Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104432 articles
Browse latest View live

Nimeshakuwa sasa, kiukweli nina kiu ya mume – Johari

0
0
Msanii wa filamu, Johari Chagula amefunguka kwa kusema kuwa kwa sasa ana kiu yakumpata mume sahihi ambaye ataingia naye kwenye maisha ya ndoa.

Mwigizaji huyo ambaye ni mama wa mtoto mmoja, amesema umri wake kwa sasa unamruhusu kuingia kwenye maisha ya ndoa

“Mimi ni mwanamke kamili, ni mtu mzima. Nimeshakuwa sasa, kwahiyo kiukweli nina kiu ya mume,” Johari aliliambia gazeti la Mtanzania. “Mungu akinipa mume bora, nitaolewa. Sitaki kuzungumzia sana mambo yaliyopita, lakini muhimu kwa sasa ni mume,”

Mbali na hayo mwingizaji huyo amewataka kukaa mkao wa kula kwa ajili ya filamu yake mpya ambayo amewashirikisha wasanii wachanga kutoka mkoani Mwanza.

Harmonize: Nivae dela ndio mseme simkopi Diamond?

0
0
Shutuma kuwa amekuwa akimuiga bosi wake Diamond, zimemchosha Harmonize na sasa ameamua kujibu.

Baada ya video ya wimbo Inde alioshirikishwa na Dully Sykes kutoka, mashabiki ndio wamezidi kuendelea kusisitiza kuwa msanii huyo anamuiga kwa kiasi kikubwa Diamond.

Harmonize ambaye mara nyingi amekuwa akisisitiza kuwa ndivyo yeye alivyo na yeye sasa ameonekana kuchoshwa na malalamiko ya mashabiki hao ambapo amejikuta akiandika ujumbe wenye utata kwenye Instagram:

Mhhh copy! copy! copy!….. mwisho wa siku hata ukinya utaambiwa kunya kama wewe usimcopy@diamondplatnumz ebwana mzee#simbaa video ijayo wacha nianze kuvaa Dera maana nguo zote ushazivaa 😃😃😃#INDE in my BIO though😊

Malaika Afungukia Alivyoingizwa Mjini China

0
0
MSANII wa Bongo Fleva, Malaika Exervery amesema katika vitu ambavyo haviwezi kutoweka kichwani mwake ni pamoja na kutapeliwa wakati alipoingia nchini China kwa mara ya kwanza kwenye Jiji la Hong Kong.


Akizunguza na Juma3tata, Malaika anasema kuwa tukio la yeye kuingizwa mjini lilitokea mara baada ya yeye kuwekwa kuzuizini kwenye uwanja wa ndege kwa saa 16 akihisiwa kuwa amebeba madawa ya kulevya.

“Nilinyang’anywa mizigo yangu yote hadi simu, nilikaa pale kwa muda mrefu mpaka naachiwa usiku ulikuwa tayari umeingia na nilirudishiwa simu tu bila laini kwahiyo ikabidi nianze kutafuta duka ili ninunue laini niwasiliane na mwenyeji wangu,” anasema.

Akaongeza: “Bahati nzuri akatokea Mchina mmoja ambaye alikuwa akiuza laini. Kwasababu nilikuwa na umuhimu nayo kwa haraka, nilinunua bila kuuliza mara mbili. Nikafanya mawasiliano na mwenyeji wangu, kisha nikaondoka.

“Lakini baadaye nilipokuja kufuatilia nikagundua kuwa ameniuzia kwa bei ya juu sana. Yaani sikuwa na hamu. Kweli mjini usipokuwa mjanja unapigwa.”

Mzee Yussuf Ataendelea Kusikika Japo Anasema Amestaafu Muziki - Khadija Yusuf

0
0
Zikiwa zimepita siku kadhaa tangu Mzee Yussuf kutangaza kuacha rasmi kazi ya muziki na kumrudia Mungu, mdogo wa mzee Yussuf, Khadja Yussuf ambaye ni muimbaji katika bendi ya Jahazi Modern Taraab amefunguka na kusema Mzee Yusuph lazima atasikika.

Khadja Yussuf
Amesema kuwa licha ya kaka yake huyo kuacha muziki lakini 'band' hiyo itaendelea kufanya kazi ya muziki na wataendelea kutoa kazi ambazo Mzee Yussuf alishiriki.

Akiongea kwenye kipindi cha eNewz ya EATV Khadja alisema kuwa ni kweli mzee amemrudia Mungu lakini jambo hilo haliwazuii wao kuendelea na kazi ya muziki na kudai Mzee Yussuf atake asitake lazima katika baadhi ya kazi ambazo tayari alishafanya kwenye bendi hiyo ataonekana tu kwani hawawezi kufanya marekebisho na kumuondoa katika kazi hizo ambazo zinatarajiwa kutoka siku za karibuni.

"Hata kama Mzee amemrudia Mungu muache huko huko na Mungu wake, lakini sisi tutaendelea kufanya kazi na kutoa kazi nzuri zaidi hata ya hizo, kwani waimbaji wapo wengi siyo mzee tu, nachoweza kusema ni kwamba kuna kazi ambazo tulishafanya na Mzee Yussuf nyingine amepiga kinanda kwenye wimbo wa mkewe, na nyingine ameonekana au ameimba, hizo kazi zitaendelea kutoka, tunachoweza kufanya tunaweza kuondoa picha yake kwenye band lakini kazi ambazo ameshiriki lazima ataonekana tu zitakapotoka hilo hawezi kulikwepa" alisema Khadja Yussuf

Madada wa The Kardashians Wakanusha Kauli ya The Game Kuwa ‘Alipita’ na 3 Kati yao

0
0
Madada wa The Kardashians wanadai kuwa rapper The Game anadanganya anaposema kuwa amewahi kulala na watatu kati yao kwenye wimbo wake mpya, Sauce.

Kwa mujibu wa TMZ, Game alipita na mmoja tu. Vyanzo vilivyo karibu na familia hiyo maarufu, imewaondoa Kylie, Kendall, Khloe, Kourtney na Kris kwenye orodha hiyo na kwamba hakuna kati yao aliyekula uroda na Game.

Vyanzo hivyo vimekubali kuwa mke wa Kanye West, Kim Kardashian ndiye aliyewahi kuwa na uhusiano na Game miaka ya nyuma. Khloe na Game wamekuwa marafiki kwa muda, lakini vyanzo hivyo vimesema haukuwa uhusiano zaidi ya ule wa kawaida.

Inasemekana kuwa Game alimfuata Kanye kuomba ruhusa ya kuutoa wimbo huo na Yeezy alitoa baraka zake. Hata hivyo, Game anashikilia msimamo wake kuwa alipita na watatu kati yao.

Zifahamu Sababu za Justine Bieber Kufuta Account yake ya Instagram

0
0
Moja kati ya mastaa wanaongoza kuwa na Followers wengi katika mitandao ya kijamii huwezi kuaacha kumtaja Justine Bieber ambaye account yake ya Instagram ina jumla ya wafuasi milion 77.8 , Mtu wangu headlines zimechukuliwa leo na Staa huyo anayemiliki hitsong ya ‘Sorry‘ kuamua kuifuta account yake ya instagram

Kisa kimeanzia pale Justin Bieber alipokuwa anapost picha na msichana ambaye ni mtoto wa mwanamuziki Lione Richie mwanamitindo Sofia Richie mwenye umri wa miaka 17 ambapo ameonekana akiwa na Justin Bieber kwenye mitoko mingi hivi karibuni.

Baada ya Justin Bieber kupost picha akiwa na msichana huyo mashabiki wake wamekuwa wakicomment maneno yalioonesha kuwa ya chuki na kutopendezwa kwa Justin kuwa karibu na msichana huyo, maneno yalivyozidi Justin akaamua kupost picha na kuandika maneno haya …

’Nitaifanya account yangu iwe private kama hamtaacha chuki, kama nyie kweli ni mashabiki zangu hamuwezi kuchukia watu ninaowapenda mimi‘

Mkasa ukazidi pale mwanamuziki Selena Gomez ambae ni Ex wake Justin kupost picha na kuandika maneno yaliomlenga Justin Bieber na kuandika hivi …
’Kama huwezi kuvumilia chuki acha kumpost girlfriend wako, wekeni iwe muhimu kwenu wawili tu usikasirikie mashabiki wako wanakupenda na walikuwa na wewe kabla ya mtu yeyote yule‘

Mambo yalibadilika na JB kujibu:

‘It’s funny to see people that used me for attention and still trying to point the finger this way. Sad. All love. I’m not one for anyone receiving hate.’

Ujumbe wa Bieber ulimchokonoa zaidi Gomez aliyejibu:
Funny how the ones that cheated multiple times, are pointing the finger at the ones that were forgiving and supportive, no wonder fans are mad. Sad. All love.’

Na baada ya majibizano katika comments Justin na Ex wake, Justin amechukuwa maamuzi ya kufuta Instagram account yake na kwa sasa imebaki facebook na twitter yake tu.

Wema Sepetu Aelezea Bidhaa yake Mpya na Alikopata wazo la Biashara hiyo

0
0
Nguvu ya mwigizaji staa wa Tanzania Wema Sepetu  kutengeneza zaidi bidhaa zenye jina lake na kuziuza kwa Watanzania inaendelea kuonekana, ni juzijuzi tu alileta lipstick zenye jina la KISS BY WEMA.

Wema kazungumzia kuhusu bidhaa yake nyingine ambayo hii ni ya mguuni na kuyaongea haya
Mimi naweza kusema kwamba idea imetoka kwa Mama  kwamba anapenda sana vitu vya asili ukienda nyumba kwa Mama yangu utakuta viatu vyake vingi vya kimasai na hii ni idea yake’

‘Baada ya hapo tukaanza kutafuta Jinsi ya kutengeneza za kwetu mwisho wa siku tukapata sample nzuri kwahiyo ni kitu ambacho nimemfanyia Mama yangu’- Wema

Jibu la Mwimbaji Emmanuel Mbasha Kuhusu Kurudiana na Flora Mbasha

0
0
Kama utakuwa unakumbuka mnamo September 21,2015 moja ya stori kubwa iliyogusa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania ni ishu ya Hukumu ya Kesi ya Mwimbaji wa Gospel Tanzania, Emmanuel Mbasha ambapo alikuwa anakabiliwa na Kesi ya kumbaka shemeji yake na kesi imekuwa Mahakamani tangu 2014.

Wengi tunafahamu kwamba mwimbaji huyo aliachiwa huru baada ya Mahakama kumkuta hana hatia kwenye Kesi hiyo, sasa leo kajibu swali kuhusu kurudiana na mkewe Flora Mbasha na kuyaongea haya:

‘Mimi kurudiana na Flora Mbasha ni ngumu kwasababu yeye ndio aliniacha mimi na yeye ndio aliandaa mazingira yake ya kuniacha mimi mpaka ikafika wakati Familia yangu, viongozi mbalimbali wa Dini wakawa wanamshauri lakini akutaka kurudiana na mimi kwahiyo naweza sema ni ngumu kurudiana na Flora’

Mtangazaji Edo Kumwembe Aula Supersport..Apata Deal la Uchambuzi wa Soka....

0
0
Mchambuzi Mahiri wa Michezo Edo Kumwembe apata deal nono ya kuwa mchambuzi wa Kiswahili wa Supersport chini ya DSTV, Ameandika haya katika ukurasa wake wa Facebook mara baada ya kusaini mkataba:

"DEAL DONE. Am happy kuwatangazia kuwa nimesaini deal na Supersport kwa ajili ya kuwa Mchambuzi wao katika matangazo ya Ligi Kuu England kwa kiswahili. Nitakuwa naenda Johannesburg kila Ijumaa na kurudi Dar es salaam Jumatatu...Thanks everyone"

Wizkid Asema Kidogo ya Diamond Ndio Nyimbo Bora na Anayoikubali Kwa Sasa

0
0
Msanii mkali wa africa na dunia kutoka nigeria wizkid akiongea na clouds fm amesema kwa sasa nyimbo ya diamond platnumz aliowashilikisha psquare kidogo ndio nyimbo bora kwake na ndio anayoukubali.

Wizkid pia hakusita kumpongeza diamond platnumz baada ya nyimbo hiyo kuingia kwenye chat za BBC 1xtra UK na kupata rotation.

Katika chat hiyo ni wasanii 2 tu kutoka africa walioingiza nyimbo zao , kidogo ya diamond na shabba ya wizkid mwenyewe akiwa na chriss brown, french montana na trey songz.
Wizkid jumamosi hii atakuwa Tanzania jijini mwanza kutumbuiza kwenye show ya fiesta

Picha za Masanja na Mke wake Zazua Maswali Kwa Mashabiki wake..Wadai Mke wa Mchungaji Apaswi Kuvaa Hivyo

0
0
Baada ya Harusi ya Mchekeshaji Masanja na Mkewe iliyofungwa Jumapili iliyopita wawili hao wameonekana kwenye picha mbali mbali wakijivinjari Honey Moon huku mavazi yao yakileta mabishano kama kweli ni Baba Mchungaji na Mama Mchungaji....

Baadhi ya Comments kwenye picha hizo hizi Hapa:

"Wachungaji wa mwendo kasi.."

"Kwa jinsi walivyovaa Biblia Takatifu inatufundisha kuwa utaweza kuwatambua kama ni nkweli wachungaji wa Kanisa la Mungu au watumishi wa kitapeli. Hivi vitu havijifichi. Mtumishi wa Mungu haachi maswali na hata akijifanya kwamba hamfahamu Mungu atajulikana tu kuwa ni mtumishi wa Mungu. Kumbuka Petro alipojaribu kusema hamfahamu Yesu na akaanza kuondoka ila waliokuwepo wakasema kuwa hata anavyotembea inadhihirisha yeye ni mtu wa Kristo. Je kwa muonekano wa Masanja, yeye ni mtumishi wa Mungu aliye hai????"


"Don't judge by looks....THE LORD GOD ALMIGHTY knows the hearts of everyone"


"Mavazi yanaonyesha uhalisia wa mtu. Kuna mavazi ambayo KAMWE mtu wa Mungu hawezi kuyavaa au kumruhusu mtu anayemmiliki kuvaa. Ila sijayaongelea mavazi aliyovaa Masanja"

"The Bible teaches us how to distinguish false from true prophets. Follow the Bible!!!"

"Dah!Mke wa masanja ana ugonjwa wangu kwa kweli"

Na wewe toa Maoni yako:



Madudu Dodoma

0
0
WAKATI serikali ikijiandaa kuhamia Mkoa wa Dodoma, Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Serikali za Mitaa imebaini kuwepo kwa madudu katika Sekretarieti ya mkoa huo, anaandika Dany Tibason.
Kamati hiyo imebaini kuwepo kwa matumizi mabaya ya fedha za serikali ikiwa ni pamoja na kujiuzia magari ya serikali bila kufuata utaratibu.

Japhet Hasunga, Mwenyekiti wa Kikao cha Kamati ya PAC ambaye ni Mbunge wa Vwawa (CCM) amesema, watumishi wamekuwa wakijiuzia magari ya serikali, wakipeana pia wakiyatengeneza katika gereji bubu.

Mbali na hayo pia kuna sintofahamu kuhusu ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ambao kamati hiyo imehoji sababu ya kununuliwa kwa vifaa vipya wakati jengo halijakamilika.
Kutokana na kuwepo kwa madudu hayo katika Sekretalieti ya Mkoa wa Dodoma, PAC imetoa maagizo saba kwa uongozi wa mkoa kutokana na kushindwa kujibu hoja kutokana na Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG).

Hasunga ameagiza mambo saba; kwanza, kamati imeitaka idara ya usimamizi wa mali za serikali kufanya uhakiki maalum wa mali za serikali katika fungu 72 hasa magari yanayofanya kazi, yaliyoharibika na yaliyouzwa na kuwasilisha taarifa ya uhakiki huo maalumu kwa kamati ndani ya miezi mitatu.

Amemtaka Ofisa Masuhuri kusimamia kitengo cha uhasibu ili kuzingatia viwango vya kimataifa ya utayarishaji wa mahesabu katika utayarishaji wa mahesabu ya serikali ili kuepuka hati za ukaguzi zenye dosari.

Akitoa maagizo amesema, kamati inamwagiza Ofisa Masuhuri kuzingatia sheria ya manunuzi ya mali ya umma na kanuni zake katika shughuli za sekretalieti ikiwa ni pamoja na kupata vibari kwenye mamlaka husika anapofanyika uhamisho wa fedha katika vifungu mbalimbali.
Mbali na hilo kamati imemuomba CAG kwa kushirikiana idara ya mali za serikali kufanya tathimini ya kina kuiridhisha kamati iwapo garama za Sh. 12.5 Mil zilizotumika katika ujenzi wa jengo la ofisi ya mkuu wa mkoa kama zinakidhi thamani halisi ya sasa.

Hasunga pia ametoa agizo la tano kuwa Ofisa Masuhuri awasilishe taarifa ya maandishi kuhusu matumizi ya kiasi cha Sh. 665.3 Mil na chanzo cha fedha hizo kabla ya muda wa kazi kesho.
Ofisa huyo ametakiwa kuwasiliana na Ofisi ya Rais Utumishi ili kuhakikisha nafasi za kazi zinazokaimiwa zinajazwa mapema iwezekanavyo ili kuongeza ufanisi wa sekretalieti katika Mkoa wa Dodoma.

Agizo la saba lililotolewa na PAC kwa Mkoa wa Dodoma amesema, kwa kuwa hoja nyingi za ukaguzi bado hazijapata majibu sahihi, kamati kamati inatoa muda wa miezi sita kwa sekretarieti kukamilisho hoja za kukaguzi na taarifa ya utekelezaji ziwasilishwe kwa CAG na kwa kamati kabla ya miezi sita kuisha.

KIMENUKA:Waliotafuna Fedha za Mikopo Wapewa Siku Saba Kuzirejesha

0
0
Wafanyakazi wa Bodi ya Mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu (HELSB)na wa vyuo vilivyohusika kufanikisha malipo ya fedha za mikopo kwa wanafunzi hewa kuchukuliwa hatua kali za kisheria pamoja na kurudisha fedha zilizochukuliwa na wanafunzi hao.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mh. Joyce Ndalichako .

“Kutokana na mambo yaliyobainika serikali imechukua hatua ikiwemo kuvitaka vyuo vikuu vilivyopokea fedha za wanafunzi ambao hawapo chuoni vinatakiwa virejeshe fedha hizo ndani ya siku Saba kuanzia leo, ” amesema.

Amesema vyuo vinatakiwa kuweka mfumo mzuri wa kuhifadhi kumbukumbu za wanafunzi kuanzia usajili, matokeo ya majaribio na ya mitihani na namba za akaunti za benki ambazo fedha za mikopo hulipwa ili kuondoa udanganyifu.

“Bodi ya mikopo inapaswa kuchambua na kuingiza mara moja mabadiliko ya taarifa zote za wanafunzi kama zilivyopokelewa kutoka vyuoni ili kuepusha ulipaji wa fedha kwa wanafunzi wasiostahili,” amesema

Timu ya Simba Sasa Kuendeshwa Kwa Hisa..Mo Dewji Akabithiwa Timu

0
0
Kamati ya Utendaji ya Simba na mfanyabiashara, Mo Dewji leo wafikia makubaliano ya kuendesha Klabu ya Simba kwa mfumo wa hisa.

Hisa zitauzwa kwa wanachama wapya kwa taratibu mahususi, wanachama wa zamani watagawiwa hisa za bure.

Dk. Tulia Afunguka, Asema Ukawa Walimtukana Tusi Kubwa

0
0
SIKU mbili baada ya Spika wa Bunge, Job Ndugai kuahidi kufanyika maridhiano kati ya uongozi wa Bunge na wabunge wa upinzani katika kikao kijacho kinachotarajiwa kuanza Septemba 6, mwaka huu, Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson amesema hataki kuwasikia wabunge wa upinzani wala kuwawaza.

Kauli hiyo ya Naibu Spika huenda ikazidi kutonesha kidonda hasa baada ya Bunge la Bajeti lililofanyika Mei mwaka huu kuacha majeraha kutokana na wabunge wa upinzani wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kususia vikao vyote vilivyoendeshwa na kiongozi huyo.

Juzi wakati akihojiwa kupitia kipindi cha Funguka kinachorushwa na Kituo cha Luninga cha Azam, Spika Ndugai,  alisema anatafuta mbinu ya kuweka sawa mambo hayo kwa kufanya maridhiano  ikiwemo kushirisha maspika wastaafu.

Akizungumza na gazeti la Mtanzania juzi katika mahojiano maalumu ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Dk. Tulia alisema hapendi kuwawazia wabunge hao wa upinzani.

“Kwa kuwa Spika yeye kazungumza siwezi kucomment chochote kwa sababu sipendi kuwawazia wabunge hao,”alisema.

Alipoulizwa kwamba ni kwanini migogoro ilizidi wakati yeye akiwa anaendesha vikao, alisema alichokuwa anafuata ni kanuni na kwamba malalamiko hayawezi kukosekana.

“Nashangaa wengine wanasema kuendesha vikao ni mpaka uwe na uzoefu…unajua zile kanuni hata ukipewa uendeshe wewe ukishazielewa hazihitaji uzoefu wowote. Kulalamika kuwa nawapendelea ni jambo la kawaida.

“Kwa mfano siku iliyotokea vurugu wakati wabunge wa upinzani wanadai kutorushwa matangazo ya Bunge live, aliyekuwepo kwenye kiti alikuwa ni mwenyekiti ambaye ni mzoefu wa siku nyingi na ni yeye aliyepeleka majina yao kwenye Kamati ya Maadili, sasa sidhani kama hiyo ni hoja,”alisema Dk. Tulia

Alieleza kushangazwa kwa kitendo cha wabunge wa upinzani katika barua yao waliyomwandikia Spika kwamba hawana imani naye, huku akihusishwa na fedha zilizorejeshwa serikalini.

“Katika ile barua walieleza sababu nyingine kuwa hawana imani na mimi, wakanihusisha na zile Shilingi bilioni 6 zilizorejeshwa serikalini wakati sheria na utaratibu upo wazi kwa sababu Spika au Naibu Spika hauhisiki na masuala ya fedha bali anayehusika ni Katibu wa Bunge.

“Kwa hiyo ni jambo la kushangaza kwamba Naibu Spika karudisha fedha, mimi si mshika mafungu lakini pia ni namna watu walivyopokea huwezi kuwazuia wanavyokuwazia,” alisema.

Akizungumzia kauli ya Spika Ndugai kwamba kwa kuwa Bunge la 11 lina wabunge wapya wengi na kwamba kuwaongoza kunahitaji uvumilivu mkubwa alisema: “Nisingependa kuongelea kauli ya Spika…lakini uvumilivu wa mtu kutakiwa akae hadi mara 11 halafu ameendelea kusimama ni uvumilivu gani huo?,” alihoji.

Pamoja na mambo mengine alisema wakati wabunge wanawake wa Ukawa walipojitoa kwenye  Chama cha Wabunge Wanawake (TWPG), alitukanwa tusi kubwa lakini alinyamaza.

Mei 5, mwaka huu wakati akichangia mjadala wa hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria, Mbunge wa Ulanga Mashariki, Gudluck Mlinga (CCM), alidai kuwa ili kuwa mbunge wa viti maalumu Chadema lazima uwe ‘baby’ wa mtu.

“Laiti ungeona Hansard tusi walilonitukana siku ile, actually Mlinga hajatukana lakini ulisikia nikilalamika mahali kwamba nimetukanwa? wao wanaongee vibaya…watukane, mimi bado ni kiongozi wao na siwezi kuanza kuwakasirikia itakuwa sasa nashindwa kuwaongoza mimi ni kama mzazi wao,” alisema Dk. Tulia.

Alisema kitendo cha watu kudai kwamba anafanya upendeleo bungeni ni changamoto ya kawaida, kwa sababu hata katika mabunge ya Jumuiya ya Madola malalamiko ya aina hiyo yapo.

“Pale bungeni  wako wabunge 389, hawa ni wengi sana wote hawawezi kupata nafasi ya kuongea. Kwa mfano uliomba nafasi jana ukapewa ukaomba leo, hata ukisimama mara 11 katika hali ya kawaida huwezi kupewa kwa sababu wako wengi ambao hawajachangia.

“Kama kiongozi naona ni sehemu mojawapo ya kusimamia jamii ni changamoto na itaendelea kuwepo kwa miaka mitano,”alisema Dk. Tulia.

Soma Nafasi za Ajira Zilizotangazwa leo Katika Magazeti na Mitandaoni

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na Wenzake 8 Wafikishwa Mahakamani

0
0
Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya vitambulisho vya taifa-NIDA- Dickson Maimu (wa tatu kushoto) na viongozi wengine  nane wa taasisi hiyo wamefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu mapema leo.Habari zaidi tutawaletea.

Mnamo mwezi January 2016, Rais Magufuli aliamua kutengua uteuzi wa Mkurugenzi wa mamlaka ya vitambulisho vya taifa (NIDA) Bwana Dickson Maimu na kumsimamisha kazi yeye na wafanyakazi wengine ili kupisha uchunguzi wa namna ilivyotumika kiasi cha shilingi bilioni 179.6 katika zoezi la upatikanaji wa vitambulisho vya taifa wakati bado kuna malalamiko kwamba watu wengi hawajapata vitambulisho hivyo. .

Wasanii wanne wa Orijino Komedi Wakamatwa na Kuhojiwa Polisi....Masanja Mkandamizaji Aendelea Kusakwa

0
0
Wasanii wanne wa kundi la vichekesho la Orijino Komedi akiwamo meneja wao wamekamatwa na kuhojiwa na jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwa kosa la kuwa na sare za polisi.

Juzi, jeshi hilo lilitoa onyo kwa mtu ama kikundi chochote kuacha kutumia mavazi yanayofanana na sare zinazovaliwa na majeshi ya ulinzi na usalama nchini na kwamba atakayebainika atachukuliwa hatua za kisheria.

Kwa mujibu wa Sheria ya Kanuni za Makosa ya Jinai, sura ya 16 na marejeo yake ya mwaka 2002, kifungu cha 178 (1) na (2) kinachozungumzia makosa dhidi ya sare za majeshi ya ulinzi na usalama, kinabainisha kuwa ni kosa kisheria kwa mtu yeyote ambaye siyo mtumishi wa majeshi ya ulinzi na usalama kuvaa mavazi yanayotumiwa au kushabihiana na sare za majeshi hayo bila kibali kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kaimu Kamanda wa Kanda hiyo, Hezron Gyimbi alisema wasanii hao walikamatwa juzi saa 10 jioni baada ya kusambaa kwa video kwenye mitandao ya kijamii wakiwa wamevalia sare hizo kwenye sherehe ya harusi ya Emmanuel Mgaya maarufu ‘Masanja’.

Gyimbi aliwataja watuhumiwa wengine kuwa ni Lucas Lazaro (Joti), Alex John (McRegan) na Isaya Gidion (Wakuvanga) na Sekioni David (Seki) ambaye ni meneja wao.

Alisema sare walizokutwa nazo watuhumiwa hao ni za kazi za kawaida za jeshi la polisi hilo ikiwamo kofia, filimbi, shati, suruali, cheo na mkanda.

“Tunaendelea kuwachunguza zaidi kama wana vitu vingine vya jeshi la polisi na tunataka kujua kuwa sare hizi wamepa- ta kibali kwa nani na uhalali wa kuwa nazo,” alisema Gyimbi.

Alisema jeshi hilo linaendelea kumtafuta Masanja ili kujibu tuhuma zinazomkabili. Kaimu kamanda huyo alisema watuhumiwa hao walihojiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi kuanzia juzi saa 10 jioni hadi jana jioni huku na dhamana zao zilikuwa wazi.

Serikali Kuchunguza Mali za Vigogo 500, Wamo Wabunge, Mawaziri, Makatibu Wakuu na Wakurugenzi

0
0
WAKATI takribani asilimia 20 ya viongozi wa umma kwa mwaka 2011 hadi mwaka jana hawakuwasilisha matamko ya mali zao kwa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa wakati, mwaka huu serikali imetangaza kuhakiki matamko ya mali za viongozi 500.

Aidha, serikali hiyo imebainisha wazi kuwa haitowafumbia macho viongozi, watakaoshindwa kuwasilisha matamko ya mali zao kwa mujibu wa sheria, ikiwemo viongozi watakaowasilisha matamko ya mali yatakayobainika kuwa na udanganyifu.

Hayo yalibainishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki wakati akifungua warsha ya wadau, kujadili taarifa ya matokeo ya utafiti kuhusu hali ya maadili nchini Dar es Salaam jana.

Kairuki alikiri kuwa hata katika tafiti nyingine ndogo, zilizofanyika kuhusu hali ya maadili nchini pamoja na takwimu kubadilikabadilika, lakini zilibainisha kuwepo kwa viongozi wasiowasilisha matamko yao ya mali na wengine kutowasilisha kwa wakati.

Alisema taarifa hiyo ya utafiti kuhusu hali ya maadili ya viongozi nchini kwa miaka mitano kuanzia 2011 hadi mwaka jana, ilibainisha kuwa pamoja na kuwepo kwa mwamko wa viongozi kuhusu suala zima la maadili, bado asilimia 20 ya viongozi hao wa umma hawakuwasilisha matamko yao ya mali kwa wakati.

“Tumepokea taarifa hii na imetutia hamasa kwa kweli, tumeona asilimia 20 hawarejeshi kwa wakati matamko yao, hawa ni wengi sana ikizingatiwa kuwa ni viongozi, tunatoa onyo hakuna atakayefumbiwa macho endapo atakiuka Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, kwani atachukuliwa hatua stahiki za kisheria,” alisisitiza.

Alisema kwa kawaida endapo kiongozi asipowasilisha tamko la mali zake hadi ifikapo Desemba 31, huhojiwa na Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma, lakini pia inapothibitika kuwa alikiuka kwa makusudi sheria hiyo ya maadili ya viongozi huchukuliwa hatua za kisheria.

Alisema mwaka huu, kuna jumla ya viongozi wa umma 15,624 kati ya hao viongozi 500 tayari wameshatengewa fedha kwa ajili ya mali zao kuhakikiwa na endapo fedha zitapatikana idadi hiyo inaweza kuongezeka na kufikia 1,000.

“Miaka ya nyuma tulikuwa tunahakiki kwa mwaka viongozi 100 hadi 200, safari hii tumejipanga kuanza na viongozi 500. Lakini katika hili tunaomba wananchi nao watusaidie kuhakiki mali za viongozi hawa wa umma kwani sheria inawa ruhusu kufanya hivyo, ili kuweza kubaini viongozi wadanganyifu,” alisema.

Akiwasilisha matokeo ya utafiti huo, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), Profesa Kessy aliyefanya utafiti huo kwa kushirikiana na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi, alisema lengo la utafiti huo ni kuangalia hali halisi ya maadili nchini kuanzia viongozi hadi kwa wananchi.

Mapacha Waliofanyiwa Upasuaji Kupasuliwa Tena

0
0

Madaktari bingwa nchini wakisaidiana na wataalamu kutoka Misri, wanajipanga kuwafanyia upasuaji watoto pacha waliotenganishwa, Eliud na Elikana Mwakyusa (3) wakazi wa Kasumulu, Kyela mkoani Mbeya.

Katika upasuaji waliofanyiwa awali, waliwekewa njia za dharura na muda mfupi za haja ndogo na kubwa, hivyo wanafanyiwa upasuaji mwingine kuwekewa njia za kudumu.

Ofisa Habari wa MNH, John Stephen amesema upasuaji wa pacha hao umefuatia baada ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kuanza upasuaji kwa watoto wanane, wenye matatizo ya njia ya mkojo na mfumo wa hewa na chakula.

Viewing all 104432 articles
Browse latest View live




Latest Images