mpango unaofanywa na wabunge wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, wa kutaka kumng’oa Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson na kimewataka kufuata kanuni za uendeshaji wa Bunge.

Hayo yamo kwenye taarifa ya Mwenyekiti wa Taifa wa CCK, Constantine Akitanda aliyoitoa kwa vyombo vya habari jana, iliyotokana na tathmini ya Bunge tangu kurejeshwa Mfumo wa vyama vingi vya siasa, chanzo na kupevuka kwa ususaji wa shughuli za Bunge.

Kuhusu mpango wa kutaka kumng’oa Dk Tulia, Mwenyekiti huyo wa CCK alisema; “Hivi sasa kuna propaganda inayoenezwa ya kutaka kumng’oa Naibu Spika, Dk Tulia Ackson kwa madai ametumwa na Rais kuminya uhuru na demokrasia ndani ya Bunge.

“Hii si mara ya kwanza kwa kambi ya rasmi ya upinzani kulalamikia kiti cha Spika. Pia si mara ya kwanza kwa kambi hiyo kususa na kutoka nje ya bunge, pia si mara ya kwanza wabunge wa upinzani kukorofishana na kiti cha spika na kususa,” alisema.

Akitanda alisema tatizo la kambi hiyo ni pale spika anaposimamia kanuni huku wao wakikataa kwa makusudi, kufuata taratibu na kanuni za uendeshaji wa shughuli za Bunge, jambo alilosema haliwezi kufumbiwa macho.

“Kanuni zipo wazi kama hujaridhika na maamuzi ya kiti cha Spika unaruhusiwa kukata rufaa na hoja ikajadiliwa, sasa wabunge wetu wa Kambi Rasmi ya Upinzani sijui ni kwa nini hawataki kufuata utaratibu huu, ambao ni wa kikanuni. Wao wanataka kumng’oa Naibu Spika tu basi, kanuni je?”

Alisema dalili za kukataliwa kwa Naibu Spika na wabunge hao zilionekana tangu mwanzo kwani walimkataa hata kabla ya kuanza kazi kwa madai kuwa ametumwa na Ikulu, na hata siku ya kujieleza akiomba kura alikuwa anazomewa na wabunge wa kambi hiyo.

“Kimsingi tangu mwanzo wabunge wetu wa upinzani hawakumtaka Dk Tulia kutokana na umahiri wake wa kuzijua na kuzisimamia kanuni kwa ustadi mkubwa.”

Akitanda alisema tangu Bunge la vyama vingi lianze mwaka 1995, wabunge wa upinzani kutokana na uchache wao wamekuwa wanalalamikia kiti cha Spika na kutofautiana na Spika au kudai wanaburuzwa na wenzao wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Alisema katika kipindi cha mwaka 2010 hadi sasa ambapo Chadema kwa mara ya pili imetoa kiongozi wa upinzani bungeni, nchi imeshuhudia wabunge wa upinzani wakitumia muda mwingi kulalamikia kiti cha Spika.

“Kwa kipindi cha 2010 hadi 2015, Spika wa Bunge alikuwa Anne Makinda na Naibu Spika Job Ndugai. Wapinzani walimlalamikia sana spika wakimtuhumu kuwa anailinda serikali na kuwa kiti cha Spika kimemshinda."

Alisema picha ambayo Watanzania wanaipata kutoka kwa Kambi Rasmi ya Upinzani yenye nia ya kumng’oa Dk Tulia kwa kupiga kura ya kutokuwa na imani naye, ni mwendelezo wa wazi wa udhalilishaji wa wanawake kuwa hawana uwezo wa kuongoza.

Watu 50 Wauawa Baada ya mtu Mmoja Kushambulia klabu ya Mashoga Marekani

$
0
0
Raia wa Marekani, Omar Mateen, 29, ameishambulia kwa bunduki klabu ya mashoga iliyopo Orlando nchini Marekani.

Mateen, anayetokea Port St. Lucie Florida, ameua takriban watu 50 na kujeruhi wengine 53 na kushikilia mateka.


Polisi walitumia mabomu kumchanganya mtu huyo na kuwaokoa watu karibu 30 waliokuwa wameshikiliwa mateka. Mateen alipigwa risasi na polisi saa kumi na moja alfajiri baada ya tukio hilo kudumu kwa masaa matatu.

Hilo ni tukio baya zaidi la aina hiyo kuwahi kutokea Marekani. Maofisa kwenye hospitali ya Orlando wamedai vifo vinaweza kuongeza.  Muda mfupi kabla ya shambulio hilo, Mateen alipiga simu 911 kuelezea utii kwa kundi la ISIS.

Baba yake Mateen, Mir Seddique, aliiambia NBC News kuwa mwanae alichukia baada ya kuwaona wanaume wawili wakipigana busu huko Miami miezi kadhaa iliyopita.

Kulikuwa na takriban watu 320 ndani ya klabu hiyo na karibu 100 walishikiliwa mateka.

Freeman Mbowe na Viongozi Wengine wa Chadema Wakamatwa.....Alipo Zitto Kabwe Bado ni Utata

$
0
0
Wakati Polisi ikimshikilia kwa saa mbili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe mkoani Mwanza, jeshi hilo limefuta kongamano la kujadili Bajeti ya Serikali lililoandaliwa na ACT Wazalendo jijini Dar es Salaam huku kiongozi wake, Zitto Kabwe akisakwa.

Jeshi hilo lilizuia mkutano wa hadhara wa Chadema uliokuwa ufanyike wiki iliyopita mjini Kahama ambako lilitumia mabomu ya machozi kuwatawanya wanachama na wafuasi wa chama hicho, katika kile kilichoelezwa kulikuwa na dalili za uvunjifu wa amani.

Jeshi hilo pia lilizuia msafara wa viongozi wa chama hicho kuingia katika ofisi zake za Shinyanga walipokuwa wakielekea Mwanza.

Taarifa iliyotolewa jana na msemaji wa chama hicho, Tumaini Makene ilieleza kuwa mbali na Mbowe, jeshi hilo pia lilikuwa linawashikilia Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha), Patrobas Katambi na Katibu Mkuu wa Bavicha, Julius Mwita.

Wengine ni Mbunge wa Tunduma, Frank Mwakajoka na viongozi wengine na wanachama wa chama hicho waliokuwa wanashikiliwa katika kituo cha Polisi Nyakato, jijini Mwanza.

Makene alisema tangu asubuhi ya jana, Mbowe na viongozi wenzake walikuwa wakizunguka katika maeneo kadhaa ya jijini Mwanza kuwasalimia wananchi katika ‘vijiwe’ mbalimbali kabla hawajakamatwa.

Alisema, “Hadi sasa (saa 11 jioni) hakuna maelezo ya kushikiliwa kwao.”

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alithibitisha kukamatwa kwa viongozi hao na kubainisha kuwa waliachiwa bila kufunguliwa kesi yoyote.

“Walikutwa Igoma Sokoni wakizungumza na wananchi. Mikutano ya namna hii imezuiwa. Wamefungua kesi mahakamani, hivyo hakuna haja ya kufanya tofauti mpaka itakapohukumiwa,” alisema Msangi.

Alifafanua kuwa jeshi hilo halina uhasama wowote na Chadema au chama kingine chochote na "hatuwezi kukiingilia kinapofanya mikutano yake ya ndani au hotelini. Kilichozuiwa ni mikutano ya hadhara.”

Wakati Msangi akisema hayo, kongamano la ACT Wazalendo ambalo lilitakiwa lifanyike jana kuanzia saa 7:00 mchana kwenye Ukumbi wa Jengo la LAPF; Millennium Towers, Kijitonyama lilizuiwa na polisi.

Tangu mapema asubuhi, askari polisi walitanda katika eneo la ukumbi huo kuzuia kongomano hilo.

Ukumbini hapo, waandaaji walisema hakuna anayeruhusiwa kuingia kwani wamepewa maelezo ya kuufunga baada ya tukio lililoandaliwa kuahirishwa.

Zaidi ya viti 210 vilikuwa vimepangwa kwa ajili ya kongamano hilo na mmoja wa viongozi wa ukumbi huo alionekana akiondoa mabango yaliyokuwa yanautambulisha mkutano huo wa ACT.

Viongozi watatu wa ukumbi huo walikataa kueleza kinagaubaga juu ya sakata hilo, lakini taarifa za jumla zilisema mkutano umezuiwa.

Mmoja wa watumishi wa ukumbi huo, alisema: “Tuliandaa kila kitu, ila shughuli imeahirishwa. Ukumbi unatakiwa kufungwa. Hautatumika kwa leo.”

Ilipofika saa 5:00 asubuhi, Msemaji wa ACT-Wazalendo, Abdallah Khamis alisema chama kinafanya mkutano wa dharura kwenye ofisi zake za makao makuu na baadaye kingezungumza na waandishi wa habari.

Saa 8:00 mchana, Mwenyekiti wa ACT Wazalendo, Anna Mghwira akiwa na viongozi wenzake, isipokuwa Kiongozi wa Chama, Zitto Kabwe alikuwa mbele ya kamera za wanahabari akifafanua kilichotokea kwa wanachama, wafuasi wa chama hicho na Watanzania kwa ujumla.

Alisema ilipotimu saa 4:00 asubuhi walipewa taarifa na mwenye ukumbi kuwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni limemjulisha kuwa chama hicho hakina kibali cha kuendesha kongamano hilo na kwamba kisiruhusiwe kufanya hivyo.

“Huku ni kufifisha demokrasia. Wapigania haki za kiraia wasimame imara na vyama vya upinzani katika kuilinda,” alisema Mghwira.

Wakati kongamano hilo likizuiwa, kuna taarifa za kukanganya juu ya alipo Zitto baada ya kudaiwa alikuwa anasakwa na polisi tangu juzi.

Taarifa hizo zinakuja siku chache baada ya kiongozi huyo kuitwa Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam na kuhojiwa juu ya kauli alizozitoa kwenye mkutano wa hadhara zinazokosoa utendaji wa Serikali na kupinga matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar.

Baadaye jioni, Kaimu Katibu Mkuu wa chama hicho, Msafiri Mtemelwa alitoa taarifa kuwa Zitto ametoweka na hajulikani alipo. Hiyo ilikuwa ni baada ya askari kanzu kumtafuta kwa muda kwa saa kadhaa.

“Zitto amekuwa akitafutwa kwa muda mrefu. Askari wanalinda nyumbani kwake tangu jana (juzi) usiku. Hivi sasa ametoweka, hatujui alipo. Lolote litakalompata, Jeshi la Polisi litajibu,” alisema Mtemelwa.

Awali, Mghwira alipoulizwa imekuwaje kuhusu Zitto alijibu kuwa mkutano ulikuwa wa dharura ndiyo maana viongozi wote hawakuwapo.

Exclusive: Wastara Juma Anasa Ujauzito.......

$
0
0
Exclusive! Habari mpya ya motomoto ni kwamba, staa wa sinema za Kibongo, Wastara Juma amenasa ujauzito, Risasi Jumamosi linakuwa la kwanza kukupa mchapo huu!
Ujauzito huo ni wa aliyekuwa mumewe, Sadifa Juma, mbunge wa Jimbo la Donge, Visiwani Zanzibar ambapo kitendo cha mimba hiyo kuwa ya mbunge, kimemsumbua Wastara hadi kuamua kuondoka ili akapate muda mzuri wa kutafakari nchini Msumbiji.

Taarifa kutoka kwa vyanzo, zinaeleza kuwa Wastara alipoondoka nchini, aliwaaga baadhi ya mastaa wenzake kuwa anakwenda kufuata biashara zake za nguo nchini humo lakini Risasi Jumamosi lilichimba na kupata ubuyu ulionyooka kuwa aliondoka nchini kwa ajili ya kwenda kutafakari ujauzito huo.

NDUGU AVUJISHA UBUYU KAMILI
Ndugu wa karibu na Wastara ambaye hakupenda jina lake lichorwe gazeti, amefunguka kuwa baada ya Wastara kuachika, aligundua ni mjamzito hivyo alichanganyikiwa na kuamua kwenda Msumbiji kwa ajili ya kutafakari zaidi ujauzito huo.
“Hakuwa na jinsi kwani akiangalia alishatoka kwa mwanaume, angewezaje kumwambia kuwa ana ujauzito wake? Akaamua kukimbilia huko kwa ajili ya kujipanga ingawa anavyoonekana anatamani amzalie mbunge huyo,” alisema ndugu huyo.

NDUGU AZIDI KUTIRIRIKA
Ndugu huyo alizidi kushusha ‘vesi’ kuwa mimba ya Wastara inasadikiwa kuwa na miezi miwili au mitatu kwani tangu aachane na mumewe huyo, alikuwa akiumwaumwa na wakati mwingine alikuwa akitapika hovyo ambapo mwanzo alificha lakini yalipomfika shingoni alifunguka.
“Alitufichaficha lakini baadaye akawa hana jinsi, akaona atueleze na sisi tumemshauri tu aende akapumzike na ajiandae kutuletea kiumbe kipya,” alisema ndugu huyo.
Baada ya habari hiyo kutua Risasi Jumamosi,  Wastara alitafutwa kwa njia ya simu ya mkononi, akafunguka:

“Dah! Sijui niseme nini, kiukweli watu wanaongea sana, nimeondoka nchini kwa shughuli zangu binafsi lakini maneno ni mengi, wewe si wa kwanza kunipigia simu. Sikutaka kuongea kabisa juu ya masuala yangu ya ndoa iliyopita wala maisha yangu kwa jumla.”

Risasi Jumamosi: Kwa nini unaongea hivyo wewe funguka swali nililokuuliza, una ujauzito au la?
Wastara: Ndiyo, kwani cha ajabu ni nini? Yule niliyekuwa nalala naye si shangazi yangu, kila mtu anajua niliolewa na aliyenioa (Sadifa) wala si mjomba wangu.

TUJIKUMBUSHE
Wastara aliachika Aprili, mwaka huu baada ya kufunga ndoa na Mbunge wa Jimbo la Donge, Sadifa Juma ambapo ndoa yao ilidumu kwa muda kwa miezi mitatu tu na kuvunjika.

GPL

Freeman Mbowe Azungumza Haya Baada ya Yeye na Wenzake Kukamatwa na Polisi Mwanza

$
0
0
Baada ya kukamwatwa jana na kuhojiwa na polisi, jijini Mwanza, akiwa na baadhi ya viongozi wa Kanda ya Ziwa na wanachama wakati akizungumza katika ‘vijiwe’ vya chama hicho, Mwenyekiti wa (Chadema), Freeman Mbowe, amesema kukamatwa kwake kunaonyesha polisi wanavyoleta utawala wa kutisha wananchi ili wawe na hofu. “Polisi wasilete utawala wa kutisha wananchi. Viongozi ni wajibu wao kuzungumza na wananchi ili kufahamu matatizo yao pamoja na kuimarisha chama,” amesema Mbowe.
Toa maoni yako huku ukituambia unadhani nani ni tatizo?

Nuh Mziwanda Amuumbua Upya Shilole

$
0
0
Msanii anayefanya poa kwenye Bongo Fleva, Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ amemuumbua upya aliyekuwa mwandani wake, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ kwa kuanika A-Z ya namna alivyokuwa anamnyanyasa kwenye uhusiano wao wa kimapenzi kiasi cha kuamua kuachana naye. Wikenda limeinyaka.

Akizungumza na Wikienda mara baada ya kuachia video ya wimbo wake mpya wa Jike Shupa huku ndani yake akigusia kiduchu figisufigisu alizokutana nazo kwenye uhusiano huo akimtumia mrembo anayefanana na Shilole ‘Shilole bandia’.

Nuh aliliambia gazeti hili kuwa alishindwa kustahimili kuacha matukio ya uhusiano wake yapite hivihivi bila kuyagusia kidogo kwenye wimbo wake huo kwa sababu alihisi watu hawamuelewi kile alichokuwa anakisema juu ya Shilole.

“Nimeamua kufanya hivi ili Watanzania waone jinsi Shilole alivyokuwa ananifanyia kupitia mtiririko wa matukio kwenye kichupa changu. Kiukweli inaumiza sana lakini hivyo ndivyo roho yake ilivyo, sijali ataumbuka kwa kiasi gani lakini hizo ni hisia zangu ambazo nimeamua kuziweka upya,” alisema Nuh huku akiongeza kuwa kwa sasa yuko kwenye uhusiano na mwanadada aitwaye Nawal.

Hata hivyo, baada ya gazeti hili kuchonga na Nuh lilimtafuta Shilole ambaye alipoulizwa juu ya sakata hilo alidai kuwa hataki kumzungumzia Nuh wala kusikia habari zake maana hata video yenyewe hawezi kuiangalia.

“Sitaki kusungumzia habari za mtu mwingine, no coment, labda kama kuna ishu nyingine unaweza
kuniambia,” alisema Shilole. Shilole na Nuh waliachana miezi kadhaa iliyopita ambapo mrembo huyo alidai alikuwa akimlea jamaa huyo hivyo Nuh naye ameamua kueleza ukweli namna ambavyo Shilole aligeuka mwanamasumbwi ndani ya nyumba.

Zitto Kabwe Ajitokeza Adai Polisi Wanamsaka..Asema Magufuli Alienda Rwanda Kujifunza Kubana Upinzania

$
0
0



DAR: Zitto Kabwe ajitokeza, adai Polisi wanamsaka. Asema Rais Magufuli alienda Rwanda kujifunza jinsi ya kubana Vyama vya Upinzani.

Ataka CCM imdhibiti Rais Magufuli, asema wakishindwa wao wapinzani watamdhibiti



Mwigulu Nchemba Aapishwa Rasmi Kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.......Atoa ONYO Kali kwa Wauza Dawa za Kulevya

$
0
0

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba amewataka wafanyabiashara haramu ya kuuza madawa ya kulevya kuacha mara moja biashara hiyo badala yake watafute shughuli halali za kujiingizia kipato.

Waziri Nchemba ametoa agizo hilo mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyemteua kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Mh.Charles Kitwanga ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

Aidha Waziri Nchemba alisema kuwa atahakikisha anasimamia Ulinzi na Usalama wa Raia na Mali zao kwa kuziba mianya inayohatarisha amani na utulivu katika nchi.

Naye Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba amesema kuwa atahakikisha anashirikiana na wataalum wa sekta tatu zilizo katika Wizara yake ili kufanya mapinduzi katika maeneo hayo yaliyoajiri zaidi ya asiimia 80 ya Watanzania.

Pia Waziri Dkt. Tizeba alisema kuwa Wizara itahakikisha inashugahulikia changamoto zinazozokabili vyama vya ushirika ambavyo vimekuwa havifanyi vizuri katika miaka ya hivi karibuni.

Mawaziri walioapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam ni Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba aliyekuwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi anayejaza nafasi iliyoachwa wazi baada ya Rais kutengua uteuzi wa Mh. Charles Kitwanga.

Gwajima Afyatuka Tena, Amshauri Magufuli Aihame CCM....Adai Amenasa Njama Mbaya

$
0
0
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima ambaye anafahamika kwa kutoa kauli ‘tata’, amefyatuka tena akimshauri Rais John Magufuli kuihama CCM endapo kile alichokiita ‘njama alizozibaini’ ndani ya chama hicho zitaletwa mezani.

Gwajima ambaye amekiri kuwa katika kampeni alikuwa hamkubali Dk. Magufuli kutokana na kutokuwa na imani na CCM, amesema amemkubali  sana baada ya kuanza kazi ya urais kutokana na hatua ambazo amekuwa akizichukua ndani ya muda mfupi.

Akizungumza katika ibada ya Jumapili kanisani kwake, Gwajima ameeleza kuwa amebaini njama za baadhi ya wanachama wa CCM ambao ‘dili’ zao mbalimbali ikiwa ni pamoja na ‘flow meter’ ya mafuta yaingiayo nchini na makontena yaliyokamatwa yalikuwa yanawahusu, wameanza kampeni ya chinichini nchi nzima kutaka Rais Magufuli asipewe uenyekiti wa chama hicho.

Amesema kuwa watu hao wanazunguka nchi nzima kuwashawishi wanachama wa CCM kuridhia hoja ya kutenga uenyekiti wa chama na urais, ili kumnyima nafasi hiyo Rais Magufuli ambaye utendaji wake umewabana bila kujali ni wa chama chake.

Hivyo, amemshauri Rais Magufuli kuwa endapo itatokea hilo, akihame chama hicho na kuendelea na kazi yake kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Msikilize Hapa:

Video ya wimbo ‘Jike Shuka’ ya Nuh Mziwanda yamtoa povu Shilole..Adai Nuhu ni Mshamba Asiyejua Hata Kubadilisha Boxer

$
0
0
Ikiwa ni siku chache toka Ex wa Shilole, Nuh Mziwanda aachie video ya wimbo ‘Jike Shupa’ ambayo inaelezea jinsi alivyoishi na mpenzi wake huyo, Shilole ameonyesha kukasirishwa na kazi hiyo.

Nuh amethibitisha kwamba Shilole ndiye aliyemuimbia kwenye wimbo huo, kwa kumtumia video queen anayefanana na Shilole kama pacha katika video ya wimbo huo.



Sholole baada ya kuona video hiyo, aliandika ujumbe instagram ambao baadae aliutoa:

"Wale unaongozana nao wanaweza kuwa mizigo au Baraka. Shukrani za dhati kwani kwenye mashabiki zangu ambao ni baraka na pole sana wasanii wote mnaodhani bado tupo dhama za kutumia mgongo wa mtu mwingine kuweza kutoboa. Kipaji siyo maneno ila ni vitengo. Umemiss mkong’oto?. Sipendagi mwanaume mjinga ndiyo maana umekula mkong’oto wa kutosha… Mshamba usiyejua hata kubadilisha boxer, niweke mbali na maisha yako. Nikifungua mdomo wangu utadhalilika....." Shilole

Shilole na Nuh Mziwanda waliachana miezi kadhaa iliyopita ambapo Nuh amekuwa alizungumzia mengi yaliyomkuta wakati akiwa kwenye mahusiano na mwanadada huyo, huku Shilole akitaa kuzungumzia kilichotokea.

Zitto Kabwe Afunguka Tena ''CCM Wamdhibiti Magufuli, na Wasipomdhibiti Sisi na Watanzania Tutamdhibiti"

$
0
0
Baada ya taarifa za kutoweka, Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ameibuka leo na kusema yuko salama wa afya huku akilaani mbinu za Jeshi la Polisi kutaka kumkamata kwa siri bila kufuata utaratibu unaotakiwa.

Tangu Jumamosi usiku, vyombo mbalimbali vya habari viliripoti Zitto kutofahamika alikokuwa baada ya simu zake zote kutopatikana huku viongozi wa chama hicho wakihofia kukamatwa na polisi baada ya kubaini njia za uviziaji wa kumkamata nyumbani
kwake.

"Ilikuwa Jumamosi , walikuja nyumbani kwangu wakiwa na magari matatu ila hawakufanikiwa, siwezi kukamatwa kwa `terms' zao ila nitakuwa tayari kukamatwa kwa `terms' zetu na wala siyo kuviziana, kama nina makosa kwa nini wanivizie," amesema Zitto Kabwe na kuongeza;

''Watu wetu wa Usalama wa Chama walihakikisha kwamba sitakamatwa ili niweze leo kupata fursa kuzungumza na watanzania kupitia nyie wana habari

''Hatufahamu Watawala wanaogopa nini mpaka kuzuia mikutano ya wanasiasa

''Nasikia Jana Walimkamata Mwenyekiti Mbowe wa Chadema Huko Mwanza kisa eti kawasalimia wananchi, huu ni uvunjwaji na ukiukwaji mkubwa wa utawala wa kidemokrasia

''Tunalaani tabia za Kidikteta za Rais Magufuli .Magufuli ameanza na vyama vya siasa kuonyesha Udikteta wake, nawahakikishia akimalizana na Vyama vya siasa atahamia kwenu Wanahabari, Tumkatalie

''Ndio maana Magufuli Ziara yake ya Kwanza alifanya Rwanda, tumegundua kuwa alikwenda kujifunza namna ya Kudhibiti Demokrasia na Kuongoza Kidikteta

''Hauwezi kupambana na Ufisadi kama haumpi nguvu ya Kiutendaji wa CAG. Kwa hali Hii anayokwenda Magufuli ajiandae kuwa rais wa term moja kwa sababu watanzania hawataweza kuvumilia kutawaliwa, kuminywa na kuburuzwa .

''CCM wamdhibiti Magufuli, na wasipomdhibiti sisi na Watanzania Tutamdhibiti

''Hatutakaa Kimya hata kama atatufunga, akimfunga Zitto watazaliwa wakina Zitto wengine, na kwenye hili hatutakaa Kimya, tutasimama kidete mpaka nchi irudi kwenye misingi''

''IGP ameagizwa na Magufuli anikamate, lakini hawezi kunikamata bila kufuata utaratibu, hawawezi kunikamata kwa kunivizia, viongozi hatukamatwi kwa kuviziwa viziwa, tumewaonyesha kwamba Polisi wanaweza kutukamata kwa kufuata terms zetu na sio zao

''Karibuni kesho saa tisa kwenye Kongamano letu, Hatuwezi kuacha kufanya siasa, lazima tuendelee kufanya siasa, mmehudhuria mikutano yetu hamjaona hata sisimizi amekanyagwa

''Wanasema Bajeti imeongezeka kwa 32% ukweli ni kwamba Bajeti imeshuka kwa maana Dola imeporomoka''

Manispaa ya Ilala Yakusanya Sh Bilioni Moja Ndani ya Siku Tano

$
0
0

Manispaa ya Ilala imekusanya Sh1 bilioni ndani ya siku tano, ikiwa ni mkakati wao wa kuhakikisha wanafikia lengo la kupata mapato ya Sh55 bilioni katika miezi sita ya mwanzo ya Serikali ya awamu ya tano.

Meya wa Ilala, Charles Kuyeko aliyembatana na Naibu Meya Omary Kumbilamoto na Mkurugenzi wa manispaa hiyo, Isaya Mngurumi  amewaambia wanahabari  leo kuwa mapato hayo yamekusanywa  kutoka katika vyanzo mbalimbali ikiwamo kodi ya majengo.

Kuyeko amesema mafanikio hayo ya kukusanya kiasi hicho cha fedha pia,  yametokana na kikosi kazi kilichoundwa na manispaa hiyo ambacho kina lengo ya kufuatilia ukusanyaji wa mapato kwa muda wa mwezi mmoja.

“Kila hatua tutakayofikia tutakuwa tukitoa taarifa. Kuhusu kampeni  hii ya ufuatiliaji wa ukusanyaji wa mapato,” amesema Kuyeko.


Askari Wasiopigia Saluti Wabunge Kukatwa Mishahara

$
0
0


Agizo hilo limetolewa leo bungeni na Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, William Tate Ole-Nasha wakati akijibu swali la nyongeza kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani la mbunge wa viti maalum kutoka Zanzibar Fakharia Shomari aliyetaka kujua ni kwanini askari wa jeshi la polisi hawapigi saluti kwa wabunge.

Katika maelezo yake, Ole Nasha amesema kuwa askari wote nchini ni lazima wazingatie taratibu hizo, na kwamba wanapaswa kupiga saluti kwa wabunge kila wanapowaona, na endapo hawatafanya hivyo, watakumbana na adhabu za kijeshi.

Ametaja baadhi ya adhabu watakazokabiliana nazo kuwa ni pamoja na kukatwa mshahara, kufanyausafi wa mazingira, kuondolewa kikosini kwa muda n.k. na amewataka wabunge ambao hawatapigiwa saluti, kuripoti haraka mahali husika.

Akiongozea majibu hayo, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi amesema agizo hilo linakwenda hadi kwa askari wa makampuni binafsi ya ulinzi ambao mara nyingi hupuuza kutoa heshima hiyo kwa viongozi hususani katika mabenki.


Wanasayansi: Mugabe ana Vinasaba vya Kuishi Milele

$
0
0

WANASAYANSI maarufu kutoka Taasisi moja kubwa ya Sayansi nchini Uingereza wametoa ripoti ya utafiti walioufanya ikithibitisha kwamba, Rais wa Zimbabwe, Komrade Robert Mugabe amegundulika kuwa na vinasaba (genes) ambavyo vitamfanya aishi milele (asife).



Robert Mugabemiaka ya 1980.


Utafiti huo wa siri unaongozwa na Daktari Irvin Koch umegharimu mabilioni ya fedha na kugundua pia kwamba Bob Robert mwenye miaka 92 sasa haweki dawa kichwani (SUPER BLACK) wala hajawahi kukata nywele zake licha ya kutojihangaisha na kula vyakula vya mimea (veggies) ama kwenda gym kufanya mazoezi.


Katika tafiti hiyo, Wanasayansi hao walichukua sampuli mbalimbali kutoka kwa Bob ikiwemo damu yake, nguo zake, miswaki aliyokuwa akitumia, na hata chanuo kwa miongo kadhaa na kugundua kuwa hakuna hata chembe ya umauti kwa Mugabe.

Baadhi ya watu wameanza kuamini kuamini tafiti hizo baada ya kugundua kutoka kwenye picha za Mugabe akiendelea kupeta katika muonekano huohuo huku akiwa mwenye siha ya haja kwa miaka mingi sasa.


Mpinzani wake mkuu kwenye siasa za Zimbabwe ambaye ni Kongozi wa Chama cha MDC, Morgan Tsvangirai (ama kwa kuguswa kwamba ausahau uraisi) amejibu kwa kejeli kwamba ‘Mugabe ni makusanyo ya nyama na mifupa kama hayawani wengine wote’ na kwamba kila nafsi itaonja mauti (Kulu ‘nafsi dhaaikatul ‘maut).

Inasemekana kwamba utafiti huo unaendelea mpaka mwaka 2018 ndipo utakamilika.

Source: Newssa/Mzansi Satire



Prof. Ibrahim Lipumba Aomba Kurudia Nafasi yake ya Uenyekiti wa CUF

$
0
0
Aliyekuwa mwenyekiti wa CUF Prof. Ibrahim Haruna Lipumba amemuandikia barua Katibu Mkuu wa Chama hicho Maalim Seif Sharif Hamadi ya kuomba kutengua barua yake ya mwaka yana ya kujiuzulu nafasi yake ya uenyekiti wa chama hicho

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Prof Lipumba amesema kwamba ameandika barua hiyo na anasubiri uamuzi wa chama hicho kama utaamua kumrejesha au la.
Hatua ya Lipumba inatokana na Chama cha CUF kutangaza uchaguzi wa kuziba nafasi zilizo wazi katika chama hicho ikiwemo nafasi ya uenyekiti iliyokuwa iliyokuwa wazi baada ya kujiuzulu kwa lipumba.

Nisha Amjibu JackWolper

$
0
0
Staa wa sinema za vichekesho Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’ ameibuka na kumjibu mwigizaji mwenzake, Jacqueline Wolper Massawe kuwa hajawahi kutaka ‘kiki’ za kijinga wala ugomvi na anachoangalia yeye ni biashara na maisha yanaenda.

Nisha aliliambia Wikienda kuwa ameshangazwa na habari zinazozagaa mitandaoni baada ya yeye kuweka picha za wasanii wanne kisha msanii mwenzake, Wolper kuanza kumrushia maneno wakati yeye aliandaa shoo ya Harmonize (mpenzi wa Wolper) wiki mbili zilizopita na yupo kibiashara zaidi kwani bado ana shoo mbili ameandaa ikiwa ni pamoja na shoo ya mwezi huu wa Ramadhani ambayo itakuwa ni ya mahadhi ya mwezi huu.


“Huwa nawashangaa wasanii wengine, mimi sijawahi kupenda alipopenda msanii mwenzangu, tena ambapo ninajua kabisa kuwa huyu yupo huwa siingii kabisa kwa wakati huo, kama mnavyojua uhusiano wao uko wazi hivi naingiaje?

“Kuhusu kiki kuwa imepangwa ili kumuangusha Mr Blue na wimbo wake (Mboga Saba) ni ishu za uongo labda kama wamepanga wao,” alisema Nisha.

Chanzo cha maneno haya yote ni baada ya ujumbe unaosambaa mtandaoni kuwa Nisha alitaka kujiweka kwa Harmonize ndiyo maana akaandaa shoo kwao na msanii huyo ambapo Wolper aliishtukia na kuamua kuongozana na mpenzi wake huyo.

Waziri Mwigulu Nchemba Apokelewa Makao Makuu Ya Wizara Ya Mambo Ya Ndani.

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akiweka saini mara baada ya kuwasili Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi muda mfupi baada ya kuapishwa kwake. Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Balozi Yahya Simba.(Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).

Polisi Wamtia Mikononi Zitto Kabwe Wamhoji Kwa Dakika 90.....

$
0
0
Kiongozi mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe  asubuhi ya leo June 13 2016 alikutana na wanahabari na kuzungumzia kuhusu polisi kuzuia kongamano ambalo liliandaliwa na chama hicho ili kujadili bajeti. Pia alizungumzia kuhusu yeye kusakwa na polisi kwa kuviziwa na sio kwa utaratibu wa wito.

Leo jioni  Zitto Kabwe alipokea wito wa kuhitajika Central polisi kwa mahojiano ambayo yalichukua zaidi ya dakika 90 .

Baada ya  kutoka kwenye mahojiano aliyepata nafasi ya kuzungumza ni wakili wa chama hicho Steven Mwakibolwa ambaye ameeleza sababu za wito huo kituoni hapo.

"Wamechukua maelezo ya Zitto kufuatana na kongamano la chama lililokuwa limezuiliwa jana.Baada ya mahojiano na mazungumzo na polisi, chama kitatoa taarifa rasmi juu ya nini kitafuta baada ya hapa." Amesema Mwakibolwa

"Kama alivyoeleza mwanasheria tumemaliza mahojiano na polisi kwa hiyo kesho tutatoa kauli yetu ya hatua inayofuata, nimeitwa polisi nimekuja, wanachama watulie tunaendelea na majadiliano na polisi ili tuendelee na kazi zetu za kisiasa kama kawaida" Amesema Zitto Kabwe

Madai ya Sumu Ofisini Kwa Meya wa jiji la Mwanza yasababisha Kikao Kuvunjika....

$
0
0
Kikao cha kamati ya fedha na uongozi cha halmashauri ya jiji la Mwanza, kimevunjika baada ya Meya wa jiji hilo James Bwire kulalamikia harufu kali, inayohisiwa kuwa ni sumu iliyokuwa ikitoka kwenye kiyoyozi ndani ya ofisi yake, huku watumishi wawili wa jiji hilo wakishikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi.

Mkurugenzi wa jiji la Mwanza, Adam Mgoyi amethibitisha kusambaratika kwa wajumbe wa kikao hicho.

Watumishi wanaohojiwa na jeshi la polisi ni katibu muhtasi wa ofisi ya mstahiki Meya Gladys Chiduo pamoja na karani wa ofisi hiyo Anselemi Mtobesya.

Mstahiki Meya James Bwire, ambaye mwezi aprili mwaka huu alilazwa katika hospitali moja jijini Nairobi nchini Kenya kwa muda wa mwezi mmoja baada ya kudaiwa kuanguka ghafla ofisini kwake, anaeleza hali aliyoikuta ofisini kwake wakati alipoingia maliwatoni kwa ajili ya kujisaidia wakati kikao hicho kilipokuwa kinaendelea.

Diwani wa kata ya Mbugani Mahamoud Jama pamoja na Hanifa Mhere ambaye ni diwani wa viti maalum wanasimulia kwa kina kuhusiana na tukio hilo ambalo limetokea hii leo baada ya wajumbe wa kamati hiyo kumaliza kutembelea miradi ya jiji iliyopo eneo la Community Centre kata ya Mirongo na Sinai kata ya Mabatini ambako eneo kwa ajili ya machinga limetengwa.
Viewing all 104701 articles
Browse latest View live




Latest Images