Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104775 articles
Browse latest View live

Moshi Mweupe Waanza Kuonekana CUF, Haya Hapa Majina Matatu Yaliyopitishwa Nafasi ya Uenyekiti

$
0
0
Baraza Kuu la CUF limepitisha majina 3 yatakayopigiwa kura kujaza nafasi ya Uenyekiti, iliyoachwa wazi na Prof. Lipumba mwaka jana.

Majina hayo ni Twaha Taslima, Riziki Shahari Mngwali na Juma Nkumbi.


Diamond Platnumz Amwagia Sifa za Kumwaga Zari Hassan...Aongelea Kuhusu Mimba ya Pili

$
0
0
Mkali wa smash hit iitwayo ‘Kidogo’, Diamond Platnumz amethibitisha ujio wa mtoto wake wa pili kutoka kwa mpenzi wake Zari.

Taarifa hizo staa huyo alizitoa leo August 21, 2016 kwenye mtandao wake wa instagram na kuyaandika haya:
Ukiwa na Mwanamke Mzuri, Superstar, Ambae shilingi Mia miambili haimpigi chenga, Halaf ana akili, Akakuzalia Mtoto wa kike’‘Halaf mtoto nae Star, halaf akawa na Mimba yako Nyingine ya mtoto wakiume.. basi unajionea Mashia Muruaaaaaaaaaaaaaaaa😊😄😍😚😍…Lol yani Hapa najikuta kama sjui Biligeti Mzee wa Kwio😊😆 😘😍💞💕💝 Mi nampenda huyu dada’– Diamond Platnumz

Baraka Da Prince Kayatoa ya Moyoni Waliosema Ameshindwa Kuongea Kiingereza

$
0
0
Kama utakuwa unakumbuka hivi karibuni msanii wa Bongo Fleva, Baraka Da Prince kutoka kwenye label ya Rockstar 4000 aliingia kwenye headlines baada ya mpenzi wake Najma kuonekana kuwa kama mkalimani wake kwenye interview ya MTV Base.

Baraka Da Prince na kuyaongea ya moyoni:
Unajua watanzania asilimia kubwa wanakuwa wanakurupuka sana mimi sijaona kwanza kitu cha ajabu cha mimi kutumia lugha ya Kiswahili, mimi nimeenda MTV Base nimeulizwa Je unataka kutumia lugha gani ili uwe huru nikawajibu ninaweza nikatumia lugha ya Kiingereza lakini sitokuwa huru’–
‘Sasa wabongo walifurahi wengine wakasema nimeshindwa kuongea kingereza kwangu mimi nimeitangaza  lugha yangu ya kiswahili halafu Najma hakuwa mkalimani wangu mimi bali alikuwa anawambia yule mtangazaji kile ninachokizungumza mimi’- Baraka Da Prince

Msanii Ruby na Clouds FM Hapatoshi..Aikacha Show ya Fiesta Mwanza Kisa Maslahi Madogo

$
0
0
Mtandaoni wa Tizneez ametoa exclusive ya kwanini Msanii Ruby hakuonekana Mwanza wala kupanda katika jukwaa la Fiesta wakati alikuwa mmoja wa wasanii waliosajiliwa...
Hivi Ndivyo mtandao huo ulivyoandika
Exclusive Ruby Amezungumza mengi ila kati ya machache ni "Maslahi yamenifanya nisiende kwenye Fiesta, Kisa ni Clouds ndio nisiwe free na kuongea, end of the day it's not about clouds it's about my future.Katika shindano la super diva ilikuwa super diva mshindi atafanya Fiesta, wakati umefika lakini ntafanya Fiesta for nothing? Mimi sitaki kuongelea price ambayo naipata sababu nahisi nikiongea sijui watu watajiskiaje ukubwa wa show ulivyo. ...Tunakuwa na menejiment ambazo zinaendesha wasanii kimabavu, unadhani kwanini @jidejaydee wanamuita komando?? 

JE Mdau Unaona Huo Ndio Mwisho wa Ruby ? Au Clouds FM ndio wanamakosa... ?
Kwanza migogoro ilianza na Mkubwa na Wanawe , Sasa imegeuka kwa Clouds FM ambao ndio waliomtoa na kumkuza mpaka hapo alipo sasa....

Kajala: Nataka Kuzaa Mtoto wa Kiume

$
0
0
Kajala na Mwanae Paula
“Nahitaji kuzaa mtoto wa kiume ili Pamela naye ajivunie kuwa na kaka, siku zote nilitamani nipate watoto wenye jinsia tofauti, tayari ninaye wa kike sasa ni zamu ya kumpata mwingine wa kiume.” Ni kauli ya Kajala Masanja mwanadada anayefanya vyema kwenye soko la filamu nchini.

Kauli hiyo ya Kajala imekuja siku chache baada ya kuulizwa na Global Digital kama ana ndoto za kupata mtoto mwingine siku za hivi karibuni wakati mumewe akiwa bado yupo gerezani.

Mwanadada huyo alifunguka zaidi na kusema, “Hakuna mwanamke asiyependa kuwa na mtoto wa kiume japokuwa mtoto ni mtoto, na nipo tayari kuzaa na mwanaume yeyote aliye tayari na anayejitambua na kuwa tayari kuitwa baba na kugharamia gharama za matunzo ya mtoto kwa kushirikiana.” Alisisitiza.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya Agosti 22, Ikiwemo ya Lipumba Aipasua CUF

$
0
0


Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya Agosti 22, Ikiwemo ya Lipumba Aipasua CUF

Wakili Atolea Ufafanuzi Madai ya Reginald Mengi Kuitwa Mahakamani Kujieleza Kwa Nini Asifungwe

$
0
0
Wakili Atolea Ufafanuzi Madai ya Reginald Mengi Kuitwa Mahakamani Kujieleza Kwa Nini Asifungwe

Lema Amjibu Waziri Mwigulu. Asema Yupo Tayari Kufa Akipigania Haki Operation Ukuta

$
0
0
Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini amemjibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba kuwa Arusha tumejiandaa vyema kwa ajili ya Operesheni UKUTA, na kwamba Mwigulu siyo wa kwanza duniani kutoa lugha za vitisho duniani. Lema amesema kuwa tumejiandaa kufa ama kuuawa na Jeshi la Polisi wakipigania haki na kuikumbusha serikali kuacha kuvunja katiba ya nchi ambayo Rais na viongozi wote waliapa kuilinda.

Mh Lema ameyasema hayo kumjibu Mwigulu Nchemba aliyesema anawaonya chadema wasitingishe kiberiti, kwamba viberiti vingine vimejaa gesi.

Lema amesema kuwa kauli za hovyo zinazotolewa na serikali zinaweza kuingiza nchi kwenye machafuko. Amesema Farao Mungu alimfanya moyo wake uwe mgumu ili Apate kujitukuza mbele ya wana Israel, na kinachoonekana hivi sasa ni kwamba Mungu ameufanya moyo wa Magufuli kuwa mgumu ili Tanzania ili iweze kukombolewa.

Lema amesema kuwa hatumjaribu mtu bali wakati wa kuandamana bali tunatetea utawala wa sheria uzingatiwe, tutaandamana kutetea haki yetu ya kikatiba kufanya mikutano.

Amesema kwamba kwa sababu wamejiandaa kutupiga, nasi tumejiandaa kwa kila kitu, kwamba tunajua tarehe moja siyo siku ya harusi, kwamba tarehe moja tumejiandaa kwenda jela ama kuawa.

Tunajua tunakwenda kukumbana na polisi wakiwa na silaha na mabomu lakini tumejiandaa.

Kama Mauti imepoteza utukufu wake kwangu, hakuna statement yoyote inayoweza kurudisha Arusha kuandamana.

Amemuonya Mwigulu apime kauli zake kabla hajaitoa.

Lema amesema madai ya chadema ni madai ya msingi na endapo madai yake yatapuuzwa nchi inaweza kuingia kwenye machafuko.

Mh Lema amesema hatuandamani bei ya konyagi ipungue, bali tunaandamana utawala wa sheria katika taifa hili uzingatiwe.

Kama leo haturuhusiwi kufanya mikutano ya hadhara kwasababu rais amesema, iko siku misikitini ama makanisani itafungwa kwasababu rais amesema. Hii vita ni ya kila mtu katika taifa hili, siyo vita ya chadema

Nitakuja kumalizia baadaye kidogo nimalizie natafuta namna ya kuiweka clip hapa

Lipumba Aipasua CUF, Wajumbe Warushiana Viti na Kutukanana, Mkutano Wavunjika

$
0
0
Mkutano Mkuu Maalum wa Chama Cha Wananchi (CUF), uliofanyika jana jijini Dar es Salaam ukilenga kuwachagua Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho ulivunjika baada ya wajumbe kuanza kurushiana viti na matusi baada ya kupishana katika hoja ya kumtosa aliyekuwa Mwenyekiti wake, Profesa Ibrahim Lipumba.

Profesa Lipumba alijiuzulu nafasi yake kabla ya kampeni za uchaguzi Mkuu mwaka jana akieleza kuwa roho inamsuta kumnadi mgombea urais aliyeungwa mkono na vyama vya Ukawa. Lakini mwaka huu alirejea na kuandika barua akiomba kurejea kwenye nafasi yake hali iliyozua sintofahamu.

Taarifa kutoka ndani ya Mkutano huo zimeeleza kuwa wajumbe 832 walihudhuria lakini hoja ya kumjadili Profesa Lipumba ilipofikiwa, baadhi ya wajumbe ambao wanamuunga Mwenyekiti huyo wa zamani walizua vurugu wakipinga utaratibu uliotumika.

Baadhi ya wajumbe hao waliwaambia waandishi wa habari kuwa viongozi waliopo madarakani walifanya ubabe kwa kulazimisha kura ya kukubali au kukataa ombi la Lipumba ipigwe kwa uwazi na sio siri kama Katiba inavyoeleza.

“Haki haikutendeka, ni ubabe. Wala mkutano haikuzingatia kutimia kwa akidi. Tulilazimishwa kupiga kura kwa kunyoosha mikono wakati mazingira yaliyopo na usahihi, kura ni siri,” mmoja wa wajumbe hao alikaririwa.

Baada ya kupiga kura za wazi, Lipumba alipata kura 14 kati ya kura 832 hivyo kuonekana kukataliwa kwa kishindo, lakini vurugu zilizuka ghafla kutokana na maamuzi hayo na mkutano ukashindwa kufanikisha zoezi zima la kuwapata viongozi hao wapya.

Katika hatua nyingine, Juma Haji Duni alijiengeu katika kinyang’anyiro cha uchaguzi huo, baada ya baadhi ya wajumbe kusisitiza kuwa katiba inamtaka mtu aliyejiuzulu na kuhamia chama kingine kusubiri miaka miwili ili agombee nafasi ya uongozi ndani ya chama pale atakaporejea.

Mkurugenzi wa Uchaguzi na Mipango wa CUF, Shaweji Mketo, alisema kuwa Duni alijiondoa kutokana na maadui wa Ukawa kutaka kukihujumu chama hicho.

Mkutano huo umeahirishwa hadi utakapotangazwa tena.

Wema Sepetu ampigia magoti Idris Sultan

$
0
0
Uhusiano wa Wema Sepetu na Idris Sultan unaanza kutukumbusha ule wa Chris Brown na Karrueche Tran ule wazungu wanauiita ‘off and on.’

Baada ya hivi karibuni kuzinguana tena hadi kumfanya Idris ajiondoe Instagram hadi sasa, wawili hao wanaonesha kuanza kutafuta suluhu.

Wema amepost picha hiyo juu Instagram inayoonesha walikuwa wakiwasiliana kutumia app ya Facetime, aliandika: That moment you realise how much u miss a special someone… Rudi basi… hata kidogo tu… 😔

Wawili hao waliingia kwenye mgogoro baada ya Wema kuisusia show ya Idris, Funny Fellas kwa mara nyingine tena huku mshindi huyo wa Big Brother akihudhuria za mpenziwe, ikiwemo Black and Tie iliyofanyika mwezi uliopita.

Baada ya kuchoshwa na tabia ya mpenzi wake kutompa support kwenye show zake, Idris naye aliamua kuipotezea show ya Usiku wa Vigoma iliyoandaliwa na Sepetunga mwishoni mwa wiki – na hapo ndipo mambo yalipoharibika.

Mashabiki wa Wema walikasirika baada ya shemeji yao kuikwepa show hiyo na wanamshambulia Instagram. Kutokana na kuandamwa, Idris amelazimika kuongea:

Sipendi kuona watu wakiingia na kuongea kama wanajua maisha yangu na watu wangu wa karibu, makosa wakifanya wengine mnakuja kwangu mnaanza “Ndio asingefanya vile kama sio wewe kufanya hivi” mnakazana kusema eti naposti wanawake mara ooo porojo kibao. Sina freedom ya kumpost dada angu ? Kweli ? Au rafiki yangu kazindua brand mpya siwezi mpost nikampongeza?

Mnauliza kwanini sijaenda vigoma nimesema because show yangu hakuja hata moja na nimeenda show zake zote na yeye halalamiki because anajua nimesema siendi fair enough mbona hamjaongelea hilo? I repeat nikikaa kimya is for a pure reason that it’s not anyones business this is my personal life kama mnaongeleaga fair basi mngefanya kuuliza kwanini mpaka am selling out hajaja.

“Give me a break sina maisha ya kuigiza lets have respect for each other bana. Na nimesema msiniite shemeji for one big good reason, imekua too much i am a brand na jina idris linamezwa na shem, ningejua this from the beginning nisingeruhusu mniite tangu mwanzo so msiwe kila kitu mnafikiria negative tu. Na sikuwa na haja ya kuandika yote haya pia TusichukulianePoa.

Hata hivyo Wema naye alimpigilia msumari wa moto Idris kwa kupost picha ya wanaume anaowapenda #MCM (Man Crush Monday) na mmoja wao ni Diamond.

Ubishoo Kwenye Muziki Niliuanzisha Mimi – Mr Blue

$
0
0
Mr Blue
Mkali wa wimbo ‘Mboga Saba’ Mr Blue amesema yeye ana mchango mkubwa katika mabadiliko ya muziki wa bongofleva nchini.

Akiongea katika kipindi cha Ndoto Kubwa cha Clouds TV Jumapili hii, Mr Blue amesema yeye ndiye msanii wa kwanza kufanya muziki akiwa na swagga.

“Mimi baada ya kuingia kwenye muziki kuna vitu ambavyo nilivifanya mimi kama mimi ili kuonyesha utofauti, kuanzia kwenye kuvaa, swagga za kuimba, kutoboa masikio. Kwa hiyo hivyo vyote kwa wakati ule watu walikuwa wananiona huyu jamaa vipi, kumbe mimi tayari nilikuwa nimeshaiona future, ndio maana wasanii wengi waofanya muziki kwa swagga, utasikia ana flow kama Mr Blue, tayari tulishaacha alama huko ndiyo maana tunaendelea kufanishwa,”

Katika hatua nyingine Blue amesema yeye alikuwa anapenda kusoma kuliko kufanya muziki, lakini akaamua kujifunza kufanya muziki mpaka akaweza.

Soma Nafasi za Kazi Zilizotangazwa leo Katika Magazeti na Mitandaoni

$
0
0

UVCCM Waitisha Maandamano Nchi Nzima Agosti 31

$
0
0
Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) wanatarajia kufanya maandamano ya Amani nchi nzima Agosti 31 kwa ajili ya kueleza utendaji kazi wa Rais Dk.John Pombe Magufuli kwa Watanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja huo, Shaka Hamdu Shaka amesema kuwa wameshamwandikia barua mkuu wa jeshi la Polisi kwa ajili ya kupata ulinzi siku hiyo

Amesema kuwa wasipopata ulinzi watafanya kwa kujilinda wenyewe ikiwa ni lengo la kufikisha ujumbe kwa wananchi juu ya utendaji kazi wa Rais Dk. John Pombe Magufuli.

Shaka amesema kuwa Rais Dk.John Pombe Magufuli amefanya watendaji kuwa na utii pamoja na maadili katika utoaji wa huduma kwa wananchi.

Aidha amesema kuwa katika maandamano hayo wanaawalika na vijana wa vyama vingine kushiriki kwa lengo moja tuu,la kuunga mkono utendaji wa Rais Dkt.John Pombe Magufuli.

Mtangazaji Gerald Hando Afunda Ndoa

$
0
0
Mtangazaji maarufu wa Kipindi cha Joto la Asubuhi katika Kituo cha Radio cha Efm, Gerald Hando amefunga ndoa juzi Jumamosi, Agosti 20, 2026 na mpenzi wake, Miriam Kitenge.

Sherehe ya harusi hiyo iliyokuwa ya aina yake ilifanyika katika Ukumbi wa Golden Tulip uliyopo maeneo ya Posta jijini Dar es Salaam ambapo baadhi ya mastaa walihudhuria huku mwanamitindo maarufu, Sheria Ngowi akiwa ndiye mbunifu wa mavazi ya maharusi hao.

Hando ameuaga ukapera na kuanza kufurahia maisha mapya ya ndoa na mkewe Miriam kama walivyofanya mastaa kadhaa hivi karibuni wakiwemo mchekeshaji maarufu, Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’ wa Orijino Komedi na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe.

Habib Mchange Amshukia Julius Mtatiro, Adai Amemgeuka Prof Lipumba Baada ya Kumfikisha Hapo Alipo

$
0
0
Mwanasiasa Habib Mchange Amemshukua Julius Mtatiro kama ifuatavyo:

"Siasa bwana wakati mwengine hovyo kabisa.
Eti Leo ‪#‎JULIUSMTATIRO‬ aliyechukuliwa na ‪#‎Lipumba‬ baada ya kuhitimu UDSM na Hekaheka za serikali ya wanafunzi DARUSO na kutelekezwa na Mnyika na Chadema anamwita #LIPUMBA msaliti!

..Duh kweli shikamoo Siasa,
Lipumba huyu huyu aliyempa Ukurugenzi wa sheria na haki za Binaadamu cheo kilichokuwa kikishikiliwa na Mbarala Maharagande Leo amemsaliti aliyemteua na kumpa mshahara kama njia ya kuwatia moyo vijana waliokuwa vyuoni wakifanya harakati.

Yaani #LIPUMBA aliyempa ‪#‎MTATIRO‬ unaibu Katibu Mkuu wa CUF from nowhere akimtosa ‪#‎WILFREDLWAKATARE‬ na kumpa muhitimu wa chuo kama chachu ya kuwatia vijana wengine Siasa bila kuwa na uzoefu wowote katika Siasa Leo amegeuka MSALITI mbele yake? ...
Kweli ukiwa unafanya Siasa uwe na ngozi ngumu aisee.

Ndio mana siasa inahusianishwa na uongo uongo na maneno mengi
Ukianza kuongea saaana unasmbiwa usilete siasa hapa. Ukiwa kigeugeu unaambiwa usilete siasa hapa.

Na Ndio mana naelewa Sasa kwanini #Mtatiro aliweza kuandika makala tuliyoipenda Sana ya ‪#‎NJAAMPAKAmakanisani‬ akiwalaumu viongozi wa Dini wanaopokea pesa za Lowassa lakini baadae akasimama kidete kumnadi huyo huyo Lowassa.
Nazidi kuelewa aisee. Siasa haihitaji uwe mkweli, ni kuongopa tu mwanzo mwisho ukisema ukweli inakula kwako.

Ni kama yule aliyewashauri watu wa Arusha wamzomee Lowassa kwa sababu ni Fisadi lakini alipohamia Chama chake akasimama kumnadi.

Ama yule mchungaji aliyesema "atakayemuunga mkono Lowassa akapimwe akili "...miezi michache baadae akawa mpiga debe wake Mkuu na fulana zenye picha yake akavaa.

Mwishowe watu wenye akili timamu watawadhalau wanasiasa kwa Unafiki wa namna hii.
Ndimi"

Habib Mchange

Bashe na Mtazamo Wake Juu ya UKUTA "Jamhuri Inacheza Ngoma ya Chadema"

$
0
0
Bashe na mtazamo wake juu ya #UKUTA
Wanachokifanya hawa UKUTA ni kuitia Serikali hasara. Zaidi ya hilo Chadema wamekuwa PRO ACTIVE na kuwalazimisha "JAMHURI" kuwa REACTIVE. Sasa Jamhuri inacheza ngoma ya Chadema badala ya Chadema kucheza ngoma ya Jamhuri. -
#UKUTA

Taarifa ya Polisi Dar kuhusu wanaojihusisha na ‘UKUTA’

$
0
0
Licha ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kutangaza kufanya maandamano ya nchi nzima Septembe 1 2016, Jeshi la Polisi kanda maalum Dar es salaam limemkamata mtu mmoja anayejulikana kwa jina la Yoram Mbyellah kwa kupatikana na kuuza sare aina ya fulana zenye maneno yanayodaiwa kuwa ni yakichochezi zikiwa na alama ya CHADEMA huku nyingine zikiwa na maneno ‘UKUTA’

Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es salaam Simon Sirro amesema…>>>’August 20 2016 Jeshi la Polisi lilipata taarifa toka kwa raia wema kuwa maeneo ya Kinondoni kuna duka linauza flana zenye maneno ya uchochezi yaliyoandikwa ‘’TUJIPANGE TUKATAE UDIKITETA UCHWARA’’ , ‘UKUTA’ ‘

‘Aidha Polisi baada ya kupata taarifa hizo walifika eneo la tukio na kumkamata mtuhumiwa aitwaye YORAM SETHY MBYELLAH miaka 42, mfanyabiashara na mkazi wa Mburahati akiwa anauza fulana hizo dukani kwake‘ –Kamanda Sirro

‘Ili tuishi kwa amani ni lazima tutii sheria na kama hutaki kutii sheria tutashughulika naye, Kama kuna mtu anataka kuvunja amani katika mkoa wetu ajue kabisa hatoweza na niseme tu kwamba kama wanataka kujenga ukuta wajenge ukuta mwingine maana huu umeshadondoka‘ –Kamanda Sirro

‘Na wapo watu wanasema kwanini tunafanya mazoezi, nikwamba Jeshi la Polisi ni kawaida kufanya hivyo na muhimu watu wajue hiyo September 1 hakutakuwa na maandamano ya aina yoyote kwahiyo watu wasiwe na hofu bali wachape kazi‘ –Kamanda Sirro

Ruby ni Pasua Kichwa, ana Dharau, Anajisikia – Asema Msanii wa THT

$
0
0
Kwa mujibu wa msanii wa THT, Max Spesho ambaye ni muigizaji wa tamthilia ya Kelele ya Clouds TV, Ruby ni pasua kichwa, ana dharau, anajisikia na mgumu kufanya naye kazi.

Max amejitokeza kusema hayo baada ya Ruby kutangaza kujitoa kwenda kutumbuiza kwenye Fiesta Mwanza licha ya kusaini mkataba wiki chache zilizopita. Ruby ameitupia lawama Clouds na management ya THT kuwa hawathamini wasanii.

Lakini Max anadai kuwa kwa wasiomjua Ruby wanaweza kuhisi anaonewa lakini wanaomjua wanafahamu alivyo na matatizo.

“Ruby ni msichana ambaye hawezi kuishi na watu wote vizuri kutokana na the way anavyojiweka yaani mtu fulani hivi wa ususa susa na kukera kera, vitu ambavyo watu wengi hawapendi kufanyiwa kibinadamu japo ana uwezo mkubwa wa kuimba,” Max ameiambia Bongo5.
“Na kwa upande mwingne tunasema bado hajakuwa kiujumla,” anasema Max.

“Kwa sababu inasikitisha sana ..mama yako alokulea ukaanza kumtukana, si utapata laana? Hata kama kakukosea waswahili wanasema mama ni mama tu hata awe chizi atabakia kuwa mama. Uamuzi aliochukua anaweza akaona amefanya kitu poa lakini nina uhakika amefanya kitu ambacho atakuja kujuta maisha yake yote,” amesisitiza.

“No way out…jiulize wasanii wangapi wapo Clouds wasanii wangapi wapo THT na ushawahi kusikia wanalamika eti pesa ndogo wanayolipwa kwenye show au kaz yoyote! Mimi nIpo pale THT inaenda 1 year and a half sasa, sijaona mtu akidhulumiwa,sana labda utachelewa kulipwa tu.”

“Tukienda mbali Ruby amekuwa akitukosea hadi sisi wasanii wenzie, imagine tuko wote kituo kimoja halafu hatuongeleshani, huongei na wenzio, bingwa wa kushushua wasanii wenzio kutukana yaan she is out of discipline na kibaya zaidi anasahau kuwa mabosi walikuwa wakimfichia machafu yake anayoyafanya ilimradi tu brand yake iendelee kukua. Anatukosea wala haadhibiwi, nafikiri ndio amejisahau na kujiona kuwa hakuna kama yeye sababu anajua kuimba na vile show zote alikuwa hakosi basi ndio akajihakikishia hivyo na kujikuta na yeye commando. Huwezi kujicompare na commando [Lady Jaydee] she is a legend, hayo ni mambo ya wakubwa yaan Ruby ni worst,” amesisitiza Max.

“Niulize kitu, unaweza ukasaini mkataba kabisa wa show halafu imebakia masaa show ifanyike ndio unasema eti huwez kufanya show maslahi maduchu? Sasa ulisaini ili iweje? Hukusoma pale pale mkataba ulipopewa? Mazoezi yote kafanya ya show na kwenye social anaandika kabisa kwamba yuko excited na kuchukuliwa Fiesta na kusaini, few hours before unazngua! Mimi nafikiri cha kumshauri Ruby kwa sasa angerudi tu kanisani aendelee na nyimbo za dini, atapata vihela huko maana na kanisani kwenyewe nako pia alichafua akapewa laana ya kanisani.”

Bongo5

Hamisa Mobetto Aukata Mzizi wa Fitina kuhusu Tetesi za Kutoka na Diamond

$
0
0
Kwa muda sasa mlimbwende wa Tanzania, Hamisa Mobetto amekuwa akituhumiwa kutaka kumpindua Zari the Bosslady kwa Diamond Platnumz.

Skendo hizo zilivuma zaidi mwezi na kitu uliopita baada ya kudaiwa kuwa uwepo wa mrembo huyo kwenye sherehe ya kuzaliwa ya mama yake Diamond kulitaka kusababisha timbwili kwakuwa Zari alikuwepo.

Na sasa Hamisa amefunguka kuwa yeye na Diamond hata hawajuani kihivyo!

“Hiyo sio kweli,” alisema Hamisa kwenye mahojiano na gazeti la The Citizen baada ya kuulizwa kuhusu tetesi hizo.

“Pia sijawahi kuwa karibu na Diamond na siku ya kwanza tumekutana ilikuwa ni siku anazindua video ya Number 1 pale Serena,” aliongeza. “Tena wakati hiyo habari imeanza kusambaa nilikuwa nje ya nchi.”

Habari hizo zilivuma zaidi wiki kama tatu zilizopita baada ya kuonekana picha ya Hamisa akiwa kwenye chumba kile kile Diamond alilala na Zari Afrika Kusini.

Diamond alilazimika kutolea ufafanuzi picha hizo kupitia kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM. Pia alielezea tetesi za kuwa na uhusiano na mrembo huyo.

“Hamisa nimeanza kumjua zamani sana na sina uhusiano wa kimapenzi na yeye, juzi kati alikuwa kwenye video yangu mpya nimefanya na Ray Vanny na hiyo ndo imeleta maneno maneno yote hayo,” alisema Diamond.

Na kuhusu picha iliyounganishwa wote wakiwa wametumia chumba kimoja alisema, “Pale ni South Africa sehemu ile inaitwa Capital ni apartment ambazo vyumba vyake vyote vinafanana kama unavyoona hata Madam Rita pia ana share katika hizo apartment naye anayo yake na pia wabongo wengi tunapenda kufikia hapo kidogo huwa ni rahisi.”

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya Agosti 23, Ikiwemo ya CUF Kumeguka

$
0
0

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya Agosti 23, Ikiwemo ya CUF Kumeguka
Viewing all 104775 articles
Browse latest View live




Latest Images