Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live

Aliyelawiti Watoto Wawili Akijifanya Polisi Ahukumiwa Kifungo cha Miaka 60 Jela

$
0
0
MAHAKAMA ya Wilaya ya Bunda, mkoani Mara imemhukumu, Ally Mpemba au Ustadhi (32), Mkazi wa Mtaa wa Bunda Stoo mjini Bunda kifungo cha miaka 60 jela baada ya kupatikana na hatia ya kubaka watoto wawili kwa zamu akijifanya polisi.

Adhabu hiyo ilitolewa juzi na Hakimu wa Mahakama ya wilaya ya Bunda, Said Kasonso, baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo pasipo kuacha shaka yoyote.

Awali ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Hamuza Mdogwa, kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo mnamo Januari 17 mwaka huu, majira ya saa 8:30 mchana, katika kijiji cha Kitaramanka wilayani hapa.

Alisema kuwa mshtakiwa huyo aliwakuta watoto hao wakiwa katika eneo hilo na akawatisha kuwakamata akidai kuwa yeye ni askari Polisi na kwamba wamefanya kosa hivyo atawachukua maelezo yao na baadaye awapeleke kituoni.

Aliongeza kuwa mshtakiwa huyo alitoa Sh 200 na kumpatia mtoto mmoja aende akanunue daftari la kuandikia maelezo yao, na baada ya mtoto huyo kwenda ndipo alipombaka aliyebaki na kisha kumwambia adhabu yake imekwisha sasa aende nyumbani.

Alisema kuwa baada ya yule aliyetumwa daftari kurudi, Mpemba alimbaka pia na kumuamuru arudi nyumbani adhabu yake imekwisha na kwamba watoto hao baada ya kufanyiwa unyama huo walikwenda kutoa taarifa nyumbani kwa wazazi wao.

Aidha alisema kuwa Ofisa Mtendaji wa kata hiyo kwa kushirikiana na wananchi wa kijiji hicho walimkamata mshtakiwa huyo na kumfikisha Polisi.

Kabla ya adhabu kutolewa mshtakiwa huyo alipewa fursa ya kujitetea na akaiomba Mahakama hiyo impunguzie adhabu.

Hata hivyo mwendesha mashitaka huyo aliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa mshtakiwa huyo kwa sababu makosa aliyofanya ni ya kinyama na ya udhalilishaji mkubwa kwa watoto hao wenye umri wa miaka 16 kila mmoja.

Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Kasonso, alisema kuwa ameridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na kwamba kwa kosa la kwanza la kubaka mtoto wa kwanza ataenda jela miaka miaka 30 na la pili pia atatumikia kifungo cha miaka 30 jela na adhabu zote zinakwenda kwa pamoja hivyo atatumikia kifungo cha miaka 30 jela ili iwe fundisho kwake na kwa watu wengine wenye nia na tabia kama hiyo.

VIDEO: Ronaldo Alivyowazuia Askari Kumkamata Shabiki Aliyetaka Kupiga Selfie na yeye

$
0
0
Licha ya machungu ya kushindwa kupata ushindi kwenye mchezo wa Ureno vs Austria, superstar wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo aliwazuia walinzi wa uwanja waliokuwa wanataka kumwondosha shabiki aliyevamia uwanjani na kupiga naye selfie.

Baada ya mchezo kumalizika, ghafla shabiki alishuka toka jukwaani na kuvamia uwanjani kisha kumwelekea Ronaldo akitaka kupiga naye picha ‘selfie’. Walinzi wa uwanjani wakamkimbilia shabiki huyo na kutaka kumtoa uwanjani lakini Ronaldo aliwazuia kisha kupozi na shabiki huyo kwa ajili ya picha.

Wakati mashindano ya Euro yakiendelea, nchini Ufaransa kumekuwa na hali ya wasiwasi huenda matukio ya kigaidi yakatokea katika kipindi hiki. Ulinzi umekuwa ukiimarishwa kila kukicha lakini bado matatizo madogomadogo yamekuwa yakijitokeza.

Kila mtu amekuwa akifurahia hali ya utulivu ya sasa huku kukiwa hakujaripotiwa vurugu za mitaani pamoja na urushaji wa mafataki uwanjani, shabiki huyo alijitosa uwanjani na kuwaacha watazamaji wakisubiri kuona walinzi watachukua hatua gani.

Hii hapa video inayokupa fursa ya kushuhudia tukio zima:

Mrembo Malkia Afunguka "Nimechoshwa Kufananishwa na Lulu Michael"

$
0
0
MSANII wa Muziki wa Kizazi Kipya anayefanya vizuri, Malaika Exavery amesema anakerwa na kitendo cha watu wengi kumfananisha na muigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’.

Akizungumza na gazeti hili, Malaika alisema huko nyuma alipokuwa akifananishwa na msanii huyo hakujali, lakini kadiri siku zinavyozidi kwenda imekuwa ni shida hadi wengine wanamsimamisha.

“Unajua kufananishwa na mtu siyo tatizo, lakini kwa hali ilivyo hivi sasa lazima mtu usikie kuchoka kabisa kwa sababu hata wakati mwingine unaendesha gari mtu anakusi mamisha halafu akikuangalia usoni vizuri anaondoka, anasema alidhani ni Lulu,” alisema Malaika.

List ya Nchi 11 zinazoongoza Kwa Amani na Usalama Duniani

$
0
0
List ya nchi zenye usalama zaidi duniani kwa mwaka 2016 imetoka hivi karibuni ambapo nchi 11 zimetajwa kuongoza kwa kuwa na usalama na amani zaidi. List hiyo ilihusisha mataifa 163 ambapo ilijulikana yale yanayoongoza kwa amani na usalama pamoja na yale ambayo ni hatari zaidi kuishi kutokana na hali ya usalama.

Toleo la 10 la kila mwaka lililotolewa June 8 2016 limetaja viwango vya amani na usalama kupitia system ya ramani  shirikishi ya mtindo wa rangi za kujificha, kila nchi ilitolewa alama kati ya 5, nchi zenye alama chini ya 5 ndio zenye hali kubwa ya usalama na amani na zilizoizidi namba 5 ndizo hatari zaidi.

Ulifanyika uchambuzi wa mambo 23 chini ya makundi matatu, Usalama na amani ya taifa, Migogogro ya ndani na nje ya nchi pamoja na huduma za kijeshi. Nchi ya Iceland inatajwa kuongoza kwa kuwa na amani zaidi kutokana na utulivu wa jamii yake.

Nchi za ulaya zinaongoza kutokana na kutokuwa na migogoro ya ndani na nje pamoja ya hali ya utulivu kwa ujumla, japokuwa Afrika inasifika kuwa na nchi zenye  amani hakuna hata nchi moja ya Afrika iliyopo katika list. Hata hivyo imetoka pia list ya nchi ambazo usalama wake ni wa chini sana ambapo nchi za Syria, Iraq, Sudan Kusini, na Afghanistan .

CHANZO: independent.co.uk

ORODHA YA NCHI 11 ZINAZOONGOZA KWA KUWA NA USALAMA NA AMANI ZAIDI DUNIANI

11.Finland – 1.429

10. Slovenia – 1.408

9. Japan – 1.395

8. Canada – 1.388

7. Switzerland – 1.37

6. Czech Republic – 1.36

5. Portugal – 1.356

4. New Zealand – 1.287

3. Austria – 1.278

2. Denmark – 1.246

1. Iceland – 1.192

Alikiba:Unaweza Nichukia, Ukapenda Muziki Wangu

$
0
0
Msanii Alikiba amefunguka na kusema kuwa muziki hauna siri na muziki hauna tofauti kati ya mtu na mtu kwani unaweza kuwa una chuki na yeye lakini akiimba muziki mzuri ukapenda kazi yake na kuimba.

Alikiba alizidi kutoa ufafanuzi kuwa kama binadamu inawezekana ukatoa labda humpendi mtu fulani au msanii fulani kutokana na mambo yake lakini inapokuja kwenye muziki inakuwa tofauti maana msanii anapofanya wimbo mzuri, utajikuta tu unaimba wimbo ule kwa kuwa muziki una nguvu na haina mipaka, wala tofauti.

Alikiba alizidi kusema kuwa hata kama unaweza kuwa unamchukia mtu inafika wakati unasahau na kupotezea na maisha ya kawaida yanaendelea na kujikuta ule utofauti wenu umepotea

Mtoto Mdogo wa Miaka 3 Abakwa na Baba yake Mzazi

$
0
0
Jeshi la polisi wilayani Kishapu, mkoani Shinyanga linamshikiria mtu moja Ngasa Sakwa mwenye umri wa miaka 23 mkazi wa kitongoji cha lukelege, kijiji cha Masagala, kata ya Maganzo, wilayani humo, kwa tuhuma za kumbaka mwanae wa kike, Shida Ngasa, mwenye umri wa miaka 3, na kumsababishia maumivu makali, tukio hilo lilitokea juni 9, mwaka huu katika mji mdogo wa Maganzo wilayani humo.

Kesi hiyo yenye namba MGZ/IR/256 imefunguliwa katika kituo kidogo cha polisi Maganzo na bibi wa mtoto huyo, Milembe Luhende wa kijiji hicho kufuatia kubaini mjukuu wake kufanyia kitendo hicho cha kikatili na mwanae wa kiume ambapo siku ya tukio kijana huyo, anayefanya kazi ya ulinzi katika nyumba ya kulala wageni ya Nsamaka iliyopo Maganzo  alimchukua mtoto huyo na kwenda naye kazini kwake ambapo baada ya kumrejesha nyumbani ndipo walipogundua kufanyiwa kitendo hicho.

Kitendo hicho kinahusishwa na imani za kishirikina na matumizi ya dawa za kulenywa kutokana na uhalisia wa eneo la maganzo wakazi wake kujihusisha shughuli za uchimbaji madini huku serikali ikisisitiza mhusika achukuliwe hatua kali za kisheria.

Wanawe Kagame Waichezea Timu ya Rwanda

$
0
0
Kwa mara ya Kwanza wanawe rais wa Rwanda Paul Kagame, Bryan Kagame na Ian Kagame waliiwakilisha timu ya taifa ya Rwanda kwa wachezaji wasiozidi miaka 20 katika mechi ya kuadhimisha miaka 22 tangu mauaji ya kimbari nchini Rwanda. Mchuano huo wa kumbukumbu, kati ya Rwanda na Morocco ulioandaliwa katika uwanja wa Amahoro, mjini Kigali ulikamilika kwa sare ya goli moja.

Ingawa wote wawili hawakukamilisha mechi hiyo. Kocha wa Rwanda Kayiranga Jean Baptista aliwapa nafasi ikiwa ni mechi yao ya kwanza kuvaa sare ya timu ya taifa ya soka.
Ian Kigenza Kagame alijumuishwa katika kikosi kilichoanza kabla ya kumpisha Park Udahemuka kunako dakika ya 27.

Rwanda maarufu nyigu wachanga walitangulia katika dakika ya kwanza kupitia Blaise Itangishaka. Hata hivyo Morocco ilisawazisha katika dakika ya 43 baada ya Morocco Dari Achraf kumuandalia krosi Hicham Boussoufiane.


Kunako dakika ya 74, Kitinda mimba wa familia ya kagame, Bryan Kagame alichukua nafasi yake Djabel Manishimwe.

Baba yao wawili hao, Rais Paul Kagame ni shabiki wa soka na tenisi na ni shabiki sugu wa klabu ya Arsenal ya Uingereza.

Watatu Wafa Wakidaiwa Kula Mihogo yenye Sumu

$
0
0
Watu watatu wamefariki dunia baada ya kula mihogo inayodhaniwa kuwa na sumu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei amesema jana kuwa tukio hilo juzi saa tisa mchana katika Kijiji cha Kauzeni, Manispaa ya Morogoro.

Amesema watu hao ni kati ya watano waliokula mihogo hiyo, lakini wawili walinusurika baada ya kuwahishwa Hospitali ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Mzinga kwa matibabu.


SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu Ya June 20, Ikiwemo ya Msaidizi wa Askofu Gwajima Atoa Tamko

$
0
0


SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu Ya June 20, Ikiwemo ya Msaidizi wa Askofu Gwajima Atoa Tamko

JESHI la Polisi Laendelea Kuikaba Chadema, Mahafali Mengine ya CHADEMA Yatawanywa

$
0
0
Jeshi la Polisi mkoa Kilimanjaro jana liliwatawanya wahitimu wa vyuo vikuu kupitia umoja wa Chadema (Chaso), waliokuwa wamekusanyika mjini Moshi kwa ajili ya mahafali yao.

Dalili za ‘kibano’ hicho zilianza kuonekana asubuhi wakati polisi na askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) wakiwa wamejihami kwa mabomu ya machozi, walipozingira hoteli ya Keys inayomilikiwa na Philemon Ndesamburo.

Hoteli hiyo iliyopo maeneo ya Kwa Alfonsi nje kidogo ya mji wa Moshi, ndipo ambako mahafali hayo ambayo yalikuwa yahusishe wahitimu 70 kutoka vyuo vikuu vinne yalikuwa yafanyike.

Wanafunzi hao ni kutoka Chuo Kikuu cha Mwenge (Mwekau), Chuo cha Kikuu cha Ushirika Moshi (Mocu), Chuo Kikuu cha Masoka na Chuo Kikuu cha Tiba KCMC (KCMU Co).

Hata hivyo, polisi wakiwa na magari yaliyokuwa yakipeperusha bendera nyekundu, walivamia hoteli hiyo na kuwataka wahitimu hao kutawanyika kwa amani, kwa vile mikusanyiko ya aina hiyo imezuiwa.

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chadema (Bavicha) mkoani Kilimanjaro, Dickson Kibona alilaani tukio hilo akisema hakukuwa na sababu yoyote ya kuzuia mahafali hayo.

“Wamezuia bila sababu yoyote na hii inakiuka misingi ya kidemokrasia, Katiba ya nchi na sheria ya vyama vya siasa,” adai Kibona.

Kibona alidai kama isingekuwa kuhofia maslahi ya kibiashara ya Hoteli ya Keys ambapo kulikuwapo pia watalii, wangegoma kuondoka kwa kuwa hawakuvunja sheria yoyote ya nchi.

Mmiliki wa hoteli hiyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema Mkoa Kilimanjaro, Philemon Ndesamburo, alisema ndiye aliyewashauri vijana hao kutawanyika kwa amani na kuwataka wasibishane na polisi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa alisema polisi walipata taarifa kuwa wahitimu hao wangekuwa na mkutano wa kisiasa ambao ulijificha kwa mwavuli wa mahafali.

“Tumewaita viongozi wao na kuwaeleza kuwa mikutano yote ya kisiasa imezuiwa na watawanyike. Walituelewa na wakatawanyika, lakini sisi bado tunaendelea kuimarisha doria mitaani,” alisema.

Hili ni tukio la pili kwa wanachama wa Chaso kutawanywa na Polisi ambapo juzi katika hoteli ya African Dream mjini Dodoma, wahitimu wa vyuo vikuu mjini Dodoma nao walitawanywa na FFU.

Mkuu wa Idara ya Habari wa Chadema, Tumaini Makene alisema Chadema inaendelea kuhifadhi kumbukumbu za matukio yote yanayoendelea nchini, ili kujenga ushahidi utakaojitosheleza pindi itakapoonekana ni mwafaka kuchukua hatua zaidi.

Alifafanua kuwa chama hicho kinatambua hila zinazofanywa na Serikali kwa kulitumia Jeshi la Polisi, na kuwa wanatambua amri zinazotolewa na watendaji wa chama tawala kupitia wakuu wa mikoa na wilaya.

Alisema wanao ushahidi wa matukio yote utakaotumika muda wowote, watakapoamua kuishtaki Serikali ndani au nje ya nchi.

YANGA Yashindwa Kutamba Kwa Waarabu..Yapokea Kichapo Bila Ubishi.....

$
0
0
Mabingwa wa soka la Tanzania bara Yanga SC wameanza vibaya kampeni zao za kuwania kombe la Shirikisho Afrika baada ya kupoteza mchezo wao wa kwanza kwa bao 1-0 dhidi ya MO Bejaia ukiwa ni chezo wa Kundi A.

Yassin Sahli alifunga bao pekee kwenye mchezo huo na kuipa pointi tatu MO Bejaia iliyokuwa ikicheza kwenye uwanja wake wa nyumbani Stade de I’Unite Maghrebine mjini Bejaia, Algeria.


Matokeo hayo yanaiacha Yanga katika nafasi ya tatu huku TP Mazembe wakiwa ndiyo vinara wa Kundi baada ya kushinda mchezo wao kwa magoli 3-0 dhidi ya Medeama ambayo inaburuza mkia.

Mazembe na MO Bejaia zinapointi sawa (pointi tatu) lakini TP Mazembe anaongoza kundi kwa tofauti ya magoli wakati Yanga na Medeama zikiwa hazina pointi lakini Yanga inakaa nafasi ya tatu kwa tofauti ya magoli. Medeama imefungwa magoli matatu wakati Yanga wameruhusu bao moja pekee.


Mchezo ujao wa Yanga utakuwa nyumbani (Dar es Salaam) June 28 itakapowaalika TP Mazembe kwenye uwanja wa taifa.

Kubenea Athibitisha Umiliki wa Kiwanja Alichokataa Hussein Mwinyi, Ataka Ajiuzulu Kama Alivyoahidi

$
0
0
Mbunge wa Ubungo Said Kubenea ameonyesha nakala zinazothibitisha umiliki wa kiwanja alichokataa waziri wa ulinzi Hussein Mwinyi na ametaka mbunge huyo kujiuzulu.

Amesema kiwanja hicho alikitaja bungeni na Dk. Mwinyi akadai madai yake yote ni ya uwongo mtupu na kukiwa hata na chembe ya ukweli atajiuzulu na sasa amemtaka ajiuzulu kweli kama alivyoahidi.

Mbunge huyo pia amesema ameapanga kumshitaki naibu spika kwenye kamati ya maadili kwa madai kuwa anatumia kanuni za bunge isivyo kikanuni

 Angalia Video:

VIDEO: Highlights na Goli la Mechi ya MO Bejaia vs Yanga June 20, Full Time 1-0

$
0
0
Usiku wa June 20 2016 Dar es Salaam Young Africans walikuwa Algeria kucheza mchezo wao wa kwanza wa Kundi A wa hatua ya nane bora dhidi ya wenyeji wao MO Bejaia, katika mchezo huo Yanga walifungwa na MO Bejaia kwa goli 1-0, goli ambalo lilifungwa na Armando Sadiku dakika ya 20.

Video:

Huu Ndio Utajiri Mkubwa Utakaoupata, Kama Utaamua Kufanya Biashara Hii.

$
0
0
MAKALA HII IMEANDIKWA NA MESHACK MAGANGA WA IRINGA TANZANIA.
Kwa muda mrefu nimekuwa nikitoa hamasa kwa vijana wenzangu wa kike na kiume na watu wa kada mbalimbali, wito wangu umekuwa nikuwataka vijana wenzangu kauanza utamaduni wa kuwekeza kwa muda mrefu na kujifunza ujasiriamali. Ninaandika makala hii kutoa ushuhuda wa niliyoyafanya kwa muda wa zaidi ya miaka miwili iliyopita na kuniletea mafanikio makubwa.

Nilianza kujishighulisha na ujasiriamali nilipokuwa chuo kikuu mwaka wa pili, kwa kuuza vocha na  kazi ya ‘steshenari’ na uuzaji wa laptop, sikuendelea nazo sana kwa sababu ya kubanwa na masomo yachuo. Nilipomaliza chuo 2010, nilianza kilimo cha mboga na kufuga kuku hapa Iringa mjini, baada ya hapo kaka yangu alianza kunihimiza kuhusu kilimo cha miti ambacho yeye mwenyewe anafanya.

Na baadaye nikakutana na rafiki yangu Albert Sanga ambaye pia anajishughulisha sana na kilimo cha miti. Tangu 2011 nilinunua shamba la ekari 10 na kuzipanda miti hela ambayo niliipata baada ya kuuza matango niliyolima kijijini Kalenga, nikaongeza bidii zaidi ya kulima matango na kununua mashamba, leo nina ekari nyingi.

Albert sanga, mjasirimali na mwekezaji alipata kuandika haya kuhusu mimi:- “UNASUBIRI UPATE MTAJI? OPSss! UNAWEZA KUFA MASIKINI! Nina rafiki yangu mpambanaji kweli kweli na msomi wa chuo kikuu wa mambo ya maendeleo na elimu; na mtaalamu wa IT, anaitwa Meshack Maganga. Wakati fulani huko nyuma alinifuata na kuniambia, "Sanga nimeamua kuanza kui-invest katika mashamba ya miti; mtaji wa kuanzia nina tsh elfu ishirini na tano, (25,000?/=).

Nikamwambia "Kupata ekari moja si chini ya laki sita na wewe una tsh 25,000/= utawezaje?" Akanijibu "Nitaweza!", Sikumwelewa! Kumbe alikuwa anaona mbali! Alichofanya alichukua hiyo 25,000/= akaenda nayo eneo moja linaitwa Kalenga (km 20 kutoka Iringa mjini) huko akalima matango. Angalia mchanganuo: Shamba nusu eka akakodi kwa tsh 10,000/=, mbegu za matango akanunua Tsh. 7,000/=.

Kwenye kulima akalima kwa mikono yake akisaidiana na kibarua mmoja. Fedha iliyobaki 8,000/= akalipa kibarua na kununulia dawa ya kuua wadudu. Alipokuja kuvuna akapata tsh 800,000/= (laki nane). Alipokuja na fedha hii tukaenda kutafuta shamba la miti akaanza na ekari moja huku pesa nyingine akairudisha shambani.

Hivi leo Bw. Maganga ana ekari zisizopungua hamsini za mashamba ya miti na anaendelea na kilimo cha umwagiliaji. Lakini HAPO amefika kwa kutumia tsh 25,000/= tu. Tunaposema hauhitaji mamilioni kujiajiri tunatamani ujifunze kutoka kwa waliofanikiwa kama Bw. Maganga. Unaweza kumwandikia” Akaendelea kwa kusema:-

Kuhusu kilimo cha miti ninacho kifanya mimi na nimepania kwelikweli ndani ya nchi yangu niipendayo Tanzania ni kwamba, kimepata umaarufu wa ghafla miaka ya hivi karibuni kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ongezeko la mahitaji ya mazao ya miti na changamoto ya mazingira. Katika Tanzania mkoa wa Iringa ni moja ya mikoa maarufu inayoongoza kwa misitu mikubwa ya kupandwa.

Miti inatumika kwa mbao, nguzo za umeme, nguzo za kujengea pamoja na utengenezeaji wa karatasi. Ukiacha mahitaji haya tuliyoyazoea; hivi sasa kumeibuka fursa nyingine mpya ambapo mashirika ya kimazingira kutoka Magharibi yananunua hewa ukaa. Kwa maana hiyo unaweza kupanda shamba la miti halafu ukawa unakusanya dola kwa kuuza hewa ukaa wakati ukisubiri miti ikomae uvune mbao, nguzo ama miti ghafi ya kutengenezea karatasi.

Hii ni sawa na kutegeneza hela ukiwa umelala. Mbali na kuuza hewa ukaa, vile vile unaweza kufuga nyuki na kuendelea kuvuna asali wakati unasubiri kukusanya mamilioni kwa kuuza miti ya nguzo, karatasi ama mbao.Kilimo hiki cha miti ni uwekezaji wa muda wa kati na mrefu (middle& long term investments). Kiutamaduni watanzania wengi huwa hawavutiwi na uwekezaji wa muda mrefu.

Hata hivyo kama una mpango wa kuwa na “financial freedom” usikwepe kufikiria uwekezaji wa muda mrefu. Waingereza husema “Information is power”. Wengi hawajachangamkia fursa hii kwa kukosa taarifa tu. Kazi yangu leo ni kukupa taarifa hizi za utajirisho. Miti ya mbao inatumia wastani wa miaka sita hadi 8 au saba, tangu kupandwa hadi kuvunwa kwake.

Hii ina maana inapofikisha umri wa miaka sita huwa tayari kwa kuanza kuvunwa kwa mbao ndogo. Ekari moja ya shamba inachukua wastani wa miti mia sita (600). Wastani wa chini wa mti mmoja kwa sasa uliokomaa ni shilingi elfu ishirini (30,000 hadi 60,000,inategemea na ukubwa wa mti). Ina maana katika ekari moja ukiwa na miti iliyokomaa unakusanya jumla ya shilingi milioni kumi na nane (18,000,000).

Fedha hiyo (kadirio la chini kabisa) utaipata ikiwa unaamua kuuza kwa bei ya jumla miti ikiwa shambani. Lakini kama ukiamua kupasua mbao wewe mwenyewe unaweza kuvuna mbao hadi za milioni thelathini na mbili (32,000,000) kwa ekari moja. Hadi sasa uhitaji (demand) wa mbao katika soko ni mkubwa kuliko ugavi (supply) hivyo kwa miaka 10 ijayo hatutarajii kushuka kwa soko la mbao, nguzo ama malighafi za karatasi.

Gharama ya kununua shamba tupu ni kati ya shilingi  laki moja na 20 elfu (120,000) na laki moja, kutegemea na maeneo husika unayotaka ama kupata. Gharama za kuandaa shamba, kununua miche na kupanda ni kati ya shilingi laki moja  na nusu,na laki moja. Hii ina maana unaweza kumiliki ekari moja ya msitu wa miti kwa hadi shilingi laki sita tu! Kutegemea na umri wa miti unayotaka.

Mtu unaweza kuona kuwa pengine kununua shamba tupu na kuanza kuhangaika na upandaji miti itakuwa ni mlolongo mkubwa; kukusaidia katika hilo nimekuwa na utaratibu wa kumilikisha mashamba yenye miti (kuuza) kwa bei nafuu sana. Yapo mashamba yenye miti ya kuanzia mwaka mmoja, miaka miwili, miaka mitatu na miaka minne.

Uponunua mashamba haya kutoka kwangu, mimi naendelea na upandaji wa mashamba mapya kupitia fedha hizo. Kilimo cha miti ni rahisi sana kwa sababu ukishapanda hakihitaji uangalizi mkubwa sana na wala hauhitajiki uwe karibu na shamba/mradi muda wote. Kuna kazi chache ambazo zinahitajika ukishapanda shamba lako.

Mvua inyeshe ama isinyeshe mti wa mbao, nguzo ama karatasi ukishachipua huwa haufi kwani huendelea kutumia unyevu wa ardhini. Kazi namba moja unapokuwa umeshakamilisha upandaji wa miti kwenye shamba; ni kutengeneza njia za kuzuia moto walau mara moja kwa mwaka, kazi ya pili ni kufyekea miti inapokua walau kwa mwaka mara moja (prooning).

Gharama zote hizo yaani kutengeneza njia za moto, kufyekea na kulinda moto haizidi laki mbili kwa mwaka mzima. Kwa maana hii gharama za kuhudumia shamba la miti ekari moja kutoka kupandwa hadi kuvunwa ni wastani wa shilingi milioni moja tu. Gharama hizi ninazopiga ni ikiwa utaamua kununua shamba leo na kama ungekuwa tayari una shamba ambalo unalihudumia leo.

Hata hivyo nadhani wote tunafahamu kuwa ardhi ni rasilimali inayopanda thamani kila siku. Vile vile tunatambua kuwa suala la mazingira ni tete kwa sasa na katika karne zijazo kama wataalamu wanavyotuthibitishia. Hii ina maana kuwa ukiwa na shamba la miti leo; thamani ya ardhi hiyo inazidi kupanda kila siku na miti uliyopanda inazidi kupanda thamani kila kukicha.

Jambo la uhakika ni kuwa hata kama bei ya miti, mbao, nguzo itayumba hutaweza kupoteza mtaji uliotumia na wala hutakosa kuzalisha faida kwa shamba utakalokuwa umemiliki, iwe ni eka moja, kumi, mia ama elfu moja. Mbali na hivyo unaweza ukaona, ahaa, miaka sita hadi kumi ni mingi mno; bado una nafasi ya kupata faida hata ndani ya mwaka mmoja, miwili au mitatu.

Ukishapanda shamba la miti ekari moja kisha baada ya mwaka mmoja ukaamua uuze utauza si chini ya milioni mbili hadi nne. Kukusanya milioni nne kwa mtaji wa laki sita, pasipo kutumia muda mwingi ama usumbufu wa kusimamia; hakika ni faida nono.

Huenda hadi kufika hapa unaweza ukawa umeshavutiwa na biashara hii. Wengi wenu mnaweza kujiuliza maswali mkubwa mawili; “Ninatamani nifanye mradi huu lakini Iringa sikufahamu na hata kama nakufahamu nitaanzia wapi kupata hayo maeneo?” Pili: Niko mbali na sina muda wa kushinda Iringa, Je, ni nani atanisaidia kupanda, kusimamia na kuendesha hayo mashamba?

Ili kutimiza ndoto yangu hiyo nimeweka utaratibu ufuatao utakaohakikisha kila mwenye ndoto, kiu na hamasiko la kuwekeza kwenye kilimo cha miti anafanikiwa.  Jisikie huru wakati wowote kuwasiliana nami kwa ufafanuzi na msaada wa fursa hii. Natamani watanzania tuache kulalamika kuhusu wageni kuvamia ardhi yetu, badala yake tuchangamke kumiliki na kufanya uzalishaji katika ardhi yetu.

Inawezekana! Kwa kutumia sheria ya ardhi ya mwaka 1999 sheria namba 5 utapata documents za umiliki; kwa kuzingatia taratibu na tamaduni zote za wenyeji zinazohusiana na umilikaji ardhi nitahakikisha nakusaidia ili ndoto yako itimie.

Yupo Baba yangu anaishi Mafinga ambae siku za karibuni amepewa Tuzo ya Rais kwa kuwa mpandaji namba moja wa miti na utunzaji wa mazingira, ameahidi kutoa msaada kwa Mtanzania wa ndani na nje ya Tanzania kumsadia kupata eneo la kupanda miti na kauli ya siku zote ni “USIKUBALI KUWA MNYONGE WA KIUCHUMI NDANI YA TANZANIA.

Mtemi wa Wasukuma afariki dunia

$
0
0
Mteni wa kabila la Wasukuma wilayani hapa Mkoa wa Mwanza, John Nyanza (70), amefariki dunia.

Katibu wa Umoja wa Watemi wa Usukuma, Charles Itale, amesema jana kuwa mtemi huyo alifariki dunia Juni 15, mwaka huu  majira ya alfajiri kwa ugonjwa wa saratani.

 “Mtemi mwenzetu alifariki dunia katikati ya wiki iliyopita wakati akiendelea kupatiwa matibabu Hospitali ya Rufaa Bugando (BMC),” amesema Itale.

Utemi wa Usukuma ambao makao makuu yake yapo Bujora, unaundwa na mikoa ya Shinyanga, Simiyu na Mwanza.

Breaking News: Wabunge wa Upinzani Waziba Midomo yao Kwa Karatasi na Plasta na Kisha Kutoka Nje

$
0
0
Wabunge wa Kambi ya Upinzani Bungeni leo wametumia mtindo mpya kueleza hisia zao baada ya kuamua kutoka kwenye ukumbi wa Bunge wakiwa wamejifunika midomo kwa karatasi.

Hii ni wiki ya pili mfululizo wabunge hao wamekuwa wakitoka bungeni baada ya kutangaza kutohudhuria kikao cha bunge kinachoongozwa na Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson.

Mbunge wa Vunjo (NCCR-Mageuzi), James Mbatia amesema wameamua kutumia mtindo huo mpya kwa sababu Bunge limekataa kuwasikiliza hoja zao.

Msaidizi wa Askofu Gwajima Afunguka na Kutoa Tamko 'Adui wa Rais wetu Awe Adui yetu Sote'

$
0
0
Waumini wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, jana walisali bila kuwapo kwa Askofu wao, Josephat Gwajima ambaye anatafutwa na Jeshi la Polisi.

Mara nyingi Jumapili, Gwajima ndiye amekuwa akiongoza ibada katika kanisa hilo lililopo Ubungo Kibo, lakini jana iliongozwa na mchungaji Edward Adriano ambaye hata hivyo, hakueleza chochote kuhusu alipo askofu huyo.

Gwajima anatafutwa na polisi baada ya kusambaa kwa sauti inayosikika kama yake akitaka Rais mstaafu, Jakaya Kikwete afikishwe mahakamani kwa yote yaliyofanyika wakati wa utawala wake.

Jana, Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro alisema suala la Askofu Gwajima atalizungumza leo.

Alhamisi iliyopita Polisi walizingira nyumbani kwa Gwajima kwa saa saba, wakitaka kumkamata bila mafanikio.

Kamanda Sirro alisema wanamtafuta askofu huyo ili athibitishe kama maneno yenye uchochezi, yanayosambaa kwenye mitandao ni ya kwake.

Ulinzi kanisani
Ulinzi katika kanisa hilo jana uliimarishwa na vijana waliovaa vizibao vya njano, vilivyoandikwa polisi jamii tii sheria bila shuruti. Idadi ya vijana hao wanaokadiriwa kufika 40, walikuwa wengi kuliko Jumapili nyingine zilizopita.

Licha ya kutokuwapo kwa askofu huyo kanisani hapo, waumini walijaa na wengine kukosa viti huku wengine wakionekana kusimama nje ya kanisa hilo.

Kauli ya  Msaidizi wa Gwajima
Msaidizi wa Askofu Gwajima, Yekonia Bihagaze, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Facebook, alisema juzi kuwa taratibu, sheria na kanuni zinapaswa kufuatwa kumkamata kiongozi wao.

"Kanisa la Ufufuo Na Uzima ni makini, tulivu na halikurupuki kwenye maamuzi yake. Na nchi haiongozwi mitandaoni, kama serikali inamtaka mtu ziko taratibu, sheria kanuni za kuzifuata," sehemu ya taarifa ya Mchungaji Bihagaze ilisomeka.

"Kwa sasa kila mmoja anaona nchi inapiga hatua kimaendeleo, ni vema wananchi sasa tukaachana na propaganda kama hizi, ni vema tukaweka shabaha yetu moja kushirikiana na Rais tulijenge taifa Letu. Taifa hili si mali ya mtu mmoja, ni mali yetu sote kwa manufaa yetu na vizazi vingine vitavyokuja.

"Adui wa Rais wetu awe adui yetu sote. Siasa zitakuja tu baadaye ila kwa sasa nchi itulie, watu tuchape kazi, tulipe kodi kwa sababu kuna Rais mwenye nia ya kuipeleka mbele.

"Hakuna duniani Taifa linaloweza kuendelea pasipo wananchi kushirikiana bega kwa bega na kiongozi wao."

Nape Asema Lowassa ni Alama ya Ufisadi, ampa ushauri mgumu

$
0
0
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye amenena tena kuhusu uamuzi wa waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa kukihama chama hicho na kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kupewa nafasi ya kugombea urais.

Nape ameeleza kuwa uamuzi huo uliwasaidia kwa kiasi kikubwa kwani mwanasiasa huyo aliyekuwa na nguvu kubwa ndani ya chama hicho alikuwa alama ya ufisadi kutokana na kukabiliwa na tuhuma nyingi za ufisadi.

“Lowassa alikuwa alama ya ufisadi, alipoondoka aliturahisishia kazi. Watu walikuwa wanahusisha ufisadi na umasikini, walichoka na walikuwa radhi kuchagua hata jiwe lakini sio CCM,” alisema Nape.

Alisema kuwa angepata nafasi ya kumshauri Lowassa katika siasa, angemshauri ajiuzulu siasa kabla hajaondolewa kwa aibu katika medani za siasa.

Kadhalika, Nape alisema kuwa kosa kubwa ambalo lilifanywa na vyama vya upinzani ni kumpokea Lowassa ambaye amedai alikuwa amesababisha CCM kupakwa matope ya uchafu kutokana na kuwa na tuhuma nyingi.

Hata hivyo, Nape alimpongeza Lowassa kwa kukubali matokeo ya uchaguzi mkuu kwa kuwa uamuzi huo ulisaidia kuliweka Taifa katika hali ya amani baada ya uchaguzi.

Lowassa amekuwa akikanusha tuhuma zote zilizokuwa zikielekezwa kwake hususan tuhuma za kuhusika na sakata la Richmond lililosababisha ajiuzulu nafasi ya Uwaziri Mkuu katika Serikali ya Awamu ya Nne.

Alijiunga na Chadema na kugombea nafasi ya urais akiungwa mkono na vyama vya siasa vinavyounda Ukawa.

Alipata kura takribani milioni 6 na kusaidia kupata wabunge wengi zaidi wa upinzani akiweka historia ya ushindani mkubwa zaidi kuwahi kutokea kwenye uchaguzi mkuu tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini.

ZariTheBossLady Amtaja Ivan kwenye Post Moja na Diamond Platnumz

$
0
0
Kwenye siku ya BABA duniani wasanii tofauti wameonyesha ukaribu wao kwa watoto na familia zao kupitia instagram na mitandao tofauti ya kijamii.

Couple inayopewa attention kubwa kwa sasa bongo ya Zari na Diamond imechukua nafasi kubwa leo kwenye mitandao baada ya Zari kumtaja Ex wake ambaye ni Ivan [Baba wa watoto watatu wa Zari] kwenye post moja na Diamond Platnumz kitu ambacho hakijawahi kutokea.

Zari aliandika hivi 
"God has his timing for everything and he knows better why he does things at his own time. I know u felt this day would never come in your life but with God, NOTHING IS IMPOSSIBLE. Happy father’s day to you @diamondplatnumz and to the rest of the dads playing great roles in thier kids lives @ivandon. Happy father’s day to all women out there playing both roles"

Picha: Maisha ya Siwema wa Nay wa Mitego baada ya kutoka jela

$
0
0
Mzazi mwenzake na msanii wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, Siwema Edson anaendelea kufurahia maisha ya uraiani ikiwa ni mwezi mmoja toka mahakama ya Mwanza kutengua kifungo cha miaka miwili jela na kumhukumu kifungo cha nje cha miaka miwili.

Aprili mwaka huu mahakama hiyo ilimtia hatiani mrembo huyo kwa kosa la kutukana matusi kwa njia ya mtandao.

Hata hivyo mpenzi wake wa zamani Nay wa Mitego ndiye aliyemsaidia kutenguliwa kwa kifungo hicho cha miaka miwili jela na kuwa cha nje.
Siwema akiwa na kijana anayedaiwa kuwa mpenzi wake
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live


Latest Images