Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104428 articles
Browse latest View live

USHAURI; Jinsi Ya Kuondokana Na Matumizi Mabaya Ya Mtandao Wa Intaneti Na Kutumia Vizuri Muda Wako Kujiongezea Kipato.

0
0
Kama kuna mapinduzi ambayo kizazi hiki kinayashuhudia kwa macho basi ni mapinduzi ya kiteknolojia hasa kwenye kompyuta na mtandao wa intaneti. Mapinduzi mengi yaliyotokea huko nyuma hatukuwepo, tumekuwa tunayasikia tu kama mapinduzi ya viwanda.

Uzuri wa kuwa hai wakati wa mapinduzi ni kwamba unakuwa na nafasi kubwa ya kunufaika na mapinduzi hayo kuliko wale wanaokuja baadaye au waliochelewa kuyatumia mapinduzi hayo.

Kwa mfano watu wengi ambao wanashikilia rekodi ya kuwa matajiri sana duniani walitokana na mapinduzi ya viwanda yaliyotokea karne ya 19 ulaya na marekani.

Watu kama John Rockefeller walitumia vizuri mapinduzi ya viwanda kujijengea utajiri mkubwa.

Tukija kwenye zama zetu hizi za mapinduzi ya kiteknolojia, tunaona jinsi ambavyo mtandao wa intaneti umezalisha mabilionea wakubwa duniani.

Watu kama Mark Zuckerberg, mmiliki wa mtandao wa Facebook ni bilionea aliyezalishwa na mapinduzi haya ya kiteknolojia.

Wapo wengi ambao wananufaika sana na mapinduzi haya, swali ni je wewe unanufaikaje na mapinduzi haya? Hili ni swali muhimu tunalopaswa kujiuliza kila siku.

Mtandao wa intaneti umekuja na faida nyingi sana kwetu, kuanzia kuboresha kazi zetu, biashara zetu na hata maisha yetu kwa ujumla. Sasa hivi ni rahisi kutangaza biashara na hata kuwafikia wateja popote walipo duniani. Ni rahisi kuwasiliana na ndugu jamaa na marafiki popote pale walipo.

Lakini kila chenye faida hakikosi hasara, na mtandao wa intaneti umekuwa na hasara nyingi ambazo zimewazuia watu kupata mafanikio makubwa kwenye maisha yao. Mtandao wa intaneti umekuwa na ulevi mkubwa hasa kwa watumiaji ambao unawafanya washindwe kuweka muda kwenye yale mambo ya muhimu kwao.

 Leo kupitia makala hii ya ushauri wa changamoto tutaona jinsi ya kuondokana na ulevi huu ili kuweza kutumia muda wetu vizuri na kufikia malengo yetu.

Kabla hatujaangalia kwa undani hatua za kuchukua, tupate maoni ya msomaji mwenzetu aliyetuandikia kuhusiana na changamoto hii.

Jambo la kwanza; kuwa na utaratibu maalumu wa kutembelea mitandao hii. 
Moja ya kitu kinachofanya matumizi ya mitandao kuwa changamoto ni ukaribu wake na urahisi wa kuitumia. Kwa kuwa mitandao hii ipo kwenye mikono yetu, nikimaanisha simu zetu za mkononi, ni rahisi sana kuingia hasa pale unapopata hata dakika moja.

Urahisi huu unafanya tukiwa na upweke kidogo tu tufungue mitandao. Baadaye tunaingiwa na hofu kamba tusipofungua muda mrefu basi tunapitwa, na hivyo tunajikuta kila baada ya dakika chache tunachungulia tena tuone kipi kipya.

Utafiti uliowahi kufanywa, kuhusiana na simu hizi za kiganjani, unaonesha watu wanazishika simu zao mara nyingi mno, na mara zote ni kwenye mitandao ya kijamii.

Ili kuondokana na ulevi huu, jiwekee utaratibu wa kuingia kwenye mitandao hii ya kijamii kwa muda fulani wa siku. usikubali kila dakika uwe ‘online’, jitengee muda maalumu kila siku au kila baada ya masaa fulani ndiyo uingie kwenye mitandao hii. Muda mwingine uweke kwa ajili ya kazi na zima kabisa data kwenye simu yako.

Unapokuwa kwenye kazi ambayo inahitaji umakini, usikatishe ili kuingia kwenye mitandao, kwani unaporudi kwenye kazi yako unapoteza muda mwingi zaidi.

Jambo la pili; ondoa taarifa za mitandao ya kijamii unazopata kupitia simu yako.
Kwenye simu zetu kuna kitu kinaitwa ‘notification’ hii ni ile taarifa ambayo simu yako inakupa kwamba kuna mtu kakutumia ujumbe, au kapenda picha yako kwenye mtandao.

Taarifa hizi zina nguvu ya kukusukuma uchukue hatua haraka kuona ni ujumbe gani umetumiwa au nani kasema nini kuhusu ulichoweka kwenye mitandao.

Ili kuondokana na hili, futa kabisa kupotea taarifa hizi za kila kinachoendelea kwenye mitandao. Kwa njia hii hutasukumwa kufungua badala yake utafungua pale muda wako uliojipangia unapokuwa umefika.

Na kama unaona huwezi kuondoa notification, ondoa kabisa zile application ambazo ni za mitandao ya kijamii, na badala yake uwe unaingia moja kwa moja kupitia mtandao. Siyo lazima uwe na app zote za kufungua kila aina ya mtandao, kwa sababu kwa kuwa nazo utajikuta umetengeneza utaratibu wa kuzunguka kwenye mitandao hii.

 Kwa mfano unaanza na facebook, unaangalia kisha unaenda instagram, ukimaliza unaenda snapchat, unatoka hapo unaingia wasap, kisha telegram, ukifika huko ni muda unarudi kuangalia tena kama kuna jipya facebook, kisha instagram, na unajikuta unarudia mzunguko mzima hata mara tatu. Ukiondoa zile app ambazo siyo muhimu sana utapunguza kutembelea ile mitandao ambayo siyo muhimu kwako.

Jambo la tatu; nufaika na mitandao hii. 
Kama umeshafanya njia hizo mbili lakini bado huwezi kujizuia kutembelea mitandao hii kila mara, basi angalia ni kwa namna gani unaweza kunufaika na itandao hii. Yaani angalia unawezaje kuitumia kujiingizia kipato.

Na habari njema sana kwako ni kwamba kila mtu, narudia tena KILA MTU anaweza kutengeneza kipato kupitia mtandao wa intaneti.

Kwa kuanza, angalia ni vitu gani unapenda sana kutembelea kwenye mitandao hii, ni vitu gani unapenda kufuatilia zaidi. Ukishajua vitu hivyo angalia ni kwa namna gani unaweza kuwasaidia wengine wanaohitaji taarifa zinazohusiana na vile unavyopenda kufuatilia. Na hapo unaweza kuanzisha ukurasa maalumu kwa ajili ya mambo hayo na hata kuwa na blog au tovuti.

Pia unaweza kutumia mitandao hii kuboresha kazi unayofanya au biashara yako. unaweza kutumia mitandao hii kupata wateja wa kile unachofanya au kutoa taarifa kwa wale wanaohusika na unachofanya. Pia unaweza kutumia mitandao hii kufanya tafiti zinazohusu kazi au biashara yako. zipo njia nyingi za kunufaika ni wewe kuchagua kipi kinakufaa.

Install Application ya Blog Hii ya Udaku Special Kwenye Simu yako Kutoka Google Play Kusoma Habari Kirahisi

0
0

Download  Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu yako Kutoka Play Store Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi

Bonyeza Hapa CLICK HERE 



Breaking News!! Kiwanda Cha Polister Kinaungua Moto Kihonda Morogoro

0
0
Kiwanda cha nguo ambacho ni moja ya viwanda vichache vinavyo fanya kazi ambapo kwa sasa kilikua kinatengeneza khanga na vitenge vilivyoanzishwa na baba wa taifa mwalimu julias nyerere kimeungua moto asubuhi ya leo.

Mpaka sasa bado moto unaendelea karibu nusu ya kiwanda kimeteketea na magari ya zimamoto yameishiwa maji, wanaendelea kufuata maji mengine na jeshi la polisi limelazimika kutia maji ya katika gari ili kuongeza nguvu kuuzima moto.Taarifa zaidi tujiunge katika taarifa ya habari ya Channel ten.

Download Wimbo Mpya wa Chid Benz Feat. Rayvany Unaitwa Chuma

TCU kuanza kudahili wanafunzi wa kujiunga vyuo vikuu kesho

0
0
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), itaanza kudahili wanafunzi waliomaliza kidato cha sita wanaoomba kujiunga na vyuo vikuu kuanzia kesho.

Akizungumza jana, Kaimu Mkurugenzi wa Udahili na Nyaraka wa TCU, Dk Kokubelwa Mollel alisema udahili kwa wenye diploma utaanza Julai 31.

Dk Mollel alisema kazi hiyo itaendelea kwa mwezi mzima ili kuruhusu wananchi wengi zaidi kupata fursa ya kuomba kudahiliwa na udahili huo utafanyika kwa njia ya mtandao.

Alisema ili wanafunzi waweze kuelewa programu zinazotolewa na vyuo vikuu, tume hiyo imeandaa maonyesho ya 11 yatakayofanyika kuanzia Julai 20 hadi 22, mwaka huu.

Alisema maonyesho hayo yatafanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam na kufunguliwa na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako.

Bavicha: Msimamo Wetu ni Ule Ule, Lazima Nasisi Tufanye Kikao Chetu Dodoma

0
0
Ikiwa zimebaki siku tatu kabla ya Mkutano Mkuu wa CCM kufanyika, Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) limesema azma yao ya kufanya kikao chao cha kamati ya utendaji mjini Dodoma ipo palepale.

Julai 16, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa alisema kikao cha Bavicha hakitofanyika kwa sababu itakuwa ni mwendelezo wa vurugu zao.

Mkutano Mkuu wa CCM, utakuwa na ajenda mbalimbali ikiwamo ya Mwenyekiti wa chama hicho, Jakaya Kikwete kumkabidhi kijiti cha uongozi Rais John Magufuli.

Katibu Mkuu wa Bavicha, Julius Mwita jana alisema  baraza hilo lipo kwenye hatua ya mwisho ya maandalizi ya kikao hicho kitakachohudhuriwa na zaidi ya wajumbe 50 kutoka mikoa yote.

“Wajumbe wataanza kuwasili kesho (leo) mjini Dodoma. Hatuna wasiwasi na kikao hiki kwa sababu ni cha ndani siyo mkutano wa hadhara, ambao umepigwa marufuku na polisi,” alisema Mwita.

Mwita alisema kikao hicho kitakuwa cha siku mbili kuanzia Julai 20 hadi 21 na kwamba, kitahudhuriwa na mameya na wenyeviti vijana wa halmshauri zinazoongozwa na Chadema.

Alipotafutwa Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Boniface Jacob ambaye ni mwanachama wa Bavicha kujua kama atahudhuria kikao hicho alijibu: “Nitakwenda kwa sababu mimi ni kijana, sina sababu ya kukataa wito wa viongozi wangu wa juu wa Bavicha taifa.”

Kuhusu kauli ya Kamanda Mambosasa, Mwita alisema polisi ilishatoa maelekezo ya kuruhusu vikao vya ndani.

“Taarifa ya Mambosasa hatujaishangaa kwa sababu ni desturi yake kujichanganya, leo anasema hivi kesho vile. Tunamtaka atulie asubiri tumpe taarifa ni wapi kikao chetu kitanyika kwa njia ya amani,” alisema Mwita

Siwema: Nay Hajanikatisha Tamaa ya Kuwa na Staa Kimapenzi

0
0
Mrembo aliyezaa na Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, Siwema Edson amefunguka kuwa, kuingia doa kwa penzi lake na jamaa huyo hakujamkatisha tamaa kuingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na mwanaume ambaye ni staa.
Siwema na Nay wa Mitego

Siwema ameliambia Wikienda kuwa hawezi kuapa kwamba hatakaa atumbukie tena kwenye penzi la msanii kwa kuwa hakuna anayejua huko mbeleni ataangukia kwa nani.

“Siwezi kusema kuwa Nay amenikatisha tamaa au sitaingia tena kwenye penzi la staa kwa sababu naweza kuapa halafu ikawa sivyo,” alisema Siwema.

Mapya Mtanzania Aliyewekwa Rehani Kwa Unga Pakistan.

0
0
NI mateso. Ndivyo unavyoweza kusema, hasa baada ya kundi la maharamia linalojishughulisha na bishara ya ‘unga’ nchini Pakistan kuelezwa kumtesa kijana Mtanzania, Adamu Akida.

Kutokana na hali hiyo, timu ya MTANZANIA ilipiga kambi jana katika eneo la Magomeni, Mtaa wa Idrissa, ambako pamoja na mambo mengine, ilifanikiwa kuzungumza na kaka wa Adamu aliyejitambulisha kwa jina la Hemed Abdallah (si jina lake halisi).

Akisimulia mkasa huo, alisema miezi minane iliyopita, Adamu alikwenda kwa kaka yake ambaye ni mtoto wa mama yake mdogo aliyetambulika kwa jina la Juma, na kuomba msaada wa mtaji kwani kazi yake ya kinyozi haikuwa ikilipa na hali ya maisha ilikuwa ngumu.

Baada ya kueleza shida yake hiyo, kaka yake huyo (Juma) alimuhoji kama yupo tayari kwa ajili ya kutafuta maisha nje ya nchi, na Adamu alikubali kufanya kazi ya aina yoyote ili mradi aweze kupata pesa.

“Adamu kwa sasa ameshikiliwa kwa muda wa miezi minane, hatujui kama alikuwa ameingia katika janga hili hadi pale tulipoona video zake katika mitandao ya kijamii. Hapa aliyepo ni baba yake mdogo, Kessy Baharia na baba yake mzazi yupo Bagamoyo Mlingotini, ndiko anakoendelea na maisha yake.

“Awali alikwenda kwa kaka yake mtoto wa mama yake mdogo anaitwa Juma na kuomba asaidiwe mtaji kwani amekuwa na maisha magumu sana. Baada ya hali hiyo aliambiwa kuna safari ya kwenda Pakistan ambayo waliondoka wakiwa wameambatana watu watatu pamoja na Juma na kijana mwengine ambaye jina lake limenitoka, ila anaishi Kinondoni.

“Walipofika kule, Juma akachukua mzigo akiwa na yule kijana wa Kinondoni, huku Adamu akiachwa Pakistan kwa maelezo kuwa baada ya siku tano atakuja nchini na mzigo mwingine. Muda wote hata tukihoji alipo Adamu tunaambiwa yupo anaendelea na kazi huko aliko ana angerudi mwezi wa tisa nane.

“Sasa hii video ndiyo imetupa picha halisi ya Adamu, maskini sijui kama tutampata akiwa hai. Hata hivyo kwa kipindi cha hivi karibuni, tulikuwa tukishangazwa na mwenendo wa Juma kwani amekuwa na fedha nyingi sana hadi kufikia kuwajengea nyumba dada zake pamoja na kuwanunulia magari,” alisema Abdallah huku akibubujikwa na machozi.

Mke wake

Inaelezwa kuwa mke wa Adamu ambaye alikuwa akiishi Mtaa wa Sunna, Magomeni, alihamia Kijitonyama.

Kwamba alihamishwa na shemeji yake, Juma ambaye ndiye aliyempangia nyumba nyingine Kijitonyama.

“Katika suala hilo, tuna shaka kuwa hata mke wa Adamu anajua kinachoendelea, maana miezi mitatu iliyopita alihama Magomeni na kuhamia Kijitonyama, tena huku akisema mume wake karibu anarejea nchini.

“Lakini baada ya video kuanza kuonekana, sasa hata kupatikana hapatikani, na hatujui amehamia nyumba gani huko Kijitonyama,” alisema Abdallah.

Serikali ya Mtaa

Akizungumza na MTANZANIA, Mwenyekiti wa Srikali ya Mtaa wa Idrissa, Issa Mpangile, alisema kuwa jana askari kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi walifika katika ofisi yake na kumtaka waongozane kwenda katika nyumba ya baba mdogo wa Adamu.

Alisema walipofika nyumbani kwa Kessy Baharia, ambaye ndiye baba mdogo wa Adamu, polisi walichukua maelezo yake na baadaye wakarudi katika ofisi ya Serikali ya Mtaa kuchukua maelezo ya mwenyekiti huyo.

Akizungumza kuhusu kijana huyo, Mpangile alisema kuwa ni mzaliwa wa mtaa huo, lakini baadaye alihamia Mtaa wa Suna ambao ni jirani na Mtaa wa Idrissa, Kata ya Magomeni.

Alisema wakati kijana huyo anahama mtaa huo, alikuwa bado ni kinyozi na hakuwa na rekodi ya kusafiri kwenda nje ya nchi.

“Wakati Adamu anahama Mtaa wa Idrissa, alikuwa bado ni kinyozi na hakuna rekodi kwamba alikuwa anasafiri nje ya nchi,” alisema Mpangile.

Alisema katika mazungumzo na Baharia, alimweleza kuwa amewasiliana na baba wa kijana huyo ambaye anaishi Bagamoyo mkoani Pwani.

Mpangile alisema kwa mujibu wa Baharia, baba wa kijana huyo anayejulikana kwa jina la Akida, amesikia habari za mtoto wake na kwamba atakwenda kuripoti kituo cha polisi.

Naye mama mdogo wa Adamu, aliyetambulika kwa jina la Khadija Katundu, alikiri maofisa wa polisi kumuhoji mume wake.

Alisema wameendelea kutoa ushirikiano kwa watu wanaofika nyumbani kuhoji kuhusu suala hilo, na kwamba wanaamini ufumbuzi utapatikana.

Serikali yahaha

Baada ya taarifa hizo kuripotiwa na gazeti hili jana, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Jeshi la Polisi wanafanya mawasiliano na Serikali ya Pakistan ili kuangalia namna ya kumwokoa Adamu katika mikono ya maharamia hao.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Msemaji wa Polisi, Advera Bulimba, alisema tayari wamepata taarifa dhidi ya Mtanzania huyo.

“Kwa sasa tunafanya mawasiliano na wenzetu wa Pakistan tuone namna ya kumtoa kijana huyo katika mikono ya hao watekaji, na tukikamilisha hilo tutatoa taarifa rasmi juu ya jambo hili,” alisema Advera.

Wakati hayo yakiendelea, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, kupitia mmoja wa maofisa wa idara ya habari ambaye hakupenda kutajwa jina lake gazetini, alisema wamepata taarifa ya tukio hilo, na sasa wanafanya mawasiliano na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Source: Mtanzania

Rais Magufuli: 5,000/= Wanazoomba Trafiki Barabarani Hazina Shida

0
0
Rais Magufuli Anaonekana akisema:
Saa zingine tunawaonea ninyi polisi, unakuta traffic amekaa mvua inanyesha lakini hata kumshukuru hamna kila siku anaambiwa anakula rushwa rushwa, sasa lakini hata akipewa sh 5000 ya kwenda kubrushi kiatu chake nayo ni rushwa?

Msikilize Hapa:

Dokta Mwaka Awazidi Kete Serilali..Abadili Gia Angani na Sasa anauza Bidhaa za Urembo

0
0

BAADA ya Serikali kukifutia usajili Kituo cha Tiba Asili cha ForePlan cha Dk. Juma Mwaka, hivi sasa amekigeuza kuwa kampuni inayojishughulisha na bidhaa za afya, usafi na urembo.

Julai 12 mwaka huu, Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala ilivifutia usajili vituo vitatu vya tiba asili kikiwamo cha ForePlan kwa madai ya kukiuka taratibu za kitabibu za tiba asili, huku wakiwa wameonywa lakini walishindwa kubadilika.

Sababu nyingine ya kufungiwa kliniki hiyo, Serikali ilisema katika matangazo ya kituo chake, Dk. Mwaka alikuwa akitangaza kuwa anatoa tiba za kisasa huku akiwa hana elimu inayomruhusu kufanya hivyo.

Akizungumza na Kituo cha Redio cha Clouds FM Julai 15, mwaka huu, Dk. Mwaka aliwataka Watanzania kuwa tayari kupokea bidhaa zitakazokuwa zikisambazwa na kampuni yake ya ForePlan.

“Ninachoweza kusema ni kwamba kaa tayari kwa bidhaa ya FP ambayo itakuwa adimu, watu wanaoijua wameanza kuitolea oda, kwa bahati nzuri imesajiliwa ndani na nje ya nchi,” alisema Dk. Mwaka.

Aliwataka wafike ofisini kwao na kupata maelekezo sahihi wanayoyahitaji  na  kwa watu wa mikoani watapata huduma zao kwa kupiga namba za simu 0767600600 na 0762 400400, hivyo watapata bidhaa zao huko walipo.

“Unapozungumzia afya, urembo na usafi, unazungumzia Kampuni ya ForePlan, ofisi za kampuni zinapatikana Ilala Bungoni Dar es Salaam, ukifika Ilala ulizia ForePlan na hata ukimuuliza mtu kwa jina maarufu kwa Dk. Mwaka atakuonyesha,” alisema.

“Unachotakiwa kufanya ni kutoa maelezo ya bidhaa  unazozitaka na ambacho unakitaka, utapewa ushauri wa bidhaa za kutumia na ikiwa utachagua kutumia bidhaa za forePlan, utapewa gharama za bidhaa hizo halafu ukishatuma fedha kwa njia ya M.pesa utatumiwa bidhaa huko uliko.

“Ninachoweza kusisitiza ni kwamba ukiongelea afya, urembo na usafi, unazungumzia kampuni ya ForePlan. Kwa hiyo usisite kuwasiliana nasi na kutembelea ofisi zetu zilizopo jijini Dar es Salaam au kutupigia kwa namba za simu ambazo nimekutajia,” alisema Dk. Mwaka.

Mtoto Aliyewekewa Betri Kwenye Moyo Afunguka, Atamani Kuwa Daktari Bingwa

0
0
MTOTO Happiness Josephati (5) aliyefanyiwa upasuaji wa kuwekewa betri maalum kwenye moyo ambayo kitaalam inaitwa ‘pacemaker’ katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)  amesema anatamani aje kuwa daktari bingwa hapo baadae.

Akizungumza na MTANZANIA katika mapumziko ndani ya chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) Dar es Salaam jana alisema hivi sasa anaendelea vizuri huku akimshukuru Mungu, wauguzi na madaktari waliomsaidia kufika hatua aliyo nayo sasa.

“Nikiwa mkubwa nami natamani niwe daktari bingwa ili niweze kuwasaidia watu wengi dhidi ya magonjwa kama haya yanayowasumbua, “alisema Happiness.

Naye Daktari bingwa wa nusu kaputi wa JKCI, Angela Muhozya alisema kwa sasa Happiness anaendelea vizuri wakati wowote ataondolewa ICU.

“Wakati alipoletwa mapigo yake ya moyo yalikuwa 20, hali hiyo kwa mtoto si ya kawaida kwani anapaswa kuwa na wastani wa 60 hadi 100 kwa umri wake.

Alisema Happines alizaliwa na tatizo lakini mara nyingi hali hii huwakumba watu wazima.

“Katika uumbaji wa Mungu kwenye moyo wa mwanadamu kuna kitu kama betri ambacho huzalisha umeme na kila mmoja huzaliwa nacho lakini Happiness hakuzaliwa nacho, ” alisema.

Daktari huyo alisema kwa sasa wanakabiliwa na uhaba wa vifaa hivyo (pacemaker)  kwa ajili ya kuwafanyia watu upasuaji na kuomba wale wenye uwezo kujitokeza ili kusaidia kukabili changamoto hiyo.

” Vifaa hivi vinauzwa ghali na vinapatikana nje ya nchi, kuna idadi kubwa ya wagonjwa ambao ni watu wazima wanasubiri  upasuaji lakini vifaa hivyo hatuna, ” alisema

Mama wa Happiness, Elitruda Malley alisema alikuwa anazimia kila mara.

” Alikuwa anachoka haraka ilibidi tumuachishe shule, nikampeleka hospitalini wakampima wakajua tatizo la moyo wakanipa rufaa ya kuja JKCI, “alisema.

Alisema hata hivyo aliambiwa gharama za matibabu yake ni Sh milioni nane ambazo hata hivyo hakuwa nazo kwa wakati huo.

” Ilibidi nirudi Arusha kwenda kutafuta fedha hizo lakini uongozi wa JKCI walisema iwapo atatokea mfadhili watanijulisha.  Ndipo wakaja hawa madaktari wa Marekani wakanisaidia.

Kati ya Wanafunzi 7,805 waliofukuzwa UDOM, ni 382 tu ndio wenye sifa

0
0
Serikali imetangaza orodha ya wanafunzi ambao watarejea kuendelea na masomo katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) baada ya uchambuzi kumalizika na kupatikana idadi ya wanafunzi ambao wana sifa za kuendelea na masomo.

Akizungumza na waandishi wa habari, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako alisema kuwa kwa kipindi chote walikuwa wakifanya uchambuzi ili kuona ni wanafunzi gani walikuwa na sifa za kusoma kozi hiyo maalum ambayo ilianzishwa kutokana na tatizo la walimu wa Sayansi.

Alisema kuwa programu hiyo ilikuwa inahitaji walimu ambao watakwenda kufundisha shule za sekondari lakini kulikuwa na wanafunzi 1,210 ambao walikuwa wanachukua stashahada ya ualimu wa shule za msingi ambao ni kinyume na malengo na 6,595 wakichukua stashahada ya kufundisha shule za sekondari.

“Baada ya hatua ya kuwaondoa wanafunzi chuoni kuchukuliwa, serikali ilifanya uchambuzi wa wanafunzi hao kwa lengo la kujiridhisha na sifa zao. Sifa zilizotakiwa ni ufaulu wa daraja la 1 hadi daraja la 3 na krediti mbili au zaidi katika masomo ya Sayansi na Hisabati,

“Lakini baada ya uchambuzi kufanyika kati ya wanafunzi wanaosomea ualimu wa sekondari 6,595 ni wanafunzi 382 pekee ndiyo wana sifa za kuendelea na masomo yao, 134 ni mwaka wa kwanza na 248 ni mwaka wa pili,” alisema Prof. Ndalichako.

Aidha alisema kuwa wengine 4,586 wa mwaka wa kwanza wa programu maalum wa stashahada ya ualimu wa sekondari waliokidhi vigezo vya ufaulu watahamishiwa katika vyuo vya ualimu vya serikali ambavyo ni Morogoro, Butimba, Mpwapwa, Songea na Tukuyu kuendelea na masomo na wanafunzi 1,337 wa mwaka wa pili watahamishiwa vyuo vya Korogwe na Kasulu ili kumalizia masomo yao.

Pia alisema kuwa serikali itaendelea kuwapatia mikopo wanafunzi watakaoendelea kusoma UDOM na watarejea chuoni mwezi Oktoba mwaka huu, huku wale wa vyuo vya ualimu watakuwa wakilipiwa ada ya 600,000 kwa mwaka ambayo ndiyo ada ya vyuo hivyo na wataripoti chuoni mwezi Septemba.

Kwa upande wa wanafunzi wa kufundisha elimu ya shule ya msingi, Prof. Ndalichako alisema wanafunzi 29 wa mwaka wa pili ambao wana cheti cha daraja A la ualimu watahamishiwa Chuo cha Ualimu Kasulu ili wamalize masomo yao ila tu kwa gharama zao huku wengine 1,181 akiwataka waombe nafasi katika vyuo vingine katika masomo ambayo wana sifa zinazolingana nao.

Aidha katika hatua nyingine, Prof. Ndalichako alisema kuwa migomo iliyokuwa ikitokea chuoni UDOM kwa walimu kugoma kuwafundisha wanafunzi hao yawezekana ilikuwa ikichangiwa na wanafunzi hao kwani uwezo wa chuo cha UDOM ilikuwa ni kupokea wanafunzi 1,180 lakini wakapokea wanafunzi 7,805.

“Walimu kwao mzigo ulikuwa ni mzito wewe utafanya nini?, kwahiyo tukubali kuwa wingi wa wanafunzi ulichangia kutokea mgomo sababu walimu wameajiriwa kufundisha na wengine wa digrii sasa kupokea wanafunzi 7,805 na ilitakiwa 1,180 walikuwa wengi,” alisema Prof. Ndalichako.

Mlinzi Adaiwa Kujinyonga kwa Kuambukizwa VVU

0
0
Mlinzi wa  Kampuni ya  Ulinzi ya Imara , Samwel Alcado (39) amekutwa akiwa amejinyonga ndani ya chumba chake kutokana na kile kinachodaiwa ni kugundulika kuwa ana virusi vya Ukimwi (VVU).
Mlinzi huyo ambaye ni mkazi wa mtaa wa Mji wa Zamani Manispaa ya Mpanda amejinyonga kwa kutumia shati lake.
Mwenyekiti wa mtaa huo, Margret John amesema tukio hilo  limetokea  leo  majira  saa kumi na moja alfajiri ndani ya   chumba alichokuwa  akiishi   Alcado.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Damas Nyanda amethibitisha kutokea kwa kifo hicho akisema uchunguzi zaidi unaendelea kufanyika ili kubaini ukweli halisi wa tukio hilo.

Jose Chameleone Afunguka Baada ya Kusemekana Ana Bifu na Diamond...

0
0

Msanii mkongwe wa muziki kutoka nchini Uganda, Jose Chameleone amefunguka kwa kusema kuwa hana tatizo na hit maker wa wimbo ‘Kidogo’, Diamond Platnumz.


Mitandao ya kijamii ilidai wawili hao hawakuwa sawa kwa muda mrefu kutokana na madai ya kuwa Jose Chameleone kumdengulia Diamond baada ya kuombwa kolabo, lakini hakuna aliyewai kuzungumzia tetesi hizo.

Jumanne hii Jose amesema hakuwai kuwa na tatizo na Diamond kama baadhi ya watu wanavyozungumza.

“I know how much hard work it takes to build a name and how we are all relevant to flying Africa Music to the world. I can see people trying to build beef lines between me and Diamond Platnumz all these years,” aliandika Jose kupitia instagrm.

Aliongeza, “All I can say is go higher my brother the sky ain’t the limit.Stay strong and God bless you more,”

Baada ya kusema hivyo, mashabiki wa Diamond pamoja na wadau mbalimbali wa muziki katika mitandao ya wamempongeza Jose Chameleone.

Diamond na Mama Mtoto Wake Zari Hassan Wathibitisha Tetesi za Kuwa Wamenunua Nyumba ya Kifahari South Africa

0
0

Diamond na Zari wathibitisha uwepo wa Jumba kubwa la kifahari walilonunua South Africa kwaajili ya mtoto wao Tiffah! !! Hakika hapa wametisha mbayaa...unaambiwa hilo Jumba ni shidaaaa...
#ubuyuuuuu

Mahakama Yamsaka Meneja wa Diamond ‘Babu Tale’

0
0
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetoa hati ya kukamatwa kwa Hamis Tale ‘Babu Tale,’ ambaye ni meneja wa mwanamuziki wa bongo fleva, Diamond Platnumz, anaandika Faki Sosi.
Mahakama imetoa hati hiyo kutokana na Babu Tale kutotii amri ya mahakama iliyomtaka amlipe Shekhe Hamis Mbonde Sh. 250 milioni.

Babu Tale anatakiwa alipe fedha hizo kutokana na kuvunja mkataba kati yake na Shekhe Mbonde, kwa kuuza na kusambaza nakala za mawaidha (DVDs) bila ridhaa ya shekhe huyo, jambo ambalo ni kinyume na haki miliki.

Kutokana na Babu Tale na mwenzake Iddi Tale kushindwa kulipa fedha hizo kama ilivyoamriwa tarehe 18, Februari  mwaka huu, mahakama ilitoa hati ya kukamatwa kwa wadaiwa hao tarehe 8 Julai mwaka huu.

Katika hati hiyo, mahakama ilimuelekeza Kamanda wa Polisi Kanda ya Ilala kuwa, hadi leo tarehe 19 Julai mwaka huu awe amewakamata wadaiwa hao ili wafike mahakamani kueleza kwanini wasipewe adhabu kwa kukiuka amri ya mahakama.

Shauri hilo limetajwa tena leo mbele ya Juma Hassan, Kaimu Msajili wa Wilaya wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ambapo ametoa hati nyingine kumuelekeza Kamanda wa Polisi Kanda ya Kinondoni kuwakamata wadaiwa hao.

Msajili Juma ametoa hati hiyo baada ya Mwesigwa Muhingo, Wakili wa Shekhe Mbonde,  kuomba hati hiyo ipekwe Kinondoni kwa kuwa Babu Tale anaishi huko na si Wilaya ya Ilala kama hali ya kwanza ilivyoeleza.

Tarehe 18 Februari mwaka huu, Jaji Augustine Shangwa, aliwaamuru wadaiwa kulipa Sh. 200 milioni  kama fidia ya kuvunja haki miliki ya Shekhe Mbonde na Sh. 50 milioni kama fidia ya hasara aliyoipata kutokana na kuvunja makubaliano.

Katika uamuzi wake Jaji Shangwa amesema, Juni 16, 2013, Mbonde aliingia makubaliano na wadaiwa hao na wenzake ya kufanya biashara ya kurekodi mawaidha na kutengeneza nakala DVDs kwa ajili ya kuziuza nchini.

Wadaiwa hao waliahidi kumjengea nyumba, kumnunulia gari na kuitangaza kazi yake pia walimpa Sh milioni mbili na kumnunulia kanzu na kofia (baraghashia) na kurekodi DVDs zenye ujumbe Uzito wa Kifo, Fitina Juu ya Wanawake, Umuhimu wa Swala, Mwanadamu Yumo Ndani ya Hasara na Maadui wa Uislam.

Amesema, makubaliano ya awali yalikuwa kurekodi halafu baadaye wakubaliane kuhusu bei na jinsi ya kuziuza, badala yake waliziuza na kuzisambaza nakala hizo na kujipatia faida bila kumshirikisha Mbonde ambaye alitumia ujuzi wake.

Mbonde kupitia wakili wake Muhingo, Gwamaka Mwaikugile na Clement Kihoko,  alifungua kesi ya madai namba 185/2013 akiiomba mahakama iamuru wadaiwa wamlipe Sh. 700 milioni kama  fidia ya kuvunja makubaliano na Sh. 50 milioni kama fidia ya hasara aliyoipata kutokana na kuvunjwa kwa makubaliano.

Kutana na Mtandao Mpya wa Kijamii Kwa Ajili ya Kukuza Secta ya Utalii Tanzania 'EZYLINC '

0
0
Ezylinc ni mtandao mpya wa kijamii, ambapo watu binafsi na makampuni wanaweza kuweka
picha na kuandika makala kuhusu vivutio vya utalii vilivyopo nchini.

Mtu yeyote anaweza kujiunga na mtandao huu wa kijamii bure kabisa kwa kujisajili
www.ezylinc.com , baada ya hapo anaweza kuweza picha, kuandika makala kuhusu vivutio vya
utalii, kutengeneza magroup, kukutana na marafiki wengi zaidi kutoka sehemu mbalimbali
duniani na mengine mengi.

Ezylinc inaunganisha makundi mawili. Upande mmoja tuna watalii, na kwa upande mwingine
watu wanaofanya kazi zinazoendana na shughuli za kitalii.

Hapa Tanzania kama mfano, utalii ni sekta inayoliingizia taifa fedha nyingi za kigeni. Katika mwaka
2014 sekta ya utalii, imechangia asilimia 17 katika pato la taifa na kuchangia kwa asilimia 25 ya
mapato yote ya fedha za kigeni, ambapo bilioni 2 za Kimarekani zilipatikana.

Tanzania ni nchi yenye vivutio vingi vya utalii katika bara la Afrika. Kilimanjaro mlima mrefu kuliko
yote Africa, Visiwa vya Zanzibar, hifadhi za taifa za Serengeti na Ngorongoro, Tarangire, Ziwa
Manyara, Ruaha na Selous, ni mifano hai michache ya vivutio vinavyopatikana Tanzania.

Kwa kutumia mtandao huu mpya wa kijamii tunaweza kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini
kwetu kwa urahisi zaidi, na kupata watalii wengi zaidi.

Hii ni moja ya sababu kubwa kutengeneza mtandao mpya huu wa kijamii. Tunalenga kusaidia
ukuaji zaidi wa sekta ya utalii nchini, na hiyo itasaidia watu wengi zaidi kupata ajira katika shuguli
zinazoendana na sekta hii.

Karibu - Kujiunga Ezylinc, Ingia: www.ezylinc.com

Lulu Usitukane Wakunga, Uzazi Ungalipo!

0
0
KWAKO mtoto mzuri ndani ya Bongo Muvi, Elizabeth Michael ‘Lulu’. Hujambo? Habari ya huko ulipo? Wazima wote na familia yako? Shemeji yetu naye hajambo? Hongera maana naona siku hizi umeamua kumuanika hadharani.

Ukitaka kujua afya ya mimi kaka yako, sijambo. Namshukuru Mungu, naendelea kupambana ndani ya mjengo wa magazeti Pendwa, Global Publishers Ltd. Hapa sisi ni kazi tu!

Nimekukumbuka leo kwa barua. Kitambo kidogo sijakuona. Siku hizi umekuwa mzito sana kuzurura kwenye viwanja vyetu vya kujidai. Sikulaumu katika hilo, huenda ni utaratibu mpya ambao mwenyewe umejipangia. Ni jambo zuri pia. Staa anapaswa kupotea kidogo siyo kila kiwanja awepo.

Historia ya maisha yako inaonesha umeweza kukutana na changamoto nyingi ambazo naamini zilikuwa kubwa kuliko umri wako. Umejitahidi sana kuzikabili na maisha yanaendelea vizuri, mshukuru Mungu pia kwa hilo. Si akili zako bali ni kwa neema na rehema zake.

Madhumuni ya mimi kukuandikia barua hii, nina jambo. Nataka kukumbusha kwamba; usitukane wakunga wakati uzazi ungalipo. Sikufurahishwa na kitendo cha wewe kuwatukana waandishi wa Global Publisher hivi karibuni.

Wewe na vyombo vya habari (hususan Global) ni kama chanda na pete. Ukubali ukatae, magazeti yake yamechangia kwa kiasi kikubwa sana kukufikisha ulipo leo. Hata kama yanauza kupitia habari za mastaa lakini mchango wake katika maendeleo yenu ni mkubwa.

Kwa kuandika habari zako, zimesaidia kwa kiasi kikubwa kuwashawishi Watanzania kukufuatilia. Kujua unafanya nini kwa wakati husika na kisha kukusapoti kwa kununua kazi zako.

Hata pale ulipopata majanga mbalimbali, kama kampuni kwa namna moja au nyingine iliweza kutoa mchango wake. Hata usipokiri hilo hadharani, lakini moyoni unajua. Siwezi kufafanulia kila kitu lakini ukweli unaujua.

Katika hilo si wewe tu, hata familia hususan mama yako anajua mchango wa Global katika maisha yako. Haujavuka mto kiasi cha kutukana mamba. Unaanzaje kuwatukana waandishi wa Global? Ujasiri huo unautoa wapi? Mafanikio gani yanayokupa jeuri?

Unawatukana waandishi wa kampuni ambayo unajua imekutoa wapi kweli? Kwani ukiwapa majibu ya kwamba hilo siwezi kulizungumzia, utapungua nini? Hujisikii kuongea, unaweza ukakaa kimya, hakuna atakayekulazimisha. Maana misingi ya habari inatoa nafasi kubalansi, ukiwa hautaki wao wanajua nini cha kufanya.

Global ina watu wanaokuzidi umri mara tatu au nne. Kuna wafanyakazi ambao wanaweza kukuzaa, unapata wapi ujasiri wa kuwatukana? Unaweza kumtukana mtu aliye sawa na umri wa wazazi wako? Au unataka kutuaminisha kwamba huwa unafanya hivyo kwa wazazi wako? Naamini jibu ni hapana, sasa kwa nini ufanye hivyo kwa watu ambao unajua wana umri sawa au zaidi ya wazazi wako?

Mdogo wangu nataka uelewe kwamba ulikosea, unapaswa kuomba radhi. Hupaswi kuwavimbia kichwa waandishi wa habari wakati haohao bado utawahitaji huko mbeleni. Haohao wanaweza kukusaidia jambo kubwa sana pengine huko uendako.

Nakushauri kuwa muungwana, omba radhi na maisha yataendelea kama kawaida. Kwa umri wako hauna sababu ya kuweka bifu na waandishi wa habari, si wa Global tu hata wa vyombo vigine vya habari. Unahitaji sapoti yao ili uweze kusonga mbele.

Yangu mimi ni hayo tu kwa leo, ni matumaini yangu utakuwa umenielewa na utatumia busara katika hili. Mungu akusimamie!

Mimi ni kaka yako;

GPL

Zari Hassan Awafungukia Wote Wanadai Kuwa Yeye ni Gold Digger Kwa Diamond

0
0
Kuna Baadhi ya watu huko mitandaoni wanalalamika kuwa Baby Mama wa Diamond Zari Hassan ni Gold Digger, Kuwa yupo kimaslahi zaidi kwa Diamond na anamchuna ipasavyo...
Baby Mama huyo maneno yamemkuna na kuwafungukia kama ifuatavyo:

'When people call you a gold digger show them how you dig, too much money out there for all of us. Why hate? Stop BITCHCRAFTY it's the 21st century'


Akaendelea Hivi:

'Say YES to this type of gold digging or digging gold. And if your man happens to spoil you its because he can afford it and your his 👑ueen you deserve it..... yes am a GOLD DIGGER 😊 coz I earn every that comes my way. Now let's all go and dig some gold.'

Madhara ya Kufanya Mapenzi au Tendo la Ndoa Mara Nyingi Kupita Kiasi

0
0

Katika hali ya kawaida kufanya mapenzi kuna faida nyingi, lakini linapokuja suala la kuzidi kiasi tunapata matatizo ya msingi ambayo huleta madhara kwa watu wanaoendekeza sana ngono.

Kuna watu ambao hawezi kulala bila kufanya mapenzi na huku wengine wakikosa uwezo wa kuvumilia hata kwa siku mbili au tatu.  

 Mtu anaweza kuwa na mke na kujikuta kila siku anatumia ‘chakula cha usiku’ kwa sababu tu hakuna wa kumkataza na kwamba ana haki ya kufanya hivyo kwa sababu amelipa mahari.

Hilo linaweza kuwa jambo jema kwa upande mwingine, lakini uchunguzi unaonyesha kuwa watu wengi kati ya watu wanaolalamika kupoteza hisia za kimapenzi hutoka katika kundi la watu wapenda ngono. 

 Pamoja na tatizo hilo, yapo madhara mengine mengi ambayo mtu asiyekuwa na kiasi katika tendo la ndoa anaweza kukabiliana nayo, hivyo ni vema tukajifunza ili tusiwe watu wa kuendekeza miili kiasi cha kulazimika kufanya mapenzi kila tunapokutana hata kwenye nguzo ya umeme na chini ya miti kwa vile tu miili imetaka kufurahika. 

 KUPOTEZA HAMU YA TENDO

Watu wenye pupa za kufanya mapenzi hupoteza haraka hisia za kimapenzi kwa wapenzi wao kutokana na sababu za kisaikolojia zinazoweza kujitokeza wakati wa ufanyaji wa tendo la ndoa mara kwa mara. 


 Sababu hizo zinaweza kuwa ni pamoja na zile za kumzoea mwenza kiasi cha kukosa msisimko hata anapomuona akiwa mtupu.



 Aidha kukinai haraka staili za kimapenzi  kunatajwa kujitokeza kutokana na kukutana mara kwa mara kwa aina zile zile za mapenzi na pengine sehemu moja, kitanda kimoja na chumba kile kile, jambo ambalo linaweza kumfanya mhusika asione jipya kutoka kwa mwenza wake na hivyo kupoteza hamu naye na kuhisi kama hawezi tena kushiriki tendo la ndoa kikamilifu.


 KUUJAZA MWILI TAMAA KUBWA

Tabia ya kufanya mapenzi mara kwa mara huongeza uzalishaji wa homoni mwilini na kuufanya mwili uwe na msukumo mkubwa wa kutaka kuridhishwa kwa tendo la ndoa bila kukosa na hivyo kumfanya mhusika asiwe mtu mwenye uwezo wa kuzuia tamaa na kukosa chaguo la nani wa kufanya naye mapenzi na kwa wakati gani

 Watu wanaojiendekeza katika kufanya mapenzi mara kwa mara ndiyo wale ambao kila wanayemtazama barabarani humtamani bila kujali hadhi yake.  

Hawa ndiyo wanaobaka, kusaliti ndoa zao hata kwa watumishi wa ndani au kufanya mapenzi na watoto wao wa kuwazaa kwa vile akili zao huwa zimeathirika kwa tamaa ya mapenzi. 


Unapokuwa mtu wa kufanya mapenzi mara kwa mara huwezi kuwa na uwezo wa kuzuia tamaa yako. Mumeo akiondoka siku mbili unatamani kuwa hata na houseboy ili akukate kiu ya penzi.  

 KUPOTEZA RAHA KAMILI YA TENDO
Raha ya tendo hutegemea sana hisia iliyokuzwa kutokana na mapenzi sahihi na kiu ya kufanya mapenzi, hivyo basi ukiwa mtu wa kufanya mapenzi kila mara unaweza kupoteza msisimko wa tendo na kujikuta unapata furaha ambayo haikutoshi kumaliza tamaa yako. 

 Kama ni mapenzi utakuwa unayafanya kwa mazoea tu na msisimko wako utakuwa mdogo! 

 KUPOTEZA NGUVU ZA MWILI

Madhara mengine yanayoweza kupatikana kwa kufanya mapenzi mara kwa mara ni pamoja na kupoteza nguvu nyingi za mwili.

Kama tujuavyo tendo la ndoa hasa kwa wanaume huwafanya watumie nguvu nyingi, hivyo kuufanya mwili uchoke.  

Aidha lishe inapokuwa ndogo kwa wafanya mapenzi mwili hukosa nguvu za kutosha kuhimili misukosuko ya kimaisha. 

 Sambamba na hilo mbegu za uzazi zinazotoka kwa wanaume wanaofanya mapenzi mara kwa mara huwa dhaifu.

 KUPATA MAGONJWA
Kama tulivyojifunza kuwa watu wanaofanya mapenzi mara kwa mara huwa na tamaa na hujikuta wanafanya mapenzi holela ambayo huweza kuwasababishia magonjwa ya zinaa ukiwemo ukimwi. 

Ufanyaji wa mapenzi usiokuwa na msukumo wa kutosha hasa kwa wanawake huwafanya waishiwe msisimko na kuzifanya sehemu zao za siri kutotoa ute unaoweza kuwakinga na michubuko wakati wa kujamiiana na hivyo kuwasababishia michubuko itakayoweza kuleta maambukizi ya haraka ya magonjwa ya zinaa ukiwemo ukimwi. 

 Baada ya kungalia madhara hayo machache ni vema kwa wapenzi kupunguza kiwango cha kufanya mapenzi ili kuifanya miili iwe na uvumilivu unaoweza kumsaidia mtu kukaa kwa muda mrefu bila kumsaliti mpenzi wake hata kama atakuwa amesafiri mbali naye kimasomo, kikazi au kibiashara.
Viewing all 104428 articles
Browse latest View live




Latest Images