Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

Vanessa Mdee Afungukia Bata Walizokula Singita Hoteli....

$
0
0
Wanamuziki, Vanessa Mdee na mpenzi wake Juma Jux ‘Jux’ baada ya manenomaneno kuzagaa kuwa wameachana juzikati wapenzi hao walionekana kwenye mbuga ya wanyama ya Serengeti iliyopo mkoani Mara kisha kwenda kula bata kwenye hoteli ya bei mbaya ya Singita.

Akipiga stori na safu hii juzi akiwa Serengeti, Vanessa alisema kuwa, wameamua kwenda huko kwa mapumziko ya siku nne ikiwa ni sehemu ya kufanya utalii wa ndani na wamekula bata za kutosha.

“Ni mambo ya utalii wa ndani, tumekuja huku kupumzika kidogo, siyo lazima kwenda nchi za nje kwa mapumziko, humuhumu Bongo kuna sehemu unakwenda na unajisikia furaha,” alisema mwanadada huyo.

Singita ni hoteli ya kifahari iliyopo mkoani Mara ambayo inaiingizia nchi fedha nyingi za kigeni.

Nina Furaha Toka Nitoke CCM - Edward Lowassa

$
0
0
Lowassa kupitia ukurasa wake wa Facebook ameelezea furaha yake namna ambavyo ameimarika zaidi baada ya kujitoa ndani ya CCM hadi sasa ambapo ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA.

''Nina furaha kutimiza mwaka mmoja toka nilipojitoa CCM na kujiunga na CHADEMA.Uamuzi ule haukuwa rahisi,lakini kwa ushupavu, ujasiri na mwongozo wa Mungu nilifanya hivyo. Nilifanya uamuzi wa kihistoria katika nchi yetu'' Amesema Lowassa.

Ameongeza kuwa watanzania bado wanataka mabadiliko na hali hiyo imezidi kuthibitika kuwa wananchi hawawezi kuyapata ndani ya CCM .

Amesema watanzania wanataka sera na mtu mbadala wa kuongoza mabadiliko hayo na kwamba vyote hivyo watavipata ndani ya CHADEMA na UKAWA kwa jumla.

Aidha amewataka watanzania wanaomuunga mkono na ambao walihama CCM kwa ajili yake waendelee kumuunga mkono na kuiunga mkono CHADEMA.

Koffi Olomide aachiwa baada ya kuwekwa kizuizini kwa saa 24

$
0
0
Baada ya Koffi Olomide kukamatwa Jumanne July 26 2016 nyumbani kwake Kinshasa kwa tuhuma za kumshambulia dancer wake wa kike wakati wakiwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyata Nairobi na baadaye ikawa imeripotiwa kuwa amehukumiwa kwenda jela miezi 18 na adhabu hiyo kutajwa kuwa haitakuwa na faini.

Taarifa zilizoripotiwa ni kwamba Koffi Olomide kaachiwa huru baada ya kutumikia kifungo cha siku mbili kati ya miezi 18 aliyohukumiwa awali, BBC imeripoti kuwa kuachiwa kwa koffi Olomide kumekuja baada ya Mahakama ya Kinshasa kusema kuwa hawakuona sababu za kutosha za kuhukumiwa kwa Koffi Olomide kutokana na tukio alilofanya JKIA.

Pamoja na baadhi ya vyombo vya habari Afrika kuripoti kwamba Koffi alihukumiwa kifungo cha miezi 18 jela , Promoter wake wa nchini  Kenya Jules Nsana amekanusha madai hayo  na kusema  kesi dhidi ya Koffi ilikuwa bado iko kwenye uchunguzi na kwamba baada ya uchunguzi wamebaini hakuna ushahidi wa kutosha wa kumtia hatiani Koffi Olomide.

Promoter Jules amesema Olomide alimpigia simu akamtaka aombe msamaha kwa wakenya wote kwa niaba yake…..

’Koffi alinipigia mwenyewe baada tu ya kuachiwa na akaniomba niombe msamaha kwa wakenya kwa niaba yake, tumpe siku mbili, tatu atazungumza mwenyewe’

Mfanyabiashara Mohamed Dewji Apigia Simba Magoti Awaomba Muuzie Timu

$
0
0
Mfanyabiashara Mohamed Dewji aongea na wanahabari. Aiomba Klabu ya Simba imuuzie asilimia 51 ya hisa kwa bilioni 20 ili alete mafanikio. “Kama unataka mafanikio kwenye mpira, hakuna zaidi ya fedha. Simba haiwezi kuwa na miaka 80 leo haina hata uwanja wa mazoezi. Alisema Dewji

Amesema bajeti ya Yanga na ile ya Azam FC ni mara mbili ya ile ya Simba, jambo linaloifanya klabu hiyo kuendelea kubaki kuwa msindikizaji.

Navy Kenzo Wala Shavu Jingine la Ubalozi wa Kampuni ya KLOBAA...Kukinukisha Kesho Jumamosi Viwanja vya Posta Sayansi...

$
0
0
Kwa Wale Mnaosikia Kuhusu Klobaa na Hamjui Maana yake , Klobaa ni Application ya simu ambayo inahusika  kuwakutanisha watumiaji wa hiyo App na sehemu mbali mbali za burudani za usiku kama Clubs na lounges pamoja na matukio mbali mbali ya burudani...
Kampuni hii ya Klobaa iliundwa Mwaka 2015 huko US na sasa tunayofuraha kuwa imesajiliwa kufanya biashara hapa Tanzania pia..

Dhumuni letu kubwa ni kuwakutanisha wapenda starehe , watalii pamoja na watu wa kawaida  sehemu moja ambayo watafurahia kwa pamoja na kuondoka wakiwa wameridhika na huduma, Sehemu hizo ni kama Club za usiku, Lounges, Baa, Migahawa, matamasha na vivutio vya utalii
Kwahiyo tunaweza sema Klobaa si tu ni Application ya simu lakini ni mtindo wa maisha ya kila siku
Klobaa App Kwa mara ya Kwanza inazinduliwa Tanzania Kesho Tarehe 30 July 2016 Hapa Dar es salaam Viwanja vya Posta Sayansi, Uzinduzi huo utaambatana na Tamasha Kubwa la Music Ambalo litahusisha wasanii Wakubwa hapa Tanzania na Kenya Wakiwemo Navy Kenzo , Ali Kiba , Sauti Soul , Christian Bella na Wengine Wengi

Kama wote mlivyosikia Tamasha Hilo ambalo limepewa Jina la "MWENDO KASI Festival" litakuwa la kwanza Africa lakini tutaendelea kufanya matamasha mbali mbali East Africa na Kwinginepo Afrika ili kuunganisha utamaduni wa kiafrika , Utalii na burudani
Kama njia ya Kurudisha Kwa jamii Klobaa miezi kadhaa ijayo inampango wakutoa Misaada kwa Vijana Kwa Kuwalipia ada baadhi ya Vijana waweze kusoma Elimu ya Juu hasa wale wasio na uwezo wa kujisomesha

Pia Tutakuwa tukifanya matamasha mbali mbali ya kuinua vipaji kwa wasanii na kuwasaidia kufanya kazi zao kupitia njia sahihi zitakazo wafikisha mbali zaidi...

Tunayofurahi Kuwatangazia Watanzania kuwa tumeamua Kuwachukua Kundi la mziki la Navy Kenzo Linaloundwa na Aika Marealle na Nahreel Kuwa wawakilishi wa Application ya KLOBAA Tanzania, Tumekuwa tukiwafatilia Navy Kenzo kwa muda mrefu na tumefurahishwa na maendeleo yao kimuziki kila siku zinavyoenda , Navy Kenzo Ambao kwa sasa wanamiliki Lebo ya Muziki ya The Industry wameonyesha mwamko mkubwa katika kukuza muziki wa Tanzania hivyo kufanya nao kazi imekuwa furaha yetu kubwa kwa kuwa tutafanya kazi na watu wanaojielewa katika ulimwengu wa burudani

Tunatumaini Huu ushirikiano kati ya Navy Kenzo na KLOBAA utatujenga wote kwa pamoja katika kutoa huduma nzuri kwa jamii Kwa ujumla hapa Tanzania na Kwinginepo Afrika....
Mwisho Kabisa Tunawakaribisha Kesho Kuja Kufurahi na sisi katika tamasha la Muziki la Mwendo Kasi Festival litakalofanyika Viwanja vya posta Kijitonyama kuanzia saa nane Mchana....


Wasanii Watakao Kuwepo Kwenye Tamasha hilo ni :
Navy Kenzo
Juma Nature
Ali Kiba
Sauti Soul
Manfongo
Christian Bella
Mr Blue
Isha Mashauzi
Roma
Nay wa Mitego
Joh Makini
G Nako
Nuh Mziwanda
Quick Rocka
Ruck Beiby




Lowassa Akoleza Moto CCM, Awata Wanaomuunga Mkono Ndani ya CCM Waendelee Kumpa Siri za Serikali

$
0
0
Aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema na Ukawa, Edward Lowassa ana uhakika kuwa bado kuna wanachama wanaomuunga mkono ndani ya CCM na sasa anawataka waendelee kushikamana naye, kauli ambayo inaweza kuchochea moto ndani ya CCM.

Katika taarifa yake fupi kwa vyombo vya habari aliyoitoa jana, Lowassa amewahakikishia wananchi kuwa kwa sasa ana “ari, nguvu na hamasa kuliko wakati mwingine wowote”.

Lowassa, ambaye alikuwa waziri mkuu wa kwanza wa Serikali ya Awamu ya Nne, alijiondoa kwenye chama tawala Julai 28 mwaka jana baada ya jina lake kuondolewa kwenye orodha ya wagombea urais kwa tiketi ya CCM.

Kuondoka kwake kulisababisha mawaziri wa zamani, wabunge, wenyeviti wa mikoa, madiwani na wanachama wengine wa CCM, wakiongozwa na waziri mwingine mkuu wa zamani, Frederick Sumaye kukihama chama hicho, hali iliyosababisha ushindani kuwa mkubwa kwenye Uchaguzi Mkuu uliopita, huku CCM ikilalamikia kusalitiwa.

Wakati CCM ikifikiria hatua za kuchukua dhidi ya wasaliti wa chama wanaotuhumiwa kuunga mkono harakati za upinzani wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopita, Lowassa ameongeza petroli kwenye moto ulioanza kuwaka.

“Kwa wale wenzangu waliobaki CCM na wanaoniunga mkono, tuendelee kushikamana na kunipatia taarifa kwa hatima ya nchi yetu,” amesema Lowassa ambaye kwa sasa ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema.

“Nawashukuru Watanzania kwa kuendelea kuniunga mkono mimi na wenzangu ndani Chadema.”

Kauli hiyo kuwa kuna watu ndani ya CCM ambao wanampatia taarifa mbunge huyo wa zamani wa Monduli na ombi lake la kutaka waendelee kumpa taarifa, inaweza kusababisha hali ngumu zaidi kwa chama hicho, ambacho kinaamini kuwa makada wake walikihujumu wakati wa uchaguzi kwa kumfanyia kampeni kisiri.

Katika uchaguzi huo, Rais John Magufuli alishinda kwa kupata asilimia ndogo ya kura kulinganisha na watangulizi wake.

Ingawa alipata kura milioni 8.8 na Lowassa kufuatia kwa kupata kura milioni 6.07, ushindi huo ni wa asilimia 58.46 dhidi ya asilimia 39.67 kulinganisha na ushindi wa asilimia 61.17 aliopata Kikwete mwaka 2010 dhidi ya asilimia 26.34 alizopata Dk Willibrod Slaa wa Chadema.

Tangu Januari mwaka huu, CCM imekuwa ikijadili wasaliti hao katika ngazi ya wilaya na taarifa za mapendekezo ya hatua dhidi yao kutumwa Halmashauri Kuu kwa ajili ya uamuzi wa mwisho.

Katika hotuba yake ya kuaga, Jakaya Kikwete alimkabidhi mwenyekiti mpya wa CCM, Rais Magufuli ripoti ya hali ilivyokuwa kwenye uchaguzi, akisema yeye ndiye atakayeamua adhabu dhidi ya wale wote walioonekana kufanya makosa. CCM imeshasema kuwa wasaliti wote ni lazima washughulikiwe.

Katika taarifa yake ya jana, Lowassa ameeleza kuwa uamuzi alioufanya wa kuihama CCM na kujiunga na Chadema “haukuwa rahisi, lakini kwa ushupavu, ujasiri na mwongozo wa Mungu nilifanya hivyo” na kwamba huo ni “uamuzi wa kihistoria katika nchi yetu.

“Najivunia kwa uamuzi ule, kwani umewafungua macho Watanzania wengi na kuimarisha demokrasia. Nimeingia Chadema nimewakuta viongozi na wanachama walio na moyo wa dhati wa kuliletea maendeleo Taifa lao kivitendo,” anasema Lowassa katika taarifa yake fupi.

“Watanzania bado wanataka mabadiliko na imezidi kuthibitisha kuwa hawawezi kuyapata ndani ya CCM. Watanzania wanataka sera na mtu mbadala wa kuongoza mabadiliko hayo. Vyote hivyo watavipata ndani ya Chadema na Ukawa kwa jumla.”

Walimu 4 wamvua nguo na kumchangia viboko binti wa Kidato cha IV Mbeya huku Mwalimu Mwingine Akimtomasa Sehemu za Siri

$
0
0
VITENDO vya ukatili wa kijinsia na dhuluma dhidi ya watoto wa kike vimekuwa vikishamiri kila siku pamoja na kuwepo kwa taasisi za kutetea haki za wanawake  na kuanzishwa kwa madawati ya Kijinsia kwenye vituo vya polisi nchini.

Msichana wa kidato cha Nne mwenye umri wa miaka 17,(jina tunalo) anayesoma shule moja ya sekondari ya Kata mkoani Mbeya amekumbwa na kadhia ya kuvuliwa nguo zake za ndani na kucharazwa bakora zisizo na idadi na walimu wanne wa shule hiyo.

Tukio hilo ambalo limeripotiwa katika kituo kidogo cha  Polisi Mbalizi wilaya ya Mbeya kwenye jalada la uchunguzi namba MBI/IR/967/2016 na kuwekwa kwenye taarifa yenye namba MBI/RB/2653/2016 linadaiwa kuwahusisha walimu wanne akiwemo Mkuu wa shule hiyo pamoja na walimu watatu.

Akizungumza huku akiwa na maumivu makali katika Hospitali Teule ya Ifisi ambako amelazwa akipatiwa matibabu, mwanafunzi huyo alisema kuwa aliitwa na mwalimu wa nidhamu aliyemtaja kwa jina la Neema Mwaikenda aliyekuwa pamoja na Mkuu wa shule hiyo aliyemtaja kwa jina la Mariamu Mwanisenga na mwalimu wa kiume aliyemtaja kwa jina la Adili.

Alisema walimu hao walianza kumuadhibu kwa viboko visivyo na idadi huku akiwa amechojolewa nguo zake ambapo mwalimu wa kiume aliyemtaja kwa jina la Adili akaanza kumshikashika sehemu zake za siri.

‘’Wakati naadhibiwa na walimu wote, huyu mwalimu wa kiume alianza kunishika  huku chini,na kunitaka niwataje wanaume zangu,nikawa nabana miguu wakazidi kunishambulia kwa vibao na mateke na fimbo,’’alisema mwanafunzi huyo.

Alisema sababu zilizosababisha aadhibiwe ilikuwa ni utoro na kuwa siku moja alipokuwa shuleni alioneshwa na walimu fimbo na kuelezwa kuwa fimbo hizo zitamuishia mwilini ndipo akaogopa kufika shuleni kwa siku tatu.

Anafafanua kuwa siku aliyofika shuleni ndipo alipokutana na kadhia ya kupigwa na walimu wanne hadi  alipowaponyoka walimu hao na kukimbilia mitaani na kujificha.

‘’Niliwaponyoka walimu nikakimbilia kwenye nyumba ya jirani na shule nikajificha hadi jioni na baadaye kwenda nyumbani, kesho yake mama na dada walinichukua na kunileta hospitali,’’alisema.

Mwandishi wa habari hizi alifika shuleni anakosoma mwanafunzi huyo kwa nia ya kukutana na uongozi wa shuleni hiyo ambapo Makamu Mkuu wa shule hiyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Mwansanga alikataa kuelezea chochote.

‘’Mie sijui lolote kwanza mie sio msemaji wa shule, kwahiyo sijui lolote juu ya taarifa mnazohitaji,’’alijibu Makamu Mkuu wa shule na kuondoka zake.

Kwa upande wake Ofisa Elimu wa Mkoa Charles Mwakalila alisema kuwa adhabu aliyopewa mwanafunzi huyo ni kubwa kupitiliza kwa kuwa zipo taratibu za adhabu kulingana na makosa na kuwa mwanafunzi anapaswa kupigwa viboko vitatu na viboko visivyozidi sita au adhabu mbadala.

‘’Adhabu aliyopewa ni kubwa, tutafuatilia na waliokiuka taratibu watachukuliwa hatua za kinidhamu,’’alisema Mwakalila.

Naye Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mbeya Dhahiri Kidavashari alipoulizwa juu ya tukio hili alidai kuwa halijafika ofisini kwake na kuwa kwa sasa yeye yupo kikazi wilayani Chunya na mara atakapofika ofisini atafuatilia na kuchukua hatua za kisheria kwa wahusika wa tukio hilo.

Awali Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya Mariamu Mtunguja ambaye alifika Hospitalini alikolazwa mwanafunzi huyo alisema kuwa amemuangalia mwanafunzi huyo na kuona namna ambavyo damu imevilia kwenye sehemu zake za makalio na kwenye mapaja.

Mtunguja alisema kuwa kitendo kilichofanywa na walimu hao ni cha kinyama ambacho hakipaswi kuvumiliwa na kuwa mara itakapobainika atahakikisha walimu hao wanachukuliwa hatua za kinidhamu.

Muuguzi Mkuu Msaidizi wa Hospitali Teule ya Ifisi Elimati Sanga alisema kuwa mwanafunzi huyo alifikishwa hospitalini hapo Julai 21 saa 7:00 mchana ambapo alipatiwa matibabu na kulazwa kutokana na majeraha na damu iliyovilia mwilini sehemu za makalio na mapaja.

‘’Ameshambuliwa sehemu za mapaja, damu na masikio yake hasikii vyema kutokana na kipigo, anaendelea na matitabu hapa hospitali,’’alisema Sanga.

Faiza Ally na Wema Sepetu Ndani ya Bifu Nzito

$
0
0
MTIFUANO wa maneno makali umeibuka kati ya wasanii wa fi lamu Bongo, Wema Sepetu na Faiza Ali chanzo kikiwa ni Faiza kuposti maneno ya ‘kumdis’ Wema kutokana na mfumo wake wa maisha ya kimapenzi.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Faiza aliandika kuwa Wema anapenda sana ‘ving’asti’ (dogodogo) akitolea mfano Idris Sultan aliyekuwa mpenzi wake, kisha akasema kuwa anaomba Mungu asije akapata mtoto wa kiume atakayependa ku-date na wanawake waliomzidi umri.

Kutokana na maneno hayo yaliyojaa shari ndani yake, Ijumaa lilimtafuta Wema kuzungumzia posti hiyo ambapo alipopatikana alikuwa na haya ya kusema: “Yaani mimi simpendi kabisa yule binti, namuona ni mpumba** tu, ndiyo maana hata Sugu akaona si mwanamke anayefaa kuwa mkewe. Hana akili kabisa.”

By Imelta, Global Publishers

Professor Jay: Kutokujua kimombo si dhambi

$
0
0
Msanii wa muziki wa Hip Hop na mbunge wa Mikumi, Professor Jay amesema kuwa kutokujua Kiingereza siyo dhambi.

Rapper huyo kwa sasa anakiki na wimbo wake mpya ‘Kazi Kazi’ aliomshirikisha msanii wa nyimbo za visingeli, Sholo Mwamba. Akiongea na kipindi cha Hatua Tatu cha Times FM, Professor Jay alisema, “Hii sijui kiingereza, Kiingereza ni Kushoboka tu. Viongozi wengi mbona tunaona wanakuja hapa Tanzania hawajui Kiingereza.”

Aidha kiongozi huyo ameongeza kuwa kwa wasanii mameneja ndio wanapaswa wajue lugha hiyo ili wawe kama wakalimani kwa wasanii wao.

Bongo5

Rais Magufuli Atoa ONYO Kali....."Mimi sijaribiwi, wasije kunijaribu. Atakayeleta vurugu atashughulikiwa bila huruma!

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 29 Julai, 2016 ameanza ziara ya siku nne katika mikoa ya Singida, Tabora, Shinyanga na Geita akitokea mkoani Dodoma, ambapo amezungumza na wananchi kwa lengo la kuwashukuru kwa kumpigia kura katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana  na kueleza juhudi zinazofanywa na serikali katika kutatua kero za wananchi na kuwaletea maendeleo.

Akiwa Mkoani Singida, Rais Magufuli aliyeongozana na mkewe Mama Janeth Magufuli amewasihi watanzania kufanya kazi kwa juhudi na kujiepusha na vitendo vya vurugu vinavyohamasishwa na baadhi ya wanasiasa huku akionya kuwa serikali yake haitamvumilia mtu yeyote ambaye atathubutu kuchochea vurugu ikiwemo maandamano kinyume cha sheria.

“Sitaki nchi hii iwe ya vurugu, watakaoleta vurugu mimi nitawashughulikia kikamilifu bila huruma, na wasije wakanijaribu, mimi ni tofauti sana na kama wapo watu wanaowatumia wakawaeleze vizuri, mimi sijaribiwi na wala sitajaribiwa.

“Wananchi hawa wana shida, na siasa nzuri ni wananchi washibe, siasa nzuri ni wananchi wetu wapate dawa” Amesema Rais Magufuli.

Kuhusu hatua mbalimbali zilizochukuliwa na Serikali yake ya awamu ya tano tangu aingie madarakani Rais Magufuli ametaja baadhi ya  hatua hizo kuwa ni kufuta ada kwa shule za msingi na sekondari, kutoa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu zaidi ya laki moja na kuongeza fedha za miradi ya maendeleo katika bajeti ya serikali kutoka asilimia 26 ya mwaka 2015/2016 hadi kufikia asilimia 40 katika bajeti ya mwaka huu 2016/2017.

Hatua nyingine ni kuondoa wafanyakazi hewa 12,500 katika orodha ya waliokuwa wanalipwa mshahara na serikali, kudhibiti upotevu wa mapato serikalini, kutenga shilingi Trilioni moja kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Reli ya kati kwa kiwango cha kisasa yaani Standard gauge na pia akazungumzia hatua zilizochukuliwa dhidi ya wala rushwa na wanaojihusisha na ufisadi kwa kuunda mahakama ya mafisadi huku akiapa kuwa katika kipindi chake hakuna fisadi atakayeendelea kutamba.

Akiwa njiani Rais Magufuli amewasalimu wananchi wa Ikungi na baadaye amefanya mkutano wa hadhara Singida Mjini ambako amesisitiza kuwa serikali yake haiko tayari kumvumilia mtu yeyote atakayekwamisha utekelezaji wa Ahadi na Ilani ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Singida

29 Julai, 2016

Trafiki Wakusanya Milioni 320 Kwa Siku Nne DSM

$
0
0
Jeshi la Polisi Kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Dar es Salaam limekusanya shilingi milioni 320.2 ambapo fedha hizo ni kutokana na tozo za makosa ya usalama barabarani.

Askari wa kikosi cha usalama barabarani Jijini Dar es salaam akiwa kazini.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Kamanda wa wa polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Simon Sirro amesema fedha hizo ni kutokana na makosa 10,676 ambayo yamefanywa na watumiaji wa vyombo vya moto.

‘’Toka tarehe 25 hadi tarehe 28 tumefanikiwa kukusanya kiasi nilichotaja ambapo makosa mengi ya madereva wa bodaboda tumeanza kuona kwamb tunapowatoza faini ya elfu 30 au 60 haiwapi fundisho lolote ndiyo maana tumekuwa tumekuwa tukiwapeleka mahakamani ili kupunguza matukio ya uvunjifu wa sheria barabarani’’ Amesema Kamanda Sirro

Aidha Kamishna Sirro ametumia wasaa huo kuwataka watanzania kutii sheria bila shurti wanapokuwa wanatumia vyombo vya moto barabarani na katika maeneo yao ya kuishi.

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumamosi ya July 30, Ikiwemo ya Mpambano wa Magufuli na Chadema

$
0
0


SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumamosi ya July 30, Ikiwemo ya Mpambano wa Magufuli na Chadema

Rais Magufuli: Chadema Msiwape Vijana Viroba Ili Watangulie Kwenye Maandamanmo....Tangulieni Ninyi Viongozi Wao Ili Mkione Cha Mtema Kuni

$
0
0
Juzi Chama cha Demokrasia na maendeleo ‘CHADEMA’ kilitangaza mikakati mitatu ya kupinga ilichokiita ukandamizaji wa haki na demokrasia na kuitangaza siku ya September mosi mwaka kuwa ni siku ya maandamano nchi nzima.

Jana July 29 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alianza ziara ya siku nne katika mikoa ya Singida, Tabora, Shinyanga na Geita akitokea mkoani Dodoma, ambapo alizungumza na wananchi  wa Manyoni Singida na kutoa onyo kwa watakaoanzisha maandamano.

"Wasije wakanijaribu mimi ni tofauti sana, na kama wapo watu wanawatumia wakawaeleze vizuri mimi sijaribiwi na wala sitajaribiwa, siasa nzuri wananchi wetu washibe, wapate madawa, nataka hao wanaotetea maandamano watangulie wao halafu wataona cha mtemakuni"- Alisema Rais Magufuli

Hapa chini ni sauti ya Rais Magufuli sehemu ya kwanza na ya pili. Msikilize.

Sehemu ya Kwanza: Sehemu ya Pili:

Majengo ya Serikali Dar es Salaam kupigwa mnada ili wale wasiotaka kuhamia Dodoma, wahame kwa lazima

$
0
0
WAKATI suala la serikali kuhamia mkoani Dodoma likiwa dhahiri zaidi kila siku moja inayoongezeka, Rais John Magufuli ametangaza kuuza majengo ya wizara Dar es Salaam, mara atakapohamia yeye katika makao makuu hayo ya nchi.

Akizungumza jana kwenye mkutano wa hadhara mkoani Singida, katika siku ya kwanza ya ziara yake itakayomfikisha mikoa minne, Rais Magufuli alisema atahakikisha anauza baadhi ya majengo hayo kwa mnada, ili wale wasiotaka kuhama, wahame kwa lazima.

Mbali na Singida, mikoa mingine atakayotembelea katika ziara hiyo aliyoanza jana ni Tabora, Shinyanga na Geita, ambako atazungumza na wananchi katika mikutano ya hadhara.

Katika mikutano hiyo, Rais Magufuli anatarajiwa kushukuru wananchi kwa kumpigia kura katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, na kueleza juhudi zinazofanywa na serikali kutatua kero zao na kuwaletea maendeleo.

Majengo mazuri
Katika tangazo hilo, Rais Magufuli amesema majengo atakayoanza nayo, ni yale yanayotazama bahari; ambayo ndiyo mazuri zaidi, yenye mwonekano mzuri kutoka ofisini.

“Atakayeng’ang’ania kubaki huko, ajue hana kazi wala mshahara. Hatuwezi kuendelea kukaa miaka hamsini tunaimba tu kuhamia Dodoma, wakati hatutekelezi uamuzi wetu hadi wengine wameshatangulia mbele za haki,” alisema.

Alisema anajua akiitisha zabuni ya ofisi hizo, wateja watayakimbilia kwa wingi, hivyo wataong’ang’ania kubaki Dar es Salaaam, watakuwa wamejifukuzisha kazi wenyewe.

Uamuzi huo wa serikali kuhamia Dodoma japo ni wa siku nyingi na utekelezaji wake ulikuwa ukifanyika kidogokidogo kwa baadhi ya wizara na ofisi nyeti kujenga majengo yake katika mji huo, lakini hivi karibuni umepata kasi ambayo haijawahi kupatikana, baada ya Rais Magufuli kutangaza kuhakikisha serikali yote inahamia Dodoma kabla ya 2020.

Tamko hilo la Rais Magufuli lililotolewa wakati wa Mkutano Mkuu wa CCM wiki iliyopita na kurejewa katika Sikukuu ya Mashujaa mwanzoni mwa wiki hii, liliungwa mkono mara moja na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, ambaye alitangaza kuharakisha umaliziaji wa ujenzi wa nyumba yake, ili ahamie katika mji huo Septemba mwaka huu.

Wizara zenyewe
Baadhi ya mawaziri waliohojiwa na vyombo mbalimbali vya habari, walikaririwa wiki hii wakisema kuwa suala hilo halina mjadala ni la kutekeleza mara moja.

Mbali na waliohojiwa, mawaziri na watendaji wakuu wengine serikalini, walitangaza muda maalumu kwa watendaji wao kuanza kuhamia katika mkoa huo.

Miongoni mwa mawaziri hao, ni pamoja Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Charles Tizeba, ambaye naye wiki hii alikutana na vyombo vya habari na kutangaza kuwa baadhi ya watendaji wa wizara hiyo, wataanza kuhamia Dodoma kuanzia wiki ijayo.

Dk Tizeba alikaririwa akisema tayari watendaji wa wizara hiyo wanaotakiwa kuhamia Dodoma wameanza kufanya maandalizi ya safari.

Wakati Tizeba akitajwa kuwa waziri atakayewahi kuhamia pamoja na wizara yake Dodoma, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa, naye alitaja utaratibu wa kuhamia Dodoma.

Profesa Ntalikwa aliwataka wakuu wa idara na vitengo wote wa wizara hiyo, kuanza maandalizi ya kuhamia Dodoma na kuwa wametekeleza agizo hilo ifikapo Septemba, mwaka huu, muda ambao Waziri Mkuu naye anatarajiwa kuwa Dodoma.

Agizo hilo la Wizara ya Nishati na Madini, liliwekwa katika waraka uliotolewa na watendaji na nakala yake kutumwa pia kwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.

Madalali viwanja
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana jana alipiga marufuku uuzaji wa viwanja ndani ya mji wa Dodoma, baada ya kubaini kuwepo kwa kundi la madalali kutoka mikoa mbalimbali ikiwemo kutoka Dar es Salaam kuhamia katika mji huo.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari Rugimbana alisema amepiga marufuku uuzaji huo mpaka baada ya siku 14 baada ya Waziri Mkuu kuhamia Dodoma, wakati Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA), ikishirikiana na kikosi kazi kilichoundwa na serikali chini Ofisi ya Waziri Mkuu, watakapotoa utaratibu.

Alisema kumezuka kundi la madalali kutoka mikoa mingine walioanza biashara ya viwanja na mashamba bila kufuata utaratibu na kanuni, hivyo uongozi wa mkoa wamezuia suala hilo, kwani linaweza kuvuruga na wananchi watakaotoa viwanja kwa madalali hao itakuwa imekula kwao.

Lengo la serikali kwa mujibu wa Rugimbana, ni kuhakikisha kila Mtanzania mahali alipo anaweza kupata kiwanja huko alipo. Rugimbana alisema mji wa Dodoma ulipangwa siku nyingi; kila eneo na matumizi yake ya ardhi hivyo kuwataka wanaotaka kununua ardhi kuwa makini, ili wasiuziwe maeneo ya makaburi au masoko.

“CDA watafanya kazi vizuri na Mtanzania yeyote anayeweza kununua eneo huko alipo bila ya kuja Dodoma na atakuja hapa wakati wa kukabidhiwa hati na kiwanja,” alisema.

“Ndani ya siku 14 tutatoa maelekezo namna ya kupata viwanja Watanzania wawe watulivu utaratibu mzuri unakuja na hakuna Mtanzania ambaye anataka kujenga Dodoma atakosa kiwanja.

“Mtu anayetaka, asubiri na mfumo utakuwa wazi kwa kila mmoja na utaratibu wa kisheria utafuatwa,” alisema.

Miji miwili
Pamoja na hayo Mkuu huyo wa Mkoa alisema baada ya wizara mbalimbali kuhamia Dodoma, maeneo ya mjini yatakuwa kwa ajili ya biashara na mji wa serikali utakuwa kuanzia Ihumwa hadi Chamwino Ikulu ambapo zitajengwa ofisi za serikali.

Kuhusu ofisi zitakazotumiwa na wizara mara baada ya kuhamia Dodoma mwaka huu, Rugimbana alisema watatumia ofisi zilizopo mjini kabla ya ujenzi katika eneo la Ihumwa ambako kutakuwa na ofisi hizo za muda.

‘’Wizara zikija Dodoma zitaanza kutumia ofisi zilizopo ambazo zilikuwa zikitumika awali kabla ya ujenzi wa ofisi katika eneo la Ihumwa kukamilika,’’ alisema.

Alisema sababu ya kupeleka mji wa kiserikali Ihumwa, ni kuondoa msongamano wa magari kama ilivyo katika jiji la Dar es Salaam.

Alifafanua kuwa kutakuwa na miji miwili; mji wa serikali utakaokuwa Ihumwa na mji wa kibiashara utakaokuwa katika Mji wa Dodoma. Aliwatoa hofu watumishi wa wizara mbalimbali watakaohamia Dodoma kuwa kuna nyumba za kutosha za wao kuishi.

‘’Dodoma tuna nyumba nyingi sana, watumishi hawawezi kukosa nyumba, tutawakodishia hata nyumba binafsi ili waishi,’’ alisema.

Madai: Flora Amwangukia Mbasha

$
0
0
Habari ya mjini ni Mwimba Injili Bongo, Flora Mbasha kudaiwa kumwangukia mumewe waliyetengana, Emmanuel Mbasha kwa kumuomba radhi ndoa yao ichipuke upya kama zamani.
ema-mbashaEmmanuel Mbasha

Kwa mujibu wa mtoa ubuyu ambaye ni muumini wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God Tanzania (EAGT) ‘Mito ya Baraka’, Kariakoo, Dar linaloongozwa na mchungaji Bruno Mwakibolwa, ambalo zamani wawili hao walikuwa wakisali, baada ya jitihada za kurudiana kugonga mwamba, Flora alimfuata mchungaji ili aweze kumsaidia arudiane na mumewe.
“Iko hivi, Flora awali alikuwa mzito kuomba radhi lakini hivi karibuni aliamua kujisalimisha pale kanisani EAGT, akakutana na mchungaji, akamuelezea matatizo yake.

MBASHA3.jpg“Mchungaji alimwambia atalifanyia kazi suala hilo. Akamuita Mbasha (Emmanuel), akamhoji kwa saa tatu, lakini hoja alizozitoa Mbasha, mchungaji mwenyewe alinyoosha mikono na kumwambia awe huru,” alisema mtoa ubuyu huyo akiomba hifadhi ya jina lake.
“Mbasha alifunguka sana. Alimueleza kuwa, Flora alifikia hatua ya kutamka kuwa mchungaji wake ni Gwajima. Sasa iweje leo amuone Mwakibolwa?

“Pia Ima alimueleza mchungaji kuwa, Flora alizaa mtoto na mwanaume mwingine wakati yeye ana matatizo. Flora huyohuyo alikomaa kuhakikisha yeye anafungwa kwa kusimamia ile kesi ya ubakaji.
“Lakini pia, mara baada ya Mbasha kushinda kesi, Flora alienda kukata rufaa japo alishindwa kwa kuchelewa muda wa kukata rufaa. Kwa hoja hizo, mchungaji akaona hakuna jinsi zaidi ya kila mtu kuishi kivyake,” alisema mtoa taarifa huyo.

Nje ya kanisa hilo juzi, paparazi wetu alikutana na mmoja wa waumini aliyesema anaitwa Masasi ambaye alikiri Flora kufika kanisani hapo kuongea na mchungaji lakini alidai hajui maongezi yao yalihusu nini.

Jitihada za kumpata mchungaji Mwakibolwa ziligonga mwamba kwa kuambiwa alikuwa bize na majukumu ya huduma ya Bwana.

Alipotafutwa Flora ili aweze kuzungumzia suala hilo, simu yake haikupatikana hewani lakini paparazi  wetu alifanikiwa kumpata Mbasha ambapo alipoelezwa ‘full’ stori, majibu yake yalikuwa hivi:

“Nyie mmeipata hiyo? Aisee nyie kiboko, mko makini na matukio. Labda mimi niseme tu hayo yalishapita, sipendi kuyazungumzia kwa sasa maana nilishayasahau. Kwa sasa mimi namshukuru Mungu naendelea vizuri na akipenda nitapata mwenzangu na nitawajulisha.”
Mwaka 2014, wawili hao walimwagana lakini miezi michache mbele, Mbasha alipata kesi ya kudaiwa kumbaka shemejiye mwenye miaka 17.

Uhasama wao ulizidi, ikadaiwa Flora alikuwa nyuma ya kesi hiyo. Mwaka jana, Mahakama ya Wilaya Ilala, ilimwona Mbasha hana hatia hivyo kuwa huru na kila mmoja kuishi maisha yake huku Flora akisali Kanisa la Ufufuo na Uzima kwa mchungaji Josephat Gwajima na Mbasha akisali Mito ya Baraka.

‘Matiti ya Kajala, Dawa za Kichina zinahusika’

$
0
0
Baada ya gumzo kubwa kuibuka juu ya muonekano mpya wa matiti ya msanii wa filamu Bongo, Kajala Masanja, shostito wake wa karibu amemwaga ubuyu kuwa, dawa za kuongeza matiti za Kichina zinahusika.

Akipigia stori na Ijumaa hivi karibuni, mtoa ubuyu wetu ambaye aliomba hifadhi ya jina lake alisema kuwa, huko nyuma matiti ya Kajala yalikuwa ‘ndala’ akawa anatumia dawa f’lani za kupaka ili kuyafanya yatune.

“Nyie muoneni vile tu lakini zile nido zake za sasa Mchina anahusika sana, hawezi kuanika ukweli lakini habari ndiyo hiyo,” alisema mtoa ubuyu huyo.

Paparazi wetu alibahatika kuongea na Kajala juu ya madai hayo ambapo alisema: “Watu bwana wanaongea sana, je nikiamua sasa kutumia hizo dawa itakuwaje? Niseme tu kwamba matiti yangu ni orijino na siku zote yana mvuto ndiyo maana sionagi hatari kuyaanika.”

Source:Global Publishers

Mwanamuziki Shilole Adaiwa Kumfanyia Figisu Nuh Mziwanda Asiendelee Kimuziki

$
0
0
KUNA tetesi kuwa mwanadada asiyekauka kwenye ‘media’ ambaye pia anafanya Muziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ amemuundia jeshi aliyekuwa mwandani wake Naftari Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ kuhakikisha linamfanyia fujo mara kwa mara ili asiishi kwa amani wala kufanya vizuri kimuziki.

Baada ya tetesi hizo kuenea, Burudani Mwanzo Mwisho (BMM), lilimvutia waya Shilole ili kufungukia madai hayo na alipopatikana ‘aliwaka’ na kudai hataki kumzungumzia Nuh wala hajui lolote kuhusu madai hayo.

“Sihitaji kabisa kuzungumza ishu yoyote kuhusu huyo mtu, niacheni kabisa na wala sifahamu lolote kuhusu madai hayo,” alisema Shilole.

Alipotafutwa Nuh, alisema amesikia ishu hiyo lakini anaamini haitafanikiwa kwani Mungu anampigania.

Juma Nature Hajaua Mtu Kwetu - Mh. Temba

$
0
0
Mkongwe wa Bongo Fleva amesema kwamba ambaye anaweza kuwaweka mezani yeye na Juma Nature na kuwapatanisha na wakafanya kazi yeye hana shida.

“Kwa kuwa Juma ni rafiki yangu na hakuna ugomvi wowote kati yetu kwani Juma ni rafiki yangu tangu zamani na Juma hajaua mtu kwetu” alisema Mh. Temba.
Akipiga stori na eNewz Temba amesema kwamba “Sisi kama sisi tulishawahi kulizungumza mi nikamwambia ni muhimu tuwe na watu wenye busara watuongoze katika kazi zetu kwa kuwa sisi ni wasanii wakubwa katika nchi hii isije ikatokea tukapishana kauli kidogo mambo yasiende kama tulivyokuwa tukitarajia”

Aliongeza kuwa “Hata hivyo sisi wenyewe tunaweza kujiongoza lakini akili ya muziki mi naifahamu. Nawasihi Watanzania wasubiri kazi nzuri kutoka kwetu”.

Kundi la Navy Kenzo Laula Marekani..Leo Kukiwasha Viwanja vya Posta Kijitonyama Jukwaa Moja na Ali Kiba na Sauti Soul

$
0
0
Kundi la muziki wa kizazi kipya nchini linaloundwa na Aika na Nahreel, Navy Kenzo, limeingia mkataba wa kuwa mabalozi wa Klobaa App ya nchini Marekani.

App hiyo ya simu inatarajiwa kuzinduliwa leo katika tamasha la 'Mwendokasi Festival' litakalofanyika viwanja vya Posta Kijitonyama.

App hiyo ni mara ya kwanza kuingia Afrika na inazinduliwa kwa mara ya kwanza nchini Tanzania.

Navy Kenzo watapamba jukwaani moja na wasanii mbali mbali wa Bongo kama Ali Kiba, Sauti Soul, Christian Bella, Juma Nature, Man Fongo, Nay wa Mitego, Nuh Mziwanda, Mr Blue , Isha Mashauzi, Roma, Quick Rocka, Ruck Beibe na Wengine Wengi ...Usikose kiingilio Buku kumi tu Mlangoni


Zari Hassan wa Diamond Mjamzito Tena...Wategemea Mtoto wa Pili...

$
0
0
Zari The Boss Lady has shared this Wonderful Pic of Her On Bed with Diamond Platnumz Proving that she is caring Diamond Platnumz's second child..Ooh Yes A Baby Boy This Time and she said..
"This Kiss Goes To My Unborn SON..."

Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images