Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live

Uongozi wa Geita Gold Mine Wakanusha Tuhuma za Wanawake Kulazimishwa Kufanya Mapenzi na Mbwa zilizotolewa na Mbunge

$
0
0
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Afisa Uhusiano na mawasiliano wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita(GGM), Tenga B. Tenga jijini Dar es Salaam leo.

UONGOZI wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) umekanusha tuhuma zilizotolewa na Mbunge wa Geita vijijini kwa tiketi ya CCM, ndugu Joseph Kasheku (Msukuma) kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Juni 10, mwaka huu katika kijiji cha Nyakabale Mkoani Geita.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Afisa Uhusiano na mawasiliano wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita(GGM), Tenga B. Tenga amesema kuwa tuhuma hizo hazina ukweli wowote.

"Mbunge huyo alisikika katika mkutano wa hadhara kuwa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) huwalazimisha wanawake wanaoingia mgodini bila kibali kufanya mapenzi na Mbwa watumikao kulinda eneo la Ngodi"

Tenga amesema kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa kwa uzito mkubwa dhidi ya Mbunge huyo kwani taarifa hizo ni za uongo na zinalenga kuchafua na kutuharibia sifa mbele ya serikali, wadau mbalimbali wa maendeleo pamoja na jamii kwa ujumla.

Amesema kuwa Mbunge wa Geita vijijini kwa tiketi ya CCM, ndugu Joseph Kasheku (Msukuma) amekuwa akitoa kauli mbalimbali kuwa ni za kichochezi na zinapelekea uvunjifu wa amani kwa wakazi wa Mkoani Geita.

Pia ameviomba vyombo husika vilivyopewaa maagizo kuchunguza tuhuma hizo vifanye kazi yake kwa kuzingatia haki na sheria ili ukweliujulikane na sheria ichukue mkondo wake amesema Tenga.

Nape NNAUYE amewapongeza Dk. SLAA na Prof. LIPUMBA, amesema wamejitambua kisiasa na kujitenga

$
0
0
Siku za karibuni kumekua na picha nyingi zmesambaa zikimwonyesha Wema Sepetu akiwa na umbo ambalo watu wengi hawakulielewa na wengi walikimbilia kusema kua Wema anatumia dawa za mchina kungeza makalio. Team Wema wengi walijitokeza na kumtetea Wema kua zile picha zilikua Edited huku wengine wakimlaumu Wema kwa hali aiyofikia.

Waswahili wanasema mtoto kwa mama hakua na ara tu baada ya mama Wema kuzisikia habari hizo aliamua kuvunja ukimya na kuwachamba wale wote wanaomsema vibaya mwanae kua katumia mchina. Unaweza tazama video hii hapa 

Hivi vichwa vya habari Magazeti ya leo ni hatari kwa uhai wa Taifa, Serikali ijitazame upya

$
0
0
Sitaki niseme mengi ila tu nashauri Serikali ijitafakari, vichwa vya habari kama hivi tumezoea kuvisikia kwenye vyombo vya habari vya wenzetu, kwa kifupi vichwa hivi vya habari si vya kuvichekelea kwa sababu tu hayajakupata au kwa sababu yanaowafika si wa kundi lako ila ni vya kuchukua tahadhari sana, madhara yake huwa si madogo.

Serikali kuna mahali inakosea lazima ikosolewe, huwezi kutumia nguvu nyingi kiasi hiki kubinya Demokrasia, mshaurini vizuri Mkuu wa Kaya, Uhuru hauzuiliki kwa kitisho cha Bunduki na Mahakama zisizotenda Haki.

Hii ni dalili mbaya. "Taifa la hofu , mwisho wake ni majuto".

Wapo wenye akili ndogo watakaosema "Ukawa yamewafika, wameanza kulalama mitandaoni", lakini na mimi nawaambia "Si kila anayesema kweli ni UKAWA" sisi wengine hatuna hata mpango wa kutafuta Kadi za vyama, Chama chetu ni "Tanzania". Tusizibe midomo na Gundi za Mbao kisa tu tunatafuta Ukuu wa Wilaya

Huu ni Ushauri wangu

Msanii Rashid Abdallah Makwiro 'Chid Benz' ajiunga katika lebo ya WCB

$
0
0
Msanii maarufu wa miondoko ya kufoka/kurapu Rashid Abdallah Makwiro al maarufu kama CHID BENZ amejiunga rasmi katika lebo ya Wasafi Classic Baby WCB mchana Iliyo chini ya mwanamuziki machachari kabisa Diamond platnumz.

Taarifa hizi zimepatikana kupitia mtu wa karibu sana wa Babu Tale. Na pia kituo cha kuaminika cha redio yaani CloudsFM kimetaarifu mchana wa leo.....

Naibu Spika Aendelea Kuwatesa Wapinzani Kwa Kuendelea Kuendesha Bunge Licha ya Wapinzani Kugoma Kuingia Bungeni

$
0
0
Kwa kawaida, Spika wa Bunge, Job Ndugai au naibu wake wanapokuwa na shughuli nyingine, huachia kiti hicho kwa wenyeviti watatu wa Bunge kuendesha vikao, lakini safari hii Dk Tulia amekuwa akiingia kila siku asubuhi na jioni.


Mei 31, mwaka huu wabunge wote wa upinzani walianza kususa vikao vinavyoendeshwa na kiongozi huyo kwa madai ya kutokuwa na imani naye, hasa baada ya kuzuia hoja ya kufukuzwa kwa wanafunzi 7,802 katika chuo cha Udom.


Hoja hiyo iliwasilishwa na Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari lakini Dk Tulia alisema haikuwa na umuhimu kwa wakati huo, jambo lililozua tafrani baina ya kiongozi huyo na wabunge wote wa upinzani.


Kutokana na hali hiyo, wabunge hao walipitisha azimio la kususa vikao vinavyoendeshwa na kiongozi huyo na tangu siku hiyo, kila anapoingia bungeni kuongoza kikao wamekuwa wakitoka ukumbini.


Spika wa Bunge, Job Ndugai ambaye kwa sasa yuko nchini India kwa matibabu, amekuwa akisaidiwa na Dk Tulia pamoja na wenyeviti watatu wa Bunge ambao ni Mbunge wa Ilala (CCM), Mussa Azzan Zungu, Mbunge wa Bariadi Andrew Chenge
Tangu wabunge wa upinzani waanze kususa vikao vinavyoongozwa na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson, kiongozi huyo wa Bunge ameamua ‘kukomaa’ na kiti hicho, hatua inayosababisha wapinzani wasipate fursa ya kutia mguu bungeni.

Mbunge wa Arumeru Joshua Nassari na Wenzake Wanne Wafikishwa Mahakani

$
0
0
MBUNGE wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari na wenzake wanne ambao ni madiwani wa Halmashauri ya Meru wilayani Arumeru, wamesomewa shitaka la kuharibu uzio eneo la Leganga wilayani humo.


Walisomewa shitaka lao mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Augustine Rwezile jana.


Mwanasheria wa Serikali, Gaudensia Joseph alidai Nassari na wenzake ambao ni Paulo Samuel, Japhet Joseph, Zephania Mwanuo na Anderson Sikawa kwa pamoja na madiwani wenzao 24, ambao walisomewa shitaka lao awali waliharibu uzio wa Naftani Makere.


Joseph alimuomba Hakimu Rwezile kuwaongeza washtakiwa hao watano akiwemo Mbunge Nassari, ambapo awali katika shitaka lao linalowakabili mahakamani hapo, hawakuwepo mahakamani kwa sababu mbalimbali. Alidai wanashtakiwa kwa kuharibu uzio, Mei 4 mwaka huu, eneo la Leganga wilaya ya Meru.


Alidai walisababisha hasara ya Sh milioni 7 kwa kuharibu uzio huo. Wote walikana mashitaka. Mawakili wanaowatetea watuhumiwa hao ambao ni Charles Abraham na Gift Joshua, waliomba dhamana kwa wateja wao.


Hakimu Rwezile alikubali ombi la wakili huyo kutoa masharti ya dhamana ya kusaini Sh milioni moja na kila mmoja kuwa na mdhamini mmoja. Walitimiza masharti hayo na kuachiwa kwa dhamana.


Washtakiwa wengine waliofikishwa awali ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Meru, Willy Njau (Chadema) na Makamu Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Nelson William. Wengine ni Elisa Stephen, Digna John, Dina Erick, Wilson Fanuel, Josephine Anael, Samuel Ismail, Agness Eliya, Isack Afitwe na Neema Isack.


Washtakiwa wengine ni Gadiel Stanley, Jeremiah Masawe, Peter Efatha, Benard Wilson, Henry Benjamin, Emanuel Pendael, Fadhila Joseph, Penzila Palangyo, Mary Antony, Roman Laurance, Bryson Mosses, Franck Ngoye na Eveline Julius.


Kesi hiyo iliahirishwa hadi Juni 28 mwaka huu itakapotajwa tena kwa kuwa upelelezi haujakamilika.

Mwanamuziki Linah Sanga Aweka Hisia zake za Mapenzi Kwa Mwanamuziki Darasa..Adai Anatamani Kuzaa Naye

$
0
0
Linah amesema anatamani kuzaa na mwanaume mwenye sifa kama za rapper Darassa.

Muimbaji huyo amesema kwa jinsi ambavyo amewahi kukaa na Darassa na kumsikia akiongea kwa muda mfupi, alibaini kuwa anaweza kuwa baba mzuri.

“Ni mtu ambaye ana sifa zote za kuweza kuwa mwanaume ambaye namtaka. Namchukulia kama kaka yangu yaani sijawahi kumfeel kimapenzi lakini nimekaa naye kwa muda mfupi, nimemuona ni mtu fulani mwenye busara. Ni mwanaume ambaye nikimuona nasema ‘this guy, I wish ningekuwa nina hisia za kimapenzi naye. Katika wasanii wote I wish my boyfriend angekuwa hivi,” Linah ameiambia 255 kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM.

Ameongeza kuwa Darassa anajua kuwa anakumbali na rapper huyo pia anamkubali Linah na ukaribu wao ni wa kama kaka na dada tu.

Wasomi Wamponda Zitto Kabwe Kujadili Bajeti

$
0
0
HATUA ya Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe (ACT- Wazalendo) kuanzisha mjadala wa bajeti ya serikali kwa mwaka ujao wa fedha nje ya Bunge, imekosolewa ukitajwa kwamba hauna tija zaidi ya kuwavuruga wananchi.

Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa, waliohojiwa jana, walisema kitendo hicho ni mkakati usio na tija huku wengine wakisema ni maoni ya kujifurahisha. Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Benson Bana alisema kitendo hicho cha Zitto ni ‘mkakati usio na tija’. Naibu Katibu wa Bunge, John Joel alisema ‘ni maoni ya kujifurahisha’ wakati Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba alisema atajitokeza hadharani baadaye kutoa maoni ya kuliunganisha Taifa.

Baada ya kusimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge hivi karibuni kutokana na kukiuka taratibu, Zitto amekuwa akitumia majukwaa kukosoa bajeti na Serikali ya Rais John Magufuli, hatua ambayo imeelezwa pia kuwa inashusha heshima ya Mbunge huyo. Warioba kufunguka Warioba ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Tume ya Marekebisho ya Katiba, alipotakiwa kutoa maoni yake kwa hatua hiyo, alisema wakati utakapofika atajitokeza na kueleza namna wanasiasa wanavyotumia vibaya nafasi zao za kisiasa.

Kwa sasa tumekaa kimya, lakini wakati utafika ambapo tutajitokeza na kutoa maoni yetu kwa maslahi mapana ya taifa pamoja na kwamba tunaona namna wanasiasa wanavyotumia vibaya nafasi zao za kisiasa na kuligawanya Taifa. Kazi yetu sisi ni kuliunganisha taifa kuwa moja,” alisema Jaji Warioba.

Mhadhiri amshangaa Zitto Kwa upande wake, Dk Bana akizungumza na gazeti hili jana alisema; “ Zitto alipaswa kukusanya maoni ya wananchi ili kuyapeleka bungeni.” “Wakati serikali ilipokuwa inaandaa bajeti yake ya mwaka huu na hata Mpango wa Taifa wa Maendeleo, Zitto alipata fursa ya kushiriki maandalizi yake katika hatua mbalimbali akiwa Mbunge.

Ni wakati huo ndipo Zitto alipaswa kukusanya maoni ya chama chake au makundi mengine ya kijamii wakiwemo wananchi wake ili baadaye ayawasilishe serikalini au bungeni ili kuwezesha kupatikana kwa bajeti bora na si hatua hii anayoichukua sasa,” alisema Bana.

Alisema Mbunge huyo pamoja na kuzijua fika taratibu za Bunge, aliamua kwa makusudi kuzikiuka na hivyo kupoteza dhamana aliyokabidhiwa na wananchi ya kuwawakilisha ndani ya Bunge ili kujadili masuala yenye maslahi mapana kwa taifa ikiwemo bajeti na sasa amebuni mkakati usio na tija.

Alisema pamoja na kufahamu umahiri wa mbunge huyo katika medani ya siasa hatua ambayo iliwezesha wananchi kuwa na imani kubwa na mustakabali wake kisiasa, kwa bahati mbaya Mbunge huyo amepoteza mwelekeo na kuanza kutoa kauli alizosema hazina manufaa kwa wananchi.

“Anachoendelea kukifanya Zitto ni mwendelezo wa kile alichokifanya Mbagala alipotoa lugha ya kuudhi dhidi ya Rais (John Magufuli). Wote tunajua mambo ya bungeni yanajadiliwa bungeni. “Haiwezekani leo mwanasiasa anayejiita mahiri anaitisha mjadala kuhusu bajeti wakati hotuba ya bajeti ikiwa mezani na wananchi wakifuatilia mjadala wake bungeni, huku ni kuwavuruga wananchi na si jambo la msingi kwa taifa,” alisema Profesa Banna.

Akizungumzia mwelekeo wa kisiasa kwa Mbunge huyo wa Kigoma Mjini, Bana alisema pamoja na kuaminiwa kuwa na sauti yenye ushawishi na mvuto wa kisiasa, lakini wasomi wamekuwa wakimchukulia Zitto kama mwanasiasa anayeanzisha hoja na kuziacha hewani bila kuzimaliza.

Ni tofauti na Kafulila (David- Mbunge wa zamani wa Kigoma Kusini). Zitto anapenda kuanzisha hoja na kuziacha zikielea. Kila siku anakuja na hoja mpya, mara bajeti, mara fedha zilizofichwa nje, mara Escrow, mara rais hivi. Ni mtu ambaye hoja zake zinafichwa na ajenda binafsi nyuma yake,” alisema Bana.

Ofisi ya Bunge yafafanua Kwa upande wake, akitoa maoni kuhusu msimamo wa Bunge kwa hatua hiyo ya Mbunge Zitto kuhamishia mjadala wa bajeti nje ya Bunge, Naibu Katibu wa Bunge , John Joel alisema pamoja na kuwa kitendo hicho hakizuiliwi, lakini hakina tija kwa wananchi.

“Zitto anaendesha mjadala ili apate maoni ya kumpelekea nani?” Alihoji Joel na kusema kuwa Mbunge huyo angeweza kukubalika zaidi endapo angetumia jukwaa la Bunge kujadili kile anachokiona katika bajeti ya serikali kwa mwaka ujao wa fedha.

Naibu Katibu huyo wa Bunge alisema kinachoshangaza zaidi ni kuona kuwa mkakati huo wa kujadili bajeti, hata pale unapoonekana kuvalishwa joho la chama cha ACT – Wazalendo ambapo Zitto ni Kiongozi Mkuu, lakini haufanywi kwa vikao vya ndani vya chama na badala yake unaelezwa kuwa ni mjadala wa wazi, hatua inayochanganya wananchi.

Ben Pol Afunguka 'Muungano wa Diamond Platnumz na Rich Mavoko Utaleta Mapinduzi Makubwa Kwenye Muziki'

$
0
0

Mkali wa wimbo ‘Moyo Mashine’, Ben Pol amefunguka na kuzungumzia hatua ya Diamond Platnumz kumsani msanii kubwa kama Rich Mavoko katika label yake WCB.

Akiongea na Bongo5 hivi karibuni, Ben Pol amesema hatua ya Diamond kuamua kumsaini Rich Mavoko katika label ya WCB, itafungua njia kwa wasanii wengine kuwa na moyo wa kusaidiana wenyewe kwa wenyewe.

Ni vizuri sisi kwa sisi tukaaminiana na kufanya kolabo kwenye kazi,” alisema Ben Pol. “Diamond ni mpiganaji na Mavoko ni mtu ambaye ana kipaji na mjanja mjanja, kwa hiyo muungano wao unaweza kuleta mapinduzi makubwa katika muziki,”

Pia muimbaji huyo amewataka wale wasanii wenye uwezo wa kuwasaidia wenzao wasisite, kwani hiyo ndiyo njia sahihi ya kuupeleka muziki wa Tanzania mbele zaidi.

Malecela Aendelea Kuijadili Serikali ya Magufuli...

$
0
0
Waziri Mkuu mstaafu, John Malecela amesema Serikali ya Rais John Magufuli imeanza vizuri mikakati yake na imejengwa katika misingi ya kila kiongozi kuwa na wajibu wa kumhudumia Mtanzania.

 Pamoja na hilo, amesema si sahihi kumfananisha na  mtu mwingine kama aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Sokoine wala Rais wa Kwanza, Mwalimu Julius Nyerere.

 Akizungumza katika mahojiano maalumu yaliyofanyika nyumbani kwake mjini Dodoma, Malecela alisema, “Rais Magufuli katika mambo anayofanya, tusimlinganishe na mtu mwingine, hatutamtendea haki.”

Viongozi wa CUF Wamkataa Profesa Ibrahim Lipumba...Wadai Sababu Zilizomuondoa Zingalipo, Kinachomrudisha ni Nini??

$
0
0
Wakati aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba akitengua uamuzi wake wa kung’atuka kwenye wadhifa huo na kuomba kurejea, viongozi wa juu wa chama hicho wamepinga hatua hiyo wakisema katiba yao hairuhusu na kwamba anakwenda kukiua chama.

Kauli za viongozi hao, zimekuja muda mfupi baada ya Profesa Lipumba kutangaza nia hiyo jana kwenye ofisi za makao makuu ya chama hicho, Buguruni huku akibainisha kuwa amefanya hivyo baada ya kuombwa.

Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui alisema Lipumba hawezi kuwa na nia njema ya kukijenga chama hicho endapo atarudishwa kwenye nafasi aliyoikataa.

“Anataka kuja kukiharibu chama,” alisema Mazrui. Alifafanua kuwa tayari chama hicho kimefanya mambo mengi bila Lipumba ambaye alikuwa anaona kila kinachoendelea, hivyo alichokisema hakina mashiko kwani CUF ilisharidhia kuitisha mkutano wa uchaguzi kujaza hiyo.

Akieleza sababu alizozitoa mwenyekiti huyo, Mazrui alisema haoni chochote cha maana. “Sababu zilizomuondoa zingalipo. Kinachomrudisha ni nini?” alihoji naibu katibu mkuu huyo.

 Alisisitiza kuwa Wazanzibari wanaendelea na mchakato wa kuidai haki yao iliyoporwa Oktoba 25 na hawana nafasi ya kushughulika na masuala yasiyokuwa na tija kwao, hivyo haoni kama kuna sababu ya kumjadili Lipumba na nafasi yake badala ya kuendelea pale walipo.

 “CCM wanaona kinachoendelea, hivyo wameona wamtumie Lipumba kuja kuharibu mipango yetu. Hatuna muda wa kumjadili.Tunataka haki iliyoporwa,” alisisitiza.

Msimamo wa Mazrui haukutofautiana sana na ule wa Kaimu Mwenyekiti wa chama hicho, Twaha Taslima aliyebainisha kuwa amesikia taarifa za kurudi kwa Profesa Lipumba, lakini haoni uwezekano huo.

“Katiba hairuhusu hilo.Hakuna kifungu kinachotoa nafasi kwa kiongozi aliyejiuzulu kurudi kwenye nafasi yake pindi atakapotaka kufanya hivyo,” alisema Taslima.

Aliielezea Ibara ya 117 (2) iliyotumiwa na Profesa huyo kuandika barua ya kutengua uamuzi wake, kuwa inatoa tafsiri zaidi ya moja hivyo kuwapo haja ya viongozi kukutana na kujadili suala hilo kabla ya kutoa maamuzi.

Kwa kuwa hakuwapo kwenye mkutano huo, Taslima alisema: “Tunahitaji kukutana haraka na kujadili. Tutafanya mkutano wetu na tutavijulisha vyombo vya habari ndani ya wiki hii.”

Taslima alisema kipindi alichoongoza kilikuwa na changamoto nyingi ambazo ni tofauti na sasa, hivyo haoni haja ya mtu mwingine kuja wakati mambo yametulia. Chama hicho kilipanga kufanya uchaguzi wa kuziba nafasi hiyo Agosti mwaka huu.

Baada ya kung’atuka kwa Lipumba, Taslima alichukua mikoba yake na kukivusha chama hicho kwenye kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka jana, pamoja na ule wa Zanzibar ambao uliahirishwa na chama hicho kususia marudio yake Machi 20 mwaka huu.

Hata hivyo, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa chama hicho, Abdul Kambaya alisema upo uwezekano wa Lipumba kurudi kwenye nafasi yake kwasababu mpaka sasa haijazibwa.

“Mwenyekiti huchaguliwa au kutenguliwa na halmashauri kuu. Haikupitisha kujizulu. Barua ya kujiuzulu itaenda pamoja na hii ya kutengua uamuzi wa awali,” alisema Kambaya.

Kauli ya Lipumba
Awali, Profesa Lipumba alisema mara kadhaa amekutana na viongozi wa dini na chama pamoja na wanachama wa CUF na wote walikuwa na ujumbe mmoja tu…’rudi tukijenge chama.’

Profesa Lipumba hakushiriki mchakato wa uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana ambao kwa upande wa Zanzibar, kutokana na hitilafu zilizojitokeza ulifutwa na kurejewa Machi 20 mwaka huu huku chama hicho kikiwa kimesusia marudio hayo.

Pamoja na hayo yote, Lipumba alisema ametafakari sana juu ya hali ya kisiasa Zanzibar na kuona umuhimu wa kutoa ushirikiano ili mambo yaende kwa manufaa ya taifa.

“Ni lazima nchi iendeshwe kwa misingi ya demokrasia ambayo itapatikana kwa umoja wetu.Nimerudi kushirikiana na wenzangu kutimiza malengo hayo ili kuchangia maendeleo ya Tanzania,” alisema Profesa Lipumba.

Lipumba aliachana na uongozi wa chama hicho, Agosti 8, mwaka jana, siku chache baada ya vyama vinavyounda Ukawa kukubaliana kumsimamisha Edward Lowassa.

Alimuandikia barua Katibu Mkuu wake, Maalim Seif Shariff Hamad kuwa hakubaliani na uamuzi wa chama chake kuridhia makada waliohama Chama cha Mapinduzi (CCM), akiwemo Lowassa, kupewa fursa ya kugombea nafasi za uongozi.

Baada ya kukatwa kwenye mchujo wa ndani ya CCM, Lowassa akiwa na makada kadhaa wa chama hicho akiwamo aliyewahi kuwa waziri mkuu, Frederick Sumaye, alihamia Chadema ambako alipewa fursa ya kupeperusha bendera ya chama hicho kilichomo ndani ya Ukawa.

Lipumba hakukubaliana na hilo, alikaa pembeni na kuachia ngazi ingawa alishiriki tukio la kumkaribisha Lowassa ndani ya Ukawa.

Jana, wakati anatangaza kufanya mabadiliko ya kile alichokiamua miezi 10 iliyopita, hakuruhusu maswali, ila alifafanua kile kitakachofuata baada ya kuwasilisha ombi hilo, kwa mujibu wa Katiba ya chama hicho: “Katibu Mkuu anashauriana na wanasheria kabla suala langu halijapelekwa kwenye halmashauri kuu kama katiba inavyosema,” alisema Profesa Lipumba.

Tundu Lissu na Mhariri wa Mawio kizimbani Leo Kwa Uchochezi

$
0
0
Serikali itawafikisha Mahakama ya Kisutu leo, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na mmiliki wa gazeti lililofungiwa la Mawio, Simon Mkina kwa kuandika habari za uchochezi.

Mkina alisema baada ya kuripoti Kituo Kikuu cha Polisi kuwa kwa mara ya kwanza watafikishwa mahakamani.

“Nimekuja kama ilivyo amri kufika hapa kila siku asubuhi, ila nimeambiwa kesho ( leo )  tunatakiwa kufika mahakamani na wenzangu,” alisema Mkina.

Katika kesi hiyo, atakuwapo pia mhariri na mwandishi wa habari iliyosababisha kufungiwa, Jabir Idrisa pamoja na mchapishaji wa gazeti hilo.

Lissu ameunganishwa katika kesi hiyo kwa madai ya kutoa kauli za uchochezi zilizoandikwa kwenye gazeti hilo.

Pamoja na Gazeti la MAWIO kufungiwa Januari mwaka huu baada ya kudaiwa kuandika habari za uchochezi zilizohusu mgogoro wa kisiasa visiwani Zanzibar ikiwa na kichwa cha habari ‘Machafuko yaja Z’bar’ katika toleo lake la 182 la Januari 14-20, 2016, bado serikali inawang’ang’ania.

Akizungumza na wanahabari Mkina alilaumu kitendo cha polisi kukamata hadi watoa maoni wa gazeti.

Mkina alisema, serikali inabana uhuru wa habari pia kunyima fursa ya kuikosoa hata kama imefanya mabaya.

Quick Rocka: Penzi la Kajala halinitesi

$
0
0
MSANII anayekimbiza katika Tasnia ya Muziki wa Bongo Fleva, Quick Rocka amedai kuwa penzi la muuza sura kwenye Filamu za Kibongo, Kajala Masanja halimtesi maana ni la kishkaji na kila mmoja kati yao ana uhuru wa kufanya mambo yake binafsi kutokana na matakwa yake bila kumbana mwenziye.

Akipiga stori na safu hii ya burudani Quick ambaye kwa sasa ameachia ngoma mpya iitwayo Hapo aliyomshirikisha G Nako alisema, tofauti na watu wengi waliyoko kwenye mapenzi wanaokuwa wanabanwa na wapenzi wao katika shughuli za kawaida kwa ajili ya kujitafutia kipato, kwake haiko hivyo, yeye na Kajala wamepeana uhuru.

“Sijui nikweleze vipi kuhusu penzi langu na huyo diva, wewe elewa tu liko kishkaji, kila mtu ana uhuru wa kufanya mambo yake na haina kubanana, hata hivyo wakati mwingi ninakuwa naye,” alisema Quick Rocka.

Alipoulizwa juu ya tetesi zinazosambaa za Kajala kutoka na msanii wa Bongo Fleva, Msami alisema hajui chochote kuhusu wawili hao.

Picha: Professor Jay atembelea ‘WCB’ ya Diamond, afurahishwa na uwekezaji uliyofanywa

$
0
0
Mbunge wa Mikumi ambaye ni msanii mkongwe wa muziki wa Hip Hop, Joseph Haule ‘Professor Jay’ Jumatatu hii alitembelea ofisi za WCB na kujionea uwekezaji uliyofanywa na rais wa label hiyo Diamond Platunmz.

Akiongea na Bongo5 Jumanne hii, Professor Jay amemsifia Diamond kwa uwekezaji aliyoufanya.

“Kikubwa kwanza nitumie nafasi hii kumpongeza Diamond kwa kuwa na mawazo mapana zaidi kwa sababu kiukweli kwa wasanii wengi wa Tanzania na Waafrika wengi tunaweza tukawa na kipaji lakini mazingira yetu ya kazi yanakuwa magumu,” alisema Professor.

Aliongeza, “Kwa mfano pale kwa Daimond jana nimeenda nimekuta kuna studio hapo hapo, pamoja na kurecord lakini pia anachumba ambacho amekitengeneza cha kutengeneza photoshoot. Lakini pia ana sehemu ya kufanya editing ya kazi zake na ana watu special ambao amewaajiri kwa ajili ya kazi hizo, hii ni hatua kubwa sana kwa msanii,”

Maneno Mazito ya Mtatiro kwa Prof. Lipumba Baada ya Kuutaka Uenyekiti wa Chama Tena...

$
0
0

NGOJA NIWAELEZE UKWELI!

Kama mzee wetu anao washauri, wamwambie kuwa "DALILI ZA MVUA NI MAWINGU". Na kwamba, NGOMA ivumapo sana hupasuka na tena ajulishwe kuwa VITANI hakuna michezo ya KUJIFICHA na KUONEKANA baadaye, jana niliwaambia kuwa najua CUF inao watu makini wanaojua nini haki ya PROFESA LIPUMBA na nini haki ya CUF kama chama. Kwa wale ambao hawakuelewa ujumbe wangu wa jana nilikuwa namaanisha viongozi wa CUF watakuwa upande wa chama, hawatafuata matakwa ya mtu, na dalili zimeanza kuwa hivyo. Mwisho wa siku mshindi wa mchezo huu ni CHAMA na WANACHAMA wenye UTII na COMMITMENT kwa chama chao, na siyo MTU!

Kuna watu nasikia wanasema WATAGAWANA MBAO, ukweli ni kuwa CUF ni taasisi imara na haiwezi kuwa na MBAO za kugawana. Kutakuwa na machaguo mawili tu, aidha kuondoka na mtu au kubaki na chama, wale watakaobaki na chama watabaki na mbao zote, na wale watakaoondoka na mtu hawatandoka na hata kipande cha ubao - kwa sababu mchezo huu hautahitaji hasira. Siasa ni maisha halisi ya watu, vyama vikiruhusu zigeuke kuwa mchezo wa KOMBOLELA, zitakosa maana na hapa lazima ieleweke, kwamba kuna mambo ambayo vyama vya upinzani vikiyaruhusu yaendelee kutendeka, vitakuwa vinafanya ujinga wa kiwango cha PhD na Uwendawazimu wa Kiwango cha MWENDOKASI!

Profesa Lipumba ambaye kila mtu anamheshimu sana, apishe kwenye uongozi ili chama kijiandalie ZAMA mpya. Nawarejesha kwenye nukuu yangu ya mwaka jana wakati anajiuzulu, kwamba "Kamanda wa vita akiuawa katikati ya vita, siyo muda wa kuanza kulia na kuomboleza, siyo muda wa kulaumiana, anatafutwa askari mwingine na kutwaa bunduki yake, mapambano yanaendelea mbele".

Ninaamini kuwa, CUF inao watu wenye sifa za kuwa wenyeviti wa chama na tena kisiasa wapo watu bora sana. Chama kisiogope kufanya maamuzi sahihi kwa ajili yake na siyo kwa ajili ya mtu. Na iwe fundisho kwa wanasiasa kuwa HISIA za wafuasi wa vyama hazichezewi, na iwe FUNDISHO kwa viongozi wa kisiasa kwamba MISIMAMO na KUTOYUMBA ni wajibu wao usiokwepeka.

Katika mgogoro huu wa kutengenezwa makusudi, wanachama imara wanajua wajibu wao, wasimame upande wa chama, wasimame upande wa taasisi, maana taasisi itakuwepo siku zote. Mtu na watu watapita haraka na kunyauka kama maua.

Namshauri Prof. Lipumba, kwa namna yoyote ile, asikubali kutumikia matakwa ya kundi lolote lile, iwe ndani ya chama au nje ya chama. Asikubali kuwa sehemu ya kuanzisha mgogoro na vurumai kubwa ndani ya chama, asikubali kuwa chanzo cha kuleta sintofahamu kama hii, namtambua Mwenyekiti wangu kama mtu makini na muumini safi wa dini ya kiislamu na huu ni mwezi mtukufu wa Ramadhani, hebu na ajitafakari upya ikiwa NIA yake ni salama kwa ajili ya wanachama wa CUF na nchi yetu.

Binafsi nisingelipenda kuona mgogoro mwingine mkubwa CUF, ambao matokeo yake sote tunayajua, kwamba chama ndicho kitashinda na kitabaki salama salmini, na kwamba watu wachache ndiyo wataumia na kufedheheka, akiwemo mtu anayeheshimiwa sana na aliyewahi kushiriki kukijenga chama hiki kwa nguvu zake na akili zake zote.

Mtatiro J


ZITTO KABWE "Rais Magufuli Atakuwa Rais Kwa Muhula Mmoja Tu"

$
0
0
Kiongozi mkuu wa chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe amesema udikteta anouonyesha Rais John Magufuli ndio kitanzi cha kumfanya awe Rais wa muhula mmoja, kwa kuwa wananchi hawatakuwa tayari kumvumilia uchaguzi ujao....Maneno hayo ameyasema wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za chama hicho Kijitonyama...

Je Kwa Unavyoona Wewe Maneno Hayo Yanaukweli?

Zari is insecure over Jackline Wolper, not Wema Sepetu anymore

$
0
0
Hear this hot gossip......according to insiders Zari is neither insecure about Wema Sepetu nor Kajala Masanja as many people think. According to a source from Diamond's team, Zari's insecurity of her love life with Diamond Platnumz is actress Jacqueline Wolper who is Diamond ex. You may ask why Wolper as she is now dating Harmonize?...Well, our snitch revealed that Wolper's closeness to Diamond is what frightens Zari and she thinks Wolper is more gorgeous than Wema and Kajala.....do you agree?. The source says that Wolper may be dating Harmonize but since she is also close to her ex Diamond and shows a bit fondness of Zari it is easy Zari to be cheated on unknowingly, her friends have warned her.

Wema Sepetu is no more in close contact with Diamond after their break up. And Months ago Zari was warned about Kajala after her rumored secret relationship with Diamond, but none of these two stars make Zari sleepless , it is Wolper..

"Zari is insecure, she is insecure about Wolper not Wema or Kajala, friends keep telling her Wolper might be with Diamond

Dully Sykes: Sioi Leo Wala Kesho, Hata Baba Yangu Hakuwahi Kuoa

$
0
0
Baada ya kupost picha akiwa na Mwana FA baada ya kuoa na kuandika maneno yanayoashiria naye hivi karibuni atafuata nyayo za Mwana Fa, Dully Sykes ameruka viunzi na kusema hana mpango wa kuvuta jiko leo wala kesho.

Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Dully amesema yeye kwake kuoa ni sawa na maji kufuata mkondo, kwana hata marehemu baba yake hakuwahi kuoa wakati wa uhai wake.

“Kila mtu ana mipango yake, maji hufuata mkondo, wewe nafikiri mzazi wako alioa, mi baba yangu hakuwahi kuoa”, alisikika Dully akielezea sababu ya yeye kutoamua kuoa mpaka leo.

Pamoja na hayo Dully amesema akiona kuna umuhimu na ikiwezekana ataoa, hivyo amewataka wadau wake wamuombee ili aweze kuwa na mawazo ya kuoa na kuwa na mke rasmi.

“Kama inawezekana naweza kuvuta jiko, na kama haitowezekana sitavuta jiko, kwa sababu sijafikiria bado, mniombee nipate mawazo ya kuchukua jiko, sio kwa vile FA amefanya basi ndo uone inawezekana, nina sababu zangu tu mwenyewe, nikikwambia ntakuvunja moyo kama umeoa wewe”, alisema Dully Sykes.

Fake Kenyan 'Billionaire' Cons Facebook User

$
0
0
A Kenyan woman residing in South Africa is in distress after she was conned on Facebook by a Kenyan man she met in 2015.

Mary Wangari Mwangi became friends with one Nathan Ochieng' who identified himself as one of the youngest billionaires in the country.

Ms Wangari told the court that Ochieng posed as a wealthy businessman in the petroleum industry and coerced her to invest in the venture then later defrauded her Sh400,000.

“He gave me a newspaper cutting that highlighted success stories of billionaires. When I checked the internet, I realised he inserted his picture in an article that was not about him,” Mwangi was quoted by the Nation.

The victim revealed that she learnt that Ochieng' was a fraudster when she tried to make a Sh2 Million deposit to his account in Kenya. During the transaction, South African Bank told her that the account she was sending money to was dormant.

Upon probing the matter further, Ms Mwangi discovered that Apex Petroleum, the company Ochieng' mentioned, no longer existed after it defaulted on loan payments.

She added that the self-proclaimed billionaire did not invest the money she had sent and ended up cutting communication with her.

Ms Wangari decided to report the matter to the Kenyan authorities but noted that if Ochieng' refunded the money she was ready to drop the case.

The accused reportedly told Wangari that he was a 'Man of God' and the money was an offering which could not be given back. He was later arrested at a church in Nairobi.

JE Uamuzi wa Professor Lipumba Kurudi CUF ni wa Kukurupuka ?

$
0
0
Jana professor lipumba aliitisha kikao na wanahabari kueleza kwamba anatengua barua yake ya kujiudhuru umwenyekiti wa CUF.

Kwamaana anarejerea kwenye nafasi yake ya mwenyekiti taifa kuokoa jahazi la CUF.
Swali, professor hakufanya mawasiliano na uongozi wote wa juu wa chama chake ?.kama alifanya ,basi walimuingza mkenge kummaliza kisiasa.
Haiwezekani jana atangaze kurejerea nafasi yake ,Leo tena viongozi wandamizi wapinge maamuzi yake .
Hili ni pigo kwa professor na litaleta mgogoro pia ndani ya CUF bara na visiwani .

Nashauri kwa viongozi wote wa kitaifa kutafakari kwa kina kabla ya kuitisha media na kutoa matamko yoyote Yale kwani yanaweza kuwabomoa kisiasa.
pia, wawe wanapata maoni ya wadau kabla ya kutoka hadharani .

Toa Maoni yako
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live




Latest Images