Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104694 articles
Browse latest View live

Picha za Zari Hassan Akijiachia Kuonyesha Ujauzito Wake

$
0
0
Mpenzi wa Diamond Platnumz, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ akijiachia kuonyesha mimba yake, wanatarajia kupata mtoto wa pili na mpenzi wake mkali wa wimbo ‘Kidogo’, Diamond Platnumz





Tanzia:Rais wa Zamani wa Zanzibar Aboud Jumbe Mwinyi Afariki Dunia

$
0
0

ALIYEKUWA rais wa pili wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kati ya tarehe 7 Aprili 1972 hadi 30 Januari 1984, Aboud Jumbe Mwinyi amefariki dunia mchana wa leo nyumbani kwake Kigamboni, jijini Dar es Saalam baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Kifo cha mwanasiasa huyo mkongwe kimethibitishwa na mmoja wa wanafamilia ya marehemu.

Marehemu Jumbe atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa wa kuiongoza serikali ya mapinduzi ya Zanzibar akichukua nafasi ya aliyekuwa rais wa nchi hiyo marehemu Abeid Aman Karume aliyefariki mwaka 1972.

Enzi za uhai wake akiwa rais wa serikali ya mapinduzi Zanzibar alishirikiana na rais wa wakati huo wa Tanzania na mwenyekiti wa chama cha TANU marehemu Julius Nyerere kuanzisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuvunja vyama vya TANU na ASP na kuunda chama kimoja cha CCM.

Olimpiki: Brazil Yaingia Nusu Fainali Kwenye Soka la Wanaume

$
0
0
Timu ya soka ya wanaume ya Brazil, imeingia nusu fainali ya michuano ya Olimpiki baada ya kuwachapa Colombia, 2-0.

Goli la kwanza lilifungwa na mchezaji wa Barcelona, Neymar baada ya kupiga free-kick dakika 12 tu baada ya mchezo kuanza na Luan kuongeza la pili kipindi cha pili.

Brazil sasa itakipiga na Honduras Jumatano kwenye nusu fainali baada ya kuwachapa Korea Kusini, 1-0. Ujerumani itavana na Nigeria waliowafunga Denmark 2-0 na Ujerumani kuwafunga Ureno 4-0.

Spika wa Bunge Job Ndugai afunguka, aahidi kukaa na Ukawa

$
0
0
Akijibu Maswali yamoja kwa moja ya Mwandishi wa habari, Spika wa Tanzania Job Ndugai, amesema anasikitishwa na Wabunge wa UKAWA na Tabia yao ya kutoka Nje. Japo ni haki yao kutoka nje lakini hivi karibuni imezidi. Japo itaendelea hivi tutakuwa hatujengi nchi amesema.

Ameahidi yeye mwenyekiti wa Bunge na naibu Spika watakaa na UKAWA wamalize hili tatizo kwani haipendezi spika unakaa mtu anatoka nje.

Amesema Sasa Nchi hii Migogoro, utengano umezidi, ni jukumu letu kama Viongozi kumaliza hii hali.

Kasema Wabunge waliofungiwa ilitokana na matomeo ya sintofahamu. Kwani kabla ya kufungiwa tunaomba Mbunge afute kauli yake, arekebishe au alete ushahidi. Pale anapokaidi huitwa kutoa ushahidi lakini saa nyingine hukataa. Mfano kuna Mbunge alisema polisi wameleta Magari ya Washawasha 700. Tulipomwambia alete ushahidi akasema alisoma Kwenye JamiiForums. Kama bunge hatuwezi fanya kazi kwa kutengemea Mitandao

Anasema hii hali inayoendelea bungeni inachochea chuki na Migogoro. Ni bora sasa tukaa nchini kama taifa ili tumalize hii hali.

Anasema kama Spika hatavumilia vijembe na kejeli kuendelea Bungeni
Ni haki ya mbunge kutoka nje. Lakini wale waliobaki nao wanawashambulia waliotoka, hili nalo ni tatizo. Wabunge wakitoka nje mambo mengi huharibika. Inachafua hali ya hewa. Uchaguzi unapoisha, siasa huhamia Bungeni.

Tunachukulia Mbunge kama mtu mzima. Chama tawala na UKAWA na sisi tukae chini tuongelee hili swala.

Wabunge wamezoea kuona Spika na Naibu wake wakiwa wabunge wa kuchaguliwa, hii ya naibu Spika kuwa wa kuteuliwa wanahofu kwamba atakuwa anapokea maelekezo kutoka Sehemu Fulani. Naomba niwahakikishie kwamba, sisi hatupokei maelekezo kutoka sehemu yoyote bali tunatoa maamuzi yetu tunavyoona inafaa. Hivo watuamini.

Maneno ya Zitto Kabwe Baada ya Msiba wa Mzee Aboud Jumbe "Nchi Hii Wakubwa Wakigombana Huwa Hawasameheani?

$
0
0
Mzee Aboud Jumbe Mwinyi, Makamu wa Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ametangulia mbele ya Haki. Inna lillah waina ilaih raajiun.

Mzee Jumbe atakumbukwa katika historia ya Tanzania Kama Kiongozi aliyeamini na kusimamia anachoamini bila kujali madhara yake. Alipoteza nafasi zake za Uongozi Kwa sababu ya msimamo wake kuhusu muundo wa Muungano kutoka Serikali 2 kwenda Serikali 3.
Mzee Jumbe ameacha maandiko kupitia kitabu chake cha The Partnership ambacho ndugu yetu Ali Ally Saleh ' Alberto ' alipata heshima ya kukifasiri.

Pia Mzee Jumbe ameacha ' memoir ' yake ambayo ninaamini walioachiwa sasa wataweza kuitoa ili dunia ipate kujua mengi ambayo labda hatujui kuhusu Nchi yetu.

Hivi hapa Tanzania kuna Hata barabara yenye jina la Aboud Jumbe Mwinyi? Daraja? Nchi hii wakubwa wakigombana huwa hawasameheani?

Wazanzibari wanaweza kutumia msiba wa Mzee Jumbe kujenga maridhiano na kuanza kujenga Zanzibar kwa pamoja?

Watu 30 Wauawa Kinyama Mashariki mwa Congo DRC

$
0
0
Ripoti kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC zinasema kuwa wanajeshi wamepata miili ya takriban raia 30 waliouawa katika shambulizi mashariki mwa taifa hilo.
Msemaji wa jeshi Mark Azuray ameambia shirika la habari la AFP kuwa mauaji hayo yalitokea katika mji wa Beni nyakati za usiku.
Wanajeshi wanashuku kuwa kundi la wanamgambo la ADF lilitekeleza mauaji hayo.
ADF ni kundi la kujihami lililo na asili yake nchini Uganda, na linaendeleza shughuli zake karibu na mpaka.

Video 'Yaonyesha Wasichana wa Chibok Waliotoweka'

$
0
0
Kundi la kigaidi la Boko Haram limetoa kanda ya video, wanayodai inaonyesha wasichana waliotekwa nyara katika eneo la Chibok miaka miwili iliyopita.

Video hiyo, inamuonyesha mwanamume mmoja aliyejifunika uso wake, akiwa amejihami kwa silaha, akizungumza na kundi la wanawake takriban 50.
Wote wamevalia mavazi ya kidini.

Mmoja wa wanawake hao anajitambulisha kuwa, Madia na kusema kuwa anatoka Chibok.
Anasema wenzake kadhaa wamejeruhiwa vibaya kutokana na mashambulizi ya angani ya wanajeshi wa Nigeria.

Anatoa wito kwa serikali kuwaachilia wanachama wa Boko Haram, ili wasichana hao waachiliwe huru.

Inaonekana kuwa Boko Haram inatumia video hiyo kuwafanya raia wa Nigeria kuwahurumia wasichana hao, na kuilazimu serikali kutimiza matakwa yao.
Serikali ya Nigeria haijasema lolote kuhusiana na video hiyo.

Uchaguzi Mkuu wa 2015 Ulikuwa Mgumu Sana Kwa CCM - Mangula

$
0
0
Kauli hiyo imetolewa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho upande wa Bara Philip Mangula wakati akizindua Daftari la Mashina ya chama hicho ambayo ndiyo chimbuko la wanachama wake kwa lengo la kuimarisha chama hicho na kuongeza wanachama.

Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika katika kijiji cha Utiga kata na halmashauli ya Wang'ing'ombe mkoani Njombe Mangula amesema kuwa uchaguzi huo ulikuwa wa tofauti na miaka mingine ingawa kwa sasa ukirudiwa utakuwa rahisi.
Katika wilaya ya Wang'ing'ombe chama hicho kinadai wa kuongoza kuwa na wanachama wengi na kupata madiwani wote wa CCM na kuwa sasa kinazindua kitabu hicho ili kuimarika zaidi.

Kitabu hicho kinazinduliwa pamoja na shina la chama hicho huku vitabu hivyo vikigawiwa kwa mabarozi 125 na viongozi wa kata 24 na wanachama lukuki wakijiunga na chama hicho na kukabidhiwa kadi za chama hicho na Mangula.

Nisha:Sijawahi Kutembea Kimapenzi na Baraka Da Price na Wala Sintawahi Kutoka na Staa Yoyote Hapa Bongo

$
0
0
Iliwahi kuvuma kuwa anatoka kimapenzi na msanii Baraka Da Prince, lakini muigizaji asiyeisha vituko Nisha anasema hizo ni fununu tu, ambazo hazina ukweli wowote ndani yake. “Sijawahi kutoka na huyo mtu na haitakuja kutokea, tena siyo yeye tu bali sina mpango wa kutoka na msanii yeyote hapa Bongo,” anasema kwa kujiamini Nisha.

Una neno gani kwake?

Hiki Ndicho Chanzo Cha Bifu la Vera na Huddah

$
0
0
Mrembo kutokea pande za Mombasa nchini kenya, Vera Sidika ametoa sababu ya kuwa na bifu na mlimbwende mwenzake wa nchini humo, Huddah Monroe, bifu ambalo limeteka vyombo vya habari kwa muda mrefu

Akifunguka kwenye FNL ya East Africa Tv na Radio, Vera Sidika amesema wakati yeye akiwa Mombasa, Huddah Monroe tayari alishakuwa maarufu jijini Nairobi, lakini alipoenda ingawa walianza kwa kuwa marafiki, lakini baadaye Huddah alionyesha kutopenda uwepo wa Vera jijini Nairobi, kwani alihisi anamchukulia nafasi yake kwenye kazi.

"Bifu ambayo yeye anayo ilikuwa yeye amekuwa Nairobi na tayari alishakuwa star, na mimi nikatoka Mombasa nikaja Nairobi, ikawa kama nimeingilia career yake, ikawa anaaza bifu leo, anaanza kesho sasa inachosha, sasa mi nasemaga mambo kama hayo sitaki lakini anayaleta tu", alisema Vera Sidika.
Vera aliendelea kusema kuwa kitendo hicho yeye hakipendi, hasa pale inapofikia hatua ya kuchafuana kwenye mitandao kwa kutoleana habari za uongo, akitolea mfano wa hivi karibuni wa Hudda kumtangaza kuwa yeye ni muathirika wa Ukimwi.

Kweli Penzi si Kikohozi, Shilole Amuonyesha Mpenzi Wake Mpya Kistaili....

$
0
0
Baada ya kuachana na aliyekuwa mpenzi wake Shilole aliamua kukaaa muda kabla ya kumtambulisha mpenzi mpya..Siku ya leo zimezagaa picha mbali mbali ambazo zinaonyesha Shilole na Mwanaume ajulikanaye kama Hamadai wakiwa chumbani faragha ikimaanisha wenyewe ndio wameamua zitoke mtandaoni na kuanzia sasa penzi lao si siri tena.....

Makonda Amponda Kikwete

$
0
0
PAUL Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam amesema kuwa Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli ni bora kuliko serikali ya awamu ya nne, anaandika Faki Sosi.

Makonda ambaye aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni katika utawala wa awamu ya nne chini ya Rais mstaafu Jakaya Kikwete, amesema serikali iliyopita ilikuwa na matabaka kati ya viongozi na wananchi tofauti na ilivyo sasa.

Makonda alikuwa akizungumza leo katika kipindi cha Terminal cha Clouds Fm leo alasiri.
“Serikali ya sasa inafanya kazi nzuri zaidi. Kuna tofauti kubwa kati ya ya watawala na viongozi kwa sababu kiongozi anasifa ya kuwasikiliza anaowaongoza lakini mtawala hana sifa hiyo,” amesema Makonda.

Amejinasibu kuwa Mkoa wake wa Dar es Salaam umekuwa Mkoa wa kipekee kwani viongozi wanashirikiana na wananchi moja kwa moja.

Mzee Jumbe Ausia Asizikwe Kiserikali

$
0
0
"MIMI Aboud Jumbe Mwinyi, namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunibariki kuzaliwa ndani ya Uislamu na namuomba aniruzuku kufa na kufufuliwa ndani ya Uislamu".
Hayo ni sehemu ya yaliyomo katika Wasia wa Rais Mstaafu wa wa Zanzibar Alhaj Aboud Jumbe ambaye hivi sasa ametimiza umri wa miaka 80.

Akiwa na akili timamu kabisa Mzee Jumbe ameandika wasia huo wiki hii ambao nakala zake zimesambazwa kwa watu mbalimbali likiwemo gazeti hili.
Wasia huo wenye kuashiria kutahadharisha juu ya yale yanayoweza kuja kufanywa kinyume na ridhaa yake, umekuja siku chache baada ya kifo cha Rais mwingine Mstaafu wa Zanzibar Sheikh Idris Abdul Wakil.

"Ni matumaini yangu kwamba kama Mwenye Enzi Mungu alivyonirehemu kuwa Muislamu, atanijaalia nikifa kukoshwa, kuvishwa sanda, kutiwa katika jeneza, kusaliwa na kuzikwa kwa mujibu wa sunna ya Mtume Muhammad (sa.w.)", umeagiza wasia huo uliosainiwa kwa niaba
yake na Msaidizi wake Bwana Abubakar.

Agizo hilo linahusisha pia jeneza lake kutofunikwa bendera ya Taifa au ya CCM, kuwepo na utabaka katika kubeba jeneza na ufukiaji wa kaburi.

Akiwashuhudisha Mufti wa Zanzibar, Kadhi Mkuu wa Zanzibar, Naibu Kadhi Mkuu, Mwanasheria Mkuu, Sharrif Juneid, Masheikh wengine na wanawe, Alhaj Jumbe amesisitiza kuwa kufanyiwa si ombi bali ni haki yake kama binadamu, kama Muislamu na kama Mtanzania.
Amesema haki ya uhuru wa kuabudu imeelezwa katika katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kifungu cha 19 (1) na (2).

Kwa mujibu wa mafundisho ya Uislamu mtu anapokufa ni haramu kwa ndugu au jamaa zake kuomboleza kwa nyimbo, kunyoa vipara, kuvaa vitambaa au nguo nyeusi wala kulia kupita kiasi.
Aidha, imesuniwa kuwafariji (taa'zia) wafiwa kwa muda wa siku mbili tu.
"Atta'azia marrataan" ameagiza Mtume (s.a.w) akiwa maana ya kuwafariji wafiwa ni mara (siku) mbili.

Katika wasia wake Alhaj Jumbe amesema maana ya kuumbwa mauti na uhai sababu na lengo lake ni kuwafanyia wanaadamu mtihani kupimwa miongoni mwao mwenye vitendo vizuri.
"Nikiwa hai, dhamana ya vitendo vyangu inaniangukia mimi mwenyewe, nikifa dhamana ikiwa vitendo vyema au vibaya nitakavyofanyiwa itawaangukia waandalizi, watendaji na wenye kushiriki katika vitendo hivyo", amesisitiza mzee huyo aliyekuwa pia Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akimshudisha Mwenyezi Mungu katika wasia huo amekataa maziko yake kufanywa kinyume na taratibu za Kiislamu.

"Sitaki bendi, sitaki mizinga, sitaki maombolezo wala lolote lingine lenye hata chembe ya kufuru", ameandika kwa mkazo mzee huyo.
Aidha, amewaapiza kwa kumshuhudia Mwenyezi Mungu wale watakaojaribu kufanya kinyume na anavyoagiza.

"Sitaki hivyo nikiwa hai, nitakapoondoka katika dunia Mwenye Enzi Mungu anatosheka kuwa shahidi wangu, duniani na akhera", mzee Jumbe amemaliza wasia wake alioutanguliza aya ya Qur'an isemayo "Enyi wenye kuamini, mcheni Mwenyezi Mungu vile ipasavyo waja kumcha, wala msife ila Ilhali ni miongoni mwa Waislamu. (3:101)
--
Chanzo: islamtanzania.org
webmaster@islamtanzania.org
Jamii Forums

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya Agosti 15

$
0
0

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya Agosti 15

Huu ndio Uhusiano wa Mtandao wa Shule za Feza, Uislamu na Ugaidi na Mapinduzi ya Uturuki

$
0
0
Shule za Feza zimetapakaa nchi zaidi ya 16O duniani na zinamilikiwa na mtandao unaoitwa Hizmet Movement

Hawa Hizmet Movement ni wafuasi wa Imamu wa Kituruki aishiye Marekani anyefhamika kwa jina la Fethullah Gulen
Walimu wengi wa shule hizi wametoka kwenye mtandao wa Gulen japokuwa Gulen siyo mmiliki wa shule hizo

Uhusiano wa shule hizi na uislam,

Walimu wa shule hizi wnahimiza uislamu kwenye mabweni ya shule mabapo walimu huweka mfano wa aina ya maisha anayotakiwa aishi mwanafunzi na sala
Pia zinaotoa namna ya kueneza uislamu kwa upole ili kusaidia kupunguza kuenea kwa uisilamu wa itikadi kali duniani
Hata hivyo shule hizo sio kwa ajili ya waisilamu pekee na wala haziwezi kuhesabiwa kama shule za kiislam isipokuwa kuna baadhi ya shule chache ambazo ni za Kiislam kabisa
Shule hizi zipo nchi mbalimbali duniani hasa zile zenye watu wengi wenye asili ya Uturuki kama Ujerumani, Marekani, Canada

Sifa za shule hizi
Shule hizi zimekuwa zikisifika katika nchi mbalimbali zilizopo kwa kutoa elimu bora na kuwa na kiwango kidogo cha utoro na kuhama kwa wanfunzi nchini Australia shule 17 za mtando huu zinafanya vizuri ukilinganisha na shule nyingine zianvyofanya kwenye masomo

Mtando huu wa hizi shule una agenda ya siri?
Serikali nyingi na wasomi wamekuwa wakihisi shule hizi kuwa na agenda zaidi ya kutoa elimu, Profesa wa Kituruki chuo kikuu cha Utah huko Marekani alidai shule hizi na mtandao unaozimiliki zina lengo la kisiasa, lengo hilo ni kuzalisha kikundi cha watu ambao watageuza Uturuki kuwa kituo kikuu cha dini ya Uisilamu duniani, kugeuza nchi hiyo kuwa ya kiislam na kwa sasa ndio kikundi chenye nguvu zaidi Uturuki na hakina mpinzani wa kushindana nacho

Chama kimoja cha siasa nchini Georgia kilipinga kufunguliwa kwa shule hizo Georgia kwa kuwa walikuwa na lengo la kutawalisha utamaduni wa Kituruki na dini nchini kwao na kwenye mfumo wa elimu wa nchi yao

Je kwa nini shule hizi zinahusishwa na Ugaidi?
Kumekuwa na uhimizo kutoka serikali ya Uturuki kwa nchi za Afrika kama Tanzania {walishakuja mwaka 2o13 mara ya kwanza}, Nigeria, Kenya Uganda kufunga shule hizi kwa madai ya kuwa zina jihusisha na ugaidi,

serikali nyingi zimekataa kufunga shule hizo zikidai ni mambo yao ya ndani lakini kuna baadhi ya mataifa yenye kutegemea sana Uturuki yameshazifunga, Mataifa hayo ni Somalia, Kazakhstan Uzbekistan na Tajikistan zimesha funga shule hizo tangia mwaka 2O12 kutokana na aliyekuwa wairi mkuu wa Uturuki ambaye pia sasa ndie rais Recep Tayyip Erdogan kuwataka wazifunge.
Mataifa kama Iran, Syria na Saudi Arabia hayaruhusu kabisa kufunguliwa kwa shule hizi nchini kwao

Kutakiwa kufungwa kwa shule hizi sababu sio za kigaidi bali ni za kisiasa zaidi, Yadiwa aliyepo nyuma ya mtandao huu Fetullah Gulen na rais wa sasa wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan wana vita kutokana na mmoja kuonekana ana ushawishi zaidi Uturuki,

mahasimu hawa ambao walikuwa ni marafiki wa kisiasa wamekuja kuwa maadui baada ya skendo ya rushwa kukumba baraza la mawaziri la serikali ya Erdogan na mtoto wa Erdogan kuhusishwa

Rais huyu alitaka skendo hiyo ya rushwa isichunguzwe na wasikamatwe ili asichafue serikali yake lakini Imam Gulen alikuwa na ushawishi zaidi juu yake na mawaziri hao wakakamatwa, wakashtakiwa na kukutwa na hatia ambapo majaji na polisi hao walihisiwa ni ni wafuasi wa Gulen kutokana na kutosikiliza matakwa ya mkuu wao wa nchi

Kutokana na hili Erdogana akamtuhumu Gulen kutengeneza dola nyingine ndani ya dola ya Uturuki na kuanza kumuandama tangia mwaka 2O12, na kwenye uchaguzi wa mwaka 2O15 alipoteza majority ya wabunge wa serikali kwa kuwa alikuwa amekosana na Gulen

Gulen mwenye miaka 78 amekuwa na wafuasi wengi nchi Uturuki na amekuwa akihimiza uislamu usio na msimamo mkali na ameandika vitabu vingi kukemea ugaidi na amekuwa akionekana na kushambuliwa kama 'muisilamu mlaini' kutokana na msimamo wake huo,

Mapinduzi ya Uturuki yalikuwa ni mapinduzi feki
Baada ya kuona Gulen bado ana wafuasi wengi ndani ya nchi yake basi rais wa nchi hiyo akatafuta namna ya kuwakamata, rais huyo alipanga mapinduzi feki, kisha kuwasingizia wafuasi na askari wa Gulen ndio waliopanga mapinduzi hayo na akapata fursa ya kuwakamata, hadi sasa wamekamatwa watumishi wa umma zaidi ya 5o,ooo na amepanga kurudisha adhabu ya kifo kwa watu hao

Source:Jamii Forums

Ofisi za Bunge kuhamia Dodoma Septemba mwaka huu

$
0
0
Ofisi za Bunge zilizopo Jijini Dar es salaam zinatarajia kuhamishiwa Dodoma mwezi Septemba mwaka huu, ikiwa ni utekelezaji wa agiza la Rais Magufuli la kuhamishia shughuli za serikali Dodoma.

Taarifa hiyo imetolewa na Spika wa Bunge, Job Ndugai jana na kusema kuwa kwa bunge suala la luhamia Dodoma siyo gumu kwa kuwa tayari makao makuu yake yako Dodoma.

Alisema tayari alikwishatoa maagizo kwa ofisi yake kuhakikisha kuwa kufikia mwezi Septemba kila kitu kinachofanyika Dar es salaam kifanyike Dodoma isipokuwa mambo  machache.

"Nimeagiza ofisi yangu ihamie dodoma mara moja kuanzia Septemba hii, watumishi wa bunge karibu wote watahamia Dodoma, masuala ya malipo yataangaliwa baadaye, kwa sasa ni kuhamia dodoma tu, ofisi tunazo huko" Alisema Ndugai

Kama sehemu ya mwanzo wa utekelezaji wa azma hiyo, tayari ofisi ya bunge imetangaza kufanyia Dodoma vikao vyake vyote vya kamati za bunge tofauti na ilivyokuwa umepangwa mwanzo na ilivyozoeleka kufanyikia Dar es salaam.

HATIMAYE Mchekeshaji Masanja Mkandamizaji Afunga Ndoa

$
0
0
MCHEKESHAJI wa kundi la Orijino Komedi, Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’, Jana ameuaga ukapera kwa kufunga ndoa na mchumba wake wa muda mrefu aitwaye Monica.
Ndoa hiyo imefungwa katika Kanisa la Mito ya Baraka lililopo Jangwani jijini Dar es Salaam.
Miongoni mwa wageni waliohudhuria harusi huyo ni pamoja na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Dk. Tulia Ackson.

Hanscana Atemana na Wanene Entertainment

$
0
0
Muongozaji mahiri wa video nchini, Hanscana ametangaza kuacha na kampuni ya Wanene Entertainment ikiwa ni wiki chache toka wazindue studio mpya na zakisasa za kampuni hiyo.
Hanscana

Director huyo ambaye kwa sasa anafanya video nyingi za wasanii, amesema hajagombana na uongozi wa kampuni hiyo bali anaamua kuanza maisha yake binafsi.

Kupitia instagram yake alitoa taarifa hii.

Special Announcement.
Hanscana na Crew yangu nzima ya videos department HATUPO TENA WANENE ENT tangu 4Aug2016 Kwasababu .

  1. kutofautiana kimalengo baina ya HANSCANA BRAND na WANENE ENT.

Ni Juhudi kubwa sana nilizotumia kuitengenezea jina na kuitangaza NA KUIPIGANIA KAMA KITU CHANGU KABISAAA FROM ZEEEERO TO YEEAH Wanene Ent mpaka kufikia kuwa ni moja ya Kampuni kubwa ya Videos hapa E.A

  1. Nimekuwa now (23 😬)

HANSCANA nahitaji kuwa na Kampuni yangu na mimi
BUT HAKUNA UBAYA WOWOTE BAINA YANGU NA WANENE ENT. BADO NNA MAPENZI NA WANENE ENT COZ NI KITU AMBACHO NILIKIPIGANIA MWENYEWE SIWEZI KUKIONGELEA VIBAYA HATA KWA BAHATI MBAYA
Nimeamuwa kuliweka hili wazi tokana napokea simu nyingi sana toka vyombo tofaut tofauti vya habari,bloggers etc kujuwa whats happening btwn me n wanene. Na huo ndo ukweli NO MORE 🙏🏾

BASATA Yamfungulia Nay wa Mitego

$
0
0
Katikati ni katibu wa Baraza la sanaa Tanzania, BASATA, Godfrey Mungereza akizungumza na wanahabari wakati wa kutoa tamko la kumfungulia Nay. Kushoto nia msanii Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ na kulia mwenye miwani ni Meneja wake, Maneno John.

Nay wa Mitego amefunguliwa baada ya kutimiza masharti yote aliyopewa na pia kuomba msamaha kuwa hata rudia tena kufanya makosa aliyofanya.....

Una Maoni gani?

Yanga Yatupwa Nje ya Michuano ya CAF Baada ya Medeama Kuifunga TP Mazembe Usiku wa Jana

$
0
0
Wawakilishi pekee wa Tanzania kwenye michuano ya kimataifa Yanga SC, wametupwa nje kwenye Michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya TP Mazembe kuchapwa mabao 3-2 na Medeama ya Ghana katika mchezo wa kundi A uliofanyika kunako dimba la Essipong Sports huko Takoradi, Ghana.

Medeama walipata mabao yao kupitia kwa Enock Atta Agyei, Moses Amponsah Sarpong na Kwesi Donsu huku Mazembe wakipata mabao yao yote mawili kupitia kwa Jonathan Bolingi.

Kufuatia matokeo hayo, Medeama ambao mchezo wa mwisho watacheza na MO Bejaia watahitaji sare ya aina yoyote ili kufuzu hatua ya nusu fainali, wakati huo Yanga watakuwa ugenini wakikipiga na TP Mazembe mjini Lubumbashi, mchezo ambao utakuwa ni wa kukamilisha ratiba tu kwa upande wa Yanga.

Mpaka sasa, TP Mazembe bado wako kileleni na pointi zao 10 baada ya michezo mitano, wakishinda mara tatu, sare mara moja na kufungwa mara moja, wakifuatiwa kwa karibu na Medeama wenye alama nane, Bejaia wakishika nafasi ya tatu na pointi zao tano na Yanga wakiburuza mkia na pointi zao nne.

Hata kama Yanga itashinda mchezo wake wa mwisho dhidi ya Mazembe, haitasaidia chochote katika kufuzu hatua ya nusu fainali kwasababu watafikisha pointi saba wakiwa wamemaliza mechi zote wakati Medeama tayari wamefikisha pointi nane ambazo haziwezi kufikiwa na Yanga.

Mchuano mkali umebaki kati ya Medeama na Bejaia mabapo kila timu inasaka nafasi ya kuungana na Mazembe kuelekea nusu fainali huku Mazembe pia ikihitaji kushinda ili kuongoza Kundi lao la A.
Viewing all 104694 articles
Browse latest View live




Latest Images