Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104689 articles
Browse latest View live

Kambi ya Lowassa Yamfungukia Jack Wolper Baada ya Kuwageuka

$
0
0
Kambi ya aliyekuwa Mgombea Urais wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kwa tiketi ya Chadema, Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowasa imemfungukia muigizaji wa Bongo Movie, Jacqueline Wolper, siku chache tu baada ya kutangaza kurejea Chama Cha Mapinduzi (CCM) mjini Dodoma.

Wakizungumza na Risasi Mchanganyiko kwa nyakati tofauti juzi jijini Dar es Salaam, wasemaji wa kambi hiyo walisema alichokifanya Wolper ni utashi wake wa kisiasa, unatokana na hisia zake, ingawa pia walimsema kama mtu asiyefahamu misingi, sera, itikadi, imani wa ilani za Chadema.

Msemaji binafsi wa Lowasa, Aboubakary Liongo, aliliambia gazeti hili kuwa ni vigumu kwa kiongozi huyo kumzungumzia Wolper kwa sababu hakukuwahi kuwa na ‘connection’ ya moja kwa moja baina yao, isipokuwa msanii huyo alijiunga na wanamabadiliko kwa utashi wake mwenyewe.
“Mzee hawezi kumzungumzia, alikuja huku kama ambavyo vijana wengine wengi walikuja wakifuata mabadiliko, kama kuna wa kumzungumzia, labda ni viongozi wa chama kwa sababu operesheni zote zilizokuwa zikifanywa wakati ule, ziliratibiwa na chama.

“Wao ndiyo wanaweza kuwa na la kusema kuhusu yeye, ila ninachokiona mimi ni kuwa Wolper ni mtu mzima, mwenye akili timamu, alikuja kwa utashi wake na kama anaondoka, pia anafanya hivyo kwa utashi wake,” alisema Liongo, ambaye ni mtangazaji mwandamizi wa redio nchini.
Kwa upande wake, msemaji wa Chadema,  Tumaini Makene, alisema Wolper ni mtu asiye na msimamo, asiyeelewa misingi, ilani, sera wala itikadi za Chadema, ndiyo maana haelewi nini anafanya.

“Sisi tuko na watu wanaoishi kwa matendo, siasa ni maisha ya binadamu, mtu ‘siriaz’ anajua misingi, itikadi, falsafa, imani na ilani za chama chake, hawezi kuwa leo anaamini hivi kesho vile, ukiona mtu kama huyo, ujue hana msimamo, anayumbishwa na ni mtu anayefuata mkumbo,” alisema Makene.
Lowassa 2Aliyekuwa Mgombea Urais wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kwa tiketi ya Chadema, Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowasa

Msemaji huyo alitolea mfano wa vyama viwili vikubwa vya siasa nchini Marekani, Republican na Democrat, akidai waumini wa taasisi hizo mbili za kisiasa, ni watu wenye weledi wanaojua nini wanafuata, hivyo siyo rahisi kuona mtu akihama ovyo kutoka upande mmoja kwenda mwingine.
Wolper ambaye aliwahi kuwasuta waigizaji wenzake walioamua kujiunga na CCM kwenye kampeni za uchaguzi mkuu uliopita, akisema ni watu wasioitakia mema taifa kwa kushindwa kuungana ili kulikomboa, hivi karibuni alitangaza kurejea chama tawala, akisema anarudi nyumbani kwani alipotea njia.

“Nimerudi na sifikiri tena kugeuka nyuma, nimeona jinsi rais wetu anavyopigana na chama hiki kuwakomboa wanyonge na sasa hivi kina kasi ya ajabu na nitaendeleza niliyoyaacha,” alisema msanii huyo wakati wa hafla ya kumuaga Mwenyekiti Mstaafu wa CCM, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete mjini Dodoma.

Makonda aomba mkataba wa Machinga Complex kuvunjwa

$
0
0
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametoa rai kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene, kuvunja mkataba uliopo katika mradi wa Machinga Complex ili kuokoa fedha za wananchi zinazopotea kupitia mkataba huo.

Makonda alitoa rai hiyo jana jijini hapa alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu tathmini ya mkataba uliopo katika mradi huo baada ya Simbachawene kumkabidhiwa asimamia jengo.

Alisema mkataba uliopo kati ya Jiji na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) hauridhishi hivyo amemuomba waziri huyo kuuvunja mkataba huo na kuchukua eneo hilo kwa makubaliano ya kwamba Halmashauri ya Jiji walipwe kodi ya ardhi, jambo ambalo linaweza kufanyika kwa urahisi kupitia NSSF na Jiji kumiliki hisa kwa pamoja.

Makonda alisema shirika hilo liliingia mkataba wa mkopo wa Sh bilioni 10 na Jiji kwa kujenga jengo la Machinga Complex lenye ghorofa tano na ghorofa sita ili liweze kumudu idadi ya machinga 10,000 lakini hali halisi baada ya kulitembelea jengo lina ghorofa nne zinazobeba machinga 4,000 tu.

“Tulivyopitia mkataba tuligundua kuwa una mapungufu mengi na huenda ulisainiwa na watu ambao walipofushwa na rushwa na kukubali kupoteza haki za wanyonge,” alisema Makonda.

Alisema baada ya kupitia mkataba huo pia amebaini kuwa fedha za mikopo ziliongezeka kutoka Sh bilioni 12.14 za kwenye mkataba na kufikia Sh bilioni 12.7 ikiwa ni nyongeza ya Sh milioni 560, ambayo ilifanyika bila makubaliano yoyote kati ya mkopeshaji na mkopaji hali ambayo haimtendei haki mkopaji.

“Mei 25, 2010 walikabidhiwa jengo likiwa linadaiwa riba ya Sh bilioni saba hivyo siku ya kwanza ilikuwa tayari inadaiwa jumla ya Sh bilioni 19.7 na hadi kufikia Machi mwaka huu deni lilikuwa Sh bilioni 38 lakini mpaka sasa wamelipa Sh milioni 50,” alisema Makonda.

Alisema shirika hilo lilianza kudai riba kinyume na mkataba ambao unaeleza kuwa riba italipwa baada ya miaka miwili.

Alisema katika hali ya kushangaza shirika hilo halikutoa fedha za mradi kwa Jiji na badala yake kubadilishwa utaratibu wa kifungu kidogo cha mkataba namba 4.1 kwa kusema anayekukopesha ana jukumu la kuchukua fedha na kukutana na mshauri wa mradi pamoja na mjenzi na shirika kumlipa.

Aunt Ezekiel Akimbilia Gym Kunusuru Penzi

$
0
0
Staa wa filamu, Aunt Ezekiel aliye katika mapenzi na Dansa Moses Iyobo, ameamua kukimbilia gym kwa ajili ya kupunguza unene unaomuandama ili kulinusuru penzi lake.

Akizungumza na Za Motomoto News, Aunt amesema ameanza mazoezi ya nguvu kila asubuhi ili aweze kupunguza mwili aendane na mpenzi wake kwani mwili wake ni mkubwa kuliko wa mwenzie.
“Daah, nimeona nitapoteza penzi langu bure, nimekuwa mnene kumpita baby kitu ambacho siyo sawa, nilikuwa na kilo 87, hivi sasa nimepunguza kilo sita,” alisema.

Chanzo:GPL

AJALI: Basi la UDA Laigonga Treni Eneo la Gerezani - Kariakoo, Dar

$
0
0
Ajali mbaya sana imetokea jana Kariakoo Gerezani, watu sita wamepoteza maisha papo hapo akiwemo konda wa kampuni ya Uda dereva kakimbia baada ya basi hilo kugongana na Treni...Mungu awalaze mahali pema wote waliopoteza maisha

Mwanafunzi wa DUCE Achomwa Kisu Baada ya Kufumaniwa na Mpenzi wake

$
0
0
Ni wanafunzi wa mwaka wa tatu katika chuo kikuu UDSM college ya DUCE kilichopo Chang'ombe, ilikua Jumapili ya tarehe 24/7/2016.

Jamaa aliyefahamika kwa jina la Jimmy alimfumania mpenzi wake jina Leah (wanachuo wote) na mwanaume mwingine nyumbani kwa mwanamke baada ya hapo Jimmy akawa mpole na akarudi kwake then yule mwanamke akamfuata huko kwake kwa lengo la kuomba msamaha na ndipo jamaa akamchoma kisu cha tumbo na kumpiga na chupa kichwani.

Hadi sasa mwanamke yuko hospitali ya Temeke hoi na jamaa yake sasa yuko Chang'ombe kituo cha Polisi.

Jamani mapenzi yapo na wanawake ni wengi zaidi tupende kwa akili sio moyo huyu jamaa atajuta sana kwa uamuzi wake wa kukurupuka.

Mwendelezo wa ukaguzi vyeti umeingia taasisi ya TRA, Number Zinasomeka.

$
0
0
Mwendelezo wa ukaguzi vyeti umeingia taasisi ya TRA, Number Zinasomeka.

Chadema kutoa tamko zito Leo Ambalo Litarushwa na Vituo Vitatu vya TV

$
0
0
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), leo kinatarajia kulihutubia taifa kupitia vyombo vya habari vya ndani na nje kuhusu maazimio ya Kamati Kuu iliyoketi kwa siku nne mfululizo.

Maazimio hayo ambayo yanaitwa ‘mazito na makubwa’ kuwahi kutolewa na chama hicho katika siku za hivi karibuni, yanatarajiwa kuonyeshwa moja kwa moja na vituo vitatu vya runinga   nchini.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya chama hicho kimeeleza kuwa maazimio hayo ya Kamati Kuu yatatangazwa moja kwa moja kupitia baadhi ya vituo vya runinga  kutoa fursa kwa Watanzania kusikiliza maazimio hayo.

Kamati kuu ya Chadema imefanya kikao chake kwa siku nne mfululizo kikiwa kimeghubikwa na usiri mkubwa.

Taarifa ya chama hicho kwa vyombo vya habari jana, ilisema Kamati Kuu ilimaliza kikao chake cha siku nne jana na leo maazimio yake yatawekwa wazi kwa wananchi kupitia vyombo vya habari.

Taarifa hiyo iliyotolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Chadema, Tumaini Makene, ilisema kupitia mkutano huo yatatangazwa maazimio ya kikao hicho kilichohitimishwa    Dar es Salaam jana.

Taarifa hiyo ilisema Chadema kitatoa tamko zito la ukubwa wa aina yake.

“Licha ya mambo hayo chama kitatoa matamko mazito na makubwa ya aina yake ambayo hayajawahi kutolewa na chama chetu katika siku za karibuni."

Taarifa hiyo ilisema Kamati Kuu ilipokea taarifa ya kina juu ya masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na hali ya siasa nchini kwa sasa ambayo inatishia hali ya uchumi na ustawi wa jamii nzima kwa ujumla, hivyo taifa zima kuwa katika majaribu makubwa ya kukosa mwelekeo wa  uongozi.

“Kupitia mkutano huo, Chadema kitatoa mwelekeo wa hali ya nchi hasa wakati huu ambao taifa linaonekana kukosa dira ya uongozi kwa ajili ya ustawi wa Watanzania wote kwa ujumla” kilisema chanzo hicho ambacho hakikutaka kuwekwa wazi jina lake.

“Kupitia mkutano huo, chama kitazungumzia mipango ya kujiimarisha kuendelea kuwatumikia wananchi na kusimamia dira ya mabadiliko na uhuru wa kweli nchini,”alisema Makene.

Alipoulizwa kuhusu taarifa hizo, Makene alisema suala hilo halijathibitishwa rasmi kama mkutano huo   utaonyeshwa moja kwa moja katika runinga.

“Hata mahali utakapofanyika mkutano huo bado hapajajulikana, nitakupigia simu kesho asubuhi (leo) kukujulisha wapi tamko hilo litatolewa." Alisema

Makonda aibua ufisadi ujenzi Machinga Complex

$
0
0
TAARIFA YA MRADI WA MACHINGA COMPLEX

1.0 Utangulizi

Mnamo tarehe 19 Aprili, 2016 ofisi yangu ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ilipokea barua ya agizo la waziri wa nchi TAMISEMI juu ya kusimamia uendeshaji wa mradi wa Machinga Complex. Ambapo katika kutekeleza agizo hilo nilichukua hatua ya kwanza na ya muhimu ya kuupitia mkataba wote wa mradi huu ikiwa ni pamoja na kufanya tathmini ya haki na wajibu wa pande mbili zilizohusika kwa maana ya Halmashauri ya Jiji na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF).

Kimsingi, tathmini yangu ya mkataba ililenga kubainisha na kujiridhisha juu ya mambo sita yafuatayo; aina ya jengo lililotarajiwa kujengwa, usimamizi wa fedha za mkopo, usimamizi wa ujenzi wa mradi, gharama za mradi, utaratibu wa urejeshaji wa deni na kiwango cha riba kilichoainishwa. Ikukumbukwe tu kwamba, wakati halmashauri ya jiji ikikabidhiwa mradi siku ya kwanza ilikuwa tayari inadaiwa kiasi cha bilioni 19.7 huku mpaka Machi mwaka huu deni lilishafikia kiasi cha bilioni 38 za kitanzania, kutokea kwenye mkopo wa bilioni 12.7

2.0 Uchunguzi

Baada ya kupitia kwa umakini mkataba mzima na kukagua mradi wenyewe, zoezi ambalo lilihusisha kulinganisha kati ya kilichofanyika baada ya mradi kukamilika na taarifa ya upembuzi yakinifu (feasibility study) uliofanyika kabla ya kuanza utekelezaji wa mradi nimebaini yafuatayo;-

2.1 Ukubwa halisi wa jengo

Nimebaini kwamba majengo ya sasa ya machinga complex hayakujengwa kwa ukubwa sawa na ule ambao Halmashauri ya Jiji na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) walikubaliana kwenye mkataba na kupitia kifungu cha 1.1 cha barua ya makabidhiano kinachoeleza kwamba jengo lililokabidhiwa lina sehemu yenye ghorofa 5 na ghorofa 6 ili liweze kumudu idadi ya machinga wasiopungua 10,000 wakati hali halisi baada ya kutembelea jengo hilo ni kwamba jengo lina ghorofa 4 zinazobeba machinga 4,000 tu. Kwahiyo, pamoja na kwamba barua ya makabidhiano ilisainiwa na pande zote mbili licha ya ukweli kuwa maelezo ya jengo yalikuwa tofauti na jengo lenyewe.

2.2 Usimamizi wa fedha za Mkopo

Kwenye usimamizi wa fedha za Mkopo, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ambaye ni mkopaji hakuhusika na usimamizi wa fedha za mkopo, hivyo mkopeshaji hakuwa na udhibitisho wa gharama halisi, jambo ambalo si tu limefanya mkopaji kutojua gharama halisi za jengo bali pia kulipokea likiwa limechelewa na likiwa halina ukubwa ulioelezwa kwenye mkataba. Kimsingi, haya yote yanazaliwa na maelekezo ya kifungu namba 4.1 kinachoeleza kwamba, mkopeshaji kusimamia mradi kuanzia hatua ya usanifu hadi kukamilika kwake ikiwa ni pamoja na kufanya malipo moja kwa moja kwa mkandarasi na mshauri wa mradi, kwa maneno mengine pia ni kwamba kifungu hiki kinakinzana na vifungu namba 2.1, 2.2, 10.1 na 11.1 vya mkataba huohuo ambavyo vinaelekeza kwamba mkopeshaji (NSSF) atatakiwa kutoa fedha kwa mkopaji (Halmashauri ya Jiji) kwa ajili ya kugharamia mradi pekee na kuusimamia kama ulivyokubalika kwenye mkataba.

2.3 Kuhusu gharama za mradi

Nimebaini kuwa fedha za mkopo ziliongezeka toka shilingi bilioni 12.14 za kwenye mkataba na kufikia bilioni 12.7 ikiwa ni nyongeza ya shilingi milioni 560, nyongeza ambayo ilifanyika bila makubaliano yoyote kati ya mkopeshaji na mkopaji, hali ambayo haimtendei haki mkopaji. Kwa faida tu ya wanadar es salaam na watanzania wenzangu ni kwamba, halmashauri ya jiji ilitiliana saini ya makubaliano na shirika la hifadhi ya jamii (NSSF) ya mkataba ambao unalenga kuipatia halmashauri ya jiji mkopo wa bilioni 10 kwa ajili ya kutekeleza mradi huu ingawa baada ya muda kidogo mkopeshaji (NSSF) alisema kuwa bilioni 10 na hivyo kufanya marekebisho ya mkataba na kuongeza mkopo wa bilioni 2.14

2.4 Urejeshaji wa deni

Suala la urejeshaji wa mkopo unazua utata pale mkataba unapoainisha kuwa, mkopaji ataanza kulipa marejesho ya deni kuanzia tarehe 31 Desemba, 2008 tarehe ambayo mradi ulikuwa unatarajiwa kuwa tayari umeanza lakini mkopeshaji (NSSF) alikuwa hajamaliza ujenzi, na cha ajabu mkopaji (Halmashauri ya Jiji) alitakiwa kuanza kulipa deni hata kabla ya muda wa grace period kuisha wakati jengo likiwa bado lipo mikononi mwa mkopeshaji ambaye alijitwisha jukumu la ujenzi huku akiwa bado akang’ang’ania kulipwa riba.

mara tu tarehe hiyo ilipofika hata kama mpokeshaji mwenyewe alikuwa bado hajakamilisha ujenzi huku akidai pesa ya riba.

Uwezo wa Mradi

Uwezo wa jengo hilo lililopo hata kama litafanya kazi kwa uwezo wake wote kwa maana ya kujaza nafasi zote zilizopo ni kasi cha sh124,796,666.666 kwa mwezi ambazo ni sawa na kiasi cha sh1,497,560,000 kwa mwaka. Pungufu ya 60% ya lengo la Mradi kama ilivyokuwa kwenye upembuzi yakinifu

3.0 Mapendekezo

3.1 Baada ya uchunguzi huu ulionifanya kuamini mambo makubwa matano niliyoyaainisha hapo chini na ambayo yameniongoza kutoa mapendekezo ya hatua za kuchukua;-
Deni halilipiki – ukweli ni kwamba, ukizingatia kiasi cha pesa kinachodaiwa kutoka kwa halmashauri ya Jiji ambacho mpaka sasa ni zaidi ya bilioni 38 utagundua kuwa, halmashauri haiwezi kulipa deni hilo. Ikilinganishwa na uwezo wa jengo hilo deni hili litalipwa baada ya miaka isiyopungua 24
Mkataba wote huu ni wa hovyo na haukupaswa kusainiwa hata kidogo.
Kitendo cha kusaini mkataba huu ni hakika na bayana kuwa rushwa ilitumika pande zote mbili, kwa maana haiwezekani ukaacha taaluma yako kwa kiwango hicho cha kutoona udhaifu huu wa wazi wa mkataba huu kama hujapofushwa macho na rushwa.
Mkataba huu hauna tija kwa upande wowote ule: sio NSSF kwasababu halmashauri ya Jiji hawana uwezo wa kulipa deni, wala sio kwa Jiji lenyewe kwani halina uwezo wa kutekeleza mkataba kwa kufanya malipo yanayotakiwa na hauna faida vilevile kwa machinga kwa sababu gharama ya kupanga ni kubwa.

3.2 Mapendekezo
Kuvunjwa kwa mkataba na NSSF kuchukua eneo lao, kwa makubalino ya kwamba, Halmashauri ya Jiji walipwe kodi ya ardhi jambo ambalo linaweza kufanyika kwa urahisi kupitia NSSF na halmashauri ya Jiji kumiliki hisa kwa pamoja.

Au NSSF wakabidhi jengo kwa halmashauri ya Jiji, lakini wakae na kukubaliana upya na hivyo kuandika mkataba tofauti na ule wa mwanzo.

Mwisho, wahusika wote wa pande zote mbili wachukuliwe hatua kwani hatuwezi kutumia fedha za mifuko za hifadhi ya jamii ambazo ni fedha za wanyonge wa taifa hili kwa faida ya wachache waliotanguliza ubinafsi,.

Imetolewa na:

Paul Makonda
Mkuu wa Mkoa – Dar es Salaam.

Askari Aliyemuua Mwandishi wa Habari Daudi Mwangosi Ahukumiwa Kifungo

$
0
0
‪#‎HABARI‬ Askari aliyemuua mwandishi wa habari Daudi Mwangosi bila kukusudia leo amehukumiwa kifungo cha miaka 15 jela.
Toa maoni yako hapa

Aliyemtoa Baraka Da Prince Kimuziki Afunguka ya Moyoni Baada ya Kuchukuliwa na RockStar 4000

$
0
0
Aliyemtoa Baraka Da Prince kupitia rekodi yake ya Jitunze 'Kidbway' ameongelea uhamaji wa Baraka kwenda RockStar 4000 nakusema ni njia nzuri kama atafikia malengo aliyojiwekea.

KidBway anasema "Nitafurahi akifikia yale malengo niliyokuwa nayo kichwani wakati naanza kufanya naye kazi, hata kama atayafikia kwenye njia tofauti na nilizoona mimi ,nitafurahia kwa mafanikio yake kama ndio njia itakayomfikisha"

Pia Kid amesema "Muda mwingine unatakiwa kujitoa hata kama utaumiza watu ili ufanikiwe, siwezi mtakia mabaya,sio vizuri kumuombea mtu vitu vibaya".

Jay Moe Afunguka Kutoka Kimapenzi na Shilole

$
0
0
Mwanamuziki rapa nchini anayetikisa kwa ngoma ya 'Pesa Madafu', Jay Moe amekuwa akionekana karibu sana na rapa Bilnass ambaye anatikisa na ngoma ya 'Chafu Pozi' kitu ambacho ni njia pekee ya Jay Moe kumpata mrembo Shilole.

Baada ya kuwepo kwa tetesi za wawili hao kutoka kimapenzi na zaidi kuonekana picha wako pamoja kwenye moja ya eneo za kula bata wakati wa usiku, ENewz ilimtafuta rapa Jay Moe avunje mzizi huo wa fitna kama ni kweli anaanguka kwa Shilole lakini alikanusha nakusema ndio mara ya kwanza yeye kusikia habari hizo.

"Ndio kwanza nasikia mambo hayo, sijui mamneno hayo yametoka wapi, ni mambo ya muziki tu na uvumi wa stori tofauti, kama picha mimi ni msanii na kama wasanii picha ni kawaida tu ila hakuna kinachoendelea kati yangu na Shilole"
Jay Moe anatajwa kuwa karibu na Shilole kutokana na urafiki wake na Billnas.

Ney wa mitego afungiwa kujihusisha na muziki

$
0
0

Rapa wa muziki wa kizazi kipya nchini Ney wa Mitego amefungiwa kujihusisha na muziki kwa kipindi kisichojulikana kufuatia wimbo wake alioutoa hivi karibuni.

Wimbo huo unaitwa ‘Pale kati patamu’.

Akizungumza Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mngereza amesema Ney anatakiwa pia kulipa faini ya Sh1 milioni.

RPC Amtaka Muuaji wa Askari wa Barabarani Akiwa Hai au Mfu

$
0
0

KAMANDA wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro amewaagiza askari kuhakikisha wanampata akiwa hai au amekufa mhalifu aliyetekeleza mauaji ya kinyama ya askari wa kikosi cha usalama barabarani, Sajini Mensah Ponda Dishe.

Aidha, amesema hata kama mtu aliyefanya unyama huo yuko ndani ya familia, jeshi hilo litahakikisha linamshughulikia ipasavyo ili haki ipatikane.

Aliyasema hayo jana wakati akiongoza mamia ya askari na wananchi waliojitokeza kuuaga mwili wa askari huyo katika viwanja vya nyumba za polisi Kunduchi. “…Nimewaambia askari walio chini yangu wafanye kila liwezekanalo ili mhalifu aliyehusika kufanya tukio hili la kinyama akamatwe akiwa mzima au akamatwe akiwa amekufa ili haki itendeke,” alisema Kamanda Sirro.

Alisema hata kama mhalifu huyo atabainika kuwa yuko ndani ya familia ya askari huyo, Jeshi la Polisi halitasita kumchukulia hatua za kisheria ili kuhakikisha haki imepatikana.

Kamanda Sirro alisema, alipopata taarifa za askari huyo kupigwa risasi alikwenda hadi Hospitali ya Taifa Muhimbili, lakini aliambiwa kuwa amepelekwa Hospitali ya Mwananyamala ambapo alipofika aliambiwa kuwa ameshapoteza maisha kwa kuwa alipigwa risasi kwa karibu sana.

Alisisitiza askari wote kuhakikisha wanatenda haki, wanakataa rushwa ili hata siku ya mwisho wakati wa hukumu ya Mwenyezi Mungu waweze kwenda sehemu salama.

Tickets Kwa Ajili ya Show ya Mwendokasi Festival Zimeanza Kuuzwa Kama Njugu...Hivi Hapa Vituo Zinapopatikana

$
0
0

Pata tiketi za MwendoKasi Festival katika vituo vilivyopo karibu yako... Kwa maelezo zaidi tupigie 0719619602

Tiketi za kawaida ni 10000TZS

VIP ni 100000 TZS (Watu wawili na vinywaji vya 40000TZS)

VVIP ni 500000TZS (Watu wanne na Vinywaji vya 100000TZS)

Chadema watangaza mikutano ya hadhara Na Maandamano Nchi Nzima kuanzia Septemba Mosi....

$
0
0
Kufuatia kile walichokiita 'matukio ya ukandamizaji wa haki na demokrasia',   Chadema kimetangaza Septemba Mosi mwaka huu kuwa siku ya mikutano ya hadhara nchi nzima.

Chama hicho pia kimezindua Operesheni Ukuta (Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania),  huku kikiwataka wananchi wote waliokumbana na 'rungu' la Serikali ya Awamu ya Tano kuungana na Operesheni hiyo,  wakiwemo mama ntilie na waendesha bodaboda.

Chama hicho kimetaja mambo 11 kinachodai kuwa yamefanywa na Serikali bila kufuata sheria na kanuni za nchi,  likiwemo la kuzuiwa kwa shughuli za kisiasa na kutaja sababu 24 za kuibuka na Operesheni Ukuta

Shibuda: Msindai, Mpendazowe Wanafiki

$
0
0
HATUA ya Fredy Mpendazowe na Mgana Msindai kurudi Chama Cha Mapinduzi (CCM), inatokana na kuhangaikia maslahi binafsi, anaandika Dany Tibason.

Msindai, aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida alijiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kabla ya Uchaguzi Mkuu mwaka jana kwa madai, ndani ya CCM hakuna demokrasia.

John Shibuda, Katibu Mkuu wa Chama cha ADA TADEA amesema, wakongwe hao katika siasa waliondoka CCM kwa madai ya kukerwa na chama hicho lakini cha kushangaza wamerejea kwa mbwembwe.

Shibuda amesema kwamba, wanasiasa hao ni wanafiki ndani ya siasa na kuwa “mnafiki hafi hadi ameumbuka.” Amedai hatua ya kurejea CCM imewaumbua.
“Waliishambulia CCM wakiwa kwenye majukwaa ya Chadema, leo wamerejea kule walikokuwa wakishambulia,” amesema Shibuda.

Amesema, Mpendazowe na Msindai wamekuwa wakiuaminisha umma kwamba CCM ni chama cha hovyo “iweje leo warejee kule kule kwa hovyo?

“Watu wazima kama hao ni wanafiki ndani ya siasa na wamekula matapishi yao. Hawawezi kuaminika tena katika jamii na katika ulingo wa siasa kwa kuwa, ni wanasiasa maslahi.
“Siyo wanasiasa bali wamevaa vazi la siasa huku uhalisia ukiwa ni wanasiasa maslahi. Hakukuwa na maana kutumia majukwaa kuitukana CCM na baadaye kurudi.

“Walipotoka CCM kwenda Chadema walitumia majukwaa kuishambulia CCM na sasa wamerudi CCM kwa kuishambulia Chadema.”

Shibuda amesema, umri wa wanasiasa hao ulitakiwa kutumiwa kuwajenga vijana kifikra juu ya kuwepo kwa siasa safi ambazo ni za ukombozi.

“Kwa umri wa Msindai na Mpendazowe walitakiwa kuwa shamba darasa na urithi wa mawazo kwa vijana chipukizi wa kisiasa.

“Tujikumbushe jinsi Mpendazoe alivyoweza kutunga kitabu ambacho kiliweza kuelezea mambo mengi, leo ni aibu kwa msomi huyo kuonesha udhaifu wa kisiasa na kujidhalilisha,” amesema Shibuda.

Pia ameishangaa CCM kwa kuwapokea wanasiasa wachafu na ambao wamekuwa wakikisema chama hicho vibaya hadharani.

“Kauli ya Rais John Magufuli kudai anataka usafi ndani ya chama ni unafiki, sidahi kama kuna kanisa ambalo linaweza kumpokea muumini ambaye aliyemkataa Yesu au msikiti ambao unaweza kumkaribisha muumini ambaye alimkataa Mtume.

“Je, muumini wa Dini ya Kiislamu anaweza kuitukana Qur’an na baadaye akaanza kuisifia? hilo jambo haliwezekani.”

VIDEO:Aliyepigwa Picha za Utupu na Kusambazwa Mitandaoni Huyu Hapa, Ahojiwa na Kunena Haya

$
0
0
Mhanga wa picha za utupu zilizosambaa mtandaoni amehojiwa na na kudai kuwa ni kweli pcha hizo alizopiga ni za kwake na alizipiga akiwa anajitambua na mwenzi wake huyoa liyekuwa amepiga nae picha walishaachana baada ya kuwa na mahusianano waliyoyaanza mwaka 2014 na kudumu kwenye mapenzi kwa miezi 6 lakini hawakujuana kundani kwa muda waliokuwepo pamoja

Anadai baada ya kuona picha hizo alimtafuta mpenzi wake huyo wa zamani na kumuuliza kulikoni na kudai kuwa amepoteza simu.

Alitoa taarifa polisi na polisi walikuwa na taarifa tayari baada ya hpo alimtafuta mpenzi wake huyo aitwa Vincet na kukuta hapatikani na amem block kwenye mitandao ya kijamii ya WhatsApp na Instagram
Amesema kisa cha mwanaume huyo kuvujisha picha hizo ni kuwa waliachana baada ya kumfuma na mwanamke mwingine ambaye alikuwa ni ndugu yake na kisha kumuacha na kuanzisha mahusiano na mwanaume mwingine,
Mwanaume huyo akadai atamuharibia kwa kuwa yeye alimuharibia mipango yake na msichana aliyemfuma naye kwa hiyo na yeye lazima atalipiza kisasi Angalia Video Hapa:

CHADEMA Watangaza Kuanza Operesheni ''Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania (UKUTA)''

$
0
0
Leo Kamati Kuu ya CHADEMA imefanya kikao chake katika Hoteli ya Bahari Beach Ledger Plaza.

Mojawapo ya Maazimio ya Kikao hicho ni kuundwa kwa kile walichokiita Umoja Wa Kupinga Udikteta Tanzania(UKUTA). Tuweke Kumbukumbu sahihi, Kamati Kuu ya CHADEMA iliyoketi siyo Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).

Hii ina maana kwamba maazimio ya kuundwa kwa UKUTA ni matakwa ya Chama kimoja yaani CHADEMA. Ikumbukwe kuwa UKAWA uliundwa kwa makubaliano ya vyama vinne vya CHADEMA, CUF, NCCR-MAGEUZI na NLD. Hakuna namna yoyote ya kuwashawishi Watanzania kuwa hiki wanachokiita UKUTA ni Umoja, Umoja lazima ushirikishe pande watu zaidi ya mmoja au zaidi ya vikundi viwili au zaidi ya vyama viwili.

Mtazamo: Kabla ya UKAWA, Kambi rasmi ya Upinzani iliundwa na chama kimoja cha CHADEMA. Ni katika kipindi hicho ambapo Chadema na CUF walikuwa na msuguano mkubwa hadi kupelekea CHADEMA kuwaita CUF , CCM B huku CUF wakiwaita CHADEMA chama cha MASHOGA.

Baada ya Chadema kuondokewa na Makada wake maarufu walioshiriki kikamikifu kukijenga chama wakiongozwa na Zitto Kabwe, Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba, CHADEMA kiliyumba sana na kutafuta kila namna ya kukinusuru na anguko kuu. Ndipo Mungu aliposikiliza maombi yao na bila kutarajia, Ibrahim Harouna Lipumba akaibuka na wazo la kuundwa kwa UKAWA wakati wa Bunge Maalum la Katiba.

CHADEMA wakaingia kwenye umoja huu kwa malengo makubwa ya kufufuka jambo ambalo CUF, NCCR-MAGEUZI na NLD hawakujua. Haraka sana, Mbowe akaenda kutangaza kulivunja baraza kivuli lililokuwa na Wabunge wa Chadema pekee na kuunda jipya lenye kujumuisha Wabunge wa UKAWA. Ni katika umoja huo wa wajanja CHADEMA na mambumbumbu wa CUF, NCCR na NLD uliokipaisha chadema na kwa ujanjajanja hio CUF, NCCR na NLD wakajikuta wanamuunga mkono mgombea urais wa CHADEMA huku viongozi wa CUF, NCCR na NLD wakitumiwa kama vibaraka na wale wa CHADEMA. NCCR, NLD na CUF vimebaki majina.

Uamuzi wa CHADEMA leo wa kuuda UKUTA si chochote wala si lolote. Hizi ni hila tu vinafanyiwa vyama vya NCCR, CUF na NLD. Chadema wameona wameshajiweza, wanaamua kujivua GAMBA kutoka katika mikono ya UKAWA ili wajitegemee
Swali ni je CUF, NCCR na NLD wanalijua hilo? Wako tayari kuitwa washirika wa UKUTA wakati UKUTA umetokana na maazimio ya KAMATI KUU YA CHADEMA? Je UKUTA hautawapoteza viongozi makini kama ambavyo UKAWA ukiwapoteza akina Dr. Slaa na Prof. Ibrahim Harouna Lipumba?

Tusubiri tuone.

Bodi ya Mikopo yatangaza majina 1,091 ya wadaiwa Ambao Hawataki Kulipa (Awamu ya kwanza).....Bonyeza Hapa Ujitazame Kama na Wewe Jina Lako Lipo

$
0
0
Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu (HESLB), inawaarifu wadaiwa wote ambao mpaka hivi sasa hawajaanza kulipa mikopo waliochukua kipindi wanasoma, na wenye majina yao kwenye orodha hii kwamba wamevunja mkataba kutokana na sheria ya bodi hiyo No. 9 ya 2004 (kama ilivyorekebishwa) sehemu ya 19 (1).

Na wanataarifiwa kwamba, kulingana na sheria hiyo ya bodi (HESLB)  No. 9 ya 2004, Bodi imedhamiria kutenda yafuatayo:-

(i) Bodi itachukua hatua za kisheria kulingana na kipengele cha 19 (a) (1) cha sheria ya bodi.

(ii) Mdaiwa atapewa penati ya 5%  juu ya ile 5% iliyokua ikitozwa kabla kwa kila mwezi kwenye deni lililobakia au alilonalo.

(iii) Mdaiwa ataongezewa gharama za kumtafuta alipo ili alipe deni zilizoingiwa na bodi.

(iv) Mdaiwa atawekwa kwenye ‘blacklist’ na maelezo yake yatapelekwa  kitengo cha kumbukumbu ya wakopaji na hivyo kushindwa kukopa sehemu nyingine yoyote.

(v) Mdaiwa atazuiliwa kupata udhamini wa Serikali au udahili wa masomo ya juu kwenye vyuo vyovyote ndani na nje ya nchi.

(vi) Maelezo yao yatapelekwa kwenye Wizara ya mambo ya ndani, kitengo cha Uhamiaji na balozi zote ambako watakataliwa safari zozote za kwenda nje ya nchi.

Wadaiwa wote ambao majina yamechapishwa kwenye magazeti na kwenye tovuti ya bodi ya mikopo (Bonyeza hapa kuyasoma majina hayo) wanatakiwa kulipa madeni yao mapema iwezekanavyo kuzuia wao kupata adhabu hizo zilizotajwa hapo juu.

==>Bonyeza Hapa Kuyasoma Majina Hayo

Maumivu Makali Ukeni Wakati wa Tendo la Ndoa.....

$
0
0
Habari zenu jamani,

Mwenzeni ninatatizo yaani toka nijue mapenzi sijawahi kufurahia tendo hilo. Kila nikifanya mapenzi napata maumivu makali mno muda mwingine nahisi maumivu hadi kwenye kizazi. Nikimaliza tu maumivu siyapati mpaka nikifanya tena. Nifanyeje jamani, msinitukane tafadhali.

Karibuni kwa ushauri
Viewing all 104689 articles
Browse latest View live




Latest Images