Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104416 articles
Browse latest View live

MCHEZA MPIRA TAMBWE ATANGAZA KUONDOKA SIMBA

0
0
Na Sweetbert Lukonge
STRAIKA wa kimataifa wa Simba, Amissi Tambwe huenda akavunja mkataba wake na klabu hiyo na kuondoka zake mara baada ya kumalizika kwa msimu huu, ikiwa timu hiyo haitapata nafasi ya kuwakilisha taifa kwenye mashindano ya kimataifa.

Tambwe ambaye ndiye kinara wa mabao katika Ligi Kuu Bara akiwa na mabao 19, amesema kuwa matarajio yake wakati anajiunga na klabu hiyo yalikuwa ni kuiona ikishiriki mashindano ya kimataifa, hivyo kukosa kushiriki michuano hiyo kutamtibulia mipango yake na ametamka wazi anafikiria kuondoka klabuni hapo.

Simba ipo katika nafasi ya nne na haina matumaini ya kushika nafasi ya kwanza wala ya pili kwa kuwa imesaliwa na michezo minne, ambapo imezidiwa pointi 10 na Yanga inayoshika nafasi ya pili.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Tambwe, raia wa Burundi alisema hatma yake ya kuendelea kubakia Simba itajulikana baada ya kumalizika kwa ligi ya msimu huu ambayo ipo katika hatua za lala salama.
Alisema anaweza kuondoka au asiondoke Simba lakini alisisitiza kuwa kila kitu kitajulikana baada ya Aprili 19 ambapo ligi itakuwa inafikia tamati.
GPL

VIDEO:UKWELI WA KUTISHA KUHUSU MALAYA WA UWANJA WA FISI

0
0
Uwanja wa Fisi (2007)in Dar Es Salaam is the favoured hang out for Tanzania's young prostitutes. Their heartbreaking stories reveal brutal histories of poverty and exploitation, yet they still find hope for the future.

WAPINZANI NA SWALA LA SEREKALI TATU..KUNA NINI?

0
0

Kwanini wapinzani wamenga'nga'na sana na swala la serikali tatu? Ni kweli ni kwa ajili ya maslahi ya watanzania au maslahi ya kisiasa?

Wapinzania hawajawahi kuwa pamoja kwenye maswala ya msingi wala hata kuungana tu kwenye chaguzi ili kutengeneza nguvu ya kuing'oa CCM, ila hapa kwenye serikali 3 wamekua pamoja hasa?

Kwenye kampeni za Lipumba misikitini anawaponda CHADEMA, na CHADEMA wanafahamu hilo, yaani hawa jamaa nje ya malumbano ya serikali 3 ni maadui.

Kwanini tusilazimishe serikali 1 au turekebishe makosa yaliyopo?

USA ilinunua Alaska na New Mexico ili kujiongezea rasilimali watu na ardhi, Huyu Nyerere ambaye wapinzani wanajidai kumuenzi alisema ili tuendelee tunahitaji WATU, ARDHI, SIASA SAFI NA UONGOZI BORA.

Hapa tunachokosa ni SIASA SAFI NA UONGOZI BORA sasa tuna sababu gani ya kupunguza ardhi na rasilimali watu?

Tukirekebisha kasoro za muungano na wapinzani wakasimamia maswala ya msingi ya nchi hii ambayo CCM wamekua wakibabaisha kama UFISADI ULIOKITHIRI, RUSHWA ELIMU DUNI NA MENGINE LUKUKI TUNAYAFAHAMU.

Nitakuwa wa mstari wa mbele kwenye maandano yatakayoitishwa na wapinzani. Hili la serikali 3 likifanikiwa we will be the f***in' loosers.

TANZANIAN GOVERNMENT IN SHOCK OVER NEW DAILY MAIL ON SUNDAY REPORT

0
0
Daily Mail on Sunday repays Tanzania’s hospitality with an even more damning article

Regular and usually well informed sources in Dar es Salaam confirmed that there is a mood of incredulity if not outright shock in Tanzanian government circles, as a sponsored visit by a Daily Mail on Sunday journalist spectacularly backfired with a follow up report about his experiences in the country, to which he was flown and hosted entirely at the expense of the Tanzanian government.
The article in last Sunday’s edition showed that some 34.000 tusks were kept in a central store in Dar es Salaam, constituting over 17.000 elephants, some of which died of natural causes with the ivory collected by park personnel and sent to the store but most apparently, at least going by the Daily Mail on Sunday report, originating from confiscated blood ivory.
The PR consultants the Tanzanian government hired, and which most likely recommended that the journalist be flown to Dar for a fact finding mission, clearly misread intent and purpose of Martin Fletcher’s trip and to have to pay them adds injury to insult, as the entire response now is exposed as one bodged operation, over which many surely must hang their head in shame to have so misjudged the final outcome.
The story also insists that President Kikwete is in possession of the names of the alleged ringleaders responsible for the unprecedented elephant slaughter in recent years, when little if anything was done to prevent the massacres in the Selous and in Ruaha, which decimated the great elephant herds from the previous game count standing at between 65 – 70.000 elephant in 2005 to a mere 13.000 as of late last year.
President Kikwete will go into the history books with this black mark against his name for having presided over the globally worst elecide in human history, perhaps only comparable with the wiping out of the bisons in North America in the 19th century.
For the Tanzanian government it is surely back to the drawing board now, to find ways and means to deal with the PR disaster now unfolding, and is well advised to fast track the return of Operation Tokomeza with real tangible results, including the naming, shaming and prosecution of those fund involved, by funding and trading and influence peddling to facilitate the killings of what once was Tanzania’s prized natural wildlife heritage. But going by past experience, results may be a long way off as more political horse trading is presently going on in Tanzania with a new constitution in the making, which may perhaps preclude, until its completion, to rock the boat and bring regime sycophants behind the poaching tsunami to justice while they are needed to swing crucial opinion the way of the ruling party. Observers in fact expect that while actual footsoldiers of the poaching syndicates may be arrested, even killed in the field, the big shots behind it all, those 50 on that nebulous list compiled by former minister Amb. Khamis Kagesheki, who was then put to the political sword, will remain foot loose and fancy free to recruit more to continue their bloody handiwork.
In a notable development yesterday in Arusha did Kenyan President Uhuru Kenyatta, when addressing the East African Legislative Assembly, liken poaching with terrorism and called for a unified approach to fight a war on poaching in the same fashion like fighting a war on terror, as after all evidence is at hand that at least Uganda’s LRA and Somalia’s Al Shabaab have in the past financed operations and fresh supplies from proceeds of blood ivory and of rhino horn. Watch this space for what will undoubtedly see more twists in the tail of this monstrous saga.
About these ads
Share this:

D'BANJ AKANUSHA FUNUNU KUWA HAYUPO TENA KWENYE LABEL YA KANYE WEST..GOOD MUSIC

0
0
D’banj amekanusha fununu kuwa hayupo tena chini ya label ya Kanye WestG.O.O.D Music. Tetesi hizo zilianza mwezi uliopita baada ya staa huyo wa Nigeria kufuta ‘G.O.O.D Music’ kwenye biography ya Twitter na hivyo kuamsha fununu kuwa hayupo tena kwenye label hiyo.

Hata hivyo D’banj amesisitiza kuwa yeye na Kanye bado ni watu wa karibu kwenye biashara.

“Me and Ye (Kanye) are cool; the last time we spoke we talked generally about my career and what his visions are. He is still my mentor, he is still the one I go to when I need something,” D’banj alimuambia mtangazaji wa Uingereza Tim Westwood.

Koko Master pia alisema kuwa yeye na Kanye West wamepanga kufanya video ya wimbo wao are ‘Scape Goat’. “We are still working together. ‘Scape Goat’ is still in the working and we are still trying to work on the video. We just want to get everything right because we have done so much music together,” alisema.
-Bongo5

DIAMOND ACHEFUA WAISLAM..ACHEZA NGOLOLO MAULIDINI

0
0
Stori: Hamida Hassan na Shakor Jongo

KIJOGOO wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amewachefua waumini wenzake wa Kiislamu baada ya kutupia swaga za staili ya Ngololo kwenye shughuli ya Maulidi.
Tukio hilo lililowagusa waumini hao lilitokea juzikati ambapo kulifanyika Maulidi ya kumtoa nje mtoto wa dansa wake aitwaye Moze Lyobo maeneo ya Mbagala, jijini Dar.

Awali watu waliokuwepo eneo hilo walifurahia uwepo wake lakini kadiri walivyoaanza kugundua kasoro ndipo mambo yalipoanza kuharibika.

“Watu hawakumshtukia, lakini walipomkagua kwa makini na kugundua licha ya kuvaa mavazi ya
Kiislamu ndani yake ana macheni ya dhahabu shingoni kitu ambacho dini hairuhusu,” kilidai
chanzo baada ya mwandishi wetu kufika eneo la tukio na kukuta shughuli imeisha.

Kama hiyo haitoshi, ikaelezwa kuwa Diamond alizidi kuchafua hali ya hewa baada ya kucheza
staili ya Ngololo kwenye kaswida kitu ambacho kiliwashangaza wengi.

“Mwanzo alianza vizuri lakini kadiri dufu lilivyokuwa linakolea, akawa anajisahau na kucheza
Ngololo, kimsingi aliwaboa baadhi ya Waislamu waliokuwa pale,” alisema shuhuda wetu.
Hata hivyo paparazi wetu alitonywa kuwa, baada ya kucheza sana, Diamond alichoka huku jasho
likimchuruzika ambapo aliamua kupumzika na kuwaacha wengine wakiendelea.
GPL

WACHINA KESI YA SAMAKI WA MAGUFURI WASHINDA RUFAA

0
0
RAIA WA KIGENI wawili Tsu Chin Tai na Zhao Hanqueing waliokuwa wanatetewa na wakili John Mapinduzi na Ibrahim Bendera, Februali 23 Mwaka 2012 Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ,iliwakuta na hatia katika kwa kosa la kufanya uvuvi haramu katika bahari ya Hindi Ukanda wa Tanzania, maarufu kesi samaki wa Magufuli"kifungo Cha jumla ya Miaka 30 Jela au KULIPA faini ya sh. Bilioni 22,Leo Mahakama ya Rufaa imewaachilia Huru baada ya kuona hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu ilikuwa na makosa ya kisheria. Ila washitakiwa Hao wamerejeshwa gerezani kwaajili ya Taratibu nyingine za JESHI Hilo la Magereza ili wawe za KUACHILIWA Huru.

NA HII NDIO KAULI YA WAZIRI WA CCM ILIYOZUA KIZAA ZAA JANA BUNGENI LIVE

0
0
Naibu Katibu wa Fedha, Mwigulu Nchemba  jana  katika Bunge Maalum La Katiba alichafua hali ya hewa baada ya kumwambia Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe na mwakilishi wa Mji Mkongwe, Ismail Jussa kwamba wanataka wabunge wa bunge hilo watumie kura ya siri badala ya wazi kwa kuwa ni mashoga.

"Wanaotetea kura ya siri itumike katika kupitisha Katiba ya Watanzania, wanaunga mkono sera za ushoga, ni wale ambao vyama vyao vinazaminiwa na wanaotetea sera za ushioga," alisema Nchemba bungeni.

Kutokana na Kauli ya Nchemba, bunge hilo lilipuka likitaka aombe radhi huku akionyesha kusita kuomba radhi, lakini Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samia Suluhu Hassan alimtaka aombe radhi mara kadhaa.

"Mheshimiwa Mwigulu, naomba usimame na kuomba radhi wabunge wenzako, tafadhali simama," alisema Samia

Baada ya kauli ya Makamu Mwenyekiti Samia, Mwigulu alisimama na kusema: "Mheshimwa Makamu Mwenyekiti, Naomba radhi kwa wote wanaodhani wao wako hivyo kama nilivyosema."

Kauli hiyo ilionekana kuendelea kuwachefua wabunge wa bunge hilo huku wakimzomea na kumtaka aombe radhi kwa kuwa bado alikuwa hajaomba radhi moja kwa moja bali kauli yake ilionekana kuwa na utata.

Kwa mara nyingine, Makamu Mwenyekiti, Samia alisimama tena na kumtaka aombe radhi. "Mheshimiwa Mwigulu tafadhali omba radhi bila condition, tafadhali, bila kuomba radhi, Bunge haliwezi kuendela, na ninyi wabunge wengine kaeni kimya bila utulivu hatuwezi kusikilizana, tafadhali," alisema Samia.

Baada ya kauli kauli ya Makamu Mwenyekiti, Samia, Mwigulu alisimama tena na kuomba radhi kwa heshima na bunge kuendelea na utaratibu wake.

"Mheshimiwa Makamu Mwenyekiti, nakiheshimu hicho kiti hapo mbele, siwezi kudharau, Naomba radhi kwa wote nilowaudhi," alisema Mwigukulu na kukaa chini.

Baada ya kauli ya Mwigulu ya kuomba radhi, shughuli za bunge ziliendelea kama kawaida

SINTAH KUINGIA JUMBA LA BIG BROTHER AFRICA MWAKA HUU ....MWEEE!

0
0
Baada ya Sinta Kupost Instagram akimshukuru Boss Lady Zari wa Uganda na watu kuanza kuanza kusema anajipendekeza na kuwa hana hadhi ya Zari Sintah aliamua kuwajibu hao baadhi ya watu kupitia Blog yake na katika majibu hayo amegusia kuwa subiri tumuone kwenye Jumba la Big Brother Africa ..na Kwamba alimwambia Zari See you Soon akiwa na maana wataonana kwenye Jumba Hilo.....Jisomeee hapo chini Mwenyewe na Ujumlishe na Kutoa kama ndio hivyo navyohisi mimi.....


"Kadiri ninavyokuwa ninaamini adui ya mwanamke ni mwanamke aisee,ila kuna kaboy kamoja sijui ni kenyewe ama kametumika kama chambo hapo sasa hawa ndio wanaanzia utotoni ku comment ujinga hivyo,  daah jana i had a long talk wit Zee over the phone, of course was down she was trynaa to cheer me up, hee nikajisikia tu kumuweka kama my friend ona akili nyingine za wasiojielewa zilipotokea ooh huwezi kufanana kama yeye kwani nilikuwa najifananisha? ooh kwakuwa tajiri kwahio matajiri hawana marafiki na je atazikwa na mali zake? mnamkuza dada wa watu wala  hana shauwo kihivyo mwenye nacho anacho tu, sio wale wakipata matako hulia mbwata......

yaani watu wengine mnataka tuwanike whatever we do in Social Media my dear some of us, went to school and learn Ethics in Diplomacy, hapa nimeandika coz naingiza hela nilikwambia nitukane IG,fb, Twitter siwezi kukujibu hapa nipo kama sintah na kule nipo kama Christine John Manongi

kama unaona nafaidi angekuita wewe Ug n you know what i never slept in the hotel nimeishi kwao na wazazi wake of course is not something to be proud of ndio maana nilinyamaza

sasa wewe unaeonekana kituko maana baada ya kuona ule upuuzi ambao mlio comment  auone dada wa watu aliniuliza whats wrong with Tanzanians? maana anakijua kiswahili fika nikamwambia those are small minds pipo they think i benefit alot from you
sasa wewe unayeyaona maisha yake kwenye IG subiri na mimi unione ktk jumba lile la Big bro soon SA, ndio maana nilimwambia see you soon, take note ..... Cheers ukipata maumivu meza Hedex

kwa kifupi mmejichoresha mlio comment utumbo kawaona hamna akili kweli eti najigonga angekuwa anakupigia wewe simu   basi unatamani sana lolest " SINTAH

JE, MH. SITTA AMECHUJA AU AMEPAUKA?

0
0
Alipokuwa spika wa bunge la 9,alitupa mwamko wa kufuatilia vikao vya bunge.Hasa pale aliporuhusu uundwaji wa kamati ya Mwakyembe iliyochunguza dili la richmond na hatimaye kupelekea kumwagika kwa unga wa EL.Wengi tulijua kuwa mzee amedhamilia kuleta mapinduzi ya kisiasa,kwamba hajali ni mtu wa chama gani,ila anachojali ni viwango na kasi.

Juzi ameaminika na kuchaguliwa kwa kishindo pale bungeni ili kuongoza bunge la katiba,akarudia katika maelezo yake kuwa atakuwa yule yule wa viwango na kasi,wengi wakampigia vigelegele,hata mimi nilifurahi na kurukaruka nikijua jembe limerudi shambani.

Ghafla,akatuacha solemba,akatuduwaza na kutuacha na mshangao mkubwa.Hii ilikuwa ni wiki jana pale alipokubali kanuni zisivunjwe ila zipindishwe.Ilikua amkaribishe JK aanze kuzindua bunge kisha afuatiwe na Warioba.Yeye 6,akapiga tiktaka akiwa amevaa taulo,akamleta kwanza Warioba ! Hii haikuwa kwa bahati mbaya,ila ilikuwa planned kabsaa! Yakawa yaliyokuwa na wote tumeshuhudia na kuhudhunika.Hivi kanuni walizojitungia zitafuatwa kweli kama wa kwanza kuzivunja ni 6 na rais wa nchi!?

Wadukuzi wa siasa zetu wanasema 6 alipewa shinikizo na chama chake ili aruhusu kwanza mwenyemeza wao(mwenyekiti) atanguliwe na Mzee Warioba ili baadae mwenyekiti aje kujibu mapigo.Vipi kama angetangulia mwenyekiti na kisha Warioba angefuata,je,mwenyekiti angesomeka kwa ile hotuba yake kweli?

Kwanini 6 anaonekana kuwa refa anayebeba timu fulani waziwazi? Mmeona kwenye kamati za uongozi alivyoteua?

Je, 6 amechuja au amepauka ?

KASEJA AMHENYESHA DIDA YANGA

0
0
UMAHIRI wa kipa, Juma Kaseja na Ally Mustapha ‘Barthez’, umemhenyesha Deo Munishi ‘Dida’ ambaye analazimika kukesha mazoezini ili asichuje.

Dida ametamka kuwa ubora wa makipa hao unamfanya afanye kazi ya ziada ambayo anahisi hakuwahi kuifanya katika klabu nyingine zote alizowahi kucheza, pia anaogopa kupigwa benchi na Kaseja kama enzi hizo walipokuwa Simba pamoja.

Kiwango cha Dida kimeimarika kwa sasa na mwenyewe anasema: “Ubora wangu umeongezeka na kuwa juu kwa sababu ya uwepo wa Kaseja na Barthez, ni makipa mahiri kwenye ligi.

“Kwa sababu ya ubora wao, inanifanya nisibweteke, nijitume ili niwe bora zaidi na zaidi. Kama nitabweteka na kuwa chini ya kiwango hata kidogo tu, ni wazi sitapata namba.

“Lakini kama ningekua nacheza kikosi kimoja na makipa wengine wasio na uwezo, lazima ningebweteka kwa sababu ningekosa ushindani na kiwango kingebaki kama kilivyo kwa kukosa changamoto.”

Dida anatarajia kuanza mazoezi mwishoni mwa wiki hii, alikuwa kwenye mapumziko akiuguza kidonda kwenye bega la kushoto.

Alijikata na geti nyumbani kwake, lakini aliibua tatizo lingine baada ya kupakaa dawa ya spiriti nyingi iliyomuunguza na kusababisha kidonda hicho kuongezeka. Yeye amesisitiza anaendelea vizuri na atarudi uwanjani akiwa na kasi hiyo hiyo.

KASHFA YA USHOGA YAMTESA ASHLEY COLE..AKUNUSHA

0
0
MAPEMA wiki iliyopita uvumi ulisambaa nchini England kwamba gazeti maarufu la The Sun lilikuwa mbioni kuchapisha stori ndefu iliyohusu kashfa ya ushoga ya mlinzi mmoja wa sasa wa kushoto wa timu ya taifa ya England.

Hata hivyo, Gazeti la The Sun la juzi Jumapili lilikanusha kutaka kuandika stori hiyo, lakini bado mlinzi wa kushoto wa England na Chelsea, Ashley Cole akawahi kukanusha kwamba alikuwa hahusiki na kashfa hiyo.

Cole ameimiliki nafasi ya ulinzi upande wa kushoto tangu Machi 2001 na ndiye mchezaji wa pembeni aliyecheza mechi nyingi zaidi katika kikosi cha timu ya taifa ya England.

Na kama kutakuwa na ukwlei wowote katika habari hiyo ni wazi kwamba hilo litakuwa pigo jingine kwa mchezaji huyo ambaye kwa sasa anahaha kupata namba hiyo hiyo aliyoitawala muda mrefu katika kikosi cha Chelsea na hivyo hiyo kuwa nuksi nyingine inayomuandama mchezaji huyo.

Mashabiki wengi waliamini kwamba Cole alikuwa anahusika na kashfa hiyo.

Mwingine aliyeonekana kuhisiwa katika kashfa hiyo ni mlinzi kinda, Luke Shaw ambaye ameanza kuichezea timu ya taifa ya England katika pambano la kirafiki dhidi ya Denmark Machi 8 mwaka huu. Hata hivyo wote wawili wametumia mitandao yao ya mawasiliano kukanusha uwepo wa habari hiyo.

Cole aliandika katika mtandao wake akisema ‘strictly chicks only’, akimaanisha anapenda wasichana tu, wakati Shaw aliandika kwa kusema ‘Si mimi’. Cole alikuwa katika ndoa na mwanamuziki maarufu wa Kundi la Girls Aloud, Cheryl Cole ambaye pia aliwahi kuwa jaji wa michuano ya kusaka vipaji ya X Factor lakini ndoa yao ikavunjika mwaka 2010 kutokana na kile kilichodaiwa kuwa Cole hakuwa mwaminifu katika ndoa hiyo.

Uvumi ulitanda Jumamosi usiku iliyopita katika mitandao ya kijamii kwamba The Sun la Jumapili lingemtaja mchezaji mmoja katika kikosi cha kocha Roy Hodgson ambaye anahusika na kashfa ya ushoga.

Kama gazeti hilo lingefanya hivyo, huyo angekuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya timu ya taifa ya England kujitangaza kuwa shoga. Hata hivyo gazeti hilo lilikanusha waziwazi kwamba stori hiyo ilikuwa imepikwa na watu wasiojulikana.

Huo ni mwendelezo wa habari za ushoga zikuibuka katika vyombo vya habari vya Uingereza baada ya staa wa zamani wa timu ya taifa ya Ujerumani, Thomas Hitzlspelger kujitangaza kuwa shoga Januari mwaka huu.

Nyota huyo wa zamani wa Aston Villa, Everton na West Ham amekuwa mchezaji wa kwanza wa Ligi Kuu England katika mfumo mpya kujitangaza kuwa shoga.

KURA MCHANGANYIKO BUNGE LA KATIBA-UWAZI NA SIRI SASA ZOTE RUKSA

0
0
Wajumbe wa Kamati ya Maridhiano jana walinusuru Bunge Maalumu la Katiba kuvunjika, baada ya kukubaliana kutumika kwa utaratibu wa upigaji kura wa wazi na siri kama ilivyopendekezwa na Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge.

Wajumbe hao walitangaza uamuzi huo bungeni kutokana na makubaliano yaliyofikiwa katika kamati ndogo ya maridhiano iliyofanyika jana asubuhi baada ya kushindwa kuafikiana katika kikao cha awali kilichofanyika juzi kuanzia saa 3:00 usiku hadi usiku wa manane ili kunusuru kukwama kwa Bunge hilo.

Kabla ya uamuzi huo, Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta alisema juzi usiku walikutana hadi usiku wa manane baada ya hapo, walikabidhi kamati ndogo yenye mchanganyiko wa wajumbe kutoka Kamati ya Kanuni na Kamati ya Maridhiano.

“Baada ya kukamilisha kazi, wajumbe wa kamati ndogo watatoa taarifa hapa ambao ni John Mnyika, Profesa Ibrahimu Lipumba, Vual Ali Vual na Askofu Donald Mtetemela,”alisema Sitta.

Akitoa taarifa ya maridhiano hayo, kwa niaba Freeman Mbowe, Mjumbe John Mnyika alisema, alianza kwa kunukuu kitabu kilichoandikwa na Mwalimu Nyerere, mwaka 1962 chenye ujumbe mahususi kwa Chama cha TANU akisema ujumbe huo kwa sasa ni sahihi kwa watu wengi na taasisi ikiwamo CCM.

Mnyika pia alisema Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) hawana nia yoyote ya kuvuruga mchakato wa katiba kama ambavyo imeelezwa katika siku za karibuni na viongozi, kwani wazo la kutaka Katiba Mpya imekuwa ni kilio chao cha muda mrefu.

Naye Profesa Lipumba alisema suala ambalo tumekuwa tukisimamia kwa muda mrefu suala ambalo lina utata, kati ambao wanapenda kura za uwazi na wale wa siri.

Alisema: “Tuliletewa mchanganyiko wa uwazi na siri, lakini maana yake ni kura ya uwazi, wenzetu wamekuwa na msimamo mkali hata hili la kufanya uamuzi ilikuwa tufanye kwa siri, lakini hata hivyo hawakukubali.”

“Tulifanya uamuzi ili tusonge mbele, basi tulipendekeza upigaji kura wa kuamua tupige kura kwa mfumo wa siri, lakini pia wenzetu walikataa,”alisema Profesa Lipumba.

Alisema kwa kuzingatia kutokwama kwa zoezi la kuanza kujadili rasimu, wameamua kukubali kutokubaliana.

“Ili kusonga mbele tunahitaji kusonga mbele tuanze kujadili Katiba, natoa wito kwa wenzangu wa chama tawala kwa kuwa mpo wengi mnadhamana kubwa, ni vyema mkawa na utaratibu wa kuwasikiliza wachache,” alisema.

Mjumbe Vuai Ali Vuai alisema, wamefikia maridhiano hayo, ili kuwezesha kuendelea na mchakato wa katiba mpya kwani kila upande uliendelea kutetea msimamo wake hata katika kikao cha maridhiano.

KWANINI WANAWAKE WENGI WAKISHAJIFUNGUA WANAKUWA RAHISI KUCHUKULIWA NA VIDUME

0
0
Katika pita pita zangu wale wadada wanajidai wana misimamo wanapozalishwa na wanaume na kuachwa alone huwa wanashuka chini na inakuwa rahisi kupiga sound ya kawaida na kuchukua mzigo ila kipindi kabla ilikuwa hata kusalimia watu ni tabu kwake.Najiuliza kwa nini hulainika na kuwa na heshima pindi wanapo kuzalishwa?

MAFURIKO YATIKISA JIJI LA DAR..HALI NI MBAYA

0
0
MVUA zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam zimesababisha uharibufu wa miundombinu ya barabara, nguzo za umeme na mingine kuharibika, hali iliyokwamisha shughuli nyingi jana.

Mvua hizo zilizonyesha usiku mzima wa kuamkia jana, ziliambatana na upepo mkali, radi na ngurumo nzito zilizowatia hofu wakazi wengi wa Jiji la Dar es Salaam.

Wakazi waishio mabondeni walikuwa na kazi ya ziada kwani wengi nyumba zao ziliingia maji na kusababisha baadhi yao kuhama makazi yao usiku, huku wengine wakipoteza vitu  na samani mbalimbali.

Kutokana na barabara za Jiji la Dar es Salaam kufurika maji, askari wa Usalaama Barabarani (Trafiki), walikuwa na kazi ya ziada kuyaruhusu magari kupita njia ambazo ziko salama bila kujali sheria.

Tanzania Daima ilishuhudia barabara kuu zote na maeneo mengine kufurika maji na kusababisha wakazi wa jiji hilo kupita kwa shida.

Aidha, baadhi ya wakazi  waliokuwa wakitoka Pugu, walilazimika kupanda magari ya kubeba ng’ombe yaliyokuwa yakitokea mnadani baada ya daladala nyingi kusitisha safari zake.

Wakati hali ikiwa hivyo, eneo la Jangwani maji hayo  yalizoa miundombinu ya mabomba ya maji ikiwemo yale yaliyojengwa hivi karibuni kupisha ujenzi wa barabara ya magari yaendayo haraka (DART).

Pia kulikuwa na baadhi ya vijana katika eneo hilo waliokuwa wakijiokotea vitu mbalimbali vilivyokuwa vikielea juu ya maji.

Akizungumzia kufurika kwa maji kwenye barabara hizo kuu, Sajenti James Walter, alisema ilibidi kuyaruhusu magari ya abiria yapite njia nyingine kinyume cha  sheria, lengo likiwa kuwafikisha salama abiria kule wanakokwenda.

“Kwa kweli hali ni mbaya lakini tumejipanga vizuri kuhakikisha abiria na watumiaji wa barabara hizi hawakwami njiani,” alisema Walter.


KANGA MOKO, VIGODORO NA T-SHIRT NDEMBENDEMBE VYAOIGWA MARUFUKU MISS TANZANIA

0
0
BARAZA la Sanaa la Taifa (Basata), limeitaka Kamati ya Miss Tanzania kutohusisha burudani zinazokiuka maadili ya Mtanzania wakati wa mashindano yao mwaka huu.

Akizungumza wakati wa kikao cha tathmini ya mashindano ya Miss Tanzania 2013 kilichofanyika kwenye ukumbi wa baraza hilo, Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Idaya ya Ukuzaji Sanaa Basata, Vivian Shalua, alisema kuwa, maadili ni muhimu kuzingatiwa katika mashindano hayo ili kuepukana na dhana potofu kuwa, yanahusiana na uhuni.

“Maadili yazingatiwe katika mashindano ya mwaka huu, kuanzia kwa washiriki hadi burudani zitakazohusishwa, kama ‘vigodoro’, ‘kanga moja mbendembende’ na nasikia siku hizi kuna ‘tisheti ndembendembe’,” alisema mkurugenzi huyo.

Alisema kuwa, Basata ipo tayari kuyapigania mashindano ya Miss Tanzania kuhakikisha yanakuwa katika ubora wa hali ya juu, kwa kushirikiana na Kampuni ya Lino International Agency ambao ndio waandaaji.

Mkurugenzi huyo pia aliitaka Lino kuwaelimisha mawakala wanaoandaa mashindano hayo juu ya umuhimu wa kuwa na vibali kutoka Basata, ikiwa ni pamoja na kutowavumilia watovu wa nidhamu bila kujali ukongwe wao katika tasnia hiyo.

Kwa upande wake, Ofisa Sanaa Kitengo cha Matukio, Kurwijira Maregesi, aliitaka Lino kujipanga kujiweka tayari kufanya mashindano hata pale inapokosa mdhamini, huku mjumbe mwingine katika kikao hicho, ambaye ni Ofisa Sanaa Basata, Philemon Mwasanga, akisisitiza mawakala kuwekeana mikataba na warembo kabla ya mashindano kuanza.

“Lino isiwafumbie macho mawakala wasiojali mikataba na warembo, na warembo waisome na kuielewa ili kuepusha migogoro inayoweza kutokea,” alisema.

Akijibu hoja kadhaa zilizoibuliwa katika kikao hicho, Mkurugenzi wa Lino International Agency, Hashimu Lundenga, alisema kuwa, wamejipanga ili kuweza kufanya mashindano yao bila kutegemea wadhamini, huku akiitaka Basata kuwasaidia katika hilo.

“Tatizo mashindano yetu gharama yake ni kubwa sana, nasi hatupendi kuona ubora wake ukishuka kutokana na kushindwa kumudu gharama, ndio maana tumekuwa tukihangaika kuomba udhamini kutoka katika makampuni mbalimbali makubwa hapa nchini,” alisema.

Juu ya mikataba baina ya warembo na mawakala, Lundenga alisema: “Mwaka huu tumesisitiza mawakala waingie mikataba na washiriki kabla ya mashindano na tutakuwa makini katika kufuatilia hilo na changamoto nyinginezo zilizoibuliwa katika kikao hiki.”

Mmoja wa warembo walioshiriki mashindano ya mwaka jana ambaye ni Miss Sinza 2013, Prisca Clement, alisema kuwa, kuna umuhimu wa kuongezwa kwa zawadi katika ngazi za chini ili kumwezesha mshiriki kujivunia na kujitosa kwake katika mashindano hayo bila kujali kama ameshinda au la.

Mashindano ya Miss Tanzania 2014 yamezinduliwa mapema wiki hii, ambapo fainali zake zinatarajiwa kuwa kati ya Septemba na Novemba mwaka huu chini ya udhamini wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia kinywaji chake cha Redd’s Original.

NAHISI ANA MWANAMKE ZAIDI YANGU..NATAKA NIMFUMANIE KWA SUPRISE VISIT KWAKE

0
0
Nina age ya 22 nipo kwenye relationship na mwanaume kama miezi 3 saizi tatizo limeanza baada ya mimi kuwa mbali kama 3weeks hivi.
Nahisi anamwanamke zaidi yangu kwasababu hata namna ya kuongea
inanitia mashaka.
Kuna wakati akiongea na mimi anaongea vizuri sana but sometimes nikimpigia simu anaweza akaongea haraka haraka and mda huo najua yupo nyumbani kwahivo hayupo bize.
Nkimuuliza mbonahivo upo na nani? anakata simu then anafunga simu kabisa, kesho yake anaweza kuniambia simu imezima haikuwa na chaji au hapendi maswali yangu kwani
naonyesha kama simuamin.
Nataka nimfanyie suprise visit, sababu nimesharudi safari naye hajui kama nipo hapa mjini ili nijue kama kweli anakua bize au maswali yangu yanamkera na hamna kingine.

Je hii suprise ndio itaua kabisa mapenzi au nifanyaje?

TAZAMA PICHA HIZI ZINAZOONYESHA TASWIRA YA TRENI ILIYOPINDUKA NA KUUA

0
0
Wafanyakazi walioajiriwa na shirika la Reli Tanzania (TRL) wakitoa mchanga kwenye kichwa cha treni ya mizigo kilichopata ajali usiku wa kuamkia katika stesheni ya Gulwe, Wilaya ya Mpwampwa. Katika ajali hiyo watu wawili wamefariki dunia na wengine saba kujeruhiwa na kulazwa katika hospital ya Benjamin Mkapa Wilayani Mpwampwa.
Sehemu ya mabehewa ya mafuta na ngano ambayo hayakusombwa na maji katika ajali iliyotokea usiku wa kuamkia leo katika stesheni ya Gulwe, hiyo imetokea saa 9.15 usiku. Treni hiyo ya Mizigo ilikuwa ikitokea Dar es Salaam na kuelekea Mkoani Kigoma na ilikuwa na mabehewa yaliyobeba ngano, sukari na mafuta.

Njia ya Reli iliyoondolewa na maji katika stesheni ya Gulwe Wilaya ya Mpwampwa kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha maeneno mbambali nchini.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Shaaban Mwinjaka akitoka kwenye maji baada ya kuangalia kichwa cha treni kilichopata ajali na kusombwa na maji katika stesheni ya Gulwe, Wilaya ya Mpwampwa, usiku wa kuamkia leo, kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha sehemu mbalimbali za nchi. Ajali hiyo imesababisha kifo cha watu wawili na wengine saba kujeruhiwa na kulazwa katika hospital ya Benjamin Mkapa iliyoko wilayani Mpwampwa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk, Shaaban Mwinjaka akimfariji mmoja wa Majeruhi wa Ajali ya treni ya mizigo iliyotokea katika Stesheni ya Gulwe Bw. Michael Lupatu wakati alipomtembelea katika hospitali ya Benjamin Mkapa iliyopo Wilayani Mpwampwa leo mchana. Ajali hiyo ya treni ya mizigo imetokea usiku wa kuamkia leo na kusababisha kifo cha watu wawili na wengine saba kujeruhiwa.
(Picha na kitengo cha Mawasiliano Serikalini uchukuzi)

DAVID MOYES AJITETEA ..."HATA INGEKUWA NI FERGUSON MSIMU HUU ANGEPATA WAKATI MGUMU"

0
0
Meneja wa klabu ya Manchester United, David Moyes amedai kwamba msimu huu wa kwanza kwake hata ungekuwa kwa Sir Alex Ferguson angepata shida kufanya la maana ndani ya msimu ukilinganisha na wachezaji wake wenye umri mkubwa.
“Ukweli nadhai kwamba kama Sir Alex angekua hapa mwaka huu ingekua ngumu kwa Sir Alex pia,nina uhakika hata yeye analijua hilo. Nafikiri watu wanatambua kwamba kuna kikosi ambacho kimepita umri, kwa maana hiyo nadhani ingekua ni msimu mgumu labda kwa yeyote ambaye angekabidhiwa Manchester United mwaka huu,” alisema Moyes

Kauli hiyo ya Moyes imekuja huku Jumamosi hii kundi la mashabiki wa Manchester United likipanga kukodisha ndege itakayopeperusha kibendera chenye maandishi ya kumpinga kocha huyo. Manchester United imekuwa na msimu mbaya kiasi cha mashabiki wa timu hiyo kuanza kulalamika vikali wakimtaka Moyes afutwe kazi.

SHIRIKISHO LA FILAMU TANZANIA "HATUITAMBUI BONGO MOVIE UNITY YA STEVE NYERERE"

0
0
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania(TAFF) Simon Mwakifwamba amedai shirikisho lake haliwatambui wasanii wanaounda kundi la Bongo Movie Unity na kudai kuwa kundi hilo linaundwa na watu sita tu huku wengine wakifuata mkumbo.

Akizungumza na Global Publishers, Mwakifwamba ambaye pia ni muigizaji wa muda mrefu na muongozaji wa filamu amesema hawatambui wasanii hao na anawashauri wajiunge ili watambulike. “Bifu la nini? Mimi ni baba, wao ni watoto. Kwanza sikia… wale sio wanachama wangu.Nawashauri wajiunge kwenye vyama vyangu ili niwatambue kama sehemu ya shirikisho,” alisema.

“Unajua wale wanaongozwa na ustaa. Wanaamini ustaa upo juu ya sheria, sio kweli. Mimi naamini katika uelewa na uwezo.Isitoshe mtu wa kwanza aliyetoa wazo la Bongo Muvi ni mimi. Nakumbuka nilikuwa mimi, Dude (Kulwa Kikumba), William na Ruge Mutahaba, tukaunda Bongo Muvi ili tucheze mechi na Bongo Fleva kwa ajili ya kuchangisha fedha za waathirika wa mabomu ya Gongo la Mboto. Tulifanikiwa sana. Hapo sasa walafi wachache wakalazimisha wasanii waende Mwanza wakacheze mechi nyingine ili wapate fedha, nikakataa hilo wazo, ndiyo mwanzo wa kutengana nao. Niwaambie tu Watanzania, chombo mama cha wasanii wa filamu nchini ni TAFF, si vinginevyo,” aliongeza.

“Kwanza Bongo Muvi si chama kama wengi wanavyofikiri, ni kampuni na ina wamiliki wake tisa, hao wengine wanafuata mkumbo kwa sababu hawajitambui. Kama wanabisha, waonyeshe usajili wao wa Basata, maana chombo pekee kinachosajili kazi za wasanii ni Basata.”

Hata hivyo Bongo5 imejaribu kumtafuta mwenyekiti wa BMU, Steve Nyerere kuzungumzia kauli hiyo, lakini amekuwa hapokei simu.
-Bongo5
Viewing all 104416 articles
Browse latest View live




Latest Images