Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104414 articles
Browse latest View live

Alikiba Kuisimamisha Dunia August 25

0
0
Hii ni kwa wale wakuu wote waliochoshwa na mziki wa maigizo, Kiki za kipuuzi, sarakasi, show za play back, video za kucopy na kuungaunga, show off za kitoto na mziki wa big jii.

Mark the date 25 August mwaka huu, Kingkiba Kuachia Laana Mpya mjini Original Aje Remix featuring Rapper mahiri kutoka Nigeria M.I, Wimbo huu ni tofauti by 90% ya ule uliovuja, Video directed by director Mejialabi, South Africa.

Wenye Akaunti ‘Feki’ Mitandaoni kukiona - TCRA

0
0
MAMLAKA ya Udhibiti wa Mawasiliano hapa Nchini (TCRA) imewaonya watumiaji wa mitandao ya kijamii wanaojisajili katika mitandao hiyo kwa kutumia majina na taarifa za uongo, anaandika Charles William.

James Kilaba Kaimu Mkurugenzi wa TCRA amesema, vitendo vya watu kujisajili katika mitandao ya kijamii kwa kutumia majina na taarifa zisizo sahihi, ni kosa kisheria na kwamba wanaofanya hivyo watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Kilaba ameyasema hayo leo, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuongeza ufahamu kuhusu matumizi sahihi na salama ya mitandao ambayo inasimamiwa na Kitengo cha dharura cha kuitikia matukio ya usalama kwenye mitandao hapa nchini (TZ-CERT).

“Tumeamua kuzindua kampeni hii ili kuwasaidia wananchi kuepuka makosa ya kimtandao na kuepuka kufanyiwa utapeli au wizi mitandaoni kwa sababu matukio mengi ambayo yamekuwa yakiripotiwa au kulalamikiwa yanazuilika kwa watu kupewa elimu ya matumizi sahihi ya mitandao,” amesema Kilaba.

Kampeni hiyo ya kuongeza ufahamu kuhusu matumizi sahihi na salama ya mitandao, itafanyika kupitia matangazo ya redio, televisheni, magazeti pamoja na mitandao ya kijamii ambapo katika mitandao ya kijamii itajulikana kama, “Darasa mtandao”.

“Miongoni mwa mambo ambayo tutawafundisha wananchi ni kutoweka wazi taarifa zao binafsi zote katika mitandao, kubadili na kutunza neon la siri (password), kutojibu ujumbe unaosema umeshinda bahati nasibu na mengineyo mengi,” amesisitiza Kilaba.

Mwanamke Akikujibu Hivi Achana nae Haraka Sana Ujue Hakuna Kitu Hapo....

0
0
Wanawake wa uswahilini wa siku hizi wamekuwa na swagger ya aina moja wanapotongozwa.utasikia "MIMI NAWAOGOPA WANAUME",ukiuliza wewe ni bikra kwani? Atajibu hapana,ukiuliza kwa nini unawaogopa wanaume wakati we sio bikra atakujibu" NISHATENDWA SANA".ndugu yangu nakushauri,kama ukijibiwa hivo basi ondoka fasta ujue hapo hakuna mwanamke kabisa,kwa sababu haiwezekani mtu atendwe yeye tu na kila mwanaume,ujue huyo ana mapungufu ambayo hata wewe hutaweza kuvumilia ,mapungufu ambayo hata wewe utamtenda tu na mwisho wa siku utamuongezea idadi ya wanaume waliomtenda.ila mara nyingi wanawake wanaojibu hivo au wanaotendwa hivo unakuta ni hawajatulia kabisa(vicheche).

Kama Umesoma au Unasoma Kwa Lengo la Kuja Kupata Pesa; Unaweza Kuja Kujidharau na Kuwa 'Disappointed'

0
0
Kama umesoma[au unasoma], kwa lengo la kuja kupata pesa; unaweza kuja kujidharau na kuwa "disappointed". Kwa sababu huku mtaani kuna watu ni ama la saba au hata la saba hawakumaliza lakini ndio wanaoongoza kumiliki pesa za kutisha. Ukipata nafasi ya kusoma; soma kwa bidii, lakini ni vema ukatambua kuwa [fedha za maana] ni nadra sana kukaa kwenye vyeti. Vyeti vikijitahidi sana vitaishia kukupa pesa ya kubadilishia mboga. Akili inayokupa vyeti madarasani ni tofauti kabisa na akili inayotumika mtaani katika utafutaji wa pesa! ‪#‎SmartMind‬

Ni Kosa Kumwangalia Mwanamke Kwa Sekunde 14 Nchini India

0
0
Watumiaji wa mitandao ya kijamii wamelalamika kuhusu tamko la afisa mmoja aliyesema kuwa ni kinyume na sheria kumuangalia mwanamke kwa zaidi ya sekunde 14 katika jimbo la Kerala nchini India.

Hakuna sheria kama hiyo nchini India lakini afisa huyo Rishiraj Singh ambaye ni kamshna amesema kuwa kumuangalia mwanamke kwa mda mrefu kunaweza kukutia mashakani.

Watu mitandaoni wanauliza itakuwaje iwapo mwanamume atafunga jicho mara moja na kulifungua akimwangalia mwanamke wakiongezea kuwa huenda bei ya miwani ya kujilinda dhidi ya jua ikapanda.

Lakini wengine wanasema kuwa bwana Signh amezua hoja nzuri sana kuhusu usalama wa wanawake.

”Mtu anaweza kushtakiwa kwa kumuangalia mwanamke kwa sekunde 14”,alisema bwana Singh katika eneo la Kochi siku ya Jumamosi.

Tamko hilo lililofanywa katika kanda ya video limesambaa katika jimbo hilo na kuzua ucheshi miongoni mwa mitandao ya kijamii.

Source:BBC

Wema Sepetu na Petit Man Wamaliza Tofauti zao

0
0
Kwa miezi kadhaa sasa Wema Sepetu na Petit Man walikuwa wakichuniana hadi kuwafanya mashabiki waanze kuuliza maswali kupitia mitandao ya kijamii kutaka kujua kunani!

Lakini usiku wa August 16, wawili hao walionekana wakijirekodi video fupi na Wema akaiweka katika account yake ya SnapChat. Baadaye kulivyokucha Wema alionekana kupost video clip ile ile ya SnapChat kwenye Instagram kuandika hivi: Yes…! He has a piece of me… @officialpetitman_wakuachetz”

“Mimi sidhani kama nina tatizo na Wema. Ndiye aliyenifanya mimi nijulikane na Wema ndiye mtu ambaye mimi nimetoka naye mbali sana miaka tisa. Kwahiyo hata kama nikiwa nimegombana naye siwezi nikasema siongei naye, kwahiyo mimi nahesabia sina tatizo naye kama watu wanavyodhani,” alisema.

Soma Nafasi za Kazi Zilizotangazwa Katika Magazeti na Mitandaoni leo 18 Aug 2016

0
0

Huu Ndiyo Utofauti wa Diamond na Kiba

0
0
KUNA vita ya maneno kati ya makundi mawili ya mashabiki wa Muziki wa Bongo Fleva, wanaowashabikia wasanii Alikiba na Nasibu Abdul ‘Diamond’, kila upande ukidai mtu wao ndiye anajua zaidi kuliko mwingine.

Ni mjadala mpana katika mitandao ya kijamii, mitaani na hata miongoni mwa wasanii wenyewe ambao kwa kificho au waziwazi, wamewahi kuzungumzia nani mkali katika wawili hao ambao wote ni vijana wenye asili ya Kigoma.

Alikiba ama King Kiba, ndiye wa kwanza kuingia na kupata jina katika Muziki wa Bongo Fleva, katikati ya miaka ya 2000 akiwa na singo yake ya kwanza, Cinderella ndiyo ilimfungulia milango, kwani alichomoza hadi juu ambako alidumu kwa muda mrefu.

Huenda Diamond amewahi kuimba kwa kuiga baadhi ya nyimbo za Alikiba, kwa sababu yeye alianza kupata jina mwaka 2009, mwaka ambao mwenzake tayari alishakuwa na albamu mtaani.

Unapotaka kufanya ulinganisho wa wawili hawa ni lazima uchague unataka kuwalinganisha nini, vinginevyo unaweza kujikuta umewekeza katika chuki au ushabiki, kitu ambacho hakitakiwi. Kwa mfano, vigumu kupata idadi kamili ya mashabiki wa wasanii hao, ingawa mapokeo ya kazi zao yanaweza kumuongoza mtu kuelewa.

Kitu kimoja cha msingi ambacho wengi wanakubaliana ni kwamba Alikiba ana uwezo mkubwa wa kuimba na mwenye sauti nzuri kuliko Diamond. Msanii mmoja chipukizi, Ibrahim Kidugu ‘Wizzy Rapper’ katika kibao chake cha Kote Nisikike, kwenye mojawapo ya vesi anasema “Ali ni mwanamuziki, Nasibu Mfanyabiashara.”

Maana ya Wizzy Rapper ni kuwa Diamond anafanya biashara ya muziki, ndiyo maana anaonekana kuwa juu ya Alikiba ambaye anafanya muziki kwa mazoea.

Katika ubora wake, Alikiba aliwahi kukutana na mkali wa R&B duniani, R Kelly, katika projekti iliyoitwa One8, ambapo wakali nane wa Afrika walifanya ngoma moja iliyoitwa Hands Across Africa ambao walikuwa ni yeye, Fally Ipupa, 2Face, Amani, Movaizhaleine, 4X4, Navio na JK.

Licha ya Kiba kufika nyumbani kwa R Kelly, studio kwake, alishindwa kutumia ushawishi wa msanii huyo mkubwa ili aweze kumsaidia kuingia katika soko la Marekani. Mbaya zaidi, alishindwa pia kujitangaza kimataifa kupitia Fally Ipupa na 2Face ambao ni maarufu kuliko yeye.

Ambwene Yessaya ‘AY’ alimkutanisha Diamond na Davido wa Nigeria na akafanya naye Ngoma ya Number One Remix. Hapa kijana yule wa Tandale hakutaka kuishia kwa msanii huyo pekee, akaingia nchini humo na kufanya kazi na wasanii karibu wote wakubwa, wakiwemo waliofanikiwa zaidi, P Square.

Hiyo imempa Diamond kujulikana zaidi na kumfanya kuwa mmoja wa wasanii wakubwa Afrika, kiasi cha wengi kuhitaji kolabo naye kutoka Afrika Kusini, Zimbabwe, Ivory Coast na kwingineko Afrika.

Alikiba haonekani kuwekeza akili yake yote katika muziki anaoufanya. Ni kama mtu ambaye anafanya muziki kwa kujifurahisha na siyo kufikia malengo ambayo mashabiki wake wangependa aende. Ana uwezo mkubwa nyuma ya Mic, lakini ameshindwa kuutumia ili kuliteka soko.

Kiba anaridhika au labda niseme, mvivu. Katika uhalisia ni makosa kumshindanisha na Diamond kwa sababu haoneshi kama ni mshindani wake. Alipokuwa katika ziara yake Ulaya, akaitumia nafasi adimu aliyoipata kukutana na marehemu Papa Wemba na kufanya naye wimbo.

Baada ya kuliweza soko la Afrika, Diamond anaonekana wazi kulitamani la Ulaya na Marekani na hii ndiyo sababu ya yeye kuwa msanii anayelipwa zaidi kuliko wote kwa sasa hapa Bongo.

Kiba hatafuti kolabo na watu wa nje kwa vile anadhani ataonekana anamuiga mwenzake, wakati katika maisha, kuiga vitu vizuri na vya maendeleo ni jambo la kupongezwa.

Hata hivyo, Kiba anayo nafasi ya kubadilika ili aweze kuwa mshindani wa kweli wa Diamond, vinginevyo asahau.

Chanzo:GPL

Dereva Taxi Jela Maisha Kwa Kulawiti Mtoto Ndani ya Gari

0
0

Mahakama ya Wilaya ya Ilala, imemhukumu kifungo cha maisha jela, dereva taksi Ally Mzako (29) baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mtoto wa miaka mitano.

Mzako ambaye ni mkazi wa Kinondoni, anadaiwa kumbaka mtoto huyo ndani ya gari, wakati mama wa mtoto huyo alipomuacha katika gari hiyo na kwenda duka la kubadilishia fedha za kigeni.

Hakimu mkazi, Flora Haule amesema Mahakama imeridhishwa na ushahidi wa mashahidi sita wa  upande wa mashtaka dhidi ya mshtakiwa.

Mzako alifanya kosa hilo, Julai 19, 2014, eneo la Clock Tower, mtaa wa Samora.

Soma Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Agosti 19

0
0


Soma Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Agosti 19

Salamu ya Maalim Seif yabamba Mitandaoni Nchini

0
0
 Picha inayomuonyesha Maalim Seif Sharrif Hamad akiwa ameinama mikono ikiwa tumboni, huku Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein akiwa amenyoosha mkono kuashiria kutaka kusalimiana na katibu huyo mkuu wa CUF, sasa imekuwa moto mtandaoni.

Picha hiyo ilichukuliwa wakati wa shughuli za mazishi ya Rais wa Pili wa Zanzibar, Aboud Jumbe Mwinyi kisiwani humo mapema wiki hii, na sasa inaigizwa na watu wa kariba tofauti wanaotuma mitandaoni picha inayofanana na tukio hilo.

Picha hizo zinaonyesha watoto, vijana na hata watu wa makamo wakiigiza tukio hilo.

Wawili hao walipambana kwenye Uchaguzi Mkuu wa Rais wa Zanzibar uliofutwa na mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (ZEC), Jecha Salim Jecha Oktoba 28, siku ambayo alitakiwa atangaze mshindi wa mbio za urais. CUF ilisusia uchaguzi mpya uliotangazwa na Jecha.

Vitendo hivyo vya kuigiza matukio ya watu muhimu sasa vimepamba moto mitandaoni. Miongoni mwa matukio yaliyoigwa sana mitandaoni ni la waziri wa zamani wa kilimo, Steven Wasira kupiga picha akiwa hajafunga vizuri vifungo vya koti na Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe kudondoka.

Pia tukio jingine lililoigwa sana ni la Rais wa Uganda, Yoweri Museveni kuonekana amekaa kwenye kiti pembeni ya barabara akiongea na simu huku msafara wake ukiwa unamsubiri.

Kilichomng’oa Mkuu wa Mkoa Arusha

0
0
Daudi Felix Ntibenda jana asubuhi alikuwa na majukumu ya kufungua mikutano miwili na kufanya shughuli nyingine kwa nafasi yake ya mkuu wa Mkoa wa Arusha, lakini hakuweza kuyatimiza kikamilifu majukumu hayo kwa kuwa Rais John Magufuli alikuwa na mawazo tofauti na mipango yake.

Ingawa haikufahamika sababu ya kuondolewa kwake, huenda mvutano baina yake na Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa ukawa umechangia.

Saa 2:12 asubuhi jana, Ofisi ya Waziri Mkuu ilikuwa imeshatoa taarifa kuwa uteuzi wa Ntibenda umetenguliwa na nafasi yake imechukuliwa na Mrisho Gambo ambaye aliteuliwa hivi karibuni kuwa mkuu wa Wilaya ya Arusha.

Taarifa hiyo ya Ofisi ya Waziri Mkuu haikueleza sababu za kutenguliwa uteuzi wa Ntibenda ambaye amekuwa Arusha tangu mwaka 2014.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Ntibenda, ambaye alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Karatu kabla ya kuteuliwa kushika wadhifa huo mwaka 2014, amehamishiwa ofisi ya Waziri Mkuu ambako atapangiwa kazi nyingine.

Jana, Ntibenda alikuwa akisubiriwa kufungua mkutano wa shirika la kimataifa la afya kwa vijana (AMREF) na tayari tangu asubuhi alikuwa ofisini kwake kujiandaa kwa majukumu hayo ya siku.

Mbali na mkutano huo, Ntibenda alitarajiwa kushiriki kama mwenyeji katika mkutano wa Mfuko wa Maendeleo (Tasaf) ambao ulishirikisha wakuu wote wa mikoa ya Kanda ya Kaskazini pamoja na wakuu wa wilaya.

Kwenye mkutano wa AMREF, Ntibenda alisubiriwa kwa muda mrefu hadi habari za kutenguliwa kwa uteuzi wake ziliposambaa, ndipo akateuliwa mganga mkuu wa mkoa, Frida Mokiti kufungua mkutano huo.

Habari za uhakika kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa zinasema kuwa kabla ya kuibuka kwa taarifa za kutenguliwa kwake, Ntibenda alikuwa na mazungumzo na Gambo ofisini kwake.

Haikujulikana mara moja mambo waliyozungumza wawili hao, ingawa tangu Ntibenda ateuliwe kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha kumekuwa na utulivu wa kisiasa.

Ntibenda alikuwa kwenye mzozo na viongozi wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), ambao walikuwa wakimlalamikia kuingilia majukumu ya jumuiya hiyo.

Mwenyekiti wa UVCCM wa mkoa, Lengai ole Sabaya aliwaambia waandishi wa habari mapema wiki iliyopita wakati akisoma maazimo ya kamati ya utekelezaji, kuwa mkuu huyo anakwamisha utendaji wao.

Katika taarifa hiyo UVCCM ilisema kitendo cha Ntibenda kuingilia kati sakata la mikataba ya wapangaji katika maduka ya jumuiya hiyo ni kuwakwamisha.

Baadaye kundi la viongozi hao wa UVCCM pia lilidaiwa kuandika barua ya kumlalamikia Ntibenda kutokana na kutoridhishwa na utendaji wake.

Hata hivyo, Ntibenda alikanusha tuhuma zote za UVCCM kumtetea mmoja wa wapangaji na kusema anasikitishwa na madai hayo dhidi yake.

Vijana CCM wafurahia

uteuzi wa Gambo

Wakati Ntibenda akienguliwa, baadhi ya viongozi wa UVCCM jana walikuwa wenye furaha baada ya Gambo kupandishwa cheo.

Mbunge wa viti maalumu, Catherine Magige alimpongeza Rais Magufuli kwa uteuzi wa Gambo ambaye alisema ni zao la jumuiya hiyo.

Magige alisema uteuzi huo unaonyesha jinsi gani Rais Magufuli alivyo na imani na vijana na akawataka kuendelea kumuunga mkono.

“Tunaamini Gambo ataleta mabadiliko makubwa ya utendaji katika Mkoa wa Arusha kwa kuwa ni mchapakazi,” alisema.

Wakati Magige akisema hayo, Ole Sabaya alisema Rais Magufuli amesikia kilio chao.

“UVCCM tulikuwa na malalamiko juu ya utendaji wa mkuu wa mkoa, sasa tunashukuru sana Rais Magufuli kusikiliza kilio chetu,” alisema Ole Sabaya.

Lema asikitishwa

kuondolewa Ntibenda

Lakini hali ilikuwa tofauti kwa mbunge wa Arusha, Godbless Lema aliyesema anaona vurugu zikirudi na kwamba uteuzi wa Gambo ni kama mkakati wa kuhakikisha wapinzani wanasambaratishwa mkoani Arusha ambako ni moja ya ngome za Chadema.

Lema, ambaye amekuwa katika mgogoro na Gambo katika siku za karibuni, alisema kada huyo ameteuliwa ili kuidhibiti Chadema, jambo ambalo chama hicho hakitakubali.

“Hivi karibuni nilimwambia mkuu wa mkoa Ntibenda kuna watu wanakutafuta, sasa wamefanikiwa. Lakini mimi naona Arusha ijayo itakuwa na vurugu tofauti na utulivu uliopo sasa,” alisema.

Hata hivyo, alisema Chadema imejipanga kuendelea kufanya siasa za kistaarabu na kamwe haitakubali kuhujumiwa na mtu yeyote yule.

Gambo ahudhuria mkutano

Alipotafutwa jana asubuhi, Gambo alisema hana cha kuzungumza na kwamba hakuwa na taarifa rasmi.

Gambo, ambaye jana alishiriki mkutano wa Tasaf kwa nafasi yake ya mkuu wa Wilaya ya Arusha na baadaye kuondoka, alisema alikuwa hajapata taarifa rasmi.

Hata hivyo, akiwa kwenye mkutano baadhi ya wakuu wa mkoa na wakuu wa wilaya za mikoa ya Kanda ya Kaskazini, walimpongeza kwa uteuzi huo.

RAS azungumzia uteuzi

Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Richard Kwitega alisema alipata taarifa za uteuzi huo jana asubuhi na alipata maelekezo kuwa Gambo anatakiwa Dar es Salaam.

“Nilipata taarifa rasmi ya uteuzi wake na tayari tulikuwa naye hapa ofisini ili kuweka taratibu za kwenda kuapishwa,” alisema.

Alisema Gambo atarejea Jumamosi na atapokewa na wafanyakazi na baadaye kushiriki mapokezi ya Mwenge wa Uhuru wilayani Ngorongoro.

Mwananchi

Je Unapenda Kuwa na Makalio na Miguu Mizuri ? Markson Beauty Products Zipo Hapa Kwa Ajili yako

0
0
HABARI NJEMA MARKSON BEAUTY PRODUCTS
Baada ya kupata cheti cha bidhaa bora kwa mwaka 2015-2016, Sasa kampuni hii inasambaza huduma zake ndani na nje ya nchi kwa vibali maalum. Bidhaa zetu zimetengenezwa kwa mimea na matunda na kudhibitishwa. Hazina kemikali wala madhara. DAWA ZETU NI YA:-

  1. kurefusha nywele na kuzuia kukatika ovyo @100,000/=
  2. Kuongeza shepu (hips na makalio) kwa/= (a)Dawa ya kunywa au kupaka @150,000/=(b)Vidonge @170,000/=
  3. Kuwa mweupe na softi mwili mzima kwa:- (1)Mafuta @100,000/= (11)Vidonge @150,000/=
  4. Kupunguza unene na manyama uzembe @120,000/=
  5. Kuongeza uume pamoja na nguvu za kiume kwa:-(a) Gely ya kupaka @100,000/= (b) Vidonge maalum @120,000/= (c) Handsome up original @170,000
  6. Kuondoa mvi milele zisiludi tena @100,000/=
  7. Kuongeza unene wa mwili mzima na uzito @120,000/=
  8. Kupunguza tumbo (kitambi) na nyama za pembeni kwa:- (a) Dawa ya kunywa au kupaka @120,000/= (b) Mkanda wa kawaida @100,000/= (c) micro-computer belt unaovaibret @200,000/=
  9. Kupunguza maziwa na kuyasimamisha @90,000/=
  10. Kushepu miguu na kuwa minene @100,000/=
  11. Kuondoa mipasuko mwilini (michirizi) @90,000/=
  12. kubana uke na kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa mwanamke @100,000/=
  13. Taiti za hips na makalio @150,000/=           
NB: Hakikisha unapata risiti yenye muhuri halisi wa MARKSON CO pamoja na garantii kwa bidhaa halisi. Wasiliana nasi :-(+255) 0767447444 na 0714335378 Google MARKSON BEAUTY.
Follow us
@Markson_beauty_pr
@Markson_beauty_pr

Mahakama Yamwamuru Reginald Mengi Afike Kujieleza ni Kwa nini Asifungwe Gerezani Kwa Kupuuza Hukumu ya Mahakamagwe

0
0
MAHAKAMA Kuu Kitengo cha Biashara imeamuru Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi afike mahakamani kujieleza kwa nini asifungwe gerezani kwa kushindwa kutekeleza hukumu inayohusu malipo ya Sh bilioni 1.2.

Mengi anatakiwa kufika mahakamani hapo Agosti 24, mwaka huu kujieleza kutokana na kushindwa kutekeleza hukumu iliyomtaka kuwalipa wafanyabiashara watatu, Muganyizi Lutagwaba, Eric Mshauri na Charles Mgweo,  Sh bilioni 1.2.

Alitakiwa kuwalipa fedha hizo kutokana na mgogoro wa malipo ya uuzwaji wa hisa katika Kampuni ya Douglas Lake Minerals Ltd ambayo kwa sasa inaitwa Handeni Gold Inc.

Kwa mujibu wa hati ya wito wa kufika mahakamani, Mengi anatakiwa kufika mahakamani hapo Agosti 24, mwaka huu ili ajieleze kwa nini asifungwe gerezani kama mfungwa wa madai kama sehemu ya kukazia hukumu hiyo.

Mahakama imetoa hati hiyo kutokana na wafanyabiashara hao kuwasilisha maombi katika hatua ya kukazia hukumu iliyotolewa Januari 28, mwaka huu na Jaji Agathon Nchimbi wa mahakama hiyo.

Katika hati ya kiapo ya wafanyabiashara hao, inadaiwa walifungua kesi dhidi ya Mengi na Kampuni ya K.M. Prospecting Limited, wakidai malipo yaliyokuwa yamebakia ya dola 428,750, 100,000 na 70,000, kwa kila mmoja.

Masanja asema Orijino Komedi imemalizana na polisi, ni issue ya kuvaa sare za polisi

0
0
Baada ya Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam kuwakamata baadhi ya wasanii wa Kundi la Orijino Komedi kwa kosa la kuvaa mavazi yanayoshabihiana na sare za polisi, mmoja wa wasanii wa kundi hilo, Masanja Mkandamizaji amedai tayari wameshamalizana na jeshi hilo baada ya kuomba msamaha.

Mchekeshaji huyo ambaye kwa sasa yupo honey moon visiwani Zanzibar, amesema ameamua kutoa taarifa hiyo ili kuwaondoa hofu baadhi ya mashabiki pamoja na ndugu.

“Jamani asanteni kwa maombi na meseji zenu kuulizia juu ya inshu ya polisi, tunamshukuru mungu tumewaomba msamaha na wametusamehe hivyo imekwisha,” aliandika Masanja facebook.

Aliongeza, “Tumesema tulinogewa na harusi tukasahau kwenda kuomba kibali. Lakini akina Joti, Seki, Maclegan,na Wakuvanga wamepata kautamu kidogo kamahojiano. Na mimi ningekuwa kwenye jiji la Makonda ingenihusu,”

Wasanii hao walikamatwa na jeshi la polisi na kuhojiwa baada ya kuvaa sare zinazofanana ya za jeshi la polisi katika harusi ya msanii mwenzao Masanja Mkanadamizaji.

Barua kwa Mheshimiwa Waziri Nape Nnauye

0
0
Habari mheshimiwa waziri, nina imani ni mzima wa afya, pole na hongera kwa kazi ngumu unayofanya kwa moyo mmoja katika wizara yako. Mimi ni kati ya wananchi tuliojiajiri katika tasnia ya filamu hapa nchini, japo hali ni mbaya mno lakini tunaendelea kujikongoja hivyo hivyo tukisubiri uharamia ukomeshwe kwa asilimia kubwa ili tupumue kidogo kama watu wa shuguli zingine za kiuchumi.


Mheshimiwa kisa cha kushika hii kalamu ni baada ya kusoma habari za kukamatwa kwa vijana wa Orijino Komedi hapo majuzi kwa kosa la kuvaa sare za jeshi la polisi kitendo ambacho ni kinyume na sheria za nchi yetu. Lengo ni kuzungumzia hilo suala ila kwakuwa hii nafasi ya kuongea na wewe ni adimu, acha nitaongeza na mengine kidogo nje ya suala la sare.

Mheshimiwa mlivyosema kurasimisha tasnia ya filamu nina imani mlimaanisha kwa ujumla wake, lakini kuna kipindi nashawishika kuwa maana ya kurasimisha iliishia kwenye kuweka stika za TRA kwenye kava za DVD basi. Maana mi ninaamini kama tasnia ingerasimishwa katika ujumla wake na ikafuatiliwa haswa, mpaka muda huu tungekuwa pazuri maana muda umepita kidogo mheshimiwa

Kwa suala la sare mheshimiwa ni kitu kidogo mno ambacho kama kweli kuna urasimishaji, kusingekuwa na tatizo kama la Orijino Komedi sasa hivi. Najua kuna wazo linaweza kuja kuwa wale mabwana wamevaa kwenye harusi kwahiyo wana makosa na hoja yangu kuwa sio ya msingi hapa. Orijino Komedi wanajulikana kazi yao na pale walikuwepo kazini bila kujali walilipwa au walimfanyia free mwenzao. Ile ni kazi ya sanaa, ila cha muhimu wamefanya kitu ambacho wamezua mjadala na labda tuombe Mungu ndio uwe mwanzo wa kujadili kati ya wadau wa filamu na serikali kuhusu mambo hayo ambayo ndio mjumuiko sahihi wa maana ya urasimishaji.

Nilisema sare ni jambo rahisi kwa sababu tunataka hadi silaha zenyewe, sio sare tu. katika filamu kuna kutumia bunduki zenyewe au za bandia zinazofanana na za halisi(pellets guns), mheshimiwa tunahitaji vituo halisi vya polisi kabla hatujaanza kujenga spesho kwa ajili ya filamu, tunabezwa filamu zetu hazina uhalisia kwakuwa selo zetu watazamaji wetu wanajua kabisa sio selo bali ni dukani kwa Mangi!

Mheshimiwa majiji kama New York, idara ya polisi (New York Police Department /NYPD) wana kitengo kipo maalum kwa ajili ya kutoa msaada kwa filamu, iwe sare, silaha, vituo vya polisi, mahakama, helikopta na hata polisi wenyewe ikitakiwa watumike na vingine vingi na kuweka polisi kadhaa katika location kufuatilia.

Mheshimiwa, New York, Los Angeles na majiji mengine huko Marekani na Ulaya nimeenda mbali, hapa jirani yetu Afrika ya Kusini hata ukikitaka kituo cha polisi wanakutajia bei ukilipa wanahamia uani mheshimiwa. Siongei mambo ya kijiweni. Nina uhakika na ninachoongea, kumbukumbu zangu za mwisho ilikuwa 2011 Afrika Kusini ukitaka helikopta ya polisi ilikuwa milioni mbili kwa saa, kumkodi polisi mmoja na sare zake ilikuwa shilingi 130,000 kwa saa. Gari la polisi ilikuwa laki mbili kasoro kidogo kwa saa. Ila pia unaweza kuomba kibali ukaweka helikopta yeyote stika ya polisi, au hata magari. Mheshimiwa, serikali ya Afrika Kusini inatoa ushirikiano wa ajabu katika filamu, cha kushangaza zaidi wizara ya viwanda na biashara wana kitengo cha kukopesha hela kwa wazalishaji ili watengeneze filamu.

Mheshimiwa waziri, serikali ya Ufilipino ikimkuta mtu na kosa la kuvaa sare za polisi (Philippines National Police /PNP) inamfunga jela miaka minne na miezi miwili, lakini waigizaji wameruhusiwa kuvaa sare hizo katika kazi zao. Mgogoro umetokea hapo majuzi baada ya muigizaji kuigiza akisaula sare hizo katika muziki mbele za watu, ndani ya tamthilia iitwayo ‘On the Wings of Love.’ Kwahiyo mheshimiwa, waigizaji waruhusiwe ila kwa masharti maalum kama walivyofanya PNP Ufilipino.

Mheshimiwa, sisemi kila muigizaji au kampuni ya uzalishaji iwe na sare au silaha la hasha, iwepo kampuni itakayoaminiwa na serikali au kitengo katika wizara yako ambacho kitakuwa na mamlaka ya kumiliki silaha, sare za polisi trafiki na kadhalika ambapo wazalishaji watakuwa wanaenda kukodi kwa gharama nafuu na pia kinasimamia maeneo ambayo vifaa hivyo vinatumika. Vitu hivyo vinaonekana ni vitu vidogo lakini ukweli hufanya filamu ziwe na msisimko wa kipekee.

Mheshimiwa waziri, serikali ikisema kurasimisha tasnia ya filamu isimaanishe kukusanya kodi tu peke yake, bali dhamira kuu iwe kuinua filamu na kodi itapatikana, maAna hata hizo stika za TRA imekuwa ni tisha toto tu maana wezi wapo wengi na wanajua stika zimewekwa kwa mikwara hakuna anayezifuatilia. Tangu tasnia irasimishwe filamu ndio hamna biashara kabisaaa afadhali hata kabla.

Kazi ya kufanya filamu ziuzike na wahusika tunufaike na serikali ipate kodi yake ni kazi ndogo mno, ilimradi serikali iamue tu mheshimiwa. Naomba wizara yako iamue sasa ili tunufaike na uwezo wetu tuliopewa na mwenyezi Mungu.

Nawapa pole Orijino Komedi kwa matatizo yaliyowakuta, lakini nashukuru pia maana imekuwa ni njia moja wapo ya kulizungumzia na kulipa umakini jambo hili, kama kifo cha Kanumba kilivyotuumiza lakini ikawa ni njia iliyofanya serikali istuke na igundue nguvu ya sanaa katika jamii.

Mheshimiwa naomba uwasaidie vijana wa Orijino Komedi wasamehewe na uliweke sawa jambo hili, tunataka sare, silaha, vituo vya polisi, mahakama, kufunga mitaa wakati tunashuti barabarani na mambo mengine mengi.Mheshimiwa kuigiza vizuri hakupeleki sanaa ya filamu kokote kama hakuna vitu vya uhalisia ndani ya filamu hizo.

Nashukuru kwa kutumia muda wako kusoma waraka huu mheshimiwa waziri, kwa uchapakazi wako nina imani tasnia yetu ya filamu itafika mbali kwa wakati huu ambapo ipo katika mikono yako. Asante.

Paul Sekaboyi 0753 666 444

Olimpiki: Mwanariadha wa Kenya Apokonywa Medali Kwa Kosa la Udanganyifu

0
0
Mwanariadha kutoka nchini Kenya aliyeshinda medali ya shaba kwenye riadha na kuruka vihunzi pamoja na maji, Ezekiel Kemboi amepokonywa medali yake kwa kosa la udanganyifu mchezoni kwenye mashindano ya Olimpiki yanayoendelea huko nchini Brazil.

Kemboi (34) alimaliza kwenye nafasi ya tatu ya mashindano hayo ya kukimbia ya mita 3000 kwa kutumia muda wa 8:08.47. Ufaransa ilipinga ushindi huo wa Kemboi kwa kukata rufaa baada ya kubainika kuwa mwanariadha huyo wakati akiendelea na mbio hizo baada ya kuruka kiunzi na maji, alikanyaga nje ya mstari.

Kamati ya mashindano hayo imekubali rufaa hiyo na kuamuru kumpatia medali hiyo ya shaba, Mahiedine Mekhissi kutoka Ufaransa aliyeshika nafasi ya nne baada ya kukimbia kwa muda wa 8:11.52.

Hata hivyo Kemboi ambaye alikuwa bingwa wa mbio hizo kwenye mashindano ya Olimpiki ya 2012 ya nchini Uingereza amedaiwa kutangaza kustaafu kucheza mchezo huo.

Jifunze Haya Wewe Mwanamke Uliye Single

0
0
1- Kamwe usisahau kumuomba Mungu wako kabla hujasema "YES" kwa yule unaedhani anapaswa kujenga maisha na wewe. Usikimbilie kuolewa. Kama utakimbilia kuolewa, utaikimbia ndoa na tena kwa majeraha makubwa.

2- Tambua lengo lako kabla hujaingia kwenye ndoa. Fanya biashara yoyote, tafuta shughuli ya kufanya. Usimsubiri mwanaume ndio useme unaanza maisha. Ongeza thamani ya maisha yako kwa kujenga maisha yako.

3- Usimkimbilie mwanaume kwa sababu ya pesa zake, magari, connection, cheo, kipaji, ucheshi, au background ya familia yake. Olewa na mwanaume aliye na hofu ya Mungu. Hapo utakua umekula BINGO...!

4- Jenga tabia ya kula vizuri kwa afya. Usile alimradi umekula. Kula vyakula vya kujenga mwili na uwe mlo kamili. Fanya mazoezi mara kwa mara kuepuka unene usio wa lazima.

5- Vaa vizuri. "first impression counts" hii inamaanisha kwamba muonekano wa mwanzo unamaana sana kwa mtu atakayekuona. Usiache maeneo yako ya siri yakaonwa na mwanaume yeyote, vinginevyo utawavutia wale wanaume wakware ambao sio waoaji.

6- Usililie au kulazimisha mwanaume akuoe. Wewe ni wa thamani mno kufanya hivyo. Usilazimishe ndoa kwa kumbebea mimba, wenzako wamefanya hivyo na leo wengi wao wanajuta. Wamebaki wakilea peke yao.

7- Tabia yako ndio Ndoa yako. Hiyo ndio itakayoamua mwanaume aishi na wewe au laa. Jitathimini tabia yako. Uzuri sio kila kitu, kama unajivunia na uzuri wako na unaamini kama ndio utakaokupa mume utapoteza nafasi yako kwa aliye mzuri zaidi yako kwa tabia na sura.

8- Usichoke kujifunza kupika, kujua kupika wali, ugali, mboga na chapati haitoshi. Jifunze zaidi, tizama vipindi vya mapishi, soma vitabu mbalimbali vya mapishi, tembelea page mbalimbali zinazofundisha kupika vyakula aina mbalimbali.

Wanaume mara nyingi wanapenda wanawake wanaojua kupika, wale ambao kila siku wana suprise ya aina mpya ya mapishi. Kwa sababu njia nyingine rahisi ya kutambua moyo wa mwanaume ni kupitia tumbo lake (chakula kizuri)

9- Usiishi kwa mazoea utakapoolewa, soma vitabu vya mahusiano, ndoa na familia. Ongea na wazazi wako na wazee wengine wakupe busara zao. Kupitia kwao akili itaweza kupanuka na kupata ufahamu wa nani haswa atapaswa kuishi na wewe.

10- Acha ushabiki kwenye mitandao ya kijamii mambo ya Team Zari, Team Wema, Team Chura, na mengineyo hayatakusaidia. Wenzako wana maisha yao, muda huo tumia kuhudhuria semina mbalimbali za ndoa, tembelea washauri wa mahusiano na ndoa.

Msome Chriss Mauki, Tweve Hezron, Eliado Tarimo, Prince Naahjum Alsina na wengineo kwa dondoo mbalimbali za mahusiano, kupitia huko ufahamu wako waweza kuongezeka kwa kiasi fulani, hii itaepusha sana kuja kuishi kwa mazoea.

******************

Ni hayo tu sina la ziada, Binafsi wanawake nawakubali sana, sijui kwanini...!? labda kupitia ujasiri wa mama yangu. Ninafahamu kupitia ninyi tunaweza tukawa na familia bora ambako huko ndiko maadili ya taifa huanzia.

Heshima ya mwanamke ni NDOA, heshima ya mwanaume ni MAJUKUMU.

Life is full of joy, Enjoy it!

PRINCE NAAHJUM ALSINA
The Great Pioneer

Wema Akanusha Kurudiana na Diamond, Awasifia Zari na Tiffah

0
0
Wema, Diamond na Zari
Mambo mengi yametokea wiki hii kuanzia Wema Sepetu kuachana na mpenzi wake Idris Sultan hadi Miss Tanzania huyo wa mwaka 2016 kuhudhuria birthday party ya binamu wa Diamond, Romeo na kukutana na vijana wa WCB.


Kutokana na Wema kujumuika na vijana wa himaya ya WCB, kumezuka tetesi kuwa huenda ukaribu kati ya muigizaji huyo na Diamond unaweza ukawa ni zaidi ya maex wawili walioamua kuacha bifu zao zipite.

“Yaani watu wakianza tu kuongea vizuri, bifu zao zikiisha wamerudiana, maisha lazima yaendelee, mwisho wa siku hatuwezi kuwa tunakaa tunachuniana miaka yote tutakayoishi, life is too short,” Wema alimweleza Soudy Brown kupitia U Heard ya Clouds FM.

“Mimi mwenyewe najisikia hadi amani kwamba there is no beef, maisha yanaendelea, mimi sijarudiana na Diamond, mimi namrespect kama msanii, nampenda Diamond kama msanii and I love his music and I am so glad tumeweka all this behind,” aliongeza.

Kuhusu kama anampenda mtoto wa Diamond, Tiffah, Wema alisema, “Tiffah amenikosea nini katika maisha yangu? Nimchukie Tiffah si nitakuwa mwendawazimu jamani,” alisisitiza.

Kuhusu tetesi kuwa aliwahi kumuita Tiffah zombie kama Zari alivyowahi kudai lakini Wema amezikanusha, “Hayo maneno sio ya kwangu, sijawahi hata siku moja, kwanza the way I adore babies, siwezi nikamuita baby zombie hata awe vipi.”

Kuhusu Zari staa huyo alisisitiza kuwa hana bifu naye.

“Mimi sina bifu na Zari na sijawahi kuwa na bifu na mwanamke wake yeyote Nasib, kwasababu huwa naona matatizo yangu mimi na Nasib ni mimi na yeye, Zari hana makosa, katongozwa, amedetiwa, amewekwa ndani, hana makosa hata kidogo huyo mwanamke.”

Ajali Yaua 1 Maeneo ya Mlimani City Dar

0
0
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilitokea ajali mbaya ya gari ndogo ambayo haikuweza kufahamika kwa haraka kutokana na kugongwa na lori lililovuka na kuingia hadi kituo cha mafuta kilichopo jirani na mataa hayo.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo, gari ndogo ilikuwa ikiendeshwa na mwanamke ambaye mwili wake haukuweza kuokolewa kutokana na kubanwa.

Alipopigiwa simu ili kufafanua kama amepata taarifa za ajali hiyo, Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kinondoni amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa mtu mmoja ndiye aliyefariki na kueleza kuwa yupo kwenye kikao hivyo taarifa kamili ataitoa baadaye.

Viewing all 104414 articles
Browse latest View live




Latest Images