Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live

Diamond:Sio Kila Rafiki Yangu Basi Anatembea na Dada Yangu

$
0
0
Jana wakati akitolea ufafanuzi suala la yeye kuchepeka Hamisa Mobeto,Diamond alisema anashangazwa sana na tabia ya watu kuhusianisha kila rafiki wa dada yake basi yeye anatembea naye huku akienda mbele zaidi na kudai hali iko hivyohivyo sio kila rafiki yake basi anamkaza dada yake
"MAANA KILA MSHIKAJI WANGU MIMI A******* {ANALALA} DADA YANGU" Aliuliza Diamond Platinumz

Mwana FA Awataja Hawa Ndiyo Wasanii Wake Bora wa Hip Hop Bongo

$
0
0
Mwanamuziki Mwana FA amefunguka na kuwataja wasanii wawili ambao yeye siku zote amekuwa akiwakubali kutokana na uwezo wao na kazi kubwa waliyoifanya katika muziki wa Hip Hop Tanzania kiasi cha kuwafanya watu waamini muziki huo siyo uhuni bali ni kazi.

Mwana FA kupitia kipindi cha Friday Night Live (FNL) kinachorushwa na EATV alisema Professor Jay pamoja na marehemu Albert Mangwea ndiyo wasanii wake wawili bora wa siku zote katika muziki wa Hip hop Tanzania.

“Wasanii wangu bora kwa kipindi chote kwenye muziki wa Hip hop ni marehemu Albert Mangwea pamoja na Professor Jay hiyo nasema na kuna siku nilishawahi kuandika hilo, mpka Professor alinipigia simu na kuniuliza mzee una nini unataka kufa nini?. Watu hawajui tu huyu Professor Jay kwanza ndiyo mtu aliyefanya muziki wetu huu kwanza uanze kuheshimiwa, mwanzoni nyimbo zilikuwa na ujumbe wa fujo fujo fulani, kwa hiyo muziki wetu ulikuwa hauchukuliwi ‘serious’ lakini baada ya chemsha bongo kila kitu kikabadilika” alisema Mwana FA

Mbali na hilo Mwana FA alisema kuwa Professor Jay ni msanii ambaye alifanya yeye kidogo aache muziki sababu Mwana FA alikuwa anataka kufanya muziki bora lakini alipokuwa anasikiliza kazi za Professor Jay akaona hawezi kufanya kazi bora kama hizo.

“Unajua mimi siku zote huwa nataka kuwa best kwa kile nachofanya sijui kwa wasanii wengine, sasa baada ya kusikia ngoma ya Professor Jay ‘Chemsha bongo’ mimi nina nyimbo zangu nilikuwa nimeandika nikarudi nyuma nakajiuliza sasa mimi nawezaje kuwa ‘best’ kwa ngoma hizi? Yaani alinikatisha tamaa lakini nikarudi na kuanza kujipanga upya” alisema Mwana FA

Lulu Michael Aelezea Kwanini Alimblock Mpenzi wake Majizo Kwenye Instagram

$
0
0
Bongo Movies actress, Elizabeth Michael 'Lulu' has replied about what her Boyfriend, Majjizo after he complained abut the reason why she had blocked on Instagram, On his Instagram account, Majjizo complained concerning what lulu did.


Here is what Lulu posted on her account;

Kauli ya Magufuli Yawachanganya ACT Wazalendo

$
0
0
Chama cha ACT Wazalendo kimesema kauli ya Rais John Magufuli kuruhusu wabunge kufanya mikutano ya hadhara katika majimbo yao pekee ni kukiua chama hicho.

Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ya ACT Wazalendo, Bakari Licapo amemtaka Rais kutoa ufafanuzi zaidi kuhusu kauli hiyo ambayo alidai inahatarisha ustawi wa chama hicho.

“Mwenyekiti wa ACT Wazalendo, Anna Mgwira alifanya kampeni nchi nzima ila kwa sasa atashindwa kuzungumza na wananchi wachache waliompa kura kutokana na kauli iliyotolewa,” amesema Licapo jana.

 Licapo, amewaomba vijana bila kujali itikadi, kutekeleza azimio lililotolewa na Zitto la kuandika barua zitakazotumwa Ikulu kueleza masikitiko yao juu ya ukandamizaji wa demokrasia.

Gabo Zigamba anusurika kifo katika ajali ya gari

$
0
0
Muigizaji wa filamu ya ‘Bado Natafuta’ Gabo Zigamba amenusurika kifo katika ajali ya gari wakati akielekea hifadhi ya Ruaha akiwa na wenzake wawili ambao wamejeruhiwa huku yeye akisalimika katika ajali hiyo.

Gabo amekanusha taarifa ambazo zimezagaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa amefariki katika ajali hiyo.

“Uongo unaoishi ndiyo ukweli mpaka ukanushwe, nami naanzia hapa kwenye kukanusha, ni kweli nimepata ajali lakini sijafa na maumivu ni ya ndani sana,” aliandika Gabo katika istagram yake. “Na sijavunjika kama watu wanavyosema ila naumia na jinsi watu wanavyo waombea wenzio Mabaya,”

Aliongeza, “Nilikuwa na lengo zuri la kugawana umasikini na wanyonge wenzangu na hata Mungu akanisimamia. Eee Mollah wasamehe kwani na mimi nimewasamehe, naamini utaniongoza na kunisimamia leo, kesho na hata milele,”

Rais wa klabu ya Simba Evans Aveva akamatwa na Takukuru

$
0
0
Rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva anashikiliwa na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru).

Taarifa zinaelezwa kuwa Takukuru wanamshikilia Aveva kwa tuhuma za rushwa ingawa haijaelezwa ni tuhuma zipi.

Habari za uhakika zinaeleza, Aveva amekamatwa jana na amelala katika moja ya vituo vya polisi jijini Dar es Salaam.

Source: salehjembe.blogspot.com

Kiama cha madereva walevi na wazembe Chawadia, Serikali yazindua mkakati wa mambo 14 kukabiliana na ajali

$
0
0
Na Jonas Kamaleki-Maelezo
Serikali yajipanga kupunguza ajali za barabarani kwa kiwango cha takribani asilimia 10 hapa nchini ili kupunguza vifo na majeruhi.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Yusuf Hamad Masauni  kuwa baraza la Usalama Barbarani linakerwa sana na kadhia ya ajali za barabarani ambazo zimekuwa zikitokea mara kwa mara.

“Kukithiri kwa ajali za barabarani kwa siku za hivi karibuni, umewezesha Baraza kuibuka na Mkakati wa Miezi Sita (6) unaolenga katika kukabiliana na ajali za barabarani nchini, mkakati huu ni wa muda mfupi kuanzia mwezi Agosti, 2016  hadi Februari 2017 tutakapokaa na kutathmini matokeo yake”, alisema Masauni.

Masauni amesema ajali za barabarani zimewaacha watoto wakiwa yatima  na kuwafanya akina mama kuwa wajane, hivyo  juhudi za makusudi inabidi zifanywe ili kupunguza kama sio kuondoa kabisa ajali hizo.

Ametaja vyanzo vikuu vya ajali za barabarani nchini kuwa ni pamoja na Makosa ya Kibinadamu, mazingira ya barabara na ubovu wa vyombo vya moto.

Naibu waziri huyo amesema takwimu za ajali barabarani katika miaka mitatu tangu 2012 ajali ziliongezeka toka 23,578 hadi 23, 842 kwa mwaka 2013, vifo vilikuwa 3,969 kwa mwaka huo hadi kufikia 1,043 mwaka 2013.

Vifo hivyo vilipungua hadi kufikia 3,760 mwaka 2014, upungufu huo ulitokana na usimamiaji madhubuti wa Sheria na kanuni za Usalama barabarani pamoja na juhudi zilizofanya na Baraza kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi.

Kwa mujibu wa Masauni, Mkakati uliozinduliwa unalenga kudhibiti makosa yanayosababisha madhara makubwa na ambayo husababisha kuongezeka kwa ajali za barabarani.

Ameyataja mambo hayo kuwa  ni:
 1. Udhibiti wa madereva walevi na kuendesha kwa uzembe.

2. Udhibiti wa mwendokasi kwa madereva na wamiliki wa magari; kuwa na madereva wenza

3. Uendeshaji magari bila sifa/leseni ya udereva na bima

4. Udhibiti wa usafirishaji wa abiria kutumia magari madogo yenye muundo wa tairi moja nyuma kwa mfano; Noah, Probox

5. Kudhibiti ajali za pikipiki za magurudumu mawili ‘bodaboda’ na magurudumu matatu

6. Abiria kufunga mikanda ya usalama wanapotumia vyombo vya usafiri

7. Kuyabaini na kuyadhibiti maeneotete na hartarishi ya ajali za barbarani ‘black spots/kilometers’

8. Kuangalia uwezekano wa kufanya marekebisho ya sheria za usalama barabarani.

9. Kuanza kwa mfumo wa nukta ‘point system’ kwenye leseni za udereva.

10. Kutoa mafunzo ya msasa yanayolenga katika kuimarisha utendaji wa askari wa usalama barabarani.

11. Kuhakikisha kuwa waendesha bodaboda wanafikiwa na kupewa mafunzo yaa uhakika juu namna na jinsi ya kuzitumia barabara kwa usalama zaidi.

12. Kudhibiti rushwa na kuwaadhibu watoaji na wapokeaji wa rushwa katika barabara zetu nchini.

13. kuwahusisha wamiliki wa magari ya abiria na ya mizigo, katika kuutekeleza mkakati.

14. Mkakati mwingine waliouweka ni kuwa Dereva ukikamatwa unapelekwa rumande na baadae mahakamani kujibu shitaka litakalokuwa linakukabili.

Taarifa za Ndani ya Familia… Diamond ‘Mchafu’

$
0
0
Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amejikuta akiwatibua baadhi ya ndugu zake huku wengine wakimuita mchafu kutokana na kitendo cha kumpachika mimba mpenzi wake Zarinah Hassan ‘Zari’ kisha kuwepo madai kuwa ‘amewajaza’ pia mamodo Hamisa Hassan ‘Mobeto’ na Irene Hilary ‘Lynn’.

Mmoja wa ndugu wa karibu wa Diamond aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema kuwa, familia imeshtushwa na madai kuwa kijana wao huyo mbali na kwamba Zari a.k.a Mama Tiffah ni mjamzito, amewapa mimba tena Mobeto na Lynn.

ILIKUWAJE?
Miezi kadhaa nyuma, yaliibuka madai kuwa Zari ni mjamzito lakini Diamond amekuwa mgumu kulizungumzia hilo licha ya hivi karibuni mazazi mwenziye huyo kutundika picha akionesha kitumbo chake kilichodhihirisha kuwa ndani yake kuna kiumbe.

LYNN NAYE
Huku mashabiki wa Zari ‘Team Zari’ wakionesha furaha ya staa wao ‘kumshika’ mwanamuziki huyo kwa kumbebea ujauzito mwingine, zikaibuka taarifa nyingine kuwa, modo wa Wasafi Classic Baby (WCB) Lynn naye ana mimba ya jamaa huyo.
Ikadaiwa kuwa, kubeba ujauzito kwa Lynn kumekuja baada ya yeye na Diamond kuwa kwenye uhusiano wa siri huku mama Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ akidaiwa kujua kila kitu na kubariki ujio wa mjukuu mwingine.

MIMBA YA MOBETO
Katika kile kilichoonesha kuwachefua baadhi ya wanandugu, hivi karibuni yakaibuka madai kuwa, mwanamitindo Mobeto naye ana mimba na mhusika ni baba Tiffah.
Taarifa hizo zimeonesha kuwashitua wengi akiwemo mama mzazi wa modo huyo, Shufaa Lutigunga ambaye alipoongea na mwandishi wetu alisema kuwa, amezishangaa ila anayeweza kueleza ukweli ni Mobeto.

Jitihada za kumpata modo huyo ili kuzungumzia madai hayo hazikuzaa matunda licha ya kwamba aliwahi kuongea na gazeti hili na kukanusha madai yaliyokuwa yamezagaa kuwa anatoka na Diamond.

FAMILIA YA DIAMOND ‘YAMAINDI’
Kufuatia madai hayo, ndugu wa karibu wa Diamond aliyeongea na gazeti hili alisema kuwa, hivi karibuni familia ilikaa kikao kujadili mambo ya kifamilia lakini pia wakaonesha kukasirishwa na taarifa ya Diamond kuwapachika mimba wasichana watatu.

“Hilo la madai kuwa Diamond amewapa mimba wanawake watatu licha ya kwamba hatuna uhakika nazo, zimetuchefua sana, zimetufanya tumuone Diamond ni mchafu au kwa maana nyingine ni mchafuzi.

“Nasema hivi kwa sababu, haiwezekani iwe amempa mimba Zari halafu wakati huohuo awe amempa tena Lynn na Mobeto, sisi kama familia tutaficha wapi nyuso zetu wakijifungua?
“Ishu hiyo imemfanya kila mtu kwenye familia awe muoga, kwani pamoja na hayo yote kutokea, kubwa wanalohofia ni namna watakavyomwangalia Zari (wifi yao), sasa wakijifungua sijui watamjibu nini au wataweka wapi sura zao.

“Hapa ninavyokwambia mama Diamond na Esma hawaongei vizuri na Zari kufuatia kuendelea kuwahisi wao ndiyo kikwazo kikubwa cha kumuunganisha Diamond na warembo hao,” kilidai chanzo hicho.

DIAMOND HUYU HAPA
Gazeti hili baada ya kupenyezewa taarifa hizo lilimtafuta Diamond ili kumpa nafasi ya kulizungumzia kinagaubaga suala hilo, alipopatikana alisema kwamba yote yanayozungumzwa ni maneno ya watu na hakuna hata moja la kweli.
“Hakuna hata moja la ukweli, mwenyewe najionea kwenye mitandao kama nyinyi, kwani ‘social network’ kila mmoja ana uhuru wake wa kuongea anachokiwaza na siwezi kuwafuata na kuwauliza.
“Kwa hilo sina la kuongea zaidi maana naona ni mambo ya kipuuzi tu ambayo siwezi kuyapatia nafasi yoyote kwangu, naona tuachane nayo tu,” alisema Diamond.

TUJIKUMBUSHE KIDOGO
Diomond amekuwa na skendo kibao za ku-date na wasichana mbalimbali wakiwemo mastaa ambapo mbali na Zari, Mobeto na Lyn, jamaa huyo aliwahi pia kutoka na Wema Sepetu, Jokate Mwegelo, Jacqueline Wolper, Upendo Mushi, Penniel Mungilwa ‘Penny’, Aunt Ezekiel na wengineo.

Source:Global Publishers

Mchungaji Afariki kwa Kufunga Siku 30 Akijaribu Kuvunja Rekodi ya Yesu

$
0
0
LILE andiko la usimjaribu bwana Mungu wako lililosemwa na Yesu Kristu limejidhihirisha baada ya mchungaji maarufu nchini Afrika Kusini, Alfred Ndlovu (44), kufariki dunia baada ya kufunga usiku na mchana kwa takribani siku 30 akitaka kuvunja rekodi ya Yesu Kristu aliyefunga siku 40 bila kula kitu chochote.

Kama alivyofanya Yesu Kristu, Mchungaji Ndlovu naye aliondoka nyumbani kwake Juni  17 mwaka huu na kuelekea nyikani kwa ajili ya kufunga na kuomba, huku akiweka pembeni anasa za dunia.
Kifo cha mchungaji huyo kimeishangaza sana familia yake, waumini wa kanisa lake na jamii nzima kwa ujumla.

Mchungaji huyo alijulikana kwa imani yake thabiti ambayo  ingeweza hata kuhamisha milima.
Mmoja wa wanafamilia ya mchungaji huyo alisikika akilalamika; “Alikuwa mtu wa imani sana. Lakini kwa bahati mbaya amefariki kifo hicho. Baada ya mwezi ndipo tumepata taarifa za kifo chake”

Akijaribu kuvunja rekodi ya Yesu, Mchungaji Ndlovu alifariki baada ya kufunga kwa takribani siku 30 japokuwa hakuwahi kuripotiwa kuwa na ugonjwa wowote hapo awali. Alikuwa peke yake nyikani na maiti yake iligunduliwa na mpita njia mmoja aliyetoa taarifa polisi.

Vigogo wa Shirika la Ndege Tanzania ATC Watumbuliwa

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa  Makame Mbarawa amewasimamisha vigogo wawili wa Shirika la Ndege Tanzania (ATC) kwa tuhuma za kufanya figisufigisu katika masuala ya uteuzi wa marubani wanaotakiwa kwenda kusoma nje ya nchi.

Mbarawa amedokeza hayo leo alipokuwa akizungumza na wafanyakazi wa walio chini ya wizara yake katika Bandari ya Itunge wilayani Kyela ambapo alisisitiza kwamba hawataki wafanyakazi wababaishaji.

“Leo asubuhi nimewasimamisha kazi  Mkurugenzi Mkuu  Kapteni  Johnson Mfinanga  wa ATC na Mkurugenzi wa Kitengo cha Uendeshaji katika shirika hilo, Sadick Muze wa shirika hilo kwa sababu za kufanya kazi  kwa ubabaisha’’ amesema.

Maendelea ya Mwanamuziki Ray C Baada ya Kupelekwa Kituo cha Wahanga wa Madawa ya Kulevya

$
0
0
MSANII mkongwe wa Muziki wa Kizazi Kipya aliye katika majaribu makubwa ya matumizi ya madawa ya kulevya, hivi sasa anadaiwa kuwa full kicheko kufuatia mabadiliko makubwa ya afya yake tangu alipoanza kupata matibabu katika kituo cha wahanga wa ‘sembe’, Sober House kilichopo Bagamoyo mkoani Pwani.

Kwa mujibu wa bosi wa kituo hicho, Karim Bhanji, Ray C hivi sasa yupo vizuri tofauti na zamani na kwamba kwa jinsi anavyoendelea, hali yake inazidi kutengemaa.

Ray-new“Unajua tatizo kubwa kwa Ray C ilikuwa kwamba alikuwa anapatiwa matibabu bila uangalizi wa kutosha. Ingawa alikuwa akinywa dawa, lakini kilichokuwa kinatokea ni kuwa anakwenda Mwananyamala kunywa dawa halafu anarudi nyumbani, huko mtaani anakutana tena na watu walewale anaendelea kutumia.

“Lakini kwa kuja hapa, baada ya dawa anadhibitiwa, hatoki hivyo hapati nafasi ya kujaribu tena kutumia unga, nina imani hali yake itaimarika kadiri muda unavyoenda,” alisema Bhanji na kuongeza kuwa akiwa kituoni, Ray C ameshaanza kuandika baadhi ya mistari ya Bongo Fleva.
Ray C alipelekwa katika kituo hicho na wasamaria wema Juni 18, mwaka huu, baada ya video kusambaa mitandaoni, ikimuonesha akiokolewa na polisi baada ya kudaiwa kutaka kujidhuru kutokana na kuzidiwa na matumizi ya madawa ya kulevya.

Kituo hicho cha Sober House pia kiliwahi kumpokea Mbongo Fleva mwingine, Chid Benz ambaye hata hivyo hakukaa kwa muda mrefu.

Meneja wa Diamond Ahenyeshwa na Hukumu ya Utapeli...

$
0
0
BAADA ya juzikati Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kutoa hati ya kukamatwa kwa meneja wa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Hamis Taletale ‘Babu Tale’ (picha kubwa) kwa kutotii amri ya mahakama iliyomtaka kumlipa Shehe Hamis Mbonde Sh. Milioni 250 kwa kupatikana na hatia ya kumtapeli kazi zake za mawaidha, meneja huyo alijikuta akirudishwa kortini hapo huku akihenyeshwa.

Kesi hiyo ambayo ilisikilizwa kwa zaidi ya miaka miwili na kutolewa hukumu, Februari, mwaka huu ilionesha kuwa, Kampuni ya Tip Top Connection ambayo Babu Tale ni mmoja wa wamiliki, ilitoa na kusambaza kwa kuuza DVDs za mawaidha ya Shehe Mbonde (mojawapo Uzito wa Kifo) bila makubaliano maalum.

Kwa mujibu wa chanzo, Babu Tale alifikishwa mahakamani hapo, Jumanne iliyopita chini ya ulinzi mkali wa jeshi la polisi huku akionekana kuchoka sana, pengine kwa mawazo au kwa kutolala sawasawa kama binadamu.

Mbali na hali hiyo, pia Babu Tale siku hiyo alivaa suruali ya jinZi iliyochanika kwenye magoti. Haikujulikana ni fasheni au kulikuwa na misukosuko alikotokea. Chini, kwa maana ya miguuni alivaa ndala au kandambili hali iliyompotezea uhalisia wake.

Afande mmoja aliyekuwa kwenye msafara wa gari lililombeba Babu Tale, aliliambia Amani kuwa, jamaa huyo  alitokea Mahabusu ya Kituo cha Polisi, Mbezi Kwa Yusuf jijini Dar ambako alilala kwa siku moja baada ya kukamatwa, Jumatatu jioni, nyumbani kwake, Mbezi ya Kimara.
Hata hivyo, mahakamani hapo, Babu Tale alikuwa na mawakili wanne kwa ajili ya kutengua hukumu ya awali ya mahakama kuhusu kutakiwa kulipa kiasi hicho cha pesa, lakini baada ya shauri hilo kusikilizwa kwa zaidi ya dakika 45, ilishindikana.

Mawakili wake wakaomba muda wa kwenda kupitia tena shauri zima mwanzo hadi mwisho jambo lililomsukuma hakimu  kuahirisha kesi hiyo mpaka Ijumaa (kesho).
Ilizungumzwa mahakamani hapo kuwa, Babu Tale aliachiwa huru kwa masharti ya kufika mwenyewe Ijumaa bila kukosa.

Gazeti hili lilimtafuta Babu Tale bila mafanikio yoyote kwani simu yake ya mkononi haikupatikana hewani baada ya kutoka mahakamani.

Kesi ya msingi ya Babu Tale ilishasikilizwa na hukumu kutolewa ambapo alitakiwa kulipa fidia hiyo kwa mlalamikaji lakini ikadaiwa kuwa, meneja huyo hakutii hukumu hiyo.

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Ijumaa ya August 5

$
0
0


SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Ijumaa ya August 5

Polisi Wamnyima Tundu Lissu Dhamana, Atupwa Rumande

$
0
0
JESHI la Polisi, kanda Maalumu ya Dar es Salaam limemnyima dhamana, Tundu Lissu, Mwanasheria Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), baada ya kumaliza kuhojiwa katika kituo kikuu cha polisi.

Baadhi ya viongozi waliofika kumwekea dhamana  ni pamoja na  Freeman Mbowe Mwenyekiti wa Chadema, Edward Lowassa Waziri Mkuu wa zamani na mjumbe wa kamati kuu wa Chama hicho, aliyefika saa 12:14 jioni akiungana na viongozi na wanachama wa chama hicho.

Baada ya kufika Lowassa wanachama na wafuasi wa Chadema waliokuwa nje ya ofisi hizo za polisi walianza kuimba wimbo wa kumuita rais, rais, rais ikiwemo na kauli mbiu ya maarufu ya Peoles power.

Mara baada ya kufika alipokelewa na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe aliyekuwa amepanda gari moja na Meya wa Kinondoni, Boniface Jacob waliokuwa nje ya geti.

Viongozi hao waliokuwa nje baada ya kuzuiwa kuingia ndani na polisi waliongozana na Lowassa kuomba kuingia lakini walizuiwa hali iliyofanya wachukue uamuzi wa kuondoka.

Kiongozi aliyeruhusiwa kuingia alikuwa ni Meya wa Dar es Salaam, Isaya Mwita.

Akizungumzia kuhusu hilo, Peter Kibatala mwanasheria wa Lissu alisema kwamba mahojiano kati ya jeshi hilo na mtuhumiwa yalianza saa 9:30 hadi saa 12:30.

“Katika maelezo ya polisi wanasema kwamba wakati Lissu akitoka mahakamani juzi kwenye kesi yake  alitamka maneno ya uchochezi, lakini haya yote yanahitaji ushahidi,” alisema Kibatala.

Wakili huyo alisema kwamba polisi baada ya kumaliza mahojiano na wao wakiwa wameandaa utaratibu wa dhamana walikataliwa hadi leo Ijumaa atakapofikishwa mahakamani.

Uwanja Mpya wa Ndege Dar Kukamilika Mwakani

$
0
0
MAMLAKA ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA) imeainisha mikakati yake ya kufanya maboresho katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kwa kuboresha jengo la abiria (terminal II), ambayo yataenda sambamba na ujenzi wa terminal III.

Aidha, imesema iko kwenye mchakato wa kufanya upembuzi yakinifu kwa ajili ya ujenzi wa njia ya kurukia ndege. Pia, imepanga kuoanisha mifumo ya mawasiliano na usalama katika majengo matatu ya abiria ya uwanja huo (terminal I, II, III).

Hayo yameelezwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Ramadhan Maleta wakati akizungumza na viongozi wa dini na wajumbe wa Kamati ya Amani ya Mkoa wa Dar es Salaam, waliotembelea ujenzi wa mradi huo wa jengo hilo. Maleta alisema maboresho ya jengo la terminal II, yataanza mwakani na kwamba kwa sasa Serikali iko katika mchakato wa kutafuta pesa kwa ajili ya kufanya maboresho hayo.

“Tunataka kujenga njia nyingine ya kurukia ndege, kwa sababu wataalamu walifanya utafiti wakasema kwamba kufikia mwaka 2025, barabara hii moja ya sasa haitatosha kwa matumizi,” alisema Maleta.

Awali, akizungumza kwenye ziara hiyo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo na Shehe wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum alisema mradi huo kama utakamilika kwa wakati, utawasaidia Watanzania na pia utaongeza idadi ya ndege kubwa kutua nchini.

Alisema ujenzi wa jengo hilo ni ishara tosha kuwa Serikali inafanya kazi kubwa ya kuwaletea wananchi wake maendeleo na kwamba kamati hiyo itashirikiana na Serikali si tu katika kuhamasisha masuala ya amani bali hata maendeleo.

“Mradi huu si tu utawasaidia Watanzania, lakini pia utaleta heshima kwa nchi kwa kuwa na viwanja vinavyoendana na hadhi ya Watanzania. Sisi tunaunga mkono juhudi za Serikali kuwaletea maendeleo wananchi,” alisema Shehe Alhad.

Katibu wa Kamati hiyo, Padri John Solomon alisema kikubwa kilichowafanya kutembelea mradi huo ni kutaka kuona juhudi za Serikali, kuhakikisha Tanzania inakuwa na uwanja mkubwa wa kisasa.

Mbali na ziara hiyo, kamati hiyo pia ilitumia nafasi hiyo kufanya maombi na dua kwa ajili ya mradi huo ili uweze kukamilika salama, bila kutokea kwa tatizo la aina yoyote ambalo linaweza kukwamisha.

Akitoa ufafanuzi wa mradi huo, Mkurugenzi wa Mradi huo, Mohammed Millanga alisema, ujenzi wa jengo hilo litakalohudumia abiria milioni sita kwa mwaka, unatarajiwa kukamilika Desemba mwakani.

Alisema hadi sasa mradi huo ambao ulikuwa utekelezwe kwa awamu mbili kwa sasa, awamu hizo zinatekelezwa kwa pamoja na umekamilika kwa asilimia 45.

Hata hivyo, Millanga alitaja baadhi ya changamoto, kuwa ni maandalizi ya ufunguzi wa jengo hilo, ambapo alisema wameshaanza kulifanyia kazi jambo hilo. Changamoto nyingine ni jinsi ya kuoanisha mifumo ya mawasiliano na usalama katika majengo matatu ya abiria.

“Kitu kingine ni kwamba wadau walikuwa wanataka mambo mbalimbali, lakini sisi inabidi tufanye kazi ndani ya bajeti iliyopangwa ili mambo yaweze kwenda vizuri,” alisema Millanga.

Ushindi wa KRC Genk ya Samatta Uliyoipeleka round ya 3 Europa League

$
0
0
Ni muendelezo wa good news kwa nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars anayeichezea klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta kuwa sehemu ya kikosi cha KRC Genk kilichoisaidia timu kupata matokeo ugenini dhidi ya wenyeji wao Cork City.

Katika mchezo huo wa pili wa round ya pili KRC Genk wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya wenyeji wao Cork City ya Ireland, mchezo huo ambao umechezwa katika uwanja wa Turners Cross nchini Ireland, umekuwa ni furaha kwa watanzania kuona Samatta anaelekea kutimiza lengo lake la kucheza hatua ya Makundi ya michuano ya Europa League.

Tazama Video Mpya ya Chege ft. Diamond ‘Waache Waoane’ Humo Ndani Mh. Temba Ndio Kaoa

$
0
0
So Chege Chigunda na Diamond wametuletea single mpya inaitwa ‘waache waoane‘ na video imefanywa South Africa, ni ngoma ya Chege ambayo kamshirikisha Diamond… ukishaitazama usiache kutoa comment yako maana ni lazima watapita kusoma watu wao wameipokeaje.
Video:

Vinywaji Vya Kutia Mwili Nguvu, Vina Athari Za Kiafya

$
0
0
Wengine, hasa madereva, hupenda kutumia vinywaji hivi ili kuondoa uchovu na kuwafanya wasipate usingizi. Hufanya hivyo ili wasisinzie na kusababisha wasababishe ajali.

Kwa upande mwingine pia, wapo wanaokunywa vinywaji hivi vya kuongeza nguvu kama starehe au mbadala pale wanapokuwa hawatumii vilevi.

Duniani kote matumizi ya vinywaji vya kuongeza nguvu kwa sasa yameongezeka kuliko unavyofikiria. Takwimu zilizotolewa katika utafiti uliochapishwa mwaka 2009 katika jarida la ‘Drug Alcohol Dependence’ toleo la 99(1–3), zinaonyesha kuwa mwaka 2006 pekee, takribani aina mpya 500 za vinywaji hivi ziliingizwa sokoni.

Ongezeko hili kubwa la vinywaji vya kuongeza nguvu, linazua mashaka kwa wataalamu wa afya kuhusu usalama wa afya ya jamii. Hii ni kutokana na ukweli kuwa, matumizi makubwa ya vinywaji hivi yanaambatana na madhara ya afya ya mwili na akili kwa watumiaji.

Watanzania wengi hasa vijana kwa sasa wanapendelea kutumia vinywaji hivi kwa wingi. Kwa sasa soko la vinywaji baridi limejaa vinywaji vya kuongeza nguvu. Ni jambo la kawaida kuona watu wazima na watoto wakinywa vinywaji hivi safarini, katika sherehe mbalimbali na katika kumbi za starehe. Vinywaji hivi huuzwa kwa wingi katika maduka makubwa (Super markets), maduka madogo, hotelini na katika migahawa.

Miongoni wa watumiaji wakubwa wa vinywaji hivi ni wanamichezo na madreva hasa wa magari yanayofanya safari za masafa marefu, ambao wanaamini kuwa kwa kutumia vinywaji hivi huongeza nguvu za mwili, kasi ya vitendo, umakini na kupunguza uwezekano wa kupata usingizi. Watu wengi wanapotumia vinywaji hivi pia huvichanganya na pombe.

Vinywaji vya kuongeza nguvu, visivyo na kilevi,  kisayansi vinaelezwa vina kiasi kikubwa cha kafeini, vitamini pamoja na kemikali za taurine, glucuronolactone.

Wakati mwingine pia huongezewa dawa aina ya guarana pamoja na mitishamba aina ya ginseng kwa lengo la kusisimua akili na kuongeza nguvu za mwili.

Mtafiti wa madhara ya dawa za kulevya wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Dk Stephen Nsimba anasema kwamba vinywaji hivi vina kiasi kikubwa cha kafeini ambayo ni dawa inayosisimua ubongo na kwa kuvichanganya na pombe athari zake kwenye mfumo wa fahamu za mwili huongezeka.

“Baada ya kuchanganya vinywaji hivi, kafeini katika vinywaji vya kuongeza nguvu, hupunguza athari za kilevi na kumfanya mtumiaji asibaini haraka kuwa amekunywa kiasi kikubwa cha kilevi. Hili ni jambo la hatari” anaonya Dk Nsimba.

Habari mbaya zaidi ni kwamba baadhi ya watengenezaji wa vinywaji hivi huweka kiasi kikubwa cha kemikali kuliko inavyotazamiwa katika hali ya kawaida na hawaonyeshi katika lebo ama karatasi ya maelezo inayobandikwa kwenye kifungashio.

April mwaka jana, Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TDFA) ilikamata makopo 1,526 ya vinywaji vya kuongeza nguvu katika soko la Tanzania ambavyo vilikuwa havikidhi viwango vya ubora na usalama kwa matumizi ya binadamu.

Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya Mkurugezi wa TFDA, Hiiti Sillo aliyoitoa Aprili  3, 2014 wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Matokeo ya utafiti mmoja yaliyowasilishwa katika mkutano wa mwaka 2013 wa Chama cha Afya ya Moyo cha Marekani (American Heart Association) uliofanyika katika mji wa New Orleans, ilibainika kuwa kunywa kopo moja hadi matatu ya vinywaji vya kuongeza nguvu, kunaweza kusababisha moyo udunde bila mpangilio na kuongeza shinikizo la damu.

Utafiti huo unaongeza kusema kuwa, hali kama hiyo inaweza kusababisha  kifo cha ghafla au magonjwa sugu kama vile shinikizo la damu, kisukari na kiharusi kwa baadhi ya watu.

Dk Gordon F. Tomaselli, ambaye ni msemaji wa American Heart Association (AHA) anasema: “Ingawa jambo hili linaoneka kama dogo lakini linaweza kusababisha madhara makubwa kwa baadhi ya watu. Wale walio na magonjwa ya moyo au historia ya magonjwa hayo katika familia zao, ni lazima wajiepushe na utumiaji wa vinywaji vya kuongeza nguvu.”

Baadhi ya watu wanaokuwa hawana habari kuwa wana magonjwa ya moyo hasa pale, ugonjwa unapokuwa katika hatua za mwanzo, wanaweza kuhatarisha maisha yao kwa kunywa vinywaji vya kuongeza nguvu ambavyo vina kiasi kikubwa cha kafeini.

Kiasi kikubwa cha kafeini kinaweza kusababisha shinikizo la damu, kuweweseka, kukosa usingizi, maumivu ya kichwa na degedege.

Baadhi ya watafiti wanabainisha kuwa vinywaji hivi pia vinaweza kusababisha ugonjwa wa kisukari.

Utafiti wa Dk. D.C. Greenwood na wenzake uliochapishwa katika jarida lijulikanalo kama Europian Journal of Epidemiology, toleo la 25(4) la mwaka 2010, unabainisha kuwa matumizi ya vinywaji vya kuongeza nguvu wakati wa ujauzito, unaweza kusababisha mimba kuharibika, kuzaa mtoto mfu au kuzaa mtoto mwenye uzito pungufu.

Kina mama wanaonyonyesha pia wanapotumia vinywaji hivi huwasababishia watoto wao matatizo ya kiakili ikiwa ni pamoja na kulia kupita kiasi.

Vijana wanaotumia vinywaji hivi, pia wanakabiliwa na hatari ya kutumbukia katika matumizi ya dawa za kulevya, tumbaku na ulevi wa pombe wa kupindukia.

Utafiti wa hivi karibuni nao umebaini kuwa vijana na watoto wanaotumia vinywaji hivi hupata athari za kiakili kiasi kwamba uwezo wao wa kujifunza na kutambua mambo unaathirika.

Hii ni kwa mujibu wa utafiti wa T. Van Batenburg-Eddes na wenzake uliochapishwa katika jarida la Front Psychology toleo la 5, mwaka 2014.

Utafiti wa jeshi la Marekana uliochapishwa mwaka jana unabainisha kuwa, wanajeshi wengi wanaokunywa vinywaji vya kuongeza nguvu wanakabiliwa na hatari ya kujiua.

Utafiti huo unaongeza kusema kuwa wanajeshi wanaochanganya vinywaji vya kuongeza nguvu pamoja na pombe wanakabiliwa na hatari kubwa zaidi ya kujiua. Hii ni kwa mujibu wa utafiti wa H.B. Mash na wenzake uliochapishwa katika jarida la Social Psychiatry and Psychiatric Epidemiology, toleo la 49(9).

Kutokana na athari za vinywaji hivi kiafya, jamii inashauriwa kupunguza au kujiepusha na matumizi yake.

Ni busara pia mamlaka za kiserikali na kidini zinazohusika na usalama wa afya ya watoto zikasaidia kuielimisha jamii kwamba watoto na vijana walio chini ya miaka 18 wasitumie vinywaji hivi. Ni vyema vinywaji kama hivi vikapigwa marufuku.

Sababu za TAKUKURU Kumkamata Rais wa Simba Evans Aveva

$
0
0
Asubuhi ya August 4 2016 taarifa zilianza kusambaa katika mitandao ya kijamii kuhusiana na Rais wa Simba Evans Aveva kutiwa mikononi mwa Polisi kutokana na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) kuagizwa kukamatwa kwa kiongozi huyo. millardayo.com ilifanikiwa kumpata kaimu afisa msemaji wa TAKUKURU Tunu Mleli na kuweka wazi.

“Ni kweli Aveva amekamatwa na polisi baada ya TAKUKURU kuagiza hivyo kutokana na tuhuma za rushwa zinazomkabili, tuhuma zinazomkabili ni uchepushwaji wa fedha kutoka account ya Simba kwenda katika account yake na baadae kuanza kufanyiwa mgawanyo katika account nyingine, ni fedha za usajili wa Okwi kutoka Etoile du Sahel”

Gigy Money Afunguka 'Nazaa na Idris Sultan wa Wema Sepetu'

$
0
0
Msanii wa muziki ambaye pia anafanya ‘modeling’ na utangazaji kwenye Kituo cha Redio cha Choice FM cha jijini Dar, Gift Stanford ‘Gigy Money’ amejitangazia ushindi wa kumnasa aliyekuwa mpenzi wa Wema Sepetu, Idris Sultan huku akitamba kuwa, sasa atamzalia mtoto.

Awali kulikuwa na vita nzito kati ya Wema na Gigy ambapo wakati Wema akiendelea kupalilia penzi lake, Gigy aliibuka na kudai kuwa, atahakikisha anampata Idris akiamini kuwa ndiye mwanaume wa ndoto zake.

Kufuatia vita hiyo ambayo iliibuka baada ya Gigy kunaswa na Idris usiku wakiwa kimahaba kwenye ukumbi mmoja wa burudani uliopo Mikocheni jijini Dar, Wema hakuonesha kujali badala yale aliendeleza msimamo wake kuwa yeye ndiye ‘Mrs’ Idris na wengine waliokuwa wakijipendekeza hawakuwa na chao.

Gigy ajiweka pembeni

Kufuatia Wema kukomalia penzi lake, Gigy alijishtukia na kuamua kukaa pembeni licha ya kwamba mara kadhaa alikuwa akisema kuwa ipo siku atatimiza ndoto yake ya kutoka na Idris.

“Mimi kwa kweli nampenda sana Idris, najua yuko na Wema lakini ipo siku kile ninachokiwaza kitatimia,” alisema Gigy miezi kadhaa iliyopita akionesha kuwa hatakata tamaa kupigania penzi la mshikaji huyo.

Wema, Idris watibuana

Katika kile ambacho kilionekana ni furaha kwa Gigy, hivi karibuni Idris aliibuka na kusema kuwa, yeye na Wema wameachana na vile walivyoonekana pamoja kwenye ile shoo ya Black Tie iliyofanyika kwenye Ukumbi wa King Solomoni, Upanga jijini Dar mwezi uliopita ilikuwa ‘kupritendi’ tu.

Katika kuonesha kuwa kweli amefunga ukurasa wa mapenzi na Wema, Idris alisema kuwa, siku si nyingi atamtangaza mpenzi wake mpya, jambo ambalo lilikuwa likisubiriwa kwa hamu na wengi.

Baada ya Idris kutoa tamko hilo, siku chache baadaye alionekana akijiachia ‘kimalovee’ na Gigy ambapo alipoulizwa kama mwanadada huyo aliyefungashia kinoma ndiye aliyechukua nafasi ya Wema, hakuwa tayari kuongea lolote ila Gigy alipotafutwa alisema kuwa, sasa ni mwendo wa mahaba niue.

Gigy atangaza kumzalia Idris

Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Gigy alisema kuwa, Wema amechemka katika suala la kumzalia Idris aliyekuwa na hamu ya kuitwa baba, sasa yeye atahakikisha ndani ya siku chache zijazo anabeba mimba.

“Nilisema kwamba ipo siku ndoto yangu itatimia, Mungu kaniona na sasa najitahidi sana nisichukue siku nyingi niwe nimembebea mimba Idris na kumzalia mtoto.

“Unajua mimi nikimpenda mtu bwana inakuwa ni shida na lazima nimfanyie kitu ambacho kitakuwa historia, naweza kusema nina jini mahaba ambaye ananisumbua hivyo mkiniona kitumbo ndii, mjue ndiyo vile…” alisema Gigy.

Idris huyu hapa

Kufuatia kujigamba huko kwa Gigy, Ijumaa lilimtafuta Idris na kumuuliza kama kweli amejiandaa kuzaa na msanii huyo ambapo kama kawaida yake alisema ni kweli wako karibu na ukaribu wao unatokana na kwamba wanafanya kazi pamoja katika Kituo cha Redio cha Choice FM ila hayo mengine hataki kuyazungumzia.

Ikumbukwe kwamba, hata wakati Idris anaingia kwenye uhusiano na Wema alikuwa mzito kukubali lakini baadaye Wema akaamua kuweka mambo hadharani kwani mwanadada huyo si mtu wa kuwa kwenye penzi la kificho.

Chanzo:GPL
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live




Latest Images