Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104712 articles
Browse latest View live

Tundu Lissu Aibwaga Serikali Mahakamani

$
0
0
Serikali imeendelea kupigwa mweleka katika kesi ya uchochezi dhidi ya mshitakiwa Tundu Lissu baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutupa pingamizi la Wakili wa Serikali wakitaka wakili Peter Kibatala kujitoa kumtetea mwanasiasa huyo.

Lissu, ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki kwa tiketi ya Chadema alipandishwa kizimbani Agosti 5, na kusomewa mashtaka matatu, mawili kati yake yakiwa ni ya uchochezi na moja la kuidharau mahakama.

Pigo la kwanza la upande wa mashtaka ni pale Lissu alipopangua hoja na kufanikiwa kupata dhamana, wakati kesi hiyo ilipofikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza.

Jana ilikuwa ushindi mwingine kwa upande wa utetezi, baada ya Mahakama kutupa pingamizi la upande wa mashtaka lililotaka Kibatala ajitoe katika jopo la mawakili wanaomtetea Lissu.

Upande wa mashtaka ulioongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi, uliweka pingamizi hilo kwa maelezo Kibatala ni shahidi wao kwa kuwa alikuwapo siku na mahali wakati Lissu akitoa maneno yanayodaiwa ya uchochezi.

Wakili Kibatala ambaye ni kiongozi wa jopo la mawakili wanaomtetea Lissu, alipinga hoja za Serikali za kutaka ajitoe katika kesi hiyo, mvutano ambao ulisababisha kesi hiyo kuahirishwa mara mbili.

Wakili Kibatala alipinga kuwa hakuna kifungu cha sheria kinachomzuia wakili kumtetea mteja wake kwa sababu tu ya kushuhudia akitoa maelezo yake Polisi.

Akitoa uamuzi wa pingamizi hilo la Serikali, Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha anayesikiliza kesi hiyo, hakukubaliana na hoja za upande wa Jamhuri (mashtaka) na hivyo akalitupa pingamizi hilo.

Hakimu Mkeha alikubaliana na hoja za wakili Kibatala kuwa hakuna kifungu chochote cha sheria kinachomzuia kumtetea Lissu.

Alisisitiza kuwa Kibatala ataendelea kuwa wakili wa Lissu katika kesi hiyo na kwamba kama upande wa mashtaka ukimhitaji awe shahidi wao utalazimika kumuomba. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 19.


Mwili wa Mtoto Albino Wafukuliwa Kwa Uchunguzi

$
0
0
MWILI wa mtoto mwenye albinism aliyefariki kwa maradhi hivi karibuni na kuzikwa Jumapili iliyopita, umefukuliwa chini ya ulinzi wa polisi ili ufanyiwe uchunguzi kutokana na kuibuka maneno yenye kutatanisha kuwa wakati akiugua alikuwa akivuja damu nyingi puani na kuvimba mwili.

Mtoto huyo, Michael Juma aliyekuwa na umri wa miaka miwili na nusu, alizikwa pembeni mwa nyumba yao Alhamisi wiki hii katika kijiji cha Bunambiyu, wilayani hapa na kuwashangaza wakazi wa eneo hilo.

Katibu wa Chama cha Watu Wenye Albino Nchini (TAS), tawi la mkoa wa Shinyanga, Lazaro Anael alisema kitendo cha kuufukua mwili kimewashangaza na kwamba tangu taarifa za kifo cha mtoto huyo kujulikana, yamezuka maneno kuwa kifo hicho kina utata.

Alisema alishiriki mazishi, lakini kabla ya kufika nyumbani kwa wazazi wa mtoto huyo akiambatana na Mkurugenzi wa Shirika la Under the Same Sun, Vicky Mtetema, waliukagua mwili wa mtoto huyo na kubaini haukuwa na tatizo.

“Mimi nasema hivi maneno haya yanatoka wapi wakati mwili tuliukagua haukuwa na dosari yoyote wakati huo tulikuwa na Vicky Mtetema akiwa anaupiga mwili picha, viongozi wa kijiji na kata walikuwepo pamoja na majirani wakishuhudia kuwa salama na ndipo shughuli za maziko zilifanyika… sasa kitendo cha kufukua mwili hapo serikali inataka kuleta hofu,” alisema.

Diwani wa Kata ya Bunambiyu, Richard Sangisangi aliyekuwa amekataa mwili huo kufukuliwa na kugoma kuwaita majirani kwa ajili ya kufukua mwili ili ufanyiwe uchunguzi aliondoka na kusema kamwe hawezi kuchuma dhambi kwa kile alichokieleza walishuhudia mwili ukiwa salama na alifariki kwa mapenzi ya Mungu sio ushirikina au kukatwa mapanga kama ilivyozoeleka maeneo mengine.

Mwenyekiti wa kijiji hicho, Jonathan Katela alisema kitendo cha kufukua mwili huo sawa na kurudisha majonzi kwa jamii na familia, lakini akasisitiza ameridhia kwa kuwa serikali imetaka mwili ufukuliwe kwa uchunguzi.

Kauli kama hiyo ilitolewa na baba wa marehemu, Juma Masudi aliyesema ametii amri ya serikali, lakini yeye binafsi hakuridhika kuufukua mwili wa mwanawe aliyedai aliugua maradhi ya kawaida na kupata matibabu kituo cha afya Bunambiyu.

Hata hivyo, baada ya mvutano, polisi walifanikiwa kufukua mwili huku Dk Hellen Kaunda aliyekuwepo eneo la tukio akiufanyia uchunguzi na kueleza haukuwa na dosari yoyote na kwamba alifariki kwa maradhi.

Msafara wa Polisi, Kitengo cha Upelelezi wilayani Kishapu kupitia msemaji wake kwenye eneo la tukio, Meshack Sumuni aliwaomba radhi wananchi na wazazi huku akiwatoa hofu kwa kitendo cha kufukua kaburi kuwa ni jambo la kawaida unapotoa utata.

Kesi ya CHADEMA kutaka maandamano na mikutano yatupwa.

$
0
0
HATIMAYE Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es Salaam, imelikataa ombi la kuiomba Mahakama hiyo iwapatie Kibali cha Kufungua mahakamani hapo ombi la kuomba Mahakama hiyo iifute amri /uamuzi wa Inspekta Jenerali wa Polisi Ernest Mangu ya kuzuia maandamano na mikutano ya kisiasa nchini kwasababu ya dosari za kisheria .

Uamuzi huo ulitolewa Juzi na Jaji Kiongozi Fredinand Wambali wakati Katika ombi Na. 52/2016 lililowasilishwa Mbele yake na Baraza la Udhamini la Chadema lilokuwa kikitetewa na wakili wa kujitegemea Peter Kibatara dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Inspekta Jenerali wa Polisi waliokuwa wakitetewa na Mawakili wa serikali Haruna Matagane na Daniel Nyakeha.

Jaji Wambali alisema mlalamikaji alikuwa na Maombi mawili.Ombi la kwanza Chadema ilikuwa ikiomba Mahakama hiyo iwapatie Kibali cha Kufungua Kesi ya kupinga amri na uamuzi wa IGP wa Kuzuia mikutano na maandano ya vyama Vya siasa nchini na ombi la pili waliomba Mahakama hiyo itoe tamko la Kusema amri na uamuzi Huo wa IGP Si halali kisheria.

Uamuzi huo ulitolewa Juzi na Jaji Kiongozi Fredinand Wambali ambapo alisema amekubaliana mapingamizi yaliyowasilishwa na upande wa utetezi kwamba huwezi kuomba amri ya mapitio ya amri ya IGP Mahakamani hapo wakati mlalamikaji alikuwa na Mlango mwingine wa kupinga amri ya IGP na Mlango huo ni kwa mlalamikaji Kupenda kupinga amri ya IGP kwa Waziri wa Mambo ya Ndani na alishindwa kufanya hivyo.

" Chadema walipaswa kukatia rufaa amri hiyo ya IGP ya Kuzuia maandamano ya vyama Vya siasa Kwa Waziri wa Mambo ya Ndani na sio kwenda kushitaki mahakamani' alisema Jaji Wambali na hiyo ikapatikana Katika Kifungu Cha 43(6) sura 322 ya Mwaka 2002 ya Judicial Review .

Aidha Jaji Wambali alisema anakubaliana na pingamizi la pili la Mawakili wa serikali ambalo lilidai Kuwa ombi Hilo la Chadema litupwe kwasababu ombi Hilo la Chadema halikuambatanishwa na maelezo ya mlalamikaji na hayo maelezo yakidhi matakwa ya Kanuni ya 5(2) of The Judicial Reviews Rules of 2014 ambayo inataka hiyo hati ya mlalamikaji ifafanue maelezo na jina la mlalamikaji.

" Chadema Katika shauri Hili hayo yote walishindwa kuyafanya hivyo Mahakama hii inatupilia Mbali ombi Lao la kutaka Mahakama hii itamke amri ya IGP Kuzuia maandamano ni batiri kwa gharama kwasababu ombi la Mlalamikaji halijakidhi matakwa ya kisheria.

CHADEMA pia wameamuliwa kulipa gharama za kesi.

Zijue Sababu za Kwa Nini Tunazima Simu Ndege Inapotaka Kupaa na Kutua

$
0
0
Najua kama ni mtumiaji wa usafiri wa ndege utakuwa ushasikia taratibu za abiria kuzima simu wakati ndege inataka kupaa na kutua ila huenda hukawa hujui sababu kwa nini unatakiwa kufanya hivyo, inawezekana ulishajiuliza usipozima unaweza kusababisha ndege kupata ajali au? jibu ni Hapana, isipokuwa unaweza kusababisha muingiliano wa mawasiliano kati ya rubani na waongozaji.

Vibrations au miungurumo ya simu na vifaa vingine vya electronics vinahusika kwa kiasi kikubwa kuvuruga mawasiliano mazuri kati ya rubani na wanaomuongoza, hivyo huwa tunashauriwa kuzima simu na vifaa vingine vya electronics wakati wa kupaa na kutua kwa ndege. Hiyo ni moja kati ya sababu kuu zilizotajwa juu ya swali la ”Kwanini tuzime simu wakati ndege inaporuka na kutua”?.

Watakaochakachua Mitihani Kidato cha Nne Kukiona

$
0
0
WAZIRI wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako amesema haafiki uchakachuaji kwenye mitihani na kusema wakuu wa shule watakaobainika kufanya udanganyifu huo hawatapona.

Profesa Ndalichako alisema hayo kwenye kikao kati ya Ofisi ya Rais, Tamisemi, Maofisa Elimu wa Mikoa, Wakuu wa shule kongwe na wakuu wa shule zilizoungua moto.

Alisema ikiwa imebaki miezi mitatu kwa wanafunzi wa kidato cha nne kufanya mitihani aliwataka wakuu wa shule kujipanga kupata ufaulu mzuri.

“Bado siafiki suala la uchakachuaji kwenye mitihani wanafunzi waachwe wafanye mitihani wenyewe na si kupitia kamati za ufundi, sasa Wizara inaangalia ubora wa elimu na wakuu wa shule watakaokiuka agizo hilo watachukuliwa hatua,” alisema.

Alisema pia matokeo ya mitihani ya shule za sekondari ya mwaka jana yalimhuzunisha sana lakini anaamini wakuu wa shule watajipanga kuhakikisha wanafunzi wanafanya vizuri zaidi.

“Nilipokuwa Baraza la Mitihani nilisema nisiulizwe kutokana na matokeo kuwa mabaya lakini sasa niko Wizara ya Elimu siwezi kukwepa hilo tena,” alisema.

Waziri Ndalichako alisema watabadilisha mfumo wa namna maofisa elimu watakavyofanya kazi zao ili kuongeza kiwango cha ufaulu katika shule za serikali na kuwataka wakuu wa shule na maofisa elimu kila mmoja ajipange.

Aidha alisema mkuu wa shule ni mdhibiti wa taaluma katika eneo lake na hatakiwi kumuogopa mtu anayemuongoza. Waziri huyo pia alisema katika mtihani wa kidato cha sita uliopita shule 100 za kwanza shule za serikali zilikuwa tatu na kuwa nafasi ya 53 ndio ilishikwa na Ilboru ya Arusha.

“Mpaka namba 100 shule za serikali ni tatu tu, sio kitu cha kawaida hapa ndio mahali pa kuzungumza kama serikali tunashindwa kuonesha mfano tuachie sekta binafsi,” alisema

Zlatan Ibrahimovic Aipa Man United Ushindi Dhidi ya Southampton

$
0
0
Ligi Kuu England iliendelea usiku wa August 19 kwa klabu ya Man United kuwakabribisha Southampton katika dimba lao la Old Trafford kucheza mchezo wao wa pili wa baada ya mchezo wao wa awali kuibuka na ushindi wa goli 3-1 dhidi ya AFC Bournemouth ugenini.

Zlatan lifunga goli la kwanza baada ya kupokea krosi maridhawa kutoka upande wa kulia na Wayne Rooney baadae tena Zlatan alifunga bao la pili kwa njia ya penati baada ya beki wa kushoto wa Man United Luke Shaw kufanyiwa madhambi na Jordy Clasie na mechi hiyo kumalizika kwa Man United kupata ushindi wa 2-0.

Isabela ala bata Uganda na Ex wa Aunt Ezekiel, Jack Pemba

$
0
0
Aliyekuwa mpenzi wa msanii wa filamu Aunty Ezekiel, Jack Pemba ameonekana akila bata nchini Uganda na aliyekuwa mpenzi wa zamani wa Luteni Karama, Isabela Mpanda.

Muimbaji huyo wa Kundi la Scorpion Girl pamoja na wenzake wapo nchini Uganda kwa ajili ya tuzo za Uganda Entertainment Award ambazo zinafanyika weekend hii.
AuntJack
Jack Pemba akiwa na mpenzi wake wa zamani Aunt Ezekiel

Mfanyabishara huyo maarufu ameithitishia Bongo5 kutoka na mrembo huyo.

“Wiki ijayo nakuja Dar es salaam, sasa hivi nipo na baby wangu, huyu ndio kila kitu kwangu,” alisema Jack Pemba.


Mabasi ya mikoani Kusimamisha huduma Jumatatu

$
0
0
Kuanzia Jumatatu wiki ijayo hakutakuwa na usafiri wa mabasi nchi nzima, baada ya Wamiliki wa mabasi yaendayo mikoani (Taboa) kuamua kusimamisha huduma hiyo ili yafanyiwe ukaguzi na Polisi.

Katibu Mkuu wa Taboa, Enea Mrutu amesema zaidi ya mabasi 4,000 yanayohudumia safari za mikoani, yatasimamisha huduma kuruhusu ukaguzi uliolenga kupunguza ajali za barabarani na kwamba, wameshaiandikia Sumatra barua kuitaarifu juu ya suala hilo.

“Tunataka mabasi yetu yakaguliwe kwa pamoja ili mamlaka husika zithibitishe ubora na kama yanaweza kuendelea kutoa huduma za usafiri bila wasiwasi wowote,” amesema.

Source: Mwananchi

Idris Sultan Yamemfika Hapaa

$
0
0
Msanii wa kuchekesha Idris Sultan amejitoa Rasmi katika mtandao wa kijamii wa Instagram baada ya kinachosemekana kuwa ni maji kumfika shingoni. Watu wa karibu wa Idris wanasema kuwa Mchekeshaji huyo maarufu Tz amekerwa na tabia ya mashabiki wake kumuita Shemeji wakati yeye Kula hali. Mmmmmh..!

Amesema kwamba yeye ana jina lake na kama angejua kama haya yote yatatokea leo basi asingekubali toka mwanzo kuitwa shemeji, amekasirishwa sana na matusi anayotukanwa pindi akiwaposti wanawake wengine hata dada zake. Pia wapo waliodai kuwa anatafuta kiki na anamuiga Justine Beiber kwasababu siku sio nyingi ataifungua tena na kuendelea na vichekesho vyake kama kawa.

Haya sasa Wenye shemeji mpo?

Mo Dewji Aanza Na Mishahara Simba SC

$
0
0
MFANYABIASHARA anayetaka kununua hisa ndani ya Klabu ya Simba, Mohamed Dewji ‘Mo’, ameanza kasi ya kuitumikia klabu hiyo ya Simba kwa kuanza kulipa mishahara ya wachezaji kuanzia mwezi huu huku suala la kununua hisa likitarajiwa kukamilika ndani ya mwaka mmoja.
Hatua hiyo ya Mo imekuja baada ya Kamati ya Utendaji ya Simba kuridhia kubadili mfumo wa uendeshaji wa klabu kutoka wa sasa wa wanachama na kwenda kwenye mfumo wa hisa, kufuatia Mo kuhitaji kununua hisa asilimia 51.

Mohamed Dewji ‘Mo’ (kushoto)  akisalimiana na viongozi wa Simba.
Aidha, kamati itaandaa mkataba wa maridhiano ili kila upande uweze kutekeleza majukumu yake ambapo Mo alieleza kuwa ataisaidia timu hiyo huku akiwa anaendelea kusubiria mchakato wa hisa kukamilika.

Akizungumza na Championi Jumamosi, mjumbe mmoja wa Kamati ya Utendaji Simba ambaye aliomba jina lake lifichwe, alisema Mo ataanza kuwalipa wachezaji mishahara kuanzia mwezi huu.
“Kwa sasa kuna kamati imepewa kazi ya kuwaelimisha wanachama juu ya suala hilo ili kuweza kufahamu faida gani watakayoipata juu ya suala hilo ili mwisho wa siku yafanyike maamuzi sahihi.


“Kwa kuanza, ataanza na kuwalipa mishahara wachezaji ambapo itaanzia mwezi huu na atapewa majina ya wachezaji wanaotakiwa kulipwa mishahara ili aweze kuwalipa wachezaji wote lakini jukumu alilopewa ni juu ya timu tu kwa sasa lakini mambo mengine yote yatabaki chini ya uongozi.
“Suala lake nadhani litachukua muda mrefu hata mwaka mmoja hadi kufikia kukamilika kwa mchakato mzima kufuatia kupata maoni mbalimbali na makubaliano kutoka kwa wanachama baada ya kupata elimu ya kutosha.

“Hata hivyo asilimia kubwa ya wanachama hawataki auziwe hisa kubwa ya asilimia 51 na badala yake auziwe asilimia 48,” alisema bosi huyo.

Alipotafutwa Msemaji wa Simba, Haji Manara kuzungumzia suala hilo, simu yake iliita bila ya kupokelewa hata katibu, Patrick Kahemele naye simu yake haikupokelewa.

Tayari Mo alishatoa msaada wa shilingi milioni 100 kwa ajili ya kusaidia usajili, kiasi ambacho Simba ilikitumia kwa ajili ya kukamilisha usajili wa wachezaji kadhaa nyota walionao hivi sasa.

Picha: Wizkid akiwa na wasanii mbalimbali wa Bongo Mwanza

$
0
0
Wakazi wa Mwanza Jumamosi wanakuwa wa kwanza kupata shangwe za Fiesta huku wakimshuhudia star boy, Wizkid kwa mara ya kwanza. Hizi ni picha mbalimbali za staa huyo akiwa na wasanii wa Bongo.

Ukimya wa Tip Top Connection Unaniumiza – Kassim Mganga

$
0
0
Msanii Kassim Mganga ambaye awali alikuwa ni moja kati ya wasanii kutoka katika kundi la Tip Top Connection amesema ukimya wa kundi hilo unamuumiza na kumgusa sababu yeye bado ni mwanafamilia wa Tip Top Connection licha ya kutofautiana kibiashara.

Kassim Mganga akiwa kwenye kipindi cha Planet Bongo alisema yeye bado ni mwanafamilia wa Tip Top Connection hivyo alikuwa anapenda kuona familia yake hiyo inaendelea na moto ule ule kama zamani.

“Unajua unapoongelea Tip Top Connection na Kassim Mganga ni kama familia, hivyo ile ni familia yangu japo tulipishana kwenye masuala ya biashara tu. Hivyo kama mwanafamilia wa Tip Top Connection ukimya wao unanigusa na kuniumiza sababu nilikuwa natamani kuona chama linaendelea na moto ule ule kama zamani” alisema Kassim Mganga

Mbali na hilo Kassim Mganga ameahidi kuja na band yake katika siku zijazo kwani anatamani kufanya muziki wa live kwenye show zake.

Naj wa Baraka da Prince Aitingisha Ndoa ya Mr Blue, Mkewe Arusha Kijembe

$
0
0
Mr Blue na Mkewe Walda Katika Pozi 
Baada ya kuibuka kwa madai ya kuwa Mr Blue na Ex wake wa zamani Naj huwenda wakawa wanawasiliana, kumekuwa na vijembe vya maneno kutoka kwenye kambi ya Mr Blue ambavo vinahisiwa huwenda vikawa vinaelekezwa katika kambi ya Barakah Da Prince na Naj.
mr blue

Ilo limeibuka baada ya kipindi cha U-Heard cha Clouds FM kudai Barakah Da Prince ambaye ni mpenzi wa Naj, wiki chache zilizopita akiwa ameshika simu ya mpenzi wake huyo, alipiga mtu ambaye namba yake ‘iliseviwa’ Zai na baada ya Barakah kupokea alikuta sio mwanamke bali ni mwanaume ambaye alidaiwa kuwa ni Mr Blue.

Sakata hilo linadaiwa kuitikisa kambi ya Mr Blue, ambapo wiki hii rapper huyo alipost picha ya mke wake aitwae Walda na kuandika ujumbe wa kumfariji mpenzi wake huyo.

“Hakuna zaidi yako ndo maana nimekuoa,” aliandika Mr Blue kupitia instagram yake.

Baada ya kauli hiyo, Ijumaa hii mke wa Mr Blue ameonyesha kuguzwa na mambo yanayoendelea katika mitandao ya kijamii na kuamua kufunguka.

“Mke na mume hatutoi kiki endelea kuhangaika @mrbluebyser1988,” aliandika Walda instagram katika picha akiwa na mume wake.

Hata hivyo kambi ya Barakah Da Prince na Naj inaonyesha iko sawa kwani wawili hao wanaonekana kuwa na furaha.

Rais Obama Achukizwa na Tabia ya Mwanae Malia Baada ya Kunaswa Akipuliza Bangi

$
0
0
Obama na Mwanae Malia
Hivi karibuni, Malia alionekana akivuta bangi kwenye tamasha moja maarufu.

Kwa mujibu wa tovuti ya RadarOnline, vitendo vya hivi karibuni vya Malia vimemsononesha sana Obama anayemaliza muda wake mwaka huu kama rais wa Marekani.

Awali, video ilisambaa mtandaoni ikimuonesha Malia Obama, 18, akionekana kuvuta bangi kwenye tamasha la Lollapalooza huko Chicago mwezi uliopita.

Kisha Malia alihudhuria kwenye party iliyopo kwenye kisiwa ambacho familia yake ipo mapumzikoni iliyofungwa na polisi. Malia alihitimu mwaka huu kwenye shule maalum ya Sidwell Friends ya Washington, DC, na anatarajiwa kujiunga na chuo kikuu cha Harvard mwaka 2017.

Msikilize Gwajima akitoa Laana kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha

$
0
0
Askofu Gwajima
Msikilize Gwajima akitoa Laana kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Bonyeza Hapa Chini:

Mfanyabiashara Moshi Ajimwagia Petroli na Kujipiga Kiberiti

$
0
0
Moto 
lnawezekana likawa tukio baya lililoacha gumzo na simanzi baada ya mfanyabiashara wa mjini Moshi, Romani Shirima (74), kujiua kwa kujilipua kwa petroli nje ya nyumba yake.

Habari kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo zinasema mfanyabiashara huyo alijifunika kwa blanketi, kisha kujimwagia petroli na kutumia kibiriti kuwasha moto ambao ulimlipua na kusababisha kifo chake.

Ingawa hakuna taarifa rasmi ya nini kiini cha mfanyabiashara huyo kuchukua uamuzi huo mgumu ulioacha maswali mengi, lakini baadhi walidai ni msongo wa mawazo uliotokana na madeni.

Hili ni tukio la pili kwa mfanyabiashara mkazi wa mkoa wa Kilimanjaro, kwani miaka kadhaa iliyopita, mfanyabiashara anayemiliki hoteli eneo la Marangu alijilipua kwa petroli akiwa katika gari lake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa alisema  jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi, saa 11.25 asubuhi maeneo ya Mjohotoni.

Alisema, mfanyabiashara huyo ni mmiliki wa shule ya sekondari ya Merinyo iliyopo mjini Moshi, na kusema kuwa aliamka asubuhi nyumbani kwake na kujimwagia mafuta hayo na kisha kujilipua na kiberiti.

Kamanda Mutafungwa alisema chanzo cha kifo chake bado hakijafahamika ingawa kuna maneno yanayoongelewa na watu, lakini hawawezi kuyachukua moja kwa moja na kwamba jeshi hilo linachunguza ili kubaini chanzo chake.

Taarifa za tukio hilo la aina yake zimekuwa gumzo katika maeneo mbalimbali ya mji wa Moshi na vitongoji vyake, hasa njia aliyoitumia kukatisha uhai wake.

Kumbe si Kenya tu,hata Ethiopia Hutumia Mlima K'njaro Kujinadi kwa Utalii

$
0
0
Wakuu week jana nilisafiri na ET805 kutoka KIA kupitia Mombasa then BOLE International Airport pale Adis Abbaba,nikiwa na safari yangu kwenda ughaibuni.

Nikiwa BOLE nikisubiri connection ya karibu masaa sita,nikashuhudia moja ya ndege za Ethiopia zilizopachikwa jina la "The Mount Kilimanjaro".Nikakumbuka kuliwahi kuwa na mjadala mkubwa sana kuwa Kenya kwa kutumia ndege yao aina ya Boeing777 wanautangaza mlima Kilimanjaro na kuonyesha kama upo kwao na si Tanzania.Mjadala huo uliwahi kufika bungeni ukichagizwa na Mama Anna Kilango wakati huo akiwa mbunge wa Same Mashariki.Wakati sisi tukilala,wenzetu wanatumia fursa za vivutio vyetu kujinadi

Nilipoona na Ethiopia Airways wametumia jina la "Mount Kilimanjaro" nikataka kudadisi,je na wao wanasadikisha huo mlima upo Ethiopia?Lkn jibu nililopata ni kuwa wao wameandika ili kuwaonyesha watalii mbalimbali duniani wanaopenda kuja kuutazama mlima huo kuwa unaweza kufika Kilimanjaro kwa kupanda Ethiopia Airways kupitia Addis Ababa hadi KIA,na ndio maana wao hupenda kuipeleka ndege hiyo kwa "route" za KIA na BOLE.
Ethiopian Air line

Mlima wetu unatangazwa na mataifa mengine,tuombee nia ya Rais kuifufua ATCL ili na sisi tutumie ndege zetu kuutangaza mlima wetu na vivutio vingine vya utalii,Kwani KQ wana ndege wamezipa jina la "Maasai Mara","Serengeti","Ngorongoro" nk.We are waiting for you dear ATCL.

RC Makonda Awaambia Watu wa Mikoani: Unaruhusiwa Kuja Dar Kwa Ruhusa Maalum tu

$
0
0
Unaruhusiwa kuja Dar es salaam lakini lazima uwe na sifa maalum ila unaruhusiwa kuja kumsalimia ndugu yako lakini usikae sana"- Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda


Download Application ya SIASA HURU Blog Kwenye Simu yako Kupata Habari za Siasa Kwa Urahisi

$
0
0
Kama wewe ni mpenzi wa Habari za Siasa basi hii ni habari njema kwako...Download Siasa Huru Application Kutoka Google Play Store Kwenye Simu yako itakurahisishia upataji wa Habari na Breaking News za Siasa kwa urahisi....

Bonyeza HAPA Kuinstall Kwenye Simu yako fasta....

Au Nenda Google Play Store Kwenye Simu yako Alafu Search 'Siasa Huru' Kisha Install


Chadema Watangaza Safu ya Maandamano ya UKUTA, Lowassa Amepangiwa Mbeya, Katibu Mkuu Kapangiwa Mwanza

$
0
0
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe jana alitangaza mkakati wa chama hicho kufanikisha mikutano na maandamano ya walichokiita Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (Ukuta), huku jeshi la polisi nao wakijiandaa kukabiliana nao.

Mbowe aliitaja mikakati hiyo ikiwamo kamati za kuhamasisha Ukuta ambapo aliyekuwa mgombea urais kupitia Ukawa Edward Lowassa amepangiwa Mbeya, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji atakuwa Mwanza, Makamu Mwenyekiti Profesa Abdallah Safari atakuwa Tabora huku Mwenyekiti wa Bawacha Taifa, Halima Mdee na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema Mabere Marando wakipangiwa Dar es Salaam.

Alisema yeye (Mbowe) ataongoza Kanda ya Kaskazini wakati Profesa Mwesiga Baregu amepewa jukumu la kufafanua Ukuta kwa taasisi za kimataifa, viongozi wa dini na wastaafu.

Mwanasheria Mkuu wa chama hicho Tundu Lissu na mawakili 12 wao watajifungia Dar es Salaam kufungua kesi 21 kutetea mikutano.

Lakini, Jeshi la Polisi limesema litatoa taarifa rasmi baadaye huku CCM wakisisitiza msimamo wao wa kupinga maandamano hayo.

Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Advera Bulimba alisema jeshi hilo litatoa taarifa siku chache zijazo. “Tutawaita na tutazungumza, naomba tujaribu tu kuvuta subira,”alijibu kwa ufupi msemaji huyo wa polisi.

Hata hivyo kikosi cha Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) katika mikoa mbalimbali ikiwamo Dar es Salaam na Kilimanjaro walionekana wakifanya mazoezi wakiwa na silaha na magari ya maji ya kuwasha kwa siku tofauti.

CCM watoa ushauri
Msemaji wa CCM, Christopher ole Sendeka alisema licha ya chama kuzungumza mara kadhaa, wanatarajia kutoa tamko kwa lengo la kuwaeleza Watanzania tahadhari juu ya mchezo unaojaribiwa na Chadema.

Sendeka alisema viongozi wa dini na makundi mbalimbali yameshauri juu ya mipango yao, lakini hawataki kusikia.

 “Jambo hilo limezungumzwa mara nyingi sana, viongozi wa dini wameshasema, watu wenye mapenzi na nchi yao wakishauri waache huo mchezo wao ambao sidhani kama watafanikiwa, kwa hivyo tunatarajia kutoa tamko letu siku yoyote kuanzia kesho (leo),”alisema.

Mbowe na safu yake
Akizungumza wakati akifungua mkutano wa viongozi wa Chadema Kanda ya Kaskazini jana katika Hoteli ya Coridol Springs jijini hapa, Mbowe alisema chama hicho kimejipanga kufanya mikutano na maandamano ya amani nchi nzima Septemba Mosi ili kutetea utawala wa sheria na Katiba.

Mbowe alisema Rais Magufuli aliapa kuilinda Katiba, Wabunge waliapa kuilinda Katiba, madiwani waliapa kuilinda Katiba ili nchi iongozwe katika misingi ya sheria na utawala bora.

Alisema haiwezekani nchi kuongozwa kwa matamko ambayo yanakiuka katiba na Chadema kama chama kikuu cha upinzani kina wajibu wa kuishauri na kuikosoa serikali na hawawezi kukaa kimya.

Alisema matamko ya Rais kuwa hakuna ruhusa ya kufanya mikutano ya kisiasa kwa vyama vingine na kuacha chama chake kufanya mikutano na pia kuzuia mikutano hadi mwaka 2020 haikubaliki.

“Sisi tunataka nchi iongozwe kwa kufuata sheria na siyo matakwa ya viongozi ambayo yanakinzana na sheria na Katiba ya nchi,” alisema Mbowe.

Alisema wanafanya mikutano na maandamano kama sehemu ya kueleza malalamiko yao, hasa kutokana na kauli za viongozi ambazo zinakiuka sheria.

Mbowe alisema vyama vyote vikiamua kukaa kimya na kuacha mambo yaliyotokea Zanzibar, yaliyotokea Dodoma na yanayotokea sasa kutokana na kauli za viongozi, ni wazi nchi haitakuwa salama.

“Tukiamua sote kujifanya wanafiki kusema hewala nchi haitakuwa salama itazaa taifa la watu wenye hofu na ndiyo sababu tumeamua kamati kuu kuanzia sasa kufanya kazi kila siku kuisaidia sekretarieti,” alisema.

Mbowe alisema kutokana na unyeti wa Ukuta, Kamati Kuu ya Chadema imeunda kamati ndogo tano, ambazo zitasaidia kufikiwa malengo yaliyokusudiwa kwa kuhusisha taasisi na vyombo vingine.

Alisema pia kuna kamati ya maandalizi ya Ukuta ambayo tayari imeanza kazi ya kufafanua maamuzi ya kamati kuu, ambayo sasa imesambaa katika kanda zote kutoa elimu kwa viongozi wa Chadema.

“Katika kanda zote nchi nzima viongozi watakwenda kuzungumza na wanachama wa kada zote na kuwaelimisha kwanini Kamati Kuu imefikia maamuzi ya kuanzisha Ukuta kabla ya kushiriki mikutano na maandamano Septemba Mosi,” alisema
Viewing all 104712 articles
Browse latest View live




Latest Images