Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104431 articles
Browse latest View live

MBUNGE Ajilipua Kwa Bomu Katika Shambulio la Ugaidi Somalia

0
0
Mmoja wa washambuliaji wa kujitoa mhanga waliohusika katika shambulio lililotekelezwa karibu na kambi ya vikosi vya Umoja wa Afrika (AU) mjini Mogadishu mnamo Jumanne aliwahi kuwa mbunge.

Salah Nuh Ismail, 57, alikuwa miongoni mwa watu 13 waliofariki kwenye milipuko miwili iliyotokea karibu na uwanja wa ndege, kundi la al-Shabab lilisema.

Alijulikana sana kama Badbado, jina ambalo maana yake ni ‘Usalama’ au ‘Yule Salama’.

Alijiunga na Bunge la Somalia mwaka 2000 lakini akajiuzulu na kujiunga na al-Shabab mwaka 2010.

Anakumbukwa sana kwa kuwaita wabunge wenzake “makafiri”, baada yake kujiunga na kundi hilo la Kiislamu.

Kambi kuu ya Amisom yavamiwa Mogadishu

Alipokelewa kwa heshima kubwa na maafisa wakuu wa kundi hilo ambao walisema “alijutia makosa aliyokuwa ameyatenda”.

Washambuliaji wawili wa kujitoa mhanga walihusika

Tofauti na washambuliaji wengine wa kujitoa mhanga, ambao huwa vijana na watu wasiosoma sana na ambao si maarufu, yeye alikuwa mtu mzee kwa umri, aliyeelimika na mtu maarufu.

Al-Shabab wamekuwa wakikabiliana na serikali ya Somalia ambayo huungwa mkono na Umoja wa Afrika na jamii ya kimataifa.

Eneo la karibu na uwanja wa Mogadishu hulindwa sana na hutumiwa kwa shughuli za Umoja wa Mataifa.

Mataifa mengi yana afisi za kibalozi eneo hilo.

GEITA: Waziri Mwigulu Aweka Gwaride la Utambuzi, Amkamata Mchina Aliyemtesa Mtanzania

0
0
Nimefika Mgodi wa Nyamhuna unaodaiwa kuwa raia wa china ambao ni sehemu ya wamiliki wa mgodi huo wakishirikiana na watanzania walimtesa kinyama na kumjeruhi mmoja wa mtanzania mwenzetu aliyekuwa akifanya kazi katika mgodi huo uliopo Katoro-Geita.

Imenilazimu kufika gereza la Geita kukutana na kijana huyo ambae yupo hai tofauti na taarifa za awali kuwa alifariki.Baada ya kujiridhisha kuanzia mavazi,majeraha,picha,sura na umbo lake kuwa ndiye kijana aliyeteswa vibaya na picha zake kusambaa mitandaoni na vyombo mbalimbali vya habari,niliamua kwenda naye hadi mgodini lilipofanyika tukio hilo la kinyama,aliwatambua wahusika ambao NI KWELI WALIFANYA TUKIO HILO LA KINYAMA NA LISILOKUBALIKI HAPA NCHINI.

Hivyo walioshiriki tukio hilo tumeshawashikilia kupitia jeshi la polisi tayari kwa kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Nalaani tukio hilo vikali sana,serikali hii ipo tayari kushirikiana na kila mmoja rai mwema kutoa taarifa popote pale za matukio au viashiria viovu na vinavyohatarisha usalama wetu.

"Usalama wetu,jukumu letu sote"

Copy and Paste from Mwigulu Nchemba Facebook Wall

My take
Huu Unyama unaofanywa na Raia wa Kigeni hapa Nchini kwetu unatakiwa kuchukuliwa kwa hatua kama hizi tena haraka sana iwezekanavyo. Mijitu isiyokuwa na Huruma pamoja na Kumtesa kwa kumsurubu Mtanzania mwenzetu, bado haikutosheka Ikambambika kesi na kumsweka Lupango ndugu yetu huyu.

Haya hayafanywi tu huko Migodini, Hata hawa Wahindi wanawanyanyapaa sana Dada zetu wanaofanya kazi za Nyumbani kwenye Makazi yao. Serikali inapaswa kupanua jicho kuangalia wananchi wake wanavyonyanyapaliwa na hawa wageni huku wao wakiishi kama wako kwao.

Heko Mwigulu Nchemba.

Habari Zlizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi ya July 28, Ikiwemo ya Chadema Kubadili Gia Angani....

0
0


Habari Zlizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi ya July 28, Ikiwemo ya Chadema Kubadili Gia Angani....

TP Mazembe Wameimarisha Matumaini ya Yanga Kufuzu Nusu Fainali ya CAF

0
0
Maombi na furaha ya watanzania wote wazalendo ni kuona Yanga ikifanikiwa kuingia katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la shirikisho barani Afrika CAF, licha ya kuwa nafasi yao kwa sasa inatajwa kuwa ndogo, lakini Yanga wanayo nafasi ya kusonga mbele licha ya kuwa na point moja na wapo mkiani.

Safari ya Yanga kutinga hatua ya nusu fainali ya CAF inamlazimu ashinde mechi zake zote mbili zilizosalia za MO Bejaia atakayocheza nyumbani na mechi dhidi ya TP Mazembe atakayocheza ugenini, huku akiombea mechi ya mwisho kati ya MO Bejaia ya Algeria dhidi ya Medeama imalizike kwa sare ya aina yoyote ile.



TP Mazembe bado imeendelea kuipa matumaini Yanga baada ya mchezo wa leo kufanikiwa kuifunga MO Bejaia kwa goli 1-0, goli ambalo lilifungwa na Rainford Kalaba dakika ya 62, kwani kama TP Mazembe angefungwa leo Yanga wangekuwa rasmi wameaga michuano hiyo wakiwa wamesalia na michezo yao miwili mkononi.

Mbunge Professor Jay Katuletea Wimbo Wake Mpya ‘Kazi Kazi’ UdownloadHapa

0
0
Ni July 27, 2016 ambapo headlines zinamilikiwa na Mbunge wa jimbo la Mikumi, Joseph Haule aka Professor Jay kwa kuachia single yake mpya iitwayo Kazi Kazi aliyomshirikisha Sholo Mwamba.

Unaweza ukabonyeza HAPAKuudownload kisha sio mbaya ukituachia na comment yako wakali hawa watapita hapa kujua Watanzania wameipokeaje.

Mrembo Tunda Afunguka Kumwagana na Mwanamuziki Young D

0
0
MUUZA nyago macha-chari Bongo, Tunda Sebastian amefunguka kumwagana na mwandani wake wa muda mrefu, ambaye ni staa wa Bongo Fleva, David Genzi ‘Young D’ na kusema ameamua kujiweka kando kwenye maswala ya mapenzi.

Akipiga stori na Showbiz Xtra baada ya kumbananisha kuhusiana na tetesi za uhusiano wake kuvunjika kutokana Young D kubaini anatoka na mwanamuziki mwenziye (jina kapuni) ndipo akaeleza kuwa, ishu hiyo haina ukweli ila ameachana na mwandani wake huyo kwa sababu ambazo hawezi kuzianika kwa sasa.

“Hayo ya kutoka na huyo msanii si kweli na kuhusu Young D nimeshaachana, sifikirii kuwa na msanii yeyote na sihitaji mpenzi kwa sasa,” alisema.

Kajala Aenda Kumlilia Mumewe Gerezani!

0
0
Staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja ‘Kay’ hivi karibuni amekwenda kumlilia mumewe, Faraji Chambo anayetumikia kifungo cha miaka kumi na mbili gerezani.

Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho ni mtu wa karibu wa Kajala, mwanamama huyo alitinga kwenye Gereza la Ukonga, Dar alikofungwa mumewe ambapo alipata nafasi ya kumjulia hali kisha kumwaga machozi akimuonea huruma anavyosota gerezani hasa akikumbuka walivyokuwa wakiishi kabla ya msala huo.

Katika safari hiyo, Kajala aliongozana na mwanaye, Paula Paul na mdogo wake Kajala ambao ndiyo waliokuwa wakimtuliza staa huyo ambaye alisababisha mumewe naye kutokwa machozi.
Akizungumzia ishu hiyo, Kajala ambaye wiki iliyopita alizindua filamu yake kali ya Sikitu alisema kuwa ni utaratibu wake wa mara kwa mara kwenda kumjulia hali mumewe huyo ila mara zote huwa anakwenda kimyakimya.

“Huwa nakwenda mara nyingi tu sema ndiyo hivyo huwa sipendi kuongozana na msururu mrefu, namshukuru Mungu anaendelea vizuri,” alisema Kajala. Machi 2013, Kajala na Faraji walihukumiwa ambapo Kajala alitakiwa kwenda jela miaka mitano au faini ya shilingi milioni kumi na tatu na mumewe miaka kumi na mbili au faini ya shilingi milioni mia mbili kwa kosa la kutakatisha fedha haramu kwenye Benki ya NBC, Tawi la Dar.

KajalacropHarusiHata hivyo, Faraji alishindwa kulipa kiasi hicho cha fedha na kujikuta ‘akiozea’ gerezani huku Wema Sepetu ‘Madam’ akimlipia Kajala faini ya shilingi milioni kumi na tatu, iliyomnusuru kwenda jela.

Chanzo:Global Publishers

Mamia wafurika kununua viwanja Dodoma

0
0

MAMIA ya wananchi wameanza kupeleka maombi ya viwanja katika ofisi za Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA), imeelezwa.


Hali hiyo imetokea baada ya Rais Dk. John Magufuli kutangaza nia ya Serikali kuhamia mjini hapa kwa kuwa ndiko yaliko makao makuu ya nchi.


Kutokana na idadi kubwa ya watu wanaofika katika ofisi za Idara ya Ardhi katika mamlaka hiyo, Jeshi la Polisi mkoani hapa limelazimika kuimarisha ulinzi ili kukabiliana na hali hiyo.


Mmoja wa watu waliokutwa ofisini hapo na kujitambulisha kwa jina la Salum Kijuu, mkazi wa Area A, alimwambia mwandishi wa habari hizi aliyeshuhudia mamia ya watu ofisini hapo jana, kwamba alifika ofisini hapo kulipia kiwanja chake kilichopo eneo la Miganga.


“Kaka hii foleni ya watu karibia wote wanaulizia viwanja, mimi nimekuja kulipia kiwanja changu ili niweze kukimiliki kihalali kwani mambo yameshabadilika,”alisema Kijuu.


Wakati hali ikiwa hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa CDA, Paskasi Muragili, alisema ardhi mjini hapa itauzwa kwa bei ya kawaida ili watu wengi waweze kumiliki viwanja.


“Kwa mfano, ‘square’ mita moja ya kiwanja cha makazi itauzwa kwa Sh 5,500 hadi Sh 10,000 katika maeneo ambayo kitaalamu tunayaita ‘medium density’.


“Kwa sasa maeneo yanayouzwa ni Miganga na Mkalama yaliyopo nje kidogo ya mji wa Dodoma.


“Viwanja kwa ajili ya uwekezaji mkubwa ‘square’ mita moja itauzwa kwa Sh 13,300 na maeneo hayo kitaalamu tunayaita ‘low density’.


“Pamoja na uwepo wa mahitaji makubwa, nasema ardhi ipo ya kutosha, yaani hata kama watakuja wananchi wote wa Dar es Salaam, watapata ardhi ya kutosha.


“Narudia tena, ardhi ipo ya kutosha, hata kama watu watakuja baada ya miaka 30, wataipata kwa sababu hata Mwalimu Nyerere alipoamua Dodoma iwe makao makuu, alijua kuna ardhi ya kutosha kwa idadi yoyote ya watu,” alisema Muragili.


Akizungumzia mpangilio wa mji utakavyokuwa, alisema mji wa kiserikali utaanzia katika Kijiji cha Mtumba hadi eneo la Ikulu ndogo ya Chamwino, ambako kutakuwa na ofisi za wizara na mabalozi.


“Mji wa kibiashara, utakuwa ni eneo lote la mji wa Dodoma kwa sababu hii ramani ninayokwambia iko katika ‘master plan’ ya mwaka 2010-2030 ya kuhakikisha makao makuu ya nchi yanakuwa vizuri kuanzia kwenye barabara za kuingia na kutoka ili kusiwe na msongamano wa aina yoyote,”alisema.


Pamoja na hayo, mkurugenzi huyo alitoa angalizo kwa wanaohitaji kununua viwanja mjini Dodoma na kusema watatakiwa kupitia CDA kwa kuwa ndiko vinakopatikana.


“Viwanja tusinunue kienyeji, tufuate taratibu kwani najua watatokea wapigaji wa dili watakaowaumiza watu. Nawaombeni mje ofisini kwetu, kama mnataka viwanja mtapata tu kwa kufuata utaratibu,’’ alisema.


Naye Ofisa Uwekezaji wa CDA, Abeid Msangi, alisema wametenga maeneo maalumu ya Itega na Njendengwa kwa ajili ya kujenga mahoteli makubwa na nyumba mbalimbali za kupanga.


“Lakini kwa sasa eneo la Itega limeshajaa, ila Ndejengwa tumetenga zaidi ya ekari 1,500 kwa ajili ya uwekezaji mkubwa.


“Kuonyesha kwamba tulijipanga mapema katika eneo la uwekezaji, kule Ndejengwa miundombinu iliishafika mapema, kwani kuna maji, umeme pamoja na barabara za lami,” alisema Msangi.


Hivi karibuni, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, alisema watazalisha umeme wa megawati 60 ili kuondoa tatizo la kukatika kwa umeme katika Mkoa wa Dodoma.


Profesa Muhongo alitoa kauli hiyo hivi karibuni alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya mradi wa kujenga njia ya kusafirisha umeme wa kilovoti 400 kutoka Iringa hadi Shinyanga kupitia Dodoma na Singida.


Naye Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka, Mkoa wa Dodoma (Duwasa), David Pallangyo, ameshasema wamejipanga kuhakikisha maeneo yatakayopimwa, yanapata maji safi na salama.


Kwa upande wake, Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Mkoa wa Dodoma, Bernard Chimagu, naye alishasema wamejipanga kukabiliana na ongezeko la magari.

Ndesamburo wa Chadema azushiwa kifo

0
0

Msemaji wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, Boniface Makene amekanusha uvumi unaonezwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Mwenyekiti wa chama hicho mkoani Kilimanjaro, Philimon Ndesamburo amefariki dunia usiku huu.

Makene amewataka Watanzania kuupuuza kwani huenda walioutengeneza wana malengo yao binafsi.

“Nimefuatilia na kupata uhakika kutoka mfumo wa chama hadi mkoani Kilimanjaro na kubaini kuwa habari hizo ni uongo mkubwa nawaomba watu na vyombo vya habari kuzipuuza,” amesema Makene.

Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT) Chakanusha vyuo vyake kuzuiwa Kudahili

0
0

CHUO Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT), kimetoa ufafanuzi wa taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa vyuo vyake vishiriki vimezuiwa na Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) kufanya udahili wa wanafunzi.

Taarifa hizo zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zimedai kuwa vyuo vishiriki vya SAUT ambavyo ni Stella Maris Mtwara University College (STEMMUCO) na Archbishop James University College (AJUCO) vimefungiwa na TCU kufanya udahili wa wanafunzi kwa mwaka wa masomo 2016/2017.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Makamu Mkuu wa Chuo cha SAUT, Dk Thadeus Mkamwa, taarifa hizo ni za upotoshaji na kuwa hawajapokea taarifa kutoka TCU ikivizuia vyuo hivyo viwili kufanya udahili.

Aidha, Dk Mkamwa aliiomba jamii na wadau wa elimu kwa ujumla kupuuzia taarifa hizo kwa kuwa zina uwezekano wa kuwa ni mbinu chafu zinazofanywa na baadhi ya watu kuuhadaa umma hasa katika kipindi hiki ambacho ni muafaka kwa waombaji kufanya maombi katika vyuo vikuu.

“Tunauomba umma wa Watanzania kufahamu kuwa, Chuo Kikuu cha SAUT na vyuo vyake vikuu vishiriki vilivyotajwa hapo juu vinaendelea na udahili wa wanafunzi kwa mwaka wa masomo 2016/2017,” alisema Dk Mkamwa.

Alisema SAUT ni Chuo Kikuu kinachomilikiwa na Kanisa Katoliki Tanzania, na kwamba kimepiga hatua kubwa katika kujiendeleza na kufanikiwa kuanzishwa kwa vyuo vingine vikuu vishiriki vya SAUT ambavyo ni STEMMUCO kilichopo Mtwara, AJUCO kilichopo Songea na Jordan University College (JUCO) kilichopo Morogoro.

Vyuo vingine ni St. Francis University College of Health and Allied Sciences (SFUCHAS)- Morogoro, Archbishop Mihayo University College (AMUCTA)- Tabora, na Cardinal Rugambwa Memorial University College (CARUMUCO) kilichopo Bukoba, Marian University College (MARUCO) kilichopo Bagamoyo.

Dk Mkamwa aliongeza kuwa, chuo kimeweza kuanzisha vituo vingine vitatu vya SAUT vilivyoko Mbeya, Arusha na Dar es Salaam.

Papa Francis Aanguka Ghafla Akiongoza Misa

0
0

POLAND: Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis, ameanguka ghafla wakati akiwa anaongoza misa, baada ya kujisikia vibaya.
Inadaiwa Papa husumbuliwa na tatizo la maumivu ya miguu na mgongo

Al-Shabab Washambulia Mtambo wa Mawasiliano Kenya

0
0
Washukiwa wa kundi la Al-Shabaab mapema leo Alhamisi wameshambulia na kulipua mtambo wa mawasiliano ulioko katika mji wa Fino, Lafey katika kaunti ndogo ya Mandera nchini Kenya.

Afisa mkuu wa Polisi huko Lafey, Bosita Omukolongolo, amesema kuwa kisa hicho kilitokea saa nane usiku.

Afisa huyo wa Polisi anasema kuwa walikabiliana vikali na wanamgambo hao, lakini hakuna maafa yaliyoripotiwa upande wa polisi waliokuwa wakiulinda mlingoti huo wenye vifaa vya kupeperusha mawasiliano.

Kundi la Al- Shaabab, ambalo lina makao yake nchini Somalia, limehusika na mashambulizi ya mara kwa mara pamoja na mauaji nchini Kenya na mataifa kadhaa ya Afrika Mashariki na upembe wa Afrika.

Meya wa Kinondoni Atumbua Majipu Kwa Kufuata Taratibu Sio Misifa Kama Wale

0
0
Baraza la madiwani chini ya meya wa manispaa ya Kinondoni Jacob Steven limewachukulia hatua watumishi 18 waliokuwa na tuhuma mbalimbali, watumishi 9 wa uhandisi, 8 afya na 1 wa utumishi fedha na biashara,

Watumishi wa 4 afya wamefukuzwa kazi kwa utoro na rushwa, watumishi 3 uhandisi wamekutwa na hatia kwa kushushwa vyeo na madaraja na mtumishi wa fedha na biashara amepewa onyo kali
uamuzi kwa wahandisi umetokana na wao kushindwa kutumia taaluma zao vizuri kwenye ujenzi wa barabara.
watumishai hao walichukuliwa hatua baada ya kufunguliwa mashtaka, kufanyiwa uchunguzi wa tuhuma zao na wao kupewa muda wa kujitetea.

Baraza la madiwani limewapandisha vyeo watumishi 372, kuwabadilisha vyeo watumishi 9, na kuwathibitisha kazini watumishi 206 ambao walimaliza vipindi vya majaribio na kuonekana kuwa wanafaa kuwa watumishi wa umma

Nawapa hongera kwa kufanya kazi hii kwa weledi na sio kwa show off, wanaofanya kazi kwa show off ili kuonekana wanafanya kazi na wanapenda haki kumbe wana sura mbili wangeiga mfano huu

VIDEO:

Hii ndiyo sura ya Saint West mtoto wa Kim na Kanye

0
0
MKE wa rapa maarufu Kanye West kutoka Marekani, Kim Kardashian amemuonesha mtoto wao Saint West kwa mara ya kwanza mbele ya umati.

Kim amemwonesha mwanaye huyo wa pili mwenye umri wa miezi saba wakati wa kipindi cha Keeping Up With The Kardashians kinachoruka kwenye runika kikielezea maisha halisi ya Kim Kardashian na familia yake.

Msajili wa Vyama vya Siasa Alaani Tamko la CHADEMA

0
0
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mutungi amelaani vikali  tamko la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) lililotolewa jana tarehe 27 Julai, 2016 kupitia vyombo vya habari, kuhusu hali ya demokrasia ya vyama vingi hapa nchini la kuazimia kufanya mikutano na maandamano nchi nzima akidai kuwa tamko hilo ni la kichochezi lililolenga kuleta uvunjifu wa Amani.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini cha Ofisi ya Msajili wa Vya Siasa na kusainiwa na Jaji Francis Mutungi imebainisha kuwa tamko hilo linaenda kinyume na Sheria ya Vyama vya Siasa namba 5 ya mwaka 1992 kifungu 9 (2) (c) inayokataza chama cha siasa kutumia au kuhamasisha matumizi ya nguvu au vurugu kama njia ya kufikia malengo yake ya kisiasa.

“Nimepokea kwa masikitiko tamko la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) lililotolewa jana tarehe 27 Julai, 2016 kupitia vyombo vya habari, kuhusu hali ya demokrasia ya vyama vingi hapa nchini. Tamko hilo limejaa lugha ya uchochezi, kashfa, kuudhi na lenye kuhamasisha uvunjifu wa amani. Ili kuepuka kurejea tamko lote, nimeona ni vyema nitoe mfano wa maneno yafuatayo yaliyosemwa, ambayo yanakiuka Sheria ya Vyama vya Siasa”. Ilisema taarifa hiyo.

Aidha, taarifa hiyo iliongeza kuwa kifungu cha 9(2) (f) kinakataza chama cha siasa kuruhusu viongozi au wanachama wake kutumia lugha ya matusi, kashfa na uchochezi ambayo inaweza kusababisha au ikapelekea kutokea uvunjifu wa amani. Vile vile kanuni za Maadili ya Vyama vya Siasa, Tangazo la Serikali namba 215 la mwaka 2017, zinakataza chama cha siasa kutumia lugha za matusi, kashfa, uongo na uchochezi.

Nakuongeza kuwa kanuni ya 5(1) (d) inakitaka kila chama cha siasa kutotoa maneno yoyote au maandishi ambayo ni uongo. Kuhusu mtu yoyote au chama cha siasa chochote.

Katika taarifa yake Jaji Mutungi amesema kutokana na Kanuni hizo tamko la CHADEMA ni ukiukwaji wa Sheria ya Vyama vya Siasa.

Aidha, hii siyo mara ya kwanza kwa CHADEMA kutumia lugha za namna hii za kuhamasisha uvunjifu wa amani (civil disorder).

Natumia fursa hii kukemea tamko hilo hadharani, kwa mujibu wa kanuni ya 6(2) ya Kanuni za Maadili ya Vyama vya Siasa. Pia nawaasa CHADEMA wasiendeleze tabia hii.

Jaji Mutungi ametoa rai kwa  Viongozi wa Vyama vya Siasa  waonyeshe ukomavu katika medani za Siasa badala ya kujikita katika vitendo, kauli au matamshi yenye mlengo wa kusababisha uchochezi au kufarakanisha Umma na Serikali yao.

Katika tamko lao CHADEMA wameitangaza siku ya tarehe mosi Septemba kama ni siku maalum kwao kufanya mikutano nchi nzima ikiwamo maandamano ambapo ngazi zote za chama kuanzia ngazi ya msingi hadi Taifa zitahusika.

Mimba Nusura Imutoe Roho Wastara!

0
0
Siku chache zilizopita, staa wa sinema za Kibongo, Wastara Juma alikiri na kufunguka kuwa ni mama kijacho baada ya kunasa ujauzito lakini taarifa za kusikitisha zilizolifikia gazeti hili mapema wiki hii zimedai kwamba, mimba hiyo imechoropoka katika mazingira ambayo yalitaka kuutoa uhai wake.

Chanzo makini ambacho ni ndugu wa mwigizaji huyo kilichoomba hifadhi ya jina kilidai kuwa, kweli Wastara alikuwa na mimba lakini haikuwa riziki kwani imechoropoka katika mazingira ya ajabu.

“Baada ya kuzinguana na Sadifa (Khamis Juma) Wastara aliamua kuchukua hamsini zake. Baadaye aligundua amenasa na tulipomuuliza alisema si ya mtu mwingine zaidi ya mumewe Sadifa.

“Sasa, hivi karibuni alikwenda Msumbiji kufanya biashara zake za madini. Akiwa kule, akajiwa na hali f’lani mbaya ambayo ilimuweka kwenye wakati mgumu sana.

“Alichodai ni kwamba mimba imemsumbua sana na nusura imuue, tukamuuliza ameamua kuitoa au imetoka yenyewe? Hakutujibu chochote,” alisema mtoa habari huyo na kuongeza:

“Siku chache baadaye alinitumia SMS na kuniambia anamshukuru Mungu anaendelea vizuri. Hata alipotua Bongo, sikumsikia tena akizungumzia habari ya mimba na hata kwa kumuangalia tu ilionesha kwamba imechoropoka.

IJUMAA LAMSAKA WASTARA

Baada ya kunasa ubuyu huo, Jumatatu iliyopita, Ijumaa lilifanya jitihada za kumsaka Wastara kupitia simu yake ya kiganjani lakini mara kadhaa ilikuwa ikiita bila kupokelewa.

Siku iliyofuatia paparazi wetu alimpigia tena. Pia haikupokelewa na baadaye msanii huyo akatuma SMS aliyoandika ‘tuma meseji’.

Ijumaa: Mimi ni Mwandishi wa Ijumaa, naitwa (mwandishi anajitambulisha), kuna habari kuwa mimba yako ambayo ilikuwa inadaiwa ni ya aliyekuwa mumeo imetoka, kuna ukweli wowote?

Wastara: Nani kawaletea hizo habari?

Ijumaa: Ni vyazo vyetu, tukaona ni busara kukuuliza wewe ili kupata ukweli.

Wastara: Jamani niseme tu kwamba napitia kipindi kigumu sana kwa hiyo naomba uniache.

Ijumaa: Kipindi gani kigumu? Au ndiyo kutokana na mimba hiyo kuchoropoka?

Wastara: Hujui niko kwenye hali gani, kwa hiyo niache, muda wa kulizungumzia hilo ukifika nitasema.

Chanzo:GPL

Wema Afunguka baada ya Kuchoshwa na Majungu ya Watu

0
0
Msanii wa filamu nchini Wema Sepetu ameonesha kuchoka na maneno mbalimbali kutoka kwa watu hususani kwenye mitandao ya kijamii kiasi cha kuamua kutoa yake ya moyoni kwa watu wote ambao wamekuwa wakimfuatilia maisha yake.

Ameonesha kukasirishwa na baadhi ya watu wanaomsema kwenye mitandao ya kijamii hususani kuhusu mapungufu yake.

Wema Sepetu ametumia mtandao wake wa Instagram kuweka ujumbe mrefu kwa watu hao, huku akiwataka wamuache aishi maisha yake kwani hajawahi hata siku moja kwenda kuomba msaada kwao, na kusema hata siku atakapokufa atakufa mwenyewe na kama ni majibu kwa Mungu atajibu mwenyewe.

"Naomba niseme kitu na nieleweke tafadhalli, sijawahi hata siku moja kwenda kwa hata mmoja wenu na kumgongea kuomba hata hela ya chumvi. Maisha yangu yananihusu mimi na hata siku nikifa nakufa mwenyewe, majibu kwa Mungu naenda kujibu peke yangu. Niacheni jamani nimechoka" aliandika Wema Sepetu

Mbali na hilo Wema Sepetu amewataka watu ambao wanakereka na aina ya maisha ambayo yeye anaishi waache kuyafuatilia kwani si lazima kufuatilia kile akifanyacho au maisha anayoishi yeye.

 "Kama nakukera na maisha yangu basi usiyafuatilie siyo lazima. Nisiheme sasa jamanii. Naomba tafadhari kama mapungufu ni ya kwangu mimi. Niacheni mimi nafanya kile kinachoridhisha nafsi yangu maana sipendi kujikasirisha. Kwani nikitajirika mimi au nikiwa masikini wewe unapata faida gani. Jiulize kwanza hilo swali ndiyo uanze kutoa maneno yako" alisema Wema Sepetu

Kama Ulikuwa Unajiuliza Wanawake wa Mjini Wanaishije Bila Kazi na Huku Wanamaisha Mazuri Soma Hii

0
0
Msichana akitaka PERUVIAN HAIR mpya wala
hahangaiki sana...Anaingia kwenye PHONEBOOK yake
anachagua Madanga yake 20 anayoyaamini kwamba
hayawezi kumuangusha...AnaCOMPOSE Meseji
Tamuuu ambayo kila danga likipokea linahisi hiyo ni
Meseji yake peke yake. "Babe Mambo,Nimekumiss leo hadi nimekuota yaani
nimeamka So Wet I really miss my Pompolimpo,pole
na kazi mme wangu I wish I was there nikumassage
na Ulimi hadi usinzie..Leo Niko zangu tu home sijatoka
nlikuwa naangalia Muvi mara LUKU imekata hapa na
sina hata Salio.Una Sh 30,000 unitumie ninunue Luku babe wangu?Please maana kutoka mpaka ATM saa
hizi usiku.Love you xoxoxo"
Akimaliza Anatengeneza BROADCAST LIST
anawaweka yale Madanga humo halafu anatafuta
Option inaitwa SEND TO MANY,anafowadi lile meseji
TWAAAAP!!Anauchuna kama dakika 5 hivi,meseji za Muamala zinaanza kutiririka kutoka Ukonga mpaka
Tegeta,Sinza mpaka Makongo Juu
"Imethibitishwa umepokea 30,000 kutoka kwa Rajabu
Kistuli"
"Imethibitishwa umepokea 32,000 kutoka kwa Justine
Kipipa" Nusu saa tu kashakusanya LAKI 6 kesho yake
anaamka anaenda dukani kwa @heavenhairtz @
heavenhairtz
anaagiza Peruvian yake ya Inchi 6 jioni unamkuta
NEWS CAFE anawaka huku anakunywa Milkshake ya
Vanilla. We unabaki kujiuliza Demu wa 1st year ana iPhone 6s
kaipata wapi na Bodi ya Mikopo haijaingiza
BOOM,wenzio wana MABOOM BINAFSI wanaCLICK tu
hela kibwena.
Demu akiamua Kupauka ni Maamuzi binafsi tu,Wana
Mbinu hawa Viumbe Balaa,kufa njaa labda awe Mgoloko wa Tandahimba amekuja juzijuzi na Fuso la
Mafenesi ila watoto wa mjini hawaishiwi!

Sitaki Tena Bongo Movie -Sinta

0
0
Mkali wa zamani wa maigizo, Sinta ambae alitamba na skendo kibao kipindi hicho na unaambiwa yeye ndiyo wa kwanza kuwa na skendo kubwa Bongo,  amefunguka  na kueleza kwa sasa ana ishu gani mjini.

Sinta ambaye alikuwa pia muigizaji mahiri anasema “Kwa sasa sitaki tena kujiingiza katika bongo move najishughulisha na biashara zangu binafsi na nipo katika hatua za mwisho kukamilisha lebo yangu ya wasanii wa bongo fleva.”

Hata hivyo Sinta alimalizia kwa kusema kwa sasa anawaachia machipukizi wanaoibukia katika bongo move nao kufanya vizuri na kusongeza saana ya bongo na pia hataki tena maswala ya skendo za aina yeyote huku akisema kwa sasa anamsimamia msaniianayejulikana kwa jina la Tino ndo ambaye taari yupo katika lebo yake.

eatv.tv

Kijana Mwanza mbaroni kwa kumtukana Rais Magufuli ndani ya Noah

0
0
Mgomo wa daladala Jijini Mwanza umesababisha kijana mmoja Jijini humo kutamka lugha chafu ndani ya gari ambayo alipewa lifti limemsababishia kuishia mikononi kwa sheria.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi akizungumza katika kipindi cha East Africa Breakfast dereva wa wa gari likitoa lifti Hassan Bushagama mkazi wa Buhongwa Jijini Mwanza asema alipofika eneo la Buhongwa akiwa na usafiri wake aina ya Toyota Noah kutokana mgomo wa daladala aliamua kutoa lifti kwa abiria aliowakuta hapo.

"Walipanda watu kama nane ambapo Dada mmoja akasema watu walivyo hawatakawia kusema Rais Magufuli ndiye anatakiwa aulizwe,kijana mmoja wa umri wa miaka kama 27 au 28 hivi akadakia akasema Rais ni '******** 'mzee mmoja akamwambia kijana tengua kauli lakini akakataa na kusisitiza ,abiria wakataka kumpiga nikawaambia mwacheni tumpeleke 'polisi " Amesema Bwana Bushagama.

Bushagama ameendelea kusema kwamba "Baada ya hapo niliendesha gari langu hadi kituo cha polisi tulipofika pale nikawaambia polisi hali halisi askari akawahoji abiria wakaelezea hali hiyo na yeye alipoulizwa akasema ,amesema hivyo lakini hakujua kama ingepelekea kufika huko.

Aidha Bushagama ameongeza kuwa wameamua kusitisha kazi zao na kuonesha uzalendo ili kuonesha kwamba Rais hawezi kutukanwa namna hiyo.

Kwa upande wake Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Mwanza Ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kwama kijana huyo amejitetea na kusema kwamba alisema alimaanisha wanaogoma wanajifanya wapumbavu lakini Rais ni ******** zaidi yao jambo liliwakasirisha wenzake na kuamua kumfikisha kituo cha Polisi.

Kamanda ameongeza kuwa suala hilo tayari limefikishwa Polisi kitachoendelea ni ushahidi ukitosheleza kijana huyo atapelekwa mahakamani.
Viewing all 104431 articles
Browse latest View live




Latest Images