Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

TOYOTA CELICA SPORT INAUZWA KWA BEI POA..CALL 0714604974

$
0
0
 ABOUT 2000 TOYOTA CELICA :

Vehicle Type: Sports Car
Price: TZS 8,500,000
Negotiable: Yes
Kilometers: 130,000
Transmission: Automatic
Four Wheel Drive: No
Vehicle Current Location: In Tanzania
Import Duty is Paid: Yes
Date Listed: 29-03-2014

Its a Toyota Celica, Sport Car , Engine capacity 1800, Its in Dar es Salaam,
CONTACTS:
Location: Dar Es Salaam 
Tel: +255 (0) 714 604 974
Tel: +255 (0) 655 463 056

Viti vya Nyuma
Viti Vya Mbele


Dash Board



KUNUKA KIKWAPA NA WEUSI KATIKATI YA MAPAJA YANGU VINANINYIMA RAHA

$
0
0
Naomba niombe msaada kwenu wadau,nina matatizo sijui niseme shida  ambazo kiukweli zinanikosesha raha,nimekua nikihangaika sana kutafuta dawa ya kumaliza harufu ya kikwapa,yaani ni kwamba nimejaribu kila aina ya deodorant,na perfumes za kila aina lakini harufu haiishi,itokee bahati mbaya nisahau kupata Deodorant jamani sio siri najisikia hata mimi mwenyewe jinsi ninavyotoa harufu kali,zaidi ya harufu makwapa yangu ni meusi,ajabu,niliambiwa deodorant za Forever Living zinasaidia kumaliza weusi makwapani lakini wapi sioni tofauti,nawaombeni mnisaidie jamani nakosa raha,kifupi harufu utadhani lile jasho wanalonuka wanaume,wakati mwingine nafikia hata kujinyanyapaa mwenyewe,kwa kutokwenda kwenye shuhuli,nahisi wenzangu wananisema,shida inakuja muda wa kazi,kwani siwezi kukwepa kwenda ofisini,kiukweli it is so embarrassing.

La pili,huohuo weusi,katikati ya mapaja nako hakufai,yaani nikipanua miguu utadhani nimesilibwa lami hapo kati,nimejaribu kutumia mikorogo,haikusaidia,cream zile za hospitali za ngozi,pia nimejaribu,angalau kidogo utaona natakata,tatizo lake baada ya muda yanatoka mapele kama vijipu nashindwa hata kutembea shauri ya friction,nilipata ushauri wa kuvaa skin tight ili kuepusha friction,lakini lile la weusi lipo palepale,wenzangu nawaomba,kama kuna mtu alishawahi pata  matatizo kama yangu,naomba msaada tutani,jamani siyo siri,pamoja na kutaka nionekane maridadi,lakini pia wakati wa majambos si mwajua kuna muda wa mahabuba kwenda down,sasa inapofikia hapo,dah,najisikia aibu kwa maana naona kama vile najichoresha,na jamaa yangu huwa hakubali bila kunipagawisha kwa njia hiyo,sasa nipo na wakati mgumu
.
Huwa napendelea sana kusoma story kila wikiendi ila wamama/wadada saa nyingine mna maneno makali ambayo yanatukatisha tamaa kuomba ushauri humu,nawaombeni jamani,wengine hatuna pa kusemea wala wa kutupa ushauri wa kweli,tusaidiane jamani,Samahani kama nimewakwaza

WAJUMBE WA BUNGE MAALUMU WASUSIA BUNGE

$
0
0
Dodoma/Dar. Wakati Bunge Maalumu la Katiba linatarajia kuanza kujadili Rasimu ya Katiba kesho, baadhi ya wajumbe wa Bunge hilo wameanza kuondoka bungeni, kupinga mwenendo wa Bunge hilo.

Hatua hiyo ya wabunge hao inakuja wakati Bunge Maalumu la Katiba juzi lilipitisha azimio la kutumia kura ya siri na wazi katika kuamua vifungu vya rasimu.

Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samia Saluhu alisema baada ya kupitishwa kwa utaratibu wa kupiga kura za siri na wazi katika Bunge hilo, kuanzia Jumatatu wataanza kujadili sura ya kwanza na sita ambayo inahusu Muundo wa Muungano.

Katika sura ya kwanza, mambo ambayo yanatakiwa kujadiliwa ni Jina, Mipaka, Alama, Lugha na Tunu za Taifa wakati sura ya sita mambo ambayo yanapaswa kujadiliwa ni Muundo wa Muungano.

SAFARI YA DIAMOND KWENDA NIGERIA KUFANYA VIDEO INGINE YAIVA-WEMA AMSINDIKIZA AIRPORT

$
0
0
Mrembo Wema Sepetu Akiwa na Baby Wake Diamond leo Asubuhi Uwanja wa Ndege wa JK , Diamond Anaelekea Nigeria Kufanya Video yake mpya na Pia Kufanya Collabo Mpya na Wanaigeria pamoja na Waghana...Diamond Ameambatana na Manager Wake Babu Tale....Have a Nice Trip Brodaaa

KINANA AICHAMBUA KAMA KARANGA TUME YA WARIOBA

$
0
0
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ameikosoa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, akidai imeshindwa kuwasilisha kwa usahihi maoni yaliyotolewa na wananchi.

Alisema Tume hiyo iliyokuwa ikiongozwa na Jaji Joseph Warioba iliwasilisha maoni yaliyokuwa yakiunga mkono mlengo wake badala ya maoni halisi yaliyotolewa na Mabaraza ya Katiba.

Madai hayo mapya ya Kinana yamekuja wakati tayari Tume hiyo imevunjwa rasmi na Rais, kwa mujibu wa sheria.

“Kulikuwa na utaratibu wa kupata maoni kutoka kwenye mabaraza na kuna kata zilihojiwa, tume haijatuambia kwa sababu gani hawakuyasema wanayoyataka wao,” alisema Kinana.

Alisena kuwa kulikuwa na mabaraza 171, lakini Tume pia ilishindwa kutoa takwimu za watu wangapi walikuwa wakiunga muundo wa muungano wa serikali mbili au tatu katika mabaraza hayo.

“Majaji walisema masilahi ya nchi yapo kwenye serikali mbili na wakuu wa mikoa hali kadhalika, lakini mbona Tume hawakusema hayo?” alihoji Kinana.

Katibu Mkuu huyo alikuwa akizungumza katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na CCM Mkoa wa Dar es Salaam jana, kumpongeza Rais Jakaya Kikwete kwa hotuba aliyoitoa katika Bunge Maalumu la Katiba hivi karibuni.

Alisema chama chake kinaunga mkono mchakato wa kupata Katiba Mpya, lakini lazima wahakikishe katiba hiyo ni ya wananchi.

Hii ni mara ya pili kwa viongozi wa juu wa chama hicho kukosoa takwimu za Tume, mara ya kwanza Rais Kikwete alitilia shaka takwimu zilizomo katika ripoti ya Tume hiyo wakati akitoa hotuba yake bungeni.

Kinana alisema pamoja na kuhoji weledi wa Tume ya Warioba pia alitetea hoja ya wingi wa wajumbe wa CCM katika Bunge Maalumu la Katiba.

“Kuna watu kila siku wanalia eti wao wapo wachache na sisi tupo wengi, hii ni lugha ya ajabu kweli kweli, usiku na mchana wanakutana kujadiliana na walipoona chama kimoja kimoja hakiwezi wakaanzisha Ukawa.

“Hao wanaosema tunatumia wingi kupinga masilahi ya nchi, sasa ni masilahi gani yasiyowahusisha CCM?” alihoji Kinana huku akishangaliwa na wafuasi wa chama hicho.

ROONEY, MATA WAMUOKOA DAVID MOYES

$
0
0
MABAO mawili yaliyofungwa na straika Wayne Rooney katika ushindi wa  Manchester United wa mabao 4-1
dhidi ya Aston Villa, umempa ahueni kocha wa man United David Moyes ambaye amekuwa akiandamwa na mabango ya kufukuzwa.

Mchezo huo, uliopigwa kwenye Uwanja wa Old Trafford, maskani kwa Man United, wageni ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 13 Ashley Westwood kwa mpira wa adhabu uliokwenda moja kwa moja golini.

Kuingia kwa bao hilo, liliwaamusha Man United kwa kulisakama bao la Aston Villa na kufanikiwa kujipatia bao dakika saba baadaye kupitia kwa Rooney kwa kumalizia kichwa mpira uliopigwa na kiungo Shinji Kagawa.

Wakati Villa wakipigana kusawazisha bao hilo, Mata alididimiza matumaini yao kwa kuongeza bao la tatu katika dakika ya 57, likiwa ni bao lake la kwanza tangu ajiunga na timi hiyo akitokea Chelsea msimu huu.
Chicharito, aliyeingia kuchukua nafasi ya Rooney, alishindilia msumari wa mwisho katika jeneza la Villa katika dakika 90 na kumpa ahueni Moyes ambaye amekuwa akiandamwa na mashabiki wakimtaka kuachia ngazi kutokana na mwenendo wa mbaya wa timu hiyo.

KIGOGO IKULU AMHONGA KAJALA GARI

$
0
0
NI madai mazito! Kwamba, nyota wa muvi za Kibongo, Kajala Masanja amehongwa gari na mtu anayedaiwa kuwa ni kigogo wa Ikulu. Hii ndiyo habari ya mjini kwa sasa na  Risasi Jumamosi limeifukunyua.

Kwa mujibu wa habari hizo ambazo zipo hadi kwenye mitandao ya kijamii, hasa Instagram, Kajala alinunuliwa gari hilo aina ya Toyota Brevis lenye rangi ya bluu iliyoiva  wiki mbili zilizopita mara baada ya kutua Bongo akitokea nchini China ambako alikwenda kwa mambo yake binafsi.

TAARIFA ZINAVYODAI
Wasambaza taarifa hao walidai kuwa, kigogo huyo wa Ikulu ni yule Clement ambaye amewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi wa Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu.

“Mmeisikia hii? Kajala amenunuliwa gari na Kile (Clement), lina thamani ya shilingi milioni kumi na moja, Wema alie tu nakwambia. We ukisema cha nini wenzako wanajiuliza watakipata lini?

“Kwanza mnajua kama bifu la Wema na Kajala lilitokana na Clement? Alipoachana na Wema akatua kwa msichana anaitwa Naima, lakini akaona bado akaenda hadi kwa Kajala. Wema alipogundua ndiyo akamnunia na kuanza ushoga na Aunt Ezekiel,” msambaza habari za mjini mmoja aliliambia Risasi Jumamosi juzi.

Akaendelea: “Unajua nini? Naamini Wema alimwacha yule bwana na akurudi kwa Diamond baada ya kuona mambo yake siyo mazuri, lakini sasa jamaa (kigogo wa Ikulu) mambo ni safi kwa hiyo anataka kumwoneshea Wema ndiyo maana ameamua kumnunulia gari Kajala baada ya kuwa naye.”

RISASI LALISAKA MITAANI  
Baada ya kuzinyaka habari hizo za kimjini, timu ya waandishi wa Risasi Jumamosi, Jumatano iliyopita iliingia mitaani kulisaka gari hilo hasa baada ya Kajala kutopokea simu.

Awali, mtoa habari mmoja alisema Kajala yupo na gari hilo Kinondoni kwa Manyanya, lakini alipofuatwa hapo hakuonekana.
Habari zikapatikana kwamba, alikuwa kwenye Mgahawa wa Steers uliopo jengo la Millennium Tower, lakini pia alipofuatwa eneo hilo hakuonekana.

ALHAMISI SAA 9:06 ALASIRI
Juzi, saa 9:06 alasiri, Kajala alipigiwa simu ambapo alipokea na mahojiano yakawa hivi:
Risasi: Mambo Kajala?
Kajala: Poa tu, mambo?

Risasi: Mambo poa. Eti, namba za gari lako Toyota  Brevis ni ngapi?
Kajala: Mh! Yaani hata mimi mwenyewe sizijui, sijazishika kabisa.
Risasi: Sasa, kuna habari kwamba hilo gari umenunuliwa na Clement, yule aliyekuwa na Wema zamani. Kuna ukweli wowote?

Kajala: Mh! Hizo habari si za kweli. Wapo watu wanajiita Team Wema ndiyo wameamua kunipakazia hivyo, wameandika hadi kwenye Instagram, lakini siyo kweli kabisa.

“Mimi nimelinunua hili gari kwa mtu. Aliniuzia kwa shilingi milioni kumi na moja (11,000,000). Sijahongwa wala sijanunuliwa. Kuna watu wanataka kunichafua tu.

KUHUSU USHOGA WAO KUFA
Kuhusu kufa kwa ushoga wao, awali Kajala hakutaka kulizungumzia suala hilo lakini alipobanwa alidai hana tatizo na Wema na kwamba kwa sasa yuko bize kutengeneza filamu zake.

WEMA AKWEPA SIMU
Kwa upande wake, Wema alipopigiwa simu hakupokea lakini siku za nyuma aliwahi kuanika kwamba haamini kama Kajala anaweza kutembea na Clement. Hapo ni wakati ule wakiwa mashoga.

TUJIKUMBUSHE
Katika gazeti la Ijumaa, Machi 21, mwaka huu ukurasa wa mbele kulikuwa na habari ndogo yenye kichwa;

WEMA, KAJALA KIMENUKA!
Katika habari hiyo, ilidaiwa kuwa, wawili hao si mashoga tena huku sababu mbalimbali zikianikwa.
Ilidaiwa kuwa, kisa kilianzia kwenye saluni moja Kinondoni, Dar ambapo Kajala alifika akiendesha baiskeli iliyosababisha kuloa jasho sehemu kubwa ya mwili.

Chanzo kilisema, Wema alipomuona Kajala alitaka kumkumbatia lakini Kajala alimkwepa kwa sababu alikuwa na jasho jambo lililomfedhehesha Wema na kununa.
“Alichokifanya Wema, alimrushia Kajala maneno makali akimhoji kwa nini alimfanyia hivyo wakati hawana tatizo lolote kati yao,” kilidai chanzo.

Siku nyingine ilidaiwa kwamba Kajala alikwenda nyumbani kwa Wema, Kijitonyama  kwa lengo la kumchukua waende location (sehemu ya kurekodia sinema), lakini alipofika aliambiwa ‘bimkubwa’ huyo alilala na Diamond hawezi kuamshwa.

Chanzo hicho kilisema Kajala aliwasiliana na Wema kwa njia ya simu ya mkononi akamwambia asubiri lakini alikaa kwa muda mrefu bila mafanikio hivyo hawakwenda kushuti siku hiyo.

Chanzo hicho kilidai pia kwamba ushosti wa wawili hao ulianza kupepesuka muda mrefu lakini uzi wa mwisho umekuja kukatwa na Diamond mara baada ya kurudiana na Wema.
GPL

WAKOREA WAAGIZWA KUNYOA KIDUKU KAMA RAISI WAO KIM

$
0
0
Wanaume Korea Kaskazini wanakabiliwa na mtihani mpya katika taifa lao; wa kunyoa nywele kwa mtindo ulioamuliwa na rais wao.

Watake, wasitake kuanzia sasa kila mwanamume atalazimika kunyoa nywele zake kwa mtindo anaoupenda Rais Kim Jong- un.

Kiongozi huyo kijana, aliyerithi wadhifa huo baada ya kifo cha baba yake, hana mzaha hasa kutokana na nia yake ya kujenga mfumo mpya wa utawala ambao matakwa yake tu ndiyo ya kufuatwa.

Ni wiki mbili sasa tangu serikali ya nchi hiyo kutoa agizo linalowataka wanaume kunyoa kama rais wao, huku wanawake nao wakielekezwa kutengeneza nywele zao kwa aina 18 tofauti na si zaidi ya hapo.

Hilo ni moja ya maagizo yenye utata kuwahi kutolewa chini ya utawala wake, ambapo amekuwa akifanya jitihada za kujijengea mizizi, ikiwamo kuwaondoa na kuwaadhibu wale waliokuwa katika utawala wa baba yake wanaoonekana kutokubaliana na aina yake ya uongozi.

INSTAGRAM KUNA MAMBO ETI HUYU NDIO DEMU MWINGINE ANAYETOKA NA DIAMOND

$
0
0
Kwamujibu wa TeamUkwelinaUwazi instagram.... Nanukuu....
Umbea wa mjini ambao unajulikana Dar nzima na kwa watu wa karibu wa dangote na madame ila kuna watu ambao hawaujui Pia nimeona niwajuze na nyie ambao hamjaupata .. Huyu ndio demu anaetoka na dangote tena alikua ni demu wa mtu wa karibu yake kama mnamjua Prezi Tito.. Huyo prez Tito na alikua best. Sana na petitman ila kwa sasa naona urafiki umeyumba sababu Ya hii ishu .. Demu anaitwa latifa almaarufu kama Latifah Tito .. Sasa dangote hapo ndio anapomalizia stress Za jiji na madame anajua hilo yaani sio Siri demu yupo na sangote kwenye starehe zote mara kwa mara utawaona skylite pamoja na group la akina sheta.. Amefikia hatua hadi kapangiwa na dangote kinondoni kwa manyanya pale wanapouza baiskel.. Prezitito hana sauti maana na yeye ni Mario kama alivyo petitman si unajua tena hawa Mario hua hawanaga kitu basi hata sauti hawana wanaishiaga kulalamika chini kwa chini .. Basi sasa hiyo ndio ishu inayoendelea mjin hata madame analijua hilo ila ndio atafanya nini maana Latifah mbabe balaa hahaha chezaea Halima kimwana wewe harafu mnamtukana Halima nyooo hamjui kama ndio tulizo la dangote kwani dangote si anajua kabisa kua Halima na wema haziendani harafu si wema ndio ubavu wa dangote plus kwani dangote na Halima wameshare tumbo moja lakini hamjiulizi kwanini bado dangote hatengenezi njia hawa watu wakaelewana ndio kwanza yupo na Halima wake kipenzi .. Mwenyewe anakwambia salamu zangu Za pili ziende kwa dada yangu Halima mwambieni nampenda sana.. Halima ana nguvu kuliko madameeeee... Sisi bado tunangojea movie .... Oopszion haha madame eti anasema Latifah mbaya hamuingiii haya basi amuuluze dangote kamfatia nini huyo latifah ???? Harafu walikuaga wanaelewana sana dah huyu dangote anapenda vya karibu kama Clement vile..........Ufafanuzi:Dangote- Diamond, Madame-Wemasepatu
Teamukwelina uwazi mara nyingi huwahawakosei
credit : swahilitz 


SHUKA CHINI KUTOA MAONI YAKO

LULU ASHAMBULIWA INSTAGRAM KWA KUCOPY NA KUPASTE KUTOKA KWA RIHANNA

$
0
0
Masaa machache tu baada ya lulu kupost mwonekano wa mbele wa jarida la VIBE utavyoonekana,  Watu wengi wameanza kumshambulia kwa kuiga pozi la Rihana alilotumia katika Jarida GQ mwaka jana. WEngi wamelalamika na kusema kua amejishusha sana na uchafua sifa ya gazei hilo kwa kucopy na kupaste.

Baada ya taarifa hizo kumfikia lulu alikua na haya ya kusema. "Doh naona imekuwa TOPIC ila sishangai Nina hiyo damu ya kufanya kitu na kikawa gumzoooo...!nadhani kitu kimoja watu hamuelewi Ku Copy na Ku Paste huko mnakosema nyinyi cdhani Kama mnakuelewa...!hapa kilichofanana ni idea only not otherwise...!n ofcoz dunia tunayoishi hakuna kitu kipya ni vitu vile vile ila vinafanyika kwa namna ya tofauti....majadiliano hayakuwa mabaya coz ndo inamaanisha habari imefika vilivyo....nimejaribu kuiweka clear mana watu mpk vidole vinakaribia kupata sugu kwa kuandika comment hehehe...!tuachane na hayo ila dada @badgalriri dah nimekukimbiza kwa mbali heheheh.... @badgalriri @badgalriri @badgalriri @badgalriri @badgalriri @badgalriri ��������nione basi������....haya namalizia Kama bdo hutaki kukubaliana na maelezo yangu njia hii apa������������������������������������������������������������������Haina mafuriko,madimbwi wala foleni....kweupeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!��Nawapenda lkn��"

MWANAUME UKITAKA KUWEKA HESHIMA KWA MPENZI WAKO FANYA HAYA

$
0
0
Mwanaume acha kucheka cheka hovyo na upuuzi ukiwa mjini MKEO ATAKUWA ANAPAKULIWA HOVYO...haya fuata haya UTAONA MAPENZI yatakavyo nyooka...wanawake viumbe vilivyoumbwa kwa kudanganya danganywa...so do this steps wala usiongee maneno...then rudi hapa utoe ushuhuda...
1: Kama una bastola na mkeo au mpenzi wako
humwelewi...akiwa yuko home...ww chukua uwe
unaiosha osha...huku unaiandaa vizuri akiwa
anaona...usiongee sana nae...
..2.. kama huna bastola..chukua hata PANGA...noa
vizuriiii...paka mafuta huku unaicheki...huku ukipita
pita karibu yake...na weka somewhere kabatini...

..3..Basi kama huna panga...noa vizuriiii kisuu na
kiandae huku akiona na unapita pita karibu yake
USIONGEE KITU...akikusemesha ww mwambie
kilikuwa BUTU...usijibu sana...ila usicheke cheke

....HUKU UNAIMBA KIFOO KIFOO...kifoo...kifooo ..oooh kifo hakina huruma....

...Mwanaume usiongee sana kwani ushajua message
sent....then mwonyeshe dalili kuwa ana kucheat...ila
...usimwambie...ww tulia tu...utaona mabadiliko makubwa ajabu...atanyooka...

...mwanaume acha kucheka cheka hovyo au kusema
hovyo na mkeo atakuzunguka..

MUST WATCH VIDEO:THE FABULOUS LIFE OF JAY Z AND BEYONCE

$
0
0
Jay Z and Beyonce are one of world's richest and most talented couples. Their net worth is estimated to be about $775 million. With that kind of money, you can live..not exist...but live! Lol.

When it comes to gifts, Beyoncé and Jay Z only buy the best of the best. By the time their daughter Blue Ivy was 2 days old, she had already amassed a collection of baby gear worth $1.5 million. For Beyoncé's 25th birthday, Jay got her a vintage Rolls Royce for a cool million bucks. Bey returned the favor and got him a $2 million Bugatti Veyron Sport, one of the most expensive cars in the world.

Beyoncé and Jay Z have exceptional taste and always look amazing from head to toe. From Bey's wig collection worth $1 million, to Jay's $2500 custom sneakers covered in nine animals skins and $4000 custom Tom Ford suits, these two truly are style icons.

When the King and Queen of Hip Hop need some R & R, they head to some of the most luxurious locales in the world. Dropping $20,000 a night for a Penthouse in Paris and $400,000 for a mansion in the Hamptons. Together, Beyoncé and Jay Z are the highest earning celeb couple in the world and have no qualms about spending a ton of cash on whatever they want! Check their fab life after the cut

COLONEL MUSTAPHA OPENS UP ABOUT HAVING SE'X WITH HUDDAH

$
0
0
I don't usually listen to 1Fm in the morning. I actually like a lot less noise from the radio. i don't like all the shouting and hooting that takes place. But I am sure now that Lulu Saida has found her voice, she will take charge of the show -and she has already begun to show some promising signs that she is coming up from under the noisey shadow.

That said, today's topic was a very interesting topic and once you could filter the noise from the fact, Saida came top asking all the right questions. She was hosting Colonel Moustapha and he was put under the third degree by a very able interviewer who like a piranha caught scent of blood and homed in.

The most interesting question that was asked was how Colonel Moustapha would rate sleeping with Huddah. how was the experience. Colonel Moustapha got cagy. He feigned and dipped from the question and at some point it seemed like he was going to be let off the hook but Saida stuck to her guns.

And he eventually answered thus, "Yuko tu. Siezi sema nini ama nini, yuko tu."

So she isn't all that plus a bag of chips Mr. Moustapha?

CHAMELEONE ANYANG'ANYWA GARI AINA YA ESCALADE KWA KUSHINDWA KULIPA KODI

$
0
0
Jose Chameleone amenyang’anywa gari yake aina ya Escalade na maofisa wa URA baada ya mamlaka hiyo kudai kwamba msanii huyo ameshindwa kulipa kodi yenye thamani ya shilingi milioni saba ya Uganda.
Muda mchache kabla ya kuanza kwa onyesho kubwa la Tubonge la msanii huyo, maofisa wa URA waliikamata gari yake hiyo ya kifahari.
Kwa mujibu wa mtandao wa Redpapper wa nchini Uganda,msanii huyo alijaribu kuwakatalia wasikuchukue gari lake akidai atakufa na mtu atakayeichukua lakini kauli hiyo haikufua dafu kwa mamlaka hiyo. “Hii ni gari yangu binafsi na nina haki yake, mtu yeyote akigusa Escalade yangu, nami tufe pamoja naye,” alidai Chameleone.

Hata hivyo Chameleone alidai kuwa hana tatizo lolote kulipa kodi lakini mamlaka hiyo haikutolea vigezo walivyotumia kupata jumla ya shilingi milioni 7 za Uganda ambazo ndizo pesa wanazomdai

POLICE MURDER AL SHABAAB TERRORISTS WHO KILLED 6 AND LEFT A BULLET IN BABY SATRIN'S BRAIN

$
0
0
Barely a week after the Government of President Uhuru Kenyatta and his Deputy, William Ruto, gave the shoot to kill order against Al-Shabaab terrorists and radical Muslims, it has finally yielded fruits.

This is after police in Mombasa gunned down 2 of the terrorists who attacked a church in Likoni, killing 6 people and maiming scores among them baby Satrin Osinya, who was left with a terrorist bullet embedded in his brain.

Speaking yesterday, Mombasa Police Commander, Robert Kitur, confirmed the killing, saying the terrorists were fleeing on a motorbike and were gunned down on sight just as ordered.

Kitur noted that the gunmen, who were on the motorbike, were stopped by the police but they opened fire, the police returned fire and killed 2 on the spot but one escaped with a gunshot wound.

A pistol and several rounds of ammunition, similar to the ones used to kill the six people in church, were recovered.

Mombasa County Commissioner, Nelson Marwa, said the one who escaped with gunshot wounds would be tracked down and will be killed on sight.

MASHALI AMPIGA KASEBA KWA POINTI

$
0
0
Bondia Thomas Mashali (kushoto) akikwepa konde la Japhet Kaseba, wakati wa pambano lao kuwania Ubingwa wa WBO uliofanyika kwenye ukumbi wa UBO Africa Mashali.  Sabasaba jijini Dar es Salaam. Katika pambano hilo Mashali alimshinda mpinzani wake kwa Pointi.

TOYOTA CELICA SPORT INAUZWA KWA BEI POA..CALL 0714604974

$
0
0
ABOUT 2000 TOYOTA CELICA :

Vehicle Type: Sports Car
Price: TZS 8,000,000
Negotiable: Yes
Kilometers: 130,000
Transmission: Automatic
Four Wheel Drive: No
Vehicle Current Location: In Tanzania
Import Duty is Paid: Yes
Date Listed: 29-03-2014

Its a Toyota Celica, Sport Car , Engine capacity 1800, Its in Dar es Salaam,
CONTACTS:
Location: Dar Es Salaam 
Tel: +255 (0) 714 604 974











ABOUT 2000 TOYOTA CELICA :

Vehicle Type: Sports Car
Price: TZS 8,000,000
Negotiable: Yes
Kilometers: 130,000
Transmission: Automatic
Four Wheel Drive: No
Vehicle Current Location: In Tanzania
Import Duty is Paid: Yes
Date Listed: 29-03-2014

Its a Toyota Celica, Sport Car , Engine capacity 1800, Its in Dar es Salaam,
CONTACTS:
Location: Dar Es Salaam 
Tel: +255 (0) 714 604 974
Tel: +255 (0) 655 463 056

CCM WAZIDI KULIA NA WARIOBA

$
0
0
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimezidi kuilaumu iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwa kuandika rasimu iliyojaa mawazo ya wajumbe wake waliotaka muundo wa serikali tatu.

Lawama hizo zilitolewa jana na Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana, katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Mwembeyanga jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo uliandaliwa kwa lengo la kumpongeza Rais Jakaya Kikwete, kwa hotuba aliyoitoa bungeni Machi 21, ambapo Kinana alisema tume hiyo iliyokuwa chini ya kada wao Jaji Joseph Warioba, haikueleza ni makundi mangapi yalitaka serikali tatu.

Kinana alisema Tume ya Mabadiliko ya Katiba walisubiri Mwalimu Julius Nyerere afe ndipo waseme serikali tatu, kwani walikuwepo enzi hizo.

“Muungwana angesema nani kasema nini wakati wa kuchukua maoni, tume haijasema katika mabaraza 171 ni mangapi yalitaka serikali tatu, ukiwauliza mara makaratasi yamepotea, hatukumbuki.

“Tusitoane meno na macho kwa ajili ya Katiba, kwani ikishatengenezwa itawekwa kabatini na viongozi wataendelea kula kuku, umaskini upo palepale, ufisadi upo palepale, alichokisema Rais Jakaya Kikwete ni tahadhari tu, yapo maisha baada ya Katiba,” alisema.

Kinana alibainisha kuwa wamepata taarifa kuwa baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalumu kutoka upinzani wamedhamiria kuvuruga vikao vya Bunge ili Katiba mpya isipatikane.

Alisema wajumbe hao wanafanya hivyo baada ya kuona hawawezi kuingiza matakwa yao, kwakuwa wingi wa wajumbe wa CCM unawatisha.

Katika hatua nyingine, Kinana alisema kuwa ziara yake ya siku nne jijini Dar es Salaam ya kukagua miradi imeonyesha namna CCM ilivyopiga hatua katika utekelezaji wa ilani.

Alisema kuhusiana na suala la maji alitembelea Ruvu Chini na Juu na kubaini kuwa ifikapo mwaka 2015 asilimia 72 ya wakazi wa Dar es Salaam watapata maji ingawa Wizara ya Maji inakabiliwa na uhaba wa fedha.

Akizungumzia masuala ya umeme, Kinana alisema anayetaka umeme wa bei nafuu ahamie kijijini, kwani gharama za umeme mijini na vijijini ni tofauti.

Kuhusu mji mpya wa Kigamboni, alisema kuwa watalizungumza suala hilo ili kulipatia ufumbuzi.

“Hatujawahi kuona mji mpya unajengwa kwa kuhamisha watu, kama serikali imeamua mbona hawakuuliza wananchi?” alihoji.

Alisema kuwa matatizo ya walimu yataendelea kutatuliwa ikiwemo serikali kuendelea kujenga nyumba za walimu na kuwapunguzia makali ya ugumu wa maisha.

Kawa upande wa tatizo la ajira, aliitaka serikali kutafuta mbinu zisizo za kawaida za kutengeneza ajira nyingi zaidi ili watu wengi waajiriwe, hasa watu wa chini kwa kutengeneza viwanda vingi.

“Watu wanaojiajiri wapewe nafasi, si mgambo kuwasumbua na kuwadai kodi zisizo na msingi, kodi ndogondogo zinasumbua watu na kupoteza muda,” alisema.

Kuhusiana na tatizo la wizi wa dawa hospitalini, Kinana alisema kuwa serikali imepata suluhisho ambapo dawa zote zitaandikwa Serikali ya Tanzania.

Kinana alisema ifike mahali matatizo yanayoikabili nchi yatatuliwe, kwani wao kazi yao ni kuisimamia serikali na kuwajibishana pale panapokosewa.

Naye Mbunge wa Ilala, Idd Zungu, alisema Bunge halikutunga sheria kandamizi kwa bodaboda na wafanyabiashara bali Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini  (Sumatra) ndio waliotunga kanuni kandamizi.

NDOTO ZA URAIS ZAMPONZA SITTA BUNGE LA KATIBA

$
0
0
MWENENDO wa Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta, umeanza kutiliwa shaka huku baadhi ya wajumbe wenzake wakidai anateswa na dhambi ya unafiki.

Sitta, ambaye aliongoza Bunge la Tisa la Jamhuri ya Muungano kwa uwezo mkubwa chini ya falsafa yake ya viwango na kasi, alichaguliwa kwa kura nyingi kuongoza Bunge la Katiba akiahidi kuendeleza falsafa hiyo.

Hata hivyo Sitta ameanza kushindwa kuitekeleza ahadi hiyo baada ya kuruhusu kufinyangwa kwa kanuni za Bunge pamoja na kufanya uteuzi wa wajumbe wa kamati ya uongozi akiwapendelea wajumbe kutoka CCM.

Tanzania Daima Jumapili limedokezwa kuwa kuyumba huko kwa Sitta kunachangiwa na ndoto zake za kutaka kuwania urais mwaka 2015, hivyo anatafuta kuungwa mkono na CCM.

Sitta anatafuta kuungwa mkono na CCM kwakuwa chama hicho mwaka 2010 mara baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu kilimtosa kuwania uspika kwa madai ni zamu ya mwanamke.

Miongoni mwa sababu zilizokuwa zikitajwa chinichini ni kuwa kiongozi huyo wakati akiwa spika aliruhusu mijadala iliyozusha makundi ndani ya chama na serikali.

Katika utawala wake Sitta, aliunda Kamati Teule ya Bunge kuchunguza zabuni iliyoipa ushindi wa kuleta mitambo ya kuzalisha umeme wa dharura Kampuni ya Richmond, iliyokuwa ikilipwa sh milioni 152 kwa siku.

Kamati teule hiyo iliyokuwa chini ya Dk. Harrison Mwakyembe, ilitoa ripoti iliyobaini kulikuwa na utata katika kuipa ushindi zabuni ya Richmond, waliodai ni ‘hewa’ na yenye mkono wa ‘bwana mkubwa’.

Kashafa hiyo ilimfanya aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, kujiuzulu baada ya kuguswa na kashfa hiyo.

Hata hivyo mchakato huo ulifungwa na Sitta, katika mazingira ya aliyekuwa Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz (CCM), aliyeguswa pia na kashfa hiyo akitaka iundwe tume huru ya majaji watatu kuchunguza sakata hilo.

Tangu hapo Sitta, amekuwa kwenye uahasama mkubwa na makada wenzake pamoja na chama ambacho kinaamini utawala wake ndio uliozalisha wapinzani wengi bungeni hivi sasa.

Kutokana na dhana hiyo, Sitta hivi sasa amekuwa akifanya mambo yanayoonekana kutafuta huruma ya chama chake ambapo pia nusuru kisimpe ridhaa ya kuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalumu, nafasi iliyokuwa ikitajwa kukaliwa na Andrew Chenge.

Miongoni mwa mambo anayoshutumiwa kuyafanya Sitta ni kuwakemea wenzake kwa ufisadi wanaoufanya wanapotoa fedha kwenye harambee na shughuli za kijamii ilhali naye amekuwa akipita makanisani kuomba huruma ya wananchi.

Sitta pia analaumiwa kwa kuruhusu uvunjwaji wa kanuni za kuliongoza Bunge kwa kuruhusu Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba awasilishe rasimu ya katiba kabla ya Rais Jakaya Kikwete.

Inadaiwa alifanya hivyo ili kumtengenezea mazingira Rais Kikwete, kujibu mapendekezo yaliyokuwamo kwenye Rasimu ya Katiba ili kuipa ahueni CCM inayopinga mfumo wa serikali tatu uliopendekezwa kwenye rasimu.

Sitta pia anadaiwa kufanya uteuzi wa wajumbe watatu kati ya watano kuingia katika kamati ya uongozi ambayo inaongozwa na wenyeviti 12 kutoka CCM.

Miongoni mwa walioteuliwa kwenye kamati hiyo ni Profesa Ibrahim Lipumba, ambaye alikataa uteuzi huo huku akimlaumu Sitta kwa kufanya uteuzi unaoangalia zaidi masilahi ya chama chake kuliko taifa.

Baadhi ya wajumbe hususan wapinzani wanadai Sitta anayumbishwa na Chama chake Cha Mapinduzi (CCM), hivyo kufikia hatua ya kuzivunja kanuni za Bunge na kuibua mivutano.

Udhaifu wa Sitta

Baadhi ya wajumbe wa upinzani wanasema tabia ya kutokuwa na msimamo aliyoanza kuionyesha Sitta hivi sasa kwa kufuata matakwa ya chama chake bila kujali uzito wa hoja husika kumemvunjia heshima.

Hoja yao ni kuwa falsafa ya ‘Kasi na Viwango’ aliyoitangaza ameshindwa kuionyesha katika Bunge Maalumu kiasi cha kuyumbisha mchakato wa mijadala bungeni.

Pia ndani ya CCM, Sitta anatazamika kwa sura mbili. Mosi, washindani wake kisiasa wanadai anaongoza Bunge hilo kwa kuwasikiliza zaidi wapinzani ili kujijengea uhalali wa kugombea urais 2015.

Kundi la wafuasi wake, lenyewe linaona kama Sitta yuko imara kusimamia mchakato wa Katiba isipokuwa anakwazwa na mahasimu wake ndani ya chama wanaomuundia zengwe aonekane dhaifu.

Kangi Lugola (CCM), alikuwa wa kwanza kumtahadharisha Sitta kuhusiana na uongozi wake, akisema nafasi yake ni sawa na Jaji wa Mahakama Kuu aliyepelekewa mtuhumiwa wa mauaji amhukumu.

“Sitta ndiye amepewa jukumu la kuhakikisha anasimamia mchakato huu ili wananchi wapate Katiba mpya na nzuri, kushindwa kufanya hivyo wananchi wataondoa imani kwake na chama,” alisema Lugola ambaye pia ni Mbunge wa Mwibara.

Lugola aliongeza kwamba licha ya CCM kuwa na wajumbe wengi katika Bunge hilo lakini Sitta alichaguliwa kwa kuaminiwa kutokana na utashi wake wa kisiasa, hivyo anapaswa kutumia busara.

Naye Godbless Lema (CHADEMA) alimtaka Sitta kuwa makini na kila iana ya ushauri anaopewa na wenzake ndani ya CCM, kwamba mwingine una lengo la kumchafulia rekodi yake.

Lema ambaye pia ni Mbunge wa Arusha Mjini, alisema kuwa wabaya wa Sitta wamekuwa wakijidai kumshauri hata mambo ambayo baadaye yanaleta matatizo kwa lengo la kutaka kuonyesha kuwa alishindwa kusimamia mchakato wa kuandika katiba.

“Wako wabaya wako wanataka mchakato huo usifanikiwe ili ionekane ulishindwa kusimamia wananchi wapate katiba, hivyo waseme haufai hata kugombea urais,” alisema Lema bungeni.

Naye  John Shibuda, anasema Sitta anatafunwa na dhambi ya unafiki wake ambao hauwezi kumfikisha katika anachokifikiria.

Shibuda alisema Sitta amejikuta wakati mwingine akifanya uamuzi wa kuibeba CCM ili kujinafikisha aonekane ni kada mwaminifu na wakati huo huo anataka kujijengea ushujaa ili katiba mpya ipatikane, atumie turufu hiyo kujipigia debe la urais 2015.

Wiki iliyopita Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, alisema Sitta ni dhaifu na ndiyo maana anashindwa kuongoza Bunge Maalumu la Katiba kwa sababu ya kuegemea zaidi kwenye chama chake.

Dk. Slaa alisema uongozi wa Sitta bungeni utasababisha mivurugano mikubwa na kutoelewana baina ya wajumbe waliopewa jukumu la kuandika Katiba inayopendekezwa, ambayo itakwenda kupigiwa kura ya maoni na wananchi.

Sitta amekuwa akilalamikiwa na baadhi ya wajumbe tangu siku ya kwanza alipokalia kiti hicho kuwa anavunja kanuni alizotamba kuzisimamia kwa kasi na viwango.

PIGO TAKATIFU LAIKUMBA YANGA....KAMA CHELSEA VILE

$
0
0
KAMA ilivyokuwa kwa Chelsea katika Ligi Kuu ya England juzi kwa kufungwa na kutibuliwa mbio za kuwania taji la nchi hiyo, Yanga jana ilipata pigo kama hilo kutoka kwa Mgambo JKT ya Tanga.

Wakati Chelsea ikilala kwa bao 1-0 kutoka kwa Crystal Palace na kocha wake mbwatukaji, Jose Mourinho akikiri mbio za ubingwa zimekwisha, mabingwa watetezi wa Bara, Yanga jana walichapwa mabao 2-1 na timu hiyo ya Kabuku wilayani Handeni na kuwapa pigo kubwa katika mbio za ubingwa.

Kwa matokeo hayo, Yanga imebakiwa na pointi 46 katika nafasi ya pili huku timu waliyokuwa wakibanana nayo, Azam FC imefikisha pointi 53 baada ya jana kuishinda Simba kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Yanga sasa imebakiwa na mechi nne dhidi ya JKT Ruvu, Kagera Sugar, JKT Oljoro na Simba, ambazo kama ikishinda zote, itafikisha 58 wakati Azam FC imebakiza mechi tatu dhidi ya Ruvu Shooting, Mbeya City na JKT Ruvu ambazo ikishinda zote, itafikisha pointi 62 na kutawazwa bingwa msimu wa 2013/14.

Kwa Yanga, matokeo ya jana kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, ni pigo kubwa kwao kwani sasa inabidi waiombee dua mbaya Azam FC na yenyewe ikihitaji kushinda mechi zilizobaki ili itetee ubingwa.

Mgambo JKT ilikuwa ya kwanza kuandika bao katika dakika ya pili tu lililofungwa na Fully Maganga, ambalo lilidumu hadi mapumziko.

Iliwachukua Yanga dakika nane za kipindi cha pili kusawazisha kwa penalti iliyokwamishwa wavuni na nahodha Nadir Haroub.

Bao lililoipa pigo Yanga lilifungwa kwa penalti katika dakika ya 65 baada ya mwamuzi Alex Mahagi wa Mwanza kuamuru pigo hilo la adhabu kubwa kutokana na beki Kelvin Yondani kumfanyia madhambi Malimi Busungu akielekea kufunga.

Busungu alipiga penalti hiyo na kumfunga kipa Juma Kaseja, na kuandika bao la pili ambalo licha ya juhudi kubwa za Yanga kutaka kusawazisha, hali haikuwa rahisi na hivyo Mgambo JKT kuandika ushindi wake wa pili mkubwa msimu huu, kwani kwenye uwanja huo, waliifunga Simba kwa bao 1-0.
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images