Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104689 articles
Browse latest View live

DAR: Askari wa Usalama barabarani (Trafiki) auawa kwa kupigwa risasi

$
0
0

Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Sajenti Mensah wa Kituo cha Polisi Oysterbay ameuawa usiku huu kwa kupigwa risasi akiwa kazini eneo la Sayansi Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Christopher Fuime amesema tukio hilo lilitokea majira ya saa mbili usiku huu na chanzo cha mauaji hayo hakijafahamika.

“Tukipata chanzo itakuwa tayari upelelezi wetu umetimia, hivyo kwa sasa tunalifanyia kazi ili kubaini wahusika wa mauaji hayo,” amesema Fuime.


Uamuzi wa Bodi ya Mikopo kuhusu Wanafunzi ambao hawajarejesha mikopo yao hadi leo

$
0
0
Mnamo mwezi Machi, 2016, Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu ilitoa notisi ya siku 60 ikiwataka wanufaika wa mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu kujitokeza na kuanza kurejesha mikopo yao.

Aidha, taarifa hiyo pia iliwataka waajiri kuwasilisha taarifa za waajiriwa wao na makato ya marejesho.  Baada ya kipindi hicho kumalizika, kipindi cha notisi hiyo kiliongezwa ambacho pia kimekwisha.

Kufuatia hatua hiyo, Bodi inapenda kuwataarifu wanufaika wote wa mikopo kwamba kuanzia wiki ijayo itaanza kutangaza majina ya wale wote ambao hawajaweza kujitokeza na kuanza kurejesha mikopo yao.

Zoezi hili litajumuisha pia waajiri ambao hawajawasilisha taarifa za waajiriwa wao.  Hatua hiyo itafuatiwa na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wale wote watakaoshindwa kutimiza matakwa hayo kwa mujibu wa kifungu cha 19A (1) cha sheria Na. 9 ya mwaka 2004.

Hivyo basi, wanufaika wa mikopo wanahimizwa kuanza kulipa madeni yao na waajiri kuwasilisha taarifa za waajiriwa au kufika kwenye ofisi za Bodi ya Mikopo ili kupata Ankara za madeni yao kabla ya zoezi la kutangaza majina halijafanyika. Marejesho yanaweza kufanyika kupitia Akaunti:

A/C No. 2011100205 – NMB

A/C No. 01J1028467503 – CRDB

A/C No. CCA0240000032 – TPB

Ni muhimu kuzingatia taarifa hii ili kuepuka usumbufu utakaojitokeza kutokana na hatua zitakazochukuliwa.

Imetolewa na:
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu

Vigogo wote Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) Watumbuliwa MAJIPU

$
0
0
SERIKALI imemuondoa katika nafasi yake Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS), Gerald Kamwenda na wakurugenzi wenzake, katika jitihada za kufumua na kusuka upya shirika hilo.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, ametangaza hatua hiyo ya serikali jana alipokutana na vyombo vya habari na kuongeza kuwa, watumishi wengine 41 wamehamishwa vituo vya kazi.

Alifafanua kuwa hatua hizo ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, lililotaka kufumuliwa na kusukwa upya kwa TFS ili kuongeza ufanisi.

Kutokana na hatua hiyo, Waziri Maghembe alisema Profesa Dos Santos Silayo ameteuliwa kuwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa TFS, wakati Kamwenda anahamishiwa Chuo cha Viwanda vya Misitu kilichopo Moshi.

Aidha, Mwanaidi Kijazi aliyekuwa Mkurugenzi wa Usimamizi wa Raslimali za Misitu na Nyuki, yeye amekwenda kuwa Mhifadhi Mkuu Amani Nature Reserve na nafasi yake inachukuliwa na Zawadi Mbwambo.

Waziri Maghembe alisema Mohamed Kilongo aliyesimamishwa kazi Januari 5, mwaka huu uchunguzi umeonekana hana hatia na hivyo anaendelea kuwa Mkurugenzi Mipango na Matumizi Endelevu ya Rasilimali za Misitu.

Alisema Wizara imeamua Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Gladnes Mkamba ahamishiwe Idara ya Mipango makao makuu na nafasi hiyo kuteuliwa Dk Ezekiel Mwakalukwa, kuwa Kaimu Mkurugenzi.

Aidha Monica Kagya aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Ufugaji Nyuki, anakuwa Mtafiti Mwandamizi Idara ya Nyuki (Tawiri). Alisema Kagya ni mtaalamu wa masuala ya nyuki, hivyo atahamishiwa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori, ili ashughulikie utafiti wa masuala ya nyuki.

Pia alisema katika Idara ya Wanyamapori, Profesa Alexander Songorwa anakuwa Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, nafasi ambayo ilikuwa ikishikiliwa na Herman Kerayo ambaye anahamishiwa Idara ya Mipango Makao Makuu.

Profesa Ramadhan Kideghesho, yeye anakwenda kuwa Mkuu wa Chuo cha Mweka wakati Mabula Misungwi aliyekuwa Meneja Mradi Selous, anakwenda Chuo cha Wanyamapori Pasiansi na nafasi yake inachukuliwa na Jaffary Lyimo, huku Robert Mande akipelekwa kuwa Kaimu Mkurugenzi msaidizi Uzuiaji Ujangili.

Waziri Maghembe alisema Majjid Ally ameteuliwa kuwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Leseni, nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Haji Mpya ambaye amehamishiwa Shamba Jipya Songea kuwa Ofisa Misitu Alisema Julai 18, mwaka huu Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikutana na viongozi na watumishi wa Wizara hiyo na watendaji wakuu na watumishi wa TFS na kuagiza kufumuliwa na kusukwa upya kwa wakala huo.

Katika mkutano huo, Waziri Mkuu alitaka kuondolewa kwa utitiri wa vituo vya ukaguzi na kuwekwa vituo vichache na kuondolewa kwa ofisi za makontena yanayotumiwa na ofisi ya TFS, badala yake watumishi wanaofanya ukaguzi wasimame mahali pa wazi ili kuondoa mianya ya rushwa na kuweka uwazi katika utendaji.

Vyeti ni gonjwa kwa watumishi, wengi wahaha kutangaza vimepotea

$
0
0
Wakati serikali ikiendelea kuhakikisha vyeti kubaini watumishi wasiokuwa na sifa, watu wengi wamejitokeza kutangaza kupotelewa na vyeti magazetini

Katika kipindi ambacho taasisi mbalimbali zinaendelea na zoezi hilo imebainika kuwa siku za nyuma kulikuwa na matangazo ya aina tofauti lakini kwa juzi kumetokea mtiririko wa watu kutangaza kupotelewa na vyeti hali isiyo ya kawaida kwa taifa.

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia na Ufundi , Profesa Joyce Ndalichako alisema juzi kuwa serikali itafanya uhakiki wa vyeti katika vyuo na sehemu za kazi.

Naye Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF)Godius Kahyarara juzi alitoa waraka akisema wafanyakazi watakaoshindwa kuwasilisha vyeti vyao halisi hawatalipwa mishahara.

JK: Haikuwa rahisi kumshawishi JPM kuwa Mwenyekiti wa CCM

$
0
0
Mwenyekiti wa CCM anayemaliza muda wake anasema kuwa alitumia kila aina ya ushawishi ili Magufuli akubali kumpokea kijiti kabla ya Novemba 2017. Anasema kuwa alimuendea Ikulu kumshawishi ampokee kijiti. Hata hivyo, Rais Magufuli alimjibu kuwa ana mambo mengi ya kushughulikia ndani ya CCM hivyo haoni kuwa ni muda muafaka wa yeye kubeba dhamana ya kuwa Mwenyekiti wa CCM. Kikwete anasema kuwa pamoja na maelezo yake ya kina, hakika Magufuli hakukubali kubeba dhamana hiyo. Mwisho na kwa lengo la kukata mazungumzo hayo, Rais Magufuli alimkaribisha ugali na hivyo jitihada zake zikagonga mwamba.

Anasema kuwa kutokana na hali hiyo, alimtuma Makamu Mwenyekiti Philip Mangula akamshawishi Rais kwani uzee ni dawa. Baada ya mwezi na nusu, Mangula akarudisha jibu kuwa Rais amekubali kuwa Mwenyekiti wa CCM na ndipo tarehe ikapangwa.

Kikwete anasema kuwa hata yeye alimkatalia mzee Mkapa mwaka 2006 kwa sababu kama hizo hizo ambazo. Hata hivyo anasema kuwa tofauti na 2006 ambapo hakukuwa na magazeti chonganishi na mitandao ya kijamii, mwaka huu wamemtungia uongo kuwa eti yeye anang’ang’ania madaraka na kwamba hataki kumkabidhi madaraka Magufuli. Shabaha yao ni kuchochea mfarakano na baada ya kuona CCM ni moja. Anawaomba wana CCM kuwa wamoja kwa vile wapinzani wao kila wanachokamata hakikamatiki.

Anasema kuwa kama angekuwa hataki kuachia nafasi, baada ya awali Rais kusema kuwa hana haraka ya kuwa mwenyekiti wa CCM, asingemtuma mzee Mangula. Aliamua kumtuma mzee Mangula kutokana na umuhimu wa kofia mbili kwa chama na serikali. Anasema kuwa mfumo huu wa kofia mbili una faida kubwa kwa chama na walioasisi mfumo huu waliona mbali. Anasema kuwa yeye hakutaka guu lake liote tende kwa kufanya maamuzi ya kutenganisha kofia.

Koffi Olomide deported following JKIA assault

$
0
0
Congolese musician Koffi Olomide has been deported to Kinshasa, DR Congo following his Friday morning altercation at the Jomo Kenyatta International Airport (JKIA).

Olomide was filmed attacking one of his female dancers at the airport – an incident that lead to his arrest at Royal Media Services following a live TV interview where he denied assaulting his dancer.

Olomide was expected to headline a mega show at the Bomas of Kenya on Saturday. Citizen Digital reached out to event promoters following Olomide’s deportation, but they refused to comment on the issue.

This comes just hours after Nairobi Police Boss Japheth Koome said police have launched an investigation into the incident.

On Friday night, Gender Cabinet Secretary Sicily Kariuki called for the immediate deportation of the Congolese artist over the incident.

“Kenya does not condone dehumanizing acts against women. We hope that this action will be a lesson to him and others of his ilk that gender based violence will not be tolerated and all who engage in such archaic behavior will face the full force of the law regardless of their economic stature and economic standing,” Kariuki’s statement read.

HILLARY Clinton amteua Tim Kaine kuwa mgombea mwenza

$
0
0
Mgombea Urais wa Marekani kupitia chama cha Democratic Hillary Clinton amemteuwa Seneta Tim Kaine, kutoka Virginia kuwa mgombea wake mwenza katika uchaguzi mkuu utakaofanyika nchini humo tarehe 8 Novemba.

Bi Clinton alitangaza uteuzi huo kupitia akaunti yake ya Twitter akimtaja mgombea mwenza huyo kuwa ni mfuasi mkubwa wa makubaliano huru ya biashara na anatarajia kumtambulisha rasmi leo katika mkutano wa hadhara huko Miami.

Kaine ambaye anaongea kihispania vizuri anatarajia kuwavutia wapiga kura wamarekani wenye asili ya Uhispania kundi ambalo ni kubwa katika chaguzi za Marekani.

Mtazame Shilole Akiongea Kingereza na Mwalimu Wake

$
0
0
Lugha ya Kingereza imekuwa shida sana kwa wasanii wengi hapa Bongo lakini mwanadada mrembo Shilole ameamua kuweka aibu pembeni na kujifunza lugha hiyo huko akifanya mizaa kupitia mdandao wa Instagram

Mtanzame Hapa Akiongea na Mwalimu wake kwa simu:


Mzee Makamba: Mchungaji Gwajima anayo laana ya kumtukana Kardinali Pengo

$
0
0
Mzee Makamba anadai kuwa Mchungaji Gwajima anayo laana ya kumtukana Kardinali Pengo. Na kwa tafsiri ya kiafrika mtu mwenye laana siku zote hufanana na mtu aliyechanganyikiwa. Ayafanyayo huwa kituko kwa wanaomzunguka, huwafanya watu waingiwe na huruma.

Lakini naamini lengo la Mzee Makamba kumsema Askofu Gwajima ni kumuongezea uadui miongoni mwa wanajamii kwa kuanzia na watu wanaosali kwake. Lengo jingine ni kumchongea kwa Mwenyekiti Mtarajiwa wa CCM.

Kama CCM itamrudisha Kinana, Mapungufu ya Mashinji wa CHADEMA sasa Kuonekana Dhahiri

$
0
0
Ni muda sasa kumekua na fukuto kutoka kwa wana CCM wakitilia shaka utendaji kazi wa Mashinji jambo ambalo tumekua tukilipuuza na nakulipinga aidha kwa makusudi ama tukifahamu kinachosemwa ni kweli ila tumeamua kupinga tu.

Ni kweli kwamba adui hawezi kukueleza udhaifu wako lakini si wakati wote kwani kinachotokea sasa ni chama kuchekwa kwa makosa ya kumteua mtu ambaye anapolinganishwa na Dr Slaa anaonekana kupungukiwa na vingi sana kisiasa.

Licha ya kua tunapinga ila mpaka sasa sisi kama chama bado hutajampata mrithi wakufanana na Dr Slaa hivyo kujikuta kwa sasa chama kinakosa mbinu na mikakati yakujipambanua nakujitangaza kwa wananchi.

Kama CCM watamrudisha Kinana kwenye nafasi yake hapo ndipo tutaacha ubishi kwani kwa uzoefu na mikakati aliokua nayo Kinana ni muda mfupi sana hakuna atakae bisha tena juu ya kupwaya kwa Mashinji.

Mrema Atoa Mpya 'Nawashangaa Wapinzani Mnavyozira Ovyo, Kwetu Anayezira no Mwanamke, Wanaume Gani Nyie?'

$
0
0

Mrema Afunguka:
"Tarehe 16 Saa mbili asubuhi nilipigiwa simu na Rais Magufuli akanambia anataka kunipa kazi sikuamini, wala Mimi sikukataa kataa kama nikasema na iwe utakavyo Rais, Mbatia na wenzake walinichangia kama Mpira wa kona mwaka Jana, nashangaa wapinzani mnavyozira ovyo!! Kule kwetu Vunjo anayezira ni Mwanamke, nyie mnakimbia yule mama Bungeni ni Wanaume gani Nyie??" Mrema

#MkutanoWaCCMDodoma kumpata mwenyekiti.

Jakaya Kikwete: Mtu uliwahi kuwa Waziri Mkuu, sasa unagombea Uenyekiti wa Wilaya ya Kibaha

$
0
0
Mwenyekiti anayestafu wa CCM naona katupa jiwe gizani kwa Sumaye. Baada ya kushangazwa na hatua yake ya kugombea uenyekiti wa wilaya Kibaha (Chadema) huku aliwahi kuwa waziri Mkuu..

Je Una Maoni gani?

Breaking News: Rais Magufuli Achaguliwa Rasmi Kuwa Mwenyekiti wa CCM

$
0
0

Katika Mkutano Mkuu wa CCM unaoendelea leo mjini Dodoma, CCM wamemchagua Rais John Pombe Magufuli kuwa Mwenyekiti wa tano wa Chama cha Mapinduzi.....

Sentensi Tano za Yusuph Makamba Kwenye Mkutano Mkuu wa CCM

$
0
0
Leo July 23 2016  Mjini Dodoma unafanyika mkutano mkuu maalum wa CCM ambao ajenda yake kubwa ni ya kumchagua Rais Dk. John Magufuli kuwa mwenyekiti wa tano wa chama cha Mapinduzi ‘CCM’. Baada ya hotuba ya Mwenyekiti wa chama hicho Jakaya Kikwete, katibu mkuu mstaafu Yusuph Makamba alipata nafasi ya kuzungumza na kusema haya……

'Askofu Gwajima alisema uongo kwamba Jakaya Kikwete hakutaka kumpisha Magufuli kuwa mwenyekiti' - Yusufu Makamba #MkutanoMkuuCCM
'Chama kinatoka mikononi mwa kada anayekataa ufisadi kiasi cha kumtosa rafiki yake Lowassa'- Yusuph Makamba #MkutanoMkuuCCM
'Chama kinakwenda mikononi mwa muasisi wa Mahakama ya mafisadi'-Yusuph Makamba #MkutanoMkuuCCM
'Wapinzani nataka mjue JK alikuwa anawabatiza kwa maji huyu ajaye atawabatiza kwa moto'-Yusuph Makamba #MkutanoMkuuCCM
'Rais Magufuli hakukataa ushauri alikataa vimemo kikiwemo cha kwangu, kuna mtu nilikuwa nampigia debe awe DC'-Yusuph Makamba #MkutanoMkuuCCM

Magufuli Amteua Kinana Kuwa Katibu Mkuu CCM Licha ya Kuomba Kujiuzulu

$
0
0

Mwenyekiti mpya wa CCM Dkt. John Pombe Magufuli amemteua ndugu Abdulrahman Kinana kuendelea na nafasi yake ya Katibu Mkuu wa chama hicho, licha ya Kinana kuomba kujiuzulu nafasi hiyo

Nini maoni yako kuhusu uamuzi huo?

Zitto Kabwe afunguka haya baada ya Rais Magufuli kukabidhiwa uenyekiti wa CCM

$
0
0

Leo July 23 2016  Rais John Pombe Magufuli amekabidhiwa rasmi nafasi ya uenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM   baada ya kupigiwa kura za ndio 2398  kutoka kwa wanachama wa chama hicho ambapo hakuna kura hata moja ya hapana wala iliyoharibika

Baadhi ya viongozi wakiwemo wa vyama vya upinzania walishiri akiwemo mwenyekiti wa TLP Augustino Mrema, lakini wapo pia waliotamani kufikisha hisia zao kuhusu tukio hilo na mmojawapo ni mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe kupitia account yake ya facebook aliandika maneno haya…

>>’Napenda kumpongeza Rais John Magufuli kwa kuchaguliwa kwake kuwa Kiongozi wa Chama chake cha CCM akiwa Mwenyekiti wa Tano chama hicho. CCM imeendelea kudumisha utamaduni wa kukabidhiana Uongozi kila baada ya muda‘

‘Jambo ambalo ni la kujifunza hasa kwa vyama vya Siasa nchini na barani Afrika. Nataraji kwamba Rais na Mwenyekiti mpya wa CCM ataona umuhimu wa Vyama vya Siasa kuendelea kufanya Siasa bila vikwazo na kwa mujibu wa Sheria za Nchi yetu.’ –Zitto Kabwe

‘Demokrasia inaimarisha Amani kwa kupaza sauti za HAKI. Karibu kwenye changamoto za kuongoza Vyama vya Siasa ndugu Rais.‘ –Zitto Kabwe

Kikwete amkabidhi Magufuli 'majipu' ndani ya CCM

$
0
0

Mwenyekiti mstaafu wa CCM Dkt Jakaya Kikwete, amekabidhi nafasi ya uenyekiti wa chama hicho kwa Dkt John Pombe Magufuli, huku akimtaka kushughulikia baadhi ya mapungufu yanayokitia hasara chama ikiwemo kuokoa mali za chama.

Kikwete ambaye pia ni Rais Mstaafu wa Tanzania, ametoa hotuba yake ya mwisho kama mwenyekiti wa chama hicho leo katika mkutano mkuu maalum uliofanyika mjini Dodoma, na kutoa onyo kwa watu wote wanaoshikilia mali za chama kwa manufaa yao binafsi.

Akitaja baadhi ya mali hizo, Jakaya Kikwete amesema kuna wanachama ambao wamejimilikisha viwanja vya chama hicho bila utaratibu rasmi na kuwapa tahadhari ya kuvirejesha katika chama haraka.

Amemtaka mwenyekiti mpya mpya wa chama hicho kushughulikia suala la viwanja ambavyo bado havijapewa hati ili viendelezwe na kugeuzwa kuwa vitega uchumi na kuongeza wigo wa mapato ya chama.

“Mkoa wa Dar es salaam pekee una viwanja 279 lakini ni 45 pekee ndivyo vina hati angalau UVCCM wanajitahidi kujenga majengo ya vitega uchumi na kuna wazee wengine wa chama wameamua kujimilikisha viwanja vya chama, sisemi kwamba ni MAJIPU hapana, nawakumbusha ili viwanja hivyo viendelezwe, chama kipate mapato”
Aidha Kikwete amewakumbusha wakuu wa wilaya kuwa wanapaswa kutambua mojawapo ya jukumu walilonalo ni kulinda maslahi ya chama katika ngazi ya wilaya.

“Kuna wakuu wa wilaya wamesema eti wao ni wasomi na kwamba siasa haiwahusu, lakini wajue kuwa wao ni wajumbe wa kamati za siasa za wilaya, hivyo wajue kuwa wamewekwa kule kwa makusudi kama kiungo kati ya chama na serikali”
Amesisitiza kuwa ana imani kubwa kuwa Dkt Magufuli anatosha na ataweza kukisimamia vizuri chama hicho.

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya July 24

$
0
0


SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya July 24

Mwigizaji Jackline Wolper atangaza kuhama CHADEMA na kijiunga na CCM

$
0
0
Mwigizaji wa filamu nchini Tanzania Jackline Wolper aliyakuwa akimuunga mkono Edward Lowassa katika uchaguzi Mkuu 2015, ametangaza kujiunga na CCM rasmi jana

Wolper alikaribishwa na mwenyekiti aliyemaliza muda wake Dkt Jakaya Kikwete baada ya kutangaza kujiunga na CCM.

Kitendo hicho kilifanyika katika Mkutano Mkuu Maalum wa CCM uliofanyika jana Julai 23, mkoani Dodoma.

Wasanii Wamlilia Kikwete Walipokuwa Wakimuaga Kwa Kustaafu Uwenyekiti Wa Chama Cha Mapinduzi

$
0
0
Wasanii wa Bongo Movie na muziki wa kizazi kimpya wamesema watamkumbuka sana Mwenyekiti Mstaafu wa CCM, Jakaya Kikwete kwa msaada aliyowapatia kipiti cha utawala wake akiwa Rais na Mwenyekiti wa chama hicho.

Wasanii wameyasema hayo usiku wa kuamkia leo mjini Dodoma walipofanya tamasha la Usiku wa Wasanii kwa ajili ya kumuaga baada ya kustaafu rasmi uwenyekiti wa chama hicho na kumuachia uongozi Rais John Magufuli

Viewing all 104689 articles
Browse latest View live


Latest Images