Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104429 articles
Browse latest View live

Mwanamuziki Diamond Amwandikia Ujumbe Mtoto wake Tiffah Ujumbe Leo Siku ya Kuzaliwa Kwake

0
0
My @princess_tiffah You are certainly the most beautiful gift that i have received in my lifetime....This day is very important for us and to everyone who knows you...Only God Knows how much you mean to me...am so Proud for the first time in my Life to wish my own daughter Happy Birthday... trust me, in my Heart you are the most wonderful daughter in the whole world!....May you always be surrounded with beauty and happiness!.....My Angel, my little Cupcake, my sweet daughter, My Miss World, me and Your Cute Mom loves you so much.....Happy Birthday! @princess_tiffah 🎉🎂🎉

Salam za Wema Sepetu kwa mtoto wa Diamond Platnumz ‘Tiffah’

0
0
Msanii wa filamu Wema Sepetu anaendelea kuuthibitishia umma kwamba hana tena kinyongo na Ex wake wa zamani Diamond Platnumz baada ya Jumamosi hii kumwandikia ujumbe mzuri bintiye Diamond, Tiffah katika siku yake ya kuzaliwa.

Wawili hao hivi karibuni wameonyesha kushirikiana mambo kadhaa katika mitandao ya kijamii licha ya wiki mbili zilizopita kusambaa kwa tetesi ya kurudiana na baadae kukanushwa na Wema Sepetu.

Muigizaji huyo kupitia instagram ameandika ujumbe huu:

Happy Birthday Princess Tee…🎈🎉🎁🎊🎀💝 May Allah bless your precious lil self… You will definitely turn out to be a phenomenal young woman… Princess_tiffah.

Jumamosi hii bintiye Diamond, Tiffah, ametimiza mwaka mmoja ambapo amewashukuru wote waliomtakia heri katika siku hiyo.

“Today a year ago at 4:40 am in the wee hours of the morning I was brought into this world. Thank-you for all my bday wishes & God bless all of you😘. HAPPY BIRTHDAY TO ME,” Ujumbe huu uliandikwa instagram ya binti huyo.

Mgeja Ampinga Rais Magufuli

0
0
ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja, amesema hatua ya Rais John Magufuli kuzuia kufanyika kwa mikutano ya kisiasa nchini, imelenga kuminya demokrasia na serikali kutaka kutokosolewa.

Mgeja, ambaye kwa sasa ni mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Mendeleo (Chadema), alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa hatua hiyo haikubaliki katika nchi ya kidemokrasia duniani kwa kuwa uhai wa vyama vya siasa upo katika mikutano.

Pia amemtaka Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, kushughulikia migogoro ya vyama badala ya kusubiri hadi nchi ikielekea katika mgogoro mkubwa.

Alisema kauli ya Rais Magufuli kwamba shughuli za kisiasa hadi mwaka 2020, inakiuka katiba kwa kuwa mikutano na shughuli za vyama vya siasa vipo kikatiba.

Alieleza kuwa kinachotokea sasa kwa viongozi wa upinzani ni kupigania demokrasia hali ambayo inaweza kuhatarisha amani ya nchi.

“Serikali inakosolewa kupitia mikutano ya vyama vya siasa na serikali isitupangie cha kuzungumza. Kutokana na kauli ya rais tunaonya likitokea lolote katika mikutano ambayo itafanyika nchi nzima, kupitia operesheni ya Umoja wa Kuondoa Udikteta Tanzania (Ukuta), Rais atawajibika iwapo nguvu ya jeshi polisi itatumika,” alisema.

Nay wa Mitego: Siwezi kurudiana na Siwema, Skiner wala Shamsa

0
0
Rapa wa muziki wa kizazi kipya nchini, Nay wa Mitego amesema hana ndoto za kurudiana na mwanamke yeyote kati ya aliwaowahi kuwa nao katika uhusiano wa mapenzi.

Nay alisema iwapo itatokea nafasi kwa yeye kurudiana na mmoja kati yao, atampa nafasi mwanamke aliyezaa naye mtoto wake wa kwanza.

Alisema kwa sasa hana mapenzi na yeyote kati yao, kwa sababu amekuwa akilea watoto wake kwa muda mrefu, hivyo hadhani kuna kitu kinachoweza kumvutia tena kwa wapenzi wake hao.

“Hamna hata mmoja ambaye ninaweza kurudiana naye, labda yule ambaye nilizaa naye mtoto wa kwanza japokuwa yeye alishaolewa, huwa napenda kumwita Mama Vishma maana mtoto wangu wa kwanza anaitwa jina hilo,” anasema Nay wa Mitego.

Nay anasema hana sababu ya kuwasogeza mama wa watoto wake karibu tena, kwani kukaa karibu na watoto hao kummemfanya ajifunze mengi katika malezi.

Anasema japokuwa wengi bado wanashangaa kwa jinsi anavvyomudu maisha bila mama zao, kwake anafaidi mengi ikiwamo kupata baraka katika kazi zake anazoamini zinatokana na watoto.

“Wazazi wa kiume wengi hawapo karibu na watoto hawajengi mazoea mazuri na hata mtoto anakosa upendo kwao, nimejifunza ukiwa nao karibu kuna baraka hata Mungu akiangalia upendo ulionao kwa watoto wako anakupa riziki zaidi,” anasema Nay.

Mkali huyo wa wimbo “Saka Hela” ambaye wimbo wake “Pale Kati” ulifungiwa na Basata baada ya kuonekana hauna maadili, amesema kwa sasa anajipanga ili atakaporudi kwa mara nyingine awe amebadilika zaidi.

Anasema licha ya kudaiwa amekuwa akiimba nyimbo zisizo na maadili, amejipanga atakaporudi kwa mara nyingine.

“Siwezi kufanya muziki wa kuvunja maadili kwa makusudi hakuna mtu ambaye anacheza na kazi yake, huwezi kubadilisha aina ya muziki, lakini nitawashirikisha zaidi wao ili yasitokee haya yaliyotokea,” anasisitiza.

Majibu ya Sober House kuhusu maendeleo ya msanii Ray C…..

0
0
Usiku wa June 16 2016 kuamkia June 17 kuna video ya mwimbaji wa longtime Bongoflevani Rehema Chalamila au Ray C ilisambaa mitandaoni akiwa anachukuliwa na gari la Polisi Kinondoni Dar es salaam ambapo baadae ilikuja kugundulika alipelekwa Hospitali.

Kesho yake mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji Clouds Media Group Ruge Mutahaba aliongea na Amplifaya ya CloudsFM pamoja na millardayo.com na kuthibitisha kwamba mwimbaji huyu amekubali mwenyewe kwa hiari yake na kupelekwa kwenye nyumba ya matibabu ya kuachana na dawa za kulevya huko Bagamoyo Pwani.

Sasa leo Agosti 6, 2016 tumepata taarifa nyingine kwamba staa huyo kahamishwa kutoka Sober House ya Bagamoyo  na kuhamishiwa Sober House ya wanawake tu walioathirika na madawa ya kulevya iliyopo Kigamboni.

Akizungumza na millardayo.com & Ayo TV mmiliki wa kituo hicho Nuru kayaongea haya..
Mimi naitwa Nuru ni mmiliki wa Sober House ya wanawake tu iliyopo Kigambo juzi tulipata ugeni kutoka kwa Msanii Ray C alikuja kuomba matibabu kwasasa yuko anaendelea vizuri na amekubaliana na hali yake’- Nuru

‘Tumempokea vizuri na yeye mwenyewe amefarijika sana kiufupi tu mashabiki wake wamuombee dua sana na mpaka sasa hivi afya yake inaendelea vizuri’- Nuru

Polisi wamsaka Dk Mwaka

0
0
Kamishina msaidizi wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Salum Hamdan amesema bado wanamtafuta mmiliki wa kampuni ya Foreplan Juma Mwaka kama walivyoagizwa na Naibu Waziri wa Afya.

Alisema vijana wake wapo kazini kuhakikisha wanampata ndani ya saa 24 kama walivyoagizwa hapo jana.

Hatua hiyo ni utekelezaji wa agizo la Naibu Waziri wa  Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk  Hamisi Kigwangalla la kumtafuta baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika jengo hilo na kukuta huduma zinaendelea.

Akiwa katika jengo hilo akikagua ndani mara baada ya kupata kibali cha Polisi cha kufanya upekuzi, wateja wa Dk Mwaka walikuwa wanaendelea kuingia kufuata huduma ya matibabu huku wengi wao wakiwa kina mama.

Bongo Flava ni sawa na mtoto anayelelewa na mama peke yake

0
0
Bongo Flava ni muziki wa kisasa ambao umedumu kwa miaka mingi na utaendelea kudumu zaidi na zaidi na hiyo yote ni kutokana na kuongezeka kwa mashabiki ambao idadi yao inazidi kuwa kubwa ukilinganisha na hapo awali kipindi muziki huu unaanza.

Kutokana na waendeshaji wa muziki huu, hapa namaanisha wasanii ambao wengi wao ni vijana, nawafananisha na mtoto ambaye analelewa na mzazi mmoja ambaye ni mama peke yake licha ya kuwa kuna baba ambaye pengine tu hayupo tayari kumsaidia huyu mama ili mtoto apate malezi yaliyo bora yanayoweza kumfanikishia ndoto zake.

Ninapo sema wazazi wa Bongo Flava hapa nazungumzia vyombo vya habari’ ambaye ni mama wa Bongo Flava na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) ambaye ni baba wa Bongo Flava.

Najua utajiuliza kwanini BASATA awe baba na vyombo vya habari viwe mama. Basata ndio wasimamizi wa sanaa nchini na ndio wenye mamlaka ya kutoa zuio la kazi yoyote ya msanii isichezwe katika media endapo hawataridhika na maudhui au maadili ya kazi hiyo na vyombo vya habari ndio wanaosupport kazi za sanaa kwa kuzifikisha kwa hadhira/jamii. Nadhani hapo unaweza kupata picha nini namaanisha katika makala hii.

Tukija kuwaangalia hawa wazazi wawili wa Bongo Flava mlezi mmoja ambaye ni ‘media house’ ndio anaonekana kuwa ana kiu ya kuona mwanaye anafika mbali japo wigo wake ni mdogo tofauti na baba ambaye ni Basata.

Vyombo vya habari nchini ndio vinawapa tumaini kubwa sana wasanii wa hapa nyumbani kwani chochote kinachotokea kwa msanii hasa katika suala zima la maendeleo/matatizo vyombo vya habari huwa vinakuwa na kipaumbele.

Mfano kwa wasanii wetu wanapokuwa katika vinyang’anyilo vya tunzo haijalishi iwe ndani ama nje vyombo vya habari lazima vitatoa support yake kwa hali na mali na tulitazamie katika upande wa pili wa matatizo. Tumeona makubwa mengi sana yakifanywa na vyombo vya habari mfano katika msiba wa Albert Mangwea,Mez B,Geez Mabovu na wengine wengi vyombo vya habari vilionesha jitihada zao na kufikia hatua hata msanii anapofungiwa kazi yake na Basata huwa vyombo vya habari vinajitahidi kutafuta suluhisho kwa kuchukua mawazo pande zote mbili ili kuleta maelewano kati ya BASATA na msanii(baba na mtoto).

Vyombo vya habari huwa haviyafanyi hayo tu kwani imefikia hatua ya kuandaa show mbalimbali na matamasha ambayo yamekuwa msaada mkubwa kwa wasanii wa Bongo Flava kujipatia kipato lakini cha kushangaza Basata(baba) huwa hawajitokezi hata kudhamini hizo show na matamasha yanayokuWa yameandaliwa na media(mama).

Basata(baba) wanaendelea kubaki nyuma hata katika kuibua vipaji vipya vya wasanii wetu ambavyo huwa vimejificha huko mitaani lakini vyombo vya habari huwa vinatumia vipindi na matamasha mfano Hawavumi ila wamo(ITV) Club Raha Leo Show (TBC1) na Fiesta (CLOUDS FM) kwa kuthamini kazi za wasanii media zimekwisha kubali mpango wa serikali kuanza kuwalipa wasanii kwa kucheza kazi zao.

Kwa upande wa Basata(baba) ambao ndio waangalizi wakuu wa sanaa nchini wamekuwa ni watu wa kutoa pongezi tu kwa vijana wetu wanaofanya vizuri na kusikika zaidi kuzungumza makosa ya kazi za wasanii. Wana umuhimu mkubwa sana lakini hawapo karibu na wasanii kama inavyotakaiwa na kwa sababu hiyo inapelekea kuwepo na uhasama wa chini kwa chini ambao ni vigumu kuja kujionesha katika jamii.

Ni ukweli usiopingika kuwa Basata(baba) wangekuwa wana uhusiano mzuri na wasanii hasa katika kuzisimamia kazi zao,kusimamia mikataba yao kama ya matangazo nakadhalika,kuzipitia kazi zao kabla hazijatoka ili migogoro ya kufungia kazi zibaki kuwa stori katika sanaa yetu na pia kuwa kipaumbele hasa kwa wasanii wanaoipeperusha bendera yetu nje ya nchi kwa kuwapa hata medani za dhahabu zitakazowapa motivation/motisha ya kujituma zaidi na kufika mbali kutokana na msaada unaotoka kwa Basata.

Niwape pongezi sana media na wasanii wote ambao wanaendelea kufanya vizuri kila mmoja kwa nafasi yake japo kuwa wote wanahitaji kutegemeana ili kuweza kuisukuma sanaa yetu kimataifa zaidi pia hata Basata(baba) nao wanahitaji pongezi pia na kwani mchango wao upo japo hawauoneshi kwa kiwango kinachostahiri.

NA JOHN SIMWANZA

Makamba: Adui wa nne nchini ni usawa kati ya walionacho na wasionacho

0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira na Muungano), January Makamba amesema tangu nchi ipate uhuru miaka 50 iliyopita, maadui watatu ambao ni maradhi, umaskini na ujinga wapo pale pale lakini kuna adui wa nne aliyeongezeka.

makamba

Ameyasema hayo Ijumaa hii jijini Dar es Salaam alipokuwa akizindua ripoti ya hali ya kipato cha uchumi Afrika Mashariki iliyotolewa na Taasisi ya Society for International and Development (SID).

Alimtaja adui huyo kuwa ni tofauti kubwa ya usawa kati ya walichonacho na wasichonacho.

“Katika safari ya nchi yetu tumepata wazungu wapya ambao ni Waafrika wenzetu. Watu wanaishi maisha mazuri sana, watoto wao wanapata elimu nzuri sana, sasa hivi tofauti imekuwa ni kubwa sana,” alitoa mfano huo Makamba.

“Kama nchi inataka kujenga taifa la watu walio sawa hakuna budi kukabiliana na suala hilo, kwani usawa katika fursa ndiyo nyenzo muhimu ya kukabiliana na usawa katika jamii,” aliongeza.

BY: EMMY MWAIPOPO

Serikali Yatangaza Mwongozo Mpya wa Elimu Kuwa Masomo ya Sayansi ni Lazima Yasomwe Na Wanafunzi Wote

0
0
SERIKALI imetangaza mwongozo mpya kuwa kuanzia sasa masomo ya sayansi ni lazima kusomwa na wanafunzi wote wanaosoma elimu ya sekondari kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne.

Kwa mujibu wa Sera ya Elimu iliyopo, wanafunzi wanaosoma elimu ya sekondari wanaweza kuchagua aina ya masomo watakayo wafikapo kidato cha tatu na kuacha mengine.

Uamuzi huo ulitangazwa jana mjini Tanga  na Waziri wa Elimu, Teknolojia, Sayansi na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako wakati akizungumza na mamia ya walimu wa elimu ya msingi kwenye mafunzo ya muda mfupi kuhusu mtaala mpya wa kufundishia wanafunzi wa darasa la tatu na nne.

Alisema hivi sasa nchi imedhamiria kuingia kwenye uchumi wa kati ambao ni wa viwanda, hivyo suala la sayansi haliwezi kuepukwa kwa sababu ni wakati sasa wa kuwa na wataalamu wengi wa fani za sayansi watakaoweza kutosheleza mahitaji ya sekta ya viwanda nchini.

Alisema kutokana na uhaba wa wataalamu wa sayansi nchini kwenye maeneo mengi, wizara imeamua kuanzia sasa wanafunzi wote wa elimu ya sekondari kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne, watalazimika kusoma masomo ya sayansi na kufanya mtihani wa masomo hayo, na kwamba baada ya matokeo kutoka ndipo watafanya uamuzi ama wa kuendelea nayo au la.

Hatua hii kwa mujibu wa Profesa Ndalichako, itamlazimisha mwanafunzi kusoma kwa bidii ili kuhakikisha anafaulu masomo hayo ingawa hivi sasa wanafunzi walio wengi wanadai masomo hayo ni magumu, ndiyo maana wanachagua kusoma masomo ya sanaa.

Alisema ili kuhakikisha azma ya serikali ya wanafunzi wanapata vitendea kazi vya masomo hayo, Sh bilioni 12 zimetengwa kwenye bajeti ya fedha ya mwaka huu kwa ajili ya kununulia vifaa vya maabara kwenye shule zote za sekondari nchini ili kuwepo na zana za kufundishia kwa ajili ya masomo ya sayansi.

"Mafunzo ya vitendo sasa sio mbadala ni lazima, na yatafanywa kama sehemu ya masomo na wanafunzi wote watalazimika kuyafanya kwa vitendo ili wawe na uelewa wa walichosoma kwa manufaa ya taifa,” alisema Profesa Ndalichako.

Alisema Serikali ya Awamu ya tano imedhamiria kuona kiwango cha elimu kinachotolewa nchini kina hadhi sawa na elimu itolewayo na mataifa mengine ili kupata wataalamu wenye sifa zinazokidhi mahitaji ya soko hata kama sio wote wataajiriwa ila hata wale wasiopata ajira wajiajiri kupitia elimu waliyopata.

Aliwataka walimu waliohudhuria mafunzo hayo kuhakikisha wanatumia uwezo wao na elimu waliyopata kufanya kazi kwa mujibu wa maadili ya taaluma ya ualimu ili kuwajengea msingi mzuri wa elimu wanafunzi wa shule za msingi.

Akizungumzia kauli ya Profesa Ndalichako, Mwenyekiti wa Wamiliki wa Shule Binafsi Tanzania (TAMANGOSCO), Mahmoud Mringo alisema ni uamuzi mzuri ila umekuja kwa kuchelewa kwa sababu mahitaji ya wataalamu wa sayansi nchini ni makubwa kuliko idadi ya wanafunzi wanaosoma masomo hayo.

Alisema pamoja na uamuzi huo mzuri uliochukuliwa na serikali, lakini bado kutakuwa na changamoto ya uhaba wa walimu wa masomo hayo, maabara na maktaba na kwamba hali hiyo inaweza kusababisha mahitaji ya walimu hao kutoka nje yakaongezeka.

Katibu wa Tamangosco, Benjamin Mkonya alisema ni hatua nzuri ingawa utekelezaji wake utakuwa na changamoto nyingi kwa sababu hali halisi ya mazingira ilivyo nchini.

Alisema ikiwa serikali inadhamiria kutekeleza azma hiyo ni vyema kipengele cha vigezo vya shule kuwepo ambavyo vimeainishwa ndani ya sheria ya elimu nchini, vikaangaliwa ambavyo ni uwepo wa maabara ya kutosha, maktaba yenye vifaa na walimu wa kutosha.

Alisema iwapo vigezo hivyo vikiangaliwa shule ambazo hazijakidhi vigezo hivyo zikafutwa na vifaa vilivyopo kwenye maabara na maktaba hizo zikaongezwa kwenye shule zenye vifaa hivyo ili kusaidia utekelezaji wa azma hiyo ya kufundisha masomo ya sayansi kwa wanafunzi wote kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne.

Walimu washiriki wameishukuru serikali kwa mafunzo hayo ambayo walisema ni mazuri na yameongeza kiwango chao cha uelewa na kuwaongezea mbinu za ufundishaji sambamba na kukuza morali ya kazi zao.

Pamoja na kushukuru, wameomba wizara hiyo iangalie jinsi ya kuweka posho kwa baadhi ya maeneo ya kazi, hususan kwenye vituo vya kazi vilivyopo pembezoni na kwenye mazingira magumu ili kuwajengea walimu motisha wa kufundisha maeneo hayo.

Walimu waliohudhuria mafunzo hayo ni 480 wanaotoka halmashauri za Bumbuli, Mji wa Handeni na Halmashauri ya Wilaya ya Handeni.

Takukuru yafafanua soo la Aveva

0
0
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru), imefunguka rasmi sababu za kumshikilia na kumweka ndani Rais wa Simba, Evans Aveva.

Aveva alishikiliwa tangu juzi Jumatano na kulala ndani kwenye Kituo cha Polisi cha Urafiki jijini Dar kabla ya kutolewa kwa dhamana Alhamisi huku chanzo cha yote kikiwa ni baada ya Takukuru kubaini alifanya uchepushaji wa fedha za mauzo ya fowadi, Emmanuel Okwi walizolipwa Simba na Etoile du Sahel dola laki tatu ambazo zilitolewa kwenye akaunti ya klabu na kuhamishiwa kwenye akaunti yake kabla ya kuanza kusambazwa huku nyingine zikihamishiwa katika akaunti moja ya nchini Hong Kong.

Msemaji wa Takukuru, Tunu Mlei ameliambia Championi Jumamosi kuwa kutokana na mazingira hayo, walihisi uwepo wa rushwa hivyo kuanza kuchunguza.

Tunu amefunguka huku akisisitiza kuwa iwapo atabainika na makosa katika sheria ya uchepushwaji, anaweza kufunguliwa mashtaka mahakamani.

“Kwa sasa bado tunaendelea na uchunguzi na kwa mujibu wa sheria zetu haziniruhusu kusema nini kinaendelea kwenye uchunguzi,” alisema.

“Muda wa kuwachunguza itategemea. Kuna process (mchakato) zake. Kwa sasa tupo katika sheria No.11 kifungu cha 29 ya mwaka 2007 inayohusu uchepushwaji wa fedha, tukimaliza uchunguzi kazi yetu ni kupeleka faili kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka nchini, ndiye mwenye kuamua kesi iende mahakamani ama la.”

Akafunguka zaidi kuwa kwa sasa wanafanya kazi na Serikali ya Hong Kong.
“Kama unavyojua uchunguzi unahusishwa na nje ya nchi kwa kuwa kuna hela zimekwenda Hong Kong, hivyo tunashirikiana na serikali ya huko kujua zilikwenda kufanya kitu gani,” aliongeza.
Tunu amesema iwapo uchunguzi utabaini kuna mazingira ya rushwa, sheria itachukua mkondo wake lakini sheria ya uchepushaji wa hela pia ina adhabu yake.

“Kama nilivyosema tupo kwenye sheria ya uchepushaji, ambayo pia ina adhabu yake lakini siwezi kuisema maana vifungu vinaweza kuongezeka kulingana na uchunguzi utakavyofungua mambo mengine,” alisema Tunu.

Licha ya mwenyekiti wa zamani wa Simba, Ismail Aden Rage kusisitiza Etoile du Sahel kuilipa Simba fedha hizo muda mrefu, viongozi chini ya Aveva wamekuwa wakiruka kimanga wakisema bado hela hiyo haijaingia kwenye akaunti zao.

Simba ilimuuza Okwi mwaka 2013 wakati wa utawala wa Mwenyekiti Ismail Aden Rage, hata hivyo hakukaa sana kabla ya kwenda SC Villa ya Uganda, kisha Yanga kabla ya kurejea Simba ambako alikaa msimu mmoja kabla ya kuuzwa kwa dola 110,000 kwenda SonderjyskE ya nchini Denmark, mwaka juzi.

Kilichoandikwa na mashabiki wa Ex wa Zari, Ivan baada ya kum-wish Tiffah

0
0
Leo ni birthday ya mtoto wa Diamond, Tiffah ambapo ndugu, jamaa pamoja na marafiki katika mitandao ya kijamii wanaendelea kum-wish binti huyo.
Zai

Mmoja kati ya watu ambao wamem-wish binti huyo ni Ex wa Zari, Ivan ambapo amemtakia binti huyo afya njema katika maisha yake. Lakini ujumbe huo umezua upya vuguvugu kwa mashabiki ambao bado wanaamini Tiffah ni mtoto wa Ivan licha ya Diamond kukanusha uvumi huo mara kadhaa.

“Big shoutout to this innocent beautiful soul. May you live to blow more candles to come Princess_tiffah,” aliandika Ivan katika ukurasa wake wa instagram huku akiwa ameweka picha ya binti huyo.

Baada ya kuandika ujumbe huo, mashabiki katika mitandao ya kijamii wamekuwa na maoni tofauti. Haya ni baadhi ya maoni ya mashabiki hao.

Mtoto karudi kwa baba jaman, Damu nzito nyie @ivandon ongera Ivan kwakupigania mpaka mwanao kaja atimaye mungu mkubwa jaman khaa.

Sweet_verosa
Hahaha yani nimecheka mpaka nimelia heti Mungu mkubwa tifa karudi kwa baba yake.

Didiz_buu
Nimempenda Bure uyu mzungu wa kiganda sijui kisauz…. Big up bro Ivan…. U gat a unique heart… Happy birthday baby teepher

Angellyamuya
Congratulation big Boss I salute you.

Aniveraaaaa
Ivan Don Kai u re a man,dis jst gt me crying a u re a nice man.God will perfect everything dat concerns u and gve h a better companion amen.

Nelyhassan
Sure she is beautiful innocent soul happy birthday girl @princess_tiffah

Cassandra_jolly
Happy birthday to her…..u r a gentleman Ivan

Johnson_willo
Now i realize how gentle ur.@ivandon conglatulation men.And happybornday to the one and only.@princess_tiffah.

Binti_wa_bagoka
My love @christinamboy aiseeee njoo umuone mume wa zari alivyo zungu ametishaaaa

Katibu wa Chadema Kanda ya Ziwa Akamatwa Akituhumiwa Kufanya Uchochezi Kwa Kutumia Mitandao ya Kijamii

0
0
Wakati Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu akiwa nje kwa dhamana baada ya kupandishwa kizimbani kwa makosa matatu yakiwamo ya uchochezi, Jeshi la polisi mkoani Geita limevamia Hoteli ya KG iliyopo mjini Geita aliyokuwa amefikia Katibu wa Chadema Kanda ya Ziwa, Meshack Miku na Mwenyekiti wa Bavicha Mkoa wa Geita, Neema Chazaile na kuwashikilia kwa tuhuma za uchochezi wa kutumia mitandao ya kijamii.

Taarifa zilizopatikana kutoka kwa uongozi wa Chadema Mkoa wa Geita na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa, Mponjoli Mwabulambo zimedai kuwa katibu huyo alikamatwa jana saa 12 asubuhi.

Katibu wa Chadema Mkoa wa Geita, Sudy Mtanyagala alidai kwamba askari wa polisi zaidi ya 10 wakiongozwa na Kamanda wa Upelelezi Mkoa (RCO) waliizunguka hoteli aliyokuwa amelala katibu huyo wakidai wanatafuta majambazi yenye silaha.

 Mtanyagala alidai kuwa polisi hao waliingia chumba baada ya chumba na walipofika katika chumba cha mwisho ambacho ndicho alichokuwa amelala katibu huyo walimkamata na kuchukua simu yake.

Alisema baada ya kumkamata walisoma nyaraka za chama alizokuwa nazo kisha kumtaka yeye na mwenyekiti wa Bavicha kuongozana na polisi hadi kituoni kwa uchunguzi zaidi.

 Alisema katibu huyo wa kanda pamoja na mwenyekiti wa Bavicha mkoa walikuwa wakijiandaa kwa kwenda katika ziara Wilaya ya Nyang’wale ambako wangefanya mikutano ya ndani na viongozi wa chama hicho.

Katibu wa Chadema Wilaya ya Geita, Hellena Thobias alisema walipata taarifa za kukamatwa kwa viongozi hao asubuhi na kufika polisi.

Alisema baada ya kufika polisi, maelezo yalibadilika na kuelezwa katibu wao anatuhumiwa kwa uchochezi kwa kutumia mitandao ya kijamii.

Alisema wamejitahidi kuomba dhamana lakini imeshindikana baada ya kuelezwa kuwa watuhumiwa hao watakuwa chini ya uangalizi wa polisi kwa uchunguzi zaidi.

“Polisi wametunyima dhamana hadi saa 10 jioni tuko polisi tumeomba dhamana wamekataa sijui ni sheria gani inayomzuia mtu kupata dhamana lakini pia sijui ni sheria gani ya polisi kumnyang’anya mtu simu yake bila ridhaa na kuichunguza. Hatutanyamaza juu ya uonevu huu,” alisema.

Alisema Serikali imekataza mikutano  ya hadhara na kueleza kusikitishwa kwake na hatua ya jeshi la polisi kufuatilia hadi mikutano ya ndani ya chama hicho ambayo ni haki yao kikatiba.

Akizungumza kwa simu na mwandishi, Kamanda Mwabulambo alikiri jeshi lake kuwashikilia katibu huyo wa Chadema wa kanda na mwenyekiti wa Bavicha mkoa lakini akasema yupo nje ya ofisi hivyo hawezi kulizungumzia jambo hilo kwa undani.

Wazazi Wamuua Mtoto Wao Kwa Kipigo

0
0
MWANAFUNZI aliyekuwa akisoma Darasa la Saba katika Shule ya Msingi Zimba, Bonde la Ziwa Rukwa wilayani Sumbawanga, Susana Kauzeni (15) ameuawa baada ya kupigwa na wazazi wake wakimtuhumu kuwa ni mtoro sugu wa shule.

Ofisa Elimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga (Shule za Msingi), Peter Fusi amesema kuwa mwanafunzi huyo alizikwa kijijini humo Julai 23, mwaka huu.

“Baba na mama yake walichangia kumpiga binti yao huyo wakimtuhumu kuwa ni mtoro sugu wa shule pia nyumbani amekuwa haonekani. Baba yake mzazi amekimbia baada ya kufanya uhalifu huo huku mama yake akiwa ameshikiliwa na Jeshi la Polisi,” alieleza Fusi.

Fusi alieleza kuwa kuanzia Agosti 3 na 4, mwaka huu alitembelea baadhi ya shule za msingi zilizopo kwenye Bonde la Ziwa Rukwa ikiwemo Shule ya Msingi Zimba kufuatilia kazi ya utengenezaji wa madawati mapya kwa ajili ya shule za msingi pia kufuatilia takwimu sahihi za wanafunzi ili kubaini wanafunzi hewa.

“Nilipofika kwenye Shule ya msingi Zimba, Mratibu Elimu Kata, Daudi Moga na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Fidelis Mwangurumba walithibitisha kutokea kwa mauaji hayo ya mwanafunzi huyo,” alisema.

Kwa mujibu wa Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Mwangurumba, mwanafunzi huyo alikuwa ni miongoni mwa wanafunzi watoro sugu shuleni hapo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, George Kyando amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo.

Diamond Analipa Fadhila kwa Chid Benz

0
0
Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Diamond Platnumz amesema anafanya hivyo kwa Chid Benz kutokana na kitendo alichomuonyesha kabla hajawa maarufu, kukubali kufanya naye collabo ya wimbo wa ‘nalia na mengi’, bila kumzungusha na kumtoza hela kama ilivyo kwa wasanii wengine.

“Mimi nimefanya collabo na Chid, kipindi hicho nilimwambia, hakunitoza hata sh. kumi wala hakunizungusha hata kidogo, ndio maana linapokuja suala la Chidi nakuwa wa kwanza, wakati mimi namfuata Chidi, Chidi hasa nikajua atanikatalia kwanza mimi mbana pua, lakini hakunizungusha na wala hakuniomba hata mia”, alisema Diamond Platnumz.

Tujikumbushe hivi karibuni msanii Chid Benzi alipata matatizo ya matumizi ya madawa ya kulevya, na Diamond alichukua jukumu la kumpeleka hospitali na kumbadilisha damu, kabla hajapelekwa rehab kupata tiba ya urahibu.

Lady Jay Dee na Mwarabu Wazua Utata

0
0
MKONGWE wa Bongo Fleva, Judith Wambura ‘Jide’ na Mwarabu mmoja ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja, wamezua utata wa aina yake kufuatia msanii huyo ‘kumposti’ mara kwa mara kwenye mtandao wake wa Instagram.

Risasi Jumamosi lilianza kumfuatilia Jide baada ya kutonywa na chanzo kuwa msanii huyo amekuwa akimposti Mwarabu huyo na kwamba kuna kila dalili ni mtu wake aliyerithi mikoba ya aliyekuwa mumewe, Gardner Habash.

JIDE“Nyie kama vipi fuatilieni kwa makini kwenye Instagram yake, mtagundua tu ukweli, kuna kitu maana hata akimposti huyo jamaa huwa anaweka maneno yenye utata, hataki kufunguka moja kwa moja kama ni mpenzi wake au vipi,” kilisema chanzo hicho.

Baada ya chanzo hicho kulitonya Risasi Jumamosi, mwanahabari wetu aliingia kwenye ukurasa wa Jide na kuziona picha tofauti zikimuonesha akiwa amekaa na Mwarabu huyo huku akisindikiza na ujumbe ambao hautoi majibu ya moja kwa moja kama ni mtu wake au la.

JideAlipotafutwa mrembo huyo kupitia simu yake ya mkononi, iliita bila kupokelewa lakini mmoja wa mameneja wake alisema mwanaume huyo ni rafiki wa karibu wa Jide na kama kutakuwa na lolote, atafafanua baadaye.

“Ni rafiki yake tu na nisingependa kumtaja jina lake maana sidhani kama ni jambo zuri, nyie msiwe na wasiwasi, kila kitu kitakuwa wazi tu muda muafaka utakapowadia, najua watu wengi mnataka kumjua shemeji mpya, wawe wavumilivu tu watamjua,” alisema meneja huyo huku akiomba hifadhi ya jina.

Oscar Pistorius Ajeruhiwa Gerezani

0
0
Maafisa wa magereza nchini Afrika Kusini, wanasema kuwa mwanariadha mlemavu wa nchi hiyo Oscar Pistorius, ametibiwa hospitalini baada ya kupata majeraha akiwa korokoroni.

Msemaji wa idara ya magereza nchini humo, amesema kuwa Pistorius alianguka kutoka juu ya kitanda

Msemaji wa idara ya magereza nchini humo, amesema kuwa Pistorius alianguka kutoka juu ya kitanda chake

Msemaji wa idara ya magereza nchini humo, amesema kuwa Pistorius alianguka kutoka juu ya kitanda chake, lakini kwa sasa amerejeshwa gerezani anakohudumia kifungo cha miaka sita kwa kosa la kumuuwa mpenziwe wa kike Reeva Steenkamp.

Kuna ripoti inayosema kuwa alikuwa amejeruhiwa kwenye kifundo cha mkono.
Kumeibuku uvumi katika mitandao ya kijamii nchini Afrika Kusini kuwa Pistorius alikuwa amejaribu kujitia kitanzi lakini hilo limekanushwa na familia ya mwanariadha huyo.


Mwezi uliopita, waendesha mashtaka nchini Afrika Kusini, walisema kuwa watakata rufaa kupinga hukumu ya miaka sita ya Pistorius, wakisema kuwa ni hukumu ndogo mno.

Mwanariadha huyo alimuuwa mpenziwe wa kike , kwa kumpiga risasi nyumbani kwake wakati wa siku kuu ya wapendanao mnamo mwaka wa 2013, akisema kuwa alidhania ni mwizi.

Askofu Gwajima Uso Kwa Uso na Waziri Mkuu Majaliwa..

0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Askofu Josephat Gwajima wa Kanisa la Uzima na Ufufuo katika hafla ya harusi ya Naibu Waziri wa Sheria na Katiba Amon Mpanju na mkewe Analises iliyofanyiak kwenye ukumbi wa jeshi wa Lugalo jijini Dar es salaam Agosti 6, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Sheria na Katiba, Amon Mpanju akilishwa keki na mkewe , Analises katika tafrija ya harusi yao iliyofanyika kwenye ukumbi wa Jeshi Lugalo jijini Dar es salaam Agosti 6, 2016. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary walihudhuria katika tafrija hiyo (Picha na Ofisiya Waziri Mkuu).

Mwanaume Anaepetipeti VS Mwanaume Mtundu Kitandani

0
0
Leo nina swali dogo tu kwa ladies. Assume una wanaume wawili mmoja ni mzee wa kupetipeti, yaani utabembelezwa, maneno matamu yakukufanya ujihisi wewe mzuri kuliko malkia cleopatra, utapewa kila ukitakacho mtoto wa kike, utasikilizwa, utaheshimiwa, utaachiwa uhuru nk. Lakini mkiingia uwanjana jamaa anaishia kukupakaza jasho tu, in short jamaaa ni lazy sana kwa bed. Lakini Kwa upande mwingine una jemba nyingine ambayo kupetipeti kumeipitia kushoto kubembeleza hajui, bahiri, maneno matamu hana. Ila ukija kwa bed anapiga mzigo balaaaa, unahisi utamu mpaka mboni ya jicho inavibrate.

Sasa inafikia wakati inabidi ubaki na mmoja tu. Kwa wewe mdada ungempa kibuti nani na kumpa shavu nani? Kati ya jamaaa hizi mbili

Utafiti: Kati ya Wanaume Kumi, Saba Wana Michepuko

0
0
Jamani. Kama utafiti huu wa gazeti la Mwananchi ni kweli basi tatizo la Michepuko limegeuka janga la kitaifa. Ni nini kinasababisha hali hii? Mlioko kwenye ndoa, kuna nini huko jamani mpaka mchepuke kiasi hiki?

Mwimbaji Rayvanny Afunguka Haya Baada ya Muonekano Wake Mpya Kuwakwaza Mashabiki Wake

0
0
"Nimeona comments nyingi kuhusu rasta nilizoweka lakini naomba watu waelewe kwamba haikuwa style yangu na wala sina mpango wa kufuga rasta nitabaki na style yangu moja tu maana nimeona jinsi nilivyowakwaza mashabiki wangu."- Raymond

Nini maoni yako?
Viewing all 104429 articles
Browse latest View live




Latest Images