Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104747 articles
Browse latest View live

Juma Nature: Sifanyi collabo na Diamond mpaka..

$
0
0
Rapper mkongwe, Juma Nature amedai kuwa hawezi kufanya wimbo na Diamond mpaka pale dhamira yake ya kushindana naye jukwaani itakapo timia.

Mapema mwezi April mwaka huu Nature alikiambia kipindi cha Ladha 3600 cha EFM kuwa Diamond ndiye mpinzani wake pekee kwa sasa na hakuisema kwa ubaya.

Akiongea na Times FM msanii huyo amesema, “Collabo na Diamond bado mpaka tupambane tushindanishwe kwenye jukwaa moja nani mkali wa kupiga show ndio labda ifate collabo.”

Nature ameongeza kuwa mashabiki wasifikirie vibaya kuhusiana na kauli yake hiyo lengo lake ni kujenga ushindani wenye faida kati yao.

Naj na Mr Blue wadaiwa kuwasiliana, Naj aeleza kwanini alisave namba ya Mr Blue kwa jina la ‘Zai’

$
0
0
Msanii wa muziki Naj amekanusha tetesi za kugombana na mpenzi wake Barakah Da Prince baada ya kudaiwa kupigiwa simu usiku wa manane na aliyekuwa mpenzi wake wa zamani Mr Blue.


Inadaiwa wakati Barakah ameshika simu ya mpenzi wake Naj, alipiga mtu ambaye namba yake ‘iliseviwa’ Zai na baada ya Barakah kupokea alikuta sio mwanamke bali ni mwanaume ambaye alidaiwa kuwa ni Mr Blue.

Akiongea katika kipindi cha U-Heard cha Clouds FM cha Jumatano hii, Naj amekiri kusave kimakosa namba ya Mr Blue kwa jina la Zai.

“Kuna watu wanaongea vibaya lakini hawajui, kwanza mimi siwasiliani na Mr Blue, unajua mimi mtu nikishakuwa naye hatuwezi kuwa marafiki, mnakuwa marafiki mnaongea nini sasa,” alisema Naj.

“Na mimi zamani sana hata kabla sijaanza mahusiano na Barakah, nikapata missed call kwenye hiyo namba, sasa mimi nikaisave ‘Zai’ kwa haraka haraka ili niingie whatsapp ili nijue ni nani, kwa sababu mimi mara nyingi nikipataga missed call sitakagi kumpigia mtu ambaye simjui, kwa hiyo baada ya kufanya hivyo ndo nikamjua ni nani. Kwa hiyo ilikuwa kitambo sana halafu mimi mwenyewe nilikuwa sijafuta wala nini na sio kwamba ni namba ambayo naitumia wala nini,” alifafanua zaidi.

Pia Naj ameeleza jinsi mpenzi wake Barakah alivyoigundua namba ya Mr Blue kwenye simu yake.

“Nilimpa Barakah simu yangu akawa anaitumia hata sijui kati yao nani alimpigia mwenzake kwa sababu namba ilikuwa kwenye majina. Kama ningekuwa na mambo mengi nisingejiamini kumpatia simu mpenzi wangu, kwa hiyo hata sijui nani alimpigia mwenzake kati yao, lakini namba ilitokea kama Zai,” alisema Naj.

Hata hivyo hivi karibuni katika kipindi cha U-Heard, rapper Mr Blue ambaye alifunga ndoa mapema mwaka huu na mwanadada aitwae Warda, alikana kuwasiliana na Naj.

Source:Bongo5

Mtoto wa OBAMA arekodiwa Akivuta Bangi

$
0
0
Mtoto mkubwa wa Rais Barack Obama – Malia Obama – anahisiwa siku kadhaa nyuma alikuwa amepewa kipisi cha bangi kuvuta na akavuta na kujikuta akirekodiwa na video za mapaparazi wa Marekani. Tukio hilo limekuja siku chache tu baada ya video nyingine kumuonesha binti huyo akikata viuno kwenye moja ya matamasha ya muziki huko Marekani.

Inasadikiwa Malia alivuta sigara hiyo ‘haramu’ kwenye tamasha la lollapalooza kwenye Jiji la Chicago, jimbo la Illinois ambalo ni jimbo la nyumbani kwa Rais Obama. Mmoja wa wahudhuriaji wa tamasha hilo Jerrdin Selwyn mwenye umri wa miaka 18 alidai kuwa alimkuta Malia akiwa anavuta ganja na marafiki zake na hakukuwa na shaka ya hilo kwani harufu ya bangi ilikuwa wazi
“Kulikuwa na kijana mmoja pale ambaye alikuwa anavuta na akampasia Malia ambaye alishikilia kama kwa dakika moja kisha akampatia mtu mwingine” alidai binti huyo. Na alidai pia kuwa alikuwa na picha zinazoonesha mtoto huyo wa Rais wa Marekani akivuta bangi hiyo

Chadema Inavyopangua Kete za CCM

$
0
0
Wakati Serikali ya CCM imekuwa ikijenga mazingira ya kuzuia uwezekano wa vyama vya upinzani kufurukuta, Chadema imekuwa ikichanga karata zake na kuendelea kujiimarisha na kushindana kisiasa na chama tawala.

Kwa mujibu wa baadhi ya wasomi na wanasiasa nchini, matukio makubwa ya kisiasa yanayoandaliwa na Chadema na kuibua mijadala imekuwa ikifanywa kimkakati sambamba na ya chama tawala, CCM.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Richard Mbunda aliliambia Mwananchi kwamba aonavyo yeye matukio mbalimbali ya Chadema ni mikakati ya kisiasa. “Inabidi wafanye matukio ili chama kiendelee kubaki katika ramani ya siasa,”alisema Mbunda.

Mwenyeki wa Chadema, Freeman Mbowe amesema tofauti na mawazo ya baadhi ya watu, matukio hayo zikiwamo operesheni mbalimbali za chama si mikakati ya kudumu bali ni za muda maalumu kwa malengo maalumu ambayo ikikamilika wanabuni mbinu nyingine.

Chadema wamekuwa wakibuni mikakati mbalimbali ya kuwafikia wananchi tangu mikutano na maandamano ya vyama vya siasa ilipopigwa marufuku na Rais John Magufuli hadi mwaka 2020. Mikutano iliyoruhusiwa ni ya wabunge tu tena katika majimbo yao, lakini si ya wanasiasa.

Katika Bunge la Bajeti, wabunge wa Chadema wakishirikiana na wenzao kutoka vyama vya siasa vinavyounda Ukawa walikuwa wakisusa vikao kwa staili tofauti. Kuna siku walitoka nje wakiwa wamevaa mavazi meusi, siku nyingine walibandika vitambaa mdomoni na kuna siku walibeba mabango yenye ujumbe mbalimbali.

Julai mwaka huu, CCM ilipoandaa mkutano maalumu uliopangwa kwa ajili ya kumkabidhi Rais Magufuli kijiti cha uenyekiti wa chama hicho, Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha) lilizua hofu lilipotangaza kwamba litakwenda pia Dodoma kulisaidia Jeshi la Polisi kuzuia mkutano huo kwa kuwa Serikali ilipiga marufuku mikutano ya ndani na nje.

Hatua hiyo ya Bavicha ilisababisha Jeshi la Polisi kuweka ulinzi mkali kila kona mjini Dodoma kuzuia uwezekano wa Bavicha kuvuruga mkutano huo wa CCM. Hata hivyo, Bavicha walipiga chenga, walikutana Dar es Salaam ambako walifanya mkutano wao.

Wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM walipokuwa katika shangwe na nderemo baada ya kukamilisha ajenda yao ya kumchagua kwa asilimia 100 Rais Magufuli, Kamati Kuu ya Chadema iliketi Dar es Salaam na kutoka na mkakati wa kupinga uvunjaji wa Katiba na sheria waliouita operesheni Ukuta ambao unasumbua vyombo vya usalama hadi sasa.

Matukio hayo ambayo yametokea kwa kufuatana yamekuwa yakigonga vichwa vya habari huku baadhi wakidai ni dalili za vurugu na uchochezi, lakini pia yanakiweka chama hicho kwenye mjadala kuliko vingine.



Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa waliotafutwa na gazeti hili jana kuzungumzia namna Chadema inavyocheza karata zake kuhakikisha inasikika sawa au hata kuifunika CCM, wamesema huo ni mkakati wa upinzani kuendelea kutamba kwenye ‘ulingo wa siasa.’ Baadhi ya operesheni zilizoijengea umaarufu ni kama Sangara na Movement For Change (M4C).

Akizungumzia mfuatano wa matukio hayo, Mbunda amesema aonavyo yeye matukio hayo ni mikakati ya kisiasa akibainisha kuwa kila chama kina wapangaji mikakati ambao hupanga na kutathmini mikakati hiyo. “…Siyo mikakati yote inayofaulu. Wakiona huu haufai wanaweza kubadili.”

Mhadhiri huyo alitoa mfano wa Operesheni Ukuta ya Chadema iliyopangwa kufanyika Septemba Mosi mwaka huu kwamba huenda wakati ukifika chama hicho kikabadili uamuzi wake baada ya kufanya tathmini ya operesheni hiyo.

Mbunda amesema kwamba hizo ni amsha amsha ambazo husaidia vyama hasa vya upinzani kuendelea kuonekana katika uso wa siasa na kwamba vyama mbalimbali duniani hutumia mbinu hizo hivyo siyo jambo la kushangaza. “Wasipofanya hivyo hata watu watahoji kwa sababu hayo ndiyo maisha ya siasa,”alisema Mbunda.

Kauli hiyo iliungwa mkono na Dk Benson Bana ambaye alisema kinachofanywa sasa na Chadema ni mkakati wa kuendelea kubaki na kusikika kwenye uwanja wa siasa.

Dk Bana, ambaye ni mhadhiri wa UDSM amesema chama hicho kinafanya hivyo ili kisipotee kwenye ramani ya siasa hadi Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

Mchambuzi huyo wa masuala ya siasa alibainisha kuwa chama hicho kikuu cha upinzani kinafanya hivyo kwa sababu kilikuwa hakijajipanga kuona Serikali ya awamu ya tano inatekeleza baadhi ya ajenda zao.

“Hawajajipanga kuwa na mikakati endelevu…wanaona wamenyang’anywa tonge mdomoni. Mikakati yao ni ya kuziba ombwe hilo,” alisema.

Pia, Dk Bana amesema  jambo hilo siyo baya kwenye ulimwengu wa siasa tatizo ni aina ya mikakati kwamba Chadema inapaswa kuja na mikakati ambayo inakidhi haja ya Watanzania siyo mikakati ya kumwita Rais John Magufuli dikteta. “Watathmini mikakati yao. Waje na mikakati yenye mashiko,”amesema Dk Bana.

Taarifa Toka IKULU Kuhusu Maagizo ya Rais Magufuli Aliyoyatoa Jana Jijini Mwanza

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameviagiza vyombo vya dola kuchunguza na kuchukua hatua za kurejesha mali za Chama Kikuu cha Ushirika cha  Nyanza ambazo zilinunuliwa na kutwaliwa na watu binafsi kwa njia za ujanja ujanja.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo tarehe 11 Agosti, 2016 alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Mwanza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza.

Dkt. Magufuli alisema Serikali yake haipo tayari kuwafumbia macho watu wachache waliovifilisi vyama vya ushirika vya wakulima kwa kujimilikisha mali za ushirika yakiwemo majengo, viwanda na mashamba na ametaka mali hizo zirudishwe mikononi mwa wananchi.

"Hata kama walichukua miaka 20 iliyopita, vyombo vya dola vichukue hatua na mali hizo zirudishwe kwa umma" Alisema Rais Magufuli.

Katika Mkutano huo Rais Magufuli pia alisema Serikali itafanya oparesheni kubwa ya kuteketeza Makokoro katika ziwa Victoria ikiwa ni juhudi za kukabiliana na tatizo la uvuvi haramu uliosababisha kupungua kwa samaki na kuathiri shughuli za uvuvi na usindikaji wa minofu ya samaki katika viwanda.

Alibainisha kuwa lengo la kuchukua hatua hiyo ni kuwezesha samaki wengi kuzaliana ili lengo la Serikali la kujenga viwanda vya kusindika mazao ikiwemo viwanda vya kusindika minofu ya samaki lifanikiwe.

Kabla ya kuhutubia mkutano huo Rais Magufuli aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja la waenda kwa miguu la Furahisha linalokatiza barabara ya Uwanja wa Ndege kwenda katikati ya Jiji la Mwanza.

Daraja hilo litakuwa na urefu wa meta 46, upana wa meta 3.6 na kimo cha meta 5.5 na ujenzi wake unatarajiwa kukamilika Mwezi Desemba Mwaka huu kwa gharama ya Shilingi Bilioni 6.455

Akizungumzia ujenzi huo Rais Magufuli alimtaka Mkandarasi anayejenga Daraja la Furahisha kukamilisha kazi hiyo Mwezi Desemba Mwaka huu kwa mujibu wa mkataba, na pia ameagiza Mkandarasi aliyekuwa akifanya upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Mwanza kuendelea na kazi hiyo ndani ya wiki moja kwa kuwa Serikali imejipanga kumlipa fedha za kazi hiyo.

Pia Dkt. Magufuli ameahidi kuongeza fedha katika ujenzi wa barabara ya njia nne kutoka Katikati ya Jiji la Mwanza hadi Uwanja wa Ndege wa Mwanza ili barabara hiyo ifike hadi uwanjani badala ya kuishia eneo la Pasiansi.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Mwanza

11 Agosti, 2016

Maamuzi ya Juan Mata baada ya kuhisi maisha Old Trafford yatakuwa magumu kwake

$
0
0
Kitendo cha kocha mpya wa Man United Jose Mourinho kumuingiza Juan Mata dakika ya 63 na kumtoa katika dakika za nyongeza katika mchezo wa ngao ya hisani dhidi ya Leicester City, kinaonekana kuchukuliwa tofauti na kutabiriwa kuwa maisha ya nyota huyo Old Trafford yatakuwa magumu.

Stori kutoka The Times inaripoti kuwa Juan Mata kwa sasa analazimisha klabu imuachie aondoke licha ya kuwa uongozi wa Man United hawana mpango wa kumuuza kwa sasa, lakini gazeti hilo pia linaripoti kuwa kocha wa Everton Ronald Koeman kaonesha dhamira ya kumuhitaji staa huyo.

Kama utakuwa unakumbuka vizuri suala la Juan Mata kuhusishwa kuondoka linatarajiwa kutokea kutokana na Jose Mourinho kudaiwa kutomuhitaji, hali kama hiyo iliwahi kumkuta Juan Mata wakati yupo Chelsea na Jose Mourinho ila mwaka 2014 aliamua kuondoka klabu hiyo na kujiunga na Man United.

Wastara Amnasa Kigogo Morogoro

$
0
0
IMEVUJA! Safari za mara kwa mara mkoani Morogoro, zinazofanywa na staa wa filamu za Kibongo, Wastara Juma zinadaiwa kuchangizwa baada ya kumnasa kigogo mmoja mkoani humo.

Chanzo makini kililiambia Risasi Mchanganyiko kuwa muigizaji huyo amempata mfanyabiashara na kiongozi wa serikali mkoani humo, kitu kinachomfanya afanye safari zaidi ya mara nne kwa mwezi.
“Yaani siku hizi Wastara hatulii Dar ilipo familia yake, amekuwa akisafiri Morogoro kila kukicha, yaani hivi sasa ni mapenzi motomoto, lakini ni kwa siri sana hataki ijulikane,” kilisema chanzo chetu hicho.
Baada ya kuunyaka ‘ubuyu’ huo, paparazi wetu alimtafuta Wastara na alipopatikana, alikana taarifa hizo na kudai safari zake za mara kwa  mara mkoani humo ni kwa vile huko ni nyumbani kwao.

“Hizo habari siyo kweli, watu wanapenda tu kuongea, Morogoro huwa naenda kwa sababu ya mambo mawili, kwanza kule ndiko nilikozaliwa hivyo huwa naenda kuwaona ndugu zangu na pili huwa naenda kwa sababu nina kituo cha kulelea watoto yatima, kwa hiyo huwa naenda kuwaangalia,” alisema Wastara.

Source:GPL

Kitale Katoa Ufafanuzi Juu ya Mali za Marehemu Sharo Milionea…

$
0
0
Ni August 11, 2016 ambapo Mchekeshaji wa filamu Kitale amefunguka kuhusiana na mali zilizoachwa na marehemu Sharo Milionea.

Staa huyo aliipa heshima millardayo.com & Ayo TV na kuyaongea haya>>>>Wakati mimi niko nae alipofikia level fulani ilinibidi nimtafutie uongozi ambae HK alihusika kumsimamia ila baadhi ya vitu hususani kama viwanja, bajaji, kodi alipokuwa akiishi pale sinza vile vyote nilijitahidi akakabidhiwa mama mzazi’– Kitale

‘Mama wa Sharo tulimuuliza kwamba kiwanja kilichonunuliwa na Sharo Je kiuzwa alituambia tukiuze atajenga nyumba Tanga pamoja na fedha zilizokuwa zinatoka kwenye makampuni ya ringtone’= Kitale

Rais Magufuli Akerwa na Uozo Uliopo Ndani ya CCM

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuna mambo ya hovyo ambayo yapo ndani ya Chama cha Mapinduzi ambayo yanahitaji kuhojiwa na kupatiwa majibu yenye tija.

Aikihutubia maelfu ya wananchi jana waliojitokeza kumsikiliza katika viwanja vya Furahisha Jijini Mwanza Dkt. Magufuli alisema anafahamu kwamba ndani ya CCM kuna mambo ya hovyo na mfano ni uwanja wa CCM Kirumba na majengo mengine ya CCM ambayo ukiuliza maduka na ofisi zinazozunguka majengo hayo mapato yake yako wapi huwezi kupata majibu ya kuridhisha.

"Ninyi wananchi wa Mwanza na wanachama wa CCM hojini haya na atakayewauliza mwambieni ni mimi Mwenyekiti wa CCM nimesema muwaulize, nataka chama ambacho mali zake zinajulikana kwa sababu ukienda kuwauliza mnakusanya shilingi ngapi kwa chumba kimoja wanaweza kukuambia ni elfu 50 kumbe wanaingiza laki 5" Alisema Rais Dkt. Magufuli

Rais Magufuli alisisitiza kwamba anaitaka CCM ya Rais wa kwanza wa Tanzania Mwl. Julius Nyerere siyo CCM ya watu ambao mchana wapo CCM na usiku wapo vyama vingine, wanaofanya hivyo ni bora wahamie huko moja kwa moja.

Aidha katika hatua nyingine Rais Dkt. Magufuli ameagiza uongozi wa Jiji la Mwanza kutowatoza ushuru wajasiriamali wadogo wadogo kwa kuwa wanatakiwa wanufaike na taifa lao na pia wamachinga waachwe mjini kwanza hadi hapo watakapo andaliwa mazingira mazuri ya kufanyia biashara yatakayokuwa na wateja.

Vera Sidika amtaja anayemsikiliza kati ya Diamond na Alikiba

$
0
0
Mrembo wa Kenya, Vera Sidika amejibu swali la ni nyimbo za msanii yupi anazozisikiliza zaidi kati ya Diamond na Alikiba.

“Mimi namsikiliza Diamond,” anasema Vera. “Style yake tofauti kisha nzuri, kisha naona kuwa amejikakamua anatoa hits after hits hatulii, yeye hutia bidii kila siku. Halafu pia si muziki peke yake, ameweza kusaidia vijana kuwapatia nafasi ya ku-explore talent zao, kama sasa hivi yuko na artists ambao wako chini yake which is a good thing,” ameongeza.

Vera amedai pia kuwa anampenda Diamond kwasababu ni baba mzuri na anayetimiza majukumu yake.
Bongo5

A New Travelers Social Network is Here..Check It Out

$
0
0
A new interactive social network, developed mainly for travelers; backpackers, hikers, holiday
makers and those who simply enjoy exploring the world.

Anyone can join the social network freely by login to www.ezylinc.com and post photos of
World's heritage sites, Historical sites, Parks, Hotels, Restaurants, write articles about
destinations, Legends, form groups, messaging, add friends and much more.

Ezylinc connects two groups. On one side we have travelers and adventurists and on the other
side local businesses connected to travel and tourism. The social network is developed by a
Tanzanian startup.
Let’s take Tanzania as an example, where travel and tourism is one of the leading industries.
The country is harboring a diversity of an unmatched fauna and flora, a unique destination on
the African continent. Kilimanjaro, the highest free standing snow-capped mountain in Africa,
the Islands of Zanzibar, the national parks of Serengeti, Ngorongoro Crater, Tarangire, Lake
Manyara, Ruaha, Selous and the Marine Park of Mafia Island are few of the living examples
found in Tanzania.

In 2014 The tourism sector in Tanzania, contributed 17 per cent to the country’s GDP and
accounted for 25 per cent of all the foreign exchange earnings, with 2 billion USD in revenues.
The country ranks 5th among African countries with the highest growth in the tourism
industry.

This is why we have created a new social network. We want to support travel, local
businesses, and create more jobs in tourism along the way.
Join Ezylinc by login to http://ezylinc.com/`

Rais Magufuli: TAKUKURU Chunguzeni Kampuni ya Robert Kisena (Simon Group)

$
0
0
RAIS John Magufuli ameutaka uongozi wa Mkoa wa Mwanza na TAKUKURU, kuhakikisha kuwa watu waliopora mali za Chama cha Ushirika cha Nyanza (NCU), wanapatikana na kuzirudisha mali hizo mara moja, huku akiitaja Kampuni ya Simon Group yenye umiliki katika kampuni za UDA na mabasi ya haraka Dar es Salaam (UDA-RT).

“RC (mkuu wa mkoa) umezungumza kwamba katika miaka yote aliyepewa alikuwa anunue kwa zaidi ya bilioni moja lakini amelipa milioni 34 tu na nasikia ni Simon Group.” alisema Rais Magufuli.

Simon Group ni kampuni iliyozaliwa na kampuni ya Simon Agency iliyoanzishwa mkoani Shinyanga na Robert Kisena, kushughulika na ununuzi na uchambuaji wa pamba karibu miaka minane iliyopita.

Kampuni hiyo ina historia ya kuingia kwenye migogoro mikubwa ya kibiashara na Vyama Vikuu vya Ushirika vya Kanda ya Ziwa, vikiwamo Chama Kikuu cha Ushirika cha Mkoa wa Mwanza (NCU) na Chama Kikuu cha Ushirika cha Mkoa wa Shinyanga (SHIRECU), ambavyo vinaidai mamilioni ya fedha kwa kukiuka mikataba mbalimbali, ikiwamo ya kukodi vinu vya kuchambulia pamba na ununuzi wa rasilimali.

Simon Agency inahusishwa pia na kununua kiwanda cha kusindika mafuta cha NCU kijulikanacho kama "New Era", na nyumba za ushirika huo kwa bei ya kutupa.

Inadaiwa kuwa, wakati kampuni hiyo iliweza kununua kiwanda hicho kwa Sh. milioni 34 tu, bei halisi ya kiwanda hicho na miundombinu yake ilikuwa zaidi ya Sh. bilioni 1.5.

Robert Simon Kisena, kwa kutaka mambo yamnyokee zaidi, mwaka 2008 alijaribu bahati yake kwa kugombea ujumbe wa Halmashauri ya Mkoa (CCM) kuwakilisha Wilaya ya Maswa, lakini hakubahatika kuchaguliwa.

Kuanzia hapo alijipambanua kama kada wa CCM na tajiri anayeibukia. Kipindi hiki kilishuhudia wafanyabiashara wengi nchini wakifadhili au wakiteuliwa kuwa makamanda wa Umoja wa Vijana wa CCM ili wasiweze kuguswa na kwa biashara zao zinawiri.

Mwaka 2010, Robert Kisena, alijitosa kugombea ubunge Jimbo la Maswa Magharibi kwa tiketi ya CCM, lakini akashindwa na John Magalle Shibuda wa CHADEMA, katika uchaguzi uliojaa fujo za kila aina na umwagaji damu.

Katika hali iliyoashiria kwamba alikuwa tayari ameingia katika "pepo ya wasioguswa", alidiriki kumkata "mtama" (kumpiga ngwala hadi chini) Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Maswa, kofia na "crown" yake ikabwagwa chini na kuchaniwa sare, kwa sababu tu alitaka kumhoji kuhusiana na ghasia za uchaguzi.

Kwa dhambi hiyo kuu ya kudhalilisha dola, Robert Simon aliachwa huru bila kukamatwa wala kuchukuliwa hatua za kisheria kwa sababu alikuwa na kinga ya wakubwa, wakati Shibuda akisota mahabusu kwa kugeuziwa kibao.

Ni baada ya uchaguzi huo, Robert Kisena alipohamia Dar es Salaam kutafuta "malisho mapya", kwa wito au kwa kubebwa na "makada" wenzake wa CCM, baada ya kuthibitika anao ujasiri wa kutosha kuweza kuingia kambi ya "makada wa zama hizi wa CCM." Tazama Video:
Source:Jamii Forums

Tamko la Vyama vya Siasa Kufuatia Hali ya Kisiasa Nchini. Vyaipinga operesheni UKUTA ya CHADEMA

$
0
0
Vyama vya siasa nchi jana vilikutana na kufanya tafakuri ya kina juu ya hali ya kisiasa nchini pamoja na tamko la Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Augustino Mrema: Mimi ni mpinzani mstaarabu

$
0
0
Mwenyekiti wa chama cha TLP, Augustino Mrema amewaonya wapinzani wenzake kuacha kupanga kufanya maandamano Septemba, 1 na watumie muda wao kushirikiana na Rais Magufuli kufanya kazi ili kuleta maendeleo kwa watanzania.

Mrema ameyasema hayo wakati akizungumza katika kipindi cha Power Breakfast cha Clouds Fm na kusema kuwa wanatakiwa kufanya siasa kama anayoifanya yeye ya kuwa mpinzani mstaarabu ambaye anaunga mkono kazi zinazofanywa na Rais Magufuli.

“Mimi ni mpinzani mstaarabu, upinzani wa kijinga siutaki kama wewe ni mpinzani wa kweli inatakiwa ukae bungeni ili kutoa matatizo ya watanzania lakini sasa wao wanatoka ningekuwa mimi nisingetoka, niwashauri tu wakae wafanye kazi,” alisema Mrema.

Aidha Mrema aliwaonya Chadema kuacha kupanga kufanya maandamano ya UKUTA kwani rais wa sasa ana nia ya dhati kuwafanyia kazi watanzania na kama wamekosa kazi ya kufanya waende shambani kulima au kusaidia kutatua tatizo la madawati.

“Rais ameshasema apewe muda kuleta maendeleo kwa watanzania na yeye ndiyo mwenye majeshi kama wamepanga kufanya maandamano wasidhani kitawakuta kama kilichonikuta mimi mwaka 1995, rais anataka tu kazi kama hawana ya kufanya waende mashambani kulima au wakatafute madawati,” alisema Mrema.

Ridhiwani Kikwete Awapongeza AliKiba na Diamond ‘Mmeonyesha Umuhimu wa Kuwa Mastaa’

$
0
0
Mbunge wa Chalinze Mhe. Ridhawani Kikwete amewapongeza wasanii wa muziki, Diamond Platnumz na AliKiba kwa kutoa msaada wa tsh 41milioni kwa ‘GSM Foundation’ ili kusaidia jitihada za taasisi hiyo za upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi.
Diamond na Ali Kiba

Mtoto huyo wa Rais mtaafu, amewapongeza wasanii hao kwa kuonyesha kuguswa na kusaidia matatizo ambayo yanatokea katika jamii.

“Katika vitu vimeonyesha umuhimu wa kuwa stars katika jamii yetu ni hili mlilolifanya wadogo zangu. Ni jambo la kusifiwa na Mungu atawalipa kwa kuwaongezea maarifa ya kufanya kazi zenu vizuri,” Ridhiwani aliandika katika instagram yake.

Aliongeza, “Pia niwapongeze sana GSM Foundation kwa kazi nzuri mnayoifanya. Kutoa si utajiri, ni moyo na mungu atakuzidishia ndugu mkurugenzi Gharib pale ulipotoa. Kila la kheri katika kusaidia jamii yetu yenye mahitaji. Peace to you,”

Siku chache zilizopita Diamond Platnumz alitoa msaada kwa taasisi hiyo wa tsh 20 Milioni na baadae AliKiba na yeye aliamua kutoa tsh 21 Milioni.

Bongo5

Wanawake, Msing'ang'anie Wanaume Ambao Hawawataki

$
0
0
Zaidi ya watu wa 5 wameshakueleza kwamba jamaa hana time na wewe na ameshachumbia mtu mwingine hukuamini. Mungu sio Mwigulu Nchemba, siku 1 akiwa kwenye mishemishe za kuchepuka simu yake ikajipiga ukamsikia anaongea na msichana mwingine na baada ya muda ukawasikia wanapiga kwinchi kwinchi Live wakati alikuaga muda huo yuko kwenye kikao cha harusi. Mungu akaamua kukuonyesha kitu live.

Ulipomuuliza akaruka futi elfu 6 kwamba unamsingizia una kila ushahidi kwamba huyo jamaa ni kimeo ila kwa sababu akili yako ina ujibwa ulezi uliochanganywa na alizeti ukamsamehe, sasa leo amekuoa na tabia zilezile walizokuonya rafiki zako zimeendelea, unashinda unalia na kuimba Pambio la bwana tenda miujiza usiaache mpaka mwaka huu upite.

Alishatenda muujiza kukuonyesha ushahidi hukutaka kumsikia, ukapenda zaidi matarumbeta ya harusi bila kujali ndoa itakuwaje. Pole hakuna muujiza hapo, jipigie matarumbeta kwa kujitendea muujiza. Kamwe usidharau Mungu akikuonyesha (clear Signs) kwamba mtu uliyenaye ni shida. Using'ang'anie kuwa mjumbe wa bunge la katiba kama unahisi posho haitoshi achia ngazi.

Heri ukose harusi leo ujiandae kwa ndoa bora ya keshokutwa.

Mchungaji Alowa Maneno ya Mama Wema Sepetu

$
0
0
Yule mchungaji aliyejitokeza hivi karibuni kumuombea muigizaji wa sinema za Kibongo, Wema Sepetu, Daudi Mashimo, amedaiwa kuvurumishiwa matusi na mama wa staa huyo, Mariam Sepetu alipokuwa akimpigia simu kumuombea.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, mchungaji huyo anayeongoza kondoo katika Huduma ya Injili ya Maumivu na Uponyaji iliyopo Mbezi-Msakuzi jijini Dar, anadaiwa kukutwa na dhahama hiyo hivi karibuni ambapo pasipo kuelewa sababu, alijikuta akilowa mvua ya matusi.

“Mchungaji baada ya kumuombea Wema kanisani kwake, alipewa namba ya  simu ya mama Wema ili aweze kuzungumza naye kama mzazi kuhusu kumhimiza mwanaye afanye maombi. Sasa bahati mbaya siku alipompigia mama Wema alikuwa hajisikii vizuri.

“Akamuangushia maombi, mama Wema akashukuru na wakawa wanaendelea kuwasiliana. Sasa kuna siku mchungaji akampigia mama Wema, ghafla akashangaa anaporomoshewa matusi.

“Inadaiwa mama Wema alisikia kuwa, mchungaji huyo amekuwa akimchoresha kwa waandishi wa habari kila anapozungumza naye anawaambia waandishi. Siku moja aliongea naye, walipomaliza, akapigiwa simu na waandishi na kuulizwa jambo waliloongea na mchungaji huyo, ndipo akaona kumbe anamchoresha, ndiyo maana akamshushia matusi,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:

“Kama unavyomjua tena mama Wema ni mtu wa kampa… kampa tena. Alimpa mazimamazima, mchungaji mwenyewe akawa mpole.”

Baada ya Amani kumegewa ubuyu huo, lilimtafuta bi mkubwa huyo ili kumuuliza kulikoni hadi afikie hatua ya kumporomoshea matusi mtumishi huyo wa Mungu ambapo alipopatikana, alisema hamfahamu mchungaji huyo na hajui anataka nini kwake.

“Mimi simjui huyo mchungaji, atakuwa anatafuta kiki kupitia jina langu. Kwanza hata aliposema anamuombea mwanangu, alisikia ni mgumba? Hana lolote huyo! Sijui namba yangu ya simu aliipata wapi, akawa ananipigiapigia simu,” alisema mama Wema.

Kwa upande wake, mchungaji Mashimo alipotafutwa na Amani, alishtuka na kudai analishughulikia suala hilo kiroho zaidi.

“Nyinyi hilo suala mmelisikia wapi? Tambueni tu nalishughulikia kiroho hivyo nisingependa kulizungumzia kwa kirefu kwa sasa kwani Mungu ni mwema sana kwetu,” alisema mchungaji huyo.

Usitegemee Kumuona Pogba Akiichezea Man United Weekend hii, Kafungiwa

$
0
0
Najua inawezekana wewe ni mmoja kati ya mashabiki wa soka duniani wanaosubiri kumuona staa wa kimataifa wa Ufaransa aliyejiunga na Man United akitokea Juventus ya Italia Paul Pogba akiichezea Man United katika mchezo wa ufunguzi wa Man United dhidi ya Bournemouth weekend hii.

Stori kutoka chama cha soka cha England FA kimethibitisha staa huyo kufungiwa kucheza mechi ya ufunguzi kutokana na kuwa na adhabu ya kadi mbili za njano alizooneshwa katika michuano ya Copa Italia akiwa na Juventus ya Italia, adhabu ambayo kwa mujibu wa kanuni anahama nayo.


Paul Pogba alijiunga na Man United akitokea Juventus ya Italia kwa ada ya uhamisho wa rekodi ya dunia wa pound milioni zaidi ya 100, lakini Paul Pogba anaungana na Robert Huth, Moussa Dembele na Chris Smalling  waliofungiwa na FA kucheza mechi za ufunguzi.

Rais Magufuli Atoa Mpya..Awataka Watanzania Waendelee Kufyatua Watoto Bila Hofu

$
0
0
August 12 2016 Rais wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli alikutana na wakazi wa Dar es salaam na kuzungumza nao kuhusu maendeleo ya nchi lakini hakuacha kukumbushia lengo lake kuu la kuruhusu elimu bure kwa kila mwanafunzi wa Tanzania kuanzia darasa la kwanza hadi sekondari.

Rais Magufuli amesema…
’Ndugu zangu msiwe na hofu kuhusu kuwa na watoto, nyie fyatueni watoto wa kutosha maana watasoma bure‘

Shilole Afungukia Tatuu Zake za Kichina

$
0
0
Na Leonard Msigwa
MWANADADA anayefanya poa kwenye game la muziki Bongo, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ amefungukia maana halisi ya tatuu zake mpya alizojichora baada ya kufuta zile za awali ikiwemo ile ya X- wake, Nuh Mziwanda.

Shilole aliiambia safu hii kuwa, mbali na zile zinazosomeka kama jina lake la Shishi, zile za Kichina ni alama za kimuziki ambazo zinaonesha jinsi anavyoipenda kazi yake.

“Tatuu zangu zimechorwa kwa lugha ya Kichina na Kiingereza, hii ya bega la kulia ni jina langu la Shishi Baby na hizi nyingine za Kichina ni ala za muziki kuonesha hisia zangu za dhati juu ya muziki na nimefuta zile za zamani zote,” alisema Shilole
GPL
Viewing all 104747 articles
Browse latest View live




Latest Images