Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104781 articles
Browse latest View live

Tundu Lissu Anavyomuelezea Marehemu Jumbe

$
0
0
Alhaj Aboud Jumbe Mwinyi amefariki dunia. Akiwa na miaka 96, Jumbe aliishi muda mrefu sana kwa kigezo chochote kile. Alikuwa mwasisi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar mara baada ya Mapinduzi ya January 1964. Alikuwa pia mwasisi wa Muungano ulioizaa Tanzania miezi michache baadae.

Baada ya Sheikh Abedi Amani Karume kuuawa mwezi April 1972, Jumbe aliteuliwa kuwa Rais wa Pili wa Zanzibar, na alishikilia madaraka hayo hadi January 1984. Wasomi wa Muungano wameandika kwamba wakati Karume anauawa mahusiano yake na Mwalimu Nyerere yalikuwa yameharibika kiasi kwamba Jumbe (kwa upande wa Zanzibar) na Bhoke Munanka (kwa upande wa Tanganyika) ndio walikuwa kiunganishi cha mawasiliano kati ya Mwalimu na Karume. Hii pengine ndio sababu Mwalimu alitumia ushawishi wake kuhakikisha Jumbe anateuliwa kumrithi Karume.

Hata hivyo, Jumbe atakumbukwa zaidi na historia kwa upinzani wake kwa mfumo wa sasa wa Muungano kuliko, pengine, kwa jambo jingine lolote. Jumbe alikuwa mwanasiasa wa kwanza, baada ya era ya Karume, kutambua kwamba muundo wa serikali mbili ulikuwa umeipokonya Zanzibar mamlaka yake na kuyahamishia Tanganyika. Alikuwa wa kwanza kutambua kwamba kuzaliwa kwa CCM, katika context ya Muungano, kulimaanisha mwisho wa mamlaka yaliyokuwa reserved kwa Zanzibar chini ya Makubaliano ya Muungano ya mwaka 1964.

Sio tu alitambua bali pia Jumbe alichukua hatua kupinga Zanzibar kupokonywa mamlaka yake hayo. Ili kufanikisha azma yake, Jumbe alilazimika kumwachisha kazi Mwanasheria Mkuu wake aliyepewa na Mwalimu Nyerere, Damian Lubuva, na kumwajiri Bashir Ebassuah Kwaw Swanzy, raia wa Ghana, kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar. Kwaw Swanzy ndiye aliyeandaa 'hati ya mashtaka' dhidi ya Muungano iliyokamatwa na watu wa usalama wa Mwalimu na baadae kutumika kumsulubu Jumbe kwenye kikao cha NEC ya CCM Dodoma January 1984.

Kwa sababu ya upinzani huo, Jumbe aling'olewa madarakani pamoja na Waziri Kiongozi wake Ramadhani Haji Faki na Mwanasheria Mkuu Kwaw Swanzy alitangazwa persona non grata na kufukuzwa nchini. Mwalimu akatangaza 'kuchafuka kwa hali ya hewa ya kisiasa' Zanzibar na waZanzibari wengi wapinzani wa Muungano, kama Mwanasheria Mkuu wa kwanza Wolfgang Dourado, kuwekwa kizuizini.

Miaka kumi baada ya kuondolewa madarakani, Alhaj Aboud Jumbe alichapisha kitabu chake juu ya Muungano, 'Miaka Thelathini ya Dhoruba', ambako aliweka bayana ugomvi wake na Mwalimu juu ya Muungano. Jumbe ni kiongozi pekee wa juu wa rika la wapigania uhuru wa Tanzania kuandika memoirs zake juu ya Tanzania na matatizo ya Muungano wake. Hata Mwalimu hakufanya hivyo na alikufa na siri zake juu ya mambo mengi makubwa yalitokea wakati wa utawala wake.

Kwangu mimi, hii ndio merit kubwa na mchango mkubwa wa Alhaj Aboud Jumbe kwa kizazi cha sasa na vijavyo vya waTanzania. Alikuwa na ujasiri wa kusema na kuandika juu ya 'The Forbidden Subject', tena katika kipindi cha Mwalimu Nyerere ambapo ujasiri wa aina hiyo ulikuwa ni jambo la hatari kubwa. Kwa sababu hiyo hiyo, Jumbe alilazimika kuishi theluthi ya mwisho ya maisha yake 'kifungoni' Mji Mwema, Kigamboni, ambako alipelekwa mara baada ya kung'olewa madarakani mwaka '84.

Sikuwahi kubahatika kuonana na Alhaj Aboud Jumbe wakati wa uhai wake. Hata hivyo, nimejifunza mengi sana kutoka kwake, hasa ujasiri wa kuuhoji Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Jumbe amekuwa na ushawishi mkubwa sana kwenye mjadala wa Muungano kwa zaidi ya miongo mitatu sasa. Ninadiriki kusema kwamba hoja ya Serikali Tatu ilianzia kwa Jumbe.

Roho, spirit, yake ilikuwa kila mahali wakati wa mchakato wa Katiba Mpya kati ya 2011 na 2014. Kivuli chake kilikuwa kila mahali wakati wa Bunge Maalum la Katiba mwaka 2014. Pengine kuliko hata Mwalimu Nyerere, Jumbe ndiye aliyetufundisha kuufahamu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Atakumbukwa kama mmoja wa waTanzania maarufu na wapigania uhuru wakubwa wa Zanzibar ya baada ya Muungano.

CHADEMA yaipigia Magoti ACT Wazalendo

$
0
0
MBOWE :-CHADEMA TUTAUNGANISHA NGUVU NA ACT WAZALENDO KUPINGA UDIKTETA.
Waswahili walisema usitukane Mamba ujavuka mto, msema huo waelekea kutimia kwa Freeman Mbowe na cdm yake kufuatia kudorora kwa mpango wao wa Ukuta sasa akimbilia kuomba msaada wa Zitto Kabwe na chama cha ACT Wazalendo.

"Hatuwezi Kukaribisha Watu Kama Mrema Au Cheyo Ambo Vyama Vyao Vimeamua Kushirikiana Na CCM, Tutazungumza Na ACT WAZALENDO Tulioshirikiana Bungeni, Wameonyesha Kuwa Wanapingana Na Udikteta Kwa Hivyo Milango Ipo Wazi Kwa Sisi Kuungana Nao (WAZALENDO) Kuunganisha Nguvu Za Vyama Vyetu"

Amenukuliwa Mbowe Na Gazeti la Citizen
Nini maoni yako? .sasa wale walo karirishwa eti Zitto Kabwe ana tumiwa na ccm, mamluki, anataka kuoa kwa kikwete. Awaaulize chadema kwa nini waliwadanganya? Maana leo zitto na ACT WAZALENDO wanaonekana wapinzani wa kweli, na sio ccm tena. Siku zote uongo huwa haudumu. Mtaendelea kuumbuka tu.

(MUNGU HAMTUPI MTU MWENYE DHAMIRA YA KWELI. HAWEZI SHINDWA WALA HAWEZI KATA TAMAA) Na bado

Taarifa za Kifo cha Sarafina si za Kweli

$
0
0
Tetesi za kifo cha muigizaji maarufu wa Afrika Kusini, Leleti Khumalo maarufu kwa jina la Sarafina si za kweli kwa mujibu wa vyombo vya habari vya nchi hiyo.

Hivi karibuni kupitia mitandao zilienea taarifa za kifo cha muigizaji huyo aliyewahi kufanya vizuri kwenye filamu ya ‘Sarafina’ amefariki dunia.

Vyombo hivyo vya habari vimeziita habari hizo kuwa ni uongo wa kupindukia. Mtandao wa wasanii nchini Afrika Kusini unaojulikana kama ‘Mzansi’ ulikanusha taarifa hizo za kifo cha Leleti na kusema ni za uongo na umewatoa hofu mashabiki waliopatwa na mshtuko baada ya kupata taarifa hizo.

Msanii huyo alifanikiwa kutembelea Tanzania mapema mwezi Julai mwaka jana kwenye tamasha la ZIFF lililofanyika visiwani Zanzibar na alialikwa kama mgeni rasmi wa tamasha hilo.

Nafasi za Kazi zilizotangazwa Leo na Makampuni Mbali Mbali Kwenye Magazeti na Mitandaoni

$
0
0

Peter Msechu Aingia 18 za AT, Achambwa Mpaka Huruma...

$
0
0
Mwimbaji AT kutoka Zanzibar amemtupia Mwimbaji Peter Msechu Maneno ya Shombo ambayo yamemwacha kila mtu mdomo wazi:

“Mvuto Sifuri Bikaka @peter_msechu Nene km Lori Hivi kuongelea wembamba wangu unalipwa sitaki shobo km lakufanya huna jikate minyama yako ujichome mishkaki usi nitekenye mdomo ukataka niongee,” ameandika AT kwenye Instagram.
“Tumbo Tumbo km Umeficha Kobe wewe nipotezee usilazimishe mimi niwe karibu na wewe sina shida ya kukuazima tumbo nende nalo harusini Mifulana km Turubali za Msimbani Babu kaa mbali na mimi kwani hivi na wewe ni msanii wanchi hii au Muuza kufia za Oliva Mtukuzi?”
“Pyuuuuuuuuuuuuu ukiona nipo kimya ujue sihitaji varangati na mtu kiki zime adimika huna utakapopatia usinione Mwembamba ingia 18 uhadithie wenzio Mr Machupi ya kushonesha.”

Wema Sepetu Amenishangaza Kwa Kauli ya "Mimi na Uzungu Wangu"

$
0
0
Jana usiku katika taarifa ya habari ya TV1, habari ikielezea uhamasishaji wa wasanii kuupa kipaumbele miziki yenye mahadhi ya uswahili kama segere na singeli nimemsikia Wema Sepetu akihojiwa na kuzungumza haya:-

"Mimi pamoja na uzungu wangu lakini huwa napenda nyimbo zenye uswahili kama hizi"

Kwa aliyeelewa vizuri hiyo kauli ya Wema ilimaanisha nini? Je Kweli Wema ni Mzungu?

Nawasilisha.

Mashabiki Watokwa na Povu Baada ya Wema Kuwataja Wanaume Anaowafagilia Akiwemo Diamond Huku Idriss Akiwa Hayupo Katika List

$
0
0

Hii ndio picha aliyoweka Wema Sepetu Kwenye page yake Kama MCM, ikiwa na maana ya Man Crash Monday...

Mashabiki wake wengi walihoji kwanini Diamond yupo kwenye list na huku mpenzi wake wa sasa Idriss hayupo katika list hiyo kitu ambacho kinazidisha tetesi kuwa wameachana...

Mashabiki wengine wameenda mbele zaidi na kudai Wema Sepetu Ameshindwa kumove on kwani bado anampenda Diamond sana..

Haya ni baadhi ya maoni kutoka kwa mashabiki:


elsie647438
Why do you act lyk a desperate b**ch @wemasepetu there's lyf afta diamond.....move on and stop forcing on zari's man.

josephinaamani
unajua kutuvuruga 🙌🙌🙌🙌🙌

juliethmkai
I think Wema is fooling herself... Btw the whole thing is funny

khassimelizabeth
@queen_platinumz INAWEZAKANA LENGO SIO HUYO DAIMOND ILA YUKO STRESSED KIASI KWAMBA KUNA SIKU ATAMPOST ZARI HUMU, KASHAPOST MAMA DAI,TIFA DIAMOND, BADO ZARI TUU SASA SIKU ANAKUJA KUANGALIA MAISHA YAKE KAFIKA WAPI INAKUA TOO LATE!!

ashurathy22
Anajua kuwatoa w2 povuuu khaaa wamemuona dai tu kwan kamikaze hajulikan jmn 🏃🏃🏃🏃

hotsalmabbyi
Watu mipovu inawatoka loooh @wemasepetu safi sanaaaaa @diamondplatnumz hebu mpost na ww wema mijitu iiumbuke huku mmemuona dai tu hao wengine nivisiki mnapenda watu wagombabe tu looh

simaluasha
Wanaume wamekuwa bidhaa adimu sanaa duniani

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumanne ya Agosti 16

$
0
0


Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumanne ya Agosti 16

Watu Watano Akiwemo Askari wa JWTZ Watiwa Mbaroni kwa tuhuma za Kutengeneza Vyeti Feki

$
0
0
POLISI mkoani Kigoma imewatia mbaroni watu watano akiwemo askari mmoja wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa tuhuma za kutengeneza vyeti bandia vya kitaaluma, miongoni mwake vikiwemo 90 vya uuguzi, ambavyo vilikutwa vikisubiri kugawiwa kwa wahusika.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Ferdinand Mtui alisema kuwa pamoja na vyeti hivyo vya uuguzi vilivyokamatwa, pia katika operesheni hiyo walikamata vyeti 37 vya wataalamu wa maabara na vyeti tisa vya ufamasia.

Alisema kuwa katika operesheni hiyo iliyofanywa kwa pamoja na maofisa kutoka Baraza la Wafamasia nchini, walikamata jumla ya vyeti 936 vikiwa kwenye hatua ya ukamilishaji vikiwa bado havijaandikwa majina, miongoni mwake vikiwemo vyeti 667 vya wauguzi wasaidizi, vyeti 126 vya wataalam wa maabara, cheti kimoja cha mafunzo ya afya ya jamii na vyeti viwili vya utoaji huduma ya kwanza.

Katika kuhakikisha wanakuwa na uthibitisho wa tuhuma hizo, Kamanda Mtui alisema kuwa pia wamekamata mihuri 25 ya taasisi mbalimbali ikiwemo nyundo mbili, ambazo hutumika kutengenezea mihuri mbalimbali ya moto.

Aliwataja watu waliokamatwa katika operesheni hiyo ambayo inahusisha mtandao wa watu mbalimbali kuwa ni askari wa JWTZ, Mgeni Nyamubozi ambaye ni mume wa mmiliki wa Duka la Vifaa vya Ofisi la Upendo, lililopo Mwanga mjini Kigoma, ambalo linatuhumiwa kuhusika na utengenezaji wa vyeti hivyo.

Katika duka hilo, Kamanda huyo wa polisi alisema polisi walikamata kompyuta mpakato moja, ikiwa na nakala za vyeti mbalimbali za vyuo na idara za serikali.

Mwingine aliyekamatwa ni Dickson Mshahili, muuguzi katika Hospitali ya Mkoa Kigoma ambaye katika upekuzi nyumbani kwake, alikutwa na nyaraka mbalimbali ikiwemo madaftari 12 yakiwa na kumbukumbu za vyeti anavyotengeneza na mihuri ya waganga wakuu wa mikoa ya Kigoma, Kagera, Mwanza, Singida na Tabora.

Sambamba nao alikamatwa Zawadi James, muuguzi wa Kituo cha Afya Ujiji ambaye baada ya kupekuliwa nyumbani kwake, alikutwa na vyeti vitatu na kabuleta ya pikipiki ambayo hutumika kutengeneza mihuri ya moto.

Wengine waliokamatwa ni Johnson Nyabuzoka, mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Mlole ya mjini Kigoma, ambaye ni mtaalam wa kompyuta aliyekuwa akitumika kufanya kazi hiyo; na Stephano Erasto ambaye alikamatwa katika siku yake ya kwanza tangu ajiunge na duka hilo kwa ajili ya kusaidia kazi.

Mateso Zanzibar ‘yamponza’ Kubenea, Ajisalimisha Polisi

$
0
0
SAED Kubenea Mbunge wa Jimbo la Ubungo amejisalimisha Kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam na kuhojiwa kabla ya kupewa dhamana kufuatia tuhuma za kuandika makala inayodaiwa kuwa ya uchochezi kuhusu hali ya kisiasa Zanzibar.

Kubenea ambaye pia Mkurugenzi wa Hali Halisi Publishers inayomiliki magazeti ya MwanaHALISI na MSETO anadaiwa kufanya uchochezi kwa kuandika makala katika gazeti la MwanaHALISI toleo la 349 la Julai 25-31 yenye kichwa cha habari, ‘Yuko wapi atakayeiokoa Zanzibar?’

Kubenea amefika katika kituo hicho cha Polisi leo saa saba na robo mchana (13:15) akiwa na Tundu Lissu Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) pamoja na Frederick Kihwelu wakili mwandamizi wa Chama hicho.

Baaada ya kuhojiwa kwa zaidi ya masaa mawili, saa tisa na robo alasiri (15:45) alitoka na kuondoka huku wandishi wa habari wakishindwa kuzungumza naye baada Jeshi la Polisi kuwazuia waandishi wa habari kuingia katika eneo la kituo hicho.

Akizungumza kwa njia ya simu, Lissu ambaye ndiye mwanasheria wa Kubenea katika sakata hilo amesema kuwa, Kubenea amehojiwa kwa madai ya uchochezi lakini alichokiandika ni hali halisi ya Zanzibar hususani visiwa vya Pemba.

“Kubenea amechiwa kwa dhamana na ameamriwa kurudi tena kituoni hapo tarehe 18 Agosti, mwaka huu,” amesema Lissu.

Katika makala yake inayodaiwa kuwa ni ya kichochezi iliyokuwa na kichwa cha habari, “Yuko wapi atakayeiokoa Zanzibar?” Kubenea alielezea jinsi Jeshi Polisi Visiwani Pemba wanadaiwa kuwabambikia kesi wananchi, kuwapiga na kuwatesa kwa madai kuwa wananchi hao wanaipinga serikali.

Kubenea aliandika Makala hiyo baada ya kusafiri kutoka Dar es Salaam Mpaka Zanzibar kufuatilia kile alichokitaja kama mateso, unyanyasaji na ukiukwaji wa haki za binadamu dhidi ya wananchi wasio na hatia visiwani humo.

Miongoni mwa vijana na wahanga wa kubambikiwa kesi, kupingwa na kuteswa visiwani Pemba waliotajwa na Kubenea katika makala yake ni ni Hijja Hassani aliyetangazwa kuwa ni Mwakilishi wa Jimbo la Kiwani kabla ya Jecha Salim Jecha Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kufuta uchaguzi.

Eneo la Ikulu Lauzwa Kinyemela

$
0
0
ENEO lililokuwa limetengwa ili ijengwe Ikulu ndogo ya Mkoa wa Mbeya limemegwa na kuuzwa. Limeuzwa kutokana na kile kinachotajwa kuwa ni maofisa wa ardhi Jiji la Mbeya, kutumia fursa ya eneo hilo kujinufaisha kwa kuuza viwanja.

Inaelezwa kuwa baadhi ya maofisa ardhi wa halmashauri ya jiji, wamepima viwanja kwenye eneo hilo wakishirikiana na wakazi ambao ilikuwa walipwe fidia kwa mashamba yao, na wakazi hao wanatumiwa kutafuta wateja wa viwanja hivyo ili ionekane wao ndiyo walioviuza kwa watu wanaojenga sasa.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla jana alitembelea eneo hilo lililopo Veta jijini Mbeya  na kujionea majengo yaliyojengwa kwenye ardhi, iliyokuwa sehemu ya uwanja wa kujengwa Ikulu ndogo ya Mkoa.

Diwani wa Kata ya Ilomba, Dickson Mwakilasa alimwambia Mkuu wa Mkoa kuwa eneo lilikojengwa nyumba za watu binafsi, lilikuwa la serikali na kilichotakiwa ni kulipa fidia kwa wakazi waliokuwa na mashamba maeneo ya jirani.

Kufuatia hali hiyo, Makalla alilazimika kuwahoji maofisa wa halmashauri ya jiji, lakini wote wakaonekana kutoijua vyema historia ya eneo hilo, hivyo ikamlazimu Mkuu huyo wa Mkoa kuahidi kufuatilia kwa haraka nyaraka husika.

Alisema anachotaka kujua ni ramani inayoonesha ukubwa wa eneo la awali; na pia matumizi yaliyopangwa, huku akisema anachojua yeye mpaka sasa ni kuwa maofisa ardhi wameuza kinyemela sehemu ya uwanja wa Ikulu ya Mkoa.

Jinsi Mwanamke Anavyoweza Kuongeza Hips na Makalio kwa Vyakula na Mazoezi

$
0
0
Miaka ya hivi karibuni kua na makalio makubwa imekua ni fasheni muhimu sana kiasi kwamba wanawake wasio na makalio makubwa wamejikuta wakipata tabu na hata kufanya upasuaji hatari ili kuongeza makalio na wengi wameharibika kabisa au kupoteza maisha kwenye oparesheni hizo hatari. lakini kama jinsi wanaume wanavyobeba vyuma na kuongeza vifua na mikono hivyohivyo wanawake wanaweza kuongeza misuli hiyo muhimu ya makalio ambayo kitaalamu inaitwa gluteal maximus, gluteal minimus na gluteal medias.

Hiyo ndio misuli mikuu mitatu ambayo kwa pamoja inaitwa makalio na ikifanyiwa mazoezi vizuri huongezeka na kua mikubwa. ni kweli ukubwa wa makalio na kiungo chochote cha mwili hufuata ukoo lakini pia mazoezi husaidia sana kukuza makalio au kiungo chochote cha mwili chenye misuli lakini sio kua makubwa tu lakini hata kuyafanya kua na shepu nzuri na kuvutia.. unaweza kua hujaamini bado lakini kwa kukuthibitishia habari hizi ni kwamba jeniffer lopez mwanamuziki na muigizaji wa filamu nchini marekani ambaye anaongoza kwa kua na makalio makubwa zaidi kuliko wasanii wote mpaka akayakatia bima yaani insurance anafanya mazoezi haya kama ifuatavyo..

1. Mazoezi ya squat;
mazoezi haya huanzwa kwa kusimama na miguu yote miwili kisha kuanza kama unakaa hewani halafu unainuka, mazoezi haya huvuta misuli ya makalio na kuibana kisha kuongeza upana na siku za kwanza za mazoezi haya mtu hujisikia maumivu na kuanza kuhisi nguo zimeanza kubana mpaka mapajani. ni zoezi kuu na muhimu katika kukuza makalio.fanya zoezi hili kwa raundi tatu kila raundi fanya mara kumi na tano au unaweza ukaanza kama picha inavyoonyesha hapo kwa mwezi mmoja kisha ukaendelea na mazoezi ya kawaida kama nilivyoelekeza.
2. Zoezi la bridge;
watu wengi wanashinda wamekaa kwenye viti  mashuleni au maofisini muda mwingi na hali hii hufanya hata mtu mwenye makalio makubwa ya kuzaliwa nayo kuanza kupoteza shepu yake nzuri ya mwanzoni. zoezi hili huanza kwa kulala chini kwa mgongo kisha inua kiuno kwa juu, sasa bakia kwa hali hii kwa muda kisha nyoosha mguu mmoja kwa mbele kwa sekunde kadhaa afu rudisha chini halafu badilisha mguu.fanya hivi kwa kila mguu mara kumi kwa raundi tatu huku ukipumzika dakika mbili kila baada ya raundi.

3. Donkey kick;
piga magoti kisha weka mikono chini kama mbuzi anavyosimama kisha inua mguu mmoja wa nyuma mpaka uangalie juu kisha rudisha chini taratibu.fanya hivi raundi tatu huku kila mguu ukiinua na kuurudisha mara 20.

4. Kula protini nyingi:
vyakula vya protini ni muhimu kujenga misuli na mifupa hivo kula sana maharage, nyama, samaki,maziwa, karanga, korosho na kadhalika. hii itakujenga haraka sana na kukupa matokeo mazuri kwani mwili unajengwa na chakula.

5. Chagua aina nzuri ya wanga;
ulaji wa mikaango kama chips, chapati, maandazi na kadhalika sio wanga nzuri kwani huleta vitambi na kukufanya ue na shepu mbaya ni vizuri kula wanga asili kama ugali,viazi,mihogo,wali na kadhalika.

6. Tumia mboga za majani; 
mboga za majani ni muhimu sana kwani husaidia chakula ulichokula kiweze kunyonywa na mwili kirahisi na kupunguza uwezekanao wa kupata kitambi.

 7. Tumia virutubisho vya kutosha;
virutubisho vyenye madini mbalimbali na protini ni muhimu sana kwani vyenyewe vinaenda moja kwa moja kufanya kazi kwenye mwili na kuanza kujenga misuli hii bila kuanza kufyonzwa taratibu tumboni kama vyakula vingine. utafiti unaonyesha wanaotumia virutubsho hivi hufanikiwa sana kuliko wasiotumia kabisa.jinsi ya kutumia; chota kijiko kimoja kilichowekwa kwenye virutubisho vyako kisha changanya na maziwa kwa upande wa protein shake na kwa upande wa argi changanya kijiko kimoja cha unga na maziwa ya mgando au juice.kunywa mara moja au mbili kwa siku huku ukiendelea na mazoezi.

Mwisho: kama ilivyokua kwa mazoezi mengine yeyote itakuchukua muda angalau wiki mbili au mwezi mmoja kuanza kuona matokeo na haimaanishi kwamba ndio matokeo mazuri yakipatikana ndio unaacha hapana, mazoezi ni muhimu kwa mwili wa binadamu, unaweza ukaanza na zoezi la mwezi yaani mara moja kwa siku kisha endelea na zoezi hili mara tano kwa wiki baada ya mwezi wa kwanza. kumbuka kama ilivyo kwa mazoezi mengine ya mwili, unahitaji moyo wa mazoezi kufanikiwa, usije ukafanya zoezi siku mbili ukaacha afu ukategemea mabadiliko..unaweza ukatutafuta kupata virutubisho hivyo, kupata video za mazoezi na kwa msaada wa kitaalamu zaidi.

Walichokusudia Kufanya Wanachama wa Yanga Leo Kuhusu Yusuph Manji Kuibwaga Yanga

$
0
0
Baada  ya taarifa za mfanyabiashara na mwenyekiti wa klabu ya Dar es Salaam Young Africans Yusuph Manji kuripotiwa kukusudia kujiuzulu wadhifa wake huo ndani ya klabu ya Yanga kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kuandamwa na maneno na baadhi ya watu huku wana Yanga wengine wakiwa kimya.

Taarifa za Manji kujitoa zinakuja kwa sababu ya kudaiwa kujihisi mpweke kwani licha ya kushambuliwa kwa maneno na baadhi ya ya watu ikiwemo wanasiasa, hakuna mwanayanga aliyekuwa pamoja nae hivyo anajihisi mpweke na ana kusudia kujiweka pembeni.

Kufuatia taarifa za Manji kukusudia kujitoa viognozi wa Yanga wa kanda zote wamekusudia kufanya kikao leo saa 4 asubuhi makao makuu ya klabu hiyo kutoa tamko la pamoja kuhusianna maamuzi ya Manji, kujitoa kwa kuona anatengwa na wanachama.

Makonda Kuwajengea BAKWATA Ofisi ya Kisasa

$
0
0
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amekabidhi ramani ya jengo la Ofisi ya Makao Makuu ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), ikiwa ni ahadi ya kuwajengea jengo hilo.

Akizungumza wakati akikabidhi ramani hiyo, Makonda alisema jengo hilo linatarajiwa kuwa na ghorofa tatu na litagharimu zaidi ya Sh bilioni tano.

“Ijumaa nitakuja hapa kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi na niseme tu ujenzi utaanza hivi karibuni na nimeshawaambia watu wangu wahakikishe jengo hilo linajengwa kwa muda usiozidi miezi 14 tu,” alisema Makonda.

Licha ya kukabidhi ramani hiyo, Makonda pia aliwataka viongozi hao wa dini kuendelea kuhubiri amani ili taifa liendelee kuwa na amani na mshikamano. Alisema ujenzi wa jengo hilo, umekuja baada ya kuona kuwa Bakwata imekuwa na mchango mkubwa kwa taifa ikiwemo kuhubiri amani na mshikamano.

“Viongozi wa dini ni watu muhimu sana wamekuwa wakituhubiria amani na pia viongozi hao wamekuwa wakituongoza katika safari ya kutupeleka kwa mola, endeleeni kudumisha na kuihubiri amani ili taifa ili liendelee kusifika,” alisema Makonda.

Kwa upande wake, Mufti wa Tanzania, Shehe Mkuu Abubakar bin Zubeir alimshukuru Makonda kwa uamuzi alioufanya; na kusema ameonesha njia kwa wadau wengine walio na wasio waislamu kujitolea kuchangia.

“Najua jamii inaweza kushangaa kwa nini nimepokea msaada kutoka kwa mtu ambaye si Muislamu, lakini niseme tu hata Mtume alipokea misaada kutoka kwa watu kama hawa, ni rai yangu kuwaombeni na ninyi Waislamu mjitokeze kuunga mkoa juhudi hizi kwa hali na mali,” alisema.

WEMA Sepetu na Idriss Sultan Wakomoana..Idriss Mapovu Yamtoka Akataa Kuitwa Shemeji

$
0
0
Hali ya hewa upande wa Wema Sepetu na Mpenzi wake Idriss Sultan inaonekana kuwa si shwari kabisa , Baada ya jana Wema Kupost Wanaume wengine anaowafagilia akiwemo Mpenzi wake wa zamani Diamond leo Idriss na yeye amepost kuwa Hataki kuitwa shemeji kuanzia sasa na pia ameongelea kwanini hakwenda kumsupport Wema Sepetu kwenye party ya Usiku wa Vigoma

Ameandika Hivi:

"Sipendi kuona watu wakiingia na kuongea kama wanajua maisha yangu na watu wangu wa karibu, makosa wakifanya wengine mnakuja kwangu mnaanza "Ndio asingefanya vile kama sio wewe kufanya hivi" mnakazana kusema eti naposti wanawake mara ooo porojo kibao. Sina freedom ya kumpost dada angu ? Kweli ? Au rafiki yangu kazindua brand mpya siwezi mpost nikampongeza ? Mnauliza kwanini sijaenda vigoma nimesema because show yangu hakuja hata moja na nimeenda show zake zote na yeye halalamiki because anajua nimesema siendi fair enough mbona hamjaongelea hilo ? I repeat nikikaa kimya is for a pure reason that its not anyones business this is my personal life kama mnaongeleaga fair basi mngefanya kuuliza kwanini mpaka am selling out hajaja. Give me a break sina maisha ya kuigiza lets have respect for each other bana. Na nimesema msiniite shemeji for one big good reason, imekua too much i am a brand na jina idris linamezwa na shem, ningejua this from the beginning nisingeruhusu mniite tangu mwanzo so msiwe kila kitu mnafikiria negative tu. Na sikua na haja ya kuandika yote haya pia 😊✌🏽️ #TusichukulianePoa"

SOMA Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Katika Magazeti na Mitandaoni Leo 16 Aug 2016

Dr. Kigwangalla Aishtukia Asasi ya Kiraia inayohamasisha Mapenzi ya Jinsia Moja...Mapya yaibuka!

$
0
0

  •  Yabainika walikuwa na mradi wa kuhamasisha mapenzi ya jinsia moja ukifadhiliwa na JHPIEGO


  • Baadhi ya watendaji wa Asasi hiyo walikuwa kwenye asasi iliyofutiwa usajili ya "Sisi kwa Sisi"

Dkt. Kigwangalla, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, wazee na watoto Na Mbunge wa Jimbo la Nzega Vijijini, Leo jioni ameendesha Operesheni Maalum ya ukaguzi wa ofisi za shirika lisilo la kiserikali la Community Health Education Services and Advocacy (CHESA), ikiwa ni muendelezo wa vita ya uhamasishaji wa vitendo Vya mapenzi ya jinsia moja ulioanza kuota mizizi nchini.

Shirika la CHESA, pamoja na Mashirika mengine (sintoyataja hapa) yanasemwa kuwa yanaendesha shughuli ambazo hayakusajiliwa kufanya, ikiwemo tuhuma za kuhamasisha watu wanaofanya mapenzi ya jinsia moja kudai haki zao kupitia miradi yao na harakati nyingine mbalimbali.

Mashaka yametanda kwenye nchi nyingi Afrika, dunia ya waarabu na nchi zenye wakristo wa Katoliki kuhusiana na marafiki zetu wanaoruhusu mambo haya kwenye sheria, mila na desturi zao kuanzisha mikakati ya kichini chini ya kusambaza pesa kwenye vikundi mbalimbali vya kijamii na asasi zisizo za kiserikali ili kuwahudumia, kuwaunga mkono, kuwaunganisha, kuwatetea, kuwalinda, kuwawezesha, na kuhamasisha jitihada za siri sana na makini za kueneza mapenzi ya jinsia moja nchini. Pia kuhalalisha kama utamaduni Mpya kwa kisingizio cha "Haki za binadamu".

Tanzania imesaini International Bill of Rights (mkataba wa kimataifa wa Haki za binadamu) lakini kwenye mkataba huo Hakuna kipengele hata kimoja kinachoelezea uwepo wa Haki zinazodaiwa na kundi hili.

"Serikali itaendesha harakati nzito za uchunguzi wa pesa zote zinazoenda kwenye NGOs Na vikundi mbalimbali na kufuatilia pesa hizo zimeenda kufanya nini kwenye jamii," alisema Dkt. Kigwangalla.

"Nimewapa agizo wataalamu kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kushirikiana na jeshi letu la polisi kufanya kazi hiyo na kuyafikisha mahakamani Mashirika yote yatakayokutwa na hatia na pia kuchukua hatua ya kuyafutia usajili mashirika yote yatakayobainika kukiuka masharti ya usajili wao kwa mujibu wa sheria. Kwa mfano, 'coincidentally', tayari shirika hili litapaswa kutoa maelezo juu ya pesa lilizopokea kutoka shirika la kimataifa la JHPIEGO kutekeleza mradi wa SAUTI, ambao kwenye taarifa zake za mwaka limezificha. Mradi wa SAUTI unahudumia watu wanaofanya mapenzi ya jinsia moja" aliendelea kusema Dkt. Kigwangalla.

Shirika la CHESA kwenye usajili wake hakuna mahali linaeleza kwenye Katiba inayolianzisha kuwa litatoa huduma hizo. Na sababu ni rahisi, kwamba lisingeweka huduma hizo Kwa kuwa lisingesajiliwa.

Miaka ya hivi karibuni Serikali ilifuta usajili wa NGO moja iliyojulikana kama 'Sisi Kwa Sisi' Kwa tuhuma kama hizi. Kwenye uchunguzi huu, imebainika kuwa baadhi ya viongozi wa iliyokuwa Sisi Kwa Sisi ni waandamizi kwenye CHESA. Je, Sisi Kwa Sisi Siyo CHESA kwenye rangi nyingine?

MOVIE: Hansel & Gretel (Imetafasiliwa Kiswahili) | Download Now

$
0
0
http://www.shmee.me/wp-content/uploads/2014/02/hansel_gretel_witch_hunters.jpg 
 http://muvikaonline.com/watch-hansel-gretel


Watch Trailer
Attachments area Preview YouTube video Hansel and Gretel - Official Trailer [Muvikaonline.Com]

Kundi la Original Comedy Matatani Kwa Kuvaa Sare za Jeshi la Polisi Kwenye Sherehe ya Masanja Mkandamizaji

$
0
0
katika  siku za hivi karibuni, kumejitokeza  tabia kwa baadhi ya watu wakiwemo wasanii watu wengine mmoja mmoja kutumia mavazi yanayofanana na sare za Majeshi ya Ulinzi na usalama hapa nchini likiwemo Jeshi la Polisi katika shughuli zao za kisanii au katika kazi mbalimbali, Jambo ambalo ni kinyume cha sheria, kanuni na taratibu za Nchi.

Kwa mujibu wa Sheria ya kanuni za makosa ya Jinai, sura ya 16 na  marejeo yake ya mwaka 2002,  kifungu cha 178 (1) na  (2) kinachozungumzia makosa dhidi ya sare za majeshi ya ulinzi na usalama,  kinabainisha wazi kuwa ni kosa kisheria kwa mtu yeyote ambaye siyo mtumishi wa majeshi ya ulinzi na usalama kuvaa mavazi yanayotumiwa au kushabihiana na sare za majeshi hayo  bila kibali kutoka kwa  Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kufuatia  kitendo kilichofanywa na kundi la kisanii la “ Original Comedy” kuvaa mavazi yanayoshabihiana na sare za Jeshi la Polisi, Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam linachukua  hatua za kisheria dhidi ya wasanii hao.

Aidha Jeshi la Polisi nchini, linatoa onyo kali kwa mtu ama kikundi chochote kuacha kutumia  mavazi yanayofanana na sare zinazovaliwa na  majeshi ya ulinzi na usalama hapa nchini na atakayebainika hatutasita kuchukua hatua kali za kisheria dhidi yake.

Jeshi la Polisi linatoa rai kwa wale wote wenye mavazi yanayoshabihiana na sare za majeshi ya ulinzi na usalama  kuzisalimisha mara moja katika vituo vya Polisi vilivyokaribu nao.

 Imetolewa na:
Advera John  Bulimba – Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP)
Msemaji wa Jeshi la Polisi.

Makao Makuu ya Polisi.      

Marufuku kutumia mafuta ya Transfoma kukaangia Chipsi - Profesa Muhongo

$
0
0
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amepiga marufuku matumizi ya mafuta ya transfoma kwa ajili ya kukaangia chips na kutengeneza mikorogo.

Profesa Muhongo ameyasema hayo alipokuwa akihutubia wakazi wa kijiji cha Kirongo wilayani Muheza mkoani Tanga alipokuwa katika ziara ya kukagua miradi ya umeme  vijijini inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) katika mkoa huo.
Viewing all 104781 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>