Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live

Shamsa Ford: Baada ya Posa Muda Wowote Naolewa

$
0
0
BAADA ya kutolewa barua ya uchumba na mpenzi wake mpya, Chidi Mapenzi, mwigizaji, Shamsa Ford, amefunguka kwamba wakati wowote atafunga ndoa na mwanaume huyo kwa kuwa mipango yao imeshakamilika.

Shamsa aliliambia MTANZANIA kwamba licha ya kupitia katika changamoto za wapenzi wengi, mpenzi wake huyo wa sasa ndiye aliyeonyesha ushawishi hadi kutaka kumuoa.

“Kwa hatua hii najivunia, hadi mwanaume akushawishi muoane huyo ana nia njema na heshima kwangu,” alisema Shamsa.

Pia Shamsa aliwaeleza wapenzi wa filamu zake kwamba wataendelea kupata burudani zake hata kipindi atakachokuwa ameolewa.



Tundu Lissu Funga Kazi, Polisi Watweta

$
0
0
TUNDU Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki amefikishwa katika Kituo cha Polisi cha Kati jijini Dar es Salaam kwa mahojiano, polisi wamekuwa na kazi ya ziada, anaandika Shaban Matutu.

Idadi ya polisi kwenye kituo hicho imeongezwa wakati alipofikishwa huku shughuli nyingine ndani ya kituo hicho zikionekana kusimama.

Awali, Lissu ambaye ni Mwanasheria wa Chadema hakua akijulikana alipo kutokana na polisi kutotoa taarifa kamili baada ya kumkamata jana jioni.

Lissu amefikishwa kwenye kituo hicho leo saa 7:54 mchana na gari aina ya Land Cruser lenye namba za usajili T 312 CWM akiwa chini ya ulinzi mkali.

Amefikishwa kwenye kituo hicho kwa ajili ya mahojiano kutokana na madai ya kutoa kauli ya kichochezi ‘dikteta uchwara’ juzi wakati akiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu alipoenda kusikiliza kesi ya uchochezi iliyohusu kauli yake ya awali ya ‘dikteta uchwara’.

Wakati Lissu akifikishwa eneo la kituo hicho, polisi walikuwa wamezunguka eneo hilo huku kukiwa na  ulinzi mkali pamoja na silaha za moto.

Askari waliokuwa eneo hilo walikuwa wakiwaondoa wananchi na waandishi wa habari waliokuwa wakifuatilia matukio katika eneo hilo.

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema Taifa alifika kituoni hapo saa kumi kasoro, hata hivyo alizuiwa kuingia ndani.

Saa 4:02 Isaya Mwita, Meya wa Jiji la Dar es Salaam kituoni hapo na gari lenye namba za usajili SM 10584 ambapo aliruhusiwa kuingia ndani kumuona Lissu ambaye anahojiwa.
Lissu bado anaendelea hojiwa…

Zamaradi: Kumhoji Shoga Clouds TV ilikuwa ni Ushindi Kwangu, Sijutii

$
0
0
Mtangazji wa kipindi cha Take One cha Clouds Tv amefunguka na kusema hajutii kitendo kitendo cha yeye kumhoji shoga kwenye television na kusababisha 'outrage' kutoka kwa wadau mbalimbali mtandaoni na hadharani
Anasema kipindi hicho ndio kiliwafungua watu na kujua kuwa kumbe kuna tatizo kama hili linaendelea Tanzania na serikali ikaanza kufumbua macho na kuanza kutoa matamko

Nimenusurika Ajali ya Ndege Dubai, ni Jambo la Kumshukuru Mungu

$
0
0
Wakuu nawasalimu!!
Ama hakika kama siku haijafika haijafika tu.July 16 2016 nilimsindikiza binamu yangu kwa ajili ya matibabu nchini India,yeye alikuwa atangulie na ndege ya Oman Air kupitia Muscat mpaka India ambapo mimi ningefuata siku tisa au kumi baadae.Kwa bahati mbaya siku hiyo ilitokea "dhahama" uwanjani hapo na safari kuahilishwa,hivyo waliondoka siku inayofuata.

Mimi niliondoka tarehe 26 July 2016 na Fly Emirates kupitia Dubai(DXB) mpaka India,nakumbuka ndege hiyo kutoka Dsm ilikuwa flight #EK726 A6-EMW B777-300(Hii ndio ndege iliyoungua jana Dubai).Tuliondoka Dsm majira ya saa kumi na moja na madakika kuja Dubai.Hakika safari ilikuwa nzuri na tamu wakati wote.Nilifika India salama kwa kufanya "connection" Dubai mpaka Mji wa Hospital tuliyokusudiwa kumpeleka mgonjwa.

Mgonjwa wangu anasumbuliwa na pingiri za mgongo,kiasi amepata matatizo ya baadhi ya vidole na sehemu fulani fulani z mwili zisiwe na mawasiliano(nisizungumzie sana ugonjwa na mambo yake).Walipofika India,Walionana na "Specialist" tuliyopangiwa kuonana nae,ambae alimtazama mgonjwa wetu,hata baada ya matibabu,alishauri mgonjwa apelekwe kwenye tiba fulani ya asili huko huko India,ambayo inapatikana katika mji(?) wa Trivandrum,Kusini mwa India.

Kwa sababu jamaa ndio alielekeza huko,ghalama fulani za kwenda huko zikawa juu yake,as yeye tulishamlipa pesa nyingi tu kama "familia".Huko kuna tiba asili za hatari sana,na hakika mgonjwa wetu amepata nafuu na anaendelea na matibabu vizuri kabisa kabisa.

Kwa vile mie nilikuwa na kalikizo kama ka week mbili,ilinibidi nirudi mapema nyumbani,Tukaondoka siku ya Jumatano hapo Thiruvananthapuram, India(TVR) majira kama ya saa 0950(local Time) kupitia Dubai(DXB) ili nifanye connection ya kuja Dsm the same day.Unfortunately ndege niliyotoka nayo Dsm-DXB ile 26/07/2016 ndio hiyohiyo ilikuja TVR,hivyo ilikuwa Flight #EK521 A6-EMW B777-300.

Tulisafiri kwa raha mustarehe na mavyakula ya kihindi,full pilipili hadi kwenye hotsoup,ni safari ya zaidi ya masaa matatu na dakika kama 45 hadi 50.Njia nzima huko juu hakukuwa na tatizo lolote.Ni tabasamu za wahudumu wa ndege na mwendo wa movie na music mwanzo mwenga.Tulipokaribia kutuwa kama dakika kumi hivi,tukaambiwa tufunge mikanda na tuwe tayari kwa kutuwa,wale wenye "Air sickness" wakagawiwa kama tuvitambaa kujiziba macho ili wasibabaike na kizunguzungu wakati wa kutuwa.

Tukiwa tumeshaambiwa sasa "tupo tayari kutua" na ndio tumeingua DXB,ghafla tukaona tena ndege inarudi juu,yaani kama imetaka kutuwa halafu ikanyanyuka tena kwa kasi sana,baadae tukasikia sauti tu,tukae kwa amani,rubani ataenda kama feet4000 then tutarudi kutuwa kwa amani.Hata hivyo tukazungukaaa weeee,huku tunauona uwanja kwa pembeni...kama baada ya nusu saa hivi,tukaona wale wahudumu wanaanza kutuelekeza yalipo maboya(?) ya kujiokolea,na ule mlango wa emergency exit akahamishwa mtu akaletwa abiria mwingine,ambaye aliekezwa jinsi ya kuubandua ule na kupitisha wengine.

Baada ya hapo ikasikika sauti ya "emergency landing....May day May day"(kama nilisikia vizuri).Hapo ndio sasa matumbo jotooo...Lakini wahudumu hapo walizidi kusisitiza hali itakuwa shwari tusiogope maana hata watu wa uokoaji wapo tayari na kuna matatizo katika tairi za ndege ni kama zimegoma kutoka ili tutue...na tukaelekezwa kuwa milango itajifungua kama puto/pulizo,hivyo wakati wa kushuka ni kuserereka/sliding na sio kutembea....Haikuchukua muda tukajibamiza chini,ghafla moto mkubwa na moshi wa hatari...Mimi hata nilivyobebwa sijui nilibebwaje,nikajikuta eneo fulani zimejaa ambulance,polisi,madaktari na manesi tu...huku wengine waliopata mshituko wakiingizwa humo kwenda Hospital.

Kifupi wapo waliojikojolea(mimi nilijkuta nimelowa tu,sasa sijui nilijikojolea au jirani yangu alichafua).Kwa kweli nilikumbuka mpaka sala ya "Malaika Mlinzi" aliyonifundisha Mama nikiwa darasa la kwanza,niliona ujirani wa dunia na mbingu,uhai na kifo...hakika ndani ya saa nzima nilikuwa karibu na Mungu kuliko wakati wowote ule maishani.Wenzetu wanajiandaa sana,pale palikuwa na Sheikh na Mapadre(Wachungaji) kwa ajili ya kuombea ama waliotaka kufa au waliozidiwa..Mpaka nilijiuliza,hili tukio "lilipangwa" au wenzetu wana utayari sana wa matukio kama haya??

Baada ya hapo kila mtu alitazamwa afya yake,kupimwa pressure,sukari na kila kitu...na tukapelekwa hotelini,na jamaa wanasema asiondoke mtu kama anajisikia vibaya,tukae mpaka mtu anapoona afya yake ipo timamu..kwa kweli mimi sikuumia chochote zaidi ya mshituko na kuteguka "enka" wakati naserereka mlangoni,maana milangoni kulikuwa na kama maboya yale ya Watoto Kunduchi beach.Lakini nimepewa matibabu babu kubwa,na nipo hotel...wakaniuliza nahisi siku ngapi za kupumzika,nimewaambia siku 10 ntakuwa ok!!

Hapa nipo Hotel ya Five Star toka jana wakuu,nakula tu na kulala..kila baada ya muda anakuja Dr kunijulia hali,mpaka "najuta" kusema siku 10...ningeongezapo kidogo.Mizigo yetu imeunguwa,ikiwepo laptop yangu na simu mpya nilizonunua India Duty Free,jamaa wanasema wanatulipa kwa kilo na si kwa thamani ya vitu vilivyokuwemo.

Nawasalimu toka hapa DXB(Hotel kapuni maana nilitoroka kazini),nikiwa mzima wa afya,baada ya siku kumi nitarudi nyumbani na kwenda "kutambika" moja kwa moja kijijini kwa bibi.Nahitaji kutoa sadaka kubwa mbele za Muumba,kwa makubwa yaliyotokea.Hakika hautaji Mungu kuhamisha mlima toka sehemu moja kwenda nyingine ndio uamini ukuu wake.Ahimidiwe yeye aliyeumba mbingu na dunia

Yuneda Entertainment Yarejea Sokoni

$
0
0
Kwakipindi kirefu sasa kampuni ya usambazaji wa filamu za kibongo nchini na nje ya nchi kukaa kimya kwa muda mrefu sasa  imerejea tena katika soko kwa kasi ya hajabu,

Kutokana na taarifa za mmoja ya watu wa ndani ya kampuni hiyo na aliomba jina lake lisitajwe, kampuni hiyo kwa sasa imeingia mikataba na baadhi ya wasanii wakubwa hapa bongo na walio lishika soko la filamu nchini, pia mtu huyo aliendelea kusema kuwa kwa sasa kampuni hiyo inamalizia kushoot filamu yake nchini China na  wataelekea South Africa kumalizia scen nyingine kisha watarejea tanzania.

Chanzo hicho kilieleza kuwa Kampu inayo mambo mengi mapya na kuwa Yuneda Entertainment itakuwa sokoni mnamo tarehe 10/08/2016 wakitoa filamu yao ya SITA MARA MBIRI (6X2)na kufuatiwa na  filamu zinazo julikana kwa majina ya  BIRIKA na CASE + CASE.

Hii ndio filamu inayo sadikika kuwa inatoka tarehe 10/08/2016 ijulikano kwa jina la SITA MARA MBIRI (6x2)

Undani Askofu Aliyefunga Siku 40 Kufia Chumbani

$
0
0
Imefichuka!  Kifo cha Askofu wa Kanisa la Taliteha, Ubungo jijini Dar, Fred Mwarusi (45) kilichotokea chumbani kwake, Makuburi, Jumapili iliyopita kimezua mengi na mazito, Amani limefuatilia kwa kina.

 Mwili wa marehemu huyo ulibainika na majirani baada ya kusikia harufu kali kutokea kwenye chumba chake kutokana na kutomwona akiingia wala kutoka kwa siku kadhaa.


 Kwa mujibu wa chanzo makini, kabla ya kifo chake, Askofu Mwalusi alijifungia chumbani mwake kwa siku kadhaa nyuma kwa ajili ya kufanya maombi ya uponyaji kwa maradhi yaliyokuwa yakimsumbua ambayo hayajajulikana mara moja.


 ALIKATAA KWENDA HOSPITALI


“Askofu Mwalusi alikuwa akisumbuliwa na maradhi f’lani hivi, yalimfanya afya yake kudhoofu. Majirani zake na  waumini wake walimshauri mara kwa mara kwenda kutibiwa hospitali ili arejeshe afya yake, lakini alikuwa akigoma kwa maelezo kwamba, atafanya maombi, atapona kwa Jina la Yesu.


 “Alikuwa akisema dawa pekee kwenye matatizo yake ya kiafya ni maombi tu na kuonesha kuwashangaa sana waliokuwa wakimshauri habari ya kwenda hospitali,” kilisema chanzo.


MMOJA WA MAJIRANI ANENA
Akizungumza na Amani juzi kwenye msiba wa askofu huyo, mmoja wa majirani zake aliyekataa katakata jina lake kuandikwa gazetini, alisema siku ya mwisho kumuona marehemu huyo ilikuwa Ijumaa ya Julai 29, mwaka huu ambapo aliingia ndani kwake halafu akasikika akifanya maombi kwa kumuomba Mungu ampe afya njema.


 “Nilimsikia akimwomba Mungu ampe afya njema. Lakini baada ya maombi hayo ya nguvu, nikamsikia akikemea pepo kwa sauti ya chini sana kisha sikumsikia tena mpaka leo (Jumapili) ndiyo tukaanza kusikia harufu ikitoka chumbani.”


 WASIWASI ULIANZA
“Lakini kuna wakati tuliingiwa na wasiwasi kwa kutomuona mwenzetu akifungua mlango wake tangu Ijumaa jambo ambalo halikuwa la kawaida kwake. Alikuwa mtumishi wa Mungu mwenye harakati za kiroho kila wakati, akiingia na kutoka, pengine akiwa anaimba nyimbo mbalimbali.”



 “Kufuatia hali hiyo, tuliambizana kuwa tupige simu polisi ambao walifika hapa na kuvunja chumba chake, wakamkuta amefariki dunia,” alisema jirani huyo.


 SERIKALI YA MTAA
Akizungumzia tukio hilo Jumatatu iliyopita, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Makuburi Kibangu, Moshi Kaftani alisema alipewa taarifa za kifo cha mtumishi huyo wa Mungu na mmiliki wa nyumba, Peter Mrema ambapo alishirikiana na polisi kuvunja mlango na kumkuta ameshafariki dunia huku kukiwa na harufu kali chumbani humo.

“Huyu marehemu ni mwananchi wangu ambaye alikuwa askofu na baadhi ya waumini wake ni wale pale unaowaona na wachungaji wake walikuwepo hapa lakini sasa hivi wameshaondoka.”


 ALIKATAA KUOA MPAKA…
“Marehemu licha ya kuwa na umri wa miaka 45 lakini hakuwa na mke wala mtoto. Alipokuwa akiulizwa sababu ya kuishi bila mke alisema anasubiri aoteshwe na  Mungu kwa kuoneshwa ndotoni ndiyo amuoe.

“Licha ya kuisubiri ndoto hiyo kwa muda mrefu lakini haikuwa imemtokea mpaka umauti ulipomfika,” alisema mwenyekiti huyo.


 POLISI WATOA MWILI, MAJIRANI WALIA
Paparazi wetu aliushuhudia mwili wa baba askofu ukitolewa nyumbani hapo alipokuwa akiishi na Askari wa Kituo cha Polisi Mbezi Louis jijini Dar kwa ajili ya kwenda kuufanyia uchunguzi huku majirani zake wakisikitika, wengine wakilia kwa uchungu.


MZOZO WA MAZISHI?
Juzi Jumanne, kulidaiwa kuibuka kwa mzozo wa eneo sahihi la kumzikia marehemu huyo ambapo, baadhi ya ndugu walisema asafirishwe kwenda Mbeya lakini mama wa marehemu akisema azikwe jijini Dar. Hata hivyo, mwenyekiti wa serikali ya mtaa alikanusha kuwepo kwa mzozo.

Mwili wa marehemu ulizikwa Jumanne iliyopita kwenye Makaburi ya Ubungo Maji jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na waumini wake, majirani na wachungaji huku ibada ya mazishi ikiongozwa na Askofu David Mwasota wa Kanisa la Naioth Gospel Assembly la jijini Dar.

KAMANDA WA POLISI
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Christopher Fuime alithibitisha kutokea kwa tukio hilo bila kufafanua zaidi.

Waandishi: Richard Bukos na Gladness Mallya.

Source: Global Publisher

MABASI ya Dar Mbeya, Mwanza Sasa Kuchukua Siku Mbili Njiani Badala ya Siku Moja..

$
0
0
Waliozoea kusafiri kwa mabasi kwa siku moja kutoka Dar es salaam kwenda Mbeya na kutoka Dar es salaam kwenda Mwanza na kwingineko kwenye umbali sawa na huo, sasa inabidi wajipange kisaikolojia kutumia siku mbili kukamilisha safari hizo. Hayo yamebainishwa na Meneja Usalama Barabarani na Mazingira wa SUMATRA, Geofrey Silanda. Uamuzi huo umetokana na utafiti uliofanywa na mamlaka hiyo na kubaini kwamba mabasi yanayofanya safari kwenye mikoa hiyo hayapaswi kusafiri kwa siku moja.

Toa maoni yako

Baba Amwandaa Mtoto Wake Aje Kuwa Raid wa Tanzania 2050, Wasafiri Kwa Baiskeli Kutoka Singida Hadi Dar

$
0
0
Huyu dogo anaitwa Yusuph Mohamed Nassor (2), baba yake Mzee Ahmed Nassor (67) amesema wakati ana mwaka mmoja na nusu alisema anataka kuwa Rais hivyo anamuandaa kuja kuwa Rais wa Tanzania mwaka 2050 kupitia Chama Cha CCM. Yeye na Baba yake wamekuja Dar es Salaam kutoka Singida kwa usafiri wa baiskeli kuja kuonana na Rais Magufuli

Nini maoni yako hapo?

Send Off ya Mchumba wa Masanja Mkandamizaji iliyofanyika Tar 4 Aug 2016

$
0
0

Send Off ya Mchumba wa Masanja Mkandamizaji iliyofanyika Tar 4 Aug 2016, Nimekuwekea Video Hapa Chini:

VIDEO:Kama Jeshi Ndio hivi Mimi Siendi Hata kwa Dawa

$
0
0
Hii Video inaonyesha wanajeshi wakiwa katika mafunzo yao ya kila siku ili kuwa mkakamavu kuhimili mikiki ya vitani...Embu tazama hii video utawaonea huruma, Hao ni wanajeshi wa West Africa.....

Huu ndio Utajiri wa Zari The Boss Lady. Wema Sepetu Hagusi Hata Robo

$
0
0
Je unamjua Vizuri Zari Hassan Mama Mtoto wa Mwanamuziki Diamond Platnumz?
Video hii Hapa chini itakupa kujua Zari ni Nani pamoja na thamani ya utajiri wake
Tazama Video:

Rage amemtaka Hans Poppe kumuomba radhi la sivyo atampeleka Mahakamani

$
0
0
Mwenyekiti wa zamani wa Simba Ismail Aden Rage, amemtaka Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe kumuomba radhi ndani ya siku tatu.

"Nadhani mtu mwendawazimu tu anaweza kufanya hivyo, mke wangu hana hata akaunti. Nimeshamuambia wakili wangu amshughulikie, aniombe radhi ndani ya siku tatu. La sivyo suala hili litaenda mahakamani,” alisema Rage.

“Sasa hivi tunazungumzia suala la fedha za Okwi na si fedha za Samatta,” aliongeza Rage.

Rage amemtaka Hans Poppe kumuomba radhi kutokana na kauli yake kwamba fedha za malipo ya Mbwana Samatta kutoka TP Mazembe, zilipitia kwenye akaunti ya mkewe.

Hans Poppe alisema hayo jana wakati akifafanua kuhusiana na suala lililo Takukuru baada ya Rais wa Simba, Evans Aveva kushikiliwa, kuhojiwa. Baadaye wakahojiwa wajumbe wa kamati ya utendaji.


Rage amezieleza taarifa hizo za Hans Poppe kuwa ni uzushi usiokuwa na maana, hivyo anasisitiza anatoa siku tatu za kuombwa radhi.

Source: salehjembe.blogspot.com

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumamosi ya Agosti 6

$
0
0


SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumamosi ya Agosti 6

Ommy Dimpoz afungukuka kuhusu gharama alizotumia hadi kupiga picha na Rooney

$
0
0
Msanii Omy Dimpoz amefunguka kuhusu vacation yake ya Ibiza na kudai gharama za maisha kule ni juu sana
Akaongezea kile kisiwa alichoenda na kupiga picha na Wayne Rooney ku book meza kwa ajili ya lunch ilikuwa ni Euro 10,000 ambazo ni around milion 25 za Tanzania
Akizungumzia kuhusu watu kusema yule sio Rooney Originala amedai hiyo ni kawaida kwani inawezekana hata mtu akatoka mkoani na kupiga nae picha kisha akawaonyesha wenzake na kumbishia wewe huwezi kupiga picha na Ommy Dimpoz Video:

Hirizi ya Tiffah yaibua jipya!

$
0
0
Mtoto wa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Tiffah Dangote Agosti 3, mwaka huu ametimiza mwaka mmoja lakini jipya lililoibuka ni kuhusiana na dawa ‘hirizi’ aliyovalishwa mkononi na bibi yake mzaa baba, Sanura Kassim ‘Sandra’, Risasi limenyetishiwa ubuyu.

Chanzo kutoka ndani ya familia ya mastaa hao kilichoomba hifadhi ya jina lake kimedai kuwa, awali Tiffah alivishwa dawa hiyo lengo likiwa ni kumkinga na matatizo lakini Zari alipokwenda Sauzi akamvua kwa kuwa yeye si ‘muumini’ wa mambo hayo.

tiffaIkadaiwa kuwa, baada ya Zari kumvua walikaa muda mrefu bila Tiffah kuwa na ‘kadawa’ hako hali iliyomfanya mtoto huyo achelewe kutembea.

“Unajua ile dawa ina mambo mengi kwa watoto, inamsaidia kumkinga na matatizo lakini pia inamfanya atembee haraka, sasa walipoivua ikamfanya achelewe kutembea,” alisema mtoa habari huyo na kuongeza:

“Hali hiyo ilisababisha Zari na Diamond kutofautiana na mwisho wakakubaliana hirizi irejeshwe mkononi mwa Tiffah ndipo mtoto huyo alipoanza kutembea.”

Ikaelezwa kuwa, kuanza kutembea kwa Tiffah kumeibua furaha upya kwenye familia hiyo kwani walishaanza kuwa na hofu hasa ikichukuliwa kuwa, Zari ana mimba nyingine na anatarajiwa kujifungua Desemba, mwaka huu.

Kufuatia madai hayo, mwandishi wetu alimtafuta Diamond na alipopatikana alisema kuwa ni kweli mtoto wao ameanza kutembea lakini si kwa sababu ya dawa hiyo aliyofungwa mkononi.

“Hayo mambo ya kumvalisha na kumvua Tiffah ile dawa ya mkononi ni uamuzi tu lakini huwezi kusema ina uhusiano na kutembea kwake,” alisema Diamond.

Source:GPL

Mwambaji Malaika na Aliyekuwa Mpenzi Wake Eddy Hapatoshi...Wanyanganyana Magari

$
0
0
MREMBO anayesumbua na Wimbo wa Rarua Rarua, Diana Exavery ‘Malaika’ na mpenzi wake aitwaye Eddy wapo kwenye bifu zito baada ya mrembo huyo kudaiwa kutaka apewe gari na mpenzi wake huyo baada ya kumwagana.

Chanzo kinaeleza kuwa, baada ya kumwagana miezi kadhaa iliyopita, Malaika alienda kumfungulia mashtaka Eddy aliyeishi naye kwa zaidi ya miaka mitatu akidai anamdhulumu gari lake.

“Yaani hapatoshi, Eddy kakataa kumpa gari, Malaika anahangaika na hana ushahidi wa kumiliki gari alilokwenda kushtaki polisi, Eddy kamaindi kuona anamletea polisi wakati si mhalifu,” kilisema chanzo.

Mrembo huyo alipotafutwa hakutaka kuzungumzia ishu hiyo lakini Eddy alipopatikana alisema Malaika atakuwa kaishiwa ndiyo maana anamfungulia kesi za ajabu lakini kamwe hatamuweza.

Source:GPL

Mkuu wa Mkoa wa DSM Paul Makonda Apiga Marufuku Maandamano ya UKUTA, Awapa Rungu FFU

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ameliagiza jeshi la polisi mkoa wa Dar es salaam kuhakikisha kwamba sheria zinafuatwa na kusiwepo kitu kinaitwa UKUTA ili wananchi waendelee na kazi zao kama kawaida.

Akizungumza na kikosi cha kutuliza ghasia katika kambi ya Ukonga Jijini Dar es salaam Mkuu wa Mkoa amesema kwa kuwa askari wanafahamu sheria wasisubiri mtu yeyote kuja kuwakumbusha juu ya jambo hilo au maelekezo mengine kwa kuwa Amiri Jeshi ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameshaagiza kinachotakiwa ni utekelezaji.

‘’Msisubiri maelekezo yoyote kutoka juu, asiwepo mtu yeyote atafunga duka kwa sababu ya UKUTA nyie ni matrekta hakuna UKUTA unaweza kusimama mbele yenu, mimi kama Mkuu wa Mkoa ninaamini hatutakuwa na vurugu kwenye Mkoa wetu na hatuwezi kuruhusu vurugu kwa kuwa tunajua madhara ya vurugu’’ Amesema Makonda.

Aidha kwa upande wake Kamanda wa Oparesheni Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Lucas Mkondya amesema jeshi la polisi lipo vizuri na vijana wameandaliwa vizuri na wameandaliwa kuwa tayari siku nyingi na hakuna mtu yeyote atakayethubutu kufanya UKUTA na watakaofanya hivyo watazimwa kabla hawajafanya chochote.

Kamada amewataka wananchi wote Jijini Dar es Salaam kuto jitokeza kwenye oparesheni UKUTA kwa kuwa maandamano hayo siyo halali na watakaojitokeza watapata matatizo yasiyowahusu.

Oparesheni UKUTA ilitangazwa na CHADEMA ikiwa na maana Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania na ikatajwa tarehe Mosi Septemba nchi nzima chama hicho kitafanya mikutano ya hadhara jambo ambalo limepingwa na serikali kuanzia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kufuatia wakuu wa mikoa.

Flora Mvungi adai wakati anaanza mahusiano na H.Baba alikuwa na wasiwasi

$
0
0
Msanii wa filamu na Mama wa watoto wawili, Flora Mvungi amesema yeye ni mmoja kati ya watu ambao walikuwa hawaamini kama kuna mahusiano ya mapenzi ya kweli kati ya msanii na msanii.

Muigizaji huyo ambaye ni mke wa msanii wa muziki na filamu, H. Baba ameiambia Bongo5 kuwa alichukua muda mrefu kuamini kile kilichotokea kwenye maisha yake.

“Kama mimi nilikuwa siamini mahusiano ya msanii na msanii kama wanaweza wakakaa sehemu moja na kutengeneza familia,” alisema Flora Mvungi. “Kwa hiyo kwa mara ya kwanza nilikuwa na wasiwasi sana lakini mpaka kufikia malengo ya kufunga ndoa, nilikuwa nimeshaondoa wasiwasi wangu, nikaamua kuingia kwenye maisha ya ndoa ya kusema kweli ni mazuri sana,”

Muigizaji huyo amesema kwa sasa anayafurahia maisha yake kwa kuwa yupo sehemu sahihi katika maisha yake.

Nuh Mziwanda asema jina la wimbo ‘Jike Shupa’ ni wazo la AliKiba

$
0
0
Mkali wa wimbo ‘Jike Shupa’ Nuh Mziwanda amefunguka kwa kusema kuwa wazo la jina la wimbo huo alikuja nalo AliKiba.

Muimbaji huyo ambaye alikiri wimbo huo kumwimbia aliyekuwa mpenzi wake wa zamani Shilole, amekiambia kipindi cha Ngaz Kwa Ngaz cha EATV kuwa hakuwa na wazo la jina la wimbo huo mpaka AliKiba alivyozungumzia ‘Jike Shupa’ kwenye chorus na wimbo huo.

“AliKiba ndiyo kila kitu, yeye ndiye aliyetoa neno la ‘Jike Shupa’,” alisema Nuh. “Wimbo kanikuta nimeshaurekodi na nimeshafanya chorus yangu, na sikutaka kuiachia nikaenda kumshirikisha AliKiba akaniambia nyimbo imekamilika nitaingiza nini humu, na nyimbo nzuri nikamwambia no, kwa sababu nimekaa kimya muda mrefu nahitaji utofauti kwa sababu sijawai kufanya kolabo, basi akasema okey, tukaenda studio tukamute chorus yangu AliKiba akaingiza yake, ambapo katika kuandika kwake akaimba neno ‘Jike Shupa’, kwa hiyo tilte ya nyimbo Ali anahusika,”

Wimbo huo umefanya vizuri katika vituo mbalimbali vya radio na kumtambulisha rasmi Nuh Mziwanda katika muziki wa bongofleva.

Ajali za Pikipiki Janga..Hospitali ya Moi Kupokea Majeruhi 40 Kila Siku wa Ajali za Boda Boda

$
0
0
Meneja Uhusiano na Ustawi wa Jamii wa Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu Muhimbili (MOI), Jumaa Almasi amesema kwa siku wanapokea wagonjwa 40 wengi wao wakiwa majeruhi wa ajali za bodaboda.

Kauli hiyo imekuja siku moja baada ya Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kuitaka taasisi hiyo kurejesha kambi za upasuaji ili kupunguza idadi ya wanaosubiri upasuaji.

“Awali walikuwa 20 kwa siku, lakini kwa sasa ni 40 na asilimia 80 ya wagonjwa hao wanahitaji upasiaji wa dharura na kiutaratibu, mwenye dharura anahudumiwa mapema ili kuokoa maisha,” amesema huku akisisitiza kuwa taarifa zilizoripotiwa kuhusu msongamano huo na kubana matumizi siyo za kweli.

Lakini wakati Almasi akisema hayo, juzi, Waziri Ummy alifanya ziara ya kushtukiza MOI na kuagiza kambi za upasuaji zilizokuwa zikifanyika mwishoni mwa wiki zirudi mara moja ili kupunguza idadi ya wagonjwa wanaosubiri upasuaji.

Viewing all 104785 articles
Browse latest View live




Latest Images