Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104775 articles
Browse latest View live

Akaunti ya Instagram ya Linah yenye Followers milioni 1.3 Yadukuliwa (hacked)

$
0
0
Akaunti ya Instagram ya Linah yenye followers milioni 1.3 imedukuliwa (hacked) Jumanne hii.

Tayari hacker huyo ameibadilisha jina akaunti yake na kuipa jina ‘suponzetrie’ huku akifuta picha zake zote alizoziweka mwaka huu.

Post ya mwisho inayoonekana sasa ni video ya tamthilia ya Empire aliyoiweka December 27, 2015. Haijulikani nini lengo la hacker huyo na kama ni wa hapa hapa Tanzania.

Linah anakuwa msanii wa hivi karibuni ambaye akaunti yake ya Instagram imedukuliwa. Miezi kadhaa iliyopita akaunti ya Shilole pia ilidukuliwa japo alifanikiwa kuirejesha.

“Jamani daaaah ndo kama hivyo watu washafanya yao pole kwa uwezo wa Allah itarudi,” Shishi amempa pole Linah.

Zaidi ya kujitangaza, miaka ya hivi karibuni akaunti za mastaa zimekuwa moja ya vyanzo vyao muhimu vya kipato na wale wenye followers wengi wamekuwa wakipata deals zenye hela nyingi.

Ni wazi Linah atakuwa kwenye wakati mgumu kwa sasa.

Jenerali Ulimwengu: Tumerudi Nyuma Miaka 50 Kwenye Demokrasia, Kikwete Apelekwe Mahakamani

$
0
0
Jenerali Ulimwengu akiwa kwenye kongamano la kigoda cha mwalimu Nyerere chuo kikuu cha Dar es Salaam, amesema pamoja na hatua nzuri anazochukua Rais wa sasa, Mheshimiwa John Magufuli ambazo zimepongezwa lakini ukiangalia picha kubwa ni kwamba tumerudi nyuma kama miaka 50 kwenye demokrasia.

Ulimwengu amesema ni kutokana na kufinya uhuru wa kujieleza na hususan kwa kufinya uhuru wa wawakilishi wa wananchi ndani ya bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Ulimwengu ameendelea kwa kusema katika hili hamna kifimbo cha uchawi cha kujinasua isipokuwa mchakato wa katiba ambao ulichukua fedha nyingi kisha ukaachwa njiani na Mheshimiwa Kikwete.

Mwandishi huyo wa habari na mchambuzi wa masuala ya kisiasa ametaka Raisi mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete kufikishwa mahakamani kwa kosa la kuisababishia serikali hasara baada ya kutokuufanikisha mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya.

Jenerali Ulimwengu alisema katika kipindi cha mchakato wa katiba mpya, fedha nyingi ambazo zilitokana na kodi za wananchi zilitumika katika shughuli mbalimbali lakini katiba mpya haikupatikana.

“Katika kipindi hiki tumeona viongozi mbalimbali waliopita wakichukuliwa hatua kwa kuisababishia serikali hasara… Kikwete anapaswa kufikishwa mahakamani kuelezea zile pesa za mchakato wa katiba zitarudi vipi,” alisisitiza.

Akijibu hoja hiyo, mwenyekiti wa mdahalo huo, Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa amesema wakati wa mchakato huo yeye hakuwa mshauri wa rais hivyo hawezi kulijibia suala hilo.

“Mimi sikuwahi kuwa mshauri wa raisi wala mshauri wa chama juu ya mchakato huo, ila niliombwa kutoa maoni kama wananchi wengine,” alisema Mkapa na kuongeza kuwa wasomi wanapaswa kufanya uchambuzi makini kabla ya kutoa hoja kwani kuna baadhi ya hoja hutolewa lakini sio muhimu kwa maendeleo ya taifa. Video:

Watu Hawajui Sisi Tuna Picha ya Diamond na Ali Kiba Wakiwa Wanaongea – Babu Tale

$
0
0
Mmoja kati ya viongozi wa juu wa label ya ‘WCB’, Babu Tale amesema watu hawajui kama Ali Kiba na Diamond wakikutana wanazungumza kama kawaida.
dd

Amesema hayo baada ya weekend hii kuzagaa picha katika mitandao ya kijamii inayomuonyesha Babu Tale, Sallam, Ommy Dimpoz, Mwana FA pamoja Ali Kiba wote wakiwa na nyuso za furaha hali ambayo liibua maswali mengi kwa mashabiki.

Akiongea katika kipindi cha XXL cha Clouds Fm, Jumanne hii, Babu Tale amewataka mashabiki wa muziki kuamiani kwamba yeye pamoja na Diamond hawana tatizo na Ali Kiba.

“Unajua binadamu wanatakiwa kubadilika, huwezi ukatengeneza dhana sisi tuna matatizo hatuwezi hata kupiga picha, hatuwezi kukaa pamoja, hatujafikia hatua hiyo, sisi tunabishana kimuziki na tunatengeneza value ya muziki ili muziki wa Tanzania ukue,” alisema Tale.

Aliongeza, “Haimaanishi Diamond na Ali Kiba wakikaa hawaongei, watu hawajui kuna picha ambazo sisi tunazo Diamond na Kiba wanaongea wapo studio kabisa. Hata kama tukiamua kizipost hizo watu wangeanza kuzungumza zitu vingine, picha ni kitu cha kawaida. Katika hii picha ambayo inazungumziwa alianza kuitwa Mwana FA, akaitwa Omary, akaitwa Ali, tukaitwa mimi na Sallam, kama ningekuwa sitaki kukaa karibu na Kiba ningekimbilia moja kwa moja kwa na Sallam kwa sababu sisi ni wamwisho kuitwa,”

Diamond na Ali Kiba ni wasanii ambao wanadaiwa hawaelewani kitu ambacho kimekuwa kikikanushwa na pande zote mbili.

Abdul Kiba Atolea Ufafanuzi Kuhusu Kujiunga na WCB Wasafi

$
0
0
Staa wa Bongo Fleva, Abdul Kiba  ametolea ufafanuzi kuhusu taarifa iliyosambaa mitandaoni kujiunga na WCB WASAFI ambayo inamilikiwa na Diamond Platnumz.

Akiaongea na cloudsfm.com Abdul Kiba ambae ni mdogowake na msanii Abdul Kiba alieleza.

‘’Ni kweli nilizungumza hiyo lakini wengi wao waliitafsiri vibaya kauli yangu kwasababu ukizungumzia mtonyo nilimaanisha kwamba nina uwezo wa kufanya nao kazi aidha ikitokea labda ‘featuring’ au kuna shoo naweza nikashirikiana nao kwa sababu ni mkataba utatakiwa upite hapo then pesa imwagike nifanye nao kazi ila siku maanisha kwamba nina uwezo wa kuhama ‘lebo’ kutoka hapa nilipo kwenda kwao, nadhani wengi wao waliipokea kauli yangu vibaya’

Steve Nyerere Awapongeza Harmonize na Iyobo Kwa Kuwatuliza Wolper na Aunty Ezekiel

$
0
0
Kiongozi wa zamani wa Bongo Movie Unit,  Steve Nyerere amempongeza msanii wa muziki, Harmonize pamoja na dancer wa Diamond, Mosei Iyobo kwa kuwapa utulivu wasanii wenzake wa filamu Aunt Ezekiel na Jacqueline wolper.

Muigizaji huyo ambaye alikuwa MC katika iftar ya GSM iliyofanyika Kigamboni weekend hii na kuhudhuriwa na mastaa mbalimbali, alisema anawashukuru wasanii hao wa muziki kwa uwamuzi wa kuwahifadhi dada zake hao.

“Mimi nashukuru wasanii wa bongofleva kwa kuwahifadhi dada zetu, Aunt yupo poa, na Wolper naona safi,” alisema Steve Nyerere huku akicheka.

Wolper na Harmonize kwa sasa ni wapenzi na kila mmoja anaonyesha anampenda mwenzake, na Aunt Ezekiel na Mose Iyobo ni wapenzi wa muda mrefu na wanaishi kama familia na mtoto wao mmoja aitwae Cookie.

Serikali Yapiga Marufuku Uagizaji wa Transfoma za Umeme Kutoka nje ya Nchi.

$
0
0
Serikali imeliagiza Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO) kutoagiza transfoma nje ya nchi na badala yake kutumia zinazotengenezwa hapa nchini na kampuni ya Tanalec.

Agizo hilo limetolewa leo Bungeni Dodoma na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Dkt. Medard Kalemani alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Tunduru Kusini, Mhe. Daimu Iddi Mpakate aliyetaka kujua ni lini Serikali itatoa pesa kukamilisha miradi ya umeme wa Wakala wa Umeme Vijijini (REA).

Dkt. Kalemani alisema uzalishaji wa transforma ni mkubwa ikilinganishwa na mahitaji ya bidhaa hizo kwa mwezi, hivyo hakuna sababu ya kuagiza transforma hizo kwa bei kubwa wakati zinapatikana hapa nchini.

Kuhusu suala la kugharamia nguzo kwa Mpango wa REA Dkt. Kalemani alisema mteja hatakiwi kutozwa gharama yoyote ziadi ya Tshs. 27,000 fedha ya kuunganishiwa umeme kwa mpango huu.Dkt. Kalemani alisema kuwa Serikali inatekeleza Mradi wa REA Awamu ya II katika Wilaya ya Tunduru na kazi hii inategemewa kukamilika mwishoni mwa mwezi Juni, 2016.

Alisema Kazi ya kupeleka umeme katika wilaya hiyo ni pamoja na ujenzi wa njia ya umeme msongo wa kilovoti 33 yenye urefu wa Kilomita 293. 2, na ujenzi wa njia nyingine yenye msongo wa kilovoti 0.4 yenye urefu wa kilomita 76.1 na ufungaji wa transfoma 38 pamoja na kuwaunganishia umeme wateja wa awali 3,330

“Gharama ya Mradi kwa Mkoa wa Ruvuma ikiwemo Wilaya ya Tunduru ni Tsh. Bilioni 32.56,” alisema Dkt Kalemani na kuongeza kuwa mkandarasi amekwishalipwa bilioni 27.22 sawa na asilimia 83.6 ya fedha.

Dkt. Kalemani amesema kuwa katika Wilaya ya Tunduru ni vijiji vinne ambavyo vimeunganishiwa miundombinu ya umeme na kufanyiwa majaribio kabla ya kuwashiwa umeme.

Kwa mujibu wa Dkt. Kalemani mkandarasi anaendelea kufunga transforma na Mita za Luku katika vijiji 34 vilivyosalia kwa Wilaya ya Tunduru ili viweze kupatiwa huduma ya umeme ifikapo tarehe 30 Juni, 2016.

Ukweli Afya ya Spika Job Ndugai

$
0
0
KUFUATIA uvumi wa mara kwa mara kwenye mitandao ya kijamii juu ya kufariki dunia kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai, Risasi Mchanganyiko limetafuta na kufanikiwa kupata ukweli juu ya afya ya kiongozi huyo mkuu wa wabunge Tanzania.

Awali, kulikuwa na taarifa katika mitandao ya kijamii, ikitoa madai hayo, hasa kutokana na kutoonekana kwa muda mrefu kwa Spika akiongoza vikao vya Bunge vinavyoendelea kujadili bajeti kuu ya serikali mjini Dodoma.

Kutotolewa kwa maendeleo ya afya yake ndilo jambo linalowafanya wengi kuziamini taarifa hizo za mitandaoni na hivyo kupiga simu chumba cha habari kutaka kujua uhakika wake hasa kwa kuwa hii siyo mara ya kwanza kwa Spika kwenda nchini humo kuangaliwa afya yake.

Gazeti hili lilimtafuta Katibu wa Bunge, Thomas Kashililah ili kupata ufafanuzi wa taarifa za mitandao zilizokuwa zikitembea juzi (Jumatatu) kuwa mbunge huyo wa jimbo la Kongwa mkoani Dodoma amefariki, lakini simu yake haikupo-kelewa.

Lakini Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel alipatikana na kuhusu ‘ishu’ hiyo, alisema ingawa alikuwa Dar es Salaam, anavyofahamu ofisi ya mhimili huo wa dola, haina taarifa tofauti na zilizotolewa awali.

“Watu bwana sijui wakoje, mimi huu uvumi niliusikia, lakini afya ya Spika ni nzuri na anaendelea na uchunguzi wa afya yake kama kawaida,” alisema.

Juni 8 mwaka huu, ofisi ya Bunge ilitoa taarifa rasmi za kukanusha uvumi huo, ikidai hali ya mbunge huyo inaendelea vizuri katika hospitali anayotibiwa nchini India.

Taarifa hiyo iliwataka watu kupuuza uvumi huo unaowapa hofu wananchi na viongozi, kwani yupo huko akiangaliwa afya yake, kama alivyotakiwa kufanya hivyo na daktari wake mapema mwaka huu.

Chanzo:GPL

Jack Wolper Nusura Apigwe Risasi Kituo cha Mafuta‘Sheli’

$
0
0
Chupuchupu! Mwanadada anayeng’ara kunako tasnia ya filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper, juzikati almanusra apigwe risasi kwenye kituo kimoja cha mafuta kilichopo Tegeta (jina linahifadhiwa) jijini Dar es Salaam, baada ya kuibuka kwa timbwili zito eneo hilo, Risasi Mchanganyiko linakupa mkasa mzima.

Tukio hilo la aina yake, lilijiri mishale ya saa tano usiku wa Juni 12, mwaka huu ambapo kwa mujibu wa chanzo chetu cha kuaminika, Wolper alinusurika kupigwa risasi na mlinzi wa kituo hicho cha mafuta baada ya kutokea hali ya sintofahamu kati yake na mfanyakazi mmoja kwenye kituo hicho.

“Ishu yenyewe ni kwamba, kuna muda Wolper alifika pale sheli (Sheli ni neno lililozoeleka likimaanisha kituo cha mafuta, lakini ukweli ni kuwa jina hilo ni la kampuni ya mafuta yenye makao makuu yake Nchini Marekani) akiwa ndani ya gari aina ya Toyota Mark X, lile linalodaiwa kuwa ni la mpenzi wake wa sasa, Harmonize (Rajab Abdulkan).

“Akaongeza mafuta na kuondoka zake, dakika kadhaa baadaye, tulishangaa kumuona Wolper akirudi tena na kwenda mpaka kwa yule dada aliyemuuzia mafuta lakini safari hii alionekana kuja kwa shari.

“Akashuka kwenye gari na kuanza kumuwakia yule dada kwa madai kwamba amemuibia mafuta na kusababisha gari lake limzimikie njiani wakati alitoa shilingi elfu ishirini,” kilisema chanzo chetu.

Kwa mujibu wa chanzo, timbwili la aina yake lilizuka eneo hilo baada ya msichana huyo kuanza kumjibu mbovu msanii huyo ambaye hakukubali, Wolper akakinukisha kwa kumvaa na kuanza kumshushia kichapo, tukio lililokusanya umati wa watu.

Ilibidi mlinzi wa kituo hicho cha mafuta, aingilie ugomvi huo. Hata hivyo, mlinzi huyo alionekana kumtetea zaidi mfanyakazi mwenzake na kumkandamiza Wolper, jambo lililozidi kumpa hasira msanii huyo.

“Alipoona wanasaidiana, Wolper aliwachenjia wote wawili, jambo lililosababisha mlinzi huyo aondoke eneo hilo lakini aliporejea, alikuwa na bunduki yake ya lindo mkononi, akaikoki na kutaka kumpiga risasi Wolper,” kilisema chanzo chetu na kuongeza kuwa kuona hivyo, Wolper alikimbilia ndani ya gari lake na kutoka nduki, akiacha watu wengi wakiwa wamekusanyika kituoni hapo.

Baada ya kusikia maelezo hayo kutoka kwa chanzo chetu, Risasi Mchanganyiko lilimtafuta Wolper ambaye baada ya kusomewa mashtaka hayo, alikiri kutokea kwa tukio hilo.

“Dah, ni kweli nilikutana na matatizo hayo usiku, ambapo nilikuwa naenda Tegeta baada ya kufika njiapanda flani pale, gari lilipungua mafuta nikaingia kituoni na kuongeza ya elfu 20, wakati naongeza nilihisi kabisa yule dada ananiibia lakini sikumjali, nikalipa na kuondoka.

Nilipofika mbele kidogo tu gari lilizima,” alisema Wolper na kuongeza: “Ilibidi nifanye utaratibu wa kupata mafuta mengine kisha nikageuza na kurudi mpaka pale sheli kwa lengo la kudai haki yangu ndiyo kukatokea timbwili hilo kwani mlinzi wa pale alikuwa anamsaidia yule dada aliyeniibia.”

“Wakati nikiwa najihami maana yule mlinzi alikuwa akinikaba, nilimpiga kibao, akakimbilia bunduki yake na kuanza kuikoki akitaka kunipiga risasi.

“Baada ya kuona amefikia hatua hiyo niliingia haraka kwenye gari langu na kuondoka zangu kwani nilihisi walikuwa na njama moja ya kuniibia mafuta na walipoona nimerudi kulalamika ndiyo wakaamua kunifanyia vurugu, kweli sikufurahishwa na tabia yao kwanza ni wezi wakubwa wa mafuta hao,” alisema Wolper.

Gazeti hili lilifika kwenye kituo hicho cha mafuta kwa lengo la kupata maelezo ya upande wa pili, lakini wafanyakazi waliokuwepo walisema wao wameingia asubuhi ya siku hiyo (Jumatatu) hivyo hawaelewi lolote.

Chanzo:Risasi Magazine

Kanuni Haziruhusu Wabunge Kususia Vikao - Tulia

$
0
0
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson amelazimika kutolea ufafanuzi sakata la wabunge wa upinzani kutoka nje ya bunge.

Dkt Tulia ametoa ufafanuzi baada ya hoja hiyo kuibuliwa na baadhi ya wabunge waliokuwa wakichangia mjadala wa bajeti katika kikao cha 42 mkutano wa 3.

Baadhi ya wabunge waliogusia suala hilo ni Livingston Lusinde pamoja na Daniel Nsazugwako ambao wameelezea kuwa wabunge hao wanataka kurudi bungeni na kumuomba Naibu Spika kuwasamehe.

Baada ya hoja hizo kuibuliwa ndipo Naibu Spika akalieleza bunge kuwa hakuwatoa yeye bungeni wabunge hao na badala yake alieleza kinachoendelea kuhusu wabunge hao ambao wameendelea kutoka nje kila mara ambapo vikao vya bunge vinapoongozwa na Naibu Spika.

Katika ufafanuzi wake, Dkt Tulia amesema kuwa wapinzani tayari wamekwisha peleka hoja kwa Spika ya kutokuwa na imani na Naibu Spika kwa mujibu wa kanuni ya 138, na kuongeza kuwa kanuni hizo hizo haziwapi haki ya kususia vikao, hivyo hana la kufanya hivi sasa zaidi ya kusubiri maamuzi ya Spika.

"Wapinzani wamepeleka hoja kwa Spika kwa mujibu wa kanuni ya 138, na ni haki yao, lakini suala la kutokuwa na imani siyo jipya, hoja kama hiyo imewahi kutolewa siku za nyuma dhidi ya Spika Makinda lakini hawakususia vikao, na hizo kanuni haziruhusu, katika kanuni hizi hakuna sehemu yoyote inayoruhusu wabunge kususia vikao" Amesema Dkt Tulia.

Aidha katika hatua nyingine wabunge wameendelea kutaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG ) aongezewe bajeti ili aendelee kuwa na uwezo mkubwa katika kudhibiti hesabu za serikali.

Wastara Ana Mimba ya Mbunge Aliyekuwa Mume Wake?

$
0
0
Mashabiki katika mitandao ya kijamii wanamshinikiza staa wa filamu, Wastara Juma kuwapa ukweli kama ana mimba ya Mbunge wa Jimbo la Donge Zanzibar, Sadifa Khamis ambaye ameachana naye miezi kadhaa iliyopita.

Muigizaji huyo ambaye ni mama wa watoto watutu, ameona asikae kimya kushuhu swala hilo na kuamua kuwajibu mashabiki hao akiwataka kutulia kama ana mimba wanaiona baada ya miezi tisa.

Haya ni majibu wa Wastara kuhumu kuwa na mimba.

Idris Asema Wema Kutumia Tsh Milioni 4.8 kwa Ajili ya Nywele kwa Mwezi ni Hadhi yake

$
0
0
Baada ya mashabiki na wadau mbalimbali kujadili kauli ya Wema Sepetu ya kwamba anatumia Tsh 4.8 kwa ajili ya nywele zake kwa mwezi mmoja, mpenzi wake Idris Sultan amesema matumizi hayo yanaendana na hadhi ya mrembo huyo.

Aidha katika kauli nyingine ambayo Wema aliitoa mapema mwaka huu, alisema anatumia Sh 30,000 kwa ajili ya chakula kwa siku na kama atanunua na chakula cha mbwa wake huwa anatumia Sh 50,000 kwa siku.

Akiongea na Bongo5 wiki hii, Idris Sultan ambaye ni mshindi wa shindano la Big Brother 2014, amesema haoni tatizo kwa mpenzi wake huyo kuwa namataumizi makubwa kwa kuwa yeye mwenyewe ni mtafutaji.

“Kwa level yake anafaa, kila mtu na level yake,” alisema Idris. “Kwa hiyo nina maanisha kila mtu ana thamani yake, na kila siku hadhi ya maisha yake inapanda na pia anafanya kazi ndiyo maana anafikia katika level hiyo,”

Pia Idris alisema watu wanatakiwa kutambua kwamba jinsi uchumi wa mtu binafsi unavyokuwa basi pia na maisha yake hudabilika pamoja na muonekano.

Ripoti ya Lugumi Yarudishwa Kamati Ndogo

$
0
0
Ripoti ya Kampuni  ya Lugumi kudaiwa kushindwa kutekeleza mradi wa utambuzi wa vidole kwenye vituo vya polisi imerudishwa kwenye kamati ndogo iliyoundwa kuchunguza sakata hilo baada kubaini mapungufu.

Akizungumza katika viwanja vya Bunge, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali, (PAC) Aeshi Hillaly alisema baada ya kukamilisha ripoti hiyo itapelekwa katika kamati yake ili iweze kujadiliwa.

“Kamati ndogo yenyewe iligundua kuwa kuna mapungufu kwenye hiyo ripoti, kwa hiyo imeirejesha tena kwao ili kurekebisha mapungufu hayo kabla ya kuileta kwenye kamati yangu tuijadili,” alisema.

PAC iliunda kamati hiyo ndogo iliyokuwa inaongozwa na Japhet Hasunga (Vwawa-CCM), ambayo imepewa kazi ya kuchunguza undani wa mkataba huo wenye thamani ya Sh37 bilioni.

Aprili 23, mwaka huu, PAC ilikutana na kuteua wajumbe tisa watakaounda kamati ndogo kuchunguza sakata hilo kwa undani, na kuandaa hadidu za rejea za kufanyia kazi.

Baadhi ya adidu za rejea zilizojadiliwa na PAC ni pamoja na kuangalia thamani ya vifaa vilivyonunuliwa na hali halisi ya soko na kama kulikuwa na ulazima wa kutoa kazi hiyo kwa mbia mmoja.

Kampuni hiyo ilitakiwa kufunga mashine 108 katika vituo vya polisi lakini ilifunga 14 tu.

Is Tanzania ousting Kenya as East Africa's powerhouse?

$
0
0
Less than a year after President Magufuli took office, Tanzania is already gaining influence among its neighbors and moving away from its reputation as a lone ranger in the region. So what does this mean for Kenya?

Tansania Präsident John Magufuli
Despite having the largest population in East Africa, Tanzania has often been sidelined in regional politics. While Kenya's influence surged, Tanzania was accused of being too slow and cautious when it came to plans for regional integration and infrastructure.

But since John Magufuli's surprise election win last October, it seems Kenya could be losing its grip on East African politics as Tanzania increasingly presents itself as a viable alternative for regional cooperation.



Just last week, the Ugandan government announced it would route the country's valuable oil exports through Tanzania rather than Kenya, opting for a pipeline to the Tanzanian port city of Tanga.

A report commissioned by the Ugandan government in March found that the pipeline route through Tanzania was cheaper and would be in operation more quickly than the Kenyan option. The decision was a blow for Kenya, which will now have to go through with its own ambitious oil pipeline project alone, or find new partners.

An international railway project, championed by Kenya, has also come up against difficulties as regional players consider their options. Widespread media reports claimed that Rwanda was pulling out of plans to develop rail links to Indian Ocean ports through Kenya in favour of routes through Tanzania. But the Rwandan government has now said it plans to continue with both routes.

Magufuli's new approach

The readiness of Uganda and Rwanda to embark on projects and agreements with Tanzania, particularly when it means breaking off deals with Kenya, is a mark of the shift of influence within the region. Kenyan political analyst and commentator Martin Oloo told DW that President Magufuli's pragmatic, hands-on approach is making this possible. "It is changing the way business can be done: in a more efficient and effective way," he said.

Rwandan President Paul Kagame shakes hands with President Magufuli
President Magufuli visited his Rwandan counterpart Paul Kagame last month
One of Magufuli's key policies is cracking down on corruption. "What is endearing him to his own people and perhaps what is making sense economically for the region is that business can be done in cheaper ways, business can be done by minimizing corruption," Oloo said. "And corruption is expensive, so countries where there is runaway corruption, like in Kenya. That's impeding its competitiveness, its impeding its relevance within the region," he added.

Stability and growth

But Tanzania's recent political gains are not only down to Magufuli's leadership style. The country has enjoyed a steady growth rate of 6 - 7 percent over the past decade and is already starting to overtake Kenya economically. "Magufuli's performance will only be helping that to happen faster," Oloo said.

Despite widespread poverty, long term political stability has provided a solid foundation for growth and development. "You can decide to look at Kenya as a powerhouse maybe on the economic side, but you've got to accept that Tanzania is a powerhouse in terms of stabilizing these countries," said Richard Shaba, Program Coordinator at the Konrad Adenauer Foundation in Tanzania, a German political foundation. "We take most of the refugees. We do most of the reconciliation whenever these countries have a problem," Shaba told DW.

When it comes to stability, Kenya is struggling. Security has become a growing fear, not only for Kenyans but also investors. The country's border with Somalia makes it vulnerable to attacks from Somali terrorist group al-Shabab, making Tanzania an attractive alternative.

Kenyan police carry the body of a man killed in an al-Shabab attack
Kenyan police deal with casualties following an al-Shabab attack on a village on Kenya's border with Somalia last year
What's next for East Africa?

In the face of these difficulties, Kenya will now have to up its game if it wants to retain its regional strength. "What should be worrying Kenyans is that we need to take on runaway corruption, we need to improve efficiency, we need to make ourselves competitive within the region," said analyst Oloo. "And unless we do that, then our neighbors like Tanzania and Rwanda are actually going to run away with the opportunities."

If the latest developments in terms of regional cooperation are anything to go by, that is already happening. But according to Richard Shaba, even Magufuli's unconventional approach won't completely change Tanzania's traditionally guarded politics when it comes to cooperation and integration in East Africa.

"I think Tanzania will pursue more or less the same regional politics - being a bit cautious - because when the East African Community collapsed in 1977 we got our fingers burned very badly," he told DW. "Willingness is always there, but the approach will be cautious."

2016 Deutsche Welle
Date 20.05.2016
Author Loveday Wright
Karte Ostafrikanische Gemeinschaft Englisch
Infrastructure projects

Jerry Slaa Ala Mwereka Tena...Kesi Aliyofungua Kupinga Ubunge wa Mwita Waitara Yatupwa

$
0
0
Mahakama Kuu imetupilia mbali kesi ya kupinga ushindi wa Mbunge wa jimbo la Ukonga Mwita Waitara (CHADEMA) iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea wa CCM, Jerry Slaa. Sababu za kutupilia mbali shauri hilo ni kile kilichoelezwa kuwa ni kufunguliwa kwa kesi hiyo nje ya muda wake.

Toa maoni yako

Taarifa Ya Utekelezaji Wa Maagizo Ya Serikali Kuhusu Ukomo Wa Matumizi Ya Simu Bandia Nchini Ifikapo 16 Juni 2016

$
0
0
1.0   UTANGULIZI

1.1. Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ni taasisi ya Serikali yenye dhamana ya kusimamia shughuli za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta hapa nchini. Kuwepo kwa Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) ya 2010 na Kanuni za EPOCA (CEIR) za mwaka 2011 zimewezesha kutekelezwa kwa mfumo wa rajisi ya namba za utambulisho wa vifaa vya mawasiliano vya mkononi.


1.2. Mfumo huu wa kielektroniki ulizinduliwa rasmi tarehe 17 Desemba 2015 na unahifadhi kumbukumbu za namba tambulishi za vifaa vya mawasiliano vya mkononi  (IMEI) kwa lengo la kufuatilia namba tambulishi za vifaa vinavyoibiwa, kuharibika, kupotea au ambavyo havikidhi viwango (bandia) vya matumizi katika soko la mawasiliano. Namba tambulishi za vifaa vyote vya mawasiliano vya mkononi ambavyo vimeibiwa, vimeharibika, kupotea au visivyokidhi viwango vya matumizi katika soko la mawasiliano havitaruhusiwa kuunganishwa kwenye mitandao ya watoa huduma ifikapo kesho tarehe 16 Juni 2016.

1.3. Kipindi cha mpito cha kuelimisha umma pamoja na zoezi la wateja kuhakiki simu walizo nazo au wakati wanataka kununua simu mpya lilianza mwezi Desemba 2015 wakati mfumo ulipozinduliwa na litamalizika kesho tarehe 16 Juni 2016. Hata hivyo, elimu kwa umma kuhusu simu bandia imekuwa ikitolewa nchini tangu mwezi Novemba 2011 baada ya Kanuni za CEIR kutoka, kufuatia kupitishwa na Bunge Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta tarehe 20 Juni 2010 ikielekeza kuwekwa kwa mfumo wa namba za utambulisho wa vifaa vya Mawasiliano vya kiganjani.

2.0    KAZI ZILIZOFANYIKA TANGU KUZINDULIWA KWA MFUMO

2.1 Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania imeendelea kusimamia kwa karibu makampuni ya simu hapa nchini katika uendeshaji wa kila siku wa mfumo wa rajisi ya namba za utambulisho wa vifaa vya mawasiliano vya mkononi. Hii imesaidia pamoja na mambo mengine kupata taarifa za namba tambulishi (IMEI) na kuzifanyia uchambuzi wa kina ili kupata mwelekeo halisi kabla ya kipindi cha mpito kuisha hapo tarehe 16 Juni, 2016.


2.2 Mamlaka ya Mawasiliano iliendelea pia na kampeni za kutoa elimu kwa umma kuhusu jinsi ya kuhakiki namba tambulishi (IMEI) za vifaa vya mkononi (mobile devices). Katika kampeni hizo wananchi walipata uelewa wa kutambua uhalisia wa simu zao ikiwa ni pamoja na mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa kununua simu mpya. Makampuni yote ya simu hapa nchini kwa nyakati tofauti wameshiriki pia katika kuelimisha umma, ikiwa ni pamoja na kuwapelekea ujumbe mahususi moja kwa moja kwa watumiaji wote wa simu za mkononi. Hali kadhalika Shirika la Viwango Tanzania na Tume ya Ushindani nchini, wameshiriki moja kwa moja katika kutoa elimu kwa umma sambamba na Mamlaka ya Mawasiliano.


2.3     Kipindi cha kuanzia Desemba 2015 mpaka mwezi Mei 2016 Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ilitoa elimu kwa umma katika mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Mbeya, Rukwa, Ruvuma, Iringa, Dodoma, Singida, Tabora, Mwanza, Shinyanga, Geita, Simiyu, Mara na Kagera. Pia elimu kwa umma ilitolewa Zanzibar. Mamlaka imefanya pia elimu kwa umma katika miji ya, Morogoro, Pwani, Lindi na Mtwara wiki iliyopita pamoja na wiki hii. Aidha kesho ambayo ndio siku ya ukomo wa matumizi ya simu bandia nchini, kutakua na mkutano wa wafanya biashara wa simu wa mkoa wa Dar es Salaam. Mkutano huo utawahusisha pia mafundi wa simu, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa. Pamoja na mikutano ya hadhara na mikutano ya barabarani (road shows), elimu imetolewa kwa wauzaji wa simu, Mafundi wa Simu na Maafisa Biashara pamoja na Kamati za Ulinzi na Usalama za maeneo husika.


3.0     UCHAMBUZI WA NAMBA TAMBULISHI (IMEI)


Wakati mfumo wa rajisi ya namba za utambulisho wa vifaa vya mawasiliano vya mkononi unazinduliwa mwezi Desemba 2015, idadi ya namba tambulishi ambazo zilikuwa hazina viwango (bandia) zilikuwa sawa na 4% na zile ambazo zilikuwa zimenakiliwa (duplicates) zilikuwa ni sawa na 30%. Hii ikiwa na maana 66% ni sio simu bandia. Uchambuzi huu haukuhusisha taarifa za makampuni ya Viettel na Smile.




Kielelezo 1: Uchambuzi wa takwimu za namba tambulishi (IMEI) za Disemba, 2015


Uchambuzi wa mwezi Februari 2016 ulionyesha idadi ya namba tambulishi ambazo zilikuwa hazina viwango zilikuwa sawa na 3%, vilevile idadi ya namba tambulishi ambazo zimenakiliwa zilikuwa sawa na 18%. Simu halisi zilikuwa sawa na 79%.


Kielelezo 2. Uchambuzi wa takwimu za namba tambulishi (IMEI)February 2016


Uchambuzi wa mwezi Machi 2016 ulionyesha idadi ya namba tambulishi ambazo zilikuwa hazina viwango zilikuwa sawa na 4%, na idadi ya namba tambulishi ambazo zimenakiliwa zilikuwa sawa na 13%. 83% zikiwa simu halisi. Uchambuzi huu unahusisha taarifa za makampuni yote ya simu nchini.




Kielelezo 3: Uchambuzi wa takwimu za namba tambulishi (IMEI) za Machi, 2016


Uchambuzi wa mwezi Aprili 2016 unaonyesha hakuna mabadiliko yoyote ya idadi ya namba tambulishi ambazo zilikuwa hazina viwango (invalid) hivyo kubakia 4%, na idadi ya namba tambulishi ambazo zimenakiliwa ziliongezeka kutoka 13% na kufikia 14%. Vilevile idadi ya namba tambulishi za simu halisia ilipungua kutoka 83% mpaka 82% kama ilivyoonyeshwa katika kielelezo kifuatacho.




Kielelezo 4: Uchambuzi wa takwimu za namba tambulishi (IMEI) za Aprili, 2016


Matokeo ya uchambuzi wa mwezi Aprili, 2016 umeonyesha namba tambulishi ambazo zilikua zimenakiliwa kuongezeka na kuleta taswira kuwa kuna uwezekano mkubwa kwa wauzaji wa simu wasio waaminifu kupunguza bei za simu zao zenye namba tambulishi zilizonakiliwa na kuwafanya watumiaji wa simu katika maeneo husika ambayo elimu kwa umma ilikua bado haijawafikia kushawishika kununua simu hizo. Matokeo haya yalitoa msukumo kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania pamoja na wadau wote kuongeza nguvu zaidi kuelimisha wananchi katika maeneo yaliyobakia kuhusu umuhimu wa kuhakiki simu zao ikiwa ni pamoja na kuelewa zaidi utaratibu wa kufuata wakati mtu atakapo hitaji kununua simu mpya.


Kielelezo 5: Uchambuzi wa takwimu za namba tambulishi (IMEI) za Mei, 2016


Uchambuzi wa mwezi Mei, 2016 ulionyesha idadi ya namba tambulishi ambazo zilikuwa hazina viwango zilikuwa sawa na 3%, na idadi ya namba tambulishi ambazo zimenakiliwa zilikuwa sawa na 2% ambapo 95% zikiwa simu halisi. Uchambuzi huu unahusisha taarifa za makampuni yote ya simu nchini.


Matokeo haya mazuri yanaonyesha matokeo ya jitihada mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Makampuni ya simu hapa nchini pamoja na wadau wengine katika kuelimisha umma juu ya kuhakiki uhalisia wa simu walizo nazo ikiwa ni pamoja na mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa kununua simu mpya.


Kielelezo 6: Uchambuzi wa takwimu za namba tambulishi (IMEI) za Juni, 2016


Uchambuzi uliofanywa tarehe 14 Juni 2016 unaonyesha mabadiliko chanya ya idadi ya namba tambulishi ambazo zilikuwa hazina viwango (invalid) kupungua kutoka 3% hadi kufikia 2.96%, na idadi ya namba tambulishi ambazo zimenakiliwa zikipungua kutoka 2% hadi kufikia 0.09%. Vilevile idadi ya namba tambulishi za simu halisia zimeongezeka kutoka 85% mpaka 96.95% kama ilivyoonyeshwa katika kielelezo 6 hapo juu.


Matokea haya yanaonyesha mwitikio mzuri wa wananchi juu ya uelewa wao katika suala zima la uzimaji wa simu ambazo hazikidhi viwango. Matokeo hayo yanatoa picha nzuri hasa tunapoelekea kuhitimisha zoezi la uzimaji wa simu bandia kesho tarehe 16 Juni 2016.


4.0     CHANGAMOTO

Pamoja na jitihada mbalimbali zilizofanywa na Mamlaka pamoja na wadau wengine bado kuna changamoto ambazo zinahitajika kutatuliwa. Changamoto hizo ni pamoja na:


(i)  Uaminifu mdogo kwa baadhi waauzaji wa simu kwa kutoa punguzo kwa wananchi ili kuwashawishi kuzinunua simu bandia kwa bei nafuu;


(ii) Gharama zinazohitajika katika kuwafikia wananchi na kuelimisha ili waweze kuelewa zaidi juu ya mpango mzima wa kuhakiki simu zao; na


(iii) Uelewa mdogo wa baadhi ya wananchi katika kuitikia wito wa kuhakiki simu zao katika kipindi cha mpito.


5.0     HITIMISHO


Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania inaendelea kumbusha watanzania wote kuwa ni jukumu la kila mmoja wetu kuhakikisha kuwa simu yake ni halisi na sio bandia kwani kuanzia kesho, hakuna simu bandia itakayoweza kufanya kazi nchini. Vilevile Mamlaka inawakumbusha wauzaji wa vifaa vya mawasiliano vya mkononi kutambua kuwa ni kosa kubadilisha namba tambulishi za vifaa vya simu za mkononi (mobile devices) kwani adhabu yake ni kifungo kisichozidi miaka kumi (10) au faini isiyopungua TZS millioni 30 au vyote kwa pamoja.


Mamlaka inatoa wito kwa wale wote wote wanaofanya biashara za kuingingiza simu hapa nchini kutoka nje wahakikishe kuwa simu wanazoleta zinakidhi viwango, zimehakikiwa kwa mujibu wa Shirika la Viwango Tanzania. Aidha Mamlaka inawakumbusha kwa mara nyingine kuwa wanapaswa kuwa na leseni ya Mamlaka ya Mawasiliano kwa mujibu wa Sheria. Hii pia ni kwa mafundi wote wa simu nchini, wanatakiwa kuanza mchakato wa kupata leseni ya kutengeneza simu, ikiwa ni pamoja na kuweka utaratibu wa kuwaorodhesha wanaoleta simu zao kutengenezwa ili kuepuka kuwa sehemu ya mtandao wa wizi wa simu.


Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania inayapongeza makampuni ya simu kwa ushirikiano mzuri wanaondelea kuuonesha katika kutekeleza agizo hili la Serikali kupitia Mamlaka. Hali kadhalika, jitihada zao za kushiriki elimu kwa umma kwa wateja wao pamoja na kuwapatia simu wateja waliokuwa wanatumia simu bandia, kumepelekea agizo hili kufanikiwa kwa kiwango cha hali ya juu. Mafanikio ya jambo hili, kwa kiasi kikubwa yametokana na ushirikiano wa wadau mbalimbali wa Mawasiliano, wakiwemo jeshi la Polisi, Tume ya Ushindani pamoja na Shirika la Viwango Tanzania.


Mhandisi James Kilaba

KAIMU MKURUGENZI MKUU

15 Juni, 2016


Maelezo ya ziada kwa Wahariri


FAIDA ZA MFUMO WA RAJISI YA NAMBA TAMBULISHI


Mfumo huu wa rajisi una faida zifuatazo:

  1. Kuthibiti wizi wa simu. Iwapo mtu atapoteza au ameibiwa simu ya kiganjani na akatoa taarifa kwa mtoa huduma, simu hiyo itafungiwa isiweze kutumika kwenye mtandao mwingine wowote wa simu za kiganjani. Mteja anaponunua simu ni lazima adai risiti halali na halisi  na pia garantiii ya miezi 12. Mteja anatakiwa aihifadhi risiti hiyo angalau kwa miezi mitatu. Baada ya hapo, iwapo simu imekuwa inatumika, taarifa za matumizi zinaweza kutumika kama uthibitisho mbadala wa milki ya simu husika.
  1. Kuhimiza utii wa sheria: Kifungu cha 128 cha EPOCA kinamtaka mtumiaji wa simu kutoa taarifa ya kupotea au kuibiwa kwa simu au laini ya simu. Kifungu cha 134 kinayataka makampuni ya simu kutokutoa huduma kwa simu ambayo imefungiwa kama ilivyoelezwa hapo juu. Mara tu mteja anapopoteza simu yake ya kiganjani anatakiwa kutoa taarifa kwa kituo cha Polisi  cha karibu ambapo atapewa namba ya kumbukumbu ya taarifa ya tukio, maarufu kama RB. Anatakiwa aende kwa mtoa huduma kutoa taarifa ya tukio akiwa na hiyo RB na uthibitisho wa umilki wa simu iliyopotea (risiti aliyopewa wakati wa kununua iwapo itakuwepo).
Mtoa huduma kwanza atahakiki umilki wa simu iliyopotea au kuibiwa na atampatia mteja namba ya kumbukumbu kwamba simu hiyo imefungiwa isutumike kwenye mitandao ya simu na hatimaye ataifungia simu hiyo ndani ya saa 24.


  1. Kujenga misingi ya matumizi ya simu halisi, zisizo bandia. Mtumiaji ataweza kutambua iwapo simu aliyo nayo inakidhi viwango, ni halisi na sio bandia.

Mashabiki ‘Wamteka’ Mwamuzi Mechi ikiendelea

$
0
0

MASHABIKI wa timu ya Friends Rangers, jana Jumanne uvumilivu uliwashinda baada ya kuchukua maamuzi magumu ya ‘kumteka’ mwamuzi wa pembeni aliyekuwa akichezesha mchezo wao dhidi ya Misosi FC kwenye Uwanja wa Makurumla, Magomeni, Dar.

Mchezo huo wa hatua ya 32 Bora ya michuano ya Sports Extra Ndondo Cup, ulimalizika kwa Misosi kuibuka na ushindi wa bao 1-0 lilofungwa na Idd Selemani dakika ya 31.

Championi lililokuwepo uwanjani hapo, liliwashuhudia mashabiki hao dakika ya 80 wakimbeba mwamuzi huyo ambaye jina lake halikufahamika haraka kwa madai kuwa alikuwa akiionea timu yao.

Hata hivyo, mwamuzi huyo aliachiliwa na kurudi uwanjani kumalizia mchezo huo ambao muda mwingi ulitawaliwa na vurugu zilizokuwa zikifanywa na mashabiki wa Friends.

Shinyanga: Amnyonga Mkewe kwa Kuchelewa Kurudi Nyumbani!

$
0
0

MWANAMKE mmoja aliyejulikana kwa jina la Rehema Tumbo amenyongwa hadi kufa na mumewe, Raphael Kazembe kwa kutumia khanga kisa kikuu kikidaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Graiftoni Mushi, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na inadaiwa kuwa mwanamke huyo alichelewa kurudi na alipomgongea mumewe huyo chumbani wanakolala hakumfungulia mlango, ndipo alipoamua kwenda kulala kwenye chumba cha watoto.

Baada ya Rehema kulala kwenye chumba hicho cha watoto mumewe huyo aliamua kumfuata na kuanza kumpiga kisha kumnyonga hadi kumuua.

Baada ya mtuhumiwa kutenda unyama huo inadaiwa kuwa alikimbia ambapo mpaka sasa polisi mkoani humo bado wanaendelea na juhudi za kumsaka ili afikishwe kwenye mikono ya sheria.

Aidha Mwenyekiti wa Mtaa huo Bw. Edward Mihayo amesema taarifa zilimfikia kutoka kwa wanamtaa waliomfuata kumwambia mara baada ya kushuhudia maiti ya Rehema ikiwa imenyongwa kwa khanga.

Kinana: Watawala Wawe na Ujasiri wa Kuomba Radhi

$
0
0

Kinana amekazia haya wakati wa kongamano la Kigoda cha Mwalimu. Amemtumia Mwalimu kuwataka watawala kuomba radhi pale wanapowakosea wananchi!!


Hivi karibuni watawala wamekuwa wakifanya mambo kwa kukurupuka mfano Uhaba wa Sukari, na kuita vijana wetu vilaza,lakini wamekuwa wabishi kukiri makosa.

Bus la TAHMEED lateketea kwa moto

$
0
0

Leo BASI LA TAHMEED LATEKETEA KWA MOTO MCHANA HUU

Basi la abiria mali ya Kampuni ya Tahmeed, lililokuwa likitokea Jijini Tanga kuelekea Jijini Dar es salaam, likiteketea kwa moto mchana huu katika eneo la Komkonga.  Inaelezwa kuwa Ajali hiyo imetokea wakati Basi hilo likiwa limesimama baada ya Abiria mmoja kuomba msaada tutani "WA KENDA KUCHIMBA DAWA" ambapo baadhi ya Abiria wengine nao walishuka na kusikia harufu ya tairi linaloungua. muda mchache tu tairi hilo lilipasuka na moto kuanza kusambaa hadi kwenye tanki la Mafuta.
Hakuna mtu yeyote aliepoteza Maisha kwenye ajali hii na hakuna mali iliyoweza kuokolewa.

Maalim Seif afunguka kuhusu Lipumba, amesema alijiuzulu mwenyewe hakulazimishwa

$
0
0

Katibu mkuu wa CUF Maalim Seif amejitokeza na kuongelea hatua ya aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho, Prof. LIpumba ya kuomba kurudia nafasi ya Uenyekiti.

Amesema kwamba maamuzi ya CUF hufanywa kwenye vikao, tayari kuna kamati ya muda iliyoundwa na Baraza Kuu na hakuwezi kuwa na uongozi juu ya uongozi.

Amesema kuwa Lipumba alijiuzulu mwenyewe, bila kulazimishwa, alibembelezwa hadi na viongozi wa dini na akakataa na kuondoka.
Viewing all 104775 articles
Browse latest View live




Latest Images