Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live

Kikwete Atoa Dongo "Wapo Watu Walidhani CCM ingekufa na Walishajiandaa na Salamu za Rambirambi"

$
0
0
MWENYEKITI wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais mstaafu Jakaya Kikwete, amekata mzizi wa fitna kwa kutangaza rasmi kuwa Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM, utakaofanyika mjini Dodoma kesho utafanya kazi moja tu ya kumchagua Rais John Magufuli kuwa Mwenyekiti mpya wa chama hicho.

Kikwete alisema hayo alipofungua kikao cha Kamati Kuu ya CCM kwenye ukumbi wa White House, makao makuu ya CCM, mjini hapa jana. Kauli hiyo ya Kikwete inamaliza minong’ono ya muda kuwa hapangekuwa na kupokezana kijiti katika mkutano huo.

Pia kauli hiyo imezima madai kwamba kungekuwa na mchujo katika uchaguzi wa Mwenyekiti, ambapo majina hadi matano yangependekezwa na Kamati Kuu na kupelekwa katika Halmashauri Kuu ambayo ingekata mawili na kupeleka matatu kwenye Mkutano Mkuu Maalumu, ili yapigiwe kura kumchagua Mwenyekiti.

“Ajenda yetu kubwa leo (jana) ni moja tu; nayo ni kupendekeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ili nayo Halmashauri Kuu ya Taifa ipendekeze kwa Mkutano Mkuu wa CCM ili achaguliwe kuwa Mwenyekiti wa CCM,” alisema Kikwete kwenye ufunguzi huo wa Kamati Kuu, akitumia dakika tano tu, kisha wajumbe wakaendelea na ajenda. Rais Magufuli alichaguliwa kuongoza Tanzania Oktoba mwaka jana.

Katika hotuba yake hiyo ya jana, Kikwete aliwajia juu ‘wafitini’ walioombea chama hicho kife katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.

Alisema “Wapo watu walidhani CCM ingekufa na walishajiandaa na salamu za rambirambi. Walidhani wataibuka. Hawakuibuka na hawataibuka kamwe.”

Kikwete aliwaeleza wajumbe wa kikao hicho kuwa kilikuwa kikao chake cha mwisho cha Kamati Kuu, kauli iliyobainisha wazi kuwa anang’atuka kumwachia kijiti Rais Magufuli kuongoza chama.

Alisema amekuwa Mwenyekiti wa Chama kwa miaka 10, hivyo aliwashukuru wajumbe wa Kamati Kuu kwa kumsaidia katika kipindi chote hicho huku akisisitiza; “Bila msaada wenu CCM isingekuwa imara kama ilivyo hivi leo.”

Wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, Rais Magufuli alikuwa akifahamika kama Tingatinga na kwenye mikutano kadhaa, Rais mstaafu Kikwete aliweza kumuita kwa jina hilo.

Wakati huo huo Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete jana alikagua ukumbi wa mikutano wa CCM na kuoneshwa sehemu mbalimbali ambapo alisema ameridhika na maandalizi ya mkutano kwamba yanaenda vyema.

Maeneo mengine aliyotembelea ni mabanda ya mama na baba lishe, sehemu za kutolea huduma za Benki na mabanda ya maonesho ya wajasiriamali.

Katika ziara hiyo aliambatana na Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana, makamu Mwenyekiti Bara, Phillip Mangula, waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Nape Nnauye, msemaji wa CCM Christopher Ole sendeka, naibu katibu mkuu wa CCM Bara Rajab Luhwavi na wajumbe wa Kamati Kuu Pindi Chana na Mohamed Seif Khatib. Wajumbe wa mkutano Mkuu maalum wa CCm walianza kuwasili jana na wengine wengi wanatarajiwa leo.

Uhakiki wa vyeti: Watumishi 3,600 hatihati kukosa mishahara Pwani

$
0
0
Uhakiki wa vyeti vya watumishi wa umma mkoani Pwani kuwaweka watumishi 3,600 kwenye hatari ya kukosa mishahara ya Agosti mwaka huu baada ya kubaini mapungufu katika taarifa zao.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Angela Kairuki amesema kati ya hao, watumishi 3,569 taarifa zao za kielimu hazionekani,36 wana zaidi ya miaka 60 lakini wako kazini badala ya wamestaafu, sita akaunti zao hazitambuliki na 21 vyeo vyao havijabainishwa.

Amesema hivyo haitawezekana kulipwa mishahara kuanzia Agosti hadi hapo mapungufu ya taarifa zao zitakaporekebishwa.

Akizungumza na watumishi wa umma Pwani, Kairuki amesema Bagamoyo ina watumishi 2,175 wenye taarifa zenye upungufu, Rufiji (912), Kibaha Mji(465), Mkuranga (21) Kibaha Vijijini (14), Mafia na Kisarawe (8).

Chanzo: Mwananchi

Samatta Kaisaidia KRC Genk Kutinga Round ya Pili ya Europa League

$
0
0
Mtanzania Mbwana Samatta bado anaendelea kufanya vizuri na kuzidi kuaminiwa na kocha wake Peter Maes ambaye kwa sasa amekuwa akimpa nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza na kucheza dakika zote 90, usiku wa July 21 2016 Mbwana Samatta aliichezea KRC Genk mchezo wa pili wa Europa League dhidi ya Buducnost ya Montenegro.

Genk imecheza mchezo wake wa pili na kulazimishwa kucheza kwa dakika 120 na baadae mikwaju ya penati, dakika 120 zilimalizika kwa Buducnost kuongoza kwa goli 2-0, goli ambazo zilifungwa na Djalovic dakika ya 2 na Raickovic dakika ya 40 lakini mchezo uliamuliwa kwa mikwaju ya penati kutokana na KRC Genk kuibuka na ushindi kama huo katika mchezo wao wa kwanza.

Katika mikwaju ya penati Genk imefanikiwa kuibuka  na ushindi wa penati 4-2, penati za ushindi wa Genk zilipigwa na nahodha wao Thomas Buffel, Heynen, Mbwana Samatta na Walsh, hivyo kwa matokeo hayo sasa Genk itacheza round ya pili ya Europa League dhidi ya Cork City ya Jamhuri ya Ireland.

Kutana na Jamaa Anayelipwa Pesa Kutoa Watoto Wadogo Bikira Kuondoa Mikosi

$
0
0
Habari hii imeripotiwa na BBC Swahili kuhusu jamii moja nchini Malawi ambayo haithamini ubikira wa watoto wao wa kike. BBC Swahili wameripoti kuwa katika jamii hiyo wazazi wanamlipa mwanaume kumbikiri binti yao punde tu anapopata hedhi yake ya kwanza.

Jamii hiyo inaamini kwamba kuwa na binti ambaye ni bikira ni mkosi kwa jamii, wazazi na jamii kwa ujumla katika maeneo mengi ya kusini mwa Malawi wamekuwa wakishikilia tamaduni hii kwa miaka na miaka.

Wanaume wanaowabikiri watoto wa kike huchaguliwa na wazazi kuwaondolea mikosi, na huwa ni sherehe kubwa inayomtangulia binti kupelekwa unyagoni kisha kuwatembelea shangazi wake kabla ya kujulishwa kwa ‘fisi’.

Mafisi hulipwa takriban dola 7 ambayo ni kama Tsh 15,324 kwa kila kitendo cha ngono na hao mabinti ambao wengi huwa na kati ya umri wa miaka 11-14. Fisi mmoja katika kijiji cha Nsanje, Eric Aniva ameiambia BBC kuwa hajui kwa kweli amewabikiri wasichana wangapi……
”kwa kweli mimi nimewabikiri zaidi ya wasichana 104, hiyo ndio tamaduni zetu pia hapa mwanamke akifiwa lazima aje kwangu nimuondolee mkosi hata kabla ya kuzikwa kwa mumewe’‘.

Katiba Mkuu Chadema Dkt Vicent Mashinji Awafunda Bavicha, Awapatia Mbinu za Kushinda 2020

$
0
0
Katibu Mkuu Chama cha Demokrasia na Maendeleo Dkt Vicent Mashinji amewataka vijana wa Bavicha kutokuwa wazembe wakufikiria bali kujipanga kwa ajili ya kushika dola mwaka wa uchaguzi mkuu 2020 huku akiwapatia kanuni za kushinda uchaguzi huo.

Akizungumza na vijana hao jana jijini Dar es salaam Mashinji aliwaambia vijana hao chama chao kimejipanga kushika dola hivyo wao kama vijana wanatakiwa kuhakikisha wanatekeleza majukumu ya kufanya uchaguzi na kuwatambua wanachama hai, pia kuhakikisha kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa vijana wanashiriki nafasi mbali mbali na kushinda

”Nataka niwape majukumu matatu ambayo mkiyafanya hayo 2020 tutashinda nakutangazwa, moja hakikisheni tunaingiza wanachama wapya na kuwahakiki walio hai, nendeni 2019 kwenye serikali za mitaa vijana mgombee na tupate viongozi ngazi ya chini viijana wasomi, na tatu kwa mwaka huu kila kijana ajue nafasi zitakozogombewa katika eneo lake hiyo itatusaidia kushinda nafasi nyingi za madiwani  kwa Tanzania bara na visiwani  na haya ndiyo majukumu makubwa ninayowapatia”   Alisema Mashinji.

Pamoja na hayo aliwataka vijana hao kuendelea kupigania haki za wanyonge na kushinda vita ya demokrasia bila kuvunja sheria huku akiwaasa kuwa askari mzuri na shujaa ni yule anayepambana bila risasi.

”Askari mzuri ni yule ashindaye vita bila kutumia risasi zake, mkawe mabalozi wa kuwatetea wanyonge na haki zao, msiwe waoga kudai katiba ya wananchi, pia kuna watu Geita, Shinyanga na Simiyu tunataarifa wanapigwa kisa itikadi ya upinzani wa vyama hivyo kama vijana mnatakiwa mpaze sauti kwa ajili yao”. aliwaambia Mashinji.

Hata hivyo Mashinji aliwaasa vijana hao kuwa wapole na kusubiri maamuzi ya viongozi wa chama kwani yanabusara. Aidha aliwapongeza vijana hao kwa kuwa na umoja wa kupigania haki na misingi ya demokrasia.

Mwenyekiti wa Bavicha Taifa Patrobas Katambi alimweleza Katibu huyo wa chama kuwa wao wapo tayari kwa pambano japo wanasikiliza na kutii kauli ya chama hivyo wao  watatoa msimamo wao.

”Sisi vijana tupo tayari miili yetu ilale makaburini na tukumbukwe kama mashujaa waliokufa wakipigania haki, tumesikiliza maagizo ya viongozi wetu lakini pia sisi leo tutatoa msimamo wetu”.- Katambi

Nay wa Mitego Afungukia Picha za ‘Pale Kati’ Zilizo Mdhalilisha Mwanamke, Azikana

$
0
0
Msanii Nay wa Mitego ambaye siku za karibuni wimbo wake mpya ‘Pale kati’ umefungiwa na Baraza la sanaa Taifa (BASATA) amefunguka na kusema kuwa suala la watu kusambaza picha kwenye mitandao ya jamii huku zikiwaonyesha wanawake wakiwa hawana nguo kabisa siyo kosa lake yeye kwani hakufanya hicho kitu bali kuna watu walitengeneza hizo picha wakiwa na malengo yao.

Nay wa Mitego amesema hayo katika kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio na kudai kuwa kuna watu walikuwa wanatengeneza picha hizo na kuzisambaza ila yeye hajafanya hivyo, na kudai kuwa alishajaribu kuwaripoti watu wengine ambao walikuwa wanafanya mchezo huo.

“Suala la picha za wimbo huo kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii huku zikionyesha wanawake wakiwa nusu uchi si suala langu mimi, maana dunia ya sasa kuna watu wanafanya ‘editing’ ya picha sana, kama mtakumbuka hata kipindi nimetoa ‘Shika adabu yako’watu walinitengeneza sana kwenye picha na kusambaza kwenye mitandao ya jamii, hivyo suala la picha hilo siyo tatizo langu” alisema Nay wa Mitego.

Mbali na hilo Nay wa Mitego amesema kuwa yeye hajaridhishwa na maamuzi ya BASATA kufungia wimbo wake mpya kwa kigezo cha picha kwani walipaswa kusubiri video itoke ndiyo inaeleza vizuri maana ya wimbo wake huo.

“Huwezi kufungia ‘Audio’ kwa sababu ya picha BASATA walitakiwa kusubiri nitoe video kwani video inatoa tafsiri nzuri ya wimbo huo na kama kungekuwa na tatizo kwenye video ndiyo tulipaswa kukaa na hawa walezi wetu katika muziki BASATA ili kuona tunaweza kurekebisha jambo gani katika video” alimalizia Nay wa Mitego

Maalim Seif kutinga Mahakama ya ICC leo Kuwashitaki Viongozi wa Serikali

$
0
0
Chama cha Wananchi (CUF) kimesema katibu wake mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad leo atakwenda katika Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa (ICC) kuwashtaki viongozi wa Serikali kwa madai walitumia mamlaka yao vibaya wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana na kisha kuwatesa, kuwakamata na kuwapiga wafuasi wa chama hicho bila makosa.

Chama hicho kikuu cha upinzani Zanzibar, kimesema taratibu zote za kufungua mashtaka hayo zimeshakamilika, ikiwa ni pamoja na kuweka wakili.

Mei 22 mwaka huu, chama hicho kilizindua ripoti yake ya uvunjwaji wa haki za binadamu Zanzibar wakati wa uchaguzi huo na kutangaza azma yake ya kwenda ICC kuwashtaki Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP).

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui alisema mpango huo umekamilika na Maalim Seif ambaye yuko nje ya nchi kwa ziara ya kueleza alichodai ‘figisufigisu’ zilizotokea katika uchaguzi mkuu, ataweka wazi kila kitu kilichotokea na jinsi ukiukwaji wa demokrasia ulivyoshika kasi nchini.

Mazrui alimtuhumu IGP Mangu kuwa anatumiwa na CCM kuwakamata viongozi wa CUF ili wasitimize azma yao ya kueleza ukweli wa yaliyotokea katika uchaguzi, huku akimtaka afute azma yake ya kumkamata Maalim Seif kwa maelezo kuwa “ataitumbukiza Zanzibar kwenye machafuko”.

Siku tano zilizopita, IGP Mangu wakati akihojiwa na Azam TV alisema Jeshi la Polisi wakati wowote litamburuza mahakamani Maalim Seif kwa kuhamasisha uchochezi Zanzibar. Iwapo CUF itatekeleza azima hiyo, itakuwa tukio la kwanza kwa Tanzania kupeleka viongozi wake kwenye mahakama hiyo.

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na naibu wake, William Ruto wameshafikishwa huko, lakini kesi dhidi yao zilikosa nguvu na kuondolewa.

Katika Uchaguzi Mkuu uliopita, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (ZEC), Salim Jecha Salim alifuta matokeo ya rais, wawakilishi na madiwani Oktoba 28, mwaka jana siku ambayo alitakiwa atangaze mshindi wa mbio za urais.

CUF ilidai kuwa ilishinda uchaguzi huo na Jecha alipotangaza uchaguzi wa marudio uliofanyika Machi 20 mwaka huu, chama hicho kilijitoa na hivyo CCM kushinda viti vyote.

Mazrui ambaye aliambatana na viongozi wengine wa chama hicho alisema: “Mpango wa kuishawishi dunia kuwachukulia hatua wahusika wote wa ukiukwaji wa haki za binadamu na uvunjwaji wa demokrasia uko palepale, hautasitishwa kwa vitisho vyovyote.

 “Lengo ni kuhakikisha unyama dhidi ya raia wasio na hatia unakomeshwa na uzingatiwaji wa sheria za nchi unatamalaki. Tunawaambia polisi kuwa tumechoshwa na figisufigisu maana zitazaa timbwiri.”

Mazrui alisema wanaotaka kuzuia mpango wa CUF kueleza ukweli na kwenda ICC, wanaandaa utaratibu wa kumkamata Maalim Seif aliyedai; “Ni kipenzi cha Wazanzibari”, akisisitiza kuwa jambo hilo ni hatari kwa sababu litaivuruga Zanzibar.

Akifafanua zaidi kile alichokiita mikakati ya CCM kupitia kwa IGP Mangu kuficha ukweli, Mazrui alidai kuwa polisi wamekuwa wakiwakamata wanachama wa CUF mara kwa mara.

"Niongeavyo hapa wanachama zaidi ya 400 wa CUF wamekamatwa na wengine wapo nje wa dhamana,” alisema.

Alisema ni jambo la ajabu kuona IGP Mangu akishindwa kutoa kauli yoyote baada ya Naibu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DDCI), Salum Msangi kuwatishia mawakili kuwatetea wananchi wanaokamatwa kwa tuhuma  mbalimbali.

Alisema viongozi wa CUF hawatatishwa wala kunyamazishwa katika kudai haki ya ushindi wa Wazanzibari kutokana na uamuzi wao wa uchaguzi mkuu.

Katika mkutano huo, Mkurugenzi wa Uchaguzi na Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Shaweji Mketto alisema endapo IGP Mangu ataendelea kuwatisha viongozi wa CUF, watajipanga kwenda kumtembelea ofisini kwake.

IGP Mangu ajibu
Alipoulizwa kuhusu kauli za CUF, IGP Mangu alisema tayari ameshatoa msimamo wa Jeshi la Polisi na walichokifanya viongozi wa chama hicho ni kumjibu tu.

“Ukipendwa sana ukafanya uhalifu tukuache? Tukikutuhumu unafanya makosa tutakukamata hatuwezi kuogopa umaarufu wako,” alisema huku akisisitiza kuwa jalada kuhusu Maalim Seif lipo kwa DPP (Mkurugenzi wa Mashtaka).

“Umesema hao CUF wamesema kuna wanachama wao wamekamatwa, sasa wamekueleza hao wanachama ni kina nani?… kama wamekamatiwa Zanzibar wapo maofisa wa polisi wa mikoa wanaoweza kuzungumzia hilo huko Zanzibar.”

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai alisema: “CCM hatuwezi kujiingiza katika hoja za IGP na CUF tumewaachia wenyewe. Kwa sasa tupo katika maandalizi ya kuhakikisha Rais (John) Magufuli anashinda kwa kishindo kuwa mwenyekiti wa CCM.” Alisema chama hicho hakina sababu ya kutumia Jeshi la Polisi kukandamiza wanachama na viongozi wa CUF.

Zuio la Mikutano ya Kisiasa ni Kumyima Mwanchi Uhuru wa Haki ya Kujumuika- Kijo Bisimba.

$
0
0
Serikali imetakiwa kufanya marekebisho ya sheria mbalimbali ambazo zimeonekana kuwa kandamizi ikiwepo ile sheria za vyombo vya habari ambazo zinakandamiza uhuru wa vyombo vya habari pamoja na waandishi wenyewe.

Akitoa ripoti ya nusu mwaka mbele ya wanahabari kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za binadamu Bi Hellen Kijo Bisimba amesema kuwa vyombo vya habari havifanyi kazi kwa uhuru kwani zipo sheria ambazo bado ni kandamizi.

”Vyombo vya habari bado havina uhuru kwani sheria kandamizi bado zinatumika mfano, gazeti la mawio kufungiwa na kutakiwa kutoandika nakala zake hata kwenye mitandao bila sababu maalumu”.Ilielezwa katika ripoti ya kituo hicho

Aidha ripoti hiyo ya miezi sita imesema kuwa wananchi bado wananyimwa haki zao za msingi  ikiwa ni pamoja na  kunyimwa haki ya habari kwasababu  serikali imeamua kutorusha matangazo ya bunge kwa sababu mbalimbali ambazo zinakinzana.

Katika ripoti hiyo pia imegusa haki za kujumuika ambapo kituo hicho kimesema matamko ya jeshi la polisi hasa katika kuzuia mikutano ya vyama imeonekana  kupendelea chama tawala huku vyama vya upinzani  vikiwa vinakandamizwa.

”Mfano mkutano wa Chadema shinyanga ulipewa vibali vyote lakini baadae ukaja kutawanyishwa kwa kutumia nguvu mpaka mabomu, aidha ACT walikuwa na kongamano la kuchambua bajeti lakini jeshi la polisi walizuia lakini wakati huo huo CCM walikubaliwa kufanya mkusanyiko” Ilieleza semu ya ripoti ya Kijo Bisimba.

Pamoja na hayo ripoti hiyo imetoa mapendekezo kwa Serikali  ikiwa kuboresha sheria hizo kandamizi kwa wananchi pamoja na kuachia vyombo vya habari kufanya kazi zake pasipo kuingiliwa sambamba na Vyama vya siasa kupewa haki sawa.

TANZIA: KUNDAMBANDA afariki Dunia

$
0
0
Msanii maarufu wa VICHEKESHO (Komedi) Ndugu. Ismail Issa Makombe a.k.a KUNDAMBANDA, amefariki Dunia usiku wa kuamkia leo.

Kundambanda alikuwa mgombea ubunge wa CUF na UKAWA kwenye jimbo la Masasi - Mtwara katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi Disemba 2015 baada ya ule wa Oktoba kutofanyika kutokana na kifo cha aliyekuwa mgombea wa awali wa UKAWA, Mhe. Emmanuel Makaidi (NLD). Katika uchaguzi huo wa Disemba 2015 Kundambanda alipata kura 14,069 dhidi ya kura 16,597 za (mshindi) Rashid Chua Chua kutoka CCM. Taratibu za mazishi zinafanyikia nyumbani kwao Masasi.  Inna lillah wainailayna rajiun. RIP Kundambanda.

Chidi Benz afunguka mazito adai Joh Makini na Nay wa Mitego ni wasanii wakutengenezwa

$
0
0
Rapper Chidi Benz amefunguka kwa kusema kuwa hakuna msanii wa Hip Hop ambaye amefikia mafanikio yake huku akidai Joh Makini na Nay wa Mitego wametengenezwa ili waje kulishika game la muziki.

Akiongea na Uhuru FM Alhamisi hii, Chidi Benz amedai mpaka sasa hakuna msanii ambaye ameweza kufanikiwa na kufikia mafanikio ambayo aliyafikia katika kipindi cha nyuma.

“Sijamsikia yule mtu ambaye anafanya matukio kama mimi, yakuwa na msafara wa gari kumi, kusafiri kwenye show na watu 30, ukasikia watu 7 wamezimia kwenye show, bado sijawai kusikia matukio kama hayo labda bwana Joh Makini amefanya show Arusha wakazimia watu 9?,” alisema Chidi Benz.

 “Lakini nawasikia hao, kama Joh Makini namsikia na namuona kwenye muziki huu the way wametengeneza yeye ndo awe ameshika hili game, lakini hana nguvu, sisemi hivyo kama namblock hapana, hata mashabiki wake ambao wananisikiliza wamwambie nakubali hapo alipo na watu wamekutengeneza wewe ukae pale na hauna nguvu yakusema mimi ni Joh Makini, najua ni msanii mzuri lakini mimi ni The King Kong,”

Aliongeza, “Kwa hiyo wapo wasanii wengi wametengenezwa, mfano Nay wa Mitego pia, ni kitu fulani kimetengenezwa. Shetta hafadhali toka ameanza kutoka alikuwa anatengenezwa ili afanye game yake,”

Rapper huyo kwa sasa anafanya poa na wimbo wake mpya ‘Chuma’ aliyomshirikisha msanii kutoka WCB, Raymond.

Ripoti ya Jeshi la Polisi Dar es Salaam Baada ya Kumalizika kwa zoezi la uhakiki wa silaha, Pia Wamezungumzia Kiasi Walichokusanya Ndani ya Siku 6

$
0
0
Jeshi la Polis kanda Maalumu jijini Dar es salaam limekamata watuhumiwa sugu 1,065 kwa makosa mbalimbali yakiwemo unyang’anyi wa kutumia nguvu, wizi wa maungoni, wapiga debe, wavuta bangi, kikosi cha mbwa mwitu, watuhumiwa hao wamekamatwa kwa nyakati tofauti tofauti katika maeneo mbalimbali jijini Dar es salaam.

Hayo yamesemwa na kamishina wa polisi kanda maalumu ya Dar es salaam Simon Sirro alipokua akiongea na waandishi wa habari mapema hii leo, Sirro alisema kuwa kukamatwa kwa watuhumiwa hao kumekuja baada ya kufanya operesheni kali katika maeneo mbalimbali jijini humo.

Aidha pamoja na kufanikisha zoezi hilo kwa watuhumiwa hao,jeshi hilo pia wamekamata lita 952 za pombe aina ya gongo,bangi puli 227, kete 210, na misokoto144 kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam.

Katika hatua nyingine ,kikosi cha kupambana  na wizi wa simu cha polisi kimefanikiwa kuwatia hatiani watuhumiwa watatu(3) kwa makosa ya uporaji wa simu katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa kinondoni,watuhumiwa hao ni Richard Augustino (18), Abdallah Chande (36),Abdallah Said (22) wote wakazi wa jijini  Dar es salaam.

Hata hivyo kamanda Sirro aligusia  zoezi zima la uhakiki wa silaha na kusema kuwa lilienda vizuri na watu walijitokeza kwa wingi japo kuna changamoto kadhaa zilizojitokeza

Kamanda  Sirro amesema  idadi ya watu waliojitokeza kuhakiki silaha kwa wilaya zote tatu ni 11,602 na jumla ya silaha 14107 zilihakikiwa.

Pia kasema Jumla ya silaha 66 zilisalimishwa kutokana sababu mbalimbali ikiwamo mmiliki wa silaha kuwa na umri mkubwa na kushindwa kumudu silaha. Zoezi la uhakiki wa silaha limeiingizia Serikali mapato kiasi cha Mil 198.8

Jeshi hilo kupitia kikosi cha usalama barabarani kanda maalumu ya Dar es salaam limeweza kujikusanyia kiasi  cha shilingi 562,860,000/= kutokana na ukamataji wa makossa mbalimbali ya usalama barabarani kuanzia tar 15/7/2016 hadi 21/7/2016.
   Idadi Ya Pikipiki Zilizokamatwa  -1,413
     Idadi Ya Magari Yaliyokamatwa  –17,349
     Daladala Zilizokamatwa           -7220
     Magari Mengine (Binafsi Na Malori)- 10,129
     Jumla Ya Makosa Yaliyokamtw-  18,762
6. Bodaboda Waliofikishwa Mahakamani Kwa Makosa Ya Kutovaa Helmet Na Kupakia Mishkaki   ni 49

Programu za vyuo vikuu ambazo hazijasajiliwa na TCU na NACTE kufutwa

$
0
0
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Bi. Maimuna Tarishi ameitaka Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE)   kufuta programu zinazotolewa na vyuo vikuu hapa nchini ambazo hazijafanyiwa tathmini wala kusajiliwa.

Katibu Mkuu huyo ameyasema hayo leo alipokuwa akifunga maonyesho ya kumi na moja ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yaliyoanza Julai 20 katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

“Wakati mwingine najiuliza inakuwaje chuo kinafundisha programu ambayo haijatathminiwa wala kusajiliwa na TCU au NACTE, ni lazima tuwe makini kwani tunahitaji elimu bora katika vyuo vyote nchini bila kuangalia kama ni cha Serikali au ni Binafsi,” alifafanua Bi. Tarishi.

Aliendelea kwa kusema kuwa, TCU na NACTE wanajukumu ya kuzifuta programu hizo na kuanzisha programu zenye uhitaji mkubwa kama vile shahada ya mafuta na gesi, Kompyuta na Ualimu wa Sayansi ambapo wataalamu katika maeneo hayo wamekuwa wakihitajika zaidi katika kipindi hiki ambacho Serikali ya Awamu ya Tano inajikita zaidi katika uanzishwaji wa viwanda.

Aidha Bi. Tarishi amewataka TCU na NACTE kudahili wanafunzi wenye vigezo vinavyohitajika na kusisitiza kuwa ni bora kuwa na wanafunzi wachache katika vyuo vikuu kuliko kuwa na wanafunzi wengi ambao hawana sifa.

Wakati huo huo Mkuu wa Kitivo cha Biashara Chuo Kikuu cha Zanzibar Salehe Mwinyi amesema kuwa wanafunzi wengi wamejitokeza kutembelea banda la Chuo hicho kutaka kujua pogramu zinazotolewa na wengi wao wameonyesha nia ya kujiunga katika Chuo hiko.

Vile vile Mwinyi amesema kuwa mwaka huu idadi ya wanafunzi waliotembelea maonyesho hayo ni wengi zaidi kutokana na eneo lililochaguliwa kufikika kwa urahisi kutoka pande zote za jiji la Dar es Salaam ukilinganisha na mwaka jana ambapo yalifanyika viwanja vya Saba Saba na kutembelewa na idadi ndogo ya wanafunzi na wazazi.

Kwa upande wake, Fadia Suleiman mwanafunzi anayetegemea kujiunga na Chuo Kikuu mwaka huu, amesema kuwa maonyesho hayo yamemsaidia kwa kiasi kikubwa kujua ni programu gani asome kutokana na ufaulu wake wa kidato sita.

Maonyesho ya  Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia ambayo huandaliwa na TCU hufanyika kila mwaka yakitoa fursa kwa Vyuo Vikuu vya ndani na nje ya nchi kutoa elimu kwa wazazi na wanafunzi wanaotegemea kujiunga na vyuo vikuu kwa mwaka husika juu ya programu zinazotolewa na vyuo hivyo pamoja na kutoa ushauri ni programu gani mwanafunzi asome kwa kuangalia ufaulu wake.

Vyakula vya Aina 6 Vinavyozeesha Ngozi yako

$
0
0
Vifuatavyo ni vyakula 6 vinavyozeesha ngozi na unashauriwa kuvitoa katika mlo wako:

1. Chumvi
Chumvi hasa yenye madini ya iodine ni mbaya sana kwa afya ya ngozi. Inasababisha chembechembe za nyama katika ngozi kuvimba.

2. Sukari
Sukari japo tunaipenda sana ni adui mkubwa wa afya ya binadamu. Inadhoofisha mfumo wa kinga za mwili. Kiasi kingi cha sukari mwilini kinafanya ngozi kuwa kavu na kufanya mwili utengeneze makunyazi kwa sababu inaharibu kemikali ya collagen na elastin ambazo zinafanya kazi ya matengenezo ya ngozi kuifanya isiharibike na kuwa chakavu.

3. Vyakula Vya Kukaangwa
Vyakula vya kukaangwa kama chipsi,nyama za kukaanga vinasababisha uingizaji wa mafuta mengi mwilini. Mafuta haya yenye vitu vinavyoitwa “Free Radicals” yanasababisha uzibaji wa vijitundu katika ngozi. Ukiachia ngozi mafuta mengi mwilini yanasababisha madhara mengi mengine yakiwemo magonjwa ya moyo na kisukari.

4. Mkate Mweupe,Tambi Na Keki
Vyakula hivi vina kemikali ya glucemic kwa kiwango kikubwa ambayo inaleta madhara ya magonjwa ya ngozi (Ugonjwa wa madoa katika ngozi)

5. Pombe
Unywaji wa pombe unasababhisha kupoteza maji mengi mwilini kwa njia ya mkojo na huleta madhara mabaya kwa ngozi kwa kuifanya iwe kavu.

6. Kahawa (Caffeine)
Kemikali ya caffeine iliyomo katika kahawa na vinywaji vingine inasababisha ukosefu wa maji ya kutosha katika ngozi na kuifanya iwe kavu. Lakini pia caffeine inasababisha utengenezwaji wa kemikali ya cortisol ambayo inachangia uzeekaji wa ngozi.

Utafiti: Pombe ni Chazo Cha Ugonjwa wa Saratani

$
0
0
Watafiti wa afya kupitia jarida la Addiction wamedai kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya unywaji wa pombe na aina saba za saratani.
Aidha wataalamu hao wamegundua kuwa saratani ambazo imegunduliwa zina uhusiano mkubwa na unywaji pombe ni pamoja na saratani ya mdomo na koo, saratani ya kikoromeo, saratani ya ini, saratani ya utumbo mpana, saratani ya matumbo na saratani ya matiti.
Aidha mwezi Januari mwaka huu, afisa mkuu wa afya kutoka nchini Uingereza alitoa tahadhari kuwa unywaji wa pombe kwa kiwango chochote kile kina madhara ndani ya mwili.
Mpaka sasa watu zaidi ya laki tano wanakadiriwa kufa kutokan ana ugonjwa wa saratani kwa mwaka 2012 pekee. Hata hivyo mpaka sasa bado haijabainika kibaiolojia uhusiano wa pombe na saratani inatokeaje


Chanzo: Bongo5

DEAL DONE: Pogba Avunja Rekodi ya Uhamisho wa Dunia

$
0
0
WAZUNGU wanasema kwa Kiingereza chao, Deal done. Yaani biashara imekwishamalizika. Watu wananyanyuka katika viti vyao, wanapeana mikono, wanakumbatiana, wanaondoka. Uhamisho wa Paul Pogba inasemekana umemalizika.

Manchester United imefanikiwa kumnasa kiungo huyo mahiri wa Juventus kwa dau la Pauni 100 milioni ambalo litaweka rekodi mpya ya uhamisho duniani na kulipiku dau la Pauni 85 milioni ambalo Real Madrid walilipa mwaka 2013 kumchukua Gareth Bale kutoka Tottenham.

Licha ya kulipa dau hilo, United watamlipa Pogba mshahara wa pauni 210,000 kwa wiki kwa mkataba wa miaka mitano ikiwa ni miaka minne tangu alipomruhusu kuondoka bure kwenda Juventus Julai 2012 akiwa mchezaji kinda.

Bosi wa Man United, Ed Woodward alikacha kwenda katika ziara ya United nchini China na alikutana na Wakurugenzi wa Juventus, Giuseppe Marotta na Fabio Paratici, pamoja na wakala wa Pogba, Mino Raiola kwa ajili ya kumaliza dili hilo.

Juventus iling’ang’ania dau hilo licha ya Man United kujaribu kushusha, lakini mwishowe Man United imekubali kulipa dau hilo kwa staa huyo mwenye umri wa miaka 23 ambaye amezaliwa nchini Ufaransa na wazazi wake waliotokea Guinea barani Afrika.

Kocha wa Man United, Jose Mourinho alikuwa anamtaka staa huyo kabla ya pambano la ngao la hisani kati yao na Leicester City Agosti 7 na atajiunga nao mara baada ya timu hiyo kurejea katika ziara ya maandalizi ya msimu mpya nchini China ambako wametua juzi.

Pogba aliondoka Old Trafford katika utawala wa kocha mkongwe, Sir Alex Ferguson baada kushindwa kuhakikishiwa nafasi katika kikosi cha kwanza kilichokuwa kimesheheni mastaa wakongwe kama Paul Scholes ambaye Ferguson hakutaka kumuweka benchi na alimuamini zaidi.

Tangu hapo, Pogba ameibuka kuwa mmoja kati ya viungo bora barani Ulaya huku akiiwezesha Juventus kutwaa ubingwa wa Serie A mara nne, akiifikisha pia katika fainali za Ulaya pamoja na kuipeleka Ufaransa katika fainali za Euro 2016 ambapo walichapwa 1-0 na Ureno.

Mfaransa huyo atakuwa mchezaji wa nne kusajiliwa na Man United dhini ya Mourinho baada ya kuwanasa Eric Bailly kutoka Villarreal, Zlatan Ibrahimovic aliyenaswa bure kutoka PSG na Henrikh Mhkitaryan aliyechukuliwa kutoka Borussia Dortmund.

Wakati dau la Pogba likianza kulalamikiwa na wadau wengi wa soka kwamba haliendani na kiwango chake, tayari nyota huyo ameanza kupata watetezi akiwemo staa wa zamani wa Arsenal na timu ya taifa ya Ufaransa, Thierry Henry.

“Sahau kuhusu Ufaransa, nadhani anaweza kuwa mmoja kati ya viungo bora katika historia. Ana ubora wa kufanya hivyo. Anahitaji kuwa makini tu na kitu anachoweza kukifanya vizuri.” Alisema Henry katika michuano ya Euro.

Koffi Olomide Akamatwa na Kuzuiliwa Nairobi....

$
0
0
Mwanamuziki mashuhuri kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Koffi Olomide amekamatwa na kuzuiliwa na maafisa wa polisi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta.
Olomide amekamatwa muda mfupi baada ya kumaliza mahojiano katika kituo kimoja cha runinga jijini Nairobi.

Mkuu wa polisi nchini Kenya Joseph Boinnet alikuwa ametoa taarifa na kuwaagiza polisi wachukue hatua.

Mwanamuziki huyo alikuwa amekabiliwa na shutuma baada ya kanda ya video kuenea mtandaoni ikionekana kumuonyesha akimshambulia mwanamke uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta Ijumaa asubuhi, muda mfupi baada ya kuwasili.

Mwanamke huyo anadaiwa kuwa mmoja wa wachezaji ngoma wake.

Akiongea katika kituo cha televisheni ya Citizen, muda mfupi kabla ya kukamatwa, Olomide alijitetea na kusema hakukusudia kumshambulia mwanamke huyo.

Alisema alikuwa ameingilia kisa ambacho aliamini ni mtu aliyetaka kumpokonya mmoja wa wachezaji densi wake pochi yake au kulikuwa na vurugu fulani.
Awali, kwenye ujumbe katika ukurasa wake wa Facebook, alisema tukio hilo lilieleweka vibaya.

Alisema alikuwa anajaribu kumtetea mwanamke huyo kwani mmoja wa maafisa wa kike katika uwanja huo wa ndege alikuwa akiwasumbua wasichana hao wachezaji ngoma aliokuwa wakiandamana naye.

Katika video hiyo msichana huyo mchezaji anaonekana kukubaliana naye.
Mwanamuziki huyo, alikuwa amepangiwa kutumbuiza mashabiki katika ukumbi wa Bomas siku ya Jumamosi.

Baada ya kuenea kwa habari kuhusu kisa hicho cha uwanja wa ndege, wengi wa Wakenya wamemshutumu na kutoa wito kwao watu kutohudhuria tamasha hilo na badala yake wakitaka akamatwe.

Wengine kupitia kitambulisha mada #KickKoffiOlomideBackToCongo kwenye Twitter wakipendekeza afurushwe kutoka Kenya.

Mo Dewji Aamua Kugawa Nusu ya Mali zake

$
0
0
MKURUGENZI Mtendaji wa makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (METL Group), Mohammed Dewji, ameungana na matajiri wakubwa duniani, kutangaza azma ya kugawa nusu ya mali zake kusaidia jamii.

Taarifa kutoka mtandao mashuhuri duniani wa Forbes, imesema kuwa Dewji, ambaye ni bilionea kijana kuliko wote barani Afrika, ameingia katika kundi la matajiri hao ambao wametoa ahadi ya kutoa nusu ya mali zao, kusaidia jamii.

“Baada ya kushuhudia umasikini mkali wakati nikilelewa, siku zote nimekuwa nikijisikia kuwajibika kutoa kwa ajili ya jamii yangu,” amesema Dewji katika barua yake ya kutangaza ahadi hiyo, ambayo ameiweka wazi kwa waandishi wa habari.

Alishukuru wazazi wake kwa kumuunga mkono na kumjengea moyo wa kusaidia jamii na kipekee katika wajibu wake kwa dini yake ya Uislamu wa kutoa na kujali wahitaji na jamii.

Bilionea huyo anakuwa Mtanzania wa kwanza kuungana na matajiri duniani, Bill Gates na Warren Buffett katika kutangaza nia hiyo tangu 2010 na kushauri watu wengine wenye uwezo kujitolea kwa ajili ya jamii.

Kundi la matajiri waliokwisha kutangaza nia hiyo ya kutoa sehemu ya mali zao kwa jamii, limeshafikia 155 kutoka nchi 17, ambapo Juni mwaka huu, kundi hilo linalotambuliwa kwa jina The Giving Pledge, lilitangaza kupata wajumbe wapya 17.

Wajumbe wa mwanzo wa kundi hilo ni pamoja na Eli Broad na mkewe Edythe, John Doerr na mkewe Ann pamoja na mmoja wa wamiliki wa Facebook, Mark Zuckerberg na mkewe, Priscilla Chan.

Mtandao mashuhuri wa Forbes, umemkadiria Dewji kuwa anamiliki mali zenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 1.1, akiongoza kundi la makampuni ya METL nchini Tanzania, linalojihusisha na biashara za viwanda vya nguo, vinu vya unga na viwanda vya mafuta ya kula, huku kinywaji chake cha Mo Cola, kikiuzwa bei rahisi kuliko kununua Coca-Cola.

KAULI ya Diamond Kwa Mtoto Wake "Ukikua Chonde Mama Ukitunze Wasikile Sana" Yazua Maneno

$
0
0
Diamond Platnumz si mgeni kwenye jumbe tata kwenye mitandao ya kijamii.

Lakini ujumbe wake mpya kwa bintiye, Tiffah umesababisha mjadala mkubwa.

Akiweka picha ya binti yake huyo ambaye mwezi ujao anatimiza mwaka mmoja, Diamond aliandika: Buff day Girl! my little Pumpkin😍 My Miss World 👸 @princess_tiffah kua mama, nikupe Raha ya Dunia na ujifaidie Ustar wako….. ila dah ukikua chonde mama ukitunze wasikile sana #KIDOGO tu, Maana ntalificha wapi hili sura langu.”

Maneno: Ukikua chonde mama ukitunze wasikile sana #KIDOGO tu’ ndiyo yaliyosababisha povu la haja.

Hizi ni baadhi ya comments:

Twinsrebeccita: Hivi mtoto hajafikisha hata miaka miwili ushaanza kufikiria masuala yake ya ngono!!!! Maneno ya bure kwako, usitumie utupu wa mwanao kutangaza biashara yako.

Precioushamis: Mungu auTunze usichana wako /ujana wako tiffah, kinywa cha baba yako kishindwe kwa jina la yesu amina

Jahmolbiggz: Daym 😁 did u just wrote that? Any real Dad out there won’t even think of writing such words to her dota.. Shit is Crazy

Madimwashiti: @princess_tiffah never follow your parents foot steps. U need more prayer. @diamondplatnumz better pray for this little girl coz what goes around comes around. Many many little SIMBAS out there want spare you dear. That is my own thoughts. Think about it NASSEB

Neyesu Daniel: Diamond ww sio baba mwema! Utaanzaje kumwambia bint ako ivo!? Umenikera mbna unakosa madil ya kiafrika?? Acha izo bna kama ww una njia ambazo si nzur bc mfunze mwanao akue vema!

Rajabu Mussa: Tena atakua amefuata Tabia Za Huku na huku(kwa maza n baba) maana kote kote hakuna mwenye afazali…….ukila nawe utaliwaaaaa japo #Kidogo

Tuzo Hella: Atii aliwe kidogooo!!! Labda wakati anaandika hiyo post hakuwa poa!!alionja kidogo ile kitu ya Arusha inarushanga akili,coz diamond hukogi na akili mingi sasa alifikiri nn kuandika hayo maneno hayo!!eti mtt akulwe kidogo kweliii!!!! D your not serious

Unaounaje ujumbe huo?

Marufuku ya Mafuta ya Kulainisha KY Jelly yazua Mjadala

$
0
0
Mjadala mkali umeendelea nchini Tanzania Kufuatia waziri wa afya wa nchi hiyo kupiga marufuku utumiaji na usambazaji wa vilainishi vinavyotumiwa na wapenzi wa jinsia moja.

Waziri huyo wa Afya Ummy Mwalimu hapo juzi alitanganza kupiga marufuku vilainishi hivyo kwa madai kwamba vimekuwa vikitumiwa vibaya na wapenzi wa jinsia moja na hivyo kusababisha kuenea kwa maambukizi ya virusi vya Ukimwi.

Hata hivyo muda mfupi baada ya marufuku hiyo raia wa nchi hiyo walikuwa maoni tofauti.
Mjadala huu uliibuka siku chache baada ya kauli ya hiyo ya waziri wa Afya wa Tanzania Ummy Mwalimu alipozungumza na waandishi wa habari kuthibitisha kuzuiwa usambazaji wa vilainishi hivyo akidai kuwa inatumika kwa namna ambayo sio sahihi.

Wananchi wa nchi hiyo wengi wanataka suala hilo kujadiliwa kwa upana na serikali ifahamu wapi penye tatizo ili liweze kutatuliwa.

Vilainishi hivi vinavyotajwa kuwa chanzo cha maambukizi ya virusi vya Ukimwi kwa kuhusishwa zaidi na watu wa mapenzi ya jinsia moja.

Hata hivyo,Wataalam wa masuala ya afya wanathibitisha kuwa yapo matumizi mengi yatokanayo na vilainishi hivi iwapo vitatumika ipasavyo.

Man United yapewa kipigo cha kwanza chini Mourinho..Mwenye Atatea Timu yake

$
0
0
Jose Mourinho amesisitiza kwamba hawezi kujaji wachezaji wake wa Manchester United kutokana na kipigo cha mabao 4-1 walichokipata kutoka kwa  Borussia Dortmund na kusema kwamba: “Injini ilikuwepo ilikuwa ni tofauti kabisa, iliku ni kati ya Formula One against Formula Three”

“Mawazo yangu ni rahisi mno,” alisema Mourinho. “Najua kwamba wakati huu wa pre-season timu ambayo iko vizuri kwenye maandalizi lazima iwe vizuri zaidi ya rimu nyingine.”

“Hii hutokea kila mwaka. Baadhi ya timu bora hupoteza kwa magoli mengi. Nadhani hili lipo wazi kabisa. Baada ya dakika 10, tulianza kujua kwamba timu moja ilianza mazoezi siku 10 zilizopita na kucheza mchezo mmoja na nyingine ilianza mwezi mmoja uliopita na imeshacheza michezo minne. Ni rahisi mno kuona kuona utofauti wa ugumu wa mchezo na umakini wa wachezi. Kwa upande wetu ulikuwa ni mchezo mgumu sana.

Kipindi cha pili tulikuwa wazuri na kuuzoea zaidi mchezo. Nadhani matokeo ya mabao 3-2 yangekuwa sahihi zaidi ya 4-1 lakini Dortmund walionesha ubora mkubwa waliokuwa nao, kwa mchezaji mmoja-mmoja na timu nzima. Walionesha kwamba walikuwa wameshapiga hatua kubwa kwenye mazoezi zaidi yetu.

Alipoulizwa kama angewajaji wachezaji wake kutokana na mchezo ule, Mourinho akajibu: “Mimi nadhani ni muunganiko wa sababu vitu mbalimbali. Lakini kwa kuzungumzia uhalisia wenyewe, sidhani kama naweza kuwafanyia tathmini ilhali kulikuwa na utofauti mkubwa kati ya timu hizi. Kwa sasa injini zina utofauti mkubwa. Formula One dhidi ya Formular Three.

‘Kwa sasa, wapo vizuri zaidi na unaweza kuona hilo kirahisi zaidi, hivyo ni vigumu sana kuwajaji wachezaji wangu. Hata kwenye masuala kama haya, unaweza kupata wachezaji watatu, wanne au watano. Vinginevyo ni vigumu sana japo unaweza kuona ubora uliopo.”
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live




Latest Images