Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live

Nay wa Mitego Apokea Rungu Jingine Kutoka Basata..Wimbo Wake wa Pale Kati Patamu Wahusika

$
0
0

KUFUNGIWA NA KUPIGWA MARUFUKU KWA WIMBO WA ‘PALE KATI PATAMU’ WA MSANII EMMANUEL ELIBARIKI ‘AKA’ NEY WA MITEGO
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limeufungia rasmi wimbo wa ‘pale kati patamu’ ulioimbwa na Msanii Ney wa Mitengo kutokana na ukiukwaji mkubwa wa maadili.

Msanii huyu amekuwa na tabia na mienendo yenye kuchafua Sekta ya Sanaa yeye binafsi kupitia kutoa kazi chafu na kufanya maonesho yenye kukiuka maadili. Kazi zake zikikiuka maadili na kudhalilisha utu wa mwanamke sambamba na kutoa lugha za matusi na za kudhalilisha watu wa kada mbalimbali.

Ieleweke kwamba kwa mujibu wa kifungu namba 4(L) cha Sheria ya BASATA namba 23 ya mwaka 1984, Baraza limepewa jukumu la kuhakikisha linalinda maadili miongoni mwa wasanii wanapokuwa jukwaani au wanapobuni kazi yoyote ya sanaa.

ikumbukwe kwamba BASATA limeshamuita na kumuonya msanii huyu mara kadhaa kutokana na tabia yake ya kutoa kazi zisizokuwa na maadili na aliahidi kubadilika na kuachana na tabia hiyo. Kwa hiyo kuendelea kwake kufanya matukio haya kwa makusudi ni uthibitisho kwamba hajabadilika na kwa maana hiyo ameendelea kuidhalilisha Sanaa na wasanii wa kitanzania wenye kujitambua na kuiheshimu kazi ya sanaa kama kazi nyingine. Kwa sasa Msanii huyu ametoa wimbo mwingine wa Pale Kati patamu ambao uko mitandaoni ukipambwa na picha chafu zinazoonesha mwanamke akiwa mtupu yaani uchi wa mnyama.
Kwa mantiki hii BASATA halitavumilia wasanii wachache ambao wanataka kuigeuza tasnia ya sanaa na wasanii genge la wahuni wasio na staha na wanaojipanga kuibomoa jamii. BASATA linapenda kueleza ya kufuatayo · BASATA linatamka kuwa limeufungia wimbo huu rasmi kutumika kwa namna yoyote ile. · Aidha pamoja na adhabu ya kufungia wimbo huu hatua nyingine za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Aidha, BASATA linawataka Wasanii wote nchini kufuata sheria, kanuni na taratibu mara wanapotengeneza kazi zao.
SANAA NI KAZI, TUIKUZE, TUILINDE NA KUITHAMINI
Godfrey Mngereza 
KATIBU MTENDAJI

Hatimaye Agustine MREMA Apewa Kazi na Rais Magufuli...Ateuliwa Kuwa Mwenyekiti wa Bodi...

$
0
0

Rais John Magufuli amemteua Mwenyekiti wa Chama cha TLP, Agustine Mrema kuwa Mwenyekiti mpya wa Bodi ya PAROLE Tanzania.
Prof. William R. Mahalu, ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete. Uteuzi huu umeanza leo tarehe 16 Julai, 2016.

Wanajeshi 104 Waliotaka Kumpindua Raisi wa Uturuki Wauwa Katika Jaribio la Mapinduzi

$
0
0

Naibu mkuu wa jeshi la Uturuki ametangaza kwa njia ya runinga kuwa jaribio la mapinduzi ya kijeshi limeshindwa.

Jenerali Umit Dundar alisema kuwa wapanga mapinduzi 104 wameuauwa. Pia amesema kuwa watu wengine 90 wakiwemo polisi na raia wameuawa.

Usiku kucha miji ya Ankara na Istanbul ilikumbwa na milio ya risasi na milipuko baada ya wanajeshi waasi kufanya mashambulizi wakitumia vifaru na helikopta.

Maafisa wanasema kuwa zaidi ya wanajeshi 1500 wamekamatwa huku wale wa vyeo vya juu wakiwemo majerali wakipokonywa nyadhifa zao.

Yanga wa Kimataifa Hoi Taifa Yatoka1-1 Dhidi Ya Madeama

$
0
0
YANGA  imeshindwa kutamba kwa mara nyingine tena kwenye uwanja wa  nyumbani baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Medeama SC ya Ghana katika mchezo wa Kundi A michuano ya kombe la Shirikisho Afrika.

Donald Ngoma alianza kuifungia Yanga bao la kuongoza dakika ya pili ya mchezo huo akitumia vema makosa ya safu ya ulinzi ya Medeama na kuiweka timu yake mbele ya Medeama kwa bao 1-0.
Dakika 15 za kwanza watoto wa Jangwani walitawala mchezo kwa pasi za haraka huku wakiliandama lango la Medeama kitendo kilichosababisha wapate kona kadhaa.
yanga 2Donald Ngoma akishangilia baada ya kuifungia Yanga bao.

Medeama walisawazisha bao hilo dakika ya 17 baada ya Bernard Danso kuunganisha mpira wa kona na kufanya matokeo kuwa 1-1 ambayo yalidumu hadi dakika 90 zinamalizika.
Mechi ya leo ilikuwa ni muhimu kwa vijana wa Hans van Pluijm kupata ushindi ambao ungewapa pointi tatu na kunyanyua morali ya kufanya vizuri kwenye kundi lao.

Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Deogratius Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Oscar Joshua/Juma Mahadhi, Kelvin Yondani, Mtogo Vincent Bossou, Mbuyu Twite, Thabani Kamusoko, Simon Msuva, Obrey Chirwa, Amissi Tambwe/Haruna Niyonzima dk na Donald Ngoma.

Medeama FC; Daniel Adjei, Samuel Adade, Moses Sapong, Paul Adoo/Salufu Moro dk62, Daniel Amouah, Kwesi Donsu, Erick Kwakwa, Kwame Boahene, Abbas Mohamed, Bernard Ofori na Enock Atta Agyei/Malik Akowuah dk79.

Faiza Ally Aeleza Jinsi Wasanii wa Filamu wa Kike Wanavyotafuta ‘Kiki’ Zisizo na Faida

$
0
0
Msanii wa filamu Faiza Ally amewataka wasanii wenzake wa filamu kuacha kutafuta ‘kiki’ ambazo haziwanufaishi katika kazi zao.
Faiza akihojiwa na TV 1

Akiongea wiki hii, Faiza amesema wasanii wengi wa kike wa filamu wanatafuta kiki za mapenzi bila kujua kiki hizo zitawasaidiaje.

“Kiki sio mbaya lakini hiyo kiki inakusaidiaje?, mimi ukiona nafanya kiki ujue kuna kazi ambayo inakuja, sio kufanya kiki alafu unakaa kimya ilimradi uonekana na wewe upo, kwa hiyo mimi ningewashauri wasanii wenzangu wa filamu tufanye kazi,” alisema Faiza.

Muigizaji huyo kwa sasa anajipanga kuachia filamu yake mpya iitwayo ‘Baby Mama Drama’.

Hawa Ndio Watu Wanaochukiwa Zaidi Duniani

$
0
0

1. WATU WEUSI.
Hawa ndio wanaongoza kwa kuchukiwa na kubaguliwa zaidi duniani. Wanateswa na kunyanyaswa kila sehemu walipo. Ulaya, Marekani, Australia Arabuni, Mashariki ya Kati, Mashariki ya Mbali, na Marekani Kusini. Mbaya zaidi hata huku Africa bado tunaendelea kunyanyaswa na wageni wanaokuja kwa vigezo Vya uwekezaji. Hawa wanapora ardhi ya wanyonge 

2. WAISLAM
Hili ni kundi linalofuatia kwa kuchukiwa. Sababu kuu ikiwa ni
propaganda za kimagharibi na dhana ya ugaidi.

3. WAYAHUDI
Hawa wanachukiwa zaidi na nchi za Kiarabu na mataifa ya Kiislam. Sababu kubwa hasa zikiwa ni za kihistoria na mgogoro wa Mashariki ya Kati.
WAYAHUDI pia wameshawahi kuteswa na utawala wa Ki Nazi chini ya Adolf Hitler . Sababu kubwa ilikuwa ni mafanikio ya kiuchumi waliyokuwa nayo WAYAHUDI nchini Ujerumani na Ulaya kwa ujumla.

4. WAARABU
Licha wa kuwa si wote ni magaidi, Bali wamekuwa wakihukumiwa kwa asili yao. Nchi nyingi zinawaogopa na hazina imani nao

Hatimaye Geryson Msigwa Athibitshwa Kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu.

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli amemthibitisha Geryson Msigwa kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu. Kabla Geryson Msigwa alikuwa akikaimu cheo hicho.
Aidha Mh. Rais amemteu Jerry Muro aliyekuwa msemaji wa Timu ya Mpira wa Miguu Yanga kuwa msaidizi wake.

Hongereni Kurugenzi ya Habari Ikulu kwa nafasi hizo

Nchi 10 Zinazolipa Vizuri Mishahara Duniani...

$
0
0
Je, ulishawai kujiuliza nchi ambazo wafanyakazi wanalipwa mishahara ya juu? Hebu tuangalie nchi kumi ambazo wafanyakazi wanapata malipo makubwa ya kazi zao wanazofanya


#10 Ufaransa
Ufaransa ni nchi ya 7 yenye uchumi mkubwa zaidi duniani, Wafanyao kazi Ufaransa wanafanya kazi kwa mda mchache ni kama masaa 35 kwa wiki. Kwa wastani  kipato cha mfanyakazi wa Ufaransa ni $28,799 kwa mwaka baada ya kulipa kodi zote.


#9 Sweden
Kutokana na data za Bank kuu ya dunia,hii nchi nzuri ya kiscandinavia ni ya sita kwa uchumi wa ndani duniani. Sweden ni wazalishaji wakubwa wa mbao. Kwa wastani kipato chao ni $29,185 kwa mwaka baada ya makato yote ya kodi


#8 Canada
Canada majirani wa Marekani,ni nchi ya tatu yenye uhifadhi mkubwa wa mafuta duniani ikipitwa na
Venezuela na Saudi Arabia. Nchi hii pia ina utajiri mkubwa wa zinc, uranium, dhahabu na aluminium.
Kwa wastani kipato chao ni $29,356 kwa mwaka baada ya makato yote ya kodi


#7 Austria
Austria ni nchi ambayo ipo katikati ya Ulaya, Imeendelea sana kiviwanda na sekta ya utalii
inachangia asilimia 9 ya pato la ndani la taifa. Kwa wastani kipato chao ni $31,173 kwa mwaka baada ya makato yote ya kodi


#6 Germany
Germany ni nchi ya kwanza yenye uchumi mkubwa zaidi ulaya. Kwa wastani kipato chao ni $31,252 kwa mwaka baada ya makato yote ya kodi



#5 Australia
Australia ni moja kati ya nchi zenye uchumi imara zaidi duniani,ni wasafirishaji wakubwa wa madini na wanaagiza bidhaa chache sana kutoka nje.Katika swala la wastani wa utajiri, Australia ilishika nafasi ya pili duniani baada ya Switzerland mwaka 2013. Kwa wastani kipato chao ni $31,588 kwa mwaka baada ya makato yote ya kodi


#4 Switzerland
Uswisi inashika nafasi za juu katika utendaji bora wa serikali yao, ikiwa ni pamoja na uwazi wa serikali yao, uhuru wa raia, ubora wa maisha, ushindani wa kiuchumi na maendeleo ya binadamu. Kwa wastani kipato chao ni $33,491 kwa mwaka na wanafanya kazi masaa 35 tu kwa wiki.


#3 Norway
Norway ina utajiri mkubwa  wa maliasili ikiwa pamoja na mafuta,umeme wa maji,uvuvi na madini.Kwa wastani kipato chao ni $33,492 kwa mwaka


#2 Luxembourg
Luxembourg ni wasambazaji wakubwa wa chuma ulaya. Kwa wastani kipato chao ni $38,951 kwa mwaka


#1 USA
Pato la ndani kwa mwaka ni $55,000 na makato ya taxi ni asilimia 23.Wafanyakazi wa Marekani wanafanya kazi masaa 44 kwa wiki.

Uwoya: Nikilala, Nikiamka Nawaza Siasa Tu

$
0
0
STAA mkali Bongo Muvi, Irene Uwoya amefunguka kuwa bado hajakata tamaa ya kuwa mwanasiasa japokuwa mwaka jana alishindwa lakini hiyo imempa nguvu ya kujipanga zaidi na kwamba kwa sasa akili yake yote akilala, akiamka ni kuwaza siasa tu.

Akizungumza na Amani Uwoya alisema kuwa, changamoto alizozipitia kipindi cha kampeni zimemfundisha mambo mengi na pia zimemkomaza na kufanya damu yake izidi kupenda siasa.

“Bado siasa ipo kwenye damu na nimepata changamoto kubwa sana kipindi kile cha nyuma na sasa nipo tayari kuingia vitani  tena ili niweze kuongoza wananchi wangu na nifanye kila ambacho wamekikosa kwa muda mrefu,” alisema Uwoya.

Uwoya alikuwa akigombea Ubunge wa Viti Maalum Tabora,  kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) lakini alishindwa kwenye ngazi ya Taifa.

Zari Hassan Amsifia Mama Yake, Asema Sio Mswahili na Mwenye Hekima...

$
0
0
Lile timbwili la madale bado linaendelea kuwaka moto , hivi karibuni mzazi mwenzie na Diamond, Zari Hassan amepost picha akiwa na mama yake mzazi huku akimwagia sifa kemkem kuwa Mama yake huyo ana tabia nzuri ,ana hekima na kumfananisha na queen ,kitendo hicho kimetafsiriwa na wapenda ubuyu mjini kuwa zari alimrushia dongo mama wa mzazi mwenzie Diamond ambaye amekua na sifa ya kuwa mkorofi,mshari na asiyependa amani na mkwe wake huyo mtarajiwa

Ameandika hivi:

Zarithebosslady
She was born and raised like a Queen, acts like a Queen, behaves like a Queen, slays like a Queen, moves gracefully like a Queen. Even If she knows she ain't a Royal deep down she is one. Slay Queen, Mama Africa Mrs Halima Hassan

Nape: Ukinunua CD isiyo na stika, wewe ni mwizi kama wezi wengine na utashughulikiwa

$
0
0
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye baada ya kufanya ziara Ijumaa hii katika maeneo ya Kariakoo kukagua na kukamata CD ambazo hazina stika ya TRA, amewataka watanzania kuacha tabia ya kukunua CD ambazo hazina stika za TRA.

Akiongea na waandishi wa Habari katika msako huyo, Nape amesema yeyote anayekamatwa na CD ambao haina stika ya TRA atashtakiwa kwa kosa la kuhujumu uchumi.

“Kila anayenunua sasa kazi ya sanaa ambayo haina stika ya TRA naye ni mwizi kwa kama mwizi yoyote sababu ameshirikiana na muuzaji ambaye hajalipa kodi, hata tukikukuta na CD moja haina stika wewe ni mwizi kama mwizi mwingine tutashughulika na wewe,” alisema Nape.

Katika ziara hiyo zaidia ya maduka 40 yamefungwa huku CD fake zikichukuliwa kwa ajili ya kuaribiwa.

Tume ya Vyuo Vikuu(TCU) yatoa Ufafanuzi Kuhusu Alama za Kudahiliwa Vyuoni

$
0
0
TCU wamefanya marekebisho kuhusu tangazo lao la hapo awali kwa kusema uwe na principal pass mbili walau zifikie point 4 kwenye masomo mawili. Ina maana at least uwe na DD,CE,BE,AE na zaidi ya hapo.

MC Pilipili Apata Ajali Mbaya ya Gari....

$
0
0
MC Pilipili ametupia Picha katika Ukurasa wake wa Facebook akiwa ameandika "Nimepata Ajali mbaya ya Gari namshukuru Mungu nimetoka salama"

Baada ya Mungwana Blog kuwasiliana nae akasema kuwa Alipata Ajali usiku wa jana Saa 8 Maeneo ya Chole Road Masaki karibu na Fish Market, Aligongana na Gari ndogo IST uso kwa uso.. Dereva wa IST alikuwa kalewa.

Ndani ya Gari alikuwa na Team yake, alikuwepo Stella Secretary wake, Joseph Meneja wake, Shazymelody Rais wa Band yake ya Pilipili Band..

Wanafunzi Elimu ya Juu Waipa Bodi ya Mikopo Masaa 72

$
0
0
Kamati ya mawaziri wa mikopo ya serikali za wanafunzi wa Elimu ya juu nchini Tanzania inayoundwa na mawaziri, Manaibu waziri na makatibu wa wizara ya mikopo kutoka vyuo vyote nchini leo July 16 2016 wamkutana na waandishi wa habari jijini Dar es salaam.

Akizungumza kwa niaba ya kamati hiyo, Mwenyekiti wa kamati Taifa, Shitindi Venance amesema kipindi cha mwisho wa mwezi huu wanafunzi wa elimu ya juu watatakiwa kufika katika vituo vyao vya kazi vilivyosambaa nchi nzima ili kuendelea kupata mafunzo kwa vitendo ila wamesikitishwa kwamba wakati wakijiandaa na hilo  hakuna mchakato wowote unaoendelea kupelekea kupata fedha hizo, Shitindi amesema…….

>>>Mpaka sasa hivi tukiwa tumebakiwa na takribani siku tano kabla ya kufunga chuo hakuna hata karatasi za kusaini zilizotumwa vyuoni ili kukamilisha zoezi hilo na mchakato wa kusaini hukuchukua muda wa siku tatu mpaka tano

>>>Kutokana na ucheleweshaji huo tunatoa muda wa saa 72 kuanzia leo Jumamosi, mpaka Jumanne ya wiki ijayo kwa bodi ya mikopo kufikisha fedha za kujikimu wakati wa mafunzo kwa vitendo katika vyuo vyote hapa nchini ili wanafunzi waweze kusaini na kupokea malipo yao:-Shitindi

Marekani Yakana Kuhusika na Mapinduzi Uturuki

$
0
0
Marekani imeitaka Uturuki kujizuia baada ya jaribio la mapinduzi lililozimwa siku ya Ijumaa ambapo maelfu ya maafisa wa kijeshi wamekamatwa.

Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni nchini Marekani John Kerry ameutaka utawala nchini Uturuki kuheshimu sheria wakati wa uchunguzi wao kuhusu mapinduzi hayo.

Kerry amesema kuwa madai kwamba Marekani ilihusika katika mapinduzi hayo inasababisha madhara kwa uhusiano kati ya washirika hao wawili wa NATO.


 Mapema kupitia kwa hotuba yake, rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alitoa wito kwa rais Obama kumrejesha nchini humo kiongozi wa kidini raia wa Uturukli anayeishi nchini humo Fethullah Gulen ambaye analaumiwa kwa kupanga mapinduzi hayo.


 Marekani inasema kuwa Uturuki ni lazima ithibitishwa hayo kabla ya uamuzi wa kumrejesha Gulen kufanyika.

Mapema nchini Uturuki maelfu ya watu walijitokeza wakiimba na kupeperusha bendera ya taifa katika barabara za mji wa Istanbul na Ankara kumuunga mkono rais Erdogan.


Bustani nyingi mjini Istanbul zilijaa watu waliokuwa wakiimba wakisema kuwa ardhi yao na demokrasia haviwezi kuchukuliwa na jeshi.

Serikali imetawaka wafuasi wake kusalia katika bustani kuu usiku kucha. Mashirika kadha ya ndege yalirejea safari zao kwenda Istanbul Jumamosi jioni.

Vijana Chadema Walianzisha Tena Dodoma

$
0
0
Vijana wa Chadema wanatua tena Dodoma ambako CCM inaendelea na maandalizi ya mwisho mwisho kwa ajili ya mkutano mkuu maalumu wa kumkabidhi Rais John Magufuli kiti cha uenyekiti.

Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha), Patrobas Katambi amesema wanatarajia kutua mjini humo kufanya mkutano wa kamati ya utendaji Julai 20 na Mwenyekiti wa chama chao, Freeman Mbowe atahudhuria.

“Polisi imepiga marufuku mikutano ya hadhara, siyo ya ndani. Sidhani kama kikao hiki watakizuia kwa sababu ni cha ndani,” amesema Katambi.

Amesema kikao hicho, kitajadili na kutoa mwelekeo wa masuala mbalimbali ikiwamo mkakati wao mpya wa kutafuta haki na demokrasia aliyodai inaminywa.

Augustino Mrema azungumzia hatua ya Rais kumteua na hatma yake ndani ya TLP

$
0
0
Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party, Augustino Lyatonga Marema amezungumzia hatua ya Rais Magufuli kumteua kuwa Mwenyekiti wa Parole Taifa na kuwa ni ipi hatma yake ndani ya TLP.

Kumsikiliza Mrema akiongea, bonyeza hapo chini:

Rais Magufuli Kafanya Uteuzi Mwingine Leo July 17 2016

$
0
0
July 17 2016 headline kutoka Ikulu Dar es salaam ni pamoja na hii Rais John Pombe Magufuli kumteua Profesa Longinus Rutasitara kuwa makamu mwenyekiti wa bodi ya mamlaka ya usafiri wa anga (TCAA), Rutasitara anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dk. Nyamajeje Weggoro ambaye muda wake umemalizika.

Pia Rais Magufuli amempandisha cheo kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Kedmon Mnubi kuwa kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi (SACP)

​Diamond Asherehekea Video ya Kidogo Kufikisha Views Milioni 1 Ndani ya Siku 4

$
0
0
Diamond Platnumz anasherehekea mafanikio ya video ya wimbo wake mpya, Kidogo.
Ndani ya siku nne, video ya wimbo huo aliowashirikisha P-Square imefikisha views zaidi ya milioni moja kwenye mtandao wa Youtube. Staa huyo hakusita kusherehekea hatua hiyo na mashabiki wake:

Ameandika Haya:

Diamondplatnumz
AND THE AFRICAN HISTORY WAS MADE!!!!!! 1Million + VIEWES WITHIN 4 DAYS!!!!! #KIDOGO by @DiamondPlatnumz ft P-SQUARE ....many thanks to my brothers @peterpsquare @rudeboypsquare ...Media /Fans and all Behind this Project....🙏
(Nawashukuru wote mloniwezesha kuweka Historia hii kubwa Africa ya video kutazamwa zaidi ya mara Milioni 1 ndani ya siku nne, hakikia huu ni upendo wa Mkubwa na wa Dhati, shukran sana sana kwa wote walio Husika na Project hii bila kuwasahau Media na Nyinyi mashabiki zangu pendwa kwa kuupokea kwa kishindo Wimbo huu!!!.... waambie Malalamiko Baadae kwa sasa tuna cheza #KIDOGO ) Clik the link in my BIO to watch full VIDEO!!!!

Haji Manara Atoa ya Moyoni akiwa Safarini Kuelekea India kwaajili ya Matibabu

$
0
0
Ni wiki mbili kamili zitakazotimia leo majira ya saa nane usiku. Muda huo bila shaka nitakuwa katika  anga la dunia nikisafiri kuelekea New Delhi nchini  India kupitia Muscat Oman kwa ajili ya matibabu yangu ya macho.

Usiku wa siku kama ya leo (yaani Jumapili ya tarehe 3-7-2016) niliamka usiku kwa ajili ya daku, Ndipo nilipogundua jicho langu la kushoto halioni kabisa na  jicho langu la kulia lina uoni wake ulikuwa mdogo.Ni siku ambayo sitakaa niisahau maishani mwangu.

Najua madaktari mbali mbali wa hapa nchini walifanya kila jitihada za kunusuru macho yangu ila bado ufumbuzi wa tiba yangu bado haujapatikana. Ndio maana naenda kujaribu India.na Insha Allah Mungu atanivua mtihani huu.

Kiukweli hawa madaktari niwashukuru sana kwa jitihada zao.Rafiki yangu na kaka yangu Dkt. Mohammed wa wizara ya afya, Dkt. Mahunda wa Ocean Road, Dkt. Dalla, Dkt. Chibuga na Dkt. Hassan wa CCBRT na pia Dkt. Datoo wa clinic ya pale Shoppers Plaza Miikocheni. Vile vile Madaktari wa Kituruki pale katika hospitali yao ya International eye clinic maeneo ya Moroco pamoja na wauguzi wao.Mungu atawalipa Insha Allah.

Kipekee niwashukuru ndugu na rafiki zangu wa KT shop. Hapo mimi ndio maskani yangu jioni.Hawa ni zaidi ya binadaam. Kisasa tungesema show nzima ya safari wanasimamia wao.Wamefanya jitihada zote na kiukweli bila wao sijui ingekuwaje.Kwa wiki zote mbili wamekimbizana na mimi ugonjwa wangu bila kuchoka.

Pia niishukuru ofisi yangu klabu ya Simba kwa zaidi ya wema walionifanyia.Niwashukuru viongozi wote, Friends of Simba.wanachama na wapenzi wote wa Unyamani kwa kila jambo na dua zao walizonifanyia..Kiukweli sijutii kupenda na kufanya kazi Simba.

Niishukuru pia serikali ya nchi hii. Nimepokea salaam kutoka kwa Waziri wangu wa michezo.Mhe Nape. Salaam toka kwa waziri na naibu waziri wa afya.Mh Ummy  na Dkt. Kigwangallah. Nimepokea pia salam toka kwa rafiki zangu manaibu waziri Mh Mavunde na Dkt. Possi.

Lakini kipekee kwa waziri wangu wa mambo ya ndani ya nchi. mtani wangu Mh Mwigulu Nchemba ambae yeye mwenyew alikuja kuniona na kwa niaba ya serikali ameahidi kunisaidia kwa kila hali niweze kupona.

Na kwa hapa nisiache kumshukru mwambata wetu wa afya katika  ubalozi wetu nchini India.Dkt.  Goroka kwa kusaidia kupatikana kwa hospitali India.Pia nimshukuru Profesa Mohamed Janabi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ya hospitali Taifa Muhimbili kwa ushauri wake wa kitaalam (nafurahi kusikia jana amethibitiwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo nyeti, homgera sana Prof! Unastahili kabisa) .sambamba na daktari wetu wa Simba.

Sitatenda haki kama sitawashukuru viongozi wakuu wa TFF Rais Jamal Malinzi na katibu mkuu wake Mwesigwa kwa kila jambo walilonifanyia. Kipekee niwashukuru viongozi wa dini. mashekh na maustaadh kwa dua zao kwangu.sambamba na wachungaji ambao walikuja hadi kwangu kuniombea..Asanteni sana  watu wa Mungu.

Nisisahau kuwashukuru watani zangu Yanga kwa mchango wao kwangu... Hususan mropokaji 😃😃 wao Jerry Muro.

Nita-mmiss sana kwa fujo na kebehi zake. Ninamuomba awaandikie TFF kuomba radhi na kisha  yeye naye  ajirekibishe kidogo bana....Nna imani TFF  nao wanaweza kupitia kamati zao wanaweza kuangalia namna sahihi ya kulimaliza hili kwa maslahi ya mpira wa miguu nchini. Muhimu Jerry apime tu kauli zake. Mpira si kashfa wala kebehi za kuudhi..na si uadui hata kidogo.

Mwisho niwashukuru ndugu zangu wa Kariakoo Family Development Foundation (KFDF) chini ya mwenyekiti wetu Mohamed Bhinda. Hawa ni Alfa na Omega kwangu Kuanzia niliokuwa nao vjana wa Al-Ahly hadi KFDF. Pamoja nao watu wangu wa nguvu.whatsapp groups zote ambazo zimeniombea sana na kunifariji katiika kipindi hiki kigumu.sambamba na kuja kunijulia hali.

Nikiwasahau wanahabari nitakuwa wa ajabu..Wamefanya kazi kubwa ya kuwahabarisha na kuwapa maendeleo yangu kila siku kupitia vyombo vyao.

Asanteni sana wote! My family. ndugu zangu. jamaa na marafiki wote.nimejua kwa sasa Haji nna watu na nnamuomba mungu niendelee hivihivi na tabia zangu njema nizilojaaliwa na Manani.Msiache kuniombea kwa kila hatua.kuanzia safari yangu.matibabu na kuiombea familia yangu inayobaki hapa nyumbani.

Nawapenda sana. Mungu awabariki sana.
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live




Latest Images