Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live

Wolper: Ninakuja na Mradi Mkubwa wa Fashion

0
0
Jacqueline Wolper amesema anakuja na mradi mkubwa wa fashion huku akidai kuwa ndio kitu anachokipenda zaidi katika maisha yake.

Amedai kuwa kwa sasa yupo kwenye ujenzi mkubwa wa ofisi yake maeneo ya Kinondoni na kwamba akimaliza ataeleza nini hasa anachofungua.

“Sasa hivi nipo kwenye hatua za mwisho, nipo kwenye tiles ndio namalizia kuweka, nikimaliza pale ndio nitawaambia watanzania, mashabiki wangu na wanaopenda kupendeza ni kitu gani nafanya,” ameiambia Bongo5.

Amedai kuwa hiyo ni sababu kubwa imemfanya apumzike kwa muda kwenye filamu kwasababu suala la usambazaji limegeuka kuwa na changamoto.

Kufanya Mapenzi na Binamu ni Halali Kenya..Mahakama Yapitisha

0
0
Mahakama ya juu nchini Kenya imehalalisha ngono baina ya mabinamu kwa sababu inakubalika katika baadhi ya jamii nchini humo.

Mahakama hiyo imemuachilia huru mtu mmoja aliyekuwa amefungwa kwa kosa la kushiriki ngono na binamu yake mwaka wa 2014 kwa sababu sio makosa nchini Kenya.

Jaji wa mahakama ya juu James Makau, alisema katika uamuzi kuwa kujamiana kwa maharimu sio haramu nchini Kenya.

''Ibara maalum inachoshughulikia ngono ya maharimu hajata binamu kuwa mmoja wa wale ambao kujamiana nao ni haramu maksudi, kwa sababu baadhi ya jamii nchini Kenya zinaruhusu sio tu ngono bali hata ndo baina yao''

Jaji wa mahakama ya juu James Makau, alisema katika uamuzi kuwa kujamiana kwa maharimu sio haramu nchini Kenya.

''jamii ya wahindi, waislamu na baadhi ya makabila humuhumu Kenya hukubali ndoa baina ya mabinamu'' alisema jaji Makau.

Bwana huyo ambaye anatambulika kama WOO alikamatwa mwaka wa 2014 kwa kushiriki ngono na mpenzi wake wa kike ambaye pia ni binamu yake na akahukumiwa kifungo cha miaka 10 gerezani.

''Kwa ufupi hakuna ushahidi wowote uliotolewa kuthibitisha kuwa ngono baina ya wawili hao ni kinyume cha sheria na kwa sababu hiyo ninaamuru mtu huyo aachiwe huru mara moja'' hukumu ya jaji Makau.

Kiba Adaiwa Kutapeli Wakenya, Shahidi Wake Akamatwa!

0
0
Kashfa! Staa wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘Alikiba’ anadaiwa kuwatapeli Wakenya baada ya kupewa Sh. Milioni 33 kwa ajili ya kushirikishwa kwenye wimbo kisha kuingia mitini, hali iliyosababisha shahidi wake, Rajabu Salum ‘Mchafu’ kutaitiwa, Risasi Mchanganyiko lina full data.
Kwa mujibu wa Mchafu ambaye ni meneja wa wasanii wa Bongo Fleva, Nuh Mziwanda na Billnas, alipigiwa simu na Wakenya hao kumuomba awaunganishe na Ali Kiba.

“Mmoja kati ya Wakenya hao ni mwanamuziki ambaye anaitwa Brown Mauzo, lengo lao kubwa lilikuwa ni Brown kufanya kolabo na Ali, hivyo nikawasiliana naye akakubali kwa sharti la kulipwa dola elfu 15 (zaidi ya milioni 30 za Kibongo).

“Walikuja Bongo, tukakutana nao Mlimani City, nikiwa shahidi wa Ali na wao walikuwa na wanasheria wawili. Wakaingia benki ili kutoa kiasi cha Sh. milioni 10 lakini wakaniomba wasitoe kwanza na kwamba nikabadilishe mkataba kwa kiasi hicho cha pesa watakachoanza nacho maana awali makubaliano ilikuwa ni kiasi hicho cha pesa (shilingi mil. 32) kwa ajili ya video, malazi na makazi.”

“Upande wa video, Ali alitaka dairekta asiwe Mbongo, hivyo tukampata Justin Campos wa Sauz. Kwa upande wa audio, Brown alimhitaji Prodyuza Manecky lakini Ali napo alikataa na kumtaka prodyuza wake ambaye ni Aby Daddy wa Chaiderz Records, hivyo akataka iongezwe tena shilingi milioni moja kumlipa prodyuza huyo, jamaa wakamaindi na kuondoka bila dili kufanyika.

 “Ali akaniambia nikaongee nao kwani hela ya prodyuza lazima ilipwe. Basi nikawafuata hotelini kuongea nao vizuri, tukaelewana wakapanga tuonane usiku, tukasaini na kumkabidhi Ali milioni 20 huku kesho yake wakiahidi kumalizia milioni 13 ili jumla iwe 33.

“Kesho yake, tukakutana studio kwa Aby, wakarekodi na kurudi nchini kwao kusubiri ikamilike. Baada ya siku chache jamaa wakawa wanahitaji wimbo wao.

“Wakatumiwa lakini hawakuridhika wakidai ulitengenezwa chini ya kiwango na haukuwa na ubora. Wakaja Bongo na kushauri ukaboreshwe kwa Man Water (Combination Sound), tukachukua mafaili ya wimbo huo kutoka kwa Aby hadi kwa Man Water.

Kufika huko, Man Walter akashauri irekodiwe upya, naye akahitaji hela nyingine. Ikabidi niwasiliane na bosi wa Brown, Kenya akatuma kiasi kingine cha shilingi milioni moja na nusu, Brown akaingiza tena sauti ikabaki kwa Ali.

“Kila akitafutwa Ali alikuwa akikwepa, akipigiwa simu ikawa hapokei. Siku alipopatikana akadai hawezi kuingiza mara ya pili.

Baadaye katika kupeleleza, tukaja kugundua kumbe Aby alipewa shilingi laki moja na nusu badala ya milioni moja. Aliposikia kwamba Ali amepewa pesa nyingi na yeye amepewa kiduchu, akapoteza morali ya kazi. Tulibishana sana lakini mwishowe, akakubali akaingiza.

“Baada ya kumaliza audio kibishi, jamaa wakawa wanahitaji namba ya pasipoti ya Ali na meneja wake ili wafanye michakato ya kusafirishwa kwenda kutengeneza hiyo video.

“Ikawa kila tukimfuatilia Ali tunaambiwa mara yupo Sauz na Barakah The Prince, mara amerudi yupo kwenye shoo za Bongo, tukimpigia simu anatupiga chenga, hapokei,” alisema Mchafu.
Imeelezwa kuwa, baadaye mabosi hao wa Kenya walipoona mambo hayaeleweki, walimkamata Mchafu kwa muda kama mmoja wa waliosaini mkataba na kwamba baada ya kuongea na Ali,
aliwataka wamlipe fedha aliyofanya wimbo kwa mara ya pili na Man Water, baadaye wakamuachia.
Hata hivyo, Mchafu baada ya kusikika kwenye moja ya redio Bongo akilalamika kwa aliyotendewa, Ali alimpigia simu na kumlaumu sana, baadaye akamwambia amekubali kutengeneza video hiyo ambapo Agosti 10, mwaka huu (leo), wanatarajiwa kusafiri kwenda ‘kushoot’ Sauz.
Baada ya madai hayo, Risasi Mchanganyiko lilimtafuta Prodyuza Aby kutaka kujua kama kuna ukweli ambapo alifunguka;

“Kwa sasa sitaki kuongelea kabisa habari hizo ila ninachoweza kusema ni kwamba Wakenya hao walikuja kuchukua mafaili ya wimbo na kupeleka kwa Man Water.”

Baada ya kumsaka Kiba bila mafanikio, Risasi Mchanganyiko lilimtafuta meneja wa msanii huyo, Seven Mosha ambaye alisema habari hizo hazina ukweli wowote.

“Ni uzushi tu huo, hakuna kitu kama hicho,” alisema Seven kwa kifupi na kuondoka hewani.

Source:GPL

Harmonize Akanusha Kuchunwa Pesa na Jack Wolper

0
0
Jack Wolper na Harmonize
Mwanamuziki wa Bongo Flava anayesimamiwa na Wasafi, Harmonize, amekanusha kuchunwa pesa na mpenzi wake Jackline Wolper kutokana na mwanamke huyo kuonekana kuwa na maisha ya kifahari.

Harmonize amekanusha hayo kwa kusema “Nyumbani kwa Wolper kuna kaunta ambayo anaweza kunywa vinywaji atakavyo, pia sioni sababu ya mimi kupendeza na mwanamke wangu asipendeleze ni lazima nitahakikisha anapendeza kwa kuwa ninampenda”.

Harmonize pia alizidi kuweka wazi kuwa mapenzi yake na Wolper hajaathiri kitu chochote kwenye kusaidia familia ya kwao kwa kuwa hata kama asingekuwa na Wolper ni lazima angekuwa kwenye mahusiano.

“Siyo kwamba ninatumia pesa nyingi kumridhisha mpenzi wangu na kusahau familia yangu, Mama yangu na ndugu zangu wanapata pesa za matumizi kama kawaida kwa kuwa ninafanya kazi”.alisema Hrmonize.

'Mauno Yangu Yamechangia Kunikuza Kimuziki'- Snura

0
0
Msanii Snura ambaye mara nyingi amekuwa akikumbwa na rungu la BASATA kutokana na video zake ambazo zinakuwa na utata, amesema mauno ambayo BASATA 'wanamind' ndio yamemfikisha hapo alipo.

Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Snura amesema mauno yake ndiyo yamechangia kwa kiasi kikubwa kuinua muziki wake, kutokana na jinsi anavyoyamwaga akiwa jukwaani, na kuwavutia mashabiki wake.

"Nimeimba sana laini kiuno changu kimenisaidia sana kunitambulisha, ukisikia kuna show ya Snura jua mauno yanamwagwa kweli, na sijaanza leo nilianzia kwenye ngoma za asili", alisema Snura.
Snura aliendelea kusema kuwa ingawa mauno hayo humpa wakati mgumu akiwa kwenye kazi zake kutokana na uchu wa baadhi ya wanaume wanaomsumbua, lakini amekuwa akijitahidi sana kujilinda ili asiharibu kazi yake.

"Usumbufu kiukweli upo,wengine wananipenda kweli wengine wananitamani, kikubwa nazingatia sana kazi yangu, nashinda sana vishawishi kwa sababu vile ninavyokatika wengine wanadhani nafanya promotion ya biashara", alisema Snura.

Picha Inayowaonyesha AliKiba na Diamond Wakishikana Mikono Yawatoa Povu Mashabiki

0
0
Katika mitandao ya kijamii Jumatato hii kumezuka mjadala mkubwa baada ya mashabiki wa Diamond Platnumz na AliKiba kuona picha yakutengenezwa inayowaonyesha wawili hao wakipeana mkono.

Wachache kati ya mashabiki hao wanaamini picha hiyo ni yakutengenezwa huku wengi wao wanaamini wawili hao kweli wamepatana.

Pia miongoni mwa mashabiki hao waamini endapo wawili hao watapana basi na muziki wao utashuka kutokana na kupoteza ushindani.

Haya ni baadhi ya maoni ya mashabiki hao kutoka katika mitandao ya kijamii.

Francis Michael
Tukubali kuwa hakuna jambo lisilokuwa na mwisho kwa upendo wao wenyewe wameona tukiendelea hivi mpaka lini tutamaliza tofauti zetu kwa kuwa wasanii hawa wote wanapeperusha bendela yetu ya TZ, Nimefurahi sana kusikia hivi tofauti zao zimekwisha nawaomba kama kweli umekwisha wafanye kolabo yao wasanii hawa wawili watuchezeshe sasa turuke.

Glory Shayo
Haitawezekana kamwe coz Diamond ana wivu na nyimbo za King Kibaa hiyo itabaki tu story.

Joseph Salvatory
Haitatokea kumaliza tofauti zao hadi Diamond arudishe ile kolabo aliyo mshilikisha Kiba na Kiba kumfunika Diamond, kwa roho mbaya ya Diamond akaifuta.

Veronica Godluck
Elewa kwamba kuna maisha mengine baada ya muziki, na uwezi jua mungu amepanga nini juu yako, so haina haja ya mabifu chamsingi kila mtu awangalie mashabiki wake wanataka nini. Kumake money ndio kila kitu.

Albert Kariuki Tz
Binafsi nita jihisi vibaya kwa kuwa ule ushindani hautakuwepo na muziki yao ni kama vile ita chuja.

Juma Masifia
Umesema ukweli wote coz kama hawa mastari wangekuwa wana bifu lazima serikali au baraza lao lingeingilia kati na kupelekana mahakamani siyo daily tunasikia mambo tofauti mengi kwenye media na midomo ya watu kumbe hakuna chochote isipokuwa ushabiki wa watu na media

Haruna Hamisi
Kama wakiungana muziki nao utakuwa umekwisha kwa Diamond & Ally Kiba kwakuwa sasa hivi upinzani wa wasanii hao tu ni gumzo unafanya kuwapa mafanikio makubwa sana kiukweli sasa hivi muziki wa bongo fleva, kwenye soko wameliteka Diamond & Ali Kiba, yaani tunawaangalia wao tu Kiba katoa nini na Mond katoa nn? Sasa wakiungana muziki kwao hakuna tena, kwa hiyo bifu linachangia muziki kwenda mbal

Sakata la Supu ya Pweza Latolewa Ufafanuzi..Utafiti Kama Kweli Inaongeza Nguvu za Kiume Bado Waendelea

0
0
Akizungumza na East Africa Radio katika kipindi cha East Africa Break Fast Prof. Kaale amesema taarifa za utafiti wa wanafunzi wa Muhimbili bado haujakamilika kwani umeishia katika hatua ya wanyama panya na majaribio kabla hayajaenda kwa binadamu lazima yafanyike kwa wanyama wenye mfumo unaofanana kwa kiasi fulani na binadamu.

"Mwanafunzi alinunua pweza akamchemsha mwenyewe, akawapa panya mchuzi akawafuatilia kwa muda wa siku 29 na aliwatenga panya katika makundi mawili kundi moja likapewa maji na lingine likapewa mchuzi wa pweza na mfumo wa ‘genetics’ unafanana sana na binadamu kwa zaidi ya asilimia 95 lakini hatuwezi kusema kwamba umethibitishwa kwa binadamu bila hatua zote kukamilika" Amesema Prof. Kaale

Prof. ameendelea kufafanua kwamba waliopewa supu walionekana kufanya tendo la kujamiiana mara nyingi kuliko wale waliopewa maji hivyo kisayansi huwezi kusema moja kwa moja kwamba tayari na kwa binadamu supu hiyo inaweza kufanya kazi.

Aidha Prof. Kaale ambaye ndiye alisimamia utafiti huo wa awali, amesema hatua zaidi juu ya utafiti huo zitaendele ili kuangalia tena wanyama wengine kabla ya majaribio ya kuja kujiridhisha kwa binadamu.

Magufuli: Nataka Kutengeneza Tanzania Mpya

0
0
RAIS John Magufuli amewaambia wananchi wa Sengerema mkoani Mwanza na Watanzania kwa ujumla kuwa wana deni kubwa kwake baada ya kumchagua kwa kura nyingi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, lakini akawaahidi kuwa hatawaangusha na anataka kutengeneza Tanzania mpya.

“Nataka niwaeleze deni limebaki kwetu, nyie mmemaliza kazi yenu. Deni ni ahadi nataka niwaahidi kama nilivyokuja kuwaomba kura sitawaangusha, nataka kutengeneza Tanzania mpya,” alisisitiza Rais Magufuli huku akiwataka wananchi kuendelea kuiamini serikali yake, kwa kuwa iko pamoja nao.

Aidha, Rais Magufuli alisisitiza suala la watendaji wa serikali, kuacha kuwanyanyasa wananchi wanyonge, na badala yake wahangaike na mafisadi na wafanyabiashara wakubwa wanaokwepa kodi, badala ya kuwatoza ushuru wanyonge.

“Kusanyeni kodi kwa wafanyabiashara wakubwa na sio kwa wananchi wanyonge,” alisema Rais Magufuli na kupiga marufuku kwa halmashauri kuwatoza ushuru wakulima wanaosafirisha mazao yao kutoka shambani, na badala yake aliwataka wakurugenzi watendaji wa halmashauri zote nchini kutoza ushuru huo kwa wafanyabiashara wakubwa wanaosafirisha mazao kwa magari makubwa aina ya Fuso.

“Madiwani mlichaguliwa na wananchi kama nilivyochaguliwa mimi, kama kuna by laws (sheria ndogo) ya kukusanya ushuru wa gunia mbili hadi tatu mkaifute sheria hiyo,” alisema.

Aliongeza kuwa wananchi wanatumia muda na nguvu nyingi katika kulima mazao yao, halafu wanatoka shambani wanakuta mtu anawasubiri akiwa na risiti za ushuru, ambapo aliwataka wakuu wa mikoa na wilaya kulichukulia suala hilo kwa umuhimu wa kipekee.

“Tafuteni kodi kwa watu wenye biashara kubwa na sio wananchi wanyonge, maana watu wakubwa walikuwa hawalipi kodi, na sasa wafanyabiashara wakubwa walipe kodi na wanyonge wastarehe,” alisema na kuongeza kuwa serikali yake inapenda kukusanya kodi, lakini sio kodi inayokusanywa kwa wananchi wanyonge hasa wakulima.

Aidha, alisisitiza kuwa serikali yake haitatoa chakula cha bure kwa Watanzania ambao hawafanyi kazi wakiwa na mawazo ya kusubiri msaada wa chakula kutoka serikalini.

Akiwahutubia maelfu ya wakazi wa Sengerema kwenye Viwanja vya Mnadani wakati wa ziara yake ya siku mbili ya kikazi mkoani Mwanza, Rais Magufuli alisema, “Serikali yangu haina chakula cha bure kwa mtu ambaye hafanyi kazi.”

Aliwashukuru kwa kuwachagua wabunge wazuri wa CCM, William Ngeleja (Sengerema) na Dk Charles Tizeba (Buchosa) ambao alikiri kuwa wote ni wazuri na walishiriki kikamilifu katika kupitisha Bajeti ya Serikali kutenga kiasi cha Sh bilioni 2.5 kwa ajili ya Mahakama ya Mafisadi nchini.

Alisema kuna wakati ilimuwia vigumu wakati anataka kumteua Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, kwa kukiri Dk Tizeba na Ngeleja wote walikuwa na vigezo sawa.

Aidha, alisema serikali itatafuta fedha za ujenzi wa barabara ya Sengerema- Kamanga kwa kiwango cha lami ambayo kwa sasa inafanyiwa upembuzi yakinifu, huku akiwaahidi wananchi wa Busisi kuwa serikali imetenga fedha za ujenzi wa Daraja la Kigongo – Busisi, ambalo alisema litafanana na daraja lililojengwa Kigamboni, Dar es Salaam.

Jokate Asisitiza Kuitamani Collabo ya Diamond na Alikiba

0
0
Jokate Mpenzi wa Ali Kiba
Jokate Mwegelo amesisitiza kauli yake aliyoitoa kwenye Instagram mwezi uliopita kuwa anatamani kuona Alikiba na Diamond siku moja wanafanya collabo.

Akiongea kwenye kipindi cha 5 Select cha EATV hivi karibuni, Jokate alidai kuwa ili collabo hiyo iwe nzuri, ni muhimu iwe halisi na wala isilazimishwe.

“It’s has to be natural for it to be great,” alisema Jokate na kudai kuwa ni Diamond na Alikiba ndio kiini cha muziki wa Bongo Flava kwa sasa.

Pia alidai kuwa haoni sababu tena ya kujenga bifu na ex wake, Diamond kwakuwa ameshakua kiumri na kwamba ni muhimu kushirikiana ili kuonesha ushawishi wao.

Hata hivyo Jokate aliendelea kusisitiza kuwa yeye na Alikiba ni marafiki tu na kukanusha kuwa na uhusiano.

“We are just friends, we are better than that,” alisema.

Dr Mwaka Ajisalimisha Polisi.....

0
0
Siku chache baada ya Polisi wa Dar es Salaam kutangaza kumsaka mmiliki wa iliyokuwa kliniki ya tiba asilia ya Foreplan, Juma Mwaka ‘Dk Mwaka’ kwa agizo la Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamis Kigwangallah, tabibu huyo ameamua kujisalimisha polisi.

Dk Kiwangallah alitoa agizo hilo siku sita zilizopita baada ya kutembelea kliniki hiyo kwa mara ya pili. Dk Mwaka alijisalimisha jana saa nne asubuhi katika Kituo cha Kikuu cha Polisi, jijini Dar es Salaam na kuhojiwa kwa saa kadhaa kabla ya kuachiwa kwa dhamana.

Msako wa Dk Mwaka unachagizwa na madai ya ukiukwaji wa agizo la Serikali la kuendelea na utoaji wa tiba licha ya kufungiwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Salum Hamdani alisema jana kuwa baada ya kujisalimisha muda huo, alihojiwa na kuachiwa kwa dhamana lakini akatakiwa kuripoti leo kwa mahojiano zaidi.

“Kuhusu kupelekwa mahakamani, ni mpaka jeshi la Polisi litakapomaliza kukusanya ushahidi na kumkabidhi DPP ambaye atautumia kufungua kesi,” alisema.

Peter Msigwa Ainanga TCRA, Adai Wanatumiwa Iwaje Wakipige Faini Kituo cha ITV Wakati yeye ndo Aliyeongea

0
0
MCHUNGAJI Peter Msigwa Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini ameinanga Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Nchini (TCRA) na kuitaka iache kutumika, anaandika Charles William.

Msigwa ameyasema hayo hii leo kufuatia TCRA kutangaza kukitoza faini ya Tsh. 5 Milioni kituo cha televisheni cha ITV kwa madai ya kurusha kipindi ambacho Msigwa alimkashifu Dk. Tulia Ackson Naibu Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Niliwahi kusema Bungeni Kuwa tumezalisha taifa la watu wanafiki, waoga na wanaojipendekeza pendekeza, ITV kosa lao ni nini? Mimi ndiye nilikuwa naongea, aliyenihoji angejuaje kuwa naenda kuongea nilichoongea?” Ameng’aka.

Msigwa amesema kama maneno aliyoyazungumza katika kipindi cha “Kumekucha” kilichorushwa na ITV yalikuwa yanamkashifu Naibu Spika wa Bunge, aliyepaswa kulalamika kukashifiwa ni Dk. Tulia na siyo Mamlaka hiyo ya mawasiliano na pia kama kuna faini aliyepaswa kutozwa ni yeye (Msigwa) na siyo kituo hicho cha televisheni.

“Aliyekashifiwa kwa mujibu wa TCRA ni Ndugu Tulia, yeye ndiye alipaswa kunipeleka mahakamani kama anahisi kukashifiwa. Naiona hii ni njama ya kutisha vyombo vya habari visiwe vinatualika kwenye mahojiano kwenye vipindi vyao,” ameeleza Msigwa.

Msigwa ametadharisha kuwa ni vyema TCRA na mamlaka zingine za serikali zikafanya kazi kwa uhuru na weledi badala ya kufanya kazi kwa hofu na kujipendekeza kwa viongozi wakuu wa serikali kwani hali hiyo inatia dosari utendaji wa mamlaka hizo.

“Watu wamejaa hofu, uoga, mashaka na kutojiamini, maisha ya kujipendekeza ni magumu mno,” amesema Msigwa.

Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania jana ilitangaza kuvitoza faini inayofikia jumla ya Tsh.19 milioni vituo vya utangazaji vya ITV, Clouds TV na Clouds Fm kwa kukiuka kanuni za utangazaji.

AmbapoTCRA ilisema Clouds Media imepigwa faini hiyo kutokana na kosa la kushabikia mapenzi ya mbuzi na binadamu kwenye chombo chao cha habari pamoja na kupiga wimbo wa ‘Ahsanteni kwa kuja’ wa msanii Mwana FA ambao ni wa kudhalilisha utu wa mwanamke na unapaswa kupigwa muda maalum (usiku) kama ambavyo imeagizwa.

ITV wakipigwa faini kutokana na kipindi chake kinachojulikana kama ‘Kumekucha’ ambacho mgeni mualikwa Mchungaji Peter Msigwa Mbunge wa Iringa Mjini anadaiwa kusikika akisema, “Naibu Spika amekuwa kama anavaa pampasi, hataki kubanduka kwenye kiti cha kuongozea Bunge,” maneno yanayodaiwa kuwa ni ya kumkashifu kiongozi huyo wa Bunge.

Njemba Avamia Makao Makuu ya Trump, Adakwa!

0
0
NEW YORK: Njemba mmoja nchini Marekani aliyejiita kuwa ni mtafiti binafsi na shabiki wa Donald Trump, jana Agosti 10, 2016 alitumia masaa matatu kupanda jengo la mfanyabiashara huyo maaufu duniani ambaye pia ni mgombea urais wa nchi hiyo kwa tiketi ya Chama cha Republican lililopo jijini New York.

Taarifa zimeeleza kuwa njemba huyo mwenye umri wa miaka 21 mkazi wa Virginia alitumia vifaa maalum kupanda ghorofa hilo lililojengwa kwa vioo ambalo pia ni Makao Makuu ya Kampeni za Bwana Trump na ndiyo Makao yake Makuu Kibiashaa kabla ya polisi kumtoa akiwa amefikia ghorofa ya 21 huku akiwa amechomwa vibaya na vioo vya jengo hilo.

Trump anaishi kwenye ghorofa ya ya juu kabisa ya jengo hilo lakini kwa sasa anafanya kampeni zake nje ya mji.

Mpandaji alijivuta huku akiwa akionekana kuwa amelewa, akitaka kuingia ndani ya jengo hilo. Polisi waliofika eneo la tukio wamesema hawakuweza kutambua nini haswa lilikuwa lengo lake.

Hukumu Kesi Ya Babu Tale Bofya Hapa!

0
0
ILE kesi inayomkabili Meneja wa Staa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, Babu Tale ya kusambaza na kuuza DVD za mawaidha ya Shehe Hamis Mbonde bila ridhaa yake imeahirishwa tena na Mahakama Kuu ya Kanda ya Dar es Salaam hadi Agosti 24, mwaka ambapo hukumu itatolewa.
Akizungumza mbele ya mawakili na wahusika wa pande zote mbili leo asubuhi, Msajili wa Mahakama, Kayonza alianza kwa kutupilia mbali hoja ya mawakili wa upande wa Babu Tale, Robert Mkoba na Augustino Aluta iliyoomba kupewa muda zaidi kwa sababu ya mmoja kati ya mawakili wao (Paul Mgaya) ana udhuru na kwamba yupo jijini Arusha kwa semina.

“Mawakili mnaosikiliza kesi hii kwa upande wa Tale mpo watano, siwezi kuruhusu tena kuahirishwa kwa kesi hii kisa mmoja hayupo. Agosti 24 itakuwa siku ya hukumu na kutekelezwa ambacho kipo na niwaombe wote muwepo,” alisema Kayonza.

Awali kesi hiyo ilitakiwa itolewe hukumu Agosti 1 lakini kutokana na Mgaya kuumwa ilibidi kuahirishwa hadi leo (Agosti 10).

Wakili wa Shehe Mbonde, Mwesiga Muhingo akitolea ufafanuzi kuahirishwa kwa kesi hiyo alisema, siku hiyo ya hukumu iliyotolewa na msajili ni kuhusu kutekeleza yale ambayo mahakama iliagiza ambayo ni Tale kumlipa mteja wao (Shehe Mbonde) Sh. milioni 250 ama kwenda jela.

Soma Nafasi za Kazi Zilizotangazwa Katika Magazeti na Mitandaoni Leo 11 Aug 2016

0
0

Maalim Seif ahojiwa juu ya tuhuma za ufisadi

0
0
MAMLAKA ya Kupambana na Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar (ZAECA), imemhoji Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, baada ya kuwahusisha baadhi ya viongozi na watendaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na tuhuma za ufisadi.

Ofisa wa Kitengo cha Elimu kwa Umma cha ZAECA, Abubakari Mohamed Lunda, alisema jana kuwa Maalim Seif alihojiwa na Mkurugenzi wa ZAEC, Mussa Haji Ali, ili athibitishe tuhuma hizo.

Lunda alisema tuhuma zilizotolewa dhidi ya watendaji na viongozi ni nzito ndiyo maana mamlaka hiyo imeamua kuchunguza ukweli wake kwa manufaa ya Zanzibar na wananchi wake.

Lunda alisema kazi kubwa ya mamlaka hiyo ni kuchunguza jambo lolote ambalo linahusu maslahi ya Zanzibar katika kupambana na vitendo vya rushwa na uhujumu uchumi.

“Tayari mamlaka imemhoji Maalim Seif ili kutafuta ukweli juu ya tuhuma alizotoa za kuwapo viongozi wanaomiliki fedha chafu na mali nje ya nchi,” alieleza Lunda.

Alisema nia ya kumhoji Maalim Seif ilikuwa kupata ukweli wa tuhuma alizotoa dhidi ya viongozi na watendaji aliowatuhumu kwa kumiliki fedha chafu na mali nje ya nchi.

Picha Mpya za Shilole Zinazowatoa Udenda Midume Mikware Huko Mitandaoni Hizi Hapa

0
0
Bongo fleva singer, Zuwena Mohamed 'Shilole' has put on display her $exy tattooed thighs, through her Instagram account Shilole shared her amazing pics as she does daily showing off her hot body, see her another pic;

VIDEO: Gigy Money Akifunguka Kuhusu kutembea na ALIKIBA na ABDUKIBA Msikilize

0
0
Tangu watu wameanza kumfahamu Huyu binti kila mmoja anabaki mdomo wazi kwa kukosa majibu kwa yale anayo ya fanya huyu Binti.

Ukimtazama ni mdogo kiumri ila mambo yake hakuna anayeyafikia, Hivi juzi wakati Gigy Money akiojiwa katika Kipindi cha Take One cha Zamaradi Mtetema Gigy alifunguka LIVE kuhusu kutembea na ALIKIBA na ABDUKIBA.. Nisikumalizie Uhondo jionee Mwenyewe Katika  VIDEO  

Vyombo vya HABARI Vitakavyo Ripoti Mikutano, Maandamano na HABARI za Kichochezi Vitachukuliwa Hatua-Nape

0
0
Waziri Nape Nnauye amesema Waandishi na Vyombo vya Habari vitakavyoripoti mikutano, maandamano au habari za kichochezi vitachukuliwa hatua ikiwemo kufungiwa kwa kueneza uchochezi.

Amesema Vyombo vya Habari havipaswi kuripoti habari za kuichonganisha Serikali na wananchi wake.

Je yupo sahihiii?

Jela Miaka Mitatu Kwa Kumuibia Mkewe Dhahabu

0
0
Mahakama ya Wilaya ya Ilala, imemhukumu Hussein Janga kifungo cha miaka mitatu jela baada ya kupatikana na hatia ya wizi wa dhahabu zenye thamani ya Sh5 milioni mali ya mkewe, Saida Mwakitete.

Pia, mahakama hiyo imemtaka mshtakiwa huyo kumlipa mkewe Sh5 milioni ambazo ni thamani ya dhahabu aliyoiba.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi, Said Mkasiwa alisema ameridhishwa na mashahidi watatu wa upande wa mashtaka waliotoa dhidi ya mshtakiwa huyo.

Alisema upande wa Jamhuri uliwasilisha mashahidi watatu ambao wamethibitisha shtaka hilo pasi na kuacha shaka.

“Kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani hapa nimejiridhisha pasi na kuacha shaka hivyo mshtakiwa ninamtia hatiani kama alivyoshtakiwa,’’ alisema Hakimu Mkasiwa na kuongeza:

“Hivyo Mahakama imekuhukumu kifungo cha miaka mitatu jela baada ya kupatikana na kosa la kuiba seti moja ya dhahabu yenye ya Sh5 milioni.”

Kabla ya kutolewa kwa adhabu hiyo, Wakili wa Serikali, Sylvia Mitanto aliiomba Mahakama kutoa adhabu kali kwa mshtakiwa ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hizo.

Akijitetea kwa nini asihukumiwe kifungo hicho, Janga aliiomba Mahakama impunguzie adhabu kwa madai kuwa hali yake ya kiafya siyo mzuri. Aliomba apewe kifungo cha nje.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, Janga alitenda kosa hilo Oktoba 27, 2014 katika maeneo ya Upanga wilayani Ilala. Alidaiwa kuiba dhahabu ambayo ni cheni ya shingoni, cheni ya mkononi na hereni mali ya mkewe.

Inadaiwa kuwa wawili hao walidumu katika ndoa kwa mwezi mmoja.

BREAKING NEWS: Serikali laifungia gazeti la MSETO kwa miezi 36 lisichapishwe nchini

0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye leo Agosti 11.2016, ametangaza rasmi kulifungia gazeti la MSETO kwa miezi 36 lisichapishe Habari zake hapa nchini kwa njia yoyote ile kutokana na kukiuka maadili ya taaluma ya Habari.


Waziri Nape Nnauye ametoa tamko hilo huku akizitaja tuhuma mbalimbali zikiwemo:  Uchochezi, Uongo na Upotoshaji ambapo hazizingatii kanuni za taaluma ya uandishi wa habari.


 Amri hiyo ya kulifungia gazeti la mseto imetokana na tangazo la Serikali namba 242 la tarehe 10/8/2016 kwa mujibu wa sheria ya magazeti ya mwaka 1976 sura 229 kifungu cha 25(1)


Aidha, Waziri Nape amesema gazeti hilo linaandika habari na taarifa za uongo ambazo zina nia ya kupotosha jamii ikiwa ni pamoja na kutumia nyaraka za serikali ambazo zimegushiwa ili kuwachafua viongozi wa serikali na seerikali yao.
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live




Latest Images